Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

MESSAGE YA FUNDI UMEME - 1

  


IMEANDIKWA NA : KIZARO MWAKOBA

*********************************************************************************

Chombezo : Message Ya Fundi Umeme 

Sehemu Ya Kwanza (1)


SEHEMU YA KWANZA


Kwa jina naitwa Priscaria, nilikuwa ni mke wa kijana mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Magesa. Tulikuwa tukiishi maeneo ya Kimara jijini Dare Salaam. Nilikuwa nikimpenda sana mume wangu naye alikuwa akinipenda pia. Kwa ufupi naweza kusema kuwa tulikuwa tukipendana sana. Tuliishi kwa raha na amani ndani ya ndoa yetu kwa kipindi kirefu huku kila mmoja akiwa na imani juu ya mwenzake.

Nakumbuka ilikuwa ni siku ya Jumamosi ambayo ilikuwa bado imetawaliwa na kigiza ambacho kilikuwa kikikaribisha jua la asubuhi. Niliamka na kupeleka macho yangu ukutani kuangalia saa. Ilikuwa imetimia saa tisa na robo Alfajiri. Niliteremka kitandani na kusimama pembeni huku nikijinyoosha viungo vya mwili wangu na miayo mfurulizo.

Nilisogea hadi usawa wa Kioo cha kabati la nguo ili kujitazama jinsi nilivyo umbwa na Mwenzezi Mungu. Kwanza kabisa nilijiangalia usoni ambapo niliweza kuyaona macho yangu yaliyo makubwa kidogo jinsi yalivyo kuwa yamelegea. Nilikuwa nikiyapenda sana macho yangu kiasi ambacho nikashindwa kujizuia kutoa tabasamu la amani ambalo lilipelekea mashavu yangu kuponyea kwa pembeni, wengi wanaita dimpoz. Meno yangu madogo yaliyo kuwa yametenganishwa na mwanya mdogo kati kati nayo yalionekana kutokana na lile tabasamu langu lililokuwa na mvuto. Nikapeleka mkono kuikuna pua yangu iliyo kuwa imechongoka kidogo kama pua ya msomali.

Niliyashusha macho yangu hadi kwenye usawa wa kifua changu kupitia kioo kile. Niliweza kuyaona jinsi matikiti yangu ya kifuani yalivyo kuwa yametuna kidogo yakikaribia kutoboa night dress yangu niliyo kuwa nimeivaa. Rangi nyeupe ya ngozi yangu iliweza kuonekana vyema juu ya nguo hiyo ya kulalia.

Macho yangu yaliendelea kuteremka hadi usawa wa kitovu. Tumbo langu la wastani ambalo halikuwa dogo sana na pia halikuwa kubwa kiasi cha kuchukiza lilikuwa limepambwa kwa kishimo kidogo cha kitovu.

Nilijigeuza upande na kuweka mkono wangu wa kushoto kiunoni. Mungu alikuwa amenijaalia nyonga iliyokuwa imetanuka vyema kiasi cha kuweza kuubeba mzigo wa madafu mawili uliokuwa ukining’inia chini ya kiuno changu kwa nyuma. Nilivuta hatua kadhaa na kuweza kuona jinsi ambavyo mzigo ule ulivyokuwa ukienda sawa na hatua za miguu yangu. Madafu yale mawili yalikuwa yakidondoka moja moja huku yakipishana kwa zamu.

Mboni za macho yangu hazikuishia hapo, niliziteremsha tena hadi sehemu za kwenye mapaja yangu. Mguu wangu wa kushoto niliuinua kidogo na kuusimamisha kwa vidole. Niliivuta nguo yangu ya kulalia taratiibu kwa mkono wangu wa kushoto huku mkono wa kulia nikiwa nimeupachika kiunoni kwa nyuma. Mapaja yangu yaliyo kuwa yamenona na yenye ngozi laini yalinipa faraja ndani ya moyo wangu na kujiona kama vile ni mwanamke wa pekee hapa ulimwenguni ambaye nilikuwa nimependelewa katika uumbaji. Baada ya kujipapasa kwa sekunde kadhaa, mikono yangu yote miwili ilihamia kichwani ambako ilizikamata vyema nywele zangu ndefu na kuzilazia kwa nyuma. Nywele zile ziliponigusa maeneo ya shingoni nilihisi msisimko jambo ambalo lilinifanya nifumbe macho kuisikilizia hali ile.

Niligeuka nyuma na kumtazama mume wangu Mr. Magesa ambaye alikuwa kati kati ya usingizi huku amelala chali. Niliweza kukiona kifua chake kilicho kuwa na nywele nyingi jinsi kilivyo kuwa kimetanuka kisawa sawa kutokana na mazoezi aliyo kuwa akiyafanya mara kwa mara. Nilipeleka macho yangu hadi kwenye mikono yake na kuiona jinsi ilivyo kuwa imejazia vizuri. Taratiibu macho yangu yaliteremka hadi kwenye tumbo lake dogo lililokuwa limegawanyika sehemu nne zilizokuwa zimekaza kiasi cha kuleta mvuto. Tumbo lile la kuvutia lilipokea nywele zilizokuwa zimeanzia kifuani na kumalizikia chini ya kitovu. Nilijikuta mwili wangu ukisisimka kiasi cha kuleta mtetemeko. Nilipanda kitandani kwa haraka na kwenda kumparamia Magesa. Midomo yangu ikanata kwenye dafu lake moja la kifuani na kuanza kulinyonya. Wakati mdomo wangu ukinyonya dafu lile la upande wa kushoto vidole vya mkono wangu wa kulia vilikuwa vikicheza na ncha ya dafu lake la kulia.

Magesa alikuwa kama vile amenitegea kwasababu hakuchelewa kujibu mashambulizi. Wakati mimi nilipokuwa nikicheza na madafu yake, yeye alipeleka mikono yake kwenye mzingo wa madafu yangu ya nyuma na kuanza kucheza nao. Magesa alikuwa fundi sana wa kucheza na mzigo wangu kiasi ambacho alinifanya nami nifurahie. Nilipeleka midomo yangu hadi kwenye lipsi zake na kuzinasa kama sumaku. Nilimsikia Magesa akiguna kama vile alikuwa amebebeshwa gunia zito la chumvi kichwani kwake.

Bila kutegemea niligeuzwa kama vile kipande kidogo cha chapati na kuwekwa chini. Magesa akaja juu huku mimi nikitapatapa kawa vile nilikuwa nimepatwa na kifafa.

Magesa alipojaribu kuinama tu nilimdaka na kumvutia chini. Kwakuwa alikuwa hakujiandaa alikuja mzima mzima na kudondokea kwenye madafu yangu ya kifuani na kubonyeza ncha zake jambo ambalo lilinisababishia michomo fulani ya utamu wa kipekee.

“Oomnh!” Nilijikuta nikilalamika kwa sauti iliyo tokea puani.

Mikono ya Magesa ilikuwa shapu sana kama sumaku, mara moja ilikwenda kukamata maenea ya jirani na malkia na kucheza nayo kiufundi.

“Aaaoo!...Eshssss….Omnhm!” Nilitoa sauti ambazo hata mimi mwenyewe sikuzielewa. Wakati vidole vya mkono wa kushoto wa Magesa vikifanya mashambulizi karibu na ngome ya malkia wangu, ulimi wake ulikuwa ukizisabahi ncha za madafu yangu ya kifuani. Jamani nyie Magesa!

“Ngoj…kwa..mage…Ooo….yeah!...camoon…like…that!...Omnh!” Nilishindwa kujizuia kulalamika mtoto wa kike tena kwa lugha ya kimombo. Katika maisha yangu ya kimahaba sikuwahi kukutana na mwanaume kama Magesa, hadi hivi ninavyo zungumza sasa hivi. Kuna wanaume wamebarikiwa jamani! nyie acheni tu.

Hata hivyo nami sikujilegeza kiasi cha kumkatisha tamaa mwanaume wangu, kwa kutumia viungo vya mwili wangu ambavyo nimezawadiwa na muumba nili jitahidi kumpagawisha mwanamume yule. Basi kama kuna mtu alikuwa anapita karibu na dirisha la chumbani kwetu basi siku hiyo alifaidi sana kutokana na sauti zilizokuwa zikitoka chumbani mle.

“Priscssss….Aaaah…No…ommnh” Nilimsikia mwanaume akilalamika utafikiri mtoto wa kike pale nilipo jaribu kupeleka mkono wangu karibu kabisa na ngome ya mfalme pimbi.

“Osshsscccs…..yeah…I like it…do it again….Ooooyeah!” na mimi nikajikuta nikilalamika mwenzenu, wahenga wanasema ncha ya mkuki haipigwi kwa konzi. Kitendo cha mimi kucheza karibu na ngome ya watu kimeniponza kwani Magesa aliweza kufanikiwa kuilinda ngome yake kwa kombora moja takatifu lililofumua kila kitu kwenye ngome ya malkia wangu kiasi cha kumfanya ashindwe kujizuia kutapika mfurulizo kutokana na kiwewe cha makombora ya mume wangu kipenzi.

“Taya…tay…oomnh…Ndiba mume…nipe…wa…bas...ngu…” Nilijikuta

nguvu zikiniishia na kuzungumza lugha ambayo hata mimi mwenyewe sikuielewa, lakini nahisi Magesa aliielewa kwani nilimsikia akijibu.

“Nakupa Prisca wangu nakupa” Majibu ya Magesa ndiyo yaliyo nifanya nifahamu nilikuwa nazungumza nini. Kumbe nilikuwa nataka kupewa haki yangu ya kumiliki himaya ya mfalme Pimbi.

“Oooh…sas..chelew…bona…mpenzi?” Nilizungumza kwa taabu na sauti ya chini sana iliyo tokea puani kama vile nilikuwa mgonjwa mahututi niliyekuwa nakaribia kukata roho. Kiukweli nilikuwa mahututi kiasi cha kutamani matibabu ingawa tabibu wangu pekee niliyekuwa nikimtegemea alikuwa ni mume wangu kipenzi Magesa.

Jamani nyie mwenzenu hapa sasa ndipo alipokuwa akinikera mwanaume yule. Yaani chakula kilikuwa kimekwisha iva kiasi cha kutosha kuliwa lakini yeye alikuwa hasikii wala haoni na kuendelea kupika. Nikajikuta nimeishiwa nguvu kiasi cha kushindwa hata kuomba msaada kwa njaa niliyokuwa nayo. Viungo niliviona vizito, macho yalinilegea zaidi ya pale nilipokuwa nikijitazama kwenye kioo, mapigo ya moyo yakabadilika na kuongezeka kasi nikawa napumua nusu nusu. Nilikuwa kama vile kitimoto aliyepigwa marungu na kulala chini akisubiria kisu kiingie shingoni mwake.

Kuzima kwangu ndiko kulikuwa ahuweni yangu, jamani nyie mwanaume yule. Hiyo ndiyo ilikuwa kawaida yake kila tulipokutana kwenye kumi na nane zetu, lakini mie nasema afadhali na Magesa wangu ambaye anapika chakula kwa muda mrefu na kuchelewa kula, kuliko ukutane na mianaume miroho na mivivu ambayo inajua kula tu, haina haja ya kupika wala kuandaa chakula mezani kwaajili ya kuliwa.

Magesa alitumia ujuzi wake alio upata kutoka kwa babu yake kama mwenyewe alivyokuwa akiniambia mara kwa mara. Aliniinua kidogo na kuniweka usawa wa kifua chake, na mimi kwakuwa sikuwa mgeni wa mkao ule wa kula aliokuwa anataka kuniweka nikampa ushirikiano. Mara nyingi kwenye chai ya asubuhi alikuwa akipendelea sana nikae mkao ule kwasababu alifahamu kuwa nilikuwa mbovu sana na sikuchelewa kushiba. Jamani nyie katika wanaume walio kuwa wamebarikiwa, Magesa alikuwa zaidi. Aliweza kukamata usukani vyema na kwenda kwa spidi ile ambayo abiria wake ingemfurahisha. Kwenye mabonde aliweza kupunguza mwendo na kwenye tambarare aliyakanyaga mafuta ipasavyo. Kwa mkao ule aliokuwa amenichagulia mume wangu mpenzi, hakupata tabu kunituliza mapepe. Ndani ya nusu saa tu mambo yote yalikuwa sawia kabisa.

*****

Mlio wa simu ya mume wangu ndio ulio nigutusha kutoka usingizini na kunifanya nikurupuke kama mwizi pale kitandani. Saa ya ukutani ilikuwa ikionesha kuwa ilikuwa imekwisha fika saa kumi na mbili asubuhi. Nilichukua simu ya mume wangu ambayo ilikuwa bado ikiita na kuiangalia. Niliona jina la mpigaji kuwa ni FUNDI UMEME.

“Mpenzi amka utachelewa” nilimuamsha mume wangu kwa upole. Alipoamka alishituka sana alipoona kuwa imefika saa kumi na mbili.

“Mungu wangu! nimechelewa” Alisema Magesa kwa kuhamaki.

“Simu yako hiyo inaita” Nilimwambia huku nikimkabidhi ile simu

“Ni nani?”

“Sijui” Nilijibu na kujifanya sikuiangalia.

Aliichukua na kuiweka usawa wa macho yake. Baada ya kuiona namba ya mpigaji aliachia msonyo kuikata.

“Vipi mbona unamkatia simu” Nilihoji ingawa sikuwa na hata chembe ya wasiwasi kutokana na kitendo kile cha kukata simu mbele yangu.

“Ah! Fundi Umeme huyo ananisumbua sumbua. Simu gani za saa hizi?” Magesa alizungumza huku akiiweka simu ile kitandani na kusimama pembeni. Wakati akijinyoosha nyoosha viungo vyake vya mwili, ile simu iliita tena.

“Hebu angalia ni nani anayepiga?” aliniambia huku akiinama chini kwaajili ya kupiga pushup.

“Fundi Umeme” nilimjibu mara baada ya kuiangalia simu ile.

“Achana naye mpumbavu tu huyo”

“Labda kuna tatizo, we si umsikilize tu” Nilimwambia mume wangu kwa sauti ya upole na upendo.

“Hana jipya huyo, anataka hela tu”

“Mie napokea” Nilimwambia mumewangu huku nikitaka kuipokea ile simu. Nikamuona anashituka na kuja hadi pale nilipokuwa nimesimama. Hakuongea kitu chochote na kuichukua simu yake kisha nikamuona huyo anaelekea bafuni. Nilishangazwa na kitendo kile lakini nikaamua kutupilia pembeni kwasababu nilikuwa nikimuamini sana mume wangu.

****

Baada ya lisaa limoja wote wawili mimi na Magesa tulikuwa tumependeza sana. vijana wa siku hizi wange kwambia tulikuwa tumetokelezea. Ilikuwa ni siku ngumu sana kwangu kwasababu mume wangu kipenzi alikuwa akisafiri kwenda jijini Arusha kikazi ambako angekaa huko kwa muda wa wiki mbili nzima. Roho ilikuwa ikiniuma sana na kujawa na unyonge.

“Usijali mke wangu nitarejea tu” Magesa alinibembeleza

“Nakupenda sana mume wangu kuwa makini huko uendako” nilizungumza kwa sauti iliyokuwa imejaa huruma. Mume wangu aliendelea kunibembeleza na kunihakikishia kuwa angenikumbuka muda wote atakapokuwa kazini na kusingekuwa na tatizo lolote.

Wakati wa kutoka ulipofika Magesa alikwenda msalani na kuacha simu yake kitandani. Iliingia meseji ambayo ilikuwa imetumwa na yule Fundi Umeme. Nilijikuta nikimuonea huruma sana mtu yule ambaye tangu asubuhi alikuwa akipiga simu lakini haikuwa inapokelewa na mume wangu. Lakini nilipoifungua meseji ile sikuweza kuamini macho yangu.

“VIPI DARLING UTAONDOKA NA GARI GANI? NAKUSUBIRI KWA HAMU NIMELIMISI PENZI LAKO. LOVE U MWAAAAH!” Hivyo ndivyo ilivyokuwa imeandikwa meseji ile. Nilihisi nikiishiwa nguvu na kujiwa na duku duku rohoni. Sikuweza kuamini kama mume wangu Magesa angeweza kufanya mabo ya kifirauni kama yale. Nikaunganisha na tukio la mwanzo la kuninyang’anya simu na kwenda kuzungumzia chooni.

Nilijikuta nikitetemeka kwa wivu. Huku nimeishikilia mkononi simu ya mume wangu nilikuwa nikitembea tembea kwa kupiga piga miguu chini kwa hasira kuzunguuka chumbani mle. Kama kulikuwa na mtu ananiangalia ni lazime angehisi nilikuwa nimepandwa na kichaa



Nilihisi nikiishiwa nguvu na kujiwa na duku duku rohoni. Sikuweza kuamini kama mume wangu Magesa angeweza kufanya mabo ya kifirauni kama yale. Nikaunganisha na tukio la mwanzo la kuninyang’anya simu na kwenda kuzungumzia chooni.

Nilijikuta nikitetemeka kwa wivu. Huku nimeishikilia mkononi simu ya mume wangu nilikuwa nikitembea tembea kwa kupiga piga miguu chini kwa hasira kuzunguuka chumbani mle. Kama kulikuwa na mtu ananiangalia ni lazime angehisi nilikuwa nimepandwa na kichaa.

ENDELEA….

Niliposikia hatua za Magesa zikikaribia mlangoni, ile simu niliiweka kitandani kwa kuifunika ili asigundue kama ilikuwa ikitumika muda ule kisha nikajikausha kama vile hakuna jambo lililokuwa limetokea.

“Vipi wife upo tayari tuondoke?” Aliniuliza mara tu alipoingia chumbani. Nami nikamjibu kwa kichwa kuwa nilikuwa tayari, sikuweza kuzungumza kutokana na hasira ambazo nilikuwa nazo.

Hata hivyo pamoja na kujikausha na kujibaraguza lakini Magesa aliweza kunigundua kama sikuwa sawa.

“Vipi mbona upo hivyo! Kuna tatizo?” Magesa alihoji baada ya kunishitukia sikuwa sawa.

“Hakuna tatizo” Nilimjibu kwa taabu na kujikuta nikiangua kilio ambacho kwa muda mrefu nilikuwa nikijizuia.

Waha masihara ndugu msomaji, usiombe ukakutana na mazingira ambayo nilikuwa nimekutana nayo mimi siku hiyo. Mapenzi, tena mapenzi ya ndoa! Mungu wangu unaweza ukajikuta unaokota makopo jalalani bila kukusudia.

Kile kilio changu cha kwikwi kilichotokana na hasira pamoja na maumivu ya kusalitiwa penzi langu kilimchanganya sana mume wangu Magesa. Heti alinikumbatia na kuanza kunibembeleza huku akihisi nilikuwa nalia kwasababu alikuwa anasafiri na kuniacha peke yangu.

“Hapana mke wangu usilie, mimi nitarudi. Naenda kwaajili ya maisha yetu mimi na wewe, nakupenda sana Priscaria jikaze mke wangu” Magesa alizungumza maneno ambayo yalikuwa yakizidi kunipandisha hasira.

Niliinua macho yangu na kumtazama kwa umakini sana usoni. Taswira ya unafki udhandiki na usalini ndiyo niliyokuwa naiona imetawala kwenye sura yake. Nilikuwa tayari nimekwisha kumshitukia kuwa alikuwa ni mnafiki na muongo, pumbavu kabisa!

Yani pamoja na mapenzi yote yale moto moto niliyokuwa nikimpatia lakini mwanaume hakuridhika hadi kutafuta na mafundi umeme wa kumkamilishia dozi yake. Ama kweli wanaume sio watu wazuri.Utanisamehe sana msomaji wangu lakini Magesa ndiye aliyenifanya nizungumze yote haya.

Hata hivyo niliamua kujikaza na kuchukua begi lake na kutoka nalo nje kwaajili ya kumsindikiza kama ilivyokuwa imepangwa. Nililiingiza begi kwenye gari ndogo ambayo ndiyo niliitumia kumsindikizia mumewangu Ubungo. Njia nzima Magesa alikuwa akiendesha gari huku akinibembeleza.

“Usilie mke wangu, unajua naweza nikapata ajali kama ukiendelea kuli!” alizungumza Magesa kunishawishi nisiendelee kulia.

Pumbavuuu! Heti naye anaogopa kufa! Tangu lini wazinzi wakaogopa kufa? Kama angekuwa anaogopa kufa si angetulia na mke wake wa ndoa? Akikushika anajifanya mtaalaaamu wa mapenzi kumbe fuska kama yeye hakuna. Nikajisemea bora afe tu wala asirudi tena. Shenzi! Laana mjaa laana aliyeshindikana na Subuhana!

Kwa jinsi ambavyo nilikuwa nimemchukia mume wangu sikuwa natamani hata kusikia sauti yake. Kila alipokuwa akinisemesha nilikuwa nahisi kichefuchefu na kutaka kutapika. Kama ingekuwa ni amri yangu ninge muamuru anyamaze hadi mwisho wa safari yetu.

Nilitulia kimya hadi tulipofika kwenye kituo cha mabasi yaendayo mikoani. Tulipaki gari na kuteremka kuelekea yalipo mabasi ya kwenda jijini Arusha. Magesa aliukamata mkono wangu na kuushika kama ilivyokuwa kawaida yetu tulipokuwa tukitembea pamoja. Nilihisi kiganja cha mkono wa Magesa kikinichoma choma utafikiri kilikuwa na misumari. Nikatamani kujichomoa kutoka kwenye mkono wa mume wangu lakini nikaendelea kumuomba Mungu anipe moyo wa ujasiri.

Mara zote tulipokuwa tukitembea huku tumeshikana mikono tulikuwa na kawaida ya kuangaliana usoni huku tukizungumza na kucheka. Watu wengi waliokuwa wakituona walitamani sana ile staili yetu yamaisha.

Hali ya siku hiyo ilikuwa tofauti kabisa nasiku zote. Sura yangu ilikuwa imefura kwa chuki, ghadhabu na hasira. Macho yangu yalikuwa mbele na sikutamani kumuangalia Magea usoni hata kidogo. Sura yake nilikuwa naiona kama vile anafanana na nyumbu wa kule Serengeti.

“Siku zote huwa una hudhuni nikiondoka, lakini leo mke wangu umetia fora" Magesa alizungumza tulipokuwa tunatembea.

“Kawaida tu” nikajitahidi kujibu.

“Kawaida wapi mke wangu leo umekasirika utafikiri naenda kufa huko!” alizungumza Mageza kwa sauti ya kubembeleza.

“Aah huwa sipendi kuwa mbali na wewe” nikazungumza kwa kuongopa.

“Lakini nitarudi mke wangu” Magesa alizungumza kwa upole.

Tulifika kwenye basi la Air Bus na kukata tiketi. Magesa alinigeukia na kunishika kwenye mashavu. Ile mikono yake ilikuwa bado ikinichoma choma hata kwenye mashavu yangu. Sijui hata imekuwaje maana siku zote nilikuwa nasisimka na kufurahi kila nilipokuwa nashikwa na mume wangu.

“Nakupenda sana mke wangu, Tambua uko pekeyako na nitakulindia penzi lako” Magesa alizungumza bila hata haya.

Maneno yake yale yalizidi kunipandisha hasira na kujikuta nikianza kutetemeka. Heti niko peke yangu na atanilindia penzi langu! Hivi wanaume wote wapo kama huyu mume wangu mimi au ni yeye tu ana laana? Ee Mungu muone kiumbe huyu mwenye matendo magumu.

Niliitoa mikono ya Magesa kutoka kwenye mashavu yangu na kugeukia pembeni huku nikionekana wazi wazi sikuwa na furaha ndani ya moyo wangu.

“Naomba nikubusu basi mke wangu ili uende ukapumzike” alizungumza mume wangu kwa kubembeleza.

Jamani jamani nyie! Mnaona vituko hivi? Heti anibusu, Hovyoo! Yaani unamuacha mke wako unakwenda kwa mchepuko halafu unajifanya unajua kujibebiisha. Nikawaza sijui nimnga’te sikio asiende hiyo safari yake? Lakini nikamuomba Mungu aendelee kunipa subra na uvumilivu katika jambo lile.

Nikafumba macho kwa nguvu wakati Magesa alipokuwa analeta midomo yake kunipiga busu. Mungu wangu! Sijawahi kupigwa busu chungu kama lile alilonipiga Magesa siku hiyo. Nakwambia busu lilikuwa chungu kama shubiri! Halafu lilikuwa linawasha utafikiri pilipili kichaa.

Alipokwisha kunibusu aliingia kwenye basi huku akiniangalia kwa huruma na kunipungia mkono. Nikageuka na kuanza kuondoka pasipo hata kupunga mkoko kumuaga mwanaume yule Fedhuli.

****

Kilio ndicho pekee kilikuwa faraja kwangu. Nilijikuta nikishindwa kufanya jambo lolote zaidi ya kulala na kulia. Yote hayo yalikuwa yamesababishwa na mume wangu aliye nisaliti kwa mtu ambaye alijifanya kuwa ni Fundi Umeme. Kila nilipokuwa nikiikumbuka ile meseji ya huyo Fundi wake roho ilizidi kuniuma. Nilitamani sana kumpata mtu wa kunifariji katika kipindi kile kilichokuwa kigumu kwangu.

Nilimkumbuka rafiki yangu aliyekuwa akifahamika kwa jina la FATUMA aliyekuwa anaishi maeneo ya Tabata Kimanga. Niakaingia kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea Tabata nyumbani kwa rafiki yangu Fatuma.

Haikuwa kawaida yangu kwenda nyumbani kwa Fatuma pasipo kutoa taarifa. Lakini siku hiyo kutokana na hali niliyokuwa nayo, nikashindwa kumtafuta na kujikuta nimefika nje ya nyumba ya Fatuma.

Kabla sijaukaribia mlango wa nyumba aliyokuwa akiishi, Fatuma aliniona na kunifuata kunisabahi kwa bashasha kama ilivyokuwa kawaida yake.

“He Prisca! waao!....Karibu sana” Fatuma alinikumbatia kwa furaha bada aya.

Nikajitahidi kuficha hali yangu na kumkumbatia Fatuma huku nikijifanya kuwa na furaha kama ilivyokuwa kawaida yangu siku zote tulipokutana.

“Ahsante sana shoga” Nilimjibu huku nikiwa na furaha ya bandia.

Niliingia ndani kwa Fatuma na kumkuta shemeji Hashimu mume wa Fatuma ameketi kwenye kochi akiangalia runinga.

“Hodi jamani wenyewe” nilibisha hodi mara tu nilipomuona shemeji Hashimu.

“Oh shemu huyo, karibu sana” Hashimu alinikaribisha kwa uchangamfu.

“Ahsante shem, nimesha karibia” Nilijibu huku nikikwepesha macho yangu yaliyokuwa yamevimba kutokana na kulia kwa muda mrefu kumuangalia shemeji Hashimu.

Nilitembea hatua moja moja kuelekea kwenye kochi huku nikimtazama shemeji Hashimu kwa jicho la wizi kwasababu nilibaini kuwa alikuwa amenikazia sana macho. Haikuwa mara yake ya kwanza mwanaume yule kunitazama vile, nimekwisha kumzoea na kila nilipokutana naye alionekana kupoteza umakini wake na kuhamia kwenye mwili wangu. Sawa pamoja na kwamba macho hayana pazia lakini mwanaume huyu alikuwa amezidi. Mbaya zaidi nilikuwa nikimheshimu kama shemeji yangu, lakini tabia yake hiyo ilinifanya nijihisi kumchukia. Ndivyo hivyo nilikuwa simpendi na na kumchukia ana mume wa rafiki yangu kipenzi Fatuma.

“Karibu sana Prisca” Alisema Fatuma huku akiwa amesimama karibu na kochi nililokuwa naelekea kuketi.

“Poa nimesha karibia shost” Nilijibu huku nikijiweka kwenye kochi lile taratiibu hukubado nikiendelea kumtazama shemeji Hashimu kwa macho ya kuibia. Fatuma alifunga mlango kisha akaja pale sebuleni ambapo tulikuwa tumeketi mimi na shemeji Hashimu.

“Sasa Prisca, ongea ongea na mzee hapa mimi nikajimwagie mara moja” Fatuma alinambia.

Jamani nyie Fatuma hakuwa anatambua jinsi nilivyokuwa simpendi mume wake. Sasa kitu cha kunyongo’nyesa ni kile cha kuniambia heti nikae na mume wake yeye anakwenda kukoga. Nikatamani kupasuka lakini sikuweza.

“Haina shida we nenda kakoge tu, mi nipo na mke mdogo leo” Shemeji Hashimu alidakia maneno ya mke wake.

“Sawa Shoga si upo na amani?” Fatuma alisisitiza baada ya kuona maongezi yake yamevamiwa na mume wake.

“Haina shida shoga yangu, nipo nakusubiri” nilimjibu kwa kujilazimisha huku moyoni nikiwa na donge gumu limenikaba.

Fatuma alipoondoka tulibakia mimi na Shemeji Hashimu pale sebleni. Nilimuona Shemeji akinigeuzia macho na kunitazama kwa sekunde kadhaa kisha akameza funda la mate huku akitabasamu.

“Shemeji umependeza sana” Alisema shemeji Hasimu huku akiwa bado ananitazama.

“Jamani shemeji ahsante” Nilimjibu shemeji yangu yule ambaye macho yake yalionekana wazi kuwa na tamaa kama fisi.

“Shemeji yangu kwa kweli huwa unanikosha sana na mikato yako” Hashimu aliendelea kuzungumza nafikiri alikuwa na lengo la kuvunja ukimya pale sebleni.

“Mikato ya kivipi jamani shemeji?” nikahoji na mimi ilimradi nisionekane mtu wa ajabu.

“Yaani kwa jinsi ulivyo umbika, vazi lolote linakupendeza” shemeji Hashimu aliendelea kuchomoa tu maneno yake.

“Shemeji bwana, ahsante lakini” nilijikuta nikimjibu kwa aibu.

“Yaani mtoto kama wewe ningekupata mimi, sidhani kama ningekuwa nakwenda hata kazini” alizungumza Shemeji Hashimu kwa na kutumia mikono yake kusisitiza.




Pumbavu kabisa, kumbe mianaume yote ndiyo ileile ina fanana. Nilifikiri msaliti alikuwa ni mume wangu tu kumbe hata lile nililokuwa nazungumza nalo pale pia lilikuwa firauni. Pumbavu!

“Lakini mbona hata shoga yangu Fatuma ni mrembo jamani” nilizungumza kwa msisitizo.

“Ah sawa ni mrembo, lakini hakufikii wewe. Yaani kama mimi ndio ningekuwa Magesa, kamwe nisinge thubutu kutoka nje ya ndoa” alizungumza shemeji Hashimu na kuchukua glasi ya maji ya kunywa iliyokuwepo mezani akaipeleka mdomoni.

ITAENDELEA…

Mungu wangu! Kumbe hata Hashimu alikuwa anafahamu tabia za mshenzi mwenzie! Mungu ni mwema jamani, kadri muda ulivyokuwa ukiyoyoma ndivyo nilivyokuwa nikifunguliwa na kuyafahamu mauchafu ya mume wangu Magesa.

“Kwahiyo unataka kusema Magesa anatoka nje ya ndoa?” Nilihoji swali la mtego ili kuweza kuchimba ukweli wa jambo lile pamoja na kwamba ukweli nilikuwa nao tayari kupitia ile messege ya Fundi umeme.

“Ah unadhani atakosa? Si unajua tena sisi wanaume mambo yetu!” Shemeji Hashimu alizungumza pasipo kuwa hata na chembe ya woga wala aibu.

“Kwahiyo kumbe na wewe unamsaliti shoga yangu?” nikahoji kwa mshangao.

“Sina maana hiyo Priscaria”

“Kumbe unamaana ipi?”

“Ninamaanisha kuwa urembo wako unajitosheleza” Shemeji Hashim alijibaraguza baada ya kugundua maneno yake hayakuwa yameninogea hata chembe.

“Tusipoteze lengo shemeji, umesema wanaume mna tabia gani?” Nikamrudisha kwenye mada ileile.

“Inatosha mrembo,Vipi bwana Magesa yupo au ndio amekwisha safiri tena?” Hashimu alijitahidi kupoteza mada iliyokuwepo baada ya kuniona nimebadilika na kuwa na wasiwasi na yeye. Pasipo kuelewa kuwa mada aliyokuwa anataka kuianzisha ndiyo ilikuwa ikiniboa zaidi. nilikuwa nikilichukia sana jina hilo la Magesa ambalo alinitajia. Aliniona jinsi nilivyo poteza amani hata ile ya bandia ambayo nilikuwa nimeingia nayo mle ndani.

“Vipi mbona umebadilika hivyo kuna tatizo” Hashimu alihoji baada ya kuiona sura yangu imesawajika.

“Hakuna tatizo, ila Magesa amesafiri” Nilimjibu kwa ufupi.

“Alaaa! kumbe ndiyo maana huna amani? unaonaje mtoto mzuri uje kuishi hapa kwetu kwa kipindi chote hicho ambacho jamaa atakuwa safarini?” alizungumza shemeji Hashimu huku akiachia tabasamu.

“Usijali nitafanya hivyo” Nilimjibu shemu Hashimu kwa ufupi.

“Sio masihara mrembo, ninamaanisha!” Akasisitiza kauli yake.

Niliinua macho yangu na kumtazama usoni huku nikiwa nimevaa lile tabasamu langu la bandia. Moyoni mwangu kulikuwa kumejaa chuki dhidi yake. Nikatoa pumzi ndefu na kuongeza ukubwa wa tabasamu langu. Nilishangaa kumuona shemeji Hashimu akiwa amepumbaa huku macho ameyalegeza utafikiri alikuwa amekula kungu. Nikabaini kuwa tabasamu langu lilikuwa limemmaliza shemeji yangu yule..

“Heee!....Prisca!” shemeji Hashimu aliita kwa kuhamaki utafikiri alikuwa ameona kitu Fulani cha ajabu sana.

“Abee shemeji” nikaitika huku nikiwa na hamasa kubwa ya kutaka kufahamu shemeji yangu yule alikuwa anataka kuzungumza nini.

“Mnh we mtoto!” shemeji Hashimu aliendelea kushangaa.

“Kuna nini kwani shemeji?”  nikahoji.

“Basi na yaishe mtoto mrembo” Akazungumza kwa sauti ya chini baada ya kusikia mlango wa chumbani ukifunguliwa na Fatuma. Ndani ya moyo wangu nilishukuru sana nilipogundua kuwa shoga yangu alikuwa anakuja.

Shemeji Hashimu pamoja na mume wangu Magesa walinifanya niwachukie sana wanaume, tena wanaume wote ulimwenguni. Watu ukiwaona wapoole kumbe nyuma ya pazia kumejaa mauchafu kibao.

“Kwahiyo Magesa anarudi lini?” Shemeji Hashimu akajifanya kuhoji ili kumzuga mpenzi wake Fatuma.

Kabla sijajibu swali lile lililokuwa likinikera Fatuma akaingilia kati kwa kuzungumza maneno mengine tofauti.

“Pole shoga yangu kwa kukuwacha peke yako” Fatuma alizungumza huku akiwa anatembea kuelekea pale sebleni tulipokuwa mimi na shemeji Hashimu.

“Usijali shoga mbona shemeji alikuwepo” Nilimjibu

“Haya bwana, vipi lakini shemeji yako hajakuudhi?” Fatuma akahoji kama vile alifahamu kilichokuwa kinazungumzwa pale sebleni kati yangu na Hashimu.

“Hakuna, nimefurahia kampani yake” nikajibu huku nikijichekesha chekesha kiuongo na kweli.

“Nitake radhi Fatuma” Shemeji Hashimu alidakia.

Fatuma akamsogelea mume wake na kumshika kidevu ambacho kilikuwa na vindevu kwenye ncha ya kidevu vilivyokuwa vimechongwa kiduara.

“Basi mpenzi wangu nakutania” Fatuma alizungumza huku akiwa amelegeza sauti na macho akiyarembua kimahaba.

“Haya nibusu” Alisema Shemeji Hashimu huku akijifanya amesusa.

“Mmmmwaaaa” Fatuma akambusu.

“Haya nimekusamehe” alisema shemeji huku akijichekesha kinafki.

Fatuma akaja pale nilipokuwa nimeketi mimi na kuketi kwenye kochi la pembeni.

“Enhe niambie shoga” Fatuma akanisabahi baada ya kuketi.

“Salama shoga” Nilimjibu lakini nikajikuta ile hali ya unyonge ikinitawala tena. Fatuma akapata wasiwasi na kunikata jicho la kuniuliza kitu ambacho hakutakiwa mtu mwengine kusikia. Kwasababu tulikuwa tumezoeana sana tuliweza kuzungumza hata kwa vitendo na kuelewana pasipo mtu mwengine kugudua kama tunawasiliana.

Fatuma alifinya kidogo macho yake na kuyakaza kwangu. Hapo nikagundua kuwa alikuwa anahoji kama kulikuwa na tatizo. Nikainua macho yangu na kuangalia juu ya paa. Fatuma akabaini kuwa kulikuwa na tatizo. Alibana lipsi zake mdomoni akimaanisha kutaka kufahamu kama tungeweza kuzungumza pale sebleni. Nikatoa kitambaa cha kujifutia jasho na kujifuta mdomoni nikimaanisha kuwa haikuwa rahisi kuzungumzia tatizo langu mahala pale. Fatuma akatanua macho yake kwanguvu akimaanisha kutaka kujua cha kufanya. Nikavuta pumzi pamoja na mabega yangu kuyainua juu kama ishara ya kumfahamisha kuwa sikujua cha kufanya.

“Vipi mbona hamzungumzi mnatazamana tu kama majogoo?” Shemeji Hashimu alihoji baada ya kutuona tumekaa kimya kwa muda mrefu tukiangaliana.

“Naomba maji ya kunywa Shost” Nilijifanya kuzungumza ili kumfanya Shemeji Hashimu kutokugundua kilichokuwa kikiendelea baina yetu kwa muda mrefu pale pale sebleni.

Fatuma alielekea kwenye Friji na kumimina maji kwenye glasi kisha akarejea nayo, alipofika akasimama kidogo huku akiwa ameyashikilia yale maji.

“Shoga kuna kazi nafanya chumbani, sijui itakuwa vibaya tukienda huko?” alihoji Fatuma huku akinikonyeza.

“Hakuna tatizo shost twende tu” Nilimjibu huku nikijiinua kutoa pale kwenye kochi.

“Jamani mbona unaniondolea mgeni” Shemeji Hashimu alihoji.

“Wasiwasi wako wa nini wakati sisi sote ni wakwako” Alisema Fatuma na kunifanya na mimi nitoe kile kicheko changu cha bandia. Fatuma akatangulia nami nikawa namfuata nyuma. Nilimtupia jicho la wizi Shemeji Hasimu na kumuona akinikazia macho sehemu za makalio. Moyoni nikajawa na dukuduku juu ya tabia yake ile.

Tulipofika chumbani tu niliangua kilio cha sauti ambacho kilimshitu na kumshangaza sana Fatuma. Shoga yangu yule badala ya kunibembeleza nikamuona ameduwaa akinitumbulia macho kwa mshangao. Nilijitupa kitandani huku nikiendelea kulia kwa kwikwi. Fatuma akanisogelea na kupiga magoti kando ya kitanda na kunishika mgongoni kwa mkono wake wa kuume.

“Vipi shoga kuna nini?” alihoji Fatuma.

“Magesa….Fatuma….. Magesa” Nikazungumza kwa kulia huku nikijaribu kufuta machozi.

“Hebu nyamaza basi uniambie” Fatuma alijaribu kunibembeleza.

“Magesa ni wa kunifanyia mimi hivi?” Nilizungumza huku nikijitahidi kuwacha kulia. Fatuma akawa akinitazama kama vile alikuwa akinisubiri nimalize kulia kwanza ndipo tuzungumze.

Nilipo hakikisha kuwa nilikuwa nimemudu kujizuia kulia nikajiinua pale kitandani nilipokuwa nimelala na kuketi kitako.

“Haya nieleze sasa huyo Magesa amefanya nini?” Fatuma alihoji baada ya kuhakikisha kuwa nilikuwa nimenyamaza kulia.

“Fatuma Magesa ananisaliti….yaani kweli? Aah!” Nilizungumza kwa hasira.

“Anakusaliti?” Fatuma alihoji kwa mshangao kwasababu alikuwa akimfahamu vyema mume wangu kwamba alikuwa makini na ndoa yake kuliko kitu kingine chochote hapa ulimwenguni. Alikuwa anamfahamu mume wangu Magesa kama mwanaume aliyekuwa muaminifu katika ndoa yake na alikuwa akinipenda kwa dhati mke wake.

“Jinsi ninavyo mpenda hivi bado anani….?”

“Hapana Prisca sio kweli. Zungumza kitu kingine lakini kwa hilo unamuonea mwanaume wa watu. Magesa hawezi kufanya hivyo” Fatuma alizungumza kwa kujiamini na msisitizo mkubwa.

“Sikiliza Fatuma. Huna sababu ya kumtetea, yule mwanaume ni nyoka” nikazungumza kwa msisitizo.

“Simtetei, lakini huo ndio ukweli. Mimi namfahamu vizuri sana mume wako” Fatuma alieleza.

“Unamfahamu?” nikahoji.

“Ndio”

“Unamfahamu?” nikahoji tena.

“Ndio”

“Sasa kwa taarifa yako, nimemkuta na meseji za wapenzi wake kwenye simu nilipokuwa nataka kumsindikiza stendi” Nilizungumza kwa hasira zaidi hasa baada ya kumuona Fatuma alikuwa akimtetea mwanamume yule ambaye kwangu alikuwa ni mkosaji mkubwa sana. Nikamuona Fatuma akiishiwa na pozi huku akikaa vizuri kutaka kujua zaidi.

“Unasema kweli?” alihoji Fatuma

“Habari ndiyo hiyo”

“Mnh!” Fatuma akaguna huku akichukua kitambaa na kujifuta usoni kama vile mtu alikuwa akijifuta jasho. Machozi yalianza kunitoka tena na kujikuta nikilia kwa sauti ya chini.

“No, usilie shoga yangu. Tutajua cha kufanya” Fatuma akanibembeleza

“Tutafanya nini wakati mtu ndiyo tabia yake?”

“Sikiliza Prisca shoga yangu….”

“Enhe,”

“Dawa ya moto ni moto” Fatuma alizungumza

“Unamaanisha nini Fatuma?”

“Namaanisha hivi, mwenzako akimwaga ugali, na wewe mwaga mboga. Ngoma inakuwa droo” Alisema Fatuma kwa kujiamini.

****

Ndani ya basi Magesa alikuwa ameketi siti moja na msichana mmoja aliyekuwa amejitanda ushungi kichwani mwake. Mwanamke yule alikuwa ni chotara mwenye asili ya kiafrika na kiarabu. Umri wake ulikuwa ni kati ya miaka 23 hivi hadi 27. Msichana yule alionekana kuwa mcheshi sana kiasi cha kumzoea Magesa mapema kuliko kawaida. Mwanzoni Magesa alipata shida kumzoea msichana yule kwasababu yeye hakuwa mzungumzaji sana. Hata hivyo mwisho wa siku ilimbidi aendane na mazingira.

“Kama hautojali naomba unifahamu” alizema msichana yule huku akimenya pipi na kuitia mdomoni.

“Sawa sio mbaya kufahamiana” Magesa alizungumza kwa sauti ya chini.

“Ninaitwa Yusrah, ni mtoto wa Alhaji. Nakwenda Arusha kumsalimia shangazi yangu. Makazi yangu ni Dar, na…. sijaolewa pia” Msichana yule alijieleza kwa kirefu.

“Nashukuru kukufahamu Yusrahh, mimi naitwa Frank” Magesa aliongopa.

“Mnh!” msichana yule akaguna

“Vipi mbona unaguna?”

“Hayo majina huwa….”

“Yana nini?”

“Huwa yanakuwaga na vitu vya ziada kwenye tabia zao”

“Vitu gani?”

“Mara nyingi kama tabia zao si nzuri sana, basi ni mbaya sana”

“Kwahiyo unataka kusema Frank wote tabia zetu sio nzuri?”

“Sina maana hiyo”

“Kumbe?”

“Namaanisha kwamba, huwa hawana kiasi kwenye mambo yao”

“Mnh!”

“Ndio hivyo, sasa sijui Frank wewe upo kundi lipi?”

“Mimi nipo kwenye kundi la wale wenye tabia mbaya saaana” Magesa alijibu kwa kujiamini kama vile jina lile lilikuwa kweli ni la kwake. Msichana yule aliyekuwa amejitambulisha kwa jina la Yusrahh akacheka kidogo kabla ya kuzungumza.

“Waaao! mimi nakupongeza kwa hilo kwasababu watu wenye jina kama lako huwa ni wakweli lakini sio wawazi. Inawezekana kinyume chake kikawa ndio ukweli” Msichana yule alizungumza kwa sauti yake laini aliyokuwa akiitolea puani. Magesa hakujibu kitu zaidi ya kuachia tabasamu tu kidogo.

Walikuwa wamekwisha fika kwenye wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. Magesa alipata wazo la kunipigia ili kunifahamisha walipokuwa wamefika, lakini aliponipigia aliambiwa kuwa simu yangu haipatikani. Badaa ya dakika kadhaa akapiga tena lakini jibu halikuwa tofauti. Alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kunitafuta hewani kwa kupitia simu yangu ya mkononi lakini sikupatikana. Nakumbuka nilizima simu yangu mara tu baada ya kuzungumza na Fatuma.

Safari yake ilikuwa ngumu sana siku ile kwasababu alikuwa amezoea kuzungumza na mimi kipindi alipokuwa akisafiri safari za mikoani. Hakukata tamaa kunitafuta kila baada ya dakika chache lakini anipate wapi? Thubutuuu! mwanamke nilikuwa nimejizimia simu yangu kwa hasira.

Alijikuta akipatwa na wasiwasi kutokana na tukio lile. Hasa alipokumbuka kuwa alikuwa ameniacha katika wakati mgumu sana. Alishindwa kuelewa nilikuwa nimepatwa na kitu gani ambacho kilipelekea simu yangu kuto kupatikana.

“Lakini bado hujaniambia kama umeoa ama laa?” Yusrah alihoji swali ambalo lilimkera sana Magesa wangu. Akabakia kimya na kuwa bize na simu yake akinitafuta kipenzi cha roho yake bila ya mafanikio.

“Si nakuuliza wewe Frank?” Yusrah akahoji kwa msisitizo baada ya kuona mume wangu hakuwa anamjali.

“Yeah! nakusikiliza” Magesa akaacha kubonyeza simu na kumgeukia Yusrah.

“Inamaana hukulisikia swali langu?”

“Sio dhambi kama ukinikumbusha”

“Umekwisha o a?” Yusrah akahoji kwa sauti ya chini lakini iliyojaa msisitizo.




Magesa hakuona sababu ya kuinua mdomo wake kumjibu msichana yule ambaye alimuuliza swali la kizushi. Alichokifanya ni kuinua mkono wake wa kushoto na kumuonesha pete ya ndoa.

“Enh hongera sana” Yusrah alizungumza kwa unyonge ambao alishindwa kuuficha. Magesa aliweza kuibaini ile hali lakini akajifanya kama vile hakuna alichokihisi.

“Ahsante” Alijibu Magesa huku akibonyeza namba yangu ya simu kunipigia kwa mara nyingine.

“Lakini inaonekana mkeo ana shida sana?”

“Shida ya kivipi?” Magesa alihoji huku akikunja sura baada ya kunipigia na kuambiwa kuwa nilikuwa sipatikani kwenye simu.

“Inaonekana wazi kuwa tabia zako ni za wale wakina Frank wakorofi”

“Kwanini?”

“Unaonekana tu upo hivyo”

“Nipe vigezo” Magesa alizungumza huku akipiga tena namba yangu ya simu.

“We huoni mimi nazungumza na wewe, mwenzangu unajitia ubize na simu huna lolote” Yusrah alizungumza huku akijichekesha chekesha. Magesa akatoa msonyo mrefu ambao ulimshitua Yusrah na kumfanya amtazame kwa tahadhari. Msonyo ule ulitoka baada ya mimi kuto kupatikana kwenye simu.

“Si unaona!” Alisema Yusra

“Kitu gani?”

“Sasa unanisonya mimi nimekukosea nini?” Yusra alizungumza huku akionekana kutopendezwa na kile kitendo cha Magesa kuachia msonyo akidhani alikuwa amesonywa yeye.

“My God! sikusonyi wewe Yusrah”

“Kumbe unamsonya nani, au hiyo miti inayo rudi nyuma huko nje?”

“Kuna mtu namtafuta kwenye simu muda mrefu sana lakini hapatikani” Magesa alijieleza ili kuondoa utata.

“Ni mwenyeji wako?”

“Hapana ni Wife, tangu nimeondoka hatuja wasiliana tena na kwenye simu hapatikani”

“Oh pole sana. Wanawake ndivyo tulivyo hivyo. Mwanaume akisafiri tu, nasisi tunajitafutia safari zisizo za lazima huku nyuma” Yusra alizungumza maneno ambayo hayakuwa mazuri kwenye masikio ya Magesa.

“Unataka kusemaje?” Magesa akahoji

“Wewe unasafiri, na mwenzako naye saa hizi huko anasafiri milimani tena muda huu anakaribia kufika kileleni” Yusra alizungumza kwa mafumbo.

“Sikuelewi”

“Mke mkeo ukiwa kwako, ukiondoka si wako” alizungumza Yusra kwa nyodo huku akijibinjua binjua kwa kujishebedua mbale ya mume wangu.

“Pumbavu! unadhani mke wangu mimi ni mshenzi kihivyo?” Magesa alizungumza kwa hasira.

Magesa hakutegemea kama maneno kama yale yangemtoka kinywani mwake. Lakini ni kwasababu ya zile kauli za Yusra zilizokuwa zinatanga kuhatarisha usalama wa mapenzi yake na mimi mke wake. Siku zote hakuwa tayari kusikia maneno machafu yanatolewa kwangu. Kwa hilo tu ndugu msomaji nitampongeza Magesa milele daima ukiondolea zile tabia zake tu za mafundi umeme wake.

“Taratibu Frank, mimi sina maana hiyo” Yusra akazungumza kwa upole.

“Wacha upumbavu, mie mke wangu anajiheshimu sana” Magesa aliendelea kusisitiza.

“Nina maanisha kwamba ukiwepo nyumbani na mke wako ni rahisi kuzungumza naye kuliko mnapokuwa mbali” Yusrah akajaribu kujitetea

“Huna jipya wewe” alizungumza Magesa huku akionekana kumdharau msichana yule aliyekuwa anazungumza utafirkiri chiriku.

“Unajua hizi simu bwana hazifai. Usipokuwa makini unaweza kujikuta unavunja ndoa. Utakuta network inasumbua we undhani mwenzio amezima simu” Yusrah aliendelea kujitetea kwa kujipendekeza kwa kunitetea baada ya kugundua udhaifu wa Magesa ulikuwa kwenye penzi la mke wake.

“Netwark ndio isumbue muda wote huo?” Magesa akajikuta hasira zake akizihamishia kwangu kwa kosa la kuto patikana.

“Inawezekana pia simu imezimika chaji” alizungumza Yusra.

“Hata kama, kwanini asitafute hata simu kwa watu akanipigia?”

“Inawezekana pia simu yako ikawa na tatizo”

“Kivipi wakati naambiwa hapatikani”

“Wacha ubishi Frank, hebu nipe hiyo namba ya mkeo niijaribu kwa hii simu yangu” Alisema Yusrah huku akitoa simu yake iliyokuwa kwenye pochi ndogo ambayo alikuwa ameipakatia mapajani. Magesa akabakia kumshangaa pasipo kuzungumza neno lolote.

“Vipi mbona kimya? au huhitaji msaada wangu?” Alizungumza Yusrah kwa ile sauti yake laini ambayo ilionekana kweli kuhitaji kutoa msaada.

Pasipo kujitambua Magesa akataja namba zangu na Yusra akaziandika kwenye simu yake. Alikuwa tayari amechanganyikiwa na kukosa amani ndani ya moyo wake kwasababu ya kunikosa kwenye simu.

Yusra alinakili namba zangu kwa makini kisha akagusa kitufe cha kupigia simu na kuiweka sikioni kwake.

*****

Maneno ya Fatuma yalikuwa yamenichanganya sana akilini mwangu. Heti mwenzio akimwaga ugali wewe umwage mboga, mnh! duniani kuna mambo jamani kwa kweli nilikuwa bado sikumuelewa alichokuwa anakimaanisha.

“Unamaanisha nini Shoga yangu?” Ikabini nihoji.

“Sikiliza shoga, kumbe wewe hufahamu yaliyopo duniani….” Alizungumza Fatuma huku akijiweka kitandani na kusogea karibu kabisa na pale nilipokuwa nimeketi mimi. akawa anazungumza kwa sauti ya chini kabisa kama vile alikuwa akininong’oneza.

“Wanaume ni watu wabaya sana we waone hivi hivi na misuruali yao” Alizungumza Fatuma kwa ile sauti yake ya chini huku amenikazia macho kuashiria uzito wa jambo lile. Nilikaa kimya nikimsikiliza kwa makini shoga yangu yule.

“Dawa yao ni ndogo sana, ukiwapatia tu huwezi kusumbuka milele. We si unaniona mimi mwenzio? naishi kwa raha zangu mtoto wa kike!” Alizungumza Fatuma kwa kujidai huku akijitikisa kwa mbwembwe zilizochanganyikana na nyodo.

Nilikaa vizuri pale kitandani na kumsikiliza kwa makini shoga yangu Fatuma ambaye ndiye aliyekuwa tegemeo langu katika wakati mgumu kama ule uliokuwa ukinikabili.

“Ni ipi hiyo dawa?” Nikahoji kwa hamu kubwa ya kutaka kujua.

“Kama ungelifahamu mapema hilo, wala saa hizi usingekuwa unahangaika na kuteseka kumoyo”

“Nimekuelewa Fatuma, niambie basi hiyo dawa”

“Tafuta Kichenchede” Fatuma alizungumza na kugeuzia shingo yake pembeni akikwepa kunitazama kabisa.

“Kichedechede?” Nilihoji kwa mshangao baada ya kusikia jina la hiyo dawa.

“Sio Kichedechede, ni Kichenchede” Shoga yangu Fatuma alinisahihisha.

“Hicho ndicho kinini sasa! na nitakitoa wapi?” Nilihoji baada ya kuto kuelewa kitu.

Nilikuwa tayari kukitafuta kwa gharama yoyote hicho kichenchede ilimradi kiweze kumponya mume wangu kutoka katika ile tabia mbaya aliyokuwa ameificha nyuma ya pazia. Nikasema hata kama ni mzizi wa mti gani nakwambia nilikuwa tarai kwenda kuutafuta. Sikupenda kabisa kumuona mume wangu akiendelea kunisaliti na kunidanganya kana katoto kadogo. Nikamtazama Fatumu huku nikimsikiliza kwa makini.

“Mchuchu shogaaa…Ah! we unaishi dunia ipi?” Fatuma alizungumza kwa sauti kidogo tofauti na awali huku akinikazia macho.

Nilishituka sana niliposikia jibu lile. Hata hivyo nikajipa moyo kwa kujiambia pengine hakuwa na maana ile niliyokuwa nikifikiria mimi kwenye akili yangu.

“Unamaanisha nitafute mwanaume mwengine?” Nikahoji kwa mshangao.

“Habari ndiyo hiyo shost”

“Na Magesa naye nitampeleka wapi?”

“Magesa kitu gani? kama angekuwa anakupenda asinge kusaliti bwana”

“Hapana Fatuma, nampenda sana Magesa, siwezi kumuacha”

“Sija kwambia uachane naye”

“Kumbe?”

“Magesa unakuwa naye lakini unakuwa na Spea tairi kwa pembeni” Fatuma alizungumza huku macho yakiwa makavuu bila hata chembe ya aibu.

“Yaani niwe na wanaume wawili si ndivyo hivyo?” Nilihoji kwa umakini.

“Ewaa! Sasa tuko pamoja”


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG