ABEE SHEMEJI SEHEMU YA 2/10
ABEE SHEMEJI
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
SEHEMU YA 2 KATI YA 10
*******
‘Hi Ahmed,Mimi Hajrath.Usiku mwema,Love you’
Simu ya Hajrath,ilikuwa mikononi mwa Florian,alifanya makusudi kutuma ujumbe ili ategue kitendawili, kilichokuwa kinamtesa kwa siku nyingi,moyo wake haukuwa wa chuma.Alianza kuhisi wivu na kuchezwa na machale ya kwamba ipo siku Hajrath atamtema kwani dalili za mvua ni
mawingu,mbali na hapo hakutaka kupelekwa puta na hisia zake ndiyo maana alitaka kufanya uchunguzi,kilichomuuma zaidi ni kukuta jina la Ahmed, limeseviwa ‘IRENE’ alihisi kuchanganyikiwa, akahisi kama jasho la pua linamtoka,wivu wa mapenzi ukamkaba kohoni.
Wakati anafanya hayo,Hajrath alikuwa bafuni anaoga,akafuta meseji aliyomtumia Ahmed ili Hajrath asije kugundua chochote kile huku mawazo yake yakitafakari ni kitu gani akifanye,alihisi usaliti.Hajrath,alivyotoka bafuni aliishia kumuangalia tu bila kujua ni kitu gani amfanye.
“Baby,simu yangu iliiita?”
Hajrath,akauliza huku akijipangusa maji mwilini mwake, akitumia kanga aliyovaa!
“Hapana”
“Meseji?”
“Haijaingia”
“Irene ni nani?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Florian,bila kupepesa macho huku akimuangalia Hajrath kwa macho fulani,yaliyojaa wivu mkali na hasira.
“Irene?”
“You heard me”(Ulinisikia)
Mara ghafla Florian,akabadilika.Sura yake ikawa imechora makunyanzi,hacheki tena!Yupo Siriazi.
“Irene,Irene yupi?”
Hajrath badala ya kujibu swali,akauliza swali likawa swali juu ya swali.
“Kwani wewe unamjua Irene yupi?”
Florian nayeye akajibu kwa swali.
“Nimekuuliza swali,nijibu kwanza ndio uulize swali.Irene,unamjua?”
“Irene wapo wengi sasa mpenzi wangu”
“Irene wa kwenye simu yako”
Florian,akasimama na kuchukua simu ya Hajrath,akatafuta majina mpaka alipolifikia ‘Irene’
“Anhaa,huyu rafiki yangu baby!Ni wa kule Tengeru,dada mmoja hivi.Yupo stationary,mara nyingi huwa natype kazi zangu kwake,isitoshe amekuwa kama dada yangu huwa ananisaidia sana”
Hajrath siku hiyo alijishangaa hata yeye namna alivyokuwa anajielezea,hakuelewa majibu ya kutunga kayatoa wapi.Mbali na hapo alikuwa mkavu,hacheki hata kidogo!Na alijua sana mambo anayosema yalikuwa ni ya uwongo.Lakini angefanya nini?Ilikuwa ni lazima asuke uwongo ili aokoe penzi lake,hakuelewa Florian anajua kila kitu na anamchora tu.Hiyo ilifanya Florian ashushe pumzi ndefu na kumtizama Msichana huyu mpumbavu,anayemdanganya wakati ukweli wote anaujua!Ili kuthibitisha hilo,hapohapo akapiga simu na kuweka ‘loudspika’ hiyo ilimfanya Hajrath, aanze kutetemeka kwa hofu,akajua tayari kitumbua kimeingia mchanga!
“Griii griii….griii griiiiii”
“Griii griii…Griii griiiiii”
Simu ya Ahmed ilikuwa mezani inaita kwa staili ya ‘Vibration’aliweka hivyo kwa ajili ya kujisomea kwani hakutaka usumbufu wa aina yoyote ile mpaka amalize jambo analolifanya,hiyo ilifanya asisikie kwamba anapigiwa simu, hiyo ni kutokana na kufunikwa na begi,kitendo cha kupokea ujumbe wa Hajrath ya kuwa bado anampenda kilimfanya atafakari bado,mara mbilimbili.Pengine alidhani yu ndotoni,kwani aliuelewa msimamo wa Msichana huyo, hivyo haikuwa rahisi kwake kusamehewa kwa mtindo huo,ukilinganisha na unyama alioufanya wa kutembea na Necka Golden kimapenzi,aliamini kabisa hakustahili msamahaa wa Hajrath, hata kama siku hiyo Mtume Mohamed angeshuka.
Ndiyo maana akaamua kujikita kwenye kitabu,akapata usongo ajabu.Alitaka asome sana,apate matokeo mazuri apate kazi nzuri kisha miaka ya baadaye aje kuwa na uwezo kipesa,aliamini kivyovyote vile angepata mwanamke mzuri na mrembo, ambaye ataweza kutengeneza naye familia!Kwani pesa siku zote ni sabuni ya rohoo,hata hivyo aliamini wenda Hajrath sio fungu lake,yote akamuachia Mungu wake aliye juu Mbinguni ampe nguvu ili azidi kupambana na vita inayomkabidili mbele,hakutaka kurudi tena nyuma.Simu yake iliendelea kuita bila kugundua,mpaka inafika saa mbili ya usiku,akahisi nja inamuuma!Hapo ndipo akakumbuka kuwa hakupika,hiyo ni kutokana na kukichimba kitabu kwa hasira na usongo wa hali ya juu sana!Alihakikisha abakishi ‘topic’ yoyote ile,alivyopiga macho yake pembe zote za chumbani kwake,hakuona simu yake!Akavuta begi lililopo mezani,ndipo alipoiona.Alivyoangalia akagundua kuna ‘Missed calls’tisa, mbili zilitoka kwa rafiki yake Shadrack Mwalusambo na nyingine ni namba ngeni,alivyodadisi,akagundua namba ya Hajrath iliyomtumia meseji.
Akashusha pumzi ndefu kidogo,moyo wake ukaanza kupiga kwa nguvu ingawa hakuelewa ni kwanini hali hiyo inatokea,akahisi kama uti wake wa mgongo unapigwa na ubaridi.Ghafla nafsi mbili zikaanza kubishana ndani ya moyo wake,moja ilimwambia apige simu nyingine, ikapinga.
“No way”
Ahmed,akatamka maneno hayo na kuiweka simu mfukoni,hakutaka kurudisha moyo wake nyuma tena.
“Wanawake wazuri kila siku wanazaliwa”
Akajaribu kujifariji lakini hakuwa ana uhakika kama kauli hiyo, ingemfariji mpaka mwisho kwani bado alihisi kumpigia simu Hajrath ili walau amsikilize, ajue ni kitu gani anahitaji kutoka kwake siku hiyo.Hivyohivyo akatoka nje,ambapo huko alitafuta mgahawa ili ale kisha baadaye arudi getoni kwake ajifungie aendelee kupambana na kitabu kwani aliamini elimu kwa wakati huo ndio mkombozi wake na vitabu ndiye mpenzi wake,hivyo alitakiwa asifanye mchezo kabisa.Ilikuwa ni bora akose kimoja kuliko kuharibu vyote masomo, sambamba na kumkosa Hajrath.Hapo,hakukaa muda mrefu akawa tayari amemaliza kula,akalipa na kurudi kwake ambapo huko,mwendo ulikuwa ni ule ule.
*****
Bado Florian Fredrick,aliendelea kujiuliza maswali ambayo alishindwa kupata majibu.Bado Hajrath aliendelea kumpa wasiwasi mkubwa sana,jambo lililomfanya aumie mtima ni kitendo cha kumuongopea kwamba ‘Irene’ ni rafiki yake kumbe ni Ahmed,jambo hilo ndilo lililomtatiza kwa kiasi cha kutosha, japokuwa hakutaka kulionesha swala hilo waziwazi,ndiyo maana siku hiyo aliendelea kumuuliza maswali Hajrath bila kikomo!
“Sasa kwanini asipokee simu?”
Florian akazidi kutupa maswali,wakati mwingine alidhani Hajrath na Ahmed wamerudiana kisirisiri.
“Baby,sijui”
“Usinijibu hivyo Hajrath,usinifanye mimi mtoto mdogo”
“Kivipi Florian lakini?”
“Nakwambia tena,usinifanye mimi ni mtoto mdogo!Umenielewa?”
“ Florian mbona sikuelewi!”
“Hunielewi,sio?”
“Ndio baby”
“Huyu Irene ni nani?Nakuuliza tena kwa mara nyingine”
“Kama nilivyokwambia”
“Una uhakika?”
“Ndio”
“Nachukuwa hii namba,nitajua cha kufanya.Kama nikikuta ni tofauti?”
Florian alizungumza na kuhitimisha akiweka nukta, iliyoambatana na swali juu.
“Nifanye chochote”
“Nikufanye chochote umesema?”
“Ndio”
“Naomba maamuzi,nitakayochukua usije kunilaumu”
Sijui ilikuwaje siku hiyo lakini Hajrath alijiamini kupita maelezo yaliyojitosheleza kwani alimjibu Florian huku akimuangalia usoni.Hiyo ilimfanya Mpaka Florian aanze kuwa mpole kidogo sababu alidhani labda hata yeye alikosea Irene hakuwa Ahmed,lakini jambo hilo hakutaka kulipa kipaumbele, ilikuwa ni lazima aifuatilie namba hiyo ingawa alijuwa ni lazima itakuwa ya Ahmed tu.
Mambo hayakuishia hapo,siku iliyofuata Florian alimtaka Hajrath waongozane kwenda sehemu moja tulivu ili wazungumze mawili matatu huko walikula na kufurahi,niya ya Florian ilikuwa ni kuomba radhi kwa kila kitu alichokifanya siku iliyopita.
“Zilikuwa ni hasira tu baby”
Florian alisema wakiwa kwenye mgahawa mmoja,wanakunywa mchemsho wa kuku.
“Usijali Darling”
“Nakupenda Hajrath,nakupenda sana.Naomba baadaye uje kuwa mke wangu,tuzae watoto”
Florian alizungumza kwa hisia kali,akimtizama Hajrath aliyekuwa anaona aibu za kikekike,mara aangalie chini, mara apepese macho ilimradi mahaba.Mapenzi ya binadamu hawa wawili, yalikuwa ni motomoto na hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa tayari kumuacha mwenzake.
“Nakupenda pia Florian”
“Lakini naomba kitu kimoja,usinifiche.Sababu naujua ukweli”
“Kitu gani Baby?”
“Huyo Irene ni Ahmed,naomba uzungumze ukweli baby,siku zote ukweli umuweka mtu huru”
Moyo wa Hajrath,ulipiga paa!Almanusura apaliwe na supu,tayari jipu lilikuwa limetumbuka,alihisi kutetemeka na hilo lilionekana wazi sababu alipokaa alihisi amekuwa mdogo ghafla,hiyo ilitokana na kutotegemea kusikia kitu kama hiko kutoka kwa Florian kwani alidhani mambo tayari yameisha.
“Kuwa mkweli,kitu ambacho sipendi.Ni uwongo,bora uniambie ukweli niumie kuliko unifariji kwa uwongo.Mimi mbona huwa nakwambia ukweli,niambie kama bado unampenda Ahmed ili tusiende mbali zaidi nikuache naye,sisi ni watu wazima!Sio wanafunzi wa secondary”
Florian alizidi kusema ya moyoni,aliongea kila kitu hakuacha kitu alichokuwa amekifanya,alisema mpaka alivyotuma meseji kwa Ahmed,siku hiyo ndio akaona jina Irene juu ya kioo cha simu yake.Kuanzia hapo Hajrath,akahisi kama yupo uchi wa mnyama,alijihisi msaliti na kujuta kuficha ukweli.Hakuelewa ni pepo ama bado anampenda bado Ahmed,akashindwa kuzuia machozi yanayomlenga,yakachuluzika mpaka mashavuni, akaanza kulia kwani alijua huo ndio ungekuwa mwisho wake,yeye na Florian jambo ambalo hakutaka litokee katika maisha yake,hata siku moja!Moyo wake uliuma ajabu!
“Flori…an I’m sorr..y.Na..omba nis..amehee”
Akajikaza na kuzungumza kwa kwikwi,hakuwa ana uhakika kama atasamehewa siku hiyo!
“Nachotaka ni kujua ukweli Darling,usilie please”
“Na..umia Florian nakupenda sana,naomba niambie ki.tu chochote nikifanye ili uami..ni,kuwa nakupenda”
“Bado unampenda Ahmed?”
Florian akaibua swali.Hiyo ilichukuwa kama dakika moja nzima kwa Hajrath kutoa jibu!
“Na..kupenda wewe Florian,nakupenda wewe tu”
Hakukuwa na punje ya mzaha hata kidogo kutoka kwa Hajrath,kile alichokizungumza kilitoka kwenye uvungu wa moyo wake,licha ya hayo alizungumza kwa hisia kali sana huku akimtizama Florian usoni.Japokuwa siku hiyo alilia sana lakini haikufanya Florian amuamini moja kwa moja, bado aliendelea kutafsiri jambo hilo ni maigizo na usanii mtupu,hata hivyo alijitahidi kuamini machozi ya Hajrath,akamvuta karibu yake na kumpangusa machozi.
“Usilie Darling,don’t cry!Nakupenda sana”
“Usiniache please,nitaumia sana!Naomba unisamehee ni kweli nilikudanganya”
Kuanzia siku hiyo penzi lao likarudi upya,Hajrath akazidisha penzi. Akalikatia kachumbari na kuliweka viungo vyote likawa tamu.Ilikuwa kila akipita sehemu na kuona shati zuri ama saa kali ni lazima ainunue na apewe Florian.Ikawa hivyo pia kwa Florian akiona chochote kizuri ni lazima Hajrath anunuliwe,wakazidi kuwa maarufu chuoni.Hiyo ilifanya mpaka wawe mfano wa kuigwa na wanachuo wote!
“Mimi nasubiri ndoa tu”
Siku hiyo Amney,akaweka utani kidogo walivyokuwa wote!Mbele yake alikuwa Hajrath na kushoto aliketi Florian,sio siri mambo yalikuwa ng’aring’ari kwa wawili hawa.
“Hilo tu,tena wewe utakuwa Matron”
“Mmmh,makubwa”
“Si ndio baby?”
Hajrath kwa madoido akamgeukia Florian na kumuuliza swali huku akiwa kama anadeka.
“Wewe ndio Mama shughuli,wewe ukipitisha mimi sina neno”
“Nataka likizo ikianza nikupeleke nyumbani wakujue baby”
Siku hiyo walizungumza jambo la ndoa utadhani ilikuwa karibu kutokea,licha na hayo walikuwa wenye furaha kupindukia.Habari zao zilivuma,Ahmed alizisikia lakini aliweka masikio pamba!Alishadhamiria kupambana na hali yake na siku zote ratiba yake ilijulikana kama hayupo maktaba anasoma, basi yupo chumbani kwake anajisomea,yaani ilikuwa yeye na vitabu, vitabu nayeye!Hatimaye ‘test’ zikaisha,majibu yalivyotoka Ahmed akawa amewaburuza wanafunzi wote, kwenye kila somo, hiyo ilifanya jina lake lizungumziwe na walimu wote!Hata hivyo hakutaka kujikweza,akachukulia kama kawaida kwani aliamini alistahili sababu ya kukesha kwake usiku na mchana akisoma,japokuwa aliongoza lakini hakutaka kujibweteka.Hiyo ikampa chachu ya kuendelea na moto uleule.
Hatimaye zikabaki wiki mbili tu ili wafanye UE.Na huo ndio ulikuwa mtihani wake wa mwisho chuoni hapo,kumaanisha baada ya hapo alitakiwa kuhitimu ili aanze safari nyingine mitaani.Hiyo ilimpa hasira zaidi.Ikafanya wanafunzi wengi wamuombe kukaa naye siti ya karibu, siku ya mtihani.
“Ahmed,kwenye pepa tukae wote!Si unajua tena mshkaji,mambo Fulani yale”
“ Tatizo lako wewe Frank,msumbufu sana!Sasa unaingiaje kwenye pepa yaani hujui hata kitu kimoja?Unaingia blank.Soma soma kidogo,unakumbuka siku ile.Tulivyopanguliwa”
“Ile siku siwezi kuisahau,Kimodo kavu sana!Kaenda kuniweka mbele,kuangalia pepa.Sijui hata swali moja mzee,yaani nilikuwa naona nyota mzee”
“Ngoja nikwambie topic za kusoma,sasa hivi nenda kazitafute ili likitokea la kutokea uwe unajua hata maswali mawili matatu”
“Enhee nipe bosi”
“Nakuandikia hapa pembeni,nenda ukasome Frank”
“Poa jembe,ahsante sana!Wewe ndio rafiki wa kweli”
“Mambo ya kawaida hayo,usijali”
“Nakwambia ukweli Ahmed,ni bora mtu akufundishe kuvua samaki kuliko kukupa kila siku”
Huo ndio ulikuwa ukweli,bila choyo na kinyongo chochote kile!Ahmed akaandika chini ‘Topic’ muhimu.Siku zikazidi kusonga,chuo kikawa kimya kabisa!Siku ya siku ikafika,wanafunzi wakakusanyika ndani ya vyumba vya mitihani na kalamu zao tu.Ahmed alikuwa ni kama nabii vile kwani ‘topic’ alizomuandikia Frank,akazikuta,akamgeukia wakagonganisha macho yao.Frank akamuoneshea dole gumba huku akitabasamu kumaanisha kila kitu kipo bomba!
Kuanzia mtihani uanze,siku zilikimbia kwa kasi ya umeme.Hatimaye wakabakisha mtihani mmoja ambao huo,ilikuwa ni lazima wasubiri siku mbili ndipo waufanye.Ahmed akazidi kupata usongo,tayari ng’ombe alikuwa kashamaliza na ulibaki mkia tu.Siku ya Jumatano,saa kumi ya jioni ndipo aliweka kalamu chini na kumshukuru Mungu kwa kumaliza mtihani wake salama,alivyotoka ndani ya chumba cha Mtihani, akamtafuta Mama yake mzazi hewani ampashe habari hizo nzuri kwani huyo ndiye alikuwa rafiki yake kipenzi.
“Mama nimemaliza mtihani salama”
Ahmed aliongea huku akilia machozi ya furaha,miaka mitatu ilikuwa ni mingi lakini hakuamini kama utani imeisha.
“Hongera Mwanangu,utakuja lini baba?”
“Kesho tu”
“Karibu sana mwanangu,ngoja niongee na Baba yako tukutumie nauli”
“Ahsante Mama”
*******
Mikakati waliyopanga baada ya chuo kufungwa ilikuwa ni lazima waitimize,ndiyo maana baada ya siku tatu kufika.Florian na Hajrath wakafunga safari mpaka jijini Dar es salaam,ilikuwa ni siku ya kipekee kwa Hajrath kwani ndiyo siku ambayo alitaka wazazi wake wamtambue Florian.Aliamini akifanikisha hilo mambo mengine yangekuwa ganda la ndizi yaani mtelezo,wakiwa katikati ya safari ndani ya basi walizungumza mengi.Hatimaye jioni ya siku hiyo walishuka Kimara wakawa wamefika salama salmin,wakachukuwa taxi iliyowapeleka moja kwa moja mpaka nje ya nyumba ya Mzee Mpilla.Haikuwa rahisi kupotea sababu mzee huyo alijulikana kwa ukorofi na utata sifa hiyo ilimpa umaarufu.Walivyoingia ndani walikaribishwa na Mama,ambaye alionekana alikuwa ni mwenye furaha kuliko kawaida kumuona binti yake,kilichomfanya asite kidogo ni baada ya kumuona Hajrath ana ugeni.
“Shikamoo Mama”
Florian,alisalimia kwa adabu zote baada ya Hajrath kutoa salamu.
“Marahaba,hujambo?”
“Sijambo Mama”
“Karibuni”
Baada ya hapo,Hajrath na Florian wakaingia ndani.Ambapo hapo Mama Hajrath alizama mpaka chumbani ili kumpasha habari mumewe ya kwamba kuna ugeni.
“Nani?”
Mzee Mpilla akauliza,akiwa kitandani amepumzika baada ya uchovu wa kazi zake.
“Mwanao Hajrath,kaja na mgeni”
“Mgeni gani?”
“Baba Hajrath,si ukamuone kwanza”
Hapo hakuweka kipingamizi,akasimama na kuvaa suruali,akatungua shati lake!Akaweka mwilini,akatoka! Mkewe akaunga mkia wakatokeza seblen!Hajrath na Florian walivyomuona,wakasimama wima na kusalimia.Mzee akaitikia,wote wakakaa kitako!Kufuatia hapo,ukimya ukatawala.
“Baba na Mama”
Hajrath,akavunja ukimya na kuwaita wazazi wake, ambapo hapo walitega masikio yao ili wasikilize!
“Huyu anaitwa Florian,ni rafiki yangu.Tumeona sio uungwana akaenda likizo bila kupita hapa,nikamuomba kuja kuwasalimia”
Hajrath,akazunguka mbuyu kidogo ili apunguze ukali wa maneno.
“Mama,baada ya kumaliza chuo najua nitaolewa namimi nitaanza safari ya maisha!Maandiko yanasema,utawaacha wazazi wako na kuambatana na mumeo,huyu ni mchumba wangu”
Mzee Mpilla,akatulia kidogo na kushusha pumzi ya ndani kwa ndani,akamtizama Florian kwa kitambo na kurudisha macho yake kwa Hajrath.
“MPUMBAVU!!”
Mzee Mpilla,akatoa tusi kwa hasira na sauti kubwa.
“Una akili wewe Hajrath?Huo upuuzi sitaki kuusikia,kijana toka nje!”
Mzee Mpilla alikema kwa hasira,macho yake yalibadilika rangi.Hakuna hata mmoja kati yao, aliyeelewa kwanini mzee huyo, kapandisha maruwani namna hiyo.
Hali haikuwa nzuri hata kidogo,seblen.Mzee Mpilla aliwaka na kurusha matusi makali kupita kiasi, akimtizama Florian kwa macho makali ya chuki,yaliyojaa hasira na gadhabu.Akitaka mwanaume huyo apotee ndani ya sekunde sifuri la sivyo angepewa kesi ya mauaji.Sio Hajrath wala Mama yake,hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa tayari kukubaliana na hali inayotokea,kilikuwa ni kitendo cha kuogopesha ukizingatia mwanaume huyo ni mara yake ya kwanza kukanyaga ndani ya nyumba hiyo.Hata yeye Florian, alihisi mgongo wake umepigwa na ubaridi mkali,hakuelewa ni kitu gani akifanye ukweni kwani miguu yake ilikufa ganzi,kusimama hawezi achilia mbali kujitetea kwa kuongea!
“Kijana ondoka,sitaki kesi ya mauaji nikafungwe.Hajra,kama unampenda huyo kijana mtoe haraka.Sitorudia tena”
Mzee Mpilla alizungumza kwa sauti ya juu zaidi kupita ya mara kwanza,baada ya kuhitimisha hayo akachomoka kwa kasi na kuingia katikati ya kordo,mlango wa chumbani kwake ukasikika ukifunguliwa.Bado kila mtu alikuwa amepigwa na bumbuazi,Mzee huyo alikuwa ni mkali kuliko pilipili mbuzi hasa linapokuja swala la binti yake,alikuwa yupo radhi kufanya chochote kumtetea.Kilimchompandisha morari zaidi ni kitendo cha kusikia tetesi ya kwamba mwanaye alitaka kunywa sumu kisa mwanaume,hakuwa anawaza chochote kichwani zaidi ya kutafuta panga lake refu ambalo lina makali kotekote,kwa hasira alizokuwa nazo chochote kibaya kilikuwa mbeleni kutokea,akainama na kuingiza mkono chini ya uvungu wa kitanda, akaanza kupapasa papasa,akaligusa.Akasimama nalo mzimamzima.Kwa kasi akaufungua mlango!
“Bado upooooo?”
“Baba Hajra….”
Mkewe,alishaelewa hali ilikuwa tete,Upepo ulikuwa ni mbaya,ndiyo maana akasimama ili kumzuia lakini ilishindikana kwani panga lilirushwa usawa wa Florian,hata hivyo ilikuwa bahati mbaya kwake na nzuri kwa Florian kwani kitendo cha kusimama kwa niya ya kulikwepa, lilipiga juu ya kochi kumaanisha asingefanya hivyo lingemfikia usoni na kumchana vibaya sana.Hapo ndipo akajua hakukuwa na mzaha hata kidogo na angeendelea kubaki angecharangwa mapanga,kama ngedere Florian akauparamia mlango na kutoa mbio ndefu,akiwa anatetemeka kwa hofu.
“Mpumbavu mkubwaa,ningekuuwa kenge wewe!Malabuku”
Kifua cha mzee huyu kilipanda juu na kushuka,pua zake zilimcheza hiyo ilikuwa ni hasira ya kiwango cha juu kabisa.Hajrath alilia machozi,makamasi yalimtoka mfululizo.Kitendo alichokifanya baba yake mzazi kilikuwa ni cha kinyama,mwanaume anayempenda kuliko wote chini ya jua,leo hii anakimbizwa kama ameiba vile.Akahisi kama kuna lidudu limemkaba kohoni,hiyo ilikuwa ni hasira kali sababu ilipelekea akashindwa mpaka kuongea,akabaki anamtizama baba yake kwa chuki!
“Baba....na..kuchukiaaa”
Hajrath,akazungumza huku akibubujikwa na machozi.Licha ya kuwa na hasira za mkizi lakini hakuweza kubadilisha chochote kile,alivyotaka kutoka nje ya geti baba yake alimzuia na kumrudisha ndani.
Siku hiyo kwake ilikuwa ni siku mbaya kuliko zote,moyo wake ulivuja damu.Alichofanya ni kunyoosha mpaka chumbani kwake,akabamiza mlango kwa nguvu.Huko alijitupa kitandani na kuendelea kulia,hakuelewa ni kwanini baba yake mzazi anamfanyia unyama wa namna hiyo!Akiwa katikati ya majonzi makali,akahisi mlango wa chumbani kwake unafunguliwa.
“Hajrath mwa….”
“Ma….am niacheee”
“Naomba nisikilize kwa makini”
“Ma..ma nim..esema siwe..zi,naom..mba uniache”
Mama,alijawa na huruma mbali na kelele za kufukuzwa na mwanaye,akasogea mpaka karibu ya kitanda.Akakaa kitako na kumvuta binti yake karibu,hapo akapata kibarua cha kumbembeleza na kumpa maneno ya faraja,hiyo ndiyo ilikuwa kawaida ya Wamama wote duniani lakini kwa mama huyu,upendo wake ulizidi kwani hata yeye alitamani kulia lakini alijikaza.
“Baba yako,hakuamka vizuri leo”
Mama akazidi kumlainisha mwanaye,hayo yalikuwa ni maneno tu ya kumpa matumaini kwanza na alikuwa ana kila sababu ya kufanya hivyo!
“Kwa..nini anifanyie mi..mi hivi?”
“Ni hasira tu,leo hakuamka vizuri,nitaongea naye”
“Una..mtetea,ndio alivyo!Naku..mbuka hata Kwa Ramla ilikuwa hivihivi,kwanini la..kini?”
Hajrath,alizungumza kwa kwikwi na hasira huku akivuta kamasi,tabia ya baba yake aliilewa ndiyo maana akamkumbuka binamu yake anayeitwa Ramla,ambaye alilelewa katika familia hiyo,alivyoleta mwanaume alitolewa mkuku!
“Na..mimi nitatoroka kama Ramla”
“Usifanye hivyo mwanangu,baba yako anafanya hivyo sababu anakupenda”
“Sio kwe..li Ma..ma,nampenda Yule mwanaume.Au anataka anioe yeye?”
Hajrath aliropoka sentensi hiyo kwa hasira bila kuichuja, japokuwa mama yake alichukia lakini hakutaka kulionesha jambo hilo waziwazi,akaendelea kumtuliza akamfuta machozi kama mtoto mchanga anavyofutwa machozi na Mama yake,hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Kutokana na uchovu wa safari pamoja na misukosuko ya hapa na pale usingizi mzito ukamchukua!Saa moja ya jioni ndipo alipokurupuka kutoka kitandani,kitu cha kwanza kukikumbuka ni tukio zima lililotokea siku hiyo.Sura ya Florian,akikimbizwa kama mwizi, ikampitia kichwani akawa kama anatizama sinema mbaya ya kutisha,moyo ukaanza kumuuma upya!Kuendelea kubaki kitandani kusingebadilisha chochote,akatoa shuka na kushuka kitandani, akanyoosha mpaka seblen ambapo huko alichukua simu yake!Japokuwa alimuona Baba yake,ametanda juu ya kochi hakumsemesha,akabeba simu na kuingia chumbani kwake ambapo huko alianza kumtafuta Florian ili ampigie na kumuomba radhi kwa kila kitu kilichotokea,alielewa fika ni kwa namna gani, mwanaume huyo atakuwa amekasirika vya kutosha,hivyo kabla ya yote ilikuwa ni lazima ampe kisomo kwanza!Moyo wake ulipiga kwa nguvu baada ya kusikia simu haipatikani,akajaribu tena lakini hali ilikuwa ileile.Jambo hilo likazidi kumvuruga akili yake vya kutosha,hakutaka kukubaliana na jambo hilo,akajaribu tena na tena lakini hali ilikuwa ni ileile.Taa jekundu inayoashiria hatari, ikaanza kuwaka kichwani kwake wenda Florian,amekasirika na hataki kumsikia tena lakini upande wa pili wa nafsi ulimwambia wenda simu yake imezima kwa kukosa chaji,hapo ndipo wazo la kwanza akalitupilia mbali,akiliita la kishetani.
*******
“Shikamoo Mama”
“Marahaba,chai ipo mezani”
“Ahsante”
“Wewe Hajrath”
“Abee Mama”
“Baba yako,hujamuona au?”
Huo ndio ulikuwa ukweli wa mambo,Hajrath na Baba yake walikuwa ni kama mtu na mke mwenza!Hawakusemeshana.Hajrath, hakutaka kumuongelesha baba yake,hata kama angepishana naye mlangoni ama kukutana naye seblen.Bado alikuwa ana hasira naye!Hiyo ndiyo ilikuwa sifa ya Hajrath,kununa nuna!Tabia hiyo ilitokana na kudekezwa sana na Mama yake mzazi.Kwa mzee Mpilla kwake ilikuwa ni shwari tu,hakuwa ana habari yoyote ile ndio kwanza alikuwa ameshika gazeti,anasoma kwani alichokifanya aliamini ni sahihi kwa Baba anayempenda binti yake!Kununiwa na binti yake,hakukumfanya ashindwe kufanya shughuli nyingine za kutafuta mkate wa kila siku, alichohakikisha tu familia yake inakula vizuri.
Kama Hajrath,angekuwa ana uwezo angeondoka nyumbani hapo lakini jambo hilo,halikuwezekana habadani.Mbali na kununa ama kukasirika lakini hakutaka kuwavunjia wazazi wake heshima kwa kutoroka.Aliendelea kumtafuta Florian kwa njia ya simu bila mafanikio ya aina yoyote yale.Akatamani,chuo kifunguliwe ili akakutane naye lakini badala yake,siku zilijisogeza kwa mwendo wa Ajuza!
******
Kichwa chake,kilikuwa kinatizama ukuta!Amejibinua kwa nyuma akiwa ameshika meza,kwa mbali anazungusha nyonga yake!Yu uchi wa mnyama,kiuno chake kimeshikwa vizuri.Jambo lililokuwa linaendelea hapo hata kama ulikuwa hujui kusoma kwa picha tu,ungeelewa!Kifupi walikuwa katika shughuli pevu na aliyemshika nyuma yake ilielekea alikuwa fundi wa michezo hiyo ya chumbani,kwani alimshika vizuri mguu wake mmoja na kuuweka juu mezani,akazidi kupeleka majeshi majeshi.
“Ka..ssiim aaaaah”
Msichana huyu maji ya kunde,alitaja jina hilo bila kutarajia,ilielekea alikuwa amekunwa barabara.Kassim ama kwa jina lingine tajiri wa Mahaba,aliongeza njonjo!Akawa anazungusha kiuno chake,ndani kwa ndani.
“Aaaah aaaah,beiibiiii ilove yuuu”
Mrembo,huyo alishindwa kuvumilia akajikuta anazungusha shingo yake na kutoa ulimi,wakaanza kunyonyana ndimi,akabebwa kutoka ukutani na kutupwa kitandani puu!Mambo yakaendelea,alipopagawa zaidi ni kitendo cha muwa kuwa ndani ya ikulu yake huku ulimi wa Kassim ukiwa juu ya chuchu zake,hapo ndipo akahisi kama roho yake inataka kuacha mwili.Akazidi kumng’angania kwa nguvu,akimvutia kwake hiyo ilimaanisha kwamba tayari anakaribia kufika Kigoma,mwisho wa reli.Hakuchukuwa sekunde hata mbili,akawa chali katulia!Kassim,hakutaka kuchelewa nayeye akasawazisha wakawa wamefika wote!Mbali na kufika mshindo lakini alitulia juu ya kifua cha mrembo huyo,gari ikiwa bado imepaki ndani.
“Bebiiiii,nani anakufundisha hivi?”
Msichana huyo aliyekuwa ana sura ya kitoto,ama mdoli aliyefahamika kwa jina la Habiba ilibidi ahoji kwanza sababu dozi aliyopewa na Kassim,ilikuwa ni moto wa kuotea mbali!
“Sijui,wewe ndio umenifundisha”
“Kwenda zakoo”
Hiyo ndio ilikuwa siku yao ya kwanza kuzini tangu mahusiano yao yaanze,Habiba!Akatoa sifa zake zote na hilo hakutania,Kassim alikuwa fundi na mtundu kitandani tofauti na wanaume wake aliowahi kukutana nao kipindi cha nyuma.
“Darling naondoka”
“Unaenda wapi tena love?”
“Kumpokea Broo!Si unajua,anakuja leo.Si ajabu atakuwa tayari keshafika”
“Anatokea wapi?”
“A town”
“Arusha?”
“Ndio”
“Basi,utanidrop Shekilango hapo”
“Poa,twende tukaoge basi”
Kassim na Habiba,wakatoka kitandani na kuingia bafuni ambapo huko pia walianza kuchokozana mwishowe wakaingia tena kweye mchezo wa mapenzi,baada ya hapo walivaa na kuingia ndani ya gari.
Kitendo cha kuliwasha,simu ikaanza kuita na aliyekuwa anapiga hakuwa mwingine bali ni baba yake!
“Ushafika Ubungo?”
Hilo ndilo swali la kwanza kuhoji,mzee huyo simuni.
“Hapana Baba”
“Mpaka sasa hivi?Ulikuwa wapi?Nahitaji gari hilo sasa hivi,fanya haraka kampokee kaka yako.Straight mje nyumbani”
“Sawa baba”
Kuanzia hapo,ilibidi aongeze mwendo wa gari.Alivyofika Shekilango akamteremsha Habiba kisha kusonga mbele na safari,alivyokaribia Ubungo akakunja kushoto moja kwa moja kwenye ofisi za mabasi ya kampuni ya Kilimanjaro na hilo ndilo basi aliloambiwa kwamba Kaka yake,Ahmed ndio amepanda.
Alivyopaki gari na kushuka akatupa macho huku na kule.Kwa mbali alimuona kaka yake,akatabasamu na kumuendea kwa kasi.
“Broo shikamoo….”
Kwa furaha wakakumbatiana na kupiganapigana migongoni,hao walikuwa ni mtu na mdogo wake.Japokuwa walipishana miaka saba lakini walikuwa kama watoto mapacha sababu walipendana mno,mbali na hapo walizaliwa wawili tu kwa baba na Mama,hivyo walikuwa wana kila sababu ya kuoneshana upendo wao waziwazi.Mbali na baadhi ya tabia zao kufanana lakini Kassim alikuwa ni tofauti kabisa kwani alipenda sana sketi,hiyo ilimfanya mpaka ashindwe kufanya vizuri kidato cha sita.Alifeli,lakini hakukoma staili yake ilikuwa ni ileile kuwachanganya wanawake kama pilau na kachumbari,hakuna mtu aliyejuwa tabia hiyo karithi wapi kwani kaka yake pamoja na wazazi wao wote hawakuwa na tabia kama hiyo ya umalaya,alikemewa na kupelekwa mpaka msikitini wakidhani wenda ana pepo la ngono lakini hiyo haikusaidia,Kassim aliendelea kufunua sketi za kina dada, mwanzo mwisho!
“Karibu Bongo”
“Ahsante dogo,umekuja na nani?”
“Nipo mwenyewe”
“Maza yuko wapi?”
“Home”
“Dingi?”
“Wote wapo home,wanakusubiri kwa hamu,umeniletea nini kwanza?”
“Baadaye tukifika home,nina mizigo mingine ipo kule”
Mchakato wa kuanza kubeba mizigo na kuingiza ndani ya gari ukaanza hapohapo!Ahmed,alijawa na furaha sana kurudi nyumbani salama akiwa amemaliza elimu yake ya ngazi za juu,alitamani kufika haraka nyumbani aungane na wazazi wake!
******
“Ulifanikiwa?”
“No baby”
“Sasa unasubiri nini?”
“Namvuta karibu,ajae kingi.Ndio iwe rahisi kuanza”
“Unadhani bado hajakolea,au humpi dozi ya kutosha?”
“Tayari, nadhani unanijua mimi kitandani sibahatishi,niachie mimi Darling”
“Muda unakwenda lakini baby”
“Naelewa,mambo mazuri hayataki haraka!Mambo yakiwa tayari,mwenyewe utapenda.Binti mwenyewe anaitwa Hajrath”
“Najua,ushawahi kuniambia.I love you,kuwa makini.Nasikia wivu lakini.Tambua hilo”
“Sipendi iwe hivi lakini sina jinsi,nakupenda sana!”
“Mimi pia”
Amini usiamini,Florian ndiye alikuwa hewani anazungumza na mpenzi wake shombeshombe aliyekuwa nje ya nchi,kupitia mtandao wa ‘skype’ wanaonana.Na ilikuwa wazi kabisa waliyekuwa wanamteta hapo hakuwa mwingine bali ni Hajrath Mpilla.
Mawasiliano kati ya Florian Fredrick na mwanamke huyo shombeshombe mrembo, aliyefahamika kwa jina la Sporah Treves,yalizidi kupamba moto.Na kila siku walizidi kufanya hivyo ili kukamilisha adhma yao,mbali na hapo maongezi yao yalitisha, kupita kiasi.Ilifika kipindi Sporah alimuhadithia Florian unyama anaoufanya kama akihisi kuna mtu anataka kumuingilia kwenye biashara zake.
“Unamkumbuka Mackdonald?”
Sporah siku hiyo aliuliza simuni.
“Mackdonald yupi?”
“Tulivyokuwa Mogadishu,unamfahamu bwanaaa.Mrefu maji ya kunde,alikuja na gari moja kali sana!Ukasema umelipenda,Rolls royse”
“Nishamkumbuka tayari,si alikuwa ana ndevu nyingi sana, sio muongeaji. Kama paroko?”
“Exactly,Yule mpaka leo.Anatafutwa haonekani”
“Ulimfanya nini?”
“Usicheze namimi.Yule hata kama watokee FBI kutoka sayari ya Pluto,hawatoweza kujua alipo wala kupata mabaki yake”
“Yuko wapi kwani?”
“Hata mimi sijui alipo vilevile,sijui atakuwa majivu ama ameliwa na simba wangu”
Mbali na urembo wake asilia lakini mwanamke huyu ndani ya moyo wake alikuwa ni zaidi ya shetani mwenye mapembe marefu,sababu unyama aliokuwa anaufanya hata shetani mwenyewe huko kuzimu alimvulia kofia,Sporah alitisha mno!Yeye swala la kuuwa ilikuwa ni sawa na kuweka kikombe cha supu mdomoni.Na sio kuuwa peke yake,aliuwa binadamu wenzake kiukatili hakuwa muungwana katika swala hilo, yeye kumtoboa mtu tumbo na kunyofoa figo pamoja na maini lilikuwa ni kawaida kwake,alichojali yeye ni maslai yake ya pesa kwanza.Sporah, alikuwa gwiji wa kuuza madawa ya kulevya aina ya Coccaine na Herroiene!Alisafiri nchi mbalimbali kama Afghanstan,Mexico,Uingereza,Somalia mpaka Afrika Kusini huko kote alisambaza mawakala wake,alitumia akili kubwa sana katika biashara hiyo haramu ambayo kwa siku ilimuingizia sio chini ya dolla elfu moja za Kimarekani.Akavuna pesa nyingi sana, ndipo baadaye akaunda kikundi kingine alichokiita ‘Black Monsters’ndani ya kundi hilo kulikuwa na wafanyabiashara wakubwa pamoja na wanamuziki maarufu mbalimbali ambao hao aliwatumia kupitisha madawa ya kulevya,akaona haitoshi akatanua kampuni yake, akitumia matumbo ya watu kubeba kete za madawa.Meneja wa tawi hilo la kubeba kete kwa kutumia tumbo alikuwa ni Florian,ambapo Mwanzo walikuwa kama marafiki lakini baadaye wakawa wapenzi,Sporah alimpenda sana Florian!Aliamini ingekuwa rahisi kumvuta mtu yoyote karibu hususani wanawake,sababu mwanaume huyo alikuwa mzuri wa sura na ilikuwa wazi kabisa akitongoza tu ni lazima mwanamke ajae kingi.
Mwanamke wa kwanza kumtongoza ilikuwa ni Mkoani Mbeya huko Kyela,baada ya siku tatu mwanamke huyo akapotea katika mazingira ya kutatanisha.Kijiji kikatoa taarifa polisi lakini haikusaidia kwani walimtafuta bila mafanikio,baada ya hapo Florian akahama kambi na kuibuka mkoani Mwanza,akaweka kambi CCM Kirumba,akatega mtego wake na kumuopoa mwanamke wa Kisukuma akawa anamuhonga pesa nyingi.Mwanamke huyo baada ya mwezi mmoja,akapotea vilevile,likatokea gumzo kubwa sana sababu alikuwa ni mtoto wa Mwenyekiti wa Kitongoji lakini hiyo haikusaidia.Alivyoona msako ni mkali na wangemshtukia akapanda ndege na kuingia jijini Dar es salaam huko akanyuti kidogo kujificha.Hakukaa sana,akaopoa kigoli mmoja akaingia kwa gia ya mapenzi ya dhati ili kumlewesha zaidi akamtangazia mpaka ndoa,kwa miyadi ya kwamba wangeenda Afrika Kusini kula kuku kwa mrija lakini matokeo yake,akadungwa sindano na kuchanwa tumbo lake,akapakiwa kete gramu hamsini za Madawa ya kulevya,alivyofikishwa Jijini Cape Town nchini Afrika Kusini,wakapakua mzigo na kuupeleka Somalia.Tangia Florian awe meneja katika kitendo hiko,alimuingizia Sporah kipato kikubwa sana,mapenzi yakaongezeka ikawa kila mwisho wa Mwezi ni lazima wakajipongeze nchini Marekani,mbali na Florian Fredrick kuwa makini katika biashara hiyo lakini alikuwa anajituma kitandani,baada ya kuingia Tanzania,akafikia jijini Arusha hapo akaomba nafasi chuo cha Makumira ili afanye kazi yake tena ya kuwanasa warembo.Bila kujisumbua msichana anayeitwa Hajrath Mpilla,akawa amejaa mwenyewe ndani ya kumi na nane zake,akajifanya kumpenda sana na kuonesha kila ukarimu.Akamlewesha msichana huyo kwa mapenzi ya kufa mtu na kufanya kila jambo kumpagawisha,hatimaye akajaa kingi.Akichokuwa anasubiri ni kitu kimoja tu,amfanye Hajrath Mpilla kama kontena la kubebea kete za madawa ya kulevya.
*******
Moyo wa Hajrath bado uliwaka moto,aliumia mtima.Akakosa raha ya maisha kabisa,kitendo alichokifanya baba yake kilimfanya amchukie kupita kiasi, mbaya zaidi Florian hakupatikana hewani kwa takribani wiki moja sasa,hiyo ilimfanya apungue uzito kwa kiasi cha kutosha.Aliamini kivyovyote ni lazima Florian alimuacha kwenye mataa na kama ingekuwa ni kweli aliapia kutokumsamehee baba yake kwani ndiye mkandarasi wa kila kitu kutokea,kitendo cha kukosa raha kilimfanya Mama yake pia akose usingizi usiku.Kila wakati alijaribu kumsihi binti yake arudi katika hali yake ya kawaida lakini hiyo ilikuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu yasagike.Hajrath,hakuelewa lolote sababu bila Florian aliamini ilikuwa ni sawa na basi bila konda ama gari bila mafuta.
“Mme wangu”
Siku hiyo Mama alimuita Mumewe katikati ya usiku wakiwa kitandani wamelala,Mzee Mpilla badala ya kuitikia alimgeukia mkewe.
“Kuna nini?”
“Hajrath,hana raha kabisa”
“Kwanini hana rahaa?”
“Hujui?”
“Kuna nini Aisha?Ebu niambie unachotaka kuniambia”
Mzee Mpilla alipenda kumuita Mkewe jina halisi kwasababu moja tu,hakutaka kumzeesha mkewe kwa kumuita mama fulani.Aliamini kabisa mkewe bado analipa na alijisikia raha kwa kumuita jina lake.
“Kuhusu Yule kijana aliyekuja naye”
“Kafanya nini?”
“Ulichofanya sio vizuri,kumfukuza namna ile”
“Kama ndio hivyo,niache nilale.Nina usingizi nimechoka Aisha.Naomba uliheshimu hilo”
“Lak…”
“Tafadhali,kama hauna swala lingine la kuzungumza.Lala nisije nikakuharibia usiku wako,sitaki tufike huko”
Mzee Mpilla aliweka nukta sentensi yake,akageukia ukuta kisha kuvuta shuka,akapotelea usingizini.
*******
Alikuwa ni mzee mrefu kwenda hewani,ndevu zake nyeupe kiasi.Sio mnene sio mwembamba ni wastani tu.Alifahamika kwa jina la Mohamed Kajeme,kazini walizoea kumwita ‘Captain’ japokuwa hakuwa nahodha wa meli.Baadhi ya wafanyakazi ambao hawakumzoea walimuita Mkuu,hiyo ni kutokana na madaraka yake kazini kwani alikuwa ni polisi katika kitengo cha upelelezi.Mzee huyu alipenda sana kuswali na siku zote alitenda haki katika kazi yake,hakupokea rushwa hata kidogo hiyo ilimfanya ajenge uadui mkubwa sana na wafanyabiashara waliokuwa wanaingiza magendo nchini.Figisu zikawa kubwa akahamishwa mkoa na kupelekwa jijini Dar es salaam, akitokea mkoani Tanga,yeye pamoja na familia yake wakaanzisha makazi mapya jijini hapo.
Lakini swala lilikuwa ni lilelile,hakupokea rushwa na kutingishwa na pesa.Kumuhamishia jijini Dar es laam wakiamini kwamba wamemkomoa kumbe ilikuwa ni sawa na kumpiga chura teke,kwani baada ya miaka mitatu akapata fursa na kupandishwa cheo kutokana na uchapakazi wake hodari,ilikuwa ni furaha sana kwake.Hakuna siku ambayo alikuwa anaisubiri kwa hamu kama hiyo,Mwanaye Ahmed mtoto wake wa kwanza kuhitimu masomo yake ya ngazi za juu.Ndiyo maana siku hiyo hakutaka kwenda popote pale,akamwambia mkewe atafute mbuzi mzima achinjwe nyama nyingine ipikwe kama mboga nyingine ichomwe nyumbani.Hiyo ikiwa kama ishara ya kumpongeza mwanaye akimshukuru kwa kuwa mvumilivu kwani vijana wengi ama watoto wa marafiki zake, waliishia katikati na kuwa wavuta bangi,kwake yeye akajisikia furaha sana.
Kitendo cha kusikia honi getini alisimama wima na kuundea mlango huku nyuma mkewe akiunga mkia,walijua sana ni lazima atakuwa Ahmed na dereva alikuwa ni mtoto wake mwingine,Kassim.Geti lilivyofunguliwa na mlinzi,gari likaingia ndani.Kitendo cha Ahmed kushuka ndani ya gari.Mama akashindwa kusubiri akakimbia kwa kasi na kumrukia mtoto wake wakadondoka wote mpaka chini,mama huyu alikuwa mwenye furaha ya ajabu.
“Hongera mwanaaangu”
Mama alimpongeza mwana kwa furaha huku akilia machozi,japokuwa hakujua niya mwanaye kumaliza chuo kikuu ama furaha ya kumuona.Mzee Mohamed Kajeme nayeye akasogea karibu,wakakumbatiana huku akimpiga piga mwanaye mgongoni.
“Hongera Son,hongera sana Ahmed.Karibu ndani”
Sio siri Mzee Kajeme ulikuwa umwambii kitu kwa Ahmed,aliamini huyo ndio siku moja atakuja kusimamia vitu vyake endapo kama siku moja hatokuwepo duniani ama akizeeka, ndio maana alijinyima na kuomba mikopo mbalimbali benki ili mwanaye asome mpaka chuo kikuu atoe ujinga,akiamini kila kitu kitaenda sawa.Siku hiyo ilikuwa ni furaha sana,walikula na kunywa!
“Karibu mtaani”
Baba akavunja ukimya huku akiwa na kipande cha nyama choma mkononi.
“Ahsante Baba”
“Una mpango gani baada ya hapo?”
“Kuanza kutafuta kazi”
“Hapana mwanangu,kuna kitu nataka kukushauri kwanza”
“Kitu gani baba?”
“Nataka ukasome Masters,unajua mwanangu hakuna kitu kizuri kama kuwa na elimu ya juu.Mimi baba yako sikupata bahati ya kusoma,niliishia form four lakini ningepata mtu wa kunisomesha,ningesoma mpaka PHD”
“Lakini baba,ngoja kwanza nitafute ajira kidogo”
“Sijakataa na wala sijakulazimisha,ni mawazo tu.Kwanza mtoto wa kiume unatakiwa uwe umejikoki,mtu akikukugusa huku humo.Kule humo,unakuwa na vyeti vyote”
“Sawa baba,nimekuelewa”
Kilichofuata hapo ulikuwa mlio wa sahani na vijiko kugongana,wote walikuwa wakijichana.
*********
Kila kitu kilipangwa hatua kwa hatua,mpango wa kupakia kete za madawa ya kulevya ndani ya tumbo la Hajrath ulikuwa tayari ushasukwa vizuri .Hiyo ni baada ya Florian Fredrick, kusafiri mpaka nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya kikao kidogo lakini kizito na mpenzi wake ama bosi wake, Sporah Treves.Ndani ya hotel ya nyota tano, mrembo huyo alikuwa amewekwa mbuzi kagoma kwenda majanini,Florian yupo nyuma yake anamshughulikia kama kawaida,raha alizokuwa anahisi alitamani mpaka kumkabidhi dunia nzima iwe ya Florian.Mwanamke huyu alikuwa gaidi kuliko Idd Adim dada lakini kiboko yake alikuwa ni Florian,hakujiweza tena kwa mwanaume huyo, ambaye kitandani alikuwa ni moto wa kuotea mbali.Alipopagawa zaidi ni baada ya kulazwa kifudifudi yaani kalalia tumbo huku Florian akiwa juu yake,kama ungeangalia vibaya ungedhani wenda Florian anafanya vitu ambavyo Mungu aliiteketeza kwa moto somola na gomola lakini haikuwa hivyo kwani mashine yake haikuwa uwani, ilikuwa mlango wa mbele,Sporah Trevez alikuwa hafanyi kitu zaidi ya kuguna na kutoa mihemo ya ndani kwa ndani,mara avute mashuka mara amkwaruze Florian mgongoni ilimradi vurugu tupu.Mtanange huo uliisha lisaa limoja baadaye,kila mtu akabaki kumsifia mwenzake.
“Florian nakupenda sana”
Sporah Trevez alideka huku akiweka nywele zake ndefu za singasinga vizuri,akalala kifuani kwa Florian.
“Hata mimi mtoto mzuri”
“Mimi sio mzuri”
“Wewe ni mzuri,sijaona kama wewe.Mtoto mlaini kama umeumbwa kwa pamba”
“Ha!Haa!Haaa!Hajrath je?”
“Hajrath kafanya nini?Unajua kabisa,namfanyia usanii.Tupige pesa!Arafat anasemaje?”
“Anasubiri kete zake,yupo Sudan sasa hivi.Akitoka huko nitakuwa naye Comoro kuonana naye”
“Sawa baby”
“Kuwa makini,make sure ukifika unawasha simu.Nina uhakika Hajrath anakutafuta sana”
“Najua hilo,nikiingia leo nawasha simu”
“Kuwa makini baby,nitakumisi sana ujue. Uchunge utamu wangu mademu wa kibongo wasije kukuchanganya ukasahau biashara”
Baada ya hapo, Sporah akasimama na kumkabidhi Florian kitita cha dola za kimarekani elfu nne ambazo kwa Tanzaina ilikuwa ni zaidi ya shillingi milioni saba,hizo zingetosha kabisa kuwalaghai wanawake wa kibongo ambao siku zote walipenda pesa kuliko kitu chochote kile.
“Good luck sweetheart”(Kila la kheri Mpenzi)
Waliagana siku hiyo kwa mabusu mengi yasiyokuwa na idadi kamili,Florian alikuwa tayari keshavaa, begi mkononi kwa kazi moja tu,kurejea nchini Tanzania jijini Dar es salaam na kumlaghai Hajrath kwa njia ya mapenzi kisha baadaye amtumie kama kontena la kubebea madawa ya kulevya baada ya hapo,amuuwe na kumtupa popote pale ili asionekane!Shirika la ndege ya Ethiopian Arlines ndio alikata tiketi siku hiyo mchana,akiamini ndege hiyo ingemfikisha Tanzania uwanja wa ndege Mwalimu Nyerere.
Akiwa ndani ya ndege Florian aliwaza vitu vingi sana,alitafakari mambo chungu mzima kichwani hususani Hajrath, ambaye alitakiwa kumuuwa hapo baadaye,moyo ulimuuma lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kufanya kazi yake wala hakutaka kurudisha moyo wake nyuma.Saa moja jioni siku hiyo, ndege ya shirika la Ethiopian Airlines, lilifungua matairi yake na kukanyaga uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es salaam.
Ikatingishika kidogo na kukaa sawa,ambapo hapo ilienda kwa kasi ya kimondo na kisha baadaye kusimama taratibu mpaka kwenye maegesho yake.Gari maalum lililobeba ngazi likasogea mpaka mlangoni.Florian akashusha pumzi kidogo na kusimama ambapo alichukua begi lake dogo lililokuwa juu sehemu maalum,hakuwa ana mizigo mingine.Kitendo cha kutoka nje ya uwanja,akawasha simu nyingine yenye line ya Tigo,alichosikia ni msululu wa meseji na robo tatu zilitoka kwa Hajrath,hapohapo akampandia hewani.
******
Hakuwa tayari kuamini kama simu yake inaita na aliyekuwa anapiga ni mpenzi wake Florian ama ini mkalia nyongo,ambaye kwa takribani zaidi ya wiki tatu hakuwa hewani kabisa!Akafikicha macho yake na kujipiga kofi ili ni kama ndoto ashtuke,lakini haikuwa hivyo.Hapohapo akapokea na kuiweka sikioni.
“Hallooo”
Upande wa pili wa simu ukasikika,moyo wa Hajrath ukapiga mkambo!Ni kitendo cha kuisikia sauti ya Florian simuni.
“Floriaan!!”
“Yes Darling,how are you?Nimekumiss sana baby”
“Hata mimi Florian,ulikuwa wapi mpenzi wangu?”
“Simu yangu iliibiwa,nilipata msiba honey.Baadaye nitakupigia tuongee nikitulia, bado nipo kwenye matanga”
“Sawa Florian,nakupenda Mwaa mwaa.Nani amefariki lakini?”
“Nitakwambia love,nakupenda sana.Nakupenda kuliko unavyodhani”
Yalikuwa ni maneno matamu yaliyomzuzua akili Hajrath,akajihisi yeye ndiye yeye akajiona kama yeye ni malaika yupo peponi.Siku hiyo baada ya kuongea na simu muda wote alikuwa ana furaha hata kula halikuwa tatizo siku hiyo akala,akawa anasubiri saa ziende kwa haraka ili ifike usiku aongee na Florian wake,bila kujua tayari yupo kwenye mtego mkali sana.
Wazazi wake walimshangaa siku hiyo,ilikuwa ni tofauti kabisa walivyomzoea wiki chache nyuma zilizopita, siku hiyo uso wake ulionesha tabasamu mwanana.Alikula akashiba,akanywa maji mengi akaosha vyombo na kumsaidia mama yake kila kazi jikoni.Mama yake alivyotaka kuuliza alisita kidogo kwa mara ya kwanza, lakini uvumilivu ukamshinda.
“Unaonekana una furaha leo”
Mama akavunja ukimya,japokuwa halikuwa swali lakini Mama alitaka kujua ni kwanini binti yake ana furaha namna hiyo.
“We acha tu mama”
“Namimi nipunguzie furaha”
“Kesho,nitakupunguzia.Acha nikusaidie nenda tu ukalale”
Hivyo ndivyo ilivyokuwa na si vinginevyo!Siku hiyo Hajrath,alifagia jikoni akaosha vyombo,akasafisha meza!Akaenda seblen na kuweka kila kitu sawa,niya yake ikiwa ni kuvuta muda ili usiku uingie azungumze na kipenzi chake,Florian.Mapigo yake ya moyo yalimwenda kasi, hiyo ni baada ya kuingia chumbani na kuona simu yake inaita,akatembea kwa kasi na kuichukua.Mtima wake uchanua tabasamu, baada ya kuona juu ya kioo mpigaji alikuwa ni Florian,akashusha pumzi ndefu kidogo,akaipokea simu na kuiweka sikioni.
“Daaaarling”
Ni Hajrath,ndiye alikuwa ameanza kuita simuni,mwili wake ulimsisimka kuliko kawaida, akisubiri Florian azungumze chochote.
“Honey”
“Nilikumisi sana,nilikuwa nasubiri simu yako hapa, Mpenzi wangu”
“Hata mimi nilikumisi balaa,nilishindwa kukutafuta nilipata matatizo chungu mzima”
“Pole Darling,ndio maisha.Changamoto tumeumbiwa sisi binadamu”
“Ahsante Mke wangu”
Sauti ya Florian ilimfanya asahau kila kitu,hakutaka kuuliza ni matatizo ya aina gani aliyapitia, kazi yake ilikuwa ni kumfariji tu sababu aliamini angemuuliza wenda atamtonesha tena vidonda,siku hiyo walizungumza mambo mengi sana.Hususani mchakato mzima na safari ya mapenzi yao itakavyokuwa.Mbali na kuongea yote hayo Hajrath hakusahau kumuomba msamaha kwa tukio lililotokea la Baba yake mzazi kumtimua kama mbwa,alijisikia uchungu na machozi yalimlenga kwani tukio hilo lilikuwa ni zaidi ya unyama kwake.
“Usijali Hajrath.Baba yako anakupenda sana,hata mimi ningekuwa yeye ningefanya aliyofanya”
“Si..o hivyo Florian,mimi sijapenda”
Hajrath akazungumza kwa kwikwi huku akibubujikwa na machozi.Msichana huyu alikuwa ana mapenzi ya ajabu sana na alikiri mwenyewe kuwa akipenda huwaa,anapenda kweli.
******
Alichokuwa anasubiri Ahmed ni matokeo yake,kama amefaulu ama ana vimeo.Aliomba Mungu matokeo yake yawe vizuri ili aanze mchakato wa kutafuta vibarua vya hapa na pale.Akiwa nyumbani kwao hakutaka kubweteka,alihakikisha kila kitu kipo sawa.Alikuwa akiamka mapema na kuhakikisha kila kitu kipo sehemu husika ndani ya nyumba mpaka nje,kuna kipindi alidiriki kuosha gari la Baba yake kila asubuhi.Akaenda mbali zaidi na kutaka kujua ni kitu gani Baba yake anafanya,kila wakati alitamani kuwa naye karibu.Ndiyo maana akiwa amelala usiku akimsikia amerudi nyumbani basi ni lazima akurupuke kitandani,amfuate seblen huko alitumia muda huo kumdadisi na kumuhoiji maswali mengi tofauti, hususani swala zima la maisha na mambo mbalimbali ya maendeleo.Hiyo ilikuwa ni tofauti na Mdogo wake,Kassim.Huyo hakuweza kukaa na baba yake hata kwa dakika thelathini tu.
“Hivi nikitaka kukupeleka ukawe askari utakubali?”
Baba akatupa swali siku hiyo,wakiwa wanaangalia taarifa ya habari ya saa mbili usiku.
“Sidhani kama nitaweza”
“Kwanini?”
“Nina hasira za karibu sana,isitoshe sio hobby yangu”
“Unataka kuja kufanya nini?”
“Biashara"
“Mfanya biashara?”
“Ndio Baba”
“Kwanini?”
“Basi tu napenda”
“Vipi kuhusu kuajiriwa?”
“Kuajiriwa sikatai lakini mbeleni huko,inabidi nijiajiri mwenyewe”
“Majuzi kuna jambo nilikuambia”
“Jambo gani?”
“Kuhusu kusoma Masters,nina rafiki yangu.Ana staaf baada ya miaka mitatu.Nafasi hiyo itakuwa wazi,ningependa uichukuwe wewe Mwanangu Ahmed,ujue nakutegemea sana”
Kwa Ahmed kuingia tena darasani ulikuwa ni mtihani mwingine mkubwa sana,akamtizama Baba yake kwa umakini kidogo na kushusha pumzi ndefu ya ndani kwa ndani.
“Ngoja nisubiri majibu kwanza”
Hayo ndiyo yalikuwa maongezi ya mtu na baba yake, siku hiyo usiku.
******
Siku zilitembea na kukimbia sana,hatimaye mwezi ukakatika vyuo vingi vikawa vimefunguliwa kikiwemo chuo cha Makumira,kilichopo mkoani Arusha!Mwanafunzi mmoja baada ya mwingine akaanza kuripoti, wale waliokuwa na masomo ya kurudia waliwahi mapema ili kujisomea lakini siku hiyo wengi wa wanafunzi walisimama kwenye ubao mkubwa wa matangazo.Kila mtu alikuwa akikodolea macho makaratasi yaliyobandikwa juu ya ubao huo.
“Ahmed huyu,hii ni 1st class!Kaburuza,wanafunzi woooote.Respect,wa pili huyu demu Beatrice Bigize nuksi sana huyu manzi,bado kidogo tu angemfikia Ahmed”
“Ebu niangalizie jina la Meshack Zackaria”
“Ana sap tatu,kafeli”
“Duu,Mariam Said?”
“Ana sap moja”
“Thomas Michael?”
“Kaka,njoo mwenyewe ucheki unanichosha ujue.Shingo inaniuma”
Juu ya ubao huo kulikuwa na makaratasi yenye majina ya wanafunzi wa mwaka wa tatu, ambao walitakiwa kupewa shahada,katika kundi la wanafunzi hao Hajrath alikuwepo.Alitabasamu baada ya kuona jina la Ahmed lipo kileleni na ameongoza wanafunzi wote.Japokuwa walikuwa hawaongei lakini siku hiyo alihisi kumpigia simu na kumpongeza,ndiyo maana alivyotoka tu pembeni akaanza kuisaka namba ya Ahmed,mbali na kuifuta kwenye simu yake lakini alikuwa nayo kichwani.Jambo hilo lilimshangaza sana kwasababu moja tu,mkataba wake wa mapenzi na Ahmed ulishaisha siku nyingi sana, iweje namba zake awe anazikumbuka kichwani?Siku zote alitamani namba hizo azifute ubongoni lakini ilishindikana.Akatembea umbali wa kama mita kumi na kukaa mwenyewe katikati ya bustani ya maua huku akibonyeza namba fulani fulani,japokuwa alielewa kwa kufanya hivyo ni kosa la jinai endapo Florian akigundua lakini akapiga moyo konde akausikiliza mtima wake,alikuwa tayari keshapanga baada ya hapo afute namba hizo ili usije ukatokea mzozo mkubwa kati yake na asali wa moyo wake,Florian.
“Grii griiii”
Upande wa pili wa simu ulisikika ukiita,kumaanisha ya kwamba namba hiyo ipo hewani.
“Griii griiii”
Kadri simu ilivyoendelea kuita,ndipo mapigo yake ya moyo yalizidi kwenda resi,hakuelewa ni kwanini hali hiyo inamtokea.
“Halloo”
Upande wa pili ukasikika,sauti hiyo haikuwahi kumtoka hata kidogo,alikuwa ni Ahmed mwenyewe!Moyo wake ukalia paa!Kwa nguvu.
“Ahmed”
“Yes,nani anaongea?”
“Hajrath,Hajrath Mpilla”
“Mambo”
“Safi tu,za masiku?”
“Mungu anasaidia”
“Nimekupigia simu,nataka kukupa hongera zako!Umeongoza una first class”
“Ahsante sana Hajra”
“Utakuja kwenye graduu?”
“Sina uhakika,naweza nikaja ama nisije”
“Kwanini,huna uhakika?”
“Basi tu”
“Hii ni siku yako Ahmed,uje ufurahi.Haitoweza kujirudia ujue”
“Sawa,ahsante!Nitajitahidi”
“Siku njema”
Japokuwa Ahmed,alishtuka kupokea simu kutoka kwa Hajrath siku hiyo lakini sio sana kama kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wana uhusiano wa kimapenzi,hiyo ilitosha kusema kwamba hana tena mapenzi naye kwani katika kipindi kifupi alikuwa tayari ametengeneza urafiki wa karibu na msichana anayeitwa Yusrath Suleiman,alikuwa ni binti mdogo!Mweupe wa rangi,ilikuwa ni vigumu sana kuziona nywele za msichana huyu Yusrath Suleiman ambaye kadri siku zilivyozidi kwenda mbele alikuwa akiunyanyasa moyo wa Ahmed.Muda wote msichana huyu alivaa ushungi na alijistili na nguo ndefu,ilikuwa ni wazi kabisa alikuwa ni msichana aliyeshika dini,hakukosa swala hata moja.Swala zote tano,alihudhuria msikitini.Sifa hiyo kubwa ndiyo ilimfanya Ahmed azimike na kujiwekea moja kwa moja huyo ndiye angekuwa mke wake wa ndoa ingawa mpaka wakati huo, hakumueleza ya moyoni!
Mazoea ya Ahmed na Yusrath yalikuwa kwa kasi ya kimbunga,kila siku walizungumza usiku,kilichomfanya Ahmed apagawe zaidi ni sauti ya kimwana huyo,mbali na hapo stori zake siku zote zilikuwa za maendeleo tu.Mara nikipata kazi nitajenga fremu kubwa na kufungua maduka,mara nikipata pesa nyingi nitawekeza kwenye mifugo!Malengo kama hayo yalimfurahisha sana Ahmed,kwani nayeye alikuwa mwenye kiu ya kufanikiwa.
“Mimi nimemaliza Form six”
Ahmed alipigwa na bumbuazi siku hiyo baada ya kusikia Yusrath ni mwanafuzi aliyemaliza kidato cha sita tu,kilichomshangaza sio hiko tu bali mazungumzo yake,hayakufanana na umri wake.Aliamini siku zote wasichana wenye umri kama Yusrath hawakuwaza mengine isipokuwa anasa kwani ndiyo umri ambao vijana wengi huaribikiwa.
“Yusrath,you can’t be serious!”
Ahmed akashangaa,akitumia ung’eng’e kuonesha msisitizo.
“Niko Siriazi Ahmed,sina sababu ya kukudanganya”
“Umemaliza shule gani?”
“Benjamin Mkapa”
“Sasa hivi unafanya nini?Ukiwa una subiri matokeo?”
“Nipo dukani kwa Mama,namsaidia”
“Wapi hapo?”
“Kariakoo,ana maduka ya vipodozi”
“Nice,unapenda kuja kuwa nani baadaye?”
“Mjasiriamali kama Baba yangu”
Siku zote hayo ndiyo yalikuwa aina ya maongezi yao,Ahmed alivutiwa sana na binti huyo.Akapanga siku amwambie ya moyoni lakini moyo wake ulisita,alihofia vitu vingi sana.
“Atanichukuliaje?Mimi ni kama kaka yake,potelea mbali.Ngoja nimwambie ukweli,akinikataa basi.Mimi mwanaume siwezi kuogopa,leo nitamwambia kila kitu”
Siku hiyo Ahmed alikuwa akiwaza namna ya kumuingia Yusrath, amtongoze na kumwambia jinsi anavyoteseka juu yake,kama kawaida usiku ulivyofika akaweka vocha na kujiunga kifurushi, cha dakika nyingi akiamini hizo zingetosha kabisa kumuimbisha,barafu wa moyo wake,Yusrath.
“Nilijua umelala?”
Ahmed,akaanza kuzungumza baada ya salamu za hapa na pale.
“Hapana,nilikuwa naosha vyombo”
“Kwani hamna house girl?”
“Wanini sasa?Wakati mimi nipo”
“Si unachoka lakini?”
“Mimi ni msichana wa kiafrika”
“Nimeipenda hiyo,nikuulize kitu?”
“Niulize tu”
“Shemeji yuko wapi?Hivi huwa haoni wivu,tunaongea usiku kama hivi?Hakuulizi?”
Ahmed,alizunguka kidogo!Hakutaka kuuliza swali moja kwa moja,Mwanaume huyo alikuwa ana akili na auliza swali hilo kwa mtego, hapo angejua kwamba Yusrath ana mwanaume ama hana.
“Kivipi sijakuelewa”
Badala ya Yusrath kujibu swali,nayeye akaibua swali likawa swali kwa swali.Hiyo ilimfanya Ahmed agundue kwamba Yusrath ana upeo mkubwa na alimzidi akili.
“Shemeji,anyway.Una boyfriend?”
Hakuwa na jinsi zaidi ya kuuliza moja kwa moja,ukimya ukatawala wa kama sekunde mbili nzima.
“Halloo”
“Yes Ahmed”
“Una boyfriend?”
“Kwanini umeniuliza hivyo?”
Yusrath akajibu kwa swali.
“Hapana na wala sitegemei kuwa naye”
“Kwanini?”
“Kwa sasa hivi,sitaki kujiingiza huko”
“By the way,tunaweza kuonana Jumapili?”
“Jumapili ipi?”
“Hii inayokuja”
“Nitakujibu kesho naomba nilale”
Sauti ya Yusrath kwa Ahmed ilikuwa ni sawa na kinanda kinachopigwa taratibu kwenye masikio yake,mbali na kujaaliwa uzuri wa sura lakini pia Mungu alimtunukia sauti ya kuimbia Kaswida,hapo ndipo alipom-maliza Ahmed mzima mzima.Kila kukicha hakuacha kumjulia hali huku akisisitiza Jumapili waonane, walau wazungumze mawili matatu,ilikuwa kama bahati kwa Ahmed kwani Yusrath alikubali kuonana naye siku ya Jumapili,lakini kwa sharti moja tu.Hawatokaa kwa muda mrefu.
“Nikitoka msikitini,nitakuona”
“Wapi sasa?”
“Njoo Ilala,mtaa wa Shauri moyo”
“Sawa”
Siku hiyo mapigo ya moyo ya Ahmed yalikita mtindo mmoja,akatamani siku ziende mbele kwa kasi lakini badala yake zilienda kwa mwendo wa ajuza.Furaha ya mahafali yake ya ‘Graduation’ akayaweka kando, shamrashamra zikapungua,hiyo yote ilikuwa ni kwa sababu ya mrembo Yusrath,ambaye tayari kwa wakati huo alitokea kuutingisha mtima wake.Ilivyofika siku ya Jumamosi jioni, ilibidi wazungumze kidogo na mdogo wake,Kassim.
“Kesho una ratiba gani dogo?”
Ahmed hakupendelea kumuita mdogo wake kwa jina lake kamili,alipenda kumuita DOGO.
“Nipo tu,jioni nitatoka lakini”
“Nataka unipeleke sehemu kabla hujaenda misele yako”
“Na ndinga?”
“Ndio”
“Mshua atakubali kuachia key kweli?”
“Mimi nitamuomba,tutatoka wote alafu utakuja kunipitia”
“Fresh broo!Saa ngapi?”
“Nitakwambia,ngoja nimseti dingi kwanza”
“Aminia”
Ingawa walitumia kiswahili cha geto lakini waliheshimiana sana,siku hiyo usiku Ahmed alizungumza na baba yake na kumuomba gari.Hilo halikuwa na kipingamizi sababu Mzee huyo alimpenda sana Ahmed,akatoa funguo za gari usiku huohuo, bila kuhoji kitu.
*****
Jumapili ilikuwa tulivu sana,siku hiyo Ahmed alipanga kukutana na Yusrat maeneo ya Ilala mtaa wa shauri moyo,katikati ya safari alikuwa akiwasiliana naye kwenye simu.Ambapo hapo alimpa maelekezo Kassim aliyekuwa nyuma ya usukani anaendesha gari.Hazikuchukuwa dakika hamsini, wakawa wamefika nje ya mgahawa mmoja wa kiarabu,hapo wakapaki gari na Ahmed kushuka.Akachukuwa simu na kumtafuta mwenyeji wake hewani,sekunde tano zikawa nyingi.Wakawa tayari wameonana!
“Yusrath”
Kassim,akaita kwa mshangao baada ya kumuona msichana huyo mahali hapo,hiyo ilifanya Ahmed ageuke nyuma na kumuangalia mdogo wake,akashindwa kuelewa watu hao wamejuana vipi.Hata Yusrath,alionekana kupigwa na butwaa la waziwazi baada ya kumuona Kassim,kila mtu alikumbwa na hali ya sintofahamu!
Kassim hakupata jibu la harakahakara ni kivipi Yusrath amefika eneo kama hilo,haikuwezekana kitu kama hiko kutokea,zaidi ya hayo na kilichomfanya aongeze maswali mengine kichwani ni kivipi walijuana na kaka yake,Ahmed.Kitendawili hiko alishindwa kukitegua kwa wakati huo,hata kwa Ahmed ilikuwa ni kitu hikohiko. Alimgeukia mdogo wake kwa sekunde moja kisha kutupa macho yake kwa Yusrath.
“Kumbe mnafahamiana?”
“Yeah,namfahamu.Ni rafiki yake na cousine yangu”
“Oooh sawa”
“Ni ndugu yako?”
“Mdogo wangu”
“Ndio maana mmefanana kwa mbaaali”
Baada ya utambulisho huo mfupi kidogo ilibidi Kassim aage na kuondoka zake kwani alikuwa teyari, keshamfikisha Ahmed na walihaidiana jioni angefika mahali hapo tena, kumpitia.Moyo wake uliumia na ilionesha aliitikia kila kitu kishingo upande,hiyo ni kutokana na kwa muda mrefu sana alimfukuzia Yusrath bila mafanikio yoyote yale,alitumia kila njia ili ampate lakini hakuweza kuambulia chochote kile,alichomolewa na kupigwa cha mbavu.Jambo hilo lilimfanya akose raha ya maisha!Hakutaka kuyapa mawazo yake kipaumbele ya kwamba kaka yake ndiye anataka kumnyang’nya tonge lake mdomoni.Kama ni kweli,hakutaka jambo hilo litokee hata kidogo kwa gharama yoyote ile.Akiwa anaendesha gari, kuelekea Keko kwa msichana anayeitwa Wahda,ghafla wazo moja likamjia.
“Haiwezekani,nampenda Yusrath.Nitapambana mpaka nimpate!Kwahiyo Ahmed anataka kunizunguka anajifanya mwamba.Hanijui vizuri,subiri nimuoneshe kazi.Acheze na vitu vyangu vyote lakini sio kwa mtu ninaye mpenda na udugu utaisha”
Kassim aliapia kufanya kitu kibaya, ambacho mpaka wakati huo hakuelewa ni njia gani aitumie ili kumkomoa kaka yake,akiwa katikati ya safari ghafla simu yake ikaita.Hakuwa mwingine bali ni Wahda,msichana aliyekuwa mtundu kitandani.Sifa moja ya mrembo huyo, aliyompendea ni moja tu,namna anavyojua kuitumikia koki yake.
“Wahda mpenzi wangu”
“Baby!Umefika wapii?Nakusubiri sana,upo karibu?”
“Nipo karibu kufika,foleni tu.Nikifika kama kawaida”
“Usijali kwa hilo.Mwaa mwaaa”
Walizungumza kimahaba na kupigana mabusu simuni huku kila mtu akiwa mwenye furaha moyoni mwake.
*****
“Yusrath,najua utanifikiria vibaya lakini inabidi nikueleze ukweli.Na sina maana mbaya kama wengine walivyo.Nisingependa nikuharibie maisha yako,hustahili kuumizwa hata kidogo!Sitaki uwe mpenzi wangu,wala mchumba wangu.Ningependa baadaye uje uwe mke wangu”
“Ahmed,nilianza kujua hayo yote.Hapana sitoweza,kifupi nyie wanaume mna maneno matamu sana.Lakini mwisho wa siku,mnabadilika”
“Sio wote”
“Nilikuwa na boyfriend wangu,tangu nipo Form four.Nilimuamini sana,alinipa ahadi nyingi sana.Ikiwemo kunioa kama wewe unavyosema!Hakuwa mkweli kabisa,nikaja kugundua baadaye ana mke isitoshe ana watoto.Niliumia mno, kwa sasa naomba niache Ahmed.Siwezi kupenda tena, labda baadaye sana”
“Yusrath,mimi sio muhuni kama unavyofikiria.Nipo tayari kwa lolote lile sasa hivi, ili mradi uwe mke wangu”
“Hapana siwezi”
“Nipe nafasi japo kwa siku chache, to prove you wrong”
“Siwezi Ahmed,isitoshe wewe ni kama kaka yangu tu.Haitoweza kutokea”
Ilikuwa kama masihara vile lakini ukweli wa mambo ulikuwa huo,Ahmed alichomolewa mchana kweupe!Yusrath hakuwa tayari kukubaliana naye,aliogopa kutendwa kimapenzi kwa mara nyingine kwani aliamini siku zote kosa sio kosa bali kurudia kosa ndio kosa,hata hivyo kidonda chake cha kutendwa kilikuwa bado kibichi.
“Jaribu kufikiria Yusrath”
“Siwezi Ahmed,kuna makosa mengi ya sisi binadamu tunatakiwa kuyafanya, lakini sio kurudia yaleyale”
Yusrath alijaribu kutengeneza hoja za msingi za kumkatalia Ahmed,japokuwa alikuwa bado ni msichana mdogo mwenye umri wa miaka 19, lakini alikuwa mwenye upeo mkubwa na maneno mengi sana,hiyo ilimshangaza sana Ahmed,ikapelekea mpaka ashindwe kutumia gia nyingine.Sababu ilitokana na gia zake kupanguliwa na hoja za Yusrath,hakutaka kukubali jambo hilo, akatumia ushawishi mkubwa sana na kuchomekea mithali mbalimbali huku akijaribu kutoa mifano ya hapa na pale lakini wapi.
“Hata vidole vyetu ni tofauti,tizama kuna virefu.Vifupi,vinene.Na ndio tulivyo binadamu,hatuna tabia zinazofanana”
Sentensi hiyo ilimfanya Yusrath atabasamu kidogo na kumuangalia Ahmed machoni,aliyekuwa siriazi anajitetea.
“Ahmed,tuwe marafiki hivihivi.Nahofia kukupoteza”
“Kunipoteza?Kivipi?”
“Tukiwa wapenzi,najua ipo siku tutakosana tu.Na nitakupoteza,sitaki jambo hilo litokee nakuomba”
“Haitoweza kutokea”
“Hata watoto mapacha wakati mwingine wanagombana,tukiwa wapenzi ni lazima ipo siku tutapishana maneno”
Yusrath,aliendelea kusimamia msimamo wake uleule bila kutingishwa na maneno yoyote yale.Hiyo ilimfanya Ahmed atulie kidogo!Akamtizama Yusrath,usoni.Akaanza kuukagua uzuri wake asilia.Msichana aliyekuwa mbele yake sio siri, alikuwa ni mrembo kwelikweli,macho yake yalikuwa makubwa kiasi, tena ya kusinzia,midomo yake ilikuwa midogo, ‘lips’ zake zilikuwa nyembamba na nyekundu kwa mbali.
Ahmed,akahisi kama damu yake imeacha kutembea kwa muda,uzuri wa Yusrath ulivuruga almashauri nzima ya ubongo wake,akashindwa afanye nini.Lakini moyoni mwake,aliapia ni lazima atumie njia yoyote ile ili ampate Yusrath hata kama ingemchukuwa miaka mia moja,alikuwa yupo tayari kuvuta subira!
“Ahmed,naomba niende.Tutaonana siku nyingine”
Alisema Yusrath huku akijiandaa kwa safari ya kuondoka zake,hakutaka kuendelea kubaki eneo hilo kwa muda mrefu,alihofia kufokewa na Mama yake.Kitu ambacho alikichukia katika maisha yake ni kumuona mama yake,amekasirika na kumkaripia.
“Subiri kidogo,malizia juisi kwanza”
“Hapana Ahmed,acha niwahi”
Hakukuwa na njia nyingine yoyote ile ya kumfanya Yusrath aendelee kubaki eneo hilo.
******
Moyo wa Ahmed uliendelea kutapatapa,alitamani siku moja Yusrath awe wake, aliapia kabisa ya kwamba endapo akimpata ni lazima angefanya sherehe sababu moja tu,tayari amepata mwanamke wa maisha yake.Si kwamba alikuwa hajui ya kuwa, Yusrath ni mwanafunzi na bado ana safari ndefu,jambo hilo alilitambua fika lakini alikuwa yupo tayari kumsubiri mpaka amalize masomo yake kwanza.
Kila siku alimuimbisha na kumsihi amkubalie lakini hiyo ikaonekana kama kero kwa Yusrath kwani alisikia mambo mengi juu ya Ahmed.
“Kama nilivyokwambia,yule ni kaka angu.Namfahamu vizuri,uko naye vipi kwani?”
“Ni rafiki yangu tu”
“Demu wake,unamfahamu?”
“Hajawahi kuniambia kuwa ana demu”
“Ana demu wake lakini kwa sasa hivi,hayupo hapa”
“Nashukuru,Mambo mengine vipi Kassim?”
“Fresh tu,nahitaji kuonana nawewe”
“Sidhani kama itawezekana”
“Kwanini?”
“Niko bize sana”
“Tafuta siku ukiwa free,tuongee.Kuna mambo nataka kukwambia”
“Mungu akipenda”
“Mungu atapenda tu,labda wewe usiwe tayari”
“Poa,baadaye”
Wakati Ahmed,anajipigia debe akitumia kila mbinu kumnasa Yusrath, yeye Kassim kazi yake ilikuwa ni kuharibu kwani siku zote alitamani kuiona nguo ya ndani ya Yusrath, lakini kabla ya yote ilikuwa ni lazima amuharibie kaka yake.Siku hiyo Ahmed alivyopiga simu kwa Yusrath, haikupokelewa,ikaita mpaka basi.Akajaribu tena ikapokelewa lakini Yusrath hakuongea kama siku zote anavyochangamka.
“Unaumwa au?”
Ahmed,akahoji.
“Niko sawa,sema shida yako”
Yusrath,akawa tofauti kabisa na siku nyingine zote.Aliyakumbuka maneno ya Kassim.
“Yusrath,upo sawa kweli?”
“Nipo sawa Ahmed,sema shida yako nataka kulala”
Akazungumza kwa ukali kidogo.
“Inaelekea leo,kuna mtu amekukera ni nani huyo tena?Sijakuzoea ukiwa hivi”
“Hivi Ahmed,nikuulize kitu?”
“Uliza”
“Unanichukuliaje mimi kwa mfano?”
“Sijakuelewa”
“Hujanielewa nini sasa?Hujanielewa, unadhani sijui njama zako?Hivi nyie wanaume,mtaacha lini tamaa na uwongo,nilijua tu.Sasa sikiliza kwa umakini kuanzia leo,hii namba yangu ione kama kituo cha polisi.Nadhani umenielewa ukome Ahmed”
“Lakini Yusrat..”
“Lakini nini?ACHANA NAMIMI”
Hakukuwa tena na mjadala,Yusrath akakata simu kwa hasira huku kifua chake kikipanda juu na kushuka kwa hasira,kila kitu kilivurugika kabisa,alihisi kumpenda Ahmed lakini maneno aliyosikia kutoka kwa Kassim, yalimvuruga akili kabisa japokuwa hakutaka kuyapa kipaumbele.Kwa majibu ya hasira aliyotoa kwa Ahmed alihisi kuumia lakini aliamini kwamba hizo ni hasira, zikiisha atazungumza naye kwani hata maji ya moto, hupoa mapema yakipepewa.Masaaa mawili baadaye, hasira zake zilipungua,akachukuwa mwenyewe simu na kumtumia Ahmed ujumbe mfupi wa simu,akimtakia usiku mwema.
******
Kazi ilikuwa ikienda vizuri na ilifanyika hatua kwa hatua.Hajrath alikuwa katika mdomo wa mamba,hakuelewa lolote linaloendelea.Hakuhisi hata kidogo kwamba Florian ni shetani mwenye mapembe makali na muda mfupi angeingia katika hatari na pengine kuuwawa kabisa, sababu hiyo ndio ilikuwa sifa ya kikundi hiko hatari cha ‘Black Monsters’.Walikuwa ni lazima wauwe endapo kazi yao ikiisha.Hajrath,alikuwa haambiliki kwa Florian ni wazi kwamba alikuwa kafa kaoza,hakuelewa kwamba anajichimbia mwenyewe kaburi kwa kuendelea kubakia na Florian,hata hivyo halikuwa kosa lake bali ni Mungu aliyeuficha moyo wa mtu.Ni wazi kabisa moyo ni kichaka,huwezi kujua yupi mkweli na yupo muongo!Maigizo aliyokuwa anafanya Florian ya kumpenda Hajrath,hata angekuwa mwanamke wa aina gani,asingepindua.Florian alijua kuhudumia,mbaya zaidi alitumia pesa kufanya starehe mbalimbali.Zaidi na hapo alijituma sana kitandani,hiyo ilimfanya Hajrath kila wakati akikutana na Florian faragha,atake kufanya naye tendo hilo lililohalalishwa na wanandoa tu.
Siku hiyo mchana baada ya kujifungia hostel kwake alitumia muda mwingi, kuingia kwenye tovuti mbalimbali za wacheza sinema za ngono,alichotaka yeye kuangalia mikao na kuiga njonjo mbalimbali wanazofanya wanawake.Akaziweka kichwani ili usiku wa siku hiyo amtafute Florian na kumuonesha kila utundu,hiyo yote ni kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo!Hivyo kumkabidhi mwili wake aufanye atakavyo kwake aliona ni sawa,usiku ulivyokuwa mwingi akamuibukia kwenye hotel, aliyokuwa amekodi Florian, chumba namba 21.
“Leo,nina mambo nataka kukuonesha baby wangu”
Kitendo cha Hajrath kufunga mlango,alitembea kwa kasi mpaka kitandani na kumsogelea Florian karibu zaidi,wakaanza kunyonyana ndimi na kubadilishana mate huku taratibu akimvua nguo zake, kimahaba.Wakati huo wote Florian, alikuwa ametulia kwanza kwa sababu hakuwahi kumuona Hajrath akiwa mwenye moto kama siku hiyo,ndani ya dakika moja akawa amebakiwa na boxa peke yake!Hajrath,akabinuliwa na kuwekwa vizuri.Nguo zake zikachojolewa moja baada ya nyingine,akabakiwa na chupi na sidiria tu.Mikono ya Florian ikaanza kufanya kazi yake,hakutaka kuuweka usiku.Akapitisha mkono wake moja kwa moja mpaka chini kwenye mapango na kuanza kupima oil,mkono wake mwingine ukawa na kazi moja tu,kutomasa chuchu!Akamsogelea shingoni na kuanza kumnyonya,akatoa ulimi wake na kuupitisha sikioni mwa Hajrath,mrembo huyo akatulia na kutamani mechi hiyo ianze,kuna vitu alianza kuvihisi mwilini mwake.Nguo yake ya ndani ambayo, alibaki nayo,ikashushwa,sidiria ikafunguliwa akabaki kama alivyozaliwa!Kufuatia hapo Florian, hakutaka kulemba,akashuka chini kidogo.Akashika miguu ya Hajrath huku na kule akatoa ulimi na kuanza kupiga deki bahari,hapo ndipo Hajrath akaishiwa nguvu,zile mbwembwe na madoido aliyotaka kuyafanya yote yakaisha,kazi aliyofanya ni kumshika Florian kichwani huku akimkandamiza.Florian aliendelea na zoezi hilo mpaka alipohisi Hajrath,anataka kubana miguu, hapo ndipo akamuwahi na kuchomoka,akavuta boxa yake na kumtoa nyoka aliyekuwa tayari amesimama,akauchukua mguu mmoja wa Hajrath na kuuweka begani kwake.Kilichofuata hapo,mimi nawewe hatujui!
********
“Baby,hivi ipo siku utaniacha?!Siku hiyo sijui itakuwaje?Maana ninavyokupenda,ningekuwa na uwezo ningesimama juu angani na kusema namna navyokupenda”
Sauti ya Hajrath akiwa juu,kifuani kwa Florian ilisikika huku akimkwaruza na kucha zake, zilizokuwa ndefu ndefu kiasi baada ya kutoka kufanya tendo lililowaleta duniani.
“Naanzaje kukuacha?Nitampata wapi kama wewe unadhani”
“Nafurahi kusikia maneno hayo,nipo tayari kufanya chochote.Najua baba yangu hakupendi lakini mimi sijali,nishakupenda hiyo inatosha”
“Unasema ukweli baby?”
“Wallah laazim”
Wakiwa kama walivyozaliwa,mguu mmoja wa Hajrath umepanda kiunoni kwa Florian, wamejifunika shuka moja,walizungumza vitu vingi sana hususani swala lao zima la mapenzi.Kwa Florian,mawazo yake hayakuwa hapo,alikuwa akisubiria simu yake iite.Ilikuwa ni lazima siku hiyo Hajrath,apewe madawa alale nusu kaputi kisha baadaye tumbo lake lichanwe madawa yapakiwe!Dakika tano baadaye simu yake ikaita,akasimama taratibu na kwenda kuipokea,maneno aliyosikia Hajrath ni ‘Ndio’ ‘Kila kitu kipo sawa’ ‘Nakuja’
“Baby,nani alipiga?”
Alikuwa ana kila sababu ya kuuliza, kigugumizi cha Florian kilimuogopesha,akadhani wenda alikuwa anazungumza na mchepuko.
“Kuna jamaa angu mmoja ananisubiri,vaa twende wote”
“Wapi love?”
“Utapajua tu,jiandae”
“Naenda kujimwagia maji kwanza”
Maskini ya Mungu, hakuelewa kwamba hiyo ndiyo ingekuwa siku yake ya mwisho,bila kujua chochote tena akiwa mwenye furaha,akasimama na kumbusu Florian, akapitiliza mpaka bafuni,ambapo huko alioga na kujipangusa vizuri,akafungua mlango na kutokeza chumbani akiwa na kanga moja peke yake.
“Usiniangalie hivyo,naona aibu bwanaa”
Hajrath akasema kwa sauti ya huba,hiyo ni kutokana na Florian kumtizama kwa macho fulani ya kulegea,ilikuwa wazi kabisa umbo la Hajrath,halikuzoeleka hata kidogo, mbaya zaidi alivaa kanga moja yaani ilianzia kifuani,kumaanisha nusu ya mapaja yake yalikuwa wazi.
“Mwenyezi Mungu ni fundi sana ujue”
“Umeanza baby,nenda kaogee bwanaaa”
“Poa,dakika sifuri”
Florian,akaingia bafuni,akimuacha Hajrath anajiandaa.Akiwa katika harakati za kujipaka poda na kujiremba,kuna kitu kilimshangaza baada ya kugeuka nyuma,kwa chini ya uvungu.
Lilikuwa ni begi jeusi,lenye mikanda mirefu.Moyo wake haukutaka kukubali, akawa mwenye shauku ya kujua lina nini sababu hakuwahi kuliona kabla,akalivuta na kulishika vizuri.Akalifungua taratibu.Moyo wake ukapiga kwa nguvu, baada ya kuona risasi,alivyopekenyua vizuri akakutana na bastola.Vitu kama hivyo hakuwahi kuviona katika maisha yake, isipokuwa kwenye filamu za kijasusi,alihisi mwili wake unakosa nguvu.Kuna vitu kama pakiti ambazo ndani zilikuwa na unga wa rangi nyeupe vilikuwepo,akapagawa zaidi.Akahisi kutetemeka,akatamani kumuita Florian, amuulize lakini hakutaka kufanya hivyo,aliogopa zaidi.Akavaa harakaharaka huku akitetemeka akiwa mwenye wasiwasi mwingi.Baada ya kumaliza kuvaa ‘top’ Florian akawa ametoka bafuni,hata yeye alionekana kushtuka alivyoona begi lake, analo Hajrath.
“Vipi?”
Florian,akahoji huku akimtizama machoni.
“Hakuna kitu,nataka kuondoka”
“Kwenda wapi?”
“Hostel”
“Hatuendi tena sasa?”
“Hapana Florian,naondoka”
Hajrath alihisi kutetemeka,bastola ya Florian ilimtisha.Hofu ilimtanda mno,upande mwingine wa pili ulimwambia kwamba mwanaume huyo sio mtu mzuri,akili yake ikahama kabisa!
“Mbona sikuelewi?”
“Niko poa,kichwa kinaniuma.Nataka nikapumzike tutaenda siku nyingine”Hajrath akaongea, bila kumeza mate!
Florian akawa amechezwa na machale,kwa asilimia zote mia moja, akaamini kwamba Hajrath aliona kila kitu ndani ya begi,hiyo ilimaanisha ni lazima atumie njia ya ziada, kumthibiti.
“Nisubiri basi nikupeleke”
“No,nitaenda tu usijali baby”
Hakukuwa na namna nyingine yoyote ya kumzuia Hajrath,aliyekuwa tayari ameranduka.Florian hakutaka jambo hilo litokee kabisa, ndio maana akawahi mlangoni na kutanda.
“Huwezi kuondoka hapa”
“Florian nipishe”
“Hapana”
Alivyotaka kutumia nguvu ilishindikana kwani Florian alimvuta na kumtuliza,Hajrath akawa mbishi na kuanza kupiga kelele.Hiyo ilimfanya Florian apandwe na hasira,akamzaba kibao cha nguvu!Hajrath akadondoka chini,hapo ndipo alipojua tayari amekwisha.Maumivu yalikuwa makali mno shavuni,akaamini kivyovyote vile kuna hatari mbeleni, ndio maana akatulia kidogo,alivyoona Florian amezubaa akasimama mzimamzima na kuchomoka kuelekea mlangoni,lakini hakufanikiwa kwani Florian alimkamata vizuri na kumvuta kitandani,ambapo hapo alitoa kitambaa ndani ya begi,akamuwekea puani kwa nguvu.
“I’m sorry Hajrath”(Nisamehe Hajrath)Florian,akasema maneno hayo kwa sauti ya chini!
Kwa mara ya kwanza Hajrath hakuelewa, maana yake lakini kadri sekunde zilivyozidi kwenda mbele,alihisi nguvu zinamuishia,taratibu.Macho yake yakawa yanapata ukungu mzito mno,alivyojaribu kurusha mikono akashindwa,kwa haraka akajua tayari kitambaa alichowekewa puani kina dawa hatari za kulevya!Sekunde kumi na tano zikawa nyingi, macho yakawa yanafumba taratibu kama redio inayoisha mabetri,mbele yake akaona giza kubwa!Hapohapo,akapoteza fahamu.
Hajrath alikuwa ametulia,azungumzi chochote kile,ajitingishi wala kujisogeza.Hiyo ilitokana na dawa kali za valium dex zilizopakwa juu ya kitambaa,kikawekwa puani kwake.Dawa hizo kali hutumika kwa wanyama endapo wana sayansi watahitaji kwa ajili ya majaribio lakini siku hiyo ilikuwa kinyume kwani aliwekewa Hajrath,ikampelekea azirai hapohapo.
Hakuwa anaelewa chochote kuanzia hapo,Florian alibaki akiwa amesimama,mapigo yake ya moyo yanamwenda mbio kwa kiasi,hakuelewa ni kitu gani akifanye.Alichotakiwa kukifanya ni kumtoa Hajrath akiwa mzima kutoka ndani ya hoteli hiyo kisha baadaye kumzimisha,mpaka muda huo zoezi likawa limebadilika, akawa amebugi stepu!
Asingeweza kutoka naye nje akiwa hana fahamu ni lazima angeulizwa mapokezi,mbali na hapo hotel hiyo ilikuwa ya kisasa,Kamera za CCTV zilikuwepo katikati ya kordo mpaka nje,hivyo isingekuwa rahisi kwa Florian kupita na Hajrath akiwa amemuweka begani bila kuonekana!Akili yake ikaanza kufanya kazi kwa haraka,licha ya kutafakari kwa muda mrefu, alishindwa kubuni njia ya kufanikisha zoezi hilo lililoonekana kuwa ni gumu sana kwake,hakuwa na jinsi ilibidi ampigie mtu anayeitwa Khaleed,amueleze kila kitu kilichotokea,bila ya kuficha chochote,akamuweka wazi.
“Ulisema sasa hivi hapo.Hana fahamu?”
Khaleed,akauliza simuni.
“Ndio,bila kumfanyia hivi.Ingekuwa hatari kubwa”
“Imekuaje akagundua sasa nawewe?”
“Kama nilivyokwambia,aliona begi langu.Lilikuwa chini ya uvungu”
“Huo ni uzembe mkubwa”
“Kwahiyo,utanisaidia au unanisakama?”
“Sio kukusakama,kwenye ukweli lazima nikuchane”
“Sawa nimekuelewa,niambie cha kufanya”
“Nakuja subiri,upo room namba ngapi?”
“Nipo room namba 21”
“Nitakuja hapo,kama mgeni”
“Enhee…”
“The rest,niachie mimi”
“Sawa,kwahiyo nikusubiri?”
“Ndio,nisubiri.Nikifika nitakupigia simu”
Katika watu waliokuwa na akili za kufikiria haraka alikuwa ni huyu Khaleed,alikuwa ni mjanja kuliko sungura, ndiyo maana wenzake walimbatiza jina na kumuita ‘Michael Scolfied’hiyo ilitokana na tabia zao kuendana na muigizaji huyo aliyejichukulia umaarufu kwenye sinema inayoitwa ‘Prison Break’.Usiku huo huo akiwa na jamaa zake watano,alitoka mpaka kwenye chumba alichopanga,kwa kuwa alikuwa ana begi kubwa,alilitafuta mpaka kulipata.
Lilikuwa juu kidogo,akapanda na kuliteremsha,ambapo hapo alitoa baadhi ya nguo na kuziweka kitandani,akachukuwa begi kubwa na kutafuta Taxi, ambayo ilimpeleka moja kwa moja, mpaka katika hotel ya nyota tano iliyoitwa Green Mountain,alivyowasili hapo. Akajifanya ametokea nchini Uganda,hivyo anahitaji chumba kwa muda wa siku moja ili apumzike.
“Sawa,karibu sana”
“Ahsante,umependeza sana.Unaitwa nani?”
Khaleed akajaribu kumzoea mrembo huyo,aliyekuwa mapokezi amevalia sketi nyeusi na shati jeupe.Ilikuwa ni wazi kabisa ukitaka kumteka mtoto wa kike ni lazima kidogo, umpambe kwa maneno matamu.
“Naitwa Dorothea”
“Nimependa midomo yako una lips nzuri,umeolewa?”
Khaleed,akataka kumzoea zaidi huku akiyaongezea maneno yake, kachumbari!
“Hapana lakini nina mchumba”
“Ikitokea,mmeachana.Nitafute”
“Hatuwezi kuachana”
“Sijasema,muachane.Ikitokea mmeachana,anayway.Ni huku juu ama?”
“Ndio,panda hapo kushoto kwako”
“Okay,ahsante”
Khaleed,akapanda ngazi na kukipita chumba namba 21, ambapo humo alikuwepo Florian,akapitiliza mpaka chumba namba 27,akatulia kidogo na kumtaarifu Florian kuwa amewasili tayari,bila kupoteza sekunde Florian,akawa ameingia.
“Hili begi,nimeleta,tumuweke humu.Alafu mimi nitaondoka naye,nitazuga kuna dharura”
“Kuna kamera lakini”
“Najua,hawatoweza kujua humu kuna mtu.Wakija kujua,watakuwa tayari wamechelewa,ebu fanya haraka basi”
“Njoo tusaidiane”
“Poa,tangulia nakuja”
Mikakati mathubuti ilipangwa.Kila kilichotokea, waliamini ilikuwa ni vigumu sana kugundulika.Hajrath alikuwa bado kitandani,haelewi lolote,walichofanya ni kutoa nguo zote,wakafungua begi na kumuweka Hajrath ndani yake,wakamkunja kunja.
“Zipu haifungi”
“Mguu huu ukunje,mkono uweke vizuri,Florian Changamka mbona legelege hivyo”
Kila kitu kilipelekwa mkuku mkuku,Hajrath akakunjwa vizuri na zipu ya begi ikafungwa.Khaleed,akakamata begi mkononi na kuanza kuliburuza akitembea,kuelekea kwenye lifti,aliamini angetumia ngazi ingempa shida kidogo.Alivyoingia ndani ya lifti,ikashuka mpaka mapokezi,ambapo huko alianza kuburuza begi mpaka mapokezi.
“Chaurembo,nimepata dharura.Sasa kamata hii,utanunua soda unywe”
Khaleed alizungumza hivyo huku akichomoa noti ya dolla mia.
“Hapana kaka”
“Shika,usiogope.Wala sitotaka chochote kutoka kwako,nimefurahishwa tu.Na uchangamfu wako una ukarimu sana”
“Aya kaka Ahsante”
Kutokana na mshahara,mdogo ambao usingeweza kukidhi haja zote za mrembo huyo kama kununua mafuta ya gharama na manukato ya bei mbaya, akajikuta anapokea huku akitoa tabasamu mwanana, hiyo ikapelekea kusahau mpaka kuliangalia begi la Khaleed,lilioonekana kuwa zito kuliburuza.Pesa zikawa zimempumbaza,Khaleed akatumia mwanya huo kutoka nje na kukodi taxi,ambayo ilimpeleka mpaka Usariva,hapo alimtaarifu Florian kwamba wakutane na usiku huohuo wachukuwe gari mpaka Dar es salaam ambapo huko,wangeanza mikakati ya kupakia mzigo wa madawa ya kulenya ndani ya tumbo la Hajrath,jambo hilo lilikuwa rahisi sana kufanyika kwani Usiku huo huo,Florian na Khaleed,wakaonana.Mikakati ikaanza mara moja!
“Pale tutafikia Vingunguti kwa Mr.Sarara”
“Poa,ushapata gari?”
“Kila kitu kipo tayari,Kenny kesharekebisha”
“Hapo shwari,njiani sasa. Tatizo siku hizi barrier nyingi”
“Hilo swala niachie mimi,cha kufanya huyo.Tunamuweka kwenye siti.Tunamfunga kamba”
“Nakuaminia Scolfield,master plan”
Kila alichosema Khaleed,kiliungwa mkono.Na haikuwahi hata siku moja ikatokea akapingwa katika hoja zake,sababu zilionekana kuwa na tija na mashiko.Ndiyo maana kila mtu akikwama ni lazima amtafute Khaleed ili mambo yanyooke,saa nane ya usiku gari aina ya Prado,new Model. Ilikuwa nje tayari,inaunguruma.Hiyo ndiyo gari, iliyotakiwa imsafirishe Hajrath kutoka Arusha Mpaka Dar es salaam,kisha huko ndio taratibu nyingine ziendelee kufanyika.
“Mfunge kamba vizuri,mpitishe hapo katikati”
Hajrath,akafungwa kamba za mikono.Akakalishwa katikati,bado hakuwa na fahamu hata moja,kushoto alikaa Florian, kulia aliketi jamaa mmoja anayeitwa Sospeter Alfred,dereva akapanda na kuketi nyuma ya usukani.Huku kushoto akiwa ameketi mwanaume mwingine aliyependa kujiita ‘Jitu baya’ huyu alikuwa ana sifa moja tu,hacheki wala hatabasamu wengi walisema hakuwa na bandama,hiyo iliambatana na ukatili aliokuwa nao,pembeni ya gia kulikuwa na bastola iliyojaa risasi kumi na nane.Lolote litakalo tokea njiani, walikuwa tayari kujihami.Hata Florian nayeye,alikuwa ana bastola kiunoni.
“Tuanze safari sasa,hatuna muda wa kupoteza!Mzigo unatakiwa kupakiwa asubuhi sana”
“Pale tunapokelewa na nani?”
“Sarara,kwani wewe kiziwi?Tushaongea hilo.Boni washa gari”
Gia ikawekwa,gari likaanza kuondoka mara moja.Ilikuwa ni lazima waingie Jijini Dar es salaam,asubuhi na mapema,ndiyo maana dereva Boni, alikimbiza gari kwa umbali wa Kilomita kumi kwa dakika,ilikuwa kasi isiyoweza kuelezeka kiwepesi.Ndiyo maana, waliingia njia panda Mkoani Kilimanjaro,baada ya lisaa limoja na nusu.Haikuwa kasi ya kawaida,hiyo ilitokana na barabara kuwa tambarare, hakuna magari wala tochi za usalama barabarani.Florian alikuwa akiwaza vitu vingi sana kichwani,alijisikia mkosaji sana mbele za Mungu,hususani alivyomtizama Hajrath usoni,moyo ulimuuma ajabu kwani Msichana huyo hakustahili kufanyiwa unyama wa namna hiyo,licha ya kutafakari hayo yote.
Hakutaka kurudisha moyo wake nyuma,walitembea umbali mrefu sana.Walivyofika Mkoa wa Tanga,eneo linaloitwa Mombo, ilibidi wapaki gari ili wajaze mafuta kisha waanze safari tena,hapo ndipo dawa aliyokuwa amepakwa Hajrath ikawa tayari imeisha nguvu.
“Weka ya Elfu themanini”
Boni,alizungumza kioo cha mlango wa mbele kikiwa wazi,anamwambia mjaza mafuta.Mwanamke huyo,akabonyeza bonyeza mashine na kuanza kujaza mafuta.Fahamu za Hajrath, zikaanza kurudi taratibu kama mtu aliyetoka kulala usingizi wa muda mrefu,picha ilimjia kwa haraka ni kofi kali la Florian,baada ya hapo akawekewa kitambaa puani,hakuelewa kilichoendelea kila alipojaribu kuvuta kumbukumbu.
Picha, iliyomjia kichwani na watu waliokuwepo ndani ya gari,akiwemo Florian ilitosha kabisa kujua ni kitu gani kinaenda kutokea mbeleni, mbaya zaidi mikono yake ilikuwa imefungwa kamba.Gari lilisimama linajaza mafuta,akajua hiyo ndiyo ingekuwa nafasi yake ya kujikomboa.
“Nisaidieeeniiiiiii,nisaidie tafadhali.Majambaziii”
“Hajrath nyamaza”Florian,alisema huku akijaribu kumziba mdomo na kumvuta.
“Florianiii,kwani..ni lakini? Niachie, nisaidieni jamaaniii”
Ndani ya gari kuliibuka, mtafaruku mkubwa sana,Hajrath alipiga kelele kuomba msaada huku akirusha rusha mateke,kwa nguvu za ajabu akachomoka na kutoa kichwa chake nje, kupitia dirisha la dereva,hiyo ilifanya mjaza mafuta asitishe na kumtizama.
“Dada naombaa unisaidieee wana..taka kuniua”
Kitumbua kilikuwa tayari kimeingia mchanga,Hajrath alikuwa akilia kwa sauti akiomba msaada.Sio Florian wala Jitu baya, kila mtu alichanganyikiwa kwa kiasi cha kutosha,wakajua tayari mwisho wao ulikuwa umefika.
“Anti pole kwa usumbufu”
Khaleed,alizungumza bila wasiwasi huku akimtizama dada aliyekuwa anashangaa tukio hilo,ameshika mpira wa mafuta ya petrol.
“Kuna nini kwani?”
“Huyu ni ndugu yetu,ana matatizo ya akili ni chizi.Tunamuwahisha hospitali!Tangu juzi alikuwa anapiga kelel…”
“Dada mimi si..o chi..zi nisaid...e wanaenda kuniua…”
“Tujazie mafuta harakaharaka tuwahi,hali yake sio nzuri”
Khaleed,hakuwa na wasiwasi hata punje.Ndio kwanza akazunguka upande mwingine, mikono yake ikiwa mfukoni hana presha,tofauti na Florian pamoja na wenzake, ambao muda huo walikuwa wakitetemeka ndani kwa ndani.
“Da…da mimi sio chizi,nifanye nini uniamini.Naitw..a Hajrath,naju..a kusoma na kuandika”
Maneno hayo ndiyo kabisa yalimfanya dada anayejaza mafuta aamini kama Hajrath amerukwa na akili,hata yeye alidhani hivyo.
Hajrath alilia machozi ya uchungu,akatoa mikono nje huku akiomba msaada,alichoharibu zaidi ni kumshika dada huyo shati na kuanza kumvuta vuta.Jambo hilo lilimfanya arudi nyuma na kuwapa pole.
“Poleni sana,muwahisheni hospitalini hii ni hatari,mfungeni kamba vizuri.Msije mkapata ajali njiani kuweni makini”
Kila kitu kilivyokamilika, wakaingia ndani ya gari,wakiwa na hasira za mbogo,licha ya kuponea chup chup lakini kitendo cha Hajrath kupiga kelele kiliwafanya wakasirike ajabu.
“Florian,mnyamazishe Malaya wako”
Jitu baya akasema,kelele za Hajrath zilionekana kuwa kero kwenye masikio yake.Hajrath muda wote alikuwa analia machozi ya uchungu,mpaka sauti ikamkauka.Bado hakutaka kuamini kama jambo linalotokea ni kweli,hiyo ilitokana na Florian pia kuwepo kwenye mchongo huo,kila alipo jaribu kufikiria,haikumuingia akilini kabisa.Mwanaume,aliyempenda leo hii anaenda kumuuza,japokuwa hakuelewa ni wapi anapelekwa lakini alijua yupo mbioni, kufanyiwa unyama.
“Flo..rian..Plea..se don’t do this…Naom..ba niach..e niende I’m begging you”
Hajrath,alitumia kila lugha kumshawishi Florian,asifanye anayotaka kufanya lakini ilikuwa ni kazi bure.
Aliendelea kulia bila kupatiwa msaada wowote ule,akatamani siku zirudi nyuma abadilishe kila kitu.Lakini alikuwa tayari amechelewa.Ghafla maneno ya Baba yake yakamjia kichwani,yakimsihii kwamba aachane na Florian,akahisi kujuta kupindukia.Kwikwi ilimkaba,alivyoangalia nje kulikuwa na giza kubwa sana,gari lilikuwa katika kasi ya ajabu mno!Akili yake ikafanya kazi kwa kasi ya kompyuta isiyokuwa na mafaili,ilikuwa ni bora afe kwa kujiua mwenyewe kuliko kufa kikondoo.Kufumba na kufumbua akachomoka na kumvaa dereva,akaviringisha mikono yake shongoni kwa dereva huku akimvuta kwa nguvu,hiyo ilimfanya dereva ashindwe kulimudu gari,kutokana na kasi ya ajabu aliyokuwa nayo,ilimfanya ahame barabarani,gari likaingia msituni na kutimua vumbi la ajabu.
Hajrath akavutwa na jamaa aliyekuwa nyuma na kupigwa kibao cha uso,akatulizwa na ngumi ya pua.Dereva,akaweka mguu kati gari, ikasimama kwa kuteleza.
“Floriaaan,nilikwambia umtulize malaya wako,mpuuzi wewe.Wewe Malaya,nitakuuuwa sasa hivi!Nitakunyonga humuhumu ndani ya gari,pumbavu usiye na akili kunguru wewe.Florian,huelewi au?” Jitu baya,alizungumza kwa kufoka,hasira zilimpanda kilikuwa ni kitendo cha hatari!Kila mtu alikuwa akihema juujuu,baada ya kunusurika ajali hiyo mbaya,isingekuwa dereva kukanyaga breki za ghafla,gari lingeingia mtaroni na kupinduka.Kufuatia hapo,Hajrath akawekewa tena kitambaa chenye madawa puani,haikuchukuwa sekunde mbili,akapoteza fahamu.Baada ya hapo,safari ikaanza upya,wakaingia barabarani lakini cha ajabu baada ya kufika Korogwe,wakakutana na ‘barrier’ yaani barabara imefungwa,chini kuna machuma maalum, kando kando kuna difenda za polisi saba,maaskari wametanda barabarani,wameshika mitutu.Jitu baya, alivyotaka kutoa bastola,Khaleed akamshika mkono kumaanisha atulie kwanza ili ajaribu kuwapiga Kiswahili.Gari likasogea taratibu mpaka kwenye kizuizi,dereva akashusha kioo.
“Washa taa za ndani”
Aliamuru Kamanda Massatu Mjanja,askari huyo alikuwa mrefu mweusi tii.Hacheki wala atabasamu,begani alikuwa na mtutu, mkononi ana tochi kubwa.
“Nimesema washeni taa za ndani”
Sauti hiyo ikasikika tena,kulikuwa na kila dalili mbaya siku hiyo, kwani Kamanda Massatu,alimulika tochi ili asome namba za gari,akawaita wenzake.
“Ndio lenyewe”
Baada ya kusema hivyo,wakasogea karibu zaidi.
“Tumepigiwa simu kutoka Mombo,wote teremkeni ndani ya gari.Dereva naomba leseni yako”
Hapo ndipo kila mtu alitokwa na jasho jembamba,hata Khaleed mwenyewe ilibidi atulie kwanza,akamkumbuka msichana waliyejaza mafuta, kwake.Dalili zote ya kwamba alipiga simu polisi,zilikuwepo sababu walianza kulimulika gari hilo ndani,kuashiria kwamba kuna kitu wanakitafuta.
“Nimesema teremkeni ndani ya gari”
Kamanda Massatu,aliamuru kwa mara nyingine huku akishika mtutu wake vizuri!
Askari walilizunguka gari hilo na kuliweka katikati,hiyo iliwafanya Florian na wenzake wapate kitete.Waliogopa na kujua tayari wamekwisha na huo ndio ungekuwa mwisho wao,walichoomba Mungu ni Hajrath aendelee na hali hiyohiyo na dawa isije kuisha nguvu,kitendo cha kuzinduka kingewafanya wawekwe hatiani na kusingekuwa na mjadala wowote ule sababu gereza lingewahusu.Kila mtu alitetemeka ndani ya gari, wakabaki wanatizamana hawajui wafanye nini,askari nje waliendelea kuwasisitiza wateremke garini lakini wao walikuwa bado wanatafakari ni kitu gani wakifanye,mmoja wao alivyotaka kuchomoa bastola wakamzuia, kwa kufanya hivyo wangekufa hapohapo kwa kumiminiwa risasi na askari hao,waliokuwa nje na mitutu mikononi mwao.
“Khaleed,tuambie tufanye nini?”
Mmoja wapo, alimtizama Khaleed na kumuuliza swali hilo ili atoe wazo ni njia gani watumie ili kuwatoka askari,hata Khaleed mwenyewe alionekana, kusanda!
“Tushuke”
Akasema kwa upole huku akionekana kama alikuwa anatafakari kitu kichwani.
“Unasemajee!?”
“Tushuke,msiongee chochote niachieni mimi”
Khaleed alivyomaliza sentensi hiyo akawa wa kwanza kuteremka garini, kumaanisha ya kwamba wengine wamfuate.Akapiga magoti moja kwa moja na kuweka mikono yake hewani huku akiwatizama askari hao, ambao wote macho yao, yalikuwa kwake.
“Simama juu”
Askari mmoja akatoa amri hiyo,Khaleed akatii na kusimama.Hapo wenzake walikuwa tayari wameteremka na wao wameweka mikono yao hewani, kumaanisha kwamba wamesalimu amri.
“Mnatoka wapi?Na mnaelekea wapi?”
“Tunatokea Arusha”
“Arusha kwa nani?”
Kama kasumba ya maaskari,kuhoji maswali yasiyo na kichwa wala miguu.
“Kwa Mtoto wa Shangazi”
“Mtoto wa Shangazi?Wapi?”
“Tengeru”
“Kamanda Shabani,sachi gari”
Hivyo ndivyo ilivyokuwa,mmoja wa maaskari aliyekuwa na mtutu akafungua mlango wa gari na kuanza kukagua,akamuona msichana mdogo akiwa amefungwa kamba mikononi amepoteza fahamu,akatoka nje na kuwataarifu wenzake, ambao hata wao ilibidi waingie na kuhakikisha.
“Ni kweli kumbe,nyie ni watekaji”
“Hapana Afande”
“Kumbe nini?Kamanda,wawekeni chini ya ulinzi hawa majambazi sugu.Tunashindwa kulala kwa ajili yenu”
Hakukuwa na dalili yoyote ile ya wao kutoka salama usiku huo,Khaleed akashusha pumzi kidogo na kuwatizama wenzake ambao walikuwa wanafungwa pingu.
“Kamanda,mnafanya makosa”
Khaleed akaanza kujaribu anachotaka kufanya.
“Unatufundisha kazi?”
“Siwafundishi kazi mkuu,Yule ni ndugu yetu.Ana matatizo makubwa,tuna shida.Yapata mwezi sasa anasumbuliwa na ugonjwa wa ajabu”
“Utaeleza hayo yote kituoni al…”
“Naomba ujaribu kunisikiliza,tuongee kibinadamu afande.Binadamu sisi ni kama ndugu,ngoja nikwambie ukweli”
“Ukweli gani?”
Katika makosa ambayo afande huyu hakutakiwa kufanya ni kumpa nafasi Khaleed,ajitetee. Hapo ndipo alipobugi,kwa mwanya huo,Khaleed akitia huruma huku machozi yakimlenga, alianza kusimulia hadithi ya uwongo,akasema namna alivyozunguka hospitalini na kuteketeza pesa nyingi,lakini ugonjwa wa ndugu yake haikujulikana.Hivyo waliamua kumfunga kamba sababu ana tabia ya kung’ata watu na kufanya fujo, endapo akizinduka.Hiyo ilimfanya Afande huyo,atulie kidogo na kumtizama Khaleed machoni anayeongea kwa huzuni mkubwa,kama binadamu na kuachana na jezi za kipolisi alizovaa akajawa na huruma .
“Kwaio anaumwa sana?”
“Ndio,nilienda kwa fundi mmoja akaniambia ana mashetani.Mbaya zaidi ana nguvu za ajabu,akizinduka pale afande,hatutoweza kumtuliza tena anaweza hata kukata kamba”
Khaleed alizidi kupigilia uwongo wake msumari,akaweka na mambo mengine ya kutisha zaidi.Alichofanya Kamanda Shabani,ni kuwaita wenzake na kuwapa mkasa kidogo uliotokea na kuwaamuru wawaachie huru,bila kuelewa ya kwamba wanafanya kosa kubwa la jinai.
“Sisi tulipigiwa simu,kuna binti alikuwa anapiga kelele ndani ya gari lenu kumbe ndiye huyo mgonjwa”
“Ndio huyo afande,anaumwa sana”
“Muwahisheni basi”
“Ahsante”
Kitendo cha kushukuru, wakaingia ndani ya gari lao,bila kupoteza muda gia ikapigwa gari likaondoka kwa kasi ya ajabu.Kila mtu akashusha pumzi ndefu ya kuchoka na kumtizama Khaleed, ambaye hata yeye alikuwa bado haamini kama amenusurika kwenye mdomo wa mamba.
“Khaleed….”
“Subiri kwanza,tuvuke Segera”
Khaleed alimkata ndimi mwenzake,ambaye alionekana alitaka kujua ni kitu gani aliwaambia askari mpaka wakaachiwa huru,walivyofika Segera ilibidi awahadithie kila kitu.Pongezi zote walimpa na kum-mwagia sifa nyingi sana.Walizidi kusonga mbele mpaka walipowasili,jijini Dar es salaam mishale ya saa tatu, asubuhi.
Hapo hawakutaka kupumzika, mpaka walipoingia Vingunguti,ndani ya nyumba ya mzee Sarara,wakapokelewa Hajrath akashushwa na kuingizwa ndani ya chumba maalum,hiyo ilimaanisha baada ya muda mfupi watayapakia madawa ya kulevya ndani ya tumbo lake na safari ya kuyasafirisha itaanza mara moja!
******
Ahmed aliendelea kumuimbisha Yusrath,kila kukicha.Hakukoma,alimpigia simu asubuhi,mchana na usiku akitaka kujua hali yake.Na katika maongezi yake hakuacha kumgusia swala zima la mapenzi na namna ambavyo ana mpenda kuliko kitu chochote kile,akamuhaidi vitu chungu mzima,likiwemo swala la kutaka kujitambulisha kwa wazazi wake na Mungu akijalia kumuoa kabisa,wajenge familia.Jambo hilo linakuwa gumu kidogo kwa Yusrath, sababu hakutaka kuamini moja kwa moja kwamba Ahmed alikuwa ni mkweli ama laghai,alichukulia hayo ni maneno ya wanaume wakiwa katika kampeni zao.
Hakuwatofautisha wanaume na wanasiasa katika kupiga kampeni za kuomba kura lakini baada ya hapo,wanabadilika mno.Msimamo wa Yusrat ukawa vilevile,akaendelea kumchomolea Ahmed,kilichompa nguvu ni maneno ya Kassim,aliyokuwa akimwambia ya kwamba Ahmed ana mwanamke wake mwingine.Mbali na kuambiwa hivyo lakini alihisi kumpenda mwanaume huyo,licha ya yote hakutaka kumkubalia haraka,alitaka kwanza amzungushe,hakutaka kuonekana mrahisi kiasi hicho.Ahmed,akatumia kila njia lakini hakufua dafu,wakati mwingine alidhani wenda ana kasoro!
“Au nina kasoro?”
Ahmed akauliza siku hiyo simuni,alitaka kujua nini tatizo mpaka Yusrath,asimkubalie.
“Hapana Ahmed,hauna kasoro yoyote ile.Ni mwanaume ambaye kila mwanamke aliyekamilika anatamani kuwa nawewe.Ujue kuna aina tatu za jinsia yenu kuna Boy,Man na Gentleman,wewe ni Gentleman”
“Sasa mbona hunipendi?”
“Sio kwamba sikupendi”
“Sasa kwanini, hunitaki?”
“Naogopa”
“Unaogopa nini?”
“Kuumizwa,mimi ni mwepesi sana kuumia nina moyo mdogo”
“Nishakuhaidi,haitoweza kutokea hata kidogo”
“Ni haidi”
“I promise you”(Nakuhaidi)
“Are you sure?”(Una uhakika)
“Ndio”
“Ahmed,naomba uwe mwanaume wangu wa mwisho!Nisingependa nije kujuta baadaye”
Hiyo ilimaanisha msichana huyo tayari ameelekea kibra,kuweka masharti hayo kulimaanisha kila kitu kipo sawa.Ahmed,hakuamini kile anachosikia,alihisi moyo wake unapiga sarakasi ndani kwa ndani.
Alitamani sana jambo hilo lisiwe ndoto,hakuamini kwamba hatimaye anam-miliki kisura huyo ambaye alimuwinda kwa takribani miezi miwili kasoro!Haikuchukuwa siku mbili,Ahmed akaomba wakutane uso kwa uso na Yusrath,hilo halikuwa tatizo wakakutana. Hapo walizungumza mambo mengi,alichosisitiza Yusrath ni kitu kimoja tu,Ahmed awe muwazi kwa kila jambo na muaminifu pia, asije akambwaga!
“Nakupenda Yusrath,amini nachokwambia ipo siku utalia kwa furaha.Nataka tufike mbali pamoja”
Ahmed,alizungumza kwa hisia zote huku akimtizama Yusrath machoni,ambaye muda mwingi alikuwa anaangalia chini,kwa aibu.Bado alikuwa ana haya za kikekike na hakuweza, kumwangalia Ahmed machoni kwa sekunde tano nzima,huo ndio ulikuwa mwanzo wa mapenzi ya Ahmed na Yusrath!
******
Ni kweli,haukuwa utani.Ahmed,akawa amekufa ameoza kwa mara nyingine!Akauhaidi moyo wake na kuukanya utulie tuli kwa Yusrath,usitamani tena wanawake wengine.Tayari akawa amejiwekea malengo na Yusrath,kwa kuwa alikuwa bado ni mwanafunzi alimsihi sana aishike elimu sababu hiyo ndiyo ingewakomboa mbeleni,Ahmed hakutaka kuja kuoa mwanamke bogazi,alitaka siku moja asipokuwepo duniani ama akiwa mbali, mkewe aendeshe biashara zake,hilo aliliamini sababu katika kujituma Yusrath,alijitahidi kuliko kawaida.Akiwa nyumbani Ahmed,aliomba ‘Assesment Sheet’ yaani matokeo yake ya chuo,ambayo aliamini yangemsaidia kuomba vibarua vya hapa na pale,hakutaka kubaki nyumbani,alivyompelekea baba yake wazo hilo, akaonekana kidogo kupinga.
“Hapana Baba,siwezi kukaa nyumbani bila kushughulika”
“Naelewa Ahmed,naelewa sana.Sio kwamba nakunyima usifanye kazi.Lakini maana yangu ni kwamba,ukianza kushika pesa sasa hivi,ule mpango hutaufanya”
“Mpango gani baba?”
“Masters,ama umesahau?Kwenda kusoma masters”
“Huo utakuwa palepale,nakuhaidi”
“Kweli?”
“Ndio”
“Basi subiri,nikuombee sehemu ujishikishe kidogo.Nitaongea na Mr. Muna,akuweke kwenye ofisi yake”
“Sawa baba”
“Kesho nitakujibu”
Mzee hakuwa mwenye longolongo,alichohaidi ndicho alichoenda kukifanya.Asubuhi hiyohiyo akamtafuta Mr.Muna simuni na kumueleza kuhusu kijana wake, aliyemaliza chuo kikuu. Kwakuwa wazee hao waliheshimiana hakukuwa na tatizo lolote lile,ilibidi Ahmed apewe taarifa hiyo na siku inayofuata alitakiwa kuanza kazi mara moja.
Hilo hakutaka kuliweka siri,siku hiyohiyo Yusrath alijua na alimpongeza na kumpa moyo wa kufanya kazi,simuni.
“Katafute mkate Mme wangu,uji wa baadaye wa watoto wetu”
“Ahsante honey”
“Uwe na kazi njema,kuwa makini na vidada vya huko.Nitamtoa mtu rohoo wallai”
“Usiwe na shaka baby wangu,hamna yoyote atakaye nitingisha”
“Sawa baby,naamini hilo.Pia nakuamini sana”
Siku hiyo Ahmed,alikuwa nyuma ya kioo kikubwa ameshikilia tai yake, anaiweka vizuri,mkanda nje!Hakuna siku aliyopendeza kama hiyo,chini alivaa kiatu aina ya moka!Suruali nyeusi,shati jeupe.
“Duu,kama Afsa mikopo vilee,hapa sasa mambo bombaa”
Ahmed akajisemesha mwenyewe,akaanza kutoka na kufika mpaka seblen ambapo huko alikutana na Mama yake,akam-mwagia sifa.
“Upo smart mwanangu”
“Ahsante Mama, shikamoo”
“Marahaba,kunywa chai basi kwanza”
“Hapana nawahi ofisini”
Kutoka anapoishi nyumbani kwao, mpaka Posta katika ofisi za Transcontinental General Supplies Limited,kulikuwa kuna umbali kidogo.Hiyo ilimlazimu awahi ili akimbizane na muda,akapanda daladala mpaka Ubungo, ambapo hapo akachukua daladala nyingine ya Posta,kutokana na msongamano wa magari ulifanya foleni iwe ndefu,ikapelekea kufika ofisini saa mbili na nusu.Ofisi hiyo, haikuwa ngeni kwake,akafika na kumuona sekretari.
“Namuulizia Mr.Muna,nimemkuta?”
Ahmed,aliuliza alivyofika kwenye meza hiyo kubwa.
“Yes yupo,una muhitaji kikazi ama bi…”
Kabla ya kumalizia sentensi yake Mzee mnene kiasi,mfupi mwenye kitambi cha kiaina akafungua mlango!Sekretari akatulia kidogo,akaonekana kama anachomekea vizuri na kujiweka sawa.
“Bosi,kulikuwa na mgeni wako hapaa”
“Aaaah kijana,Ahmed.Njoo ofisini,pita pita pita pita”
“Ahsante,Shikamoo”
Mzee akamchangamkia sana Ahmed,wote wakaingia ofisini na kumwambia akae kwenye kochi la wageni.Ofisi,ilikuwa kubwa ya kisasa yenye ‘Furnitures’ za gharama,mbele yake kulikuwa na meza kubwa, ambayo juu ina kompyuta ya kampuni ya ‘Apple’ kando kuna ‘laptop’ ilielekea haikuwa ofisi ya mchezomchezio,hiyo ilimfanya mpaka Ahmed,aanze kuogopa ingawa hakujua ni kwanini.
Baada ya salam za hapa na pale,wote wakasimama na kutoka nje ambapo, walinyoosha na kuingia ndani ya mlango mwingine, hapo kulikuwa na ofisi pia,nyuma ya meza aliketi mwanamke mwenye rangi ya maji ya kunde,akawa karibisha kwa tabasamu mwanana.
“Rebecca”
“Abee boss”
“Huyu,ndiye Ahmed.Yule kijana niliyekueleza,utamfundisha namna ya kufanya kazi.Mtashirikiana”
“Ahmed,hapa ndio ofisi yako.Utakaa pale!Rebeca atakuwa anakufundisha mambo ya hapa na pale,hapa ofisini kuna itfaki.Zingatia”
“Sawa,ahsante”
“Kazi njema”
Mzee Muna,akawa tayari amemaliza zoezi lake!Jukumu hilo akamuachia Rebeca,ambaye kwa wakati huo alikuwa kama meneja manunuzi, ndani ya kampuni ya Transcontinental General supplies.
*******
Ukubwa wa chumba hiko ulitosha kabisa kuhifadhi madawa ya kila aina,hivyo dawa zote waliziweka ndani ya chumba hiko.Katikati kulikuwa na vitanda viwili tu ambavyo chini, vilikuwa na magurudumu,madaktari walikuwa makini na mikasi pamoja na sindano.Kifupi chumba hiko kilikuwa kama hospitali ndogo,ambayo haikusajiliwa sababu serikali haikuitambua!Juu ya kitanda kimoja wapo alilazwa Hajrath,haelewi kitu chochote yupo nusu kaputi hana nguo hata moja.Ilikuwa ni lazima zoezi hilo lifanyike,apasuliwe tumbo ili kete za madawa ya kulevya yapakiwe,mzigo usafirishwe.
“Ushamchoma hiyo dawa?”
Daktari mmoja alimuuliza mwenzake.
“Tayari”
“Nipatie mkasi”
“Huu hapa”
Dokta Thomas Mnyali,alishika mkasi mrefu ili afanye kazi hiyo ya kuchana tumbo la Hajrath.Lakini kabla ya kufanya hivyo aliomba ruksa kutoka kando,akachukua simu yake na kutuma ujumbe mfupi ‘TAYARI INGIENI’Baada ya kuweka simu juu ya meza,akachomoa bastola kutoka ndani ya draw.
“Upo chini ya ulinzi,kaa chini”
Dokta Thomas Mnyali,alizungumza huku akichomoa kitambulisho kilichoonesha alikuwa ni mpelelezi.Tayari jumba hilo lilizungukwa na makachelo kutoka jeshi la polisi,wakaliweka kati tayari kwa kumkomboa, Hajrath Mpilla.
Kila kitu kilikuwa kimepangwa na watu makini, kuanzia usalama wa taifa mpaka jeshi la polisi la Tanzania ambalo miaka yote lilipiga vita sana, juu ya matumizi ya madawa haramu ya kulevya,baada ya kufanya uchunguzi wa chinichini ilibidi wamtume Kachero mmoja, akaombe kazi ya udaktari,ni kweli alikuwa ana taaluma hiyo,akagushi kitambulisho na cheti kilichoandikwa Thomas Mnyali,hapo alifanikiwa kuingia ndani ya jumba hilo huku akichora ramani na kuwapa jeshi la polisi.
Kila kitu kilichotokea, ilikuwa ni lazima atoe taarifa,ngazi za juu.Huko walijiandaa sababu nyumba hiyo ililindwa na walinzi waliokuwa na silaha za moto ili kuingia ulihitajika umakini mkubwa zaidi.Askari walikuwa nje ya nyumba hiyo,jinsi walivyoizingira hakukuwa na njia yoyote ya mtu kuingia ama kutoka bila ya wao kumuona, kifupi waliiweka nyumba kati wakiwa makini na Diffenda zao!Na kitendo cha Dokta Thomas Mnyali,kutuma ujumbe ya kwamba wazame ndani, wakapiga teke geti na kuanza kurusha risasi.Walinzi nao walijibu mapigo.Hiyo ilimfanya Florian aliyekuwa ndani, anakunywa mvinyo kwa kujipongeza ashtuke,akainuka na kusimama wima mpaka dirishani,akavuta pazia.Lundo la maaskari lilimtisha.
“Hamisi,tumevamiwa na maaskari.Tuondoke”
Florian alizungumza huku akimtaarifu mwenzake, ambaye walikuwa wanakunywa wote mvinyo,hapohapo wakachukua bastola zao tayari kwa kuanza kukimbia.Wakatembea kwa haraka na kushuka ngazi,ambapo wakaingia ndani ya chumba alicholazwa Hajrath!
“Paa! Paaaa!”
Kitendo cha Dokta Thomas Mnyale kugeuka na kuachia risasi kwa ghafla,Hamis nayeye akavuta triga yake.Alivyofyatua Hamisi ilimfikia Dokta Thomas ya tumbo.Hamisi,akapigwa risasi ya bega akayumba mpaka ukutani.
“Paaaaaa!”
Florian nayeye hakuwa nyuma,akafyatua risasi ambayo ilimfikia Dokta Thomas kichwani,akamuuwa!
“Hamisi,vipi?”
“Mkoonooo,fanya tuondoke eneo hili sitaki kwendaa jela”Hamisi alizungumza huku akijikaza kisabuni,damu zilikuwa zinamvuja mkononi,akachana shati lake na kujifunga.
“Poa”
Mambo aliyokuwa anafanya Florian,siku hiyo ungekataa.Kila kitu alikifanya kimafia.Hakuwa yule Florian ‘Romantic’mpenda mapenzi,siku hiyo alikuwa kama mwanajeshi.Akasogea mpaka kwenye kitanda alicholala Hajrath,akamfunika vizuri na nguo, akaweka bastola yake kando.
“Bonifasi,kafunguwe ule mlango tuondoke humu.Fanya haraka”
Wakati Florian anasema hayo alikuwa bize, kukusanya kila kitu cha muhimu ikiwemo begi kubwa lililojaa madawa ya kulevya,akaingia ndani ya chumba kidogo ambapo huko kulikuwa na silaha nyingine za moto.Akachukuwa bastola moja na kuiweka kiunoni,akabeba na kitu kama duara kilichofanana na tufe,lakini kwa juu kidogo kilikuwa na kitobo.Hilo lilikuwa ni bomu la machozi!Alichofanya ni kumbeba Hajrath mikononi,akatembea mpaka seblen ambapo huko walisaidiana na Bonifasi kusukumiza kabati dogo,baada ya kufanya hivyo likaonekana tobo kubwa sana.
Hiyo ndio ilikuwa njia yao ya siri, endapo mambo yao yataharibika.Walielewa fika ya kwamba biashara yao ni haramu, hivyo ilikuwa ni lazima, wajihami.
“Mpitishe kwanza”
“Mkamate kwa huko,nataka nimpigie simu Lukundo”
“Baadaye ngoja,askari wapo nje”
Mikakati kabambe ilipangwa,Hajarth akaingizwa ndani ya uwazi huo ambapo kwao ulikuwa ni kama mlango wa dharura,Florian akafuatia nyuma yake na wengine wote wakaunga mkia,Bonifasi alivyoingia wakasaidiana na Florian tena kulivuta kabati ili kuliweka sehemu yake.
Kitendo cha kumalizia kulivuta kabati,polisi wakazama ndani seblen.Hakuna hata mmoja kati yao aliyeelewa kwamba nyuma ya kabati kuna njia,japokuwa wote walilipita kabati hilo karibu kabisa na kuanza upekuzi chumba kwa chumba, wakiwa na bastola zao mikononi, tayari kwa mashambulizi sababu walisikia mirindimo ya bastola.
“Mkuuu”
Afande,mmoja aliyezama ndani ya chumba alimuita mwenzake, baada ya kuona vitu kama mikasi,madawa na vitanda vya wagonjwa.Chini kulikuwa na kachero waliyemtuma, amekufa kapigwa risasi!Damu nyingine zipo chini,hiyo iliwapandisha mori zaidi,wakapandwa na hasira mno.
“Ovaa ova mkuu,unanipata.Kuna maiti ova ova kishiiiiii”
Kwa njia ya redio upepo,taarifa zilikuwa zinatolewa, askari wakazidi kuzunguka nyumba hiyo bila kuambulia chochote,hiyo ilifanya wazidishe msako.Lakini wapi!Kwa kupitia bomba kubwa lililofanana na ‘Pvc pipe’ humo walikuwa wakitembea kwa staili ya kutambaa kama mtoto mdogo,Hajrath akawa anaburuzwa.Ndani kulikuwa na giza nene,kwa kutumia tochi ya simu waliweza kuona njia.Mmoja wapo, akatoa simu ili awasiliane na mtu atakayewapokea,njia hiyo ya chini kwa chini, iliunganishwa mpaka nyumba ya jirani, ambapo hapo walitakiwa watokee uwani kwenye chemba.
Ungeangalia Chemba hiyo ungedhani ni maalum kwa ajili ya haja kubwa lakini ilikuwa niya kufanya tukio kama hilo la dharura.Bwana Lukundo alikuwa tayari amewasiliana nao,akalifungua na baada ya dakika mbili.Florian na wenzake wakawa wametokeza.
“Nilizani mmekamatwa tayari”
Bwana Lukundo, alizungumza huku akiteremsha ngazi chini ya shimo.Wakapanda ngazi na kuibuka kwa juu ambapo baada ya hapo,walifunika na mfuniko.Bwana Lukundo, akachungulia nje akaona bado kuna askari wengi!
“Mtatumia gari langu kutoka,tutawasiliana”
Hakukuwa na muda wa kupoteza kwa wakati huo tena,taratibu za kumpakia Hajrath zikaanza upya ili mpango wao uendelee,gari aina ya Suzuki Vitara yenye namba za Usajili, TZP 4537 lilikuwa linatoka ndani ya geti,ndani alipakiwa Hajrath pamoja na Florian wakiwemo na wenzake,tayari kwa kuwatoka maaskari ambao walikuwa mita kumi mbele yao!Bila kuwekewa mashaka ya aina yoyote ile walifanikiwa kuondoka mahali hapo,bila kuamini muujiza huo kwani kila mmoja ndani ya gari hilo alikuwa mwenye wasiwasi sana!
******
Kitendo cha Hajrath kupotea katika mazingira ya kutatanisha,kiliwafanya marafiki zake washindwe kuelewa ni kitu gani wakifanye.Mbaya zaidi simu yake haikupatikana hewani,siku ya nne ilivyofika bila kumpata, ilibidi waanze kuuliza ni wapi Florian alipo ili wajue kama anajua lolote,kwani kivyovyote vile walijua yupo naye kama sio hivyo angejuwa ni wapi angepatikana.
“Kwani Florian,anaishi wapi?”
Swali hilo lilitoka kwa Mpangw’a, akimuuliza Amney.
“Mimi sipajui,ngoja nikamuulize Julius Saki”
“Ndio anapafahamu?”
“Nadhani”
Mguu kwa mguu,nyuma Mpangw’a mbele Amney,wakaongozana mpaka kwa mwanafunzi anayeitwa Julius Saki.Ambaye mara nyingi, huonekana na Florian.Hata huyo ilionekana kumpata haikuwa kazi rahisi kama walivyodhani.
“Alikuwa hapa sasa hivi,sijui yuko wapi”
Alijibu jamaa huyo,akiwa na laptop yake mezani.
“Huna namba yake ya simu?”
“Simu yake,mbovu”
“Sasa itakuwaje?”
“Kwani mna shida naye gani?”
“Kuna mambo fulani nataka kumuuliza”
“Huo mtihani sasa,msubirini kidogo anaweza akaja”
“Ah,tutakuja baadaye”
“Sijui kama mtanikuta”
“Tupe namba zako,tutakupigia”
Jamaa,akatoa namba. Amney na Mpangw’a wakaondoka zao, wakiwa na wasiwasi mkubwa sana,haikuwezekana hata kidogo Hajrath achukuwe siku zote hizo bila ya kuwasiliana nao!Ndiyo maana, walikuwa na wasiwasi mkubwa.
“Usikute mwenzetu yupo Ulaya,sisi tunapuyanga tu hapa”
“Asituage?”
“Si unajua tabia yake ya usiri”
“Hajrath,namfahamu.Angepost picha WatsApp”
“Kwani kule mtandao upo?Ana laini ya kule?”
“Lakini inawezekana,si aliniambia Dada yake Florian yupo Oman, sijui Uingereza”
“Basi nina uhakika yupo huko”
“Nitamchamba akirudi,kwanini atuweke rohoo juu juu”
“Mimi kama hajaniletea zawadi,atanikoma”
Hakuna hata mmoja kati yao, aliyeweza kubashiri ni wapi Hajrath alipo,hapo walikuwa ni kama wanahisi tu,hawakujua kama rafiki yao yupo katikati ya mateso na yupo mbioni kupakiwa madawa ya kulevya tumboni kisha baadaye asafirishwe yakashushwe,auwawe kwa kifo kibaya sana!Japokuwa waliwaza hayo, lakini hiyo haikuwafanya wasitishe kumsaka rafiki yao kipenzi Hajrath,kwani kutokuwepo kwake lilionekana pengo kubwa.Hajrath alikuwa ni mcheshi,mwenye stori nyingi zisizoisha mbali na upole wake lakini upande mwingine wa shilingi alikuwa ni muongeaji kuliko chiriku!Jambo hilo ndilo lilimfanya wamkumbuke zaidi na zaidi.Usiku wa siku hiyo,wakamtafuta jamaa ili wajue ni kwa njia gani watampata Julius Saki hewani ili kujua ni wapi Florian alipo,ulikuwa ni mlolongo kidogo lakini hawakukata tamaa.Hawakuwa na budi,usiku huohuo wa saa mbili wakamuibukia Julius Saki hosteli kwake,ambapo tayari waliambiwa kwamba yupo.
“Hodi,hodi mpaka ndani”
Amney,alizungumza huku akianza kuvua viatu vyake.
“Usivue viatu,ingieni tu msijali”
“Tutachafua”
“Msijali,nitadeki”
Chumba kilikuwa kisafi,lakini hakutaka kuwapa shida warembo hao ambao hata siku moja hawakuwahi kuingia chumbani kwake.Kwa mawazo yake,akajua tayari ameokota embe chini ya mpera ama zali la Mentali.Hasa alivyomuangalia Amney,mawazo yake yakajua msichana huyo mrembo amekuja kwa ajili yake!
“Karibu,karibuni.Kuna juisi,maji.Soda..Nakadhalika”
“Mimi nipe nakadhalika”
Mpangw’a akasema kwa niya ya kuweka utani,wote wakacheka na kutulia kidogo!
“Sisi sio wakaaji”
Amney,akaanza mazungumzo.
“Hata maji basi…”
“Siku nyingine Julius.Tunamuulizia Florian,hivi yuko wapi?”
“Florian Fredrick?”
“Ndio”
“Mimi mwenyewe,namtafuta sana”
Jambo hilo lilifanya kila mtu ashangae,kwa Julius kusema hivyo, lilikuwa ni jambo la kutisha sana kwao.
“Hujui kivipi!?Si rafiki yako?”
“Ndio,lakini hizi siku mbili tatu hizi,alikuwa bize sana.Kuonana naye mara mwisho ilikuwa last week.Tena ilikuwa Tengeru kule,alikuwa mwenye haraka sana”
“Duuuu!”
“Vipi kwani?”
“Hapana,hamna kitu”
Wakaaga na kuondoka zao!Jitihada za kumtafuta Hajrath zilikuwa palepale,hawakuchoka.Hatimaye mwezi,ukakatika ‘test’ zilianza lakini hakukuwa na dalili za Hajrath kuonekana wala Florian.
Siku ya ‘Graduation’ ilivyofika,wakategemea wenda Hajrath angetokea lakini hola.Taa nyekundu zikaanza kuwaka vichwani mwao!Siku hiyo ilibidi wajitose kimasomaso mpaka kwa Ahmed,ambaye alikuwa amevaa joo jeusi,kumaanisha kwamba tayari amehitimu masomo yake.Alikuwa mwenye furaha siku hiyo isiyo kifani,kikofia chake kipo juu.Kila mtu anaomba apige naye picha.
“Ahmed,tupige picha moja.Asha,shika simu nipige picha.Piga nzuri nataka kurusha Instagram,sio hivyo.Tumia 360”
Siku hiyo Ahmed,akageuka na kuwa mashuhuri na kichwa cha habari chuoni.Hiyo pia ilitokana na kutangazwa kuwa amefikisha 1st class.Walimu walijivunia,hata wao muda wote walikuwa beneti naye kupiga picha.Wazazi wake ndio usiseme, walipewa hongera zisizokuwa na idadi kamili, wakavimba kichwa kwa sifa.
“Hongera Ahmed”
Sauti hiyo ilisikika baada ya kutoka kupiga picha na msichana anayeitwa Salma Mosha,alivyogeuka akagundua alikuwa ni Amney.Akatabasamu na kumpa mkono,tofauti zao akaweka kando!
“Ahsante Amney”
“Za masiku?”
“Salama”
“Naona ushaanza mpaka kunenepa,kitabu kilikuwa kinakupa stress,kweli mtaani kuzuri”
“We acha tu”
Haukuwa utani Ahmed,alinawiri.Mashavu yake yalikuwa makubwa kiasi,kitambi cha wastani.Hilo lilikuwa waziwazi kabisa kwamba alinenepa na pesa zilianza kumfuata.
“Hongera tena,nakuonea mpaka wivu.Natamani kumaliza chuo,nishachoka na msoto.Stress tu kila kukicha”
“Bado mwaka,vumilia tu.Ushakula Ng’ombe mzima,kabaki mkia”
“Mkia,ndio unakuwa mgumu kuisha.Ebu nikupe mfano hakuna supu ya gharama kama ya mkia,ndio ujue sasa”
Amney na Ahmed,walikuwa katika stori kubwa kana kwamba hawakuwahi kuwa na ugomvi kabisa.Hapo ndipo,Amney akapata nafasi ya kuchomekea jambo la Hajrath kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
“Atakuwa na boyfriend wake,Florian”
“Hata yeye,hajulikani alipo”
“Namfahamu Hajrath,msichana makini sana!Huko alipo najua,yupo salama”
“Mmmh,kweli?”
“Ndio”
Ahmed akaondoka eneo hilo ili kuongea na rafiki zake,akatumia nafasi hiyo kuwapa moyo na kuwaambia hata wao wana uwezo wa kufaulu endapo tu,wakizingatia masomo!
“Hakuna kitu kirahisi Rameck,hata uende wapi.Kila kitu lazima upambane,hata ukitaka demu lazima utumie mbinu za kumpata ni sawa katika kila kitu hapa duniani”
“Kweli kabisa kaka”
“Ndio hivyo,maisha ni vita isiyokuwa na mwisho piga kitabu mzee”
Ahmed akaondoka,picha zote alizopiga akamtumia mpenzi wake Yusrath,kila kitu kikageuka na kuwa furaha kubwa sana!
Wakati siku hiyo akiwa kwenye sherehe ya kuhitimu masomo yake,chuo kikuu.Huku nyuma aliacha mchakato wa 'passport' za viza ili aelekee nchini Malaysia kwa ajili ya kujiendeleza na kupata masters!Ilikuwa furaha sana kwake,lakini huzuni tele kwa Yusrath, ambaye kwa muda mchache alikuwa tayari amemzoea,alijipa moyo kwa kuwa aliamini ya kwamba ipo siku, Ahmed atarudi tena na ndoto yake ilikuwa wafunge ndoa,wawe mme na mke!
“Ukirudi mpenzi,utanikuta.Mimi ni wako”
Hayo ndiyo yalikuwa maneno ya Yusrath,kila Ahmed alipogusia swala la ngono,hakuwa na hiyana.Yote yalikuwa sawa tu,sababu alimuamini sana Yusrath wake,wiki moja baadaye baada ya mahafali,viza ikawa tayari kwa safari ya kuelekea nchini Malaysia jijini Kuala Lampur,Malven International University,chuo hiko kilikuwa nje kidogo na jiji hilo karibu kabisa na mji wa Cheras!Huko ndipo Ahmed,alitakiwa kwenda.Alisikitika lakini hakuwa na jinsi.Siku ya siku ikawadia,hakuna siku ambayo ilikuwa ngumu kama hiyo kwa Yusrath,alilia mpaka basi simuni.
“Yusrath,usilie Mke wangu.Safari sio kifo,nitarudi mamii”
“Nime..kuzoea sa..na Ahmed wangu,miaka miwili ni Mi..ngi sana.Usije ukani..saliti taf..adhali”
“Siwezi kufanya hivyo, I promise you!To the moon and back,wewe ndio mke wangu”
“Promise me kama hutonisaliti”
“Siwezi i promise you,au tukale yamini?”
“Hapana mpenzi,nakuamini”
“Ahsante kwa hilo”
“Kes..ho safari saa ngapi?”
Yusrath,alizungumza kwa kwikwi.Akafuta machozi.
“Saa mbili asubuhi mpenzi”
“Natamani,ningekuepo nikuage.Lakini sitoruhusiwa”
“Naelewa Baby,usijali.Tutazidi kuwasiliana,naamini hilo ndilo litatuweka karibu zaidi”
Siku hiyo walikuwa simuni wakizungumza mambo mengi sana kwa Yusrath ilikuwa ngumu kumeza lakini hakuwa na jinsi kulia kwake kusingebadilisha kitu.
Siku iliyofuata Ahmed alikuwa njiani,kuelekea uwanja wa Kimataifa Mwalimu Nyerere International Airport,kwa ajili ya kusafiri na shirika la ndege ya Malaysia Airlines,njia nzima Ahmed alizungumza na kuwahaidi wazazi wake,atasoma na hatowaangusha.Baba yake,alifurahishwa sana na ahadi hiyo.
“Kama tulivyoongea Ahmed,ukirudi tu mambo yatakuwa vizuri”
“Sawa Baba”
Wakaingia uwanja wa ndege na kuegesha gari vizuri kwenye maegesho,hapo walishuka na kuanza kutembea kwa haraka mpaka walipofika sehemu maalum, ambapo abiria wanasubiri ndege!
“Sina cha kuongeza zaidi mwanangu yote tushaongea,nakutakia kila la kheri.Uko mbali na wazazi.Cha msingi ujue kinachokupeleka”
Mama alimsihi mwana kwa mara nyingine,haikuwa mara ya kwanza kumueleza vitu kama hivyo,kifupi alikuwa kama anapigilia msumari tu swala lake!Nusu saa baadaye,kipaza sauti kutoka kwenye spika kilisikika,ndege aliyokuwa anatakiwa kupanda Ahmed, ilikuwa tayari imetua.
Hapohapo, bila kuchelewa akaanza kuburuza mabegi yake,akasimama mpaka kwenye kimlango maalum, ambapo hapo walihitajika wasafiri tu,akawapungia wazazi wake mkono kwa ishara ya kuwaaga kisha akaingia ndani, ambapo humo aliweka begi lake sehemu maalum,likaanza kupitishwa ndani ya mashine, yeye akavua saa pamoja na mkanda.Akaviweka wenye kapu na kuingia,akatokea upande wa pili!Taratibu zilivyokamilika akaingia ‘Boarding pass’ na kukamilisha kila kitu,kama kugongewa mihuli na kupewa namba ya siti yake.Kitendo cha kusubiri geti namba 23,aligeuka pembeni na kuona sura ambayo ilimshtua kidogo! Hakuelewa kama ameifananisha ama macho yake,yalimdanganya.Kichwa chake kilimuwaza Yusrath tu,akamtumia meseji ya kwamba ndio anaanza safari,kipaza sauti kikasikika ya kwamba waingie ndani ya ndege,akiwa na tiketi yake mkononi akaanza kutembea kuelekea kwenye mlango mkubwa, hapo kulikuwa na staili ya kupita mmoja baada ya mwingine ukionesha tiketi yako kwanza.
“Florian Fredrick,have a safe flight”
Moyo wa Ahmed ukapiga paaa!Baada ya kusikia jina hilo limetamkwa na mhudumu wa kiarabu, aliyeshika tiketi ya mwanaume aliyekuwa mbele yake,hapo ndipo alijuwa kuwa hakumfananisha bali ni kweli ni Florian Fredrick.Wote wakaingia ndani ya ndege,akitegemea kwamba Hajrath pia,angekuwepo lakini wapi.Alisubiri sana,lakini hakumuona.Hakutaka kusubiri zaidi,akamsogelea Florian mpaka siti aliyokaa na mwanamke shombeshombe!
“Florian,mambo vipi kaka!Niwewe,sitaki kuamini”
Ahmed,akasalimia kwa uchangamfu lakini cha ajabu, Florian akamtizama kama hamjui vile.
“Sorry,do i know you?”(Samahani sijui tunafahamiana)
“Aaaah Florian,acha masihara.Mambo vipi?Unaelekea wapi?Nawewe unaenda Malaysia?Basi tutakuwa wote kaka siti yangu iko pale,nimekaa na yule mchina ala…”
“I don’t speak your language”(Siongei lugha hiyo)
Kwa Ahmed,alidhani wenda Florian anamtania na kumzingua lakini haikuwa hivyo,Florian alikaza na kujifanya hamjui akamtolea nje.Hiyo ilifanya wenda Ahmed adhani ni kweli amemfananisha,lakini hakutaka kulipa swala hilo kipaumbele,kuna kitu alianza kuhisi cha hatari hasa alipoona mwanamke aliyekaa pembeni ya Florian,kamuegamia begani.
“Excuse me”
Mtu aliyemshtua ni Mzungu aliyekuwa nyuma yake,anataka kupita, huyo ndiye aliyemzindua kutoka kwenye mawazo ya kumtizama Florian ya kuunganisha tukio la Hajrath kutoonekana Chuoni,Makumira!
Kelele za abiria ndani ya ndege wakiwa wanapita kila mtu kutafuta siti yake zilimfanya Ahmed,ashindwe kuendelea kusimama eneo hilo,kumuhoji Florian ambaye alimkana kama Petro,akaachana naye na kurudi kwenye siti aliyopangiwa ambapo hapo,pembeni yake aliketi mwanamke wa kichina,dirishani alikaa mwanamme wa kizungu amevaa miwani anasoma kitabu.Ghafla sura ya mpenzi wake Yusrath,ikamjia kichwani.Akakumbuka vitu vingi sana hususani mpango wao mzima wa mapenzi na safari yao iliyojaa changamoto chungumzima.
Japokuwa aliamini fimbo ya mbali haiuwi nyoka lakini alijipa moyo, Yusrath ataendelea kuwa mvumilivu na mwaminifu mno kama alivyomuhaidi.Matukio yakawa yanapita kichwani kwake akawa kama anaangalia sinema fulani ya kihindi.Kilichomshtua katika dimbwi hilo la mawazo ni kipaza sauti nyororo kilichotoka kwenye spika kikiwataka abiria wote, wafunge mikanda.Abiria wote wakawa bize kufunga mikanda yao,hiyo haikutosha wahudumu waliovalia sketi za rangi ya kijani na mashati meupe, wakaanza kupita kukagua abiria mmoja baada ya mwingine ili kuhakikisha kama zoezi hilo limefanyika.Kila kitu kilivyokwenda sawa,matangazo yakaanza kurushwa, namna ya kutumia parashuti na mitungi ya gesi endapo ndege italeta itlafu.Hazikupita hata sekunde tatu taratibu ndege ikaanza kutembea,kadri dakika zilivyozidi kwenda mbele, ndipo ndege ilizidi kuchanganya mwendo,hatimaye ikaanza kutembea kwa kasi ya kimondo!Ilivyofika kwenye barabara yake,kichwa kikaanza kuinuka matairi yakaanza kuachia ardhi ya Tanzania kisha matairi ya nyuma yakafuata, ikazidi kwenda juu angani,huko matairi yakaingia ndani ikapotelea kwenye mawingu.
*******
Yalikuwa ni majonzi makubwa sana kwa Yusrath Suleiman,moyo ulimuuma ajabu.Japokuwa alijaribu kujifariji lakini hali ilikuwa ni ileile,akajipa moyo ya kwamba Miaka miwili ni michache lakini nafsi ilikataa kukubaliana na jambo hilo,mbaya zaidi masaa yalijivuta kwa mwendo wa kinyonga,hilo ndilo lilimchanganya zaidi.Alibaki mpweke,usiku alizoea kuongea na Ahmed, hiyo ikawa kama tabia sasa.Licha ya kutafakari hayo yote alimuomba Mungu wake, Ahmed afike Nchini Malaysia salama salmin,siku hiyo usiku.Siku ambayo Ahmed amesafiri alikuwa kama kinda la ndege aliyeachwa na mama yake,hakuwa ana hamu ya kula chakula cha usiku.Hata Mama yake alivyomfuata na kumuhitaji mezani wajumuike kwa pamoja,alitoa sababu ya kwamba anajisikia vibaya hana hamu ya kula.
“Una Malaria?”
Mama akamuuliza mwana huku akimgusa shingoni,Yusrath alikuwa chumbani.Amejifunika shuka tayari,hiyo ilimaanisha ya kuwa anataka kulala.
“Hapana Mama,nipo okay”
“Sasa shida nini?”
“Nitakuwa tu sawa lakini kwa sasa,sijisikii kula”
“Basi tutakuachia chakula mezani,uamke usiku ule”
“Sawa Mama”
Mama akatoka chumbani na kufunga mlango,akimuacha Yusrath katika dimbwi la mawazo tele,sababu iliyomfanya asile ilikuwa ni moja tu,Ahmed.Kitandani alijaribu kuusaka usingizi lakini zoezi hilo, likaonekana kuwa gumu kwani kitu usingizi kilikuwa ni hadimu sana kupatikana usiku huo,alitamani usiku huo asikie sauti ya Ahmed,akimwambia maneno matamu na mazuri na kumtakia usiku mwema!Mpaka saa tano usiku, usingizi haukupatikana,akaona bora apoteze muda kwa kuchukua simu yake ili kutembelea mitandao ya kijamii kama Facebook na WatsApp,huko aliamini angefanya muda uwende.Akazama Facebook na kuangalia picha mbalimbali,alivyotoka akafungua WatsApp huko akawa online,baada ya dakika moja akasikia ujumbe umeingia alivyoangalia vizuri, akagundua umetoka kwa Kassim,akaufungua.
‘Bado,hujalala?’
Ujumbe huo ulitoka kwa Kassim.
‘Hapana’
‘Usiku wote huu?’
‘Ndio,lakini nataka kulala sasa hivi’
‘Sijakuona Airport leo’
‘Yeah,sikuweza kuja.Mom,alikataa nitoke’
‘Pole sana,Ahmed kaondoka.Umebaki mpweke sana’
‘Nitazoea tu’
‘Sio rahisi lakini’
‘Naelewa lakini nitaweza’
‘Mmh,nitakuwa nakupa kampani usijali’
‘Ahsante,usijali’
‘Najali,nataka tutoke next week.Nikutoe outing’
‘Sitoweza’
Japokuwa alielewa ya kwamba kaka yake tayari yupo na Yusrat lakini hilo hakujali,alitaka ale naye sahani moja japokuwa alijuwa kwa kufanya hivyo lilikuwa ni kosa kubwa sana,ndiyo maana tangu asikie Ahmed yupo na Yusrath,alijisikia vibaya na kuanza chuki za chini kwa chini.Ndio maana siku hiyo usiku baada ya Ahmed kuondoka alitaka kuutumia mwanya huo,kupeleka majeshi yake kwa Yusrath.Msichana aliyetamani amvue nguo yake ya ndani.
Ingekuwa kila msichana ama mwanamke akitembea na Kassim, anamtoboa usoni basi sura yake ingefanana na Chandarua ama nyavu ya kuvulia samaki kwani angekuwa na matobo mengi sana,Kassim katika maisha yake hakutaka kupenda.Starehe yake yeye siku zote ilikuwa ni wanawake,aliona ufahali kuwachanganya kama karata,sio siri kama ingetokea ungemsikia namna anavyotongoza ungesema huyu ni mwanaume mwenye mapenzi yake kumbe ni fisadi aliyejaa uzandiki mkubwa.Tabia hiyo haikujulikana kama karidhi ama ana pepo la ngono na ilikuwa ni lazima baada ya kufanya ngono na msichana mpya, ajipongeze kidogo.
“Huyu nitampata,tu.Mbio za sakafuni huishia ukingoni”
Siku hiyo Kassim alijipa moyo akiapia ya kwamba ni lazima angemnasa Yusrath,akiwa amemaliza kuchat na msichanna huyo,akainua simu na kumtafuta demu wake anayeitwa Monalisa Japhet, akimtakia usiku mwema.
“Mbona hujalala Kassim?”
Monalisa aliuliza simuni.
“Wewe mbona hujalala?”
“Hilo sio jibu lakini.Kassim,mbona siku hizi umebadilika sana?”
“Nimekuaje tena?”
“Sikuelewi,haupo kama zamani!”
“Kwani zamani nilikuwaje Mona?Nilikua wa kijani kibichi?”
“Ulikuwa unanipenda”
“Usiku mwema,naomba nilale”
Hiyo ndiyo ilikuwa tabia ya Kassim,swala la kuanza kubembeleza mtoto wa kike lilimpitia kushoto hususani akiwa tayari keshaona nguo ya ndani,alikata simu na kulala akitafakari njia mbalimbali na gia tofauti tofauti za kumnasa Yusrath.
******
Licha ya Kassim kuendelea kumpigia simu usiku na kumsumbua akimtaka kimapenzi lakini msimamo uliendelea kuwa palepale,Kassim hakukoma.Akazidi kutupa mawe na kumuimbisha kila nyimbo ili siku moja aje kuwa wake,niya na madhumuni yake yakiwa ni kumvua nguo yake ya ndani, afanye naye ngono.Lakini hilo lilionekana kuwa gumu,Yusrath alimchomolea akampiga mkwara akimwambia kama angeendeleza habari hizo, zingefika kwa kaka yake,hapo Kassim akatulia kidogo sababu alijua ni kitu gani kingetokea endapo, Ahmed angegundua swala hilo.Mapenzi yao yalikuwa vilevile,mawasiliano kati ya Ahmed na Yusrath yaliendelea kila siku,akiwa nchini Malaysia alimpigia wakitumia mtandao wa ‘Skype’ usiku walikuwa wakiongea huku wakionana.
“Nakumisi Ahmed”
Siku hiyo Yusrath,alideka huku simu yake ikiwa juu,amelala chali.Amejifunika na shuka!Anamuona Ahmed simuni.
“Mimi pia,mama watoto”
“Miaka miwili ni mingi sana”
“Sio mingi baby wangu”
“Ni mingi Ahmed.Naomba usinisaliti”
“Hilo usijali,ondoa shaka”
“Ujaona wadada wazuri huko Ahmed?Hawajakuchanganya?”
“Wapo,lakini hawakufikii wewe hata kidogo!Kama ni gari kwako nimefunga breki”
“Nakupenda sana Ahmed,nimeamua kukuchagua wewe.Uje kuwa mme wangu,sitaki nije kujuta baadaye.Kila nachofanya sasa hivi ni kwa ajili yetu”
“Nina kuhaidi hilo,nikirudi tu.Nitakuja kwenu!Kujitambulisha kwa wazazi wako wanijuwe”
“Kweli Ahmed?”
“Yes Baby”
Baada ya maongezi hayo kuisha,ghafla wakaanzisha hadithi nyingine za mahaba.Ahmed,akamgusia Yusrath kuhusu swala zima la tendo lililowaleta duniani.
“Usijali kuhusu hilo,hata mimi nina hamu sana ya kukutana nawewe.I need to sex with you”
Jinsi Yusrath alivyozungumza, ilifanya mwili wa Ahmed,usisimke ajabu.Hata siku moja hakuwahi kuyaona macho ya Yusrath yakiwa yamelegea namna hiyo,ikapelekea mpaka damu yake iende mbio, karoti yake ikasimama wima,blanketi alilojifunika likatuna.Mbaya zaidi,mabega ya Yusrath yalikuwa nje,shuka liliishia kifuani hiyo ilimfanya Ahmed apagawe zaidi na zaidi.Rangi ya Yusrath ilimpagawisha,ukizingatia hakuwahi hata kumpiga denda,hiyo ndio ikampandisha Mori zaidi.
“Same story here,mimi pia natamani”
“I’m hot,sijui kwanini love,itakuwa ile movie ya Desperado niliyoangalia mchana”
“Huwa unafanya nini ukiwa hot baby?”
“Naenda kuoga maji ya baridi”
“Sure?”
“Yeah, sure love”
“Naomba nitunzie please,ukinisaliti nitaumia”
“Hilo pigia mstari.Kama niliweza kujitunza mwaka mmoja na nusu,kwanini nishindwe hiyo mingine Ahmed?Niamini”
“Nakuamini”
“Masomo yameshaanza?”
“Yes,tayari baby.Tushaanza kufanya research,niombee niifanye vizuri!Si unajua love,kufaulu kwangu ndio mafanikio yetu ya baadaye”
“Naamini hilo”
Kila mtu alitumia imani yake kuamini ya kwamba ipo siku watafunga ndoa na kuishi ndani ya nyumba moja,wakitumia shuka moja kisha baadaye wazae watoto,Yusrath awe Mama, Ahmed baba.
Maongezi yao kwa njia ya simu yalizidi kupamba moto kila usiku ukifika.Hakika walikuwa wenye furaha iliyozidi kifani.Kutoka na Ahmed kimapenzi haikufanya awe na alama kichwani ama kuwa na bango mgongoni,wanaume waliendelea kumtongoza kila kukicha wakimgasi,hawakutaka kuelewa ya kwamba tayari ana mwanaume ambaye yupo nje ya nchi.
“Yupo nje ya nchi?”
“Ndio, kuwa mwelewa.Si nilishakwambia sikutaki,mbona mbishi.Nitumie lugha gani unielewe?”
“Una uhakika gani kama hakuchit?Sisi ni wanaume unajua,hatuwezi kukaa mbali bila kuchiti”
“Sio kwa Ahmed”
“Yeye,huyooo.Ahmed,mchungaji au mgonjwa?Au labda kama hana nguvu za kiume”
“Hapana,sio mchungaji wala Shekh”
“Basi juwa una mwenzako kule.Huo ndio ukweli mchungu”
“Ahsante,siku njema”
Yusrath akakata simu,moyo wake ukachoma kama pasi, wivu ukamkaba maneno ya Ditoo,yalimuumiza moyo akatingishwa,siku hiyohiyo usiku akaanza kumtolea mapovu Ahmed simuni.
“Yusrath,nisikilize”
“Nikusikilize nini,wanaume ndio mlivyo”
“Tupoje?”
“Uko mbali najua utapata mwanamke mwingine”
“Siwezi kufanya hivyo niamini kwa hilo”
“Muongo mkubwa,kwanza nimekumbuka”
“Umekumbuka nini?”
“Nasikia una mwanamke huku Tanzania,unataka kumuoa yeye.Kwenu wanamjua”
“Yusrath,una nini?Unasikia unachokiongea?”
“Kwaio mimi sijielewi au?”
“Sina maana hiyo”
“Kumbe una maana gani?Tuachane Ahmed,achana namimi”
“Yusrath,una nini lakini?”
“Unataka kujua nina nini?Nakuuliza unataka kujua nina nini?Kassim,kaniambia kila kitu.Una mwanamke wako,yupo huku Tanzania,tena unataka kufunga naye ndoa”
“Unasemajeeeee?”
Siku hiyo Yusrath,alitibuka kama kiboko mtoni.Akabadilisha hali ya hewa,akajikuta anaropoka vitu ambavyo hana uhakika navyo,hakuwa yeye bali ni wivu ulimpeleka puta.Jambo hilo lilimuumiza sana Ahmed,hasa alivyokatiwa simu akitaka kujitetea.
*********
Wazazi wa Hajrath waliingia jijini Arusha saa kumi na mbili ya jioni na basi la kampuni ya Kilimanjaro,japokuwa walichoka sana kutokana na basi hilo kusimamishwa njiani na askari wa usalama barabarani lakini hawakutaka kupumzika,iliwalazimu wachukuwe taxi ambayo iliwapeleka mpaka chuo cha Makumira.Kupotea hewani kwa binti yao,takribani mwezi mzima kuliwafanya wafunge safari hiyo ndefu,kwao binti yao alikuwa kila kitu.Japokuwa mzee Mpilla, alimnunia binti yake lakini siku hiyo alikuwa mwenye shauku kubwa sana ya kujua nini tatizo.Hakutaka kuyapa mawazo yake kipaumbele ya kwamba Hajrath katoroka na mwanaume, aliyemtimua nyumbani kwake,katika mtu aliyeonekana kuchanganyikiwa zaidi ni Mama Hajrath.Muda wote machozi yalimlenga,yeye alijuwa ni moja kwa moja itakuwa amekunywa sumu na safari hiyo ni lazima atakuwa amekufa tu japokuwa aliomba Mungu, isiwe kama anavyofikiria.
“Yote umeyataka wewe”
Mama alimtupia lawama njia nzima mumewe.
“Sio muda wa kulaumiana huu.Cha kufanya ni kujua ni wapi alipo,si ajabu kabadili namba za simu tu”
“Angenipigia mimi”
Waliendelea kuzozana huku wakielekea katika lango la chuo,huko walishindwa kupata walimu kwani muda ulikuwa umekwenda tayari,ilibidi siku inayofuata wadamke asubuhi na mapema ili kurejea tena chuoni.Kwao ilikuwa kazi ngumu kidogo kumpata binti yao,sababu ya ukubwa wa chuo hiko kilichokuwa na wanafunzi wengi mno!Wakaulizia mpaka ofisi ya utawala,wakakaribishwa ofisini na kuketi kiti cha wageni.
“Naitwa Mr.Mpilla,namuulizia binti yangu anaitwa Hajrath!”
Kitendo cha kuzungumza hivyo kilimfanya Mr.Raymond Sakaya,ashushe pumzi ndefu kidogo,akawatizama wazazi hawa wawili.
“Ebu,subirini kidogo.Mmesema mnamuulizia nani?”
“Hajrath Mpilla”
“Yupo mwaka wa tatu?”
“Ndio”
“Chuoni hapa hayupo,huu mwezi sasa na nusu”
“Kwahiyo,mmechukuwa maamuzi gani?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Mzee Mpilla,hacheki. Sura amejikunja ilielekea jibu hilo, lilimkera na kumfanya amtizame Mwalimu huyo anayejibu kirahisi namna hiyo.
“Tulimuulizia kwa wanafunzi wenzake,tulivyoona hayupo.Tukadhani labda yupo nyumbani”
“Ukadhani labda?Kwahiyo uka assume tu,atakuwa nyumbani?”
“Ndio mzee”
“Una watoto?”
“Ndio Mzee”
“Ungekuwa wewe ndio mimi ungefanya nini?Hivi una akili sawasawa?Au akili zako zipo matakoni”
Lilikuwa ni swali lililoambatana na sauti kali ya hasira na tusi juu,mkewe aliyekuwa pembeni alishaelewa ni kitu gani kipo mbioni kutokea,ndiyo maana akaingilia kati.
“Kwani,unawafahamu marafiki zake?”
Mama,akauliza kwa niya ya kumtoa mumewe kwenye laini.
“Ndio anao”
“Unaweza ukatuitia ili tuwaulize”
“Hakuna shaka”
Sir.Raymond Sakaya, akasimama na kuanza kuzunguka huku na kule,niya yake ilikuwa ni kumuulizia Amney ni wapi alipo,haikuchukuwa dakika hata mbili,akatokeza akiwa na mwanafunzi huyo wa kike.
“Shikamoo,Shikamoo”
Amney,akasalimia huku akipeleka goti moja chini kidogo kwa adabu zote,ilielekea Sir.Raymond alimuelezea kinagaubaga juu ya wageni hao waliofanya ziara ya kushtukiza ofisini kwake.
“Hajrath yuko wapi?”
Mzee Mpilla bila kuitikia salam,akamdaka na swali.
“Sijui baba”
“Hujuiiiiiii?”
“Ndio Baba”
“Ebu,kaa hapo unieleze vizuri”
Hakukuwa na namna,ilibidi Amney azungumze kila kitu kilichotokea,mpaka Hajrath alivyopotea na mwisho akahitimisha alikuwa ana mahusiano na kijana anayeitwa Florian Fredrick,huyo naye hakuonekana chuoni pia.
“Florian!”
Mzee Mpilla akalikumbuka jina hilo,akamtizama mkewe!Jibu alilopata ni kwamba ni lazima Hajrath katoroka na kivyovyote vile,atakuwa na Florian lakini hakujua ni wapi walipo.Kilichofanyika hapo ni uongozi wa chuo hiko kuandika barua ipelekwe kituo cha polisi ili mchakato wa kumsaka Florian, uanze mara moja!
*******
“Nina mashaka naye,kaniona ananifahamu yule!I have a feeling,atatoboa siri,mambo yataharibika”
“Kwani,alishukia wapi?”
“Malaysia,Kuala Lampur”
“Kuala Lampur?”
“Yes Sweatheart”
“Pale yupo Kingkong,atamaliza kila kitu.Ngoja nimpigie simu”
“Okay Darling”
Florian,hakuwa mwenye amani tena baada ya kuonana na Ahmed ndani ya ndege akiwa na Sporah Treves wanaelekea nchini Israel,moyo wake ulikuwa mzito.Ndio maana akashtaki kwa Sporah ili wajuwe watafanya nini ili kumfunga mdomo!Kifupi mtandao wa Sporah Trevez,ulikuwa na mkono mrefu kuliko Serikali, swala la kumkamata Ahmed ilikuwa ni sawa na kumshika kuku bandani ili achinjwe.Suluisho lililopatikana ni moja tu,kutumwa watu nchini Malaysia, wamuuwe ili wamzibe mdomo mazima!Shobo za Ahmed,zikawa zimemponza ni bora angekaa kimya ndani ya ndege kuliko kujifanya anamjua sana, Florian Fredrick.
Mikakati na mipango ya kumnasa Ahmed ilianza kusukwa punde tu,mtu anayeitwa Kingkong,kuambiwa afanye hivyo.Mawasiliano baina ya Spora Trevez pamoja na Kingkong yalizidi kupamba moto,kila siku iendayo kwa Mungu ilikuwa ni lazima Kingkong, atoe ripoti amefikia wapi na Ahmed anapatikana chuo gani,swala hilo lilikuwa dogo sana kwa mtu kama Kingkong kufahamu.Kwanza alijuana na watu uhamihaji pamoja na uwanja wa ndege Kuala Lampur,hivyo mgeni yoyote yule atakayeingia nchini humo, akitaka kujua ni wapi anaishi kilikuwa ni kitendo cha dakika sifuri,ndiyo maana ikawa rahisi kwake kujua kwamba Ahmed Mohamed Kajeme, anasoma Chuo kikuu cha Malven International University.Taarifa hizo alizipata kwa rafiki yake anayefanya kazi uhamiaji wa nchi hiyo, aliyefahamika kwa jina la Rayyan Danish,kulikuwa kuna uwezekano mkubwa sana wa kutokujulikana ni wapi Ahmed anasoma kama kusingekuwa na taratibu za kuandika,barua ya chuo na kuiacha uhamiaji.
“Nitakupa fungu lako,nitakutumia Westen Union”
“Shukrani”
Siku hiyo alivyopata taarifa hiyo ya Ahmed,akamueleza Sporah simuni kwamba mpango wao, ulikuwa tayari umekamilika, kilichotakiwa ni Ahmed kuchukuliwa na kuuwawa tu.
“Msitumie nguvu,ndio protocol za kazi yetu si mnajua?”
“Nakusikiliza Madam”
“Sharom, yupo huko?”
“Hayupo”
“Trisha?”
“Yupo London”
“Nani yupo?”
“Yupo Sophia,Alicia na Nurin”
“Mwambie Nurin anipigie”
“Sawa Madam”
Hapohapo simu ikakatwa!
******
Kilichompeleka nchini Malaysia, kilikuwa ni masomo tu na si vinginevyo.Aliamini miaka miwili ilikuwa michache lakini ingekuwa changamoto kwa upande mwingine,kutokana na kutenganishwa na mpenzi wake Yusrath ambaye siku zote msichana huyo alimuhesabia ndiye atakuja kuwa mkewe wa ndoa!Hawakuacha kuzungumza kwenye simu kila siku usiku.Ingawa umbali ndio ilikuwa changamoto kubwa lakini mawasiliano yaliwaweka karibu.Masomo kwake yalienda vizuri,alikuwa mwenye furaha na amani, alichoshukuru Mungu alipata rafiki anayeitwa Ashraff,huyo alikuwa raia wa nchi hiyo Malaysia,mrefu kwenda hewani.Hakuwa mwenye mambo mengi kama wanafunzi wengine wenye mashauzi.Hiyo ndio sababu kubwa iliyomfanya Ahmed atokee kuzipenda tabia zake,wakawa kila siku wanaambatana pamoja.Urafiki wao ukakuwa kwa kasi wakawa kama ndugu,tatizo la Ahmed lilikuwa la Ashraff alkadhalika kwa Ashraff.Ndiyo maana hata siku ambayo Ahmed amegombana simuni na Yusrath,akamshirikisha Ashraff ili amuombe ushauri afanye kitu gani.
“Kwani ilikuwaje?”
Ashraff akauliza, siku hiyo wakiwa kwenye mgahawa wa Chicago Bulls,katikati ya Jiji la Kuala Lampur,mkabala na jengo la Alladi Mall.
“Ana hasira za karibu tu”
“Ndio inavyokuwaga,hasa kwa mtu anayekupenda rafiki yangu.Hata mimi, wake zangu wapo hivyo hivyo”
“Ashraff,una mke?!”
Ahmed akauliza kwa mshangao, ilielekea habari hiyo ilikuwa mpya kwake kwani tangu wafahamiane, hakuwahi kusikia kitu kama hicho.
“Sio nina mke,nina wake”
“Acha utani”
“Huo ndio ukweli,nina wake wanne”
“Haaa,ndio nasikia leo.Wapo wapi?”
“Oman mmoja,mwingine Dubai.Lakini waliobaki wapo hapahapa Kuala Lampur”
“Sasa,unawezaje kuwamudu wote hao?”
“Kila kitu kinawezekana rafiki yangu,nawamudu lakini kuna wawili ndio wakorofi sana.Wana hasira za karibu,unajua ngoja nikupe siri moja!Unajua kwanini wazazi wetu walidumu kwenye ndoa zao?”
“Hapana sijui.Ni kwanini?”
“Ujue katika ndoa ama mahusiano,lazima mmoja ajifanye fala”
“Una maana gani?”
“Nina maana kwamba mmoja awe mnyenyekevu,wote mkiwa wakorofi.Hamtodumu Ahmed,ndio maana mpaka leo nipo na wake zangu,huu mwaka wa tano sasa”
“Kuna kitu nimejifunza”
“Ahsante kwa kujifunza,endelea kumuomba msamahaa shemeji.Usijali kwa hilo”
“Lakini hata mimi nina hasira za karibu mno”
“Usiwe hivyo”
Siku hiyo Ahmed alijifunza kitu kutoka kwa rafiki yake Ashraff,ki ukweli alikuwa tayari amesusa na aliapia hatomtafuta tena Yusrath simuni,hiyo ni baada ya kuomba msamahaa kila siku bila mafanikio.Siku hiyo usiku akapiga simu mara kumi lakini haikupokelewa,akaamua kuandika ujumbe mrefu sana wa kuomba msamahaa na kuongezea maneno matamu.Siku iliyofuata akafanya hivyo hivyo bila kukoma,siku ya tatu akarudia tena.Siku ya nne, mchana akiwa darasani simu yake ikaingia ujumbe mfupi,alipofungua na kuangalia hakuamini macho yake kama ujumbe huo ulitoka kwa Yusrath,ilikuwa kidogo apige kelele kwa furaha,alichofanya ni kufunika ‘laptop’ yake na kutoka nje.Huko hakutaka kujibu meseji bali alinunua vocha ya pesa nyingi, akaweka kwenye simu na kupiga ‘direct’ kitendo cha kusikia sauti ya Yusrath, mapigo yake ya moyo yakapiga kwa nguvu.
“Naomba nisamehee Ahmed,zilikuwa ni hasira mpenzi wangu.Nakupenda sana,naomba nivumilie.Nina paniki mapema hasa kwa mtu ninaye mpenda,isitoshe sitaki kukupoteza”
“Yusr..tititi”
Simu hapohapo ikakatika,alivyoangalia akagundua kwamba vocha imeisha,akarudi tena dukani na kununua,akaweka simuni na kupiga tena.Mazungumzo yakaanza upya, lakini hawakumaliza,Ahmed akaweka tena vocha!Baadaye akapata jibu kwamba hata angeweka vocha ya shilingi milioni moja kwenye simu,wasingeweza kumaliza mazungumzo yao.Alichofanya ni kurudi darasani akachukuwa begi lake pamoja na laptop,akatoka nje ili aende hostel, huko aliamini angezungumza na Yusrath, kutumia mtandano wa ‘Skype’ kama wafanyavyo.
Kichwani kwake alitafakari vitu vingi sana,bado hakuamini kama ametoka kuzungumza na Yusrath, muda mchache uliopita wakati mwingine tukio hilo alilichukulia kama ndoto,akazidi kutembea kwa kasi na hatua mbilimbili.Bila kuangalia mbele,akashtukia amepigwa kikumbo,vitabu alivyoshika mkononi vyote vikadondoka chini,akainua shingo yake juu ili ajue ni mwanaharamu gani kampiga kikumbo namna hiyo.
“I’m so sorry”(Nisamehe)
Sauti nyororo na laini ikamfanya Ahmed,apunguze jazba kidogo!Mbele yake, alisimama mwanamke mrembo,mrefu kiasi kwenda hewani yaani ‘American Height’ japokuwa alitaka kutoa tusi lakini ilibidi ashushe pumzi ndefu kidogo,akameza fundo moja zito la mate.
“I’m so sorry once again.I didn’t spot you coming!”(Nisamehe,sikukuona unakuja)
Japokuwa alikuwa ni mwanamke mwenye asili ya kiarabu lakini alizungumza rafudhi ya kizungu kwa mbali,Ahmed alishindwa kujibu chochote alibaki akimwangalia na kushindwa kuelewa ni kwanini hali hiyo ilitokea ghafla.Mwanamke huyo,alizidi kuomba msamahaa huku akiinama chini na kuokota vitabu vya Ahmed,akazidi kuomba msamaha kwa mara nyingine.
“It’s okay”(Usijali)
Ahmed,akajibu mwanamke huyo akasimama wima, hapo ndipo Ahmed akapata kumuona vizuri, kuanzia juu mpaka chini,suruali ya ‘jeans’ aliyovaa ilimchora vizuri,vibunduki vikawa vimetokeza kwa pembeni yaani ‘hips’ juu alivaa t shirt nyeusi iliyoandikwa kwa maandishi makubwa ‘Story za Kway’.Utuli, aliojipulizia ulifanya hali ya hewa iwe nzuri mno!
“Call me Nurin…”
Mwanamke huyo Mrembo baada ya utambulisho huo, akatoa mkono na kumpa Ahmed,ambaye bado alikuwa anatumbua macho yake,akimthaminisha Nurin!
“I’m Ahmed”
“Nice to meet you”(Nafurahi kukufahamu)
Baada ya utambulisho huo Ahmed,akaondoka zake mpaka hostel ambapo huko alianza kuzungumza na Yusrath wake,siku hiyo moyo wake ulijawa na furaha ajabu!Siku zikasogea kama kawaida,kitu kilichokuwa kinamshangaza ni jinsi mwanamke anayeitwa Nurin,anavyomzoea kwa kasi.Ilikuwa kila anapoenda ni lazima akutane naye.
“Ahmed,umekuja kufanya nini huku?”
Siku hiyo Nurin,aliuliza baada ya kukutana na Ahmed mjini Ampang Jaya, nje kidogo na mji wa Kuala Lampur.
“Nimekuja kumalizia Research”
“Reseach?Woow!Nimependa sana!Hii ndio mitaa yangu,umekuja na nani?”
“Mwenyewe”
“Karibu sana,alafu.Inaelekea sio kabisa mwenyeji wa huku”
Nurin,akaanza kumsaili Ahmed taratibu akitaka kujua ni wapi alipotokea,alikuwa mwenye kila sababu ya kuhoji sababu ya kiingereza alichokuwa anazungumza Ahmed.Hilo halikuwa tatizo,Ahmed akafunguka na kusema yeye ni Mtanzania,akaenda mbali zaidi na kutaja mpaka kabila na kijiji anachotokea,kuanzia siku hiyo Ahmed na Nurin wakawa marafiki.
“Nitakuwa mwenyeji wako huku”
Nurin,akasema huku akiachia tabasamu mwanana.Mwanamke huyu alikuwa mwenye macho madogo ya kichina,mashavu makubwa kiasi.Alikuwa ni mrembo kwelikweli!
******
Mji wa Beijing ulikuwa kimya kabisa,hiyo ilitokana na baridi kuwa kali msimu huo.Ikawalazimu mpaka wachina kujifungia usiku na kuwasha hita ili wapambane na baridi.Ndio maana hata uwanja wa ndege wa Zhangjiakou,ulikuwa kimya usiku huo.Nje ya lango walisimama wanaume watatu,wawili waa -frika mmoja Mchina.Wote walikuwa wamevalia suti pamoja na masweta ya baridi.
“Mboha chewa sahaa”
Mchina aliyekuwa kushoto kwao,mfupi kiasi mwenye nywele nyeupe kwa mbali, alimuuliza mtu aliyekuwa pembeni yake,akitumia Kiswahili kibovu.Akimaanisha ‘Mbona wanachelewa sana’
“Watafika muda sio mrefu”
“Muha huu,ikuwa lala.Sema kama hana biashahaa”Mchina huyo, alilazimisha Kiswahili na kuzidi kukiharibu.
“Wanakuja,usijali”
Dakika kumi baadaye,abiria wakaanza kutoka mmoja baada ya mwingine!Akatokeza mwanamke mmoja wa kizungu,aliyenyoa kipara kabisa, akawafuata na kuwasalimia wote!
“Deal done,we should wait”(Kila kitu kipo sawa,tunatakiwa kusubiri)
Nusu saa baadaye,wakaitwa pembeni na askari, ambapo walizungumza kwa sauti ya chini,askari akapewa pesa ambapo waliondoka naye, mpaka sehemu maalum lilipokuwa jeneza,likafunguliwa.Wote wakatupa macho yao,ndani ya jeneza.Wakamuona Msichana amelala ndani yake kama maiti,wakatizamana na kutabasamu.Hiyo ilimaanisha tayari mzigo wao wa madawa ya kulevya, umeingia nchini China, kilichotakiwa ni jeneza kutolewa eneo hilo mpaka Bangkok huko ndipo mzigo upakuliwe kisha Hajrath,auwawe sababu hawakuwa tena na kazi naye.Hajrath hakuelewa lolote linaloendelea ulimwenguni,sindano ya nusu kaputi aliyochomwa ilikuwa bado kwenye damu,hakutofautishwa na maiti!
*******
“Aaaah aaaah aaah ashiii aaaah aaaaah,yes bebiii fuc*** me,fuc** me hard,yes.Lick me..On my chest,touch my nipples,like that.Kiss me aaah aaah aaah”
Sauti zilizotoka hapo,ilikuwa ni wazi kabisa kama watu hao walikuwa wanacheza michezo ya kibaba baba!Miguno ilikuwa mikubwa,Ahmed alikuwa ametumbua macho yake kama mjusi aliyebanwa na mlango, amepigwa na butwaa!Mbele ya kioo kikubwa cha televisheni, alimuona mwanamke wa kizungu,kainamishwa kwenye ‘sink’ anapiga kelele ingawa hakuelewa sauti hiyo ni kweli ama yupo kazini kwani wacheza muvi kama hizo hulamba mkwanja mrefu sana, baaada ya hapo,alitamani kusema wabadilishe sinema lakini mdomo wake ulikuwa kama umepigwa ganzi,kila kitu katika mwili wake kikashindwa kutoa maamuzi ya haraka,isipokuwa kichwa kidogo ndicho kilikuwa kimesimama dede.Nurin,aliliona hilo na mtego wake aliamini tayari umefanikiwa.Akajisogeza karibu na Ahmed ili ampagawishe zaidi,akamshika shingoni. Kwa kasi ya umeme akamvaa mdomoni na kumlaza chali!
******
“Ulisema,jina lake nani?”
“Florian Fredrick”
“Florian Fredrick?”
“Ndio”
“Kwa muda gani walikuwa na mahusiano na Hajrath Mpilla?”
“Almost zaidi ya miezi mitano”
“Okay,hawakuwahi kugombana?”
“Hata siku moja”
“Hata siku moja ndio nini?Walishawahi kugombana ama waliwahi kugombana?”
“Hapana,hawajawahi”
“Unapajua alipokuwa anaishi Florian?”
“Ndio”
“Unaweza ukatupeleka?”
“Ndio naweza”
“Aya twende”
Makachero kutoka jeshi la polisi, zaidi ya tisa walimwagwa katika chuo cha Makumira,Mzee Mpilla hakukubali hata kidogo,aliapia kwa Mungu wake ni lazima binti yake apatikane hata kama alitoroka,ndiyo maana akaenda kutoa taarifa polisi ili msako huo uanze mara moja,Polisi wakaingia kazini, wakianza na mahojiano na wanafunzi.Siku hiyo Amney alimwagiwa mvua ya maswali,akashikwa na hofu sababu alijua nini maana ya kuisaidia polisi ndiyo maana akapata kitete.
“Afande naweza nikaenda?”
Amney,akahoji baada ya kufika alipokuwa analala Florian.
“Kwenda wapi?”
“Hostel,naenda kupika”
“Hapana,huwezi kwenda”
Mahojiano yaliendelea na mtu wa pili kuhojiwa alikuwa ni Julius Saki,majibu yake hayakuwa na mashiko.Ilibidi ataje hotel aliyokuwa mara ya Mwisho Florian,mguu kwa mguu wakaongozana mpaka kwa muhudumu ambaye nayeye,alihojiwa maswali.
“Wewe mwanamke,usitucheleweshe.Fanya haraka,tuna mambo mengi ya kufanya,hatujaja kuuza nyago hapa”
Kachero mmoja alizungumza kwa hasira baada ya kumuona dada wa mapokezi,anambwela. Mara ashike kile mara aache.Hiyo ilitokana na hofu kumtanda!
“Nimekuuliza tar 13 alikuwa nani zamu?”
Polisi akahoiji tena,pembeni alisimama meneja wa hoteli hiyo.Walivyopata tarehe,wakaingia kwenye camera aina ya CCTV,wakachunguza vizuri zaidi.Kuna mwanaume walimuona amebeba begi anaingia chumba cha Florian, akatoka nalo baada ya dakika ishirini.Bila kuuliza chochote moja kwa moja wakajua begi hilo aliwekwa Hajrath ndani yake.
“Print hiyo picha ya huyo kijana,tutaanza naye.Tunaomba na majina yake kamili”
Kitendo hiko kikafanyika mara moja,picha ikatolewa na askari wakachukua majina na kuondoka zao,tayari kwa kuanza kazi nyingine!
*******
“Tayari,tunafanyaje?”
“Kazi rahisi,hakikisha unamuua kiakili sana bila mtu yoyote kuhisi wala kugundua”
“Nipe mbinu”
“Nurin,nikupe vipi mbinu?Mbona njia zipo nyingi,mtupe gorofani adondoke. Nenda naye pale Taijal Mall”
“Gorofani?”
“Ndio,kazi rahisi.Tena ufanye upesi”
“Hakuna tabu,nitajaribu”
“Usiseme utajaribu,fanya kazi Nurin”
Ahmed,alikuwa mbioni kuuliwa kifo kibaya sana cha kutupwa gorofani na Nurin, ambaye kwa wakati huo walikuwa marafiki wa faida ama ‘Friend with benefits’kwa kimombo!Hapohapo Nurin,akampigia simu akidai kwamba amemkumbuka na anataka kufanya naye ngono!
“Hapana Nurin,siwezi.Naomba mchezo huu tuache,siwezi kuendelea.Ninampenda Yusrath”
Ahmed,akagoma siku hiyo!Hakutaka tena mazoea na Nurin,alimkemea shetani kwa nguvu zake zote!Akili yake ikasafiri nyuma kwa kasi ya ajabu,akakumbuka penzi lake na Hajrath,akajiona alivyomsaliti kwa kulala na Necka Golden.Leo hii jambo hilo limejirudia tena kwa staili ile ile,akaupiga moyo wake ‘stop’.Akiuambia ya kwamba kuna makosa mengi ya kufanya binadamu,lakini sio kurudia yaleyale,hapohapo akakata simu na kumtafuta Yusrath hewani,akimwambia kwamba anampenda mno!
“NAKUPENDA SANA YUSRATH,sitaki kukusaliti.Naomba uwe mke wangu”
Ahmed,alizungumza maneno hayo kwa uchungu na hisia kali sana!Akimaanisha kile alichokuwa anakisema,alijihisi ni mkosaji sana kwa kulala na Nurin.
Usiku wa siku hiyo alizungumza vitu vingi sana na Yusrath,akiwa katikati ya usiku akasikia kishindo kikubwa mlangoni,alivyosimama kutoka kitandani.Kwa macho yake,akashuhudia mlango wake umepigwa teke,ukafunguka.Wakaingia wanaume watano wenye ndevu,wakiwa na bastola mikononi mwao.Wakamsogelea na kumfunika na kitambaa cheusi usoni,alivyojaribu kukukuruka na kupambana nao,akatulizwa na kitako cha bastola kichwani,hapohapo akapoteza fahamu.
“Sina jinsi”
“Itakuwaje,kama asipopatikana”
“Nitakuwa nimejaribu,sina cha ziada cha kufanya, lazima mwanangu apatikane”
“Lakini tutafute mbinu nyingine ya kutafuta pesa Mme wangu,sio hilo jambo unalotaka kulifanya”
“Mbinu gani?Ebu niambie,nifanye nini?”
“Kesho nitakujibu”
“Niachie mimi nimekwambia,kesho watakuja watu wa benki.Kuangalia nyumba”
“Baba Hajrath,hivi ikitokea hujampata ama mfano umempata,hizo pesa utalipa vipi?”
“Kwahiyo niache?”
“Sina maana hiyo”
“Kumbe una maana gani sasa?Ujue nashindwa kukuelewa.Nyoosha maelezo,kama una pesa nipe basi”
“Sina pesa”
“Basi niachie nitafute pesa,nimekwambia kila kitu kitakuwa sawa”
Ulikuwa ni mvutano mkali,ndani ya chumba cha Baba Hajrath na mkewe!Hakuna mtu hata mmoja kati yao aliyeweza kuamini kwamba, binti yao amepotea katika mazingira ya kutatanisha,walimtafuta binti yao mpaka wakachoka,jeshi la polisi mkoani Arusha lilizidi kupukutisha pesa zao!Kila siku wakidai kwamba wangempata Hajrath lakini wapi.Hakukuwa na matumaini yoyote ya Hajrath kuonekana mahali popote pale,vichwa viliwauma sio masihara.Hakuna hata mmoja kati yao aliyethubutu kupata lepe la usingizi,ratiba yao ilikuwa kila siku kuripoti kituo cha polisi kuuliza ni wapi wamefikia lakini matokeo yake yalikuwa ni yaleyale.
Kuzunguka huku na kule, halikuwa zoezi jepesi kama walivyodhani,hapo pesa ilitumika.Walimwaga fedha,katika vyombo vya habari mbalimbali kama redio,tv na kwenye magazeti.Ndani ya wiki moja wakawa wameteketeza shilingi milioni saba za kitanzania,jambo ambalo halikuwa la kawaida kabisa kutokea,pesa zikaanza kupungua taratibu.Mzee Mpilla, hakuishia hapo,akauza gari lake ili amsake mwanaye,mali kwake havikuwa kitu kabisa,alikuwa yupo radhi abaki maskini kuliko kumuacha binti yake, ambaye mpaka wakati huo hakujua ni wapi alipo!Walizidi kutaabika,mpaka unapita mwezi hakukuwa na dalili yoyote ile ya Hajrath kupatikana,hapo ndipo Mzee Mpilla akapata wazo jipya la kuweka hati yake ya nyumba benki ili apatiwe mkopo akiamini atakodi wapelelezi kutoka idara mbalimbali,swala hilo alivyomshirikisha mkewe akalipinga.Hakuhafiki hata kidogo,alihisi ipo siku watalala nje kwani tayari alishakata tamaa.
“Mke wangu,nyumba kitu gani?Pesa kitu gani mbele ya mtoto wetu?Nina uhakika uko alipo anateseka,anahitaji msaada wetu”
“No way,vipi kama ametoroka mwenyewe kwa hiyari yake?”
“Namfahamu Hajrath,hawezi kufanya huo upuuzi.Ana ujinga fulani fulani naufahamu,lakini hawezi kufikia huko”
“Tutailipaje hiyo pesa?”
“Niachie mimi,nishakwambia”
Haukuwa utani,kila alichokisema Mzee Mpilla,alikifanyia kazi.Kulivyokucha asubuhi na mapema,akanyoosha mpaka makao makuu ya Benki ya CRDB, aliamini benki hiyo ndiyo ingempatia mkopo kwani mara nyingi pesa zake huzihifadhi humo.Ingawa walimfahamu lakini ilitakiwa afate taratibu zote za kibenki kama kujaza fomu na kuangalia mali zote ambazo angetakiwa kuziweka bondi,ndipo mkopo utoke.
“Umesema unahitaji mkopo wa milioni ishirini?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa afsa mikopo Bwana Ezra Kimboka,alikuwa ni kijana mdogo mtanashati kanyonga tai vizuri kohoni,shati jeupe. Ndani ya ofisi hiyo walikuwa wawili tu.Ambapo kulikuwa na kiyoyozi kikali sana.
“Ndio”
“Nadhani unajua taratibu za kibenki,naelewa wewe ni mteja wetu.Inabidi ujaze na tutatuma vijana wakaangalie nyumba yako”
“Sawa”
“Mbona kama haupo sawa, Mzee wangu”
“We acha tu mwanangu”
“Kuna nini?Una uhakika na unachotaka kukifanya?”
Bwana Ezra Kimboka,akaanza udadisi kidogo.Alitaka kujua ni kitu gani kinamsumbua mteja wake,japokuwa alijuwa kwamba sio swala lake kujua mambo ya wateja.
“Nitafanyaje,unadhani?”
“Kuna nini mzee wangu?Nishirikishe naweza kukusaidia hata kwa mawazo”
“Hapana usijali mwanangu”
“Sawa,kama ndio hivyo.Inabidi kesho uje na Mama hapa,mje kusaini.Passport size pamoja na barua ya serikali za mitaa.The rest, vipo humo kwenye karatasi”
“Ahsante”
Mzee Mpilla hakuwa na raha hata kidogo,furaha yake ikatoweka ghafla,alichokuwa anakiwaza kwa wakati huo ni binti yake Hajrath,lakini pia upande mwingine wa pili alifikiria nyumba yake ambapo, asingeweza kurudisha mkopo huo,ingepigwa mnada hakuwa na jinsi ilibidi amalize alichokianza.
Hiyo ndiyo ilikuwa sifa ya mzee huyu jasiri,hakukubali kushindwa kitu.Alivyorejea nyumbani kwake na kumuelezea mkewe,likawa tatizo lingine kubwa.Mkewe alichukizwa mno!Akagoma kwenda kuweka sahihi.
“Kwahiyo,unaenda ama huendi?”
Mzee Mpilla akauliza kwa ukali huku akimtizama mkewe usoni.
“Siendi”
“Kwahiyo mtoto tumuache?”
“Baba Hajrath hi…”
“Kama huendi basi,nitajuwa cha kufanya lakini lazima huo mkopo nichukuwe”
Hakukuwa na njia nyingine za kumzuia mzee huyu mwenye msimamo kughaili,hilo mkewe alilijuwa.Alipojaribu kumshawishi usiku kwa mahaba na kutaka wafanye tendo la ndoa, mzee aligoma.
“Niache,nimechoka”
“Baba Hajrath”
“Nina mawazo siwezi”
“Jitahidi kidogo,mimi ni mkeo”
“Mke wangu?Hapana sio,huwezi ukapinga jambo nalotaka kulifanya.Tena mtoto wetu,siwezi.Niache kwanza”
Mzee aliongea kwa uchungu huku machozi yakitaka kumlenga,mkewe alipojaribu kumshawishi ilishindikana,msimamo ukawa palepale.Mpaka kunakucha hakuna hata mmoja kati yao, aliyepata usingizi.Kama walivyohaidiana,vijana watatu kutoka benki wakafika ili kuhakiki nyumba hiyo,wakaingia ndani na kufanya ukaguzi.Walivyoridhika wakaondoka zao.
Cha ajabu asubuhi hiyo, Mama Hajrath,akawa amekubali kumuunga mkono mumewe,wote wakaongozana mpaka benki ili aweke sahihi.Kila kitu kilivyokamilika wakarudi nyumbani ili wasubiri pesa iingizwe kwenye akaunti.
*****
“Mkuu,kuna watu wanahitaji kuzungumza nawewe”
“Wakina nani?Sawa waambie wapite”
Ndani ya ofisi hiyo kubwa nyuma ya kiti juu ya ukuta kulikuwa na picha kubwa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,pembeni kidogo kulikuwa na picha za maraisi wengine tofauti tofauti,ilikuwa ni ofisi kubwa kiasi,yenye hadhi zote!Juu ya kiti cha kuzunguka aliketi mwanaume mrefu mweupe,mezani kwake kulikuwa na redio upepo pamoja na kompyuta mbili,moja mpakato nyingine kubwa!Ilikuwa ni asubuhi sana,baada ya kupewa taarifa ya wageni kutaka kuingia,akajiweka vizuri na kusubiri kidogo.Mlango wake ukafunguliwa,akaingia mzee mmoja maji ya kunde,akiambatana na mwanamke mtu mzima kiasi,wakatembea kidogo.
“Karibuni sana.Mimi naitwa Mr.Mohamed Kajeme”
Mwanaume huyo akasimama na kuwapa mikono,akawakaribisha viti vya wageni,wakaketi.
“Ahsante Mimi naitwa Mr.Mpilla,huyu ni mke wangu”
“Karibuni sana”
Mzee Mohamed Kajeme,akaifunga mikono yake kwa pamoja na kuiweka chini ya kidevu,hilo ndilo lilikuwa pozi lake kama akitaka kumsikiliza mtu kwa makini sana!
******
Uzuri wa Yusrath Suleiman,uliendelea kuumiza vichwa vya watu.Wazee kwa vijana walimiminika dukani hapo, alipokuwa anauza vipodozi na manukato.Hilo lilikuwa wazi kabisa kama siku, akikaa yeye ni lazima umati wa watu utajaa,licha ya kuwa mrembo lakini jinsi alivyozungumza kwa pozi ilifanya kila mteja apende huduma yake,Yusrath hakujua kununa,aliongea na wateja vizuri na alitabasamu muda wote.Hiyo ndiyo ilifanya wazazi wake wazidi kumpenda na kumtumia yeye dukani hapo,mbali na hayo hakuwahi kusababisha shoti ya aina yoyote ile.Wanaume waliokuwa wanamtongoza na kumsifia kwake ilikuwa kawaida,hakushtuka kwani tayari alikuwa amezoea.Kilichowafanya wanaume waweze kupata nafasi nzuri ya kuzungumza naye ni muda wa chakula cha mchana, ambapo hutoka na kwenda kula chips kuku, kwenye mgahawa wa mpemba uliokuwa jirani kabisa na duka lao,hapo Kariakoo!
“Yusrath,ushalipiwa”
Mpemba,aliyekuwa anakaanga chips alimwambia Yusrath, baada ya kufika siku hiyo na kutoa pesa,jambo ambalo lilimshtua sana.
“Nimelipiwaaa?Na nani?”
“Kijana mmoja hivi”
“Mrudishie pesa yake,sina shida ya kulipiwa”
“Mmmh,sawaaa.Nikuwekeee nini asaaa humu ndani yake,vile vilee amaa?”
Mpemba,aliuliza kwa rafudhi ya kwao.
“Ndio,pili pili weka nyingi sana.Alafu jana,Kuku alikuwa na chumvi nyingi”
Ndani ya mgahawa huo,alifahamika na walimzoea.Akiwa ameketi mwenyewe meza ya mwisho,akatokea kijana mmoja maji ya kunde,akakaa pembeni yake.
“Mambo”
“Poa”
“Umependeza”
“Ahsante”
“Mimi naitwa Gasper”
“Nashukuru kukufahamu”
“Unaitwa nani?”
Kufuatia hapo Yusrath,akanyamaza.Hakujibu lolote,jambo hilo kwake alilitafsiri kama bugudha,chakula kilivyowekwa mezani,akasimama mpaka nje na kunawa mikono.Alivyomaliza kula hakutaka kumuongelesha jamaa aliyekaa pembeni yake kwenye kiti, anamtizama.
Hiyo haikuwa mara ya kwanza,kusumbuliwa na wanaume tofauti tofauti wakiingia na gia zao lakini waliambulia vibuti,kila siku simuni aliwasiliana na Ahmed,akimwambia kila kitu kilichokuwa kinaendelea nchini Tanzania.Akamwambia wanaume wote wanaomsumbua na kumtongoza!
“Baby ndio,kuna mkaka anaitwa Muba.Ndio aliyepokea pesa”
“Sasa wewe,ukamwambia nini?”
“Nilimwambia nina uwezo wa kulipa,sina shida”
“Mwambie akome,nitumie namba zake”
“Sawa baby,nakutumia.Nakupenda sana Ahmed”
Yusrath,hakutofautishwa na mtoto anayedeka.Kweli,alimdekea sana Ahmed kuliko kawaida,lakini siku moja usiku akiwa amemaliza kula chakula cha usiku,akamtafuta Ahmed hewani lakini simu iliita bila kupokelewa,simu iliita tena na tena.Hatimaye ikazima kabisa,Ahmed hakupatikana tena hewani.
*******
Wakati wa Hajrath,kuuwawa ulifika.Kazi ya kupakiwa madawa ya kulevya na kusambazwa nchi tatu kama China,Israel pamoja na Afrika kusini ikawa imetimia.Alivyofikishwa nchini Afrika Kusini jijini Capetown,alipakiwa kwenye moja ya Fuso,ndani ya mfuko mkubwa wa mataka taka.Gari hilo lilitembea umbali wa kilomita tisini,likitoka kabisa nje ya jiji la Capetown wakiwa na niya ya kwenda kum-maliza kabisa,kwa kumpiga risasi ama kumuacha katikati ya msitu mkali wakiamini huko angeliwa na wanyama pori.Gari kubwa aina ya Fuso,lilikuwa katika mwendo wa kasi ya ajabu,nyuma yake lilibeba takataka ambazo zilitakiwa kwenda kutupwa nje ya mji kabisa,hakuna mtu aliyeelewa ya kwamba katikati ya matakataka hayo kuna binadamu yupo.Hata askari wa usalama barabarani walivyolisimamisha gari hilo, zaidi ya mara kumi,hawakuelewa lolote.Hakukuwa na mtu yoyote aliyejuwa isipokuwa dereva na utingo wake,safari iliwachukuwa lisaa limoja na nusu mpaka kufika kijiji kilichoitwa Nazareth,walikiita jina hilo sababu ya uchache wa wakazi wa eneo hilo,lakini Nazareth kuliendelea,kulikuwa na barabara za kisasa.Huko,ndipo walipanga wamuangamize Hajrath,walivyoacha barabara ya lami,wakaingia ya vumbi mbele kidogo kulikuwa na mto mkubwa unaopitisha maji,wakapaki gari kando na kuteremka.Wakaweka,bastola zao viwambo vya kuzuia isitoe mlio mkubwa na kusogea mpaka nyuma ya gari.
“Mshushe,yupo kwenye mfuko gani?”
Jamaa mmoja alimuuliza mwenzake.
“Ule pale mweusi”
“Panda,tumteremshe”
“Sawa”
Wakaelewana wakiwa wanazungumza lugha ya kizulu,mmoja akapanda nyuma na kuanza kuvuta mifuko mifuko.
Mpaka mfuko mkubwa wa katikati .Akauvuta kwa nguvu!
“Nisaidie basi,njoo shika hapa”
Zoezi la kumtoa Hajrath ndani ya gari lilikuwa gumu kidogo,mfuko ulikuwa mzito.Hata hivyo,walijitahidi kuvuta mfuko huo,wakafanikiwa na kuushusha.Wakauburuza karibu na mto na kuuchana katikati,sura ya Hajrath ikaonekana.
“Pelle,kazi kwako”
Kauli hiyo ilimfanya jamaa huyo anayeitwa Pelle,amtizame Hajrath aliyekuwa amelala hajitambui kabisa ndani ya mfuko,akaikoki bastola yake na kuielekezea upande wa Hajrath.
“Pyuuu! Pyuu! Pyuu! Pyuu! Pyuu! Pyuu! Pyuuu! pyuuu! pyuuu!”
Zilikuwa ni risasi tisa,zote zilipenya mwilini mwa Hajrath,bila huruma Pelle akafyatua tena risasi ya mwisho.Mfuko mzima ukajaa damu.Wakasogea karibu ili kuhakikisha kama Hajrath amekufa tayari.
“Tayari,naona kazi imeisha”
“Mtupe mtoni,mpigie bosi”
Hilo ndilo jambo lililofanyika,Hajrath akasukumizwa akiwa ndani ya mfuko wa nailoni ‘Chumbwiii’akatua ndani ya mto wa maji yenye kina kirefu,ambao ulikuwa na mamba,huko waliamini angekuwa chakula cha mamba hao,walikuwa ni kama wametabiri.Kwa mbali waliwaona Mamba wawili wanakuja kwa kasi,hiyo ilitosha kabisa kumaanisha siku hiyo Hajrath,angekuwa chakula chao!
Fahamu zilimjia sekunde chache baada ya kupigwa na kitako cha bastola, kitambaa kilichokuwa usoni mwake, kilimfanya asione mbele lakini baada ya sekunde moja,kikatolewa.Mapigo yake ya moyo yalidunda mara mia moja kwa sekunde,hofu kubwa ilimtanda.Japokuwa, kulikuwa na baridi kali lakini kijasho chembamba kilimtoka,akawa anahema kwa pupa.Hiyo ni kutokana na watu hao, waliokuwa mbele yake wameshika bastola,kwa mara ya kwanza alidhani yupo kwenye ndoto kali ya kutisha na muda mfupi, atashtuka kumbe haikuwa hivyo,ulikuwa ni ukweli mtupu.Tumbo lilianza kumuuma ghafla,hakujua nila kuharisha ama uwoga.Mkojo ulikuwa karibu kumpenya sambamba na haja kubwa, kutaka kumtoka.
“Simama,fanya haraka”
Jitu moja liliamuru,hiyo ilimfanya Ahmed asimame kwa haraka kama mwanajeshi kwenye gwaride,Katika maisha yake hakuwahi kuiona bastola kwa macho,isipokuwa kwenye filamu za kijasusi ama kwenye mitandao ya kijamii kama sio vitabuni.Hakuelewa watu hao wanataka nini,kilichomstaajabisha ni lugha ya Kiswahili, waliyokuwa wanatumia.Alielewa nini maana yake endapo angepinga amri, mmoja wa watu hao akatoka nje ili kuangalia usalama.
Kishindo cha mlango kupigwa teke kwa nguvu, kilimshtua Ashraff aliyekuwa chumba cha jirani kwani alipanga pembeni na rafiki yake kipenzi Ahmed,hiyo ilimfanya atulie kidogo kwani muda mfupi uliopita alitoka kuswali,akautoa mkeka vizuri na kuuweka kando,akanyata taratibu mpaka mlangoni ili kusikiliza,minong’ono ya watu wasiojulikana akaingiwa na mashaka,taa nyekundu ikawaka kichwani kwake,kwa hatua za paka shume anayetaka kuiba nyama, akafanikiwa kulifikia dirisha ambapo alichungulia na kuona gari jekundu aina ya Subaru, lipo nje ya geti.Kuna picha isiyokuwa ya kawaida ilimjia kichwani kwake.Sifa ya mwanaume huyu ilikuwa ni moja tu,alikuwa mdadisi na jasiri.Hiyo ilitokana na madrassa aliyosoma kutoa kozi ya mchezo hatari wa 'Karate' hivyo alikuwa anajiweza kwenye swala zima la ndondi.Kwa tahadhari,akafungua mlango akihakikisha hautoi sauti.Akachungulia nje na kuwaona watu wanne wanatoka chumba cha Ahmed,huku watano, akiwa amemshika Ahmed kwa nyuma.Tena kwa staili ya kumuwekea bastola mgongoni,akashusha pumzi ndefu.Jambo la kwanza alilolifanya ni kupiga simu polisi,akawaelezea tukio zima lililotokea,lakini hiyo isingesaidia alielewa ni kwa namna gani, Ahmed anahitaji msaada wa haraka,alivyoona watu hao wasiojulikana wanapita.Akatembea kwa nyuma nyuma,akajificha nyuma ya chuma kubwa.Aliyekuwa anamvizia ni mtu wa nyuma kabisa ili kwanza amkomboe Ahmed,kwa utaalam wa hali ya juu tena kimya kimya,jambazi wa nyuma,alivutwa kwa nyuma akapigwa roba kali,mkono wake ukawa umekunjwa,akamvuta kwenye giza na kuupigiza mkono uliokuwa na bastola,ikadondoka chini.Hakuongea chochote,hiyo ni baada ya kupigwa ngumi takatifu ya mbavu,akamkandamiza na mguu shingoni kwa nguvu.Ilielekea jambazi huyo alikuwa mgeni ama ndiyo kwanza anaanza kazi hiyo ya ujambazi,hiyo ilitokana na kutulia kwake,alitandwa na hofu
“Ahmed,tulia hapo.Kaa chini”
Ashraff,akasema!Ahmed akawa kama mtu,aliyechanganyikiwa.Hakuelewa ni kitu gani akifanye, zaidi ya kutoa macho yake,akitaka kupiga kelele.
“Shsssi shssssiii”
Ashraff,akaweka kidole mdomoni kumuashiria,asipige kelele ya aina yoyote ile.Ahmed,akabaki ameganda kama sanamu,hajui afanye nini.Anatetemeka mwili mzima kama njiwa aliyemwagiwa maji,Ashraff alikuwa tayari amemkomboa rafiki yake na ilikuwa ni wazi kabisa ya kwamba alichokianza ni lazima akimalize,ndiyo maana aliendelea kujificha nyuma ya nguzo kubwa, akiwaangalia majambazi waliokuwa wanazidi kutokomea mbele.
Lakini walivyolifikia gari lao,wakageuka nyuma na kushtuka baada ya kuona nyuma hakuna mtu,Ahmed hayupo wala mwenzao,wakatizamana na kuangalia huku na kule,hawakuona kitu.Wakashika bastola zao vizuri na kuanza kurudi walipotokea.Hiyo ikafanya Ashraff,aanze kutetemeka sababu walikuwa wanakuja usawa aliokuwepo yeye,kuendelea kubaki hapo bila kuchukua hatua yoyote kulimaanisha kusubiri kifo chake,akajisogeza taratibu mpaka ilipodondoka bastola.Akaichukuwa na kuishika vizuri.Katika maisha yake hakuwahi kutumia bastola,hiyo ndiyo ingekuwa mara yake ya kwanza,ndiyo maana alitetemeka kwa mbali.Hata hivyo alipiga moyo konde!Kama maji alikuwa tayari keshayavulia nguo,ilikuwa ni sharti ayaoge.
“Paaaaa! Paaaaa!”
Akachomoka kama nyati msituni na kufyatua risasi upande wa majambazi walipo.Bila kuangalia analenga wapi,hiyo ilifanya majambazi hao pia waanze kurusha risasi upande wake hovyo hovyo,hali ikawa tayari imebadilika, kilichokuwa kinasikika ni mirindimo ya risasi,wanafunzi waliokuwa hostel waliingia chini ya uvungu, wengine walianza kusali sala zao za mwisho, wakajua tayari kiyama kimefika,lakini kuna baadhi yao walijikojolea ndani ya nguo zao za ndani!Ashraff aliendelea kurusha risasi,alivyoona majambazi wanamfata akaanza kutambaa kama nyoka mpaka upande mwingine,Ahmed alikuwa amekaa ameziba masikio yake,analia kama mtoto mdogo hajui ni kitu gani akifanye,mirindimo ya risasi ilimtisha.
“Ahmed,lala chini”
Asharaff alizungumza kwa nguvu huku akiwa kifudi fudi anajiburuza,akabiringika mpaka nyuma ya msingi mkubwa wa matofali hapo, akatulia kimya.
“Wiiiuu! Wiiiiu! Wiuuuu! Wiuuuuu!”
Ving’ola vya polisi vilianza kusikika kwa mbali,kumaanisha kwamba jeshi la polisi lipo karibu kufika eneo hilo,walichofanya majambazi hayo ni kumchukuwa mwenzao,wakaingia naye ndani ya gari.Dereva akaingia nyuma ya usukani kupitia dirishani,akapiga gia na kuanza kurudisha gari, kinyumenyume kwa kasi ya ajabu huku kichwa chake akiwa amekigeuza nyuma, anatizama ili apate sehemu ya kugeukia,alivyoona nafasi akaweka mguu kati na kuuzungusha usukani kwa kasi,ilikuwa ni kama sinema ya kuigiza,namna gari lilivyogeuka iliogopesha ilielekea dereva huyo alikuwa mtundu kwenye magari,kilichoonekana hapo ni vumbi tu,wakatokomea kusikojulikana.
Magari matano ya polisi,yakapiga msele eneo la tukio askari wakateremka na mitutu, lakini bahati mbaya walikuwa tayari wamechelewa kwani majambazi, walikuwa wamekimbia.Ashraff akajitokeza huku mikono yake ikiwa juu hewani,hapo ndipo wanafunzi wakaanza kufungua mapazia na kuchungulia, madirishani ili kuangalia nini kimetokea,kutokana na kutaka kulinda usalama wa wanafunzi hao Ashraff na Ahmed,ilibidi askari wawachukuwe mpaka kituoni,huko walichukuwa maelezo yao.Kulivyopambazuka tu,mkuu wa chuo akaitwa na kupewa mkasa mzima uliotokea.
“Naomba ulinzi wa kutosha kwenye hosteli za hawa wanafunzi”
Mzee huyo ambaye ndiye Mkurugenzi,aliomba jambo hilo litokee.Tukio lililotokea usiku wa kuamkia siku hiyo lilimuogopesha,hata hivyo alimpongeza sana Ashraff na kumshangaa baada ya kupewa historia ya namna alivyopambana na majambazi hayo.Lakini kila walivyomuhoji Ahmed hawakuweza kuhisi ni nani, alikuwa nyuma ya tukio hilo zima.
“Ulisema ulisikia wanazungumza lugha ya Kiswahili?”
Afande mmoja alihoji kwa mara nyingine.
“Ndio,tena kiswahili fasaha cha Tanzania”
“Una uhakika?”
“Ndio afande”
“Hapa nchini,hauna marafiki wa Kitanzania?”
“Sina”
“Huna rafiki yoyote yule?Ambaye mmekutana naye hapa nchini?Nje ya chuo?”
“Ah ah,hapana”
“Una uhakika?”
“Hapana, ninaye”
Kitendo cha Ahmed kujibu hivyo kilimfanya askari aweke kalamu chini na kumtizama kwa jicho kali la hasira.
“Unatuchanganya,mbona sikuelewi.Jibu kitu kimoja tukuelewe.Ndio ama Hapana,tuna kazi nyingi za kufanya?Una rafiki yoyote Yule hapa nchini?”
“Ndio”
“Jina lake nani?”
“Nurin”
“Mlikutana wapi?”
Hapo ilibidi Ahmed,ashushe pumzi kidogo na kuanza kuelezea kila kitu kinagaubaga, tangu walivyokutana na Nurin.
“Lakini sidhani kama anahusika,kwenye tukio hili”
“Itafahamika,una lingine la kuongeza?”
“Hapana afande”
“Bado,hatujamaliza.Tukikuhitaji tutakuita”
“Sawa”
Hatimaye,Ahmed akaruhusiwa lakini nyuma yake alipewa maaskari wa kuwalinda,hostel ikawa inalindwa na jeshi la polisi.Kitendo cha kufika hostel tu,hakuweza kufunga bakuli lake,akamtafuta Nurin hewani na kumwambia kila kitu,kilichotokea.Ahmed hakuelewa lolote,kifupi alikuwa nyuma ya pazia,hakutambua kwamba Nurin ni chui aliyejifika ngozi ya kondoo na ndiye mkandarasi wa kila kitu.
“Pole sana rafiki yangu,ungekubali tuonane usiku wa siku hiyo.Yasingekukuta hayo yote.Nina uhakika malaika, alinitumia mimi ili nikuokoe”
“Inawezekana lakini,bora ningekusikiliza”
“Ndio hivyo.Naomba leo nikuone”
“Wapi?”
“Nitakwambia,lakini ningependa tujifungie.Room moja,twende nje kabisa ya mji”
“Kesho nina kipindi lakini”
“Usijali,tutawahi kurudi.Nitakurudisha mapema”
“Sawa,umesema tukae room moja?”
“Ndio,kwani vibaya?”
Nurin,akajibu na kuibua swali.
“Sio vibaya lak…”
“Lakini nini Ahmed?Nakupenda sana.Usiniumize tafadhali”
Nurin,alilegeza sauti.Haikujulikana kama alikuwa anabana pua,ama anafanya makusudi, hiyo ilimfanya Ahmed,anyamaze kidogo.Picha ya Nurin, uzuri wake wa kitasha na kifua chake kilivyosimama kilifanya mwili wake usisimke,Nurin hakuishia hapo.Aliendelea kudeka simuni,akimsihii Ahmed awe naye usiku wa siku hiyo, wafanye ngono. Kwa Ahmed,ulikuwa ni mtego kwake!Akajifikiria mara mbilimbili na kutafakari kwa kina,nafsi mbili zikawa zinakinzana, kuna moja ilimwambia ‘Acha uboya kamdinye mtoto’Nyingine ikamwambia ‘Achana naye,Yusrath yupo’akatafakari zaidi na zaidi.
“Kwanini nje ya mji?”
Ahmed,akahoji swali baada ya kubaki kimya kwa muda mrefu.Karoti yake ilikuwa tayari inaanza kusimama,akahisi kama damu yake imeacha kutembea kwa muda.
“Nahitaji kukuonesha,mandhari ya nchi hii Ahmed,mbona una maswali mengi Laaziz?”
“Napaswa kujua,isitoshe sasa hivi ni usiku”
“Naelewa”
“Mimi ni mgeni,hata wewe ungekuwa mimi.Ungehoji maswali”
“Ni kweli Ahmed”
“Kwanini usije hapa Hostel?”
“Ahmed,siwezi kuja hapo.Nataka tulale hotelini”
Nurin,hakuwa mwanamke wa kawaida.Akatumia kila aina ya ushawishi ili kumvuta karibu Ahmed,ili auwawe kwani ndio kazi aliyopewa.Kifo ambacho walipanga kumfanyia Ahmed kilitisha hiyo ni kutokana na usumbufu ulijitokeza,Sporah Trevez alipatwa na hasira za kiwango cha juu,akataka mwenyewe ndiye amshughulikie,ikiwezekana amkate kate vipisi vipisi akiwa hai.Habari za watu wake aliowatuma kufeli zoezi hilo, lilimpandisha mori, ndiyo maana alimtuma Nurin kwa mara nyingine na kumsisitiza akishindwa basi yeye ndiye angebeba msalaba wa Ahmed,jambo hilo lilikuwa ni lazima lifanyike kabla jogoo la kwanza halijawika.
Ndiyo maana Nurin alihaha sana,alielewa nini maana ya maneno ya Sporah Trevez,unyama wake ulimuogopesha mno.Hakubanduka simuni, kila alipojaribu kumshawishi Ahmed,alichomoa na kumuwekea vikwazo.
“Yusuph,inabidi utafute watu wengine.Kijana ana Mungu sana,twende Kuala Lampur”
“Kuala Lampur?!”
“Hujanisikia au?”
“Nimekusikia”
“Sasa mbona unauliza mara mbilimbili?”
Nurin alionekana kukerwa,akaandaa vijana wake wa kazi ambao wangemsaidia katika operesheni hiyo nyepesi lakini nzito,hapohapo akamtafuta Ahmed simuni kwa mara nyingine.
“Sawa,nakuja Kuala Lampur,anza kujiandaaa kipenzi changu”
“Hakuna shaka,lakini hatutokaa sana”
“Usijali”
Ahmed,akawa amejaa ndani ya kumi na nane za Nurin,hakuelewa kwamba siku hiyo ndiyo ungekuwa mwisho wake na angeenda kufa kifo kibaya, kifupi alikuwa ana kifuata kifo chake.Mbaya zaidi alianza kufikiria namna ya kumpanga Yusrath aliyekuwa nchini Tanzania,kupitia simu yake.Akamtafuta hewani kwa njia ya Skype usiku huo ili ajifanye amechoka anataka kulala.
“Ndio baby,nimechoka Mke wangu”
“Alafu,Darling.Mbona hukuniambia ilikuwaje jana,hukupatikana hewani.Na sio kawaida yako?Ulikuwa wapi?”
“Nitakwambia Sweartheart,kuna matatizo yalitokea.Lakini nitakuhadithia,hapa nilipo nimechoka sana Mke wangu.Naomba nilale”
“Lakini baby,kuna kitu nataka kukwambia”
“Kitu gani Darling?”
“Kuna watu wananisumbua sana mme wangu,nataka uwaambie waachane namimi”
“Nitumie namba zao,sasa hivi”
“Sasa baby wangu,mimi siwapendi”
“Tatizo mke wangu wewe ni mzuri sana,ndio maana”
“Kawaida baby,wazuri wapo wengi mbona”
“Wewe umezidi”
“Najua mwamba ngoma,huvutia kwake”
Yusrath,akaisindikiza sentensi yake na methali za bongo!
“Nawewe una maneno sana”
“Naomba nikuache ulale love wangu,lakini kumbuka kuwa una mke Tanzania,umemuacha”
“Naelewa Darling”
“Mwaa mwaaaa”
Wakapigana mabusu,simu ikakatwa.Hapohapo Ahmed,akainuka kutoka kitandani na kusimama wima,akazama bafuni na kuanza kuoga harakaharaka.Alivyoingia kabatini akawa ana kazi ya kuchagua viwalo vya kuvaa, siku hiyo ili akutane na Mrembo Nurin,alichowaza kichwani kwake ni kufanya zinaa wala sio kitu kingine,hakuwa ana akili ya kawaida,kitendo cha kuvaa shati simu yake ikaanza kuita,alivyoichukua akagundua ni Nurin,akaipokea na kuiweka sikioni.
“Upo wapi?”
Nurin akauliza simuni.
“Ndio navaa”
“Nakaribia kufika,nikukute nje Dee”
“Sawa,dakika moja”
Ahmed,alivyomaliza kuvaa akatoka nje na kufunga na ufunguo kwa nje.Kitendo cha kutoka nje ya geti na kusimama dakika moja,likasimama gari la kifahari ambalo wasanii wa kimarekani wenye uwezo kifedha hupenda kutembelea,lilikuwa ni gari aina ya Escerlad New Model,kwa mara ya kwanza hakuelewa mpaka kioo cha upande wa dereva kilivyoshushwa,marashi ya kiarabu yakasambaa nje kote.
Alikuwa ni Nurin, amevimba kwenye usukani,amependeza kuliko kawaida.
“Panda ndani ya gari Mpenzi wangu”
Ahmed,akazinduliwa kutoka kwenye mawazo,akaingia ndani ya gari.Kitendo cha kukaa kwenye siti,Nurin akamsogelea karibu,akamvuta kwake,akatoa ulimi wake,wakaanza kunyonyana ndimi.
“Nakupenda”
“Mi….mi mimi pia nakupenda”
Ahmed alipata kigugumizi,hiyo ni baada ya macho yake kutua juu ya kifua cha Nurin,kilichokuwa wazi kidogo maziwa kayapandisha juu yaani ‘Boobs’kwa lugha ya kimombo!Akazidi kumkagua,kimini alichovaa ndio usiseme,kilimpagawisha kuliko kawaida,mwili ukazidi kumsisimka.
“Nataka twende sehemu moja hivi kidogo”
Nurin akasema.
“Wapi?”
“Wewe utaona”
Gari lilikuwa linanukia Utuli usiokuwa wa kawaida,kwa mwendo wa dakika thelathini wakawa wameingia kwenye mgahawa mmoja mzuri sana.Uliotulia,usingeuangalia kwa makini ungedhani ni disco lakini haikuwa hivyo,japokuwa kulikuwa na watu wanaimba, jukwaani wakifurahi.
“Hii inaitwa Karioke”
“Karioke ndio nini?”
“Kama vile,wanaimba.Hua napenda sana kuimba,ngoja nikakuimbie”
“Hapana Nurin,siku nyingine”
“Mpenzi,mbona una aibu hivyo?Ngoja basi tuagize chupa ya Takira.Twende nayo”
“Sawa”
Kwa Ahmed,kila kitu kilikuwa kigeni,macho yake kayatupa jukwaani,akimuangalia mwanamke mmoja wa kiarabu ameshika kipaza sauti, anaimba.Alivutiwa sana na pigo za mwanamke huyo pia anavyoimba nyimbo ,wakatoka hapo wakiwa na mzinga mkubwa wa pombe aina ya Takira.
Gari ikakata kona kuelekea mitaa ya Inalaska,wakaacha barabara inayoenda Ratan na kunyoosha katikati ya jiji,ambapo hapo walifika katika hoteli ya kifahari inayoitwa Rock Hill Hotel,walivyoshuka tu.Akatokeza kijana mmoja aliyevalia sare maalum,kazi yake ilikuwa ni kupaki magari sehemu husika.Wakatembea mpaka mapokezi,ambapo hapo walipewa kadi za ki ‘electronic’ kazi yake ilikuwa ni kufungua mlango.Kitendo cha kuufungua mlango na kufunga,baada ya kufika chumbani.Ahmed akawa wa kwanza kumvuta Nurin karibu,akamsogelea mdomoni wakaanza kulana denda kwa fujo.Huku wakishikana huku na kule,Nurin hakutaka kuremba nayeye kwenye michezo hiyo alikuwa gwiji kwelikweli,akaanza kumvua shati Ahmed,akawa anampapasa kifuani,akashuka mpaka chini na kuingiza mkono ndani boxa, akakumbana na nyoka aliyesimama tayari.Damu yake,ikatembea kwa kasi ya ajabu.Akaanza kumvua mkanda na kuutupa kando,akashusha suruali.Akapiga magoti na kumshika vizuri,akamtumbukiza mdomoni,Ahmed akafumba macho bila kupenda,akahisi kuna garika kubwa mwilini mwake,akakishika kichwa cha Nurin vizuri,utamu aliohisi akatamani asimame na ukucha wa mguu,isingekuwa chakula alichokula kilichomfanya ashibe ni lazima angedondoka chini,lakini alibaki wima,akashtuka ametuptwa kitandani bila kujua ni saa ngapi,suruali yake ikavutwa,viatu vyake vikavuliwa,siku hiyo akawa kama mtoto.Nurin, alimchezea pembe zote,akamlamba kila sehemu.Kuanzia machoni,puani,masikioni na kila idara husika.Alivyolambwa kifuani maeneo ya chuchu zake,ndipo hapo alipohisi roho yake inaacha mwili.
“Aaaaaah”
Ahmed akaachia mguno wa ndani kwa ndani,Nurin akawa amejua tayari ni wapi pa kucheza napo,akazidisha njonjo.Akashika koki ya Ahmed vizuri na kuanza kuichua,alivyoona tayari mambo.Akapanda juu yake na kuitumbukiza ndani ya shimo.
“Aaah! Aah! Aah! Aaah! Aaa! bebiii,aah aaaah asishiii aaah mmh mmmh,Yeees Fuc** Me haaaard yeaaah aaaah aaah”
Sauti ya Puani ilikuwa ikimtoka,Nurin.Sidhani kama alikuwa anaelewa ni kitu gani anasema lakini alichohisi kwa wakati huo, zilikuwa ni raha zilizopitiliza,Ahmed nayeye hakutaka kuonekana fala.Akamtupa Nurin na kumuweka chini,yeye akakaaa kwa juu.Mguu mmoja,akauweka begani hapo ndipo alipopata nafasi nzuri ya kumsasambua.Ahmed,hakuwa mzembe kitandani.Kila zilivyopita sekunde tano,alikuwa akimuweka mikao tofauti,alivyoona haitoshi,akamchomoa nyoka wake.Akaipanua miguu ya Nurin huku na kule,akatoa ulimi wake na kuanza kupiga deki bahari.Hapo ndipo mtoto huyu alipoanza kuongea maneno ambayo hayapo kwenye kamusi yoyote ile,zoezi lilivyoisha,akakunjwa vizuri na kuwekwa mkao ambao ulifanya nyoka afike vizuri ukingoni.Mchezo aliokuwa anachezewa Nurin,uliogopesha.Hiyo ilifanya azunguke mara saba kwa kipindi cha muda mfupi,kitu ambacho hakikuwahi kutokea katika maisha yake ya mapenzi.Ndani ya dakika tatu,akawa amefika mshindo mara kumi na moja.
“Beibiii I’m cumming,aaah aaah I’m cumming,Fuc** me haaard”
Nurin alizungumza,akimaanisha yupo njiani kushinda,ndiyo maana kelele zilizidi akazidi kunyonga kiuno huku akimng’ang’ania Ahmed.
“Nikushi..k..e wapii bebiii?”
Ahmed nayeye akauliliza.
“Nishikee ha..paaaaa”
Mikono ya Ahmed ikawa juu ya chuchu za Nurin,huku chini kazi yake ikiwa ni kukinyonga kiuno,haikuchukuwa hata sekunde tatu.Wote wakawa wamefika kwa pamoja,Ahmed,akatulia juu ya kifua cha Nurin akiwa anahema kwa mbali.Alivyotulia vizuri,akagundua kwamba simu yake inaita akamtoa Ahmed taratibu, aliyekuwa juu yake,akaivuta simu na kuiweka mkononi,akakuta ‘Missed calls’ kumi na mbili,meseji tisa.Alivyosoma akagundua watu wa kazi wapo nje,wanataka kuingia na kumchukua Ahmed ili wakamuuwe,akazitizama kwa umakini mkubwa sana meseji hizo.
“Ahmed…”Akaita na kumtizama kwa macho, yaliyokuwa yana kitu fulani.
“Yes Darling”
“Tuondoke,wanataka kukuuwa”
“Unasemajeee?Mbona sikuelewi? Nani?”
“Ahmed,tuondoke wanataka kukuuuwa,tafadhali nakuomba.Vaa haraka”
Mawazo ya Nurin,yakabadilika ghafla.Penzi alilopewa na mwanaume huyo likabadilisha akili yake,hakuwa tayari kumuona Ahmed anakufa,kifupi alitokea kumpenda ghafla kutoka ndani ya mtima wake!
Bumbuazi aliliopigwa Ahmed, halikuwa na kipimo chake,alibaki akimshangaa Nurin.Maneno aliyokuwa anaambiwa kwamba afanye haraka,atauliwa alishindwa kuyaelewa moja kwa moja.Kwa mara ya kwanza, alidhani wenda mwanamke huyo anamtania lakini haikuwa hivyo,alivutwa mkono kwa kasi huku akisisitizwa avae kwa haraka kwani watu waliotumwa kumuuwa wapo nje na wapo tayari kumkamata.
“Ahmed,vaa haraka”
Nurin,alizidi kumsisitiza Ahmed, ambaye bado alikuwa mzito kufanya jambo hilo.
“Kuna nini kwani?”
“Nakuomba,nitakwambia.Viatu vyako hivi hapa”
Wakati mwingine Ahmed, alidhani mwanamke huyo ni mke wa mtu,hivyo mumewe yupo nje tayari kwa kuwafumania,jasho jembamba lilianza kumtoka!Akakumbuka kisa cha mpemba, alivyoingiliwa kinyume na maumbile baada ya kufumaniwa na mke wa mtu,mtaani kwao.
“Nurin,ni mumeo?Niambie ukweli,kumbe umeolewa?”
“Hapana,nitakwambia”
Hekaheka ndani ya chumba hiko ziliendelea,Ahmed akavuta shati lake lililokuwa chini,akavaa kwa kasi ya umeme alivyovaa kiatu kimoja,hapohapo mlango ukagongwa!Moyo wa Nurin ukapiga paa!Akajua tayari Ahmed amekwisha.
“Ngo! Ngoo! Ngooo!”
Mlango ulizidi kugongwa,wote wakatizamana!
“Njoo”
Namna Ahmed alivyovutwa ilitisha,akaingizwa mpaka bafuni nyuma ya mlango!
“Naanii?”
“Room service”
Sauti kutoka nje ya mlango,ilimfanya Nurin ashushe pumzi nzito ya ndani kwa ndani.
“Unataka nini?”
“Nimeleta mashuka”
“Baadaye”
Kufuatia hapo,ukimya ukatawala.Nurin, alitaka kuhakikisha kama ni kweli mhudumu ama majambazi waliotumwa, walimtumia kama chambo,alivyohisi kuna usalama akaingia bafuni na kumtoa Ahmed,ambaye kwa wakati huo, alikuwa kama mtu aliyemwagiwa maji,majasho yalimtiririka sio mchezo.
“Nurin,kuna nini?”
“Nitakwambia,inabidi tutoke kwanza mahali hapa”
“Twende wapi?”
“Nitakwambia”
Walivyomaliza kujadili,wakatoka nje ambapo huko walitumia mlango mwingine wa nyuma kutokea,Nurin alielewa fika kwamba ni lazima wanaume hao watakuwa nje, mlango wa mbele.
“Subiri niite Ubber”
“Uber ndio nini?”
“Kama taxi,subiri hapa”
Kitendo cha Nurin, kubonyeza bonyeza simu yake na kutulia kwa dakika mbili, gari ndogo ikasimama kandokando yao,wakaingia ndani na kuondoka zao!
*******
Jitihada za kumsaka Hajrath Mpilla,zilionekana kuyumba na kugonga mwamba.Askari walitanda kila mahali, wakifanya upelelezi wao,wakamwagwa kama njugu chuoni Makumira ili uchunguzi ufanyike lakini ilikuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu yasagike,mwezi mzima ulikatika bila kupata ripoti yoyote ile ya kuridhisha,hiyo haikumaanisha kwamba Mzee Mpilla, kukata tamaa,akazidi kuchota pesa alizokopeshwa na benki ili kuwapa wapelelezi lakini hilo likaonekana sio kitu kabisa,pesa haikuweza kusaidia chochote.Mama Hajrath alionekana kuchanganyikiwa kuliko kawaida,ilifika kipindi akaanza kuzungumza mwenyewe kama mwehu.Alishakata tamaa, kabisa ya kumpata binti yake,akaenda mbali zaidi na kudhani wenda amekufa.
“Waambie basi,hata wakiupata mwili wake.Waulete tuuzike!Nimuage ja…po mara ya mwisho”
Mama siku hiyo alitamka maneno mazito ya uchungu, mbele ya mumewe wakiwa seblen wanatafakari.
“Usiseme hivyo mke wangu,nina amini yupo hai”
“Siku zote hizo?”
“Atapatikana tu”
Kazi ya mzee huyu zilikuwa mbili,moja kukesha na wapelelezi lakini pili alipata kibarua kingine cha kumfariji mkewe,asubuhi,mchana na usiku.Sio siri, alionekana kuchoka lakini alijikaza kisabuni,ilikuwa ni lazima kila siku asubuhi apige simu kwa Mr.Mohammed Kajeme ili apewe ripoti na mchakato mzima, ulivyokuwa.
“Ebu njoo ofisini kwangu,tuzungumze machache”
Siku hiyo Mr.Kajeme alimuhitaji Mzee Mpilla, ofisini kwake,ilikuwa wazi kabisa kulikuwa na jambo alikuwa anataka kumueleza.Bila kumwambia mkewe,akavaa kwa kasi na kutafuta pikipiki mpaka makao makuu Posta,alivyowasili tu.Akaomba aonane na Mr.Kajeme!
“Mr.Mpilla”
Akasema jina lake,alivyofika mapokezi.
“Pita,anakusubiri”
Ilielekea taarifa za Mzee Mpilla zilikuwa mezani kwa sekretari,ndiyo maana alivyojitambulisha hakuhojiwa maswali kama unamuhitaji kikazi ama binafsi!Kwa kuwa haikuwa mara ya kwanza kufika katika ofisi hizo,alijua ni wapi mlango wa Mr.Mohammed Kajeme ulipo,akanyoosha na kusukumiza mlango mkubwa wa kioo!
“Karibu,karibu kiti”
Mzee Kajeme,alisema huku akisonta kidole chake kwenye kiti cha wageni,Mzee Mpilla akaketi na kusalimiana.
“Poleni na kazi”
“Ahsante,nawewe pole kwa majukumu”
“Nashukuru sana”
“Bila kupoteza muda,nina maswali mawili matatu nataka kukuhoji”
“Hakuna shaka”
“Unamfahamu Florian?”
Mr.Mohamed Kajeme ,akatupa swali.
“Florian!Hilo jina sio ngeni kwangu.Ni Yule kijana ambaye alikuja na binti yangu nyumbani kwangu”
“Yes,ndio huyo.Yeye pia,haonekani”
“Mpaka sasa hivi,hajaonekana?”
“Yes,hajaonekana!Alivyokuja naye nyumbani kwako,ulimwambia nini?”
“Nilimfukuza,sikutaka kumuona”
“Kwanini?”
“Binti yangu,ni mwanafunzi.Isitoshe kikubwa zaidi yule kijana ni mkristo”
“Vipi,ukigundua kwamba mwanao,katoroka kwa hiyari yake?”
“Sidhani kama anaweza kufika huko,hata kama angekuwa ametoroka,angemtafuta Mama yake simuni”
“Nakwambia hivyo kwa sababu kesi kama hizo,huwa zinatufikia sana.Alafuu, baada ya miaka kumi binti anajitokeza akiwa tayari ana watoto.Hawa watoto wa kike,akili zao wanazijua wenyewe”
“Unataka kuniambia binti nay..”
“Sina maana hiyo,najaribu tu.Kukupa mifano tofauti tofauti,juzi nilikuwa pale Makumira.Sikuwa najua,mwanangu na binti yako walikuwa na mahusiano”
Sentensi hiyo ilimfanya Mzee Mpilla,akae vizuri kitini ni kumtizama Mr.Kajeme,hakuwa ana uhakika kama alisikia vizuri ama masikio yake yana uchafu.
“Kwamba nini?Sijakuelewa hapo”
“Kijana wangu Ahmed,alikuwa ana mahusiano ya kimapenzi na Hajrath binti yako,kutokana na mambo ya ujana.Baadaye ndio akaja Florian,ulikuwa unalijua hilo pia?”
“Hapana,sikuwa najua lolote”
“Nitamuuliza Ahmed leo”
“Huyo Ahmed yuko wapi?”
“Malaysia,hayupo hapa nchini”
Walizungumza vitu vingi sana,Mzee Kajeme alimuhakikishia kwamba kila kitu kitaenda sawa kabisa,aondoe shaka.
Siku hiyohiyo alivyorejea nyumbani kwake,usiku akamtafuta Ahmed hewani lakini hakumpata,akajaribu tena na tena bila mafanikio!Asubuhi kulivyokucha,akajaribu. Hapo alifanikiwa kumpata kwani simu ya Ahmed iliita na kupokelewa.
“Hallo Baba shikamoo”
Upande wa pili wa simu ulisikika kwa sauti ya mbali.
“Marahaba ,hujambo Ahmed?”
“Sijambo lakini sio sana”
“Kwanini?”
“Kuna matatizo huku kidogo”
“Matatizo gani?”
“Nilivamiwa na watu wasiojulikana,wakataka kuniteka nyara”
“Unasemajee?Kivipi?Mbona sikuelewi”
“Ndio hivyo baba”
“Ilikuwaje?”
Ahmed,bila kuficha kitu chochote kile.Akasimulia kinaga ubaga kila kitu kilichotokea,alizungumza kwa hofu na uchungu.Wakati Mazungumzo hayo yanaendelea Mama Ahmed,alikuwa kandokando kitandani,anamuangalia mumewe,ilionekana alikuwa mwenye kihoro cha kujua nini kimetokea.Simu ilivyokatwa tu,akamdaka mumewe na maswali.
“Ahmed,alivamiwa!”
“Alivamiwaaaa?!”
Mama akauliza kwa mshangao wa waziwazi.
“Ndio”
“Na akina nani?”
“Na majambazi nadhani walikuwa wana silaha”
“Mungu wangu”
“Usijali,wamewekewa ulinzi”
“Hapana,namtaka mwanangu arudi”
“Na masomo je?”
“No,hapana.Masomo na maisha kipi bora?Vyuo vipo kibao hapa,kwani lazima huko?Naomba mwanangu arudi,nakuomba”
Mama hakutaka kukubali hata kidogo,moyo ulimuuma ajabu.Siku hiyo, akachachamaa ili mwanaye arudi nchini Tanzania.Kwa kuwa alimpenda sana mkewe na kumsikiliza,hakuwa na budi zaidi ya kuanza kufanya taratibu za kutafuta nauli ili amtumie Ahmed,arejee nchini Tanzania.
*******
Mto ulizungukwa na wanakijiji wengi,mikononi walishika silaha za asili kama mishale,mapanga na sime.Hasira zao, zilikuwa waziwazi wakitizama mto huo, ambao ulikuwa na mamba,waliokuwa wanakula wanakijiji wenzao.Kilichowapandisha mori zaidi ni baada ya siku mbili nyuma mtoto wa mama mjane,alivyoliwa na Mamba,alivyokwenda kufua mtoni.Hilo ndilo lililofanya wakae kikao kizito na kujadili juu ya kuwadhibiti mamba hao,ikiwezekana wapambane nao kiume.Wazee kwa vijana walibeba silaha za jadi na kupanga mikakati ya kujitosa kimasomaso ili kupambana na mamba hao,japokuwa waliamini ingekuwa ni vita kali kwani mamba ujanja wake ni ndani ya maji.Mwenye sime alishika vizuri,mwenye mkuki aliukamata kisawasawa mkononi mwake,wakisubiri mamba.Pembeni kuna mwanamme mmoja mwenye misuli,mkakamavu,ameshika ndama,mtoto wa Ng’ombe!Kwao mnyama huyo alikuwa kama chambo ili wamvute mamba,wakahesabu mpaka tatu!Wakamtupa ndani ya mto!Hawakukaa sana,wakaona mamba wawili,wametokeza kwa juu kisha wakaingia ndani ya maji!Hiyo ndio ilikuwa staili ya mamba akitaka kuwinda,anaibuka na kuangalia kitoweo kisha anazama tena!Hapo ndipo, wanakijiji wakaishika mikuki yao,wakajitupa ndani ya maji na kuanza ambush.Haikuwa vita ndogo dhidi ya mamba hao, wenye nguvu na wazito,mafunzo ya kupambana na mamba waliyokuwa wanafanya kwa muda mrefu.Yaliwafanya wazame kwa chini kidogo na kuwatoboa kwenye matumbo,mto ulichafuka kwa kiasi cha kutosha damu zilikuwa nyingi,jambo lililowafanya wanakijiji waliokuwa kando kushangazwa sana.Dakika moja baadaye, walisikia kelele nyingi.Macho yao wakayatupa juu ya mto huo wenye maji,wanaume wawili waliibuka na mfuko mkubwa ambao ndani ulikuwa na mwili wa binadamu,una damu nyingi sana!Kichwa hakionekani vizuri,kwa kasi na nguvu wakasaidiana na kumtoa nje ya maji,ambapo hapo walichana mfuko!Damu alizokuwa anavuja,ziliwatisha mpaka wao,wakamshika vizuri shingoni na kifuani.
“Anapumua,ni mzima”
Jamaa,mmoja akasema kwa mshangao akitumia lugha yao huku akiwatizama wenzake!Wakabeba mwili huo juujuu,huku na kule mpaka katikati ya vichaka,ambapo huko kulikuwa na vijumba vidogo vya nyasi, wanawake wengi wakatokeza ili kuwasaidia.Haraka,wakaanza kumpatia huduma ya kwanza kwa njia ya asili,wakapekecha majani na kuyatumbukiza ndani ya chungu chenye maji ya moto!Mwanammke mmoja,akakimbia jikoni na kuchukua kitu kama unga mweupe,akachukuwa na majani.Akapekecha mikononi mwake na kuuwekea mwili huo kifuani,upande wa moyo.Hawakuelewa ni kitu gani kilimtokea mwanamke huyo,kwani alijawa na matobo matobo,haikuwezekana hata kidogo ya kwamba alijeruhiwa na mamba.Moja kwa moja,zilikuwa ni risasi,hapo ndipo walimlaza vizuri chali ili kumpatia huduma ya kwanza!
Kifo ndio kilikuwa halali yake,hilo lilikuwa wazi kabisa kwamba vijana wa Sporah Trevez walikuwa wenye usongo wa kumtia Ahmed mikononi mwao kisha kumkabidhi kwa bosi wao ambapo huko walipanga kumuua,aina ya kifo chake kingetisha kuliko kawaida na ilikuwa ni wazi kabisa kama jeshi la polisi wangeupata mwili wa Ahmed ni lazima wangeandika kwenye historia ama katika kumbukumbu zao,huo ndio ulikuwa mpango hatari wa Sporah Trevez.
Akiwa juu ya kochi kubwa,mkononi akiwa na glasi ya mvinyo,amevaa nguo nyepesi na laini ambayo ilionesha mapaja yake na chupi aliyovaa ndani yaani night dress,alikuwa akisubiri majibu kutoka kwa Nurin.Mwanamke aliyetumwa kwa kazi hiyo maalum,muda wote macho yake yalikuwa juu ya simu yake ya mkononi, akisubiri jibu la kwamba,Ahmed yupo mikononi mwao,hivyo aandae mazingira.Lakini matokeo yake,alisubiri na muda ulizidi kuyoyoma.Wasiwasi ukazidi kumuingia lakini akajipa moyo kwani aliwaamini sana vijana wake.
“Washamkamata?”
Sauti hiyo ilisikika kutokea upande wa juu kwenye ngazi,Florian Fredrick akiwa anashuka kutokea chumbani.Hata yeye alikuwa mwenye hamu sana ya kumtia mikononi Ahmed,alitaka kuwa shahidi namba moja wa kifo hicho cha kutisha.
“Ndio nasubiri simu hapa,nijiandae”
“Bado,hawajakupigia simu?”
“Watapiga baada ya muda mfupi.Nadhani wanaweka mambo sawa, vijana wananikera wako slow”
“Ukimpata utamfanya nini baby?”
Florian Fredrick,akauliza swali hilo huku akiisogelea chupa ya wisky,akamimina kwenye glasi.Na kupiga fundo moja ikaisha,akamimina nyingine na kuiweka tena mdomoni,akakunja sura kidogo na kumimina kwa mara nyingine kisha kumgeukia, Sporah Trevez!
“Waulize walipo”
“Haina haja,wanajua wanachokifanya”
“Sawa sawa”
Macho ya Florian Fredrick,yalitua kifuani kwa Sporah.Akamtizama vizuri jinsi kifua chake kilivyosimama.Akashuka chini zaidi na kutizama mapaja yake yalivyo wazi na malaini hayana kipele hata kimoja,mwili wake ukamsisimka zaidi.Uzalendo ukamshinda,akaweka glasi pembeni,hapohapo akamsogelea juu ya kochi,akaishika glasi ya Sporah na kuiweka juu ya meza,akamsogelea karibu na kutoa ulimi wake,ilikuwa ni kama Sporah alijua ni kitu gani Florian,anahitaji kwani alitoa mgumo wa ndani kwa ndani,akionesha ushirikiano.Wakiwa katikati ya rahaa hizo,simu ya Sporah ilianza kuita,ikaita tena na tena bila kupokelewa!Kwa wakati huo,simu haikuwa na umuhimu sana!
******
Ilikuwa ni lazima afanye njia yoyote ile ili amuokoe Kijana Ahmed asiyekuwa na hatia hata kidogo,ambaye alitokea kumpenda kuliko mwanaume yoyote yule chini ya jua la Mungu,hakuelewa ni kwanini hali hiyo ilimkumba ghafla namna hiyo alijishangaa,asingejisamehee hata kidogo endapo angemkamatisha, Ahmed.Njia pekee ya kumkomboa ilikuwa ni lazima amtoroshe japokuwa hakuelewa ni wapi,angeenda kumficha.
“Tunaenda wapi?”
Ahmed akamuuliza Nurin, baada ya kuona safari haiishi,kilichomtia wasiwasi ni kitendo cha mwanamke huyo kuonesha wasiwasi mwingi,mara aangalie nyuma mara abonyeze simu.Jambo hilo lilimtia hofu sana Ahmed.
“Ahmed,nakupenda nafanya hivi kwa ajili yako mpenzi”
“Bado sijakuelewa lakini”
“Utanielewa baadaye,lakini kwa sasa hivi naomba ujuwe kuwa.Nimejitoa muanga kwa ajili yako”
Japokuwa aliongea kwa ujasiri lakini moyo wake ulijawa na wasiwasi mkubwa mno!Alielewa ni jinsi gani mkono wa Sporah Trevez ulivyokuwa mkubwa kuliko serikali ya nchi yake,ilikuwa ni bora usakwe na FBI lakini sio jeshi la Sporah,ambalo lilikuwa na mawakala wengi kila mahali,hiyo ilimfanya aogope zaidi sababu alijua nini mwisho wake endapo angekamatwa na akigundulika kwamba alikuwa katika jaribio la kumtorosha Ahmed.
“Stop”(Simama)
Nurin,aliropoka akimwambia dereva taxi, asimamishe gari ilikuwa ni katikati ya miti mingi,hakukuwa na makazi yoyote ya watu wala dalili yoyote ile ya mtu kuwepo,hiyo ilimfanya dereva huyo,asimamishe gari na kusubiri maelekezo kutoka kwa abairia aliyempakia,kwa mara ya kwanza dereva huyo alidhani wenda abiria wake anataka kutoa haja ndogo.Cha ajabu alipewa pesa yake,na watu aliowapakia wakashuka kutoka garini.Hiyo ilimshangaza dereva huyo lakini hakuwa na jinsi,alichotaka yeye ni pesa yake mengine hayakumuhusu,akawasha gari na kuliondoa mahali hapo.Alichofanya Nurin ni kuipigiza simu yake juu ya lami, akijua ni lazima wangetumia GPRS kumsaka na kujua ni wapi alipo,kwa maana hiyo alitaka kuwapoteza kwanza.
Bado Ahmed alibaki njia panda,hakujua ni kitu gani akifanye kwa wakati huo!Kila kitu kwake kilimtia hofu kubwa na kutaka kujua ni kwanini wapo katika mazingira hayo magumu.
“Kwanini,wanataka kuniua?Ni akina nani?”
Ahmed akauliza kwa hofu kubwa sana!
“Sporah Trevez”
“Ni nani?”
“Ni mwanamke hatari sana”
“Kanijuaje?”
“Haijalishi lakini tambua anakujua na anahitaji kukuuwa kwa gharama yoyote ile,alinituma mimi nije kukuuwa Ahmed”
Ahmed,akahisi kama uti wake wa mgongo umepigwa na ubaridi mkali sana,akabaki ameganda kama barafu, anamtizama Nurin,anayezungumza habari hizo za kutisha kwake.
“Kwanini sasa?Nimefanya kitu gani?”
“Usipaniki,unachotakiwa kufanya ni kutambua.Namimi pia,nimeingia kwenye matatizo kwa ajili yako”
“Tukatoe taarifa kituo cha polisi”
“Usijaribu kufanya hivyo,huyo mwanamke ni hatari.Atajua tu,huko ana watu wake”
Swala hilo likamvunja moyo kabisa,wakaanza kutembea kuelekea katikati ya giza nene ambapo huko kulikuwa na miti mingi!Isingekuwa ujanja na Nurin kutumia akili ya kujiongeza basi siku hiyo ingekula kwao,kitendo cha kutokea mlango wa nyuma wa hoteli, kiliokoa maisha ya Ahmed kwa asilimia mia moja,hilo lilikuwa lipo wazi sababu majambazi yaliyotumwa na Sporah yalikuwa nje ya geti kubwa ambapo isingewezekana kwa mtu yoyote yule kuingia ama kutoka bila ya wao kumuona,ndio maana wakaweka kambi karibu na geti hilo.Gari la Nurin lilikuwa mita kumi tu mbele yao,wakidhani kwamba yupo ndani ya hoteli hiyo.
“Sasa Nurin,ndio anafanya nini?Anatoa mzigo mpaka anajisahau?”
Jambazi mmoja alisema baada ya kuangalia saa yake ya mkononi.
“Yupo kazini”
“Lisaa lishapita tayari,ama amenogewa?”
“Hawezi,yule jembe!Tumsubiri kidogo”
Hata kama wangesubiri kwa miaka mingapi nje ya hoteli hiyo,wasingeweza kumuona Ahmed na Nurin wanatoka.Lisaa limoja baadaye lilivyokatika,ndipo walipogundua kwamba halikuwa jambo la kawaida.Mmoja wao,akashuka na kuingia hotelin ambapo hapo,alianza kumdadisi dada wa mapokezi kuhusiana na wageni walioingia siku hiyo usiku.Haikuwa kazi ngumu kwa zoezi kama hilo dogo kukamilika,hiyo ilitokana na pesa kuongea!Msichana wa mapokezi akashikishwa dolla mia mbili,akazungumza kila kitu kwamba Nurin na Ahmed wametokea mlango wa nyuma,hapo ndipo jamaa huyo akatoka mbio mpaka mlangoni,huko hakuambulia kitu chochote kile.
Kwa haraka akatembea mpaka lilipopaki gari lao,akawaambia kila kitu kilichotokea.Hapo ndipo walipoamua kumtafuta Sporah hewani ili wamueleze tukio lililotokea,mbaya zaidi simu ya Sporah haikupokelewa.Wakazidi kuchanganyikiwa zaidi.
“Mpigie tena,huu ni msala mkubwa.Yule mwanamke atatutafuna tukiwa hai”
“Hapokei simu”
“Jaribu kupiga simu yake nyingine”
Zoezi hilo liliendelea kwa takribani nusu saa lizima, ndipo Sporah,akapokea simu.Taarifa alizopata zilionekana kumvuruga kuliko kawaida,mudi yake ikatoka kabisa akashindwa ni kitu gani akifanye.Hata hivyo, baada ya kutafakari sana kwa kina,akagundua kwamba namba ya Nurin ilikuwa kwenye simu yake nyingine kubwa, akatembea karibu nayo na kuanza kuangalia ni wapi alipo.
“Nendeni,Kartusi street 54.Ndio yupo hapo,kuweni makini.Anachokitaka atakipata,namuhitaji na Nurin pia akiwa hai”
Maelezo hayo kwao yalikuwa ni sawa na amri iliyotoka ikulu,kumaanisha kwamba ilikuwa ni lazima jambo hilo litekelezwe mara moja.Dereva akapiga gia na safari ya kwenda mtaa wa Kartus kuanza mara moja,kwa mwendo wa kawaida kuhofia kamera za barabarani kuwapiga picha, ziliwafanya wachukuwe nusu saa lizima mpaka kufika mtaa walioagizwa kwenda na bosi wao Sporah Trevez,walishindwa kuelewa ndio eneo hilo ama wamesikia vibaya, maelekezo waliyopewa!Hawakutaka kuumiza vichwa vyao,hapohapo wakapiga simu kwa Sporah na kumueleza hali halisi na mazingira waliyokutana nayo.Kulikuwa na miti mingi sana,pembezoni mwao!
“Yupo hapohapo,angalieni vizuri”
Uhakika huo alikuwa nao kwa asilimia zote mia moja!Simu yake kubwa ilimuonesha kwamba Nurin yupo eneo hilo bado.Baadaye akapewa habari za kushtusha sana.Kwamba simu ya Nurin ilikuwa chini,imepasuka pasuka.Hapo ndipo akajua ya kuwa Nurin ametoroka ingawa hakuelewa ni kwanini amefanya hivyo.
“Hawapo mbali,hakikisheni,mnauweka huo msitu kati.Nawapigia simu wakina King Kong, sasa hivi”
Sporah,akakasirika ajabu.Ndani ya sekunde chache akafanya mawasiliano na kundi lake jingine ili wauzunguke msitu huo wote,japokuwa ulikuwa mkubwa sana lakini kwake aliufananisha na seble ndogo tu,akiamini Ahmed na Nurin wangeonekana na wasingeweza kutoka salama kwenda popote pale!Wakati agizo hilo linatolewa yeye Ahmed alikuwa akilia kama mtoto mdogo.
Katika maisha yake hata siku moja,hakutegemea kwamba angejikuta yupo katika matatizo kama hayo,tayari alishakata tamaa,akajutia ni kwanini alikubali kuingia ndani ya nchi hiyo,kifupi kila kitu kilibadilika ghafla.Akawa kama yupo vitani,ama kinda la ndege,mategemeo yake yote yalikuwa kwa mwanamke Nurin ambaye hakuonesha wasiwasi wa aina yoyote ile.
“Ahmed,tusonge mbele futa machozi.Usilie,kuwa jasiri”
Faraja haikumsaidia chochote,wakazidi kusonga mbele bila kujua ni wapi wanakwenda,kwa umbali wa kama kilomita moja na nusu.Wakawa wamechoka kabisa,wanahema kama mbwa wa polisi!Kitendo cha kuweka makalio yao chini, wakaona kama miale ya mwanga upande wao wa kushoto!Wote wakatizama,wakaogopa na kutandwa na hofu kubwa.Ahmed,akatetemeka zaidi, akajuwa mwisho wake umefika,alivyokumbuka milio ya risasi alivyokuwa chuoni,aliogopa zaidi.Kifo ndicho aliamini kilikuwa halali yake,machozi yakazidi kumtoka mfululizo,mbaya zaidi alilia kwa kwikwi,Nurin akamziba mdomo akiamini kwa kutofanya hivyo wangeonekana na kuuwawa.
“Njoo sogea huku”
Ahmed,akavutwa na kujificha chini ya mzizi wa mti mkubwa,upande wao mwingine wakaona tochi kali!Mbaya zaidi zilikuwa zinamulika upande wao,kumaanisha watu hao wanasogea mpaka walipo!Hawakujigusa hata kidogo,tochi zikapita kandokando yao,kwa staili ya kutambaa wakaanza kusonga mbele,mpaka walipoona wameacha tochi hizo mbali,wakasimama na kuanza kutembea kwa haraka na hofu kubwa.
“Ahmed,nisikilizeeeeee.Kama nitakufaaaaaa,naomba ufanye kitu kimoja”
Nurin,akazungumza kwa sauti ya chini huku akihema.
“Nurin,nini unasema?”
“Nisikilize,usirudi chuo.Fanya urudi Tanzania,kwa njia yoyote ile”
“Una maana gani?”
“Usirudi pale Chuoni tena”
Kauli hizo zilimfanya Ahmed,azidi kuogopa zaidi.Wakasonga mbele ambapo huko walikutana na miale mingine ya tochi,walivyotaka kujificha wakawa tayari wameonekana!
“Paa! paaa!”
Risasi mbili zikafyatuliwa hewani,hiyo haikumaanisha Nurin kusalimu amri na kufa kikondoo,akamshika mkono Ahmed wakazidi kusonga mbele.
“Paaaa!”
Risasi moja,ikafumuka kutoka ndani ya bastola, hiyo ilizaa matunda sababu ilimdondosha Nurin chini.
“Nuriiiin”
“Kim..biaaaa,Kimbiaa..aaa.Watakuu…waaaa”
Nurin alizungumza akiwa katika maumivu makali mno,huku akimsihi Ahmed akimbie.Hakukuwa na jinsi,mbio alizotoa Ahmed zilitisha, kama swala akaanza kuruka miti na kuingia katikati ya miti mikubwa,miba hakuiona na hakusikia maumivu ya aina yoyote ile.
Tokea hapo,hakuweka kituo sehemu yoyote ile mpaka alipotokeza kwenye barabara ya lami.Kitendo cha kugeuka upande wa pili,akajua tayari amekufa kwani kulikuwa na lori kubwa lililobeba mizigo,kilichosikika hapo zilikuwa ni kelele za mikwaruzo ya lami na matairi, baada ya dereva huyo kukanyaga breki za ghafla,Ahmed alikuwa tayari amefumba macho yake,akijuwa tayari anaenda kugongwa na gari hilo kubwa kwani nguvu za kuruka upande wa pili zilimuishia,alihisi miguu yake imepalalaizi.Dereva wa gari hilo,akateremka kwa ghadhabu kubwa.
“Help me,please i need your help”(Nisaidie,tafadhali nahitaji msaada wako)
“Who are you?”(Wewe ni nani)
“Ahmed”
“I didn’t ask your name,identify yourself immediately”(Sijakuuliza jina lako,jitambulishe haraka sana)Mzee akafoka!
Bila nukta,Ahmed akaanza kujitambulisha nchi aliyotoka na kwanini yupo mahali hapo,akaeleza watu wanaomkimbiza wakitaka kumuuwa.
“Get in”(Ingia ndani)
Mzee wa makamo akaingiwa na huruma,hakuelewa ni kwanini ametokea kumuamini kijana huyo sababu msitu huo hata yeye aliuogopa.Licha ya hivyo,alishawahi kutekwa nyara kwa staili hiyohiyo,wakasonga mbele,walivyomfika mjini Ahmed akateremka na kutoa shukrani zisizokuwa na idadi, hakuelewa ni wapi aelekee,alichoomba Mungu kupambazuke kwanza,jasho jingi sana lilimtoka mwilini.Hakuelewa ni kitu gani akifanye.Akabaki eneo hilo akiwa amejificha nyuma ya gorofa kubwa,mpaka kulivyopambazuka!
Kitu cha kwanza kukumbuka ilikuwa ni simu yake,alivyoiwasha tu.Ikaanza kuita,akasubiri ikate ikaita tena.Aliyekuwa akipiga alikuwa ni baba yake,hapohapo akapokea na kumuelezea kila kitu kilivyotokea,suluisho lililotokea ni yeye kutumiwa nauli ili arejee nchini Tanzania.
*******
“Anafanya mawasiliano bado”
“Na nani mwingine?”
“Ni huko huko Tanzania”
“Anatarajia kuondoka lini?”
“Kesho”
“Hakikisha,mnafanya juu chini.Wapokee mwili wake”
“Kivipi?”
“Nataka mumuuwe ndani ya ndege”
“Ina maana tusafiri naye?”
“Kwani tatizo liko wapi?”
“Nilikuwa nauliza tu”
“Ukishajua ni ndege gani anapanda,nitaarifu.Ukate tiketi mapema,utaenda na Jacob”
“Hakuna shida”
“Sitopenda uzembe,naona huyu kijana ana irizi ya bibi yake!Safari hii,fanyeni kweli”
“Sitokuangusha”
Watu hawa walitisha kuliko ukoma,mtandao wao ulikuwa ni moto wa kuotea mbali.Ndani ya siku moja walishajua ni wapi Ahmed alipo,teknolojia ilifanya kazi yake.Wala haikudanganya kabisa,jambo walilokuwa wanateta simuni, lilikuwa la ukweli kabisa kwani Mzee Mohamed Kajeme, siku iliyofuata alituma pesa za nauli,kilichofanyika ni Ahmed kuibuka chuoni kisirisiri.Kilichomfungisha safari hiyo ilikuwa ni kuchukuwa hati yake ya kusafiria,japokuwa njiani alipata changamoto sababu hakujua njia ya kuelekea chuoni alichofanya kuuliza mpaka akafika.
Kila kitu kilivyokuwa sawa,bila kumuaga mtu yoyote yule, akaenda kupakua pesa alizotumiwa, akanyoosha mpaka uwanja wa ndege siku hiyo hiyo.Hakuelewa kwamba nyuma yake kuna wanaume wawili hatari,waliotumwa kum-maliza ndani ya ndege!Tayari walimuona,wakamuungia kwa nyuma na kuonesha tiketi zao,haikuchukuwa muda sana kuwa naye sambamba.Baada ya ukaguzi mfupi,wakawa wapo ndani ya ndege,mbaya zaidi walikaa jirani,siti ya nyuma yake.
Wanaume makini waliotumwa na Sporah Travez,walikuwa wajanja kuliko kawaida.Ilikuwa ni lazima wamuuwe Ahmed kabla hajafika nchini Tanzania,mpango uliosukwa ni kwamba watampokea Ahmed Uwanja wa kimataifa Mwalimu Nyerere akiwa maiti.Kila kitu walikuwa nacho mikononi mwao,sumu kali aina ya DDT ndani ya pakiti nyeusi ilikuwa tayari kwa ajili ya kazi hiyo nzito ya mauaji.Sumu hiyo waliiponda ponda ikasagika na kuwa kama unga wa kusongea ugali.Kilichobaki ni unga huo kuuweka kwenye kinywaji ama chakula chochote ili Ahmed ale afie angani ndani ya ndege,hilo ndilo agizo walilopewa na tajiri yao Sporah Trevez.Baada ya maelekezo kutoka katika kipaza sauti,ya kwamba abiria wote wanatakiwa kufunga mikanda yao, ndege ikaanza kukimbia kwa kasi kisha kupaa angani,huko ilikaa sawa na hapo abiria wote waliruhusiwa kufungua mikanda yao,wa kwenda msalani walienda na waliotaka kusimama ili kujinyoosha ilikuwa ruksa,wakati huo kwao ndio ukawa muafaka wakitaka kumzoea Ahmed ili watimize lengo lao hatari.
“Kiongozi, kwema”
Jacob,akamsogelea kwenye kiti na kumsalimia,mbaya zaidi alitumia Kiswahili kilichonyooka.
“Safi”
“Inakuwaje?Nimeona passport yako ya Kitanzania,mimi pia mtanzania mwenzako”
“Oooh,nawewe pia ni mbongo?”
“Ndio”
“Wapi?”
“Singida lakini biashara zangu nafanyia sana Dar es salaam!Wewe wapi?”
“Dar hapohapo”
“Aisee,bora hata nimepata mwenyeji mshkaji wangu.Hapa kuna mtu?”
“Kuna maza mmoja wa kizungu,nadhani ameenda toilet”
“Anyway mimi naitwa Thomas”
Jacob,akadanganya hakutaka jina lake lijulikane, akiamini kwamba haikuwa na haja sababu mtu aliyekuwa anazungumza naye tayari walishamuhesabia ni marehemu,hilo walilipa asilimia mia moja!Jacob alimtizama Ahmed kwa jicho la huruma lakini hakuwa na jinsi,hakuweza kurudisha moyo wake nyuma ilikuwa ni lazima afanye kazi na ikamilike, aliamini jambo hilo lingempa heshima kubwa katika kazi yake.Maongezi yao yalikatika baada ya mwanamke wa kizungu kurudi katika siti yake pembeni ya Ahmed,jambo hilo likaonekana kuwa kama kero kwa Ahmed,uchangamfu wa Jacob ulimfanya atake kujua mambo mengi kuhusu yeye,hususani mtu atakayempa kampani akiwa ndani ya ndege.Hiyo ilifanya awe anageuka geuka nyuma kila wakati.
“Au nije kukaa hapo nyuma?”
Ahmed akauliza huku shingo yake akiwa ameelekezea kwa nyuma,alihisi kuna kitu atakimisi kama atakuwa mbali na mwanaume huyo mchangamfu aliyejitambulisha kwa jina la Thomas,moyo wake ukamsukuma atake kumjua zaidi na ikiwezekana wabadilishane namba za simu, wazidi kuwa marafiki.Hakuelewa kabisa kama mtu huyo ni hatari kwake na kifupi mwenyewe alikuwa akienda kujichimbia kaburi.
“Ngoja basi tumuombe huyu mama wa kichina,akae hapo mbele alafu wewe uje hapa”
“Freshii”
Jacob,akavuta pumzi ndefu kidogo na kumtizama Mwanamke wa kichina aliyekuwa kando kando yao,anasoma kitabu ameweka miguu juu kajifunika na shuka miguuni.Siti waliyokaa ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria watatu,dirishani alikaa Dengu,huyu naye walikuwa wote safari moja lakini kwa wakati huo hakutaka kuongea chochote,akajifanya kama hawafahamiani.Kazi ya kumshawishi mama huyo wa kichina akitumia Lugha ya Kichina, akichanganya na kiingereza ilimfanya Ahmed azidi kushangaa zaidi,akavutiwa mno baada ya kusikia Jacob anazungumza lugha hiyo ya kichina kwa ufasaha na uhodari zaidi.Kilichomfanya apagawe tena ni kitendo cha kumuona mama huyo wa Kichina anacheka na kutabasamu kisha kusimama.
“Simama,tayari keshakubali”
Jacob,akasema!Moyo wa Ahmed ukalipuka kama bomu kwa furaha,akasimama na kuanza kupita siti ya nyuma, ambapo hapo aliketi pembeni ya Jacob!
“Hapo mambo mukide mukide sasa”
“Ndio maana yake,hapo shangwe ni stori mwanzo mwisho!Alafu mpaka unajua kichina ndugu yangu?Ulishawahi kuishi huko nini?Mambo yako mazito kama Jet lii vile”
“Ah wapi,nilikuwa na demu wa kichina”
“Sema ukweli”
“Sikutanii,sema alinipa msala”
“Upi huo?”
“Nilimtia Mimba,alivyoenda kuwaambia wazazi wake.Ilikuwa kisanga,walitaka kunitia jela.Ni stori ndefu lakini huyo demu alinikubali ile kinyama yaani”
“Mwanangu una zali”
“Sio zali,kuna kipindi nilikuwa baharia mzee baba”
“Enhee”
“Kashkash mwanangu,kwanza huku Malaysia umekuja kufuata nini?”
Jacob baada ya kuingizia hadithi za uwongo na kweli na porojo za hapa na pale ili amzoee Ahmed,akaibuka na swali.Hiyo ilimfanya Ahmed afunguke kwamba kilimchomfanya awepo nchini humo ni elimu tu na sio kitu kingine,japokuwa hakuweka wazi misukosuko aliyopitia ya kutaka kuuwawa.Jambo hilo likabaki kuwa siri yake moyoni.
“Vipi watoto?”
Jacob,akamdaka na swali lingine.
“Watoto gani?”
“Watoto wa Kimalaysia,ushampata hata mmoja?”
“Nilikuwa na mtoto mmoja fulani hivi,sema nilipata majanga”
“Yapi hayo Mzeiyaa?”
“Tuachane na hayo,bongo unapiga dili gani?”
Ndani ya dakika arobaini na tano Ahmed akawa tayari amejaa ndani ya kumi na nane za Jacob,wakawa kama wamejuana miaka mingi iliyopita kumbe haikuwa hivyo,stori zilinoga mno!Haikuwa rahisi kwake kujua kama mwanamme aliyekuwa anamzoea kwa kasi namna hiyo, ametumwa kuutoa uhai wake,kifupi Ahmed alikuwa katika giza nene!Alichojua yeye Jacob ni mtu mwema,mstaarabu ni kijana mtamfutaji na muhangaikaji.
“Mishe mishe tu alafu Marekani,niliishi pia!New York.Nimetembea mataifa mengi sana,nchi za uarabuni nimechafua sana”
Jacob alizidi kujitapa kwa Ahmed.
“Namimi siku moja natamani kuwa kama wewe”
“Kiviipi?”
“Nisafiri,nioshe macho”
“Kila kitu kinawezekana chini ya jua,ni wewe tu na uamuzi wako!Maisha ni kuchagua siku zote”
“Ni kweli kabisa”
Zoezi la kwanza likawa tayari limekamilika,kilichobaki ilikuwa ni kum-maliza kwa kumuwekea sumu hiyo kali.Uchovu aliokuwa nao Ahmed ulikuwa ni mkubwa sana,ndiyo maana akaanza kusinzia kwa staili ya kudonoa,anasinzia na kushtuka.Anasinzia na kushtuka, baadaye kichwa chake akakiweka begani kwa Jacob,usingizi mzito ukamchukuwa.
“Tayari huyu,sasa inakuwaje?”
Jacob,akamwambia mwenzake kwa sauti ya chini.
“Ngoja tubadilishe ndege,ile ya pili ndio tummalize”
“Kweli eeh?”
“Yes”
Hiyo ndiyo mipango waliyopanga wauaji hawa wawili, waliotumwa na Sporah Trevez!Kwa kuwa muda wakufanya mauaji hayo haukufika,trei la chakula lilivyopita hawakutaka kuweka sumu kwenye chakula cha Ahmed,bali walimuamsha na wote kuanza kula.
“Kumbe mambo ya misosi,alafu nina ubao kwelikweli yaani”
Ahmed alisema baada ya kutoka usingizini,alivyokula akanywa na maji na kuingia tena usingizini!Ndege ilikuwa inakaribia kutua nchini Amsterdam kisha wabadili ndege nyingine,hapo hawakutaka kufanya makosa hata kidogo na waliamini kwa mipango waliyosuka, ilikuwa ni lazima Ahmed afie ndani ya ndege ya pili,ambayo ingempeleka mpaka nchini Tanzania kisha baada ya hapo watokomee kusikojulikana.
Ni kweli ilikuwa ni kama walivyopanga,abiria wakapewa maelekezo kuwa wafunge mikanda kwani ndege ipo karibu kutua.Taratibu za siku zote za ndege ndiyo zilikuwa zile zile, mpaka abiria wote wanashuka usiku huo mkali,kila abiria alishukuru kufika salama salmin.Kilichobaki ni kila mtu kwenda kusubiri kwenye geti lake ili kusubiri ndege nyingine,hapo ilibidi wasubiri kwa masaa mengine mawili kisha waianze safari kwa mara nyingine!Kitendo cha geti, kufunguliwa tu,Jacob na Mwenzake wakawa wa kwanza kuingia ndani ya lango!Walivyozama ndani ya ndege tu,kitu cha kwanza kukifanya ni kuchukuwa chupa ya maji mapya!Wakafungua na kumimina sumu hiyo kali kisha kutingisha maji,dawa ikayayuka wakaiweka siti ya pembeni!Ni kweli,hazikupita dakika hata tano Ahmed akawa amefika akachukuwa chupa ya maji ya kunywa bila kuuliza chochote,akaiweka mdomoni akianza kunywa.
“Kuna kitu nimesahau nje,nakuja sasa hivi”
Jacob,alivyoona hali hiyo ilibidi atoke nje ya ndege, sekunde moja akasimama mwanaume aliyekuwa pembeni yake,niya yao ilikuwa ni kuondoka kabisa eneo hilo, ikiwezekana wapande ndege na kurudi nchini Malaysia kuhofia kugundulika sababu walielewa fika baada ya sekunde mbili tu ni lazima Ahmed,aanze kujikunja kunja kuugulia tumbo kisha kukata rohoo,hawakutaka kuhojiwa maswali kwani ilikuwa wazi kabisa,wangeshikiliwa na kuhojiwa.
*******
Lugha walizokuwa wanazungumza hazikueleweka kirahisi,pili mavazi waliyovaa yalikuwa ya ajabu.Watu hao ilikuwa ni vigumu kukutana nao sehemu za wazi,waliishi misituni tu.Mavazi yao yalikuwa ni vibwebwe,vilivyozuia sehemu za siri na kwenye makalio!Walikuwa ni watu weusi tii,waliokomaa misuli.Wanakijij hao walijitenga kabisa na kuishi misituni,ilizoeleka kwamba kila siku asubuhi wakiamka ni lazima wote waingie porini, kuwinda.Lakini siku hiyo ilikuwa ni kinyume kabisa,wanawake wengi walijaa ndani ya kijumba kidogo kilichokuwa na nyasi juu yake.Walikuwa katika masikitiko makubwa sana,kila mwanamke alijaribu kutoa msaada wake.wengine walichota maji,baadhi walikuwa jikoni wanapuliza moto ukolee wachache walikuwa wanatengeneza dawa za miti shamba,ilimradi tu wamsaidie mwanamke mwenzao aliyeokotwa kwenye mto wenye mamba!Mbaya zaidi tangu,afikishwe eneo hilo hakuwahi kufumbua macho yake,majeraha ya risasi yalikuwa ni mengi mno!Hajrath,alikuwa tayari amepoteza kiasi kikubwa cha damu mwilini,hakujitambua kwa wakati huo!Wanawake waliokuwa wanamsaidia kumpa huduma ya kwanza, walikuwa makini sana,kupekecha majani ya miti ulioitwa mtetei,wakatwanga ndani ya kinu na kumimina maji ya moto yaliyokuwa na dawa nyingine ya mizizi,baada ya hapo wakachukuwa na kuanza kubandika kwenye kila jeraha,lililokuwa mwilini mwake!Walifanya hivyo, wakiamini ya kwamba wanatoa sumu mwilini iliyosababishwa na risasi. Baada ya hapo,wakachukuwa kikopo kingine kilichokuwa na mafuta ya rangi nyeusi,wakaanza kumkanda na mafuta hayo mwili mzima,baadaye kila mtu akatoka ndani ya chumba hiko!Usiku wa siku hiyo wakafanya kama walivyofanya asubuhi yake,zoezi hilo lilivyokamilika kila mtu akaenda kulala.Kulivyopambazuka siku iliyofuata,mzee mmoja akawa amefika katika kijiji hiko,huyu alikuwa ni daktari bingwa waliyemtegemea,alikuwa mzee aliyekula chumvi nyingi sana!Waliamini kabisa siku zote Ng’ombe mzee hazeeki maini,hiyo ndiyo sababu ya kumuita babu huyo atoe tiba mbadala kama kutoa risasi ndani ya mwili wa Hajrath,babu huyo aliyefahamika kwa jina la Nkosiyabo,alimshughulikia Hajrath akitumia dawa za asili,japokuwa zoezi hilo lilionekana kuwa changamoto kubwa sana kwake,mpaka usiku akawa amefanikiwa kutoa risasi zilizokuwa mwilini mwa mgonjwa huyo mahututi.
Swala lililobakia ni Hajrath kukandwa na vidonda vyake kupakwa dawa ili aweze kurejea, katika hali yake ya kawaida.Wanakijiji walionesha ukarimu mno,japokuwa hawakumjua hata kidogo wala hawakujua ni wapi ametokea.Tiba hizo ziliendelea kwa takribani wiki tatu, mfululizo bila kukoma.Hajrath hakuwahi kulala peke yake ndani ya chumba hiko,isipokuwa wakina mama walipokezana kulala naye!Kuhakikisha kwamba anakuwa salama,siku hiyo usiku haikuwa siku ya kawaida.Mwanamke aliyelala naye hakuamini macho yake,vidole vya Hajrath vilianza kutingishika.Hatimaye taratibu alianza kufumbua macho, huo kwake ulikuwa kama muujiza mkubwa kutokea.
“Niiiipo waa…..pi?”
Hilo ndilo swali la kwanza kuuliza Hajrath kwa sauti ya mbali naya chini sana,alivyotaka kuinuka akahisi maumivu makali sana,sehemu za mbavu!
Tabia ya Kassim,ilikithiri! Japokuwa alipigwa mikwara na baadhi ya wanaume waliosadikika anatembea na wake zao lakini kwake ilikuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa acheze mziki,mwendo wake ulikuwa ni ule ule, chapa ilale.Ushenzi aliokuwa anafanya wa kuwavua nguo za ndani watoto wa kike, akitumia gia tofauti tofauti haukuishia hapo bali aliendelea pia kumsumbua Yusrath,msichana mrembo ambaye alijua kabisa ni shemeji yake lakini kwake yeye hakujali.
Sio kwamba hakuwa anaelewa anafanya kitu ambacho sio kizuri katika jamii,hilo alilijua lakini hakutaka kujali,alichotaka yeye ni kumvua nguo ya ndani Yusrath afanye naye ngono,ndiyo maana kila siku alimsumbua na kumgasi simuni.Kwa takribani mwezi mzima, aliendelea kumuimbisha na kumtupia mistari mbalimbali yenye swaga lakini ikawa ni sawa na kuchora nambari nane kwenye maji!Yusrath hakutingishika wala kubabaika na maneno yoyote yale,Kassim alivyoona hivyo akatumia gia nyingine ya kutuma vocha za simu lakini matokeo yake,zilirudishwa akachomolewa na kupigwa cha mbavu,hiyo haikuwa kawaida hata kidogo kwa Kassim kutolewa nje!Alitaka kujua ni kwanini msichana huyo anamzungusha namna hiyo,licha ya yote alijipa moyo na kuupiga moyo konde ya kwamba ipo siku Yusrath, atajaa kwenye kumi na nane zake!Akajipa muda wa siku mbili bila kumtafuta ili atingishe kiberiti akidhani wenda msichana huyo angempigia simu na kumuanza yeye lakini wapi,hakukuwa na dalili ya aina yoyote ile ya Yusrath kupiga simu wala kubip,ilivyopita siku ya tatu jambo likawa lile lile.Lakini cha kushangaza usiku wa siku hiyo, simu yake ilianza kuita na alivyoangalia juu ya kioo akaona jina la Yusrath,moyo wake ukapiga mkambo!Hakutaka kuamini kile anachokiona,ilikuwa ni kama ndoto kwake kupigiwa simu na Yusrath,bila kupoteza muda hapohapo akaipokea na kuiweka sikioni!
“Yusrath,mambo vipi?”
Kassim,alianzisha salamu.Mapigo yake ya moyo yalipiga kwa kasi,akitaka kujua ni kitu gani Yusrath angetaka kumwambia, usiku huo mzito.
“Safi,samahani kwa kukusumbua usiku”
“Bila samahani”
“Simpati Ahmed hewani,uliwasiliana naye leo?”
Maneno hayo kwa Kassim yalikuwa kama mshale wenye moto,moyo ulimuuma ajabu.Akatamani kukata simu lakini hakutaka kufanya hivyo kwanza,akahisi kama moyo wake unakatwa katwa na viwembe siku hiyo,wakati mwingine alianza kujuta ni kwanini,amepokea simu ya Yusrat kifupi sentensi hiyo ilimuharibia usiku mzima.
“Halloo,Kassim!Nimekuuliza swali”
Yusrath akarudia tena kuuliza,baada ya kuona kuna ukimya wa sekunde tatu.Kuna kitu alianza kuhisi,akajua ni kwanini Kassim amepiga kimya,kwa umri alikuwa ni msichana mdogo lakini akili yake ilichaji kwa kasi ya umeme.
“Najua unachofikiria Kassim,naomba ukubaliane na matokeo niliyokwambia.Nampenda Kaka yako,hilo halitobadilika”
“Hata kama,ndio unifanyie makusudi”
“Ningekuwa na mtu mwingine wa kumuuliza,ningemuuliza.Sina wa kumuuliza,nimejitahidi kujikaza lakini nimeshindwa,naelewa ni kwa namna gani unaumia Kassim”
“Nakupenda Yusrath,kaka yangu asiwe kikwazo cha wewe kuniumiza namna hii,cha ajabu mimi nilianza kukujua kabla yake”
“Naelewa”
“Kwanini umenifanyia makusudi?”
“Sio mimi,ni moyo Kassim.Nampeda sana Ahmed,elewa nachokwambia.Mbona wasichana wapo wengi tu,tena wazuri”
“Nimekuona wewe”
“Namimi nimemuona kaka yako”
Nyimbo zote alizomuimbisha Yusrath kumlainisha ziligonga mwamba,Yusrath siku hiyo alionesha ustaarabu wa hali ya juu,akawa anamchinja Kassim huku anamchekea. Kazi yake ilikuwa ni kutengeneza hoja za kumchomolea na kumkataa tu!Siku hiyo hakutaka kuwa mkali hata kidogo, kama afanyavyo siku zote.
“Wakati mwingine Kassim,inabidi ukubaliane na hali halisi ili maisha yaendelee,kubali tu.Huo ndio ukweli wangu,nampenda Ahmed”
“Hata mimi nakupenda”
“Sijakuzuia kunipenda”
“Nipe nafasi nijaribu,kukuonesha”
“Kassim,mapenzi hayajaribiwi.Mapenzi sio gari”
“Simaanishi hivyo”
“Kuwa mwelewa basi”
Alivyoona somo halieleweki, ilibidi awe mkali kidogo,akaongea kwa sauti ya hasira. Hapo ndipo Kassim akatulia na kukubali,nayeye akakata simu kwa hasira akiapia ya kwamba ipo siku atampata Yusrath,amvue nguo yake ya ndani.Kwake kumpata Yusrath Suleiman,ilikuwa kama ndoto na ilikuwa lazima itimie.
*******
Deffender ya polisi,ilikuwa imepaki Manzese kwa mfuga mbwa.Ndani kulikuwa na askari wawili,nyuma sita,wanatizama huku na kule.Ilikuwa ni lazima siku hiyo, wamtie mikononi mtu anayeitwa Jitu baya,kwa muda mrefu sana walimfuatilia.Hiyo ilikuwa mara ya nane kumsaka bila mafanikio, baada ya kumkosa kosa Arusha,baadaye Morogoro na walivyosikia yupo Tanga.Jeshi la polisi likaweka mtego wake lakini walimkosa aliwatoroka.Askari wakapata usongo wa ajabu.Walivyopata fununu yupo jijini Dar es salaam na makazi yake ni Manzese kwa Mfuga Mbwa wakafunga safari usiku usiku.Operesheni hiyo nzima ilisimamiwa na Kamishna wa jeshi la polisi wa wilaya ya Ilala Kamanda Matiku Wambura,hiyo ilimaanisha operesheni hiyo iende kama ilivyopangwa.Nyuma ya msako huo, kulikuwa na mkono wa mpelelezi Mohamed Kajeme,ilikuwa ni lazima wamuweke Jitu Baya chini ya ulinzi ili ataje ni wapi Hajrath Mpilla alipo,askari walikuwa wenye usongo kuliko kawaida.Hiyo ni baada ya wenzao kupigwa risasi na majambazi huko Gongo la Mboto, wakiwa katika msako huo,ndiyo maana wote walikuwa na mitutu mabegani wakisubiri oda kutoka kwa mkuu wao.Macho yao yote yalikuwa nje ya kijumba kidogo, chenye mlango mfupi,bati lililochoka choka.Maelezo waliyopata ni kwamba Jitu Baya, yupo ndani ya kijumba hiko,anavuta bangi na kujidunga madawa ya kulevya kwani alikuwa ni miongoni wa wateja wa madawa hayo makali, yanayopigwa vita,karibu Dunia nzima!
“Oyaaa,mwaaanaa!Nitembezeee cha ukuchaa”
Ndani ya kijumba hiko uwani kulikuwa na wanaume wanne,watatu walikuwa mateja waathirika wa madawa hayo,wanatoa udenda na kujikuna kabisa,aliyeonekana na afadhali kidogo ni Jitu baya,hiyo ni kutokana na afya yake kuimarika.Mkononi alikuwa na kipisi cha bangi, pembeni kulikuwa na sindano iliyojazwa dawa hizo ili baadaye ajidunge,hakuwa anajua kwamba nje kuna diffenda inamlia mingo.
“Nitembezee dawa boy”
“Poaaa babaaaaake,letaaa hiyooo basi.Hikii cha Arushaa nini Mkushiiiii?Mbona kina stimuu namna hii.Hapaa najiona nipo kwa Madibaa Mandela yuleee,wazee wa meliii walee!Alafu nini mwanangu,mimi nataka niendee mtoniii,nizamie haya maishaa ya bongo siwezi.Bongoo nyosooo mwanaa”
Hayo ndiyo maneno ya teja huyo baada ya kujidunga sindano kwenye mshipa wake wa damu,kila kitu kwake kikaonekana kuwa vizuri,akahisi kama anapaa angani.
“Oya,majita eeh.Mimi najikatua!Kesho nitatimba.Au sio?”
Jitu baya,akasimama na kuwaaga wenzake.Kitendo cha kufika nje na kutokeza tu,macho kwa macho akakumbana na diffenda,akageuza kama panya aliyeonana na paka,akarudi.
“Pilaaaaa Pilaa pilaaaaa”
Jitu baya akaropoka huku akikimbia akiwaambia wenzake akimaanisha diffenda,sekunde moja zilikuwa nyingi askari wakawa tayari wameingia ndani.Hiyo haikufanya Jitu baya asimame, kama ngedere akarukia ukuta,akaushika vizuri na kujitupa nje.
“Zungukeni….karuka ukuta”
Askari mmoja akasema,wote wakatoka nje na kuanza kumkimbiza jitu baya!Njiani watu walipigwa vikumbo,askari hawakutaka kumuacha ilikuwa ni lazima warudi naye kituoni,ndiyo maana hawakutaka kumuachia.
Mbio alizokuwa anakimbia Jitu baya,ziliishia Manzese Tip top, hiyo ni baada ya Diffenda ya Polisi kupiga msele mbele yake,askari wawili wakatua ardhini kama makomandoo,mmoja akamchota mtama kimo cha mbuzi,kabla ya kutua vizuri, akapigwa kirungu cha mgongo!Hakuna mtu aliyezungumza naye,akapigwa pingu na kupakiwa kwenye diffenda,ndani ya sekunde mbili kupita hakuna raia yoyote Yule aliyejuwa kama kuna kitu kilitokea,hatimaye Jitu baya akawa chini ya Ulinzi.
“Aroo,reo ndio arobaini yako,tunakupereka Central na utaereza kwanini mbuzi ana mkia mfupi”Afande Marwa, alipiga mkwara akitumia rafudhi ya kikurya.Hakuna maabusu iliyotisha kama Central,ilikuwa chini kama andaki humo ndimo, washtakiwa sugu hutupwa,ilikuwa wazi kabisa kwamba ilikuwa ni halali kwa Jitu Baya kuhifadhiwa humo.
******
“Drinking water”(Maji ya kunywa)
“Cold or Warm?”(Baridi au moto)
“Warm please”(Moto tafadhali)
“Okay,a moment please”(Sawa,dakika chache tafadhali)
Ahmed,alihisi kiu kikali sana!Alitaka kukikata kwa kunywa maji ya moto kutokana na baridi kali la nchi hiyo,alibakiza dakika thelathini tu ili ndege inayoelekea, barani Afrika Nchini Tanzania jijini Dar es salaam iruke angani,hiyo ilimaanisha kwamba maji hayo ilibidi anywe akiwa ndani ya ndege!Dakika mbili, zikawa zimebaki ili geti lifungwe,akaanza kutembea kwa kasi na kuyaweka maji kwenye begi dogo la mgongoni,alivyoingia ndani ya ndege akakuta kuna maji pia,akachukua lakini akakumbuka pia ana maji ndani ya begi.Kutokana na kubadilisha maji hayo kwa pembeni,Jacob hakuona. Akadhani ndiyo maji yenye sumu,ndiyo maana aliondoka haraka na mwenzake kutoka nje!Ahmed hakuelewa lolote,akaendelea kunywa maji yake.Hakutaka kuuliza chochote,lakini baada ya ndege kuanza kutembea, ilibidi amwambie Muhudumu kwamba kuna abiria amewasahau.
“Wameghaili kusafiri,wanadai kuna vitu wamesahau”
Ahmed,alisikitika sana!Kampani aliyokuwa nayo iliondoka,hakuelewa kwamba watu hao walitumwa kumuuwa yeye na ilibidi amshukuru Mungu wake aliye juu mbiguni,ndege ikaanza kupaa angani.Huko sura ya Yusrath ikamjia kichwani,akamuona jinsi anavyotabasamu.Akaenda mbali zaidi kifikra na kuanza kuwaza namna ndoa yao,itakavyofanyika!Akaongezea katika mawazo yake, atakuja kuwa baba mzuri kwa watoto wake, tena mwenye uwezo,aliapia kujituma mpaka pumzi yake ya mwisho,siku zote alitamani kuwa tajiri na alijuwa kabisa kuwa jambo la kuwa tajiri halikuwa la kuamka leo kisha kesho una mali,ilikuwa ni lazima ujinyime uumie,ukubali kusemwa na kupigwa majungu.Hilo, alilijuwa fika. Alikuwa yupo tayari kukabiliana na hali yoyote ile,kutokana na msongo wa mawazo usingizi ukamchukuwa.
*******
“Ahmeed….Nisaidieee…Ahmed…Naa…kufaaaa,please,Ahmeed,nakufaaaa”
Mbele yake,alisimama Hajrath anavuja damu mwili mzima hususani puani na mdomoni,pembeni yake kushoto alikuwepo mwanamke anayempenda Yusrath!Mbaya zaidi walikuwa katikati ya sherehe kubwa ya kuvishana pete ya uchumba,ndipo Hajrath akatokea akiwa katika hali hiyo ya kutisha kama Zombi, anaomba msaada.
“Wata.,..niuaaa,nisaidiee!Ahmed…Achaaa…na na Yusraaat,atakuuwa.Sio mwanaaa…mke mzuriiii kwako,atakuuwa!Nisaidiee”
Sio Ahmed wala Yusrath,hata wageni waalikwa wote, walikuwa katika butwaa kubwa sana,hakuna hata mmoja kati yao aliyeelewa mwanamke huyo katokea wapi,isipokuwa Ahmed peke yake!Mbaya zaidi, alizungumza mambo ya kuogopesha,eti Yusrath ni mwanamke mbaya kwake,katika hali ya kushangaza na kustaajabu Yusrath akachomoka akiwa na kisu,akamchoma nacho Ahmed tumboni.
*******
“Uwiiiiiiiiii”
Zilikuwa ni kelele kali,alizoachia Ahmed baada ya kushtuka usingizini kama kungekuwa na mtu pembeni yake basi angepigwa ngumi na kutolewa meno,Ahmed alivyoshtuka alitupa na ngumi kali,akasimama kama masai aliyekurupushwa lindoni,wazungu na baadhi ya abiria wote walimshangaa yeye wengine walishtuka.
“Are you out of your mind!”(Umerukwa na akili)
Mzee mmoja wa kizungu,alikasirishwa akaropoka kwa gadhabu, hiyo ni kutokana na kushtuka kutoka usingizini.Ahmed,hakujibu chochote,akakaa kitini,mrembo aliyevalia kimini rangi ya kijani na shati jeupe akasogea karibu yake,huyo alikuwa muhudumu wa ndege!
“Are you okay sir?”(Upo sawa Mheshimiwa)
“I’m fine,just a nightmare”(Nipo sawa,ni ndoto tu ya kutisha)
Hapo Ahmed akatulia na kuanza kuitafakari ndoto hiyo ina maana gani,licha ya kutafakari lakini hakutaka kuitilia maanani sababu hakuamini ndoto hata kidogo.Ndege ilitoboa mawingu mchana kutwa,mpaka inafika saa nne ya usiku, ndipo walipotua Jijini Dar es salaam.Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwalimu Nyerere!Bado Ahmed hakuamini kama amepona na anavuta pumzi,kila kitu kilichotokea kwake kilikuwa kama sinema ya kuigiza ama ndoto ya kutisha,machozi yalimlenga baada ya kukumbuka maswaibu aliyopitia,hakutaka kuamini kwamba amerudi nchini Tanzania akiwa salama salmin kabisa,akavuta begi lake la mgongoni na kushika hati yake ya kusafiria vizuri!Akasimama na kuanza kuutafuta mlango,alivyoshuka ngazi akaanza kutembea, kuelekea dirisha maalum ili kugonga passpot yake muhuri wa kuingia nchini Tanzania,kitendo cha kutokeza langoni.Mama yake mzazi aliachia ukelele mkali,akamkimbilia mwanaye na kumkumbatia kwa nguvu huku akilia machozi, hakuamini kama mwanaye amepona na amerejea nchini Tanzania akiwa hai,matumaini yake yote yalipotea.Mzee Mohamed Kajeme,alilengwa na machozi lakini hakutaka kulionesha swala hilo waziwazi,alichofanya ni kutoa kitambaa na kujifuta machoni,akamsogelea mwanaye!Wakakumbatiana,hakuna hata mmoja kati yao aliyeamini hilo,ulikuwa ni kama muujiza,Ahmed akamwaga machozi kama mtoto mdogo,alilia mfululizo.
“Ahmed,upo salama nyumbani.Mshukuru Mungu”
Hivyo ndivyo Baba yake,alimfariji.Hawakutaka kupoteza muda,wakanyoosha moja kwa moja mpaka walipoegesha gari,wakaingia na safari ya kurudi nyumbani kuanza mara moja!Ahmed,aliwaadithia wazazi wake kila kitu kilichotokea, alivyokuwa nchini Malaysia,misukosuko aliyopata!Usiku wote huo alitumia,kuwaeleza wazazi wake jinsi alivyonusurika kuuwawa.Walimuonea huruma na kumpa pole!Alivyokula na kuoga,akaingia chumbani,kitu cha kwanza kukumbuka ni msichana anayeitwa Yusrath,hapohapo akachukuwa simu yake na kuanza kutafuta laini kwenye kabati,bahati nzuri akaipata ambayo alikuwa anatumia zamani,akaiweka kwenye simu na kumrukia Yusrath hewani,matokeo yake simu iliita bila kupokelewa!Akapiga tena,ikapokelewa.
“Hallooo….”
Upande wa pili wa simu,ukasikika sauti nyororo ikapenya ndani ya sikio la Ahmed,moyo wake ukapiga kwa nguvu,sauti hiyo ilikuwa ya Yusrath. Bado hakuamini kama leo hii amerejea nchini Tanzania na ataongea naye,hakujua aongee neno gani baada ya hapo,alikuwa kama amepigwa na shoti ya umeme!
“Mambo Yusrath”
“Poa”
Mapigo ya Moyo ya Yusrath yakamwenda mbio,hakuwa mwenye uhakika kama sauti anayosikia anaifananisha ama sauti zinafanana fanana.
“Za masiku?”
“Nani mwenzangu?”
“Ahmed”
Moyo wa Yusrath,ukapiga paa!Akatoa simu sikioni na kuangalia ili kuhakikisha namba lakini zilikuwa ngeni.
“Ahmed,no!Haiwezi kuwa kweli,Ahmed.Is that you?”
“Yes,ndio mimi Yusrath Mke wangu”
Ki ukweli Yusrath alitamani kupiga kelele za furaha,namba zilikuwa za Tanzania kumaanisha kwamba Ahmed amerejea lakini hakuwa ana uhakika.
“Upo wapi?”
“Tanzania,Dar es salaam”
“Oh My God,naota ama?Umekuja lini baby?”
“Sasa hivi nimeingia”
“Real,likizo au?”
“Hapana,tutaongea baby.Naomba nikuone kesho”
“Wapi Darling?”
“Popote tu”
“Nambie wapi,mimi nitakuja.Imiss you”
“Golden Green hotel”
“Sawa,saa ngapi?”
“Nitakwambia”
Usiku huo walikesha wakiongea vitu mbalimbali,kila mmoja alikuwa ana kiu na mwenzake,stori zilikuwa nyingi na kufanya mpaka Ahmed aanze kusinzia.
“Baby,umelala?Halloo baby”
Ahmed,alikuwa tayari amepotelea usingizini simu ipo kitandani kamuacha Yusrath hewani peke yake!
******
Walichopanga kilienda sawa,Yusrath ilibidi atumie akili nyingi kuwadanganya wazazi wake juu ya safari ya ghafla iliyojitokeza ikiwa niya yake ni kwenda kuonana na Ahmed hotelini,alikuwa yupo tayari kwa lolote sababu alimpenda kutoka moyoni,hakupata picha ni kitu gani angekifanya endapo ataonana na Ahmed siku hiyo, macho kwa macho!Kwa Ahmed kutoka halikuwa tatizo lolote,baba yake alimpenda hata alivyomuomba gari, atumie hakukuwa na kipingamizi.Mbaya zaidi akampumbaza baba yake ya kwamba anaenda kutafuta chuo ili aendelee na masomo yake ya kupata ‘masters’ kumbe haikuwa hivyo,akanyoosha gari mpaka Ubungo maziwa na kutafuta hotel hiyo,huko alilipia chumba na kupewa funguo,akamtumia meseji Yusrath akimtajia chumba alichokuwa!Dakika ishirini, zikawa nyingi,simu ya mezani ikaita.
“Kuna mgeni wako,anaitwa Yusrath”
Upande wa pili wa simu ulisikika.
“Sawa mruhusu apite”
Ilikuwa ni hoteli ya kisasa,ambayo hauwezi kuingia bila kupitia mapokezi na simu ipigwe mteja atoe ruksa!Yusrath akapanda ngazi, mpaka chumba namba 97,akagonga mlango.Mapigo yake ya moyo yalimwenda mbio ajabu.Mlango ukafunguliwa,moyo wake ukapiga paa!Baada ya kumuona Ahmed,ametanda mlangoni!Akamrukia kwa nguvu,wakafunga mlango!Hakukuwa na maongezi mengine zaidi ya kulambana midomo kwa fujo,siku hiyo kila mtu alikuwa mwenye moto,Ahmed akaanza kuvua shati lake harakaharaka,Yusrath akaanza kuvua kitambaa alichovaa kichwani,akatoa shati na kuvuta sketi chini,sio siri msichana huyu alikuwa anawaka sio kawaida, hiyo ilimfanya Ahmed,apandishe mori.Akamsaidia kutoa sidiria.Kifua cheupe cha Yusrath kikawa wazi,chuchu zimesimama wima sio pancha!Hapo ndipo, alidata zaidi,akainama kidogo akaanza kuzilamba huku mkono mmoja ukipita kwenda kwenye ikulu ya Yusrath,hiyo ilimfanya mtoto huyu Yusrath afumbe macho yake,vitu alivyohisi ndani ya mwili wake, havikuwa vya kawaida hata kidogo,tayari alikuwa katika ulimwengu mwingine wa huba,akahisi ameota mabawa yupo juu ya dunia, vitu vyote anavitizama kwa chini.
“Mmmmmh”
Akaguna,tayari hali yake ilikuwa mbaya baada ya Ahmed,kuinyonya shingo yake,hiyo ilifanya mpaka aishiwe nguvu za miguu!
Kila mmoja kati yao aliishiwa nguvu,akili zao zilihama kabisa.Miguno na mabusu ndiyo yaliyosikika kwa wakati huo.Miili yao ndio ilizungumza tu,wakatupana kitandani wakiendelea na zoezi hilo lililowaleta duniani,wakabaki kama walivyozaliwa.Kilichofuata hapo,mimi nawewe hatujui!
Dakika ishirini na mbili baadaye, kila mtu alikuwa anahema kwa mbali,wanatabasamu. Yusrath yupo juu ya kifua cha Ahmed, anamkwaruza na kucha zake kimahaba,kila kitu kwake kilikuwa ni furaha,akajihisi kama yupo kwenye pepo ndogo!Kurejea ghafla kwa Ahmed kulimfanya atake kujua kisa nini!Hapo ndipo akaibuka na swali.
“Siamini baby,hivi niwewe ama naota?Imekuaje?Hukuniambia”
Yusrath,akauliza swali huku kichwa chake kikiwa bado kipo kifuani kwa mpenzi wake Ahmed, anadeka.
“Sio ndoto ni mimi Yusrath,hata hivyo siamini kama nimefika salama”
“Kwanini?”
“Ni stori ndefu kidogo”
“Ahmed,kuna nini?Niambie”
Hapo ilibidi Yusrath ainue kichwa chake kidogo ili asikilize kwa umakini,akamtizama Ahmed kwa macho fulani hivi ya uwoga ya kutaka kujua kilichomsibu mpenzi wake,akavuta shuka kidogo na kukaa kabisa kitako akiegemea pembe ya kitanda,hiyo ilimfanya Ahmed ajivute nayeye akae,akamvuta karibu yake na kuanza kumchezea nywele.Hapo ndipo, taratibu akaanza kumueleza kila kitu kilivyotokea kuanzia alivyofika nchini Malaysia na maswaibu aliyokumbana nayo alivyokuwa nchini humo lakini katika kuhadithia kwake hakumtaja mwanamke, anayeitwa Nurin,alielewa ni kwa namna gani Yusrath angejisikia.Wakati mwingine ilikuwa ni lazima uweke vitu vingine viwe siri ili kuepuka maswali, yasiyokuwa ya lazima,hivyo ndivyo alivyoamini Ahmed.Japokuwa Ahmed alikuwa salama salmin lakini Yusrath alilengwa na machozi,historia hiyo ilimgusa sana mtima.
“Pole sana Darling”
“Nishapoa mke wangu,nashukuru nimekuona.Things happen for a reason”
“Ukiwa na maana gani Honey?”
“Jambo lile lilitokea ili mimi niwahi kurudi nionane nawewe”
“Mmmh baby”
Kilichofuata hapo,wote kuingia bafuni kuoga walivyorudi tena kitandani shughuli ilianza upya.Mchana ulivyofika siku hiyo waliagiza chakula,walizungumza vitu chungumzima, hususani kuhusu swala lao la mahusiono.Furaha iliongezeka baada ya Yusrath kumwambia Ahmed kwamba amefaulu katika masomo yake,kila kitu kilizidi kuwa shangwe sana kwao!Mapenzi yao yalizidi kumeta,hayakuishia chumbani tu na kufanya ngono bali walipanga vitu vingi hususani juu ya maisha yao ya baadaye.Wote waliamini kwamba baada ya mapenzi kuna maisha yanaendelea.
“Baby,nimefungua account bank juzi.Nitakuwa na save kila wiki elfu ishirini”
Lilikuwa ni wazo kubwa sana kwa msichana huyu mdogo kulisema,ungemuanglia kwa haraka ni lazima ungemchukulia poa lakini kichwani kwake alikuwa mwenye kiu sana ya mafanikio na mipango mikubwa,siku hiyo alimwambia Ahmed simuni bila kumficha kwani hakuwa na mwingine wa kumueleza ndoto zake.
“Habari nzuri sana hizo,nakupenda sana.Nina amini utakuja kuwa Mama bora”
“Hata wewe baba bora pia”
“Siwezi kuwa baba bora bila wewe”
“Kweli eeh?”
“Ndio,huo ndio ukweli”
“Nataka nikufanye ujivunie kuwa namimi Ahmed”
“Nafurahi kusikia hivyo”
“Vipi kuhusu mipango yako ya maisha,chuo utaendelea tena?”
“Bado sijajua,lakini nina kiu ya kufika Masters”
“Sikia nikushauri kitu Ahmed mme wangu.Tafuta Masters huku ukiwa na kazi,chukua masomo ya usiku!Mchana unatoka kazini unaingia chuo,Yule mzee uliyekuwa unafanya kazi kwake bado yupo?”
Hayakuwa maneno ya kawaida kwa msichana mdogo kama huyo kuyatamka, ilizoelekea kwa tamaduni za kiafrika ya kwamba watu wenye ushauri ni wazee wenye umri mkubwa.Licha ya hayo Ahmed hakutaka kumpuuza,kila hoja yake alimuunga mkono, moja kwa moja.
“Baby thanks,hakika ni ushauri mzuri sana.Ushawahi kufanya kazi ustawi wa jamii nini?”
Ahmed akaweka utani kidogo ili kunogesha maongezi.
“Ha! Haa! Haaa! Haaaa! Hapana baby,alafu nina plan nyingi sana kichwani ujue.Wakati mwingine nikimwambia Mama ananichukulia mimi ni mtoto,tofauti nawewe.Unanipa sana moyo,nina uhakika tutafika mbali,naamini hilo Ahmed”
Hizo ndizo ndoto walizokuwa nazo wapendanao hawa wawili.Usiku wa siku hiyo, walitumia nafasi hiyo kuzungumza mambo mengi mno!
“Baby,kitu kimoja.Naomba usimsahau Mungu,uwe una swali.Upate swawabu”
Ukweli ndio huo,Ahmed hakutaka kuweka wazo la Yusrath kapuni,walivyotakiana usiku mwema na kukata simu,wakalala.
Kulivyopambazuka Ahmed akawa wa kwanza kuamka kutoka kitandani,akanawa uso na kunyoosha mpaka seblen,niya yake ikiwa ni kumsubiri baba yake atoke.Ilielekea kuna jambo, alitaka kuzungumza naye kabla hajaelekea kibaruani.Hakukaa sana,akasikia mlango wa chumba cha wazazi wake unafunguliwa,baba yake akatoka akiwa tayari amechomekea lakini chini bado hakuwa na viatu,hiyo ilikuwa kawaida yake kuvalia viatu seblen.
“Shikamoo Baba”
Ahmed,alisalimia akiwa amesimama na kuweka mikono nyuma kwa adabu zote.
“Marahaba,hujambo?”
“Sijambo,baba nina shida nawewe.Nina mazungumzo”
Mzee Kajeme,baada ya kusikia ombi hilo akatizama saa yake ya mkononi kama ataweza kukaa chini kwani siku hiyo alikuwa na kikao kizito.
“Jioni,nikirudi haitowezekana?”
Akajibu kwa swali.
“Sawa tu”
“Basi jioni,nikirudi nikumbushe”
“Nitakusubiri”
“Kassim yuko wapi?”
“Amelala nadhani”
“Mfundishe mdogo wako maisha”
“Sawa Baba”
“Alafu kitu kimoja”
“Naam”
“Pia,nina mazungumzo nawewe.Nadhani hiyo usiku tutaongea vizuri”
“Sawa baba”
*****
“Chukua,umepewa hii”
“Na nani?”
“Pokea kwanza”
“Amina,siwezi kupokea kitu ambacho sijui kimetoka wapi”
“Kwahiyo mimi,huniamini?”
“Sio kwa staili hiyo,nani amekupa?”
“Hans”
“Nilijua tu,yaani nilianza kujua.Sasa mwambie hivi,siwezi kuwa naye.Inshort hata wanaume wote wafe duniani abaki yeye peke yake,hawezi kuwa namimi.Alafu please,usitoe hata neno moja.Mwambie kama nilivyokwambia”
Sio siri,Yusrath hakuwa msichana wa kawaida hata kidogo,wanaume wote waliomfuata kumtongoza na kumlaghai na zawadi waligonga mwamba,waliishia kupakwa shombo na kuchomolewa,hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa mwanaume anayeitwa Hans kukataliwa.Zawadi zake zikarudishwa,hakuambulia kitu.Kama kawaida ya Yusrath usiku akampa ripoti Ahmed juu ya kijana msumbufu Hans,kuonesha msisitizo akatuma mpaka namba.
“Baby mwambie anikome,mwambie ushanichumbia.Hanielewi baby”
Siku hiyo Yusrath alilalamika simuni,akitoa mashtaka.Kutongozwa na mwanamme mwingine kwake ilikuwa kama kero kubwa sana.Ahmed hakuwa na lingine la kuongeza zaidi ya kumuhaidi swala hilo,atalifanyia kazi na kila kitu kitaenda sawa,saa nne ya usiku ndipo Mzee Kajeme, akaingia ndani.Alivyopaki gari tu,akamtaka Ahmed atoke nje wakae.Viti vikatolewa na meza ndogo.Baada ya salamu za hapa na pale,Mzee akaanza mazungumzo!
“Ulitaka kuzungumza namimi asubuhi”
“Ndio Baba”
“Niambie,jambo gani?Umepata mchumba nini?”
Mzee Kajeme,akaweka utani kidogo kama kawaida yake.Alitaka kidogo watabasamu ili Ahmed ajisikie huru!
“Hapana,ni mambo tu ya maisha”
“Mambo gani hayo?Nieleze”
Hapo ilibidi Ahmed,afunguke mpango mzima wa maisha yake anavyotaka yawe kwamba anataka kuanza kazi huku akiwa anasoma masomo ya ngazi za juu.
“Utaweza Ahmed?Kusoma na kufanya kazi?”
“Ndio baba nitaweza”
“Ushatafuta chuo?”
“Kitapatikana tu,hilo niachie mimi”
“Okay,mimi sina tatizo”
Mzee Kajeme,akashusha pumzi kidogo na kumtizama kijana wake ambaye siku zote alikuwa akimtegemea,katika mawazo na ndiye aliyeamini hata asipokuwepo Duniani ataweza kuendeleza mali zake!
“Unamfahamu Florian Fredrick?”
Moyo wa Ahmed,ukapiga paa!Jina hilo lilimshtua,wakati mwingine alidhani amesikia vibaya, sababu haikuwezekana hata kigogo kwa baba yake kumfahamu mwanaume huyo, anayeitwa Florian Fredrick.
“Florian Fredrick?!”
Ahmed akajibu,haikujulikana kama anauliza swali ama ameshangaa!
“Ndio,Florian Fredrick”
“Ndio namfahamu”
“Upo naye vipi?”
“Nilisoma naye Makumira”
“Alimaliza Chuo?”
Mzee alizidi kufanya usaili,ilikuwa ni lazima akamilishe ripoti yake.
“Hapana”
“Kwanini?”
“Sijui,mimi nilimaliza kabla yake nadhani”
“Unamfahamu Hajrath Mpilla?”
Hapo ndipo Ahmed,akaishiwa nguvu na pozi kabisa.Akatizama chini na kumuangalia baba yake, ambaye hakumuelewa ni kwanini anamuuliza maswali hayo yasiyokuwa na mbele wala nyuma kwake.
“Ndio,pia nilisoma naye!Wote walikuwa mwaka wa pili”
“Sasa wote hawaonekani,mpaka leo.Ndio maana nakuhoji”
Akili ya Ahmed,ikasafiri kwa kasi ya umeme,akakumbuka mara ya kwanza anasafiri kwenda nchini Malaysia na kukutana na Florian ndani ya ndege,akakumbuka jinsi mwanaume huyo alivyomkana kama Petro!Licha ya kuwaza hayo yote lakini hakutaka kufungua mdomo wake na kuongea lolote, akiamini ya kwamba hakuna jambo linalo muhusu hata kidogo kwani biashara yake na Hajrath ilikuwa imekwisha kitambo sana!Baba yake akazidi kumchimba, akimuuliza maswali ya hapa na pale lakini Ahmed hakutaka kuonesha ushirikiano wa aina yoyote ile,akajifanya kama hajui lolote.
****
Kilichokuwa kinamsukuma ndicho alichotaka kifanyike,alitaka aanze kazi mara moja.Ndiyo maana kila kukicha alimsumbua Baba yake amuombee nafasi kwa marafiki zake,sababu aliamini kwenye kupata ajira ni lazima ujulikane,yaani ushikwe mkono na rafiki wa baba ama ndugu.Hilo halikuwa tatizo,Mzee Kajeme alijuana na wafanyabiashara wengi sana ndani na nje ya jiji.
Hapo ndipo, akapata wazo la kumtafuta Mr.Tumain Kibangala!Mzee mwenye kampuni ya usafirishaji na kiwanda cha kutengeneza vinywaji.Haikuwa kazi ngumu hata kidogo,jambo la Ahmed kupachikwa kama H.R likafanyika mara moja,akapewa ofisi na Mzee Kibangala kupitia mgongo wa Baba yake.
“Hii ndio ofisi yako,sitaki mchezo kabisa.Tambua kwamba upo hapa kikazi.Matter of fact, hujaanza kazi upo kwenye Probation tu, nadhani unajua maana yake”
Siku zote mzee huyo aliogopeka ofisini,alikuwa ndiye mkurugenzi lakini huonekana ofisini kwa nadra sana.Ofisi ilikuwa kimya,Ahmed alikuwa akipewa maelekezo.
“Aneth”
Boss,akaita.
“Abee boss”
“Utamuelekeza huyu kidogo,ni mfanyakazi mpya.Hakikisha anaelewa kila kitu”
“Sawa boss”
Aneth aliitikia huku akitetemeka,amesimama wima mikono nyuma.Alimuogopa tajiri yake kuliko kawaida,alikuwa ana kila sababu ya kumuogopa kwani tajiri huyo, hakutaka mchezo katika kazi.Kitendo cha kumfukuza mfanyakazi ilikuwa ni mara moja tu tena bila barua ikashema ‘Toka huna kazi’hiyo ndio basi.Alivyotoa maelekezo hayo mafupi akarudi ndani ya ofisi yake,akimuacha Ahmed anaelekezwa namna ya kufanya kazi!Kama alivyoambiwa ndivyo ilivyokuwa,Ahmed alikuwa bado yupo kwenye ‘Probation’sio muajiriwa kamili lakini yupo kwenye majaribio maalum,alifanya kazi kwa bidii na utiifu akizoea taratibu. Miezi minne baadaye,bila kuamini mezani kwake akakuta barua ya kuajiriwa rasmi.
“Ahsante Mungu”
Bado hakuamini,akaisoma vizuri na kuibusu akimshukuru Mungu wake!Mshahara ulikuwa mnono kuachilia mbali posho na malupu lupu, hiyo ni kutokana na kitengo alichopewa.Akatia sahihi yake na kuirudisha mapokezi.Kila mtu alifurahi,sio wazazi tu.Furaha yake ikahamia pia kwa Yusrath ambaye siku zote,alionekana kujivunia kuwa na mwanaume kama Ahmed.
“Baby,nakupenda sana!Nije lini kujitambulisha kwenu?Nataka tuwe official,sipendi tuwe tunajificha ficha kama wanafunzi”
Lilikuwa ni pendekezo la Ahmed, siku hiyo wakiwa kwenye mgahawa maarufu ulioitwa Marry Brown,Mlimani City wanakula chakula cha mchana.Pesa tena, halikuwa tatizo kwa Ahmed,kumaanisha kwamba matumizi yote yalikuwa juu yake.
“Tatizo una haraka kuliko upesi Darling”
“Lazima niwe na haraka,nisije kuporwa tonge mdomoni”
“Hauwezi,niamini.Muda ukifika nitakwambia”
“Lini lakini?”
“Huu mwaka,hauishi.Nyumbani watakujua,ngoja niweke mambo fulani sawa Ahmed,nakupenda sana.Hata mimi natamani iwe kesho”
“Ahsante sana,ahsante kwa kunipenda Yusrath”
Mapenzi yao,hayakuwa na mfano wa kuyafananisha.Watu wote waliwaangalia tena bila kuuliza, walijua kabisa watu hao wapo katika mahaba mazito!Kilichowafanya watu wawatamani ni baada ya Yusrath kuanza kumlisha Ahmed,sio siri yalikuwa mahaba niue.Walivyosimama hapo,wakaanza kutembea kutoka nje ambapo huko walitafuta taxi mpaka Ilala anapoishi Yusrath.
“Wiki ijayo baby,usisahau.Twende kwenye lile tamasha”
“Sawa Darling”
Baada ya kuagana,wakaona haitoshi wakapigana madenda!
*****
Ahmed aliendelea kuchapa kazi,akionesha utiifu kazini.Alimuheshimu kila mtu!Awe mzee ama kijana maskini kwa tajiri,aliongea kwa uchangamfu na muda wote alikuwa katika tabasamu pana.Hiyo ilifanya kila mfanyakazi ampende lakini wachache walimchukia bila sababu kama ilivyokuwa kawaida ya binadamu,huwezi kupendwa na watu wote.Alilijua hilo lakini aliweka masikio yake pamba.Wazazi wake walijivunia kuwa naye,wanawake wakaanza kujigonga hiyo ilitokana na kuanza kupendeza.Ahmed alijua kuvaa na kuzidi kuwa mtanashati,muda wote mkanda nje,tai shingoni!Wanawake walijigonga kwake lakini waliambulia patupu,hakuona kitu kipya kwao, aliendelea kumuonesha mapenzi kemkem Yusrath,akawa kata vilimi wanawake wanaomgasi na kumuwinda.
*****
Hakuna siku waliyokuwa wanaisubiri kama hiyo,siku ya Jumamosi.Kwa mara ya kwanza kutoka na Yusrath usiku,kwenda kuangalia tamasha la watu wenye vipaji.Kwa Yusrath ilikuwa vigumu kutoka lakini ilibidi apange mpango na binamu yake kwamba atalala kwao kumbe atakuwa na Ahmed, siku hiyo,hakukuwa na kipingamizi.Kila kitu kikaenda sawa,na siku hiyo wakakutana katika ukumbi maarufu jijini Dar es salaam,muda wote wakiwa wenye furaha.Wakanunua tiketi na kuzama ndani ambapo kulikuwa na watu wengi,wakatizama huku na kule ili kutafuta sehemu ya kukaa.
“Twende kule mwisho”
Yusrath,akasema huku akinyoosha kidole kwenye moja ya kona zilizokuwa nyuma kabisa,wakaanza kutembea!Watu waliwashangaa kila mtu aliushangaa uzuri wa Yusrath,alitingisha kwani siku hiyo hakuvaa ushungi,nywele zake za usinga aliziachia.Wakatembea mpaka siti ya mwisho!Wanaume waliokuwa pembeni,karibu yao walimtizama sana Yusrath,wengine bila ustaarabu walidiriki kumkonyeza, kitendo hiko kikashuhudiwa na Ahmed,akaonesha kuchukia kwa wivu lakini hakutaka kuonesha jambo hilo waziwazi.Waliendelea kunywa na kupiga stori.
“Baby weka simu pembeni”
Ahmed alimwambia Yusrath baada ya kumuona yupo bize anachat na simu muda mwingi.
“Sorry baby”
Wakaendelea na stori lakini hazikupita dakika mbili,Yusrath akashika tena simu na kuanza kuchat.Ahmed akabaki,anamtizama moyo ukamuuma ajabu.Kitendo hiko,hakikumpendeza hata kidogo.
“Baby”
“Oooh Ahmed,sorry naweka simu mezani”
“Unachat na nani?Anayekuweka bize?”
“My cousine,Yule niliyekwambia nimemwambia Mom,nitalala kwao”
“Aya”Ahmed,akaitikia kishingo upande!
Macho yao yote yalikuwa mbele simu ikawekwa chini,tamasha lilikuwa tayari limeanza.Dakika kumi baadaye Yusrath,akawa tena anachezea simu yake amejisahau,Ahmed akamkata jicho kali la hasira lililochanganyika na wivu.
“Baby,naenda nje mara moja.Kupokea simu!Nakuja sasa hivi”
Hakusubiri jibu kutoka Kwa Ahmed,alichofanya ni kusimama wima na kuanza kuomba njia ili atoke nje.Ahmed,akamtizama!Kuna kitu alianza kuhisi ambacho hakikuwa cha kawaida,hakutaka kubaki nyuma!Akasimama na kuanza kumfuata ilikuwa ni lazima ajuwe mpenzi wake anazungumza na nani usiku huo,mbaya zaidi ametoka nje kwanini asiongelee hapohapo?Akazidi kujiuliza maswali huku akiunganisha matukio ya kuchat kwa Yusrath kila wakati,taa nyekundu ikaanza kuwaka kichwani kwake kwamba ni lazima Yusrath ana mwanamme mwingine, hakutaka kupata picha kwa namna gani angeumia kama angekuta ni kweli,ndiyo maana hakukubali kubaki.Akatoka mpaka nje ya mlango,akatizama huku na kule bila kumuona,alivyoangalia kushoto kwa mbali,akamuona kwenye ukuta yupo mwenyewe simu ipo sikioni,hakuweza kusikia ni kitu gani anazungumza.Ikabidi asogee karibu kwa mwendo wa taratibu,maneno aliyosikia kutoka kwa Yusrath,yalifanya moyo wake uchome kama pasi.
“Sawaa,nitakupigia kesho my dear!Sasa hivi usiku,kesho nipigie.Sawa eeeh al….”
“Yusraaaath”
Ahmed,akaita akimkatisha kwa hasira huku akiyabana meno yake!Bado hakutaka kuamini!
“Unaongea na nani?”
“Baby,naongea na mte…”
“Unaongea na nani nakuuliza?”
Hakuwa tena Ahmed yule anayetabasamu,sura yake ilikuwa imejikunja.Anauliza kwa hasira!Hiyo ilimfanya Yusrath aanze kuogopa lakini hakutaka kulionesha swala hilo,akatabasamu kidogo.
“Baby bwaaana,nitakwambia twende”
Yusrath akasema huku akitabasamu na kuanza kutembea,ni bora asingefanya hivyo kwani jambo hilo lilimfanya Ahmed akasirike na kulitafsiri kama dharau,akaushika mkono wake na kumvuta.Kilichosikika hapo,kilikuwa ni kibao kikali cha shavu,Yusrath akaenda chini.Ahmed,akamvuta na kumtandika kibao kingine cha uso.
“Ulikuwa unaongea na nani nakuuliza?”
Tayari,Ahmed alikuwa amebadilika rangi ana hasira zilizochanganyika na wivu, anatetemeka, kuanzia mikono mpaka midomo,hiyo ilikuwa ni dalili mbaya sana!Yusrath aliachia ukelele mkali wa maumivu,hakukaa sawa,akapigwa kofi lingine kali na kudondoka chini, mzima mzima.
Maumivu aliyokuwa anahisi hayakuwa na mfano wake,kichwa chake kilimuuma kupindukia.Mashavu yake yanawaka moto,yupo chini analia kama mtoto mdogo!Ki ukweli Ahmed, alikuwa amemuumiza na kilichomuuma zaidi tangu azaliwe hakuwahi kupigwa makofi namna hiyo,hilo ndilo lilimfanya alie kwa kwikwi mpaka kamasi nyepesi zikawa zinamtoka puani kwake,yupo chini amejikunyata. Ahmed amesimama bado ana hasira.Sio siri Yusrath, aliumia kwa kiasi cha kutosha na jambo hilo kwake alilichukulia kama unyanyasi wa kijinsia,bado hakuamini kama Ahmed ndiye kamfanyia kitendo hicho cha kinyama.Ghafla akahisi kama amepata nguvu,akasimama akiwa bado analia machozi,akamsukuma Ahmed na kuanza kutembea akielekea asipopajua,hakuelewa kwa wakati huo ni kitu gani akifanye,hakuona vizuri mbele kutokana na machozi kumtanda machoni,akawa anaona kama ukungu fulani na giza mbele yake.
“Yusraaaath”
Ahmed akaita huku akimfuata kwa nyuma,alivyomshika mkono ukatupwa mbali.Yusrath asingeweza kuongea kwa wakati huo,hasira zilikuwa katika kiwango cha juu kabisa,anahema kwa nguvu,kifua chake kinapanda juu na kushuka.Wazo lililomjia ni moja tu,kutafuta usafiri mpaka nyumbani kwao.Japokuwa alielewa wazazi wake wangemuhoji, kulikoni mbona unalia? Lakini hilo, hakujali.
“Baa…jaj”
Bahati nzuri ikawa kwake kwani kitendo cha kutokeza langoni, akaona Bajaj inapita haina mtu,akaipungia mkono,ikasimama mbele yake mita chache tu.Kabla ya kuifikia Bajaj,Ahmed akawa tayari amefika na kumshika mkono!
“Yusrath,unaenda wapi?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Ahmed akimuangalia Yusrath,moyo wake ukahisi uchungu ajabu akahisi kujuta mno!Wakati mwingine tukio la kumpiga Yusrath akalichukulia ni kama pepo baya lililomvaa.Ndiyo maana akataka kujaribu kumuomba Yusrath msamahaa, japokuwa hakuwa ana uhakika kama jaribio hilo litafanikiwa kwa asilimia mia moja!Bajaji ilikuwa mbele yake,yupo tayari kupanda na kuondoka,kitendo cha Ahmed kumshika mkono kilimuuma zaidi,alivyotaka kumjibu akahisi kama kuna li-dudu kohoni limemkaba,akashindwa kuzungumza.Midomo yake ikawa inamcheza tu machozi yanambubujika kama maji,kitendo hiko kilishuhudiwa na mwendesha bajaj,ilibidi atoe kichwa chake nje ili aangalie ni kitu gani kinaendelea.
“Yusrath,please.Naomba nisamehee ni shetani tu”
Ahmed akaamua kumtupia lawama zote shetani.
“Nia..che Ahm..ed,niache niend..e zangu!Niachie,niachie nakwambia.Siwezi,siweziii kabisa!Ha..”
Hakumalizia tena sentensi yake,akaanza kumwaga machozi upya huku akitumia nguvu kujitoa mikononi mwa Ahmed.
“Dada unaenda au?”
Dereva,ilibidi ahoji. Kuendelea kubaki eneo hilo kungezidi kumpotezea abiria mbele ya safari,ndiyo maana akahoji ili ajue mstakabadhi mzima.
“Wewe nenda”
Ahmed,akajibu.
“Kaka,nisubiri”
Yusrath nayeye,akadakia huku akijikaza na kufuta machozi.
“Yusrath..”
“Ahmed,nimekwambia niache!Usinishike,niache niondoke zangu”
Mvutano ulipamba moto,Yusrath akatumia nguvu na kuingia ndani ya bajaj lakini Ahmed hakukubali,nayeye akaingia pia. Mzozo ukahamia ndani!
“Oyaa,kaka eeeeh.Mnazogoa mjue!Kama hamuendi pigeni chini,mnanichoresha hapa. Nataka kuwahi vichwa vingine”
Dereva wa bajaj,akasema kwa ghadhabu kwani walipoteza dakika ishirini nzima.Msimamo wa Yusrath ulikuwa palepale,Ahmed amuache kwani hakutaka tena kumuona!Bado hakutaka kuamini kimasihara amepigwa makofi namna ile wakati mwingine, alidhani Ahmed amemchoka ndiyo maana aliamua kumfanyia visa vya nanma hiyo,mawazo hayo yalimfanya Yusrath azidi kuchukia zaidi.Kilichofanyika ni Ahmed kushuka ndani ya Bajaj, baada ya kumuona Yusrath yupo katika msimamo uleule,kwa macho yake akashuhudia bajaj inaondoka kwa kasi,mpaka inapotelea machoni mwake hakuamini.
Ahmed,akahisi kujuta sana!Kwa kitendo alichokifanya,alijilaumu mwenyewe akashindwa kupata majibu ya harakaharaka, ya kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake na Yusrath ama atamsamehee hasira zake zikiisha,hilo ndilo swali aliloanza kujiuliza kuanzia hapo,akatoa simu yake na kuanza kumtafuta hewani lakini simu iliita bila kupokelewa,akajaribu tena na tena, bila mafanikio ya aina yoyote ile.
*********
“Mbona bado yupo hai?”
“Nani?”
“Yule binti”
“Binti gani?Ebu nyoosha maelezo Mzee”
“Yule,mliyemtupa mtoni”
“Wapo wengi”
“Wa mara ya mwisho kabisa”
“Subiri,usikate simu”
Yalikuwa ni mazungumzo ya simu,taarifa hiyo ilikuwa ya kutisha, endapo habari hiyo ingekuwa na ukweli ndani yake.Kitu walichoogopa katika maisha yao ni kuchafua c.v zao,ndiyo maana walifanya kazi kikamilifu ili wasishushe heshima.Taarifa hizo,zilimshtua sana Pelle, mwanaume aliyesuka mpango mzima wa kifo cha Hajrath, leo hii anaambiwa yupo hai,kitu hiko kwake alikifananisha na mazingaombwe, haikuwezekana hata kidogo risasi alizopigwa Hajrath akapona ni lazima zilikuwa ni uvumi tu.
“Una uhakika?”
Pelle akauliza kwa mara nyingine, baada ya kugundua kwamba msichana anayezungumziwa hapo ni Hajrath,ilikuwa ni hatari kubwa sana endapo tajiri yake Sporah Trevez,angepata fununu juu ya taarifa hizo,ndiyo maana aliogopa kwa kiasi cha kutosha.
“Nina uhakika”
“Wewe umejuaje?”
“Mimi naishi kijiji jirani,kutokana stori nilizopewa.Ndio huyo!”
“Hapana,subiri nije kuhakikisha”
Kwa mara nyingine Hajrath,aligundulika kwamba yupo hai.Baada ya kukipiga chenga kifo kwa kipindi kirefu,hiyo iliwatia hasira wazee hao wa kazi.Pelle, hakutaka kulaza damu,ilikuwa ni lazima siku hiyo awashe gari na kusafiri mpaka katikati ya kijiji hiko cha Nazareth, akajionee kwa macho yake,siku zote alijifananisha na Thomaso,lazima ashuhudie kitu na awe ana uhakika nacho, ndiyo maana usiku huohuo akawasha gari na kuondoka kimyakimya ili akaanze mpango wake,hakupata picha kamili kama siku moja Sporah Trevez,angezipata taarifa hizo za uzembe.
Ndiyo maana alifanya kazi hiyo kimya kimya tena kwa juhudi kubwa,bastola yake ilikuwa kiunoni,kumbukumbu zake zilimwambia kwamba. Bastola hiyo ina risasi kumi na nane.Akaamini hiyo ingekuwa msaidizi wake kwa chochote kile ambacho kingetokea mbeleni.Kutoka mjini alipokuwepo mpaka Nazareth ilimchukuwa masaa matatu na dakika kumi na mbili mpaka kukamilisha safari yake hiyo nzito kwa gari,alivyowasili kitendo cha kwanza ni kutoa bastola yake ili ahakikishe kama ni kweli ina risasi za kutosha,alivyojiridhisha akairudisha kiunoni na kuanza safari ya kuingia ndani ya kichaka hiko, ambapo alipewa taarifa ya kwamba Hajrath ndipo anatibiwa humo,haikumuingia akilini hata kidogo binadamu kupigwa risasi tisa mwilini na kuwa hai,wakati mwingine akadhani ni uwongo lakini aliamini jambo hilo ni kweli kwani Mzee Nteta, hakuwa ana sababu yoyote ya kumuongopea,giza lilikuwa jingi lakini kilichomsaidia ni mwanga hafifu wa mbalamwezi.Hiyo ilifanya aone mbele,akazidi kusonga mbele zaidi!Akatokeza nyuma ya kijumba kidogo chenye makuti kwa juu,hapo akatulia na kutizama huku na kule.
*****
Kitendo cha Hajrath kufumbua macho yake na kutizama huku na kule, ulikuwa ni kama muujiza mkubwa sana kutokea ingawa bado kumbukumbuku zake hazikukaa vizuri, zilikuwa zinarudi na kuondoka kama saa mbovu ya kichina.Watu aliowaona mbele yake,wamevaa vibwebwe ndio walifanya azidi kushangaa eneo alilokuwa,alivyojilazimisha kukumbuka ilishindikana na alivyojaribu kutaka kukaa akahisi maumivu makubwa sana sehemu za mbavu na mgongoni,hiyo ilimfanya ashindwe kuelewa maumivu hayo yanatokana na nini hasa.Picha mbalimbali za wanafunzi wenzake chuo cha Makumira zilianza kumjia,akamuona Amney na Mpangw’a sura ya Ahmed ilivyomjia akaanza kulia zaidi.
Taswira ya kwanza kumjia ni siku aliyokunywa sumu akitaka kujiua kisa Ahmed,hilo ndilo lilimfanya apate picha ya kwanini yupo hapo,kumbe haikuwa hivyo.Kumbukumbu zake hazikukaa vizuri,hakuelewa kwamba alipigwa risasi nyingi mwilini na yupo nchini Afrika kusini, sio Tanzania kama alivyodhani.Wanakijiji walizidi kuingia ndani na kumwangalia,wote walitabasamu na kujipongeza kwa jambo walilolifanya la kuokoa maisha yake,wengine walimshukuru Mungu!Lugha walizoongea binadamu hao,zilizidi kumvuruga akili yake kabisa.Akabaki,anawashangaa azungumzi kitu chochote kile,mmoja wa wanawake akatokeza akiwa na bakuli kubwa lililoviringishwa majani ya migomba kwa nje,akakaa naye na kuanza kumpa,lakini ilikuwa ngumu kwa Hajrath kufungua mdomo wake,ndani ya kibakuli hiko kulikuwa na maji meusi, yenye madonge madonge.Hiyo ikawa ngumu sana kwake kufungua kinywa,mbaya zaidi ilikuwa lugha gongana hawakuweza kuzungumza lugha moja!Kilichofanyika ni mmoja wa mwanaume kutumwa aende kijiji jirani akamuite Mzee Nteta,mzee anayezungumza lugha ya kiingereza.Haraka wakafanya hivyo,dakika ishirini baadaye Mzee Nteta akawa amefika na kuanza kumuhoji maswali mbalimbali.
“What is you are name?”(Jina lako nani)
“I don’t know,what happened?!What is wrong with me?i can’t remember anything”(Sijui,nini kimetokea?Nina tatizo gani?Sikumbuki kitu chochote)
“You have been shot”(Umepigwa risasi)
“Meee?No,who are you?No Ahmed,please go!I hate you,please leave me alone!But ilove you,why are you doing this to me?Ilove you”
Kuanzia hapo,memori kadi ya Hajrath inayokaa kichwani kwake ikawa kama imeingia vidudu hatari vya virusi,mara isome mafaili mara ikatae,ndiyo maana mafaili yakawa yanapandana mara azungumze kile mara hiki.
“Relax,relax take this!You are going to be fine,medicine”(Tulia,tulia.Chukua hii,utakuwa sawa.Ni dawa)
“I feel pain”(Ninahisi maumivu)
“Take this,you are going to be fine”(Chukuwa hii,utakuwa sawa)
Kila mtu alimshangaa mzee huyo akizungumza na Hajrath akitumia Lugha hiyo iliyopanda ndege,cha jabu kila mtu alimuuliza akitaka kujua mgonjwa huyo kazungumza kitu gani mpaka akakubali kunywa dawa,Mzee akasema nayeye akahoji kilichotokea,namna walivyomuokota mtoni!Kwa mara nyingine wakamwambia jinsi ilivyokuwa,kitu cha kwanza kumjia kichwani mzee huyo ni mwanaume anayeitwa Pelle kwani siku chache zilizopita, alimwambia juu ya kazi waliyopewa,kitendo cha kuhadithiwa tukio zima kilimfanya aunge unge matukio na kumtafuta Pelle hewani ili ampashe kila kitu kilichotokea.
Hapo ndipo mwanaume huyo hakutaka kukubali,akataka kuhakikisha habari hizo!Usiku wa siku hiyo alifanya kila njia ili amuone Hajrath,akachungulia huku na kule.Kuna kibanda kimoja,aliona kuna wanawake wanaingia na kutoka,akaamini kabisa huko ni lazima Hajrath atakuwa amehifadhiwa,akatembea kwa tahadhari mpaka nyuma kabisa na kusimama kwa nyuma,akatizama huku na kule akaingiza kidole katikati ya majani na kuweka jicho lake moja ndani,hakuamini macho yake baada ya kumuona Hajrath ndani ya kijumba hiko amelala.Hio ndio ilikuwa nafasi yake ya mwisho kufanya mauaji hayo,akachukuwa bastola yake na kuikoki taratibu sana,akaipitisha ndani ya kitundu kidogo ili amfyatue hajrath kichwani,amuue hapohapo kitandani.
*******
Ofisi kwa Ahmed,ilikuwa ni chungu!Hakuweza kufanya kazi kwa ufanisi kama siku zote,mtima wake uliuma ajabu!Kitendo alichomfanyia Yusrath cha kumzaba makofi, kilimfanya amuombe msamahaa kila kukicha bila mafanikio,meseji ndefu za kuomba radhi alizokuwa anatuma na kuandika hazikuweza kubadili kitu chochote kile,mbaya zaidi hazikujibiwa hata kidogo.Kitu kilichomfanya azidi kuumia ni meseji hizo kusomwa yaani zilionesha tiki ya rangi ya ‘blue’ kwenye mtandao wa watsApp, kumaanisha kwamba zinasomwa.
Kila siku Ahmed alikuwa ni mtu wa kuomba msamahaa,akakosa raha na furaha ya maisha!Kweli akaamini ule msemo ‘Usiombe kupenda na unayempenda ajue’hilo aliliamini na kujuta ni kwanini alimuonesha Yusrath anampenda na kafa kaoza,hakuna siku aliyowahi kuumia kama hiyo.Akajaribu kutumia simu ya mezani ofisini kwake ili kumtafuta Yusrath hewani,akainua mkonga na kumpigia Yusrath!Simu,ikapokelewa,moyo wake ukapiga sambasoti kwa furaha,akapata kitete.
“Halloo Yusrath,mimi Ahmed tafadh….titititi”
Kitendo cha kujitambulisha,simu yake ikakatwa bila ya kumaliza mazungumzo yake,hiyo ndiyo ikamuuma zaidi na zaidi.Akainamisha kichwa chake chini na kuegemea meza.Alivyoingia mfanyakazi mwenzake aliyeitwa Anneth na kumkuta katika hali hiyo,ilibidi amdadisi kidogo kwani hakuwahi kumuona Ahmed akiwa hana furaha tangu aanze kumfahamu,Ahmed alionekana kama mtu mwenye mawazo tangu siku tatu nyuma zilizopita,hiyo ilimfanya siku hiyo Anneth!Ashindwe kuvumilia.
“Ahmed,unaumwa au?”
Anneth akauliza huku akimshika Ahmed mgongoni,Ahmed akainua kichwa chake na kumuangalia machoni,hiyo ilimfanya Anneth aogope!Macho ya Ahmed yalikuwa mekundu kwa kiasi cha kutosha,picha hiyo ilitosha kabisa kumwambia Anneth kwamba Ahmed ana matatizo makubwa.
“Ahmed,una nini?”
“Niko okay,usijali”
“No,sio kweli.Nambie nitakusaidia hata kwa mawazo”
Ahmed,akamtizama mwanamke huyo mwenye rangi asilia ya ‘chocolate’ mrefu kwenda hewani,anauliza kwa huruma.
“Niko sawa,Anneth ni uchovu tu.Niletee yale mafaili nisaini”
Hapo Anneth,hakuwa na kipingamizi.Akajiongeza na kuelewa kwamba Ahmed hakutaka kuhojiwa maswali mengine zaidi,akaanza kutembea kuelekea mlangoni.
“Anneth”
Ahmed,akaita!Anneth akasimama na kugeuka nyuma.Hiyo, ilimfanya Ahmed ashushe pumzi ndefu na kumuita,akae kitini.Akaanza kumuhadithia kila kitu kilichotokea na jambo lililomfanya mpaka awe katika hali kama hiyo,hakuacha kitu chochote nyuma, akamuelezea namna alivyompiga makofi Yusrath.Anneth,alionesha masikitiko makubwa sana!
“Pole sana!Kusema ukweli,mimi nikipigwa na mwanamme.Boyfriend wangu,huo ndio mwisho wake namuacha hapohapo,samahani kwa kukwambia haya.Anyway bado unampenda?”
“Ndio nampenda,nifanye nini?Nisha mess up,niambie cha kufanya”
“Umesema simu zako,hataki kupokea?”
“Ndio”
“Ebu nipe namba zake”
Ahmed,hakuwa na tatizo lolote lile!Akaanza kutaja namba za Yusrath,hapohapo Anneth akazipiga na kuweka loudspika, kumaansiha kitendo cha Yusrath kupokea simu,wangesikia wote!
“Hallooo”
Upande wa pili wa simu ukasikika sauti ikaenea ofisi nzima,Yusrath akawa kwenye laini moyo wa Ahmed ukapiga paaa!
“Mambo Yusrath”
“Safi za kwako?Naongea na nani?”
“Mimi naitwa Anneth”
“Anneth yupi?”
“Upo free hapo?Nahitaji tuzungumze”
“Sema tu,nakusikia”
“Kama nilivyokwambia naitwa Anneth ni dada yake na Ahmed,nilikuwa naomba tuongee vizuri.Una muda siku gani?”
Kuanzia hapo,ukimya ukatawala kidogo!Yusrath hakuongea lolote simuni.
“Halloo,Yusrath!Umenisikia?”
Mapigo ya moyo ya Ahmed,kuanzia hapo yakaanza kudundia mgongoni!
Majeraha aliyopata Yusrath moyoni hayakuwa na mfano wake,mtima wake uliuma ajabu!Kitendo cha kinyama cha kupigwa makofi na Ahmed,kilimfanya akumbuke vitu vingi sana nyuma!Kwake yeye, kitendo cha kupigwa vibao alikitafsiri kama dharau na kufikiria moja kwa moja tu kwamba Ahmed, amemchoka tayari.Kwanini asingeniuliza kistaarabu?Kwanini anipige?Hayo ndiyo maswali yaliyokuwa yanapita kichwani mwa Yusrath huku akilia machozi ndani ya bajaj,taswira ya kupigwa makofi ikazidi kujijenga ndani ya kichwa chake,akajiona alivyokuwa chini watu wanapita na kumshangaa.
Mapenzi kwake tayari yalibadilika badala ya kuwa tamu yakawa shubiri,ndani ya bajaji aliendelea kulia kwa kwikwi bila kunyamaza,hiyo ilimfanya muendesha bajaji,ageuze shingo yake nyuma ili kumuangalia abiria wake vizuri.Akamuona binti mrembo,anajifuta machozi akitumia kiganja chake!
“Watoto wazuri kwanini wanateswa namna hii?”
Dereva wa bajaji,akajisemesha kimoyomoyo,msichana aliyempakia ndani ya bajaj,alikuwa mrembo kwelikweli,pengine katika maisha yake tangu aanze kazi hiyo ya kuendesha bajaj, hakuwahi kumpakia msichana mrembo kama Yusrath,ndiyo maana alihisi uchungu wa ajabu.Picha nzima alianza kulihisi sababu kabla ya kumpakia alimuona akiwa na mwanaume wanabishana na kuzozana.
“Dada ulisema unaelekea wapi?”
Dereva wa bajaj akauliza,niya na madhumuni yake ikiwa ni kuanza mazungumzo na kumzoea,akijaribu bahati ya mtende!Kifupi alitaka kujaribu kuokota mpera, chini ya mti wa mwembe!
“Il..la”
Yusrath akajibu kwa kwiki.
“Ilala,sehemu gani?”
“Shauri Moyo”
“Poa”
Ukimya ukatokea kidogo,dereva huyo ambaye alijitambulisha kwa Jina la Hamisi Makuka,akaanza kumuuliza maswali ya hapa na pale Yusrath lakini hayakujibiwa, Yusrath hakujibu kitu chochote kile,ilikuwa ni kama Dereva huyo anamchochea aendelee kulia.Kitu kilichomchanganya Yusrath ni jambo gani angewaeleza wazazi wake,ndiyo maana walivyokaribia kufika akajikaza na kuanza kujifuta machozi ili asiulizwe maswali mengine,alielewa ni namna gani baba yake angemkandika maswali kwani aliaga anaenda kushinda kwa binamu yake,iweje arejee usiku tena akiwa analia machozi.Bajaj,ilivyofika Amana,Yusrath akatoa kitambaa na kujifuta machozi, akatulia kidogo na kujiweka vizuri,bajaj ilikuwa inakaribia kufika mtaa anaoishi.Ilivyofika Ilala Boma,akakohoa kidogo ili kutoa sauti ya kwikwi.Moyoni bado, alihisi uchungu wa kufa mtu,akaapia hatokuja kumsamehee Ahmed katika maisha yake yote,hiyo ilimaanisha mkataba wa mapenzi yao tayari aliuvunja.
“Kaka,hapo kwenye geti jeusi”
Yusrath akasema huku akionesha kidole,bajaji ikasimama.Yusrath akashuka na kumlipa dereva ujira wake,akatembea mpaka getini na kugonga kengele!Alitetemeka na kuanza kutafakari ni kitu gani angejibu kwa wazazi wake,akahisi uchungu mwingine.Jicho lake moja,likadondosha chozi,akajifuta hakuwa ana uhakika kama angeingia ndani bila kushtukiwa kwani alielewa fika ni namna gani machozi yake yalivyo karibu.Sekunde saba baadaye,akasikia mtu anafungua geti.Huyo alikuwa mlinzi wao wa getini,kijana mdogo ambaye pia alikuwa ana saidia kazi za hapo nyumbani.Kama kumwagilia bustani,kufagia na kuhakikisha magari ya Mzee Suleiman masafi muda wote!Ingawa alikuwa ni mfanyakazi lakini walizoeana na Yusrath kwani waliishi kama mtu na kaka yake.
“Baba yupo?”
Lilikuwa ni swali la kwanza kutoka kwa Yusrtah kuliuliza.Alimuhofia baba yake,mzee huyo alikuwa ni mtata kwa binti yake,ndiyo maana alitupa kwanza swali hilo!
“Yupo seblen”
Hapo Yusrath alishusha pumzi ndefu ya ndani kwa ndani,akahisi kama tumbo linamuuma.
“Okay”
Akaanza kutembea huku akitafakari kichwani ni majibu gani ayatoe kwa baba yake,alivyofika na kufungua mlango,aliwakuta wametanda kwenye makochi.Akawasalimia bila kuwaangalia,hapo ndipo Mama akamsimamisha.
“Yusrath”
“Abee Mama”
“Uko sawa?”
Mama akauliza.
“Ndio,nipo sawa”
Kitendo cha kujibu huku anatembea kilimfanya Mzee Suleiman!Amtizame binti yake kwani hakumzoea akiwa katika hali kama hiyo.
“Njoo”
Ni neno moja tu,lililomfanya Yusrath ahisi kama mkojo unataka kumpenya,hakuelewa ni kitu gani akifanye.
“Yusrath,sogea hapa”
Kwa mwendo wa taratibu Yusrath akasogea mpaka katikati ya Seble,akawa anaangalia chini Baba yake, akamtizama vizuri kuanzia juu mpaka chini.
“Usoni umefanya nini?Na kwanini umerudi sasa hivi?Uliniambia utalala kwa Saida,imekuaje?”
Yalikuwa ni maswali ya mfululizo,kutoka kwa baba yake,amekunja sura baada ya kuona shavu moja la Yusrath limevulia damu tena jekundu, hapo ilibidi Mama aangalie kwa umakini,nayeye akashangazwa.
“Yusrath,umefanya nini?”
Mama akaibua swali.Hapo Yusrath, akashindwa kuzuia hisia zake,akaanza kulia upya tena kwa kwikwi, hiyo ilimfanya Mzee Suleiman apatwe na mashaka kidogo.
“Yusrath,una nini?”
Lilikuwa ni swali lililomfanya Yusrath azidi kutafakari ni jibu gani alitoe,kuwaambia ukweli wazazi wake kungeleta shida mno pengine Ahmed angeenda jela, hakuwa tayari kuwaambia kwamba amepigwa na mwanaume,alielewa ni kwa namna gani wangemchukulia.Hakutaka kuonekana malaya mbele ya wazazi wake ambao siku zote walimuheshimu na walipewa sifa zake mitaani na hata sehemu zote zile,hiyo ilimfanya awe katika wakati mgumu kuliko kawaida.
Akiwa analia machozi huku amesimama akaendelea kuusumbua ubongo wake,katika maisha yake hakuwahi kudanganya, ndiyo maana alishindwa kutoa jibu la papo kwa hapo.Ghafla akapata wazo ambalo hakuelewa limekujaje.
“Nilivamiwa njiani Ba..ba”
Yusrath,akazungumza kwa kwikwi,hakuelewa kama uongo wake ungefua dafu ama ungegonga mwamba!Hapo wazazi wake walikaa makini ili kumsikiliza ilivyokuwa,hofu yao ilikuwa ni kubakwa kwa mtoto wao lakini katika mazungumzo ya Yusrath, hakuligusia hilo,akasema kwamba alivyokuwa anakwenda kwa binamu yake njiani alikabwa na kupigwa makofi lakini bahati nzuri wasamalia wema walitokea na kumsaidia.Alizungumza huku akimwaga machozi,hiyo ikafanya wazazi wake wampe pole nyingi.
“Hawaja kuumiza?”
Mama akauliza kwa uchungu,hakuelewa kama binti yake alizabwa makofi kisa mapenzi na hapo aliwapiga, changa la macho!
“Ha..pana Mama”
Wazazi wake,wakaelewa somo.Wakamruhusu akapumzike,kitendo cha kufika alitoa simu yake na kukuta ‘missed calls’ ishirini na tisa kutoka kwa Ahmed,meseji zisizo na idadi kamili.Akazidi kulia machozi,sio siri katika maisha yake hakuwahi kudhani kama atakuja kupigwa na mwanaume,alikuwa akisikia tu kwenye hadithi za kutungwa na kuona sinema za bongo movie lakini leo hii alipigwa yeye makofi na mwanaume anayempenda kutoka ndani ya moyo wake,hakuwa ana uhakika kama angemsamehee ingawa hakuelewa kama hizo ni hasira na zikipoa atamsamehee Ahmed ili warudiane.
Kwa wakati huo hakutaka kuona simu ya Ahmed wala kusikia sauti yake kwa ujumla,kifupi alimtia hasira, akatamani amtumie meseji za matusi amtukane na kumwambia mapenzi yao tayari yamekwisha,ale hamsini zake!Lakini moyo wake,ukashindwa kuchukua maamuzi hayo magumu,akahisi bado anampenda!Licha ya yote hayo hakuacha kumuomba Mungu,amsahaulishe. Hiyo ikafanya asishike tena simu muda wote, akawa bize na mambo yake ili tu,amsahau Ahmed na amtoe kabisa katika moyo wake,zoezi hilo lilionekana kuwa gumu sababu usiku alikosa usingizi kabisa,chakula alikula kwa mbinde na kujilazimisha!Alimzoea sana Ahmed,mazungumzo ya usiku wakicheka wote na kutaniana, hakuamini kama ingebaki historia!Jambo hilo hakutaka kuliacha hivi hivi,siku moja ilibidi ampigie rafiki yake ili amuombe ushauri,akamuelezea kila kitu.
“Sasa hapo nikupe ushauri gani?Kwanza akupige,kakuoa?!Wewe ni mke wake?Acha ujinga Yusrath,wanaume wapo kibao!Achana naye,kwani naniliu yake ya dhahabu mpaka umgande,achana naye!Wewe bado mdogo,mzuri tena unalipa”
Ushauri huo aliupata kwa rafiki yake,anayeitwa Tausi hiyo ikampa nguvu,akaapia hatomrudia tena Ahmed,hakutaka kuishia hapo akamtafuta rafiki yake mwingine Husna Uchuro,huyo alionekana kumshauri vitu vingine tofauti.
“Msamehee,kama unampenda kwanini ujiumize?Msamehee maisha yaendelee!Wanaume ni wachache siku hizi,tulia na huyohuyo mmoja!Mtoto wa kike kubadilisha mabwana,haileti picha nzuri Yusrath”
Siku hiyo akawa njia panda,hakuweza kutofautisha tui la nazi na maziwa!Hakuelewa amsikilize nani kati ya marafiki zake hao wawili.
Siku moja akiwa nyumbani kwao,simu yake ikaita namba ilikuwa ngeni,alivyopokea na kusikia ni Ahmed,akakata simu hapohapo!Asingeweza kujibu kitu chochote,kitendo hiko kilimuumiza lakini hakujua afanye nini,akaenda chumbani na kuanza kulia,alihisi kumpenda Ahmed lakini moyo wake ulikuwa mzito kumsamehee,akatamani kumpigia simu wazungumze lakini hakutaka kufanya hivyo,picha na taswira wakiwa kitandani wanafanya ngono,ilimjia akahisi moyo wake unachoma kama pasi ya mkaa!Akabaki analia machozi ya kwikwi,meseji za Ahmed aliziona lakini hakutaka kuzijibu, bado alikuwa na mtimanyongo,hasira bado alikuwa nazo!Siku zikasogea,wanaume wakazidi kumgasi na kumtongoza kila kukicha hata hivyo hakutingishika,Yusrath hata siku moja katika maisha yake hakuwahi kufanya vitu kwa visasi,kisa Ahmed kampiga ama amemkera ndio atembee na mwanaume mwingine,kwake yeye ilikuwa tofauti na wanawake wengine.
Japokuwa Ahmed,alimtenda vibaya lakini hakuwa tayari kuyumbishwa.Siku hiyo akiwa katika mawazo tele,simu yake ya mkononi ikaita.Alivyotoa ilikuwa ni namba ngeni,akaipokea na kuiweka sikioni.Mwanamke aliyejitambulisha, alifanya moyo wake udunde kwa kasi,akataka kukata simu lakini nafsi nyingine ikamwambia asifanye hivyo.
“Nikusaidie nini?”
Yusrath akajibu kwa swali,baada ya mwanamke huyo kujitambulisha ni dada yake na Ahmed.
“Nahitaji kuzungumza nawewe”
“Nakusikiliza,sema tu”
“Sio hapa,tunaweza kuonana?”
“Siwezi,niambie kwenye simu”
“Yusrath,upo wapi?”
“Kariakoo”
“Mimi nipo Posta,naweza nikaja.Niambie ni Karikoo sehemu gani”
Hapo ukimya ukatawala kidogo!
“Halloo”
“Nipo mtaa wa Muheza”
“Sawa,nikifika hapo nakupigia simu”
Kama kungekuwa na kipimo cha kupimia mapigo ya moyo, siku hiyo yangeonesha moyo wake unadunda mara mia moja kwa sekunde,alihisi uti wake wa mgongo umepigwa na ubaridi, mwanaume huyu Ahmed bado hakuamini kama Yusrath,angekubali kuzungumza ,akabaki anamtizama Anneth Kasera,akashindwa ni shukrani gani azitoe kwake!
“Sikia sasa Ahmed,acha kuzubaa usiwe kama zoba.Una shilingi ngapi hapo?”
Aneth Kasera akauliza.
“Hapa mfukoni?”
Ahmed akajibu kwa swali kana kwamba hakusikia vizuri.
“Ndio”
“Elfu hamsini,tigo pesa nina elfu sabini”
“Nyingi sana,hiyo elfu hamsini itatosha”
“Yanini? Unataka kufanya nini?”
“Nataka hapa tupite maduka ya zawadi,tunamnunulia zawadi yule mtoto na kadi nyingi za I’m sorry,anapenda vitu gani?”
“Nguo nguo na mapochi”
“Tutanunua”
“Sasa kazini hapa?”
“Nitaongea na Satara,ata cover kwa boss,tutumie hii chance.Huyu mtoto utamkosa,jiandae tuondoke fanya fasta”
“Aneth...”
Ahmed akaita huku akitabasamu bado hakuelewa ni kwa namna gani amshukuru Anneth,mwanamke aliyejitoa muhanga kwa ajili yake!
“Ahmed,inabidi uanze kutoka mimi nifuate.Si unajua ofisi hii walivyokuwa wambeya,hawakawii kusema tunaenda gesti. Utanisubiri pale Benjamin Mkapa”
“Poa,ahsante sana”
Ahmed,akaweka tai yake vizuri shingoni akasimama na kuvuta kiti cha matairi nyuma,akatoka ofisini kwake mpaka nje kabisa ya jengo hilo,huko alivuka barabara upande wa pili akimsubiri nje ya jengo kubwa la Benjamin Mkapa,bado hakutaka kuamini kama siku hiyo anaenda kukutana na Yusrath,licha ya yote hakuwa mwenye uhakika kama angesamehewa!
Dakika moja baadaye,Anneth akawa ametokeza, wakatafuta bajaj mpaka Kariakoo ambapo huko walizama ndani ya maduka ya nguo,wakaanza kununua zawadi kem kem kama viatu,mapochi,kadi za kuomba msamaha,marashi na vitu vingine vingi.
“Ahmed,ukifika pale jifanye kweli unamaanisha kuomba msamahaa.Kama unaweza lia kabisa,sisi watoto wa kike,asikwambie mtu!Tunapenda kubembelezwa achaa”
Anneth akawa anatoa mbinu huku akiwa na mfuko mkubwa uliojaa zawadi kedekede akamkabidhi Ahmed,wakatembea mpaka mtaa wa Muheza,hapo akachukuwa simu na kumtafuta Yusrath hewani.
“Njoo na huo mtaa moja kwa moja,kushoto kwako kuna Restaurant!Nipo hapo ndani”
“Sasa nitakufahamu vipi?”
“Nimevaa,gauni ya kijani.Mtandio wa Pink”
“Okay!”
Simu ilivyokatwa,akamgeukia Ahmed.
“Sasa mimi naanza kwenda,wewe utafuata baada ya dakika moja”
“Sawa,kwahiyo nikusubiri hapa?”
“Unisubiri vipi hapa Ahmed?Unaniangusha!Njoo nyuma nyuma kama FBI ama CIA wa kimarekani,nikikaa tu.Hesabu dakika moja,nawewe njoo pale simama mbele yangu!Ikiwezekana piga hata magoti potelea mbali,we si unataka mtoto arudi kwenye himaya yako,usiogope”
Aneth alitoa mbinu nyingi siku hiyo,ikamfanya Ahmed apigwe na bumbuazi la waziwazi,wakaanza kutembea.
Walivyowasili nje ya mgahawa, Anneth akawa wa kwanza kuingia Ahmed akasubiri,ilivyopita dakika moja,akaingia nayeye ndani.Kona ya mwisho akamuona Yusrath amekaa na Anneth,akatembea mpaka kwenye meza yao!
“Yusrath…..”
Ahmed na mifuko yake ya zawadi mkononi,akaita huku akimtizama Yusrath usoni.
“Nakupenda sana,naomba unisamehee”
Kwa hali ya kushangaza na kuwafanya watu waangalie,ni baada ya Ahmed kwenda chini na magoti,akatembea mpaka kwa Yusrath akitumia magoti na kumshika miguu.
“NAKUPENDA YUSRATH,naomba unisamehee Mpenzi wangu,bila wewe siwezi”
Ahmed,alizungumza akiwa amepiga magoti.Waliokuwa pembeni wanakula walidhani wenda watu hao wapo kwa ajili ya maigizo,lakini cha ajabu hakukuwa na kamera kumaanisha kwamba tukio hilo lilikuwa mubashara,Ahmed alikuwa akiomba msamahaa kweli.
Yusrath,alipigwa na butwaa! Moyo wake ulimuenda mbio,akahisi uchungu ajabu.Katika maisha yake,hakuwahi kupigiwa magoti!Macho yake,yakaanza kubadilika rangi taratibu machozi yakaanza kumtoka bila kutarajia,akatoa kitambaa na kuanza kujifuta!Akasimama wima na kumuinua Ahmed, wakakumbatiana bila aibu yoyote ile.
“NIMEKUSAMEHEE AHMED,NAKUPENDA SANA”
Anneth Kasera,aliyekuwa pembeni amekaa!Akapiga makofi kwa furaha isiyo kifani.
Haukuwa utani hata kidogo wala maigizo ya bongo movie,ndege hawa wawili walipendana kuliko kawaida, ndiyo maana siku hiyo walibaki wamekumbatiana huku wakilia kwa furaha,wateja waliopo ndani ya mgahawa huo, waliwakodolea macho na wengine waliwabeza.Lakini kwao hawakujali,waliweka masikio yao pamba,kwakuwa Ahmed alitoroka ofisini ilibidi apeleke mambo harakaharaka,akakabidhi mifuko ya zawadi alizonunua,hiyo ikazidi kuongeza furaha zaidi na zaidi.Yusrath alitabasamu akashukuru na tayari akawa amesahau yote yaliyopita nyuma,akakubali wagange yajayo!
“Huku kuna nini baby?”
Yusrath akauliza,alishindwa kuvumilia akataka kufungua hapohapo lakini Ahmed,akamzuia.
“Usifungue hapa,ukifika nyumbani! Ndege wako manati ya nini sasa?”
“Ina maana mpaka jioni baby?”
“Ndio love”
“Mmmh,nitaweza kweli?”
“Utaweza tu”
“Nitajitahidi”
“Wacha niwahi ofisini,nimetoroka kidogo!Huyu anaitwa Aneth Kasera,nipo naye pale ofisini.Kifupi ni dada yangu”
Ahmed,akatoa utambulisho mfupi kwa Aneth.
“Nashukuru kukufahamu,Aneth!Mlinde huyo Ahmed,nitamtoa mtu rohoo”
Yusrath akatania kidogo lakini kimoyomoyo akiwa ana maanisha, kile anachokisema.
“Usijali My wiiii,huyu hatoki popote.Ananijua mimi vizuri.Wacha sisi tuwahi”
Ahmed,alitamani kubaki na Yusrath siku hiyo lakini haikuwezakana, ilikuwa ni lazima akateteee ugali wake,wakaagana na kuondoka, moyoni akiwa mwenye furaha kuliko kawaida,alimshukuru sana Aneth Kasera,hiyo aliona haitoshi! Akatoa noti mbili za shilingi elfu kumi na kumkabidhi.
“Shika hii Aneth”
“Ya nini?”
“Utaweka tu mfukoni”
“Usijali Ahmed”
“Hapana nakuomba,kamata tu.Utakunywa maji”
Kila kitu kilikuwa sawa,kama walivyotoka ofisini ndivyo walivyoingia.Kila mtu aliingia kivyake kwa staili yake!Moyo wa Ahmed,ulikuwa mweupe sio masihara,muda wote alitabasamu na kumuwaza Yusrath, akaona haitoshi akachukua simu yake na kumtafuta hewani ili wazungumze mawili matatu,hilo halikuwa tatizo!
Walizungumza mambo mengi hususani mikakati yao katika maisha ya mapenzi,wakaenda mbali zaidi na kupanga jinsi watakavyoishi nyumba moja na kushea chumba kimoja kama mme na Mke!
“I can’t wait,under one roof”
Yusrath,akasema kwa kudeka!Akavuta picha watakavyoishi ndani ya nyumba moja,kupika kupakua mpaka maisha yao yote!
“Nitakuja kwenu kujitambulisha so soon”
“Lakini bado nasoma Ahmed”
“Utasoma ukiwa kwangu,kwani vibaya?”
“Sio vibaya,mapema mno!Isitoshe hatujajuana vizuri”
“Naelewa hilo lakini nakupenda sana”
“Hata mimi love”
“Nahitaji kukuoa”
“Hata mimi nahitaji kuolewa nawewe, leo kesho”
Haukuwa utani,mipango yao ilikuwa kabambe!Kila mtu alimpenda mwenzake kutoka ndani ya mtima wake,hakukuwa na mtu yoyote kati yao mwenye punje ya masihara hata kidogo!Mbali na hapo,hakukuwa na yoyote aliyeficha siri juu ya mwenzake,hiyo iliwafanya wapendane kama watoto mapacha.Wanaume waliokuwa wanamsumbua Yusrath, wote waliishia kupewa vibuti wengine walichongewa kwa Ahmed.
“Kaka,kuwa mwelewa!Achana na Yusrath,si ameshakwambia ana mtu wake!Kausha basi”
Siku hiyo Ahmed,alikuwa simuni anazungumza na mwanamme mbishi, asiyeelewa somo aliyeitwa Utali Savimbi,mwanaume huyo alimsumbua Yusrath kwa takribani miezi miwili bila kukata tamaa.
“Kwani wewe unaongea kama nani?”
Utali Savimbi nayeye akajibu kwa swali,wivu ulimkaba kohoni hakutaka kumkosa Yusrath!
“Mume wake”
“Mume wake bongo,sasa sikia broo!Kama huyo mkeo hutaki atongozwe,mfungie ndani!Mimi nampenda”
“Usitake matatizo,achana naye”
“Aaah,kwahiyo unanipiga mkwara sio?Sasa subiri,mkeo namgonga labda asitoke nje,jua akitoka nje wetu sote”
Ulikuwa ni mvutano mkubwa kuliko kawaida,mwanaume aliyekuwa anazungumza na Ahmed alikuwa ni mkorofi kuliko kawaida,hakutaka kuelewa somo!Hiyo ilimfanya Ahmed akate simu na kumpandia Yusrath hewani,akamwambia kila kitu kilichotokea!
“Baby,usiwe unatoa namba zako hovyo!”
“Mimi sijampa honey,kapewa na rafiki yangu.Huyo kaka mimi simjui kusema ukweli,lakini anadai ananijua.Au baby,nibadili namba?”
“Badili namba mke wangu”
Siku zote Yusrath,alimchukulia Ahmed kama mme wake halali wa ndoa, ndiyo maana alimsikiliza kwa kila kitu,kitendo cha kuambiwa abadili namba, kilimfanya achukuwe uamuzi huo bila kuchelewa,siku hiyohiyo!Akatafuta namba nyingine mpya na mtu wa kwanza kumpigia, alikuwa ni Ahmed wake.
Mbali na kuwa na elimu ya darasani kichwani, lakini hata kwenye sekta nzima ya mapenzi alikuwa mwerevu,alielewa nini maana ya mahusiano!
*****
Alikuwa ni mtoto wa mfanyabiashara mkubwa sana,ndani na nje ya Tanzania na Afrika kwa Ujumla!Mbali na hapo bahati ilikuwa kwake sababu alizaliwa mtoto wa kiume peke yake,hiyo ilimaanisha urithi wa baba yake ni wake.Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwani George, alivyomaliza masomo yake chuo kikuu nchini Marekani na kurejea nchini Tanzania, akakabidhiwa mali zote aziendeshe na baba yake,jina lake likavuma kupita kiasi,alikuwa ni mwanaume makini kupita kiasi chake!Alikuwa ni mdogo wa umri lakini mwenye akili nyingi, wengi walisema ni kwasababu alisoma nchini Marekani, ndiyo maana aliweza kuendesha mali za baba yake vizuri na kuziendeleza,George Charles akili zake siku zote zilichaji na kufanya kazi kwa kasi!Kazi yake ilikuwa ni kucheza na mikopo benki,huko aliamini angeweza kutanua mali.Ndani ya mwaka mmoja,akafungua kiwanda kingine cha vitenge na mabati,hakutaka kuishia hapo!Akaagiza malori makubwa hamsini ambayo yalikuwa yakisafiri nchi jirani kama Kenya,Uganda na Burundi.
Kwake yalikuwa ni mafanikio makubwa sana.Wanawake walijigonga sana kwake lakini hawakuambulia kitu,wakatumia kila njia kuonana naye na kumuwinda lakini wapi!Wote walitoswa,mbali na hapo mwanaume huyo hakuwa mtu wa kujivuna na kujitapa wala kuringa,hakutaka kutembea na walinzi ama na msafara wowote ule kama matajiri wengine wanavyofanya,kilichowashangaza watu ni aina ya gari alilokuwa anatumia.Gari lake lililokuwa ndogo aina ya Mazda.Kwa mtu asiyemjua angemdharau na kumuona mtu wa kawaida lakini akaunti zake zote zilisoma mabilioni ya pesa!Alivyofikisha umri wa miaka thelathini,baba yake akamjia juu na kumtaka aoe!
“Dad, i can't! Bado muda,nikipata mwanamke!Nitamleta nyumbani, nitamuoa”
Siku hiyo George alikuwa ndani ya jumba kubwa la kifahari la baba yake mzazi,maeneo ya Oysterbay.
“Umri unaenda lakini!Basi tafuta mtoto hata mmoja tuna mali nyingi sana,unataka zipotee?”
“Mwanamke nitakayezaa naye,ndio nitakaye muoa Dad.Just wait and relax”
Mbali na kuwa na pesa lakini alikuwa mzuri pia wa muonekano,urefu wake ulimkaa vizuri.Hakuwa mnene sana,mwili wake ulikuwa wa wastani,mbali na baba yake kumpigia kelele na kumsihii aoe lakini bado hakuona mwanamke wa kumuoa,siku zote aliamini kwamba wanawake wa kibongo wapo kimaslai tu na wangempendea pesa zake!Hilo hakutaka litokee,ndiyo maana akavuta subira.Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya George Charles, Duniani!
*****
“Perfume hiyo,Gucci!How much?”
“Laki tatu”
“Na bodyspray yake, unayo?”
“Zimeniishia lakini subiri,nikuangalizie hapo kwa jirani”
Wateja walikuwa wengi ndani ya duka hilo la vipodozi na marashi,siku hiyo George Charles aliamua kwenda mjini Kariakoo kuzunguka akitafuta manukato mazuri yatakayomfaa,alikuwa amevaa kawaida tu.Shati ya mikono mifupi na Jeans,chini alivaa raba!Ungemuona usingedhani huyo ni mtoto wa bilionea Charles,kilichowafanya watu wasimgundue ni miwani kubwa ya jua aliyovaa!Siku hiyo hakuwa katika hali ya kawaida,moyo wake ulipiga kwa nguvu baada ya kumuona msichana huyo anahudumia dukani, akiwa katika tabasamu mwanana,alimtizama akashusha miwani kidogo na kumkagua kuanzia juu mpaka chini,kilichomvutia zaidi ni namna msichana huyo alivyosimama,nyuma alifungasha kidogo,akawa amebinuka kiaina!Japokuwa alivaa gauni kubwa lakini umbo lake lilitokeza,akamsindikiza kwa macho mpaka alivyoishia kwenye duka lingine,alivyorejea baada ya sekunde mbili, akawa amebeba mfuko mweusi.
“Hii hapa kaka”
“Let me see”(Leta nione)
George Charles,akapewa mfuko na kutizama kitu alichokuwa anahitaji.
“Ndio haya,how much?”
“Elfu kumi”
“Only ten?”
“Yes,only ten”
“Yana harufu nzuri?”
Sio kwamba George hakujua manukato hayo yana harufu gani, lakini kuna kitu alitaka kukiona kutoka kwa msichana aliyekuwa dukani hapo,alitaka kuona namna anavyozungumza na watu,hakutaka kukurupuka hata kidogo,akaona namna alivyokuwa anazungumza na wateja vizuri akiwa amechangamka kupita kawaida,akazidi kumuuliza maswali ya hapa na pale.
“Unaitwa nani?”
“Jina langu? Mimi?”
“Ndio wewe”
“Yusrath”
“Okay Yusrath,siku nyingine!Nadhani kesho nitakuja”
“Sawa,karibu sana”
George Charles,akaondoka eneo hilo akatembea mpaka kwenye gari yake ndogo aina ya Mazda,hapo hakubanduka aliendelea kumtizama msichana huyo mrembo anayeitwa Yusrath,jinsi anavyotabasamu na kuongea na wateja kwa uchangamfu!
Kuna kitu alikihisi moyoni mwake,alihisi kumpenda,hakuelewa ni kwanini ghafla namna hiyo,akazidi kutizama namna anavyozungumza na simu huku anatabasamu,kwa kuwa gari yake ilikuwa na vioo vyeusi yaani ‘tinted’ haikuwa rahisi kwa mtu yoyote, yule kumuona akiwa ndani,akaenda mbali zaidi na kumuona jinsi atavyokuwa na msichana huyo karibu,akafikria akawaza na kuwazua.Aliamini kivyovyote vile ni lazima Yusrath angeweza kusimamia mali zake vizuri,akaapia angefanya juu chini ili awe mke wake.Hapohapo,akalipiga gari moto na kuliondoa, mahali hapo!
******
Bastola ya jambazi pelle ilikuwa tayari kwenye kitundu kidogo,ameshika kidude maalum ambacho angekivuta risasi ingefumuka na kumpiga nayo Hajrath,aliamini kwa asilimia zote angemuua hapohapo akiwa amelala sababu alikuwa amemlenga usawa wa kichwa,hakutaka kufanya makosa.Alielewa kabisa baada ya kufyatua risasi hiyo,wanakijiji wangetawanyika huku na kule kumsaka,ndiyo maana hakutaka kufanya makosa!Mpango wake ulikuwa baada ya kufyatua risasi hiyo,akimbie mbio mpaka ndani ya gari lake alitoe kwa kasi,ndiyo maana akaanza kuhesabu kimoyo moyo!
“Moja”
“Mbili”
“Tat….”
Alivyofika nambari tatu,kuna mwanamme mmoja alitokea nyuma yake,huyo alikuwa ni mwanakijiji.Mkono wa kulia ameshika mkuki na mkono wa kushoto ameshika sime ndefu,kitendo cha kumuona akashtuka na kumgeuzia bastola ili amfyatue lakini alichelewa kwani mwana kijiji huyo, alirusha sime yake kwa kasi,ikamfikia Pelle kiganjani mwake,mkono ulioshika bastola ukadondoka chini kama ulivyo ukawa umekatika damu ziliruka kama bomba la maji lililotoboka,ukelele alioachia Pelle uliwashtua wanakijiji wengine,wakataka kujua ni kitu gani kimetokea!Wakatoka nje,mbiombio.Kuendelea kubaki eneo hilo akiugulia maumivu,ilimaanisha kusubiri kifo chake,akiwa anavuja damu mkononi nyingi,kiganja chake cha mkono kikiwa chini,alianza kukimbia huku na kule!Mbaya zaidi alikimbia huku akiyumba yumba,alivyoliona gari lake,akaingia na kutoa funguo akitumia mkono wa kushoto.
Bila kupoteza wakati akawasha na kulitoa kwa kasi,alivyoangalia kioo cha gari akawaona wanakijiji wameshika sime na silaha za jadi,kumaanisha kuwa angeendelea kubaki wangem-maliza.
Gari lilitapakaa damu nyingi,hakuwa ana uhakika kama angefika anapoenda salama salmin!Alikimbiza gari kwa umbali wa masaa mawili huku akihisi kizungu zungu kikali kutokana na kupoteza damu nyingi mwilini mwake,akapiga breki nje ya nyumba kubwa yenye geti jekundu!Akashuka huku akichuruzika damu nyingi mwilini mwake.Alivyolipiga geti kwa mara ya pili,akatokeza askari mwenye mtutu begani.
“Pelle,nini kimetokea?”
Askari huyo,ambaye pia alikuwa ni mlinzi,aliuliza akitizama huku na kule akidhani wenda Pelle anakimbizwa,wote wakaingia ndani na kufunga geti.Wenzake walikuwa bado macho,akiwa katika maumivu makali,akawaambia kila kitu kichotokea!Kwamba Hajrath yupo hai na yupo katika kijiji cha Nazareth.
“Sio kweli”
Mmoja,akapinga!Bado hakutaka kuliafiki jambo hilo sababu ya risasi alizopigwa Hajrath.
“Ni ye..ye!Nendeni,mkamaliz..e”
Pelle alizungumza kwa taabu sana huku akiwahimiza wenzake wafanye hivyo,kutokana na hatari iliyokuwepo ilikuwa ni lazima,wawataarifu na wenzao!Hilo halikuwa tatizo kubwa kwao,usiku huohuo simu zikapigwa wakaambizana wakutane nyumbani hapo!Haikuchukuwa dakika kumi,magari matatu yakawa yameingia ndani tayari kwa kufanya mikakati ya kum-maliza Hajrath,kwa hasira walizokuwa nazo walipanga wateketeze kijiji kizima kwa moto ili kulipa kisasi kwa kitendo walichomfanyia Pelle!
“Dumu la Petroli,hili hapa”
Mmoja wao,akatoa dumu kubwa lililokuwa na mafuta ya petroli!Silaha walikuwa nazo za kutosha.Wakaingia ndani ya magari na safari ya kwenda kijiji cha Nazareth kuanza dakika hiyohiyo,kutokana na kasi walizotumia muda mchache wakawa wamewasili,wakateremka na kuanza kugawana upande kwa niya ya kukiweka kijiji katikati.Kwa idadi, waliyokuwa nayo,ingekuwa rahisi kabisa kwao!Kumpata Hajrath na kum-maliza dakika hiyohiyo,ni kweli!Ndani ya sekunde tano,wakafanikiwa kukiweka kijiji katikati.
“Paa! paaa! paa! paaaa!”
Kitendo cha Mwanaume anayejiita Osama kufika katika kijiji cha Nazareth,aliachia risasi nne hewani,hofu ilitanda.Wanakijiji wakaanza kukimbia huku na kule lakini hawakufika mbali, sababu wanaume hao walikuwa tayari wamekiweka kati kijiji,wasingeweza kukimbia.
“Wote pigeni magoti”
Osama alizungumza,kwa sauti ya ukali akitumia kilugha chao,kuishi sana nchini humo kulimfanya akijue kilugha hiko.
“Nasema hivi,wote pigeni magoti”
Akarudia tena na kuwanyooshea bastola,wote wakatii amri na kupiga magoti.
“Kiongozi wenu ni nani?Nahesabu mpaka tatu”
Akauliza huku akiwatizama kila mmoja kwa zamu.
“Nahesabu moja..Kiongozi wenu yuko wapi?”
“Mbili,ajitokeze”
“Tat…..”
“Mimi hapa”
Mzee mmoja mwenye mvi na nywele ndefu akasimama.
“Paaaaaa!”
Bila kuuliza chochote,Osama akafyatua bastola,risasi ikamfikia mzee huyo kichwani,ubongo wake ukawa umemwagika chini.Hiyo ilifanya kila mmoja ndani ya kijiji hiko aogope,hiyo ndiyo ilikuwa niya ya Osama,kuwatisha kwanza!
“Sasa basi,nitaendelea kuua mmoja baada ya mwingine.Kama hamtoniambia nachotaka kujua,Mwanamke anayeitwa Hajrath yuko wapi?!Mliyekuwa mkimtibu”
Osama akauliza,akamuangalia Mama mmoja aliyekuwa analia,akamuita na kumuwekea bastola kichwani,hakukuwa na utani hata kidogo!
“Yuko wapi,moja!Namuuwa huyu,mbili huyo mwanamke yuko wapi? tatuu…Paaaaaaa”
Mwanamke akadondoka chini,ubongo wake ukamwagika chini,damu nyingi zikaruka!Osama akawa ameua mtu mwingine bila huruma.
“Yuko wapi?Wewe hapo simama”Osama,akasema na kumsimamisha mtoto mdogo, mwenye umri kati ya miaka 16-19!
Wanakijiji walilia wakiomba wasiuliwe,kuendelea kubaki kimya bila kusema ni wapi Hajrath alipo, ilimaanisha kijiji chote kuuliwa kwa kupigwa risasi za kichwa, hilo lilikuwa wazi kabisa.Hawakuwa na sababu ya kujitoa muhanga na kubaki kimya kwa mtu wasiyemfahamu ndiyo maana mwanamme mmoja akasimama wima.
“Najua alipo,yupo kule”
Mwanamme huyo akaongea huku akionesha kidole,kijumba kilichokuwa pembeni! Kumaanisha Hajrath yupo humo,majambazi wawili wakaelekea huko wakiwa na bastola zao mikononi, tayari kwa kum-maliza Hajrath!
Kila kitu hakikuwa sawa kabisa,kijiji cha Nazareth kilivamiwa na mtu asiyejulikana na ilikuwa wazi kwamba mtu huyo alimfuata Hajrath ili am-malizie, hilo walilijua!Kelele zilikuwa nyingi na hawakufanikiwa kumkamata Pelle, baada ya kuingia ndani ya gari na kutokomea.Hiyo ilikuwa bahati sana kwake sababu walikuwa wenye usongo kuliko kawaida kwani wangemkatakata kama nyama buchani,Mmoja wa wanawake akaingia ndani ya kibanda alicholala Hajrath na kumuangalia,alimuonea sana huruma hakuelewa ni kwanini wanataka kumuuwa, msichana huyo ambaye bado alikuwa mdogo kufa,kifupi hakustahili kufa mapema namna hiyo sababu alikuwa mwenye ndoto nyingi za kutimiza duniani.
“Ni lazima watamfuata”
Huyu aliitwa Nkulumanzila,ndiye mwanaume aliyeshika sime na kumkata Pelle mkono!Machale yalimcheza, kuna kitu kilimwambia ni lazima mwanaume yule angerudi kama sio kurudi na wenzake ili kumalizia zoezi.Alichofanya ni kumuita mwenzake,ambaye alikuwa mkakamavu, wakaanza kujadili namna ya kumtorosha Hajrath kutoka katika hatari inayomkabili mbele.
“Tutampeleka wapi sasa?”
Jamaa huyo akauliza huku akimtizama Nkulumanzila kwa umakini.
“Popote pale lakini tumtoe katika hiki kijiji”
“Lini?”
“Sasa hivi”
Wakina mama wachache waliokuwa ndani wanampa dawa Hajrath,walipewa taarifa hizo za kutaka kutoroshwa kwa Hajrath, japokuwa kulitokea mvutano mkubwa sana kati yao, kuna wengine hawakutaka kukubali lakini mwisho wa siku waliunga mkono hoja hiyo,wote waliafiki lakini hawakuwa wenye uhakika kama jambo hilo lilikuwa sahihi kwa upande wao, wakamtayarisha vizuri wakihakikisha kwamba kwenye kumbeba hawatomtonesha vidonda vyake, vilivyokuwa bado vinahitaji huduma na uangalifu wa hali ya juu sana.Hajrath,akawekwa vizuri mgongoni,wakaanza kutoka nje wakitembea kuelekea katikati ya miti mingi,huko waliamini wangemsafirisha mpaka kijiji jirani na kumficha asionekane,wakiwa katikati ya msitu walisikia milio ya risasi,wakasimama na kutizamana wakijua tayari kijiji chao kimevamiwa,lakini hiyo haikuwafanya warudi nyuma.
“Nina familia lakini”
Mzee huyo alisema baada ya kumkumbuka mkewe na watoto wake.
“Naelewa”
“Siwezi kuiacha,wewe nenda”
“Lak…”
“Tafadhali,wacha nirudi”
Mzee Nkulumanzila,alighailisha safari yake na kutaka kurudi, alivyoikumbuka familia yake aliumia moyo,ilikuwa ni lazima arudi, swala la kumuokoa Hajrath na uzito wa familia yake ndiyo ulimfanya ageuze,akashika sime na kurudi huku akikimbia kwa kasi,akimuacha mwenzake anasonga mbele!Akiamini kwamba kijiji cha Nazareth hakikuwa salama kwa Hajrath
*******
Kijiji cha Nazareth kiliwekwa chini ya ulinzi mkali sana,wanakijiji waliuwawa na kupigwa risasi za moto!Majambazi hayo yalikuwa na hasira baada ya kumkosa Hajrath ndani ya kijumba kidogo, walichodhani kwamba Hajrath yupo humo.
“Mnajifanya,hamtaki kusema sio?”
Jamaa akauliza baada ya kuuwa wanakijiji tisa tayari,hakuna kitu kingine walichotaka zaidi ya Hajrath tu,ndiyo maana baada ya hapo wakaanza kuingia ndani ya kijumba kimoja baada ya kingine, kumsaka mwanamke huyo waliyetumwa wamuuwe lakini hawakuambulia kitu chochote kile,mchezo ukawa ni uleule, kupiga wanakijiji risasi na kuwauwa ili waseme ni wapi Hajrath, alipo.Ndani ya vifua vya wanawake wawili ndimo, kulikuwa na siri hiyo ni wapi Hajrath alipelekwa, ilibidi mmoja wa wanawake hao asimame huku akilia na kusema kila kitu kilichotokea,akasema walipoelekea na Hajrath.Jamaa,watatu wakatumwa wafuatilie lakini huko walivyofika katikati umbali wa mita ishirini, waliuwawa na Mzee Nkulumanzila,aliyetumia mishale na sime zake, zilizokuwa na makali kotekote!Mzee huyo hakuwa wa kawaida,alipambana kufa kupona akitetea uhai wake,alichoharibu ni kumkata kichwa mmoja wa majambazi na kushika kichwa chake, akielekea kijiji cha Nazareth ambapo huko alikirusha kikadondoka katikati ya uwanja,majambazi wakatamani kukimbia baada ya kuona kichwa cha mwenzao!Hiyo iliwafanya wafyatue risasi hovyohovyo huku na kule.Walivyotulia kwa dakika moja,mwenzao akapigwa mshale wa tumbo, hapo ndipo wakajuwa kwamba wasipokuwa makini wataisha wote.Wakaingia msituni wakiwa na silaha za moto, wameshika. Katika harakati za mzee huyo kushika mshale vizuri ili afyatue,akapigwa risasi ya kifua akadondoka chini chali huku damu zikimvuja nyingi sana,alishaelewa tayari huo ndio ungekuwa mwisho wake.Majambazi wakamfuata kwa kasi na kumuinua!
“Hajrath,yuko wapi?”
“Pum..bavu zenu..Haha..haaa ha..nimalizieni.Laki..ni hamuwezi kumpata mimi nawaa..mbia”
Mzee huyo alizungumza maneno ya kutia hasira na kejeli juu,kana kwamba ana uwezo wa kuwadhibiti watu hao,ukweli ni kwamba alielewa kivyovyote vile watu hao wasingeweza kumuacha salama hata siku moja,alitaka amaliziwe.Hicho ndicho kilichotokea,hapohapo akapigwa risasi moja ya kichwa na kufa!
********
“Na ninaomba picha zangu zote,unirudishie!Sikutaki,ukome na unikome kama ulivyokoma kwenye ziwa la Mama yako…Nitumie picha zangu zote ulizokuwa nazo, mshenzi wewe umekalia tu umalaya utakufa na magonjwa mbwa koko wewe”
“Umemaliza?”
“Nitumie picha zangu zote Malaya mkubwa”
“Poa”
Yalikuwa ni maneno makali,mno.Kassim alikuwa amelala kitandani na msichana mrembo,simu yake ikiwa sikioni anatukanwa matusi akipakwa shombo na mwanamke anayeitwa Dorothea,hilo halikumuumiza sana moyoni kwani alikuwa tayari, amemchoka na isitoshe alishalala naye kitandani zaidi ya mara tisa,hakuona hasara kumpoteza, kwake ikawa kama ‘Ahsante Mungu’!
“Kuna nini baby?”
Mwanamke aliyekuwa pembeni yake,akamuhoji. Hiyo ni baada ya kumuona Kassim yupo katika hali isiyo ya kawaida.
“Kuna mpuuzi,ananizingua hapa.Ebu subiri nimshughulikie”
Kassim akazungumza maneno hayo huku akiingia kwenye ‘gallery’ ya picha zake za simu,picha nyingi zilikuwa za wanawake alichokifanya ni kuchagua picha thelathini na mbili na kumtumia Dorothea,chini akaandika ‘Chagua picha zako,sura yako nimeisahau’ ilikuwa ni lazima nayeye amfanyie dharau kubwa.
“Kwanini anifanyie nyodo?”
Kassim akajikuta ameropoka kwa sauti,kitendo cha Dorothea kumpa makavu yake kilimuumiza moyo kwa upande fulani.
“Baby,unaongea na nani?”
“Darling,wewe acha tu”
“Vipi,naona haupo sawa?”
“Kuna boya kanikera”
Ili kukatisha Maongezi ilibidi Kassim amvute karibu msichana huyo Sharony,akamuendea mdomoni wakaanza kunyonyana ndimi!Zoezi hilo halikuishia hapo,wakaanza kushikana shikana, kumaanisha kwamba inabidi warudie kwa mara nyingine!Hilo ndilo lililotokea kwani Kassim alianza taratibu kumuandaa Sharony,alifanya kila juhudi ili kuhakikisha anatengeneza mazingira mazuri,hiyo ndiyo ilikuwa sifa kubwa ya Kassim,alivyohakikisha kila kitu ameweka sawa mechi kali ikaanza!
Japokuwa, alikuwa na Sharony kitandani wametoka kumaliza kufanya tendo hilo la kuzini lakini sura ya Yusrath ilivyomjia akajikuta anaumia mtima,bado alimzimia mwanmake huyo, ambaye kwa wakati huo alikuwa ana mahusiano na kaka yake,hilo alilijua lakini hakujali.Bado hakuelewa ni kwa sababu gani Yusrath anamchomolea na kumkataa,wakati ilikuwa kinyume kabisa na wasichana wengine!Hiyo ndiyo ikafanya apate usongo zaidi,msimamo wa Yusrath ukamfanya atake kujua ni kipi hasa kinamfanya awe hivyo,aliapia ni lazima ipo siku atamvua nguo yake ya ndani.Baada ya kutoka eneo hilo walipokodi chumba maeneo ya Mbagala Zakiemu,Kassim akatafuta usafiri na kumuachia Sharony shilingi elfu kumi kama pesa tu ya kuweka mfukoni na kula.
“Ahsante baby,wewe unaenda wapi?”
Sharony,akahoji baada ya wote kutoka nje wanasubiri usafiri.
“Nataka niende Sinza Mara moja”
“Kuna nini?”
“Kuna mshkaji naenda kumcheki”
“Kuwa makini,nakupenda!Si unajua hilo?”
“Ndio natambua”
Walivyoagana tu,Kassim akachukuwa simu na kumuendea hewani mpenzi wake mwingine ambaye pia siku hiyo walikuwa na miyadi ya kukutana Sinza Vatcan,waongee wanywe ikiwezekana wafungiane chumbani.Hakutaka kupoteza wakati,akapanda daladala lililomfikisha Buguruni,hapo akachukua daladala lingine la Mwenge Makumbusho,alivyofika hapo akakodi pikipiki ambayo ilimpeleka mpaka Sinza Vatcan,eneo ambalo walipanga wakutane na Irene Mriba,msichana mrembo wa Kikurya!Ambaye pia kwa muda mrefu alikuwa akimuwinda.Alivyofika ndani ya baa hiyo,akaagiza soda na kuanza kunywa huku akiwa anatizama huku na kule.
“Ndio,nipo hapa nishafika.Muda sanaaa hapa Sweat bar”
Mazungumzo hayo aliyafanya kwa njia ya simu,akimtaarifu Irene kuwa amefika tayari,ni kweli!Haikuchukuwa dakika hata mbili,Irene akawa amewasili.Sifa ya mwanamke huyo, ilikuwa moja kubwa ambayo ilimfanya Kassim adate,mwanamke huyo alikuwa ana swaga,anaongea taratibu sana kwa mapozi,mbaya zaidi alizungumza kana kwamba yupo chumbani yaani sauti ya puani.
“Mamboo”
Namna Irene,alivyoivuta salamu hiyo ilimsisimua Kassim vibaya sana,akawa kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme,japokuwa siku hiyo alitoka kufanya ngono lakini akahisi kama hali yake sio shwari tena!
“Kaa,karibu”
“Ahsante”
Mhudumu alivyofika,Irene akaagiza chupa kubwa ya dompo na nyama choma ya mbuzi!Hiyo ilimfanya Kassim ameze mate mazito,akapiga hesabu za harakaharaka kichwani, pesa aliyokuwa nayo!Akajuwa kwamba asingekuwa makini siku hiyo,angeumbuka!
“Niwekee na chips kidogo,pembeni.Alafu muite mtu wa jikoni kule.Kuna supu?”
Irene alikuwa akiagiza,hiyo ikamfanya Kassim azidi kutumbua macho kama mjusi aliyebanwa na mlango!
“Yes,supu ipo!Mkia,kongoro na nyama”
“Ulimi huna?”
“Upo pia”
“Niletee”
Irene alivyomaliza kuagiza akamgeukia Kassim na kumuangalia.
“Vipi huko,chuo vipi?”
Kassim,akauliza lakini akili yake haikuwa hapo japokuwa alipachika tabasamu la plastiki ili ijulikane kama kila kitu kipo shwari,lakini haikuwa hivyo akili yake haikuwa hapo kabisa ilikuwa kwenye mahesabu ya pesa zake mfukoni!
“Chuo safi tu,nilikumisi kweli”
“Hata mimi”
“Wewe mbona huagizi?”
“Mimi niko safi nishakula tayari labda maji tu”
Jasho jembamba lilianza kumtoka Kassim,hasa aliposikia Irene anazungumza na rafiki yake simuni kwamba afike mahali hapo pia,wazungumze!Akahisi kutetemeka kuliko kawaida,japokuwa jioni hiyo kulikuwa na upepo mwanana lakini jasho jembamba lilimtoka,akakumbuka vitu vingi sana na maigizo mbalimbali ya kwenye luninga,akidhani kwamba vitu kama vile havipo,leo hii vimemtokea yeye puani!Hakuelewa ni kitu gani akifanye,akili yake ikafanya kazi kwa kasi ya mwewe lakini hakujua ni hatua gani achukuwe.
Dakika tano baadaye,akatokea msichana mwingine mrembo sana!Rafiki yake Irene,nayeye akaagiza chips mayai na Kuku pamoja na Savvana,Kassim akajikaza kisabuni.Ki ukweli hakuwa na pesa ya kulipa kila kitu kwa siku hiyo,swala la yeye kuosha vyombo ama kunyang’anywa vitu vyake kama simu na saa, lilikuwa mbioni kutokea kama asingelipa,vitu vingi aliwaza akatamani kukimbia lakini aliamini kwa kufanya hivyo,atachafua cv yake!Ilivyofika saa mbili usiku,bill ikaletwa mezani na kusoma shilingi elfu arobaini na saba na mia tano,hizo Kassim alitakiwa kuzilipa.
“Kwahiyo,hii ndio bili yote?”
Kassim,akauliza kwa kujiamini lakini moyoni alikuwa ana wasiwasi mwingi sana kama mtu mzima, anaye oga nje!
“Ndio”
“Ya kila kitu?”
“Ndio kaka”
“Jikoni pia hapahapa?”
Kassim,alizungumza na kumtizama dada huyo muhudumu ambaye aligeuka na kumuita mtu wa jikoni!
“Hapa ongeza,huyu dada anachukua take away ya Kuku mzima”
“Nani huyu?”
Kassim,akauliza huku akimuangalia rafiki yake Irene!Ambaye alitaka kufunga chakula pia.
“Sasa sikiliza.Huyu dada kala nini na nini?Achana na hiyo take away”
“Amekula chips mayai na Savanna tano…”
“Nipe bili yake”
Karatasi,ikaletwa nyingine!Alichokifanya Kassim ni kutoa pesa ambayo rafiki yake Irene amekula.
“Na huyu dada?”
Muhudumu akauliza ili ajue hatma ya malipo yake.
“Atalipa mwenyewe”
Irene Mriba,macho yalimtoka mno wakati mwingine alidhani wenda amesikia vibaya.Akamtizama Kassim na kujichekesha.
“Baby get sericous!”
“Nipo siriazi Irene”
“No bwaanaa,dada njoo atakupa anakutania tu!Kassim mpe bwana,utani mwingine haufai,tufanyiane wenyewe lakini sio kwenye biashara za watu”
Irene,akadhani Kassim anafanya utani na baadaye angemlipia kwani katika mfuko wake hakuwa hata na thumni ya shilingi mia,alikuja kama alivyo na mkoba wake ndani ulikuwa na kioo pamoja na tishu.
“Mimi nimekuita peke yako,umekuja na mwenzako”
“Lakini ni rafiki yangu”
“Ndio,amekuwakilisha sasa,nani wewe dada samahani.Unaishi wapi?”
Kassim akamuuliza rafiki yake Irene.
“Magomeni”
“Shika hii elfu mbili,utafanya nauli”
Kile alichokuwa anakifanya Kassim,alikimaanisha ingawa hakupenda lakini hakuwa na jinsi kwani hata yeye mfukoni hakuwa na pesa, ili kutoa aibu akajifanya kukasirishwa na kitendo cha Irene kufika mahali hapo na rafiki yake.
“Basi namimi naomba nauli basi niondoke kama huwezi kulipa”
Irene alivyoona hivyo,ilibidi adai hata pesa ya nauli ili akimbie msala,akatamani ardhi ipasuke imfunike akimbie aibu.
“Nauli yako,nimempa rafiki yako”
Hakutaka kuongeza kitu kingine zaidi,alichofanya ni kusimama na kutembea mpaka kituo cha daladala akimuacha Irene,anasumbuliwa na muhudumu alipe deni alilokula.
******
Viatu,vilikuwa chini juu ya malumalu!Kando kidogo kulikuwa na viatu vya kike pamoja na mkoba,kwa pembeni ya kitanda kulikuwa na blazia pamoja na chupi!Hata kama ulikuwa hujui kusoma,picha lilionesha wazi ya kwamba nguo hizo zilivuliwa kwa haraka kwani zilitupwa tupwa huku na kule.Miguu yote miwili ya Yusrath ilikuwa begani kwa Ahmed,amekunjwa vizuri gunzi lipo ndani ya mgodi wanafanya ngono!Vitu alivyohisi Yusrath havikuwa na kipimo chake,mbaya zaidi nyoka wa Ahmed alikuwa ndani, ulimi wa Ahmed unatalizi,mara unalamba shingo yake mara masikio,kitendo cha ulimi wa Ahmed kupita juu ya chuchu zake ndipo akahisi kama roho yake inaacha mwili kabisa,rahaa alizohisi na kelele alizopiga akiwa kitandani zilimfanya Ahmed apandishe mori zaidi,akamuweka sawa kabisa na kumgeuza kwa upande!Hapo ndipo akampenyeza nyoka wake vizuri, tena!
“Aaaaah aaashiii Ahmed,beiiiiiibiiii…aaaah aaaaaah ashiiiiiii,aaaaaah aaaashiii aaaah aaaaaah”
Yusrath,alizidisha kelele akitolea puani huku akihema juu juu,hiyo ilimaanisha ameguswa sehemu husika,haukuwa utani sababu alianza kukinyonga kiuno chake taratibu huku akitoa ulimi wake nje kumaanisha anaomba denda,Ahmed akafanya hivyo, wakaanza kulambana ndimi huku chini wakizungusha viuno vyao, asteaste!
“Darling,unajua kuwa nakupenda sana”
“Hilo nalijua,hata mimi.Nahisi ni zaidi yako”
“Sio kweli,mimi zaidi.Kungekuwa na kipimo cha kupima,ungejionea mwenyewe!Tafadhali usiniache,nitaumia sana”
“Siwezi kukuacha hilo nakuhaidi,ukiwa tayari naweza nikaja kwenu wanijuwe”
“Ni mapema nahisi,alafu baby nikuombe kitu?”
“Yes,niombe”
“Kwanini usitoke pale kwenu upange,mimi kuja kuja maeneo kama haya Lodge mara gesti!Sipendelei sana,napenda kufikia kwako.Lifanyie kazi hilo swala Mme wangu,ushakuwa mtu mzima sasa”
Yalikuwa ni mazungumzo baina ya Ahmed na mpenzi wake Yusrath,wakiwa kitandani baada ya kutoka kufanya tendo hilo lililowaleta duniani,walikuwa kama walivyozaliwa lakini walijifunika shuka moja,Yusrath akiwa kifuani kwa Ahmed,anazungumza kimahaba!Kila kitu kwake kilikuwa sawa,alijiona yupo salama kwa Ahmed na ndoto zake siku moja ilikuwa awe mke halali wa Ahmed,hilo aliamini lipo mbioni kutokea!Kila siku Msichana huyo kwa Ahmed alikuwa ni kama mpya vile,ukiongezea na hapo alikuwa ni msichana anayeona maili elfu moja mbele!Alimshauri Ahmed afanye vitu hatua kwa hatua.Ndiyo maana akamwambia kwanza, apange chumba ili baadaye iwe rahisi kwake kujitambulisha,wazo hilo likamuingia vizuri sana Ahmed akilini.
“Sasa hivi unatakiwa kununua assets za ndani”
“Sawa mke wangu nitafanya hivyo”
“Unatakiwa uwe gentleman,hata siku mgeni anaingia chumbani kwako!Anasema yes,hiki chumba cha Ahmed!Fanya hivyo Ahmed,mimi ni wako nipo!”
“Baada ya hapo baby?”
Ahmed akataka kujua zaidi cha kufanya,ushauri wa Yusrath ukawa umemuingia kumoyo!
“Baada ya hapo sasa,una save pesa!”
“Enhee…”
“Ukifanikisha hayo,nitakwambia hatua nyingine”
Ahmed aliendelea kumshangaa Yusrath, hakutegemea hata siku moja kama angekutana na mwanamke wa sampuli hiyo.
“Sasa naanza kuamini”
“Kuamini nini baby?”
“Every successful Man, has strong Woman behind”(Kwa kila mwanaume mwenye mafanikio,nyuma yake kuna mwanamke imara)
Hilo lilikuwa wazi kabisa,siku hiyo walizungumza vitu chungu mzima.Wakapanga mambo ya maendeleo, katika maisha yao ya baadaye,hapo ndipo Ahmed akagundua kwamba alikuwa anataka kuanza kutembea wakati bado ajajua kutambaa!Vitu alivyoambiwa na Yusrath vikamuingia akilini,hakupuuza hata kimoja,mshahara mwisho wa mwezi, alivyolipwa akaenda kwenye duka kubwa linalouza makabati,akaingia ndani na kukaribishwa vizuri!Alitaka kwanza kuanza na kabati lake la nguo chumbani!
“Hili bei gani?”
Ahmed akauliza huku akilifungua fungua kabati kubwa la nguo lenye kioo kikubwa mbele.
“Laki mbili na nusu”
“Mbona bei ya moto sana!”
Ahmed akashangaa,akitumia Kiswahili cha geto kumaanisha bei ni kubwa!
“Ndio bei zake,hii ni kazi.Huu mkataba,huu mlango wake hadimu sana kupatikana.Alafu angalia humu ndani,lina sehemu mbili!Madroo chini hapa.Yaani full ngwamba”
Muuza makabati nayeye, akaanza kulipigia debe kabati lake ili apate pesa.
“Tatizo bei sasa”
“Wewe una ngapi?”
“Mia mbili”
“Ongeza ongeza kidogo”
“Nina hiyo tu peke yake”
“Ya bei hiyo yapo,yale pale”
“Hapana,mimi nimelipenda hili”
“Jazia jazia basi”
“Nina hiyo”
“Aya,top top ongeza ishirini”
Ahmed akapiga hesabu za harakaharaka kidogo na kutafakari kiasi gani alichokuwa nacho mfukoni,mwisho wa siku akakubali akalipa pesa!Na kukodi kigari kidogo, alimaafuru kama kirikuu,wakapakia kabati na safari ya kwenda nyumbani kwao kuanza.
Akiwa njiani,hakuacha kumwambia Yusrath kile alichokifanya kupitia meseji.Hapohapo simu yake ikaita,ni Yusrath ndiye alikuwa anapiga.Alivyopokea akasikia busu,kufuatia hapo akapongezwa sana!
“That’s my boy,nakupenda Ahmed!Ahsante kwa kunisikiliza mme wangu”
“Nawewe pia Ahsante kwa kunipa ushauri”
“Ahsante zije kwako sababu ulikuwa na uwezo pia wa kukataa na kulipuuzia wazo langu”
“Naanzaje kwa mfano”
“Wapo,wanaopuuzia!Anywei tuishie hapo.Ndo unaelekea nyumbani sasa hivi?”
“Ndio baby”
“Ushakula?”
“Bado”
“Mmmh kwanini sasa?”
“Nilivyotoka Ofisini tu,direct dukani.Lakini nitakula usijali”
“Okay sweartheart,nakupenda!Mimi ndio nataka kwenda kuchukuwa fomu za chuo”
“Kuwa makini love”
“Okay”
Yalikuwa ni mahaba mazito,kungekuwa na mzani wa kupima mapenzi yao basi mzani ungevunjika!Ahmed na Yusrath walipendana kuliko kawaida.
“Kunja kona hapo”
Ahmed akamuelekeza dereva wa Kirikuuu,akakunja kushoto wakanyoosha na barabara ya vumbi, mpaka kwenye nguzo ya umeme wakakata kulia.
“Unapaki pale kwenye geti”
“Poa”
Gari lilivyowasili getini, Ahmed akashuka na kufungua geti,akamsalimia Mama yake!Jambo hilo liliwashangaza nyumba nzima,mama akafurahi alivyomuona Mwanaye anaanza kukuwa sasa!Wakashusha kabati,dereva akapewa ujira wake na kuondoka zake!Ahmed hakuishia hapo,akamfinyia mama yake shilingi elfu thelathini mkononi.
“Usimwambie Mzee Kama nimekupa”
“Mwanangu,Ahsante.Ubarikiwe sana,pale ulipotoa paongezeke mara mia yake”
Mama akatoa Baraka,Ahmed akaingia chumbani kwake na kuliweka kabati vizuri.Moyoni alikuwa mwenye furaha kupita kiasi kwa hatua hiyo aliyopiga,akamshukuru Mungu na Yusrath wake, kiujumla!
******
*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
0 comments:
Post a Comment