Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

BONGO DAS'LAAM - 2

   


Chombezo : Bongo Das'laam 

Sehemu Ya Pili (2)


“Ayubu Nyiruka”

“Na mimi?”

“Suzy”

“Suzy nani?”

“Manyama”

“Sasa kama wewe ni Ayubu Nyiruka na mimi ni Suzy Manyama, huo undugu unatoka wapi?” alisema Suzy kwa uchungu kutokana na misimamo ya Ayubu.

Maneno ya Suzy yalimchoma sana Ayubu ndani ya moyo wake, alihisi kama vile Suzy alikuwa akimnyanyasa na nyumbani kwao. Alimtazama usoni kwa sekunde kadhaa kisha akameza funda kubwa la mate machungu.

“Una maanisha nini Suzy?”

“Unajua nataka nini Ayubu. Lakini naona undugu ndio umekuwa kikwazo”

“Suzy, mbona mimi sijui unachokitaka”

“Ok. Ni hivi nahitaji penzi lako” Suzy alizidi kuzungumza kwa msisitizo zaidi.



“What! Siwezi Suzy siwezi” alisema Ayubu kwa mkazo na kuingia chumbani kwake akimuacha Suzy amesimama pale mlangoni.

Ayubu alivua suruali na kubaki na boksa kisha akajitupa kitandani. Maneno ya Suzy yalikuwa yamemuingia ibasavyo kwenye ubongo wake, hasa alipoambiwa kuwa yeye hakuwa mtoto wa ndani mle. Pamoja na kwamba Suzy alizungumza ukweli mtupu lakini machozi yalianza kumtiririka Ayubu na kujikuta akikumbuka matatizo mbali mbali aliyokumbana nayo tangu alipofika jijini DareSalaam.

Wakati Ayubu alipokuwa amezama kwenye dimbwi la mawazo, alimsikia Suzy akipiga kelele za kuomba msaada. Ayubu akakurupuka na kuingia chumbani kwa Suzy pasipo kutambua kuwa alikuwa amevaa boksa tu. Alimkuta Suzy akigalagala chini huku ameshikilia maeneo ya tumboni.

“Vipi dada Suzy kuna nini?” alihoji Ayubu kwa wasiwasi mkubwa baada ya kumuona dada yake akigalagala chini huku akilalamika kutokana na maumivu makali.

“Tumbo….nisaidie nakufa” masikini Suzy wawatu aliendelea kulia kwa maumivu makali pale chini.

“Tumbo lina nini?” Alihoji Ayubu huku akiwaza namna ya kumsaidia ndugu yake yule.

“Naomba niminye hapa….aaaah! mama nakufa” Jamani nyie ungemuona jinsi Suzy alivyokuwa akiugulia hadi huruma.

“Pole dada Suzy” alisema Ayubu kwa huruma.

Ayubu alimhurumia sana dada yake yule. Akainama na kufanya kama vile alivyotaka Suzy afanye. Huduma ile aliyokuwa akiitoa ilionekana kuleta mafanikio kwani makelele ya kuomba msaada kwa kiasi fulani yalipungua.

“Oooh!...Ayubu…..nisaidie ndugu. Nichue hapo hapo kaka Ayubu” mnh binti yule alizungumza kwa sauti ya kutia imani. Ndugu msomaji hata kama ungekuwa ni wewe lazima ungemsaidia binti yule kutokana na mateso aliyokuwa akiyapata pale chini.

Wakati Ayubu akijitahidi kumsaidia ndugu yake yule kwa kumchua maeneo ya tumboni, Suzy alimvuta chini kaka yake na kukumbatiwa kwa nguvu.

“Fanya hivi Ayubu labda nitapona” alisema Suzy huku akimbana Ayubu kwa nguvu.

Kifua cha Ayubu ambacho hakikuwa na nguo kiligusa chuchu za Suzy na kuleta hali fulani ya msisimko kwa wote wawili. Sehemu za maapaja yao vile vile yaligusana na kuleta ladha fulani ambayo ilikuwa tofauti kwa kila mmoja.

Laahaula! Siku zote “ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu” Midomo ya Suzy na ya Ayubu ilikutana na kunasa kama sumaku. Ndani ya dakika kama tano walikuwa sale sale maua, kila mmoja alikuwa akionesha ufundi wake.

Ayubu aliona kulikuwa na ulazima wa kutunza heshima yake ya mwanaume rijali. Uvumilivu ulikuwa umekwisha mshinda. Alivitumia ipasavyo viungo vyake alivyopewa na muumba kama vile vidole vya miguu na mikono, ulimi, na mwanya uliokuwa katikati ya meno yake ya juu. Alivitumia viungo hivyo katika meneo mbalimbali ya mwili wa Suzy. Alisahau kabisa kama alikuwa ameapa kuto kuruhusu hisia zake kufanya kitu kama kile.

Suzy hakuweza kuamini kama Ayubu angekuwa mtundu kiasi kile. Hakuelewa ni kwanini siku zote hizo alikuwa akijifanya haelewi. Miguno ya mahaba iliyoambatana na sauti za chumbani ilikuwa imekipamba chumba cha Suzy. Pamoja na kupagawishwa lakini Suzy naye hakuwa nyuma kutoa ushirikiano. Alipita kila kona aliyoifahamu kuwa ni sehemu hatari kwenye mwili wa mwanaume. Ayubu naye akajikuta akitoa miguno ya mahaba kutokana na mambo aliyokuwa akipewa na Suzy.

“Ooomh!..hapo…hapo..aaah! Suzy mpenzi tara..taratibu” mtoto wa kiume alilalamika kama bwege.

“Yeaaah!!...usi…usi..Oooommn…unaweza Ayubu” Suzy naye alilalama kivyake. Yani ilikuwa kama vile wodi ya vichaa wa mahaba.

“Suzy sikujua kama…Ooomnh!..yap..ammnmny..Uph!”

“Ayubu wewe ni mtundu zai…di….Nipe haki yang…Oomnh!”

“Usiwe na wasi Darling. Nakupa”

“Mbona unachelewa sasa Ayubu mpenzi….nipe mwenzio” Suzy alilalamika na kuonekana kuwa na hali mbaya zaidi kuliko mwenzake. Ayubu alionesha maufundi yote ya kitanga. Hakuona sababu ya kupoteza uasili wake hata dakika moja. Hasa baada ya kuyaona maungo ya mtoto mrembo aliyeumbwa akaumbika. Inaonekeana siku alipokuwa akifinyangwa hakuwa mvivu kugeuka kila alipotakiwa kufanya hivyo na mfinyanzi wake.

Baada ya dakika takribani arobaini na tano walizozitumia kuandaa mazingira ya mechi kabambe kati ya Ayubu na Suzy mchezo ulianza rasmi. Ilikuwa ni mechi kali sana, kila upande wachezaji walionekana kujituma ipasavyo. Ndani ya nusu saa Suzy alikuwa amekwisha kufunga magoli matatu wakati timu ya Ayubu ilikuwa haijatupia hata goli moja. Hadi kipindi cha mapumziko Suzy alikuwa amekwisha pachika magoli matano kwa moja lililofungwa na Ayubu kwenye dakika ya mwisho.

Kila mmoja alikuwa hoi, walikuwa wamelala mithili ya samaki waliopigwa mabomu ya sumu. Ayubu alikuwa wa kwanza kujitambua. Aliinua shingo yake na kumtazama Suzy ambaye macho yake yalikuwa juu akitafakari mchezo ulivyokuwa. Macho yao yaligongana na kusababisha zao la mti wa tabasamu kumea baina yao.

“Thank you” alisema Suzy kwa sauti ya chumbani huku yale macho yake akiyazunguusha utafikiri anakata roho.

“Vipi?” alihoji Ayubu kwa sauti nzito huku akitabasamu.

“Dah! We mkali. Sijui kwanini ulikuwa unanibania”

“Hata wewe ni mjuzi Suzy. Unaweza kwenda na biti” alisema Ayubu na kufanya wote wawili kuangua kicheko. Kicheko chao walikimalizia kwa kupigana busu la mdomoni.

“Lakini Suzy baba akijua itakuwaje?” Ayubu akahoji kwa tahadhari.

“Mnh! Atatuua”

“Ataniua mimi, sio wewe”

“Hawezi kujua. Hii itabakia kuwa siri yetu mimi na wewe” Suzy alihakikisha kutunza siri ile.

“Kweli Suzy?”

“Sure!”

“lakini tusirudie tena siku nyingine” alitahadharisha Ayubu.

“Kwanini? Wewe ushakuwa wangu. Muda wowote tunaweza”

“Mimi siwezi”

“Utaweza tu” alisema Suzy kisha wote waliangua kicheko.

Kwakuwa midomo yao ilikuwa karibu, sumaku ya ajabu ilitokea na kujikuta kila mmoja akijiramba kwa aiskrim. Kulikuwepo na dalili zote za kuingia nusu ya pili ya mechi yao waliyokuwa wakiicheza na maandalizi yalikwisha anza upya.

Wawili wale wakiwa katika hatua za awali za kuingia kipindi cha pili ghafla shughuli ikageuka na kuwa nzito baada ya kusikia vishindo vya miguu mtu akitembea ndani ya nyumba yao. Wote wawili walishituka na kuachiana.

“Nani huyo Suzy” Ayubu alihoji kwa sauti ya kunong’ona na iliyojaa hofu.

“Sijui”

“Kwani ulifungua malango?”

“Ndio, mlango upo wazi. Anaweza kuwa mama au baba”

“Mungu wangu nimekwisha” alisema Ayubu huku akitetemeka kwa hofu.

Vishindo vya mtu aliyekuwa akitembea vilikuwa vikielekea kule chumbani kwa Suzy ambako Ayubu na binti wa watu walikuwemo wakibadilishana ladha.

“Ingia uvunguni” Alizungumza Suzy kwa woga.

“Ngoja niingie kabatini” Ayubu akatoa wazo.

“Hapana, anaweza akafungua kabati” alisema Suzy.

Ayubu akiwa kama alivyozaliwa alijichomeka chini ya uvungu na kujikunja kama uduvi uliokaangwa.

Sauti ya mama Suzy ilisikika ikiita nje ya mlango wa kuingilia chumbani kwa Suzy. Wakati Suzy akujiandaa kwenda kufungua malango, mama Suzy alikuwa amekwisha fungua na kuingia chumbani mle.

“Inamaana bado mmelala?” alisema mama Suzy huku akiwa amesimama na kushika kiuno mle chumbani mwa Suzy. Wakati huo Suzy alikuwa amejisitiri kwa shuka tu mwilini.

“Shikamoo mama” Suzy alisalimia huku akijifanya alikuwa kwenye usingizi mzito.

“Hadi saa nne bado umelala mtotowa kike” mama Suzy aliendelea kuzungumza kwa mshangao.

“Naomba nisamehe mama, nahisi kichwa kinaniuma”

“Kaka yako Ayubu yuko wapi?” mama Suzy alihoji na kufanya Ayubu kule chini ya uvungu moyo wake kumongo’nyoka. Moyo wa Suzy naye ulimpasuka na kujikuta akiropoka bila kujitambua.

“Kaka Ayubu aliniaga anakwenda kwa rafiki yake Moses” Suzy aliongopa.

Jambo moja zito sana ambalo hata wewe ndugu msomaji lingekushitua ni kwamba Ayubu alipoingia chini ya uvungu alikuwa ameacha boksa yake sakafuni karibu kabisa na alipokuwa amesimama mama yao.

Mungu naye aliamua kutenda muujiza wake kwa kumuonesha Mama Suzy nguo ile ya ndani ya Ayubu.

“Suzy” aliita mama Suzy kwa umakini huku akikazia macho nguo ile.

“Abee” Suzy akaitika kwa hofu huku akimuangalia mama yake kile alichokuwa anakitumbulia macho pale chini.

“Umeanza lini hii tabia?”

“Tabia gani mama?” Suzy alihoji kwa mshituko akiamini mama yake alikuwa amegundua ule mchezo wao mchafu.

Ayubu naye kule chini ya uvungu akahisi kuwa mama yao alikuwa amekwisha shitukia shughuli ile.

Mama Suzy akasogea zaidi na kuinama kuitazama kwa makini nguo ile.

“Hii nguo ni ya nani?” alihoji mama Suzy.

“Mnh!...ma..ni..Mnh!...” Suzy akashindwa kutoa jibu la swali la mama yake.

“Pumbavu! Unanifanya mimi mjinga sio?” Mama Suzy alizungumza kwa ukali na kumfanya Suzy kushituka sana.

Kule chini ya uvungu hali ya Ayubu ilizidi kuwa mbaya. Alikuwa akijutia sana uamuzi wake aliouchukua wa kumkubalia Suzy. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimuenda mbio huku kijasho chembamba kikimtoka. Alibana mdomo wake ili kuzuia pumzi zisitoke kwa sauti.



“Umeanza lini kuvaa nguo za kiume?” mama Suzy alihoji swali ambalo lilipelekea kushusha pumzi kwa Suzy na Ayubu kule chini ya kitanda.

“Samahani mama. Sitarudia tena” alizungumza Suzy huku moyo wake ukiwa na Amani kiasi.

“Usifanye ujinga mwanagu si unajua kuwa nakupenda sana” Mama Suzy alisema kwa upole.

“Ndio mama” alijibu Suzy kwa upole.

Mama Suzy alitaka kuondoka lakini alipofika mlangoni alirudi tena kama vile kuna kitu alikuwa amekisahau.

“Kuna mkebe ulikuwa huku chini ya uvungu” alisema mama Suzy huku akitaka kuinama kuchungulia chini ya mvungu.

Suzy alijikuta ni mwepesi kuliko maelezo kwani aliruka kutoka kitandani na kuinama uvunguni kabla mama yake hajainama.

“Ngoja nikusaidie mama” alisema Suzy akiwa tayari anahungulia uvunguni.

Suzy alitafuta kile kimkebe kule chini ya kitanda bila ya mafanikio. Alimkonyeza Ayubu na kumwambia atulie kimya kisha akatoka na kuinuka.

“Mama sijakiona”

“Basi ngoja nikiangalie mwenyewe” alisema mama Suzy akitaka kuinama.

“Nimekumbuka mama” Suzy alizungumza haraka.

“Nini?”

“Nilifanya usafi na kukipeleka stoo” Suzy aliongopa.

“Haya nenda ukanitafutie” Alisema mama Suzy huku akiondoka.

Mama Suzy alipotoka tu chumbani mle, Suzy alijibwaga kitandani na kupumua kwa nguvu. Hakuamini kama mama yake ametoka pasipo kugundua kitu kilichokuwa kikiendelea.

Ayubu alimgusa Suzy mguuni ili kujua kilichokuwa kikiendelea. Suzy aliinuka na kuelekea mlangoni kuchungulia nje. Alipoona hapakuwepo na mtu alimpa Ayubu ishara ya kutoka.

Ayubu alifanikiwa kutoka chumbani mwa Suzi na kuingia chumbani kwake bila kuonekana na mama Suzy. Hakuweza kuamini kama amepona kutoka kwenye mdomo wa mamba.

****

Maisha ya Ayubu na Suzy yalibadilika na kuwa kama vile mtu na mpenzi wake. Wazazi wao walipokuwepo waliitana kaka na dada. Lakini walipobaki wenyewe waliitana majina kama vile Sweety, babe, Honey, Darling, na mengine kadha wa kadha ya kimapenzi. Kila walipopata nafasi waliutumia muda wao kiufasaha. Mapenzi kati yao yalizidi kunawiri huku wazazi wao wakiamini kuwa wawili wale walikuwa ni ndugu walioshibana.

Baada ya miezi mitatu tangu walipoanza mchezo wao Suzy alianza kubadilika. Alionekana akinawiri, huku matiti yakiongezeka ukubwa. Alikuwa na kila dalili ya kuwa na ujauzito. Alipojigundua kuwa amenasa alimfahamisha haraka Ayubu.

“Ayubu” Suzy aliita akiwa amejilaza kwenye kifua cha Ayubu.

“Niambie mpenzi” alijibu Ayubu kwa kujitutumua utafikiri alikuwa baba mwenye nyumba ile.

“Nina tatizo”

“Tatizo gani? Ayubu alihoji kwa mashaka.

Kitu kilichomshangaza Ayubu ni kwamba Suzy alikuwa akilia badala ya kuzungumza maneno yale.

“Sasa kama unalia mi nitakusaidiaje?”

“Nina…nina…nina ujauzito Ayubu” alisema na kuanza kulia kwa sauti.

“Mungu wangu!! Una nini Suzy, mimba? Nimekwisha!” Ayubu alihamaki huku ameweka mikono kichwani.

Taarifa zile zilimchanganya sana kijana Ayubu. Hakuelewa angefanya muujiza gani ambao ungeweza kumtoa katika tatizo lile alilokuwa amejitafutia mwenyewe. Taswira ya matatizo aliyokumbana nayo punde alipoingia jijini Dar es salaam ilimjia tena.

Alifahamu kuwa uhai wake ulikuwa matatizoni endapo Mzee Manyama angeligundua lile. Aliinua macho na kumtazama Suzy usoni.

“Suzy, Una mimba?” Akahoji kwa msisitizo huku akihisi kama vile alikuwa ndotoni na akategemea Suzy amwambie kuwa maneno yale hayakuwa na ukweli bali ulikuwa ni utani tu.

Suzy alikubali kwa kichwa kuwa tumboni mwake kulikuwa na kijusi kilichokuwa zao la mahusiano yao ya kimapenzi.

“Baba yako ataniua” Ayubu akazungumza kwa hofu.

“No! sitakutaja” Suzy alizungumza kwa msisitizo.

“Inawezekanaje Suzy?”

“Nakupenda sana Ayubu, siwezi kukutaja”

“Sawa hautanitaja, kwahiyo utamtaja nani?” Ayubu akahoji kwa umakini.

“Tuwache muda utupe majibu” alizungumza Suzy huku akionekana kutokuwa n ahata chembe ya wasiwasi.

“Unajibu kirahisi sana Suzy, huoni kama hili ni balaa?” alizungumza Ayubu kwa hofu.

“Sasa imeshatokea mpenzi wangu, hata kama nikilia haiwezi kusaidia” Suzy alizungumza kwa kujiamini.

“Huoni kama baba yako atanikata kichwa?”

“Nimekwambia sikutaji Ayubu, mbona una wasiwasi” alizungumza Suzy kwa msisitizo.

“Unajua mimba ni pembe la ngo’mbe, halifichiki?”

“Unataka kusemaje?”

“Wakikubananisha utamtaja nani?” Ayubu aliendelea kunga’anga’ania kupata jibu la swali lake.

“Nitasema nilibakwa na watu nisiowafahamu” Suzy alieleza.

“Yani unavyojibu kirahisi utafikiri unaulizwa njia ya kwenda sehemu Fulani” Ayubu alizungumza huku akionekana kuchanganyikiwa kutokana na taarifa zile ya Suzy.

“Sikiliza Ayubu labda nikutoe wasiwasi” Suzy alizungumza huku alijiweka vizuri na kumtazama Ayubu usoni kwa umakini.

“Haya zungumza”

“Sijui nitamtaja nani, lakini hata kama nichinjwe siwezi kukutaja mpenzi wangu” alizungumza Suzy kwa msisitizo wa hali ya juu.

“Hivi yule mzee ndio utamjibu kirahisi rahisi hivyo?” Ayubu aliendelea kuonesha wasiwasi juu ya suala lile.

“Ayubu, baba yangu ananipenda sana. Hawezi kunifanyia ukatili wowote ule” Suzy alizungumza kwa kujiamini.

“Mnh sawa lakini ninavyomtambua mzee yule, sijui” Ayubu alikubaliana na Suzy kwa shingo upande.

“Usijali mpenzi wangu, yani ninavyokupenda hivi halafu nikutaje uingie kwenye matatizo, kweli inawezekana?” Alizungumza Suzy huku akichezea kidevu cha Ayubu kwa vidole vya mikono yake.

“Nashukuru sana Suzy. Hata mimi nakupenda pia” alisema Ayubu na kumkumbatia Suzy.

Pamoja na kwamba Suzy alimuhakikishia Ayubu kuwa asingemtaja hata kama baba yake angemkatakata vipande kama nyama za mshikaki kamwe asingethubutu kumtaja, Ayubu moyo wake ulipoteza amani kabisa. alikuwa akiwaza na kuwazua kitu ambacho kingetokea endapo baba yake Suzy angegundua kuwa yeye ndiye kidume kilichomjaza upepo binti yake. Kuna wakati alipata wazo la kutoroka lakini ahadi aliyopewa na Suzy ya kuto kumtaja ilimpa moyo na kuendelea kuvumilia.

Siku zilivyozidi kwenda Suzy naye ndivyo alivyozidi kubadilika. Kama alivyosema Ayubu kuwa mimba ni pembe la ngo’mbe haliwezi kufichika ndicho kilichotokea. Hatimaye Mama Suzy aligundua hali aliyokuwa nayo binti yake kipenzi.

Mama Suzy alitumia busara na hekima kuzungumza na binti yake Suzy. Mama yule aliandaa mazingira ya urafiki kutaka kufahamu mtu ambaye alikuwa amehusika na ujauzito ule aliokuwa nao mtoto wao kipenzi.

Pamoja na mbinu ile ya urafiki na upendo uliotumika lakini Suzy hakuweza kumtaja mtu ambaye alihusika na ujauzito ule.

“Suzy mwanangu, ni bora uniambie mapema kuliko baba yako akigundua jambo hili” alizungumza mama Suzy kwa upole.

“Mama mimi sina mimba” Suzy alikana pamoja na kwamba alikuwa na dalili zote za kuwa mjamzito

“Suzy unajua usitake kunisumbua, nambie nani amekupa huo ujauzito?” mama Suzy alianza kuzungumza kwa ukali kidogo baada ya kuona binti yule hampi ushirikiano wa kutosha.

“Sasa mama nitamtaja nani wakati nimekwambia sina mimba” Suzy alizungumza kwa sauti ya kulalamika kama vile alikuwa ameonewa.

Mama Suzy alisimama na kumshika Suzy kwenye mabega na kumtikisa kwa nguvu mara kadhaa na mwisho akamteremshia kofi moja takatifu kwenye shavu lake la kushoto.

“M a m a N a k u f a a a!” Suzy alilia kwa sauti baada ya kupokea kipigo kile cha kushitukiza.

“Sema umetoa wapi hiyo mimba pumbavu wewe!” mama Suzy alizungumza kwa sauti kubwa nay a ukali baada ya kubaini kiburi cha Suzy.

Kelele za mama Suzy nab inti yake zilimgutusha Ayubu ambaye alikuwa chumbani kwake amepumzika. Ilimbidi kutoka na kusimama mlangoni kwa Suzy kusikiliza kilichokuwa kikiendelea. Alipogundua kuwa binti yule alikuwa akiadhibiwa kwa kugoma kumtaja mtu aliyempa ujauzito, Ayubu alirudi chumbani kwake taratiibu na kujiweka tayari kwa matokeo yoyote.

Baada ya Ayubu kurejea chumbani kwake mzee Manyama alikuwa anarejea kutoka kazini. Kwa bahati mbaya au nzuri alisikia sauti ya mke wake akibishana na Suzy kule chumbani. Mzee yule akasimama pale mlangoni kwa Suzy kusikiliza muelekeo wa mazungumzo yale.

Mzee Manyama hakuweza kuamini masikio yake baada ya kusikia mabishano yale yalikuwa ni kuhusu binti yake Suzy kupata ujauzito. Mzee yule akasukuma mlango na kuingia chumbani mle bila kubisha hodi.

Mama Suzy na inti yake walipomuona mzee Manyama wote wawili walishituka, mama Suzy akajibaraguza ili mume wake asigundue kilichokuwa kinaendelea chumbani mle.

“Kuna nini?” alihoji mzee yule kwa umakini mkubwa.

“Hakuna kitu mume wangu” mama Suzy akajibu kwa upole.

“Pumbavu, unafuga maradhi! Nimesikia kila kitu” alisema Mzee Manyama huku mkono mmoja ameshika kiuno na mkono mwingine akimnyooshea kidole Mama Suzy.

Mzee Manyama alimtazama Suzy kwa hasira na kujikuta akipumua kwa nguvu utafikiri amebebeshwa tenga la madafu.

“Sikiliza we mbwa, Tusipotezeane muda. Sema ni nani aliyefanya huo upuuzi?” mzee Manyama alitoa amri huku akimtolea macho binti yule.



Mama Suzy aliinuka na kwenda chumbani kwa Ayubu na kupaza sauti kumuita. Ayubu moyo ulimpasuka akahisi amekwisha kutajwa. Alipotoka mama Suzy alimtuma mtaa wa pili kuchukuwa pesa zake alizokuwa akizidai kwa mama Halima. Lengo la mama Suzy ni kumfanya Ayubu asijue kilichokuwa kikiendelea kwa binti yake.

Ayubu alipokuwa akielekea kwa mama Halima alikuwa ametingwa na mawazo. Alifahamu kuwa kurudi tena nyumbani kwa mama Suzy ndio ungekuwa mwisho wa maisha yake. Alimfahamu mzee Manyama kuwa alikuwa tayari kupoteza uhai wa mtu kwaajili ya binti yake yule aliyekuwa akimpenda kama mboni ya macho yake.

Ayubu alipofika nyumbani kwa mama Halima, akakabidhiwa kiasi cha shilingi Elfu Hamsini za kitanzania. Baada ya kupokea pesa zile alianza safari ya kurudi nyumbani kwa mama Suzy. Alipokaribia nyumba ile akasimama na kutafakari aende ama asiende tena kwenye mjengo ule. Alipokumbuka ahadi ya Suzy alipata nguvu ya kwenda lakini alipowaza endapo Suzy angemtaja ingekuwaje, hapo nguvu zilimuishia kabisa.

Alikwenda moja kwa moja hadi nyuma ya nyumba na kujibanza akisikiliza kilichokuwa kikiendelea chumbani kwa Suzy. Alimsikia Suzy akilia huku akikataa kumtaja mtu aliyempa ujauzito. Mzee Manyama alipoona Suzy alikuwa akionesha kiburi, alikwenda chumbani kwake na kurudi na bastola. Alimnyooshea Suzy huku akiwa na hasira.

“Heri kuishi bila mtoto kuliko kuishi na mbwa kama wewe. Ayubu anatosha kuwa mtoto wetu. Sasa chagua moja kati ya kufa ama kumtaja mtu aliyekupa huo ujauzito” mzee yule alizungumza kwa hasira huku akiwa amenyoosha bunduki ile kwa binti yake.

“Basi….basi….baba…nam…namtaja” hapana chezea bunduki wewe! Suzy alianza kuweweseka baada ya kuona kitu ile ikimtazama kwa hamu.

“Mtaje Suzy, utakufa mwanangu” mama Suzy alisihi huku akilia.

“Ni…ni….ni..A..A…Nimebakwa baba” alizungumza Suzy.

“Buriani uwasalimie kuzimu na uwaambie huku duniani hakuna tena mambo ya kijingajinga” alizungumza mzee Manyama na kuiseti vizuri bastola yake tayari kwa kumwaga ubongo wa Suzy.

“Taja mwanangu utakufa wewe” mama Suzy akapaza sauti kwa hofu ya kumpoteza binti yake.

“Basi baba nataja mimi” alizungumza Suzy kwa hofu.

“Mtaje sasa!” Mama Suzy akasisitiza.

“Ni…ni…ni Ayubu baba naomba unisamehe” hatimaye Suzy akamtaja mwanaume aliyekuwa amehusika kumtandika mimba ile.

“What?” Mzee Manyama alihamaki kusikia kuwa Ayubu ndiye mhusika wa ujauzito ule.

Kule nje Ayubu moyo ulimpasuka ‘P a a a a!” baada ya kusikia jina lake limetajwa na Suzy. Alianza kuhisi mapigo ya moyo yakienda kasi huku mwili ukitetemeka kwa wasiwasi, hofu na woga.

Mama Suzy na mume wake hawakuamini kama kijana waliyemuokota na kumpa hifadhi, wakamuamini na kumpenda kama angeweza kuwalipa kwa kuwafanyia uchafu wa namna ile.

“Shukurani ya punda ni mateke. Lazima afe!” alisema Mzee Manyama na kufungua mlango kutoka kwa hasira kwenda kummaliza kijana aliyeharimu maisha ya binti yake.

Ayubu aliposikia Mzee Manyama alikuwa anamtafuta yeye hakuchelewa kufanya maamuzi kule nyuma ya nyumba. Aliamua kutimua mbio na kutoweka mazingira yale ya nyumbani kwa mzee Manyama.

****

Kule Tanga nyumbani kwao Ayubu, Mzee Nyiruka alikuwa akitengeneza baiskeli yake chini ya mwembe. Pembeni alikuwa amekaa mama Ayubu akichambua mboga za majani. Mama Ayubu alimtazama mume wake kwa kitambo kisha akamuita.

“Baba Ayubu”

“Unasemaje” aliitika Mzee Nyiruka huku akiendelea kugongagonga baiskeli yake.

“Hivi inakuwaje kuhusu huyu Ayubu” alihoji mama Ayubu

“Hata mimi huwa nawaza. Sijui mwanangu kama ni mzima au laa” mzee Nyiruka alizungumza kwa masikitiko.

“Maana ni muda mrefu sasa, huyo Kondo mwenyewe ndio amesema hakukutana naye huko Daslam”

“Tena usinitajie huyo Kondo, kama asingekuwa yeye wala Ayubu wangu asingeaca shule na kutoroka nyumbani…” mzee Nyiruka alizungumza kwa hasira.

“Kwahiyo tunafanyaje?” Mama Ayubu alihoji kwa umakini.

“Ah! Tumuachie mungu bwana” alisema Mzee Nyiruka akionekana hasira zote za kuondoka kijana wake bila ya kuaga zilikuwa zimetoweka. Aliumia sana kumpoteza kijana wake ambaye ndiye aliyekuwa tegemeo lake.

Wakati Mzee Nyiruka na mke wake walipokuwa wakiendelea na mazungumzo walijikuta katika mshangao mkubwa. Ayubu alikuwa amesimama pembeni akiwaangalia kwa tabasamu. Waliona tukio lile kama muujiza uliotendwa na Muumba.

Mama Ayubu alimrukia mwanawe na kumkumbatia kwa furaha huku machozi yakimtoka. Alipomuachia akamtazama usoni kwa sekunde kadhaa pasipo kuzungumza neno lolote.

“Shikamoo Mama” ayubu alivunja ukimya kwa kumsalimia mama yake lakini Mama Ayubu hakuitikia salamu ile bali alimvuta tena kijana wake na kumkumbatia kwa nguvu huku machozi yakiendelea kububujika kwenye mifereji ya mashavu yake.

****

Kitendo kilichofanywa na Ayubu hakikuweza kuaminika pale nyumbani kwa mzee Manyama. Amani ikawa imetoweka, lawama zote zikamshukia mama Suzy. Mama Suzy hakuwa na la kuzungumza zaidi ya kukubali kubeba lawama ile kwasababu yeye ndiye aliyejifanya kuwa na huruma na kumsomba Ayubu mtaani na kumleta ndani.

“Amakweli huruma huzaa dhambi” kauli hii ndiyo iliyokuwa ikijirudia kichwani mwa Mama Suzy mara kwa mara. Alifahamu wazi kuwa uhai wake ulikuwa mikononi mwa mzee Manyama kwasababu alimjua jinsi alivyokuwa hapendi masihara kwa binti yake.

Mzee Manyama alipiga teke mlango wa chumbani kwa Ayubu na ulipofunguka akaingia huku bastola akiwa ameitanguliza mbele lakini Kinyume na alivyokuwa ametegemea, hakumkuta adui yake chumbani mle. Akazunguusha macho kila sehemu mle chumbani kujaribu kumsaka lakini hakufanikiwa kumuona. Aliiweka bastola yake kiunoni na kutoka nje.

Mzee Manyama alizunguuka kila kona abayo alihisi Ayubu angekuwepo kule nje lakini pia hakufanikiwa kumpata. Alirejea ndani walipokuwepo binti yake na mke wake huku akiwa ametawaliwa na hasira.

“Nyie kunguru! Huyu mende amekwenda wpi?” Mzee Manyama alihoji kwa hasira.

“Ni…ni..nili….nili…” Mama Suzy akajikuta akishindwa kujibu.

“Nyoko nini? Ongea Ayubu yuko wapi?” mzee Manyama alifoka na kumfanya Mama Suzy kushituka kama vile alikuwa usingizini.

“Nimemtuma kwa mama Halima”

“Kefuleee!! Nimemtuma kwa mama Halima” Mzee Manyama alimgilizia mkewake kwa kutolea sauti puani.

“Lakini…..” Mama Suzy alitaka kuzungumza kitu lakini akakatizwa kauli yake.

“Komaa! Namuhitaji Ayubu hapa. Na asipotokea utakufa wewe badala yake” aliseam mzee Manyama huku akitetemeka kwa hasira na mate yakimtoka kila alipozungumza. Sura yake ilikuwa imebadilika na kuwa kama vile mnyama mkali wa porini. Alionekana wazi kuwa alikuwa akimaanisha kwa kile alichokuwa anakizungumza.

Wakati wote huo Suzy alikuwa amejikunyata akisubiria hukumu yake. Alifahamu wazi kuwa alikuwa ametenda kosa kubwa sana. Moyo wake ulikuwa ukimuuma sana kwasababu yeye ndiye aliyekuwa akimshawishi Ayubu kufanya mapenzi. Akajiona kuwa yeye ndiye aliyekuwa anapaswa kufa badala ya Ayubu.

Mzee Manyama alielekea chumbani kwake kama vile kuna kitu alikuwa anakifuata, Suzy aliinuka haraka na kutoka nje. Lengo lake lilikuwa ni kwenda kumtafuta Ayubu na kumfahamisha hali halisi iliyokuwepo pale nyumbani. Ukweli ni kwamba hakuwa anafahamu alipokuwa Ayubu wakati ule. Kitu kilichomuumiza zaidi ni kuvunja ahadi yake ya kutomtaja Ayubu.

Suzy alijaribu kwenda kwa marafiki wa karibu wa Ayubu kwa lengo la kumtafuta lakini hakuambua kitu. Akakata tamaa na kuanza safari ya kurejea nyumbani kujiandaa kushuhudia kifo kikimchukua mtu asiyekuwa na hatia.

Suzy alipokuwa njiani kuelekea nyumbani alijiuliza endapo Ayubu asingerejea ni kitu gani ambacho kingemtokea mama yake aliyekuwa akimpenda sana. Akawaza afanye nini ili awaokoe watu wale wawili wasiokuwa na hatia kutoka mikononi mwa baba yake yule aliyekuwa na roho ya kikatili. Aliamini kuwa baba yake huyo asingeweza kumdhuru yeye kwasababu alikuwa akimpenda sana.

Suzy alipokaribia nyumbani kwao akakuta mambo ni tofauti na fikira zake. Sauti ya baba yake ilisikika ikiendelea kuzungumza kwa hasira.

“Kwanini umemuacha Suzy katoka?”

“Mume wangu sikumuona wakati anaondoka”

‘Wewe umekula njama na kishetani chako! Najua kamekwenda kumzuia Ayubu asirudi. Sasa nikiiona pua yake hapa ajue ni maiti” aliseama mzee Manyama kwa hasira.

Maneno yale ya mzee Manyama yalimshitua sana Suzy ambaye alikuwa karibu na dirisha la chumba cha wazazi wake. Mapigo ya moyo wake yakaanza kwenda mbio. Alikuwa anamfahamu vizuri sana baba yake yule, hakuwa na masihara kwa jambo alilokuwa analizungumza. Ni wazi alikuwa amekusudia kumtoa roho hata Suzy binti yake ambaye awali alikuwa anampenda sana.

Suzy alijivuta nyuma taratiiibu kwa mwendo wa kunyata na alipofika hatua kadhaa kutokea pale dirishani akaanza kutimua mbio utafikiri alikuwa anakimbizwa na simba.



Pamoja na kwamba Suzy alikuwa ni mkosaji lakini hakuwa tayari kupoteza uhai wake kizembe zembe. Alifanikiwa kuyaacha mazingira ya nyumbani kwao ambayo kwa wakati ule alikuwa akiyaona kama shimo la jehanamu na yasingemfaa tena.

Akiwa chini ya mti uliompatia kivuli kizuri maeneo ya Bamaga Suzy aliendelea kuwaza na kuwazua. Kichwani mwake alikuwa akifikiria mahali pa kwenda, je ni nani angeweza kubeba jukumu la kumlea pale jijini. Akamkumbuka rafiki yake MORINE ambaye alikuwa akiishi maeneo ya Tabata kimanga.

Suzy alijikuta akitoa tabasamu la matumaini lakini ghafla likakatika baada ya kukumbuka kuwa hakuwa na hata senti moja mfukoni ambayo ingemsaidia kama nauli. Hakutaka kupoteza muda kuendelea kuwaza, alisimama na kushika barabara ya vumbi ambayo alikwenda nayo hadi Mwenge kwenye kituo cha mabasi. Alisogea hadi maeneo ambayo mabasi yaliyokuwa yakienda Tabata Kimanga yalipokuwa yakisimama.

Abiria waliokuwa wakielekea huko walikuwa ni wengi mno kitu kilichopelekea kugombania kuingia kwenye daladala. Suzy alitulia kwa muda akitafakari cha kufanya. Sio kwamba alikuwa hawezi kugombania, Laa! Tatizo lilikuwa je angelipa nini pindi konda angehitaji nauli yake?

Wakati amesimama pale stendi alitokea msichana mmoja aliyekuwa amevalia vizuri tu na kumsogelea Suzy. Sura ya yule msichana ilisomeka kuwa alikuwa na tatizo.

“Za saa hizi dada” Yule msichana alisalimia.

“Safi” Suzy alijibu kwa mkato.

“Samahani dada nimeibiwa hela, naomba unisaidie mia tatu tu ya nauli” dada yule alitoa shida zake kwa Suzy. Suzy alivuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu. “Ungejua kuwa nina matatizo zaidi yako wala usinge nisogelea” akajisemea kimoyo moyo na kumjibu kuwa hakuwa na pesa.

Msichana yule aliondoka kwa shingo upande huku akiamini kuwa Suzy alikuwa amemnyima. Alishuhudia msichana yule akimuendea mtu mwingine na kumueleza shida yake, yule aliyeelezwa shida aliingiza mkono mfukoni na kutoa noti ya shilingi mia tano akamkabidhi. Yule dada alirejea kwenye msongamano wa watu na kuanza kugombania usafiri.

Kitendo cha yule msichana kufanikiwa mbele ya macho yake kilimpa moyo Suzy. Na yeye alimsogelea mwanaume mmoja aliyekuwa ameketi kwenye kibanda cha magazeti akikagua na kusoma vichwa vya magazeti hayo. Suzy akamsemesha.

“Shikamoo”

“Marahaba” Mwanaume yule alijibu na kuendelea kusoma gazeti.

“Samahani baba”

“Unasemaje?”

“Naomba unisaidie miatatu, nimepoteza nauli”

Mwanaume yule alimtazama Suzy na kutoa msonyo kisha akaendelea kusoma. Suzy alipoona vile ankaondoka na kwenda kusimama pembeni. “kumbe inahitaji moyo” Suzy alijisemea pale alipokuwa amesimama. Alikumbuka jinsi alivyokuwa akiwafukuza na kuwatukana watu waliokuwa wakimfuata na kumuomba msaada. Akatupilia mabli mawazo yale na kumuendea mwanamke mmoja aliyekuwa akijipanga kugombania usafiri.

“Za saa hizi dada”

“Poa”

“Naomba nisaidie nauli dada yangu imepotea”

“Kwahiyo mimi ndio ATM yako? Unadhani pesa zinaokotwa? Wewe si mwanamke kama mimi? nilivyozipata hata wewe unaweza kuzipata” dada yule alimjibu kwa nyodo. Majibu aliyoyapata kutoka kwa msichana yule yalimkera sana Suzy na kujikuta akikamata barabara ya lami kwa miguu.

“Potelea mbali, nitafika tu” alijisemea huku akichanganya hatua.

Wakati akiendelea na safari yake hiyo kwa miguu hakuweza kuamini macho yake, aliokota pochi ndogo iliyoelekea kuwa na vitu ndani yake. Alichofanya ni kuingia uchochoroni na kuanza kuipekuwa.

“Mhn!” alijikuta akiguna baada ya kuona rundo la hirizi ndani ya pochi ile, akaiachia chini kwa woga huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio.

Zile hirizi zilidondoka chini na alipotazama vizuri akaona noti mbili za shilingi elfu tano tano. Aliinama na kuokota pesa zile kisha kwa haraka sana akatoka pale uchochoroni. Ingawa alijawa na woga lakini moyo wake ulifarijika baada ya kupata pesa ambazo zingemsaidia kufika kwa rafiki yake Moryne. Wakati huo alikuwa amekwisha fika maeneo ya Ubungo mataa. Alikwenda kupanda gari ya Tabata ingawa kwa taabu kutokana na mminyano wa abiria kugombania usafiri.

Alifanikiwa kufika nyumbani kwa kina Moryne mida ya saa tisa jioni. Alipobisha hodi alifunguliwa mlango na mtu ambaye hakumtegemea. Alikuwa ni yule msichana aliyemuomba amsaidie nauli kule Mwenge. Akasita kidogo na kushituka lakini akajikausha kama vile hakuwahi kukutana na binti yule siku hiyo. Msichana yule alimtazama Suzy usoni kwa sekunde kadhaa kama vile alikuwa anajaribu kumfananisha kisha akamkaribisha ndani. Alionekana kutomkumbuka vizuri Suzy.

“Karibu” Alisema binti yule.

“Moryne yupo” Suzy alihoji.

“Ndio yupo, karibu ndani” Binti yule akamkaribisha Suzy.

Moryne alipomuona Suzy akapatwa na mashaka kutokana na muonekano wake siku hiyo. Mavazi aliyokuwa amevaa hayakuwa ya kawaida yake, nywele zake zilizotiwa dawa zilikuwa zimetimka timka. Sura yake ilikuwa kavu na iliyo pauka kutokana na kutopakwa mafuta.

“Vipi Suzy kwema?”

“Sio kwema rafiki yangu Moryne”

“Una nini?”

“Nina matatizo makubwa sana Moryne. Ila njaa inaniuma sana, sijakula tangu asubuhi” Suzy alisema baada ya kukaribishwa ndani.

Moryne alimuandalia rafiki yake huyo chakula na baada ya kula mazungumzo yakaendelea. Suzy alimueleza kila kitu rafiki yake huyo. Moryne akaonekana kumuonea huruma sana rafiki yake.

“Pole sana Suzy” alisema Moryne kwa masikitiko.

“Nahitaji msaada wako Moryne”

“Mnh!”

“Mbona unaguna Moryne, nisaidie mwenzio. Sina pa kwenda”

“Sawa, lakini si unajua kuwa mimi naishi na wazazi wangu?”

“Najua hilo Moryne lakini…..”

“Sikiliza Suzy, nina moyo wa kukusaidia, tatizo wazazi wangu ni wakali sana hawawezi kukubali uishi hapa”

“Kwahiyo utanisaidiaje Moryne?”

“Mnh! Kwakweli sina msaada rafiki yangu, nikithubutu tu ujue sote tunafukuzwa hapa ndani”

“Ok. Basi ngoja mi niondoke” Suzy alisema kwa unyonge na kujiinua kutoka kwenye kochi.

Moryne alimtazama tena usoni Suzy na kujikuta huruma ikimjaa. Ni kweli alikuwa akimhurumia lakini kwa msaada wa kuishi pale kama aliokuwa akiuhitaji Suzy alishindwa kumsaidia. Wazazi wake wote walikuwa hawapendi mambo ya kipuuzi kama yale aliyoyafanya Suzy.

“Kwahiyo unaelekea wapi?” alihoji Moryne

“Sijui, ila usijali”

“No Suzy. Nimekumbuka kitu”

Suzy aligeuka na kumtazama Moryne usoni pasipo kujibu kitu. Alitamani kusikia jambo alilokuwa anataka kulizungumza rafiki yake huyo.

“Unamkumbuka Naima?”

“Yupi?’

“Naima Thomas. Yule aliyeacha shule tulipokuwa kidato cha kwanza.”

“Aaaa ndio nimemkumbuka”

“Sasa yule anaweza kukusaidia” Moryne alizungumza na kumueleza kuwa Naima alikuwa akiishi peke yake kwenye chumba cha kupanga, kwahiyo angeweza kumsaidia kwasababu hakuwa anapangiwa na mtu kufanya chochote.

Kama alivyoelekezwa na Moryne, Suzy alikwenda moja kwa moja maeneo ya UBUNGO MSEWE kumtafuta huyo rafiki yao Naima.

****

Kule Tanga kwa Ayubu pamoja na kwamba alikuwa anashukuru kuondoka salama kutoka mikononi mwa mzee Manyama lakini roho yake ilikuwa ikimuuma sana kumuacha Suzy ktika mazingira hatarishi tena akiwa na ujauzito wake.

Mara kwa mara Ayubu alikuwa akiota ndoto kuwa Suzy amejifungua mtoto mzuri sana wa kiume ambaye alikuwa amefanana naye kila kitu. Lakini maisha ya Suzy na mtoto wake huyo yalikuwa ni magumu mno. walikuwa wakinyanyasika mitaani. Lakini kila alipotaka kumshika mtoto aliweweseka na kugutuka kutoka usingizini huku akipiga makelele.

Mzee Nyiruka alifuatilia tabia ile ya kijana wake ya kupayuka hovyo usiku. Ikabidi amuite kijana wake na kuhoji sababu iliyokuwa ikipelekea kuweweseka na kupiga mayowe kila siku usiku. Ayubu alikosa majibu ya swali la baba yake kuhusiana na tabia ile ngeni. Akajibu kuwa ilikuwa ni ndoto tu.

Hata hivyo hali ile iliendelea kumtesa sana Ayubu siku hadi siku hadi kuhisi kujichukia mwenyewe. Alipoona mambo yanazidi kumuwia magumu ikambidi amueleze ukweli wote baba yake kuhusiana na mkasa mzima uliomkuta akiwa jijini Dar es salaam.

Baada ya maelezo yale ya Ayubu, mzee Nyiruka akamshauri kijana wake aende jijini Dar es salaam kumtafuta Suzy na kujua maendeleo yake. Maamuzi yale ya mzee Nyiruka yaliushitua sana moyo wa kijana yule. Hakuweza kuelewa kirahisi malengo ya baba yake dhidi ya maamuzi yake yale magumu.

“Baba nirudi tena Bongo?” Ayubu akahoji kwa mshangao.

“Lazima ufanye hivyo” alizungumza mzee Nyiruka kwa msisitizo.

“Siwezi baba”

“Tambua kuwa damu ni nzito kuliko maji. Lazima ukajue maendeleo ya mwenzio” alieleza mzee Nyiruka.

“Baba Bongo hakufai” alieleza Ayubu kwa sauti ya kukata tamaa lakini iliyojaa msisitizo.



“Sikiliza mwanangu, Jiji la Dar linahitaji utumie ubongo. Kinyume na hapo utaambulia kero na makucha ya jiji yatakurarua” mzee yule mtu mzima alieleza kwa kutumia busara zake za uzee.

“Nitafikia kwa nani baba?”

“Utafikia gest”

“Hizo pesa zitatoka wapi?”

“Nitakupatia pesa nilizozipata kwa kuuza machungwa kwenye shamba la Mkambarani” alisema Mzee Nyiruka kwa msisitizo.

Ayubu aliinamisha shingo kwa muda akitafakari maneno ya baba yake. Ni kweli alikuwa akimhurumia sana mpenzi wake Suzy, na ndoto alizokuwa akiziota zilimuweka wazi kuwa Suzy alikuwa katika wakati mgumu sana.

Ayubu alijikuta akikubali kwenda kumfuatilia Suzy wake ingawa alipomkumbuka mzee Manyama roho yake ikasita.

“Sawa baba nimekubali, lakini….”

Ayubu alitaka kuongea kitu cha mashaka na kukatisha tamaa lakini akakatizwa na mzee Nyiruka.

“Lakini nini?”

“Tatizo ni baba yake Suzy” Ayubu alizungumza kwa msisitizo.

“Hawezi kukudhuru tena”

“Haa! we baba unasema tu. Mzee Manyama sio mtu wa kuchezea” Ayubu alieleza kwa msisitizo.

“Nimekwambia nenda! Ufanye uwezalo lakini uonane na mwenzio asije akapata mawazo potofu ya kuua mtoto wetu” alisema mzee Nyiruka na kuinuka kuelekea ndani.

Ayubu akajikuta katika lindi la mawazo, hakutaka kusikia habari ya jijini Dar es Salaam tena katika maisha yake. Mateso aliyo yapata ndani ya jiji lile yalikuwa yanatosha.

Hata hivyo Ayubu hakuwa na namna zaidi ya kukubaliana na baba yake kwasababu mzee yule naye alikuwa ni mtata hasa alipokuwa akitaka jambo lake halafu lisifanyike. Kwa shingo upande Ayubu alikubali kurudi tena jijini Dar Es Salaam ili kumridhisha baba yake. Alijipa moyo kuwa mateso aliyoyapata mwanzo pengine yalitokana na kutobarikiwa na wazazi wake.

****

Kwa bahati nzuri Naima hakumuonesha roho mbaya Suzy. alimpokea na kuamua kuishi naye kwenye chumba chake kimoja kama ndugu yake.

Maisha ya kuishi mbali na wazazi yalikwishaanza kumzoea Suzy. Naima ndiye aliyekuwa mama yake na baba yake kwa wakati huo. Ingawa mara kadhaa alipata wazo la kurudi kuwaomba radhi wazazi wake lakini roho yake ilisita. Alijua kuwa kama angethubutu kuingiza mguu wake pale kwa mzee Manyama basi ndio ungekuwa mwisho wa maisha yake.

Biashara kubwa ya kukaanga samaki ndiyo iliyokuwa ikiwaweka mjini Suzy na mwenyeji wake Naima. Naima alikuwa ni mwanamke mchakarikaji ambaye hakuwa tayari kunyanyaswa na dhiki za Jijini. Mwanzoni Suzy alikuwa legelege lakini hali halisi ikamfanya naye kuwa mchakarikaji kama rafiki yake Naima.

Mbali na biashara ya samaki Naima alijishughulisha pia na biashara ya kuuza mwili. Mchana alikuwa akiuza samaki pamoja na Suzy lakini ilipofika usiku aliingia kwenye shughuli yake ya kujiuza ambayo aliifanya kwa siri pasipo hata Suzy kugundua.

Siku moja Naima alipokuwa akitoka kuelekea katika shughuli yake ya udangaji, mida ya saa mbili usiku alikuwa amevalia sketi fupi iliyokuwa ikionesha sehemu kubwa ya mapaja yake. Mapaja meupe yaliyojazia vizuri kiasi cha kuleta mvuto wa kimapenzi yaliendana vyema na miguu yake mizuri iliyopendezeshwa kwa viatu vyenye visigino virefu na kamba ambazo zilizunguushwa kiufundi kwenye mguu wa bia hadi karibu na magoti. Kutokana na ufupi wa sketi yake, kama angeangusha kitu basi asingeinama kukiokota bali angechuchumaa kwasababu kama angeinama basi sehemu ya makalio yaliyokuwa yameumbwa vizuri yangeonekana. Juu alikuwa amevalia blauzi ndogo isiyo na mikono ambayo ilishindwa kukutana na sketi yake maeneo ya kiunoni, hivyo kitovu chake kilichobonyea kwa ndani kiliweza kuonekana. Blauzi ile iliyokuwa nyeupe ya kitambaa laini kilicho tereza haikuficha matiti ya Naima yaliyo umbwa kiuchokozi ambayo katikati yake kulilala kidani cha dhahabu kilichokuwa na umbo la kopa. Miguuni alikuwa amevalia. Kiukweli Naima alikuwa ameumbwa mtoto wa watu.

Suzy alimtazama rafiki yake yule jinsi alivyokuwa amejivalisha na kujikuta katika hali ya mshangao. Pamoja na kwa Hata yeye Suzy alikuwa akipenda sana mavazi ya namna ile lakini Naima alikuwa ametia fora na kujikuta akishindwa kuvumilia.

“Naima” aliita Suzy kwa sauti ya upole.

“Sema best….”

“Umependeza sana, lakini….”

“Lakini nini?”

“Nahisi upo uchi” Suzy alisema.

Naima alimtazama Suzy kwa jicho la dharau huku amebenjua midomo yake, alimuangalia kuanzia kidole gumba cha mguu hadi kwenye unywele wa mwisho kisha akamshusha na kumpandisha tena, mwisho akaachia msonyo mrefu uliojaa chembe chembe za dharau.

“Unazungumza wewe kama nani?” alizungumza Naima kwa hasira.

“Basi Naima naomba nisamehe sikujua kama nitakuudhi”

“Naona umeota mapembe sasa unataka kuniwekea masharti nyumbani kwangu” alisema Naima huku akijitighisha tingisha na mkono mmoja ameupachika kiunoni.

“Nisamehe best” Suzy alizungumza kwa upole.

“Hivi…. ngoja nikuulizen kitu” alisema huku akijiweka kwenye kochi.

“Unadhani haka kabiashara ka samaki peke yake ndiko kanako kuweka mjini? Na hako kamimba kako kataishi vipi kama nisipo chakarika?” Naima alizungumza huku akimkodolea macho Suzy.

“Mbona sikuelewi Naima”


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG