Search This Blog

Wednesday, April 21, 2021

PENZI LA MTOTO WA BOSS - 4

   



Chombezo : Penzi La Mtoto Wa Boss  

Sehemu Ya Nne (4)



"Oohh! Kumbe nawe umo nikajua blaza man"

(Denis alizungumza na kumfanya Chris atabasamu)


"Hamna ujue mungu ndo kila kitu Denis kwahiyo napenda kumuamini sana mungu"

(Chris aliongea kwa hisia)


"Wawoohh basi utazidi kufanikiwa Chris kaoge halafu twende mda huo"


"Hayo ndo maisha mapya ya kijana machachari Chris ambae akikutana na mwanamke kwenye sita kwa sita lazima mwanamke aombe tena, baada ya wiki kadhaa kupita Chris na biashara yake ya kuuza madafu kwenye kijiwe kimoja hapo soko la mbezi biashara ilikuwa ikisonga kama kawaida"


"Unajua nini Denis"

(Chris alimuuliza Denis)


"Sasa nitajuaje mwanangu na hujaniambia"


"Daahh! Jana wakati wewe ulipoenda kuchukua mzigo wako si akaja mtoto wa kichua yaani mkali balaa yaani"

(Chris aliongea vile na kufanya Denis kukaa kwa makini yaani na kumsikiliza)


"Eehh! Nieleze sasa"


"Jana alishuka mtoto mmoja inaonesha kwao matajiri sana maana hiyo ndiga tu si ya nchii hii kali kinanoma, ila mimi sijamkubali kwa pesa wala ndiga yeye mwenyewe imenifanya nimuote usiku kama wife material"


"Hahahahaa"Denis alicheka


"Sasa mbona unacheka tena"

(Chris aliuliza)


"Wewe mimi nakucheka maana unamuanzia mtoto wa boss utamueza kweli wewe muuza madafu tu"

(Denis aliongea)


"Aahh! Ndugu kwa kuwa mimi sio mtu ama, acha zako"

(Chris aliongea kwa kuvunjika moyo kutokana na maneno ya rafiki yake)


"Sio hivyo wewe unawajua watoto wa kishua ni wanoko balaa"


"Hamna ujue Denis mtu akikupenda anaweza kukubadilisha tabia mimi naamini ipo siku nitamwambia japo anitukane"

(Chris hakuchoka alijipa moyo)


"Wakati wakiendelea na story lile gari aina ya Benz aliliona Chris na kumnyamzisha rafiki yake Denis"


"Oya lile gari linakuja kwahiyo kaa kimya umuone mtoto mnzuri"

(Chris alizungumza)


"Dakika chache gari likawasili na kushuka msichana mnzuri mwenye umbo namba 8 aliojengeka kila kona maneno ya vijana kipindi anaumbwa mungu alitulia kweli alibarikiwa unzuri wa aina yake"




"Mambo zenu jamani"

(Yule mdada alichuka kwenye gari na milizi wake mmoja ambae ndo alikuwa dereva wake)


"Safi dada karibu"Chris alimkaribisha


"Asante yaani niapenda sana madafu yako maana ni manzuri unayatolea wapi"

(Yule mdada aliongea kwa sauti ya utulivu na nyororo ambayo Chris ilimchanganya na kumfanya Chris asisikie swali alilokuwa akiuliza wakati huo alikuwa anamwangalia midomo ya ya msichana huyo minzuri ikiongea)


"Oyaa Chris si unaulizwa"

(Denis aliamua kumshitua Chris)


"Ooh! Unasemaje dada jamani"

(Chris alijikuta akiashituka na kuuliza)


"Hahahahaa yaani wewe bana sasa unadua nini jamani mpaka unaniita dada"

(Yule mdada aliongea)


"Hapana binadamu ndo tulivyo, ila kwani hupendi uitwe dada"Chris aliuliza


"Ndio, jina langu ni win"


"Ooh! Win lina maana ya ushindi eee"Chris aliuliza


"Ndio kwani wewe unaitwa nani"Win aliuliza


"Mimi naitwa Christopher Denis"


"Ooh Chris jina nzuri kama wewe mwenyewe"Win aliongea na kumfanya Chris ajianglie huku akitabasam


"Hamna kawaida tu Win mbona kawaida tu"Chris aliongea kwa kujitafuna tafuna


"Huo ndo ukawa mwanzo wa kufahamiana kati ya Win na Chris, mda mchache Win aliondoka na kuacha mjadala mkubwa baina ya Denis na Chris"


"Duuhh! Bonge la zari mwanangu"Chris aliongea


"Daahh! Naona umezoeana nae hafla wakati mimi nina miaka kadhaa hapa anapita tu"Denis aliongea


"Weee acha ipo siku nitamtamkia tu"Chris hakuchoka alizidi kujipa moyo


"Haya bana shauri yako ukilivuruga mara yeye anakuchukulia kama rafiki"Denis aliongea


"Story zikaendela, Upande wa Win alifika kwao alikuwa anaishi maeneo ya kawe aliingia Moja ndani haikuwa destuli yake hali iliyomshangaza sana"


"Chris ni kijana mnzuri ana umbo nzuri six pack nzuri hakika ana umbo lililotulia natamani awe mume wangu haijalishi hali yake ya maisha lazima awe wangu, sijui atanipenda mimi"

(Win alianza kumwanzia Chris)


"Upande wa Chris nae hakulala kumwanzia Win kila wakati, mpaka asubuhi kulipokucha Chris alifanya haraka awahi kazini ili amuone Win"


"Oya leo naona umewahi kijiweni nakuangalia home sijakuona"Denis alizungumza


"Aahh! Namsubiri shemeji yako mtarajiwa"Chris aliongea na kumfanya Denis acheke sana


"Yaani ndugu umerogwa na mtoto wa boss utamueza kweli"


"Mimi sikati tamaa"Chris alizungumza huku mda wote akiangalia gari kama linakuja lakini hakuliona, mara hafla alihisi mkono ukimshika nyuma ya bega na kumfanya asisimke na kugeuka kwa haraka


"Oohh! Win umenishitua kweli"Chris alizungumza


"Usijali leo nimeamua nije peke angu nataka twende tukatembea sehemu"


"Denis alishangaa sana kujiuliza, Duuhh huyu jamaa kashaopoa"


"Sawa haina shida twende home nikaoge tutaendaa"


"Siku zikapita toka Win wawe karibu bila kuelezana ukweli ndipo Win alipoamua kueleza yeye"


"Chris siku zimepita nazani leo siku ya pili tuonane na kuna kitu huwa natamani mda mrefu sana kukueleza"



"Jambo gani tena Win"Chris alimuuliza Win


"Ila samahani sana sina lengo kama la hao ulilonihadithi jinsi walivyokutamani ila ukweli nakupenda sana na katika maisha yangu washakuja wanaume wengi wenye vyeo na ila zao ila moyo wangu umeanguka kwako naamanisha nahitaji uwe mume wa maisha yangu"

(Win aliongea kwa hisia na kumfanya Chris ajione mwenye bahati hakuamini kama itakuwa raisi kama vile)


"Ama kweli mungu akikupa kilema hakunyimi na mwendo"Chris alijisemea moyoni mwake


"Vipi mbona kimya au hunitaki jamani"Win alimuuliza Chris


"Tatizo sio kama sikutaki ila ukweli ni kwamba najiuliza sana kuhusu familia yako watanikubali mimi kijana ambae kula yangu naipambania kutwa nzima je nitaweza kulipia hata kodi ya meza"


"Hapana nyumbani hawana shida maana nishawambia nitaleta mwanaume ambae nitampenda mimi hata awe muuza makopo kwahiyo haina shida kuhusu kunihudumia nyumbani pesa zipo Chris"Win alizidi kumshawishi Chris


"Chris alikubaliana na Win na Win kumueleza Chris,"


"Chris isiwe umenipenda kisa kwetu kuna pesa"


"Hapana mimi nakupenda sana tena nimeanza zamani tu"Chris alianza kumueleza Win jinsi alivyokuwa atamani awe nae lakini alishindwa


"Oohh! Wawoohh! Inawezekana ikawa mungu katujalia sisi ndo tuwe pamoja"Win alizungumza


"Ndio my love"kwa mara ya kwanza Chris akamwita jinsi la kimahaba na kumfanya Win mapigo ya moyo wake kwenda mbio


"Oohh! Jamani nakupenda"


"Mpenzi kesho nahitaji nikupeleke nyumbani"win alizungumza


"Jamani mbona mapema sana"Chris alistaajabu


"Si mapema my mimi nahitaji unioe mapema hata kesho"Win aliongea huku akimsogelea Chris na kumpapasa kifua chake


"Sasa jamani sina hata zawadi naenda kufanya nini"Chris alizungumza


"Usijali hata hayo madafu yako utapeleka maana kwetu ni familia ya kawaida sana usijali my"Win alizidi kumtia moyo mpenzi wake


"Sawa my"Chris aliitikia


"Siku hiyo Win alikuwa na furaha sana kiasi ya kwamba hadi baba na mama ake walibidi wamuulize binti yao"


"Mwanangu umefurahia nini hem tuambie"Baba Win alimuuliza mwanae


"Kiukweli wazazi wangu nimepata mtu wa ndoto yangu kijana chupavu na anaejua maisha nini nimetokea kumpenda na ananipenda sana anaitwa Christopher Denis"


"Christopher Denis??"Baba Win aliuliza


"Kwani unamfahamu baba"


"Sijui ila jina lake kama mtoto wa rafiki yangu anaitwa Denis na alinieleza mwanae kamfukuza miaka mingi sana"Baba Win alizungumza


"Aahh! Baba ukimuoona unaweza kumfahamu"Win aliuza


"Hapana kwasababu niliondoka mda mrefu sana kijiji hapo"


"Ila achana na hayo, kama umemridhia binti yetu basi ni wewe tu kuhusu kazi atakabiziwa hapa hapa endapo ndoa ikipita"Baba Win aliongea


"Ila mwanangu anakupenda kweli"Mama Win aligususia juu ya hilo


"Kama unavyojua tena mama kwa mtoto anakuwa makini sana maana uchungu wa mwana aujue mzazi"


"Mama ananipenda sana"


"Sawa sina maneno"


"Mwanangu itabidi tufanye sherehe ya kuwajisha Pete ya uchumba kabla ya ndoa"Baba Win aliongezea


"Sawa baba itakuwa lini hiyo aje"


"Kesho kutwa mida ya mchana katika ukumbi wa Kawe bichi"


"Ok sawa baba"


"Siku zote maneno ya wahenga wanasema siku hazigandi, ndivyo alivyokuwa kwa kijana Chris hakupata usingizi kwa siku kadhaa lakini siku iliyofika moyo ulikuwa unamdunda sana"


"Mpenzi kuwa huru acha tupitie shop uvae upendeze mume wangu mtarajiwa"Win alimtoa hofu Chris na kwenda shopping"


"Baada ya mda mchache Chris alitoka ndani na pamba kali, ilikuwa ni suti iliyomkaa na kuonekana kama tajiri fulani mwenye hela zakee kumbe muuza madafu, Win ndo alizidi kupenda"


"Ama kweli ukiona chang'aa ujue chahudumiwa"Win aliongea huku akimsogelea chris na kumueka sawa tai"


"Umependeza my tena sana"Win alizidi kumpamba mumewe


"Upande wapili kwenye ukumbi wa kawe bichi Baba ake Win alialika watu mbali mbali na marafiki zake wengi kila alipokuwa anaulizwa kuhusu mwanaume aliwambia ni sapraizi tu watu walipamba moto Dj nae hakupoteza mda aliendelea kutumwiza wakimsubiria bwana mchamba"


"Chris na Win hawakupoteza mda kutokana na mda ulikuwa ushaenda sana Moja kwa Moja waliwasili kwenye ukumbi kwa mda unaohitajika wawili hao walipendeza sana na kufanya macho ya watu kuwa na bumbu wazi Chris kwa aibu yake aliinamisha kichwa na kuona Haya mbele ya halaiki ya watu"


"Mda mfupi badae Chris aliwasili na makelele ya watu ambao walitamani kumuona, ile ananyanyua sura alikutaka macho kwa macho na mtu anaemfahamua na kufanya ashituke na kumwachia mkono Win"




"Chris alimuona mzee Denis ambae ni baba ake mzazi na kuduaa sana, watu wote kwenye hafla ile walishangaa kumuona muhusika yupo kwenye hali ile, mzee Denis john ambae sisi tunamtambua alikuwa rafiki wa mzee Chiza Kurwa miaka mingi iliyopita"


"Chris tatizo nini"Win alimsogelea Chris


"Chris alichoka na kukaa chini ilibidi watu wote wamsogelee kasoro mzee Denis john yeye alibaki na aibu mbele za halaki ya watu"


"Vipi mkwe shida nini"Baba Win aliuliza


"Chris alijikaza kiume na kunyoosha mkono kwa mzee Denis john na kuwafanya watu wageuke nyuma na kumuona mzee huyo akianza kulia"


"Kwani shida nini yule ni nani yako"Win ilibidi aulize


"Yule ni baba yangu jamani"Chris aliongea huku akilia kwa uchungu


"Kivipi Chris wakati uliniambia baba ako alikufukuza kijiji kwenu na huyu mzee ni tajiri wa mda tu hapa bongo"Win aliuliza


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG