Search This Blog

Monday, March 23, 2020

THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 5/10


THE PAINFULL SECRET
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
 SEHEMU YA 5 KATI YA 10


Siku iyo alichelewa sana kutoka ofisini kwake mpka saa tano usiku ika mkuta.
Ki uchovu aliisimama na kutoka huku akiiendea gari yake,
Aliingia na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwake, ila baada ya kufika jangwani anaona piki piki za mapolisi ziki mpita na kusimama mbele yake waki mpa ishara kuwa asimame kwani kuna tatizo,
baaada ya kusimama anaona pia deffender nyingine mbili ambapo pia.walishuka maaskari wengine wakimuendea alipo.
"Arooo arooo, habari ya kwako bwana mdogo, fungua kioo"
Aliongea mmoja wa maaskari huku akigonga kioo cha gari la Alfred.

aliongea kwa rafudhi ya kikurya , na Alfred kutii bila kipingamizi kwani aliamini hakuna kosa lolote alilofanya.
"Habari za kazi , poleni na kazi"
"Shuka ndani ya gari, tuka gue gari yako, fanya aaraka fanya upesi"

Alfred ali tafakari kwa muda kidogo huku akijishauri shauri na kushuka, na ndipo hapo maaskari wale walianza kupekua ndani ambapo Alfred hakuelewa ni nini wana tafuta,
baadae anaa mriwa afungue boneti la nyuma la gari na kulifungua.
Hakuamini alicho kiona uso kwa uso alikutana na mtu aliye kufa kwa kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya saana moyo wake ulianza kwenda mbio huku akizidi kusogea taratibu ili aweze kumtambua hakuamini baada kuona sura ambayo aliitambua sana alikuwa ni mbunge wa Mara Mheshiwa Zackaria John Mwita,
"Tulia ivyo ivyo upo chini ya urinzi aroo, Upo chini ya ulinzi mikono juu, rija mbazi sugu turi rokua tula litafuta, , una kosa kubwa sana, wewe ni Alsha baab eeh, ?"
Tayari aliwekewa mitutu kila kona , kweli Alfred aliingiwa na wasi wasi sana,
Na kuanza kuhaha leo hii anaenda kujibu kesi ya kumuuwa mbunge.
Jasho kwa mbali lili anza kumtoka huku akizidi kuangalia ile maiti iliyokutwa ndani ya gari yake mbunge wa Mara ambae alikua nae wiki chache zilizopita wakila chakula cha usiku wote, leo hii ame kufa hakutaka kuamini alichokiona pale aliona kama ni miujiza na kubaki kuitolea macho maiti ile iliyo jeruhiwa vibaya sana

"Hapana mimi sija ua"
"Jinga wewe. , rione, Afande Gregory mtie ndani ya gari huyu, ume muuwa muheshiwa, kerbu wewe, rione, , ni mbunge wetu huyu aise,. Tatata Mura"

Wali muweka chini ya ulinzi Alfred na kumpakiza ndani ya Deffender, picha ya milango.ya. jela ikifunguka nayeye kutupwa ndani gerezani kwa kosa la kuua tena mbunge ililijenga ndani ya ubongo wake na kuzidi kuchanganyikiwa sababu aliamini hakuna atae msikiliza.....



Akiwa amekalishwa nyuma ya deffender huku kukiwa na askari wawili wakiwa na mitutu mkononi,
aliweza kuwasoma vizuri na kuonekana kama akitafakari kitu kwa kuwa tazama kwa muda mrefu.
"Yaani ume muuwa kiongozi wa serikali, yaani wewe una enda kunyongwa kaka, bila ubishi wana kutia sindano ya sumu",

Askari huyo aliye kua pembeni yake ali mbeza.
"Nisikilizeni mimi sija ua, nieleweni"
"Shut up, kimnya pumbafu, PUMBAFU nani kakupa amri ya kuongea hapa, una takiwa usikilize sio kujibu, ndo ulivyo funzwa kwenu , pumbavu. Goi goi we"

Alfred alikaa kimnya na kumwacha askari yule aongee anayo taka kuongea yote ,
Alfred aliangalia angalia mule ndani ya deffender ambamo kulikua na giza lili sosababishwa na kufungwa na turubai kwa nje,
Alimuona askari yule ana pokea simu pale pale hakupoteza muda alimvaa na bega na kumtwanga kichwaa puani huku yule mwingine akimmalizia na teke la kichwa,
alichukua mtutu na kumtwanga mmoja wao juu ya utosi kwa kutumia kitako cha mtutu na kumfanya apoteze fahamu,

"Tulia kimnya, uki fanya fujo natoa uhai wako"

Alfred aliongea akiwa na mtutu ule huku akimuelekezea yule askar ambae wakati ule alianza kuumwaga mkojo, dereva wa deffender hakuwa anaelewa chochote yeye alizidi kuendesha gari.
"Ta, ..taa fadhali usi ninini ue"
Askari huyo aliji kuta ana pata kigugumizi cha ghafla na Alfred kutoamini kuwa kama ni yeye ndo aliye kua anaomfokea muda mchache uliopita na kumpiga mikwara.
"Wewe si ndo ulikua unachonga, aya nisikilize, mchukue mwenzako mfunge kamba fanya chap chap,",

Askari yule kitendo kile alikifanya haraka haraka, baada ya kumaliza Alfred alimpiga na kitako na mtutu na askari yule kudondoka kama mzigo .Alichofanya Alfred alipanda juu ya gari na kuuendea mlango aliokaa dereva huyo ,
"Kimnya weka gari pembeni, haraka sana , la sivyo nita sambaza ubongo wako"

"Sawa .. sawa hakuna shida"
Dereva yule alitii tena bila kipingamizi chochote baada ya kuona mtu aliye muwekea mtutu hana mzaha hata kidogo.
"Chukua hiyo radio call, waambie wenzako waendelee na safari, ume patwa na tatizo kidogo. Na ukiongea vitu vingine tofauti,.MEDULA OBLONGATA yako nita ifanya vibaya"
Dereva huyo ambae nayeye alikua askari hakua na jinsi alichukua redio iyo upepo na kuanza kuwapa habari askari wenzake.
"Una nipata ova,. Huku hakuna tatizo, tume shuka hapa kidogo nata futa sigara ova"
"Sawa hakuna tabu, hakikisha hilo lija mbazi hali kimbii"
"Aaah huyu hawezi kutoka kabisa, tupo nalo hapa"
Baada ya kulidhika na maongezi hayo Alfred alimuamuru nayeye aingie ndani ya gari bila kujua wapi ana kwenda kweli hakuwa na ubishi wowote aliingia kama mwana kondoo.

******************+*******
"Nani ame uwa Alfred?, Alfred Mulawa ndo kamuuwa?, "
"Ndio, mjinga wewe, kamuuwa rafiki yangu, ina kuaje Momba , nataka atiwe ndani mara moja"
"Sasa mimi mbona sina taarifa yoyote ile,"?
"Hufanyi kazi. Wewe ni mzembe, sasa sikia nakupa masaa ishirini na manne Alfredy awe amekamatwa"
Yalikua ni maongezi ya simu usiku huo baina ya Waziri mkuu KASANGA na Fredrick Momba,
Ambayo yaliishia na momba kuhimizwa kumtia ndani Alfred,
Kweli kwa upande wa Fredrick Momba hakuelewa chochote kile, ila baadae anaamini baada ya kupokea taarifa kutoka jeshi la polisi wakiwa wame mshikilia tayari Alfred,

Taarifa hizo zina mshangaza sana Fredrick na kushindwa kuelewa ivyo anapewa kazi moja tu ahakikishe Alfred ana tiwa ndani na si vinginevyo.
Hakuwa na jinsi alitii amri ya Mheshiwa waziri mkuu na kazi kuanza.
******************************
Upande wa pili Alfred tayari aliwa tupa askari wale nje ya gari na yeye kushikilia deffender iyo , na kutoelewa wapi aelekee, alichukua simu na kumtafuta mke wake Haanah. , ili ampe taaarifa
"Hannah mke wangu nisikilize, washa gari sasa hivi , nenda bagamoyo kwa bi, zahra ukakae huko,"
"Alfredy unasema nini?, mbona sikuelewi usiku wote huu mume wangu"
"Hannah sikia kwa makini, ndani ya kabati kuna kibegi changu kile kidogo ndani kuna vitu vyangu, chukua bastola yangu iweke ndani ya begi, chini ya kitanda kuna boxi za risasi ziweke tafadhali fanya haraka lazima watakua wana kuja kwako."
"Alfredy kuna nini?:, mbona unaanitisha baba"
"Ni hivi ki ufupi nime pewa kesi ya kuuua, hapa natafutwa, nikukute bagamoyo sawa, usimwambie mtu yoyote yule sawa Hannnah"?
"Lakin......."
"Lakini nini Hannah fanya niliyokwambia,"
Baada ya Alfred kutoa maagizo yale , wazo moja lili mjia la kumfuata Joyla nyumbani kwake Mbezi beach ili aweze kumwambia ukweli wote aliotaka kujua,
Kweli kwa mwendo wa kasi tayari alifika nyumbani kwa Joyla na kuona gari yake aina ya NOAH ikiwa nje ya nyumba,

Taratibu alitembea na kupitia mlango wa nyuma ambao aliufungua kwa tahadhari na kuingia,
Taratibu aliingia chumba kimoja baada ya kingine kwa kua aliki jua chumba cha Joyla,
alifika na kutega sikio na kusikia maji yakimwagika bafuni kuashiria kuna mtu anaoga, alijua kivyovyote vile atakua ni Hannah sababu ndani humo aliishi mwenyewe, taratibu aliufunga mlango na kuingia chumbani ambapo alikuta nguo za joyla zipo chini na kuamini kweli alikua anaoga bafuni,
Hakuwa na sekunde hata moja ya kupoteza kwa nguvu aliupiga teke mlango ule wa bafuni na kumkuta Joyla akiwa na sabuni huku akiwa hana nguo hata moja na kumfanya ashtuke.
"Alfredy, nini jamani,naoga"
Aliongea Joyla huku akijaribu kuficha sehemu zake za mwili, ila Alfred hakuonesha kujali chochote.

"Nime kuja kufuata ukweli,
Hivi uli fikiri nita kuachia"?
"Alfred, nilishakwambia, embu niache nivae kwanza"
"Sina muda wa kupoteza hapa natafutwa kama OSAMA"
"niache nivae bas"
"Kwani nguo zako zina mdomo, huwez kuongea ukiwa ivyo?"
"Alfredy usini chekeshe"
"Alafu ujue usinipotezee muda wangu, huko nina kesi ya kuua, sasa nita kuua ili nika fungwe kialali"

Alfred alivyoona Joyla ana mpotezea muda alimsogelea na kumvuta mkono ambapo pale pale alimkamata shingo kwa nyuma na kutumbukiza kichwa chake ndani ya shimo la choo cha kukaa ambamo kulikua na maji ya kinyesi, alimkandamiza kwa muda vile vile akiwa mtupu kwa muda wa dakika kadhaa na kumtoa ndani ya maji.
"Aa...alfredy Aa..lfredy una nionea haki amungu,"
Aliongea Joyla huku akihema kwa kukosa pumzi.
"Niambie ukweli. Nitaendelea kufanya hivi mpka uta kapo sema ukweli,Sasa iweje SUNDAY MUNA akutaje?"
"Mi sijui Alfred haki. Ya M...."
Alfred alirudia zoezi lile tena na kumuinua,
Ila Joyla alionyesha msimamo wake,
Alimuingiza tena ndani ya choo kwa muda mrefu mpka alipimuona Joyla ana tapatapa huku akirusha mikono hewani na kusogeza sogeza miguu akitafuta pumzi Alfred alimtoa na kumfanya Joyla akohoe kutokana na maji mengi ya kinyesi aliyo kunywa.
"O..kay okay,nakwambia ukwe...li,.. Alfredy,"
"Nakusikiliza"
"Kuna watu wakubwa serikalini wana husika kwenye kifo cha dada yako"
"Wakina nani nita jie majina"
"Kwa kweli kwa majina siwajui, ila kuna huyu mtu ana itwa Rodgers Mbita, kutoka kwenye kikundi cha NO MITEGO,"
"ndo aliyehusika?"
"Ndio, huyo ndo aliyeni fata na kutaka bastola ya Sunday Muna,ndo nika nika nika mpa Alfred, ndo hayo tu haki A Mungu najua hayo tu"

"Hapana, kuna kitu unani ficha"

Alfred alivuta kichwa cha Joyla na kukiingiza ndani ya chooo kile cha kukaa kama alivyo fanya awali na kumtoa tena.
"Uwwiiii Aalfredy, uta niua, sa.a huyu huyu jamaa, uki taka kumpata mta fute Fredrick Momba, mtafute Momba kweli tena ndo hayo kaka angu,, "

Alfredy alimuangalia kwa muda huku akimkazia macho yaliyo changanyika na hasira kali sana, kweli alikua kama mbogo kwa hasira zili zomfanya mpka jasho limtoke.
"Ila Alfredy nita kusaidia kila kitu,"
"Uta nisaidia kivipi?"
"Kuna namba nili pewa nimtafute mzee mmoja hivi, nahisi kuna mambo alitaka kuniambia,"
"Sasa sikia asubuhi nita kupigia simu,naomba usimwambie mtu yoyote kuwa nili fika"
Alfred alimuacha Joyla akiwa ana shangaa baada ya kutoamini kuwa amepona na kuwa mzima maana alimjua vizuri Alfred,
Alfred alitoa simu yake ya mkononi na kumtafuta mke wake ila aliiikuta haipokelewi alijaribu tena na kupokelewa.
"Haanah ume fika wapi?"
"Bado nipo nyumbani"
"Unasemaje?, uli kua una fanya nini sasa ?"
"Fredy yuko hapa ana kuulizia kaniambia nisiondoke kwanza"
"Nini, ?, ulimwambia chochote kuhusu mimi?"
" Hapana, siku mwambia chochote, na hapa nipo pembeni nime muacha sebuleni siku mwambia kuwa wewe una piga"
"Sikia nikwambie, kama nilivyo kwambia chukua begi langu, toka hapo taratibu, pitia uwani ruka ukuta nita kukuta stendi"
"Alfred, niruke ukuta, siwezi"
"Jita hidi mke wangu, fanya juu chini , najua wata kutumia wewe ili wani kamate, wata kutesa ili nije, sasa fanya niliyokwambia nakupenda sana nikukute stendi pale"
"Sawa Alfredy nakupenda pia"

Alfredy alitoka mbio mbio ila alivyo toka nje alikutana mwana ume wa kiarabu akiwa juu ya piki piki aina ya baja, ambae alionekana akimsubiri mtu, Alfred alimfuata na kumsumiza huku akilipanda baja lile,
Pale pale alivuta mafuta na tairi ya nyuma kuzunguka na piki piki ile kutoka kwa kasi huku liki toa mlio mkubwa sana,
Kitendo cha mwarabu yule kuinua shingo hakuona piki piki alipoelekea na kubaki akikimbia huku akitukana.

Alfred alikimbiza baja ile kwa kasi sana huku akitumia vichochoro huku akiwa hana uhakika kama ange mkuta Hannah stendi,
Kwa mbali alimuona Hannah akiwa na begi dogo na kusimama mbele yake na kufanya Hannah aogope.
"Haanah, panda kwenye piki piki twende fanya upesi"

Bila kipingamizi chochote Hannah alipanda juu ya piki piki na kushika kiuno cha Alfred vizuri na Alfred kutoa kasi ya ajabu.
"Alfred mume wangu, kuna nini nieleze vizuri"
Hannah aliongea kwa sauti kubwa kutokana na upepo uliokua una mpuliza na kelele za baja hilo ivyo ili mfanya apaze sauti ya juu.
"Zackaria Mwita, yule mbunge ame kufa, tena wame muweka ndani ya gari yangu,, wana dai mimi ndo nime muua"
"Mungu wangu, sasa kwanini. Tusikimbie mpka kesi hii itulie"
"Hapana Hannah mke wangu, siwezi kukimbia sababu niki kimbia ukweli hauto fahamika ina nilazimu nirudi ili nijue kila kitu, na kuanika ukweli"
"Mume wangu huoni kuwa ni hatari kubwa"
"Yaah najua sasa sina jinsi tumuombe Mungu , naomba usimpigie simu mtu yoyote yule kumwambia ulipo sawa, nita badili namba, zima simu yako niki taka kuongea nawewe nita tumia namba ya bibi sawa"
"Sawa"

Kufikia hapo ukimnya uli tawala huku Alfred akizidi kuikimbiza baja ile, ambapo safari hii wali kua wana iacha Bunju,
Baadae ali fika Bagamoyo kwa Bibi yake ali yemlea tangu yupo mdogo baada ya wazazi wake kufariki bibi huyo aliitwa Bi, zahara,
Kweli wali fika na Alfredy kumuacha Hannah,
Hakutaka kukuche alicho fanya aliwasha piki na wazo moja tu la kumpigia simu
Fredrick Momba.
"Alfredy, upo wapi?"
", Momba naomba nisa idie kitu"?
"Uko wapi kwanza"?
"Nipo dar hii hii"
"Naomba nikuone"
"Una jua kabisa siwezi kuja, natafutwa mji mzima, Momba sija ua mimi "
"Sasa mbona una kimbia kama huja ua"?
"Una fikiri nani ata nielewa, siwezi kuja , nataka kujua kitu kimoja Rodgers Mbita, nita mpata vipi?"
"Wewe wa nini?"
"Nita kwambia niki mpata"
"Nita fute kesho asubuhi sasa hivi sijui, mpka niwe ofisini"
".poa basi kesho, nita kutafuta, ila Momba, naomba usimwambie mtu yoyote kama nili kupigia simu, hii namba yangu nyingine, nita kupigia kesho"

************************
"Alfredy kani pigia simu jana usiku sasa basi, nitamwambia sehemu tuku tane, mtaenda nyie kimnya kimnya mumkamate, kimnya kimnya, Alfred ni muuaji sasa hivi, ni mtu hatari kwaio kuweni makini ana mafunzo ya kutosha kuliko mtu yoyote humu ndani, ki ufupi ni JASUSI au MAFIA naweza kusema,"

Kili kua ni kikao kidogo ambacho kilifanyika ndani ya ofisi ya Momba akitoa maagizo hayo yaliyo eleweka,
Kweli baadae Alfredy alipiga simu na kumpa maagizo kuwa wakutane Maeneo.ya Manzese tip top,
" nendeni tip top, fanyeni juu chini mumkamate sawa"
"Sawa hakuna tabu,tuta fanya ivyo"

Magari yaliwashwa na safari ya kikundi hiko cha upelelezi kuanza safari ya kwenda kumfuata Alfred na kumtia mikononi ambayo amri hiyo ilitoka kwa waziri mkuu akizidi kumpa vitisho Fredrick Momba.
"Nimevaa kofia nyekundu, na sweta jeusi lime niziba kichwani"
"Poa nakuja"

Maongezi aliyokua anaongea Alfredy na momba yalipita kwa kila mpelelezi ambapo wali sikia kila mazungumzo.
Kweli wali fika maeneo ya Manzese tip top na kazi moja tu kuanza kumtafuta Alfred, kwa mbali walimuona mtu aliye vaa sweta jeusi na kofia na taratibu kuanza kumuendea.


Taratibu walipeana ishara wapelelezi wale kutoka katika jeshi la Momba, walizidi kumsogolea kwa tahadhari mtu huyo .
"Alfredy tulia kimnya ivyo ivyo, turudi kituoni,"

Ila cha ajabu mtu yule alivyogeuka hawakuweza kuamini baada ya kumuona hakua Alfred na kubaki kuangalia angalia.
"Shiiiit. Sio yeye,"
"Duuu,"
wali baki wakishangaa soko hilo la manzese huku wakionekana kumta futa Alfred ambae hakuwa na dalili yoyote ya kuonekana.

Alfred akiwa juu ya daraja la Manzese aliweza kuwasoma kila kitu na kuwaona, kweli alidanganya baada ya kumuona mtu aliye valia mavazi hayo na kujua kivyovyote vile Momba asinge kubali yeye aje, maana alijua akili ya Momba, kwa io aliweza kuona kila mpelelezi, alivaa miwani kubwa na kofia ya duara ambayo ili mfanya mtu yoyote asimjue, aliangalia pembeni na kuona picha yake kubwa ime andikwaa WANTED , maana kuwa ana tafutwa kila sehemu.

"Aise ndio tume mkosa , hatujamuona hakuwa yeye"
"Hata kuwa mbali na hapo, mta futeni, natuma jeshi lingine hawezi kuondoka, bakini hapo hapo"
Kweli msako uliendelea bila dalili yoyote ya Alfred kuonekana na Baada ya jioni kuingia kila mtu aliingia ndani ya gari na kurudi,
"Tulia ivyo ivyo, endesha gari"
sauti iyo ili toka nyuma ya kiti cha mmoja wa wapelelezi bila kuelewa mtu huyo kaingiaje ndani ya gari wakati gari lili kua lime fungwa,
"Aa aaa fredy, Alfredy Brother,"
"Kimnya tulia ivyo ivyo,weka silaha yako juu ya dash bod taratibu, "

Alfred aliongea huku akiwa na bastola ndogo mkononi ambayo aliiweka kisogoni mwa mpelelezi yule na kufanya kichuma cha mdomo kimguse kabisa utosini.

"Vizuri, kwa vidole viwili nipe hiyo silaha taratibu,taratibu kijana"
Alfred alikabidhiwa bastola ile na kuitia ndani ya begi lake dogo.
"Alfred, bora uji salimishe tu kabla mambo haya jawa mabaya, maana una poelekea sio kuzuri"
"Hujui kitu kaa kimnya, nani kawatuma mnikamate?"
"Momba , yeye mwenyewe kapewa amri na waziri mkuu, ndo maana nakwambia usalim amri, hivi uli jua kama tuna kuja?"
"Ndio nili kua najua, naijua akili. Ya Momba nimefanya nae kazi miaka mingi namjua hani sumbui, nipe simu yako"
Alfred alichukua simu na
kuitupa nje kuhofia kua wange weza kuwa fatilia kutokana na simu zote za wapelelezi huwa zina wekewa mtambo wa GPS,

"Weka gari pembeni "
Baada ya kufika maeneo ambayo hakuna hata nyumba moja Alfred alimuamuru mpelelezi yule aweke gari na kumwambia ashuke.
"Zima gari nipe funguo, shuka chini njoo upige magoti,"
""Alfred tafadhali usiniue nakuomba, mimi sina tabu nawewe."
"Shhss kaaa kimnya KIMA WA PORINI wewe"

Mpelelezi yule alipiga magoti kama mwana funzi wa shule ya msingi huku akingalia upande mwingine na kumpa Alfred kisogo.
Alimsihi sana Alfred asimuuwe huku akisali sala ya toba.
Ki ukweli Alfred hakuwa na sababu ya kumuuwa, aliwa sha gari na kuondoka na safari hii moja kwa moja alipanga kuelekea nyumbani kwa Momba mikocheni B.
****************************
"Mama Cindy hivi uli funga mlango, maana kuna kitu nime sikia"

Ili kua ni sauti ya Momba akiwa chumbani na mke wake, baada ya kuwa na wasi wasi na kuonekana kama kusikia kitu kisicho cha kawaida,

Alishuka kitandani na bastola yake ndogo huku aki muacha mke wake kitandani, ali toka mpka sebleni na kote mpka jikoni ila hakuona kitu, ila alivyo geuza shingo alihisi kitu kama chuma kime mgusa shingoni.
"Momba tulia ivyo ivyo, weka iyo bastola chini upesi"
"Aaaaalfred"
"Weka bastola yako chini"
Momba taratibu aliji kuta akiweka bastola juu ya malu malu na kumuangalia Alfred ambapo alimuona anavua miwani aliyo vaa.
"Ipige teke ije kwangu"
Kweli jambo lile lilifanyika na Alfred kuichukua bastola ile
"Una taka nini?"
"Rodgers Mbita yuko wapi?"
Momba alimwangalia Alfred kwa kitambo na kuangalia nyuma yake,
Alfred nayeye aliya fata macho ya Momba na kugeuza shingo ambapo pale pale Momba alimrukia na kuipiga bastola ile teke na idondoke chini,
Alfred alikaa sawa na kukunja ngumi, ali mtisha na ngumi ya kushoto kama wanavyo fanya wapiganaji wa bondia ila baada ya Momba kutingishika alirusha ya kulia na kumpata vizuri puani, ambapo pale pale alimvaa na kumpiga kichwa cha mdomo na kumkaba koo.

"Momba usinijaribu , nitakuua nakwambia nita kuuaaa sasa hivi, usha nielewa, ?, niambie Rodgers alipo?"

Alfred aliongea huku mikono yake akiwa ame viringisha juu ya shingo ya Momba na kumfanya atulie kama kuku wa pasaka aliye taka kuchinjwa

" Alfred kwa nini umemuua Zackaria Mwita?"
"Hapana mimi sija muuwa, ngoja nikwambie, pale ofisini kuna Camera za nje na uhakika una recording zake angalia mwenyewe"

Alfred alichukua bastola yake na kumuelekezea Momba huku akiongoza moja kwa moja kwenye lap top yake na kuifungua, kweli alianza kuangalia kila kitu na kuona mpaka maiti ile inavyo ingizwa ndani ya gari la Alfred.
"Una weza kuzooom hii sura, huyu hapa, nisha wahi kumuona sehemu , wapi nili muona.. hii sura sio ngeni"
Alfred aliongea huku akiaaangalia picha ile kwa uma kini sana akiirudia mara mbili mbili akijaribu kuvuta kumbu kumbu.

" Yaaah nisha ikumbuka hii sura, huyu jamaa nili sha wahi kumuona na Joyla Godfrey,. Nakumbuka sana walikuja wote kwangu,"
"Una uhakika Alfred?:,
"yaah nina uhakika tena sana,"
"Okay Alfred, Rodgers Mbita sasa hivi yupo Zanzibar sehemu moja ina itwa MICHENZANI , uki ulizia No mitego tu uta pelekwa na kumpata"
Momba alitoa maelezo yale baada ya kuona kweli Alfred hana hatia,
"Ngo ngo ngo"
Ulikua ni mlio wa mlango uki gongwa na kufanya kila mtu asitishe ana cho fanya na wote kukaa kimnya.

"Nani huyu usiku ?"
Momba ali uliza.
"Mimi sadiki"
, sadiki ali kua ni mlinzi wa getini ivyo Momba hakua na wasi wasi alitembea na kuufungua mlango huku aki muacha Alfred mezani,
Ila baadae Alfred ana sikia milio ya risasi na kumuona Fredrick Momba aki dondoka na Mlinzi yule pia kupigwa risasi, Alfred kuona vile aliruka mbio na kuchomoa flash iliyo kua kwenye lap top na, kuingia mlango mwingine na kukimbia na kuruka ukuta.
Akili yake ili mtuma kitu kimoja tu kumrudia Joyla,
Aliingia ndani ya gari na kwenda mpka kwa Joyla,.
Na kumkuta akiwa mezani ana kula.
"Joyla"?
"Yes Alfred, kuna tatizo?"
" kuna mtu nataka unisaidie kumpata na una mjua sana, nipe lap top yako"
Lap top ili letwa na Alfred kuingiza flash na ile picha kuonekana.
"Ya namjua anaitwa Kalulu, namfahamu ni shemeji yangu, ila ni hatari sana, ni jambazi"
"Sasa ni tampata wapi?"
"Ina bidi twende wote niku saidie."
Alfred alimwangalia Joyla kwa umakini machoni kwa muda na kumkabidhi bastola ndogo.
"Fanya upesi twende tusipoteze muda"

Baada ya maongezi hayo Alfred alimpa kisogo Joyla na kuuendea mlango, ila Joyla anamuwekea bastola Alfred na kumuamuru Aweke silaha yake chini.,
"Alfred. Ulipata nafasi ya kuniua ila ulishindwa, sasa ndo hutopata tena, Yaani nili kua naita futa nafasi hii kwa kipindi kirefu, MBWA wewe,"

Alfred alimtazama Joyla na taratibu kuweka bastola chini na kuiweka mikono yake kichwani huku akimwangalia na kutokua na kitu cha kufanya.
"Tuchi tuchi tuchi"

Ulikua ni mlio wa bastola ambayo ili taka kufya tuliwa na kutoa mlio ule kuashiria hakuna risasi ndani ya bastola,
Joyla alibaki akitoa macho huku akipigwa na butwaa na kutokuamini kitendo kile, hasa alipo muona Alfredy ana tabasamu mbele yake.
"Joyla, siku zote bunduki haziui watu, ila risasi ndo zina ua"
Alfred aliisimama na kutoa risasi mfukoni kwake,na kumuonesha Joyla.,
"Hahahahaha, mi sio mpumbavu nikupe silaha yenye risasi, nili jua tu akili yako ya kipumbavu wewe MWANAMKE, ,"
Alfred alichukua bastola na kumuwekea Joyla usawa wa kichwa.
"Paaaaa paaaaa paaaaaa"


ulikua ni mlio wa bastola ambapo risasi tatu zili penya kati kati ya kifua cha Joyla na baadhi ya damu kumrukia Alfred ambaye wakati huo alikua amesimama akimshuhudia Joyla akidondoka taratibu huku akiwa amejishika kifuani akitokwa na damu nyingi sana,

"Aaaa...aafredy"

Joyla aliweweseka akiita jina la Alfred huku akijiburuza akitumia tumbo na kumuendea alipo simama Alfred na kumshika suruali yake ambapo akionekana akitaka apewe msaada wa huduma ya kwanza.

"Paaaaaaaaaa"
 *******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG