Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

HOUSEGIRL WA KITANGA - 4

   


Chombezo : Housegirl Wa Kitanga 

Sehemu Ya Nne (4)


“Vipi una mishe gani huko ndani?”

“Hamna, nipo tu”

“Twende basi mgahawani jamaa anakuita” alizungumza dada Bupe kwa sauti ya chini.

“Jamaa gani?” nikahoji kwa sauti ya ukauzu huku nikijifanya sielewi chochote kumbe tayari nilikuwa nafahamu alichokuwa anakizungumzia dada Bupe.

“Acha basi Tumu, si jamaa yako” dada Bupe alizungumza huku akiendelea kujichekesha chekesha.

“Jamaa! Mimi nina jamaa gani?” nilizungumza huku sura yangu ikionekana kukosa masihara.

“Unajua usinizingue Tumu, unafikiri mimi namuongelea nanai kama sio Endru?”

“Endru ndio nani? Simjui mtu huyo!” nilizungumza na kutaka kufunga geti lakini dada Bupe aliudaka mlango na kuuzuia.

“Mmnh ngoja kwanza Tumu!” dada Bupe akazungumza kwa mshangao huku akizuia mlango usifungwe.

“Unasemaje?” nikahoji kwa ule uso wangu wa kauzu.

“Kwani mtoto wa watu amekukosea nini jamani Tumu?” dada Bupe alihoji kwa sauti ya kubembeleza lakini iliyokuwa imejaa mshangao. Mwantumu aliyezoea kumuona siku zote hakuwa Mwantu yule aliyekutana naye siku hiyo.

Nilimtazama mwanamke yule mtu mzima kwa macho makali yaliyokuwa yamejaa chuki na hasira. Kwakweli sikuweza kumuelewa lengo lake juu yangu. Nikajaribu kujifikiria alikuwa amenionaje hadi kufikia hatua ya kunitafutia wanaume mtoto wa mwanamke mwenzie. Ukisikia mtu mzima hovyo basi ndio yule. Niliinua macho yangu na kumtazama usoni kwa makini.

“Unajua dada Bupe, mimi sihitaji mwanaume yoyote yule kwa sasa” nikazungumza kwa sauti ya upole lakini iliyokuwa imejaa msisitizo wa hali ya juu.

“Eh! Mara hii umeshamtema kijana wawatu?” dada Bupe alizungumza kwa mshangao.

“Kijana gani? Mbona mimi sina uhusiano wowote na huyo mtu!” nikajaribu kueleza kwa sauti ya msisitizo.

“Eh! Ndio mapenzi ya kitanga hayo?” dada Bupe aliendelea kuhoji kwa kebehi.

“Naomba unielewe dada Bupe, nimekuja hapa kufanya kazi na sikuja hapa kutafuta wanaume” nikatoa maelezo mafupi lakini yaliyokuwa yamejaa uzito.

“Mnh! Ndio kusema Imran amekwisha chukua goma nini, au ndio mapenzi motomoto na Fadhili yamenoga?” Dada Bupe akahoji kishambenga.

“Ni wewe wasema”

“Sasa nikamwambiaje?”

“Nani?”

“Si baby wako Endru”

“Kwaheri dada Bupe, naona kama vile haunielewi” nilizungumza na kuanza kufunga geti dogo ambalo mara nyingi hutumiwa na watu kuingilia.

“Kwahiyo nikamwambiaje?” alihoji dada Bupe nilipokuwa nafunga geti.

“Kamwambie simtaki, tena akome kunifuatilia!” nikazungumza kwa jazba huku nikiwa nimekwisafunga geti na kurejea ndani.

***

Maneno yangu yalimfedehesha sana dada Bupe. Hakuweza kuamini kama kauli zile kali zilikuwa zikitoka kwenye kinywa cha binti wa kitanga ambaye alifikiria ni msichana mrahisi rahisi na wa kuchezea hovyo hovyo. Nakwambia mtu mzima sura ilimshuka na kumporomoka utafikiri ftari ya magimbi. Akarudi mgahawani kwake huku amechoka hoi utafikiri ametoka kufanya kazi ya kuchanganya zege.

“Vipi sister, mrembo wangu yuko wapi?” Ilikuwa ni sauti ya Endru ambaye wakati wote alikuwa ameketi mgahawani akinisubiri kwa hamu kubwa.

“Mrembo gani?” dada Bupe alihoji kwa mkato huku akivuta kiti na kuketi.

“Kwani tumekubaliana ukamuite nani? Si mtoto wa kitanga”

“Hakuna cha mtoto wakitanga wala mtoto wa kisumbawanga” Dada Bube akazungumza kwa sauti ya kukata tamaa.

“Kwani kumetokea nini sister, mbona umepoa ghafla?”

“Mimi nilikwambia kuwa kale katoto kana mashetani ukanibishia, sasa utaamini” dada Bupe akazungumza kwa msisitizo.

“Kwani kamekuwaje?”

“Yani nakwambia kamenishushua utafikiri mtoto mwenzake” alizungumza dada Bupe kwa jazba.

“Ah we ungemwambia mimi ndio namuita”

“Haaa! Yani wewe ndio hakutambui kabisaa, utadhani hakuwahi kukuona tangu azaliwe.” Dada Bupe alieleza kwa msisitizo.

“Wewe dada Bupe bwana umeharibu, ingekuwa mimi wala asingezingua, mtoto tayari nimekwisha mseti”

“Sasa si uende mwenyewe kwani unashindwa nini?”

“Umenipeperushia ndege wangu bwana”

“We chizi nini!” dada Bupe alizungumza kwa hasira na kuamka kutoka kwenye kile kiti na kuelekea jikoni.

“Unakwenda wapi sasa?”

“Achana na mimi wewe” alizunguma dada Bupe huku akichukua ndoo na kuiweka bombani kwaajili ya kukinga maji.




“He! Kwahiyo ndio umekasirika sasa?”

“We unafikiri yule ni kama visichana vyako vya chuo ulivyozoea kuvichezea” Alizungumza dada Bupe huku akifungua bomba la maji.

“Wewe si ndiye ulinambia kapo simple”

“Yani kama unamtaka yule mtoto, unatakiwa ujipande mdogo wangu” alizungumza dada Bupe huku akifunga koki na kubeba ndoo kwa mkono wa kuume kuisogeza karibu na jiko.

“Ah hiyo kazi ndogo sister, maji nikiyavulia nguo lazima niyaoge. We mwenyewe si unanijua bwana” Endru alizungumza kwa kujitapa na kujiamini.

“Nakujua lakini kwa hiki kisirani, sijui kama utakiweza”

“Sasa ngoja nikuthibitishie kama mimi ni Endru” alizungumza kijana yule kwa kujitapa.

“Haya bwana langu mimi jicho, nasubiri kuona huo Uendru wako” alizungumza dada Bupe huku akimsindikiza kwa macho Endru akiondoka kwa vishindo vya kujiamini huku akijitanua utafikiri tai.

****

Tangu nilipokuwa nimefika nyumbani pale sikuwahi kumuona Fadhili akiwa amekarisika kama ambvyo alikuwa amekasirika siku hiyo. Hata mchana hakurudi kula chakula pamoja na kumsuiri kwa muda mrefu bila mafanikio. Niliumia sana ndani ya moyo wangu kwasababu sikuwa napenda kumuudhi mwanaume ambaye nilikuwa nampenda. Nikabakia kulaani sana kitendo alichokuwa amekifanya kaka Imrani cha kugombana na Fadhili wangu.

Nikiwa kitandani pale na mawazo yangu niligutushwa na mlango wangu wa chumbani ukigongwa. Nilikurupuka na kwenda kufungua upesi upesi.

“We vipi mbona umelala saa hizi, hatuli leo?” mama alizungumza mara tu nilipofungua mlango.

“Ah samahani mama nilikuwa nimejipumzisha kidogo tu, naona usingizi umenichukua jumla” nilizungumza huku nikitazama saa iliyokuwepo kwenye ukuta wa chumbani mle na kubaini kuwa ilikuwa saa mbili usiku.

“Hebu fanya mambo basi watu wale” alinambia mama kwa lugha ya upole baada ya kubaini kweli nilikuwa nimepitiwa na usingizi kutokana na shughuli za hapa na pale nyumbani mle.

“Chakula tayari kimeiva mama, bado kupakua tu” nikazungumza huku nikimtazama mama usoni kwa wasiwasi.

“Pakua basi watu wale, saa mbili hii upo ndani unasema chakula kimeiva, kwahiyo kijipakue chenyewe?” mama lihoji kwa msisitizo.

“Hapana mama” nikajibu kwa upole

“Au unataka tukapakue wenyewe jikoni?” mama alihoji huku akigeuka na kuondoka.

“Hapana mama, naomba nisamehe” nilizungumza huku nikimfuata nyuma na kukatiza kulia kuingia kwenye mlango wa jikoni.

Nilipofika jikoni nilianza kazi ya maandalizi ya msosi, nilipokuwa nimesimama kwenye shelfu ya vyombo nikifuta sahani kwa kitambaa nilihisi mwili ukinisisimka ghafla. Ilikuwa ni mikono ya mtu ikitambaa maeneo ya kwenye kiuno changu na kupanda hadi karibu na madafu yangu ya kifuani.

Nilitulia na kusikilizia hali ile huku nikijaribu kutafakari mtu ambaye alikuwa akifanya kitendo kile angekuwa ni nani. Niligeuka taratiibu huku nikiinua macho yangu kutazama nyuma. Nilimkuta kaka Imran akifanya kitendo kile huku akitoa tabasamu.

“Ah jamani kaka Imran wewe!” nilizungumza na kujifanya kushituka baada ya kugundua kuwa alikuwa ni kaka Imran. Muda wote nilikuwa nimetulia nikiamini kitendo kile kilikuwa kinafanywa na Fadhili wangu.

“Niambie mrembo” kaka Imran alizungumza kwa sauti ya chini.

“Niache nipakue bwana” nilizungumza huku nikikunja bega moja alipojaribu kunigusa shingoni.

“Mbona hujanambia kama nguo umezipenda?”

“Nimezipenda” nikazungumza kwa mkato.

“Leo nataka ujaribu zile ndogo nikuone zinavyokukaa”

“Mnh zipi?” nikahoji kwa mshangao niliposikia nguo ndogo.

“Zile zenye kamba kwa huku nyuma”

“He yani nguo za ndani”

“Ewaa! Hizo hizo”

“Mnh mie siwezi, kwanza za vile mie sivai”

“Acha ushamba wewe mimi nitakufundisha namna ya kuzivaa” alizungumza kaka Imran huku akirudi nyuma na kutoka jikoni mle na kuniacha katika dimbwi la wasiwasi na maswali yaliyokuwa yamejaa mashaka. Sikupenda kabisa kuwa karibu na kaka Imran kwasababu nilihofia ningemuudhi mpenzi wangu Fadhili amaye ndiye niliyeamua kuwa naye.

Wakati kaka Imran alipokuwa anatoka jikoni malangoni alikutana na Fadhili aliyekuwa akitokea chumbvani kwake. Walitazamana kwa sekunde kadhaa kama vile kila mmoja alikuwa na maswali juu ya mwenzake halafu kaka Imran alielekea ‘sittingroom’ na Fadhili akabakia amesimama karibu na mlango wa jikoni.

Kaka Imran alivyopotea kabisa Fadhili naye aliingia jikoni na kunikuta nikiendelea na mishemishe za maandalizi ya chakula cha jioni. Fadhili hakufanya kama alivyokuwa amefanya kaka Imran, yeye alipofika alisimama hatua kadhaa kutoka nilipokuwepo nimesimama mimi. Mkono mmoja alikuwa ameuweka ukutani na mkono mwingine ameuweka kiunoni. Alikuwa kama vile ananitafakari.

“Naomba unisamehe kaka Fadhili” nilizungumza mara tu nilipomuona amesimama huku sura akiwa ameikunja.

“Nikusamehe kwa lipi?” akahoji kwa sauti kavu.

“Kwa kuchelewa kuandaa meza ya chakula” nilizungumza huku nikiendelea kufanya shughuli zangu kwa haraka haraka.

Fadhli hakujibu chochote zaidi ya kutoa tabasamu la kujilazimisha kiasi ambacho nikamsoma kuwa hakuwa amenielewa.

Mama aliingia ghafla jinkoni na kumkuta Fadhili akiwa amesimama akinikodolea macho huku akitoa tabasamu lake la dharau.

“Na wewe unafanya nini huku jikoni?” mama alihoji kwa sauti.

“Leo nimekuja kuonja” Fadhili alijibu kwa masihara kama ilivyokuwa kawaida yake kupenda utani.

“Ebu toka hapa, ndomaana chakula kinachelewa kutoka kumbe unamsumbua mwenzio huku” mama alizungumza kwa sauti kali kiasi cha kufanya hata waliokuwepo sebleni kusikia maneno yale.

“Lakini mama kwani kuna kosa gani?” Fadhili alizungumza huku akitoka jikoni.

“Kwenda zako huko, utapewa kazi ya kuonja mchuzi bure” mama alimsindikiza Fadhili kwa maneno hayo.

Mama alinisaidia kuandaa chakula kutokana na muda kwenda sana jambo ambalo halikuwa limezoeleka ndani mle. Tayari ilikuwa inalekea mishale ya saa tatu usiku pasipo chakula kuonekana mezani.

****

Maneo aliyokuwa anazungumza mama kwa sauti kumwambia Fadhili yalisikika masikioni mwa kaka Imra. Moyo wake ukajaa dukuduku na hasira dhidi ya kitendo kilichokuwa kimefanywa na Fadhili kuja jikoni. Hakuelewa jikoni kule Fadhili alipokuwa ameingia alinifanyia nini. Mawazo yake yakamtuma kuwa kwakuwa yeye alipoingia alifikia kuuchezea mwili wangu basi akahisi hata Fadhili naye alifanya kama vile.

Macho ya Imran na macho ya Fadhili yakakutana wakati Fadhili alipokuwa akielekea sebleni pale.

“Hivi wewe utakua lini?” kaka Imran alihoji kwa hasira.

“Aliyekwambia utangulie kuzaliwa ni nani?” Fadhili maye akahoji kwa kiburi baada ya kubaini kuwa kaka yake alihoji kwa hasira.

“Yani mtu mzima unafanya mambo ya kipuuzi au una laana wewe!?” kaka Imran alizungumza kwa hasira.

“Jaribu kujiheshimu Bro” Fadhili alizungumza huku akiketi kwenye kochi.

“Unaniambiaje wewe?”

“Achana na mimi wewe” Fadhili alizungumza kwa ufupi.

“Mama mwanao namtwanga leo” kaka Imran alizungumza huku akiinuka alipokuwa ameketi na kutaka kwenda kumvaa Fadhili.

Fadhili naye aliinuka kutoka kwenye kochi na kujiweka sawa tayari kwa mapambano dhidi ya kaka yake.





Mama alifika na kuingilia kati huku akionekana kukasirika kutokana na tukio lile lililokuwa likiendelea kule sebleni.

“Nyie wash##@zi nini” mama alizungumza kwa kuwatusi watoto wake.

“Mwache aje aone kama sija mtoboa pua lake hilo” Fadhili alizungumza kwa hasira huku akiokota chupa ya soda iliyokuwepo mezani.

“We lete kiburi tu kwasababu umemuona mama yako hapa” kaka Imran akazungumza kwa hasira na jazba.

“Nimesema kimya!” mama alitoa amri kwa ukali.

Kwakuwa vijana wote walikuwa wakimtii mama yao kila mmoja alikaa kimya kweli na kurudi alipokuwa ameketi. Mama aliwatazama kisha akaachia msonyo wa hasira.

“Nyie wajinga nini! Alaa!”

Kule jikoni niliweza kusikia kila kitu kilichokuwa kinaendelea sebleni. Niliogopa sana kwasababu siku zote nilikuwa sipendi kugombanisha watu. Ukizingatia zaidi ni kwamba watu wenyewe walikuwa ni ndugu.

Nilitoka na kuanza kuandaa meza ya chakula haraka haraka. Nilijifanya kama vile sikuwa nawaona ama kuwasikia walichokuwa wanakizungumza.

Mama alimgeukia Fadhili na kumtazama kwa sekunde kadhaa huku akimsoma na kumtafakari.

“We Fadhili hiyo adabu umeitoa wapi, Hujui kama huyu ni kaka yako?” alisema mama kwa msisitizo.

“Hata kama ni mkubwa anatakiwa kujiheshimu bwana” Fadhili alizungumza kwa jazba.

“Mama mwanao nawaambia mtakuta siku nimembanika jikoni huyu” Imran alizungumza kwa hasira.

“Thubutuuu! Nakwambia wewe hunibabaishi hata kwa sekunde moja” Fadhili alizungumza kwa dharau huku akimuoneshea kidole kaka Imran

“Mama unamuona! Unamuona mwanao?” Imrana alizungumza kwa hasira.

“Nyie watoto mtaniua kwa presha, hebu tulieni” mama alizungumza kwa kufoka.

“Mie nitamzibua mtoto wenu huyu!” alifoka Imran

“Kwenda zako kule, kwanza sina undugu na wewe. Mama huyu sio ndugu yangu nyie mmemuokota kwenye mitaro huyu!” Fadhili alizungumza kwa jazba na kebehi.

“Mama mtanisamehe” kaka Imran alisema na kusogea kwa kasi kumfuata Fadhili alipokuwa amesimama. Mama alimdaka na kuanza kuminyana naye kumzuia asisogee kule alipo Fadhili.

“Fadhili mwanangu nenda ndani” mama alipaza sauti huku akiminyana na kaka Imran.

“Mama mwache aje nimpasue pua lake hilo lililokaa kama fungu la magimbi” Fadhili alizungumza kwa hasira huku akiwa ameshikilia chupa ya soda mkononi ambayo alikuwa ameichukua juu ya kabati.

Kumbe wakati kaka Imran na Fadhili walipokuwa wanarumbana baba alikuwa amesimama kwenye kona ya korido ya kuelekea vyumbani akiwatazama vijana wake walivyokuwa wanapimana viwango vya ubabe.

Kaka Imran alipokuwa katika harakati za kuminyana na mama alimuona baba akiwa anamtazama kwa macho makali. Imaran alitulia na kurudi nyuma kwa unyonge.

“Vipi endeleeni tu” alisema baba huku akivuta hatua kwenda kuketi kwenye kochi lililokuwepo kwenye kona sebleni pale.

Kaka Imran alirudi na kwenda kuketi kwenye kochi huku akionekana kuwa mdogo kama mdudu chungu. Fadhili naye aliweka chupa ile pembeni kisha naye akaelekea kuketi alipokuwa awali.

“Haya niambieni huwo ubondia mmeusomea wapi?” baba alihoji kwa sauti ya chini lakini iliyokuwa na msisitizo.

Fadhili na Imran wote wawili walitulia kimya pasipo kutamka neno lolote. Kila mmoja alionekana kuwa mpole kuliko mwenzake.

“Hawa watoto watakuwa na mapepo mume wangu” mama alizungumza kwa hasira.

“Heti nyie, tatizo ni nini?” baba alihoji.

Hakuna ambaye alijibu swali lile lillokuwa limeulizwa na baba.

“Si naongea na nyie! Viziwi au viburi?” baba alibadilika na kuzungumza kwa sauti kali na ya juu.

“Baba huyu mtoto mnamlea vibaya sana!”: kaka Imran alizungumza baada ya kuona baba amekasirika.

“Haya tufundishe namna ya kulea” alisema baba.

“Sio hivyo baba”

“Kumbe ni vipi?”

“Leo asubuhi nimemkuta chumbani kwa Mwamtumu” kaka Imran alijaribu kueleza.

“Unasemaje wewe?” baba alihoji kwa msahangao baada ya kusikia kauli ile.

“Ndio nimemkuta chumbani kwa Tumu, nilipomkanya akanijia juu na kunitukana” alisema kaka Imran kwa msisitizo.

Baba alimtazama Fadhili kwa sekunde kadhaa huku ndani ya moyo wake kukionekana wazi kulikuwa na dukuduku. Hali ya wivu ilitawala nafsi yake na kuhisi kuzidiawa kete na kijana wake mwenyewe. Aligeuza macho yake na kuyarudisha kwenye sura ya kaka Imran.

“Enhe na wewe hadi unamkuta Fadhili chumbani kwa Mwantumu, wewe ulikuwa unatafuta nini?” baba alihoji kwa msisitizo huku akitetemeka kwa hasira.

“Ah sio kwamba nimemkuta chumbani…”

“Kumbe aliyesema amemkuta Fadhili chumbani kwa Tumu ni nani?” baba alihoji.

“Ni mimi baba”

“Sasa mbona unakataa tena?”

“Maana yangu ni kwamba, nimemuona akitoka chumbani kwa Mwantumu” kaka Imran alirekebisha kauli yake.

“Enhe we Fadhili ni kweli maneno haya?’ alihoji baba kwa msisitizo.

“Ndio baba, nikweli nilikuwa chumbani kwa Mwantumu” Fadhili alijibu pasipo na hata chembe ya wasiwasi.

Wakati anazungumza maneno hayo nilikuwa kwenye friji nikitoa maji ya kunywa pamoja na juisi. Moyo wangu ulishituka sana kwasababu sikutegemea kama Fadhili angeweza kukubali kirahisi kiasi kile. Nilielewa wazi kuwa kasheshe ingeongezeka zaidi kama baba angebaini kuwa Fadhili aliingia chumbani kwangu.

“Unasemaje!” baba alihoji kwa kuhamaki.

“Ndio, leo mchana wakati Imran ananiita nilitokea chumbani kwa Mwantumu” Fadhili aliendelea kusisitiza jibu lake.

“Ulikuwa unafanya nini, na Mwantumu alikuwa wapi wakati huwo?” baba alihoji huku akionekana kuzidi kupandwa na hasira.

Nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kufanya haraka pale kwenye friji kisha nikaondoka. Nilihofia sana kushirikishwa katika kesi ile ambayo ilikuwa inanihusu moja kwa moja. Nilielekea jikoni na kuwaacha wakiendelea na kasheshe yao.

“Tumu alikuwepo chumbani kwake” alijibu Fadhili kwa upole.

“Kwahiyo mlikuwa pamoja?”

“Ndio baba”

“She&#zi mlikuwa mnafanya nini chumbani?”

“Tulikuwa tunapiga stori baba” alijibu Fadhili kwa kujiamini.

“Pum#$@vu! tabia hiyo mmeanza lini?” baba alifoka huku povu likimtoka mdomoni na macho ameyatoa utafikiri kingwendu.

“Mnh, lakini kwa upande wangu mimi sijaona tatizo lolote” mama ambaye alikuwa akisikiliza kwa makini mahojiano yale alizungumza.

“Hujaona tatizo mtoto wako kuingia chumbani kwa mtoto wa kike, si ndio?” Baba alihoji huku akiwa amemkazia macho mama.

“Tumu ni mtoto wa humu ndani, na Fadhili ni mtoto wa humu ndani. Sasa kukaa pamoja ubaya uko wapi?” mama aliendelea kumtetea Fadhili.

“Sikiliza we mwanamke, Fadhili ni mtoto wa kiume itawezekana vipi wasikae kooote huko waende kujifungia chumbani?” baba alihoji.

“Mimi sijaona tatizo” mama alizungumza kwa mkato.

“Jamani nawaambieni mtoto wenu huyu mnamlea vibaya, ona sasahivi amekutwa amekaa jikoni” kaka Imran alidakia na kuibua kitu kipya.

“Kwani kuingia jikoni kuna kosa gani?” Fadhili alihoji.

“We mtoto wa kiume jikoni unatafuta nini?” Imran alihoji.

“Kile ulichokuwa umekwenda kukifanya wewe ndicho hicho nilichokwenda kukifanya na mimi huko jikoni” Fadhili alijibu kwa msisitizo kwasababu alimuona kaka Imran alipokuwa anatoka jikoni.

“Haa! Baba katoto kenu haka katawaponza, mnakaona hakana hata adabu” Imran alizungumza kwa hasira baada ya kuambiwa kuwa alichokuwa anakifanya yeye kwa Mwantumu ndicho alichokuwa anakifanya Fadhili. Alikumbuka jinsi alivyokuwa akinishikashika kule jikoni, kwa maana hiyo hata Fadhili naye alikuwa akinishika shika. Akajikuta hasira zikiongezeka mara dufu. Alitamani kumfuata na kumtandika lakini uwepo wa wazazi ulimletea kikwazo.

“Wewe utakuwa na lako jambo!” mama alisema huku akionesha kidole kwa kaka Imran.

“Hivi ni kwanini unamtetea sana huyu mwanao?” baba alihoji kwa hasira kwasababu nayeye alikuwa ameshikwa na wivu dhidi juu yangu. Hakupenda kabisa kuona kijana wake yeyote yule anajiweka karibu na mimi, mwenyewe alikuwa akiniita kamchepuko.

“Mnamuonea bwana, kwani kuzungumza na mtu ni kosa?” mama aliendelea kumtetea kaka Fadhili.

“Sio kosa, lakini….” Baba alitaka kuzungumza kitu lakini akaishia njiani.

“Lakini nini? Malizia!” mama alihoji huku akiona Fadhili alikuwa anaonewa.

“Mimi nikiwa kama baba wa ndani humu, sitaki kumuona mtu yoyote yule akifanya tena mambo ya kipuuzi kama hayo. Na kama mtu anajiona amekuwa basi ndani humu ahame” baba alizungumza kwa msisitizo huku ametoa macho.

“Lakini baba….” Fadhili alitaka kuzungumza kitu lakini baba akamzuia kuendelea.

“Kimya! Sitaki kusikia chochote. Sitaki mtu yeyote humu ndani awe na mazoea na Mwantumu” alisema baba kwa amri na msisitizo.

“Na kwanini unazungumza hivyo, ni kitu gani kinaendelea?” Mama alihoji kwa mshangao huku akionekana kuhisi jambo fulani lililokuwa likiendelea kati yangu mimi na baba.

“Unanivunjia heshima enh?” baba alihoji kwa kujihami.

“Sio kukuvunjia heshima, naona sikuelewi”




“Sasa kama haunielewi utaelewa siku nitakapomkuta huyo mwanao anafanya utumbo wake tena” baba alizungumza huku akijiinua kutoka kwenye kochi alipokuwa ameketi.


“Heti marufuku mtu kuwa na mazoea na Mwantumu, kwa lipi hasa?” mama aliendelea kuzungumza kwa jazba.


“Nimekwisha sema nimemaliza” baba alizungumza huku akiondoka kuelekea chumbani kwake.


“Fadhili, usimuogope mtu yoyote yule. Unaweza kumzoea Mwantumu kwa vyovyote vile” mama alizungumza kwa jazba huku tayari wivu ulikuwa ukimtafuna ndani ya moyo wake. Hisia za kuibiwa mume wake na mwantumu tayari zilikwisha kuchipua ndani ya ubongo wake.


“We mama endelea kumdekeza tu huyo mtoto wako. Labda kama unataka kulea mimba za nje ya ndoa hapa ndani” kaka Imran alizungumza na kuinuka kwenye kochi.


“Kwendeni zenu huko, mnamuwekea mipaka mmemzaa ninyi huyu binti?” alisema mama.


“Sawa ila kukitokea matatizo tusishirikishwe” alizungumza kaka Imran huku na yeye akivuta hatua kuelekea chumbani kwake.


“Imran naona umekua sasa, unafikia hatua ya kunijibu mimi kama unajibishana na mtoto mwenzio” Mama alizungumza kwa jazba huku akimtazama Imran akipita kuelekea chumbani.


“Mama wachana nao hao wasije wakakuua kwa presha bure” Fadhili alizungumza baada ya kumuona mama yake akiwa amepaniki.


“Na kama hoja ni Mwantumu humu ndani, nitamrudisha kijijini, haki ya mungu vile anarudi kwao Tanga” mama alizungumza huku akielekea chumbani kwa mwendo wa kushindilia hatua chini utafikiri roboti.


Nikiwa nimejibanza kwenye korido karibu na mlango wa kuingilia jikoni, mapigo ya moyo yalikuwa yakienda mbio. Nilifahamu wazi kuwa mimi ndiye niliyekuwa chanzo cha mfarakano ule.


Sijui ni nani alikuwa sahihi pale lakini nilichokuwa nakifahamu mimi ni kwamba kila mmoja alikuwa akijaribu kulinda na kutetea penzi lake na binti wa kitanga. Kaka Imran alikuwa anaona wivu na kuhofia mwanamke aliyekuwa anamtaka kuchukuliwa na mdogo wake Fadhili. Baba naye alikuwa anajaribu kulinda penzi lake na binti wa kitanga lisije likamegwa na vijana wake Fadhili na Imran. Na kwa upande wa Fadhili nako alikuwa amekasirika baada ya kuhisi kaka yake Imran amemkatizia kwa mbele na kumnyakua msichana aliyetokea kumpenda ghafla.


Sittingroom alikuwa amebakia Fadhili pekeyake akiangalia TV ambayo hata hakuwa anaelewa kilichokuwa kinaendelea. Wengine wote waliondoka na kuelekea vyumbani mwao kulala. Nilijitoa pale nilipokuwa nimejibanza na kusogea taratibu hadi alipokuwa ameketi Fadhili.


“Kaka Fadhili” niliita kwa sauti ya chini nilipomkaribia.


“Nikusaidie nini?” alijibu Fadhili kwa mkato


“Kwani kuna nini?”


“Nenda ukamuulize basha wako!” Fadhili alijibu kwa mkato pasipo kunitazama.


Sikuweza kufahamu aliposema nikamuulize basha wangu alikuwa anamkusudia baba au kaka Imran.


“Basha wangu ndio nani mbona sikuelewi?”


“Bwana usinichanganye naomba uniache” Fadhili alizungumza kwa ukali na kujieka vizuri pale kwenye kochi.


“Samahani mpenzi wangu unajua nakupenda sana” nilizungumza kwa upole baada ya kuhisi dalili za kumpoteza mwanaume ambaye alikuwa ameukonga moyo wangu kuliko mtu yeyote yule ndani mle.


“Toka zako hapa! Mpenzi wako nani?” Fadhili alizungumza kwa jazba.


“Lakini Fadhili Baba, kwani mimi kosa langu ni lipi?” nilijaribu kuzungumza kwa kubembeleza.


“Koma mbwa wewe! Naomba usijishebedue shebedue mbele yangu”


“Lakini nakupenda Fadhili” nikazungumza kwa kubembeleza.


“Wewe, kwahiyo wewe ni fundi wa kupenda sio?”


“Vyovyote vile, ila elewa kuwa mimi nakupenda”


“We ni shetani wewe! Ibilisi! Pepo! Zimwi! Kibarabara! Nyang’au” Fadhili akazungumza kwa hasira na jazba huku akinioneshea kidole kuashiria msisitizo.


“Hata kama uniite kibweng au msukule utajua mwenyewe lakini mimi nakupenda” nikazungumza kwa msisitizo huku nimemkazia macho.


“Utapenda wangapi hata haya huna! Kaone vile kabayaa!”


“Sasa mimi nimempenda nani mwingine kama sio wewe pekeyako”


“Nyoko! Malaya mkubwa wewe!” Jamani nyie Fadhili alikuwa akizungumza polepole kama vile hataki lakini maneno aliyokuwa anayafyatua yalikuwa yakichoma kama mshale.


“Lakini unanionea Fadhili, mimi kukupenda wewe ndio nimekuwa Malaya jamani” nikajaribu kulalamika mtoto wa kike.


“Hivi kwanini usiniache Mwantumu, au unataka na roho yangu?”


“Fadhili mimi sikuachi, Nakupenda! Nakupenda! Nakupenda!” nikazungumza kwa msisitizo kisha nikamsogelea na kumpiga busu la kwenye mdomo na kurukia pembeni.


“Shenzi wewe!” Fadhili akazungumza kwa sauti ya ukali huku akijaribu kunikamata bila mafanikio. Akaachia msonyo wa hasira kisha akainuka na kuelekea chumbani. Alihisi kama angeendelea kubaki pale ningeweza kumtia kidole cha macho.


Nilibakia nimesimama nikimkodolea macho kijana yule akiondoka. Nikajitupa kwenye kochi huku nikiwa hoi bin taabani. Chakula nilichokuwa nimekiandaa mezani hakikuweza kupata mlaji hata mmoja. Masikini ya Mungu mwenzenu mie nilihisi kama vile nilkuwa na mkosi.


Maneno ya mama ya kunirejesha kijijini yalinijia kichwani na kunifanya niingiwe na wasiwasi zaidi. Sikutamani kabisa kuacha kazi na kurudi kijijini kwasababu tayari matamu ya mjini nilikuwa nimekwishaanza kuyazoea. Nilipokumbuka habari za kushika jembe ndio kabisaa sikutaka hata kusikia habari za kijijini. Nikainua mikono juu kumuomba Mungu anilinde dhidi ya mpango ule wa mama.


****


Usiku wa siku hiyo ulikuwa mgumu sana kwangu. Kila mara lile tukio la ugomvi lililokuwa limetokea usiku huo lilikuwa likijirudia kwenye ubongo wangu. Sikuweza kuamini kama mimi ndiye niliyekuwa chanzo kikubwa cha varangati lile la usiku ndani ya familia ya mzee Sekiza. Kwakweli Mungu anisamehe sana kwa tukio lile pamoja na kwamba sikuwa nahusika moja kwa moja.


Kitu kingine ambacho kilininyima usingizi usiku huo ni zile kauli za Fadhili alizokuwa akinitamkia bila huruma. Pamoja na kwamba nilijidhalilisha kwa kumuonesha kuwa nampenda jambo ambalo ni kinyume na maadili ya kiafrika lakini mwanaume yule hakuitambua thamani yangu. Yani kweli? Niliumia sana na kujikuta nikishindwa kuzuia machozi kufanya ziara kwenye mifereji ya mashavu yangu.


Kwa kiasi Fulani nilianza kujutia uamuzi wangu wa kumchagua Fadhili kuwa kipenzi cha roho yangu. Sijui ni kwanini nilikurupuka na kujikuta nikidondokea kwenye penzi la mtu ambaye hakuwa ananihitaji wala kujali thamani ya hisia zangu. Au sina mvuto kama wasichana wengine warembo? Au mavazi yangu ya magunia kama alivyosema dada Bupe ndiyo ambayo yanamfanya Fadhili asinikubali? Mbona walikuwepo wanaume wengi sana ambao walitamani sana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mimi? Kwakweli sikuelewa kosa langu lilikuwa wapi.


Kutokana na mambo ambayo alikuwa amenifanya Fadhili nikajikuta nikikumbuka siku niliyokuwa nimekutana na Endru kule mgahawani kwa dada Bupe. Sasa kama mtu anakuambia anakupenda halafu yule ambaye wewe unampenda yeye hana mpango na wewe, unafikiri ni kitu gani kinachofuata? Ndio nilianza kuhisi kitu juu ya Endru ndani ya moyo wangu. Mbona Endru alikuwa ni kijana mzuri, mchangamfu, mtanashati, ana alionekana ni mwanaume mwenye kujali. Sasa kwanini niiamua kumtema na kulazimisha penzi la mtu ambaye hatambui thamani yangu.


Kwa kiasi Fulani nilianza kujutia maamuzi yangu ya kumkataa Endru na kumfanyia vituko dada Bupe ambaye alikuwa kiunganishi kati yangu na Endru. Nikakumbuka jinsi nilivyo mjibu jeuri dada Bupe na kumtimua kama paka mwizi wakati alipokuja kuniita nikaonane na Endru.


“Mungu wangu kwanini nimempoteza mwanaume aliyekuwa ananipenda!” nilizungumza na kujikuta nikiketi kitako kitandani.


“Ama kweli mapenzi ni fumbo gumu sana, unaweza ukatumia nguvu nyingi sana kumpenda mtu, kumbe yeye hana hata wazo na wewe. Na hata kama ukijitoa mhanga na kumfahamisha kuwa unampenda yeye haguswi wala hatikisiki. Na hivyo ndivyo nilivyogundua kwa Fadhili.


Hata hivyo wasiwasi niliokuwa nao na hofu ya kumpoteza Fadhili ulipotezwa na mawazo yaliyojileta ghafla kichwani mwangu. Na mawazo yenyewe yalikuwa ni juu ya Endru.


Ilinijia taswila ya tukio lililokuwa likijitokeza mgahawani pale siku nilipokutana na Endru kwa mara ya kwanza. Tabasamu la matumaini likachanuya ndani ya moyo wangu. Uzuri wa kijana yule ulijitokeza mbele ya macho yangu huku sura yake nikiiona ikinitolea tabasamu la huba. Nilivuta mikono na kuikumbatia kwa upendo juu ya kifua changu.


“Endru wewe ni kijana mzuri sana” nilizungumza huku nikipapasa kifua changu na macho nikiwa nimeyafumba kidogo kwa hisia.


“Naamini wewe ndiye mwanaume uliyezaliwa kwaajili yangu” nikaendelea kuzungumza huku nikijipindua pindua kitandani kwangu.


“Naomba unisamehe sana kwa kuto thamini hisia zako” nikaendelea kuzungumza pekeyangu pale kitandani.


“Kama kweli utanioa watoto wangu watakuwa wazuri kama wewe Endru” mawazo yangu yalihama kabisa kutoka kwa Fadhili hasa baada ya kukasirikiwa na kususiwa hata chakula. Sijui ni kwanini Endru alikuwa amezivuta hisisa zangu ghafla kiasi kile.


Hali ile ya kukosa usingiz iliendelea kunitawala hadi asubuhi kulipopambazuka na jua la siku mpya kubisha hodi. Niliamka asubuhi na mapema na kufanya shughuli zangu za kila siku. Ilikuwa ni asubuhi ngumu sana kwangu kwasababu sikufahamu watu wale ambao walilala kwa kuhitilafiana wangeamka vipi. Tangu nilipokuwa nimefika nyumbani pale sikuwahi kushuhudia mgogoro kama ule uliokuwa umetokea usiku uliopita.


Baada ya kuandaa chai mezani niliendelea na shughuli nyingine za kawaida. Kitu cha kushangaza ni kwamba kila mmoja aliondoka ndani mle pasipo kupata kifungua kinywa. Na kitu cha kuchanganya zaidi ni kwamba kati yao hakuna ambaye alizungumza na mwengine zaidi ya salamu.


Sikuweza kuelewa hali ile ingedumu ndani mle hadi lini, kwasababu tangu jana usiku watu wale hawakuwa wamekula. Sasa kuondoka kwao pasipo kunywa chai ndiko kulinichanganya zaidi na kuhisi pengine nilikuwa nimesusiwa mimi chakula.


Mtu pekee ambaye angeweza kunifariji kutoka katika hali ile alikuwa ni dada Bupe. Lakini sasa ningemuingia vipi wakati siku iliyopita nilimtimua kwa maneno makali yaliyojaa shombo.


Hata hivyo ilikuwa ni lazima nionane na dada Bupe ili aweze kuniweka karibu na Endru. Ndio, kwa wakati huo niliona Endru ndio pekee angenifaa na sio wale simbilisi kule ndani. Nikamuomba Mungu aweze kunisaidia ili niweze kuwaepuka vishawishi vya wanandugu na hatimaye niweze kuishi na Endru. Hata hivyo sikuwa na uhakika kama dada Bupe angeweza kunipokea kutokana na maneno ya shombo niliyokuwa nimemtolea dada Bupe ayapeleke kwa Endru.


Pasipo kujiuliza maneno mengi, mtoto wa kike kipele kikaniwasha na kujikuta nikifungua geti na kutoka kuelekea mgahawani kwa dada Bupe huku nikiwa sielewi ningepokelewaje.



Nilitembea kwa mwendo wa kunyata huku nikiwa na vipande vya hofu ndani ya moyo wangu. Jeuri na kiburi nilichokuwa nimemletea dada Bupe jana vilisalia kuwa majuto na kilio ndani ya moyo wangu. Lakini yote yale niliyafanya ili kulinda penzi langu na Fadhili mwanaume ambaye kwa wakati huo nilikuwa nikimuona kama vile shatani.

“Hodiii” nilibisha hodi huku nikiwa nimesimama nje ya mgahawa. Siku zote nilikuwa nikiingia tu pasipo kubisha hodi, lakini siku hiyo kwa aibu na woga nikajikuta nabisha hodi.

“Karibu pita” sauti ya dada Bupe ilisikika kutokea jikoni.

Mapigo ya moyo yalizidi kuongezeka spidi baada ya kusikia sauti ya dada Bupe ikinikaribisha. Nikatembea kwa mwendo wa kunyata huku nikiuma mdomo wangu wa chini kwa meno ya juu na macho nikiyafumbafumba. Ghafla nikamuona dada Bupe amesimama mbele yangu akinikodolea macho kwa mshangao.

“Shikamoo dada Bupe!” nilimsalimia haraka haraka ili kujaribu kuondoa aibu niliyokuwa nimekwenda nayo.

“Karibu mtoto wa kitanga” dada Bupe alinikaribisha baada ya kubaini nilikuwa nimefika pale lakini nilikuwa nimejawa na hofu.

Jamani nyie kuna watu wameumbwa na mioyo migumu humu duniani, yani dada Bupe alinikaribisha utafikiri hakukuwa na jambo lolote la kupishana kauli lilikuwa limetokea kati yetu.

Nikafika na kuketi kwenye kile kiti kilichokuwepo pembeni mwa mlango wa kuelekea jikoni na mgahawani. Aibu ilikuwa bado imenijaa mtoto wawatu pamoja na kwamba dada Bupe hakunioneshea kinyongo chochote. Alikuwa na muonekana uleule wa siku zote.

“Nataka chai” nikazungumza kwa kujishaua baada ya kuketi.

“Chai nayo inakutaka wewe” alisema dada Bupe huku akisukuma unga wa ngano kwenye kibao cha chapati.

“Kwenye chupa humu kuna chai?” nikahoji huku nikiinuka kuelekea ilipo chupa ya chai. Jamani nyie aibu ni kitu kibaya sana, yani nilikuwa nafanya yote yale kwa lengo la kujibaraguza na kutafuta amani kutoka kwa dada Bupe.

“He mwenzangu huko nyumbni umefukuzwa nini?” alihoji dada Bupe kwa mshangao huku akiendelea kusukuma unga wa chapati.

“Kwanini?” nikauliza huku nikitikisa chupa ya chai kupima kama ilikuwa na kitu ndani yake.

“Mana umefika tu unaulizia chai”

“Sina shida na chai yao” nikazungumza huku nikichukua kikombe na kumimina chai ya rangi.

“Lakini maziwa bado kidogo kuiva, unaonaje ungesubiri kidogo?” alisema dada Bupe kwa sauti ya upendo ambayo ilizidi kunimaliza na kunifanya nijione mkosaji zaidi niliyestahili adhabu hata ya kutukanwa tu.

“Ah mie sitaki chai ya maziwa” nikazungumza huku nikiweka sukari kwenye kikombe cha chai.

“Basi njoo ushughulikie maziwa huku jikoni”

“Hapo sawa” nilijibu huku nikionja chai kwenye kikombe.

Nilichukua kikombe changu kilichokuwa na chai na kuelekea nacho kwenye kile kiti cha mlango wa jikoni.

“Utakunywa na maandazi au chapati?"

“Maandazi mwenzangu sitaki, labda unipe chapati” nikazungumza huku nikiweka kikombe chini na kuelekea jikoni ambako kulikuwa na sufuiria ya maziwa yakichemka.

“Haya maziwa si yamekwisha iva?” nilijizungumzisha mtoto wa watu.

“Yaepue yameshaiva, yaweke kwenye ile chupa nyekundu” dada Bupe akatoa maagizo kama ilivyokuwa kawaida yake siku zote nilipokuwa nimemtembelea pale mgahawani.

Nilichukua chupa ya chai na kujaza yale maziwa. Baada ya hapo nilichukua sufuria nyingine iliyokuwepo pembeni na maji nikainjika jikoni kisha nikatoka kwenda kuketi pale kwenye kiti na kuendelea kunywa chai.

Kimya kikatawala kidogo pasipo kuzungumza kitu kati yangu mimi na dada Bupe. Ikabidi nijizungumzishe na kutoa la moyoni ili nipate ahuweni na amani.

“Dada Bupe” nikaita.

“Unasemaje mdogo wangu wa kitanga?” aliitika dada Bupe kwa sauti kavu.

“Si utakuwa umenisamehe?” nikazungumza kwa sauti ya upole na iliyokuwa imejaa upendo.

“Kwanini unasema hivyo mdogo wangu?” akahoji kama vile hakuwa anaelewa kitu.

“Kwasababu nimekukosea”

“Au yale mambo ya Endrus?” alihoji dada Bupe.

“Ndio dada” nikajibu kwa upole.

“Ah usijali mdogo wangu, huwa mapenzi hayalazimishwi”

“Sio hivyo dada Bupe”

“Kwanza achana na huyo Endru, tuendelee na mambo mengine” dada Bupe alizungumza kama vile hakuwa anamfahamu Endrus.

“Usiseme hivyo dada Bupe, mbona mimi nimetambua makossa yangu lakini” nikaendelea kuzungumza kwa kujitetea baada ya kuona dada Bupe kunikatisha tamaa kuwa na Endrus.

“Wala usiwe na wasiwasi mdogo wangu, hata mimi nipo upande wako” aliunguma dada Bue kwa upole.

“Kweli dada Bupe?” sikuweza kuamini dada Bupe aliponambia yupo upande wangu. Moja kwa moja matumaini ya kumpata tena Endrus yakalejea baada ya kusikia dada Bupe alikuwa upande wangu.

“Kwanini nikudanganye, yani nilipotoka kwako nikaja kumueleza kinaga ubaga, nikamimina sumu na kumwambia asije akathubutu kukusumbua tena” dada Bupe alizungumza maneno ambayo alifikiri yataninogea kumbe yalinichoma na kunisababishia maumivui makali ndani ya kifua changu na kujikuta nashindwa kuvumilia.

“Mungu wangu!” nikaropoka pasipo kujitambua.

“Vipi?” alihoji dada Bupe kwa mshangao.

“Umemwambia nini Endrus?” nikahoji kwa umakini.

“Nimemwambia haumtaki, haumpendi, na akome kukufuata fuata” dada Bupe akazungumza kwa msisitizo

“Mungu wangu, nimekosa bara na pwani sasa” nikajikuta nikizungumza kwa kukata tamaa na kupoteza kabisa matumaini.

“Mbona sikuelewi Mwantumu, Bara ni wapi na Pwani ni wapi?” akahoji dada Bupe kwa msisitizo.

“Unajua dada Bupe, nilimkataa Endru kwasababu nilikuwa nimeamua kuwa na Fadhili pekeyake” nilieleza kisha nikameza funda la mate.

“Sasa kama umeamua kuwa na Fadhili, Unajuta nini kumkosa Endrus?” alihoji dada Bupe kwa umakini.

“Dada Bupe, Fadhili hanitaki tena! Fadhili hanipendi! Fadhili ananichukia!” nikazungumza kwa machungu na hasira.

“Duh hiyo tena balaa, wewe si ulinambia Fadhili ameshaanza kukupenda, sasa imekuwaje tema mara hii?” dada Bupe akahoji kishambenga.

“Fadhili unayemjua wewe siye Fadhili wa leo hii tunayemzungumzia hapa”

“Amekuwaje sasa mbona hufunguki, unazunguuka tu kama pia?”

“Fadhili anahisi mimi natoka na kaka Imran” Nikazungumza kwa ufupi.

“Eeh! Fadhili amejuaje kama Imran anakutaka?”

“Yani we dada Bupe acha tu, mana ni mauzauza”

“Basi kama ni hivyo mkubali Imran” dada Bupe akanishauri.

“Hapana! Mimi kaka Imran simpendi”

“Kumbe unampenda nani?”

“Fadhili” jibu lilinitoka bila kufikiria.

“We si umesema unamtaka Endru, au unataka kujibebea wote wawili?” alihoji dada Bupe kwa masihara.

“Aah nikweli simtaki Fadhili, namaanisha nampenda Endru” nikazungumza kwa kujiamini.

“Achana na Endru bwana, kwanza hata mimi sikushauri tena” dada Bupe akazungumza kwa msisitizo huku akionekana kutokuwa n ahata tone la masihara.

“Hapa dada Bupe, ni afadhali kuwa na Endru kuliko kuwa na wanaume wa mule ndani” nikazungumza kwa msisitizo.

“Sasa kama wanajipendekeza wenyewe, kosa lako litakuwa wapi?” alihoji dada Bupe.

“Kosa langu litakuwa ni kuchanganya wana ndugu” nikaeleza.

“Kwani ukiwachanganya utababuka?”

“sitababuka lakini naweza kusababisha tafrani kwa ndugu”

“Umeshaanza hivyo ushamba wako”

“Kweli dada Bupe mimi sihitaji tena mwanaume yoyote yule kutoka mule ndani mwetu” nikaeleza kwa msisitizo.

“Eeh! Na wewe mtoto wa kitanga ukiamua lako umeamua, hakuna wa kukurudisha nyuma” dada Bupe alizungumza.

“Sasa tatizo ni kwamba Fadhili hataki kunielewa na ameniambia hanitaki” nilielza kwa sauti ya kukata tamaa.

“Oh pole sana mdogo wangu” dada Bupe alizungumza kwa sauti iliyoashiria upendo na huruma.

“Ndiomaana nimeamua kuwa na Endru pengine anaweza kunipunguzia machungu” nikaeleza.

“Kwahiyo unamtaka Endru kwaajili ya kukupunguzia machungu unayopewa na Fadhili na siokwamba unampenda” dada akahoji.

“Aah mi nafikiri nampenda Endru” nikazungumza kwa mashaka.

“Eeh haya tena makubwa, matusi yote yale uliyonitolea kuhusu Endru, leo unasema unampenda tena” akazungumza dada Bupe kwa mshangao.

Wakati mazungumzo yetu mimi na dada Bupe yalivyokuwa yakiendelea mgahawani pale ghafla tukashitushwa na sauti ya mtu akikohoa. Sote tuligeuza shingo zetu kumtazama mtu aliyekuwa anakohoa.

“Mungu wangu!” nikajikuta nikihamaki.

Huwezi kuamini ndugu msomaji, mtu aliyekuwa amesimama pale alikuwa ni Fadhili. Alikuwa akitukodolea macho huku sura yake ikionekana kujawa na hasira.

“We binti, mbona unashangaza ulimwengu?” Fadhili alihoji huku mikono yake ameipishanisha kifuani kama vile amefunga swala.

“Habari yako Fadhili?” dada Bupe akamsalimia Fadhili.

“Mbaya!”

“He yamekuwa hayo?”

“We shubiri mwitu, sikuhizi unafanya kazi za mgahawani?” Fadhili alihoji huku menikodolea macho.

Mtoto wa kike nikajiinua kutoka pale nilipokuwa nimeketi na kusimama tayari kwa kuondoka.

“Kwani amefanya kosa gani jamani?” dada Bupe akahoji kwa jazba.

“Kimya na wewe! Unajua mshahara wake huyu au unaropoka tu!” Mhn jamani nyie Fadhili akazungumza kwa kebehi.

“Eeh basi makubwa!”

“Tena sitaki kuikuta tena hii mironjo yako iko hapa, wewe umeajiriwa nyumbani sio mgahawani” Fadhili alizungumza na kugeuka kuondoka.

Niligeuza macho yangu na kumtazama dada Bupe.

“Umeona moto huo, hapo sasa unampenda vipi mwanaume wa hivi?” nikazungumza na kuvuta hatua kuelekea nyumbani.

“Mnh kazi unayo mtoto wa kitanga” dada Bupe akazungumza huku akijikuna mkono wa kushoto.

Nilitoka mgahawani pale huku nikikimbia kuelekea nyumbani. Mazoea ndiyo yaliyoluwa yameniponza maana siku zote nilipokuwa nikimaliza kufanya kazi zangu za ndani nilikwenda mgahawani kwa dada Bupe kupiga soga hadi niliposikia sauti ya honi ya gari ndipo niliporudi ndani. Sasa siku hiyo Fadhili alikuwa amerejea nyumbani bila ya gari kwahiyo nisingeweza kusikia honi ya gari.

“Mbona leo umerudi mapema kuliko kawaida yako?” nikahoji mara tu tulipoingia ndani.

“Hebu kaa hapo” alizungumza Fadhili huku akijiweka kwenye kochi.

Pasipo kujibu wala kuzungumza neon lolote, mtoto wa kike nikaketi kwenye kochi lililokuwepo jirani na alipokaa Fadhili.

“Nitazame!” Fadhili alitoa amri kwa sauti ya amri baada ya kuniona nikikwepesha macho yangu kumuangalia.

Pasipo kujibu neno lolote nikainua shingo na kumtazama machoni.

“Nakuuliza maswali yangu nataka uyajibu kwa ufasaha, na nikibaini unanidanganya nakuchinja humuhumu ndani leo” Fadhili alizungumza kwa mkazo huku ametoa macho utafikiri amekabwa na mnofu wa nyama kooni.

Maneno ya Fadhili yaliniogopesha sana, sikuwahi kumsikia akizungumza maneno yaliyokuwa yamejaa ukakasi kama yale. Nakwambia ndugu msomaji sitakuja kuisahau siku hiyo katika maisha yangu yote.




Nilikaa vizuri kwenye kochi kuweza kumsikiliza kwa makini mwanaume yule ambaye alionekana wazi hakuwa anatania kwa kile alichokizungumza.

“Humu ndani kuna kitu gani kinaendelea?” alihoji Fadhili kwa umakini.

“Sijui, kwani kuna nini?” nikahoji kwa upole

“Nimekwambia unijibu maswali na sio kuniuliza maswali”

“Sawa”

“Huyu Imran ana biashara gani na wewe?”

“Nani kaka Imran, sina biashara yoyote na…”

“Wewe! Nimekwambia usiniongopee” akahoji kwa sauti kali iliyonifanya nishituke kidogo.

“Kaka Imran…sio mimi ni yeye mwenyewe” nikajikuta nashindwa kuzungumza hali halisi.

“Yeyemwenyewe amefanya nini?”

“Ame…ame…ameniambia ni..ni” nilitaka kuzungumza ukweli lakini moyo ulisita kabisa hasa nilipokumbuka varangati lililokuwa limetokea usiku uliopita.

“Amekutongoza?” Fadhili akahoji kwa msisitizo

“Hapana”

“Kumbe amekwambia ufanye nini?”

“Ameniambia nikimaliza kazi niwe naenda kujichangamsha mgahawani kwa dada Bupe” nilijaribu kueleza.

“Unajua Mwantumu usinichanganye, nitakufanyia kitu mbaya hadi kijijini kwenu washangae” Fadhili akazungumza kwa jazba.

“Sasa jamani Fadhili mbona sielewi unachokitaka?” mtoto wa kike ikabidi nijiongeze na kuanza kulia kwa kwikwi.

“Sasa unalia nini?”

“Mi sielewi unachokitaka sasa!” nikazungumza huku nikimwaga machozi.

“Sikiliza Mwantumu, lazima ueleze ukweli ili nikusaidie” alizungumza Fadhili kujaribu kuniondoa wasiwasi.

“Sasa nieleze nini, kila ninachokwambia wewe hauniamini” nililalamika.

“Haya nyamaza basi nitakuamini” Fadhili akashuka kidogo baada ya kuniona nalia.

Maneno ya Fadhili yalinifanya nichukue khanga yangu niliyokuwa nimejifunika na kujifuta mahozi.

“Imran alishawahi kukutongoza?” alihoji Fadhili kwa umakini.

“Hapana” nikajibu huku nikijifuta machozi.

“Una uhakika?” alihoji kwa msisitizo.

Niliitika kwa kichwa kuashiria kama kaka Imran hakuwahi kunitongoza hata siku moja. Nikamuona Fadhili akivuta pumzi na kuziachia kwa mkupuo kama vile alikuwa ametua mzigo mzito kutoka kichwani kwake.

“Kwahiyo unataka kuniambia hauna mahusiano na Imran?” akahoji kwa msisitizo zaidi.

“Imrani ni kaka tu kama ulivyo wewe”

“Sawa nimekuelewa lakini kuna kitu kinanipa shida” Fadhili alizungumza kwa sauti ya chini lakini iliyokuwa imejaa msisitizo.

“Nini?” nikahoji.

“Kule mgahawani kwa Bupe unabiashara gani?” akahoji kwa upole lakini huku amenikodolea macho.

“Hakuna kitu”

“Kwanini kila kukicha kiguu na njia, hata nikifika wewe unatokea huko huko hata kazi za ndani unasahau” Alizungumza Fadhili na kutoa dukuduku lake la moyoni.

Kumbe masikini ya mungu siku zote ninapokuwa nikitokea kwa dada Bupe kuja nyumbani kufungua geti, alikuwa anachukia kijana wa watu. Alikuwa anatamani muda wote niwe ndani nikifanya kazi na kulala.

“Lakini huwa namaliza kazi kwanza nipo naenda kwa dada Bupe” Nikaeleza.

“Ivi unamjua vizuri Bupe wewe?”

“Ana nini?”

“Unauliza ana nini, yule ni bingwa wa kutongozea watoto wa watu wanaume” Fadhili alizungumza maneno ambayo yalinigua kwakweli.

Maneno aliyokuwa anayazungumza Fadhili yalikuwa yakinigusa moja kwa moja. Ni kweli kabisa dada ndiye aliyenishawishi nikajikuta nikiingia kwenye mahusiano na Endrus. Niliinua macho yangu na kumtazama kiha nikajikuta nikitoa pumzi kwa mkupuo.

“Na kama sikosei tayari na wewe ameshakupachika kwa mwanaume” alizungumza Fadhili kwa msisitizo.

“Hapana sina mwanaume yoyote yule” nikajariu kuongopa.

“Sasa uwe na mwanaume, au usiwe na mwanaume sitaki nikuone unapeleka pua yako pale mgahawani kwa Bupe” Fdhili alizungumza kwa msisitizo.

Kabla ya kukubali ama kupinga agizo lile tulisikia sauti ya mtu mwingene akiingilia kati mazungumzo yetu yale.

“Unasemaje wewe? Nafikiri sijasikia vizuri” mu yule alizungumza.

Sote wawili mimi na Fadhili tukageuza shingo zetu kumtazama mtu aliyeingilia kati mazungumzo yetu. Alikuwa ni kaka Imran akivuta hatua kuelekea pale sittingroom tulipokuwa tumeketi mimi na Fadhili.

“Umesema asiende wapi?” Imran alizungumza huku akijiweka kwenye kochi moja dogo.

Mimi na Fadhili tukabaki kimya tukimuangalia Imran alivyokuwa ameingia kwa mbwembwe na kisirani.

“Usinitumbulie macho! Umesema Mwantumu asiende wapi?” Imran aliendelea kuhoji baada ya kuketi.

“Nilikuwa najaribu kumshauri asiwe na mazoea na Bupe” Fadhili alieleza kwa sauti ya upole.

“Wewe unamzuia Mwantumu kwenda kwa Bupe ukiwa kama nani?” Imran alihoji kwa sauti iliyokuwa imejaa ghadhabu.

“Lakini unamfahamu vizuri Bupe Bro” Fadhili aliendelea kuzungumza kwa sauti ya upole.

“Tumu ni mtu mzima bwana sio wa kupelekeshwa kiasi hicho” kaka Imran akazungumza kwa kebehi.

“Sawa Bro, lakini nimezungumza kwa nia njema tu”

“Sasa mimi nimetengua kauli hiyo, Mwantumu muda wowote ukijisikia kwenda kwa Bupe nenda, hakuna wa kukuwekea mipaka” Kaka Imran alizungumza maneno yale huku akionekana wazi alikuwa amekaa kishari shari tu. Nafikiri hakuwa amefurahishwa na kitendo cha Fadhili kuketi pamoja na mimi na kufanya mazungumzo tukiwa wenyewe wawili.

“Lakini Brother ni kweli tatizo ni hili au kuna jambo lingine nyuma ya pazia” Fadhili akahoji kwa mshangao.

“Jambo lingine lipi, au unafikiri kuna kitu gani kina endelea. Mwantumu ni mdogo wangu kama alivyo Mainaya tu, au wewe unafikiria ni nini?” Kaka Imran alijikuta akiropoka maneno mengi utafikiri amekunywa wanzuki kwa mara ya kwanza.

“Hayo yote yanatokea wapi, au ndio unataka kunifahamisha malengo yako sasa?” Fadhili akazungumza kwa mshangao.

“Kukufahamisha nini sasa? Unaniambia mimi natembea na Mwantumu?” alizungumza Imran kwa jazaba.

“Jamani hayo yote ameyazungumza nani, wewe mwenyewe si ndio mdomo wako umeyaropoka” Fadhili aliendelea kuzungumza kwa upole.

“Umeona, umeona ulivyokuwa na dharau? Yaani sijui nikukanyage kanyage!”

“Basi brother nisamehe bure ili yaishe” Fadhili akazungumza kwa upole.

“Yani ningejua kama upo hapa, wala nisingerudi mapema” alijizungumziha Imran baada ya kuona makelele yote yale aliyokuwa anayapiga mwenzake Fadhili alikuwa mpole tu.

Nilitulia tuli pale kwenye kochi nikiwaangalia wanandugu wale walivyokuwa wakizungumza. Ndani ya moyo wangu nilikuwa namuomba sana mungu aepushie mbali ugomvi kati ya wale watu wawili.

Fadhili alijiinua taratibu kutoka kwenye kochi na kuelekea chumbani kwake. Sijui kichwani mwake alikuwa anawaza nini maana siku hiyo alijitahidi kuonesha upole wake pamoja na kwamba kaka Imran alikuwa akimchokonoa kwa maneno makali.

Kaka Imran aliinua macho yake na kunitazama usoni kisha akaachia tabasamu pana. Na mimi kwa kujilazimisha nikaachia tabasamu la mbali sana ambalo ilikuwa ni ngumu kuonekana.

“Pole sana mtoto mzuri” Imran alinambia kwa sauti ya upole.

“Kwanini?” nikahoji

“Nimeona Fadhili alivyokuwa anakunyanyasa” kaka Imran alizungumza.

“Hamna alikuwa ananiambia tu” nilijaribu kumtetea Fadhili kwasababu inawezekana alikuwa ananieleza maneno ya ukweli.

“Usipende kukaa kaa na Fadhili sio mtu mzuri kabisa” alizungumza Imran.

“Kwanini?” nikahoji kwa hamasa.

“Anaweza akakujaza mimba halafu akakutelekeza, sio mara yake ya kwanza” kaka Imran alizungumza kwa sauti ya chini huku akichungulia kwenye korido kuona kama Fadhilialikuwa anamsikia.

Kile alichokuwa amekihofia kaka Imran, ndicho kilichokuwa kimetokea. Ni kweli kabisa Fadhili alikuwa amesimama kwenye korido akimsikiliza kaka Imrani alivyokuwa ananipanga. Kaka Imran alipogeuza shingo wakakutanisha macho yao.

“Kazi unayo brother”

“Kwani uwongo?” Kaka Imrana akazungumza kwa kujibaraguza.

“Haya bwana minatoka, ila Tumu naomba uzingatie niliyokueleza” alizungumza Fadhili na kutoka nje akituacha mimi na kaka Imran sittingroom.

“Kwenda zako!” alizungumza kaka Imran.

Nilijiinua kutoka kwenye kochi kutaka kuondoka na kumuacha kaka Imran pekeyake lakini kabla sijaondoka akanizuia.

“Unakwenda wapi sasa?” alihoji kaka Imran.

“Nataka nikaanze kuandaa chakula cha jioni” nikazungumza bila ya kumuangalia usoni.

“Kaa kidogo basi tuzungumze”

“Mnh nitachelewa kaka Imran”

“Utachelewa wapi bwana kwani unawahi basi?” kaka Imran alizungumza na kunifanya nirejee kwenye kochi na kuketi huku nikimtazama usoni.

“Njoo ukae hapa basi” alisema kaka Imran kwa sauti ya chini.

“Hapana kaka Imran sio vizuri” nilizungumza huku nimekaza macho yangu tofauti na siku zote alivyokuwa amenizoea.

“Au mimi nikufuate hapo?” alizungumza huku akitishia kuinuka kutoka kwenye kochi.

“Hapana kaka sitaki!” nilizungumza kwa msisitizo huku nikijiinua kutoka kwenye kochi.

Kaka Imran hakuweza kuamini kile nilichokuwa nimekifanya, siku zote alizoea kuniona mpole na mlaini kila alipokuwa anataka kuugusa mwili wangu.

“Kwani imekuwaje mtoto mzuri mbona siku hizi umekuwa hivyo?” alioji kwa umakini baada ya kuniona nimekuwa mwanamke mwenye msimamo.

Ndio nilikuwa nimeamua kuwa na msimamo katika masuala ya mahusiano kwasababu awali nilikuwa bado sijajielewa na nikaziona dalili zote za kusababisha amani kusombwa na mafuriko.

Sikutaka kuwa na mahusianona mwanaume yeyote yule wa mle ndani kwasababu ya kulinda kibarua changu. Naomba hapa nieleweke ndugu msomaji, nimeamua kuwa na Endrus kwasababu sikutaka kuwa chanzo cha migogoro ndani ya nyumba ya watu heti kwasababu ya mapenzi.

“Naomba niende nikapike” nikazungumza kwa sauti kavu.

“Tumu unataka kuniambia Fadhili amekulisha sumu gani hadi umekuwa hivyo?” alizungumza kaka Imran kwa hofu uliokuwa umechanganyikana na wivu.

“Sio hivyo kaka Imran, mimi sikuzungumza kitu chochote na Fadhili zaidi ya kuniambia nisiende mgahawani kwa dada Bupe” nilijaribu kueleza.

“Yani mimi nakutetea wewe kumbe unaniona Jajia muuza bagia?” kaka Imran alizungumza kwa jazaba.

“Basi ngoja mimi niende kupika kaka Imran” niliendelea kunga’nga’nia kuondoka jambo ambao lilizidi kumchanganya kaka Imran na kuzidi kumchukia Fadhili wawatu ambaye wala hakuwa na kosa lolote.

“Hivi unajua kama nimerudi mapema kwaajili yako?” alieleza kaka Imran kwa hasira kidogo.

“Basi sawa nakusikiliza” nilizungumza na kuketi tena kwenye kochi.

“Haya njoo ukae hapa” alizungumza kaka Imran huku akinioneshea kuketi kwenye paja lake.

Nilivuta pumzi na kuziachia kwanguvu, nilitaka kuinuka na kwenda kuketi pale kwenye paja lake lakini moyo wangu ulisita na kukumbuka ahadi yangu niliyokuwa nimejiwekea ya kutokuwakaribia wanaume wa ndani mle.




“Hapana kaka Imran, siwezi kukaa hapo” nikazungumza kwa sauti ya wasiwasi.

“Hivi huo woga umetokea wapi, mbona zamani ulikuwa unakubali?” alihoji kaka Imran kwa mshangao.

“Sio hivyo kaka Imran, unajua hata mama akinikuta hapo itakuwa sio vizuri” nilizungumza kwa msisitizo.

“Duh kweli mabadiliko! Haya na nguo nilizokuletea mbona huvai?”

“Sipendi kumuudhi mama” nikasema kwa upole.

“Mama yako gani, Bi Fatma?”

“Ndio, nilipovaa zinle nguo ulizoniletea mwanzo, mama alikasirika sana” nilieleza.

“Ah mbona hayo yaliisha na mother aliruhusu uvae nguo yoyote ile” kaka Imran akanieleza.

Pasipo kuzungumza neno lolote nilijiinua kutoka kwenye kochi na kuelekea jikoni tayari kwa kuanza maandalizi ya chakula cha jioni.

Kaka Imran akabaki ameduwaa akinikodolea macho huku akiwa haamini kile nilichokuwa nimekionesha. Ndio, hakutegemea kabisa kama na mimi ningeweza kuwa ni mwanamke mwenye msimamo kama aliouona. Najua hata wewe ndugu msomaji ulifikia hatua ya kunidharau na kuniita kichehe, sijui Malaya, mara maharage ya Mbeya wengine wakasema sijui nini! Maneno kibao. Kwahiyo naomba nisilaumiwe kwa misimamo yangu. Nataka niwaoneshe kuwa watoto wa kitanga hatupo kama mlivyokuwa mnafikiria.

***

Miongoni mwa watu ambao walikuwa wakiteseka juu yangu alikuwa ni pamoja na Baba mwenye nyumba Mzee Sekiza. Mzeeyule ndiye aliyekuwa ananipa mtihani wa hali ya juu. Mitihani aliyokuwa ananipa kwakweli ilikuwa ni zaidi ya mitihani ya chuo kikuu, halafu mwanafunzi mwenyewe nilikuwa na elimu ya darasa la saba.

Nikiwa peke yangu ndani ya nyumba ile baada ya Fadhili na kaka Imranmn kuondoa, Mawazo yangu yote yalikuwa kwa Endrus kijana niliyekutana naye kule mgahawani kwa dada Bupe. Pamoja na kwamba Fadhili alikuwa amenipinga kwenda kwa dada Bupe lakini bado nilihisi kumpenda Endrus. Naomba nisilaumiwe jamani, nimeamua kuachana na wanaume wote wa ndani, hakuna cha Fadhili wala nani. Hata kama msomaji ulitamani niwe na Fadhili au sijui nani, mwenyewe tayari nimeamua Endrus ndio chaguo langu.

Nikiwa nimesimama pembeni ya jiko la gesi nikigeuza geuza mboga iliyokuwa jikoni, ghafla nikashituliwa na mikono ya mtu aliyekua anajaribu kunishika kiuno kwa nyuma.

Ndugu msomaji, mara zote nilipokuwa nikiguswa nilikuwa najiuliza mara mbilimbili kuwa anaweza kuwa ni nani? Lakini siku hiyo ni miongoni mwa siku ambazo sitoweza kuja kuzisahau maishani mwangu. Nilinga’ta mdomo wangu wa chini kwa hasira kisha nikageuka na mwiko wa kugeuzia mboga ambao ulikuwa mkononi na kumtandika kwa nguvu sana mtu aliyekuwa amenishika kiuno changu. Nikasikia mtu anaguna Mnh!

Mungu wangu! Sikuweza kuamini baada ya kugeuka na kubaini kumbe nilikuwa nimempiga baba mwiko wa pua.

“Tumu umeniua!” baba alilalamika huku ameinama na viganja vya mikono yake vikiwa vimeshikilia pua yake. Alikuwa akikagua kagua kuona kama ilikuwa ikitoa damu masikini baba wa watu nyie hadi huruma.

“Ooh pole baba sikujua kama ni wewe!” nikazungumza kwa kuhamaki huku nikisimama kwa wasiwasi uliochanganyikana na woga.

“Mungu wangu, kwanini usingenipiga sehemu nyingine Tumu? Yani umenilenga katikati ya pua” alizungumza baba huku akisimama na kusogelea kioo cha ukutani kilichokuwepo pale jikoni.

Jamani nyie mwenzenu nilikuwa nimemtengeneza baba kisawasawa kwenye sura yake. Yani ile pua iliumuka utafikiri ilikuwa imetiwa hamira na kuwa na muonekano kama wa pilipili hoho.

“Jamani Mwantumu, kwanini umenifanya hivi?” baba alilalama baada ya kuona pua yake jinsi ilivyopendezesha sura yake. Alikuwa anaonekana kama katuni la Sunche na Kapeto.

“Nisamehe baba ni bahati mbaya” nikazungumza kwa kujihami.

“Bahati mbaya wakati umevuta mwiko kwanguvu zote kabisa!” baba alizungumza kwa kulalamika masikini ya mungu.

“Sikujua kama ni wewe baba”

“Inamaana kuna mtu mwingine humu ndani ambaye anakushika hivi?” baba alihoji kwa umakini.

“Hakuna mtu yoyote anayeweza kunigusa na ndiyomaana nikahamaki na kukupiga bahati mbaya” nikajieleza.

“Inamaana kama ungejua ni mimi usingenipiga?” baba akahoji swali la mtego.

Nikaitika kwa kichwa kuwa nisingempiga. Nikamuona akiachia tabasamu la matumaini.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG