Search This Blog

Monday, March 23, 2020

THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 3/10


THE PAINFULL SECRET
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
 SEHEMU YA 3 KATI YA 10


Alfred alizidi kusikilizia kile kishindo mpka kilivyo fika karibu yake na kika tulia huku aki subiri kinacho fata,
Ghafla tena alihisi mtu huyo anasogea tena safari hii aki zunguka upande alipo ili waweze kuonana uso kwa uso.
"Who are you,(wewe ni nani)?"

Sauti hiyo ya kike ili tokea kinywani mwa msichana wa makamo, ambae kichwani alikua ame bana nywele zake vizuri nyuma kwa haraka haraka ali onekana kama Mu-afrikast, tishit yake iliendana vizuri na jeans aliyovaa ambayo aliichomekea ndani ya viatu aina ya Travota zilizopanda juu, Alfred japo kua alikua juu aliweza kumthaminisha Msichana yule kwa kumwangalia juu chini,
"Am asking you, one more time, who are you?,( nakuuliza tena kwa mara nyingine wewe ni nani?)"
Msichana yule aliuliza tena baada ya kuona ajibiwi, aliweka mkono nyuma na kutoa bastola ambayo aliiweka nyuma kiunoni.
"Hunter, i was just hunting, please dont hurt me(muwindaji, nilikua nawinda, naomba usinidhuru)"
"Stop deceiving me, LAST CHANCE, who are you, what do you want(usinidanganye, nafasi ya mwisho, wewe ni nani, una taka nini?)
Msichana yule ali uliza safari hii aliikoki bastola yake na kuilekezea juu usawa aliopo Alfred na kuonekana hakua na masihara hata kidogo wala kuonesha sura ya mzaha aliiweka sura ya ukauzu kama afande anayeongoza magari bara barani kipindi cha jua kali la saa saba.
"Alright, okay okay, just calm down, do you real want to know who am i?, put me down first"( sawa sawa,punguza jazba, una taka kuni fahamu mimi ni nani?, kwanza nishushe chini)"
"May be i have not make my self clear, do yu think your in which position to negotiate,?(labda sija eleweka vizuri, una dhani una nafasi gani hapo ulipo ya kuomba amri)
"Trust me, am not a bad guy here, (niamini mimi sio mtu mbaya hapa).
Mabishano yale baina ya pande mbili yaliendelea huku Alfred akiwa ana jitetea kuwa endapo ata funguliwa na ndo ata kapo ongea ukweli, lakini msichana yule alionekana kukaza kamba akikataa kata kata kuiruhusu hali ile.
"You have a gun, if i do anything you dont like, pull the trigger, (una bastola, kama niki fanya kile usicho kipenda nivyatue)"
Msichana yule aliji fikiria sana huku akimwangalia Alfred machoni, na baadae alitoa kisu na kumsisitiza asije kwenda kinyume maana ange mfanya kitu kibaya, Kweli kamba ili katwa na Alfred kudondoka chini kama gunia la mpunga,.
"Start talking,(anza kuongea).
"Alfr...eeee, "
Alfred aliongea kwa sauti ya chini chini huku akiwa ameinama pale pale chini na kufanya msichana asogee ili kumsikiliza vizuri.
"What are you saying(una ongea nini??"
"Aaaaa...free"
Msichana yule alizidi kumsogelea Alfred akiwa na bastola yake mkononi
.Kwa ghafla pale pale Afred alimka na kifurushi cha majani kilicho changanyika na michanga na kumwagia msichana yule machoni na kuipiga teke silaha yake ambayo ilidondoka upande mwingine, msichana yule ali fikicha fikicha macho kuashiria kwamba michanga ile ili mwingia machoni na kukaa sawa, alimuendea Alfred mbio mbio na kurusha teke ila Alfred aliliona na kulizuia ambapo baada ya kuli zuia alihisi ngumi imepenya na kumpata juu ya koromeo, hakukaa vizuri aliona ngumi ina kuja usawa wake wa uso na kuizuia nayeye kurusha kofi ambalo lili pita hewani baada ya msichana yule kuinama ki MAFIA na kumpiga ngumi za haraka haraka kama umeme mbavuni,aliinuka msichana yule na kuagiza ngumi nyingine ambayo Alfred aliiona na kuhepa upande wa pili,
Kitendo cha msichana yule wa makamo tena mrembo kupigana vile Alfred bado alikua ana kitafakari,
Baada ya kuku mbuka kuwa amewaacha Rose na Hanna na wenda msichana yule yupo pale kwa lengo la kumzuga, ivyo ali rudi nyuma hatua mbili na kukunja ngumi, ali muangalia msichana aliye mbele yake kwa makini, ali muona ana kuja kwa kasi na kurusha teke ila alishika mguu wake na kumzaba kofi la shavu,alimnyanyua na kumbwaga chini bila huruma, ila msichana yule hakuonesha kuumia aliinuka haraka haraka na kukaa tena sawa, alirusha ngumi ambayo Alfred aliiona na kumshika mkono na kumpiga kichwa ambacho kili mpata vizuri puani na kufanya msichana yule aanze kuvuja damu, zili kua ni ngumi za shika ni kushike mpaka Alfred alivyo muweka chini na yeye kua juu huku akiwa ame muwekea kisu shingoni.
"Alfred, Alfre.....d"
Aligeuka nyuma na kumuona Rose akiwa na Hanna, . Kwa kitambo sana Rose ali mtazama msichana yule ambae Alfred alimuweka chini.
"Hajrath,..."
Rose aliita jina hilo kuashiria kua aliye kua pale chini ana mtambua,
Walianza kuongea kizulu ambacho amna mtu yoyote aliyeweza kuki fahamu kutokana na Rose kukaa ndani ya nchi hiyo kwa muda mrefu sana ili mfanya ajue kizuru,.
"Alfred, usi muuwe namfahamu huyu, ali kua ana fanya kazi pale kwa Mujuni"
"..una uhakika?"
"Ndio"
Alfred ali simama na kumpa mkono wa kumuinua na wote kusimama, ila msichana yule alitoa kitambulisho cha upelelezi kutoka kitengo cha CIA na wote kubaki kumshangaa ..
"My name is Amney not Hajrath, i was working undercover"
Walipeana mikono na pia vile vile Alfred ali jitambulisha vile na kumpa kisa cha yeye kuingia katika nchi hiyo, bahati nzuri kila mtu alikua ana nuwinda Mujuni, Amney ali wa chukua mpka ndani ya kijumba chake kidogo na kuwa karibisha chakula cha asubuhi na wote kuanza kula huku waki panga mikakati mingine.
Piki piki zikiwa katika msako na msafara mwingine ukija kiongozi wao akiwa Mujuni ndani ya msitu huo ambao wali amini wata mpata Alfred na wakina Rose, wali zidi kusonga mbele waki fata nyayo za miguu,
"Naamini , hawa takua mbali na hapa, songa mbele wewe KIMBO,. sio una tingisha tu makalio yako hapa,"
"Sawa bosi,. Tuta wapata"
"Sasa wengine piteni huku, wengine kule wewe MEKI na TYSON twendeni huku, huu msitu naujua wote, kule mbele kuna kijumba kidogo dogo bila shaka hawa takua maeneo ya mbali na pale"
Haraka haraka wali jigawa na safari ya kusonga mbele kuanza,
Kwa mbali Mujuni alikiona kijumba kile na kuona vivuli vya watu kwa ndani,
Alitembea taratibu kwa kunyata na mwishowe kufikia nyumba ile ilipo ambayo ili kua ni ndogo iliyo tengenezwa na udongo mfinyanzi,..
"Ngo ngo ngoo"
Mjuni aligonga mlango ule na kusikia kuna mtu na kuja kufungua mlango ule.


Alishusha pumzi ndefu baada ya kuona sura ya kibabu kizee kilicho jipinda mgongo huku mkononi akiwa ameshika fimbo iliyo msaidia kutembea,
akazuga zuga pale na kuendelea na safari ya kuwa tafuta watu anao wataka huku bado akiwa na mashaka na ile nyumba aliye mkuta babu kizee yule.,

"Jina lake Mujuni Jumaa, ni raia wa Kenya, sema Kenya wana jua ame kufa , kabla ya hapo alikua mwana jeshi"
Amney ndiye aliye kua akiongea maneno yale akiwa na IPAD huku akizisogeza picha za Mujuni moja baada ya nyingine akitumia kidole chake, kila aliloongea lilionekana juu ya kioo kile cha IPAD, huku akionekana kila aliloliongea lilikua na ukweli.
"Hapa ni kipindi yupo jeshini, ila alikimbia Tanzania na kuomba uraia wa kule, ili kuji ficha"
"Mmmmh, haya yote ume yajuaje?"
"Kili chofanya nijue kuhusu yeye, kipindi cha nyuma sana nili pewa mission NAIROBI,na kupewa kikundi cha interpol kufatilia ile kesi ya watu walio kufa WASTEGATE, baada ya hapo nika gundua kua, Mujuni pia ali husika, yeye pia alikua miongoni mwa kile kikundi cha Al shaabab, ila waka geukana, waka lipua bomu kwenye nyumba yake wakindhani alikufa, aka kimbilia Tanzania, Dar es salaam, maeneo ya KIBAHA,, huko akaanza kuji husisha na madawa haramu ya kulevya".
Stori hiyo fupi ili mfanya Alfred abaki akitoa macho ,
"Sasa wewe upo mwenyewe sasa hivi?"
"Kuna watu nipo nao, siwezi kuku tajia, ila Mujuni ana mtandao mkubwa, ambayo ina hitaji kazi ya ziada"
Alfred alijikuta ana mwangalia kwa kitambo sana machoni na kuji kuta haongei kitu chochote kile.
Amney alitoka nje akiliendela gari ambalo lilionekana bovu na Amney kuendelea kulitengeneza.
"Hannah ina bidi aende hospitali, hii gari itengamae tumpeleke hapo st, Elizabeth,..."
Amney aliongea huku sauti ikitokea chini ya uvungu wa gari hiyo ambayo alikua akifunga funga vitu, Alfred nayeye alijumuika nae ,
Walivyo hakikisha gari ime tengamaa,
Wali wachukua Rose na Hannah ambao wakati huo tumbo lake lilikua tayari kubwa lililoweza kuonekana na kila mtu,
Alfred alimshika Hanna taratibu na kuingia ndani ya gari hiyo HIACE ambayo ilikua na viti vitatu tu vya mbele huku nyuma kulikua hakuna kiti na kufanya uwazi mkubwa,
"Alfred, vaa hii kanzu, Rose na Hanna hizi bai bui vaeni."
"Kwanini?"
"Wewe vaa nita kwambia nini namaanisha"
Amney aliwa sha gari ambalo lilipiga kelele likikataa kuwaka alijaribu tena ila liliwaka, mbele akiwa na Alfred huku Hanna na Rose wakiwa nyuma,
Gari lile lilianza kusonga taratibu huku Amney akihangaika kubadili gia pale ina potakiwa, waletembea takribani kilometa nne katika bara bara ya vumbi na kuingia ya lami wakielekea hospitali iliyo kua kidogo nje ya DARBUN ,
wali tembea umbali mrefu wakiya pita magari mengine mwishowe wali fika kwenye kizuizi ambapo magari yalionekana kuka guliwa mpaka ndani,
" kuna nini hapo?"
Alihoji Alfred huku akizidi kuangalia mbele kwa makini na kufanya Hannah na Rose na wao kuangalia mbele.
"Hannah na Rose kaeni kimnya msitoke huko nyuma,.msijali,"
Taratibu gari zile zili zidi kusogea na mwishowe kufika zamu zao kuka guliwa ila mpka wakati huo hamna aliye jua ni nini hasa kina kaguliwa.

"Aaasalam aelekuy"
Amney ali salimia kiarabu kama wana vyofanya dini ya kiislam na kutokana na bai bui aliyovaa aliendana nayo kabisa huku pembeni akiwemo Alfred na kanzu nyeupe huku kichwani alivalia kofia mkononi akiwa na tasbii,.
"Tuna omba tuka gue gari,"
"Mka gue nini"?
"Tuna omba tuka gue gari, ndani humu kuna nini?"
"Kuna mabox, mizigo ya msikitini na vitabu vya dini, tuna hitaji kuviwa isha mara moja"
Wakati huo Alfred ali taka kucheka ila alizuia kicheko baada ya kumuona Amney hacheki wala haoneshi kama ana danganya uso wake uli kua mkavu, pale ndipo alipo gundua lengo hasa la kuvalishwa nguo zile.
"Nataka kuha kikisha"
"Tuna wahi tuna haraka"
Askari yule haku taka kuelewa chochote, na kutaka kitu kimoja tu mlango ule wa HIACE ufunguliwe,
Amney ana kubali na kushuka ila baada ya kupiga hatua mbili ali sikia mlio wa HAZANA iki ashiria kua ni muda wa kusali kwa waislam wote.
"Asta kafu-llah, Allah akbar Allah akbar, nadhani ume isika iyo hazana, OSTADH Mustapha, sidhani kama tuta wahi inshallah" aliongea na Alfred kwa nje
huku
akimshika mkono akija ribu kumsihi ila zogo lile lili tulizwa baada ya askari mwingine kuja pale na Amney akionekana kulalamika sana kwa kitendo cha kunyimwa kwenda kuswali.
"Wewe Kobero, una wazuia watu wa Mungu kuswali, una LAANA za wazazi wewe, waaruhusu wapite upesi,,."
"Lakini mk..."
"Lakini nini...., Dada wahi upesi,. Nendeni piteni piteni.."
Hannah bila kugeuka mara ya pili aliingia ndani ya gari na kutimua mbio,
Huku akibaki kuwaangalia akitumia kioo cha nje.
Safari ilizidi kwenda mpka walipo fika hospitali hiyo st.Elizabeth na wote kushuka wali mpeleka Hannah hospitali ili madaktari waanze kumpa matibabu.,
Alfred alivyoona kila kitu kipo sawa na kutokana na jioni ilianza kuingia aliwaaga ili arudi hotelini aka badili nguo na baadae kurudi hospitali hapo,
Alichukua Taxi ambayo iliyo mpeleka mpka hotelini na kumlipa dereva yule, aliwapita watu wawili ambao walionekana kumnyooshea vidole huku pembeni wakiwa na muhudumu wa hoteli ile na kuachana nao.
Ila alipo fika ndani ya chumba chake alista-aajabu baada ya kuona chumba chake kime tibuliwa kana kwamba kuna mtu alikua ana tafuta kitu,
taratibu alitembea kwa tahadhari sana akielekea bafuni,
Alikutana uso kwa uso na maiti iliyo mkodolea macho,
Alijisogeza taratibu na kwa kutumia vidole vyake viwili aliigusa shingo ya ile maiti na kugundua kua mapigo ya moyo haya fanyi kazi,.
Gafla kwa mbali ana sikia mlango wake uki gongwa alifunga mlango wa bafuni na kuuwendea mlango na kuufungua,
ila sura aliziona ni zile zilizo kua zina mnyooshea kidole huku wakiwa na muhudumu wa hoteli hiyo.
"Wewe ndo Alfred Mulawa."?
"Niwa saidie nini?"
"Wewe ndo Afred Mulawa, embu jibu swali acha kutupotezea muda"

Walitoa vita mbulisho watu wale na kuji tambulisha ni maaskari,huku wakitaka kuingia ndani ila Alfred alitanda mlangoni.
"Pisha tupite"
"Mna taka nini kwanza?"
"Kijana usi tupotezee muda aisee, toka hapo mlangoni, tufanye tunachokitaka"
Alfred alifungua mlango na wote wawili kupita, alitoa kichwa nje na kuhakikisha kama kuna watu wengine alivyoona hakuna anae kuja, aliingia nayeye ndani na ku LOCK mlango,
Aliwaona maaskari wale wakiinama chini ya uvungu mwishowe waliingia bafuni.,
"Enhee, ndo maana ulikua una goma kufungua mlango., kumbe usha fanya yako"
"Sikieni mimi sija ua, nime ikuta iyo maiti"
"Huogopi kudanganya,?, uta ongozana na sisi"
"Ah wapi hapa siendi popote"

Askari mmoja alitoa pingu na kumshika mkono Alfred ila alivyo taka kuiweka mkononi mwake , alishangaa akivutwa na kupigwa kichwa cha pua,
"MUNGU WEEE"
kile kichwa kilionekana kilimwigia na askari yule kulalamika huku akishika pua yake,., mwingine alitaka kutoa kirungu na kukipiga teke huku akimvuta mpka ukutani na kukibamiza kichwa chake, alitoka njee ila alikutana na watu watatu wana kuja na kuanza kumkimbiza, alishuka ngazi zile mbio mbio sana,.
Alipiga hatua haraka haraka na kukimbia ila alivyofika nje alikutana na wengine waliotoa mitutu na kumfanya asalimu amri huku akiweka mikono juu,
Wali mfata pale alipo na kumpiga pingu, kilicho kua kina tokea mbele yake hakujua kimesababishwa na nini,
Aliingizwa ndani ya gari ya mapolisi huku akiwa chini ya ulinzi mkali.


Kitendo cha kufikishwa maabusu walianza kumpiga na kumtesa wakimuuliza vitu ambavyo hakuvielewa,na hata hakujua kwanini wana muuliza.
"Ume kuja kufanya nini Katika nchi hii"?
"Nime kuja kutalii tuu, Sina lingine."
"Una tundanganya, NAKUULIZA WEWE BWEGE, ume kuja kufanya nini?,"
"Nisha kwambia tayari,".
Jitu lile linene liliendelea kutoa agizo kua waendelee kumpiga kila mahali mpaka ata kapo sema ukweli,

Mwishowe wali mfunika na nailoni kichwani na kuanza kumwagia maji ili asiweze kutoa pumzi yoyote,
kwa takribani dakika kadhaa. walitoa lile nailoni na kufanya Alfred atape tape aki tafuta pumzi baada ya kuikosa kwa muda mrefu.
"Kwanini ume ua, ?,
"Mimi sija ua naomba mnielewe,sija ua.. ta..fadhali nime kuja.. tu. Kuku.. talii., nili mkuta mule ndani"
"We ni Mtanzania,"?
"Ndio, Mimi ni mtanzania"
Yule kibonge mwenye kitambi alionekana akipekua pekua ndani ya begi lake dogo ambamo alitoa passpot ya kusafiria na kuonekana kuikagua kagua.
"Hii kesi lazima iende ngazi za juu, we ni kunyongwa tu, si una jua sheria za hii nchi, muinuieni tuondoke nae"
Alfred aliinuliwa akiwa amelowa damu usoni huku akiwa amevimba,
alimuona yule askari aliye mpiga kichwa ali mgungua kutokana na kumuona na plasta puani, yule askari alimfuata na kumpiga kirungu ili mradi nayeye ashushe hasira zake.
Ila baada ya kutoka njee alimuona mtu mmoja mrefu wa wastani akiwa amevalia nguo za kijeshi akiwa ameukunja uso wake na kufanya makunyanzi ya hasira huku pembeni akiwa na Amney.,
"Muachieni"
Mwana jeshi yule aliongea kwa sauti ya juu akitoa amri ya kibabe kana kwamba yeye ndo mkuu wao, kila mtu alibaki kumshangaa,
Alfred alimwangalia mwana jeshi yule ambaye begani alikua na kama picha ya bawa na kujua kuwa ana madaraka mengi na ana cheo cha UKOMANDOO.,
"Nime sema mwacheni, . Sitorudia tena"
"Muhalifu huyu"
"Unadhani nani asiye jua mnayo fanyaga, alafu msini fanye niondoke na nyie kambini , "

Maaskari wale walianza kuangaliana kwa hofu waki tafakari wataanzaje kumfungua.
Walivyoona mwana jeshi yule ana wafata haraka haraka wali mfungua pingu zile na kumuacha.
"Shenzi nyie mna bahati, PUMBAVU ZENU, na muende mkashtaki popote mimi naitwa Comandoo KELVIN KIBUMU."

Aliongea mwana jeshi yule na kumshika mkono Alfred ambae kwa wakati huo alikua hana nguvu hata kidogo.
"Vipi ndugu yangu pole sana, wame kupa vitu vyako vyote hawa WAPUUZI?,"
""usijali kaka, twende tu, ndio wame nipa, Amney Hannah hali yake vipi?,
"Anaendelea vizuri"

Amney alimwangalia kwa huruma na wote kuingia ndani ya Hammer hiyo ya kijeshi ambamo ndani yake kulikua na dereva alivalia nguo za jeshi.
"Yaani hapa wangeenda kukuuwa, hawa wazulu sio watu wazuri, najua wame fanya makusudi kuku uuzia ile kesi, ndo zao huwa wana penda kuwa fanyia wageni wa nchi,"
"Mlijuaje kama nipo huku?"
"Nili muulizia yule muhudumu alivyo nielekeza tu wale maaskari walivyo basi nika wajua, WAJINGA WAJINGA tu, "
"Alafu Alfredi huyu ni kama kaka yangu huku, nili soma nae , tukaingia wote DEPO Kipindi nipo CUBA, mpaka sasa ana nisaidia saidia huku, ni mtu mzuri sana"
"Nashukuru sana kuku fahamu kaka"

Utambulisho ule mdogo ulo fanya wapeane mikono na wote kufurahi,,

"Lakini huyu Mwana haramu Mujuni, lazima nimtie mikononi mwangu, Pumbavu sana, namtamani sana yule MREMBO, , alimuuwa best yangu"
Aliongea Kelvin Kibumu kwa sauti ya juu sana kana kwamba mtu anaye mzungumzia alikua aki mtafuta kwa kitambo sana,
Hammer ile ili egeshwa ndani ya kambi ya jeshi na mlango kufunguliwa na mmoja ya wana jeshi huku akipiga miguu chini na kuweka mkono juu kuashiria anaepita mbele yake ni mkuu wao, alivyo pita kwa wengine ili kua ivyo ivyo pia,
Alfred ana shangaa shangaa jinsi kambi hiyo ilivyo wakiwa na Kelvin Kibumu nawote kusonga mpka ndani kwenye rada.
"Huku ndo kazini kwangu , ondoeni shaka, mimi sio mtu wa mchezo mchezo ume sikia Amney"
"Una hatari sana Kelvin"
Baada ya kuzungushwa maeneo hayo japo kua Alfred hakujua kwanini aliletwa pale,
Baadae waliagana na Amney pamoja na Alfred kurudi hospitali St, Elizabeth,
ila kabla hawa ja fika st, Elizabeth waliona gari la wagonjwa liki pita kwa kasi na huku baadae waliona magari ya mapolisi yakikimbia huku na kule,
Ila wana staajabu kufika hospitali na kukuta maaskari waki chukua maelezo ya hapa na pale. wali wapita na kuingia ndani ya wodi alilolazwa ndani na kumkuta Rose akiwa amekaa chini huku askari akuchukua maelezo .
Amney haraka haraka alitoa kitambulisho na kupita ndani akimuacha Alfred nje na kumuendea Rose moja kwa moja pale alipokaa,
"What happened, why are you crying(nini kilitokea, kwanini una lia)?
"Hannah, Hannah,.... Wame mchukua"
"Niangalie, embu niangalie Rose, nani kamchukua."?
"Mujuni, kaja kauwa madaktari na kasema ata muuwa Hannah pia, .. kutokana na Alfred alimuuwa Mdogo wake"
"Whaaaaaaat"
Amney alipiga ukelele n a kufanya Alfred kufanya fujo mpka kuingia ndani ya chumba kile,
ambapo moja kwa moja alipewa habari hizo nyingine zilizofanya mapigo yake ya moyo kwenda mbio na kubaki akimwangalia Hannah, huku akiji kuta akipiga piga ukuta wa hospitali ule na kufanya ukuta utoe kelele,
Hasira zili mkaba kooni na kuji kuta ana serereka na ukuta huku akikaa chini kutokana na nguvu za miguu kumuisha.,



Alihisi kichwa chake kizito kwa muda huo.
"Alfred, tuta mpata Hannah punguza mawazo, mi naaamini usijali."
"Amney Hannah ni mke wangu kumbuka, alafu hali aliyo kua nayo haiwezekani ,"
"Mambo haya yana hitaji uta ratibu wake wa hali ya juu sana na uma kini pia Alfred, mimi nipo bega kwa bega na wewe mpka Hanah apatikane, subiri kidogo"

Amney alitoka huku akitoa simu yake huku akionekana akiiweka sikioni na kumuacha Alfred akiwa katika dimbwi la mawazo aki tafakari sana jinsi Hannah anavyo teseka,.
Amney alikuja haraka haraka na kumchukua Alfred akiwa ame mshika mkono na kutoka nae nje.
"C,I,A nipatie funguo ya gari yako"
"Sawa hizi hapa"

Aliongea na askari mmoja aliye mkuta pale nje na kuchukua gari yake,
Aliserereka nayo huku akienda kwa kasi ya ajabu.
"Tuna elekea wapi"?
, "alipo Mujuni, nime ambiwa yupo KIRMBLEY, ivyo ngoja nipitie njia hii rahisi,"
Amney alikunja kona ghafla na kuingia bara bara ya vumbi ambapo baadae ana kuta lami na kuzidi kwenda kwa kasi,
aliya pita magari mengi yaliyo kua mbele yake ,
Kwa mbali walianza kusikia milio ya risasi na baada ya kusogea karibu waliona watu wa Mujuni waki tupiana risasi na polisi ambao kwa wakati huo walionekana kuzidiwa
Milio ya risasi ilizidi kusikika huku na kule na Amney kukanyaga breki na kutoa bastola ndogo huku akisogea chini kwa chini Alfred na yeye alifuata na kuchukua mtutu aliouona chini juu ya askari aliye pigwa risasi,.
Alinyata huku nayeye akijibu masha mbulizi yale, kweli kutokana na ujuzi mzuri wa kulenga shabaha alianza kumtungua mmoja baada ya mwingine huku akihama upande huuu mara ule akitumia mbinu aliyo fundishwa kipindi yupo mazoezini, Amney pia nayeye haku cheza mbali, walienda wakisaidiana huku na kule, na mwishowe kuingia ndani ya jumba hilo ambalo lili kua bovu hali jamaliziwa

"Dereva aliye kua anaendesha ile gari siku ile, alikua mdogo wangu, Mwana ume wako Alfred amefanya ame kufa , namimi sito kuacha nataka nayeye aumie kama nilivyo umia mimi hapa, leo ndo nitakuua mimi mwenyewe".
Aliongea Mujuni akiwa amemshika Hannah mkononi na kupanda nae juu gorofani huku mkononi akiwa na bastola.
"Mujuuuni,,..Hapo hapo ulipo"
Ili kua ni sauti ya Amney akiwa na bastola mkononi, Mujuni alivyoona vile alimuweka Hanna mbele yake huku bastola akiwa amuelekezea kichwani.
"Weka silaha hiyo chini, kabla sija toa ubongo wa mwenzio, fanya ivyo uli kua una jifanya MFANYAAKAZI wangu nawewe ume jiingiza kwenye matatizo , pumbavu Hajrath, ..nasema hivi weka silaha hiyo chini, moja, mbili, taaaatu, paaaaaa"
Risasi ili sikika na Amney akibaki akitoa macho hii ni kutokana kwamba hakufyatua yeye risasi hivyo alijua ki vyovyote vile risasi ile Aliivya tua Mujuni....



Alitahamaki kuona Mujuni ana shika mkono wake wa kulia huku ukivuja damu alivyo angalia pembeni alimuona Alfred akiwa ameushika vizuri mtutu kuashiria kuwa yeye ndo aliyevyatua risasi na kwa umakini ili mpata Mujuni mkononi,
Mujuni aliji kuta ana muachia Hannah , kutokana na walikua ngazi za juu Hanaah anateleza na kudondoka kuelekea chini,
Alfred alikimbia haraka haraka akienda kumuawahi Hannah ambae kwa wakati huo alikua ameji shika kwa juu huku miguu yake ikiwa inaning'inia chini .
"Hannah. Nipe mkono wako taratibu"
"Alfred. Nadondoka naishiwa nguvu"
"Nipe mkono wako Hannah, nipe mkono wako,"

Alfred aliwahi akiwa ana msaidia Hannah ili asiweze kuporomoka chini ya hilo gorofa lenye urefu kiasi ambalo lili onekana bado lipo katika matengenezo.
"Mujuni, its over now, it is over. Your going to prison, slowly put your weapon down,.(Mujuni, yamekwisha sasa,yame kwisha, una kwenda jela, taratibu weka silaha yako chini""

Aliongea Amney huku akiwa ameishika bastola yake kwa tahadhari akiwa tayari kuivya fua endapo mujuni angeenda kinyume na anavyo taka,.
Mujuni alimuangalia Amney kwa makini huku taratibu akiiweka silaha yake chini,
"It is not that simple, stop wasting your time, let me go and nobody will hurt you, just let me walk away,(sio kirahisi, acha kupoteza muda wako,niachie niende na hakuna atakae kudhuru, niache niende zangu
"Put your hands where i can see them now,(weka mikono yako pale nitakapoweza kuiona, sasa hivi)"
Mujuni taratibu aliweka mikono yake juu huku Amney akizidi kumsogelea taratibu.
"Hannaaaaaaah,..Haaaannnnaah"

Zili kua ni kilele kutoka kwa Alfred na kumfanya Amney ashtuke na kuangalia kilichotokea,
Hakuamini alichokiona alimuona Alfred hakua ame mshika mtu yoyote maaana kwamba Hanaah alikua amejiachia katika mikono ya Alfred,
Alfred alimshuhudia Hannah akienda chini na kuzidi kuita jina lake huku akishuhudia akifika chini na kudondoka juu ya lami na kufanya damu ita pakae maeneo yale.
Alfred alisimama na kuchomoka kama mshale na kushusha ngazi tatu tatu na kufanya ayumbe ayumbe kwa kuteleza teleza,
Alitoka na kushuhudia wamesha mzunguka Hannah wakimuangalia kipindi hiko hakua na dalili yoyote ya kuongea,
Alfred alipita katikati yao na kuwa sukumiza watu aliowakuta na kumuendea mke wake Hannah,
"Hannnah. Hannah, amka mke wangu, Hannah,Hannah, Hannah,"
Alimkombatia Pale alipo huku Hannah akiwa ana vuja damu puani na maeneo ya kichwani ,
alimnyanyua kwa mbali alimuona Amney anakuja haraka haraka na kumfikia pale alipo.
Amney kuona kitendo kile alitoa simu kuagiza gari ya wagonjwa ije mara moja,
"Nime mkosa Mujuni."
"Kivipi Amney?"
"Amenitoroka"
"Haiwezekani, Haiwezekani,... Uta mpoteza vipi wakati ulikua nae"
"Ndo ivyo Alfred, kitendo cha kugeuza shingo pale ndo nilipo kosea, gari ya wagonjwa lina kuja,. Pole Alfred"
Baada ya muda mfupi tayari gari la wagonjwa lili fika na Hannah kuingizwa ndani ya gari huku Alfred nayeye aki iingia ndani.
Gari hilo lili tembea mwendo.wa kasi huku Alfred akionekana amechanganyikiwa, na kuongea vitu visivyo eleweka,
Takribani dakika thelathini zili tumika na gari hilo lili egeshwa ndani ya hospitali kubwa na wauguzi kuja haraka haraka ambao walio nekana wame valia nguo nyeupe, wali mshusha Hannah huku Alfred akionekana nayeye kusaidia na machela ile kuanza kusu kumizwa kwa kasi.
"Aaa....,,.aaafree...d, n..a..kuu..fa.., Nahi,,si ma..umivu. kichwa..ni. "
Aliongea Hanah kwa mbali sana tena kwa shida huku akiwa amemshika Alfred mkono na machela ikizidi kwenda kwa kasi .
"Haannah, haufii. usiseme ivyo Haanah, huwezi"
"Al...fre...d. nakupen..da Mume w...ng.."
"Samahani kaka, tusubiri hapo nje"
"Hapana ni mke wangu, hapana, siwezi kusubiri"
"Tuna jua ndio tuache tufanye kazi yetu"

,Alfred alibakia akiwa ameganda kama barafu na kusimama kama namba moja,
huku akiangalia mlango ule ambao alia mbiwa asiingie na ndo humo alipo ingizwa Hannah,
Matukio yali yokua yana tokea mbele yake hakuweza kuyaamini,
Baadee Amney alifika na kumfariji huku akimkombatia na kumpa moyo akimwambia kuwa ajikaze maana kila kitu kitaenda sawa, hakutaka kumsikiliza mtu yoyote yule,
"Mujuni yuko wapi"?
"Tuta mpata Alfred usijali?"
"Jibu swali langu, Mujuni yuko wapi?"
"Alfred, punguza jazba"
"Amney, sikujui hunijui, tume kutana tu muda mfupi, Mujuni yupo wapi,?,, Mujuni yuko wapi niambie sasa hivi"
"Yupo kwake sasa hivi hana sehemu ya kukimbilia"
"Asante, kaa na Hannah,. Hakikisha unaanipa taarifa kinachoendelea mi naenda kwa Mujuni"
"Alfred, Alfred..."
Amney aliita bila kujibiwa chochote na kumuona Alfred ana tokomea kwenye moja ya kona ya Hospitali hiyo,
Giza lilipo ingia tayari Alfred alikua nje ya nyumba kubwa hiyo ya Mujuni kwa nia moja tu kumuuwa Mujuni kwa mikono yake.

"Mike na Rodgers, mta ongoza timu yenu upande huu wa uwani mta pitia hapa, Wewe Sameer na Rajab timu yenu ita kua getini wengine mta kua namimi, KIMNYA KIMNYA, mta subiri amri kutoka kwangu, kabla sija sahau Moris kama kawaida hapa utakaa na SNIPER sawa, lets go boys"

Yalikua ni maagizo mafupi yaliyoeleweka kutoka kwa Amney akiwa na kikundi kidogo cha maaskari ambapo kila mmoja alishika mtutu, baada ya kutoa maagizo hayo huku wakiwa na picha nzima ya nyumba hiyo ya Mujuni ambapo wakati huo wali kua wakielekezwa kupitia ramani ambayo Amney aliichora kutokana nayeye alishawahi kuji fanya kama mfanyakazi wa Mujuni,

Taratibu kwa tahadhari kila mmoja ana chukua nafasi yake na jeshi hilo kuizunguka nyumba ya Mujuni kimnya kimnya bila mtu yoyote kujua.
Amney aliangalia huku na kule huku jeshi lake likiwa nyuma alitembea kidogo na kunyoosha mkono wenye ngumi kuashiria kuwa wasimame iyo ili kua ni ishara kuwa kuna kitu mbele,
Amney kwa umakini alitoa darubini na kuanza kuangaza angaza huku na kule akiangalia usalama,
Alivyo hakikisha kila kitu kipo sawa aliruhusu na mmoja mmoja kuanza kuruka ukuta na kutua bila kutoa kishindo chochote,
Walikutana na mlinzi na kumvisha kamba shingoni na kumuweka chini na jeshi lile lililongozwa na Amney kusonga mbele.
"Upo peke yako,. Nakuuliza upo peke yako"?
"Ndio, niko mwenyewe"
"Una tuongopea"
Lilikua ni swali kutoka kwa walinzi watatu wakimuuliza Alfred huku mmoja akiwa na bastola ndogo wakiwa wame muweka chini ya ulinzi.
"Kacha kacha, paa paaa"
Uli kua ni mlio wa risasi cha kumshangaza Alfred aliwa ona watu wale waki dondoka chini ,
akiwa bado kwenye mshangao alimuona Amney akija huku akiwa na bastola,
" uli fanikiwa kumpata Mujuni?"
"Yupo humu ndani, "

Wote wali toka pale na kuanza kumsaka chumba bada ya chumba huku wakiwaweka chini ya ulinzi walinzi waliopo ndani ya nyumba ile
Baade una sikika mlio wa risasi , Alfred alivyo angalia pembeni alimuona Amney yupo chini akiwa amepigwa risasi mbili za kifua na Mujuni ambae wakati huo alikua akikimbia.


unyonge uli mtawala Alfred na kumfata Amney alipo ambae wakati ule alikua akiweweseka, na kuhangaika.
"Alfre,,d niko sawa nina BULLET PROOF "
"Kweli,?"
"Kweli nipo sawa nina BULLET PROOF sema nashindwa kupumua vizuri"

Alfred alimvua koti alilovaa juu na mwishowe kuku tana na Bullet proof ambayo ina fanania na vest na kazi yake ni kuzuia risasi isiweze kupenya na kumdhuru mtu, .
Alfred alivyo hakikisha kampa msaada wa kutosha Amney, alisimama na kusonga mbele.

"Oyaa sasa subiri dingi alale mi nita kuja, leo MAISHA CLUB, watoto wazuri wapo kama kawaida, nataka nimuoneshe mtoto MARTHA kuwa mimi ni nani"
"Ibuka ibuka ibuka mwana, njoo na ndinga kama kawaida, wapo wa kumwaga"
""Usiwaze, usiwaze mzazi"
Yalikua ni maongezi ya simu kutoka kwa JONAS mtoto wa mfanyabiashara mkubwa wa kichaga aliyeitwa LIMO, maeneo ya Mbezi beach , jijini Dar es salaam ambamo hapo aliweeka nyumba kubwa ya kifahari hakuna asiye mfahamu mchaga huyo ambae alikua akiongoza kuwa na maduka mengi ndani na nje ya mji,
Leo hii mtoto wake ana panga njama za kutoroka usiku ili aende disco , huku baba yake akiwa hana hili wala lile akiwa amelala na mke wake,
JONAS kwa kua alijua funguo za gari za baba yake anapo ziweka aliziendea na kuchukua funguo za PRADO na taratibu kushuka ngazi za gorofa hilo akiwa amevaa vizuri aliienda nje na kufungua geti taratibu na kutoa gari hilo la baba yake, alivyo hakikisha lipo nje aliliendea geti na kufunga, ambapo aliiingia ndani ya gari huku akitabasamu sana, usiku huo mnene.
Alifungulia redio mziki mkubwa sana ndani ya gari huku akitoa kasi sana,
Baada ya muda mfupi tayari alikua nje ya club hiyo na kuingia ndani na kukutana na marafiki zake mbali mbali, pesa haikua tatizo kwake ivyo alifanya sifa na kuwanunulia kila mtu aliye mjua kweli JONAS LIMO alifanya sifa siku iyo hasa kwa watoto wa kike.
"Kunyweni kunyweni mimi ndo JONAS LIMO, , muongeze nyingine huyo Martha Msoso, mpe nyingine alafu bili niletee"

Jonas alifnya kila ana lolifanya ili mradi aweze kuwa furahisha marafiki zake,
Alivyoona muda ume kwenda aliwaaga marafiki zake na kuingia ndani ya PRADO na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwao MBEZI BEACH ,
Alivyo fika kama kawaida alishuka ndani ya gari na kwa tahadhari alifungua geti, na kuliingiza gari ila alivyo shuka ali pigwa na bumbuazi alivyoona watu watano wakiingia huku wakiwa wameziba sura zao na mikononi wakiwa na bastola, hofu ili mtanda sana na kuganda kama mti uliochomekwa kwenye tope.
"Tupeleke kwenye chumba cha baba yako fanya upesi, TUPELEKE kwa Limo, "

Bila kujibu chochote Jonas akiwa ana tetemeka aliongoza mbele huku majambazi wale wakiwa nyumba yake, waliingia na ndani kuanza kupanda ngazi , alipita chumba cha kwanza cha pili na mwishowe kukata kona na kusimama nje ya mlango akiashiria kuwa humo ndimo baba yake analala.
. "Hiki, hiki, hiki hapa, naomba msimuuwe baba yangu"
"Gonga mlango huo"

Jonas alimriwa na mmoja wa watu wale huku akiwa amewekewa bastola kisogoni, aligonga mara ya kwanza mara ya pili, mwishowe kwa mbali sauti ya kike iliitikia ikionekana kuwa ime toka katika usingizi mzito., Jonas aliitambua sauti hii ili kua ni ya mama yake mzazi Manka.
"Nani ana gonga?"
"Mimi Jonas"
"Nini tena baba sasa hivi usiku usiku."
"Mama, fungua mlango,"
"Una taka nini tena lakini?"
"Fungua Mama, kuna jambo nataka nikwambie"
"Aya baba nakuja"
Kweli ulisikika mlio wa kitanda kikipiga kelele kuashiria kua kuna mtu ana aamka, baadae kitasa kililia na Mama Jonas kufungua mlango ila alibaki aki duwaa baada ya kuona bastola iko mbele yake.
"Kimnya, ukipiga kelele una kufa, mumeo yuko wapi?"
"Mume wangu amelala"
"Ingia ndani, nawewe pia ingia ndani"
Waliingia majambazi wawili wakiwa na Jonas pamoja na Manka.,
Limo alikua kitandani alisikia kila kitu kina choendelea na kubaki kusikilizia kina choendelea, baadae ana fuatwa na kuamshwa.
"Limo, hatujaja kupoteza muda Pesa ziko wapi?"
"Pesa gani YESU NA MARIA, keleuwii sina pesa aisee"
"Limo usipotezee muda, tuta kuuwa, zile millioni mia mbili hamsini ziko wapi"?
"Zipi zipi"?

Wali mfata Limo na kumuweka juu ya sakafu huku waki mukea bastola wakitaka kumuuwa, ila mke wake Mama jonas kutokana na mapenzi huku akihofia uhai wa mume wake alijikuta akiwa tajia zilipo, ali waelekeza kwenye kabati na kuchukua begi hilo lenye pesa za mahesabu yote za maduka,
Majambazi wale walivyo hakikisha ndo zenyewe wali toka haraka haraka na kuondoka zao.
"Mbwa wewe Mama jonas, yesuu yesu yesu yesu, uta lipa pesa zangu haki ya Mungu na kwambia, yeuwiiii Manka, nani kakwambia uwaoneshe au una wajua?"
Aliongea Limo kwa rafudhi ya kichaga kweli alionekana kuchanganyikiwa sana kitendo kile cha pesa nyingi kutoweka ndani ya muda mfupi.
"Baba jonas, hizo pesa tuta tafuta nyingine, wangeekuuwa mume wangu, nawewe Jonas ndo nini kutuletea majambazi"?

Ki ukweli kila mtu alionekana kuchanganyikiwa, baadae Limo alitoa simu yake ya mkononi na kuta futa majina.
"Haki amungu huyu ata kua KIMARIO tu, niyeye peke yake ana jua nime kuja na pesa uwiii yesu wangu Manka, yesu yesu yesu yesu,."
Aliongea mwenyewe huku aki mtafuta FREDRICK rafiki yake ambae ni mpelelezi,
Muda mfupi Fredrick ana ingia na kuchukua maelezo.
Mkuu huyo katika kitengo cha CID upelelezi ana mkumbuka sana Alfred kwa vitendo vya uhalifu vinavyo jitokeza,
Anaamua kuitisha kikao kidogo na kutoa amri moja tu, waende wapelelezi wengine Africa kusini ili waweze kumsaidia Alfred na vile vile mke wake aliye tekwa nyara, kweli taratibu zinaanza na kikosi kutumwa kikiongozwa na JOYLA
 *******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG