Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

MESSAGE YA FUNDI UMEME - 4

   


Chombezo : Message Ya Fundi Umeme 

Sehemu Ya Nne (4)


“Kanyagaaa…..! kanyagaaaa…!” Kanyaga twende….Oomnh…Kanyaga baba…Oiyai oi oi. Mwandishi uko wapi njoo na mimi unipige picha kama ulivyompiga mume wangu Magesa. Twende baba twendeee!” Mwenzenu nikajikuta nimechanganyikiwa na mzigo niliopewa na shemeji Hashimu.

Yaani mwanaume yule kwa kumuangalia alikuwa akionekana mpoleee lakini kwenye masuala mengine, alikuwanimachahari balaa. Sijui ni kwanini Fatuma hatulii, kila kukicha na vibwana mchwara barabarani. Ama kweli penye miti hapana wajenzi.

“Nipe baba nipeee…Ooi Aaaya! Uyoo, chukua yako tot…tito..tutu…tetema tete tete” mtoto wa kike nilitoa ushirikiano kiasicha kujisahau kama mimi nilikuwa ni mke wa mtu.

Sauti ya mlango wa sebleni ilisikika kuashiria kuwa kulikuwa na mtu aliyekuwa anaingia ndani mle. Tulitulia kwa sekunde kadhaa huku tumetegesha msikio kusikiliza kwa makini. Nikweli mlango ulikuwa ukifunguliwa na punde tukasikia vishindo vya mtu aliyekuwa amevaa viatu vyenye visigino virefu akitembea kuelekea chumbani ambako ndiko tuliko kuwepo mimi na shemeji Hashimu tukibadilishana mawazo.

“Mungu wangu!” Nilimsikia shemeji Hashimu akihamaki huku akijisogeza pembeni.

“Vipi shemu?” nikahoji kwa mashaka.

“Fatuma huyo!” alijibu Hashimu kwa sauti iliyokuwa imejaa uwoga.

“Mamaa hii tena aibu” Nilishituka huku nikikurupuka kitandani na kukimbilia kuvaa nguo. Nikamuona Hashimu akihangaika hapa na pale na kuonekana hakujua cha kufanya.

“Tufanye nini shemu?” Nilihoji kwa wasiwasi.

“Vaa haraka” Shemu Hashimu alinisisitiza huku akiwa anahangaika asijue ha kufanya.

Wakati huo vishindo vya miguu ya Fatuma vilikuwa vimekwishafika mlangoni. Tulisikia kitasa cha mlango ambao haukuwa umefungwa kikishikwa na kuzunguushwa kisha mlango ulianza kusukumwa ndani taratibu.



Kwakweli mle chumbani mwa Fatuma mimi na shemeji Hashimu tulikuwa tumeshindwa kuchukua hatua yoyote ile ya kujitetea zaidi ya kuvaa nguo zetu tu kisha tukakaa kusubiria kasheshe. Nilikuwa natetemeka kwa woga mtoto wa kike. Chezea kufumaniwa wewe? Unaweza kufa kabla hata haujaguswa na mtu.

Mlango ule ulio kuwa umeanza kufunguliwa kidogo ulifungwa tena. Tulisikia tena vishindo vya miguu ya Fatuma vikiondoka kuelekea chooni.

“Amekwenda chooni” Shemeji Hashimu alizungumza kwa kunong’ona

“Kwahiyo?” nikahoji kwa wasiwasi huku nikitetemeka.

“Ondoka haraka” Shemeji hashimu aliniambia kwa sauti yake ile ile ya kunong’ona. Sikutaka kujishauri nilichukua kibegi changu na kuchomoka kama mwizi. Nilifungua mlango na kutimua mbio bila kuangalia nyuma. Kama kuna mtu aliniona basi atakuwa alikufa mbavu kwa kucheka.

Niliinua mikono juu kumshukuru Mungu kwa kuniepusha na aibu ile. Jamani msikie hivyo hivyo, kufumaniwa ni janga. Sikuamini kama niliweza kukimbia aibu ile ya kufumaniwa na mpenzi wa rafiki yangu wa karibu. Sijui ningeiweka wapi sura yangu hii mwenzenu mie.

Hata hivyo sikuweza kusahau mambo aliyonipa shemeji Hashimu. Nikajisemea kimoyomoyo “Piga ua shemeji Hashimu simuachi, hata iweje”. Hata hivyo kwa upande mwengine nilijihisi kuwa mkosaji mbele ya rafiki yangu kipenzi. “Ah potelea mbali, mbona yeye mwenyewe anamsaliti Hashimu wa watu. Yeye na Magesa wote ni sawa tu” Nilijifariji na kuhalalisha mambo niliyo yafanya chumbani kwa rafiki yangu na mume wake.

Ilipofika jioni nilimuona Fatuma akija nyumbani kwangu, nilipomuona tu mapigo ya moyo wangu yalinienda kasi na kuhisi amegundua uchafu tulioufanya na mpenzi wake Hashim kule chumbani kwake. Hata hivyo nilijikausha na kujikaza mtoto wa kike kama vile hakukuwa na dhambi yoyote ile niliyokuwa nimemfanyia.

“Karibu sana shoga” Nilimkaribisha kinafki huku moyoni nikihofia.

Fatuma aliketi kwenye kochi pasipo kunijibu kitu chochote. Nilitulia na kumsoma usoni kujua kama alikuwa na ubaya na mimi. Nikabaini sura yake ilikuwa ikiashiria hali ya hatari. Fatuma niliyezoea kumuona siku zote hakuwa Fatuma aliyefika nyumbani kwangu siku hiyo.

“Unaonekana haupo sawa Fatuma” Nilihoji kwa kujihami huku nikiwa na wasiwasi uliochanganyikana na woga.

“Prisca” aliita jina langu kwa sauti kavu.

“Nakusikiliza shoga yangu”

“Nahisi unayafahamu vyema maumivu ya kusalitiwa, au sio?” Fatuma alihoji na kunifanya niishiwe nguvu kabisaaa.

Kutokana na swali lile alilonitandika Fatuma niliona wazi kuwa alikuwa amekuja kunitia kibano nyumbani kwangu kwa kosa la kuiramba kwa wizi asali yake.

Nakwambia mtoto wa kike nilijikuta nikikaa vizuri kwenye kochi huku nikijikuna nywele zangu za kisogoni. Fatuma nilikuwa namfahamu vizuri sana na moto wake pia nilikuwa nauelewa. Mara kadhaa alikuwa akinialika kwenda kuliamsha dude kwa washenzi waliokuwa wakimtibua kwa namna moja ama nyingine. Sasa nikaona wazi kuwa siku yangu na mimi ilikuwa imewadia.

*****

Kwa kiasi kikubwa mambo yalikuwa magumu sana kwa upande wa mume wangu Magesa kule jijini Arusha. Msichana ambaye alikuwa akimtegemea kumsaidia kutatua matatizo yaliyopo kwenye ndoa yake naye alikuwa amemkasirikia. Alipokuwa akimpigia simu alikuwa anakata, na alipomuandikia meseji hakupata jibu. Kwa upande wangu na mimi sikuona sababu ya kupokea simu ya wazinzi. Hivyo mume wangu alipojaribu kunipigia nilikata na kuzima kabisa simu yangu. Nani apokee simu za wazinzi? Labda kama sikuzaliwa na mama yangu mzazi.

Akiwa ameegemeza kichwa chake kwenye mikono yake iliyokuwa imekitwa juu ya meza, akilini mwake alikuwa akinifikiria mke wake. kiukweli mwanaume huyu alikuwa akinipenda sana jamani, lakini ndio hivyo tena jambo lililopo kwenye moyo wa mtu ni kiza kinene. Masikini Magesa wa watu alitoa simu yake na kuishika mkononi, alikuwa akitamani sana kunipigia lakini alifahamu wazi kuwa nisinge pokea. Akawa ameduwaa asijue cha kufanya.

“Magesa….” ilikuwa ni sauti ya msichana kutokea nyuma yake. magesa aligeuka haraka ili kumtambua mtu ambaye alimuita. Macho yakamtoka baada ya kumkuta msichana akiwa amevalia kipedo na blauzi iliyo kuwa imembana kiasi cha kuruhusu umbo lake kuonekana jinsi lilivyo. Kutokana na mavazi aliyokuwa ameyavaa msihana yule yalifanya urembo wake uonekane wazi wazi na kunga’ra kila alipokuwa anapita.

“Yusrah!” Magesa aliita kwa kuhamaki baada ya kumuona msichana yule.

“Niambie baby” Yusra alijibu huku akiinama na kumpiga pusu la shingoni Magesa ambaye alionekana bado kwenye mshangao.

Kwakweli hata kama ungelikuwa wewe ndugu msomaji ungelishangaa, kwasababu tangu alipomfahamu msichana yule hakuwahi kumuona amevaa mavazi kama yale. Muda wote alikuwa ni mtu wa nguo ndefu zilizo jimwaga na majuba au hijabu. Jambo la pili ambalo lilimuacha hoi Magesa wangu ni kuitwa jina lake halisi na msichana yule ambaye alikuwa amemdanganya jina siku walipokutana kwa mara ya kwanza.

“Nilijua kuwa utashangaa. Vipi nimechukiza?” Yusrah alizungumza huku akizunguuka na kusimama mbele ya Magesa na mkono wake mmoja ukiwa kiunoni. Kwakweli mtoto wa watu wa kimanga alikuwa amependeza mno. Ingawa alikuwa ni mwembamba lakini umbo lake lilikuwa na mvuto mtoto wa watu. Kusema kweli hata magesa mwenyewe alimeza funda la mate ya tamaa.

“Una haki ya kuringa mtoto mzuri” Magesa alimwambia Yusrah ambaye alikuwa akijishebedua mbele ya macho yake.

“Kwahiyo unasemaje, niwe navaa hivi hivi, ama kama siku zote?”

“Wewe tu maamuzi yako. siwezi kukufunga.

“Aah Magesa jamani nimekupa nafasi ya kunichagulia” Yusrah alizungumza na kutaja tena jina la Magesa.

“Nani amekwambia naitwa Magesa?” Magesa alihoji kwa umakini huku akimkodolea macho Yusrah usoni.

“Kwani uwongo?”

“Jibu swali, na usiulize swali”

“Nilikuwa nakufahamu mapema tu bali nilikuwa nakuita Frank kwasababu matendo yako yanafanana na jina hilo” Yusrah alizungumza huku akivuta kiti na kuketi mbele ya Magesa.

“Hujajibu swali, ni nani amekwambia kuwa mimi naitwa M a g e s a?” Mume wangu alihoji kwa msisitizo. Yusrah hakujibu kitu bali aliingiza mkono kwenye pochi yake na kutoa kitambulisho cha magesa cha kazi ambacho kilikuwa na majina yake pamoja na picha.

“Hii ni mali yako?” Alihoji Yusrah huku akimuonesha Magesa kile kitambulisho.

“He! ni kitambulisho changu cha kazi, nilikitafuta sana!”

“Una uthibitisho wowote?”

“Inamaana huoni hiyo picha? na hilo jina je?” Magesa alizungumza pasipo kukumbuka kuwa alikuwa amedanganya jina lake kwa msichana yule.

“Umesahau kama wewe unaitwa Frank?”

“Wachana na hayo Yusrah. Mimi ni Magesa na hicho ni kitambulisho changu”

“Kwanini umenidanganya? yaani siku zote hizo mimi nakuita Frank na wewe unaitika tu kumbe sio jina lako?” Yusrah alizungumza huku akionekana kukasirika kutokana na jambo lile.

“Naomba unisamehe kwa hilo Yus…”

“Nikusamehe kitu gani Magesa? wewe sio mtu. kila nikipanga kuja kuzungumzia suala la ndoa yako unanitibua. Mwanaume gani wewe usiye bebeka.” Yusrah alizungumza kwa hasira.

“Sikiliza mtoto mzuri, Frank ni jina langu nililokulia. Na Magesa ni jina langu la kiofisi na ndilo nililosomea” alieleza Magesa kwa kumuongopea Yusrah ili kuuwa soo.

“Kwahiyo una majina mawili” Yusra alihoji huku akiwa amemkazia macho Magesa.

“Yeah, babu yangu mzaa mma alipenda sana kuniita Frank kwasababu lilikuwa ni jina lake” Magesa aliendelea kuzungumza maneno ya uwongo.

“Kwahiyo mimi nitumie jina gani?”

“Wewe tu, majina yote ni ya kwangu” Magesa alieleza.

Maelezo ya Magesa yalionekana kumuingia Yusrah na kumuamini. Alikuwa ametulia akimkodolea macho mume wangu kwa macho ya tamaa. Mwanamke ana laana yule! Yani nakwambia hadi kamevaa kimini kwaajili ya kumtega mume wangu. Viguu vyenyewe vibayaa hata kama vina mvuto. Shetwani ibilisi mkubwa!

Magesa limtazama mwanamke yule baladhuli kwa macho ya furaha huku akijiona ni mshindi ndani ya moyo wake.

“Nadhani umenielewa sasa?” alihoji Magesa huku akipeleka glasi ya juisi mdomoni kisha akairejesha mezani.

“Ok, tuwachane na hilo, kama unaniongopea utajua mwenyewe” alisema Yusra na kuchukua glasi ya juisi ya Magesa na kuipeleka kinywani mwake, alipiga funda mbili kabla ya kuishusha tena mezani.

“Haya niambie mkeo anasemaje?” Yusra alihoji kwa upole

“Dah! we acha tu ndugu yangu ni zaidi ya majanga” Magesa alizungumza kwa sauti ya kukata tamaa.

“Vipi tena Frank Magesa?” Yusrah alihoji huku akitumia majina yote mawili aliyopewa na mume wangu.

“Yaani kabla moja halijakwisha jengine limezuka” Magesa alizungumza kwa sauti ya kukata tamaa na kutoa gazeti lililokuwa limeandika habari za yeye kufumaniwa na kupigana kwaajili ya mwanamke.

“Kwahiyo unaona ufahari kutembea na gazeti lililoandika uchafu wako?” Yusrah alihamaki baada ya kuliona gazeti lile.

“Yusra, ukweli ni kwamba huyu mwanamke hakuwa mtu wangu” Magesa alijaribu kujieleza.

“Sikiliza Frank, sijui Magesa vyovyote vile. Unajua mimi sio mtoto mdogo?” Yusra alizungumza kwa msisitizo.

“Huwo ndio ukweli Yusrah mdogo wangu!” magesa lijaribu kusisitiza maelezo yake.

“Kwanza mimi sio mdogo wako, halafu utabishana vipi na ukweli ambao hata kipofu anaweza kuuona kwa kupapasa tu” alizungumza Yusrah kwa msisitizo.

“Yusrah huyu hakuwa mtu wangu”

“Kumbe alikuwa kimada wako?”

“Sikuwa na mahusiano yoyote na mwanamke huyu”

“Kwahiyo ulikuwa ukimtumia kama changudoa si ndivyo?” Mwanamke yule aliendelea kubabatiza kosa lile kwa mume wangu. Mimi kananikera! Sijui kalikuwa ni kachawi? Maana kalivyomganda mumwengu utafikiri ruba.

“Yule mwanamke alifika na kunifanyia vituko akihisi mimi ni bwana wake, mwisho akadai heti alikuwa amenifananisha na mpenzi wake na mara hiyohiyo huyo mpenzi wake alifika na kunishutumu heti namuibia mwanamke wake” Magesa alijaribu kujitetea kwa Yusrah ambaye alikwishamuona mtu wa ajabu.

“Sio rahisi kueleweka! Na huyo mke wako ameliona hili gazeti?” alihoji Yusrah kwa umakini.

“Bila shaka amepata taarifa. Kwasababu sasa hivi ndio hapokei kabisa simu yangu” Magesa alieleza.

“Mwanamke wako atakusumbua sana Magesa” yule mwaamke mshenzi aliendelea kunipondea kwa mume wangu halafu anajifanya anataka kuisaidia ndoa yangu. Hovyoo!

Mume wangu Magesa alizidi kuchanganyikiwa baada ya kusikia maneno yale kutoka kwa kale kabinti sijui mwenyewe alikuwa anakaita Yusrah.



Magesa alipumua kwa nguvu kisha akatoa neno.

“Sasa nifanye nini Yusrah? Hebu nishauri basi” Magesa alilalama kwa unyonge.

“Usiwaze nipo kwa ajili yako. Sipendi kukuona ukiteseka hivyo” Alisema Yusrah huku akishika viganja vya mikono ya mume wangu ambayo alikuwa ameikutanisha juu ya meza.

“Kwa kweli sijajua nifanye nini ili heshima yangu irejee na mke wangu anielewe” alizungumza Magesa kwa masikitiko.

“Msomi kama wewe unashindwa kutetea haki yako?” alihoji Yusrah kwa msisitizo na umakini wa hali ya juu.

“Unadhani nifanye nini?”

“Usinichekeshe Magesa” alizungumza Yusra kwa mshangao.

“Nachekeshaje sasa?”

“Unashindwaje sasa kujisimamia kwa jambo zito kama hili?”

“Unanisaidia au haunisaidii?” mume wangu lihoji baada ya kuona Yusrah akimtolea maneno ya hovyo.

“Leo nimeshagundua ni kwanini mke wako anakusumbua” alizungumza Yusrah kwa mkazo.

“Sikiliza Yusrah, mimi mwenyewe najitambua nilivyo. Uamuzi ambao nitauchukua ni lazima ulimwengu wote ushangae, sasa mimi sitaki itokee hivyo” mume wangu alieleza.

“Hakuna sababu ya kutumia nguvu Magesa”

“Ndiomaana nahitaji ushauri wako”

“Vyombo vya sheria si vipo?”

“Hata kama nikienda kwenye vyombo vya sheria, jina langu si ndio limekwisha chafuliwa?”

“Hapana Magesa. Usiwe na mawazo finyu kiasi hicho”

“Enhe”

“Wewe nenda kwenye vyombo vya sheria, haki yako utapata na heshima yako itarejea pia” alizungumza Yusrah kwa umakini na kujiamini.

“Mnh” Magesa aliguna kwa kukata tamaa.

“Ndio, vyombo vya habari haviruhusiwi kutoa taarifa zisizo na uhakika. kwanza kabisa itawalazimu kuandika kuwa taarifa zilizotolewa hazikuwa sahihi, pili watalazimika kukulipa kwa kukuchafulia jina na kukudhalilisha” Yusrah alizungumza kwa msisitizo.

“Kweli Yusrah?”

“Amini nakwambia”

“Basi ngoja nijaribu. Naamini mke wangu akibaini ukweli atanielewa na atabadilika” alizungumza Magesa kwa matumaini mapya ya kurejesha ndoa yake katika hali ya zamani.

“Magesa” Yusrah aliita kwa sauti ndogo huku shingo yake ameilazia kwenye bega lake la kushoto na macho ameyalegeza kama mtu aliyekunywa supu ya mlenda.

“Yes Yusrah” aliitika Magesa huku akimtazama Yusrah machoni.

“Nakupenda sana, nitahakikisha nakuwa nawe bega kwa bega katika kila hatua ya matatizo yako” alizungumza Yusrah kwa ile sauti yake ya kutolea puani na macho akizidi kuyalegeza.

“Nashukuru sana kwa kampani yako mrembo. Mungu atakulipa” Magesa alizungumza kisha wote wawili wakawa wameachia tabasamu la matumaini.

“Lakini bado sijakupatia dawa ya kumtibu mkeo” alisema Yusrah.

“Haya nipe basi hiyo dawa ili namimi niwe na amani kama wengine” Magesa alizungumza huku akitabasamu.

*****

Fatuma alitulia kwa sekunde kadhaa akinitazama jinsi mwanamke mwenzake nilivyokuwa nikijikanyaga kanyaga. laiti ungeniona ndugu msomaji jinsi nilivyokuwa nimelowa kwa woga, nahisi kama sio kucheka basi ungenihurumia.

“Hashimu ameingiza mwanamke chumbani kwangu!” Fatuma alizungumza kwa upole na masikitiko makubwa.

“Mnh! kwahiyo umemfumania chumbani kwako?” nikajifanya kushtushwa na taarifa zile huku bado nikiwa wasiwasi.

“Sijafanikiwa kumfumania” Fatuma alizungumza kwa taabu kutokana na hasira.

“Sasa umejuaje?” nikamtupia swali la mtego.

“Nimekuta nguo ya ndani ya kike kitandani” alisema Fatuma kwa msisitizo. Niliposikia maneno yale nilijikuta nikipumua kwa nguvu. Kumbe alikuwa hajabaini mtu aliyemuibia peremende yake.

“Au alikuwa amekununulia wewe?” nilijifanya kuchangia kwa mshangao.

“Aninunulie nguo iliyokwisha tumika?” Fatuma alizungumza.

“Mungu wangiu! Kumbe imetumika?”

“Ndiyo, inaonekana imevaliwa. Nadhani mtu mwenyewe ameisahau kutokana na haraka”

“Jamani wanaume hawa!” Nilijifanya nikiwalaani wanaume kumbe mbaya wake alikuwa naye pale pale. Ndani ya moyo wangu nilikuwa nikimshukuru Mungu kwa kunitendea muujiza. Pamojana kwamba sikuwa nimefumaniwa lakini cha moto nilikuwa nimekipata. Katika maisha yangu sidhani kama nitakuja kusahau tukio lile.

“Sijui hata nifanye nini yani hapa akili yangu imevurugika” Fatuma alizungumza huku akiuma uma midomo yake kwa hasira.

Waswahili wanakwambia mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu! Fatuma alikuwa amesahau kabisa kuwa yeye ndiye alikuwa anaongoza kwa kumsaliti mwenzake. Fatuma akikutajia majina ya wanaume wake unaweza kupata kichefuchefu. Fatuma alikuwa ni mchafu, tena mchafu kweli kweli. Leo hii mwenzake amejaribu tu kidogo kuchepuka na Priscaria heti amechanganyikiwa.

“Lakini dawa unayo shost umesahau?” nikazungumza kwa mtego.

“Dawa ya nini Priscaria, mimi huyu mwanaume amenishinda. Sihitaji dawa yoyote” Alizungumza Fatuma kwa maumivu makali moyoni.

“Inamaana umesahau vichenchede vyako?” nikahoji baada ya kumuona rafiki yangu yule anaelekea kuchanganyikiwa kwaajili ya mapenzi.

“Yap umenikumbusha! Lakini kwanini afanyie uchafu wake kwenye kitanda ninacholalia mimi?” Fatuma alizungumza kwa hasira kali.

“Fatuma, hupaswi ku complicate maisha, kama vipi twende zetu viwanja tukajiachie” nilizungumza maneno yale baada ya kubaini rafiki yangu naye alikuwa ameumizwa na lile janga la usaliti lililokuwa limenifika mimi.

Fatuma alikuwa mwepesi sana kunipatia ushari kipindi kile nilichokuwa nimebaini kuwa mume wangu alikuwa akinisaliti na mtu aliyekuwa anamuita Fundi umeme. Lakini siku hiyo mambo yalikuwa magumu kwa upande wa Fatuma na kusahau kabisa kutumia zile mbinu alizokuwa amenipatia mimi.

“Priscaria mimi sirudi kwa Hashimu, sirudi nakwambia” alizungumza Fatuma kwa hasira.

“Fatuma rafiki yangu wala usipaniki, kumbuka hata mimi ni muhanga wa mapenzi kama wewe. Cha msingi ni kuungana na kukomesha tabia za washenzi hawa” nilizungumza kwa msisitizo huku nikishika nywele za Fatuma na kuzichezea kidogo kumpa faraja.

“Unafikiri tutazikomeshaje tabia zilizokomaa na kuota mizizi tayari” alizungumza Fatuma kwa maneno ya kukata tamaa.

“Hapana Fatuma nafikiri umesahau shoga yangu” nilizungumza kwa msisitizo.

“Haya nikumbushe basi”

“Dawa ya mot ni moto au umesahau?” nilizungumza kwa msisitizo zaidi.

“Ni kweli shoga yangu, mwenzako akimwaga ugali nawe mwaga mboga” Fatuma alizungumza kwa kujifariji na kuhisi ahuweni ndani ya nafsi yake.

“Hiyo ndiyo habari ya mjini” nikakazia kauli yake huku moyoni nikisema nimemkomesha pumbavu zake.

“Potelea mbali. Twende zetu Club tukapoteze mawazo” alisema Fatuma kwa hasira.

Kwa kweli sikujisikia kabisa kutoka siku ile, lakini nikaona kama ningekataa labda angenigundua mwizi wake. Nikaenda kukoga na kuanza kujipara tayari kwa mtoko.

“Shost humalizi tu kujiandaa” alizungumza Fatuma baada ya kuona nilikuwa nachelewa.

“Nimeshamaliza shost twende zetu” nilizungumza huku nikiendelea kupanga nyusi zangu kwa kitana kidogo.

“Wewe ni mrembo tu wala huna sababu ya kujipamba saana” Fatuma alizungumza huku akinikodolea macho.

“Mnh haya tuondoke maana naona yameanza kukutoka ya maji kupwa na maji kujaa” nilizungumza huku nikichezesha midomo yangu kuweka sawa lipstic niliyokuwa nimepaka.

Tulisimamisha bajaji na kuingia tayari kwa safari ya kwenda viwanja. Kila mmoja alikuwa amechoshwa na tabia za usaliti zilizokuwa zikifanywa na mume wake. Kila mmoja ndoa yake ilikuwa na hati hati ya kuvunjika kutokana na tabia za wanaume wetu kutoka nje ya ndoa.

“Wapi jamani?” yule kijana mwenye bajaji alihoji mara tu tulipoingia.

“Vijana Social” Fatuma alijibu kwa mkato.

“Vipi mnakwenda kwenye tamasha nini?” dereva yule wa bajaji alihoji huku akikata kona na kuanza safari,

“Hayakuhusu baba, wewe endesha bajaji yako!” nilimjibu yule kijana kwa kebehi.

Fatuma alinibonyeza kuashiria nisimjibu vibaya kijana yule. Niligeuza macho yangu na kumuangalia Fatuma usoni kuhoji kulikoni? Fatuma alinikonyeza kwa kupenjua macho kuelekea kwa kijana yule akimaanisha kuwa alikuwa amemuelewa. Nikakubali kwa kichwa na kubakia mpole.

“We baba…” Fatuma aliita baada ya kimya kidogo.

“Naam mama..” kijana yule aliitika huku akipunguza mwendo kutokana na mashimo yaliyopo njiani na kukunja kona kuitafuta barabara kubwa.

“Hivi umekosa nini?” Fatuma alihoji kwa upole.

“Kwanini unt?”

“Kijana mzuri kama wewe inakuwaje unashinda ukiendesha bajaji?” Fatuma alihoji kwa mshangao wa kujifanyisha.

“Aah Sister bajaji inalipa kwa hapa town” kijana yule alizungumza kwa kujidai huku akitafuna bablish.

“Hakuna bwana, kijana mzuri mtanashati mwenye mvuto upo tu na bajaji kutwa nzima!” aliendelea kuzungumza Fatuma kwa hali ya mshangao.

“Sasa unafikiri nitafanya kazi gani, shule kwenyewe nilikimbia umande” kijana yule alieleza huku akitupa jicho moja moja kupitia kwenye kioo cha juu yake.

“Hata kama shule huna, lakini nguvu si unazo?” Fatuma alizungumza.

“Nguvu ninazo ndio, lakini hapa mjini nitazitumia kufanyia nini? Hapa sio kama kijijini nikasema nilime au nifanye sijui nini” alizungumza kijana yule huku akigeuza macho yake na kuangalia maduka yalivyokuwa yakirudi nyuma.

“Sasamimi nataka nikupe kazi yenye kulipa vizuri kama hutojali” Fatuma alizungumza kwa kujiamini.

“Aaah ilimradi mkono wende kinywani, mimi kazi yoyote ile nafanya mama” alizungumza kijana yule huku akitupa jicho kwenye kioo cha juu kumtazama vizuri Fatuma.

“Nambie kwanza umeoa?” Fatuma alihoji.

“Nimeoa wapi mama, hali yenyewe unaiona hii kuoa mwisho ilikuwa miaka mitano iliyopita” kijana yule alieleza.

“Kwanini sasa usioe kijana mzuri hivyo?” nikadakia baada ya kuona Fatuma alikuwa akizunguuka mno kumwaga ukweli.

Kijana yule aliinua macho yake na kunitazama kwa umakini kisha nikamuona akiachia tabasamu baada ya kubaini na mimi nilimuangalia kupitia kwenye kioo kile kile cha pale juu.

“Vijana wazuri huwa hawaoi siku hizi wanafanya ufuska kwanza na wakija kushituka wanakuwa wamechelewa” Fatuma alizungumza kwa sauti ya kubania kidogo.

“Hamna mama, hakuja mzuri wala mbaya sikuhizi. Kuoa imekuwa historia ya makumbusho” alizungumza kijana yule.

“Na ikitokea mwanamke ana uwezo pia hautaoa?” Fatuma alihoji.

“Kwanini sasa nisikubali kama mwanamke ana wadhfa wa kutosha. Nakubali tu”

“Na vipi kama akikupenda na kutaka mle raha tu bila kuoana?” nikahoji kwa umakini.

“Yani dada sio wadhfa tu, akitokea mtoto mkali kama wewe vile. Mi nabeba si unajua tena ujana maji ya moto” alizungumza kijana yule maneno ambayo Fatuma hayakuwa yamemfurahisha kwasababu kijana yule alitoa maneno ambayo yalilenga kunisifia mimi na sio Fatuma.

“Je kama ukipendwa na mimi?” Fatuma alihoji kwa msisitizo baada ya kuhisi ndege wake alikuwa ana hatihati ya kunasia mtego wa jirani.

“Nani wewe…?” alihoji kijana yule huku akimtazama Fatuma kwa umakini kupitia kile kioo kidogo.



“Mbona hata wewe mkali tu, yani leo nimebeba vifaa hasa. Kwa mfano nikilipata limoja kwanini nisimsaliti mama watoto wangu!” alizungumza kijana yule huku akiachia tabasamu.

Mimi na Fatuma tukatazamana na kupeana ishara ya kumalizia kumeza chakula tulichokuwa tayari tumesha kitafuna.

“Lakini wewe si umesema haujaoa” nikahoji kuvunja ukimya.

“Ni kweli sijaoa” alijibu kijana yule bila wasiwasi.

“Na huyo unayesema utamsaliti ni nani?” Fatuma akadakia na kuhoji kwa umakini.

“Kuna mwanamke naishi naye lakini sijamuoa” kijana yule alieleza.

“Hovyoo!” Fatuma alijikuta akizungumza kwa sauti ya chini.

“Sasa huyo unayeishi naye si ndiye mkeo baba?” nikazungumza kwa mshangao.

“Hakuna bwana, ni mzazi mwenzangu na sio mke wangu” kijana yule alisisitiza.

“Eeh basi makubwa” Fatuma akabaki ameshangazwa na maelezo ya kijana yule.

“Tena mabonge mabonge!” nikaongezea kauli ya Fatuma

“Unafikiri kwa kijana mzuri kama wewe kuna mwanamke anaweza akakukataa?” alizungumza Fatuma kwa mbwembwe na madoido.

“Wacha utani basi…” alizungumza kijana yule polepole huku akitutupia jicho.

“Mbona hata mimi nakupenda sasa” alizungumza Fatuma kwa sauti moja laini na nyororo sana.

“Duh..!” alishituka kijana yule baada ya kusikia kauli ile ikitokea kinywani mwa Fatuma.

“Najua ni ngumu sana kwa mwanamke kueleza hisia zake lakini mimi nimejitahidi, ujue nimedhamiria kweli” Fatuma alishuka mistari kwa kijana yule.

“We kaka hebu kuwa na huruma, dada wawatu amejieleza vya kutosha” nikazungumza kwa msisitizo.

“Unajua sister kuna kitu kinanichanganya sana” alizungumza kijana yule.

“Ki nini sasa?” nikahoji huku Fatuma akinitazama.

“Inawezekanaje wanawake warembo kama ninyi mtongoze wanaume?” kijana yule alitupa swali.

“Sio wanaume, hebu angalia kauli yako basi” nikajifanya kuzungumza kwa sauti ya hasira kidogo.

“Kwahiyo unataka kuseme mimi ni demu?”

“Sina maana hiyo bwana nini?”

“Kumbe..”

“Wewe sio mwanaume ilimradi mwanaume tu” nikajaribu kueleza ili kurekebisha kauli yangu.

“Kaka wewe ni mwanaume mwenye mvuto na una sifa ya kutambulishwa na mwanamke wa aina yoyote ile kama mume” Fatuma aliingilia kati na kueleza.

“Swadakta, hivyo ndivyo nilivyomaanisha mimi” nikaongezea kupamba maneno ya Fatuma.

“Kaka mimi sijawahi kukuona, lakini kusema kweli nimekupenda” Fatuma alizungumza kwa sauti ya deko.

“Kupenda sio lazima muwe mnafahamiana, mapenzi ya dhati yanachipuka muda wowote mahali popote na kwa mtu yeyote yule” Nakwambia nilizidi kufafanua mtoto wa kike kwa lengo la kumtia mtegoni kijana wa watu.

“Duh kweli leo nimepatikana mwanaume” alizungumza Kijana yule kwa sauti kubwa ambayo ilisikika kwenye masikio yangu na masikio ya Fatuma.

Mimi na Fatuma tukaangaliana na kupeana ishara ya ushindi. Fatuma akachezesha kope zake akiwa ananipa ishara ya kujiongeza. Kwakuwa tulikuwa tumezoea kuzungumza kwa ishara nikamuelewa shost yangu yule.

“Samahani kaka, kumbe unaitwa nani vile?” nikahoji kama vile nilishawahi kumuona sehemu.

“BOB MBASA, Naitwa Bob Mbasa” alijibu kwa ufupi yule kijana aliyejitambulisha kwa jina la Mbasa.

“Jina la kazi hilo” Fatuma akadakia.

“Mwenzangu we, hakika mwanaume umepata” nilizungumza na kutazamana na Fatuma kisha tukaangua kicheko kwa sauti ndogo ya ulimbo.

Bob Mbasa aliposikia maneno yangu alitikisa kichwa kusikitika huku akicheka. Nafikiri alikuwa akihisi amebeba vichaa siku hiyo.

“Shem Bob..” niliita kwa sauti ya chini.

Bob Mbasa aliinua macho yake na kunitazama kupitia kile kioo kidogo huku akinisikiliza kwa makini.

“Samahani naomba usimame kidogo” nikazungumza kwa upole.

“Kuna nini tena?” Bob Mbasa akahoji kwa wasiwasi.

“Shost amebanwa anataka kujisaidia” nikaeleza.

“Avumilie tu, mbona tunakaribi kufika” Bob alieleza.

“Hivi unajua maana ya kubanwa wewe?” Fatuma akahoji kwa msisitizo kiasi cha kumuogopesha Bob Mbasa.

Dereva yule wa bajaji alipunguza mwendo na kupaki kushoto kisha akageuka nyuma tulipokuwa tumekaa.

“Haya mrembo fasta basi” alizungumza Bob Mbasa.

Bajaji iliposimama tu Fatuma aliteremka kuelekea mbele kwa Bob Mbasa na kusimama akimtazama kwa tabasamu la mtego kijana wawatu.

“Vipi mtoto mzuri mbona huendi sasa?” Bob Mbasa alihoji kwa mshangao baada ya kumuona Fatuma amesimama karibu na yeye.

Fatuma hakutoa jibu lolote bali alipandisha mguu mmoja na kukita goti kwenye kiti cha Bob Mbasa.

“Vipi sasa mbona sikuelewi?” Bob Mbasa aliendelea kuhoji kwa mshangao.

“Naomba uniambie kama nafaa kuwa na mwanaume kama wewe” Fatuma alizungumza huku akinyumbulika pale kwenye kiti cha dereva wa bajaji.

Kutokana na ile sketi yake fupi aliyokuwa ameivaa Fatuma sehemu kubwa ya mapaja yake yaliweza kuonekana machoni mwa Bob Mbasa. Kijana wa watu alivuta pumzi na kuziachia kwa mkupuo huku akitupia macho kwenye lile paja lililokuwa limenona na lenye mvuto hasa kwa mwanaume yeyote aliye kamilika.

“Vipi sasa mbona hunijibu au sina mvuto?” Fatuma alizungumza kwa sauti ya kulalamika huku akiinua mkono wake wa kushoto na kuuweka kwenye bega la Bob Mbasa.

“Yea…Yeah…Yeah…Una kila sifa ya kuitwa mrembo” Kijana Bob alijibu kwa mshituko baada ya kuibuka ghafla kutoka kwenye lindi la mawazo alilokuwa amezama baada ya kuona zile paja za Fatuma. Sijui kama angepata bahati ya kuona za kwangu angefananaje. Maana mimi nilikuwa balaa kuliko hata Fatuma.

“Naomba basi leo tutoke wote” Fatuma alizungumza kwa kubembeleza huku akimpapasa Bob Mbasa kwenye mabega.

“Mnh! Sasa mbona hata kipande cha watu sijafikisha!” alizungumza Bob Mbasa huku akijikuna kwenye maotea ya nywele za utosini.

“Achana na mambo ya vipande baby, mimi nitaweka sawa kila kitu” alizungumza Fatuma huku akiuondoa mkono wake kutoka kwenye paja la Bob Mbasa na kumshika kwenye shavu la kushoto.

Ile blauzi fupi aliyokuwa amevalia Fatuma ilipanda juu kidogo na kuwacha maeneo ya kitovu wazi. Laa haulaaa! Bob mbasa alishindwa kuvumilia na kujikuta akimkamata kiuno na kumvutia kwake Fatuma kwa lengo la kumpiga busu tumboni.

Kule nyuma kwenye bajaji nakwambia nilikuwa nimetulia utafikiri sikuwepo eneo la tukio. Kumbe nilikuwa nikipiga chabo kwa ncha ya jicho langu la kulia na la kushoto kwa ukaribu zaidi.

Ndani ya nafsi yangu nilijisikia huru kwa sababu nilielewa kijana yule angekwenda kumaliza hasira zote alizokuwa nazo Fatuma baada ya kubaini mume wake alikuwa amemsaliti, tena ndani ya chumba chake na kitanda chake. Hata hivyo sikuumia sana kwa kitendo kile cha Fatuma kusalitiwa kwa sababu kama usaliti usingekuwepo na mimi nisingeweza kuonja utamu wa shemeji Hashimu.

Kule kwenye kiti cha dereva Fatuma na Bob Mbasa walijisahau kabisa na kujikuta wamezama katika mahaba mazito. Kila mmoja alionekana kuridhika kukutana na mwenzake. Nilijua kabisa Fatuma alikuwa akiyafanya yote yale kutokana na hasira za kusalitiwa na mume wake Hashimu. Hivyo alidhamiria kabisa kuisaliti ndoa yake kwa gharama yoyote ile ili kulipiza kisasi.

“We Malaya wewe!” nilisikia sauti ya mtu akitukana kwa ukali huku akipeleka mkono kumshika Fatuma kwa nyuma.

Nilishituka sana na kuketi vizuri kuweza kushuhudia kitu ambacho kilikuwa kinataka kuendelea pale nje.

Yule mtu aliyekuwa akitoa maneno ya.le makali alivuta mkono wake na kumtandika Fatuma kibao kitakatifu usoni.

“No mke wangu wacha!” nikasikia sauti ya Bob Mbasa ikisihi.

“We dada vipi…” Nikamsikia Fatuma naye akihamaki huku ameshikilia shavu lake lililokuwa limezawadiwa kipigo.

Nilichokuwa nimekibaini haraka haraka katika tukio lile ni kwamba mtu yule alikuwa ni mke wa Bob Mbasa.

Mwanamke yule alimkunja Fatuma na kumtikisa kwa nguvu na hasira huku Fatuma akionekana bado katika hali ya mshangao.

“Kila siku nasikia habari zako leo nimekunasa Malaya mkubwa wewe” mwanamke yule alizungumza kwa hasira huku akivuta mkono kutaka kumtandika tena Fatuma. Kwa Bahati nzuri Bob Mbasa alimdaka mwanamke yule na kumvuta kutoka mikononi mwa Fatuma.

Urafiki ni kufaana wakati wa shida na raha mwenzangu. Niliteremka kwenye bajaji na kumfuata yule mwanamke kwa lengo la kumsaidia shoga yangu Fatuma. Kabla sijafika eneo lile, yule mwanamke kumbe alikuwa amejiandaa kufanya fumanizi la mwaka. Alichomoa bonge la bisu kutoka kiunoni mwake huku akipiga kelele za kutaka kuachiwa afanye mauaji.

Ndugu msomaji hapana kuchezea kifo wewe! Nilijikuta nikifunga breki ghafla na kusita kumsogelea mwanamke yule ambaye tayari aliinua kisu kwa lengo la kumcharanga Fatuma usoni.

“Acha mke wangu usifanye hivyo! Utauwa!” Bob alizungumza kumsihi mwanamke wake.

Fatuma alivyoona balaa lile limekuwa kubwa hakusubiri kuonyesha umwamba wowote bali alichomoka na kutimua mbio. Nakwambi alikuwa anahomoka utafikiri anakimbiza kuku wa pasaka. Mashuhuda nao hawakuwa nyuma kushangilia na kuzomea riadha ile.

“Mwengine huyu hukuu!” nikasikia sauti ya watu wakizomea kutaka kuhamishia balaa lile kwangu.

Thubutuuu! Kufa ni lazima lakini kupigwa kupenda ndugu msomaji. Miguu si nilikuwa nayo hata mimi? Nilikunja kona na kuelekea upande wangu huku mwanamke yule wa Bob akimuacha Fatuma na kuniunganishia mimi.

Kelele za watu zilikuwa zikinichanganya na kuzidi kunitia wazimu na kunifanya nikimbie hovyo. Nilikuwa nakiona kifo changu wazi wazi siku hiyo.

“Kamata huyooo!”

“Piga huyooo!”

“Kamata Changudoa huyoo!”

Watu walikuwa wakinizomea huku wakinikimbiza utafikiri kibaka wa kuku mtaani. Kifo nyie kitu kingine yani huwa hakipigi hodi. Muda wowote na dakika yoyote ile unaweza kupotea katika ulimwengu huu na watu wakakusahau kabisa.





Hata hivyo sikukata tamaa na kuendelea kutimua mbio huku nyuma yule mwanamke alikuwa bado ameniandama na mkononi ameshikilia kisu kisawasawa kwa shambulizi la kuinyofoa roho yangu.

Mungu ni Mungu jamani, nilipokuwa nikikimbiza roho yangu ghafla ilikuja bodaboda na kusimama mbele yangu.

“Twende..” alizungumza dereva wa ile boda boda.

Nakwambia mtoto wa kike nilikwea boda boda ile kama gedere pasipo kuhoji swali lolote lile.

“Twendeee…” nikapaza sauti baada ya kukaa na kushikilia vizuri.

Siku weza kuamini kama nimefanikiwa kutoka salama mikononi mwa mwanamke yule aliyekuwa amekusudia kuondoka na roho zetu. Niliingia chumnai kwangu na kujitupa kitandani huku nikipumua kwa nguvu.

Sikujua Fatuma alikuwa wapi na katika hali gani maana tangu tulipoachana pale kwenye sheshe hatukuonana tena. Nilichukua simu yangu kutoka kwenye pochi na kuvuta namba za Fatuma. Kabla sijapiga namba zile, Fatuma alinipigia name nikapokea haraka haraka.

“Shoga vipi?” nikazungumza mara tu nilipopokea.

“Uko wapi?” Fatuma alihoji mara aliposikia swali langu.

“Niko nyumbani wewe uko wapi?” nikahoji kwa wasiwasi.

“Namimi nimefanikiwa kufika nyumbani” alijibu Fatuma huku akionekana kupata ahuweni baada ya kupata taarifa zangu.

“Shoga ningekufa mimi” nikazungumza kwa msisitizo.

“Umetokaje pale mana nilipo ona ule mbisu nilijikuta nimechomoka ghafla” Fatuma alieleza.

“Mwenzangu we acha tu ni majanga” nikazungumza.

“Shoga nakuja, leo lazima kieleweke” Fatuma alieleza huku akionekana wazi bado alikuwa na uhu wa kusaliti ndoa yake.

“Heeh Shost hujakoma tu!” nilizungumza kwa mshangao

“Kipele shoga kipele kinanisumbua mwenzio” Fatuma alizungumza.

“Basi sawa, ngoja nipumzike, lakini kama ni kutoka labda usiku sana” Nilieleza tu ilimradi kumridhisha Fatuma lakini sikuwa tayari kutoka tena usiku ule.

“Poa..” Fatuma alijibu na kukata simu.

Nilivuta tena pumzi na kuzitoa kwa mkupuo. Nilimshukuru muumba kwa wema aliokuwa ametutendea siku hiyo.

Tukio lile lilinifanya moyo wangu kusawajika na kupoteza kabisa kujiamini na kuto kujikubali kwa tabia ambayo nilikuwa nimeianzisha tangu nilipohitirafiana na mume wangu Magesa.

Nilijiona wazi kuwa nilikuwa ni mkosaji na nilikuwa nikicheza na hatari dhidi ya maisha yangu. Nikaumia sana na kutamani kuishi kama zamani na mume wangu Magesa. Sikuwa tayari kuendelea kuishi katika maisha yale niliyokuwa nikiishi kwa kushawishiana na shoga yangu Fatuma.

Nilichukua simu yangu na kumtafuta mume wangu Magesa ili nimfahamishe kuwa nilikuwa nimemsamehe kwa kila kilichokuwa kimetokea. Na kama kulikuwa na kosa lolote lile ambalo nimemkosea basi nimuombe radhi ili tuyamalize na kuishi kama zamani.

Lakini kila nilipokuwa nikipiga simu mume wangu alinikatia, nilipiga tena na tena lakini ikakatwa. Sikuchoka kupiga hadi ilipopokelewa. Lakini nilisikia sauti ya mwanamke amepokea simu yangu niliyokuwa nikimpigia mume wangu.


******

Magesa alitulia kwa makini akimsikiliza Yusrah amtajie hiyo dawa ambayo alikuwa amemuahidi kwa muda mrefu. Alikuwa akitamani sana kuona siku moja amani inarejea katika ndoa yake.

Alimtazama Yusrah na kumsikiliza kwa makini hasa kuhusu mbinu ambayo angeweza kuitumia kurejesha amani ndani ya nyumba yake.

“Dawa ni moja tu Magesa asikudanganye mtu” Yusra alizungumza kwa upole.

“Ndio naitaka sasa” alisema Magesa kwa msisitizo.

“Utaweza lakini?”

“Nampenda sana mke wangu, lazima niiweze kwa namna yoyote ile” Magesa alizungumza kwa msisitizo.

“Inabidi utafute jiko la pili?” alizungumza Yusrah kwa sauti ya upole lakini iliyokuwa imejaa uzito.

“Unasemaje wewe?” Magesa wangu alihamaki aliposikia ushauri ule.

“Ninamaanisha uoe mke mwengine” Yusrah alizungumza kwa msisitizo.

“No! No! Siwezi Yusrah siwezi” Magesa alikataa kwa herufi kubwa

“Kwanini usiweze?”

“Kwasababu nampenda sana mke wangu”

“Tatizo ni kwamba bado umelala” Yusrah alizungumza huku akijiinua kutoka pale alipokuwa ameketi na kusimama pembeni kidogo. Alijishika kiuno na kujipinda kidogo upande mmoja.

“Unanionaje?” alihoji Yusrah huku akijitingisha tingisha kwa nyodo na maringo.

“Kivipi labda?”

“Kimvuto” Yusrah alijibu na kubadilisha pozi kama vile alikuwa anashindania urimbwende.

“Unaonekana mrembo na unapendeza sana” Magesa alimjibu.

“Thank you, unadhani sina sifa za kuwa mkeo?” Yusrah alihoji huku akimsogelea Magesa pale alipoketi. Alipeleka mkono wake hadi kwenye shingo ya Magesa na kuanza kumpapasa.

“Sifa za kuwa mke wangu unazo, lakini huwezi kuwa mkewangu” alisema Magesa kwa sauti ya upole lakini yenye msisitizo.

“Kwanini jamani Frank?” Sauti ya Yusrah ilibadilika na kuanza kutokea puani. Macho yake yalikuwa yamelegea mithili ya mtu aliyekunywa supu ya mlenda.

“Kwasababu Ninampenda sana mke wangu” Magesa wangu hakutaka masihara kabisa na ndoa yake, laiti wanaume wote wangekuwa kama yeye, wanawake tungejidai sana. Msema kweli mpenzi wa Mungu jamani, Magesa wangu alikuwa ananipenda sana. Aliutoa mkono wa Yusrah kutoka shingoni mwake.

“Usifanye hivyo tafadhari Yusrah”

“Nakupenda sana Magesa, sitaki kukuona ukiteseka kwaajili ya mapenzi. Nipo radhi kuishi na wewe kama mke na mume” Yusrah aliamua kufunguka mtoto wa kike.

“Wewe! si unafahamu kuwa dini yangu hairuhusu kuoa mara mbili? na hata kama ingekuwa inaruhusu nisingeweza kumsaliti mkewangu Priscaria, nampenda sana” Magesa alieleza kwa msisitizo.

Yusrah alionekana kuishiwa na nguvu pale alipokuwa amesimama. Alirudi kwenye kiti chake na kuketi huku akikwepesha macho yake kukutana na macho ya mume wangu. Mume wangu alijiinua na kuelekea msalani huku simu yake akiwa ameiwacha pale mezani.

Magesa alipotoweka tu machoni mwa Yusrah, simu ya mume wangu iliita. Yusrah akaichukua na kumtazama mpigaji. Alipoliona jina langu akakata simu. Simu ile ikaita tena lakini Yusrah hakuchoka kuikata. Alipoona bado inaendelea kupigwa alibonyeza kitufe cha kupokelea na kuipeleka sikioni utafikiri ilikuwa simu yake.

****

Moyo wangu ulishituka sana pale niliposikia sauti ya mwanamke ikipokea simu ya mume wangu. Nilijikuta nikijawa na ghadhabu kabla hata sijazungumza neno lolote. Ile ilikuwa ni mara ya pili mume wangu kumpa simu mwanamke anipigie. Sawa najua baadhi ya wasomaji mtaniambia kuwa nilikuwa na wivu wa kijinga lakini potelea mbali, ni mume wangu! hata nikimuonea wivu si ni mume kwangu?

“Hallo we nani?” Ile sauti ya mwanamke aliyepokea simu ya mume wangu ilisikika ikihoji kwa kujiamini.

“Naomba niongee na mwenye simu” Nilijibu kwa kifupi.

“Jibu swali kwanza wewe ni nani?” sauti ile ya kike ilizungumza kwa kulazimisha.

“Wewe unaniuliza ukiwa kama nani?” na mimi nilihoji kwa jazba. Kamtu kanapokea simu ya mume wako halafu kanakuuliza heti wewe ni nani? pumbavu!

“Mimi ni Fundi umeme” alizungumza yule mwanamke kwa kujiamini.

“Vizuri! ni hivi, mimi ni mke wa Magesa” Nilijitambulisha kwa hasira ili kumkera mtu yule niliyebaini kuwa alikuwa akiniibia mume wangu na kuniharibia mfumo mzima wa ndoa yangu.

“Ahaa mke wa Magesa, kwahiyo unashida gani?” alihoji yule binti kwa nyodo.

“Nipe mwenye simu bwana nizungumze nae wacha masihara”

“We zungumza shida yako, mwenye simu unamtaka wa nini?”

“Unasemaje we malaya?” nilijikuta nikihoji kwa hasira na jazba zaidi.


“Ni hivi, saa hizi tumepumzika, hatutaki usumbufu tukiwa kwenye starehe zetu. Tena ukome kupiga simu usiku. Nungunungu we!” Jamani nyie mwanamke yule alinitusi bila hata huruma na kukata simu. Alisahau kabisa kama namimi nilikuwa na roho kama yeye. Ah! haya bwana sasa ningefanya nini wakati mimi nilikuwa nimeshika kwenye makali na yeye ameshikilia mpini?

Niliitupa simu pembeni na mimi nikajitupia upande mwingine. Hapakuwepo na kingine zaidi ya kumwaga machozi. Nilitamani sana angetokea mwanaume wa kunifariji katika hali ile. Mtu ambaye alinijia akilini mwangu alikuwa ni shemeji Hashimu ambaye niliwahi kula naye tunda mara moja tu na kujikuta nikinogewa.

Sikujisikia kabisa kwenda viwanja siku hiyo. Kwa kuwa nilijua kuwa Fatuma alikuwa ni king’ang’anizi nikajisemea kuwa hata kama angekuja na greda jioni hiyo asinge ning’oa. Nikapanga kuwa nimtafute shemeji Hashimu usiku ule wakati Fatuma atakapokuwa viwanja. Wakati nikiendelea kuwaza hayo, simu yangu ya mkononi ikaita. Nilipoona namba ya Fatuma niliguna kidogo kisha nikaipokea.

“Hallo shost” Fatuma aliita

“Niambie Bestito” Nilijitahidi kukaza sauti ili Fatuma asinibaini kama nilikuwa ninalia ama nilikuwa na tatizo lolote.

“Uko poa wewe?” alihoji Fatuma

“Hofu kwako Shoga”

“Usihofu, mimi ni mzima kabisaaa”

“Haya lete jipya, ndio unataka kutoka nini?” Nilihoji huku nikiwa na hamu kubwa ya kutaka kusikia kuwa Fatuma alikuwa anatoka na kumuacha shemeji Hashimu Nyumbani.

“Jipya hakuna shoga. Ila leo utanisamehe” alisema Fatuma kwa sauti ya kusihi.

“Kwa yapi tena mwenzangu”

“Leo nipo na shemeji yako hapahapa nyumbani, kwahiyo sitakwenda viwanja” Fatuma alieleza kwa sauti ya upole.

Fatuma aliponiambia maneno yale nikajikuta nikihisi hali ya wivu ukinitafuna utafikili shemeji Hashimu alikuwa ni mume wangu mimi. Kwakweli nilibaini kuwa kumbe nilikuwa nampenda sana mwanaume yule aliyenionjesha tone la asali yake mara moja tu. Kiranga chote cha kutamani wanaume wa watu kilikuwa kimeniisha. Nikabakia kimya nikikosa hata la kuzungumza mtoto wa kike.

“Haloo” Fatuma aliita baada ya kutosikia sauti yangu kwa sekunde kadhaa.

“Enhee shoga nakusikia” nilijibu kwa kuhamaki.

“Vipi mbona kimya? au unahisi nimekutenga kwa kuto toka na wewe leo?”

“Usiwaze shoga, lakini msalimie sana shemeji yangu Hashimu” nilijibu kwa sauti iliyokuwa imejaa unyonge.

“Wee! usitake kunitia kichefuchefu kwa kunitajia hilo jina” Kilikuwa ni kitu cha kushangaza sana baada ya kutaja jina la Hashimu. Fatuma alibadilika na kuwa mkali kama mbogo aliyejeruhiwa.

“Kichefuchefu tena! we si umesema leo upo na shemeji nyumbani?” Nilihoji kwa mshangao.

Fatuma badala ya kunijibu nikamsikia akiangua kicheko cha kishambenga na chenye kujaa kebehi.

“Sasa unacheka nini?” nilihoji kwa sauti kavu ili kutia msisitizo.

“Siwezi kuwa na mwanaume kiwembe kama Hashimu. Nimekwisha mtimua na akafie mbele” Fatuma alizungumza kwa jazba utafikiri yeye mwenyewe alikuwa msafi. Alikuwa amesahau kama alikuwa na idadi kubwa ya wanaume waliokuwa wakishea penzi na Hashimu wa watu. Wahenga wanasema ‘mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu’ siku zote anamsaliti mwenzake, yeye kugundua kuwa amesalitiwa mara moja tu amekasirika.

“Kwahiyo unataka kusema mmeachana na shemeji Hashimu?” nilihoji swali ambalo jibu lake nilikuwa nishalifahamu.

“Hatuja achana bali nimemuacha”

“Mh! lakini Fatuma….”

“Hakuna cha lakini, habari ndiyo hiyo”

“Sasa huyo shemeji yangu utakayekuwa naye leo ni yupi tena?” nilihoji swali la mtego huku ndani ya moyo wangu nikiwa na matumaini makubwa ya kummiliki Hashimu.

“Kama kawa kama dawa. Kijitu kikileta ushenzi tupa kule, vuta kingine. Hivi nikwambiavyo nina dume la nguvu linaitwa Ashrafu. Chezea mimi wewe!” Fatuma alizungumza kwa kujitapa. Nikajisemea potelea mbali kwanza ndio vizuri ili niweze kuwa huru zaidi na Hashimu wangu. Ukisema wa nini mwengine anasema nitampata lini.

“Duh! we mkali” nilimsapoti kinafki huku ndani ya moyo wangu nikiwa na furaha ya kuwa huru na shemeji Hashimu. Kabla hatuja maliza mazungumzo na Fatuma nilikata simu na kujirusha kitandani na kukumbatia mto huku nikilitaja jina la Hashimu kwa kulirudiarudia. “Magesa na Fundi umeme, Prisca na Hashimu, Fatuma na Ashrafu, ngoma droo” Nilizungumza nikijihalalishia jambo lile la kutembea na shemeji Hashimu.

******

Magesa alipotoka msalani alikuwa na rundo la hasira dhidi ya Yusrah. Hakuamini kama mwanamke yule aliyekuwa akimtegemea kwa kiasi kikubwa kujenga ndoa yake angekuwa ni miongoni mwa maadui wa ndoa hiyo. Alimkuta Yusrah ameketi huku ameshikilia glasi ya juisi yake.

“Vipi mpenzi mbona umechelewa?” Yusrah alihoji kwa sauti yake ile ya kutokea puani. Magesa hakumjibu kitu zaidi ya kumkodolea macho makali msichana yule.

“Baby, si ninakuuliza wewe jamani?”

“Sikutegemea Yusrah” alisema magesa kwa hasira.

“Najua hukutegemea kupendwa na mrembo kama mimi” alisema Yusrah maneno ambayo yalizidi kumtia hasira Magesa.

“Sikiliza wewe mwanamke, siwezi kumsaliti mke wangu” alizungumza Magesa kwa msisitizo.

“Mke wako?”

“Ndio my wife, her name is Priscaria. Nampenda sana, sijawahi kufikiria kumsaliti hata siku moja!” Magesa alizungumza kwa msisitizo.

“Hivi wakiambiwa wenye ndoa watoke na wewe utatoka?” Yusrah alizidi kumtia hasira Magesa wangu.

“Nimegundua kumbe wewe sio mtu” Magesa alizungumza maneno ambayo yalimfanya Yusrah kuangua kicheko. Alicheka kwa kitambo huku Magesa akimkodolea macho kwa mshangao.

“Kwahiyo mimi kama sio mtu ni nani?” alihoji Yusra huku akimalizia kucheka kwa kujifuta machozi yaliyotokana na kicheko kile.

“Sijui nikuite nani, kila jina baya nikikupa litakuwa zuri” Magesa alizungumza kwa hasira huku akichukua simu yake iliyokuwa mezani na kuitia mfukoni.

“Niite Mchuchu!” Yusrah alizungumza huku akitabasamu kinafki.

“Achana na mimi shetani mwitu we! na usiendelee kunifuata fuata nitakutoa roho!” Magesa alizungumza huku akimuoneshea kidole cha kumpa onyo msichana yule aliyekuwa akitishia usalama wa ndoa yetu mimi na Magesa.

“Nakupenda sana Magesa, siwezi kukuacha” Yusrah anaye alizungumza kwa mkazo mwanamke yule. Jamani nyie kuna wanawake wamekatika mishipa ya aibu! Sasa kumng’ang’ania mwanaume wa mwenzio ndio nini? kwani duniani kooote huko amekosa wanaume hadi kumng’anga’nia mume wangu mimi. Mwanamke alikuwa hasidi yule! Hata hivyo katika ndoa kunahitajika msimamo, namsifu sana mume wangu kwa kuwa na msimamo katika ndoa yetu. Na nyie wanaume wengine basi igeni msimamao wa mume wangu jamani.

“Binti, cheza na mimi na usicheze na ndoa yangu” Magesa alizungumza na kuondoka kwa spidi akimuacha Yusrah hasidi wa ndoa za watu akimkodolea macho. Aibu ilikuwa imemvaa binti yule aliyeamua kujibadilisha mavazi ili kumtega mume wangu, laana na impate huko aliko.

****

Nikiwa nimejilaza chali kitandani baada ya kuzungumza na mwanamke kupitia simu ya mume wangu na kuishia kuporomoshewa matusi. Nilijiona ni mwanamke mmoja mwenye mikosi na gundu hapa ulimwenguni. Sikujua hata mume wangu alikuwa amepatwa na kitu gani kilichokuwa kimembadilisha kiasi cha kunifanyia mambo ya ukatili kiasi kile.

Kila kulipokucha mume wangu alikuwa akinifanyia visa na vituko. Mara meseji za mapanzi kutoka kwa Fundi umeme, mara simu za ajabu ajabu kutoka kwa Abiria, mara sijui Afumaniwe na kuandikwa kwenye magazeti. Yaani vituko! Vituko! Vituko kila kulipokucha.

Sawa pamoja na vituko uchafu wote huwo bado mtu unaamaua kutupilia mbali na kurejesha moyo ili tuishi kama zamani, bado simu zako anapewa Malaya wake azungumze na wewe! Kweli jamani ni haki hiyo? Ama kweli ndoa ndoano! Wale wenzangu mnaoishi kwa amani na furaha katika ndoa zenu ombeni sana na kusali yasije yakawafika mamitihani kama yaliyokuwa yakinikabili mimi.

Pamoja na kwamba siku hiyo nilikuwa nimeponea kwenye tundu ya sindano kupoteza maisha yangu. Unafikiri yule mwanamke wa Bob Mbasa angenitia mikononi mwake na lile bisu lake ni nini kingetokea? Saa hizi ningekuwa mochwari kama sio chumba cha wagonjwa mahututi.

Kitendo cha kumpigia simu mume wangu na kupokea mwanamke kisha akaniogesha matusi kilinifanya nisahamu tukio lile la kutaka kutolewa roho na mke wa yule Bob Mbasa. Nikajikuta nikitamani kampani ya shoga yangu Fatuma kwenda naye viwanja kuponda raha na kusahau shida zote zile za kusalitiwa. Hata hivyo nisingeweza kutoka na Fatuma siku hiyo kwasababu tayari alinieleza kuwa alikuwa na mwanaume wake nyumbani kwake siku hiyo hivyo asingeweza kutoka.

Nilitamani sana ningekuwa na shemeji hashimu siku hiyo lakini bahati mbaya sikuwa na namba zake za simu. Mara nyingi sana mwanaume yule alikuwa akichukua namba yangu ya simu kwenye simu ya Fatuma alkini alipojaribu kunipigia, nilimjibu mbovu na kufutilia mbali namba zake. Sasa siku hiyo nilitamani sana kuwasiliana naye lakini sikuwa na namba za mwanaume yule aliyetokea kuukonga mtima wangu.

Potelea mbali liwalo na liwe, nikajisemea na kujiinua kutoka pale kitandani na kujiandaa tayari kwa kwenda viwanja. Nisingeweza kabisa kulala pale nyumbani kutokana na hasira nilizokuwa nazo. Mwanamke wa Magesa alikuwa ameutibua ubongo wangu kwa kiasi kikubwa siku hiyo. Tena bila hata aibu anasema kabisa “mimi FUNDI UMEME” Pumbavu kabisa na umeme wako unaotaka kumuambukiza mume wangu.Nilijisemea mwenyewe huku nikiendelea na maandalizi ya kutoka mtoto wa kike.

Siku hiyo nilikwenda Vijana-Social, kulikokuwa na tamasha moja la kukata na shoka.



***


“Weee! Weee! Ishia hapo hapo! Shoga tena unikome! Laana zako peleka hukoo kwa Malaya wenzio!” Jamani nyie mtoto yule alinitukana utafikiri tulikuwa tunalingana.

Nakwambia mwanamke likanishuka na kuwa mdogoo kama kipande cha kidonge cha piriton. Sasa sijui hata ningeomba vipi huwo msaada kwasababu hata simu yangu pia ilikuwa imeibwa na yule Sharobaro.



“Niazime basi simu yako” nikazungumza kwa upole.

“Ya nini?”

“Nataka nimpigie mtu anitumie pesa” nikazunguma kwa huruma zaidi.

Binti yule alinitazama kwa sekunde chache kisha akatikisa kichwa chake kusikitika. Aliingiza mkono kwenye droo na kunikabidha simu yake.

Nilipokea simu ile na kujaribu kukumbuka namba za Fatuma kisha nikapiga. Nikashukuru mungu kwani baada ya nusu saa Fatuma alifika na kunilipia pesa zote nilizokuwa nikidaiwa. Kwakweli nilijikuta nikiichukia sana pombe. Nikasema wacheni pombe iitwe haramu jamani.

Kuanzia asubuhi ya siku hiyo nilikuwa vibaya sana. Nilijikuta nikiichukia tabia ile niliyokuwa nimeianzisha heti mwenyewe nikidhani nilikuwa namkomesha mume wangu Magesa. Masahibu yaliyonifika usiku yalitosha kunifanya nijifunze kitu. Nilishinda nimelala kuanzia asubuhi niliporudi kutoka viwanja hadi kwenye mida ya saa kumi na moja jioni. Nilishindwa hata kula kwa mawazo. Moyo wangu ulikuwa ukilia na kujuta ndani kwa ndani. Nimetumiwa kimwili, nimeibiwa pesa, maneno machafu nikatemewa na watoto wadogo, jamani nyie!

Nilianza kuamini yale maneno waliyokuwa wanasema kuwa asiyefunzwa ma mamaye hufunzwa na ulimwengu. Hatimaye na mimi niliona wazi ulimwengu ulikuwa umenifunza. Kuanzia siku hiyo nikasema mimi tena basi, nilikuwa nimechoka kushindana na mtu hala maumivu na mateso nayapata mimi.

“Magesa mume wangu, naomba urudi tuishi pamoja! Mimi sihitaji tena kugombana na wewe mume wangu. Nakupenda sana, Fatuma ndiye aliyenipotosha mume wangu!” nilizungumza na kujilaza kitandani huku nikilia kwa kwikwi na uchungu mwingi.

****

Kitendo cha mume wangu Magesa kumzingua Yusrah kwa kumtukana na kumkataa kimapenzi kilimuuma sana huyo binti Yusra. Nafikiri katika maisha yake hakuwahi kukutana na mwanaume aliyekuwa rijali akamkataa. Mara zote yeye ndiye aliyekuwa akiwakataa wanaume, lakini kwa mume wangu Magesa alijikuta akigonga mwamba.

Binti yule alikuwa amenyongo’nyea viungo vya mwili na kujikuta akishindwa kufanya jambo lolote lile. Aliumia sana kukataliwa na mume wangu. Kitu ambacho kilimuumiza zaidi ni maneno ya mwanaume yule kumueleza kuwa alikuwa na mke na anampenda sana.

Hata hivyo binti Yusrah hakukata tamaa hasa alipokumbuka ule usemi unaosema kuwa mtafutaji hachoni, na akichoka basi amepata. Hivyo alijipa moyo na kuendelea kumsumbua mume wangu huku akiamini siku moja ilikuwepo kwaajili yake.

Alijaribu sana kupiga simu ya mume wangu lakini hakupata nafasi kwani simu ilikatwa na ilipopokelewa aliishia kutukanwa kama mtoto mdogo. Mwanamke yule aliamua kutinga ofisini kwa mume wangu.

Aligonga mlango wa ofisini kwa mume wangu mara mbili kisha akaingiza kichwa kuchungulia. Macho yake yaliweza kumuona Magesa akiwa ameegemea kiti huku macho yake yakiwa juu yamefumbwa.

Yusrah alitembea kwa kunyata hadi pale alipokuwa amesinzia mume wangu. Alimtazama kwa sekunde kama tatu hivi huku akiachia tabasamu la matumaini.

“Kumbe huyu mwanaume akilala ndio anazidi kuwa mzuri” alijisemea Yusrah huku akimeza funda la mate ya tamaa.

Jamani nyie kuna wanawake wengine hawajaumbwa na haya wala aibu! Yusrah aliinama na kupiga busu midomo ya mume wangu aliyekuwa usingizini.

Masikini Magesa wangu alishituka kutoka usingizini baada ya kile kitendo cha Yusra. Mume wangu hakuweza kuamini kile alichokuwa anakiona kwenye macho yake.

Alifikicha macho yake na kumtazama kwa makini Yusrah.

“We mwanamke!” Magesa alizungumza kwa kuhamaki.

“Mtu pekee anayeweza kukuliwaza ni mimi mpenzi wangu” Yusrah alizungumza kwa ile sauti yake ya kujishebedua.

“Hivi unanitafuta nini wewe mwanamke?”

“Nakupenda Frank, unauliza swali ambalo jibu lake unalifahamu”

“Samahani mimi sio Frank”

“Wewe ni Frank”

“Okay nikusaidie nini?”

“Shida yangu ni hii moja, ukinisaidia tu mimi naondoka” Yusraha alizungumza kwa msisitizo.

“Unataka nini?”

“Yani kama ukinibusu tu, mimi naondoka sina ugomvi na wewe” Yusrah alizungumza.

“Wewe utakuwa umerogwa wewe, haki ya mama vile wewe umerogwa. Tena nahisi unaugua zongo” mume alizungumza kwa sauti ndogo lakini yenye maneno ya kebehi.

“Magesa unajua mimi sio chizi wala mwenda wazimu. Nafanya yote haya kwasababu nakupenda Magesa” Yusra akazungumza kwa msisitizo huku akijifanya kama vile alikuwa anataka kulia.

“Hakuna chizi anayejikubali kama yeye ni chizi, hata kama akielezwa kuwa yeye ni chizi bado hawezi kukubali” Mume wangu alizungumza kwa msisitizo.

“Sawa yote hayo mimi nayakubali, lakini tambua kuwa nakupenda”

“Asante kwa kunipenda” alizungumza Magesa.

“Nakutaka pia!” binti yule akazungumza kwa msisitizo na sauti ya juu.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG