Search This Blog

Monday, March 23, 2020

THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 4/10


THE PAINFULL SECRET
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
 SEHEMU YA 4 KATI YA 10


Mpka kuna kucha Alfred alizidi kumsaka Mujuni na kuingia katikati ya kipori kidogo,
Ali mrukia Mujuni na wote kudondoka chini,
Aliinuka haraka haraka na kumpiga ngumi puani, hakuchelewa ali mfuata na kumpiga teke aina ya round kick lili mfanya Mujuni ayumbe kidogo,

kutokana na mkono wa Mujuni una kidonda ivyo alishindwa kujibu masha mbulizi na kukuta ana zidiwa na Alfred,.
Alfred aliushika mkono wake ule ule uliokua na jeraha la risasi na kutumbukiza kidole ndani ya shimo lile lililopenya risasi na kufanya Mujuni atoe ukelele wa maumivu, ali msukumiza Alfred na kumrukia teke,, lili mfanya Alfred adondoke chini, Mujuni alikuja juu yake na kumshushia ngumi, ila alivyoona kuna watu wana kuja alimuacha na kukimbia ila Alfred ana muwahi na kumshika mguu kutumia mguu mwingine Alfred ana jikuta ana pigwa na kumuona akikimbia na kupotelea mitini.
Alikuja Amney na kumuinua ambae tayari ali fika na jeshi lake na kumkuta Alfred yupo chini aliinuka na kutaka kumfuata Mujuni alipo kimbilia.
"No Alfred, una enda wapi?"
"Maswali gani una niuliza Amney,. Naenda kumta futa yule mwana haramu"
"Tuta mpata liachie jeshi, nime pigiwa simu kutoka hospitali,"
"Hannah, mzima?"
"Mi sijui kwa kweli, yupo na Rose"

Habari ya kumta futa Mujuni iliishia pale pale na safari ya kwenda hospitali kuanza,.
Akiwa na mawazo mengi sana, ali fika tayari hospitali na kuelekezwa aonane na daktari atakae mpa taarifa za Hannah,
Ali fika ofisi ya daktari na kukaa kwenye kiti, daktari alifika nayeye kukaa pia vile vile na kuonekana akitoa kara tasi na kuanza kuzisoma.
"Mr , Alfred Hanna ni mkeo"?
"Ndio, ni mke wangu, kuna nini daktari, niweke wazi".

Daktari yule alimwangalia kwa kitambo kidogo bila kusema kitu na kufanya mapigo ya moyo ya Alfred kuzidi kwenda mbio huku akimkazia daktari macho., huku akianza kunyong'onyea kama aliye mwagiwa maji ya moto.

" mkeo ana hali mbaya sana, alivyo dondoka chini, alidondokea mguu wa kushoto, ambao una uvimbe na kuufanya mguu wake uvimbe kutokana na mishipa ya damu aina ya VEINS kushindwa kupeleka damu, pia kichwani nyuma katika mishipa ya ubongo ime pata majeraha,"
"Kuna uwezekano wa yeye kupona"?
"Uwezekano upo, ila itakubidi wewe utoe maamuzi kama mwana ume, Hannah ana ujauzito wa miezi mitatu pale alipo"
"Maamuzi gani daktari?"
"Hapa kuna mambo matatu, ina kubidi ucha gue moja, mguu wake ukatwe!..,mtoto afe au Mkeo afe"

Alfred alihisi ganzi mwili mzima baada ya kusikia maneno yale kutoka kwa daktari yule,
"Fanya,maamuzi ya haraka, la sivyo vyote uta kosa"
Alfred aliji kuta ana pigwa na bumbuwazi na kushindwa kuongea kitu chochote kwa wakati ule na kubaki akimwangalia daktari.



Alipitisha mkono wake usoni kana kwamba ana futa jasho na kushusha pumzi ndefu na nzito huku akiangalia chini,
kipindi hiko daktari alibaki kumwangalia akisubiri jibu lake.

"Hakuna uwezekano wowote ule kuachia na hayo uliyoniambia"?
" kwa kweli hapana, yaani hayo niliyo kwambia moja wapo lazima lifanyike kivyovyote vile"
Taswira ya picha ya mke wake akiwa ana tembea na gongo huku akiwa na mguu mmoja vili jijenga kichwani huku akimuona anavyo teseka kutembea, pia vile vile alimuona Hannah akilia baada ya kuamuambia kuwa mtoto alikufa, huku picha ya jeneza ya sura ya Hannah akizikwa ili jijenga kichwani,
Kila chaguo aliliona gumu kwake,
"Mungu naomba nisamehe, daktari mtoe tu mtoto mke wangu apone "
"Una uhakika?"
"Kama ulivyo nisikia kwani vipi?'
"Hakuna tatizo, karatasi hizi hapa ita kubidi upitishe sahihi hapa chini"

Alfred alichukua kalamu kutia sahini kukubaliana na lita kalo tokea,
mambo mengine ali muachia Mungu maana ndo kila kitu kwa wakati huo. Daktari yule ali simama na kuchukua vifaa vifaa na kutoka nje huku akimuacha Alfred aki msindikiza kwa macho,

Waziri mkuu JOSEPH PARTSON KASANGA., tayari alikua kashafika uwanja wa ndege mwl, Nyerere baada ya kuona mambo yameenda kombo, ivyo anaa mua kukimbia na kurudi Tanzania huku nyuma akimuacha Mujuni Afrika kusini, ambapo alifika na madawa ya kulevya ndani ya begi lake,.

Kwa kuwa zili baki siku chache raisi wa dunia Barack Obama aingie ndani ya nchi iyo ivyo ana tumia fursa hiyo kuzuga kuwa alikua kwenye mkutano,
kweli uwongo wake uliweza kutia nanga na wote kuku baliana nae,
Baadae ana muomba Fredrick Momba, mkuu wa wapelelezi kuwa aimarishe ulinzi kila sehemu kutokana na ujio huo wa raisi, ila jibu lili toka kwa Fredrick lina mchanganya baada ya kusikia kuna jeshi lake dogo lipo Africa Kusini kufuatilia mtandao wa madawa ya kulevya
Kitendo hiko kina mshtua kidogo sababu katika mtandao huo kivyovyote vile nayeye ange husika na muda mfupi siri inge julikana.

Chini kwa chini Amney ali fuatilia nyenzo za Mujuni akiwa peke yake siku iyo , ali mfuatilia akiwa nyuma yake na gari ndogo ambayo aliiwekea kifaa kidogo kitakachoweza kumnasa kila anapokwenda Mujuni,
kwa kutumia IPAD yake aliweza kuuona mwenendo wa gari lile la Mujuni lina pokwenda ambamo lili simama maeneo ya bandari,
Alitoa simu na Kumtafuta Alfred na kukuta hapa tikani, aliandika ujumbe mfupi wa maneno ambao akiiwasha simu yake angeweza kujua alipo, aliiweka simu yake mfukoni na kuteremka ndani ya gari.
Baada ya kuka gua bastola yake vizuri na kuha kikisha ina risasi za kutosha aliweka MAGAZINE ndani ya bastola na kuiweka bastola ile kwa nyuma kiunoni huku akiiifunika na tshirt alilo vaa,
Alitembea upandae upande pembeni ya makontena, alioona koti kubwa zikiwa kama sare za watu wa bandari na yeye na kujichanganya na wafanyakazi wa bandari, alitembea bila wasi wasi huku akimuangalia Mujuni kwa umakini ili asiweze kumpotea,
Alimuona Mujuni anaenda upande wenye geti nayeye kuingia safari hii alishika bastola mkononi tayari
kwa kujihami maana ndani humo kulikua na ukimya wa hali ya juu
,. Alinyonga kitasa cha geti na taratibu kuingia huku akiwa ame tanguliza bastola mbele ila alishangaa ina dondoka baada ya kupigwa teke na Mujuni aliye kua nyuma ya geti lile kuashiria kwamba alijua ujio wa Amney,
Amney alikaa sawa na kuhepa ngumi iliyo kua ina kuja kutoka kwa Mujuni,
Pale pale aliruka teke lililompata Mujuni kifuani na kumfanya ayumbe alimfata na kumpiga kifuti tumboni, aliona teke lina kuja na kuinama chini hapo ndipo alimpiga ngumi sehemu za siri za Mujuni ambayo ili muingia na Mujuni kuinama kidogo,
Amney alivyoona kitendo kile , alirusha teke lingine ambalo lili mpata mdomoni vizuri,

Alivyo taka kuinuka alimpiga ngwala lili fanya Mujuni adondoke juu ya maboxi,
Ambapo aliokota chuma kama mithili ya nondo,

Amney aliiona nondo ile ina kuja na kuinama na kupita juu yake,
ila baadae ina mpata ya mbavu na kumfanya ajipinde maana ili mwingia vizuri,
Mujuni ali mfata na ku mshika nywele zake ambapo alimbamiza kwenye geti hilo la chuma, ali mfata tena na kuanza kumshambulia mateke ya tumbo aliivyoona Amney kaishiwa nguvu ali mbeba na kumshika shingoni huku aki mkandamiza ukutani kwa nguvu, na kufanya Amney atingishe tingishe akiishiwa pumzi, aliji tahidi kutoa mikono ya Mujuni shingoni mwake ila alishindwa kutokana na uhaba wa pumzi alijikuta pumzi kwa mbali inaanza kuisha huku Mujuni akiendelea kumkaba kooni, ila alimuachia baada ya kuhisi kapigwa na nondo begani,
Aligeuza kichwa na kuku tana na ngumi ili yompiga puani,.
Alikua ni Alfred tayari kafika baada ya kufungua simu na kukuta ujumbe ule aliotumiwa na Amney,.
Alirusha ngumi zisizo kua na idadi tena za hasira na zote zili zaa matunda sababu zili kua zina mpata Mujuni sawa sawa.

Alirusha teke la nguvu lili mpata Mujuni kifuani na kumfanya adondoke chini Alfred ali mfata na kumuinua akizidi kumsha mbulia ngumi za pua na mdomo na kufanya Damu zianze kutoka katika pua za Mujuni, hakuishia hapo aliendelea na masha mbulizi, huku akimuangalia Amney ambae wakati huo alikua ame poteza fahamu, kutokana na kupoteza pumzi kwa kipindi kirefu,
Aliendelea kumshushia kipondo na sasa hivi jeshi la polisi lili kua tayari lime fika huku wakimzuia Alfred asiendelee na fujo huku waki toa pingu na kumfunga kwa nyuma kwa kosa la kupigana na kufanya fujo eneo hilo la bandari...


"Nifungueni pingu zenu, nyie watu vipi?, nifungueni hizi pingu...nasema nifungueni pingu zenu"
Alifoka Alfred huku akitumia nguvu kujitoa kwa maaskari wale, ambao wali kua wana muingiza ndani ya gari kinguvu,
kwa mbali aliweza kumuona Amney pia kafungwa pingu kwa nyuma nayeye alikua ana zozana na maaskari ambao hawa kutaka kumsikiliza
"Nyie mna nijua mimi vizuri, nauliza nyie mna nijua mimi, naomba niongee na mkuu wenu"
Alifoka Amney ila hakuna hata mmoja aliye msikiliza,
Alikandamizwa ndani ya gari na magari ya polisi yakianza kutembea,
Huku wote Amney na Alfred wakiwa wame fungwa pingu kwa nyuma na kuwekwa chini ya ulinzi na safari ya kwenda kituoni kuanza., hali hiyo ina washangaza wote wawili..
Baada ya dakika ishirini magari ya polisi yali egeshwa nje ya kituo kidogo cha polisi na Alfred akiwa wa kwanza kushushwa huku akifuatiwa na Amney,
"Vua mkanda,na viatu weka kila kitu hapo mezani, fanya upesi, usini tumbulie mimacho mimi"
Aliongea Afande huyo kwa kejeli na Alfred kutii bila kufanya chochote,
Kila kitu alichoambiwa alitii na kuingizwa maabusu ambamo alikutana na waalifu wengine., chumba hiko kidogo sana chenye dirisha na chini kukiwa na uchafu ulichanganyika na vinyesi uli fanya hewa nzito itoke na kufanya Alfred apate shida.
Kesho yake asubuhi ili fika na kumfungulia waki mruhusu aende na kutoka nje ambapo ali kutana na Amney,

"Pole sana Amney, ..hawa wapuuzi ime kuaje ume kubali wakulaze"?
"We acha tu, siku taka kuwaambia mimi ni nani., . Tuondoke eneo hili upesi,."
"Ina bidi twende hospitali, nataka kujua hali ya mke wangu ina endeleaje,. Mujuni wame muachia nina apia nita muuwa kwaa mikono yangu, nita mtafuta"
Wali tafuta Taxi ambayo ili wapeleka mpka maeneo ya hospitali, baada ya kumlipa dereva taxi waliingia na kukutana Rose,
Alimuendea na daktar ambapo aliambiwa kuwa wali sha mfanyia upasuaji hivyo asubiri kidogo maana hali yake sio nzuri sana.
Masaa, siku , majuma yali pita huku hali ya Hannah ikiendelea kuwa nzuri siku baada ya siku na leo hii aki ruhusiwa kutoka hospitali,
Ana sikitishwa sana kupewa habari kuwa mimba yake ilitolewa,.ila mume wake Alfred ana mfariji na kumpa kuwa Mungu yupo na wata pata mtoto mwingine.
**********************
Waziri mkuu JOSEPH PARTSON KASANGA ana jikuta ana kosa raha kabisa
[13:56, 1/8/2015] RoDer..: Baada ya kugundua kuwa anaenda kugundulika muda mchache baadae hasa alipo sikia jeshi la Fredrick Momba lipo Afrika kusini katika msako wa wauza madawa haramu ya kulevya,.
Akiwa ndani ya ofisi yake kubwa alichukua mkonge wa simu ya mezani na kuweka sikioni huku akibonyeza bonyeza namba juu ya simu hiyo baada kusikia ina ita aliweka tai sawa na kuguna kidogo na kuvuta pumzi.

"Fredrick Momba, una ongea na Waziri mkuu"

"Oooh, Muheshimiwa waziri, habari za kazi,"?

"Salama, salama, vipi majukumu lakini, ?, .yanaenda vizuri"?

"Yanaenda muheshimiwa"
" wale vijana wako walioenda Afrika kusinii, vipi washa rudi,..?, kwa sababu nataka niwe mstari wa mbele kukuunga mkono katika hili swala, una jua nchi yetu hii madawa ya kulevya yame kithiri sana."
"Nita shukuru sana muheshimiwa Waziri mkuu, hapa nilikua na wazo niku pigie simu, sema tu ume niwahi"
"Sasa Fredy ukikwama sehemu yoyote ile niambie, ila usiache kuni julisha kinachoendelea"
"Usijali mheshimiwa asante sana"

Maongezi hayo ya simu yaliishia hapo , baada ya kuridhishwa na taarifa zile ambazo kidogo zili mfariji lakini sio sana kwa Waziri huyo mkuu ambae muda mfupi tu aliingia madarakani,
************************
Alfred ana fanya mipango ya kumrudisha mke wake pamoja na Roseline nchini Tanzania ambapo angetegemea wange kua salama ili yeye na Amney wabaki nyuma wakiendelea na zoezi hilo, japo Alfred nayeye alitaka kurudi ila Amney ana msihi sana wabaki na kumsaka Mujuni.

Kweli leo hii Alfred aliwaaga Hannah na Rose huku akiwaambia kuwa wafikie kwa Martin Phares wakae mpka ata kapo rudi,
waliagana uwanja wa ndege walivyo hakikisha kila kitu kipo sawa waliingia ndani ya vyumba vya abiria huku Alfred akibaki kuwa sindikiza kwa macho.

"Partson, mambo yasha haribika,.. nasema hivi mambo yasha haribika,. Mimi sina pa kwenda,"
"Una maana gani Mujuni,?, wewe tulia, usihofu , ondoa shaka, kila kitu kitaenda sawa"
"Hakuna cha kila kitu kitaenda sawa, wewe una madaraka yatumie, alafu ngoja nikwambie kitu, haya mambo yana kuja kuku rudia wewe, nadhani una jua namaanisha nini"
"Mujuni eeeh, usiwe kama mtoto wa kike, mimi nime kwambia usiogope,"
"Sikia nikwambie,.mimi siwezi kwenda popote pale,,Nata futwa kila sehemu,."
"Mujuni, nita kutafuta, subiri simu yangu, mpka niku pigie, ngoja niweke mambo sawa"

Yalikua ni maongezi baina ya Waziri mkuu wa Tanzania na Mujuni kupitia simu,
Baada ya kukata simu Mujuni ana washa gari na kuondoka , bila kujua gari yake ili wekewa kifaa ambacho kinaitwa TRUCKING DEVICE kipindi cha nyuma na Amney, ambacho kina weza kumuonesha mtu ana poelekea,
Taratibu taratibu Alfred na Amney wakiwa na wao nyuma walizidi kumfatilia, ambapo alifika sehemu ya kuegesha gari nje ya hotel hiyo na kuingia ndani ya hoteli hiyo huku akiangalia angalia nyuma.
Na wao wali shuka na kuingia mpaka mapokezi na kuku tana na msichana wa mapokezi ambae alikua anaongea na simu ya mezani ali waomba wampe dakika chache baada ya kutoa ishara ya mkono.
"Dada, tuna muulizia huyu mtu, yupo chumba namba ngapi?"
Aliongea Amney huku akionyesha picha ndogo ya Mujuni.
"Kwani mna miadi nae au?"
"Hapana yupo chumba namba ngapi?"
"Siwezi kuwatajia mpka mnitajie majina yenu na nimtaarifu, ndo utaratibu wa hapa"
Dada yule aliongea huku akishika mkonge wa simu ila Alfred ali muwahi na kumshika mkono wake ule ulioshika simu,aki mzuia asifanye zoezi lile.
"Kaka niachie, nita waitia polisi"
Ili bidi Amney atoe kitambulisho na kumpa kitisho,
haraka haraka dada yule alitaja na Alfred kuanza kupandisha ngazi,
Huku Amney akipandisha na dada yule wa mapokezi kwenye chumba alichotajiwa kua Mujuni yupo,
Amney alivyomuona Alfred ana taka kugonga mlango alimpa ishara kua asi fanye ivyo kwani ange haribu kila kitu, alichofanya ali mtanguliza dada wa mapokezi na kumwambia agonge mlango,
Dada yule aligonga bila kuji biwa na mtu yoyote ila baadae ana gonga tena na sauti ika sikika ikitokea ndani ya chumba hiko.
"Ni mimi dada yule wa mapokezi"
"Una shida gani?"
"Kuu....kuna ..kuuna risiti nime kuletea"
"Nita ipitia kesho"
"Kesho sito kuepo"
Alijibu dada yule wa mapokezi na kufanya ukimnya kidogo utawale ndani kwa muda,.
Ila kitasa kina sikika kiki funguliwa na mlango kufunguka, .
Pale pale bila kuongea chochote Alfred alimvaa Mujuni na kuingia nae ndani huku akimpiga ngumi za tumbo na kumfanya Mujuni ayumbe,
aliiona chupa pembeni ya pombe aina ya whisky na kumpiga nayo Mujuni ya kichwa na kumpasukia kichwani,
hakukaa sawa Amney nayeye ali mrukia teke na kumfanya Mujuni adondoke chini.
"Huu ndo mwisho wako"
Ali ongea Alfred na kumnyanyua huku aki mpiga vichwa puani na kurusha ngumi ambayo Mujuni aliidaka na kumsukumiza Alfred,
Mtanange uliendelea ngumi zile waki mchangia Mujuni ambae wakati huo alionekana kuzidiwa
Sasa hivi akiwa amevirigishiwa miguu shingoni ambayo ili jifunga na kumfanya Mujuni atulie kama kuku anaetaka kuchinjwa,
"Alfreeed"
Amney aliita na kumfanya Alfred ageuke ambamo aliona Amney ana rusha kisu na nayeye kuki daka bila kuchelewa alikidumbukiza kifuani mwa Mujuni na kufanya apige ukelele wa maumivu.
"......m.mi.. ni k..ama. kif.aa..kidogo nda..ni ya i..njini kubwa.A.lfred, hata ukiniua una fanya kazi bu..re.,"
Maneno hayo aliya toa Mujuni huku akiwa ana vuja damu nyingi.
"Huuu ndo mwisho wako, ,Mujuni,. "
.aliongea Alfred na kukizungusha kisu kile alichomoa na kuki chomeka kwa hasira,.,
baadae alimchoma shingoni na kumbeba, alienda dirishani na kumtupa nje ya gorofa hilo la hotel ambalo lili kua na urefu mkubwa , na kumshudia akidondoka chini na kupasuka kichwa,
Alimfata Amney na kumkombatia.
Huku waki pongezana kwa kazi nzito walio ifanya.
Jeshi la polisi walilotumwa na Fredrick Momba lina fika na kumkuta Alfred kasha maliza kazi, na wote kubaki kumshangaa,

Baada ya siku chache anaagana na Amney na yeye kurejea nchini Tanzania akiwa na amani sana ,
Aliiikumbuka sana familia yake akiwa ndani ya ndege.
"Broo Alfred, hongera sana, yaani siku tegemea"
"Asante sana dogo pia nawa shukuru kwa kuja,"

Wakiwa ndani ya ndege wakirejea Tanzania Alfred alipewa pongezi na wenzake,
Ki ukweli akili yake haikuwa hapo bali ilikua kwa mke wake Hanna ambae muda mfupi angeenda kumuona,

Baada ya masaa machache tayari walifika uwanja wa ndege mwalimu Nyerere ambapo wali pokelewa na watu wengi,.

Ila Alfred hakuonyesha kuwajali baada ya kumuona mke wake Hannah kwa mbali alipiga piga watu vikumbo na kumkombatia mke wake, ambae wakati huo alionekana kulia kwa furaha.
"Usilie Hannah nime rudi mke wangu"
"Siamini Alfred Mume wangu, Sikuweza kulala kwa raha,. Mungu mkubwa,",
"Amini nime rudi , Mujuni kasha kufa, .Rose yuko wapi?"
"Yupo kwenye gari na Martin, leo tunaenda nyumbani Alfredy, nakupenda mume wangu "

Hannah alichukua begi la Alfred huku wakiongozana mpka yalipo maegesho ya magari na kuingia ndani ya gari waki salimina na Rose pamoja na Martini Phares na safari ya kwenda kimara kuanza,
Alfred alimuangalia mke wake na kuanza kumpiga mabusu ya mdomoni bila aibu yoyote ile na kutamani afike haraka nyumbani ili atimize wajibu kama mume,.
Kweli kutokana na msongamano haukuwa sana, hawa kuchukua muda mwingi walikua tayari wame fika Nyumbani kwake kimara na Martin akiwaaga na kuondoka,
Ili kua furaha sana kwa watu hao siku iyo
, Alfred aliingia kuoga na kutoka na wote kujumuika kula chakula cha usiku mezani wakiwa na furaha sana,
Baadae Alfred aliingia chumbani na mke wake Hannah na kuanza kupeana mabusu kwa fujo zote maana kila mtu alikua na hamu na mwenzake, mwishowe wali fanya tendo la ndoa baada ya kuridhika wote wali choka na kulala,.
Wote wali jikuta wana shtuka baada ya kusikia mlio wa risasi ulisikika karibu kabisa na masikio yao,
"Nini hiko Alfredy?,"
"Nisubiri hapa Hannah nakuja"
"Alfredy nakuja"
"Nooo nisubiri nime sema usitoke, na ufunge mlango kwa ndani"

Alfred alitoka kimnya kimnya huku akinyata ,
Alifungua mlango wa sebuleni,
Hakuamini alichokiona mbele yake ali muona Rose akiwa ameshika maeneo ya tumbo huku damu nyingi zikiwa zime tapakaa chini na kumfanya Rose atape tape kwa maumivu makali ambayo alizidi kuya sikia., huku akipiga kelele za msaada, ili kua ni picha nyingine mbaya mbele ya macho ya Alfred
"Rose, Rose"
Alfred aliiita huku akimsogelea na kumkombatia pale pale akiwa chini.


Akiwa chini ana mtingisha tingisha dada yake Rose aliona simu pembeni ambayo kwa wakati huo ilikua hewani aliichukua na kuiweka sikioni.

"Hallloo halloo"

Ila simu ile ili katwa bila kujibiwa chochote.
Aligeuka nyuma na kumuona mke wake Hannah akiwa ameweka mikono kichwani akiwa amepigwa na bumbuazi,
Haraka haraka walisaidiana kumbeba Rose ambae wakati huo akiwa ana weweseka akita futa pumzi kwa shida huku aki tokwa na damu nyingi mdomoni,
Alfred alichukua kitambaa haraka haraka na kukandamiza tumboni ili kuzuia damu isiendelee kutoka huku akisaidia na Hanna kumuingiza ndani ya gari,
haraka haraka aliingia ndani ya gari na kutoa gari nje kama mwenda wezamu na kuji kuta ana gonga geti na kupasua taa ya mbele ya gari,
hakujali alicho jali mbele yake ni kuokoa maisha dada yake Roseline na si vinginevyo, kwa kuwa usiku ulikua mnene njia nzima ili kua nyeupe hii haikumpa shida,
Ndani ya dakika ishirini alikua tayari kafika hospitali na kutoka nje haraka haraka, alikua ni kama mtu aliye changanyikiwa , kwa haraka alizo kua nazo hata viatu hakuvaa pia vile vile hata vifungo vya shati hakufunga na kubaki kifua wazi.

"Naombeni muokoe maisha ya Dada yangu tafadhali,."
"Ime kuaje?"
"Risasi risasi"
"Tuna hitaji kibali maalumu kutoka polisi"
"Shenzi nini wewe , una nijua mimi wewe, mpuuzi mkubwa, huwezi kumtibu mpka kibali,?,, mshenzi wewe , mjinga , mjinga sana wewe"

Alfred alifoka kwa sauti kubwa ambayo ili.mfanya mpka Hana abaki akimwangalia na kutamani kumwambia anyamaze ila anaogopa kutokana na kujua mume wake ni mkorofi sana na akiwa na hasira huwa hakuna mtu wa kutuliza hasira zake,
docta yule alifanya haraka haraka na machela kuanza kusukumizwa mbio mbio huku Rose akiwa ametundikiwa dripu.
Kitanda kile kiiliingizwa thieta chumba maalumu cha upasuaji ambacho mtu yoyote haru husiwi kuingiwa isipo kua madaktari,.

Chumba kili kua tulivu sana huku madaktari bingwa waki jaribu kuya nusuru maisha ya Rose.
Akiwa nje Alfred alibaki amekaa juu ya benchi huku shati lake jeupe likiwa lime lowa damu nyingi ambazo zilizo tokana na Kumshika Rose,
Pembeni akiwa na Mke wake Hannah ambae alionekana kumfariji kipindi hiko na kumpa moyo, huku akimuomba Mungu,

Ghafla Alfred ana jikuta akisimama kama mtu aliye shtuka kwenye njonzi ndefu hii ni kutokana na kuwaona madaktari na nesi mmoja wakitoka ndani ya chumba aliichoingizwa Rose muda mfupi kwa ajili ya upasuaji,
Alipiga hatua ndefu na kumshika docto mkono

"Daktari vipi hali ya dada yangu?, anaendeeleje"?

Daktari alimuangalia kwa kitambo sana Alfred machoni na kumuangalia Hanaah pia machoni ambae kwa wakati huo kila mtu aliganda kwa butwaa ambalo lililosababishwa na daktar huyo kuwa shangaa. Daktari alitingisha kichwa akisikitika kwa huruma.

" bahati mbaya hatu kuweza kuokoa maisha yake, ame fariki dunia, pole sana"

Jibu lile kutoka kwa daktari lilimfanya Alfred atoe macho na kuangaza pembeni ambamo aliona chumba kile cha upasuaji ambacho wakati huo kili kua na uwazi kidogo, aliweza kushuhudia Rose ana funikwa na shuka la kijani,
moja kwa moja alienda na kusukuma mlango
"Rose,....R..ose dada a..ngu, ume niacha mweny..we amka dada yangu, amka tafadha...li.aa aa aam..ka,..sama..hani Rose, eeh Mungu"

Alfred alijikuta ana lia kama mtoto na kufanya nesi aliye kua pale aanze kudondosha chozi..
"Ro ro ...se.. Dada yangu k..ipenzi tume zaliwa ..wa.wili. tu ona sasa , doctor kwanini hukuokoa maisha ya dada yngu uli muacha afe niamb..ie"

Alfred alizidi kuongea kwa uchungu huku akizidi kumtingisha Rose juu ya kitanda kile ambae wakati ule wala hakusikia kitu chochote kile, , hakuwahi kusikia uchungu kama siku hiyo.
"Tunge okoa maisha yake, sema tulishindwa kutokana na yeye alikua akipasuliwa mara kwa mara katika tumbo lake, tumbo lili kua lime legea kabisa"

Alfred aliinuka na kumkata daktari yule jicho kali ambalo lili mpelekea daktari yule kukaa kimnya, alivyoangalia pembeni aliona kibakuli kidogo ambacho ndani yake kili kua na risasi mbili moja kwa moja alijua ndio hio iliyo tumiaka kumuuwa dada yake.

"Hii ndo risasi ili tumika si ndio"?
Aliuliza Alfred huku akifuta machozi
"Ndio ndo hiyo"
"Nita mpata tu huyu mtu"

Baada ya kuku baliana na matokeo kuwa dada yake tayari ame fariki dunia ivyo ana jikuta ana ingiwa na kazi nyingine ni nani aliye husika na kwanini alifanya ivyo.

Taratibu za msiba zili fanyika Alfred akiwa katika pigo jingine kubwa katika maisha yake, kweli kila kitu kilienda sawa na Rose kuzikwa pembeni ya makaburi ya wazazi wake,
Akishirikiana na mkuu wake Fredrick Momba ambae muda wote alikua nae bega kwa bega,
Baadae Alfred ana rudishwa kazini na kimnya kimnya kuanza kufa tilia risasi iliyo pelekea kifo cha dada yake.

Usiku wa siku iyo akiwa na lap top yake alibonyeza bonyeza namba fulani juu ya kibodi na kuitazama risasi ile huku akiingiza namba ambazo zilizo kuwemo juu ya kasha hilo la risasi
Aliingalia vizuri kwa makini sana jina lililojileta juu ya kioo cha komputa,

"SUNDAY J. MUNA"

alilisoma jina lile mara mbili , na kuivuta picha yake, alisoma maelezo ambayo yalimwambia kua kesho kesi yake inge somwa asubuhi. Baada ya kuhakikisha kila kitu kipo sawa,
alifunga lap top yake na kuingia chumbani ambapo alimkuta Mke wake Hannah akiwa bado yupo macho.

"Siwezi kuwaacha watu walihusika kwenye kifo cha dada yangu waendelee kuishi"
"Sasa ukiwapata uta wafanya nini mume wangu?"

"Nita hakikisha sheria ina fuata mkondo wake"

"Alfred mume wangu, mi nakujua , najua tu lazima utawauwa"

Alfred alimuangalia mke wake machoni na kumsogeza kifuani huku akimpiga busu juu ya paji la uso.

" tulale Hannah, usiku umeingia"

Ki ukweli siku hiyo Alfred hakulala hata kidogo ali subiri kukuche.

Kweli kuli kucha asubuhi na mapema alivaa shati lake jeupe ambalo alichomekea na suruali na koti jeusi na kuweka bastola yake kiunoni,
Kipindi hiko Hannah alikua amelala hakutaka kumsumbua,.
Alitoka na safari ya kwenda mahakama ya kisutu kuanza,
Baada ya kufika ali kuta kesi ipo kati kati na kweli alimuona mtu aliye kua aki mtafuta,
Kweli baada ya kesi ile kumaliza kusomwa aliomba aongee kidogo na mtu humiwa.
"Alfred Mulawa, , mbaya sana wewe, uliji fanya rafiki yangu, leo ume niweka ndani"
"Sikia Sunday,. Sikuja hapa kusikiliza lawama, nachotaka kujua kitu kimoja, dada angu hakuku sea kitu chochote, mi nili kua nisha maliza, nili kua niache kazi, KWANINI ULIMUUWA"?
"Alfred, mbona sikuelewi,sijui hata una zungumzia nini?"
"Hiii risasi ili tumika, nawewe ndo mmiliki wa silaha hii, usini potezee muda"
alitoa risasi na kumuonesha
"Naona huna sera Alfred, nenda tu mi sijui chochote"
"Okay, unataka twende ivyo, . Ulimuacha mkeo ana mtoto mchanga Dorisi,. Sasa sikia nikwambie,. Si una nielewa vizuri, nita mfanya kitu hakuna"

"Hahahaha, Alfred huwezi"

"Sawa mi naenda..."
Alfred aliinuka na kuuendea mlango ila kabla ya kufika ana sikia sauti ya Sunday iki muita .
"Alfred, sikia nikwambie, naomba nitunzie familia yangu, mi nakwambia kila kitu, mta fute mwana mke mmoja ana itwa JOYLA, JOYLA GODFREY,"
Alfred alimwangalia Sunday machoni kwa umakini na kutoa simu ambapo alimuonesha picha ya Joyla mpelelezi mwenzake, Sunday ali tingisha kichwa kuashiria kuwa ni yeye mwenyewe.
"Ndo yeye huyo huyo, ila Alfred please take care of my family".
Sunday aliongea huku akiinuliwa na maaskari,.
Moja kwa moja Alfred, aliingia ndani ya gari na safari ya kuelekea kwa Joyla kuanza,.
Kweli ali fika na kumkuta joyla yupo makini juu ya komputa
"Joyla"?
"Yes Alfred'"?
"Nakuomba sasa hivi ofisini kwangu"
Alfred alianza kutangulia huku Joyla aki fuata nyuma na baadae kuingia ofisini kwa Alfred na kukaa juu ya kiti, Alfred alivua koti na kumkazia macho joyla ambaye wakati huo aliinama inama.
"Joyla, Rose tangu sasa hivi haja fikisha hata wiki bado namkumbuka"

"Pole sana Alfred, ina kubidi usahau i....."

Kabla ya kumalizia kuongea Alisimama kama umeme kwa ghafla na kumkaba kooni Joyla ambae ali mpeleka mpka ukutani na kumkandamiza kwa hasira na kutoa bastola.

'"Kwanini ume muuwa Rose kaku kosea nini, kwanini Joyla, "?
Alfred ali foka kwa hasira na kuto kuonesha mzaha hata kidogo kweli macho yake yali badilika rangi na kuwa mekundu sana na kumfanya Joyla aliye kua uku tani jasho jembamba limtoke., huku akihema juu juu


"Alfredy mi sijui chochote"

Sauti ya joyla ilitoka kwa mbali sana akiwa amekabwa kooni jibu hilo lili mfanya Alfred akishike kichwa chake kwa nyuma juu ya shingo na kumbamiza juu ya meza iliyopo ndani ya ofisi iyo na kufanya Joyla adondoke na kuvuja damu,
alimchukua tena na kumpiga kofi zito ambalo lili lomfanya ayumbe na kudondoka tena, Joyla alipoona pata shika lile aliinuka na kuanza kuuendea mlango mbio mbio akitaka kutoka nje akiamini kua huo ndo unge kua mwanya pekee wa kutoka ,
ila kabla haja ufikia mlango tayari Alfred aliwahi kwenye mlango na kumpiga kichwa puani..
"Jamaaani nisaidie nakufa, Alfred ana niua , Nisaidieni nakufa jamani, "

Joyla alipiga kelele za msaada baada ya kuona kipigo kile ambacho hakitakuwa na mwisho.

"Msaada wako wewe hapa ni kusema ukweli, . Niambie joyla nitakuua, Nani ame husika kwenye kifo cha Rose?,"

Mlango tayari ulianza kugongwa huku Alfred akiamriwa afungue mlango ila Alikataa na kuzidi kutembeza kipigo kwa Joyla,
baadae vishindo vya mlango vina sikika kumanisha kwamba wana tumia nguvu ili kuuvunja mlango ule na waweze kumuokoa Joyla ambae wakati huo alikua ndani akiomba msaada.,

Kweli walifanikiwa kuuvunja mlango na kumkuta Joyla akiwa chini amepoteza fahamu
"Alfred, nini una fanya, una akili wewe, mtoeni mka fungie ndani selo sasa hivi"
"Fredy una fanya makosa,"
"Hakuna cha makosa Alfredy,.. mpelekeni ndani"

Alfred alifungwa pingu kwa nyuma na maaskari na kupelekwa ndani ya chumba hiko kilicho kua maalumu kwa ajili ya ualifu au mtu yoyote atakae enda kinyume na kazi.

Kesho yake asubuhi Alfred alitolewa ndani ya chumba kile na kuambiwa kuwa yupo huru na adhabu yake imeisha.

"Alfred, nini tatizo lakini?" Lili.kua ni swali kutoka kwa mkurugenzi wake katika kitengo cha CID(criminal investgation derpatment) mr, Fredrick Momba ndani ya ofisi yake kubwa.
"Sikia Fredy, kuna kitu kime jificha hapa nyuma, kifo cha dada yangu kina niuma sana, na kuna watu Joyla ana wafahamu"
"Lakin Alfred. Yote haya si tuliongea , haya mambo sio ya kukurupuka tu, ina kubidi ufanye uta fiti kwa kina, sio una enda una piga piga tu wafanya kazi wenzako, najua iyo ime kuathiri kisaikolojia ina bidi utulie sana kabla ya kuchukua maamuzi"

"Sawa bosi samahani haitojirudia tena, nafikiri Joyla anaendelea vizuri"?

"Hali.yake.ni.nzuri.alihusiwa jana sasa hivi yupo.kwake"

Baada ya maongezi kuisha Alfred alirudi ofisini na kuendelea kuta fakari.
 *******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG