Search This Blog

Monday, March 23, 2020

THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 7/10


THE PAINFULL SECRET
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
 SEHEMU YA 7 KATI YA 10


Maneno aliyo kua anaongea Flora haya kuendana na mwili wake mdogo , ambao hata akipigwa kofi moja anaweza akazimia mara moja, alikua na mwili mdogo ila mwingi wa maneno.
Waziri mkuu kasanga alibakia kumwangalia tu na kutomjibu chochote maana ali mzoea mke wake kwaio hilo hali kumpa shida.


"Na nita jua tu, hiko una chonificha, unadhani,!? nita jua tu, we subiri, endelea tu kunywa hayo mapombe uki choka utalala, usisahau kesho ile milioni mbili niliyo kuomba"

Flora aliingia kitandani na kujifunika shuka gubi gubi, akimuacha mume wake Akiburudika na pombe ile.

Asubuhi kulivyo kucha Waziri mkuu Partson Kasanga tayari alikua sebleni huku akiwa na lap top yake akionekana kutafuta kitu kwenye mtandao wa internet kwa muda mrefu , ni baada ya kupata wazo kuwa hakuna kitu kingine zaidi ya kutumia jeshi la nje ya nchi katika kitengo cha FEDERAL BUREAU INVESTIGATION (FBI)., kilichokua Marekani jimbo la Carlfonia.
Na kupata mawasiliano nao ambao waliweza kuchat kupitia mtandao huo wa internet akiwaelekeza kuwa kuna kesi na ndani ya nchi yake kuna Alshabab ivyo angehitaji msaada wa wapelelezi,
Bila kipingamizi chochote wana elewana kuhusu malipo na kumuhaidi kuwa kesho yake na mapema wange fika ndani ya Bara la Africa nchini Tanzania Mkoani Dar es salaam.

Habari zile zina mfurahisha sana Waziri mkuu na kujua kivyovyote vile Alfred asinge ruka popote pale., na wala asingeweza kumfikia alipo,.Ali amini sana hiko kitengo kutokana na historia yao nzuri na kushika chati Duniani kote., hasa kwa kitendo cha kumkamata Sadam.Hussein,

Kweli kesho yake kimnya kimnya alielekea uwanja wa ndege Mwl Nyerere na kuwa subiri wageni wake huku akimtuma Dereva wake Moses Kikwabi aende huku yeye akisubiri ndani ya gari, .
kweli kupitia kibao alichoshika Moses aliona watu watano wakiwa ndani ya suti na mmoja akiwa mwana mke, ambaye nayeye alivalia suti, na kimini kifupi huku chini akiwa amevalia viatu aina ya High hills, akiongozana na wenzake.
"Hope your Mr.Kasanga?"(natumai wewe ni mr, kasanga?".
Aliongea mtu huyo akiwa na suti nyeusi akimuendea Moses Kikwabi .
"No ',i am his driver, please follow me(hapana mimi ni dereva wake naomba mni fuate").
Wazungu wale wenye ngozi nyeusi yaani black America walimfuata Moses Kikwabi nyuma, wote wakiwa wamevaa suti nyeusi na miwani nyeusi huku wakiwa wana buruza mabegi yao, walienda mpaka kwenye maegesho ya magari na safari yao kuishia kwenye LAND CRUISER V8 ambamo ndani alikuwa amekaa waziri mkuu na kuji tanua.,
baada ya kuwa ona alishuka na kuanza kusalimiana.
"Thank you for coming, i think your the one i was chatting with",(asante kwa kuja, nafikiri wewe ndo niliye kua nachat nae)
"Yes i am, you can call me Harris Winslet, this is my back up team, meet Carlos,Larry and this is Miss. Emilia (ndio ndo mimi,unaweza ukaniita Harris Winslet, hili kundi langu saidizi, huyu ni Carlos, Larry na huyu ni Miss,Emilia")
Harris aliongea huku akimuoneshea Waziri mkuu kila mmoja wao na wote kupeana mikono na mwisho kumalizia kwa mwana mke yule ,
baada ya hapo walita futiwa gari ndogo ya kukodi na kuwafuata nyuma,
Mwishowe walifikia kwenye hotel kubwa iliyopo posta inayo fahamika kama KILIMANJARO HOTEL, baada ya kula chakula cha mchana Waziri mkuu alianza kuwa elezea jinsi wata kavyo anza kufanya kazi na kuwapa picha kubwa ya Alfred ambayo Harris aliiangalia na kuwapa wenzake.

"Give me his contanct, his formal working place location and the place he used to stay, another thing, a big room, Emilia you know what to do.(
Nipe mawasiliano yake, sehemu aliyokua ana fanyia kazi, alipo kua anaishi, kitu kingine nahitaji chumba kikubwa,Emilia una jua cha kufanya")

Maneno hayo yalimtoka Harris akiwa makini sana kwa kile anachoongea , .
"You dont have to worry about that, you will get,as longer as you will find that terrorist in my country(usiwe na shaka, utapata,nachotaka tu umpate huyo muhasi ndani ya nchi yangu"
"Hahahaha, Mr Partson, give us twenty four hours, you will receive good news from us , we'll find that son of a bitch immediately , i promise you(hahaha Mr, partson, tupe masaaa ishirini na manne, uta pokea habari nzuri kutoka, kwetu, tuta mpata huyo MWANAHARAMU, haraka iwezekanavyo, nakuhaidi.")

Harris aliupindisha mdomo akicheka kwa dharau sana huku akiwa geukia wenzake na kuwaambia kuwa hii ni kazi ndogo sana tena Africa nchi ambayo sana hasa kwa kutokua na miundo mbinu,

Baada ya hapo waliagana na waziri mkuu huku akiwa na furaha sana,.
Baadae waliingia ndani ya chumba hiko kikubwa na Emilia mwanamke huyo ambae aliye kua mtaalam katika kitengo cha I.T(information technology) alionekana kufunga funga mitambo ndani ya chumba hiko,
baada ya kumaliza hapo alitoa namba ya Alfred na kuuiandika kwenye lap top, ambayo baadae ili mletea horodha ya watu watano alio wapigia mara ya mwisho,. Baada ya kuangalia vizuri tena ana kuta jina WIFE , alichukua namba zile na kuingiza tena ambapo ili kuja picha ya mwanamke mweupe na jina lilioandikwa HANNAH MULAWA,
"Harris. You have to see this(Harris una takiwa kuona hii).
Emilia aligeuza lap top ile na kumuonesha Harris ambae alisogea na kutatazama kwa muda mrefu.
"His wife, we have to wait , i know they will communicate, this is what i was looking for,(ni mke wake, tuna takiwa tusubiri, najua wata wasiliana, hiki ndo nili kua naki tafuta".
Emilia alitulia na kuchomeka mtambo unaoitwa VOICE RECOGNIZER, ambao una uwezo mkubwa wa kuinasa sauti na kuitambua sauti ya mtu anaeongea,
Kweli baada ya kukaa kwa muda kidogo waliona simu ile ina ita na kupokelewa ambapo iliongea kwa muda kidogo na baadae kugundua kuwa kweli alikua ni Alfred Mulawa aliye kua akiongea na pale pale kuinasa ile namba ngeni aliyo kua anaitumia Alfred na kuanza kuifanyia kazi,

Emilia aliichukua ile namba na kuingiza ndani ya kimashine kidogo na kuonekana kubonyeza mashine iyo na kusubiri majibu,
alitoa skrin kubwa kidogo nyembamba na kuiweka ukutani,. Baada ya muda mchache tayari walikua wana iona picha ya Alfred akiwa kama kwenye video waki tumia mtambo wa SATELITE, Alfred alionekana kila kitu, na pembeni yake kulikua na kiramani kidogo.ambacho kili muonesha ramani pale alipo.,
."He is in Zanzibar, it is a few miles from hear, you have to take a plane, your destination will be zanzibar international airpot, when you reach there i will tell you what to do"(yupo zanzibar,ni maili chache na hapa,mna takiwa mchukue ndege, mta fikia uwanja wa, ndege wa zanzibar, mkifika huko nita waambia cha kufanya.")
Emilia aliongea akionesha kidole huku akiwa amesimama kama mwalimu wa darasani na kuwa onesha ramani iliyokua juu ya skrin ile kubwa,
wote waliiangalia skrini ile na kumuona Alfred, ambae wakati huo.alikua amekaa.
Hapo hapo walinza kujiandaa na kuvaa mitambo yao ambayo kila wana poenda wangeonekana na Emilia, na pia walivaa kifa kinachoitwa WIRELESS COMM, kidude kidogo kina chovaliwa sikioni maalumu kwa ajili ya mawasiliano ambacho mtu yoyote yule hawezi kujua kama kime valiwa, kifaa hiki hutumika kufanya upelelezi ambapo wakiongea wana sikikiana.
"What about tha weapons?, (vipi kuhusu silaha")
Aliuliza Emilia.
""There is no need of carrying weapons, come on a small job like this, NO , your kidding Emilia..okay boys it's show time, lets move"
Wote waliondoka na kumuacha Emilia ndani ya chumba kidogo wakiongozwa na Harris mkubwa wao.ambaye muda wote alionekana na dharau bila kujua mtu anae enda kukabialana nae, walivaa vizuri suti zao na miwani,
Na kuchukua gari ambalo lili wapeleka uwanja wa ndege,.
Hapo walichukua ndege ndogo ya kukodi ambayo ili wafikisha mpka Uwanja wa ndege wa Zanzibar na wote kushuka.


*************************
"Konda, we konda sasa mbona una tupitiliza, si nili kwambia ushushe hapo uuwo, wewe una tuleta mpka huku Kishingoni, aya tugee nauli ya kurudi,"

Ili kua ni sauti ya jaqlin Nyange akiwa ndani ya basi kubwa ya kampuni ya Dar Express, ambapo basi hilo mwisho wake huishia Rombo, hivyo kitendo kile cha kupitishwa kituo kilimkera sana, pembeni akiwa na Hannah Mlawa ambao waliamua kwenda kuji ficha huku Moshi mkoani Kilimanjaro.
"We dada vipi, ?.kwani hapa kishingoni na hapo uuwo kuna umbali gani?.una ropoka ropoka tu, mi sikukusikia bwana"
"Sio huku nisikia izo dharau una leta. Kelele zote nilizo kua napiga hapa, "
"Aya shuka basi chaaa, Mwana mke mrembo una ongea kama ivyo, hufananii kabisa"
"Achana na namimi"
Jaqlin aliachia misunyo mikali huku akichukua mabegi yake yaliyo po juu sehemu maalumu ya kuhifadhia mabegi.
"Hauna mabegi kwenye buti"?
Konda wa basi aliuliza.
"Sasa ninge kua nayo si ninge kwambia, Hannah tushuke"

Jaqlin alijibu huku tayari akiwa kwenye ngazi za basi ambapo basi hilo liliondoka,
Aliwa salimia watu alio wajua wa pale na kuchukua piki piki,.hapakua mbali na pale kwaio ndani ya dakika nne alikua tayari yupo Uuwo kwa wazazi wake Mr and Mrs.Bariki Nyange. Ambao wali shangazwa sana na ujio wa mtoto wao kimnya kimnya bila kutoa taarifa.
"Kuna matatizo Baba, we acha tu, naomba kwanza nile maaa nina njaa kweli,Mama yuko wapi?"
"Mama yako yupo , ameenda hospitali, jino lina msumbua, mama yako nae kwa kudeka"
"Aaah baba nawee, huyu anaitwa Hannah, kama una mkumbuka Alfred Mlawa, yule aliye kua anaishi kwa mzee Kitlya kule Rombo baada ya wazazi wake kufariki,.ukawa una nitania ni mchumba angu",
Mzee Nyange alimuangalia Hanaaha na kuendelea kumsikilza jaq.
"Sasa huyu ndo mke wake"
"Aaaah kumbe mpola"
Mpola ni neno la kichaga ambalo hupenda sana kuli tumia wakimaanisha Mkwe,
Ivyo mzee huyo alimkaribisha kwa mikono yote miwili na kuwaacha waendelee na mazungumzo huku Jaq akimwandalia maji ya kuoga.
"Jisikie upo nyumbani karibu hapa ndo kwa wazazi wangu Hannah. Alfred yeye alikua ana kaa kwa kule juu , nita kupeleka siku"
"Asante Jaq, nasikia baridi sana, Aaah tuli kujaga zamani sana huku ,"
Hanaah alivaa sweta baadee alibandika maji ya kuoga na kuingiza bafuni kuoga,

Jioni ilipo ingia walianza kula ambapo Mama jaqlin aliwaandalia mtori na wote kufurahia kwa chakula hiko kitamu sana.
*****************************

"Oya Rodgers kafa, na na na na, mimi sasa naanzisha vita wallah laazim, . Lile al shaabab lime muuwa Rodgres,"

Ilikua ni sauti ya mtu aliyeongea rafudhi ya kipemba kutoka katika kikundi cha NO MITEGO,kifo cha Rodgers kili sababisha roho ya kisasi kuwa ingia.,
"Alafu yule naweza kumpata,. Ile gari aliyo shuka ile siku ile mimi naijua, , yule demu wa Dibby, ile gari ya demu wa Dibby, napajua anapoishi"
"We bwege twende sasa, tuka msake "

Baada ya kuku baliana wote wana ingia ndani ya gari na safari ya kwenda kwa Amina kuanza,

Baada ya Alfred Mulawa kula anaenda sebleni na kufunga mlango kwa funguo na kuzima taa ila baada ya kugeuza shingo na kupiga hatua tatu ana hisi mlango una pigwa kwa nguvu na kuvunjika na watu watatu kuingia na bastola mikononi.

"Huyu hapa,hapo hapo ulipo tulia ivyo ivyo"

Alfredy aliweza kuwa tambua sana watu wale na sura zile hazi kua ngeni kwake.
"Mshenzi huyu, sogea huku,.pita mbele,"

Alfred akiwa ameweka mikono yake juu na kuwaangalia kwa umakini wa hali ya juu watu wale walio watatu, alisogea taratibu sana akipiga hatua za mtoto mdogo na kwa ghafla alifika kwenye SWITCH na kuzima taa na kufanya giza zito kutanda ndani ya nyumba hiyo kutokana na kukariri kila mtu alipo, haikumpa shida kumuendea mmoja kumpa kipondo ambapo alichukua bastola aliyo shika na kuanza kuwapiga wote risasi.
Alivyo hakikisha kila kitu kakifanya sawa sawia aliiendeea tena switch na kuiwasha,.ambapo aliweza kuwaona watu wale wakiwa chini wamelala chali huku wakiwa na majeraha ya risasi.
Alivyo geuka Pembeni alimuona Amina kashika mwiko wa kugezia ugalia na kutabasamu,
"Huo mwiko ulikua unaenda nao wapi Amina"?
"Nili kua najihami"
"Hahahaha, na mwiko, ?"

Amina aliwa tazama wale watu pale chini ambao damu zili kua zime tapakaa,
Na hapo hapo tena kuona watu wengine wame ingia wakiwa wame valia suti na miwani, watu hao wanne wali mfanya Alfred awatazame kwaa umakini sana.

"F,b,i, naitwa Harris, Alfred Mulawa weka silaha chini, tuna taka tuku saidie"

Aliongea Harris huku akitoa kitambulisho chake na kufanya Alfred ashushe pumzi ndefu sana.
"Mna taka nini?"
"Tume tumwa kuja kuku saidia"
"Na nani, sitaki msaada wenu, nani kawaambia nataka msaada wenu,"?
Harris aliaangalia zile maiti zilizo kua pale chini.
"Wewe ndo ume fanya hivi?"
"Ndio"

Harris alizidi kumsogelea Alfred taratibu huku akimuongelesha na kumuangalia machoni,
Huku mwingine aliye itwa Carlos akikaa sawa kwa lolote lita kalo tokea,
"Alfred"

Amina aliita na kumfanya ageuka kama umeme Harris alimvaa Alfred na kumkaba shingoni huku Carlos akiwa na kitambaa mkononi ambacho kili kua na dawa kali ya usingizi alimuwekea Alfred puani ambayo waliikandamiza sana na kufanya aivute dawa ile ambapo baada ya kuivuta ana lewa kwa kizungu zungu na pale pale kulala na kupoteza fahamu kutokana na dawa izo kuwa kali sana,

walimchukua Alfred na kumbeba begani huku waki toka nae nje wakimuacha Amina asielewe la kufanya, aliwaashuhudia wakimuingiza ndani ya boneti la gari kwa nyuma na gari kutoka kasi,

"Hodi humu ndani, ,habari yako dada,,samahani Alfredy nime mkuta?"
"We nani?"
"Naitwa Amney"

Ili kua ni sauti ya Amney baada ya kufika na kumkuta Amina ambae alikua hajui la kufanya baada ya kuonekana kama kuchanganyikiwa sana. Amney aliweka mabegi yake chini taratibu na kuruka maiti alizozikuta pale chini, na kumuendea Amina ambae wakati huo alikua ana majonzi sana na kuonesha kusi kitika.

"Alfred kani elekeza hapa, samahani sijui nime kosea nyumba"?
"Ndio ume kosea nyumba, hapana no samahani, ndo hapa Alfred kachukuliwa sijui na watu walikuja hapa siwa elewi, wame mteka yaani nashindwa kuelewa, na hizi maiti hapa yaani embu niache kwanza, kwani we nani yake?"

Aliongea Amina akiwa na kiwewe sana. Amney haraka haraka alivuta moja ya begi lake na kutoa IPAD yake kubwa na kuiweka kwenye charg huku akiiwasha, alibonyeza Ipad ile na kuona alama nyekundu ambayo ili kua ina sogea kupitia kifaa cha GPS tracker aliweza kuona Alfred anapo elekea akitumia simu ya Alfred ya mkononi,
"Alfred , Alfred, huyu hapa nisha mpata, samahani.una gari?"
"Ndio, ndio ninalo,vipi kwani una weza kujua alipo"?
"Nipe funguo za gari lako, fanya haraka dada"

Amina alibabaika na kutoa funguo za gari mfukoni na kumkabidhi ambapo , bila kuchelewa Aliingia ndani ya gari hiyo NOAH ya Amina na wote kuongozana,.
Alikanyaga mafuta mpka.mwisho na kufanya mshale wa spidi kugota mwisho, ikiashiria gari ipo mwendo wa mwisho .kweli ili kua ni kasi ya ajabu mpka Amina kuanza kuogopa,
hakumjua mwana mke yule ni nani ila alicho jua yeye ni wenda akawa ndugu yake na Alfred, Amney akiwa makini juu ya usukani akiushika usukani kwa mikono miwili alikua kama yupo kwenye mashindano ya magari, kuna kona ya ghafla aliiona na kuminya brek huku akivuta HANDBREK na kufanya gari izunguke na kufanya kidogo ipinduke na pale pale, ila aliweeka sawa sawia na kutulia, alikanyaga mafuta na kushusha hend brek huku mwendo.kasi ukiendelea

"Taratibu dada ndo uwendeshaji gani wa gari huo?.., mi nina presha ya kushuka jamani looo"

Aliongea Amina akiwa ana hema juu juu kama bata mzinga huku akiwa ame jikunja kwa uwoga,
.ila Amney hakumjibu chochote aliendea kukata lami na kusonga mbele,
Kupitia Ipad yake aliweza kuona jinsi gani walivyo karibu hivyo haiku mfanya apunguze mwendo kasi alikua nao, .
Mbele yake aliona gari aina ya BMW X5 na kuzidi kuisogelea.
"Yupo humo Alfred, nime waona wakimuweka ndani ya boneti ya gari hilo hapo ".

Aliobgea Amina baada ya kuikumbuka gari aliyo iona.
"Yupo kwenye buti, Mungu wangu"
Amney kwa kasi aliipita gari ile kwa mbele na kuzidi kwenda kasi, ila alivyo fika mbele alikanyaga breki ya ghafla na kufanya matairi yajikwaruze na kufanya makelele, ivyo ile gari ya nyuma BMW x5 iliji kuta ina gonga gari aliyokuwemo Amney na ndo ivyo yali kua mahesabu ya Amney yali kuwa yame tiki, haraka haraka alishuka na kuwaendea.
"Vipi hapa, ina kuaje mbona mmenigonga?"

"Ila wewe ndo una makosa"
"Mshenzi nini wewe, mpuuuzi mmoja huna akili, umenigonga kwa nyuma alafu una niambia nina makosa, embu shuka kwanza ndani ya gari, tuelewane vizuri."
"Dada samahani tuna haraka hapa "
"Haraka yako mimi hani saidiii, embu shuka"

Amney aliingiza mkono ndani ya gari kupitia dirisha lililo kuwa wazi la mlango wa mbele na kuzima gari huku akichukua funguo za gari na kufanya Harris ashuke.
"Alafu nyie wazungu mmetokea wapi?"
"Tume kuja kwenye maonyesho tu, sikia basi chukua hizi pesa nigee funguo izo"
Harris alitoa dola za kimarekani ila Amney alichukua na kutupa chini huku akiliendea gari alipo liacha na kuchukua bastola.
"Paa paa paaaa"
Alivya tua matairi ya gari lile na yote kuisha upepo na safari hii kumuwekea Harris bastola usawa wa kichwa.
"Fungua boneti, fanya upesi, paaa"
Alipiga tena risasi nyingine hewani na kufanya Harris ashtuke na kujua kweli mtu aliye shika bastola ile hana masihala hata punje,
kweli alitii na kufungua boneti,
Alimuona Alfred akiwa ndani ya boneti hana fahamu.
"Waite wenzako waje msaidiane, naomba huyo mtu mmpeleke ndani ya gari langu. HARAKA SANA KABLA SIJAUWA WOTE,"
Kweli Harris aliwa ita wenzake na kufanya kile Amney ana chotaka,
kitendo kile kili wauma sana ila hawakua na la kufanya,
Alivyo hakikisha watu wale wame muweka Alfred,
Alipiga tena risasi nyingine mbele ya gari lao ambayo ilipenya juu ya injini na kutoboa mafuta ya breki ambayo yalikua yakivuja na kujua kivyovyote vile isinge kua rahisi kuwa fuata nyuma.

Tayari waliiingia ndani ya gari na Amney kutoka kwa kasi ya ajabu,.

"This is crazy, this is bullshit, son of a bitch, how could that bitch deafeat us, impossible"

Aliongea Harris huku akipiga mguu chini na kuanza kulaumu wenzake kwa kitendo kile.
"Call Emilia. Right now, i need her to track them before they reach far"

Aliongea Harris huku akishika kichwa chake na kushusha pumzi ndefu.

Baada ya kutembea umbali mrefu kidogo huku bado Alfred akiwa haeleweni nini kinaendelea duniani,
Amney alivuta begi lake dogo jekundu na kutoa kitu kama kichupa kidogo na kukiweka puani mwa Alfred baada ya Alfred kuvuta ile harufu alipiga chafya mfululizo na kuamka.
"Aaam....ney, nini kim..e tokea?"
Alipikicha macho na kumuangalia Amney kwa makini.
"Chukua maji haya kunywa kwanza Alfred pole sana"

Amney aliongea huku akiendelea kutazama mbele akiendesha gari.
 *******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG