Chombezo : Kitumbua Cha Kihindi
Sehemu Ya Tatu (3)
“Kumbe ni nini,.. Guest? Ashura alizidi kuhoji.
“Hapana, hii sio Guest wala sio Hotel”
“Sasa kumbe ni kitu gani?”
“Hii ni nyumba” alisema Zawadi wakiwa wamesimama.
“Duh nyumba ya kuishi watu kabisa!” alizungumza Ashura kwa mshangao wa hali ya juu.
“Ndio” alijibu Zawadi kwa ufupi.
“Kwakweli kuna watu wanaishi Zawadi”
“Kwanini?”
“Sisi wengine tunasukuma siku tu ziende” Ashura alizungumza kwa mshangao huku akilitupia macho jumba lile la kifahari lililokuwepo mbele ya macho yake.
“Unataka kusemaje Ashura, mbona sikuelewi”
“Sasa Zawadi mjumba wote huu kama hoteli la kifahari unasema ni nyumba ya kuishi watu?” Ashuraalieleza.
“Hivi nikikwambia hii nyumba ni yakwangu utaelewa?” Zawadi alizungumza kwa msisiytizo.
“Nini?”
“Hii ni nyumba yangu, na mimi ninaishi humu” Zawadi akaeleza.
“Wacha uzushi Zawadi mimi sio mtoto mdogo bwana” Ashura alizidi kuhamaki na kukataa kukubaliana na yale maneno ya rafiki yake.
“Huamini Ashura?”
“Kwa kweli siwezi kuamini”
“Hebu geuka nyuma” alisema Zawadi huku akitoa tabasamu. Ashura akageuka kama alivyoambiwa na rafiki yake.
* * * *
Magosho aliendelea kumpagwawisha Bi.Fahreen ambaye alionekana kuwa hoi bin taaban na kumfanya aendelee kalalamika huku akiomba huruma ya Magosho imshukie.
“Omnh!....Go…Go..Gosooo…iko..ta..iko…kwisa…ve..ve...Com…aaaa!” maneno yalipotea mdomoni kwa Bi.Fahreen.
Mwanamke yule alikuwa hajitambui wala haeleweki alichokuwa anakizungumza. Mbwembwe zote alizokuwa ameanza nazo zilimuisha. Hakujiweza tena, hata mkono hakuweza kuuinua. Macho aliyaona mazito utafikiri alikuwa amebebeshwa mifuko ya smenti kwenye kope zake, na hata sauti nayo ikakata. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimuenda mbio kuliko kawaida na mwili ukaanza kumtetemeka utafikiri alikuwa amepatwa na degedege.
Lilikuwa ni shindano kabambe la mchezo wa riadha. Washindanaji walitakiwa kukimbia kwa kuzunguuka uwanja uliokuwa na mita mia moja kiasi cha mara tano. Mwisho mwa raundi moja kulikuwa na kilima ambacho mkimbiaji alipaswa kukipanda kabla ya kuanza kukimbia roundi ya pili.
Mashindano yale yaliwahusisha wakimbiaji wa pande mbili ambao walikuwa ni Bi.Fahreen na mpinzani wake alikuwa ni kijana Magosho. Walikuwa wakigombania medali ya dhahabu ambayo ilikuwa ni lazima ichukuliwe na mmoja kati yao. Hivyo kila mmoja alikuwa na hamu kubwa ya kujinyakulia medali hiyo ambyo ilikuwa na thamani kubwa.
Washindanaji wakajipanga kwenye mstari na punde tu kipenga kilipopulizwa wote wawili wakaanza kutimua mbio. Kila mmoja alionesha mbwembwe zake mapema. Hakuna aliyekubali kushindwa na mwenzie.
Loo! Bi.Fahreen akafyatuka kama mshale na kujikuta amefika kileleni ndani ya dakika tano tu. Magosho akajaribu kuongeza mbio lakini wapi hakufanikiwa kumfikia mama yule wa kihindi.
Magosho akiwa na matumaini ya kumfikia mpinzani wake, akashangaa Bi.Fahreen akimpita kama mshale kutokea nyuma yake. Mama yule wa kihindi alikuwa anakwenda utafikiri amekula miguu ya mbuni. Alifika kileleni kwa mara nyingine wakati Magosho hakuwa na hata dalili ya kuukaribia mlima ule pamoja na jitihada zake zote.
Kijana alionekana kuvamia fani ile ya riadha kwani aliendelea kusua sua njiani wakati Bi.Fahreen akijitwalia pointi mara kadhaa. Hata hivyo kijana Magosho hakukata tamaa ingawa alikuwa akihemea juu juu kwani aliendelea kukimbia hadi kufanikiwa kufika kileleni angalau mara moja tu.
Mshindi aliyetwaa medali ya dhahabu alikuwa ni Bi.Fahreen kwasababu aliweza kufika kwenye kilele cha mlima ule mara tano, wakati mpinzani wake yeye alifika kileleni mara moja tu. Hata hivyo wote wawili walikuwa wamechoka vilivyo na kujikuta wamelala mithili ya wahanga wa mafuriko au wa kimbunga Katrina.
Magosho alikuwa wa kwanza kupata ahuweni kutoka kwenye ule uchovu, aliinua shingo yake na kumchungulia Bi fahreen usoni. Mama wa watu alikuwa amechoka utafikiri ametoka kufanya kazi ya kuhamisha milima ya Uruguru kwenda Usambara. Alikuwa amelala huku amefumba macho utafikiri amekata Kamba. Magosho akamshika kwenye mashavu mwanamke yule na kumpiga busu usoni ambalo lilimfanya mama wa kihindi kufumbua macho.
“Mama” aliita Magosho kwa sauti iliyo kwaruza.
“Nani iko mama yako?” alihoji Bi.Fahreen kwa sauti iliyotoka kwa shida.
“Si wewe jamani”
“Mimi hapana iko mama yako” alizungumza Bi.Fahreen kwa ile sauti yake ya kujilazimisha.
“Kumbe we nani?” Magosho alihoji kwa sauti nzito
“Ita mimi penzi bhanaaa.” Bi. Fahreen naye akazungumza kwa sauti ya kujilazimisha.
“Basi baby usijali” alisema Magosho na kumpiga busu la mdomo Bi.Fahreen.
“Mambo iko ivo toto zuri. Kama taka mimi chukie veve ita mimi mama” alisema Bi.Fahreen huku akimkumbatia Magosho kwanguvu. Magosho naye akamkumbatia mwanamke yule kama vile alivyofanya yeye. Yani kama ungepata bahati ya kuwaona ungefikiri wawili wale walikuwa wanalingana umri.
Pamoja na kwamba Bi. Fahreen ndiye aliyekuwa akifanya uchokozi katika kuhakikisha amemnasa Magosho, lakini kijana naye alionekana kufurahia mchezo ule pengine nafikiri ni kwasababu ya kupewa vitu adimu vyenye mahadhi ya Kuchi kuchi Hotahe. Ndugu msomaji, Magosho alitegwa akategeka na kuingia mzima mzima katika himaya ya mwanamke yule wa kihindi.
“Vipi lakini Baby?” Magosho alihoji baada ya kuachiana na mwanamke yule.
“Tangu mimi zaliwe hapana pata kitu kama veve nipa leo” alisema Bi.Fahreen kwa furaha na kujidai.
“Mnh! Lakini hata wewe unaweza. Kumbe Nakeshiwar anafaidi kiasi hiki!” alisema Magosho na kuishika pua nyembamba ya Bi. Fahreen na kuivuta kidogo kimahaba.
“Hapana taja Nakeshi hapa bhana. Mimi lazima oa veve” alizungumza Bi. Fahreen kwa furaha kubwa.
“Wacha masihara Fahreen. Wewe si una mume wako?”
“Mume nini bhanaa, Kama veve iko nipa mimi raha hakuna bhaya!”
“Basi mtoto mzuri nitafanya unachopenda” alisema Magosho huku mkono wake ukiwa kwenye zigo la mama yule ukilipigapiga na kulitomasa tomasa kwa kiganja cha ule mkono wake.
“Kama iko sikia hamu, hapana sita ambia mimi” alisema Fahreen.
“Mnh!” Magosho akaguna.
“Kama veve iko furahisa Fahreen, basi No problem ongezea sahara kila mezi” alisema Bi.Fahreen kwa msisitizo mkubwa.
“Dah! Nitafurahisana mpenzi kama kweli” Magosho lizungumza kwa furaha aliposikia kuwa ataongezewa mshahara. Yaani raha apewe halafu na mshahara pia aongezewe? Mnh! Haya bwana sisi yetu macho mana hakuna ajuae ya mbeleni. Au sio ndugu msomaji?
“Hapana hiyo tu Goso. Mimi taka jengea nyumba veve, nunulia gari, halafu fungulia Business” alisema Bi.Fahreen akionekana wazi kufurahishwa na ile starehe aliyopewa na mtoto wa kibantu, kijana wa marehemu mama Ashura.
Magosho akahisi kama vile alikuwa ndotoni. Hakuyaamini yale maneno ya Bi.Fahreen yalikuwa yakitoka moyoni mwake. Alitamani sana ahadi ile itimie ndani ya dakika zile zile. Akajikuta akizidi kuvutiwa na penzi la mama yule wa kihindi ambaye alikuwa ni mke wa bosi wake.
* * * *
Ashura baada ya kugeuka nyumba, macho yake yalitua kwenye Starlet moja ambayo alimuona nayo Zawadi kwa mara ya kwanza kule kwenye kijiwe cha kuuzia vitumbua. Akajaribu kuangaza pengine angeona kitu ambacho kingekuwa ni uthibitisho tosha kuwa ile ilikuwa ni nyumba yake lakini hakuona chochone. Aligeuza macho na kumtazama rafiki yake.
“Kama sikosei unakusudia ile gari?” Ashura akahoji.
“Swadakta! unaikumbuka gari ile?” Zawadi alihoji
“Inafanana na ile niliyokuona nayo kwa mara ya kwanza”
“Sio ina fanana, ndiyo yenyewe”
“Kwahiyo unataka kusemaje?”
“Inatosha kuwa uthibitisho kwamba hapa ni nyumbani kwangu”
“Kwa upande wako inatosha, lakini kwa upande wangu bado ni kigugumizi” Ashura alizungumza.
“Kwani ulitegemea kuniona Zawadi mimi naendeha gari?” Zawadi akahoji.
“Kwakweli ni muujiza”
“Basi hata hii nyumba kuwa yangu na iwe muujiza”
“Mhn! basi hongera mwaya maisha ndo umesha yaweza hivyo” Ashura akazungumza kwa shingo upande huku akiamini shoga yake alikuwa anamuongopea.
“Ah kawaida, sio kazi saana kama unavyo fikiri” Zawadi alizungumza na kumshika mkono Ashura.
Walivuta hatua kuelekea kwenye mlango wa ile nyumba kubwa. Ashura alikuwa makini kuangaza pande mabali mbali kukagua mazingira ya nyumbani pale. Kiukweli ndugu msomaji mazingira yale hayakuwa ya kitoto ukizingatia hali halisi ya mazingira aliyokuwa akiishi Ashura, hakuwa na ujanja wa kujizuia kushangaa.
Walipofika mlangoni Zawadi alitoa kadi kama ya ATM na kuipitisha kwenye kitasa cha mlango ule ambao ulijifungua wenyewe. Ashura alizidi kupata mshangao. Mwenyewe alikuwa amezoea kuona na kutumia yale makufuli ya Athumani mfupi kasimama malangoni. Hakuwahi kuwaza wala kufikiri kama kulikuwa na milango iliyokuwa ikifunguliwa na kadi.
Walifika kwenye sebule moja iliyokuwa pana kiasi cha kuingiza hewa na mwanga wa kutosha. Samani za gharama zilikuwa zimejaa na kuifanya sebule ile kupendeza na kuvutia mno.
“Karibu shosti jisikie upo kwako” Zawadi alizungumza huku akimuonesha Ashura mahali pa kuketi. Ashura alibakia amesimama akitafakari maisha ya rafiki yake yule yalivyokuwa ya maajabu. Akajaribu kumkumbuka Zawadi yule waliyekuwa wakiuza wote vitumbua kule uswahilini na kumfananisha na Zawadi wa leo aliyekuwa anafungua loki za milango kwa kutumia kadi kama za benki.
"Vipi Shost mbona hukai?" Zawadi alihoji baada ya kumuona rafiki yake kama vile amekauka kwa kupigwa na shoti ya umeme. Ashura baada ya kusisitizwa na rafiki yake aliketi kwenye sofa moja la gharama ambalo hakuwahi kufikiria kama angewahi kulikalia maishani mwake.
"Dakika moja tafadhari" Alisema Zawadi na kuelekea kwenye korido moja ndefu ambayo ilimfikisha hadi kwenye mlango wa chumbani.
Baada ya sekunde kadhaa Ashura akasikia sauti ya Zawadi ikimuita kutokea kule kwenye korido. Akajiinua na kuelekea kule sauti ilipotokea.
"Shoga uko wapi?" Ashura alipaza sauti baada ya kuona milango ikimchanganya na kushindwa kuelewa rafiki yake alikuwa chumba kipi. Mlango wa chumba kimoja ulifunguliwa na zawadi akachunguli.
"Niko huku Shosti wangu" Alisema Zawadi
"Ka! shoga milango inachanganya"
"Kwasababu ni mgeni tu shoga ndiomaana unaona hivyo. Karibu ndani"
Ashura aliingia chumbani mle na kujikuta katika hali ya mshangao zaidi baada ya kuona mazingira ya chumbani mle jinsi yalivyokuwa yamejitosheleza. Ilimjaa zaidi hamu ya kutaka kufahamu jinsi ambavyo rafiki yake yule alivyoyapatia maisha yale.
"Shoga hebu nipe siri ya mafanikio yako" Ashura alihoji mara tu baada ya kuketi kitandani.
"Sio siri, ni KITUMBUA” Zawadi alizungumza huku akimimina wiski kwenye birauli.
"Kitumbua?" Ashura akahoji kwa mshangao.
"Ndio kitumbua, tena kitumbua cha kihindi"
"Unamaanisha nini?"
"Una maswali mingi kwani we ni polisi? hebu karibu kinywaji" Zawadi alizungumza huku akimkabidhi Ashura birauli ile iliyokuwa imejaa wisk.
Waswahili wanasema mramba asali harambi mara moja. Kauli hii imethibitka hasa baada ya Magosho kukutana kimwili na mke wa bosi wake ndani ya gari. Bi.Fahreen alikuwa amechanganyikiwa na kudata kabisa na penzi la mfanya kazi wao wa ndani.
Magosho alikuwa ameshikilia mpira wa maji akimwagilia maua yaliypokuwa yameoteshwa nje ya nyumba ile kwa ustadi mkubwa. Kijana yule alikuwa akiipenda sana kazi yake hasa ukizingatia ndiyo iliyokuwa ikitegemewa zaidi na familia yake, yaani yeye na mdogo wake Ashura.
Bi Fahareen alitembea kwa kunyata kuelekea pale alipokuwa amesimama Magosho akiendelea na shughuli yake. Mwanamke yule alifika na kumziba macho Magosho kwa nyuma.
Magosho aliipapasa mikono ile ya mwanamke wa kihindi na kuhisi kumfahamu vizuri sana.
“Mama…” Magosho aliita baada ya kupata harufu ya pafume aliyokuwa akiitumia Bi. Fahree.
“Nani iko mama yako?” alizungumza Bi. Fhreen huku akiwa bado ameziba macho ya mwanamke yule.
“Jamani niachie basi” Yasini alizungumza kwa sauti ya kudeka kidogo baada ya kumfahamu mtu aliyekuwa amemziba macho.
“Hapana achia veve, sema mimi iko nani?” Bi. Fahreen alizungumza huku akiwa bado amemkamata kisawasawa kijana yule.
“Darling..”
“Nop…”
“Sweetie”
“Nop..”
“Yahabibi”
“Nop..”
“Baby”
“Good! Kumbe mimi iko toto?” Bi. Fahreen alizungumza huku akimuachia Yasini.
“Mbona nilikufahamu mapema sana” Magosho akazungumza kwa kujitutumua mbele ya mwanamke yule.
“Veve iko jua mimi kuliko hata Mr. Nakeshwar!” Alizungumza mwanamke yule huku akiwa ameweka mikono yake kwenye mabega ya Magosho.
“Hapana bwana mama, Bosi Nakeshwar ndio anakufahamu zaidi kuliko mimi” Alizungumza Magosho huku akiendelea na shughuli yake na mwaname yule akiwa bado amemshika mabegani.
“Sikia Goso yangu ambie veve kitu makini” alizungumza mwanamke yule kwa umakini.
Magosho aliwacha kufanya kile alichokuwa anaendelea nacho na kumgeukia Bi. Fahreen kuweza kusikia kile alichokuwa anataka kukizungumza.
“Ile dozi veve iko patia mimi kila siku, hapana siku moya Nakeshwar iko onesa mimi” mwanamke yule alizungumza kwa sauti ya kulalamika huku akipeleka mkono wake wa kuume kwenye kidali cha Magosho kilichokuwa kimevimba kutokana na mazoezi ya viungo.
“Lakini mama…”
“Nooo! Nani iko mama yako?” Bi. Fahreen akazungumza kwa ukali kidogo baada ya Magosho kumuita mama.
“Basi baby…” Magosho akazungumza kwa sauti ya upole huku akiachia tabasamu la huba mbele ya mwanamke yule wa kihindi.
“Veve Goso kila siku iko kosea mimi bhanaa”
“Basi nisamehe mpenzi wangu” Magosho alizungumza huku akimshika Bi. Fahreen kwenye mashavu.
“Kama iko taka samehe veve tibia mimi”Bi. Fhreen alizungumza kwa sauti ya kudeka huku akizunguusha macho utafikiri roho ilikuwa inataka kuacha mwili.
“Naam..” Yasini alishituka kidogo baada ya kusikia kauli ile kutoka kwa Bi. Fahreen.
“Tibie mimi bhanaa iko gonjwa” alizungumza Bi. Fahreen kwa msisitizo.
“Mng! Acha masihara basi”
“Hapana leta sihara mimi, iko gonjwa sana”
“Hivi mume wako akirudi ghafla kutatokea nini?”
“Hapana sida yoyote, mimi ambia yeye, veve iko dokta yangu” mwanamke yule alizungumza huku akimtomasa tomasa kijana wawatu kwenye mabegani.
“Wewe mwanamke wewe usitake kuniletea balaa. Mimi huo udaktari nimeusomea wapi?” Magosho alizungumza kwa mkazo kidogo uliochanganyikana na chembechembe za mahaba.
“Kama veve iko tibia mimi, basi veve iko daktari ya mimi” mwanamke yule aliendelea kuzungumza kwa msisitizo.
“Bwana ngoja mimi nimalizie kumwagilia maua” Magoshoalizungumza huku akibana mpira wa maji na kuyarusha kwenye maua ya mbele kidogo.
“Leo mimi iko taka onja ile tamu yako hapahapa” Jamani nyie sijui watu wengine wana mapepo! Mana hata mimi mwandishi naandika lakini mwanamke huyu naona simuelewi. Amesahau kabisa kama Magosho ni kijana wa mwanamke mwenzie haipaswi kumbemenda Eboo!
“Subiri basi tukitoka Out, leo nakuahidi kukupa dozi nzito zaidi hadi ukahadithie kwenu Bombey” Magosho alizungumza kwa kujidai huku akimkata jicho la wizi Bi. Fahreen na midomo yake akiichezesha chezesha kimahaba na macho ameyalegeza kigogo mtoto wa kiume.
“Au unataka nikumwagilie na wewe” Alizungumza Magosho huku akiendelea kumwagilia yale maua yaliyokuwa yakishangilia penzi lile mtoto wa kibantu na mama wa kihindi.
“Woow! Iko taka magilia mimi?” Bi. Fahreen alionekana kufurahishwa sana na ile kauli ya kumwagiliwa aliyokuwa ameitoa Magosho.
“Kwani wewe unafikiria ni kumwagiliwa nini?” magoshoalizungumza huku akiachia kicheko kidogo ambacho kilizidi kumchanganya mwanamke mtu mzima.
“Veve iko sema taka magilia mimi. Sasa mineno mingi toka wapi?” alisema Bi Fahreen huku macho yake yakionekana wazi kulikuwa na kitu anakitafuta kutoka kwa Magosho.
Magosho alianza kuhisi hisia zake zikijitahidi kuuchota ubongo wake na kuupeleka kule alipokuwa anakutaka Bi. Fahreen.
“We mwanamke una lako jambo unalolitafuta na utalipata muda sio mrefu” alizungumza Magosho kwa sauti kavu kisha akakohoa mara mbili na kujikohoza kukuna koo lake mara tatu mfurulizo.
“Mimi taka veve tibia mimi, Veve taka magilia mimi. Mambo mukidee” Bi. Fahreen alizungumza huku akipeleka mikono yake kushika kiuno cha Magosho.
“Ngoja nikuoneshe nilichokuwa nakimaanisha” Magosho alizungumza na kugeuka na ule mpira wa maji kuanza kummwagialia mwilini mama wawatu wa Kihindi.
Bi Fahreen alishituka sana baada ya kufanyiwa kitendo kile na Magosho. Hakuwa na namna zaidi ya kutimua mbio kuyakimbia maji yale. Magosho naye alimuunganishia mama wawatu na kumkimbiza kwa nyuma huku amekamatia vyema mpira wa maji, alikuwa amedhamiria kumlowanisha mama yule.
Ndugu msomaji kama ungepata bahati ya kuwaona wawili wale nafikiri ungehisi walikuwa ni watoto wa chekechea wanacheza kidali poo. Kila mmoja alikuwa akikimbia huku akicheka kwa furaha na Amani ndani ya moyo. Magosho aliweza kusahau kabisa ile hali ya umasikini kule uswahilini kwao.
Ghafla Bi.Fahareen alijidondosha chini na Magosho kwasababu hakuwa ametegemea kitendo kile alijikuta akimvamia na kumdondokea mama yule wa kihindi. Kwakuwa walikuwa wameshazoea kupeana ushirikiano wakati wowote na mahali popote, kitendo kile kilikuwa ni sababu tosha ya kuelekea kwenye mashambulizi ya makombora ya kivita. Wale waliopata nafasi ya kusikia mkasa wa vita vya pili vya dunia wanaelewa ninachokimaanisha hapa.
Kukuru kakara kukuru kakara kwenye maua mke wa mtu na mtoto wa mtu. Yani ukiangalia kwa mbali hivi unaweza kusema pale katikati kulikuwa na mpambano mkali kati ya simba na punda milia.
Ndugu msomaji huwezi kuamini hiki ninachokwnda kukuambia sasa hivi. Kumbe muda wote ule wawili wale walipokuwa wakichokozana na kuanza kucheza kuchikuchi kwenye bustani ya watu ya Mr. Nakeshwar, kulikuwa na mtu ametulia tu pembeni akiusoma mchezo na mchezo ukasomeka vyema na kueleweka vizuri.
MANSOOR alikuwa ni mfanyabiashara aliyekuwa akishirikiana na muhindi Nakeshwar. Kwa namna Mansoor alivyokuwa akiishi na Mr. Nakeshwar ungeweza kusema walikuwa ni ndugu wa baba na mama mmoja kasoro rangi za ngozi zao tu ndizo zilizokuwa zikiwatofautisha.
Mansoor pamoja na mlinzi wa getini ndio waliokuwa pembeni wametulia wakishirikiana kuusoma mchezo ule. Hata hivyo jambo lile halikuwa geni sana machoni mwao kwasababu penzi la Bi. Fahreen na Magosho halikuwa la kuficha. Watu wengi sana walikuwa wanafahamu kilichokuwa kinaendelea.
Ilikuwa ni rahisi watu kufahamu kwasababu wawili wale hawakuwa wakifanya starehe zao kwa kujificha. Walikuwa wakifanya yote hayo kwasababu Mr. Nakeshwar alitumia muda mwingi kusafiri kibiashara. Ni mara chache sana Mr. Nakeshwar kuwa nchini Tanzania na familia yake. Pengine ndiyomaana Bi.Fahreen aliamua kutafuta kibenteni wake. Sina uhakika sana kwa hilo mana hata mimi ni mgeni.
Mansoor alijikuta akipandwa na hasira dhidi ya viumbe wale wawili waliokuwa wakifanya usafi kule kwenye maua. Alikuwa akihisi kama vile mke wake ndiye aliyekuwa fanya utumbo ule. Akasimama kwa hasira huku akitoa simu yake mfukoni na kuvuta namba za Mr. Nakeshwar.
“Kama noma na iwe noma ngoja leo tukomeshe uchafu huu” alizungumza Mansoor huku akibonyeza namba za Mr. Nakeshwar.
ENDELE…
Sijui tuseme ilikuwa ni bahati mbaya au ni bahati nzuri maana Mansoor alipiga simu ya Nakeshwar lakini haikupatikana.
“Vipi hapatikani?” alihoji mlinzi wa getini kwa hamasa kubwa.
Mansoor hakuta jibu lolote zaidi ya kusonya na kupiga kwa mara nyingine. Hata hivyo majiu yalikuwa ni yaleyale simu ya Mr. Nakeshwar haikuwa inapatikana.
“Shida ya huyu bwana ndiyo hii ya kupenda kuzima simu” alizungumza Mansor huku akionekana kukasirika zaidi.
“Kwahiyo utafanya nini sasa?” mzee yule mlinzi alihoji.
“Ngoja nikawashikishe adabu mimi mwenyewe” Alizungumza Mansoor kwa hasira huku akivuta hatua kuelekea kule bustanini kulipokuwa na purukushani za Magosho na Bi. Fahreen. Hata hivyo yule mlinzi alimuwahi na kumdaka mkono kumuomba amsikilize.
“Sikiliza baba nikwambie kitu” alizungumza mzee yule kwa sauti ya chini.
“Mzee mimi nakwenda kuwaua wale kunguni” Mansoor alizungumza kwa hasira huku akitetemeka utafikiri Bi. Fahreen alikuwa ni mke wake.
“Sikiliza baba, haya mambo hayataki haraka mwanangu” alisema mlinzi.
“Mzee huyu mama anatutia aibu, ni nani asiyefahamu ukaribu wangu na Mr. Nakeshwar?” alizungumza Mansoor.
“Ni kweli baba, lakini tafadhali usipende kufanya maamuzi wakati una hasira”
“Nisifanye maamuzi wakati bosi wangu anaibiwa huku nikishuhudia?”
“Ni kweli baba, hata mimi sipendezwi na tabia ya mwanamke huyu, lakini…”
“Lakini nini, au na wewe unashirikiana na yule kijana?” alihoji kwa jazba Mansoor.
“Aaaah huko sasa siko kijana wangu” mzee yule akazungumza kwa kuhamaki baada ya kusikia kauli ile kutoka kwa Mansoor.
“Kama kweli haushirikiani nao, niachie nikaliwashe” alizungumza Mansoor huku akijaribu kuvuta mkono wake uliokuwa umekamatwa vyema na mzee yule.
“Tafadhali sikiliza Busara zangu zitakusaidia kufanya maamuzi yenye hekima” mzee yule mlinzi alizungumza kwa kusihi.
Maneno yale ya babu mlinzi yaliyokuwa na kauli za hekima na busara ndani yake zilimfanya Mansoor kutuli kidogo na kujaribu kumsikiliza.
“Mr. Nakeshwar anampenda sana mke wake” alizungumza babu mlinzi.
“Kwahiyo kama anapendwa ndio afanye ufuska?”
“Sina maana hiyo kijana wangu”
“Kumbe unamaanisha nini?”
“Unaweza kufanya jambo kesho na keshokutwa ukaonekana wewe ndio mbaya halafu wenyewe wakaendelea na mapenzi yao” mzee yule akazungumza kwa umakini.
Maneno yale yalionekana kumuingia Mansoor na kuzidi kushusha hasira zake. Nafikiri kama kweli angekwenda kule bustanini ni lazima mtu angetolewa roho kutokana na hasira alizokuwa nazo. Akavuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu kisha akarejesha simu yake kwenye mfuko wa suti na kuondoka kwa mwendo kwa spidi pasipo kuzungumza neno lolote lile la ziada.
Babu mlinzi alimtazama mwanaume yule alivyokuwa akitembea kwa kushindilia hatua chini kutokana na hasira alizokuwa nazo. Baada ya kumshuhudia Mansoor akiingia kwenye gari yake na kuondoka, babu mlinzi kageuza macho yake na kuyatupia kule kulikokuwa na bustani ya maua kisha akatikisa kichwa chake kwa masikitiko huku akiachia tabasamu la huzuni.
*****
Kule nyumbani kwa Zawadi, Ashura aliipokea glasi ya wiski na kuitazama kwa makini,
"Nini hii? Pombe?"
"Wacha maswali bwana kunywa" Zawadi alizungumza huku akisukuma birauli yake mdomoni na kupiga funda moja dogo huku akionekana kuisikilizia ilivyokuwa ikikatiza kwenye koo lake.
“Duh inaonekana si mchezo!” Ashura alizungumza huku akimkodolea macho rafiki yake yule.
“We onja ujionee mwenyewe maswali ya nini” alisema Zawadi huku akipeleka kiganja cha mkono wake wa kushoto na kufuta midomo yake.
"Sawa nitakunywa. Turudi kwenye habari za hicho kitumbua cha kihindi ambacho kimekufanya mwenzangu uwe na maisha mazuri kiasi hiki" Alizungumza Ashura huku akiiweka ile birauli juu ya meza.
"Shost nawe uking'ang'ania kitu, Mie mwenzio nafanya biashara ya kuuza vitumbua kama ya kwako" alizungumza Zawadi kwa kujiamini.
"Wacha masihara Zawadi bwana, mwenzio mie nina hamu"
"He! yamekuwa hayo tena! Haya niambie una hamu ya nini mwenzangu?"
"Nina hamu ya kujua"
"Ujue nini tena wakati tayari nimekwambia ninafanya biashara ya kuuza vitumbua" alisema Zawadi kwa msisitizo.
"Mie hata sikuelewi" Ashura alisema na kuipeleka glasi ya wisk mdomoni.
Naam Ashura alikunja uso wakati anameza kinyaji kile utafikiri alikuwa akimeza vipande vya chupa. Alifumba jicho moja na jicho lililobaki likawa likikitazama kwa makini kile kinywaji kilichokuwemo kwenye birauli. Alikohoa mara mbili mfurulizo kisha akavuta pumzi ndefu na kuziachia taratiibu.
Zawadi alipomuona shoga yake akitapatapa baada ya kuonja kinywaji kile, aliangua kicheko kilichomfanya apaliwe na mate na kujikuta na yeye akikohoa mfurulizo.
"Nyoo! Unacheka nini sasa?" Ashura alihoji huku na yeye akijichekesha.
"Aka! wacha nicheke mwenzangu, we unameza wisk utafikiri unameza furushi la miba" alizungumza Zawadi huku akiendelea kucheka.
"Kinywaji gani hiki kinakata utafikiri viwembe. Mie ndio kimesha nishinda hivyo" Alisema Ashura huku akisogeza pembeni birauli ile huku Zawadi akIendelea kukaukia kucheka.
"Bwana zawadi wacha kucheka unipe habari za kitumbua cha kihindi mwenzio" Alisema ashura.
Zawadi alijiinua kutoka pale huku akiendelea kucheka ingawa alipunguza kidogo.
"Nifuate" alisema Zawadi huku akiuendea mlango.
Ashura aliinuka pasipo kuzungumza kitu chochote na kumfuata. Walitoka chumbani na kwenda moja kwa moja hadi jikoni. Zawadi alifingua kabati lililokuwepo ukutani na kutoa chuma cha kukaangia vitumbua na kumuonesha Ashura.
"Hii ndiyo siri ya mafanikio yangu"
"Hicho si chuma cha vitumbua?" Ashura alihoji kwa mshangao
"Kwani mimi nimekwambia nafanya biashara ya nini?"
"Lakini Zawadi una masihara wewe! Hivyo vitumbua ni vya aina gani?" Ashura alizidi kupatwa na mshangao juu ya habari za rafiki yake. Zawadi akaangua kicheko kilichodumu kwa muda wa sekunde kadhaa.
"Sasa unacheka nini?"
"Ok. Ngoja nikujibu" Zawadi alizungumza huku akiwa anajizuia kuendelea kucheka. Alipeleka mkono wake usoni na kujifuta machozi ambayo yalisababishwa ba kile kicheko chake.
"Mimi nafanya biashara ya kitumbua cha kihindi"
"Sasa hapo ndipo unapo nichanganya shoga yangu"
"Nakuchanganya kivipi?"
"We umeng'ang'ania kitumbua cha kihindi...kitumbua cha kihindi, sasa mie nitaelewaje?" Ashura alizungumza kwa kunung'unika.
Zawadi akamtazama rafiki yake usoni na kujikuta akipatwa na huruma dhidi ya Ashura. Alivuta hatua na kusogea hadi pale alipokuwa amesimama Ashura kisha akaweka mikono yake kwenye mabega ya Ashura.
"Sikiliza Shoga yangu, mimi ni mfanya biashara. Lakini biashara zangu ninashirikiana na mhindi mmoja ambaye yeye ndiye aliyenipa mtaji na kunifanya niondokane na umasikini" Zawadi alizungumza kwa upole.
"Ni biashara gani ambayo unafanya wewe na huyo muhindi?"
"Kama nilivyo kwambia mwanzo, ni biashara ya vitumbua" alizungumza Zawadi na kutoa tabasamu kwasababu alifahamu jibu lile Ashura alikuwa amelichoka na hakupenda kulisikia tena.
*****
Shughuli aliyokuwa akishughulika Magosho kwa Bi. Fahreen ilipelekea mwanamke yule wa kihindi kuwa kama chizi wa mapenzi. Kwakuwa alitamani kuwa karibu zaidi na Magosho muda wote ilimbidi kumbadilishia kazi kijana yule kutoka House boy na kuwa dereva wake. Ndiyo iliwezekana, kama udereva alimfundisha mwenyewe atashindwaje kuwa dereva wake.
Kitendo kile cha kupandishwa cheo kilimfurahisha sana Magosho na kumfanya kuwa mbunifu zaidi katika kuhakikisha mama wa kihindi anaridhika kwa kila ambacho alikuwa anakihitaji kutoka kwake.
Magosho alikubali kufanya yote hayo kwaajili ya kuhakikisha mdogo wake Ashura anaishi katika maisha ya furaha na amani. Alitamani sana siku moja nay eye awe miongoni mwa watu mbele ya watu.
Bi. Fahreen alifanikiwa kumuweka karibu zaidi Magosho baada ya kumpatia kazi ya udereva. Muda wote, wakati wote na mahali popote Bi. Fahreen na Magosho walikuwa pamoja. Wakatumia mwanya huo kuponda raha na kujirusha kwa uhuru zaidi pasipokuwa na wasiwasi wowote ule.
Pamoja na kwamba Bi. Fahreen alikuwa akihisi anafanya matendo yake kwa siri, lakini kuna baadhi ya watu walikuwa wameshawashitukia na kufahamu kila kitu. Miongoni mwa watu waliokuwa wakifahamu uchafu ule waliokuwa wakiufanya wawili wale alikuwa ni pamoja na Mansoor. Ni yule yule Mansoor aliyewahi kushuhudia gemu kwa macho yake mawili kule kwenye bustani ya maua. Ni Mansoor yule yule aliyekuwa amepiga simu kumuita Mr. Nakeshwar kushuhudia uchafu wa mke wake, ni Mansoor huyo huyo aliyekuwa amepandisha hasira na kutaka kuingilia kati mchezo wa kabumbu kule kwenye bustani ya maua.
Kichwa cha Mansoor hakikukaa sawa tangu aliposhuhudia uchafu uliokuwa ukifanywa na mke wa bosi wake. Hata shughuli zake pia hakuwa akizifanya kwa ufasaha, alijilaumu sana kwa kukubali ushauri wa yule babu mlinzi wa geti la Mr. Nakeshwar.
“Yule mzee naye ni mshenzi sana, angeniacha nikawafunza adabu kunguni wale” alizungumza Mansoor huku akipeleka mikono yake kichwana na kuikutanisha kwenye kisogo.
“Pumbavu! Siwezi kuvumilia upuuzi huu. Lazima nifanye kitu” alizungumza Mansoor huku akipiga ngumi mezani kwa hasira.
Mansoor akijisogeza kwa kujivuta na kiti chake cha matairi hadi kwenye simu ya mezani ofisini pale na kuinua mkono wa simu, akabonyeza namba za simu za Mr. Nakeshwar kisha akaiweka sikioni.
Mungu hamtupi mjawake, ile simu iliita na punde simu ile ikapokelewa upande wa pili.
“Halloo” sauti ya Mr. Nakeshwar ilisikika kwenye simu.
“Yes Mr.Nakesh, Mansoor hapa naongea” Mansoor alijitambulisha.
“Oh Mansoor, habari bhana kubha?”
“Niko sawa Bosi”
“Iko problem veve, sauti iko sikika mbaya sana” Nakeshwar aliposikia tu sauti ya Mansoor alihisi kijana yule alikuwa na tatizo.
“Mimi mzima mkuu ila nina jambo nataka kuzungumza na wewe” alisema Mansoor.
“Iko mutu chezea veve?” alihoji kwa umakini.
“Ah…ah..ni kwamba…Aah..” Mansoor alijikuta akipata kigugumizi kuzungumza kile alichokuwa anakikusudia.
“Kama iko mutu chezea veve sema bhana kubha, mimi kuje toa roho yake mara moya” alizungumza Mr. Nakeshwar kwa kujiamini na majigambo ya hali ya juu.
“Naomba unisikilize kwa makini Mr.Nakesh” alizungumza Mansoor kwa msisitizo wa hali ya juu.
“Zungumuza tu bhana kubha hapana problem” Mr. Nakeshwar aliruhusu ma kusikiliza kwa makini ili kuweza
“Ni kuhusu……” Mansoor alishindwa kuendelea
“About what?”
“Ah! unajua mzee nadhani ingekuwa bora kama tungeonana” Mansoori alizungumza kwa upole.
“Ah bhana veve acha mineno yako mingi bhana kubha”
“Usiwaze Mr.Nakeshwar bwana wewe ni wangu” Mansoor alizungumza huku akijichekesha chekesha. Moyo wake ulishindwa kutoa kile kilichomfanya kumpigia simu tajiri yule wa kihindi.
“Sasa bhana Soor….”
“Ndio Nakesh”
“This week iko safari to South Africa” alisema Nakeshwar.
“Vipi mzigo upo tayari?”
“Yes, Zawadi sema Tumbua iko tayari”
“Aisee zawadi ni jembe hapendi utani na kazi, marahii KITUMBUA kipo tayari?”
“Thus why mimi iko penda sana ile toto” alizungumza Mr. Nakeshwar kwa kujitapa.
“Basi nitajitahidi niweze kufika ofisini kwako baadae” Mansoor alizungumza.
“Hapana shaka bhana kubhaa”
“Sawa Mr.Nakesh kazi njema” Mansoor alisema na kukata simu. Alirejesha mkono wa simu mahala pake na kujiegemeza kwenye kiti. Aliinua kiganja cha mkono wake wa kulia na kukipiga kwenye paji la uso huku akijisonya kwa kushindwa kumueleza ukweli rafiki yake. Alijiona ni mtendaji wa dhambi kubwa sana kwa kuto kuzungumza ukweli.
****
Magosho alikuwa amejilaza kitandani kwenye chumba chake huku macho yakiangalia juu ya dari. Kichwani mwake alikuwa akiwaza jinsi ya kuboresha maisha yake yeye na mdogowake Ashura. Ingawa kwa kiasi fulani maisha yao yalibadilika lakini hayakufikia malengo yake.
“Gosooo…” sauti ya Bi.Fahreen ilimgutusha kutoka kwenye lindi la mawazo. Kabla hajajiinua mama yule wa kihindi alikuwa amekwishaingia mle chumbani.
“Vipi Darling” Bi.Fahreen alimsabahi kwa sauti yake ya kubana.
“Shwari” Magosho alijibu kwa ufupi huku akiwa ameketi kitandani na Bi.Fahreen amesimama mbele yake.
“Iko problem?”
“Hapana”
“Mbona iko choka sana?” Bi.Fahareen alizungumza hukua akimsogelea na kwenda kuketi kitandani pamoja na Magosho.
“Hapana sina uchovu wowote?”
“Real?”
“Kweli kabisa”
“Nipe kidogo basi” alizungumza Bi.Fahreen huku akizungusha mkono wake wa kulia mgongoni mwa Magosho na mkono wake wa kushoto akimpapasa mapajani.
` “Lakini si unajua kuwa mzee yupo?” alisema Magosho kwa tahadhari.
“Mr.Nakesh hapana rudi sasa hivi” Bi.Fahreen alizungumza huku akimsukuma kumlaza kitandani Magosho ambaye hakutegemea tukio lile.
“Ngoja kwanza mama”
“What!!” Bi.Fahreen alishituka na kukunja uso kuonesha kukasirika.
“Subiri kidogo”Magosho alijitetea
“Naitaje mimi! Veve iko ita mimi mama?”
“Basi nisamehe” Magosho alijibu kwa upole
“Hapana ita tena mimi mama, sawa?”
“Sawa mpenzi”
“Good, haya nipe kidogo” alisema Bi.Fahreen huku akimpapasa Magosho sehemu za mapajani.
“Hapana mimi namuogopa Mr. Nakesh” Magosho alijaribu kujitetea lakini mama wa kihindi alionekana kutosikia maneno yake. Alichofanya ni kusaula blauzi kwa haraka kisha akarejea kifuani kwa magosho.
Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana kwa Bi.Fahreen, midomo yake myekundu ilikuwa imekwisha nata kwenye midomo ya Magosho. Kama ilivyokuwa kawaida ya kijana yule wa kibantu yaani Magosho, alipokea mashambulizi na punde watu wakawa wamehamia dunia nyingine tofauti na hii tunayoifahamu mimi na wewe ndugu msomaji.
“Oooh!” Magosho alishituka baada ya mama yule wa kihindi kugusa sehemu za magorofa ya Tandale.
“Tulia veve!” alizungumza Bi.Fahreen kwa sauti ndogo huku akiendelea kuchangamkia shughuli ile iliyokuwa imejitokeza kwa dharura.
“D a a a r l i n g…” Ilikuwa ni sauti ya Mr.Nakeshwar iliyosikika kwenye masikio ya Magosho na Bi.Fahreen. Watu wale wawili walitulia kusikiliza tena kwa makini kama masikio yao hayakuwa yakiwadanganya.
“B a b e e e” Sauti ya Mr.Nakeshwar ilisikika tena huku vishindo vya miguu yake vikisikika vikipita mlango wa chumba cha Magosho na kuelekea chumbani kwa Bi.Fahreen.
“Unaona mama!” Magosho alizungumza kwa lawama na wasiwasi mkubwa.
“Shiiiiiii” Bi.Fahreen alimnyamazisha Magosho kisha akateremka pale kitandani taratibu na kunyata kuuendea mlangoni.
Magosho alikuwa ametulia akimtazama mke wa bosi wake alivyokuwa akitetemeka kwa woga huku akijaribu kukwepa balaa lile. Ni mara nyingi sana kijana yule alinusurika kutoka mikononi mwa Nakeshwar. Lakini siku hiyo aliamini kuwa arubaini zake zilikuwa tayari zimekamilika.
Bi Fahreen alipofika mlangoni na kutaka kushika kitasa cha mlango, alishituka baada ya kusikia vishindo vya hatua za miguu ya Mr.Nakeshwar vikielekea usawa ule wa mlango wa chumbani kwa Magosho. Punde kitasa cha mlango ule kilinyongwa na baba wa kihindi akaingia chumbani mle pasipokubisha hodi.
Msomaji nakwambia ilikuwa ni pata shika nguo kuchanika mle chumbani. Kile kitendo cha kufunguliwa kwa mlango kilienda sambamba na tumbo la kuhara kwa Magosho. Ujanja wote na kujitia maufundi kwa wake wa watu ulimuishia. Nakwambia alishindwa kuhimili vishindo na kujikuta akichafua mazingira bila kutegemea.
Kwa spidi ya haraka sana Bi.Fahreen alirudi na kujibanza nyuma ya mlango huku mikono yake akiwa ameiweka mdomoni kuziba pumzi iliyokuwa ikitoka kwa sauti kubwa isisikike na kutiwa mikononi na Mwanaume yule wa kihindi.
Mr.Nakeshwar alipofungua mlango macho yake yakakutana na Magosho ambaye naye alikuwa akihaha pale kitandani huku akiwa amejifunika kwa shuka kuficha aibu ile.
“Vipi veve Goso iko gonjwa?” Mr. Nakeshwar alihoji baada ya kumkyta Magosho ameketi kitandani.
“Leo nimeshinda vibaya sana bosi” Magosho alizungumza kwa kujitetea huku sura ya aibu ikiwa imemtawala.
“Bi. Fahreen kupe veve dawa?”
“Ndio bosi, mama amenipa dawa”
“Hali iko vipi sasa?”
“Kwasasa sijambo kabisa Bosi, naweza kusema nimepona kabisa” alizungumza Magosho kwa sauti ya upole lakini iliyokuwa imejaa wasiwasi.
“Okay, where is mama?” alihoji Mr.Nakeshwar huku akiwa anazunguusha macho yake mle chumbani utafikiri alihisi uwepo wa mali yake katika chumba kile cha wazinzi.
“Mama alikuwa huko nje” alijibu Magosho kwa wasiwasi.
Mr.Nakeswar alituliza macho yake kwa magosho kwa sekunde kadhaa kama vile alikuwa akimsoma. Lakini Magosho naye alijitahidi kuficha hofu yake mbele ya mtu yule aliyekuwa hatari kwa maisha yake hasa kwa wakati ule.
“Leo toto yangu iko kwa njia from Bombay. Go na mama Airpot kupokea yeye” alisema Mr.Nakeshwar huku akiwa amemkazia macho Magosho kuashiria uzito wa maagizo yale.
“Nani Rachna?” Magosho alijitahidi kuficha wasiwasi wake kwa kuuliza swali
“Yes iko fika hapa jioni, mimi iko sehemu kwenda” alisema Mr.Nakeshwar huku akifunga mlango ule na kuondoka kwa haraka pasipo kubaini uwepo wa mke wake ndani ya chumba dereva wao.
******
Ashura alimeza funda la mate na kuitafuna midomo yake, alivuta pumzi na kuzitoa nje kisha akamkodolea macho Zawadi pasipo kuzungumza kitu.
"Ndio, hakuna cha zaidi. Kama upo tayari shoga yangu sema nikushirikishe kwenye biashara" alisema Zawadi huku mikono yake akiikumbatia kifuani na kuwa kama vile amefunga swala.
"Mie sikatai, ila ni kwamba hicho kitumbua unachokizungumzia wewe"
"Kimekufanya nini?"
"Sikijui"
"Inamaana wewe hujui vitumbua?"
"Najua, lakini hicho kitumbua cha kihindi ndicho sikifahamu"
"Na huwezi kukifahamu kama hautakuwa tayari kufanya biashara hiyo"
"Shoga na wewe, inamaana hujui kama biashara ya vitumbua ndiyo inayo niweka hapa mjini?" Ashura alizungumza.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment