Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

BONGO DAS'LAAM - 5

   


Chombezo : Bongo Das'laam 

Sehemu Ya Tano (5)


“Usiniambie Shoga!”

“Kwani ukikaona utakadhania basi? Walaa! Kapolee”

“Sasa wewe umekapataje?”

“Hee! Chezea mimi wewe!”

“Nakuaminia shoga”

“ Haya tuachane na hayo.Niambie mbona saa hizi kwangu vipi?” alihoji Bi.Sada na kumfanya mama Suzy kubadilika na kujawa na simanzi. Aliinua macho yake na kumtazama Bi.Sada usoni.

“Shoga yangu we acha tu!”

“Kuna nini?” alihoji Bi.Sada.

Mama Suzy akamuelezea shoga yake yule mkasa mzima kuanzia kufukuzwa Kwa Suzy hadi kufukuzwa na yeye mwenyewe. Bi.Sada akajikuta akijawa na huruma kutokana na matukio yaliyomkumba mama Suzy na mtoto wake. Kwa moyo mmoja akamkaribisha shoga yake na kumwambia kuwa angeishi pale kwa kipindi chote ambacho angekuwa akimtafuta mtoto wake Suzy

*****

Suzy na Naima walikuwa wamepumzika baada ya kumtupa mtoto mchanga ambaye alionekana kuwa kikwazo kwenye mambo yao. Siku ile Naima hakutoka na kuamua kubakia nyumbani kama mapumziko huku akiangalia afya ya rafiki yake. Wakiwa kitandani baada ya mlo wa usiku. Naima akamtazama Suzy na kutoa tabasamu.

“Shoga unajisikiaje baada ya kuondokana na kale katoto” Naima alihoji.

“Kwa kweli shoga niko mwepesi, yaani kama vile nimetua zigo ziito” Suzy alijikuta akizungumza maneno mazito ambayo kwa mama yeyote mzazi ni ngumu kuyatamka. Lakini kwa binti huyu, yalikuwa kama vile kunywa maji ya kunywa.



“Sasa ulikuwa unaogopa nini?”

“Lakini inauma Naima wewe, uzae mtoto halafu ukamtupe!” alizungumza Suzy.

“Ah! Usijali watamuokota watu wenye shida na watoto, we pata nafuu hapo tuanze kusaka mkwanja. Bongo bila ya pesa ni sawa na kijijini bila ya jembe” alizungumza Naima.

“Mnh! Shoga nawewe, huishi vimisemo”

“Habari ndiyo hiyo” alizungumza Naima huku akijiweka sawa pale kitandani. Mara simu yake ya mkononi ikaita na kuiangalia.

“Shost, Kimaya huyo anapiga sijui anasemaje” alisema Naima baada ya kuona namba za Ayubu kwenye kioo cha simu yake.

“Haya mama Kimaya, kwa raha zako. Mimi nimekwisha kimbiwa na Ayubu wangu” alisema Suzy na kucheka kidogo.

“Utajiju!” Naima alimjibu Suzy kwa ufupi kisha akapeleka kidole na kugusa kitufe cha kupokelea.

“Hallo Naima” Sauiti ilisikika kupitia kwenye spika ya simu.

“Yes, Baby mambo….Oh I miss you too…..ndio…..kweli mpenzi?......nitafurahi……Nini?......wapi?.......lini?......kwahiyo…..mnh!....haya kesho basi……Mwaaa! ” Naima alianza mazungumzo yake kwa mbwembwe lakini mwisho alipomalizia alionekana kuishiwa kabisa nguvu. Suzy akamtazama na kubaini hali ya rafiki yake.

“Vipi shoga mbona hivyo tena imekuwaje” Suzy alihoji.

“Haya makubwa mwenzangu” alisema Naima huku akiitupa simu yake kitandani.

“Kumetokea kitu gani?”

“Suzy, kale katoto kame….”

“Mungu wangu! Katoto kangu kamefanya nini?” Suzi akadakia kwa wasiwasi.

“Kimaya ndiye amekaokota” Naima akajibu.

“Kwahiyo amechukua uamuzi gani?” Suzy alihoji kwa hamu.

“Amekabidhiwa na polisi amlee”

“ Kwahiyo…” Suzy alitaka kuzungumza kitu lakini akashindwa.

“Kimaya ameniita akanikabidhi huyo mtoto nimlelee mimi”

“He mbona makubwa!”

“Sikiliza Suzy, cha msingi twende ukamuone halafu katoto kake atabakia nako mwenyewe akalee. Imekuwa vizuri kumtambua mtu mwenye mtoto wako” Naima akazungumza maneno ambayo yalionekana kuvutia sana kwenye masikio ya Suzy.

***

Mzee Manyama alijikuta katika wakati mgumu sana kutokana na maamuzi aliyo yachukua ya kumfukuza binti yake akiwa mjamzito. Roho ya huruma ikawa imemtawala vyakutosha kiasi ambacho ukatili wote ulimuisha. Mbaya zaidi ni kwamba mtoto mwenyewe alikuwa ni yuleyule mmoja. Alijilaumu sana kwa tabia yake ya kuchukua maamuzi ya haraka pasipo kufikiria faida na madhara.

Hali yake ya kiafya ilikuwa imedhoofu sana kwasababu alikuwa hali wala halali. Kiukweli alikuwa akimpenda sana mtoto wake yule. Pale alipokuwa amekaa alikuwa akihisi baridi kali sana ya homa. Alitamani amtume mtu amkokee moto ili aote ama akamletee blanketi chumbani ili aweze kujifunika na kupambana na hali ile.

Alijiinua kwa taabu na maumivu makali. Akajikokota kwa msaada wa ukuta hadi chumbani kwake. Akafanikiwa kufika kitandani kwake na kujilaza. Alichukua shuka iliyokuwa kitandani na kujifunika. Hata hivyo haikusaidia kitu kwani shuka yenyewe ilikuwa ni nyepesi mno kiasi cha kushindwa kuzuia baridi ile aliyokuwa akiihisi.

“Mama Suzy” mzee Manyama alipaza sauti kwa shida kumuita mke wake ili amsaidie japo kumpatia blanketi kutoka kwenye kabati. Kutokana na hali yake kabatini alipaona ni parefu sana kutembea kwa miguu.

“Mama Suzyiii” alijikaza tena na kutoa sauti kwa taabu lakini mama Suzy hakuitika wala hakutokea. Angetoka wapi? Wakati alimfukuza pale nyumbani na kumwambia asirejee hadi ampate Suzy.

“Huyu mwanamke mjeuri sana, yaani namuita ananyamaza kimya” Mzee Manyama alijiongelesha mwenyewe huku akiendelea kutetemeka kwa ile baridi. Kiukweli kama ndugu msomaji ungemuona mzee yule alivyokuwa akiteseka hakika ungemhurumia.

“Suzy mwanangu, njoo unisaidie mama” Mzee Manyama alipoona mke wake anamuita hamuitikii akajikuta akimuita mwanawe mpendwa Suzy, lakini naye hakuitika wala kutokea. Angetokea vipi wakati binti alikuwa akimhofia baba yake utafikiri alikuwa anamhofia simba.

“Ayubu hata wewe njoo mwanangu japo unipe pole” alijikuta akitaja jina la Ayubu kijana ambaye alimchukia na hakupenda kumuona hata mara moja. Bila shaka mzee yule alikuwa na dalili ya kuchanganyikiwa, pengine ni kutokana na ile homa kali iliyokuwa imembana. Akakumbuka kuwa Ayubu alimkimbia pale nyumbani kwake.

“We Ayubu usiniogope, mimi nimekwisha kusamehe.” aliropoka mzee Manyama.

“Suzy mwanangu njoo uniletee maji ya kunywa. Ah! Kumbe nilikutimua sasa nani atanisaidia?” mzee yule alijiuliza maswali mwenyewe.

“Mama Suzy mke wangu, mama Suzy. He! Kumbe hata wewe nimekufukuza! Sasa si urudi hata kama hujampata huyo Suzy.” Mzee yule akajiinua pale kitandani kwa lengo la kwenda kuchukua maji ya kunywa jikoni. Hata hivyo alishindwa kwasababu hali yake ilizidi kuwa mbaya. Kiu kilipombana zaidi alijikuta akipata nguvu kidogo na kujiinua. Kizunguzungu kikali kilimtawala kwenye kichwa chake. Alikamata tena ukuta na kuanza kujikokota tratiibu kwenda kuchukua maji ya kunywa ili apoze koo lake.

Mzee Manyama alifanikiwa kujikokota hadi mlangoni na kuukamata mlango wa chumbani. Kizungu zungu kilimzidi na kupepesuka mara kadhaa kabla ya kudondoka chini kama mzigo.

Mzee Manyama alikuwa katika mateso mazito ambayo moyoni mwake alikuwa akijuta kwa yale yote aliyo yafanya kwa mke wake pamoja na mtoto wake Suzy. Aliwaza kuwa yale yote yasinge mfika kama mke wake ama mwanawe Suzy angekuwepo pale nyumbani wakati ule.

Kila mshale wa saa uliposogea hali ya mzee Manyama nayo ndivyo ilivyozidi kuwa mbaya pasipo kupata msaada wowote. Macho yake yakapoteza nuru na kuishiwa na nguvu kiasi cha kushindwa kuyafumbua. Alikuwa akikoroma kama kiti moto aliyeona chakula pale kwenye sakafu ya nyumba yake.

***

Ayubu alikuwa amepumzika chumbani kwake baada ya kujipatia chakula cha jioni. Akili yake haikuwa sawa kabisa usiku ule kutokana na kitendo cha kufumaniwa na mama Asha akiwa na binti yake. Maneno ya mama Asha aliyomwambia kuwa angekuja kueleza kila kitu kwa Baba Asha ndiyo yaliyokuwa yakimchanganya kabisa.

Akiwa anajigeuza geuza kitandani alishituka kusikia mlango wa chumbani kwake ukigongwa. Akili yake ikamwambia kuwa mgongaji wa mlango ule ni lazima alikuwa ni mama Asha pamoja na mume wake. Lakini kwasababu mlango ulikuwa ukigongwa taratibu akajikuta akipata matumaini, kwasababu kama angekuwa ni baba Asha asinge gonga mlango ule kwa kuubembeleza kiasi kile. Akajiinua kitandani na kusgea mlangoni.

“Nani?” Ayubu akauliza kwa sauti ya chini.

“Ni mimi fungua” mgongaji alijibu kwa kunong’ona.

Kwasababu mtu yule alinong’ona Ayubu akashindwa kumtambua.

“We nani?”

“Bwana we fungua si utaniona” mtu yule alizungumza kwa ile sauti yake ya kunong’ona.

Ayubu akawaza kwa sekunde kazaa halafu akafungua mlango. Moyo ulimpasuka na mapigo kudunda kwa kasi zaidi baada ya kumuona Mama Asha.

Ayubu alipomuona mama yule alirudisha mlango haraka sana kutaka kumfungia mama Asha lakini mama yule alimuwahi na kuingia.

Ayubu akategemea kumuona Baba Asha naye akiingia lakini mambo yakawa tofauti. Mama Asha alipoingia tu alirudisha mlango na kuufunga utafikiri yeye ndio alikuwa mwenyeji. Ayubu alikuwa bado hajaelewa kilichokuwa kikiendelea wakati ule.

Ayubu alipomuona mama Asha ameingia chumbani mwake na kufunga mlango, akahisi balaa lilikuwa limewadia. Siku nzima alikuwa akimuwaza Mama Asha na mume wake kutokana na kukutwa na inti yao Asha chumbani.

Mama Asha alipohakikisha kuwa mlango ulikuwa umefungwa akamgeukia Ayubu huku akiachia tabasamu na kunga’ata nga’ta midomo yake ya chini kwa meno ya juu. Alifunua ile night dress yake aliyokuwa amevaa hadi juu kabisa ya paja huku akijinyonga nyonga kama nyoka. Alimsogelea Ayubu na kwenda kusimama mbele yake huku madafu yake mawili akimgusa kijana wa watu kifuani. Mama yule akainua mikono yake na kumshika Ayubu kwenye mabega.

“Sikiliza Ayubu, siko hapa kupoteza muda” mama Asha akazungumza huku pua zao zikiwa karibu zigusane. Ayubu akabakia kimya akiendelea kushangaa tukio lile lililokuwa likifanywa na mama mtu mzima mwingine.

“Kwanini umelala na Asha?” alihoji mama Asha kwa sauti ndogo.

“Nisamehe mama alikuwa ni shetani tu kanipitia” Ayubu akajaribu kujitetea.

“Alikuwa ni shetani?”

“Kweli mama”

“Sasa kama ulijua ni shetaji kwanini usimkwepe” mama Asha akahoji swali ambalo halikuwa na maana huku akizisugua zile chuchu zake kwenye kifua cha Ayubu.

Ayubu akakosa jibu na kuinamisha kichwa chake chini. Aliamini kabisa mama yule alikuwa ametangulia na mume wake alikuwa anakuja nyuma.

“Umefanya kosa kubwa sana kumpa utamu mtoto wangu” mama Asha alizungumza kwa kulalamika huku akimshika kidevu Ayubu na kumuinua kichwa amtazame usoni.

“Najutia kosa hilo mama naomba mnisamehe” Ayubu aliomba radhi kwa sauti ya kubembeleza.

“Sasa tambua kuwa bado sijamwambia baba Asha”

“Naomba usimwambie mama, hakiyamungu sirudii tena” Ayubu alifurahi sana kusikia maneno yale kutoka kwa mama Asha, akamsihi amtunzie siri ile yasije yakawa kama yale ya nyumbani kwa mzee Manyama.

“Ukitaka nisimwambie sitamwambia” alizungumza mama Asha huku akimpapasa Ayubu kifuani.

“Nakuahidi mama Asha sitarudia tena, mimi ninampenzi wangu anaitwa Naima” Ayubu aliendelea kujitetea.

Mama Asha akawa kama vile hakuyasikia maneno ya Ayubu alichokifanya ni kumkamata Ayubu na kumvutia kwake. Mdomo wa mama Asha ukawa ukijitahidi kuutafuta ulimi wa kijana yule. Ayubu hakuwa tayari kurudia kosa kama alilolifanya kwa Asha mchana wa siku ile.

“Hapana mama Asha usifanye hivyo” alisema Ayubu na kumsukuma mama Asha.

Mama Asha alipepesuka kwa kurudi nyuma hatua mbili baada ya kusukumwa na Ayubu. Akamtazama kijana yule na kukunja uso kuashiria kukasirishwa na kitendo kile alichokifanya Ayubu.

“Kwanini umenisukuma?” alihoji mama Asha kwa hasira.

“Hapana mama Asha namuogopa Baba Asha” Ayubu akajibu kwa upole na woga.

“Inamaana ulivyo lala na Asha ulikuwa humuogopi baba yake?” alihoji mama Asha kwa msisitizo.

“Lakini mama tambua kuwa wewe ni mke wa mtu”

“Na Asha ni mtoto wa mtu” alizungumza mama Asha na kumsogelea tena Ayubu huku akiwa amelegeza macho yake utafikiri mlevi wa komoni




“Hapana mama Asha siwezi” Ayubu alizungumza na kusogea pembeni.

Safari hiyo Ayubu alibadilika na kuonekana alikuwa akimaanisha kwa kile alichokuwa anakizungumza. Hakutaka kabisa masihara kama yale yaendelee kuutesa utu wake.

Mama Asha naye alikutana na vitu tofauti na vile alivyokuwa ametarajia. Kichwani mwake alifikiria Ayubu alikuwa ni mwanaume Fulani hivi aliyeumbwa kwaajili ya kumburudisha kila mwanamke aliyemhitaji. Hivyo akajikuta hasira zikimpanda mama yule.

“Unasemaje Ayubu?” alihoji mama Asha kwa ukali.

“Naomba utoke chumbani kwangu usinitafutie balaa” alizungumza Ayubu kwa msisitizo.

“Unanifukuza sio?”

“Vyovyote vile”

“Alaa! Unajifanya unakiburi, si ndio?”

“Sasa mama Asha unadhani mumeo akikukuta humu ndani itakuwaje?” Ayubu alizungumza.

“Hilo wewe halikuhusu, unachotakiwa ni kunipa kile ninachokitaka” alizungumza mama Asha kwa ukali na msisitizo wa hali ya juu.

“Nenda kwako mama Asha” Ayubu naye akasisitiza msimamo wake.

“Siondoki sasa”

“Basi nipishe mimi nitoke” alisema Ayubu huku akitaka kuondoka.

“Sikiliza Ayubu, hii ni lazima na sio hiyari. Kama ukikataa nakwenda kumwambia mume wangu sasa…” mama Asha alizungumza kwa kujiamini lakini kabla hajamalizia sentensi yake Ayubu alimziba mdomo.

“Basi mama Asha”

“Unataka kunizingua hapa wakati mwenzio midudu imeshanipanda!” alizunumza mama Asha huku akimpapasa Ayubu kwenye kiuno.

Ayubu hakuwa na ujanja tena zaidi ya kutulia huku akitafakari mtego ule ambao ameuingia pasipo mwenyewe kupenda.

******

Dozi aliyokuwa amepewa Asha mchana wa siku ile na Ayubu ilikuwa ni nzito ingawa haikukamilika kutokana na kitendo cha mama yake kumuingilia na kuvuruga matibabu yake. Hivyo alikuwa akisuburi kwa hamu kubwa sana giza liingie ili arudi kwa Ayubu ama Kidume kama wenyewe walivyokuwa wamezoea kumuita mle ndani akamaliziwe tiba yake.

Asha alipohakikisha kuwa wazazi wake walikuwa wamelala alifungua mlango wa chumbani kwake na kutoka taratiibu hadi kwenye mlango wa Ayubu na kusimama. Kiunoni mwake alikuwa amevalia kanga moja tu pasipo nguo nyingine yoyote kwa lengo la kukwepa kumsumbua daktari wake wakati wa kumchoma sindano.

Moyo wa Asha ulishituka alipokuwa akiinua mkono wake kutaka kugonga mlango wa chumbani kwa Ayubu. Alisikia sauti za minong’ono ya watu wakijibishana mle chumbani. Asha akavuta pumzi na kuzitoa kwanguvu, akaamini kwa asilimia kubwa kuwa Daktari wake alikuwa amepata mgonjwa mwengine wa kumtibia. Akajikuta nguvu zikimuishia na viungo vyake vya mwili vikimnyong’onyea.

Wakati Asha akiwa ameshika kichwa chake baada ya kubaini kuzidiwa kete na mtu mwingine alishituka zaidi baada ya kusikia sauti ya Ayubu ikitaja jina la Mama Asha chumbani chumbani kwa Ayubu.

Asha akasogeza sikio lake hadi kwenye tundu la kitasa kusikiliza vizuri. Hapo ndipo akabaini kuwa mgonjwa aliyekuwa akitibiwa na daktari wake alikuwa ni Mama Asha ambaye ni mama yake mzazi. Alijikuta hasira zikimpanda hasa alipokumbuka kuwa mwanamke yule ndiye aliyemkatiza matibabu yake mchana wa siku ile.

Kwa uchungu alirudi chumbani kwake na kujitupa kitandani. Alijiona wazi kuwa alikuwa akimchukia mama yake kwa kile kitendo alichomfanyia. Akasonya na kujigeuza geuza pale kitandani. Kila alipokumbuka mziki aliopewa na Kidume mchana wa siku ile hasira zilizidi kumpanda kwasababu aliamini kuwa mama yake naye alikuwa akipewa mambo yale yale ama zaidi ya yale.

Asha akiwa katika mateso na maumivu makali ya mama yake mzazi kumuonjea asali yake ghafla akaachia tabasamu baada ya kupata wazo la kufanya. Alijiinua kwa haraka akafungua mlango wake wa chumbani na kutoka nje.

Asha alikwenda moja kwa moja hadi kwenye mlango wa chumba cha wazazi wake na kuanza kugonga taratibu. Aligonga kwa muda mrefu pasipo majibu lakini hakukata tamaa hadi aliposikia hatua za mtu akitembea kuelekea mlangoni ndipo akakoma kugonga.

“Nani?” Sauti ya Baba Asha iliyokuwa ikikwaruza kutokana na usingizi ilisikika.

“Mimi” Asha alijibu polepole.

“Wewe nani?” Baba Asha alihoji.

“Asha”

“Vipi hujalala?” Baba Asha alihoji baada ya kufungua mlango na kumkuta binti yake amesimama mlangoni. Asha alijibu swali la baba yake kwa kichwa pasipo kutoa sauti yake.

“Vipi kwema?” Alihoji tena baba Asha huku akikwepesha macho yake kumuangalia binti yake kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa.

“Mama amelala?” Asha alihoji kwa wasiwasi.

“Mama yako amelala, vipi kuna tatizo?” Alijibu baba Asha jibu ambalo lilimfanya Asha kushituka.

Asha alishindwa kumuelewa baba yake kwasababu alichokuwa anakifahamu yeye ni kwamba mama yake alikuwa chumbani kwa Kidume Ayubu, sasa iweje awe tena chumbani kwake amelala. Akabakia ameduwaa asiwe na la kuzungumza huku akiwa ameinamia chini. Akawa anajiuliza sasa aliyekuwa chumabani mwa Ayubu alikuwa ni nani? na kwanini Ayubu alikuwa akimtaja Mama Asha? na mbona sauti aliyoisikia chumbani mle ilikuwa ni sauti ya mama Asha? Asha alikuwa akijiuliza maswali ambayo yalikosa majibu.

“Kwani vipi Asha kuna tatizo?” Baba Asha alimgutusha binti yake kutoka kwenye lindi la mawazo.

Asha alipogutuka aliinua mkono wake na kujikuna nywele zake pasipo kuzungumza kitu. Baba Asha alipoona vile akahisi pengine tatizo la Asha lilikuwa likihitaji msaada wa mama yake na sio yeye, hivyo alirejea ndani kwa lengo la kumuamsha mke wake ili akamsikilize binti yao.

“Mama Asha… mama Asha….. mama Asha”Baba Asha aliita wakati alipokuwa akikisogelea kitanda lakini mama Asha hakuitika.

Baba Asha alipopapasa kitandani akabaini hapakuwepo na mtu. Kwakuwa kulikuwepo na kiza alikwenda kwenye swichi na kuwasha taa ili kuhakikisha kwa macho yake. Alipohakikisha kuwa mke wake hakuwepo alirejea mlangoni kwa binti yake.

“Msubiri atakuwa amekwenda masalani” alisema baba Asha na kurudi kitandani kwake akimuacha binti yake amesimama pale mlangoni.

Asha aliposikia aliposikia majibu yale kutoka kwa baba yake alijikuta akitoa tabasamu kwa kuupata uhakika wa kile alichokuwa anakitafuta. Alisogea taratiibu hadi kwenye mlango wa Ayubu kusikiliza tena kilichokuwa kikiendelea kati ya Daktari wake na mgonjwa mwingine ambaye alikuwa ni mama yake mzazi.

****

Mle ndani chumbani mwa Ayubu, mama Asha alimsukumia kitandani Ayubu kisha kwa haraha akapambua nguo zake na kubakiwa na kufuli tupu. Kwa mwendo wa mbwembwe na maringo akaanza kutembea kuelekea mlangoni kuhakikisha kama mlango ulikuwa umefungwa.

Wakati anatembea Ayubu alikuwa ametoa macho akimshuhudia mama yule jinsi alivyokuwa akiachia moja moja. Damu za kijana yule zilianza kumchemka kama ilivyokuwa kawaida yake. Hasa alipobaini kuwa mama yule alikuwa na umbo la pekee ambalo lilikuwa limepambwa vyema kwa mlima mkubwa uliokuwa kwa nyuma chini ya kiuno chake. Umbo la Mama Asha lilitofautiana kabisa na umbo la Asha ambaye alinyimwa kabisa hata kichuguu kidogo cha mchwa.

Mama Asha aliporejea alikwenda kitandani na kujiweka kwenye mapaja ya Ayubu ambaye kwa wakati ule alikuwa amelala chali. Ayubu naye hakutaka kuchelewa kujibu mashambulizi, alimvamia mama yule na kumgeuza kitandani halafu yeye akawa juu yake na kuanza kuvituma viungo vyake vya mwili vifanye shughuli yake. Mama Asha alishindwa kuvumilia akawa anatoa miguno ya kimahaba kwa sauti ya juu pasipo kujali chochote huku na yeye akijitahidi kuonesha mautundu ya kiutu uzima.

Ingawa mama Asha alikuwa ni mtu mzima lakini aliweza kujituma vya kutosha nayeye kumpagawisha Ayubu. Alitumia ulimi wake pamoja na vidole vya mikono yake kucheza na mwili wa Ayubu jambo ambalo lilizidi kumpa hamasa kijana yule na pepo lake la ngono kuja juu zaidi. Kimoyo moyo Ayubu alijikuta akimpongeza mama Asha kwa utundu aliokuwa amebarikiwa. Mambo aliyokuwa akimfanyiwa na mama yule, ni Suzy pekee ndiye aliyewahi kuyafanya. Ama hakika mama Asha aliweza kumpagawisha kijana wawatu na kumfanya apige saluti kwa mama yule wa kizaramu.

“Oooohhmn…..mama….Aaaaa….No….Usi….Ayaaa!” Masikini Ayubu wawatu alijikuta akilalamika kama mtoto wa kike. Hata hivyo nayeye hakukubali kushindwa, alijitahidi kuonesha mbwembwe zake za kitanga na mapenzi ya kisasa. Kwa kiasi fulani alifanikiwa kumnasa mama yule ingawa yeye alionekana kuzidiwa zaidi. Kijana alijishuhudia akicheza na mpira na kufunga magoli mawili mfurulizo kabla hata ya mechi yenyewe kuanza. Ilikuwa ni shughuli pevu kati ya Mtoto wa Kitanga na Mama wa kizaramu.

Ayubu alianza kuhisi pumzi zikimuishia kutokana na shughuli ya mama Asha, katika maisha yake alikuwa haijawahi kumtokea kitu kama kile, “amakweli kila mwalimu huwa na mwalimu wake” Ayubu alijisemea huku akitaka kukata tamaa.

Ayubu alipewa jina na kidume kutokana na sifa za uwezo wake mkubwa katika masuala ya majambozi. Na hata yeye mwenyewe alikuwa akijiona ni fundi wa mafundi pasipo kufikiri kama kungeweza kutokea mwanamke kama mama Asha wa kumtoa kijasho kiasi cha kutamani kuinua mikono juu na kuomba msamaha.

Wakati mama Asha alipokuwa akiendelea kumpelekesha kijana wa watu aliyejifanya fundi kwasababu heti amezaliwa Tanga, kwa bahati mbaya au nzuri kijana yule alipitisha mkono wake kwenye mapaja ya mama Asha na kugusa mkebe wa kuhifadhia ugolo. Mama Asha aliruka pembeni na kutoa sauti kali ya kimahaba. Hapo ndipo Ayubu akabaini kuwa kumbe alikuwa amekamatika kiasi cha kusahau hata kucheza na sehemu tata kama zile.

Ayubu alitoa tabasamu na kuutuma mkono wake tena kuanza kucheza na mkebe wa watu kwa mbinu zile ambazo mwenyewe aliziita za kitanga. Masikini kumbe mkebe ule haukuwa umehifadhi ugolo kama ilivyodhaniwa, bali ulikuwa umehifadhi akili na nguvu zote za mama Asha.

“Baasi…..A…Ay…Ayubu…we…mkali….Nipe nikalale…Oooshsss!” Mama Asha aliishiwa nguvu na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada wa matibabu kutoka kwa daktari wa Asha.

Kama ilivyokuwa kawaida yake Ayubu hakuwa na haraka katika mambo yake jambo ambalo lilizidi kumchanganya na kumtesa mama wa watu.

“Tayar..iiii…imnh….Mbona…una…aaassccc….nipe…Ayu…Oooh….usimpe tena Asha….Oshssss!” Mama Asha alilalamika kwa sauti kubwa bila hata ya hofu ya kusikiwa na wapangji wengine.

*****

Asha akiwa amelipachika vyema sikio lake la kulia kwenye tundu ya kitasa cha mlango aliweza kusikia jinsi ambavyo mama yake alivyokuwa akijilalamisha kwa mwanaume ambaye yeye alimuona kuwa ni chaguo lake.

Asha alijikuta akishindwa kuvumilia mambo yale na kurudi hadi kwenye mlango wa chumba cha baba yake akagonga tena. Safari hii haukupita muda mrefu baba Asha akafungua mlango.




“Vipi Asha? mama yako bado hajarudi sijui anatatizo gani” Alizungumza baba Asha huku akichukua shati lililokuwa likining’inia kwenye msumari na kulivaa kwa lengo la kutoka nje kumuangalia mke wake.

“Baba” Asha alimshitua baba yake wakati anatoka chumbani.

Baba Asha akageuka kumuangalia binti yake. Asha alimsogelea baba yake na kumshika mkono. Alimvuta hadi mlangoni kwa Ayubu kisha akampa ishara ya kutegesha sikio kwenye kitasa cha mlango ule.

Baba Asha alifanya kama alivyoelekezwa na binti yake pasipo kuhoji kitu chochote. Loo! hakuweza kuamini alichokisikia chumbani mle mwa Ayubu. Baba Asha aliweka tena sikio lake ili kupata uhakika zaidi kwa kile alichokuwa amekisikia.

Kwakuwa baba Asha alikuwa akiifahamu vyema miguno ya mke wake hakupata taabu kubaini ukweli uliokuwa ukiendelea chumbani mle. Alirudi nyuma hatua kadhaa kisha akajishika kiuno huku akitetemeka kwa hasira. Asha akasogea pembeni akimtazama baba yake kuona angechukua hatua gani.

Baba Asha alikwenda chumbani kwake na kuchukua panga kisha akausogelea mlango wa Ayubu na kuanza kuugonga kwa nguvu.

Mle ndani Ayubu na Mama Asha waligutushwa na sauti ya mlango uliokuwa ukigongwa kwa lile panga.

“Mungu wangu!” Alisema mama Asha.

“Nani huyo?”

“Lazima atakuwa baba Asha tu” alizungumza mama Asha huku akionekana kuishiwa nguvu. Mlango uliendelea kugongwa kwanguvu na hasira.

“Funguaaa Malaya mkubwa we leo utanitambua mimi ni nani!” Ilikuwa ni sauti ya Baba Asha ikisikika masikioni mwa Ayubu na mama Asha.

“Nilikwambia mama Asha, unaona sasa!” Ayubu alilalamika

“Huu sio muda wa kulaumiana tunatakiwa kufahamu cha kufanya” Mama Asha alizungumza huku akitetemeka.

“Tutafanya nini sasa wakati ndio tumekwisha kamatwa hivyo” alizungumza Ayubu kwa sauti ya kukata tamaa.

“Hata mimi sijui, chamsingi tushauriane cha kufanya”

“Haya nishauri sasa, mimi sina njia zaidi ya kusema kuwa nimekwisha umbuka” Alizungumza Ayubu huku akivaa pensi yake ya timbalendi.

“F u n g u a a a a ! !” Baba Asha alizidi kupaza sauti kwa hasira kuwalazimisha wagoni wake wafungue mlango.

Siku hiyo alikuwa tayari kutoa uhai wa mtu hasa yule mtu waliyekuwa wakimuita kidume. Alikwishasikia habari zake zilizokuwa zimezagaa mtaani kuwa Ayubu alikuwa ni kidume wa kuwakuna vyema mabinti na wake za watu. Sasa siku hiyo alikuwa amethibitisha kwa kumkuta akimkuna vyema mke wake.

Kelele zile za Baba Asha zilipelekea wapangaji wengine wote kuamka na kutoka nje kushuhudia kilichokuwa kimetokea. Watu wengi walipogundua kuwa aliyekuwa amefumaniwa alikuwa ni Kidume hawakushangaa sana kwasababu walikuwa wakimfahamu vyema kwa tabia yake ya kugawa dozi kwa mabinti na wake za watu.

Mama Suzy na Bi.Sada nao hawakuwa na sababu ya kubakia ndani, walitoka kushuhudia kilichotokea. Lakini Bi.Sada alipobaini kuwa mpenzi wake Ayubu ndiye aliyekuwa amefumaniwa alijikuta roho ikimuuma sana. Kwanza kabisa aliumia kwasababu alikuwa akimuonea wivu kijana yule ambaye mwenyewe alikuwa akimuita baba wa mtoto wake kutokana na yule mtoto aliyemuokota na kumpelekea amtunze. Pili aliumia kwa kuona mpenzi wake amepatwa na matatizo makubwa.

“Vipi Shoga?” Mama Suzy alihoji

“Shoga hili balaa, kile ndicho chumba cha baba watoto wangu” Bi.Sada alizungumza kwa wasiwasi.

“Hiyo ndiyo shida ya kutembea na vitoto vidogo shoga yangu” Mama suzy alisema.

“Weee! ishia hapo hapo. Kama unataka tukosane endelea na huwo upuuzi wako” Bi.Sada alijikuta akishindwa kuzuia hasira zake kwa shoga yake aliyemhifadhi usiku ule.

Bi Sada alisogea hadi pale mlangoni na kumkuta baba Asha akiendelea kuupiga ule mlango kwa panga pasipo kujali kitu chochote.

“We! Baba ukome kupiga mlango wangu hivyo” Bi.Sada alimkaripia baba Asha lakini baba yule alionekana kuto kuelewa na kuendelea kugonga mlango ule kwa nguvu zaidi.

Bi.Sada akajifanya kuwa na uchungu zaidi wa mlango wake, alikwenda kusimama mbele ya mlango ule ili kumzuia baba Asha asiendelee kuupiga mlango wake kwa panga.

Kwakuwa Baba Asha alikuwa amekwisha changanyikiwa na mambo aliyoyafanya Ayubu na mke wake, alivuta panga juu kwa lengo la kulitua kwenye bega la mama mwenye nyumba wake.

Bi.Sada alilikwepa panga lile na kumvaa baba Asha wakadondoka chini wote wawili. Bi.Sada ingawa alikuwa ni mwanamke lakini alikuwa na nguvu za kutosha. Aliendelea kuminyana na Baba Asha pale chini kwa dakika kadhaa hadi Asha alipoingilia kati na kujaribu kumsukuma Bi.Sada.

Kama ilivyokuwa kawaida ya uswahilini, watu badala ya kuamua ugomvi wao walishangilia. Shoo ile ilikuwa kabambe kwelikweli, wengine walifahamu sababu za Bi. Sada kupambana na baba Asha na wengine wakahisi ni kweli Bi. Sada alikuwa akipambana kutetea mlango wake.

Wakati Bi.Sada na baba Asha walipokuwa wakigalagazana pale mlangoni, kule chumbani Mama Asha na Ayubu walijaribu kuwaza cha kufanya ili waweze kuokoka katika balaa lile.

“Nimepata wazo” Alisema mama Asha

“Wazo gani?” Ayubu alihoji kwa sauti iliyokuwa imekata tamaa.

Mama Asha alitungua ngua za Ayubu zilizokuwa zikining’inia ukutani na kumrushia Ayubu.

“Vaa” Alisema mama Asha huku akitungua nguo nyingine.

“Halafu?” Ayubu alihoji huku akiwa ameshika zile nguo mkononi mwake.

“Wacha maswali. Nimekwambia vaa” Mama Asha alizungumza kwa mkazo na kumrushia pensi nyingine.

“Sasa nivae ipi?” Ayubu akazidi kuhoji kwa mshangao.

“Zote”

“Tatu?”

“Bado mbili”

“Mi sikuelewi mama Asha”

“Utaelewa tu” Mama Asha alijibu huku akichukua T-shirt na kumkabidhi Ayubu avae.

Ayubu hakuwa anaelewa malengo ya mama Asha. Hata hivyo alijtahidi kuitii amri aliyokuwa akipewa na mwanamke yule. Alikuwa amejivisha kiasi kikubwa cha nguo mwilini mwake akawa mnene kama baunsa.

Mama Asha alianza kuvua tena gauni lake alilokuwa amelivaa baada ya kugundua kuwa wamefumaniwa. Kitendo kile kilimchanganya zaidi Ayubu na kuzidi kujawa na mashaka.

“Sasa unafanya nini?” Alihoji Ayubu kwa mshangao

“Kuwa mpole” Mama Asha akazungumza kwa kujiamini.

“Mnh!” Ayubu akaguna.

“Vaa” Mama Asha alisema huku akimkabidhi Ayubu lile gauni lake.

“Nivae nini?” Ayubu akahoji kwa mshangao.

“Gauni”

“Yaani mimi nivae gauni?” Ayubu alizidi kushangazwa na matendo ya Mama Asha. Lakini alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kutii yale maagizo yote aliyokuwa akipewa na mwanamke yule. Alitaka kuvua zile nguo zake alizokuwa amevalishwa ili avae lile gauni lakini akazuiliwa kufanya vile.

“Vaa juu ya hizo nguo” Alisema mama Asha huku akichukua suruali ya Ayubu na kuivaa yeye.

Baada ya muda mfupi Ayubu alikuwa amevaa nguo za mama Asha na Mama Asha naye alikuwa amejivisha nguo za Ayubu yaani shati na suruali pamoja na kofia ya chepeo. Ayubu aliweza kuonekana mnene kama mama Asha kutokana na wingi wa nguo alizokuwa amevalishwa. Mama Asha akamfunga Ayubu kiremba kichwani kiasi cha kumfanya afanane kabisa na yeye mwenyewe.

Wakati wanafanya yote hayo kule nje mapambano yalikuwa yakiendelea kati ya Bi.Sada na baba Asha. Watu walijikuta wakishangilia ugomvi ule na kusahau kabisa kama chumbani kulikuwa na watu waliofumaniwa.

Mama suzy alipoona shoga yake Bi.Sada alikuwa katika wakati mgumu wa kupambana na watu wawili yaani Asha na baba yake, akaamua kuingilia kati. Purukushani zikazidi kuongezeka na watu wakazidi kushangilia. Asha akawa anapambana na mama Suzy wakati Bi.Sada mwenyewe aliendelea kuminyana na baba Asha.

Kule ndani mama Asha na Ayubu hawakukaa kimya tu kusubiria balaa litokee. Vichwa vyao vilikuwa vikifanya kazi kwa haraka kama feni. Mama Asha akajaribu kufungua dirisha ili kuona uwezekano wa kutokea dirishani lakini alichobaini ni kwamba dirisha la chumba cha Ayubu lilikuwa limezibwa kwa nondo kiasi cha kushindwa kuruhusu mtu kupita.

“Mungu wangu” Alisema mama Asha baada ya kuona jinsi dirisha lilivyotengenezwa.

“Vipi mama Asha?”

“Lengo langu lilikuwa nikupitishe dirishani”

“Kwahiyo tufanyaje?”

“Nawewe waza basi. Mimi akili yangu imeishia hapo” Mama Asha alizungumza huku akijiweka kitandani kwa kukata tamaa.

Akili ya Ayubu ilikuwa imeganda kabisa na hakuweza kutoa ushauri wowote juu ya tatizo lile lililokuwa likiwakabili. Alishindwa kuyazuia machozi kutiririka kwenye mashavu yake. Mama Asha alipomuona alipatwa na hasira.

“We ndio fala kweli. Yaani mwanaume mzima unalia baada ya kuwaza cha kufanya” Mama Asha alizungumza kwa jazba baada ya kumuona Ayubu akibubujikwa na machozi.

Mama Asha aliinamisha kichwa chake kwa sekunde kadhaa kisha akakiinua na kumtazama Ayubu ambaye alikuwa akifuta machozi.

“Nyoo! unadhani machozi yatasaidia hapa?”

“Yani ndio nakufa hivihivi mimi mwenzio mimi” alizungumza Ayubu huku akilia.

“Mianaume mingine sijui ipoje!” Mama Asha alizungumza huku akiusogelea mlango na kutega sikio lake kusikiliza kilichokuwa kikiendelea huko nje.




“Pigahuyooo……piga….waacheni…..msiwashike…..anang’ataa…” Mama Asha aliweza kusikia sauti za watu wakishangilia huko nje. Aligundua kuwa kulikuwa na watu wakipigana ingawa hakufahamu ni wakina nani, lakini alielewa miongoni mwao na mume wake naye alikuwemo kwasababu zile vurugu za kugongewa mlango zilikuwa zimetulia kwa dakika kadhaa sasa. Alimgeukia Ayubu na kuanza kumsemesha kwa sauti ya kunong’ona.

“Hadi sasa unayo nafasi moja tu ya kujiokoa” alizungumza mama Asha kwa msisitizo.

“Kivipi?”

“Tunafungua mlango halafu tunatoka na….”

“Nini mimi nitoke! Kweli wanawake akili zenu hazipo sawa. Yaani nitoke ili mumeo animalize, si ndivyo?” Ayubu alijikuta akishangazwa na maneno ya Mama Asha na kuyapinga vikali.

“We kenge nini! najaribu kukusaidia halafu unaniletea Upimbi wako hapa. Sasa endelea na ubishi wako ushuhudie jinsi panga litakavyoingia shingoni mwako” mama Asha alizungumza kwa hasira.

“Basi mama Asha nakusikiliza” Ayubu alijibu kwa upole baada ya kuona mama Asha alikuwa amekasirika.

“Pweza we!” Mama Asha alipunguza hasira zake kwa kumbeza Ayubu.

“Basi mama Asha niambie basi cha kufanya” Ayubu alisihi.

“Nafungua mlango halafu tunatoka mbio mimi nikiwa mbele. Wewe unapitia mlango wa nyuma na mimi natokea mlango wa mbele. Sawa?” Mama Asha alizungumza kwa kujiamini. Wakati Ayubu akitafakari maneno yale mama Asha alikuwa mlangoni amekamatia vyema komeo ya mlango. Akamgeukia Ayubu na kumpa ishara ya kukaa tayari. Ayubu alizidi kutetemeka na kuogopa zaidi, aliamini kuwa ule ndio ulikuwa mwisho wa maisha yake.

“Ukizubaa Lwako! unauawa” Alisema mama Asha kwa sauti kavu.

Ayubu hakuzungumza kitu zaidi ya kushika kifua chake kuona jinsi mapigo ya moyo wake yalivyokuwa yakienda mbio. Aliona waziwazi siku hiyo maisha yake alikuwa akiyachezea kamali, kufa ama kupona. Akaona ni afadhali afie njiani akijaribu kujiokoa kuliko kusubiri kufia chumbani kwa kushindwa hata kujaribu kujiokoa.

“Haya Upo tayari?” alihoji mama Asha.

Ayubu akaitika kwa kichwa kukubaliana na maneno ya mama Asha.

Mama Asha akaanza kuhesabu namba moja hadi ilipofika namba tatu akafungua kitasa cha mlango na kuchomoka mbio. Aliwaruka Bi.Sada na Baba Asha ambao walikuwa bado wakigaragazana pale chini.

Baba Asha alipobaini kuwa mbaya wake alikuwa ametoka chumbani mle aliachana na Bi.Sada na kuanza kumkimbiza nyuma huku watu wengine nao wakiwafuata nyuma yao.

Ayubu akiwa amevalia zile nguo za mama Asha akatokea mlango wa nyuma. Watu waliobahatika kumuona waliamini kwa asilimia zote kuwa alikuwa ni mama Asha. Hivyo walikuwa wakimzomea wakati alipokuwa akijipenyeza kwenye chochoro. Alikimbia hadi alipobaini kuwa alikuwa amefika mbali ndipo alipovua zile nguo za mama Asha na kuzitupa kisha akaendelea kutimua mbio.

Kule kwa upande wa mama Asha nako mambo yalikuwa magumu. Baba Asha alifanikiwa kumfikia mke wake huku akiamini kuwa alikuwa ni mwanaume aliyemuibia mke wake kutokana na mavazi aliyokuwa ameyavaa.

Baba Asha aliinua panga lake juu na kulitua kwenye bega la mkewake bila ya huruma. Mama Asha alitoa sauti ya maumivu na kudondoka chini kama mzigo. Baba Asha alijikuta akiishiwa nguvu baada ya kubaini mtu aliyempiga kwa panga lile alikuwa ni mke wake.

Baba Asha alipobaini kuwa alikuwa amemuwacha mbaya wake nyuma, aligeuka haraka na kurejea nyumbani kwaajili ya kumuwahi kabla hajaondoka. Hata hivyo alipofika alibaini kuwa Ayubu alikuwa amekwisha toweka. Alishindwa kumfuatilia kwasababu hakuweza kufahamu mahali ambapo alikuwa ameelekea, akabakia kumlaani tu.

****

Ayubu hakuweza kuamini kama alikuwa amefanikiwa kutoka salama kwenye mikono ya baba Asha. Alikuwa akitembea pasipo kujitambua hadi maeneo ya Bamaga. Alikuwa haelewi alipokuwa anaelekea kwa usiku ule ingawa alikuwa kwenye safari. Alitamani kwenda kwa mpenzi wake Naima lakini kwa bahati mbaya hakuwa anapafahamu na simu yake alikuwa ameiacha chumbani kwake wakati anatoroka.

Jambo ambalo lilikuwa likizunguuka kwenye ubongo wa kijana yule lilikuwa ni kusafiri siku iliyofuata ili kuweza kuepukana na balaa lililokuwa likimkabili. Alifahamu jinsi ambavyo baba Asha alivyokuwa akisifika kwa kuwa na roho mbaya. Inasemekana kuwa alitoroka kwao kusini kwasababu alikuwa amefanya kosa la mauaji. Hivyo Ayubu naye alifahamu wazi kuwa kifo chake kilikuwa mikononi mwa mwanaume yule.

Pamoja na kwamba Ayubu alipanga kuondoka siku iliyofuata lakini aliona sio busara kuondoka pasipo kuonana na mama Suzy ili aweze kufahamu hatua ambayo walikuwa wamefikia hadi wakati ule kwenye suala la kumtafuta mpenzi wake Suzy.

Ayubu aliweza kufika hadi kwenye nyumba ya mzee Manyama na kusimama nje. Hakugonga mlango wa nyumba ile kwa kumhofia mzee Manyama. Alikuwa akimuomba sana mungu mama Suzy atoke nje ili waonane lakini dua yake haikupokelewa. Ilikuwa vigumu mama Suzy kutokea kwasababu hakuwemo ndani siku hiyo. Nyumba aliyokuwa ametoroka yeye ndiyo nyumba ambayo mama Suzy alikuwemo amelala usiku ule.

Baada ya kukaa kwa kitambo pasipo kuona dalili yoyote ya kutoka mtu nje, Ayubu alijivuta taratibu hadi kwenye usawa wa dirisha la chumba cha Mzee Manyama na kuchungulia ndani. Hakupata shida kuona ndani mle kwasababu taa ya chumbani ilikuwa ikiwaka. Macho yake yalitua moja kwa moja kitandani na kubaini kuwa hapakuwepo na mtu.

Hakukata tamaa na kuendelea kuzunguusha macho yake chumbani mle hadi alipoona mtu amelala sakafuni. Alipomtazama vizuri mtu yule aliyekuwa amejilaza pale chini aligundua kuwa alikuwa ni mzee Manyama. Kitu kilichomshangaza zaidi ni vile ambavyo mzee yule alivyokuwa akikoroma. Kiukweli alikuwa akikoroma isivyo kawaida. Ayubu akapatwa na mashaka na kumtazama vizuri usoni. Aligundua kuwa macho yake yalikuwa yametoka kuliko kawaida.

Ayubu alipiga moyo konde na kuuendea mlango. Alipougusa mlango alibaini kuwa ulikuwa wazi. Aliingia ndani kwa tahadhari huku akiangaza pande zote za nyumba ile. Alipoukaribia mlango wa mzee Manyama ambao ulikuwa umefunguliwa aliweza kumuona mzee yule akiwa amelala pale sakafuni.

Ayubu alisimama hatua kadhaa kutokea pale alipokuwa amelala mzee Manyama na kuanza kumuita ili kuhakikisha kama alikuwa salama. Aliita kwa muda mrefu lakini Mzee yule hakuitika wala kutikisika. Ayubu akamsogelea tena na kumgusa kwa tadhadhari. Joto kali la mwili lilimuwezesha Ayubu kubaini kuwa mzee yule alikuwa na tatizo.

Ayubu alianza kupaza sauti ndani mle ili kuomba msaada lakini akabaini kuwa hapakuwepo na mtu mwingine. Alichofanya ni kutoka nje ambako alikwenda nyumba ya jirani na kuomba msaada.

Mama Angel na mume wake walijitoa na kwenda hadi ndani kwa mzee Manyama. Kwa kuwa nyumba zao hazikuwa mbali na barabara walifanikiwa kupata bajaji ambayo walimpakia Mzee yule na kumuwahisha hospitali kubwa ya Muhimbili.

Walipofika Hospitalini Ayubu alitakiwa kutoa pesa ili mzee yule aanze kupata matibabu. Kwa bahati nzuri nguo ambazo alipewa na mama Asha ndizo zilizokuwa na akiba yake ya pesa hivyo haikumuwia ngumu kulipia pesa zile za awali ili baba wa mpenzi wake aweze kutibiwa kwa haraka ilivyowezekana. Kwakuwa mzee Manyama hali yake ilikuwa mbaya sana alilazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.

*****

Baada ya shughuli za hapa na pale na kupata kifungua kinywa Naima akachukua simu yake ya mkononi na kumpigia mpenzi wake aliyekuwa akimfahamu kwa jina la Kimaya. Lakini kila alivyopiga simu ile alijibiwa kuwa ilikuwa haipatikani. Hakukata tamaa na kuendelea kupiga lakini hakuambulia mafanikio yoyote zaidi ya kuambiwa kuwa ajaribu tena baadae.

“Shenzi” Alisema Naima kwa hasira.

“Vipi tena shoga?” Suzy akahoji baada ya kumuona rafiki yake akiwa na sura iliyokuwa imekata tamaa.

“Kimaya amenizimia simu”

“Hapatikani?”

“We mwache aniletee ufedhuli wake, kumbe hanijui”

“Kwahiyo tunafanyaje?” Alihoji Suzy baada ya kusikia kuwa mwanaume aliyekuwa na mtoto wake alikuwa hapatikani.

“Jiandae tuondoke, mimi mtoto wa hapa hapa Bongo siwezi kupotea. Nakumbuka alikwisha wahi kunielekeza anapoishi” Naima alizungumza kwa kujiamini.

Baad ya lisaa limoja warembo wale walikuwa wamekwisha kujiandaa na safari ya kuelekea Stop – Over nyumbani kwa Kimaya ilianza rasmi.

Kwakuwa wote wawili Suzy na Naima walikuwa ni wenyeji kwenye jijilile la Bongo hivyo hawakupata taabu kufika nyumbani kwa Bi.Sada Ambako Kimaya alikuwa akiishi. Walipofika nyumbani pale walibisha hodi na kuwaulizia wanawake waliokuwa wameketi barazani wakionekana kuzungumzia kitu fulani ambacho kiliwavutia sana.

“Habari zenu jamani” Naima aliwasalimia wanawake wale ambao walionekana kuzama zaidi kwenye mazungumzo yao kiasi cha kushindwa kujibu salamu ile.

“Jamani nawasalimia. Habari zenu” Naima alisisitiza baada ya kuona wanawake wale walikuwa kama vile hawakuwaona.

“Salama, Karibu” msichana aliyefahamika kwa jina la Zuhura alimjibu Naima huku wengine wakiendelea kuzungumza na kucheka kwa sauti.

“Heti Kimaya anaishi nyumba hii?” Naima akahoji

“Kimaya? hapana humu ndani hamna mtu anayeitwa Kimaya” Zuhura alijibu.

“Kwani hapa si ndio kwa Bi.Sada?” Naima aliendelea kuhoji

“Ndio kwa Bi.Sada, lakini hakuna mtu anayeitwa Kimaya”

“Mghn!” Suzy akaguna kwa mshangao.

“Haya tena makubwa. Hata hivyo siamini ni lazima atakuwa anakaa hapahapa labda kuwe na Bi.Sada mwengine” Naima alisisitiza.

“Hakuna Bi.Sada mwengine, labda mtakuwa mmetapeliwa. Si mnajua tena Bongo hapa” Zuhura alizidi kuwakatisha tamaa.

Naima na Suzy wakabakia wakitazamana wasijue cha kufanya. Kiukweli walikuwa wamekwisha kata tamaa kabisa ya kumpata mwenyeji wao Kimaya. Mbaya zaidi ni kwamba kwenye simu yake alikuwa hapatikani, hivyo wakapeana ishara ya kuondoka.




“S u z y i i i ” Sauti ya mwanamke ikitokea ndani ya nyumba ile ilisikika na kuwashitua Naima na Suzy, wakageuka kuangalia sauti ile ilipokuwa ikitokea.

Suzy hakuweza kuamini macho yake, aliyekuwa akimuita alikuwa ni mama yake mzazi yaani mama Suzy.

“M a m a a a a!!” Suzy alijikuta akipaza sauti na kumkimbilia mama yake.

Naima alibakia ameduwaa akiwaangaliwa watu wale wawili waliokuwa wakifanana kama mapacha wakikumbatiana. Hakupata taabu ya kubaini kuwa walikuwa ni mtu na mama yake.


Haikuwa hali ya kawaida kwa watu wale wawili waliokutana, kila mmoja alionekana kujawa na furaha baada ya kukutana na mwenziwe. Wote wawili machozi yalikuwa yakiwatiririka kwa furaha na uchungu.

“Suzy mwanangu ni wewe?” alihoji mamaSuzy huku akichezea nywele za binti yake.

“Ni mimi mama, nisamehe mama” Suzy alilalamika huku akiwa bado amemkumbatia mama kaye.

“Nimekutafuta sana mwanangu” alisema mama Suzy.

“Nisamehe sana mama”

“Usijali mwanangu Suzy wangu!”

“Unafanya nini hapa mama?” Suzy alihoji baada ya kuachina na mama yake.

“Mwanangu we acha tu, Nimefukuzwa na mzee Manyama kwasababu yako. Na nimeambiwa kama sikukupata basi nisirudi nyumbani kwake” Mama Suzy alizungumza maneno ambayo yalizidi kumchoma Suzy na kumfanya azidi kumwaga machozi.

Suzy hakuweza kuamini kama baba yake angeweza kumuhitaji kiasi kile, akajikuta akijutia maamuzi aliyoyachukua dhidi ya mtoto wake aliyemzaa mwenyewe.

“Karibuni ndani” Mama Suzy akawakaribisha Naima na Suzy ndani kwa Bi.Sada.

Pasipo kuzungumza kitu chochote wasichana wale wawili waliingia ndani kwa Bi.Sada ambako walimkuta mwenyewe ameketi kitandani akikipatia kichanga chake maziwa ya chupa.

“Karibuni wanangu karibuni sana” Bi.Sada aliwakaribisha wageni wale ambao bado alikuwa hajawafahamu.

Suzy alikwenda kuketi karibu na Bi.Sada huku akimtumbulia macho yule mtoto mchanga. Akajikuta damu zikimsisimka baada ya kubaini kuwa kitoto kile kilikuwa kikifanana kabisa na mtoto aliyemtupa. Walitazamana na Naima kisha wakakonyezana kama ishara ya kufahamishana kuwa mtoto aliyekuwemo ndani mle ndiye yule mtoto wao waliyekuwa wamemtupa.

“Shoga Huyu ndiye Suzy, mwanangu ninayemtafuta kwa muda mrefu” Mama Suzy alivunja ukimya.

“Jamani Suzy umekuwa mkubwa hivyo! Pole sana mwanangu kwa matatizo” Bi.Sada alizungumza kwa sauti ya huruma.

“Ahsante mama” Alijibu Suzi huku akiwa ameinamisha shingo yake chini.

“Suzy mwanangu” Mama Suzy aliita

“Abee mama”

“Unaonekana umejifungua, mtoto wako yuko wapi?” Mama Suzy aliuliza swali ambalo lilimshitua sana Suzy na kumsababishia kichomi cha tumboni. Suzy na Naima wakatazamana kwa sekunde kadhaa halafu Suzy akavuta pumzi na kizitoa nje kwanguvu.

“Suzy nakuuliza wewe, mtoto yuko wapi?” Mama Suzy aliuliza kwa mkazo zaidi na kumfanya Suzy ashituke kidogo.

“Mama ni hadithi ndefu” Suzy akajaribu kujitetea baada ya kugundua kuwa mama yake alikuwa amebadilika.

“Hadithi ndefu kwenda wapi! au umeua?” Mama Suzy alizidi kumchoma binti yake kwa maswali ambayo alikuwa akiyauliza.

“Hapana mama” Suzy alijibu kwa woga.

“Kumbe sasa yuko wapi?” Mama Suzy alizidi kumlazimisha binti yake kueleza ukweli.

“Jamani mimi naona niwaache” Naima alijifanya kuaga baada ya kuona msala unaelekea kusanuka.

“Hakuna kuondoka mtu hapa hadi tufahamu ukweli” Mama Suzy alimdaka Naima na kumrejesha kwenye kochi alipokuwa ameketi.

“Nauliza mara ya mwisho, mtoto umempeleka wapi?”

“Yupo kwa Kimaya” Suzy alijikuta akiropoka pasipo kujitambua kutokana na ukali wa mama yake.

“Kimaya ndio nani?”

“Tumeambiwa anaishi humu ndani” Naima alijibu

“Hapana, humu ndani hakuna mtu anayeitwa kimaya” Bi.Sada alidakia.

“Au wanamaanisha Ayubu?” Mama Suzy alihoji

“Hakuna, wao wanasema Kimaya” Bi.Sada alisisitiza.

“Ndio Kimaya” Naima naye alisisitiza.

“Suzy hebu ongea ukweli ili upate uhuru mwanangu” mama Suzy alijaribu kumshawishi binti yake.

Suzy hakuona sababu ya kuendelea kuficha ukweli kwa yote waliyokuwa wameyafanya pamoja na rafiki yake.

Kutokana na maelezo yale ya Suzy kuanzia mwanzo hadi mwisho ikabainika kuwa mwanaume waliyekuwa wakimzungumzia alikuwa ni Ayubu, Mwanaume aliyefumaniwa usiku wa kuamkia siku ile. Mama Suzy alimsogelea Bi.Sada na kumuinamia yule mtoto mchanga.

“Shoga kumbe huyu ni mjukuu wangu”

“Shoga wacha masihara bwana, huyu ni mtoto wangu mimi na Ayubu. mjukuu wako wewe anaye Kimaya” Bi.Sada alizungumza kwa sauti kavu iliyokosa masihara hata chembe.

“Lakini mwenyewe si umesikia maelezo yao?” Mama Suzy alihoji

“Sawa lakini mtoto huyu simtoi. kama wangekuwa na shida na watoto wasingethubutu kumtupa” Bi.Sada alianza kukaza kamba na kusahau kuwa mama Suzy alikuwa ni shoga yake.

Suzy na Naima pamoja na mama Asha walichachamaa na hatimaye kufanikiwa kumchukuwa mtoto yule kutoka mikononi mwa Bi.Sada pasipo na hiyari yake.

Bi.Sada alilaani sana kitendo kile na kuahidi kulipiza kisasi kwa njia yoyote ile, ikiwezekana hata kwenda kutoa taarifa polisi. hata hivyo vitisho vya Bi.sada havikuwazuia wao kumchukua mtoto.

Baada ya kufanikiwa hawakuona sababu ya kuendelea kuabakia nyumbani pale. waliaga na kuanza safari ya kuelekea Kijitonyama nyumbani kwa mzee Manyama. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya furaha sana kwenye moyo wa Mama Suzy na hata kwenye moyo wa Suzy mwenyewe.

*****

Kule hospitalini Mzee Manyama alikuwa anahitajika kuongezewa damu haraka sana. Ayubu hakuwa na namna zaidi ya kujitoa kutoa damu. Ilimlazimu kufanya vile kwasababu hapakuwepo na mtu mwingine wa kumsaidia zaidi ya yeye pekee. Baada ya kutoa huduma ile Ayubu alitakiwa kutoa pesa kwaajili ya kununuliwa dawa za kutibiwa mgonjwa wake. Pesa zote alizokuwanazo zilikuwa zimemuishia, hivyo hakuwa na jinsi zaidi ya kumuacha mgonjwa wake na kuingia mitaani kujaribu kutafuta pesa.

Ayubu alitembea kwa muda mrefu sana akijaribu kuomba vibarua ili aweze kupata pesa lakini hakufanikiwa. Akajaribu mbinu ya kuwaeleza ukweli wananchi kuwa alikuwa na mgonjwa lakini pia hakuna ambaye alimuelewa, wengi wao walimuona tapeli wa jiji wakawa wanamtolea maneno machafu.

Njaa, uchovu, pamoja na kiu vilimfanya atafute kiuchochoro kidogo ili apumzike. Wakati yuko pale alibaini kuwa uchochoro ule haukuwa mgeni machoni mwake, hata hivyo alishindwa kukumbuka kama alikwisha wahi kufika maeneo yale. Kaupepo kalikokuwa kakipuliza kalimfanya apitiwe na usingizi.

Akiwa kwenye gari la polisi huku amezunguukwa na kundi la maaskari waliokuwa wamebeba silaha wakimtolea maneno ya kashfa na kejeli, macho yake yalikuwa yamejaa machozi. Mikononi mwake alikuwa amefungwa pingu. Gari ile ilikuwa ikitembea kwa spidi kali sana.

“P u u u u u u !” Kilikuwa ni kishindo kizito kilichosababisha gari lile la polisi kupinduka na kugeuka mara tatu. Ilikuwa ni ajali iliyosababishwa na roli kubwa la mizigo ambalo liliigonga ile gari ya polisi. Ayubu alijitahidi kujichomoa kutoaka kwenye ajali ile huku mkononi mwake akiwa na kifuko kidogo. Alipofanikiwa kutoka alijikokota hadi kwenye kiuchochoro kimoja ambacho hakukifahamu na kudondoka. Kwakuwa ulikuwa ni usiku Ayubu akachimba chini kwenye usawa wa dirisha la nyumba moja na kufukia kile kifuko. Sauti za watu waliokuwa na tochi zilimshitua na kumfanya Ayubu ainuke ili atimue mbio. Hata hivyo alishindwa na kudondoka chini “P u u u u u !”

Hakuweza kuamini macho yake, kumbe alikuwa ndotoni. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimuenda mbio huku akiangaza huku na kule. Mambo yale aliyoyaota hayakuwa mageni kwake. Ni kweli kabisa alikumbana nayo siku za mwanzoni alipoingia kwenye jiji la Bongo Daslaam. Na mazingira ambayo alikuwa amekaa wakati ule ni kweli alikuwa amefukia kifuko cha madini. Kwa ujumla akajikuta akipata picha halisi ya mazingira yale.

Hakuona sababu ya kuchelea, akajiinua na kusogea hadi karibu na lile dirisha ambalo katika kumbu kumbu zake ndipo alipofukia kifuko chake. Huku akiwa katika hali ya uchovu, Aliokota kijiti na kuanza kuchimba chimba.

“W o o o o w !” Ayubu alijikuta akipaza sauti ya furaha.

Alifanikiwa kukipata kifuko chake ambacho alikifukia siku nyingi sana zilizopita. Alikikagua na kukuta madini yake yako vile vile kama alivyo yaacha. Kwakuwa alikuwa tayari ni mwenyeji ukilinganisha na kipindi alipoyaficha, aliweza kufahamu kwa kuyapeleka ili afanye biashara.

*****

Msafara wa Mama Suzy, Naima, na Suzy pamoja na kitoto kichanga ulikuwa ukikaribia kufika kwenye nyumba ya mzee Manya. Kabla hawajaingia ndani mama Angel alifika na kuwafahamisha kuwa baba yao alikuwa mahututi hivyo amepelekwa hospitali ya Muhimbili.

Baada ya kupata taarifa zile waliongozana wote hadi hospitali ambako kweli walimkuta mzee Manyama amelazwa. Hali ya mzee Manyama ilikuwa ikiendelea vizuri ukilinganisha na vile alivyo pelekwa hospitalini pale. Kwahivyo alitolewa kwenye wodi za wagonjwa mahututi na kulazwa kwenye wodi ya wagonjwa wa kawaida.

“Babaaaa” Suzy alikwenda kumshika miguu Mzee Manyama huku amepiga magoti na kuanza kulia.

“Baba naomba unisamehe baba” Suzy alilia kwa uchungu. Mzee Manyama alimshika mkono Suzy na kumuamuru ainuke.

“Nimekusamehe Suzy, nakupenda sana mwanangu” Mzee Manyama alizungumza kwa taabu kutokana na maumivu ambayo alikuwa akiyasikia. Mama Suzy alimuinua kidogo mumewake sehemu za kichwani na kumpakata kwenye mapaja yake.

Baada ya kuombana radhi na kusameheana Suzy alimtambulisha Naima kwa wazazi wake na kuwaambia kuwa yeye ndiye aliyekuwa amechukua jukumu lote la kumlea. Mzee Manyama alimshukuru sana Naima kwa kumtunza vizuri binti yake hadi kufikia hatua ya kujifungua salama.

Wakati wanazungumza Ayubu aliingia huku mkononi mwake akiwa amekumbatia rundo la madawa ambayo alipaswa kutibiwa Mzee Manyama. Macho yake yakagongana na macho ya Suzy. Hakuweza kuamini kama msichana aliyekuwa akimtafuta kwa muda mrefu ndiye aliyekuwa amekaa pale. Alimsogelea Suzy na kutaka kumkumbatia, lakini alipotazama vizuri kitandani alimuona mama Suzy amempakata mzee Manyama huku wote wakimtumbulia macho. Ayubu akasita kumgusa Suzy na kuanza kurudi nyuma kutaka kutimua mbio. Alikuwa akimuogopa sana mzee yule ingawa alijitolea kuokoa maisha yake.



“Usiniogope Ayubu kuwa huru na mwenzio” Sauti yam zee Manyama ilitoka kwa taabu na kumgutusha Ayubu. Alihisi kama vile alichokisikia hakikuwa kimetoka mdomoni mwa mzee yule katili. Akatulia na kumkodolea macho huku akipumua kwa tahadhari.

Mzee Manyama akampa ishara Suzy ya kumfuata Ayubu na kumkumbatia. Suzy akafanya kama baba yake alivyomuagiza. Hata hivyo Ayubu akawa muoga kumkumbatia Suzy, aliinua mikono taratibu na tahadhari ya hali ya hali ya juu kisha akamkumbatia mpenzi wake Suzy.

Mzee Manyama na mama Suzy wakawa wanatoa tabasamu kwa kile kilichokuwa kikiendelea kati ya Suzy na Ayubu.

Ayubu alikwenda kitandani alipokuwa amelala mzee Manyama na kupiga magoti kuwaomba radhi wazazi wa Suzy. Wote wawili walionekana kuridhia ule msamaha aliouomba Ayubu.

“Usijali mwanangu, jisikie huru. Nawewe Mungu atakulipa kwa wema ulionitendea” Mzee Manyama alizungumza.

Suzy alimpa Ayubu ishara kuwa mtoto wao alikuwa ameshikwa na msichana aliyekuwa ameketi kwenye kitanda cha jirani na pale alipokuwa amelazwa baba yake. Ayubu alipogeuka akakutana na sura ya Naima.

“Naima” Aliita Ayubu kwa mshangao

“Kimaya” Naima naye akaita kwa kejeli kwasababu alibaini kuwa alikuwa amedanganywa jina na Ayubu.

“Lakini….” Ayubu alitaka kuzungumza jambo.

“Hakuna cha lakini. Karibu umuone mtoto wako” Naima akazungumza kama vile alikuwa hamfahamu.

Ayubu alimchukua mtoto wake na kumtazama vizuri usoni. Sura ya mtoto yule haikuwa tofautiana kabisa na sura ya mtoto yule aliyemuokota njiani na kumpelekea mama mwenye nyumba wake. Akabakia akishangaa asijue la kuzungumza.

“Ndiye huyohuyo” Naima alizungumza baada ya kumuona Ayubu ameduwaa.

“Nani?” Ayubu akahoji kwa mshtuko

“Uliyemuokota” Naima akajibu kwa ufupi.

Majibu ya Naima yalizidi kumchanganya Ayubu. Alichokuwa nakifahamu yeye ni kwamba mtoto aliyemuokota amemuachia Bi.Sada. Sasa imekuwaje wakati huwo huwo waseme ndiye yule waliyekuwa naye pale hospitali.

Kabla ya kupata majibu ya maswali yake Ayubu aliitwa na daktari. Alikwenda ofisini mwa Doctor yule na kukaribishwa kwenye kiti.

“Habari yako kijana”

“Salama Doctor”

“Hongera sana kwa kuendelea vizuri mgonjwa wako”

“Ahsante Daktari”

“Kuna dawa tulizokwambia ukanunue?”

“Ndio Doctor nimekuja nazo”

“Ok. Sasa tumetumia dawa za watu kwasababu mgonjwa wako alikuwa na hali mbaya zaidi. kwahiyo hizo ulizozileta inabidi tuzirejeshe” Alisema Daktari.

“Hakuna tatizo Daktari” Ayubu alijibu kwa kujiamini kwasababu pesa alikuwa nayo ya kutosha. Moyo wake ulijawa na furaha sana kwasababu alikuwa ameruhusiwa kumuoa mwanamke ambaye alikuwa anampenda sana. Alichukua dawa alizofika nazo na kumkabidhi Daktari.

“Vipi Doctor kuna jengine?” Ayubu alihoji kwa kujiamini.

“Jengine lipo, lakini sio la ulazima”

“We Usihofie kitu zungumza tu Daktari”

“Ni kuhusu Damu uliyoitoa”

“Damu! vipi haitoshi? imemwagika? au niongeze?” Ayubu alijikuta akiuliza maswali mfurulizo kutokana na kauli ya Daktari.

“Kwa kawaida tunapotoa damu huwa tunaipima kwanza. Majibu huwa tunampa mhusika kama akiyahitaji” Daktari alieleza.

“Hakuna tatizo Daktari, we nifahamishe tu” Ayubu lizungumza kwa kujiamini.

“Unajua unapokuwa unajifahamu ni vizuri zaidi kwasababu utajiepusha na maambukizi kama hauna, na kama una maambukizi utajilinda na kupata maambukizi mengine zaidi” Daktrari alifafanua.

“Lakini Daktari unadhani mimi naweza kuwa na maambukizi?’

“Kwa kawaida mtu yoyote anaweza kupata maambukizi haijalishi ni kijana ama mzee, mwanamke ama mwanaume”

“Daktari we nipe majibu yangu” Ayubu alizungumza kwa kujiamini.

“Ok. Naomba uwe tayari na majibu yoyote yawe positive ama negative”

“Daktari, usiwe na wasi wasi mimi nipo tayari”

“Sawa” Daktari alijibu na kuanza kufunua kitabu chake cha majina ya watu waliotoa damu.

“Kijana imeonekana damu yako ni chafu”

“Chafu kivipi Daktari mbona sikuelewi?”

“Yaani haipo salama”

“Kivipi? naomba niweke wazi”

“Damu yako ina maambukizi ya VVU”

“Nini? Haiwezekani…mimi siwezi kupata UKIMWI” Ayubu alijikuta akichanganyikiwa kutokana na taarifa zile.

“Hebu tulia basi kijana”

“Haiwezekani Daktari, hivi unanionaje, Mimi naweza kupata UKIMWI kweli?” alizungumza Ayubu huku akimuonsha Daktari mikono yake kuwa ilikuwa na afya ya kutosha.

Daktari alijitahidi kutumia uzoefu wake wa kazi kumtuliza Ayubu hadi akafanikiwa. Pesa alizozipata aliziona hazikuwa na thamani tena maishani mwake. Alichoamini yeye ni kwamba hata kama angeishi miaka hamsini mbele lakini ni lazima angekufa tu.

Alitoka kwa Daktari huku akiwa ameishiwa kabisa na nguvu. Alipomtazama mtoto wake roho yake ndio ilizidi kumuuma. Akamtazama Suzy wake na kuona wazi alikuwa anamkosa. Isingekuwa rahisi kukubali kuolewa naye wakati ameathirika. Alimchukua mtoto wake na kumshika kwa uangalifu uliojaa upendo.

Walifika askari watatu wawili wakiwa wanawake na mmoja mwanaume pale wodini. Askari wale walikwenda moja kwa moja hadi kilipokuwa kitanda cha mzee Manyama na kusimama.

“Poleni jamani” Yule askari wa kiume alisalimia.

“Ahsante baba” Mama Suzy alijibu kwa haraka.

Askari wale walitoa picha kutoka kwenye mifuko yao ya sare walizokuwa wamevaa.

“Sisi ni maofisa wa jeshi la polisi, tunawahitaji watu hawa” Alisema Askari yule wa kike huku akiwaonesha zile picha zilizokuwa na sura za Naima na Suzy. Watu wote wakajawa na mshangao.

“Wamefanya nini wanangu?” Alihoji mzee Manyama kwa sauti ingawa mwanzo sauti ile ilikuwa haitoki vizuri.

“Wanashitakiwa na Jamhuri kwa kosa la kujaribu kuua kwa kumtupa mtoto mchanga” Askari yule wa kiume alijieleza huku askari wa kike akiwafunga pingu Naima na Suzy.

“Ayubu naomba umlee mtoto wetu kwa upendo. Tambua nawapenda sana wote wawili” Suzy alizungumza kwa uchungu huku akimwaga machozi. Aliwageukia wazazi wake na kuwa tazama kwa huruma.

“Baba na Mama nawapenda sana. Mungu atakuponya baba yangu mpendwa” Suzy aliendelea kuzungumza kwa machungu.

Mama Suzy hakuweza kujibu kitu zaidi ya kuangua kilio. Mzee Manyama naye akawa kimya akimkodolea macho binti yake.

Ayubu akiwa na mtoto wake mikononi roho yake ilikuwa ikimuuma kuliko kawaida. Hakuweza kuamini jinsi ambavyo mambo yote yale yalikuwa yakimtokea kwa wakati mmoja. Alishuhudia jinsi ambavyo mpenzy wake Suzy alivyokuwa akisukumwa na askari kutolewa nje ya wodi ile.

Suzy alipofika mlangoni aligeuka nyuma na kumpungia mkono Ayubu. Kijana Ayubu alishindwa kujizuia kutoa machozi ambayo yalimdondokea mtoto wake kwenye utosi. Mzee Manyama alimtazama Ayubu kwa kitambo na kujikuta akimhurumia sana kijana yule na kumeza funda la mate ya uchungu na majuto.

“Ayubu mwanangu, Hii ndiyo BONGO unatakiwa kuishi kwa akili za kutosha. usipoutumia vizuri ubongo wako unaweza kuangukia pabaya. Sisi sote hatukutumia vizuri bongo zetu na ndiyo maana yote haya yametokea” Mzee Manyama alizungumza kwa uchungu.

Ayubu alimtazama mtoto wake kisha akavuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu kisha akasema kwa sauti “Amakweli hii ni BONGO DASLAM”


MWISHO


0 comments:

Post a Comment

BLOG