Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

BONGO DAS'LAAM - 3

   


Chombezo : Bongo Das'laam 

Sehemu Ya Tatu (3)


“Unataka kunielewa sio?”

Suzy alibaki kimya akimtazama Naima ambaye alikuwa anafyatua maneno utafikiri alikuwa akimsubiri kwa muda mrefu amuanze ili amalize.

“Sasa sikiliza, mjini hapa usipokuwa makini utaumia. Lazima bongo ifanye kazi” alisema Naima kwa msisitizo.

“Unamaanisha nini Naima?”

“Namaanisha uamke”

“Mnh! Bado sija kuelewa”

“Ni hivi, ni lazima uwe na biashara ya ziada” Naima akafafanua.

“Sasa nimekuelewa, lakini tutapata wapi mtaji wa kuongeza hiyo biashara nyingine?” Suzy alizungumza huku akionekana kuvutiwa na mawazo ya maendelea yaliyokuwa yakitolewa na rafiki yake yule.

“Usinichekeshe wewe! Mtaji gani tena unataka wakati uliokuwa nao huwezi kuutumia?” Naima alizungumza na kumuacha Suzy njia panda.

“Sasa Naima rafiki yangu, kama una mbinu mbadala ya kuuendeleza mtaji wetu wa samaki ni bora tuambiane jinsi ya kufanya.”

“Bado umelala Suzy, unahitaji kuamka” Naima alizidi kumchanganya Suzy.

“Unanichanganya Naima, hembu weka mambo wazi rafiki yangu”

“Sioni sababu ya kuendelea kukuficha Suzy. Hivi unavyoniona nakwenda kazini” Naima alieleza.

“Kazini! Unafanya kazi gani?” Suzy alihoji kwa mshangao.

“Unaona mkia wa mbwa halafu unauliza makalio yako wapi? Unadhani kwa mavazi haya nitafanya kazi gani?” Naima alisema huku akisimama na kujitingisha tingisha na kujiangalia nguo alizokuwa amevaa. Suzy alianza kuhisi alichokuwa akikimaanisha Naima, akavuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu.

“Unauza baa?” Suzi alihoji.

“Una wazimu wewe”

“Sasa unafanya kazi gani jamani mwenzangu”

“Nasaka mshiko mama, nafanya kazi ya kusaka pesa!”

“Najua unasaka pesa, lakini unafanya kazi gani?” Suzy akahoji kwa msisitizo.

“Mama nadanga mama huelewi”

“Inamaana unajiuza?”

“Hilo ndio jibu”

“Kwanini ufanye hivyo?”

“Unauliza kwanini nafanya biashara? Ok. Jibu ni kwamba nafanya biashara ili kuendesha maisha yakwako na ya kwangu. Ila kwa sasa imetosha kunyonyana. Nawe ni mwanamke kama mimi lazima tusaidiane” alisema Naima akimtazama Suzy pasipo kupepesa macho hata kidogo.

“Lakini Naima…..” Suzy alitaka kusema kitu lakini akakatizwa na Naima.

“Lakini nini?”

“Nadhani unaijua hali yangu.”

“He! makubwa! Baba wa hicho kijusi chako unamjua alipo?”

Suzy alibaki kimya akimuangalia Naima kwa jicho la mshangao. Siku zote ameishi naye hakuwahi kufahamu kama msichana yule angeweza kuwa na maneno ya shombo kiasi kile.

”Nakuuliza wewe!!” Naima alipaza sauti kukazia swali lake.

Suzy alitingisha kichwa kuonesha kuwa hakuwa anafahamu mwanaume aliyempa ujauzito alipokuwepo kwa wakati ule.

“Sasa unategemea nini?”

“Labda unishauri cha kufanya Naima. Mimi nimekwama” Suzy alizungumza kwa sauti ya kukata tamaa.

“Unataka ushauri wangu sio? Naima alihoji huku akiketi kwenye mkono wa kochi

“Ndio”

“Una uhakika?”

Suzy aliitika kwa kichwa pasipo kutoa neno lolote huku akiamini rafiki yake yule angeweza kumpa ushauri wenye manufaa.

“Tukitolee mbali hicho kijusi” Naima alizungumza huku akiangalia pembeni kama waswahili wanavyosema, “Ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni”.



Maneno ya Naima yalimuingia ipasavyo Suzy na kumsababishia kichomi kilichoanzai kwenye moyo na kusafiri hadi tumboni. Hakuamini kama rafiki yake huyo angeweza kuwa na ushauri wa kufanya mambo kama yale, akahisi kama vile alikuwa ndotoni. Alipokimbia nyumbani alihofia kuuawa na Mzee Manyama, sasa anakutana na kifo kitokanacho na kutoa mimba.

“Unasemaje Naima?” Suzy akahoji kama vile hakusikia maneno ya rafiki yake yule.

“Utoe hiyo mimba”

“No! haiwezekani Naima”

“Kwanini isiwezekane? kama ni pesa za kutolea mimi nitakupa” Naima aliendelea kushawishi.

“Napenda kuishi Naima”

“Kwani nani amekwambia ujinyonge? Mimi nimekwambia utoe mimba, Sijakwambia ujinyonge we vipi!” Naima alizungumza kwa msisitizo.

“Kutoa mimba ni kujiua Naima”

“Kwenda zako! Kama ni kufa basi mimi ningekwishakufa mara kibao” Naima alizungumza kwa msisitizo.

“Kwahiyo nawewe umekwishawahi kutoa mimba Naima?” Suzy alihoji kwa hofu

“Sio mara moja, Nimeshazichomoa kama sita hivi au saba kama sikosei” Naima alizungumza bila wasiwasi.

“Hata hukumbuki ni ngapi!” Suzy akahoji kwa mshangao.

“Siwezi kukumbuka, ni nyingi mno!”

“Mungu wangu!” Suzy alihamaki kwa sauti ya kukata tamaa.

“Sasa kinachokushangaza ni kipi? Au umeniona nimekufa? Naugua? Achana na Imani za kipuuzi wewe amka Suzy” Naima aliendelea kuzungumza kwa kushawishi.

“Hivi utakuja kuzaa kweli Naima au ndio umeshaua kizazi?”

“Nyoo! Aliyekwambia nina mpango wa kuzaa ni nani? Okay kama kweli kutoa mimba kunaharibu kizazi mbona kila nilipozitoa ziliendelea kuingia?” alizungumza Naima na kumuwacha hoi Suzy.

“Mnh!”

“Unaguna nini sasa?”

“Nampenda sana Ayubu, na sijui huko aliko kama amekufa ama yupo hai” Suzy alizungumza kwa sauti ya chini.

“Kwahiyo unataka kusemaje?”

“Huyu mtoto wake ndiye atakayenifanya nimkumbuke” Alisema Suzy na kutaka kutoka nje lakini Naima akamdaka mkono.

“Sikulazimishi binti ila nakupa siku tatu, kama haupo tayari kutoa hiyo takataka yako hapa kwangu uondoke” alisema Naima na kutoka nje kwa mwendo wa haraka.

Suzy alibaki amechoka kutokana na maneno yale machachu. Naima aliyekutana naye siku ya kwanza alikuwa ni tofauti kabisa na yule aliyekuwa akizungumza naye siku ile. Kwa upande mwingine akawa anajilaumu kwa kihelehele chake cha kuhoji mambo yasiyo mhusu. Alijitupa kitandani na kuendelea kutafakari maneno ya rafiki yake Naima.

****

Ayubu alifanikiwa kuingia kwa mara ya pili ndani ya jiji la Dar eS salaam. Safari hii hakupata tabu kama alivyo fika kwa mara ya kwanza. Kwakuwa alikuwa mwenyeji kidogo alielekea maeneo ya RIVER-SIDE ambako kulikuwa na gesti za bei rahisi. Alichukua chumba na kukilipia kwa muda wa wiki moja. Alitegemea kukaa pale kwa siku hizo na kurudi mkoani Tanga baada ya kuonana na Suzy msichana aliyekuwa na ujauzito wake.

Siku iliyofuata ilikuwa ni Jumatano, siku hiyo mzee Manyama alikuwa akienda kazini asubuhi sana na kurejea usiku. Ilipofika mida ya saa tatu na robo asubuhi, Ayubu alipanda basi lililokuwa likienda mwenge. Kutokana na foleni kubwa ya magari kwenye mataa ya Ubungo alichukua takribani muda wa dakika thelasini kufika. Akapanda tena basi lililokuwa likielekea kariakoo na kushukia Bamaga ambako alianza kutembea mdogomdogo hadi Kijitonyama ambako ndiko Suzy alikokuwa akiishi na wazazi wake.

Kila alivyokuwa akikaribia nyumbani kwa mzee Manyama mapigo ya moyo wake ndivyo yalivyo ongezeka. Alivuta picha ya tukio ambalo lingetokea endapo angemkuta mzee Manyama. Alijikuta akisali kimoyo moyo asionane na Mzee huyo. Kwa mbali akahisi kuwa hata mama Suzy naye pia alikuwa akimuogopa wakati mwanzo hakuwa na wasiwasi naye hata chembe. Akajikuta akisita kuendelea na safari ile. Alisimama na kutafakari kwa muhtasari juu ya lile tukio la hatari alilokuwa analifanya.

“Potelea mbali, liwalo na liwe” alijisemea na kusonga mbele.

Moyo wake ulizidi kumuenda mbio baada ya kuona mjengo wa nyumba ya mzee Manyama. Alipunguza mwendo na kuvuta hatua kwa tahadhari kusogelea mlango wa nyumba ile. Alikuwa kama mwizi jinsi alivyoonekana kuwa na wasiwasi. Alipofika mlangoni akawa anajishauri kugonga mlango ule au aahirishe, lakini kabla hajachukua uamuzi huo mgumu aligeuka nyuma kuangalia kama kulikuwa na mtu anamuangalia. Mawazo yake yalikuwa sahihi, alikutana na macho ya mama Suzy amesimama hatua chache kutoka pale mlangoni akishangaa vioja vile.

“Ayubu!” mama Suzy aliita kwa taharuki.

“Naam mama” Ayubu aliitika huku akitetemeka, alishindwa kuficha hali yake ya uwoga mbele ya mama Suzy.

“Wala usihofu, karibu ndani” alisema mama Suzy na kusukuma mlango.

Ayubu hakuamini macho na masikio yake, mawazo yake yalimueleza kuwa akifika pale atafukuzwa kama paka mwizi lakini akaona mambo ni tofauti.

“Karibu ndani Ayubu” alisema tena mama Suzy akimuelekeza akae kwenye kochi. Lilikuwa ni lile lile kochi alilokalia siku ya kwanza alipoletwa pale nyumbani. Akaketi huku akitegemea kuwa angemuona Suzy akitokezea kwenye korido ya nyumba ile muda wowote. Kwa upande mwengine alijiweka tayari kutimua mbio endapo angeona dalili zozote za hatari.

Mama Suzy aliketi kwenye kochi la mbele yake na kumtumbulia macho kwa dakika nzima pasipo kuzungumza neno lolote. Moyo wa Ayubu ukazidi kujawa na woga kutokana na kutofahamu alichokuwa akikiwaza mama Suzy ndani ya ukimya ule. Mama Suzy alipumua kwa nguvu kisha akameza funda la mate na kutafuna meno yake.

“Amakweli ni kheri kumfadhili mbuzi utamla mchuzi” alisema mama Suzy kwa masikitiko na hasira.

“Naomba unisamehe mama”

“Nimesha kusamehe, ila nataka kujua kitu hiki…” Alisema mama Suzy huku akinyoosha kidole kuashilia kitu kimoja. Ayubu akakubali kwa kichwa kutoa msaada huo ingawa hakuwa anafahamu ni msaada gani.

“Mwa na ngu yu ko wa pi?” alihoji mama Suzy kwa msisitizo.

“Nani?....Su…Su…Suzy?” Ayubu akajikuta akishituka na kushindwa kuzungumza. Kilichokuwa kimempeleka pale kilikuwa ni kumuangalia Suzy. Sasa akashituka kusikia kuwa mama yake anamuuliza yeye alipo huyo Suzy.

“Usijichetue Ayubu, niambie mwanangu alipo?” Alizunguma mama Suzy kwa hasira

“Mama mimi nimekuja hapa kwa lengo la kumuulizia yeye na…..”

“Koma! kunguru we! Inamaana umeniulia mwangu?” mama Suzy alifoka

“Mimi sielewi chochote mama, siku niliyo ondoka hapa nilirudi Tanga”

“Wewe ni shetani Ayubu, umeharibu kabisa amani ya humu ndani. Umemponza mwanangu, ameacha shule na sasa hajulikani alipo. Kila kukicha ni ugomvi mimi na baba yake” mama Suzy alizungumza kwa hasira.

Maneno yale ya mama Suzy yalimchoma sana Ayubu ndani ya moyo wake. Alijutia nafsi yake ingawa mambo yote yale yalikuwa yamesababishwa na binti yao wenyewe. Alitulia kimya kama vile alikuwa amebandikwa plasta mdomoni.

“Sasa sikiliza Ayubu” mama Suzy alionekana kushusha hasira na kuzungumza kwa upole lakini kwa mkazo. Ayubu aliinua shingo na kumtazama Mama Suzy usoni.

“Tushirikiane mimi na wewe kumtafuta Suzy. Baba yake anamhitaji mwanawe”

“Sawa mama. Mimi ndicho kilichonileta hapa Jijini”

“Kwa sasa umefikia wapi?”

“nimefikia Gest”

“Gest!!”

“Ndio mama”

Mama Suzy alishituka kusikia kuwa Ayubu alikuwa amefikia gest. Hali ya Ayubu alikuwa akiifahamu vizuri sana, asingeweza kupata pesa za kuishi gest kwa muda mrefu. Lakini hakutaka kuhoji chochote kwasababu alimfahamu Ayubu kuwa alikuwa habebeki.

“Una simu?” mama Suzy alihoji.

“Ndio mama”

“Nipe namba yako” alisema mama Suzy huku akitoa simu yake kwa lengo la kuchukua namba za Ayubu. Zoezi lile la kupeana namba za simu lilikatishwa na hatua za mtu aliyekuwa akielekea mlangoni kwa mama Suzy.

“Mungu wangu!” Mama Suzy akahamaki kwa hofu.

“Vipi mama?”

“Hizo ni hatua za mzee Manyama” alisema mama Suzy kwa sauti ya chini.

Ayubu aliposikia vile alitaka kuchomoka mlangoni lakini mama Suzy akamzuia.

“Hapana usitoke nje atakumaliza”

“Sasa nifanye nini?”

“Njoo huku” alisema mama Suzy huku akielekea kwenye korido iliyokwenda vyumbani.

Ayubu alijikuta akimfuata nyuma pasipo kujielewa. Walikwenda moja kwa moja hadi kwenye chumba kilichokuwa cha Ayubu zamani. Mama Suzy akafungua kabati lililokuwa na mafaili ya Mzee Manyama.

“Ingia humu, fanya haraka” Alisema mama Suzy.

Masiki ya Mungu Ayubu aliingia na kuketi ndani ya kabati la mzee Manyama. Jinsi alivyokuwa amejikunja hakutofautiana na kifaranga cha kukuu kilichotoka kunyeshewa na mvua kubwa.

Baada ya zoezi hilo la kumficha Ayubu, mama Suzy alirejea mlangoni kumfungulia mume wake ambaye muda wote huo alikuwa akibisha hodi bila ya mafanikio ya kufunguliwa mlango.

“Karibu mume wangu” alizungumza mama Suzy mara tu alipofungua mlango.

“Tangu saa hizo nagonga mlango ulikuwa unafanya nini?” Alikoroma mzee mManyama kama baba mwenye nyumba.

“Nilikuwa nimelala mume wangu” Mama Suzy alijieleza kwa kuongopa.

“Umelala saa hizi unaumwa?”

“Hapana mume wangu nilikuwa nimepumzika tu. Vipi mbona mapema sana leo?” mama Suzy alizungumza na kuhoji.

“Kunakitu nimefuata” alisema mzee Manyama na kuingia ndani.

Mzee yule alikuwa akielekea kwenye mlango wa chumba alichokuwemo Ayubu. Mama Suzy akaona balaa lilikuwa likikimbilia kuivaa tena familia yake. Haraka sana mama yule akamuwahi mume wake na kwenda kusimama mlangoni.

“Ni kitu gani umesahau mume wangu” alihoji mama Suzy huku akimpapasa kifuani baba wa watoto wake.

“Kuna faili humu kwenye kabati” Mzee Manyama alijibu huku akimsukuma kidogo mama Suzy na kuingia chumbani kwenye lile kabati alimokuwa amejificha Ayubu.

Mama Suzy alitaka kumshika mkono lakini akawa amechelewa, mzee Manya akasimama kwenye mlango wa kabati lile alilokuwemo Ayubu. Alipeleka mkono wake kwenye kitasa cha mlango wa kabati lile na kukinyonga.

“Kwani vipi Mama Suzy! Mbona kama haupo sawa?” alihoji mzee Manyama akifungua mlango wa kabati huku macho yake kayakooa kwa mke wake ambaye alikuwa akiongea naye wakati ule.

Mle ndani ya kabati Ayubu alimshuhudia mzee Manyama amesimama mbele yake akiwa amekamatia vyema kitasa cha kabati lile huku tayari mlango ukiwa wazi. Akabakia kusubiri mzee yule arudishe macho ndani ya kabati na kumuona.

Ayubu hakutegemea kama siku moja angeweza kuingia mikononi mwa mzee Manyama kirahisi kiasi kile. Lawama zote alimtupia baba yake mzee Nyiruka kule kijijini amaye ndiye aliyemlazimisha kurudi tena jijini Dar es salaam kumsaka Suzy. Sasa kabla hata hajafanikiwa kukipata kile kilichokuwa kimemrudisha jijini mle akajikuta anaingia mikononi mwa nduli Manyama. Hakupata picha ya kitu ambacho kingemtokea baada ya kukamatwa na mzee yule aliyekuwa akimsaka kwa muda mrefu.



Mama Suzy naye alikuwa kama vile amechenganyikiwa baada ya kumshuhudia mume wake akifungua mlango wa kabati lile. Akaona wazi kuwa kifo kilikuwa halali yake baada ya Ayuu kukutwa ndani ya kabati lile.

Akili ya mama Suzy ikafanya kazi kwa haraka kama kompyuta na kabla mzee Manyama hakupeleka macho yake kuangalia ndani ya kabati, Mama Suzy alijidondosha chini na kutoa sauti kali ya maumivu iliyomshitua mume wake.

Mzee manyama aliachia mlango wa kabati na kumkimbilia mke wake ambaye alikuwa amelala sakafuni kama mzoga.

“Vipi mama Suzy, unatatizo gani?” Mzee manyama alihamaki huku akimshika mke wake kuangalia kama mapigo ya moyo yalikuwa yanaendelea kuwajibika. Mzee Manyama alipoona hajibiwi na mke wake yule aliyekuwa amelala chini kama amekufa akatoka nje mbio kwa lengo la kutafuta usafiri wa kumuwahisha hospitali.

Baada ya mzee Manyama kutoka chumbani mle Mama Suzy aliamka kwa haraka na kuelekea kabatini alipokuwa amejificha Ayubu nakumpa maelekezo kwa sauti ya msisitizo.

“Hakikisha unafanya mbinu yoyote hadi utoke humu ndani”

Ayubu aliitika kwa kichwa kuashiria kuwa alikuwa ameyaelewa maneno ya mama Suzy. Viliposikika vishindo vya miguu yam zee Manyama vikirejea chumani mle, mama Suzy alijilaza haraka pale alipokuwa ameangukia awali.

Mzee Manyama alikuwa amerejea na vijana wawili ambao alisaidiana nao kumbeba Mama Suzy hadi nje ambako walimpakia kwenye gari na kumkimbiza hospitali.

Kulipokuwa kumetulia kabisa Ayubu alitoka mle kabatini huku akiwa bado anatetemeka kwa hofu. Alitembea kwa tahadhari na kuuendea mlango ambao haukumsumbua kuufungua kwasababu alikuwa ameuzoea wakati alipokuwa akiishi ndani humo. Mlango ule ulikuwa na namna ya kuufungua kwa ndani hata kama ulikuwa umefungwa kwa nje.

Ayubu alipofanikiwa kutoka nje hakuweza kuamini kama alikuwa bado yupo hai anapumua. Alijiona kama vile alikuwa ngamia aliyeponea kwenye tundu ya sindano. Kwa spidi kali kama kibaka mgeni alitoweka katika mazingira yale. Akaapa kuto kurudi tena nyumbani pale kwa mzee Manyama. Hakuwa tayari kabisa kukutana tena na mzee yule aliyekuwa na roho katili kama ya mnyama.

****

Ayubu alipofika gest ambako alifikia alijitupa kitandani chali huku macho yake yakiwa juu ya dari. Jambo lililokuwa limemrejesha tena jijini lilikuwa limekwama. Akabaki akiwaza na kuwazua namna ambavyo angeweza kumtafuta Suzy wake ndani ya jiji lile llenye upana wa bahari. Akakumbuka jinsi ambavyo alihangaika kumtafuta rafiki yake Kondo kwa muda mrefu pasipo mafanikio.

“Huu ni upuuzi. Siwezi kumtafuta mtu ambaye sifahamu alipo” alijisemea huku akitoa simu yake kutoka mfukoni. Alivuta namba ya baba yake mzee Nyiruka na kumpigia.

“Haloo…” aliita Ayubu mara tu simu ile ilipopokelewa.

“Ndio mwanajeshi wangu hujambo?” sauti ya mszee Nyiruka ilisikika kupitia kwenye spika ya simu ya Ayubu.

“Sijambo baba shikamoo”

“Marahaba. Haya niambie umefikia wapi?”

“Baba mambo ni magumu. Suzy hajulikani alipo” Ayubu alizungumza kwa sauti iliyokata tamaa.

“Kwahiyo unasemaje?”

“Baba mimi narudi”

“Hapana! usirudi hapa kama hujampata huyo binti.”

“Lakini baba…..”

“Hakuna cha lakini, damu yetu haiwezi kupotea kijinga jinga. Hakikisha unampata huyo mama na mtoto wetu wakiwa salama kabisa” alizungumza kwa msisitizo mzee Nyiruka.

“Sawa baba” Ayubu akajibu kwa unyonge kisha simu ikakatika. Aliitupa pembeni na kuendelea kuwaza na kuwazua. Hakujua aanzie wapi katika zoezi lake lile aliloliona zito kupita umri wake. Usingizi ukamchukuwa pasipo kujitambua.

****

Honi za magari na pikipiki zilimuamsha Ayubu kutoka usingizini. Alijihisi mwili ukimuuma mno, akatulia kitandani kwa muda mrefu akitafakari pa kuanzia katika zoezi lake lile la kumtafuta mpenzi wake Suzy. Alikumbuka ahadi aliyokuwa amepewa na mama Suzy kuwa angekuwa pamoja naye katika zoezi lile. Akatamani angekuwa na namba zake za simu ili awasiliane naye lakini hakuwa nazo. Alimlani sana mzee Manyama kwa kusababisha asichukue namba ya simu ya mama Suzy.

Ayubu alijiinua tayari kwa kuanza maandalizi ya kutoka kwenda kufanya msako wa mama watoto wake Suzy. Alitoka na kwenda kupata kifungua kinywa kwenye mgahawa uliokuwepo karibu na Gesti ile aliyokuwa amepanga.

Akiwa pale mgahawani alishituliwa na mtu aliyemshika begani kwa nyuma yake. Alipogeuka akakutana na sura ya msichana ambayo ilikuwa ngeni machoni mwake.

“Habari yako kaka” msichana yule alimsalimia Ayubu huku akitabasamu.

“Safi mambo vipi” Ayubu aliitika salamu ile huku akiwa na hamu kubwa ya kutaka kufahamu sababu iliyopelekea binti yule kumshika bega lake.

“Samahani kaka nimekufananisha?”

“Mmm! Sijui, Umenifananisha na nani?” alihoji Ayubu huku akibenjua mabega yake juu.

“Kuna kaka mmoja anaitwa Adam” alisema yule msichana huku akisikilizia jibu la Ayubu.

“Hapana sio mimi”

“Kweli?”

“Sasa kwanini nikudanganye” Ayubu alijibu na kupeleka kikombe cha chai mdomoni.

Kiukweli msichana yule hakuwa amemfananisha Ayubu kama alivyokuwa amejieleza, bali alikuwa amevutiwa na uzuri wa Ayubu pamoja na utanashati wake. Alimeza funda la mate kabla ya kumsemesha tena.

“Pamoja na kwamba sio wewe kaka, ilaa….” Yule msichana alisita kumalizia.

“Ila nini?” alihoji Ayubu huku akiweka kikombe cha chai kwenye kisahani kilichokuwepo mezani.

“Naweza kukaa hapa?” alihoji huku akionesha kwenye kiti kilichokuwa pembeni mwa Ayubu.

“Bila shaka, hapa ni mgahawani yeyote anaweza kukaa”

Dada yule alikaa kwenye kiti kilichokuwepo mbele ya Ayubu, wakawa wanatazamana.

Baada ya msichana yule kuketi na kumuangalia vizuri Ayubu akabaini kuwa alikuwa ni mrembo mno. Weupe wake wa asili uliopitiliza ulikuwa umepambwa vyema kwa macho yake madogo meusi. Alipotabasamu meno yake madogo meupe yalikuwa yamepangika vizuri mithili ya gwaride la askari wa usalama barabarani.

Ingawa awali Ayubu hakuwa tayari kusemeshwa na mwanadada yule, lakini alipomuona akaishiwa nguvu na kujikuta akiachia tabasamu la kujilazimisha. Yule dada akajikuta mapigo ya moyo wake yakiongezeka baada ya kuliona tabasamu la kijana Ayubu. Wakajikuta wote wawili wakitoleana tabasamu.

“Naitwa Naima, sijui mwenzangu unaitwa nani?” Msichana yule alivunja ukimya.

“Nashukuru kukufahamu, mimi naitwa Kimaya” Ayubu alijaribu kudanganya.

“Waao! Jina zuri kama ulivyo mwenyewe” Naima alitoa sifa.

“Wacha masihara bwana, lina uzuri gani jina kama mzizi” alisema Ayubu huku akiachia tabasamu na kummaliza zaidi binti wawatu.

“Kweli sikutanii. Jina lako zuri” msichana yule alisisitiza huku akirembua vile vimacho vyake.

“Ok. sio mbaya ila kama hutojali unaweza kuniita Kim” Ayubu alifafanua ili kumfanya msichana yule kuamini jina lile la uwongo.

“Nitakuita Kim kama upendavyo wewe” Naima alisema kwa kutolea sauti puani huku akijisheedua mbele ya macho ya Ayubu.

Wote wawili, Ayubu na yule msichana aliyejitambulisha kwa jina la Naima walicheka kicheko ambacho hakikuwa na sababu. Ayubu akaona jinsi mashavu ya Naima yalivyokuwa yakibonyea pale alipocheka. Akajikuta akizidi kupagawa na kusahau sababu iliyompeleka jijini Bongo.



Naima akajifanya anaharaka na kuinuka kutoka pale kwenye kiti, akatoa simu yake kutoka kwenye kipochi chake kidogo.

“Sasa ngoja nikuache kuna mahali nawahi, sijui naweza kupata namba yako?” Naima alihoji kwa sauti yake iliyojaa mitego.

Ayubu akajichekesha chekesha na kujikuta akitaja namba zake kwa msichana yule ambaye ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuonana nae. Naima akaandika namba zile kisha akambipu na Ayubu naye akasevu namba za msichana yule aliyejitambulisha kwa jina la Naima.

“Haya karibu kwetu Msewe” Naima alisema huku akivuta hatua kuondoka pale mgahawani. Ayubu akawa anamtazama mrembo yule aliyekuwa akitembea mithili ya twiga aliyeshiba mbugani. Akavuta pumzi nyingi kwa mdomo na kuzitoa kwa msukumo kupitia pua yake nyembamba ndefu.

Baaya ya Naima kuondoka, Ayubu alijishitukia na kuhisi kuwa alikuwa ametenda kosa kubwa sana ambalo hakupaswa kulifanya. Akashindwa kuelewa ni kwa vipi amekuwa mwepesi na mdhaifu kwa msichana yule asiyemfahamu hadi kufikia hatua ya kutoa namba zake za simu kirahisi vile. Akabaki akijilaumu kutokana na kitendo kile cha kipuuzi alichokifanya.

Alifanya malipo kisha akarejea gest kwenye chumba chake alichokuwa amepanga na kujitupa kitandani. Baada ya dakika chache, kumbukumbu za Suzy zilimjia kichwani mwake na kumfanya akurupuke kutoka pale kitandani.

Baada ya kuamka Ayubu alichokifanya ni kwenda stendi na kupanda gari ya Mbagara. Hakufahamu angemuona vipi lakini aliamini ni lazima angempata tu kipenzi cha roho yake ambaye ndiye aliyechangia kumuweka katika wakati mgumu kiasi kile.

***

Mzee manyama hakuweza kugundua mchezo aliochezewa na mke wake pamoja na kijana aliyekuwa akimsaka kwa muda mrefu. Alichokuwa akiamini ni kwamba kweli mke wake alikuwa anaumwa. Ama kweli usilo lijua ni sawa na usiku wa giza. Nahisi kama mzee yule angeushitukia mchezo ule basi angechinja mtu siku hiyo.

Ingawa Mama Suzy alifanikiwa kumtorosha Ayubu kutoka ndani mwake lakini alijilaumu kwa kitendo cha kuchelewa kuchukua namba za simu za kijana yule. Alipokuwa akiwaza namna ambavyo angempata akakumbuka kuwa Ayubu alimweleza kuwa alikuwa amepanga gest maeneo ya River-Side. Ingawa hakufahamu ni gest gani lakini akajipa moyo na kuanza kumtafuta. Alifahamu wazi kuwa Ayubu ndiye msaada wake mkubwa katika kumtafuta binti yake wa pekee aliyekuwa akimpenda sana.

“Nitakwenda gest zote za River-Side kumuulizia. Lazima nitampata tu” alisema mama Suzy na kujiinua kutoka kitandani alipokuwa amejipumzisha.

***

Naima aliporudi kutoka kwenye mizunguuko yake alimkuta Suzy akisafisha samaki kwaajili ya kuwakaanga kwa biashara. Sura ya Naima ilikuwa imejawa na furaha na kuonekana kuwa alikuwa na kitu alichotaka kukisema kwa Suzy.

“Niambie Mamaa wa masamaki…” alisema Naima huku akiachia tabasamu zito.

“Nikwambie nini shoga. Hebu nipe siri ya furaha yako leo” alihoji Suzy.

“Dah! We acha tu shoga. Tembea uonekane mwenzangu” alisema Naima na kuingia ndani.

Suzy alibakia katika maswali yasiyo na majibu. Alitamani kujua kitu kilichomfanya rafiki yake kujawa na furaha kiasi kile wakati alikuwa ni mtu wa kunununa muda wote.

Naima aliweka kibegi chake ndani na kujivisha upande wa kanga kisha akatoka nje kwa Suzy ambaye alikuwa akiendelea kusafisha samaki.

“Enhee nataka kujua hayo yaliyo kufurahisha kiasi hicho” Suzy alisema baada ya kumuona Naima.

“Suzy maisha yangu yote hapa Bongo sijawahi kuona” alisema Naima huku akijiweka juu ya matofari yaliyokuwa yamerundikwa pale nje.

“Sasa nawewe unanitia hamu halafu unachelewa kunipa utamu” suzi alisema maneno ambayo yakapelekea wote wawili kuangua kicheko.

“Shoga nimekutana na mwanaume ni mzuri….” Alieleza naima kwa msisitizo.

“Wacha we!..”

“Ni kijana mtanashati, mcheshi, mstaarabu, ana sura……”

Kabla hajamalizia sentensi yake Suzy alimkatisha.

“Eeeh! Hongera sana shoga.”

“Yani nikimpata yule kaka, sitakuwa na haja ya kudanga tena”

“Anaitwa nani?” Suzy alihoji kwa shauku.

“Kimaya lakini mwenyewe anapenda kuitwa Kim”

“Sasa amesha kutongoza?”

“Anitongoze! Kwa kipi nilicho nacho? Yule nitamtongoza mwenyewe”

“Haya kazi kwako. Umemuona Kim tu ni hivyo, je ungemuona Ayubu?” Suzy akasema kwa utani.

“Huyo Ayubu wako pale atasubiri sana.”

“Haya bwana nimekubali kushindwa.” Suzy alijibu na kuendelea kutengeneza samaki wake wa biashara huku akimuunga mkono rafiki yake kwa kucheka.

Naima alionekana kuwa na furaha kupita maelezo baada ya kukutana na mwanaume aliyemvutia sana.

Suzy alifahamu kuwa mwanaume yule aliyekuwa akisifiwa na Naima asingeweza kumfikia mwanaume wake yeye yaani Ayubu. Aliwaza vile pasipo kudhani hata kidogo kuwa mwanaume aliyekuwa akimzungumzia Naima ndiye huyo huyo mwanaume aliyemsababishia yeye kuwa pale kwa Naima.

***

Maisha ya Gest yalikwisha mchosa Ayubu. Mbaya zaidi ni kile kitendo cha kulipia chumba pesa nyingi kwa siku. Kwakuwa alikwisha kuwa mwenyeji pale jijini akawapa kazi madalali wamtafutie chumba cha kupanga na kwa bahati nzuri alipatiwa chumba Stop-Over maeneo ya Kimara.

Nyumba aliyokuwa amepangishwa ilikuwa na wapangaji wengi wanawake. Wengine walikuwa na waume zao na wengine hawakuwa wameolewa. Kwa wanaume waliokuwa wakiishi pale ni yeye peke yake ndiye alikuwa hajaoa.

Ilikuwa ngumu sana kwa Ayubu kuzoeleka kirahisi na wapangaji wenzake kwasababu alikuwa akiondoka asubuhi na kurejea kwake kulikuwa ni usiku. Ilimlazimu kufanya vile kwasababu ya mambo makuu mawili ambayo ni kumsaka mpenzi wake Suzy na jambo la pili kufanya vibarua ambavyo vilimuingizia pesa ya kula na kulipia kodi ya chumba. Kwa kiasi kikubwa maisha ya Ayubu hayakuwa mazuri kwasababu ndio kwanza alikuwa akianza maisha ya kujitegemea pale jijini Dar es Salaam.

Jumamosi moja Ayubu aliamua kujipa mapumziko mwenyewe. Lengo kubwa lilikuwa ni kufanya usafi wa nguo zake pamoja na chumba chake kwa ujumla.

Akiwa nje ameinamia ndoo yake akifua nguo akasikia sauti ya mwanamke ikimsalimia.

“Habari yako kaka”

Ayubu akainua macho kumuangalia mtu aliyekuwa akimsalimia. Alikuwa ni mama Asha mpangaji mwenzake kwenye nyumba ile ambaye alikuwa amejifunga upande mmoja wa kanga kifuani ambayo iliishia sehemu za magoti yake kiutokana na kuvutwa kwa kiasi kikubwa na mzigo wa kutosha wa madafu aliyokuwa amefungasha kwa nyuma.

“Salama Aunt, habari za asubuhi?” Ayubu akaitika salamu ile.

“Pole kwa kazi” alisema mama Asha kwa sauti iliyojaa shauku kubwa ya ujirani mwema.

“Aah! Usijali” Ayubu alijibu na kuinama kuendelea kufua.

Yule mwanamama alijipitisha karibu na Ayubu kuelekea maliwato. Ayubu aliinua macho kidogo kwa wizi kumuangalia mwanamke yule alivyokuwa akitembea huku akidondosha mizigo yake mmoja mmoja kila alipokuwa akipiga hatua. Mizigo ile ilikuwa ikidondoka kwa fujo utafikiri haikuwa imefungiwa kwa kufuli. Kufuli iliyokuwa imefungia mzigo ule ilikuwa ikionesha alama juu ya ile khanga iliyokuwa laini.

“Asante!” Ayubu alizungumza kwa sauti ya chini huku akigeuza macho yake na kuendelea na shughuli yake ya ufuaji.

Mama Asha alipotoka msalani alivuta hatua na kwenda kuketi kwenye ngazi za mlango mkubwa wa kuingilia ndani ambazo zilikuwa mbele ya Ayubu. Ayubu alipoinua macho alikumbana na mama Asha ameketi mbele yake akijifanya kuangalia pembeni kama vile hakuwa anamuona. Ile kanga yake ilikuwa imening’inia upande mmoja na kufanya sehemu ya paja lake la mguu wa kushoto kubaki wazi. Ayubu akarejesha macho yake haraka kwenye nguo zake alizokuwa anafua.

Mama Asha alichezesha midomo yake huku akitoa tabasamu la “Utanasa tu” huku akipeleka mkono wake kwenye paja na kufunua zaidi ile khanga.

Kitendo cha mama Asha kuketi pale mlangoni kilimpa wakati mgumu sana Ayubu. Mbaya zaidi ni kwamba mwanamke mwenyewe alikuwa amejikalisha kihasara hasara hata stara hakuwa nayo.

Kama unavyojua tabia ya jicho ndugu msomaji, Ayubu aliinua macho yake kwa lengo la kuangalia mara ya mwisho huku akijipa moyo ni lazima Mama Asha angekuwa amejishitukia na kujirekebisha.

Laa haulaa! Ayubu hakuweza kuamini yale macho yake yaliyokuwa na kimbelembele cha kuangalia angalau mara moja ya mwisho. Safari hiyo Ayubu aliweza kuona hadi kufuli la mama Asha kutokana na kufunuliwa Zaidi kwa ile khanga.

“Mungu wangu!” Ayubu alijikuta akijisemea moyoni na kukwepesha macho yake ambayo safari ile yalikutana na macho ya mama yule.

Moyo wake ulimpasuka pale aliposikia sauti ya mama Asha ikimuita kutokea pale kwenye zile ngazi.

“Baba…” mama Asha aliita.

Ayubu akajifanya hakusikia sauti ile iliyosikika kwa chini mno kutokea puani utafikiri mtu aliyeitoa alikuwa ni mgonjwa wa mafua.

“Baba mfuaji” mama Asha akaita tena

“Naam mama” Ayubu alishituka na kuinua shingo lakini alitazama pembeni kwani hakuweza kumtazama mama yule kutokana na pozi lake la kihasara alilokuwa amekaa.

“Vipi una tatizo?” Alihoji mama Asha kwa upole.

“Hapana mama, kwani Vipi?” Ayubu alihoji pasipo kumtazama.

“Basi kama huna tatizo, endelea na kazi” alisema mama Asha huku akijiinua na kuelekea ndani.

Mwanamke yule alifahamu wazi kuwa Ayubu angeuona mzigo aliokuwa amebarikiwa huko uwani. Akazidisha manjonjorinjo pale alipotembea kuingia ndani, vurugu za mizigo ilikuwa kubwa kuliko wakati alipokuwa anaingia msalani. Safari hii kulikuwa na mitetemo isiyo ya kawaida iliyosababisha maporomoko ya milima na mabonde. Ayubu akajikuta akimeza funda la mate huku suruali aliyokuwa ameivaa ikiongezeka ukubwa hasa maeneo ya kati.

“Ee Mungu nisaidie nimpate haraka Suzy wangu nirudi Bonde. Hii Bongo imeshanishinda jamani” Alijisemea Ayubu kimoyomoyo huku akiinama kuendelea na udobi. Lakini kitendo kile kilikuwa likijirudia akilini mwake.

Wakati akitafakari mambo yale yaliyofanywa na mama Asha, mama Mwenye nyumba alitoka na kusimama mlangoni. Alisimama kwa kitambo akimtazama Ayubu ambaye alikuwa amejikita kwenye kusugua nguo pamoja na kwamba mawazo yake yalikuwa kwa mama Asha.

“Ayubu…” Aliita mama mwenye nyumba kwa sauti ya chini. Ayubu aliwacha kufua na kugeuka kuangalia huko sauti ilipokuwa inatokea.

“Naam mama” Ayubu akaitika baada ya kubaini kuwa aliyekuwa anamuita alikuwa ni Mama mwenye nyumba wake..

“Nakuomba mara moja” alizungumza Mama mwenye nyumba na kuingia ndani.

Ayubu akawa ameduwaa asielewe sababu ya kuitwa na mama mwenye nyumba wake. Aliacha kufua na kwenda kumsikiliza Mama yule aliyezoeleka kwa jina la BI Sada, alipofika kwenye mlango wa chumba cha mama yule akagonga mlango. Hata hivyo Bi Sada hakutoka na badala yake akasikia akimuita na kumwambia aingie ndani. Kwa tahadhari kubwa Ayubu alisukuma mlango wa chumba kile cha Bi Sada na kuingia ndani.

Mnh! Aliyoyakuta chumbani mle mwa Bi Sada, Ayubu hakuweza kuamini macho yake.



Bi sada alikuwa amejilaza kitandani akiwa amejizunguushia taulo tu kifuani ambalo lilishindwa kufunika magoti yake.

“Naam mama.”

“Mbona unaogopa ingia tu baba” alisema Bi Sada huku akitawanya miguu yake na kusababisha taulo kushindwa kukutana katikati hivyo kuruhusu zaidi mapaja yake yaliyokuwa yakimeremeta kutokana na kupakwa mafuta mengi kuwa wazi.

Ayubu alikwenda kuketi kwenye stuli huku macho yake yakiwa chini akihofia kumtazama mwanamke yule aliyekuwa akimheshimu kama mzazi wake wa kumzaa.

“Naamini utaweza kunisaidia Ayubu” alisema Bi Sada kwa sauti iliyokuwa ya kubembeleza.

Ingawa Ayubu alikuwa bado katika hali ya woga iliyokuwa imechanganyikana na mshangao lakini alikuwa amekwisha haribikiwa. Lile pozi alilokuwa amemkuta nalo Bi Sada liliharibu ushirikiano wa ubongo wake na mishipa ya damu. Ukichanganya na vile vituko alivyofanyiwa na mama Asha kule nje, ndio akazidi kuwa katika hali mbaya kijana wa watu.

“Kitu gani mama?” Ayubu akajifanya kuzuga huku mapigo ya moyo wake yakiandamana kwa kasi.

“Njoo uone” Alisema Bi Sada huku akizidi kujifunua paja lake la kushoto pale alipokuwa amejilaza.

Ayubu akazidi kushangazwa na vitendo vya mama mwenye nyumba wake. Pamoja na kwamba mwanamke yule alikuwa ni mtu mzima lakini kwa jinsi alivyobarikiwa utasema alikuwa na miaka ishirini na mbili kushuka chini.

“Usiogope Ayubu we njoo” Bi Sada alisisitiza.

“Naam!” Ayubu akajikuta akishindwa kusimama kutokana na hali halisi ya msumari wa bati kukaa vibaya.

Bi Sada alikwisha shitukia hali ile ya Ayubu kutokana na macho yake kupoteza uwezo wake wa kuangali na sauti kuwa nzito zaidi. Mwanamke yule akawa anamtizama Yasini huku akiachia tabasamu la matumaini.

Ayubu alijiinua kwa taabu kutoka pale kwenye stuli na kutembea huku akiwa amejipinda mgongo utafikiri alikuwa ni kibabu cha miaka tisini. Alishindwa kunyooka sawasawa kwa kuhofia kushitukiwa na Bi Sada. Hakuelewa kama mwenzake tayari alikuwa ameshasoma mchezo mzima tangu mapema.

Ayubu alikwenda kuketi kwenye kitanda alichokuwa amelalia mama yule. Pembeni na pale alipokuwa amejilaza Mama mwenye nyumba kulikuwa na bakuli lililokuwa na maji pamoja na kitambaa kidogo.

“Mwangu nimeng’atwa na mdudu hapa, nilikuwa naomba unikande” alisema mama mwenye nyumba huku akimuonesha Ayubu sehemu ya paja lake. Kiukweli hapakuwa na dalili yoyote ile ya kung’atwa hata na nzi.

“Mbona hakuna kitu mama!” Ayubu alizungumza kwa mshangao huku ametumbua jicho kwenye paja la mama mwenye nyumba wake.

“Ukipaona huwezi kugundua, hebu paguse” alisema Bi Sada kwa msisitizo.

Ayubu akapeleka mkono wake taratiibu hadi juu ya paja la mwanamama yule na kulibonyeza bonyeza kuweza kutafuta sehemu aliyokuwa akiizungumzia Bi Sada.

“Asssccss….aaa…Asante mwan…hapo hapo…Ooh tamuu” Bi Sada alitoa sauti ambayo ilipenya vyema kwenye masikio ya Ayubu na kusafiri hadi kwenye moyo wake na kuweka kambi. Mwili wake ukasisimka kama vile alikuwa amemwagiwa maji ya barafu hasa pale mkono wake ulipotua juu ya paja la Mama mwenye nyumba wake na kusikia sauti za ajabu ajabu kutoka kwa mtu mzima yule.

Pasipo kuzungumza neno lolote Ayubu alisogeza bakuli lililokuwa na yale maji na kuchovya kile kitambaa. Alikipeleka kwenye paja la mama yule na Bi Sada akaanza kutoa miguno ya chumbani iliyozidi kumtibua Ayubu mtoto wawatu wa mzee Nyiruka kule Tanga.

Pepo la mahaba likaanza kumuingia taratiibu kijana wawatu, na pepo lile lilipomzidi Ayubu akabadilikana kuwa kama amechanyangikiwa. Hakuwa anajitambua tena masikini ya Mungu, na hata kile kilichokuwa kimempeleka jijini Dar hakuwa anakikumbuka tena.

Kijana yule ambaye alikuwa kama vile amepandisha mapepo, alisogeza pembeni bakuli la maji na kuinamisha shingo yake hadi pale kwenye paja la Bi Sana na kuanza kumkanda mama wa watu kwa kutumia ulimi wake alioutoa kiustadi na kuwa mrefu kama ulimi wa ng’ombe.

Sijui mwenzetu Ayubu alisomea shule gani ile staili yake ya ukandaji, maana duh! mi naona mauzauza tu hata sielewi, labda ndugu msomaji mwenzangu unaelewa elewa angalau kidogo. Anywayhayatuhusu, ya Mwandishi tumpe Mwandishi na ya Ayubu tumuachie Ayubu, ngoja sisi tuendelee na simulizi yetu.

Kitendo kile alichokifanya Ayubu kilionekana kumchanganya sana Bi Sada kiasi cha kupelekea kugalagala na kusababisha taulo alilokuwa amejifunga kifuani kufunguka.

Ayubu aliweza kuyaona madafu ya Bi Sada yaliyokuwa na umbo la mduara yalivyotuna kisawasawa na kugoma kulala kifuani. Kijana akajikuta akishindwa kufanya kazi aliyopewa na mama mwenye nyumba wake na badala yake kuhamia kifuani. Akatumia vidole na ulimi wake kucheza na madafu ya Bi Sada.

Lile jini mahaba lilikuwa limekwisha tawala vya kutosha mle chumbani mwa mama mwenye nyumba. Hakuna aliyesubiri maelekezo juu ya kitu cha kufanya kutoka kwa mwenzie, bali kila mmoja alijituma ipasavyo. Ndani ya dakika kadha kila mmoja alikuwa amepindukia kivyake akitawaliwa na uchovu.

“Yaani kijana wewe mbali na uzuri uliokuwa nao, hata mambo pia unayaweza!” alisema Bi Sada akiwa amelala juu ya kifua cha mvulana ambaye alikuwa na umri kama wa mtoto wake.

Ayubu hakujibu kitu zaidi ya kumsukuma Bi Sada pembeni na kujiinua kutoka pale kitandani. Hakuelewa ni kitu gani kilikuwa kimemtokea chumbani mle hadi kufikia hatua ya kutenda ufirauni ule na mwanamke ambaye alikuwa na umri sawa kabisa na mama yake mama Ayubu kule kijijini.

Wakati akiendelea kujutia kitendo kile akajiwa na wazo lililokuwa limemfanya arudi tena jijini Dar. Alitoka nje huku Bi Sada akibakia amelala kitandani akiwa hoi bin taaban na roho yake nyeupee kwa furaha ya kufanikiwa kumtega na kumnasa mtoto wa mwanamke mwenzie.

*****

Maisha ya Suzy pale nyumbani kwa Naima yalibadilika na kuwa magumu zaidi. Naima alisitisha msaada aliokuwa akiutoa kwa Suzy kama ambavyo alimuahidi. Hata hivyo pamoja na Naima kusitisha huduma kwa Suzy lakini alionesha ubinadamu kwa kumpatia kamtaji kadogo ka kuuza samaki wa kukaanga. Biashara hiyo ndiyo pekee aliyokuwa akiitegemea Suzy ingawa kwa kiasi Fulani nayo ilianza kuyumba. Hata hivyo Suzy alijipa moyo na kuapa kutofanya vile alivyokuwa akilazimishwa na rafiki yake kufanya, yaani kutoa mimba na kuingia kwenye biashara ya kuuza mwili.

Jioni moja kama ilivyokuwa kawaida yake Suzy alikwenda Ubungo kufanya biashara yake ya samaki. Ilimbidi kufanya biashara hiyo mchana na usiku ili kujaribu kutetea mtaji wake uliokuwa ukielekea kuporomoka.

Suzy Akiwa katikati ya wauza samaki wengine ghafla walitokea mgambo wa jioni na kuwavamia. Kwakuwa hakuna aliyekuwa tayari kukamatwa, wote wakajikuta wakitimua mbio. Wengi wao walikimbia na kuziacha biashara zao. Suzy naye alitimua na kuacha sinia lake la samaki pamoja na pesa ambazo alikuwa amekwisha uza siku hiyo. Askari wale walikusanya bidhaa zote pamoja na pesa zilizoachwa na kuondoka nazo.

Suzy aliporejea nyumbani alimkuta Naima akijiandaa kwa kutoka kuelekea kwenye biashara yake ya kudanga. Suzy akajitupa kwenye kochi na kuanza kulia kwa sauti. Naima akatoka chumbani na kusimama karibu na Suzy akimshangaa huku mikono yake akiwa ameiweka kiunoni.

“Haya mama masamaki imekuaje tena, Baba kijacho amekufa?” alihoji Naima kwa kebehi.

“Mkosi gani huu jamani?” alisema Suzy huku akiendelea kulia.

“He unamkosi shoga! Basi kaoge maji ya bahari” alisema Naima huku akipiganisha viganja vya mikono yake kuonesha hali ya mshangao.

“Usiseme hivyo Naima. Mwenzio nimepata matatizo”

“Sema basi tatizo lako. Sasa unalia mi nitajuaje?” alisema Naima kwa nyodo

“Mgambo….” Alijaribu kuzungumza lakini akajikuta akishindwa kumalizia na kuendelea kulia.

“He! Sasa mgambo we anakuhusu nini hadi ulie. Wacha ujinga bwana Suzy” Naima alizidi kumdhihaki rafiki yake.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG