Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

MESSAGE YA FUNDI UMEME - 2

   


Chombezo : Message Ya Fundi Umeme 

Sehemu Ya Pili (2)


“Yaani mimi niwe na wanaume wawili?” nikahoji kwa mshangao.

“Tatizo liko wapi? Umeona wapi figa moja likainjikwa chungu?”

“Hapana Fatuma hilo haliwezekani” Nilimkatalia Fatuma juu ya lile swala lake. Kiukweli haikuniingia akilini hata kidogo, heti mwanamke mmoja umiliki wanaume zaidi ya mmoja. Si unaona hata wewe ndugu msomaji unashangaa. Sasa hivyo ndivyo nilivyokuwa nikishawishiwa na yule rafiki yangu Fatuma.

“Kama haiwezekani basi usilielie hapa. Fweee! fweee! fweee! fwee!” Fatuma alizungumza huku akiniiga kwa kuning’ong’a jinsi nilivyokuwa nikilia. Nikabaki nimejiinamia kama vile mwanamke aliye kuwa amefumaniwa na mume wa mtu.

Kimbelembele chote cha kutafuta mtu wa kunipa ushauri kwenye matatizo yangu kiliniisha. Ni afadhali ningejifungia ndani nikalia wee hadi hasira ziniishe kuliko kumtafuta mtu akushauri badala yake anakushauri utumbo.

Nilijikuta nikipata hamu ya kuzungumza na mume wangu ingawa alikuwa amenikera. Ningefanyaje sasa wakati ndo nilikuwa nimekwisha penda. Sikuwa tayari kabisa kuona naingia kwenye mtego wa kuisaliti ndoa yangu.

Nilitoa simu yangu ambayo muda wote nilikuwa nimeiweka kwenye pochi nikaiwasha. Haikupita hata dakika moja simu yangu ikaita. Moyo ulinipasuka kwa kuhisi ni mume wangu. Nilipoangalia nikagundua kuwa namba iliyokuwa ikipiga ilikuwa ngeni kwasababu haikutoa jina.

“Halloo” Sauti ya kike ilisikika baada ya kuipokea simu ile.

“Halloo, habari za saa hizi?” nikasalimia huku nikiwa simfahamu mtu aliyenipigia simu ile.

“Salama” mtu yule aliyekuwa amenipigia simu aliitika.

“Nazungumza na nani mwenzangu?” Nilihoji kwa sauti iliyokuwa imejaa upole na upendo ingawa mpigaji nilikuwa simfahamu.

“Sio lazima kunifahamu, ongea na mumeo huyu hapa” Ile sauti iliniambia. Nikaiwacha ile simu sikioni ili kusikia hiyo sauti ya mtu niliyeambiwa kuwa ni mume wangu.

“Hallo Priscaria, mkewangu” Ni kweli ilikuwa ni sauti ya mume wangu Magesa. Nikajikuta nikipatwa na kigugumizi kiasi cha kushindwa kuzungumza neno lolote lile. Nilikuwa kama vile mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Kile kidonda changu cha kusalitiwa ambacho kilipungua maumivu kidogo kutokana na maneno ya Fatuma aliyokuwa akinishauri.

“Haloo….halooo……halooo….” Nilimsikia Magesa alivyokuwa akiniita lakini pasipo na jibu lolote kutoka kwangu.

Nilicho kifanya ni kukata simu na kuizima kisha nika angua kilio kwa mara nyingine mle chumbani mwa Fatuma. Safari hii Fatuma hakunisogelea kama awali kunibembeleza, bali aliketi kwenye kona ya kitanda na kunitazama kama vile video. Nikainua shingo na kumtizama huku nikiendelea kububujikwa na machozi utafikiri bomba la serikali.

“Kwanini amekuwa hivi? jamani mume wangu, kweli?” Nilizungumza kwa uchungu mkubwa ndani ya moyo wangu huku nikijaribu kunyamaza kulia.

“Enhe, amekufanya nini tena?” Alihoji Fatuma kwa shauku ya kishankupe.

“Anampa simu wanamke wake anipigie, inamaana yeye hana simu?”

“Kawaida hiyo mama. Unadhani kama ungekuwa na kidumu chako saa hizi ungekuwa unawaza hivyo?” Fatuma alizungumza maneno yake ambayo kwa mbali yalianza kuniingia akilini.

“Na bado, huwo ni mwanzo tu. Subiri kazi yeneyewe inakuja” Fatuma alizungumza huku akitembea kuelekea kwenye meza ambayo juu yake kulikuwa na simu yake ikiita. Alipomaliza kuzungumza na simu yake akanigeukia pale kitandani.

“Shoga wajanja wakikumegea, nawe tafuta mnyonge ummegee” Fatuma alizungumza na kuzidi kusogea hadi pale kwenye kitanda kisha akaketi karibu kabisa na nilipokuwa nimeketi mimi.

****

Kilikuwa ni kitu cha kushangaza sana kwa Magesa. Alitumia muda mwingi sana kunitafuta kwenye simu lakini sikupatikana. Alipojaribu kunitafuta kwa kutumia simu ya yule abiria mwenzie Yusrah simu iliita. Ilipokatika alijaribu kunitafuta kwenye simu yake lakini simu haikupatikana tena. Ingawa hakuwa amefanya kazi yoyote ngumu lakini alikuwa mechoka kuliko kawaida kwa tukio lile.

“Pole sana Frank” Yusrah alimuonea huruma mume wangu.

“Kwa kweli nashangaa sana, mambo haya siyo kawaida kabisa” alizungumza Magesa.

“Au ulipoondoka nyumbani ulikuwa umemuudhi”

“Mnh! sidhani, mbona amenisindikiza hadi Ubungo lakini hakusema”

“Ah! sisi wanawake tuna tofautiana bwa. mwengine hata umfanyie kosa gani hawezi kuzungumza. Sanasana utaona matendo tu yanabadilika. Nahisi na mke wako naye pia yupo hivyo” Yusrah alizungumza ukweli utafikiri alikuwa akinifahamu mwanzo hadi mwisho. kiukweli sikuwa muongeaji pale ninapo kosewa na mume wangu. Tabia yangu ilikuwa ni kwenda kuomba ushauri kwa watu wengine wa nje. Magesa aliposikia yale akahisi pengine ni kweli kulikuwa na ukweli ambao nilikuwa nimeuficha ndani ya moyo wangu.

“Inawezekana unayosema yana ukweli”

“Kwahiyo mkeo naye yupo hivyo?”

“Kabisa, yaani hata nifanye kosa gani haniulizi”

“Huyo mtu ni hatari sana. Ni afadhali uongee naye abadilike vinginevyo mtaishia pabaya” Yusrah alizungumza maneno ambayo yaliniingia ndani ya moyo wangu. Ukweli ni kwamba mara nyingi sana mume wangu alikuwa akinipigia kelele nibadilike lakini sikutaka kumuelewa.




“Mke wangu hawezi kubadilika tena” alisema Magesa

“Kwanini asibadilike? chuma tu unaweza ukakibadilisha na kukiweka unavyo take, atakuwa yeye binadamu”

“Yusrah wewe unaongea tu kwasababu humjui mke wangu”

“Huyo anabadilika bwanaaa, sema mimi nikuambie dawa yake”

“Dah nikimbadilisha mke wangu nitafurahi sana. Niambie hiyo dawa”

“Upo tayari kumbadilisha mkeo?”

“Kabisaaa. Unajua nampenda sana mke wangu?”

“Kama kweli unampenda, basi mtafutie Kidosho”

“Kinapatikana wapi hicho,na kinauzwaje?” Magesa akahoji kwa hamasa kubwa ya kuja kunitibu. Yusrah akaangua kicheko ambacho kilimfanya mume wangu kuduwaa na kumkodolea macho.

“Vipi sasa mbona unacheka?” Magesa akamkatisha kwa kumtandika swali.

“Dah! wacha nicheke mwenzangu, unanichekesha” alizungumza Yusra huku akifuta machozi yaliyokuwa yametokana na kile kicheko chake.

“Sasa kuuliza bei ya Kidosho ndio unanicheka?” Magesa alizungumza huku akitabasamu kutokana na kile kicheko cha Yusra.

“Nipe namba yako ya simu mimi nitakutafutia” Yusrah alizungumza huku akimalizia kicheko chake.

Magesa hakuwa na ujanja wa kumnyima Yusrah namba yake ya simu. Amnyime wakati alikuwa na lengo la kunitibia mimi mke wake? Alitamani sana kuniona ni mwanamke muwazi hasa pale anapokuwa amenikosea. Hakupendezwa na tabia yangu ya kumezea machungu mwenyewe pasipo kumshirikisha.

“Basi ukikipata tu naomba unishitue muda wowote ule”

“Hivi kweli Frank hujui maana ya kidosho au unanitega tu?” Yusra alihoji huku akitabasamu.

“Nielekeze basi nikakitafute mwenyewe” Alisema Magesa kwa msisitizo huku akimkodolea macho Yusra.

“Bwana wee, Kidosho ni Kimada” Yusrah alizungumza pasipo na hata chembe ya wasiwasi na macho yake yakiwa makavu kabisa.

Maneno yale ya Yusra yalimshitua sana mume wangu, hakuweza kuamini kama muda wote ule msichana yule alikuwa akizungumzia habari za kumiliki vimada, yaani michepuko. Akatikisa kichwa kidogo kuonesha masikitiko juu ya taarifa ile.

“Hakuna ambacho nakikosa kutoka kwa mke wangu” akazunguza kwa msisitizo na kujiamini.

“Una uhakika?”

“Kwa asilimia mia mia nane”

“Vipi kuhusu ukweli na uwazi wake kwa mambo unayomkera?” Yusra akahoji huku akifumba kidogo macho yake kuashiria uzito wa swali lake.

“Hilo sio tatizo, na ndiyo maana unaniona hadi leo hii nipo naye. Nampenda sana Priscaria wangu” Magesa akaeleza kwa msisitizo na kujiamini.

“Ahaa, sasa mateso yote haya ya kuzimiwa simu unayapata kwasababu unajifanya tatizo hulioni” Kile kisichana kilizungumza maneno ambayo yalimgusa mume wangu. Hata hivyo Magesa hakumjibu kitu chochote na kuwa kama vile alikuwa hamsikii.

Sauti ya mlio wa meseji wa simu ya Magesa ulimfanya achukue simu yake na kuitazama. Jina la FUNDI UMEME lilikuwa limejitokeza kwenye kioo kuonesha kuwa meseji ile ilikuwa imetumwa na huyo Fundi umeme. Alipoifungua akakuta ujumbe huu.

“SAMAHANI SANA NIMEKUTUMIA MESEJI AMBAYO SIYO YAKO” Hivyo ndivyo ujumbe ule ulivyo someka. Magesa akashangaa kwasababu hakuiona meseji yoyote ambayo iliingia kutoka kwenye ile namba siku za karibuni. Alichofanya ni kujaribu kupitia meseji zilizokuwemo kwenye kiboksi cha kuhifadhia ujumbe mfupi wa maandishi. Alisoma sana lakini hakuiona hiyo meseji iliyokuwa imetumwa kwa namba ile.

“Msg gani fundi?” Magesa akahoji kwa ujumbe mfupi wa maneno.

“Niliyo ku2mia leo asubuhi” meseji ya fundi umeme ilijibu.

“Siikumbuki, labda unitumie nipate kukumbuka” Magesa aliandika na kutuma tena.

“Kama hukuiona bac ni vizuri. Cku njema” Ilisomeka meseji ya Fundi umeme.

“Ok, kazi njema”

“Poa, U 2” Meseji ya fundi umeme ilihitimisha mazungumzo yao yaliyo fanyika kwa kuchati kwa ujumbe mfupi wa simu”

****

Zilikuwa zimepita siku mbili tangu Magesa alipo safari kwenda mkoani Arusha kikazi kama mwenyewe alivyodai, sijui kama ni kweli au alikuwa kwa Fundi umeme wake. Potelea mabli.

Maumivu ya kusalitiwa yalikuwa yameuvunja vunja mwili wangu. Viungo vya mwili vilikuwa vikininyong’onyea kiasi cha kushindwa kufanya kitu chochote kile. Kutokana na hali niliyo kuwa nayo nilishindwa hata kupika chakula changu mwenyewe. Mambo makubwa ambayo nilikuwa nayamudu kwa wakati huo yalikuwa ni kulala na kulia tu baasi.

Njaa nayo ni mwanaharamu pamoja na maumivu yote yale niliyokuwa nayo lakini bado haikunionea huruma, ilinikaba kiasi cha kupelekea nihisi kufa kufa tu. Ikabidi nijiinue mtoto wa kike na kutoka nje ili kuweza kupata chochote kitu cha kutia mdomoni.

Niliwaza na kuwazua juu ya kitu ambacho ningekula angalau kidogo tu ili nisije nikapoteza uhai wangu bure na kumuaha Magea amilikiwe na Fundi umeme wake. Nilimshukuru Mungu kwa kunipa wazo la kwenda kununua chipsi kuku. Ilibdi nitafute kile chakula ambacho nilikuwa nakipendelea sana.

Mnh! Ndugu msomaji huwezi kuamini, nilishindwa kabisa kula chipsi zile. Pamoja na kwamba ni chakula ambacho nilikuwa nikikipenda kuliko maelezo lakini siku hiyo zilinishinda. Nilijitahidi kujaza vipande vya chipsi mdomoni mwangu lakini niliishia kuzitafuna tu kwa muda mrefu na kushindwa kuzimeza. Matokeo yake nikajikuta nikila vipande viwili tu vya viazi kisha nikahisi kushiba. Yaani nilikuwa nahisi kama vile natafuna maganda ya magimbi mabichi. Nikasukuma sahani ya Chipsi pembeni na kwenda zangu kulala.

Niligala gala kitandani kwa muda mrefu lakini usingizi nao ukagoma kuja. Kitanda nilikiona kama vile kimejaa miba ya mchongoma kiasi cha kupelekea kuamua kuketi kitako. Niliwasha runinga yangu kuangalia vipindi vya muziki ili nipoteze mawazo, lakini nikahisi miziki nayo ikiniboa hasa ile ya mapenzi ambayo nilikuwa nikiipenda siku zote kuitazama.

Nilizima runinga na kuchukua kitabu kidogo cha simulizi ya BONGO DASLAAM kilicho andikwa na KIZARO MEDIA COMPANY na kuanza kukisoma. Angalau nilijikuta nikipata ahuweni ingawa na chenyewe kikanishinda kwasababu mambo yaliyokuwemo mle yalikuwa ya kimapanzi jambo ambalo lilinifanya nimkumbuke Magesa mwanaume mbwa! aliyenipotezea amani ya moyowangu na kunisababishia mateso ya nafsi.

Nilikwenda bafuni kujimwagia maji Kisha nikarejea na kukaa kwenye kioo cha dressing table. Nilipoiona sura yangu nikajikuta roho ikiniuma zaidi na kushindwa kuzuia machozi kububujika kwenye mashavu yangu. Urembo niliokuwa nao niliuona kumbe haukuwa wa kupitiliza kiasi cha kumfanya mwanaume kuto nisaliti. Nilijaribu kuvuta taswira ya huyo Fundi umeme aliye nipora penzi langu jinsi alivyo mrembo. Kumbe kuringa kote kule walikuwepo warembo ambao wamenizidi? Ndio! kama mimi ningekuwa mrembo mume wangu asinge thubutu kutoka nje ya ndoa.

“Ee Mungu mlaani huyo Fundi umeme” nilizungumza wakati naendelea kujiangalia kwenye kioo.

Huwa nilikuwa nasikiaga tu kwa watu wakisema kuwa mume anauma, kumbe ndivyo vile? Ama kweli mume ni kidonda, tena donda ndugu.

“Hivi kama ningekuwa ni mimi ndio nimefanya ule utumbo wake halafu yeye akaikuta meseji kama ile kwenye simu yangu, ingekuwaje? Saa hizi si angekuwa ameshaniua na kunipa taraka niende nayo kuzimu!” nilizungumza mwenyewe nikiwa plae kwenye dressing table.

“Wanaume bwana, wanaume ni watu wabaya sana. Sijui hata kwanini Mwenyezi Mungu amewaleta hapa duniani. Nafikiri kama tungekuwa tunaishi wanawake watupu sidhani kama kuna mtu angekuwa anasononeka na kulia kama mimi leo hii” niliendelea kuwaza hili na lile ndani ya nafsi yangu.

Nikiwa naendelea kuwaza na kuwazua nikakumbuka kuwa nilikuwa na ahadi ya kukutana na Fatuma. Nilijipa moyo na kufungua kabati la nguo. Moja kwa moja macho yangu yalitua kwenye pedo moja kali sana nyeupe na blauzi nyekundu. Nilizitoa na kuanza kuzinyoosha kwa pasi huku moyoni nikiwa bado nina duku duku na kitendo alicho kifanya mume wangu Magesa.

Kitu ambacho kilikuwa kikiniuma zaidi ni kwamba nguo zile nilizokuwa nazinyoosha, zilikuwa zimenunuliwa na mume wangu Magesa. Hivyo zikanifanya nimkumbuke mwanaume yule Baradhuli. Niliwacha kupiga pasi na kuzikunja kunja kwa hasira kisha nikazitupa chini kwa hasira.

Nilizitazama zile nguo kwa sekunde kadhaa kisha nikajongea taratiibu na kuziokota. Nilizitazama vizuri kisha nikaachi msonyo wa hasira na kuziweka mezani kwaajili ya kuendelea kupiga pasi. Ndio! Niliziokota kwasababu zilikuwa ni nguo ambazo nilikuwa nazikubali sana. Ni nguo ambazo kila nilipokuwa nikizivaa nilijihisi kuwa huru. Kwahiyo nilitupilia mbali mtu ambaye alikuwa amezinunua na kuendelea na maandalizi ya kukutana na shost yangu Fatuma.

Nilivaa zile nguo na kwenda kusimama kwenye kioo. Pedo ilikuwa imenikaa kisawasawa kiasi cha kuruhusu hipsi zangu zilizotanuka vizuri kuonekana zenye mvuto zaidi ya ulivyonizoea kunifikiria ndugu msomaji. Mzigo wangu wa madafu kule nyuma nao ulijitahidi kunifanya nivutie zaidi. Mguu wangu wa bia uliokuwa na ngozi nyororo ulionekana vizuri hasa kutokana na rangi nyeupe ya ngozi yangu.

Blauzi yangu nyekundu iliyokuwa na mikono mifupi ilikuwa imenikaa vyema. Sidiria yangu nyeupe ambayo ilikuwa imekumbatia vyema madafu yangu ya kifuani yaliyokuwa yametuna kama vichuguu vyamchwa, iliweza kuonekana kupitia kwenye kitambaa laini cha blauzi ile. Shingoni nikaning’iniza kitambaa cheupe kilichoendana na rangi ya pedo yangu. Nilijigeuza geuza kujithanimisha kama kweli nilikuwa nimependeza, “Shenzi watakoma wenyewe!” nilijikuta nikizungumza mwenyewe.

Nilikwenda kwenye dressing table na kuanza kujikwatua maeneo ya mapokezi (usoni). Nilitumia kila aina ya kipodozi nilicho kipenda mimi ambacho kilikuwepo kwenye dressing table yangu. Kioo nacho hakikuwa nyuma kunisifia kwamba hapo umependeza, hapo huja pendeza paka kipodozi kingine. Jamani nyie mwenzenu nilikuwa mrembo! hata sijui ni kwanini mume wangu Magesa aliamua kutoka nje ya ndoa. Nikakumbuka maneno ya shemeji Hashimu kuwa wanaume ni kama mbwa, ukimpa mfupa anaukimbilia na ukimrushia mwingine anaukimbilia na kuuwacha ule wa awali hata kama umenona kiasi gani. Hivyo ni kawaida yao kusaliti wapenzi wao hata kama ni warembo kiasi gani.

Nilipokuwa nikiendelea na kujipara na kujikwatua nilisikia sauti ya malango wangu ukigogwa. Nilikwenda kuufungua na kumkuta Fatuma amesimama mlangoni huku na yeye akiwa amependeza mno.

“Waao! Shoga umependeza!” Nilimsifia Fatuma na kumkumbatia.

“Asante Shost, Na wewe umependeza pia” Fatuma naye alizungumza huku akinitazama kuanzia chini na kunipandish hadi juu huku akiachia tabasamu la furaha,

“Ahsante mwaego. Niambie Shoga” nilimsabahi huku nikifunga mlango baada ya Fatuma kuingia.

“Hapa hakuna jipya shost, Paka akiondoka.......” Fatuma alisema.

“Panya hutawala” Nilimalizia ile methali ya Fatuma.

Kwa kiasi fulani nilijikuta nikipata faraja ndani ya moyo wangu baada ya kutembelewa na mgeni yule. Jamani nyie acheni tu, kusalitiwa sio kitu cha mchezo hasa awe mtu unayempenda na kumuamini. Unaweza ukajiona kama vile takataka isiyo na thamani mbele ya macho ya binadamu wenzio.

“Usitake kuniambia bado haujamaliza kujipara?” Fatuma aliniuliza baada ya kuniona nikiendelea kijikwatua.

“Namalizia shoga,au hutaki na mimi nipendeze?” nilizungumza huku nikijipaka wanja kwa umakini mkubwa.

“Mnh! unataka uweje? hapo ulipo umesha pendeza”

“Usiwe na papara shoga, kaa hapo unisubiri” nikamwambia shoga yangu yule.

“Haya mrembo endelea kujipara” Alisema Fatuma na kusogea kwenye kioo cha kabati kujitazama. Alijigeuza geuza na kujiweka mapozi mbali mbali kama vile alikuwa anapigwa picha.

“Kwakweli shoga kuna umuhimu wa kutoka. Maana akili yangu inahitaji kupata faraja na kupumzika kuwaza waza watu washenzi” Nilizungumza huku nikichana nywele zangu kuelekea nyuma.

“Habari ndiyo hiyo”

“Kwahiyo tunakwenda wapi sasa?”

“Landmark Hotel”

“Na wewe shoga, inamaana hujaona mahali pengine pazuri zaidi?”

“Inabidi twende pale kwasababu nina appointment na mtu”

“Nani? shemu Hashimu nini?”

“Hakuna cha Hashimu wala nini!”

“Kumbe nani?”

“Nina kidumu changu mwenzangu kinachonifariji” alizungumza Fatuma huku akijitingishwa kwa kujishebedua.

“He he heee! Kwa raha zako mtoto wa kike!” Nilicheka kinafki huku moyoni mwangu nikiliona jambo lile halikuwa la kawaida.

Nilikuwa naona kabisa rafiki yangu Fatuma akimfanyia ushenzi shemeji Hashimu. Kumbe mwanamke yule alikuwa anamaanisha kwa ule ushauri aliokuwa akinipatia. Sasa mbona siku zote nilizoishi na rafiki yangu yule sikuwahi kutambua tabia yake ile ya ufirauni? Nilijiuliza pasipo kuwa na majibu. Ama kweli moyo wa mtu ni msitu mnene. Nilizungumza huku nikimalizia kujikwatua.

****

Kama tulivyo panga jioni siku ile tulichukua Tax na kuelekea moja kwa moja Landmark ambako Fatuma alikuwa na appointment na mwanamuziki mmoja wa bendi ya Sikinde. Tulipofika tukawakuta vijana wawili kwenye meza moja iliyokuwepo kwenye kona. Tulikwenda na kujiunga nao. Mmoja kati ya wale vijana alikuwa ni yule kaka mwenye apointment na Fatuma. Yule mwengine alikuwa ni rafiki yake.

“Waaaao! Karibuni warembo” Alisema yule jamaa aliyekuwa na appointment na Fantuma huku akitusogezea viti vilivyo kuwepo kwenye meza ile.

“Thanks wangu, tumekwisha karibia” Fatuma alijibu kwa sauti fulani hivi ya kudeka ambayo haikuwa ya kwake. Jamaa yule nikamuona akinikodolea macho utafikiri alikuwa ameona kitu fulani cha ajabu.

Nilijisikia aibu kutokana na mwanaume yule kunitumbulia macho. Mimacho yenyewe ilikuwa mibayaaa! Mekunduuu kwa kunywa pombe kali. Kumbe kitendo kile hata rafiki yangu Fatuma alikuwa amekishitukia kiasi cha kutilia mashaka usalama wa penzi lake na mwanaume yule.



“He! we vipi?” Fatuma alimwambia mwanaume wake huku akimshika kidevu jamaa yule na kumrudisha amuangalie yeye. Jamaa akabakia akijichekesha chekesha huku akimpiga busu la shavu Fatuma.

“She is so cute” (Ni mrembo mwenye mvuto) Jamaa yule alizungumza huku akimgeukia rafiki yake ambaye walikuwa wameketi pamoja.

“Sure” (Hakika) Yule mwinziwe alimjibu huku akitabasamu.

“Karibu mrembo, jisikie huru” Jamaa alinikaribisha kwa bashasha. Alionekana kuwa mcheshi kuliko kawaida. Pasipo kujibu niliketi kwenye kiti na kutulia kimya mithili ya kuku wa kisasa. Jamaa alimsogelea Fatuma na kumwagia mvua ya mabusu mfurulizo. Baada ya hapo Fatuma alinigeukia na kunikonyeza nami nikamjibu kwa tabasamu la kubabatiza.

“Robart” Fatuma alimuita mpenzi wake kwa sauti yake ile ya bandia aliyokuwa akiitolea puani. Fatuma niliyekuwa namfahamu mimi alikuwa na lisauti moja hivi bayaaa! Lakini kwa jinsi alivyokuwa akijibebisha kwa jamaa utasema sauti si ndiyo hii bwana kumbe wizi mtupu.

“Yes mpenzi,” alizungumza mwanaume yule wa Fatuma huku akiwa ameweka mkono wake nyuma ya mgongo wa Fatuma.

“Huyu ni rafiki yangu, anaitwa Priscaria” Fatuma alinitambulisha kwa mijamaa ile.

“Ohooo! Priscaria huyooo! karibu sana bibie” Jamaa yule aliyeitwa Robart aliniambia kwa uchangamfu.

“Prica baby” Fatuma aliita huku akinigeukia.

“Abee” Niliitika kwa aibu na unyenyekevu wa kuigiza kama ambavyo Fatuma alikuwa akiigiza mbele ya mianaume ile.

“Huyu ndiye mpenzi wangu, ninayemzungumzia kila siku. Anaitwa Robert” Fatuma aliendelea na utambulisho huku akiumba na kuyaremba matamshi ya maneno aliyo kuwa akiyatamka.

“Ahaa Robert, nashukuru kukufahamu” Nilizungumza huku nikimtazama Robert kwa jicho la kumkata yaani nusu nusu.

“Huyu hapa anaitwaaaa….” Fatuma alitaka kumtambulisha yule kijana mwengine lakini alionekana kulisahau jina lake.

“Robinson” Yule kijana alidakia na kulitaja mwenyewe jina lake.

“Ahaa, Robinson na Robert” Niliyatamka majina ya wanaume wale kwa mbwembwe na mapozi utafikiri nilikuwa mgonjwa wa mafua.

“Yeah! kama mapacha vile” Fatuma alizungumza huku akitabasamu na kumshika ndevu Robert.

“Sio kama, ni mapacha” Alizungumza Robinson na kutufanya tuangue kicheko.

“Haya nashukuru kuwafahamu shemeji Robert and Mr. Robinson” nilizungumza huku nikijifanya nimejawa na aibu utafikiri nilikuwa kigori kumbe limke la mtu Fulani hivi mshenzi mshenzi.

“Ok, haya karibu, sijui unatumia kinywaji gani?” Alihoji Shemeji Robert huku akinitazama kwa macho yake ambayo yalionekana kuchangamka kutokana na pombe.

“Malta” Nilijibu pasipo kufikiria. Sikupata tabu ya kuwaza kinywaji kwasababu hicho ndicho kilikuwa kinywaji changu hata nilipokuwa nikitoka na mume wangu. Kwakweli namshukuru Mungu sikuwa mjwaji wa pombe. Na mume wangu alinipenda zaidi kwasababu ya tabia yangu hiyo ya kutokunywa pombe pamoja na kwamba rafiki yangu wa karibu Fatuma alikuwa ni mnywaji hodari.

“He! shem kwanini unywe malta?”

“Ndicho kinywaji changu Shem Robert” nilijibu huku nikitabasamu kwa aibu.

“Wacha masihara bwana” alisema Robert na kupaza sauti kumuita mhudumu. Alipofika yule mhudumu alimvuta na kumnong’oneza. Kisha mhudumu akaondoka na baada ya dakika kadhaa alirejea huku akiwa na tray lililokuwa na bia. Fatuma akanivuta kidogo kuninong’oneza kitu/

“Kunywa pombe shoga upoteze mawazo”

“Mwenzio sijawahi Fatuma”

“Usiwe na wasiwasi tupo wote”

“Nitajaribu nikishindwa naacha” nikazungumza kwa wasiwasi

“Mambo si hayo bwana” Fatuma alizungumza kwa furaha baada ya kunisikia kuwa nimekubali kujaribu kunywa bia.

Mhudumu alipofika alitufungulia chupa za bia mimi na Fatuma. Jamani nyie mtoto wa watu nilikuwa sijawahi kunywa pombe tangu nimezaliwa. Ukizingatia mume wangu alikuwa akipenda sana dini, hakuwahi kuniruhusu kunywa pombe hata siku moja.

Mwanamke nilijichanganya na wenzangu tukaendelea kupiga mtungi. Mwanzoni niliona uchungu kwenye ile bia, lakini nilivyoendelea kunywa nikajikuta nikiizoea na kuanza kuhisi utamu. Jamani nyie kuna vitu vya ajabu hapa duniani, yani bia ni chungu lakini baada ya kunywa nikaanza kuhisi utamu na kunoga. Kumbe walevi wanafaidi hivi? Nilijiuliza huku nikibugia maji yale yenye uchungu na utamu.

Hata hivyo nilijitahidi sana kunywa kwa tahadhari kwa kuhofia kuumbuka mtoto wa kike. Nilikuwa nawadharau sana wale watu waliokuwa wakidhalilika kutokana na kunywa pombe. Kitendo cha kuvua nguo, kulia bila ya sababu au kutukana hovyo hovyo ilikuwa ni jambo la kawaida kwa walevi wengi. Hivyo nikaogopa sana hali kama hiyo kunikuta mimi mke wa yule firauni msaliti mbwa mwitu Magesa.

Robert na Fatuma walikuwa wakinywa huku wakishikana shikana bila hata aibu kama ujuavyo kawaida ya wapenzi tena pombe zikiwa zimekolea kwenye bongozao.

Pasipo kutegemea na mimi nikajikuta nipo mikononi mwa Robinson yule rafiki wa Robert. Nilikuwa nimejilaza kwenye kifua cha Robinson huku nikijidekeza utafikiri nilikuwa kwenye kifua cha mume wangu Magesa. Nafikiri pombe ilikuwa ikijitahidi kufanya shughuli yake ipasavyo.

Mtoto wa kike nikajikuta nimesahau kabisa maumivu yote niliyokuwa nimesababishiwa na mume wangu Magesa. Robinson alicheza na mwili wangu vile alivyo kuwa anataka. Sikumuwekea kikwazo chochote pamoja na kwamba ningeweza kumzuia kwasababu sikuwa nimelewa nimelewa kupindukia.

Viumbe wa Mungu tuliendelea kula bata kwa kunywa pombe na nyama choma huku tukishikana na kuchezeana na wanaume wale hadi ilipofika mida ya saa nane za usiku. Nilikuwa nimejisahau kabisa kama mimi nilikuwa ni mke wa mtu. Nakwambia kama Magesa angejua huko aliko na Fundi umeme wake nafikiri angelia sana, na vile alivyokuwa na wivu mwanaume yule.

Robert na Fatuma walichukuana na kwenda kupumzika kwenye chumba cha kulala wageni. Mimi na Robinson tuliendelea kukata kilaji hadi ilipotimia mida ya saa tisa hivi za usiku.

“Kata kilaji mtoto mzuri, hapa hadi riamba” Robinson alizungumza kwa sauti ya kilevi huku akinipapasa kwenye mapaja yangu ambayo yalikuwa yamehifadhiwa kwenye ile pedo yangu nyeupe.

“No mpenzi, nahitaji kupumzika sasa” Nilizungumza kwa sauti kavu ambayo ilikuwa na pombe kwa mbali. Ni kweli nilikuwa nimelewa lakini niliweza kujitambua utafikiri nilikwisha wahi kulewa hapo nyuma. Nafikiri ni kwasababu niliamua kunywa pombe kwa kutegea kutokana na kuhofia kudhalilika mke wa mtu, Pamoja na kwamba mume wangu alikuwa ni msaliti lakini bado alikuwa ni mume wangu.

“Aaaah! Wewe, kunywa pombe kwanza. No kulala, No Usingizi” Robinson alizungumza huku akionekana kulewa chakari.

“Inatosha Robinson mimi nakwenda kulala” Nilizungumza huku nikijiinua na kupepesuka kutaka kuondoka.

“Basi mama, basi…basi usiondoke mrembo” Robinson alizungumza huku akijiinua kunifuata kwa kuyumba yumba na kunishika kiuno kisha hao tukaelekea kaunta ambako tulichukua funguo na kwenda chumbani kujipumzisha.

Sasa balaa lilianza pale tulipokuwa huko chumbani. Nikiwa nimejilaza kitandani, Robinson alifika na kuanza kunisaula viwalo vyangu huku yeye akiwa tayari amekwisha pambua na kubakiwa na nguo ndogo tu. Alifanikiwa kunivua blauzi yangu na kuniacha nikiwa na blazia. Nilimsikia akipumua kwa nguvu kama kiboko hukua akipeleka mkono wake wa kushoto kushika dafu langu moja la kifuani. Niliutoa mkono wake na kujigeuza. Nili lala kifudi fudi kwa madhumuni ya kumzuia asichezee madafu yangu. Laa haula kumbe ndio nilimpa mwanya wa kucheza na madafu yangu ya nyuma. Kiukweli nilikuwa nikijisikia hali fulani hivi maridhawa.

“Ooomnh sssccc aah” nilijikuta nikilalamika kwa sauti ya mahaba mke wa mtu.

“Mnh hakika leo ninafaidi, tangu nizaliwe sijawahi kupata mwanamke mrembo kama wewe” alizungumza Robinson kwa sauti yake ya kilevi huku akiendelea kucheza na madafu yangu ya uani. Robinson alinigeuza, nami nikageuka bila ya ubishi.

Mwanaume yule mlevi alipeleka mikono yake kutaka kufungua kifungo cha pedo yangu. Kitendo kile kilinifanya nimkumbuke Magesa wangu pamoja na kwamba alikuwa amenikosea. Kwani ni yeye mwanaume pekee ambaye nilimpa mamlaka ya kunivua ama kunivalisha nguo. Nilijikuta nikimsukuma Robinson kwa nguvu kisha nikainuka kuokota blauzi yangu na kujiziba kwenye madafu yangu ya kifuani.

“Wewe! Mimi ni mke wa mtu! Tena shika adabu yako!” Nilizungumza huku nikiwa nimemnyooshea kidole Robinson ambaye alikuwa amelala chali baada ya kumsukuma.

“Mume kitu gani wewe, hebu nipe mambo mtoto wa mwenzio” Robinson alizungumza kilevi huku akijiinua na kunifuata. Nilitulia na kumsubiri afike huku nami nikiyumba yumba kidogo.

“Hata mimi nina mke, njoo mrembo nikupe…..” Alizungumza huku akitaka kunikumbatia.

Nilimsukuma kwa nguvu zangu zote zilizokuwa zimebaki. Kwakuwa alikuwa amelewa sana alishindwa kujizuia na kudondokea kitandani kama mzigo wa dhambi ‘Puu!’.

“Unajifanya mjanja sio?” Robinson alilalamika huku akiwa kitandani.

“Nipotezee kule!” Nilizungumza huku nikivaa ile blauzi yangu.

Baada ya kumaliza kuvaa nilichukua pochi yangu na kuiweka kwapani. Nilivuta hatua kuanza kuondoka huku nikiahia msonyo.

“Kwenda zako, kwanza mwanamke mwenyewe mbayaaaa” Robinson alizungumza baada ya kuona ameshindwa kula tunda.

“Achana na mimi wewe!” nilijibu kwa ufupi huku nikifungua mlango.

“Utajuta kunikosa mwanaume handsome kama mimi wewe!”

“Kafie mbele!” Nilizungumza huku nikiyumba yumba na kutoka nje nikimuachia chumba mlevi yule.

Nilipofanikiwa kutoka chumbani mle nikaenda moja kwa moja hadi barabarani na kuchukua bajaji kwaajili ya usafiri wa kunirejesha nyumbani kwangu Kimara.

*****

Nilipofika nyumbani ilikuwa ni majira ya saa tisa na robo za usiku. Nilifungua mlango na kuingia ndani kwa mbwembwe za kilevi huku nikiimba na viatu nikiwa nimevishikilia mkononi.

Nilipowasha taa ya sebleni macho yangu yalikwenda kutua kwenye sura ya mume wangu Magesa ambaye alikuwa ameketi kwenye kochi pale sebleni akinisubiri. Moyo wangu ulinipasuka na kujikuta nikiikumbuka ile meseji ambayo ilitumwa na mtu aliyekuwa ameseviwa kwa jina la FUNDI UMEME. Hasira zikanijaa tele na kusahau kama na mimi nilikuwa nimetenda kosa la kurudi nyumbani usiku tena nikiwa nimelewa.

“We Malaya umerudi sio?” Nilipaza sauti yangu ya kilevi kumsemesha mume wangu.

Magesa alitulia tuli akiniangalia kwa masikitiko. Katika maisha yake hakuwahi kutegemea kama siku moja ningekunywa pombe. Hivyo alikuwa akishangazwa na hali ile. Pia kitendo cha kurudi nyumbani usiku kilizidi kumpa mshangao na mashaka mwanaume wa watu.

“Nakuuliza wewe, usinikodolee macho kama gorongo’ndo” Nilizungumza huku nikiyumba yumba utafikiri mnazi uliokuwa ukisukumwa na upepo wa kimbunga.

Nilimsogelea mwanaume yule aliyekuwa akinikodolea macho na kutaka kumsukuma kichwani kwa hasira huku nikiyumba yumba. Hata hivyo alinipisha na kwenda kuketi kwenye kochi jingine. Nilipitiliza na kudondokea kwenye kochi lile alilokuwa amekalia Magesa. Nahisi kama angekuwepo mahali pale basi ninge mdondokea yeye.

“Yaani pamoja na uliyo nifanyia, bado unanisukuma?” Nikalalamika kwa hasira huku nikijizoa zoa kilevi kutoka kwenye kochi.

“Nimekuchukia!…sikupendi!…ngedere weee!” Nilizungumza kwa hasira huku nikiyumba yumba kuelekea chumbani.

Kumbe Magesa alikuwa amerejea baada ya kuona amezimiwa simu kwa siku tatu mfurulizo. Alijikuta akishindwa kufanya kazizake kwa ufanisi. Alijitahidi kuvumilia lakini alishindwa na kuamua kuomba ruhusa kazini. Alifanya yote hayo kwasababu alikuwa akinipenda sana mke wake. Lakini alipofika nyumbani ndio akakutana na vituko vyangu. Ndio, kwani si alinianza mwenyewe kwa kutumiana meseji za mapenzi na huyo fundi umeme wake. Ebo! dawa ya moto ni moto mwenzangu. Kama alivyosema Fatuma, Mwenzio akimwaga mboga nawe mwaga ugali.

Kwa hali ile Magesa alijikuta akishindwa hata kulala chumbani. Alijilalia pale pale sebleni masikini wa Mungu mwanaume wa watu. Usingizi wenyewe haukumjia hata lepe hadi kulipo pambazuka.

Mwanamke niliamka saa mbili za asubuhi nikiwa hoi bin taabani. Kichwa kilikuwa kizito sana kwasababu ya hangover niliyokuwa nimeamka nayo. Nilishindwa kufahamu namna nilivyofika nyumbani. Kumbukumbu zangu ziliishia pale tulipokuwa kwenye meza tukikata kilaji. zaidi ya hapo sikukumbuka kitu. Nilijiinua kitandani huku nikipepesuka na kwenda msalani. Baada ya kutoka msalani sikuingia chumbani bali nilinyoosha moja kwa moja hadi sebleni. Nilishituka sana nilipomuona Magesa amejilaza kwenye kochi huku macho yake yakiwa juu.

“Magesa” Niliita kwa kuhamaki. Magesa hakuzungumza kitu zaidi ya kuteremsha macho na kunitazama.

“Umerudi saa ngapi jamani mume wangu?” niliuliza kwa mashauzi huku nikiwa na amani kabisa ndani ya moyo wangu. Kusema kweli nilikuwa nimekwisha msamehe juu ya ule upuuzi wake alionifanyia wa kutumiwa meseji ya mapenzi na Fundi umeme wake.

“Ndio naingia sasahivi” Magesa alinijibu kwa kifupi.

“Oh jamani mbona umewahi sana wakati ulisema utakaa huko wiki nzima?” nikahoji kwa mashaka huku nikimsogelea mume wangu kipenzi.

“Nilikumis mkewangu”

“Oh baby thank youuu!” Niliitikia kwa furaha huku nikisita kumpiga busu kutokana na kunuka pombe mdomoni.

“Vipi lakini mzima wewe?” alihoji Magesa.

“Mzima kabisaaa, buheri wa afya”

“Kweli?”

“Amini nakwambia”

“Hakuna tatizo lolote?”

“Hakuna tatizo mume wangu”

“Vizuri sana” Magesa alinijibu kwa mkato huku akigeuzia shingo yake pembeni.

“Vipi mbona unaonekana haoupo sawa mume wangu?” Masikini ya mungu nilikuwa nikiongea pasipo kukumbuka chochote ambacho kilitokea usiku uliopita.

Mume wangu naye alijikausha pasipo kunieleza chochote kile. Na mimi niliendelea kujishebedua paleee hadi jamaa aliamua kwenda chumbani na kuniacha pekeyangu pale sebleni. Nilimtazama kwa jicho la mashaka hadi alipo toweka machoni mwangu.

Nilikumbuka tena meseji ya Fundi umeme wake na kujikuta hasira zikinipanda tena. Niliona wazi mume wangu ameanza kuwa na kiburi kwasababu ya huyo mwanamke aliyemsevu kwa jina la FUNDI UMEME.

Nilipokuwa nikitafakari kile kiburi chake nilisikia mlio wa simu ya Magesa ukitokea pale kwenye kochi alipokuwa amelala. Sikujishauri bali nilikwenda kuichukua na kumuangalia mpigaji. Nilikuta jina la ABIRIA. Haikuwa kawaida yangu kupokea simu ya mume wangu lakini kutokana na yale aliyonifanyia asubuhi ile nilijikuta nikiipokea na kuiweka sikioni.

“Jamani mpenzi mbona umeondoka bila kuniaga?” Nilisikia sauti ikizungumza kwenye simu ile.

“Unasemaje wewe?” Nilijikuta nikihoji kwa hasira.

“We nani?” Ile sauti nayo nikaisikia ikihoji kwa hasira

“Usitake kujua mimi ni nani. Sema shida yako” Nilizungumza kwa hasira.

“Shida yangu wewe huwezi kuitatua. Nipe mwenye simu niongee naye” sauti ile ilizungumza kwa kujiamini.

“Sikiliza wewe kunguru maji…”

“Niambie kunguru matope, nakusikiliza” ilisikika sauti ile kwa kebehi.



“Iwe mwanzo na mwisho kumpigia mume wangu simu. Nakama hutosikia utanifahamu mimi ni nani?” Nilizungumza huku nikitetemeka kwa rundo la hasira.

“Nawe ukome kupokea simu za watu baradhuli we!” Yule mtu alinitukana kisha akakata simu. Nikabakia nimeiweka sikioni ile simu huku hasira zikifukuta ndani ya kifua changu. Sikujua ni kwanini mume wangu aliamua kunifanyia mambo kama yale.

Vishindo vya miguu ya mume wangu vilinifanya nigeuke nyuma. Nilimuona amebeba begi akitembea kuelekea pale nilipokuwa nimesimama mimi. Alichukua simu yake kutoka mkononi mwangu na kuangalia, alibaini kuwa nilikuwa nimeongea na mtu kupitia simu yake.

“Ulikuwa unaongea na nani?”

“Abiria” Nilijibu kwa mkato huku mikono yangu nikiwa nimeikumbatia kifuani kama vile nimefunga swala.

“Usirudie tena kushika simu yangu” alizungumza Magesa na kuachia msonyo wa hasira.

“Sio kushika tu, bali nitaendelea kuipokea wakati wowote ule” Nilijibu kwa kiburi kilichokuwa kimechanganyikana na hasira. Magesa alinitazama kwa jicho kali kisha akaachia tabasamu la hudhuni na dharau.

“Nakwenda kazini Arusha. Nikirudi hapa nikukute umejirekebisha” Magesa alizungumza huku akininyooshea kidole.

“We nenda, si umeamua kuwafuata huko huko hao mafundi umeme wako”

“Habari ndiyo hiyo mama” Magesa alisema na kutoka nje.

Yaani mwanaume yule angekuwa anafahamu jinsi nilivyokuwa nikimpenda wala asingekuwa akinifanyia vituko kama vile. Nilijitupa kwenye kochi na kuendelea kutafakari mambo yale aliyokuwa akinifanyia Magesa.

****

Hali ya upweke, unyonge, hasira, na wivu vilikuwa vikinitafuna mwilini mwangu. Niliyaunga mkono maneno ya waswahili yasemeyo kuwa “Ndoa ndoano”. Ndani ya siku chache penzi letu mimi na mume wangu Magesa lilichuja na kupotea kabisa. Nilijikuta nikimchukia sana mwanaume yule kiasi cha kuhisi kichefu chefu kila nilipolisikia jina lake.

“Ni afadhali kuwa na kidumu cha kunifariji” Nilijikuta nikizungumza kwa sauti nilipokuwa nimejilaza kitandani. Ingawa nilipoteza kabisa hamu ya kula lakini nikahisi njaa ikinisokota tumboni. Nikachukua simu yangu na kumpigia Undrea kijana aliyekuwa mkaanga chipsi. Nikamwambia aniletee chipsi kuku na juice ya ukwaju.

Baada ya dakika kadhaa yule muuza chipsi alinipigia simu na kunifahamisha kuwa alikuwa amekwisha fika nyumbani kwangu. Nilimruhusu aingie kwa sababu mlango nilikuwa sikuufunga.

“Karibu Undrea”

“Asante Shem”

“Nakupendea hapo tu, huwa hurembi kwenye kazi”

“Ah shemu, nitarembaje bwana wakati nipo kazini” Alisema Undrea huku akinikabidhi sahani ya Chipsi kuku.

“Mwanaume kuchakarika bwana sio unakaa tu kama bwege” Nilizungumza huku nikifunua ile sahani kuangalia msosi nilioletewa na Undrea.

“Ila shemu leo utanisamehe, vipapatio vimeisha”

“Ah, unataka kuniudhi sasa” Niliseme huku nikisogeza ile sahani pembeni.

“Ndio maana nimetanguliza samahani”

“Inabidi leo nikule wewe sasa” Nilisema huku nikiivuta ile sahani, nilichukua shingo na kuipeleka mdomoni.

“Wacha masihara shemu, unile mimi utaniweza”

“Nisikuweze wewe una kitu gani kigeni mno?” Nilizungumza huku nikiinuka na kwenda jikoni.

“Basi mi natoka shemu”

“Ngoja bwana nirudi” Nilimwambia Undrea huku nikiingia jikoni. Niliosha mikono na kurudi sebleni. Nilimkuta Undrea amesimama akinisubiri.

“Kwani unakimbilia nini huko?”

“Ah si unajua tena biashara Shemu?”

“Kwani leo Dogo Janja hayupo”

“Yupo lakini….”

“Hakuna cha lakini bwana hebu kaa unipe kampani, si unajua tena Magesa hayupo?” Nilimwambia huku nikimsukuma kidogo kwa madafu yangu ya nyuma.

Nilimuona akipepesuka na kwenda kuketi kwenye kochi bila kupenda. Alibaki kunikodolea macho nilipokuwa nikidondosha moja moja ndani ya nightdress yangu. Masikini ya mungu kijana wa watu alibaki mdomo wazi kwa kile alichokuwa akikishuhudia mbele ya macho yake. Nikamuona amegandisha macho yake kifuani kwangu akiyakodolea madafu yangu yaliyokuwa yakionekana kwenye mashina kutokana na gauni langu la kulalia nililokuwa nimelivaa kuwa wazi kidogo maeneo ya kifuani. Mdomo wake wa chini alikuwa akiuchezesha kuupishanisha na wa juu.

“Undrea…” Niliita kwa sauti niliyo itolea puani.

“Ndio shemeji” Kijana wa watu alikurupuka utafikiri alitoka usingizini. Nilishindwa kujizuia kucheka kwa jinsi alivyo shituka.

“Vipi mbona kama haukuwa hapa?”

“Aaah! Nipo shemeji, tupo pamoja” alijibu huku akijichekesha chekesha kwa aibu.

“Haya bwana, karibu tule basi” Nilisema huku nikipeleka chipsi mdomoni

“Shemu we kula tu, mie nipo fiti”

“Haya bwana ngoja sie tule” Nilisema huku mkono wangu ukichoma chipsi kwa stiki niliyokuwa nimeishika kwa kidole cha kati na kidole gumba wakati huwo vidole vingine vikiwa vimeinuka juu kimapozi.

Uwepo wa Undrea ndani pale ulinipa uwezo mkubwa wa kula siku ile. Nilijikuta moyo wangu ukifarijika kiasi cha kusahau machungu yote ambayo niliyapata kutokana na vituko vya mume wangu Magesa. nilitafuna taratiibu kiasi cha kusababisha vishimo vya kwenye mashavu yangu kuonekana. Undrea alinikata jicho la kuibia kuanzia kichwani hadi sehemu za kifuani.

“Undrea.” Niliita huku nikijifanya kushituka

“Naam”

“Hembu njoo” Nilimuita huku nikitazama kwenye sahani ya chipsi kuashiria kuwa kulikuwa na kitu kisicho cha kawaida.

“Kitu gani tena shemu?” Aliniuliza huku akionekana kuto kuwa tayari kuinuka pale kwenye kochi.

“Sasa si uje uone” Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwa nimekazia macho yangu kwenye sahani ya chipsi.

Undrea akajiinua kisha akakaa tena ghafla. Nilishindwa kumuelewa ni kwanini alifanya vile.

“Kwani kuna nini shem Prisca?” Undrea alizungumza huku akiwa bado ameketi kwenye kochi.

“Kuna nini huku umeng’ang’ania hapo kwenye kochi. Si nimekwambia uje uone?” Nilizungumza kwa sauti iliyokuwa na mkazo kidogo.

Loo! Masikini ya mungu kijana wa watu nikamuona akiinuka kwa shida na kutembea huku akiwa ameinama kidogo utafikiri alikuwa anacheza mziki wa Pinda mugongo.

“Kwani vipi Undrea?” Nilihoji kwa mshangao baada ya kumuona mtoto wa watu aitembea kama kibabu cha miaka mia na mbili.

“Hamna kitu shemu”

“Sasa mbona upo hivyo? Hebu simama sawa sawa” nikazungumza huku nimemkazia macho.

“Aaaah” Jamaa alijing’ata ng’ata na kusimama kwa taabu huku akigeukia pembeni na mikono akiiweka maeneo ya kati.

Kudadadeki kumbe jamaa chuma kilikuwa kimepata moto. Masikini ya mungu nilijikuta nikimuonea huruma kijana wa watu kwa jinsi alivyo kuwa akiteseka. Niliinuka na kusimama sambamba na yeye.

“Undrea sema unataka nini?” nilihoji kwa sauti ya mahaba huku macho nimeyalegeza na mkono wangu wa kulia nikiupitisha nyuma ya shingo yake.

“Hapana shemu Prisca” alijibu huku akiushika mkono wangu na kutaka kuutoa shingoni mwake.

Nilizidi kumsogelea kiasi cha ncha za madafu yangu ya kifuani kumgusa kwenye kifua chake. Nikamuona akihema juu juu huku macho akiwa ameyalegeza utadhani mlevi wa Cocain.

“Leo nimekula vizuri kwaajili yako Undrea ahsante sana” Nilizungumza kwa sauti ya kubembeleza huku mkono wangu mmoja ukishuka chini kwenye mkungu wa zabibu zake. Kijana yule alishituka na kuruka nyuma.

“Hapana shemeji acha basi” alizungumza Undrea huku akiwa amepinda kidogo.

“Kwani unaogopa nini?” nikahoji kwa ile sauti yangu ya mahaba

“Bro Magesa akija hapa unajua hapata tosha” alizungumza kijana yule kwa wasiwasi.

“Magesa atoke wapi? Nimekwambia amesafiri harudi leo wala kesho” nilizungumza kwa msisitizo kumuondoa wasiwasi kijana yule.

“Lakini shememu…”


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG