Chombezo : Raha Ya Dafu Uchokonolewe
Sehemu Ya Tano (5)
“Karibu sana mgeni, umesema anaitwa nani vile?” Dullah alijifanya kuhoji kwa umakini.
“Anaitwa Farida, ni dada wa kazi” Sarah akafafanua.
“Duh inawezekanaje mtoto mzuri hivi akawacha maisha ya kwao na kuja kufanya kazi za ndani?” Dullah akazungumza kwa mshangao.
“Hilo halikuhusu! Halafu mbona kama unamtamani?” Sarah alizungumza kwa jazba huku akijiinua kutoka kwenye kochi.
“Unakwenda wapi sasa?” Dullah alihoji.
“Subiri nikajisaidie kwanza, nikirudi utanieleza vizuri” Sarah alizungumza kwa hasira na kuondoka sebleni pale akituacha mimi na Dullah tukikodoleana macho.
“Siwezi kuamini kama wewe ni shetani kiasi hiki” Nikazunguma kwa jazba huku nikiangalia mlango wa chooni kuona kama Sarah hajatoka.
“Nimejua upo hapa na ndiomaana nimekufuata”
“Una shida gani na mimi?”
“Nakupenda Farida, nakupenda sana”
“Koma wewe!”
“Siwezi kukoma hadi nihakikishe nakuoa” Dullah mapenzi akazungumza kwa msisitizo.
“Sikiliza we mshenzi, Nilipo mimi hakuna mpango wowote wa kiovu unaoweza kufanikiwa” Nikazungumza kwa msisitizo.
“Kama kukupenda wewe ni uovu basi wacha niadhibiwe kwa kosa hilo”
“Kuadhibiwa utaadhibiwa tu wala usiombe, na mimi ndiye nitakayepelekea wewe uadhibiwe” Nikazungumza kwa hasira hasa baada ya kukumbuka maneno niliyoambiwa na Sarah kuwa ana mpango wa kudhulumu mali za Mwalimu James.
“Nipo tayari kwa adhabu utakayonipa kwasababu ninakupenda sana Farida” Dullah akazungumza huku akirambaramba midomo yake kwa nyodo.
“Acha uwongo mnafki mkubwa wewe! Unafikiri ufirauni wako utakufikisha wapi?” Nikazungumza.
“Najua kwanini unasema hivyo Farida lakini uelewe hao wote unaowafikiria sijawahi kufanya nao chochote kile”
“Laana kum!” Nikazungumza huku nikimeza funda la mate kwa jazba.
“Hauna sababu ya kumlaani mtu anayetaka kukusaidia” Sauti ya Sarah ilitugutusha mimi na Dullah kutoka kwenye mazungumzo yetu.
Dullah alishituka sana baada ya kusikia sauti ya Sarah ambaye hakuwepo muda wote ule. Alivuta pumzi ndefu na kuramba midomo yake huku akifumba fumba macho kwa aibu.
“Farida mama, mtu pekee wa kukusaidia katika kutimiza mipango yako ni huyu mwanaume” Sarah akazungumza maneno ambayo yalinishitua sana. Nilijiuliza amejuaje kama nilikuwa pale na mipango yangu?
“Unazungumzia mipango gani?” Nikahoji kwa hofu.
“Dullah wangu anaweza kwenda shuleni na kuwapanga walimu ukarudi na kuendelea na masomo yako” Sarah alizungumza maneno ambayo yalinipa ahuweni ndani ya moyo wangu. Kumbe hakuwa anafahamu mpango wowote niliokuwa nao ndani mle.
“Kumbe ulikuwa unasoma binti?” Dullah akahoji kwa mshangao kwasababu alikuwa amezoea kuniona mgahawani nikiuza ubwabwa wa Mama Halima.
“Huyu ni msomi baba. Ila kuna mshenzi mmoja amesababisha akafukuzwa shule halafu nyumbani nako akafukuzwa na wazazi wake” Sarah alizungumza bila hata breki na kumchanganya zaidi Dullah.
“Wazazi wake wamemfukuza?” Dullah akahoji huku akiamini kuwa mama yangu alikuwa ni mama Halima ambaye ni mama yake mkwe.
“Tena wamemfukuza kama paka mwizi!” Sarah akazungumza maneno yale na kusababisha maumivu makali sana ndani ya moyo wangu kwasababu alikuwa anazungumza ukweli pamoa na kwamba sikuelewa ni nani aliyekuwa amemueleza.
“Haiwezekani, wale watu wanawezaje kuwa na roho kavu kiasi hicho?” Dullah alizungumza kwa jazba huku akivuta taswira ya mama Halima na watoto wake jinsi walivyokuwa watu wema.
“We unazungumzia watu gani?” Sara akahoji kwa mshangao baada ya kumsikia Dullah akizungumza kama vile alikuwa ananifahamu saana.
“Wazazi wa huyu msichana” Dullah akaropoka na kujikuta nafsi yake ikimsuta kwa kuzungumza bila kufikiria.
“Kwahiyo unamfahamu vizuri Farida?” Sarah akahoji swali ambalo lilionekana kuwa gumu kidogo kwa Dullah.
“Nakuuliza wewe usinitumbulie macho kama panzi!” Sarah akahoji kwa jazba huku ametoa macho.
Wakati Dullah alipokuwa akitafakari jibu la kutoa tukasikia sauti ya mlango ukigongwa. Sote kwa pamoja tukahamishia mawazo yetu kwenye mlango ule.
Kwakuwa Sarah alishanieleza kuwa hata kufungua mlango na kukaribisha wageni lilikuwa ni jukumu langu hivyo nilivuta hatua kuelekea mlangoni.
“Wewe ngoja kwanza, Wacha kiherehere!” Sarah akanizuia huku akisogea dirishani na kuchungulia nje.
“Mungu wangu!” Sarah akahamaki huku akirudi nyuma na macho ameyakodoa kwa Dullah.
“Kuna nini?” Dullah naye kahoji kwa hofu na mashaka.
“Tumekwisha!” Sarah alijibu huku amejishika kiunoni na kajasho kakitiririka kwenye maotea ya nywele za utosini.
“Ni nani?” Dullah alizungumza huku akijiinua kutoka kwenye kochi.
“Njoo huku…” Sarah akazungumza huku akimuelekeza Dullah kuelekea chumbani.
Mlango uliendelea kugongwa, tena safari hiyo ulikuwa ukigongwa mfurulizo na kuzidi kuwachanganya wawili wale. Sarah alitaka kumshika mkono Dulah lakini kwa bahati mbaya ama nzuri Dullah alichomoka na kwenda kujibanza nyuma ya kochi pale pale sebleni. Sarah akabaki kama vile amepigwa na bumbuwazi asielewe kama uamuzi wa Dullah ulikuwa sahihi ama laa.
Wakati wote huo mimi nilikuwa nimetulia nikiwakodolea macho viumbe wale wawili jinsi walivyokuwa wakitapatapa ndani ya nyumba ya watu. Nilitikisa kichwa kwa masikitiko na kuachia tabasamu la hudhuni. Nikachukua maamuzi magumu ya kutaka kwenda kufungua mlango ule.
“Pisha huko!” Sarah akazungumza huku akinipiga kikumbo kidogo kwa ishara ya kunitaka nimpishe afungue yeye mlango ule. Sikuwa na kinyongo mtoto wa watu nikajiondokea na kuwaacha na balaa lao sebleni pale.
“Kwanini nagonga mlango muda mrefu hamnifungulii?” Nilisikia sauti ya Mwalimu James ikihoji kwa msisitizo.
“Nilikuwa nimepitiwa mume wangu kipenzi” Sarah alizungumza kwa sauti ya kudeka huku akifikicha macho na kupiga miayo mirefu kuashiria kuwa alikuwa amelala.
“Kwani ulikuwa umelala kama kawaida yako?”
“Leo sijisikii vizuri mpenzi wangu” Sarah alizungumza kwa kulalamika huku akimkumbatia Mwalimu James na kumpiga busu shingoni.
“Vipi unaumwa?”
“Hapana nilikuwa nimekumisi sana leo mpenzi wangu. Unajua haujanipa tangu juzi!” Sarah akazungumza kwa ile sauti yake ya kudeka.
“Farida yuko wapi?” Mwalimu James alihoji huku akielekea kwenye kochi ambalo Dullah alikuwa amejibanza nyuma yake na kuketi kwa kujitupa.
“Yaani mi nazungumza na wewe halafu unamuulizia mtu mwingine!” Sarah akazungumza kwa kulalamika huku akiwa amesimama na mikono ameiweka kiunoni.
“Njoo ukae hapa wacha kelele zako” Mwalimu James akazungumza kwa sauti ya chini baada ya kumuona Sarah amekasirika.
“We jishaue tu” Sarah akazungumza huku akijiweka kwenye mapaja ya Mwalimu James.
“Wivu utakuua we mtoto”
“Mi nina hamu zangu hapa halafu unanizingua” Sarah akalalamika kwa sauti ya deko.
“Kwahiyo unataka?”
“Nataka ndio swali gani hilo sasa” Sarah alizungumza huku akimkamata Mwalimu James kichwa na kumpiga mabusu mfurulizo.
“Ngoja kwanza Sarah”
“Ningoje nini?”
“Farida akituona unajua itakuwa sio vizuri”
“Farida ndio nani hadi azuie starehe zetu? Nataka sasa! Tena unipe hapahapa” Sarah akazungumza kwa msisitizo huku akimkumbatia zaidi mwalimu James.
Kwakuwa Mwalimu James alikuwa anamfahamu vyema Sarah kuwa alipokuwa amepandwa na mapepo yake wakati wa majambozi hakuna lugha aliyokuwa anaielewa zaidi ya kumpatia dozi baaasi. Hivyo alimpindua kumkalisha kwa kumuweka katikati ya mapaja yake, wakawa wanatazamana huku mikono ya Mwalimu ikiwa imekamata barabara kiuno cha binti yule.
“Nataka leo unipe dozi hadi Farida asikie wivu” Sarah akazungumza huku akijipinda na kumkamata mwalimu maeneo ya shingoni. Alimvutia kwake na kumdaka kwa lipsi mbili za midomo yake huku taratiiibu mkono wa kushoto ukiteremka chini kwa kuambaa ambaa usawa wa uti wa mgongo.
Mwalimu James alifumba macho na kuuma midomo ya chini kwa meno yake ya juu kisha akasafirisha mikono yake hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maembe na kuchagua mawili ambayo aliyatomasa kama vile anapima kujua kama yameiva au mabichi.
“Oshssss….Aaaaaaah!” Sarah akatoa sauti ya kulalamika huku akikaza macho kule nyuma ya kochi kujaribu kuwasiliana na Dullah.
“Sarah alipitisha mikono yake katikati ya miguu ya Mwalimu James na kukamata zana kwa vidole vyake akawa anazisugua kwa staili ya mzunguuko wa pia huku akijibinuabinua pale kwenye mapaja ya Mwalimu wake na sauti za miguno ya mahaba zikizidi kumpagawisha mwanaume wa watu akawa kama mlevi wa gongo.
Sauti na miguno ya mahaba kutokea pale sebleni zilinifanya nichungulie kuona kilichokuwa kinaendelea kati ya watu wale watatu niliokuwa nimewaacha. Nikajikuta nimebaki mdomo wazi baada ya kumuona Sarah akiwa anajishebedua kweye mapaja ya Mwalimu James juu ya kochi ambalo nyuma yake alikuwa amejificha Dullah mapenzi.
Nilimshuhudia Sarah alivyokuwa akihangaika kumpa ishara Dullah ya kuchomoka kutoka pale kwenye lile kochi. Nikameza funda la mate na kuramba midomo yangu kwa ncha ya ulimi. Nikaona ule ndio ulikuwa muda muafaka wa kuwaumbua Sarah na Dullah wake kisha kuweka wazi hila na njama zao kwa familia ya Mwalimu James.
Kwa haraka sana nikatembea kwa kunyata hadi mlangoni na kufunga mlango kwa funguo kisha nikazichomoa na kuondoka nazo pasipo mtu yeyote yule kuona nilichokuwa nimekifanya.
Masikini ya Mungu Mwalimu James alikuwa amepumbazwa vya kutosha akawa kama vile msukule asiyejielewa wala kujitambua. Dullah alifuata maelekezo ya Sarah na kujichomoa kutoka pale nyuma ya kochi na kuuendea mlango wa kutokea nje kwa spidi. Hakika hakuna kikwazo kisicho na ufumbuzi, hata Dullah mwenyewe hakuwa anaamini kama siku hiyo Mungu aliendelea kuwa upande wake.
Mawazo na matumaini ya Dullah yalitoweka ghafla baada ya kukamata kitasa cha mlango ule na kukinyonga. Laa haula! mlango ulikuwa umefungwa na funguo haikuwepo mlangoni pale. Ingekuwepo vipi wakati mjukuu wa Subuhana nilikuwa nimeshauchomoa na kutoweka nao kusikojulikana.????
“Unazubaa nini fungua mlango utoke” Sarah alimueleza Dullah kwa Ishara baada ya kumuona amezubaa mlangoni pale.
“Funguo ziko wapi?” Dullah alihoji kwa ishara huku akihangaika mlangoni pale kutafuta funguo.
“Hapohapo babe…Angalia tara..tara…tiibu uta..uta..toka hapooo” Sarah alipaza sauti na kuzungumza kwa Mahaba akijifanya kupagawishwa na mikono ya Mwalimu James kumbe alikuwa anazungumza na Dullah.
Dullah alikuna nywele zake huku akionekana kuchanganyikiwa kwa kitendo kile cha kushindwa kutoka ndani ya nyumba ile. Alipotupa macho usawa wa malngo wa jikoni, aliniona nimeushika ufunguo ule kwenye mkono wangu nikiutikisa kwa nyodo huku niking’ata midomo yangu kwa kebehi.
“Mungu wangu, Farida nisaidie nitoke rafiki yangu” Dula alizungumza kwa ishara huku akiweka mikono yake kifuani kuashiria kuomba radhi.
Niliachia tabasamu la furaha na kugeuza macho yangu kuwaangalia Mwalimu na mwanafunzi wake walivyokuwa wakiendelea kupagawishana kiwizi wizi.
“Babe kamata juu na…na chiniiii..halafu…halafu vuta yote miwili uta.uta..utanimalizaa! Oooh nenda…Nenda sasaaaa!” Sarah aliendelea kuzungumza kwa kulalamika huku akijibinuabinua na macho ameyakodoa mlangoni alipo Dullah akijifanya kumuelekeza Mwalimu James jinsi ya kucheza na yale maembe mawili kumbe anamuelekeza Dullaha kufungua milango yote miwili kwa pamoja.
Dullah alimtazama Sarah aliyekuwa amepakatwa kisha akarejesha macho kwangu na kufumba macho kwa nguvu huku akikuna nywele za nyuma ya kichwa chake kuashiria ugumu wa mambo yaliyokuwa yakimkabili kwa wakati huo.
Pale nilipokuwa nimesimama nilikuwa nimebanwa na kicheko kutokana na kile kilichokuwa kinawakabili Sarah na Dulah wake.
“Shenzi! Mchezo wenu umeishia hapa leo” Nikazungumza kwa sauti ya chini huku nikihisi amani ndani ya moyo wangu kwa kufanikisha zoezi langu la kukwamisha Sara na Dullah kwa urahisi pasipo hata kutumia nguvu.
“Chini juu Babe…Chini na juu… vuta…vuutaaah! Hapo..Hapooo Hapo sasa!” Sarah aliendelea kujilalamisha kwenye mapaja ya Mwalimu James.
Dullah alipofumbua macho aligeuka kwenye mlango na kufungua komeo ya juu kisha akainama na kufungua komeo ya chini. Alikamata kitasa cha mlango ule na kukivuta kwa nguvu. Sikuweza kuamini macho yangu ndugu msomaji, milango yote miwili ikaachiana na kutoa nafasi kwa Dullah Mapenzi kujinasua kwenye mtego wagu.
*****
Kile kitendo nilichokuwa nimekifanya cha kuchomoa ufunguo wa mlango ili Dulah asitoke kilimuudhi sana Sarah na kuongeza chuki zaidi kwangu.
Nakumbuka niikuwa nimepanda kwenye stuli nikifuta vumbi kwenye madirisha kwa kitambaa huku nikiwaza namna ya kukamilisha mpango wetu mimi na mzee Makwacha, lakini pia kukwamisha mpango wa Sarah na Dulah wa kufirisi mali za Madam na Mwalimu James.
“We kunguni shuka hapo!” Sauti ya Sarah ilinigutusha na kunifanya nigeuge kumuangalia.
“Usinitumbulie mimacho yako shuka hapa!” Sarah akazungumza kwa jazba.
“Lakini Sarah kwanini unakuwa mkorofi?” Nikazungumza kwa sauti ya kualamika.
“Utashuka au husuki?”
“Zungumza tu nakusikiliza” Nilimueleza huku nikiwa nimesimama pale pale juu ya stuli.
“Kwanini jana ulifunga mlango?”
“Mlango gani?”
“Usijichetue, Kwanini jana ulichomoa funguo ili Dullah asitoke? Lengo lako lilikuwa ni lipi hasa?” Sarah akahoji kwa jazba na kunifanya niangue kicheko kiasi cha kushuka pale nilipokuwa nimepanda ili nisidondoke.
“Unacheka! Kwahiyo umefurahishwa na utumbo ulioufanya?”
“Subiri Sarah! Unajua unanichekesha sana” Nilizungumza huku nikicheka.
“Kwahiyo unajiona mshindi”
“Siwezi kujiita mshindi kwasababu sijashindana. Na kama ningetaka kushindana hakuna ambaye angenishinda” Nikazungumza huku nikicheka.
“Sasa nakushauri kaa pembeni katika hili. Na kama utaendelea kunifuatilia nitakufanya kama nilivyokufanya kule shule” Sarah alizungumza maneno ambayo yalinikumbusha jinsi nilivyofukuzwa shule na kuishia kuwa chokoraa wa mtaani nisiye na mbele wa la nyuma.
“Vipi mbona umekaa kimya nimekugusa penyewe enh?”
“Sikiliza Sarah, tambua kuwa utalipa kwa kila tone la dhambi uliyonitendea.” Nilijikuta nikizungumza kwa msisitizo huku nikitetemeka kwa hasira.
“Vipi mbona umepaniki mpendwa?”
“Na kwa hili nitahakikisha nasambaratisha mpango wenu wewe na huyo kinyago mwenzio” Nikazungumza kwa msisitizo.
Maneno yangu yaligeuka na kuwa kichekesho kwani Sarah aliangua kicheko na kucheka sana zaidi ya hata vile nilivyokuwa nikicheka mimi. Nikabaki nikimtumbulia macho kwa mshangao.
“Unajua wewe binti ni mjinga sana” Akazungumza Sarah huku akifuta machozi yaliyosababishwa na kile kicheko chake.
“We chekelea tu lakini muda si mrefu utalia na kusaga meno” Nikamweleza kwa msisitizo.
“Umechelewa mama, tena umechelewa sana mpenzi. Yaani ulichofanya wewe ni kuzima moto kwa petrol” Sara akazungumza kwa kujiamini.
“Nakushauri uachane na ndoa ya Madam, kinyume na hapo hautoamini kwa nitaachokufanyia” Nilizunguma kwa hasira na uchungu mkubwa hasa ukizingatia Madam alikuwa ni mtu mwema kabisa.
“Nakusikitikia sana binti, laitani ungejua ungeungana tu na mimi” Akazungumza kwa kebehi huku akirembua vile vijicho vyake kama goroli.
“Sasa jiandae kutoka humu ndani! Nitahakikisha nakung’oa kunguni wewe!” Nikazungumza kwa jazba na hasira.
“Tutaona mimi na wewe nani atango’ka na kumuacha mwenzake” Sarah naye akazungumza huku akibinua midomo yake kwa kebehi.
“Tena umwambie huyo sisimizi wako siku akitia mguu ndani ya nyumba hii hatokaa aamini” Nikazunguma kwa msisitizo.
“Utamfanya nini?”
“Kwanini tuandikie mate? Wewe mlete utajionea kwa macho yako”
“Karagabaho na ubwezi wako! Yaani umekuja jana tu tayari umeshaota mapembe unazungumza na bosi wako utafikiri mtoto mwenzio?” Sarah alizunguma kwa kebehi huku akionekana kujawa na hasira kutokana na maneno yangu.
“Bosi Bongo! Naomba uniache nimalizie kazi yangu mimi muda wa Madam kurudi umefika” Niliunguma kwa kujiamini huku nikipanda pale kwenye stuli kwaajili ya kumalizia shughuli yangu.
Nilifanya kazi huku nikiwa na hasira utafikiri nimetukaniwa mama yangu mzazi. Katika akili yangu niliapa kuwaumbua wawili wale na ikiwezekana niwachome kabisa na Sarah afukuzwe ndani ya nyumba ile kabla mambo hayajawa mabaya.
Nilipomaliza usafi wa sebleni nikaelekea jikoni kwaajili ya kuandaa kinywaji cha jioni. Akili yangu ilikuwa ikifanya kazi kwa nguvu sana juu ya kuhakikisha naokoa ndoa ya Mwaimu James kutoka mikononi mwa Sarah na Dullah.
“Vipi bibi inamaana husikii mlango unavyogongwa?” Sauti ya Sarah ikanigutusha kutoka katika lindi la mawazo. Niligeuka na kumtazama kwa umakini mkubwa.
“Usiniangalie nenda ukafungue mlango bwana!” Sarah alizunguma kwa msisitizo huku akionekana kukereka.
“Sarah si unaona nina kazi kwanini usiende kufungua tu?” Nikahoji kwa sauti ya upole.
“Sio jukumu langu, kama huwei liache bosi lako lilale nje hadi mwalimu atakaporudi ndio nitawafungulia” Sarah alizunguma na kuondoka.
Nilipokuwa nikielekea mlangoni nilimkuta Sarah amaeketi sebleni akiangaia runinga. Nikatoa msonyo kwa hasira kisha nikakamata kitasa cha mlango na kunyonga funguo.
“Mbona leo mmechelewa sana kufungua mlango?” Alihoji Madam Manka mara tu nilipofungua mlango.
“Shikamoo Madam” Nilimsalimia huku nikipokea mfuko mdogo aliokuwa ameuning’iniza.
“Vipi umeshazoea sasa. Huyu cha uvivu anakusaidia lakini au kazi zote amaekuachia mwenyewe?” Madam alihoji huku akivua viatu na kuvisukuma pembeni na pochi yake akaitupa kwenye kochi.
“Shikamoo Madam” Sarah alidakia aliposikia swali la Madam.
“Kama kawaida yako Chauvivu wangu, umetulia tu mwenyewe unaangalia TV” Madam alimsemesha Sarah
“Kwa raha zangu, nipo kwa kaka yangu kwani kuna shida gani” Sarah akajibu huku akiketi vizuri na kubadilisha chaneli ya runinga.
“Sio vizuri hivyo wifi yangu. Uwe unamsaidia mwenzio kazi bwana. Sasa wewe ukikaa unakaa tuuu!” Madam alilalamika huku akiwa amesimama karibu na mlango.
“Madam na wewe ukisharudi tu hata panya watapata taarifa. Kazi tumeshamaliza na ndio maana nimepumzika” Sarah akazungumza kwa kulalamika.
“Eti Farida huyu anakusaidia kazi kweli?” Madam akahoji huku amenikodolea macho.
“Ndio Madam, huwa tunafanya kazi pamoja” Nikamtetea mshenzi yule.
“Haya nimewaletea msaidizi mwingine, tena safari hii nimeleta kidume cha nguvu!” Madam akazungumza huku akichungulia nje. Kumbe alikuwa ametangulizana na mtu.
Kauli ile ya Madam ilitugutusha mimi na Sarah na kutufanya tutumbue macho kule mlangoni kumuona huyo msaidizi aiyekuwa ameletwa ndani ya nyumba ile.
Kwa upande wangu nilifurahi sana na kuhisi amani ndani ya moyo wangu. Niliamini nimepata mtu wa kusaidiana naye katika kufanikisha mikakati yangu ukiwemo ule wa kukwamisha mpango wa Sarah na Dullah wake. Nikageuza macho yangu na kumuangalia Sarah kwa nyodo kisha nikaachia tabasamu la kebehi kabla ya kurejesha macho yangu mlangoni.
“Karibu mgeni pita ndani” Madam alizungumza kwa sauti ya upendo kama iivyokuwa kawaida yake kuwakarimu wageni.
Lile tabasamu langu liliyeyuka ghafla na kujikuta nimebaki mdomo wazi baada ya kuiona sura ya mgeni mwenyewe. Nikavuta pumzi na kuziachia kisha nikapeleka mkono wangu kichwani na kukuna nywele za kisogoni. Nilipomtazama Sarah nikamuona mwenzangu amejawa na tabasamu la furaha.
“Karibu uketi kwenye kochi na ujisikie upo nyumbani” Madam Manka akamkaribisha Dulah ambaye kwa wakati huo alikuwa akionekana kuwa mgeni na mnyenyekevu wa hali ya juu kwa Madam.
“Nashukuru Madam kwa kusikia kilio changu” Sarah alizungumza huku akionekana kufurahishwa na ugeni ule.
“Najua wewe ni cha uvivu wifi yangu na ndiomaana kila kukicha unahitaji msaada. Haya sema jengine nikupatie” Madam akazungumza huku akijiweka kwenye moja ya makochi pale sebleni.
“Tatizo unanipenda sana hadi mwenyewe nafahamu hilo. Hata kaka James hawezi kunifanyia mambo unayonifanyie wewe” Sarah alizungumza kwa sauti ya kudeka huku akiniangaia kwa pembe ya jicho.
“Farida keti nikutambulishe kwa mgeni. Mbona umesimama kama ziginari?” Madam alizungumza kwa sauti ya upendo.
Nilimeza funda la mate kisha nikavuta hatua na kwenda kuketi kwenye kochi la peke yangu huku nikiwa nimepigwa na putwaa kutokana na tukio lile.
“Huyu anaitwa Farida ni mdogo wangu anatusaidia kazi za humu ndani. Yeye ni mpole sana na ana moyo wa kipekee” Madam alimtambulisha Dullah kwangu.
“Nashukuru kukufahamu Fa..Fa..Faaa Nani vile?” Dulllah akajifanya kushindwa kulikumbuka jina langu kunguni yule.
“Farida bwana mbona jina simpe tu” Sarah akadakia.
“Ahaa Nashukuru kukufahamu dada Farida” Dulah akazungumza kama vile hakuwa ananifahamu hata kidogo.
“Nahuyo ni wifi yangu anaitwa Agness” Madam akamtambuisha Sarah kwa lile jina bandia.
“Hata ukiniita Agie sio mbaya” Sarah akadakia huku akicheka na kuniangaia kwa lile jicho lake la kebehi.
“Mzoee huyo ndivyo alivyo, kuzoeana na mgeni ndani ya dakika moja ni kawaida yake. Hata hivyo uchangamfu wake unaninogea sana!” Madam akaungumza kwa bashasha huku akimmwagia masifa Sarah Mungu wangu pasipo kufahamu kuwa alikuwa akijipalia makaa ya moto mwenyewe.
“Mimi ndio Agiee Mama Lao, mama mwenye nyumbaaa” Sarah akazungumza kwa lengo la kunichoma mimi.
“Jamani huyu anaitwa Dullah. Ni kijana mchapakazi mwaminifu na anampenda Mungu” Madam alizungumza maneno ambayo yalikuwa ni kinyume kabisa na ukweli kuhusu Dulah. Nikameza funda la mate kisha nikaachia tabasamu la kujilazimisha ili Madam asielewe hali ya wasiwasi niliyokuwa nayo dhidi ya yule mgeni wake.
“Kwahiyo atakuwa analala hapahapa?” Nikahoji kwa umakini huku nikiwa na wasiwasi ndani ya moyo wangu kutokana na jambo la hatari alilkuwa akilifanya Madam Manka.
“Hapana, Dullah atakuwa anakuja asubuhi anafanya kazi zake na ikifika jioni anaondoka” Madam alieleza.
“Kwanini asiwe analala hapa hapa?” Sarah akahoji kwa umakini mkubwa swali ambalo halikuwa na usalama hata kidogo kwa upande wangu.
“Kaka yenu amependekeza hivyo. Lakini hakujaharibika kitu tutajua namna ya kufanya” Madam akaungumza kwa umakini mkubwa.
“Lakini Madam mbona kazi za hapa sio nyingi kihivyo?” Nikahoji kwa mshangao.
“Hapana Farida, Unajua katika maisha yangu huwa sipendi kuona mtu anateseka kwa sababu zisio za msingi” Madam akaeleza.
“Lakini sidhani kama kuna mtu alikuwa anateseka Madam” Nikazungumza kwa umakini mkubwa.
“Wifi yangu ameomba nimtafute mtu wa kusaidiana nanyi kazi. Kwakuwa namthamini sikuona sababu ya kupinga wazo lake” Madam akazungumza kwa sauti ya upendo.
“Kupendwa raaaha!” Sarah akazungumza kwa sauti huku ameinua sura juu na kufumba macho kwa hisia.
“Kaone kanavyodeka utafikiri katoto ka paka” Madam akazungumza kwa masihara.
“Wacha nideke mwenye wivu wajinyonge my wiii!” Kaka zidi kujishaua Kasarah.
“Na watajinyonga wengi maana sio kwa kukupenda huku!” Madam naye akasisitiza upendo wake kwa Sarah.
Kusema kweli ndugu msomaji akili yangu haikuwa sawa kabisa kutokana na kile kilichokuwa kikiendelea wakati ule. Yaani nilikuwa nimevimba kwa hasira kiasi cha kuhisi kupasuka.
Nilipata wazo la kumwaga ukweli palepale walipo wote watatu ili kuweza kumuokoa Madam kutoka kwenye mtego wa tumbili wale wawili. Nikavuta pumzi na kuziachia kisha nikameza funda la mate tayari kwa kupasua jipu!
“Lakini Madam..huyu Dullah…” Nikataka kufunguka.
“Kwahiyo Madam Dullah wetu ataana kazi leo au hadi lini?” Sarah akadakia na kunikatisha nilichokuwa nataka kukizunguma.
“Leo mtampa maelekezo ya kazi, nafikiri kesho itakuwa vyema akaanza rasmi. Au unasemaje Farida wangu?” Madam akahoji.
“Swadakta Kipenzi Madam, leo tutampa malekezo halafu kesho ataanza rasmi” Sarah akadakia juu kwa juu wakati ambao nilikuwa nimebaki mdomo wazi kwa mshangao.
“Ila ninatoa angalizo mabinti zangu, huyu kijana nimefahamiana naye muda mrefu. Ni kijana anayejielewa na kujiheshimu sana. Sasa naomba heshima ichukue mkondo wake, sio siku mbili tatu mnaanza vimaneno maneno vya uchonganishi” Madam akazungumza kwa msisitizo maneno ambayo kwa upande wangu yalikuwa ni magumu mno. Nikajikuta nashindwa kulitoa la moyoni kama nilivyoamua awali.
“Kwa upande wangu hautosikia maneno ya uchonganishi kuhusu kaka…kaka…kaka nani vile?” Sarah alizungumza na kujifanya kusahau jina la Dullah.
“Naitwa Dullah”
“Sijui mwenzangu Farida ” Sarah akazungumza kwa kunitupia mpira huku akinitupia jicho la kebehi.
“Farida sina wasiwasi naye, namuaminia hanaga upuuzi” Madam akazungumza huku akijiinua kutoka kwenye kochi na kuokota pochi yake.
“Sasa nyie endeleeni kuzoeana na mgeni, mimi ngoja nikajimwagie maji ya baridi” Madam akaungumza na kuvuta hatua kuelekea chumbani mwake.
Sarah akawa ameketi huku akichezesha midomo yake na kunikodolea macho kwa kebehi na dharau.
“Vipi Bibie umekula au umeliwa?” Sarah akahoji huku akijitikisa kwa nyodo.
“Nyie watu mna laana” Nikazungumza kwa jazba.
“Huu ni moto mwengine bibie cheza nao mbali” Sarah akazungumza kwa kebehi.
“Kwani kuna nini jamani?” Dulah akahoji kwa umakini.
“Huyu kunguni anajaribu kuingilia mipango yetu” Sarah alizungumza.
“Farida hawezi kufanya hivyo Dear, labda kama hujamuweka sawa” Dullah akazungumza kwa kujiamini.
“Dullah huyu ni kichwa ngumu mpenzi wangu. Inahitajika nguvu ya ziada hadi aelewe tunachokifanya” Sarah akaungumza kwa msisitizo.
“Farida kwanini usiungane na sisi katika jambo letu? Tukifanikiwa tutaishi kwa raha sana mpendwa” Dullah alizungumza kwa sauti ya kusihi.
“Mpango gani?” Nikahoji kwa kiburi.
“Tunataka kusambaratisha ndoa ya Mwalimu James” Dullah akazungumza kwa msisitizo.
“Naombeni mniache, tena mniache kabisaa! Na kama mkiendelea na mipango yenu ya ajabu ajabu nitaweka wazi kila kitu kwa Madam” Nikazunguma kwa msisitizo.
“Kama umeshindwa kuweka wazi leo, utaweza lini?” Sarah akahoji kwa kebehi.
“Sijashindwa ila nimeamua kuwaweka akiba tu” Nikajibu.
“Kumbuka kuwa Madam ametuonya kuzungumza maneno mabovu kuhusu Dullah!” Sarah akazungumza kwa umakini huku akinitazama kwa ncha ya jicho.
“Madam ananiamini kuliko mtu yeyote hapa chini ya jua. Hivyo usijisumbue kwa lolote lile, ukweli ni kwamba mpango wetu utabaki palepale” Dullah alizungumza maneno ambayo yalinikatisha tamaa lakini pia yaliniumiza sana.
“Kwa taarifa yako huyo Madam wako ataiona nyumba chungu hii na ataondoka mwenyewe akituacha mimi na Mfalme wangu tukitawala. Au sio Baba?” Sarah alizungumza huku akimpiga busu Dullah.
“Farida mpenzi usipokuwa makini yanaweza yakakukuta mazito yasiyo elezeka” Dullah akakazia maneno ya Sarah huku akinitazama kwa jicho la onyo.
Nilivuta pumzi na kuziachia kwa mkupuo kisha nikajiinua kutoka pale nilipokuwa nimeketi na kuondoka nikiwaacha mashetani wale wakiangua kicheko cha kebehi.
****
Mzigo wa mawazo na maumivu ndani ya moyo wangu vilizidi kunitesa kadri siku zilivyokuwa zikisonga. Kila nilivyokuwa nikitafakari suluhisho la tatizo nililiona linanipiga chenga. Baada ya kuwaza sana nikapata wazo na kumeza funda la mate huku nikitabasamu kwa matumaini.
Nilitoka chumbani kwangu mbio na kuelekea bustanini ambako Dullah alikuwa akipalilia maua.
Dullah aliponiona akaacha shughuli yake na kunikodolea macho kwa mshangao kutokana na vile nilivyokuwa nikikimbia kuelekea kwake huku nikihema juu juu.
“Dullah naomba simu yako!” Nilizungumza mara tu nilipofika pale.
“Ya nini?” Akahoji kwa mshangao kwasababu tangu siku ameingia ndani mle sikuwa na stori naye.
“We nipe bwana nina kazi nayo” Nikazungumza kwa sauti ya kudeka huku nikipiga piga miguu chini na shingo nikiipindua pindua.
“Mbona kama unanifokea sasa?”
“Haya nipo chini ya miguu yako kaka mpenzi” Nikazungumza kwa sauti ya upole huku nimekutanisha viganja va mikono yangu kifuani kuashiria hitaji la huruma yake.
“Kwahiyo leo unaniita mpenzi kwasababu una shida sio?” Dullaha akahoji kwa masimango.
“Nitakuita mpenzi leo, kesho, keshokutwa na milele amina” Nikazungumza huku nimejikunyata kwa unyeyekevu.
“Inaonekana ni simu nyeti sana, mbona unaisujudia kiasi hicho?” Dullah akahoji kwa umakini.
“Ni kweli mpenzi ni simu ya msingi sana” Nikajikuta nikizungumza pasipokujitambua.
“Unataka kumpigia nani?” Dullah akahoji kwa umakini mkubwa.
“Aaam…aaa. Kuna mtu nataka kuzungumza naye”
“Funguka unataka kumpigia nani? Kama utaendelea kuficha sikupi”
“Lakini hakuna umuhimu wa wewe kumfahamu mpenzi Dullah”
“Sawa nakupa lakini sharti ni kwamba uzungumze hapahapa” Dullah alinipa sharti huku akiingiza mkono mfukoni na kuchomoa simu. Nikameza funda la mate huku nikivuta pumzi ndefu.
Siku zungumza neno lolote zaidi ya kupokea simu ile na kuingia namba haraka haraka.
“Salio limo la kutosha humu?” Nikahoji nilipokuwa nikiendelea kuandika namba za simu.
“We piga nipo full mafuta” Dullah akajibu kwa kujidai.
Baada ya kuandika namba niliweka simu sikioni na kusikia inaita. Nilivuta tena pumzi ndefu na kuramba midomo yangu kwa ncha ya ulimi.
“Halloo….” Sauti ya Babu Makwacha ikasikika kwenye spika ya simu.
“Eeh ndio shikamoo..” Nikajibu huku nikivuta hatua kusogea pembeni.
“Wewe unakwenda wapi sasa?” Dullah akahoji kwa mshangao baada ya kuona navuta hatua kuondoka. Niligeuka na kumtuliza kwa mkono nikimpa ishara ya kutulia palepale alipokuwa.
Dullah hakuwa amefurahishwa na kile kitendo. Akawa ananifuata lakini ghafla akasimama na kuniacha niendelee na mazungumzo yangu. Niliachia tabasamu na kwenda kujibanza pembezoni mwa ukuta.
“Shikamoo Mkuu…” Nikamsalimia mzee Makwacha kwenye simu kwa kumuita mkuu.
“Vipi kazi inaendeleaje komando wangu?”
“Mambo ni magumu Mkuu” Nikazungumza
“Kuna tatizo lolote?”
“Madam amemuajiri yule kijana anayetaka kusambaratisha ndoa yao”
“Kwahiyo?”
“Naona kama nguvu yao imeongezeka mara dufu, sidhani kama nitafanikiwa kuokoa ndoa ya Madam na Mwalimu James” Nikazungumza kwa hisia kali na masikitiko makubwa huku nikigeuka nyuma kuhakikisha Dullah yupo mbani na mimi.
“We mpumbavu nini! Unaacha kilichokupeleka hapo unavamia mambo yasiyokuhusu!” Mzee Makwacha akazungumza kwa hasira na jazba.
“Lakini….”
“Lakini nini Binti?”
“Kwanini nisimsaidie yule mwanamke asiye na hatia?” Nikahoji kwa umakini mkubwa huku nikionekana kuumia kutokana na tatizo lile.
“Nimekwambia hayakuhusu Farida fanya kazi yako!”
“Lakini mkuu..”
“Hakuna cha lakini, nataka ripoti ya kazi ndani ya masaa 24 tuu!” Sauti ya Mzee Makwacha ikazungumza kwa kuunguruma kiasi cha kuniogofya.
“Masaa 24 Boss?” Nikahoji kwa kuhamaki na mshangao wa hali ya juu.
“Ndio, hautakiwa kuendelea kuishi hapo baada ya masaa 24 kuisha.” Mze akasisitiza.
“Sasa kama nimeshindwa siku zote hizo, nitaweza ndani ya masaa 24 kweli Babu?” Nikahoji kwa umakini mkubwa.
“Sitaki kujua utawezaje. Ninachokitaka ni kukukabidhi kwa wazazi wako leo ama kesho” Mzee yule akazungumza kwa msisitizo.
“Sawa Mkuu nitajitahidi” Nikajibu kwa shingo upande huku ndani ya moyo wangu nikiwa sijaridhika kabisa.
“Hiyo unayotumia leo ni simu ya nani?”
“Ya huyo kijana niliyekwambia”
“Ukishakata hakikisha unafuta ushahidi kwenye hiyo simu”
“Sawa mkuu” Nikajibu kwa unyenyekevu na kukata simu huku nikipumua kwa nguvu na kujaribu kuyatafakari maneno ya mzee yule.
Ghafla nikashituka kusikia sauti ya mtu akipiga makofi kutokea hatua chache na pale nilipokuwa nikizungumza na simu. Nilipogeuza macho yangu nikakutana uso kwa uso na Sarah.
“Hongera sana Binti” Sarah akaungumza huku akiwa amejishika kiuno na kunitazama kwa makini usoni
“Umetokea wapi?” Nikahoji kwa mshangao na hofu kubwa nikiamini binti yule alikuwa ameyanasa maungumzo yangu mimi na mezee Makwacha.
“Kumbe hata wewe una Boss? Okay ni vizuri na inapendeza sana” Sarah alizunguma huku akivuta hatua kunisogelea zadi.
“Unazungumza kuhusu nini Agie”
“Mimi siitwi Agie acha unafki!”
“Sawa kwaheri…” Nilizungumza na kugeuka kutaka kuondoka mazingira yale ambayo kwa wakati ule kwangu hayakuwa salama tena.
“Njoo hapa unakwenda wapi?” Sarah akazungumza na kunivuta blauzi kwa nyuma.
“Sarah acha ukorofi ujue!” Nikazungumza kwa jazba.
“Naomba hiyo simu” Sarah akazungumza kwa amri na kunifanya nikumbuke maagizo ya mzee Makwacha kuwa nikimaliza kuzungumza nifute namba zake kwenye simu ile.
“Simu ya nini?” Nikahoji kwa jazaba.
“Sitaki maswali lete hiyo simu dogo”
“Achana na mimi wewe!” Nikazungumza kwa hasira huku nikigeuka tena kutaka kuondoka.
Nilishitukia nikivamiwa na kusukumwa kwa nguvu sana hadi nikapepesuka na kuanguka chini. Masikini ya Mungu kwakuwa sikuwa nimejiandaa nikajikuta nimeiachia simu ikadondokea hatua kadhaa kutokea pale nilipokuwa nimelala mimi.
Sarah akatembea kwa mwendo wa taratiibu huku akinitazama na kuachia tabasamu la kebehi.
“Nilipokwambia tuungane ulikataa. Kumbe upo hapa kwa kazi ya kusambaratisha mpango wetu sisi, heti Dada wa kazi?” Sarah akahoji kwa kebehi huku akiokota simu ile na midomo yake akiiuma kwa meno ya juu na kuifyatua kwa mbwembwe.
“Vipi unaogopa nitamfahamu Bosi wako?” Sarah alizungumza huku akiwasha ile simu na kufungua kiboksi cha kuhifadhia kumbukumbu ya simu zilizoingia na kutoka.
“Naomba hiyo simu Sarah” Nikazungumza kwa msisitizo huku nikijiinua na macho nimeyatoa utafikiri naingiza uzi kwenye sindano ya kushonea nguo.
“Nina kazi nayo” Akanijibu huku akivuta hatua kurudi nyuma na vidole pamoja na macho vikishirikiana kutafuta namba nilizotumia kwenye simu ile.
“Ukimaliza utaipeleka kwa Dullah” Nikazungumza na kuvuta hatua kuondoka bila ya hofu wala mashaka.
Kumbe Sarah aliponisukuma Dullah alikuwa anatuangalia. Hivyo baada ya mimi kuondoka tu naye akafika pale alipokuwa amesimama Sarah.
“Vipi Babe kipi kimejiri maana nimekuona ukikasukuma na kukanyang’anya simu” Dullah akazungumza kwa umakini.
“Haya yote umeyataka wewe Dullah sijui ni kademu kako?” Sarah akazungumza kwa kulaumu huku akionekana kukata tamaa.
“Nimefanya nini sasa?”
“Kwanini umempa simu huyu mshenzi?”
“Amesema kuna jambo la msingi sana alikuwa anataka kuzungumza na mtu”
“Huo msingi ulikuwa unachimbiwa wewe uzikwe mzima mzima” Sarah alizungumza kwa ghadhabu.
“Farida hawezi kuwa na ubavu huo!”
“Sasa kwa taarifa yako Farida ni shushushu!”
“Unasemaje?”
“Wewe upo kazini Farida naye yupo kazini. Mbaya zaidi kazi yake ni kutusambaratisha mimi na wewe” Sarah akazungumza kwa msisitizo.
“Sarah mbona unazungumza maneno makali hivyo kwa mtoto wa watu?” Dullah akashangazwa na taarifa ile.
“Nimemsikia kwa masikio yangu akimwambia mtu kuwa uwepo wako wewe unamletea ugumu wa kazi yake”
“Hebu lete hiyo namba tuione” Dullah alizungumza huku akinyoosha mkono kuchukua simu yake kutoka kwa Sarah.
“Namba gani?”
“Namba ya huyo mtu aliyekuwa anazungumza naye”
“Hakuna kitu, ameshafuta” Sarah alijibu huku amkimabidhi simu Dullah.
“Kama amefuta namba inawezekana kweli akawa ni tatizo” Dullah akazunguma kwa mashaka huku akipitia kwa makini kuangalia namba zilizoingia na kutoka kwenye simu yake.
“Tunatakiwa kuwa makini sana. Vinginevyo kila kitu kitaharibika”
“Sasa tunafanyaje mdau?”
“Lazima aondoke humu ndani, ikiwezekana hata kwa kutolewa roho” Sarah akazungumza kwa msisitizo na jazba.
“Kumuua?” Dullah akahoji kwa kuhamaki.
“Vipi unamuonea huruma? Akuanzae mmalize”
“Huoni kama kumuua kunaweza kututia hatiani?”
“Huyu hafii hapa, tunamtengenezea mazingira tofauti kabisa” Sarah akazunguma kwa msisitzizo.
“Mimi nafikiri tufanye kazi yetu haraka sana hakuna kuremba tena” Dullah akazungumza kwa msisitizo na kurejea kwenye bustani ya maua kuendelea na shughili yake. Sarah nae alielekea ndani kupumzika kama ilivyokuwa kawaida yake.
*****
Akili yangu ilikuwa kama vile imechanganyikiwa baada ya kugundua kuwa Sarah alikuwa amebaini mpango wangu. Hata hivyo nilijipa moyo na kutumia nafasi ile kukamilisha kazi niliyokuwa nimepewa na mzee Makwacha kuikamilisha ndani ya masaa 24.
Kama ilivyokuwa kawaida yangu niliamka asubuhi na mapema kwaajili ya kuandaa kifungua kinywa. Baada ya kuhakikisha Madam amekunywa chai na kuondoka nilirejea chumbani kwangu na kujivalisha guo ya kulalia kisha nikarejea sebleni kuendelea kumuandalia Mwalimu James chakula.
“Ku da da de ki !” Nikiwa nimeinama nikipaka siagi kwenye mkate nikasikia sauti ya Mwalimu James ikihamaki kutokea nyuma yangu.
“Asante Mungu!” Nikajisemea kimoyomoyo huku nikijifanya sijamuona na kuzidi kujibinua na kuyatikisa kidogo madafu ya nyuma ya nyumba.
Nilikumbuka vyema maneno ya Babu Makwacha kuwa amenipa masaa 24 tu kukamilisha kazi aliyokuwa amenituma. Hadi muda ule ilikuwa tayari yamepita masaa kama 12 pasipo kufanya jambo lolote lile.
Masikini ya Mungu mwanaume wa watu alikuwa ametoa macho na mdomo kuuacha wazi baada ya kunikuta nimejibinua katika mavazi kama yale. Alipumua kwa nguvu na kumeza funda la mate kisha akajikohoza.
“Shikamoo Mwalimu” Nilisalimia kwa kujifanya nimeshituka.
Macho ya Mwalimu yakatua kifuani kwangu na kukutana na vitoto vya madafu vikiwa vimekaa kihasara hasara bila kifungashio na kupelekea ncha zake kuchoma kitambaa cha ile nguo ya kulalalia kiasi cha kukaribia kuitoboa.
Macho ya Mwalimu James hayakuishia pale bali yalishuka hadi usawa wa chini ya kitovu na kuona nyonga iliyokuwa imechongwa vyema kama mdoli wa kuuzia nguo. Akaramba midomo yake na kushusha macho hadi usawa wa mapaja yangu na kugandisha macho yake. Ngozi laini iliyokuwa ikimeremeta kwenye mapaja yangu yaliyonona ilimfanya ahisi kutetemeka mwili.
Kwakuwa nilishabaini kuwa mtego wangu ulikuwa katika maendeleo mazuri nikalegeza macho yangu na kuuma mdomo wa chini kwa meno ya juu huku mkono wangu wa kuume ukitua juu ya paja la mguu wa kulia na kuupapasa taratiibu huku nikiipandisha ile nguo ya kulalia juu na kuzidi kuayaacha mapaja yangu wazi. Chezea mimi wewe!
“Mwalimu nakusalimia, shikamoo” Nikazungumza kwa sauti laini na nyororo kuliko aliyokuwa amezoea kuisikia siku zote kutoka kinywani mwangu.
"Agnes yuko wapi?” Mwalimu kahoji kwa kuhamaki huku akinitazama usoni na kuzidi kuchanganyikiwa kutokana na macho kumchuzi niliyokuwa nimeyatengeneza kimahaba.
“Nani Sarah?” Nikahoji huku nikijinyumbua utafikiri nafanya maonesho ya urembo.
“Amekwenda wapi?” Mwalimu alihoji huku akigeuza shingo kuangalia upande wa chumbani kwa Sarah.
“Sarah ameondoka na Madam. Nafikiri wamekwenda kufanya shoping” Nikazungumza huku nikiendelea kunyumbulika mbele ya mwanaume wa watu.
“Dullah naye yuko wapi?”
“Atakuwa nje huko anapambana na kazi zake. Tafadhali karibu kifungua kinywa usije ukachelewa kazini Babaaa” Nilizungumza kwa ile sauti yangu ya kupitia puani utadhani sikuwa na meno mdomoni.
“Leo siendi kazini” Mwalimu James akazungumza kwa sauti ya kukatakata huku akijiweka kwenye kiti pale mezani utafikiri mlevi wa pombe ya ulanzi.
“Kazi nzuri Farida” Nilizungumza huku nikimeza mate na kuziona dalili zote za mafanikio ya mipango yangu. Nikavuta hatua taratiibu kama twiga hadi pembeni ya kiti alichokuwa amekikalia Mwalimu James.
“Kwanini huendi kazini au unaumwa Babaa?” Nikahoji huku nikimuwekea mkono kwenye bega lake kwa staili ya kulitomasa tomasa hivi. Si unajua tena full kujibebisha.??
“Leo nimeamka mgonjwa mgonjwa siwezi kwenda kazini” Mwalimu James alizungumza kwa sauti nzito na yenye kukatakata kama vile Toyo imeisha mafuta.
“Lakini mbona kama macho yako yanaonekana kuna kitu unataka kukizungumza?” Nikahoji kwa mtego huku nikijipapasa kifuani kwa mkono wa kushoto na mkono wa kulia nikimtomasa tomasa begani.
Mwalimu James hakuzungumza neno lolote zaidi ya kunikamata kiunoni na kunivutia kwake. Nilijikuta nikimkalia kwenye mapaja yake na tayari mikono ya Mwalimu James ilikuwa imeshafika kwenye madafu ya kifuani na kuyatomasa kwa staili ya mpekecho. Kusema ukweli kwa mara ya kwanza niliweza kuhisi hali fulani hivi ambayo sikuwahi kukumbana nayo katika maisha yangu.
“Aaaaah..Tara…Tarati..tibu….Basi….!” Nikazungumza kwa kulalama huku nikijipindua kama funza.
“Farida nakupenda Farida wangu, sema unataka nikufanyie nini hapa duniani?” Mwalimu akaunguruma huku akipeleka midomo yake usawa wa madafu yangu ya kifuani kutaka kupiga pafu.
“Ngoja kwanza Mwalimu usi..usi…nyoyaaa!” Nikalalamika na kujikuta tayari nimeshanasa kwenye mikono ya Mwalimu James na nafsi yangu ilisharidhia kuruhusu kutumika kwa mwanaume yule. Kwa lugha nyingine naweza kusema kuwa nilikuwa nimefeli.
“Aaaaah Mwalimu..Kumbe taaaamu!” Nikalalamika huku nikinyumbulika kadri midomo ya Mwalimu ilivyokuwa ikifanya kazi kwenye madafu yangu.
Nikiwa mikononi mwa Mwalimu James nikakumbuka makubaliano niliyokuwa nimepeana na Babu Makwacha kuwa kazi yetu ilitakiwa kukamilika ndani ya masaa 24 tu. Nikapata nguvu na kumsukuma mwalimu James kutoka kifuani pangu.
“Vipi mtoto mzuri kumbe una kifua kitamu hivi?” Mwalimu James akazungumza kwa sauti yake ya kukatakata.
“Tatizo una haraka Babaaa” Nikazungumza huku nikijichomoa kutoka pale kwenye mapaja ya Mwalimu James.
“Subiri, unakwenda wapi sasa? Mwenzako nimeshapagawa hapa” Akazungumza na kunivuta kurudi kwenye mapaja yake.
“Kuku wako mwenyewe, manati ya nini?”
“Haya niambie nifanye nini niweze kumchinja taratibu?”
“Kuna jambo moja nataka unifanyie. Ukinisaidia tu basi mimi nitakuwa wako daima milele” Nikazungumza huku nikimchezea kidevu.
“Jambo gani mrembo wangu?” Mwalimu James akahoji huku akichezea midomo yangu.
“Utakubali lakini?”
“Mrembo chochote utakachokitaka mimi nitafanya” Akazunguma kwa msisitizo.
“Unanipenda kweli?”
“Mwenyewe umeona nimeshindwa hata kwenda kazini kwasababu yako”
“Kama kweli unanipenda nataka unioe na mimi” Nikazungumza kwa kudeka huku nikirembua zaidi macho yangu ya kumchuzi.
“Hilo mbona jambo dogo tu kwangu” Mwalimu akajibu kwa kujiamini.
“Kabla ya kunioa nataka umfukuze Sarah humu ndani” Nilizungumza kwa sauti ya kudeka na kubembeleza huku nikimkuna kuna udevu wake.
“Kwanini unataka nimfukuze Sarah?” Akahoji kwa kuhamaki kidogo.
“Kwasababu nina wivu”
“Inamaana niwafukuze wote Sarah pamoja na Madam?” Akahoji kwa umakini baada ya kumwambia kuwa ninawivu.
“Hapana, mi mwenzio nampenda sana Madam Manka. Usije ukathubutu kuachana naye” Nikazngumza kwa msisitizo.
“Duh! Sasa unataka nimfukuze lini?”
“Kuanzia sasa hivi sitaki kumuona Sarah humu ndani. Na kama haitoshi sitaki kukuona ukiwa na mahusiano naye tena” Nikazungumza kwa msisitizo.
“Duh kweli huo ni mtihani!”
“Kwahiyo kumbe hunipendi unataka kunichezea tu?” Nikahoji kwa kuhamaki huku nikijiondoa kutoka pale kwenye mapaja yake na kusimama pembeni.
“Sio hivyo mpenzi. Madam anajua Sarah ni mdogo wangu. Sasa nitaanzia wapi kumfukuza?” Akajaribu kujitetea.
“Hilo utajua mwenyewe, chagua kati yangu mimi na Sarah unataka kubaki na nani?” Nikazungumza kwa kujiamini kwasababu niliamini kuwa tayari nimeshamnasa mwanaume yule na kumuweka kiganjani.
“Haya njoo basi, nimeamua kuwa na wewe mrembo wangu” Alizungumza huku akionekana kujawa na tamaa ya kuutumia mwili wangu.
“Mbona una haraka hivyo Babaa, siku ambayo utakamilisha maagizo yangu ndiyo siku ambayo nitakupa halua yangu uionje”
“Kama nikikamilisha leo?”
“Nitakupa leo” Nikajibu kwa mapozi huku nikinga’ta midomo yangu kwa maringo ya kimahaba na nyodo za huba.
“Basi usiku nitakuja chumbani kwako unionjeshe hiyo halua”
“Hapana mpenzi wangu, naomba utafute Lodge nzuuuri ambako tutakaa huko na kufanya yetu kwa uhuru zaidi. Hapa ndani sio salama kabisa namuogopa mke wako” Nikazungumza kwa sauti ya maringo ya kimahaba.
“Daah utaniua we mtoto!” Alizungumza huku akinitazama meneo ya kati na kushuka chini kisha akameza funda la mate.
“Raha ya mapenzi umpate anayekupenda, kwangu ni bahati sana kwasababu ninafahamu jinsi unavyonipenda. Ninakuahidi nitakupa mapenzi motomoto ambayo haujawahi kuyapata tangu umezaliwa” Nilizungumza kwa nyodo huku nikijitikisa na kujipapasa maeneo ya kifuani.
“Kusema kweli najuta kuwahi kuoa. Kama ningejua kuwa kuna mrembo kama wewe kamwe nisingeoa abadani” Akazungumza kwa hisia mwanaume wa watu.
“Wala usijali kama kufaidi tu utafaidi. Mwenyewe si unaona utamu niliobarikiwa mkeo mtarajiwa” Nilizungumza huku nikijibinua binua kumuonesha jinsi nilivyokuwa nimeumbika mtoto wa kike.
“Naomba tukutane Moroco kwenye Lodge ya KISURA MNANA leo saa kumi jioni” Mwalimu akazungumza kwa umakini.
“Ipo maeneo gani?”
“Ukishuka kwenye daladala utachukua boda utamwambia akupeleke Kisura Manana Lodge, sio mbali kutokea stendi”
“Nikikupa utawezana lakini?” Nikahoji kwa utani huku nikiyakamata madafu yangu ya kifuani na kuyatomasa taratiibu huku nikiuma uma midomo yangu na macho nimeyafumba kuashiria kuwa nilikuwa na hamu kubwa ya kukutana na mwanaume yule.
“Farida naomba unipe sasahivi! Kuhusu ombi lako mimi nitalitekeleza tu” Masikini ya Mungu mwanaume wa watu akazungumza kwa taabu huku akionekana kuzidiwa kutokana na vituko nilivyokuwa nikimfanyia Pale sebleni.
Chezea Farida weye!?? Umeshuhudia samaki akiingia mwenyewe nyavuni?? Sasa ninakuambia ndugu msomaji mpango wangu ni kabambe hata wewe ni shahidi. Hebu nipe neno kidogo nipate moyo??
“Hapana Mwalimu! Timiza tulichokubaliana kwanza. Mengine yatafuata baadae Moroco ndani ya Kisura Mnana Lodge” Nilizungumzakwa msisitizo huku nikiachia tabasamu la matumaini na kuondoka nikimuacha mdomo wazi Mwanaume wa watu pale kwenye meza ya chakula.
Nilijawa na furaha ndani ya moyo wangu nikiamini baada ya kuondoka kwa Sarah ndani ya Nyumba ile basi ndoa ya Mwalimu James na mke wake ingebaki salama. “Asante Mungu kwa hatua hii niliyofikia, naua ndege wawili kwa jiwe moja” nikazungumza kwa furaha.
*****
Akiwa amebaki pale na mawazo akagutushwa na sauti ya mlango ukifunguliwa na mtu kutokea nje. Alipokaza macho alimshuhudia Sarah akiingia ndani ya nyumba ile.
“Wooow! Babeee!” Sarah akapaza sauti alipomuona Mwalimu James ameketi kwenye meza ya chakula.
Sura ya Mwalimu James ilikuwa imekunjana kwa hasira tofauti kabisa na siku zote walipokuwa wakikutana na binti yule.
Sarah alivuta hatua hadi pale alipokuwa ameketi Mwalimu James na kutaka kumpiga busu kwenye midomo lakini mwanaume yule akamsukuma.
“Kaa mbali na mimi!” Mwalimu James akazungumza huku amekunja sura utafikiri alikuwa amepitiwa na harufu ya kinyesi.
“Jamani Babe umepatwa na nini tena?” Sarah akahoji kwa mshangao.
“Naomba ukome kuniita Babe, tena kaa mbali na mimi!”
“Yaani mwanaume wewe unapenda utani muda wote”
“We ndezi nini! Nazungumza mambo ya msingi halafu wewe unayaita utani?”
“Hivi wewe umerogwa?”
“Wewe si ndio ulikuwa umeniroga, sasa uchawi wako umechuja. Sikupendi tena, shetani mkubwa wewe!” Mwalimu James alizungumza kwa jazba na hasira huku ametoa macho utafikiri yanango’ka.
“Mume wangu lazima kuna kitu hakipo sawa hapa!”
“Sikiliza binti, nampenda sana mke wangu. Sitaki tena mambo ya kijinga katika ndoa yangu” Akazungumza Mwalimu James kwa msisitizo.
“Inamaana umeshasahau kama umenikatisha masomo yangu na kuniweka hapa nyumbani kwako kama mkeo?” Sarah akahoji kwa jazba.
“Naomba usinipigie kelele binti, uliacha shule kwa upuuzi wako!”
“Unasemeje wewe?”
“Ulikuwa unajua wazi kuwa nina mke na tunapendana sana lakini ulivyokuwa fedhuli bado ukaingilia kati na kutaka kuitia doa ndoa yangu” Akazungumza Mwalimu James kwa msisitizo mkubwa.
“Mungu wangu! Kwanini umeamua kunifanyia hivi Mwalimu James?”
“Kwasbabu sikupendi”
“Kwahiyo unataka kusemaje?”
“Ninakupa masaa mawili tu, sitaki kukuona tena ndani ya nyumba yangu. Kwa lugha nyingine mimi na wewe basi!” Mwalimu James alizungumza kwa msisitizo kisha akainuka kwa lengo la kutoka nje.
“Naomba unisamehe mpenzi wangu, tafadhali usiniache nakupenda sana Mwalimu James” Sara alizungumza huku akiwa amepiga magoti na machozi yakitiririka kwenye mashavu yake.
“Ni a che e e e!” Mwalimu James akazungumza kwa sauti na kumsukuma pembeni Sarah.
Masikini ya Mungu kasichana kawatu kalidondokea pambeni kakawa kanalia kwa uchungu mkubwa huku machozi yakimtiririka machoni na puani.
“Naomba nikirudi nisizikute hizo mbariga zako hapa nyumbani kwangu!” Mwalimu James alizungumza na kufungua mlango kutoka nje akimuacha Sarah katika wakati mgumu wa kulia na kusaga meno.
Kila siku tunasikia waswahili wakizungumza kuwa majuto ni mjukuu. Sasa huyo majuto kwa wakati huo alikuwa ni mgeni wa Sarah masikini ya Mungu. Shule ameacha, aliyekuwa anamdanganya amemuacha, na shughuli ya magendo aliyokuwa anaifanya kwa kushirikiana na Dullah ilikuwa imeshafeli. Malipo hufanyika duniani, mbinguni tunasubiri kuhesabiwa tu.
“Ninachojiuliza ni kwamba itakuwaje kama ukiondoka kwenye nyumba hii ndani ya masaa mawili tu! Inamaana mpango wenu utakuwa umefeli?” Nikazungumza huku nikivuta hatua kutokea kwenye kona ambako nilikuwa nimejibanza nikishuhudia kila kitu kilichokuwa kinaendelea kati binti yule na Mwalimu James.
Sarah alipoinua macho yake akakutana na mimi nikiwa nimejikwatua na kupendeza utafikiri toto la kijini lipo kwenye mashindano ya ulimbwende. Nikawa namuangalia kwa kebehi na dharau utafikiri nilikuwa natazama kinyesi.
“Farida wewe ni shetani!” Sarah akazungumza kwa jazbah huku amejawa na hasira na kuwa kama chui aliyejeruhiwa.
“We mama wewe hebu tuheshimiane kwanza!”
“Kwanini umeniachanisha na James wangu?”
“James wako! We si ulisema hauna mapenzi ya dhati kwa Mwalimu James?”
“Nikweli sikuwa nampenda”
“Sasa kinachokuuma ni kipi? Huoni kama nimekusaidia kupunguza mizigo isiyo ya lazima?” Nikazungumza kwa kebehi.
“Tatizo nina mimba yake!”
“Nini! Una mimba mama? Mimba! Haya jiandae kulea toto lisilo na baba. Maana bwana wako atapigwa mvua zake 30 asubuhi kweupeee!” Nikazungumza kwa kebehi na nyodo kibao.
“Naomba unirudishie James wangu ninampenda sana” Sarah akazungumza kwa kusihi huku akilia kama mtoto.
“Mimi sielewi chochote mpendwa. Pengine Baba wa watu amebaini kosa lake na ameamua kuwa msafi katika ndoa yake. Unajua Madam anabahati sana ya kupata mwanaume mwenye mapenzi ya dhati” Nikazungumza kwa kebehi huku nikibenjua midomo yangu kwa dharau.
“Kwahiyo umefurahi kusikia nimefukuzwa?”
“Hapana mpendwa, kinachonisikitisha ni kwamba kabla ya jua kuzama Dullah naye atakuwa ameondoka ndani ya nyumba hii na kutuacha mimi na Bwana James pamoja na wifi yangu Madam Manka” Nikazungumza kwa kebehi.
“Unasema wifi yako! Madam amekuwa wifi yako tangu lini?” Sarah akahoji kwa jazba.
“Hata mimi sielewi, nimejikuta tu amekuwa wifi yangu. Hata hivyo ninampenda sana Madam Manka, ninaamini tutaishi kwa furaha na amani ndani ya nyumba hii iliyojaa upendo na mahaba” Nikazungumza kwa majivuno.
“Mshenzi wewe umeniharibia maisha yangu mbwa mkubwa wewe!” Sarah akapanda ghafla na kuzungumza kwa hasira huku ameiva macho utafikiri amepaliwa na pilipili.
“Sasa umevuka mipaka. Unawezaje kumtukana Mama mwenye nyumba?” Nikazungumza taratibu kama vile nakunywa chai ya moto.
“He! Leo hii umekuwa mama mwenye nyumba?”
“Na hivi unavyoniona naelekea Morocooo. Kuna chimbo moja linaitwa KISURA MNANA. Nitakuwa huko na Baba mwenye nyumba tukifanya yetu. Si unajua anavyonipenda?” Nikazungumza kwa kebehi huku nikijitazama jinsi nilivyokuwa nimependeza.
“Nakwambia Farida utalia na kusaga meno!” Akazungumza kwa ghadhabu mtoto wa watu.
“Kulia huko kwio! Kama mimba unayo wewe nilie mie vipi?”
“Farida nakupa masaa matatu. Nitakuwa nimeshakufundisha ya ulimwengu!”
“E e eee we mama! Usisahau umebakiza masaa mawili tu. Naomba nikirejea nisikukute humu ndani mwangu” Nilizungumza huku nikiangalia mkononi kama vile nasoma saa kumbe yalikuwa ni mabangili tu yamejazana na kugongana kama makengele ya Bomani.
“Farida, nitakachokufanyia leo hii hautokaa unisahau katika maisha yako yote!”
“Umechelewa mpenzi. Mimi ninakushauri fungasha mizigo yako na upotee mapemaaaa!” Nilizungumza kwa kebehi huku nikivuta mlango wa kutokea nje na kuondoka nikimuacha Sarah pale chini akiwa haamini kwa ambacho nilikuwa nimemfanyia
****
Dullah alikuwa akihangaika huku na kule utafikiri kulikuwa na kitu amekipoteza pale nje ya nyumba ya Mwalimu James. Macho yake yalikuwa hayatulii kuangaza maneo ya mlangoni. Ghafla mlango ulifunguliwa na Sarah akatoka huku akiwa amejawa na tabasamu la matumaini.
“Vipi mshirika mambo yamekwendaje?” Dullaha alihoji mara tu alipomuona Sarah akitokea ndani huku akiwa ameshika simu mkononi.
“Kila kitu kimekwenda kama tulivyokipanga” Sarah akajibu.
"Au Amekuzidi Maarifa nini?"
"Thubutuuu! Mie ndio Sarah bwana! Katoto kashamba kama kale kanawezaje kushindana na mimi"
“Safi sana. Huu ni mwanzo mzuri” Dullah akajibu kwa matumaini makubwa.
“Hatua inayofuata inahitaji umakini mkubwa. Kama tukifeli leo itakula kwetu” Sarah akazungumza kwa umakini mkubwa.
“Usijali kila kitu kitakwenda sawa”
“Sasa unasubiri nini? Kamilisha shughuli unajua tuna masaa mawili tu hapa ndani”
“Kila kitu kimeshakamilika na mipango inaendelea hivi nanavyozungumza” Dullah alizungumza kwa kujiamini huku akiangalia saa yake ya mkonini.
“Ndiomaana ninakupenda, sasa ole wako na wewe unizingue” Sarah akazungumza kwa msisitizo.
“Na hako kamimba kako utampa nani?” Dullah akahoji kwa masihara huku akimtazama Sarah tumbonii.
“Kamimba tunakaflash tu. Nani wa kulea mtoto wa mtu”
“Unajua madhara ya kuchomoa mimba wewe?”
“Hata kama nisipokufa leo kwa kuchoropoa ipo siku nitakufa tu”
“Kwahiyo upo tayari kufa?”
“Nzi kufia kwenye kidonda sio haramu. Kwanza tuwachane na hizo habari muda unazidi kwenda tusije tukafeli”Sarah akatahadharisha.
“Nimemtekenya Madam. Tusubiri acheke tumalize kazi” Dullah akazungumza kwa kujiamini.
“Na kama asipocheka?” Sarah akahoji kwa umakini mkubwa.
“Asicheke yeye nani?”
Wakati Sarah na Dullah walipokuwa wakiendelea na mazungumzo yao pale nje, walimuona Madam Manka akiingia ndani kwa spidi ya mwendo kasi. Wakatazamana na kuachia tabasamu la ushindi.
“Muda umetaradadi!” Alizungumza Dullah kwa msisitizo.
“Nimeyaona matunda ya kazi yako kijana” Sarah akazungumza kwa furaha na matumaini ya ushindi.
“Naona plan B imetangulia kabla ya plan A”
“Nafikiri Boss ameamua kuchezesha plan B. Pengine kuna shida au mambo yamekwenda vizuri zaidi ya tulivyotarajia” Alisema Sarah huku akitabasamu.
“Acha maneno mengi twende tukamalize mzigo” Dullah alizungumza huku akivuta hatua kuelekea ndani.
Wawili wale waliongozana moja kwa moja hadi chumbani kwa Madam ambako walimkuta mwanamke yule akiwa analia kwa uchungu huku amejilaza kitandani.
“Wifi kuna tatizo gani mpenzi?” Sarah alihoji kwa sauti iliyokuwa imejaa wasiwasi na huruma za kutengeneza huku amepiga magoti na kumpapasa kichwani Madam.
“Naomba uniache!” Madam akazungumza kwa ukali huku akiusukuma mkono wa Sarah kutoka kichwani mwake.
“Nitakuachaje ukiwa katika hali kama hii?”
“Hivi unaweza ukamsaidia mtu halafu akakuzunguuka?” Madam akalalamika huku akimtazama Sarah usoni.
“Unazungumza kuhusu nini Madam?” Dullah ambaye naye alikuwa amesimama mlangoni alihoji kwa umakini huku akivuta hatua kusogea pale alipokuwa amepiga magoti Sarah.
“Kumbe unaitwa Sarah! Unajifanya kunipenda kumbe unamchukua mume wangu? Aaah…Laana na ikutafune Malaya mkubwa wewe!” Madam alizungumza maneno ambayo yalileta mshituko na hofu kubwa kwa upande wa Sarah na Dullah.
Hali ya kufa kufa ikatawala kwenye nyoyo za wawili wale wakiamini mipango yao ilikuwa tayari kisirani mie nimeshaibumburusha. Chezea mimi weye, lazima kijasho kiwatoke.??
Lakini ndugu msoamji mambo mengine yanahitaji moyo ujue. Unaweza ukadhani unawinda kumbe wewe ndio umeingia mwenyewe kwenye nyavu za unaowawinda kudadadeki!??
Kama sielewi hivi, hebu nipe neno la kunitia moyo tafadhali maana kama kweli kuna kamchezo wamekacheza hivi hawa simbirisi.
MWISHO
Thanks for share your blog here . John Wayne Airport Sna Limousine Service
ReplyDelete