Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

MESSAGE YA FUNDI UMEME - 5

   


Chombezo : Message Ya Fundi Umeme 

Sehemu Ya Tano (5)


“Mimi sikutaki!” mume wangu naye akajibu kwa msisitizo

“Mimi nakutaka”

“Eboo! Wewe umetumwa?” Mume wangu alizungumza kwa ukali zaidi na kusimama kutaka kumtandika makofi binti yule.

“Moyo wangu ndio umenituma” alijibu binti yule huku akiwa amesogea nyuma kidogo kutaka kukimbia.

“Haya toka! Toka! Peleka moyo wako huko” mume wangu alizungumza huku akimuelekezea Yusrah mlangoni.

“Sitoki, hadi uniambie kama na wewe unanipenda” Jamani nyie binti yule aliendelea kunga’nga’nia mume wangu, sijui kweli amerogwa? Au alikuwa ni pepo!

“Sasa nitakupenda vipi Yusrah wakati nimekwambia nina mke wangu?” Mume wangu alizungumza kwa msisitizo.

“Magesa Magesa, hivi kabisa unafikiri una mke? Kwa taarifa yako hauna mke wewe una mzoga!” alizungumza Yusrah.

“We Malaya kumbe hunijui nisubiri sasa” Magesa alizungumza huku akijichomoa pale kwenye kiti na kumfuata Yusra kwa hasira.

Thubutuuu! Unafikiri yule chotara alibaki pale na kiburi chake? Nakwambia alichomoka kama mshale kutoka ofisini kwa mume wangu.

Magesa alifunga mlango kwa hasira na kurejea kwenye kiti chake na kujiweka kwa nguvu huku akisonya sonya.

Kule nje Yusrah alikuwa meshikilia viatu mkononi huku akigeuka nyuma kama Magesa likuwa anamfuata. Alipoona hakukuwa na mtu aliyekuwa anamfuatilia masikini ya mungu aliwacha kukimbia binti wa watu. Alikuwa akihema juu juu utafikiri ameponea chupuchupu kuliwa na simba.

“Shenzi!” alizungumza Yusrah huku akitoa simu yake kutoka kwenye pochi.

Msichana yule aligeuka nyuma na kulitazama lile jengo lililokuwa na ofisi ya Magesa. Hasira zikampanda kiasi cha kujikuta akitetemeka.

“Shenzi huyo mwanamke wake si ndio anamchetu, ngoja nimuoneshe kama noma na iwe noma” alizungumza Yusra na kukohoa mara mbili huku akigeuka nyuma kuhakikisha usalama wake.

Kumbe mshenzi yule alichukua namba zangu kutoka kwenye simu ya mume wangu na kuzisevu kwenye simu yake. Sasa alivuta jina langu na kunipigia simu huku akiwa anatetemeka kwa hasira mbwa yule.

****

Nikiwa nimejilaza pale kitandani nikiendelea kulia kwa kwikwi na majuto kutokana na matendo yangu ghafla simu yangu ikaita. Nikajitahidi kunyamaza na kupokea simu ile iliyokuwa ikipigwa na namba ngeni.

“Haloo” nikaitika baada ya kupokea simu ile.

“Haloo nyumba ya simu” sauti ya kike ilinijibu.

“Samahani nani mwenzangu?” nikahoji kwa wasiwasi kutokana na lile jibu nililolipata.

“Mimi mke mwenzio” sauti ile ilinijibu.

“Mke mwenzangu! Wa wapi?” nilihoji kwa mashaka.

“Kwani mume wako yuko wapi?” sauti ile ilijibu kwa nyodo.

“Unajua unazungumza na nani?” nikahoji huku nikihisi mtu yule angekuwa amekosea namba.

“Wewe si mke wa Frank?” auti ile ilipomtaja Frank nikahisi moyo wangu ukipata ahuweni kwasababu sikuwa namfahamu huyo Frank.

“Sasa si umeona, nimekwambia umekosea namba mpendwa” nikazungumza kwa sauti ya upole huku nikiamini mtu yule alikuwa amekosea nmba kweli.

“Hebu usijichetue mwanamke, wewe si mke wa Magesa wewe?” Sauti ile ikahoji kwa msisitizo.

Mapigo ya moyo yalianza kuongezeka spiti baada ya kusikia maneno yake kutoka kwa mwanamke yule. Inamaana Magea alikuwa ameoa huko Arusha? Kwakweli sikuweza kupata jibu kutoka kichwani mwangu.

“Napenda kukutaarifu kwamba mimi ni mjamzito” msichana yule alizungumza na kuufanya moyo wangu kushituka kidogo.

“Sasa ujauzito wako mimi unanihusu nini?” nikazungumza kwa kiburi.

“Unakuhusu kwasababu wewe ni mke mwenzangu, mtoto wangu mimi ni mtoto wako pia” Jamani nyie mwanamke yule alizungumza bila huruma.

“Nafikiri wewe utakuwa unaumwa dengue” nilizungumza kwa hasira huku nikihisi mikono ikitetemeka.

“Heheee! Hoyiii wanchefua mie” sauti ile ilicheka kwa dharau na kebehi.

“Hivi namba yangu umetoa wapi wewe simbirisi?” nikahoji kwa hasira mtoto wa kike.

“He unauliza tena wakati nimekwambia mimi mke mwenzio? Mume wako ndiye amenipa nikupigie na kukupa huu mzigo” mwanamke yule alizungumza kwa msisitizo.

“Haya mama asante kwa mzigo, mwambie nimeupata” nikajibu kwa sauti ya upole lakini iliyokuwa imejaa hasira.

“Tena nilitaka kusahau kitu”

“Haya nibandike lingine" Nikajibu kwa ufupi.




“Mume wangu anasema hivi, wewe endelea kuteseka. Na sisi tunaendelea kuponda raha jijini Arusha” mwanamke yule alizungumza kwa kujitapa.

Kutokana na ukali wa maneno aliyokuwa akiyamwaga mwanamke yule nilikata simu na kujitupa kitandani kwa hasira. Nilikuwa nikidhani mimi ni Malaya kumbe mume wangu alikuwa ni mchafu kuliko mimi.

Ndugu msomaji kwa kweli nilikuwa nimechoka kulia mimi jamani. mapenzi niliyaona ni kitu cha ajabu sana katika maisha ya mwanadamu. Mapenzi ukiyapelekesha na yenyewe yanakupelekesha. Usipokuwa makini unaweza ukajikuta unaokota maokopo na kuwa mwendawamu kabisa.

Sasa nasema vyovyote mtakavyonifikiria sawa tu! Vyovyote mtakavyoniita sawa tu liwalo na liwe! Kuanzia leo natangaza vita rasmi. Ama zangu ama za Magesa, Nasema mwenzangu amemwaga mboga, sasa na mimi namwaga ugali. Tena safari hii ninimeanza upya. Ari mpya, nguvu mpya na kasi ya ajabu. Kama picha sasa ndio limeanza” nikazungumza huku nikijiinua kutoka pale kitandani na kuelekea sebleni ambako niliwasha runinga yangu na kutazama taarifa ya habari.

Nikiwa pale sebleni mida ya jioni nikiendelea kuangalia runinga, simu yangu ya mkononi ikaita. Baada ya kupokea sauti ya Anthony ilisikika. Alikuwa ni mwanaume mmoja wa kisomari niliyewahi kulala naye kama mara tatu tu.

“Babeee” aliita Atoiny kwa sauti ya kubembeleza.

“Nambie Babaaa” name nikaitika kwa mbwembwe.

“Mbona hupatikani kwenye ile laini yako nyingine?” alihoji Anthony na kunikumbusha machungu yangu ya kuibiwa simu.

“Lakini si umenipata au?” nikajikuta nikizungumza kwa jazba kidogo.

“Mbona umekuwa mkali ghafla jamani baby wangu?” Anthony akazungumza kwa kunibembeleza.

“Ah naona unataka kunikoroga, kwani wapi imeandikwa ni lazima nitumie simu moja?” nikazungumza huku nikijitahidi kupunguza hasira baada ya kubaini sikuwa na sababu ya kukasirika pamoja na kwamba swali lake lile halikuwa limeninogea.

“Basi tuwachane na hayo baby wangu” alizungumza Antony kwa sauti ya upole.

“Haya niambie sasa ulikuwa unasemaje?” nikafanikiwa kupunguza jazba na kuzungumza kwa sauti ya upole.

“Naomba leo jioni niwe na wewe mrembo wangu jamani, nimekumisi sana” alizungumza Antony kwa ile sauti yake ya kubembeleza.

Wakati nilipokuwa nikitafakari lile ombi la Antny,simu yangu ya mezani ikaita. Nilikata simu ya Anthony na kupokea simu ya mezani. Ilikuwa ni sauti nzito na nene iliyokaribia kupasua spika za simu ile. Sauti ile haikuwa ngeni kwangu, ilikuwa ni sauti ya Mr.Mbega ambaye naye aliomba kutoka na mimi usiku huo. Wakati nikitafakari jibu la kumpa Mr.Mbega, mlango ulifunguliwa na Siraji akaingia sebleni mwangu.

Siraji alikuwa ni kijana mdogo lakini alikuwa na pesa nyingi sana. Kutokana na sababu hiyo nilikata ile simu pasipo kujibu kitu chochote. Nilikwisha amua kuwa na Siraji siku hiyo ili aweze kunipa majambozi na mapesa.

Ndio kama Mume wangu Magesa alikuwa ameamua kuoa na kuhama nyumbani sasa mimi ningefanya nini? Kitu kibaya na cha kudhalilisha simu za hao Malaya wake zilikuwa zikininyanyasa kila kulipokucha. WHY?

Nilimsogelea Siraji na kumsabahi kwa mabusu moto moto ya mashavuni na mdomoni. Siraji naye hakutulia bali alipeleka mkono wake wa kushoto kiunoni kwangu na kukikamata vyema huku mkono wa kuume akiwa ameuweka nyuma ya kisogo changu.

“Kwanini hupatikani kwenye simu yako?” alihoji Siraji huku akiwa amenikamata vyema kiunoni.

“Ooh baby mwenzio jana nilikwenda Kariakoo, vibaka wakaniotea” nikazungumza huku nikimshika kwenye mashavu na kumpiga busu moja matata.

“Thanks baby, lakini mbona simu hiyo hapo?” Siraji alizungumza huku akiikodolea ile simu niliyokuwa naitumia kuzungumza na Antony.

“Hii ni nyingine jamani baby, kweli kabisa mimi ni wa kutumia simu kama hii?” nkajibebisha mtoto wa kike.

“Mbona sasa unayo kama huwezi kuitumia?” Tony akanitania.

“Bwana achana nayo, mi sipendi kusikia hizo habari” nilizungumza na kumkumbatia kwa nguvu huku nikimpatia busu linguine zito zaidi ambalo lilimchanganya na kumfanya asahau ile bada ya simu na kuhamishia akili zake zote kwenye shughuli iliyokuwa imemleta pale nyumbani kwangu.

Sikuweza kuelewa jinsi ilivyokuwa lakini tulijikuta tukigalagala kwenye kochi pale pale sebleni. Yule kijana Siraji alikuwa akijitahidi kuzitafuta hisia zangu zilipo ili kufanya maandalizi ya matibabu. Naam pamoja na kwamba hakumfikia mume wangu Magesa lakini naye angalau alikuwa na kauwezo kidogo.

“Oooh Yes…mnh….mnmn…aamnm” nilijikuta nikijing’atang’ata mtoto wa kike pale kwenye sofa alilonunua mume wangu Magesa. Mambo aliyokuwa akiyafanya Siraji yaliweza kunifanya nimsahahu kabisa Magesa wangu, mwanaume niliyekuwa nikimfikiria tofauti na alivyo.

“Tayariiii…..we…sira….siraji….bwana… mie…taratiri aahmn!” Nililalama mke wa mtu kwa jinsi nilivyokuwa nikijisikia. Kama ni jukwaa lilikuwa limekwisha andaliwa vya kutosha ilikuwa imebakia kutekeleza dhumuni la kuandaa jukwaa hilio, yaani kuimba ama kucheza ngoma.

Siraji alikuwa na haraka sana, kwahiyo hakutumia muda mwingi kutawala jukwaa lile. Ndani ya dakika tano tu alikuwa hoi bin taabani. Alijilaza kwenye kochi mithili ya chatu aliyekuwa amemeza kondoo. Nilikunja sura na kusonya pasipo yeye kusikia. Nikatamani kumsukuma pembeni lakini nilipokumbuka mapesa yake nikajikaza na kumpapasa mgongoni taratiibu.

“Pole sana baba” nikazungumza huku nikimpapasa mgongoni.

“Asante mpenzi wangu, kweli wewe ni mtamu” Siraji alizungumza huku akipumua juu juu kama nguruwe.

“Leo umenifurahisha sana mpenzi, kweli mambo unayaweza” nikajifanya kumsifia vya uwongo na ukweli, si unajua tena mapenzi pesa utundu peleka hukoo kwa mkeo.

“Hii ni trela Prisca, nitakuwa nakufanyia zaidi ya haya” masikini kijana wawatu alijitutumua na kuvimba bichwa huku akijiona makaaali kumbe hakuwa na lolote kama bilinganya lililooza.

Nilimkumbatia kwa nguvu na kummiminia mabusu kibao kama matone ya mvua kwenye uso wake. Masikuni kijana wawatu akajiona yeye ndio alikuwa ni mwanaume kuliko wanaume wote hapa ulimwenguni.

Ghafla tulishituliwa na sauti ya mlango ukigongwa, kabla ya kuchukua maamuzi yoyote mlango ule ulikuwa umekwisha fungulia kwasababu hatukuwa tumeufunga kwa komeo. Hali ya wasiwasi ilikuwa imenitawala nikisubiri kuumbuka mwenzenu mie.

Kila mmoja alikimbilia nguo zake na kuanza kuvaa haraka haraka. Lakini nilipomuona mtu aliyefungua mlango akichungulia nikajikuta nikipata ahuweni. Alikuwa ni shoga yangu kipenzi Fatuma. Lakini nyuma ya Fatuma alikuwepo mtu mwingine aliyeongozana naye. Mtu yule hakuwa mwingine bali ni Ashrafu mpenzi wake mpya.

Macho yangu yalipokutana na macho ya Ashrafu nilishituka kidogo kwasababu kijana yule alikuwa ni rafiki wa karibu sana wa mume wangu Magesa. Pia kijana yule alikwisha wahi kunitongoza nikamkataa kwa kigezo cha kutopenda kumsaliti rafiki yake Magesa. Sasa siku ile alikuwa amekuja nyumbani kwangu na kunikuta nipo na mwanaume mwengine tena katika mazingira ya kutatanisha.

Fatuma alitabasamu kidogo kisha akamzuia Ashrafu asiingie ndani. Kitendo kile kilinisaidia sana kwani tulipata nafasi ya kutosha kuvaa nguo zetu mimi na Siraji na baada ya hapo nikawaruhusu Fatuma na Ashrafu waingie.

“Nimekuletea mgeni shoga” Alisema Fatuma huku akimtupia macho ya wizi yule msomali Siraji.

“Ahaa karibuni sana” Nilijibu kwa aibu, niliamini kuwa walikuwa wamekwisha fahamu kilichokuwa kikiendelea mle ndani.

“Ashrafu huyu ni shoga yangu anaitwa Priscaria” Fatuma alinitambulisha pasipo kufahamu kuwa wenyewe tulikuwa tukifahamiana zaidi ya sana.

“Nashukuru kukufahamu shemeji Prisca” Asharafu alijibu kwa kuniita shemeji, ingawa sikufahamu ushemeji ule ulikuwa kwaajili ya Fatuma ama mume wangu Magesa.

“Hata mimi nimefurahi, karibu sana nyumbani kwangu” Nilizungumza huku nikimpa mkono kinafki ili Fatuma asigundue kufahamiana kwetu mimi na Ashrafu wake.

“Priscaria” Fatuma aliniita na nilipomuangalia akanikonyeza.

“Abee shoga yangu” nami nikamkonyeza kumuashiria kuwa kama ingewezekana watupishe mimi na Msomari wangu tuendelee kupeana majambozi.

“Sisi sio wakaaji, tulikuwa tunapita tukaona tukusalimie” alisema Fatuma.

“Jamani mbona haraka hivyo”

“Wacha tuwahi tu bwana tutakuja siku nyingine”

“Basi haya karibuni tena jamani”

“Poa shemeji” Ashrafu alijibu hukua akiuelekea mlango.

Mimi na Fatuma tulikonyezana tena kisha wakaondoka na kutuacha mimi na yule msomari Siraji. Nilijiweka kwenye kochi na kutoa pumzi kwanguvu. Kitendo kile kilichotokea hakikunivutia kabisa. Hata hivyo nikajipa moyo kwa kupuuzia na kusema heti mbona Magesa huko alikokuwa alikuwa ananisaliti na kuoa kila kukicha.

*****

Ingawa siku hiyo sikupanga kutoka lakini Siraji msomali alikuwa amekuja kunitia hamu na hakuna chochote alichofanya nikaridhika. Niliingia bafuni na kujisafisha tayari kwa kuelekea kazini kutafuta mwanaume wa kuniondoa uchovu nilioletewa na Siraji msomari.

Nilijipara vya kutosha kisha nikatoka na kuelekea AMBIANCE CLUB. Nilikwenda na kukaa kwenye meza moja iliyokuwepo pembeni kabisa mwa ukumbi na kuagiza bia moja na kuanza kunywa taratibu huku nikitupa macho kila kona ya ukumbi.

Watu walikuwa ni wengi mno katika ukumbi huo. Wasanii nao hawakuwa nyuma kutumbuiza wateja. Nikiwa pale kwenye kona alifika kijana mmoja ambaye hakuwa mgeni kwangu. Kijana huyu alikuwa akiitwa Kanyeyemo. Nakumbuka nilikwisha lala naye siku moja kwenye hoteli moja ya Landmark. Kwakweli Kanyeyemo alikuwa mmbovu sana katika mambo yetu ingawaje alionekana kuwa na mwili wenye mvuto. Wenyewe wanakwambia “Bodi nzima lakini injini mbovu”.

Alifika na kuomba kampani yangu. Nikamkaribisha lakini kwa shingo upande kwasababu nilifahamu kuwa asingeweza kunitimizia haja yangu kutokana na injini yake kuwa mbovu. Baada ya kumywea vipombe vyake viwili vitatu nilimuaga kuwa nakwenda msalani. Nilipofika nikapotelea huko huko na kumuacha akinisubiria pale mezani.

Nilichukua Tax na kwenda zangu Club-Maisha. Nikaona pengine huko ningeweza kupata daktari wa kutibu maradhi yangu. Siku hiyo sikuhitaji pesa ya mtu, bali nilichokuwa nikikihitaji ni mtu wa kunirudishia hali yangu iliyo haribiwa na Siraji ambaye alinipima tu pasipo kunipa huduma yoyote na kunisababishia maradhia.

Nilipofika Club Maisha nikakuta hakujachangamka kama kulivyokuwa Ambiance. Hata hivyo sikujali kitu kwa sababu shida yangu mimi haikuwa Mziki bali ni mambo mengine. Nilisimama na kuanza kushangaa shangaa ili nijue pa kuanzia. Nikashitukia mtu akinishika bega. Nilipogeuka nikakutana na Gwasa. Mnh! moyo ukaanza kunidunda.

Gwasa akanishika kiuno na kuniomba tukakae kwenye meza aliyokuwa amekaa yeye. Nikaongozana naye kwa shingo upande huku nikiufikiria mziki wake. Gwasa alikuwa ni mwanaume mwenye injini kubwa kupita kawaida. Siku moja nilipokuwa naye uwanjani niliambulia mateso na kero tupu na sikufurahia hata chembe mechi nzima. Kwahiyo nilipokutana naye tena nikahisi kiama kilikuwa kikininyemelea kwa mara nyingine.


Kama nilivyo fanya kule Ambiance kwa Kanyeyemo ndivyo nilivyofanya kwa Gwasa. Nikajisemea kimoyomoyo ni afadhali kule kwa yule kijana wa Ambiance kuliko huku nilikokuja na kukutana na mashine ya balaa. Nikajiona kama vile niliruka mkojo na kukanyaga mavi.

Aka mwenzangu! Kunguru muoga hukimbiza ubawa wake. Nilichomoka na kuchukua pikipiki iliyonipeleka hadi Club Le-Mambo. Hali niliyokuwa nikijisikia siku hiyo nikatamani sana kama ningekuwa na shemeji Hashimu kwani yeye ndio angalau alinimudu. Lakini kwa bahati mbaya Hashimu alikuwa hapatikani kwenye simu yake pamoja na kwamba nilifanikiwa kuchukua namba zake kutoka kwenye simu ya Fatuma.

Akatokea kijana mmoja wa chuo kikuu cha mlimani na kuniomba tucheze wote. Kakijana kenyewe kalikuwa ni kadooogo hata kwenye kiganja hakajai. Nikahisi na kenyewe kangenitia shombo tu. Nilikasonya na kutaka kuondoka maeneo yale. Lakini jibu alilonipa ilibidi nisimame na kukasikiliza kwa makini.

“Dada usidharau wembamba wa reli treni inapita”

“Una uhakika na unachoongea” nilijikuta nikimuuliza swali la ajabu kutokana na hali niliyokuwa nayo. Safari hii nikasema yoyote atakayenikalia mbele ninaye.

“Habari ndiyo hiyo” alinijibu na kuendelea kucheza mziki pekeyake.

“Ukishindwa nikufanye nini?”

“Tusiandikie mate wakati wino upo”

“We dogo usilete utani unajua?” nikazungumza kwa msisitizo utafikri nilikuwa nafahamiana na kakijana kale.

“Mimi dogo kwa umbo tu. Kwa mambo ni kikongwe”

“Haya njoo” nilimuita yule kijana na kumkabidhi pesa mkononi.

“Za nini?” alihoji kijana yule kwa mshangao.

“Kachukue chumba, we si umesema mkali” nilimjibu kwa mkato na kumfanya kijana wa watu kubaki ameshangaa.

Kijana yule hakuamini kama mwenzake nilikuwa namaanisha kwa kile nilichokuwa nakizungumza. Kumbe na mwenyewe alikuwa na uchu masikini ya mungu. Bila ya kutegemea kijana wa watu alikwenda kuchukua chumba na kunifuata pale nilipokuwa nimekaa.

“Twenzetu baby mambo yapo mwake” alizungumza kijana yule huku akinikaribia.

“Inaonekana umepania dogo?” nikahoji baada ya kumuona kama vile amepagawa.

“Nimekwambia usiniite dogo banaa” kakijana kale kalikoroma heti.

“Basi haya Big”

“Hapo sawa” Alijibu kijana yule kwa kujidai.

Tulikumbatiana na kupeana mabusu pale pale katikati ya kundi la watu. Punde nikahisi nikiguswa bega. Nilipogeuka nikakutana uso kwa uso na shemeji Ashrafu yule mpenzi mpya wa Fatuma.

“Vipi?” nikajifanya kuhoji kwa mshangao

“Tafadhali Priscaria nipe japo dakika mbili tu tuongee” Ashrafu alizungumza kwa kubembeleza. Nilifahamu alichokuwa anakihitaji kutoka kwangu lakini alikuwa amechelewa. Endapo angewahi ndani ya dakika tano tu zilizopita angekipata alichokuwa anakihitaji kutoka kwangu.

“Wewe unanijua mimi?” nilihoji huku nimemkumbatia yule mwanafunzi wa chuo.

“Nakupenda sana Prisca tafadhali….” Ashraf alizungumza kwa kubembeleza huku ameweka mkono kifuani kuashiria kubembeleza.

“Koma wewe!” Nilizungumza huku nikimvuta yule mwanafunzi kuelekea Lodge. Tulimuacha Ashrafu akitukodolea macho tulivyokuwa tunatoweka kwa mapozi.Tukaelekea kwenye chumba chetu na punde tukaangukia kwenye mavituz. Mnh ama kweli usidharau wembamba wa reli....treni inapita. Kakijana kalionesha utundu wake na kunifanya mwanamke nifike peponi mara kadhaa.

****

Niliamka huku mwili wangu ukiwa mwepesiii kutokana na mzigo wote kutuliwa na kale kakijana ka chuo. Nikiwa bado kitandani simu yangu ya mkononi iliita. Alikuwa ni mume wangu Magesa.

“Enhe unataka nini?” nikahoji mara tu nilipo pokea simu ile.

“Unaniuliza nataka nini?” Magesa alihoji kwa hasira.

“Eeh mana sio kawaida yako, kila ukipiga simu ni balaa” Nilizungumza kwa kebehi.

“Hivi wewe mwanamke, umekosa nini kwangu?” Magesa lihoji kwa hasira.

“Hujui nimekosa nini? Unajifanya kuuliza sio hujui?” nikazungumza.

“Hivi huwo ufirauni wako unao ufanya huko mimi sijui?” Mume wangu aliuliza swali ambali lilinishitua kidogo.

“Ufirauni gani? Unaona unavyonitukana Magesa!” nikazungumza kwa kulalamika.

“Ni mara ngapi Asharaf amekukuta na wanaume?” Mume wangu alizungumza maneno ambayo yalinifanya nibaini mbaya wangu alikuwa ni nani.

“Wanaume! Yani mume wangu umefikia hatua ya kunitukana kiasi hicho?” nikazungumza kwa sauti ya kuigiza kulia.

“Wacha unafki wewe mwanamke, Yaani kuondoka mwezi mmoja tu umebadilika hivyo je ningekaa miezi sita ungekuwaje” Jamani nyie mume wangu alizungumza kwa kulalamika hadi huruma.

“Wewe usijifanye mjanja ukafikiri mambo yako siyajui” nikazungumza kwa kumgeuzia kibao.

“Unajua usitake kunitibua we mwanamke!”

“Nisikutibue nini, kwani ni nani ambaye hajui kuwa umeoa huko Arusha, halafu unajifanya heti kazini mimi sio mtoto mdogo ujue” Nikazungumza kwa hasira yale yaliyokuwemo moyoni mwangu.

“We mwanamke una wazimu” alizungumza mume wangu.

“Sawa mimi nina wazimu na ndiyomaana umeniacha ukaenda kuwajaza mimba wanawake wengine” nikazungumza kwa hasira.

“Nyamaza mshenzi wewe! Unanidhalilisha kila kukicha. Hivi kusafiri kikazi ndio imekuwa shida? Kwani mimi ndio wa kwanza kusafiri kikazi?” Magesa alizungumza kwa uchungu mkubwa.

“Kwanza aliyekwambia ndio alikuwa ananitaka, sasa wewe baada ya kuhoji kwanza unakurupuka na kuwaka kama moto wa kifuu!” nikaeleza huku nikijifanya kulia kwa kusingiziwa.

“Sasa olewako nikukamate unafanya huo utumbo wako utapata tabu sana” alizungumza Magesa.

“Hiyo siku haitafika, kwasababu unanionea tu” nikazungumza kwa hasira za kujilazimisha huku nafsi ikinisuta.

“Haya bwana lakini….”

“Lakini nini? Ole wako uje uniletee sijui katoto au kamwanamke ka nje ya ndoa haki ya baba vile nawaua wote!” nilizungumza kwa hasira.

“Sasa wewe jifanye bingwa wa kubadilisha mada tu”

“Unanionea sasa! Uchafu ufanye wewe huko halafu unipandilie mimi” nikazungumza kwa kulalama.

“Sasa mimi nimemuoa nani huku?”

“Unafikiri sijui unayoyafanya huko? Nimekunyamazia tu lakini nafahamu kila kitu” nikaeleza kwa msisitizo.

“Sawa lakini mimi nakaribia kurudi” alizungumza mume wangu kwa sauti ya chini.

“Wala usirudi wewe endelea kuponda raha na hao wanawake wako uliowajaza mimba” nikaeleza kwa jazba kisha nikakata simu.

Nilipatwa na hasira sana juu ya Ashrafu kwasababu alikuwa anataka kuniharibia starehe zangu. Kumbe siku ile alipotaka kuzungumza na mimi nikamkatalia yeye alimpigia simu mume wangu na kumueleza mambo ya umbea. Utafikiri mtoto wa kike kwa mambo ya uwongo uwongo.

Nikajisemea mwenyewe kuwa dawa ya moto ni moto. Ni lazima niufunge mdomo wa mwanaume huyo mwenye tabia za kike. Nilichukua simu yangu na kuvuta namba ya na kuipiga.

“Ehee unasemaje?” alipo pokea akajibu kwa ukali huku akijihami akihisi tayari mume wangu alikuwa ameshaniwashia moto.

“Jamani shemeji uko wapi” nikazungumza kwa sauti ya kudeka.

“Unataka nini?” Ashraf alihoji kwa mashaka.

“Jamani shemeji mimi nimekumisi mwenzako, unajua rafiki yako ameniacha mpweke sana” niazungumza kwa ile sauti yangu ya chumbani.

“Unasema umenimisi?” Nikamsikia akihoji kwa wasiwasi huku akiwa haamini masikio yake.

“Kweli jamani nimekumisi njoo basi japo nikuone tu” nikabembeleza mtoto wa kike.

“Sio nakuja hapo halafu unazingu! Unajua jana umeniuzi sana?” Ashrafu alilalamika.

“Jamani bwana we njoo, hayo yote tutayazungumza hukuhuku”

“Poa basi nipe dakika chache nitakuwa hapo”

“Sawa mpenzi wangu” nikazungumza kwa kubania sauti utafikiri nilikuwa nafundisha twisheni nzi.

Nilikata simu na kuachia msonyo mrefu kwa hasira na dharau. Hakuna siku ambayo nilikasirika kama ile. Sikutegemea kama mwanaume anaweza kuwa mbea kiasi kile. Sasa shida yake ilikuwa ni nini? Au alitaka niachike kwa mume wangu? Halafu iweje? Au alitaka niachike halafu anioe yeye? Pumbavu zake ngoja afike nitamkomesa.

Kwenye mida ya saa sita mchana Ashrafu alifika nyumbani kwangu na kugonga mlango. Wakati huo mimi nilikuwa chumbani kwangu. Kwakuwa sikuwa nimeufunga kwa komeo nikamwambia aingie tu. Alipofika sebleni alikaa kwenye kochi na kunisubiri kwa hamasa kubwa.

Nilitoka na kusalimiana naye huku nikiwa na nguo ya kulalia tu iliyoruhusu sehemu zangu za mwili kuonekana. Ashrafu alishituka kidogo na kumuona akimeza funda la mate. Nilitoa tabasamu na kumsemesha kwa ile sauti yangu ya kudeka.

“Vipi shemeji Ashrafu?”

“Salama tu shem. Habari za hapa?” alijibu huku akiniangalia kwa makini jinsi nilivyokuwa nimeubwa na kuumbika vizuri.

“Za hapa sio nzuri sana lakini kwa kuwa umekuja hakutaharibika kitu” nilimjibu kwa sauti ya mahaba huku nikimsogelea pale alipokuwa ameketi.




“Kuna nini?”

“Yaani bora umekuja, maana....mnh!” nilimjibu na kuondoka kuelekea chumbani kwa mwendo wa kunyumbua maungo. Niliamini huko nyuma kama alikua akiniangalia basi alikoma mwenyewe hasa kutokana na ile nguo ya kulalia niliyokuwa nimeivaa.

Nilipofika chumbani kwangu nikapiga kelele za kuomba msaada. Kwa hamaki Ashrafu alifika na kunikuta nikigalagala chini huku nimeshika tumbo. Aliinama na kutaka kujua kile kilichonikuta. Nikamshika mkono na kumuomba anikande kande kwenye tumbo pengine ningehisi ahuweni. Kwa kuwa alikuwa akinionea huruma alijikuta akifanya kama vile nilivyomuagiza. Kumbe lile ndilo lilikuwa kosa kubwa sana kwake. Nilihangaika na kufanya ile nguo kupanda juu na kuniacha mapaja yangu wazi.

Kwa jinsi nilivyokuwa nimeumbika, mwanaume yeyote rijali asingeweza kuhimili. Nilimshuhudia Ashrafu akivimba maeneo ya chini. Nami nilivyoona vile ndiyo nikazidisha manjonjorinjo. Nikamuomba anisaidie nipande kitandani. Aliponinyanyua nami nikamkumbatia ipasavyo. Kabla hatujafika kitandani, nikapeleka mdomo wangu taratiibu kwenye midomo yake.

Ashrafu alionekana kutulia na kusubiria kwa hamu lile nililokuwa nataka kulifanya. Midomo yake ilipogusana na ya kwangu kulitokea sumaku ya ajabu na kupeana ushirikiano kisha tukadondokea kitandani. Ndani ya nusu saa tukawa katika dunia nyingine tofauti kabisa na hii tunayoifahamu sisi.

Baada ya tukio lile nilikaa kitandani na shemeji Ashrafu akiwa bado amelala utafikiri alikuwa nyumbani kwake. Nilimtazama kwa jicho kali kisha nikasonya. Nikaelekea kwenye pembe ya chumba na kuchukua kitu ambacho Ashrafu hakukiona na kutoka nacho sebleni. Ilikuwa ni kamera ambayo niliitega kurekodi tukio zima. Nilitoa kopi na kuihifadhi kwenye kompyuta na nyingine kwenye flash. Nikarudi chumbani huku nimeshikilia flash mkononi. Nikachomeka kwenye deki ya runinga iliyokuwemo mle chumbani.

Nilimshuhudia Ashrafu akishika kichwa na kuinama chini. Hakuweza kuamini kama mwanamke miye nilikuwa mwanaharamu. Alivuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu kisha akanikazia macho usoni.

“Unamaanisha nini Shemeji?” Ashrafu alihoji kwa upole.

“Wewe si unajifanya mzungumzaji sana?...zungumza na hili” nilimwambia kwa kiburi.

“Hapana shemeji, usifanye hivyo”

“Lazima nije kumuonesha Magesa video hii” nilizungumza kwa msisitizo huku nimekaza macho.

“Ah….a…ah! utaharibu shemeji” Ashrafu alisema kwa upole na wasiwasi mkubwa.

“Ukitaka tuyamalize lazima ufanye nitakachokuagiza” nikazungumza kwa sauti kavu.

“We sema tu usijali shemeji” masikini Ashraf wawatu nikamuona akibabaika pale kitandani.

“Mpigie mume wangu na ufute kauli zako za kusema mimi nina msaliti” nilimwambia kwa sauti isiyo kuwa na hata chembe ya mzaha.

Pasipo kujibu kitu Ashraf alichukua simu yake na kubonyeza namba za Magesa. Masikini ya mungu kumbe alikuwa anaruka jivu na kukanyaga moto.

Alipiga mara ya kwanza simu haikupokelewa,mara ya pili, ya tatu na ya nne lakini haikupokelewa. Nikamwambia kuwa nilichokuwa nakihitaji mimi ni yeye kuongea na Mume wangu mbele ya macho yangu ili niweze kusikia umbea anaoutoa. Ndiyo, dawa ya moto ni moto, na dawa ya umbea ni kusutwa. Na ile mimi ndiyo niliyoiona kuwa ni dawa kwa wanaume wambea kama shemeji Ashrafu.

Nilipomkazania hakukata tamaa kupiga simu ingawa alikwisha piga pasipo kupokelewa. Safari hii Magesa alipokea na Ashrafu akaiweka sauti kubwa kama ambavyo nilimuagiza.

“Hallo Magesa” Ashrafu aliita

“Nikusaidie nini?” Magesa alijibu kwa mkato.

“Habari za kazi?”

“Unazitaka za nini?” Magesa alijibu kwa mkato utafikiri mchezo ule alikuwa akiushuhudia.

“Vipi kaka mbona leo hivyo”

“Nipo sawa. Unasemaje?”

“Vipi kazi unamaliza lini?”

“Siwezi kumaliza we nifanyie tu” Magesa alizungumza maneno ambayo yalizidi kumtia wasiwasi Asharaf.

“Mbona sikuelewi Magesa rafiki yangu?” Asharaf akazungumza kwa wasiwasi huku akiamini tayari video ile nilikuwa nimeituma kwa mume wangu kutokana na majibu aliyokuwa akiyapokea siku hiyo.

“Huwezi kunielewa, kama hujamaliza kumfanyia kazi mke wangu”

“Unazungumza nini Magesa?”

“Pole kwa kazi” alisema Magesa na kukata simu.

Kwakweli hata mimi mwenyewe sikumuelewa kabisa alichokuwa akimaanisha mume wangu Magesa. Kwa sababu Ashrafu ndiye aliyekuwa akimpatia taarifa zangu. Sasa ikawaje amgeuzie kibao wakati hata siku moja sikuwahi kumueleza mume wangu kuwa Ashrafu alinitongoza. Nikaona dawa ni kumpigia kwa simu yangu nione angeniambia kitu gani. Nilipopiga mara ya kwanza tu alipokea.

“Hello mume wangu” niliita kwa sauti ya mahaba.

“Niambie mke wangu” aliitikia kwa sauti ya upole tofauti na ile aliyokuwa akiongea na Asharafu. Nikajikuta nikipigwa na bumbuwazi nisiamini kile kilichokuwa kikiendelea.

“Nime kumisi mpenzi” nikazidi kudeka.

“Hata mimi mama. Ila Pole sana kwa kazi” alisema lakini neno la mwisho lilinishitua kidogo.

“Hapana mpenzi leo sikufanya kazi yoyote ngumu” nilimwambia.

“Vipi umeuonaje mziki wa Shemeji yako?” Magesa alihoji swali ambalo lilizidi kunichanganya na kuniweka katika wakati mgumu.

“Unamaanisha nini mume wangu”

“Poleni kwa kazi nzito mliyoifanya leo” Mume wangu Magesa alisema na kukata simu.

Nilimgeukia Ashrafu na kumtazama kwa jicho kali.

“Hivi wewe humo akilini mwako upo sawa kweli?”

“Nimefanya nini shemeji?” alihoji kwa mshangao Asharafu.

“Hivi unawezaje kuzungumza umbea hata ambao unakuhusu wewe mwenyewe?” nikahoji kwa mshangao.

“Mbona mimi sielewi shemeji!” Ashrafu aliendelea kujifanya haelewi kilichokuwa kinaendelea.

“Yaani wewe mwenyewe unaiba mke wa mtu halafu unajishitaki bila hata woga” niliendelea kuzungumza kwa hasira.

“Lakini unanionea bure tu Priscaria, mimi sielewi kitu” aliendelea kujitetea mwanaume yule.

Nikaamini kweli kuna watu wamekubuhu kwenye umbea. Yaani hadi yeye mwenyewe anajishitaki! Nilitoka sebleni na kurudi na mchi wa kupondea kisamvu na kuuinua juu tayari kwa kumpondelea mbali mwanaume yule cha umbea.

Mwanaume wa watu aliponiona nimebebelea mchi huku nikimfuata tayari kwa kumtoa roho, alijiinua haraka na kuchomoka mbio pasipo kujali kama alikuwa amevaa bukta tu mwilini mwake. Chezea kifo wewe!

Masikini ya mungu kijana wa watu nilikuwa namhukumu kwa kosa asilolifanya.

Kumbe wakati tulipokuwa tukiendelea kula tunda, simu yangu ya mkononi iliita. Sikuwa na taimu na kitu kingine chochote zaidi ya majambozi. Ile simu iliita kwa muda mrefu pasipo kuisikia wala kupokea. Kwa bahati mbaya tukiwa katika mishe mishe zetu tukabonyeza kwenye kitufe cha kupokelea pasipo kujitambua. Lahaula! Kumbe aliyekuwa akinipigia alikuwa ni mume wangu Mr. Magesa. Akasikia kila kitu kilichokuwa kikiendelea mle chumbani. Mbaya zaidi nilikuwa nikilitaja sana jina la Ashrafu. Hivyo mume wangu akamfahamu kabisa mtu aliyekuwa akimuibia asali yake.

Ashrafu alipoondoka nikawa nimebaki chumbani huku nikiwa na lindi la mawazo. Nilipotazama saa ya ukutani ikaonesha kuwa ilikuwa ni saa saba kasorobo mchana. Nikahisi mwili wangu kuwa mzito kupita kawaida. Nikatamani kupata wasaa wa kutosha niweze kujifariji na kutuliza mawazo. Nikapata wazo la kwenda kupata chakula cha mchana katika hoteli moja iliyokuwa ikfahamika kama KISURA BY NIGHT HOTELL. Hoteli hii ilikuwa ni tulivu mno watu waliokuwa wakienda hapo walikuwa ni wastaarabu tu. Hivyo kwa siku hiyo nikaona mahali hapo pangenifaa hata mimi.

Kama nilivyokuwa nimepanga nilifika kwenye Hoteli hiyo na kuketi sehemu iliyokuwa tulivu na yenye upepo mzuri. Niliagiza ndizi za kuchoma na kitimoto nusu kilo. Nilikula taratiibu huku nikitazama mziki kwenye runinga kubwa iliyokuwa pale hotelini. Wakati nikiendelea kujipatia lunch yangu, alifika jamaa mmoja aliyeonekana kama pedeshee Fulani na kuomba kuungana nami. Bila ya hiyana yoyote nilimkaribisha pedeshee yule aliyekuwa na asili ya kiarabu.

Pedeshee alipopewa lifti akaamua kupiga na honi. Alinyoosha mkono na kunyofoa mnofu kwenye sahani yangu ya kitimoto. Nikamwangalia kwa jicho la kiwiziwizi kisha nikaachia tabasamu la uchokozi. Pedeshee wa watu alipoliona tabasamu lile akaisha kabisa na kujikuta akinitongoza na kuniambia heti alikuwa anataka kunioa. Mnh! Hata kama ningekuwa sijaolewa mwenzangu mzee kama yule ningempeleka wapi? Hata hivyo ningefanyaje sasa wakati nilikwisha umbwa na kuwa Priscaria, ilibidi tu nimkubalie kwa sababu neno Hapana kwangu lilikuwa ni msamiati mgumu mno.

Mwarabu wa watu alijikuta akiingia gharama za kunilisha mchana ule wa Juma tano. Nami sikufanya hiyana mtoto wa kike nilikula hasa tena vitu vya gharama ya juu. Sasa ningefanyaje wakati mtu amejipendekeza mwenyewe! Ponda raha kufa kwaja. Mzee wa watu alikunywa pombe kiasi cha kuzidiwa na kushindwa hata kujitambua mchana ule. Nilipoona vile taratiibu nilichukua pochi yake na kutoweka nayo. Sijui huko nyuma kilicho jili kwasababu hata malipo alikuwa hajafanya.

Sikuelekea nyumbani kwangu bali nilikwenda moja kwa moja kwa Fatuma. Kwa bahati nilimkuta chumbani kwake akimalizia kupiga pasi viwalo vya kutokea jioni ya Juma tano hiyo. Nikakaa kitandani na kuanza kuzungumza naye hili na lile, likiwemo na lile balaa la mume wangu.

“Mwenzangu Magesa si akanipigia simu…..”

“Enhee nipe mchapo shoga” alisema Fatuma na kuacha kupiga pasi akawa ananisikiliza.

“Akasema oooh! Sijui unanisaliti, sijui nini…..?”

“Kajuaje yote hayo?”

“Sijui anasema rafikiyake gani huko kamwambia!”

“Mnh! watu wengine nao watasutwa sasa……”

“Mwenzangu!”

“Enhee! ikawaje?”

“Si nikamtega huyo rafikiyake. Naye akategeka”

“Usinambie?”

“Chezea mimi wewe!”

“Ikawaje?”

“Tukala mambo”

“Umemkomesha. Sasa na hilo akaseme basi” alisema Fatuma na kuendelea kunyoosha nguo zake.

“Aseme marangapi?”

“Nini?”

“Magesa anajua kila kitu”

“Hee! Nani kamwambia sasa?”

“Yeye mwenyewe huyo rafiki yake”

“Hee! Basi makubwa!”

“Mwenzangu umbea unaviwango”

“Kama ni viwango, basi huyo ana digirii. Sasa ikawaje?”

“Ndiyo hivyo. Magesa amekasirika, akirudi sijui itakuwaje?”




“Achana naye twendezetu tukajirushe. Kwani mwanaume yuko peke yake bwana” aliniambia Fatuma huku akiendelea kunyoosha nguo zake. Akaniambia kuwa kulikuwa na bendi moja matata sana iliyokuwa ikitumbuiza CLUB BILLCANAS. Kwahiyo huko ndiko kulikofaa kumalizia siku hiyo ya jumatano.

Nilikuwa nikimuamini sana Fatuma kwa kila jambo. Ikafikia hatua nikikorofishana na mume wangu mfariji wangu alikuwa ni yeye ingawa kuna wakati ushauri aliokuwa akinipa haukuwa unafaa. Hivyo kuwa hapo na Fatuma nikajikuta nikisahau kabisa kama nilikuwa na bifu na mume wangu. Tulitoka na kuelekea Club kuponda raha. Tulikuta watu ni wengi mno na kumechangamka vilivyo. Hatukupoteza muda nasi tukajichanganya kwenye kundi la watu na kuanza kuyakata mauno.

Alifika kaka mmoja na kuanza kucheza na mimi pasipo kunishirikisha. Nami sikuona sababu ya kukataa kucheza naye kwa sababu kilichotupeleka pale kilikuwa ni hicho. Nilicheza na yule kaka na mara akaanza kunishika sehemu adimu. Mungu wangu! nilijikuta mizuka yangu ikinipanda kichwani. Nami nikaanza kutumia mikono yangu kumchokoza zile sehemu nilizokuwa nikizifahamu kuwa mwanaume yeyote akiguswa lazima chuma kiende angani. Yule kijana alianza kutoa miguno na sauti za ajabu. Hapo nikahisi kuwa ni lazima nilikuwa nimekwisha mkamata.

Hatukuweza kufahamu lakini huo ndio ulikuwa ukweli, mimi na yule kijana tukajikuta kwenye chumba cha wageni tukioneshana mautundu. Kwa kweli kijana huyu alikuwa amebarikiwa mno. Aliweza kuliendesha gari kwa ustadi wa hali ya juu. Kwenye mabonde alijua kupunguza mwendo na kwenye tambarale alijua kuyakanyaga mafuta. Wakati yeye akijitahidi kukanyaga mafuta kuupandisha mlima wa kwanza, mimi nilikuwa nimekwisha ipita milima kama mitano na kukaribia kutumbukia mabondeni.

Wakati tukiendelea kuendeshana na yule kijana, mlango uligongwa. Kati yetu hakuna aliyejali kwasababu kila mmoja alikuwa akikimbilia kukamata kile kilichokusudiwa. Mlango uligongwa mara kadhaa, na safari hii ulikuwa ukigongwa kwa nguvu. Tulisitisha lile zoezi na kusikiliza kugongwa kwa mlango. Tulipouliza mhudumu akajibu kuwa alikuwa na shida hivyo kwa tahadhari kubwa yule kaka akafungua mlango.

Waliingia watu wanne mmoja alikuwa mhudumu, askari wawili na yule Pedeshee wa kiarabu niliye muibia mchana. Nilipowaona nikabaini kuwa walikuwa wamenifuata mimi kutokana na kuwepo kwa yule Mwarabu. Waliniweka chini ya ulinzi na kuondoka na mimi hadi kituo cha polisi.

Tulipofikishwa nikasomewa shitaka la kuiba pesa kwa yule Mwarabu. Hivyo nikaambiwa usiku huwo kusingetolewa dhamana hivyo ninge lala pale hadi kesho yake, yaani Alhamisi.

Kwakweli pamoja na matukio yote nniliyokuwa nikiyafanya lakini nilikuwa nikiogopa sana kuswekwa rumande. Nikakuna kichwa na kuchezesha akili yangu kwa kasi ili niweze kupata namna ya kutoka usiku huo. Yule mwarabu aliitwa nje na askari wa kike, bila shaka alikuwa anatakiwa kutoa chochote kwa kazi iliyofanyika. Hivyo akaniacha mimi na mkuu wa kituo pale ndani. Na mimi sikuichezea nafasi hiyo.

Nikatambaa kwa magoti hadi pale alipokuwa amekaa yule mkuu wa kituo.

“Nini wewe! unataka kufanya nini?” askari yule akahoji baaya ya kuniona nikitambaa kuelekea pale alipokuwa amekaa.

Sikutoa jibu lolote bali nilitulia huku nimepiga magoti na taratiibu nikaanza kupandisha gaunilangu lililokuwa fupi na kuwacha mapaja yangu wazi.

Weupe na umbile la sehemu zile ulimfanya askari yule kupigwa na butwaa.

“We mwanamke hivi una nini?” askari yule aliendelea kuhoji kwa mshangao.

Niliuma midomo yangu na kurebua maho utafikiri nilikuwa naelekea kukata roho. Nikapeleka mkono wangu kichwani na kuchezea nywele zangu huku nikiuma uma midomo yangu kimahaba.

“Sasa mwanamke mzuri kama wewe unahangaika nini na vizee hivi?” askari yule alihoji kwa sauti ya upole.

“Ananisingizia tu Afande, we ukimuangali ana hadhi gani ya kuwa na mimi yule mzee?” nikaeleza.

“Nyie wanawake wa mjini bwana ni shida, mkiona mtu ana visenti basi mnajisahau na kumpapaikiia. Unaona sasa ulipofika leo” alizungumza askari yule kwa sauti yake ya upendo.

Niliinuka na kupeleka lipsi zangu hadi kwenye midomo ya askari yule na kumbusu. Baada ya zoezi hilo nilirudi sehemu niliyopaswa kuwa. Aliingia yule askari wa kike na kuzungumza na mkuu wake wa kazi.

“Afande mkono ni mtupu” alisema yule askari wa kike.

“Hata harufu hauna?” alihoji mkuu wa kituo.

“Haurambiki Afande”

“Ahaa! Ni jabari sio?”

“Ndio Afande”

“Unaweza kwenda kupumzika”

“Sawa Afande” alijibu yule Askari wa kike na kuondoka akituacha tena mimi na mkuu wa kituo.

Pedeshee wa kiarabu aliingia kituoni huku akifoka. Kumbe alivyoitwa nje alikuwa akitakiwa kutoa hongo lakini akaonekana ni mgumu kutimiza maagizo. Alimfokea mkuu wa kituo utadhani alikuwa akimfokea mtoto wake. Mbaya zaidi alianza kutoa na matusi pasipo kujitambua kutokana na hasira kuzidi uwezo wake. Bila ya kutegemea kumbe nje kulikuwa na askari wengine wengi waliokuwa zamu. Mwarabu alishitukia akiwekwa chini ya ulinzi na kuamriwa kuvua mkanda na viatu kisha akaswekwa rumande.

Mkuu wa kituo akapumua kwa nguvu kisha akaniangalia usoni pasipo kufahamu kuwa lile ndilo lililokuwa kosa kwake. Nikayachezesha macho yangu kwa ufundi mkubwa na kushitukia afande akinisogelea taratibu na kuanza kuni papasa kwenye nywele zangu za kichogoni. Nikaudaka mkono wake na kumuangalia usoni kisha nikamtupia swali.

“Askari wako wakitokea je?”

“Hakuna anayekuja hapa” alijibu huku akionekana kuzama kwenye dimbwi la mahaba.

Nikamwambia nilikuwa tayari kwa chochote lakini kwanza angeniahidi kunisaidia juu ya lile swala langu. Hakunijibu kitu, alichukua jarada langu na kulitumbukiza kwenye sinkI la maji na kulichanachana baada ya kulirowanisha kisha akachukua yale mabaki ya faili na kwenda kuyatumbukiza chooni.

“Tufanye haraka basi binti” aliniambia yule afande punde aliporejea kutoka msalani.

“Punguza papara basi” nilimtuliza

“Mwenzio nimezidiwa sana” alisema Afande.

“Basi kafunge mlango kwanza”

“Wacha woga mrembo haji mtu”

“No! No! No!....kafunge mlango” nikazidi kusisitiza.

Masikini afande wa watu alijiinua na kitambi chake na kwenda mlangoni kwa ajili ya kufuunga, lakini Kabla hajafika mlangoni aliingia yule afande wa kike. Akamwambia kuwa kulikuwa na tukio la ujambazi lililokuwa likiendelea hivyo walikuwa wakihitajika vijana wa kutosha kwenda kuzuia uhalifu huo.

Habari zile zilimkera sana yule mkuu wa kituo na kujikuta akisonya na kurudi hadi pale nilipokuwa nimekaa. Akaniangalia kwa usongo mkubwa kisha akaniambia kuwa angenitafuta siku yoyote ile nimpatie haki yake. Nikakubaliana naye kisha akaniruhusu kuondoka usiku ule. Nikawaacha wao wakishughulikia tukio la ujambazi.

Kwa kutumia usafiri wa pikipiki niliingia nyumbani kwangu kwenye mida ya saa tisa za usiku. Nilifika na kujitupa kitandani. Kutokana na uchovu nikajikuta nimechukuliwa na usinginzi mida ileile punde tu nilipojilaza.

****

Siku ya Alhamisi niliamka saa tano na nusu asubuhi. Mwili ulikuwa umechoka kupita kawaida kutokana na mishe mishe za usiku wa Juma tano. Nilikwenda bafuni kujimwagia maji ya baridi niliyo yasikia yakitambaa kwenye mishipa yangu ya damu kuanzia unyayoni hadi kwenye ubongo. Kwa kiasi Fulani nilianza kujihisi kuwa mwepesi.

Baada ya kukoga nilikwenda kujipatia supu ya kuku kisha nikarudi chumbani kwangu na kuendelea kuuchapa usingizi.

Mida ya mchana nikiwa usingizini simu yangu ilinigutusha. Nilipoangalia kwenye kioo nikaona jina la Bambonenga. Huyu kijana niliwahi kutembea naye mara moja tu lakini akawa king’ang’anizi katika mapenzi ingawa nilikwisha mfahamisha kuwa mimi nilikuwa ni mke wamtu, lakini hakukoma. Nikaona dawa ni kukata simu na kuizima kabisa. Kisha nikaendelea kuuchapa usingizi wangu.

Nikiwa usingizini niliota kuwa nilikuwa najivinjari na Undrea yule muuza chipsi. Niliweweseka sana huku nikitaja jina la kijana huyo. Siku hiyo kijana yule alionesha mautaalamu tofauti kabisa na siku ambayo nilimbananisha na kushindwa kunipa majambozi. Undrea huyu wa kwenye ndoto hakuwa Undrea yule uliyemshuhudia akiadhirika mbele yangu. Undrea huyu alikuwa ni kiboko! Undrea huyu alikuwa ni tishio! Undrea huyu alikuwa ni kanyaga twende! Undrea huyu alijua kuuwasha moto na vumbi likatimka! Hapana chezea Undrea wewe.

Ndoto yangu ile kakatishwa na mtu aliyekuwa akigonga mlango. Niliposhituka nikaachia msonyo kwa hasira na kusimama kuelekea mlangoni huku sura nimeikunja kwa hasira za kukatishiwa njozi yangu. Watu wengine sijui wapoje! Mwenyewe nilikuwa nikipata mavitu adimu kutoka kwa Undrea mpya halafu mtu anakuja kugonga gonga milangu. Nilichukia sana kusema kweli!

Nilipofungua mlango sikuweza kuamini macho yangu. Mlangoni pale alikuwa amesimama Undrea muuza chipsi, mwanaume niliyekuwa namuota muda huo huo. Sasa swali likaja huyo aliyesimama mlangoni hapo alikuwa ni Undrea yupi? Ni yule mchovu aliyewahi kushindwa kula uhondo au ni yule Undrea wa ndotoni aliyekuwa akigawa dozi huku ameuma meno? Sikuwa na jibu kamili lakini nikabaki nimemkodolea macho kijana yule.



“Habari za saa hizi shemela” alizalimia kijana yule.

“Enhe unasemaje?” nikahoji huku nikiwa nimevaa sura ya mbuzi.

“Vipi Broo amesharudi?” kijana yule alihoji huku akitabasamu kama kawaida yake.

“Ulikuwa unasemaje?” nikaendelea kuhioji kwa sauti kavu.

“Aah nimeona simu yango ndo mana nikaja” Undrea alizungumza huku akiendelea kucheka cheka.

Kale katabia kake ka kucheka cheka kalinifanya nigundue kuwa yule alikuwa ni Undrea yule yule mchovu. Yule wa kwenye ndoto alikuwa ni Undrea wa kazi tu, hakuwa anacheka cheka kama huyu aliyesimama mlangoni.

“Nani amekupigia sasa?” nikahoji kwa hasira baada ya kubaini alikuwa anazungumza uwongo.

“Nimeona missed call yako shem ndomana nimekuja, sipendi kabisa uteseke” Kijana yule alizungumza.

“We utakuwa mgonjwa wa akili, jiangalie sana” nikazungumza huku nikikamata mlango tayari kwa kuufunga ili nirudi ndani kutafuta usingizi pengine Undrea wa usingizini angerejea tena.

“Ngoja kwanza shem usifunge!” Undrea alipaza sauti kuzuia nisifunge mlango.

“Unasemaje?” nikahoji kwa mkazo huku nimekunja sura.

“Vipi leo kale kamchezo ketu?” alihoji kijana yule huku akicheka cheka kama mwehu bila kujua kama alikuwa ananikera.

“Kamchezo gani?”

“Aaah shemeji umesahau, kale ka utamu utamu!”

“We unajua mchezo wewe au unaropoka tu!” nikahoji kwa jazba.

“Shem bwana wacha dharau basi”

“Sasa wewe unajua mchezo gani au wa kupika pika vikopo?” nilizungumza kwa kebehi huku nikijilazimisha kutabasamu kwa dharau.

“Kaburi usilolizikwa, huwezi kujua mateso yake” Undrea alizungumza kwa kujiamini.

“Hivi wewe unafikiri sikujui mimi? Kuguswa kidogo tu hoi hata kuonja umeshindwa” nilizungumza huku nikibenjua midomo yangu kwa dharau.

“We si unipe kidogo tu ushuhudie mziki wake!”

“Sasa nishuhudie mara ngapi?”

“Ya kale hayanuki shemu, tugange ya mbele”

“Kwenda zako, huna lolote mchovu tu!” nilizungumza na kutaka kufunga tena mlango wangu.

“Ngoja shemeji, usifunge bwana!” kijana yule alinizuia na kuzungumza pasipo kutoa lile tabasamu lake la kipuuzi.

“Untaka nini?” nikahoji kwa hasira zaidi baada ya kumuona akizidi kunizoea.

“Tafadhali shemeji naomba unipe japo nafasi moja tu nidhihirishe maneno yangu” safari hiyo Undrea alikuwa akizungumza bila kucheka.

“Kama siku ile ulishindwa leo uweze una nini?” nikahoji kwa umakini baada ya kumuona ameacha kucheka cheka.

“Mimi sio Undrea yule uliyekutana naye wewe” alizungumza kijana yule kwa sura ya mbuzi.

Kwa kiasi Fulani nikaanza kumfananisha na yule Undrea wa kwenye ndoto ambaye hakuwa anacheka cheka.

“Kumbe wewe ni nani, na una utofauti gani?”

“Mimi ni Undrea wa kazi, sio Undrea wa kuuza chipsi” kijana yule aliendelea kujieleza pasipo kutoa tabasamu lake.

“Unanifurahisha sana kijana. Unafikiri ni gemu, Leo unaweza kushindwa na kesho ukashinda?” nilizungumza kwa kebehi huku nikitabasamu kwa dharau.

“Na nitakufurahisha sana kama ukinipa nafasi” alizungumza kijana yule.

“Una uhakika?”

“Asilimia mia”

“Sasa ole wako ukimbie, utanijua mimi ni nani?”

“Kuwa na amani” alizungumza huku akiachia tena lile tabsamu lake la kizembe.

“Wewe!” nikaita kwa mshituko.

“Vipi tena?”

“Mbona unatabasamu?” nikajikuta nikihoji swali ambalo halikuwa na jibu sahihi.

“Jamani lazima nifurahi kwasababu nimepata kile ninachokitamani” kijana yule alizungumza huku akijichekesha.

“Sasa wewe cheka cheka hapo halafu uzingue. Pit huko!” nilizungumza na kumruhusu kijna yule aingie ndani kwangu.

Nilipokuwa nikivuta hatua kuelekea chumbani kale ka Undrea kalinifuata nyuma na kunidandia mgongoni kisha kakaketi kwenye madafu yangu ya nyuma huku mikono yake ameipitisha chini ya makwapa yangu na kuikutanisha kwenye madafu ya mbele.

“Aaai wewe!” nilipiga kelele kwa mshituko kwasababu lilikuwa ni tukio ambalo sikulitegemea.

“Naomba lifti” Undrea alizungumza huku amekalia kigoda kule nyuma na kihwa chake amekiegemeza mgongoni kwangu na ile mikono yake iliyokutana kwenye madafu yangu ya mbele ilikuwa ikicheza kwa ufundi na kuleta hali ya mshawasha kwenye mishipa yangu ya damu.

“Kweli leo umekuja kitofuti” nilizungumza huku nikisukuma mlango na kuingia chumbani ilhali Undrea akiwa amedandia mgongoni kwangu kma ngedere mtini.

“Lazima leo na mimi nikuoneshe mambo yangu hadi ukimbie” alizungumza Undrea kama vile sio yeye aliyeishia njiani siku niliyompa nafasi.

Tulipofika chumbani niligeuka na kumtupa kitandani kisha nikasogea nyuma na kumtazama kwa makini. Nilikuwa nahofia sana kumkabidhi mamlaka halafu ashindwe kuyatumia na kunisababishia mambo mengine ya kutoka usiku wakati mwenyewe sikuwa na mpango wa kutoka siku hiyo.

Kijana yule alivua shati na kulitupa pembeni huku akinikazia machona kunitolea lile tabasamu lake.

“Sogea basi karibu baby” Undrea alizungumza huku akifungua kifungo cha suruali yake.

“We saula tu mimi nakusubiri” nilizungumza kwa wasiwasi huku nikimtazama kwa makini.

“Unanisubiri kwenda wapi, njoo basi nikupe haki yako” alizungumza Undrea huku akiteremka kutoka kitandani kunisogelea pale nilipokuwa nimesimama.

Niliachia tabasamu huku nikimtazama kwa mashaka alivyokuwa akinisogelea. Alipofika alinikamata kiuno na kunipiga busu moja takatifu. Nikahisi mwili wangu ukisisimka kwasababu busu lile lilikuwa limefanana kabisa na busu la Undrea wa ndotoni.

“Ooooh!” nilijikuta nikitoa sauti ya hisia huku nikibenjua kichwa changu kuangalia juu.

Kijana Undrea alipoona ameniita kidogo tu nami nikaitika, akatumia mwanya huo kunibana kwenye madafu yangu ya kifuani huku akinikokota kuelekea kitandani. Sikuonesha ubishi wowote kwasababu nilikuwa nimeona dalili zote za uwepo wa utofauti kati ya Undrea muuza chips na Undrea aliyenitembelea siku hiyo.

Kabla sijatua kitandani, viganja vya mikono ya Undrea vilikuwa vimeshatarai kila idara na sekta nyeti katika mwili wangu. Kudadadeki! Nafikiri kijana yule alinijia na dawa siku hiyo, kwasababu ndani ya sekunde zile chache mtoto wa kike tayari nilikuwa nimetota chapaa kwa jasho.

“Oohnm! Kumbe ndivyo ulivyo hivi?” nilihoji huku nikihisi mwili wangu ukinitetemeka kwa hamasa za mchezo ule.

“Kuwa mpole hapo bado sijaanza” Kijana yule alizungumza kwa majivuno huku viungo vyake vya miguu na mikono vikishirikiana na kichwa chake viliendelea kutengeneza mwili wangu.

“Undrea kumbe wewe ndio yule wa ndotoni?” nilihoji huku na mimi nikijitahidi kuonesha ushirikiano isije ikawa zamu yangu kuumbuka, maana sio kwa utundu ule aliokuwa akiuonesha kijana yule. Tena alifanya yote hayo huku akicheka cheka kama kawaida yake.

Nikajikaza mke wa Magesa na kujaribu kucheza na ngome kuu iliyohifanyi bunduki na mabomu ya kila aina. Kabla mkono wangu kufika katika mazingira yale ya ugenini, nilisikia sauti ya mlango ukigongwa.

“Mungu wangu!” nilizungumza kwa wasiwasi baada ya kusikia mlango ule ukigongwa. Lkini niliposikiliza kwa makini ugongaji ule niliweza kubaini mgongaji alikuwa ni Fatuma. Ndio kwasababu siku zote Fatuma ndiye aliyekuwa akigonga mlango polepole huku akisikilizia jibu kabla ya kugonga tena.

“Huyo ni Magesa shemu?” Undrea alihoji baada ya kusikia sauti ile ya mlango.

“Hebu tulia kwanza sio Magesa” nikazungumza huku nikiteremka kutoka kitandani.

Kwa mwendo wa kujiamini nilitembea kuelekea sebleni huku nikiamini mtu aliyekuwa akigonga mlango hakuwa mwingine bali ni shoga yangu Fatuma.

“Nakujaaa!” nilipaza sauti kuitika baada ya kusikia mlango ule ukigongwa kwa mara nyingine.

Ndugu msomaji huwezi kuamini kitu nilichokiona baada ya kufungua mlango ule. Kumbe Mgongaji hakuwa Fatuma kama nilivyOkuwa nahisi mimi. Macho yakanitoka na hofu ikanijaa mtoto wa kike.



Mgeni yule aliyekuwa akinigongea mlango alikuwa ni mchungaji Mwaipopo. Kwa kweli haikuwa kawaida ya mtu kama huyu kufika nyumbani kwangu. Siku zote nilikuwa nimezoea kumuona kanisani tu tena Jumapili hadi Jumapili. Sasa sijui alikuwa amefuata nini yule mtu wa Mungu pale nyumbani kwangu.

“Bwana asifiwe baba Mchungaji” nikasalimia kwa heshima zote.

“Emen”

“Karibu ndani baba Mchungaji” Nilimkaribisha mchungaji huku nikijiona wazi mapigo ya moyo wangu yalikuwa yakienda kasi. Hata sielewi ilikuwaje lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa.

Mchungaji akaingia ndani na kuketi kwenye kochi huku mkononi mwake akiwa ameshikilia biblia. Alizunguusha macho yake ndani mle kama vile kulikuwa na kitu anakitafuta.

“Karibu baba Mchungaji”

“Emen”

Baada ya kumkaribisha mtu wa Mungu yule ndani kwangu, nikakimbia haraka chumbani na kuchukua kanga na kujifunga kiunoni na nyingine nikajitanda kichwani. Ndio ilibidi nifanye hivyo kwasababu nilikuwa nimevaa gauni la kulalia tu.

“Karibu baba mchungaji unatumia kinywaji gani?” nilihiji kwa unyenyekevu utafikiri nilikuwa mtakatifu kuliko malaika wote.

“Hapana usijali mtoto wa Mungo” alizungumza baba mchungaji kwa upole huku akiachia tabasamu la upendo.

“Hata maji tu baba mchungaji?” nikahoji kwa sauti ya upendo.

“Haya naomba maji basi ya kunywa” aliagiza maji ili kuniridhisha.

Maada ya kumletea mchungaji maji ya kunywa nilikwenda kuketi kwenye kochi la pembeni kidogo huku nikimsikiliza kwa makini.

“Mtumishi nimekuja kwaajili ya kufanya maombi” Mchungaji alizungumza kwa sauti ya upole.

“Maombi ya nini baba Mchungaji?” nikahoji kwa mashaka baada ya kusikia mtu yule wa Mungu ameamua kuja nyumbani kwangu kufanya maombi.

“Nimezungumza na mume wako bwana Magesa, tumekubaliana nije nifanye maombi” alieleza mchungaji.

“Yaani ufanye maombi hapa nyumbani?” nikahiji kwa mshangao.

“Ndio, inaonekana kuna roho chafu zinazunguuka nyumba yenu” mchungaji alieleza.

“Eeh haya karibu baba mchungaji unaweza kuendelea” nikazungumza na kumruhusu mtu wa Mungu kuendelea na ibada.

“Lakini pia…” alizungumza mchungaji na kukohoa kidogo.

“Ndio baba Mchungaji”

“Hata wewe nitaomba nikuombee”

“Mimi baba Mchungaji”

“Ndio, kwa maana inaonekana hata mwili wako umetawaliwa na roho nyingi chafu chafu” Mchungaji alizungumza na kujishitua kidogo. Sikuelewa hizo roho chafu zilikuwa zimenizunguukaje kwasababu mwenyewe nilikuwa najiona nipo sawa tu.

Mchungaji alisema kuwa alitakiwa kuingia kwenye kila chumba cha nyumba yangu ili kukemea na kuvunja nguvu zote za mapepo. Nilimruhusu hasa pale aliposema kuwa alikuwa ameagizwa na Mume wangu kufanya maombi hayo. Sasa ningefanyaje wakati baba mwenye nyumba alikuwa ameamua kufanya hivyo!

Maombi yalianzia sebleni, yakaenda jikoni, yakaanza kuingia vyumbani. Lakini alipotaka kuingia chumbani kwangu, nikamzuia.

“Hapana baba Mchungaji naomba usiingie chumbani kwangu” nilizungumza kwa msisitizo kwasababu chumbani humo alikuwemo Undrea.

“Tafadhali mtumishi naomba niifanye maombi ndani ya chumba hiki” mchungali alizungumza kwa msisitizo.

“Hapana mchungaji, huwezi kuingia chumbani kwangu” nami nikazungumza kwa msisitizo.

“Lazima niingie humu mtumishi, hiki chumba ndio ngome ya mapepo wachafu” Mchungaji alizidi kunga’nga’nia kuingia chumbani mwangu.

“Lakini hiki ni chumba changu mimi na mume wangu!” nikazungumza kwa kulalamika.

“Endapo nisipoingia chumbani humu, ni sawa na bure kwasababu ngome kuu ipo uku chumbani.

Baada ya kuona mchungaji amekazana na msimamo wake, ikabidi nikubaliane na matakwa yake japo kwa shingo upande.

“Sawa nimekuelewa baba Mchungaji, subiri niweke sawa mazingira” nikazungumza.

“Sawa wewe endelea mi nakusubiri” alijibu baba Mchungaji huku akipiga piga Biblia yake kwa viganja vya mkono.

Niliingia chumbani na kumwambia Undrea ajifiche kwa muda kidogo ili mchungaji amalize shughuli yake aliyosema kuwa alikuwa ameagizwa na mume wangu Magesa. Bila ya kipingamizi Undrea aliingia kwenye kabati nikamfungia kisha nikatoka kwa mchungaji.

“Asante baba Mungu kwa kutenda” alizungumza mchungaji uku akivuta hatua na kuingia chumbani mwangu.

Mchungaji aliendelea kufanya maombi yake humo chumbani huku mimi nikiwa katika vazi la kanga moja niliyojifunga baada ya kusikia hodi. Ibada ya chumbani ilikuwa ni ndefu kuliko ibada iliyofanyika kwenye maeneo mengine kiasi cha kuanza kunikera. Nikawaza jinsi ya kuyakatisha yale maombi ili atuondolee kiwingu Pale nyumbani kwangu.

Nikajifanya mapepo yamenipanda na kuanza kugalagala chini huku nikipiga mayowe. Nikagalagala pale chini huku nikifungua kanga niliyokuwa nimejifunga kiunoni na kufanikiwa kubaki naile night dress.

Nikaendelea kupiga mayowe na kugalagala pale chini huku nikijitahidi kujifunua lile gauni la kulalia nililokuwa nimelivaa.

Mchungaji aliinama na kutaka kunikamata ili nitulie, lakini nilimkwepa na kujibiringisha pembeni. Aliendelea kunikemea huku akinifuata na kufanikiwa kunikamata, lakini mkono wake ulikuwa umetua kwenye madafu yangu ya kifuani. Mara akashuka chini na kunikamata kiuno kunizuia nisifurukute.

Macho ya Mchungaji yalianza kumsaliti na kujikuta akiyakodoa sehemu za mapaja yangu yaliyokuwa wazi kuanza kuyapapasa taratibu huku akiendelea kuniombea. Hakuishia hapo baba yule, mikono yake ikaendelea kupapasa sehemu mbalimbali za mwili wangu, mara madafu ya kifuani mara madafu ya uwani na muda mfupi uliofuata maombi yalisimama na pepo langu kali lilimzidi nguvu mchungaji yule feki na kumfanya kuwa miongoni mwa mapepo wachafu walioitawala nyumba na mwili wangu.

Mchungaji alijitahidi kuninyanyua na kunilaza kitandani. Baada ya hapo kilichofuata kati yangu na Baba Mchungaji kilikuwa ni kitendawili.

Siku hiyo ilikuwa ni siku ya mkosi sana kwangu. Mlango wangu uligongwa kwa mara nyingine. Kwakuwa mchungaji alikwisha kuwa hoi amepitiwa na usingizi hajijui hajitambui. Nikamuacha kitandani na kwenda kufungua malango.

Mnh! sikuweza kuamini macho yangu, alikuwa ni yule Mkuu wa kituo amekuja kufuata malipo yake niliyoshindwa kumpatia usiku wa Juma tano kule kituoni.

Sikutaka kupoteza muda, nikamuongopea kuwa mume wangu alikuwa njiani kutokea safarini, hivyo kama alikuwa tayari tufanye haraka haraka kisha tuwachane. Askari yule alionekana kuwa na uchu mithili ya fisi aliye ona mifupa. Pale pale sebleni pakawa ni mahali pa kulipana madeni.

Wakati tukiendelea na biashara zetu mimi na Mkuu wa kituo, nilishituka kuona mlango ukifunguliwa. Nilipoangalia vizuri, nilitamani kuzirai baada ya kumuona aliyekuwa akifungua mlango. Nikiwa kwenye kifua cha Askari nilikutana uso kwa uso na mume wangu Magesa.

Nikaruka na kusimama pembeni huku nikitetemeka, sikutegemea kabisa kama mwanaume yule angerejea siku hiyo kwa sababu hakunifahamisha. Nilichokuwa nikikifahamu mimi ni kwamba mume wangu alisafiri kikazi kwa muda wa mwezi mzima na aliongezewa na wiki zaidi tatu zaidi.

“Poleni kwa kazi jamani” alizungumza Magesa kwa sauti ya upole na kuelekea chumbani akituacha pale sebleni tukijiuma uma kwa aibu mimi na mkuu wa kituo.

Alipofika huko chumbani ndipo akazidi kushangaa na roho yake. Alimkumkuta Mchungaji amejilaza fofofo kitandani mwake huku akiwa kama alivyo zaliwa.

Mume wangu Magesa alishangazwa na hali ile na kujikuta metumbua macho akimtazama Mchungaji akiwa usingizini kwenye kitanda chake tena bila ya nguo yoyote. Akamuamsha kwa kumtingisha taratibu pasipo kuongea kitu. Baba Mchungaji naye Pasipo kujua aliyekuwa anamuamsha alianza kuropoka vitu vya ajabu.

“Bwana Priscaria niache nilale mpenzi. Umenipa vitu adimu sana leo” Baba mchungaji alisema na kujigeuza upande wa pili.

“Wewe wewe wewe amka amka!” Magesa alimuamsha mchungaji yule kwa sauti huku akimpigapiga vikofi kwenye miguu.

Mchungaji akainua uso kumuangalia akidhani angekutana na sura ya Priscaria. Alishituka sana baada ya kugundua kuwa aliyekuwa amesimama mbele yake alikuwani Magesa mtu aliyempa kazi ya kuombea familia yake. Magesa akatoa tabasam na kumsemesha.

“Hongera sana Mchungaji. Naona kazi niliyokupa umeifanya ipasavyo” Magesa akazungumza kwa sauti ya upole utafikiri hakuna kitu kilichokuwa kikiendelea.

“Bwana asifiwe Mtumishi”

“Wacha kumdhihaki Mungu!”

“Aah…..mnmm…..eeee” Mchungaji alikosa la kuzungumza.

“Naona unawachunga vyema kondoo wa Bwana”

“A….ah…..samahani sana ndugu, ni shetani tu kanipitia”

“Usijali Mchungaji. Unaweza ukaendelea kujipumnzisha tu”

“Ha….hap…ana…hapana”

“Pole kwa kazi lakini baba Mchungaji.” Magesa alisema maneno yale huku akibadilisha shati alilokuwa amevaa na kuvaa fulana.

Undrea kule kwenye kabati alikuwa amekwisha choka. Alipitiwa na usingizi mara kadhaa na kuamka. Kwa kuwa joto lilikuwa kali alishindwa kuvumilia kuendelea kubaki mle kabatini. Aliamua kujitoa pasipo kuelewa huko nje kulikuwa kunaendelea kitu gani.

Undrea alifungua mlango wa kabati na kutoka akamkuta mwenye nyumba akiwa anabadilisha nguo. Akataka kutimua mbio lakini alipokumbuka kuwa alikuwa amevaa boksa tu akatulia na kutetemeka kwa baridi ya woga huku jasho likimtiririka.

Magesa hakuweza kuamini macho yake. Alijikuta akimtazama Undrea kwa mshangao na kushindwa kuelewa wanaume wote hao mke wake aliwezaje kuwahudumia kwa wakati mmoja.

“Ama kweli duniani kuna mambo” alizungumza Magesa huku akimtumbulia maho Undrea kwa mshangao.

“Vipi Undrea imekuwaje tena?” mume wangu alioji.

“Hapa…hap….ana. nilimletea shemeji chipsi” alisema Undrea kwa kujikanyaga.

“Kwa hiyo ulienda kumtafuta kabatini?” Magesa akaoji kwa ile sauti yake ya upole.

“Ah….nilikuwa……nilikuwa…….”

“Au ulikuwa unapika huko kabatini?”

“Hapana kaka Magesa”

“Nilidhani jiko la chipsi limehamia kwenye kabati langu?”

“Hapana kaka”

“Kumbe ulikuwa unafanya nini sasa kwenye kabati langu?” Magesa aliendelea kuzungumza kwa upole.

“Nilikuwa….. nilikuwa……”

“Huna jipya. Ulikuwa nini na kichupi chako kama Jonsina?”



“Naomba unisamehe, ni shetani tu kanipitia”

“Pumbavu, kila mtu anamsingizia shetani. Chukua nguo zako uondoke haraka” Magesa alimwambia Undrea.

Undrea akavaa nguo zake haraka haraka na kutimua mbio. Alinipita mlangoni nikiwa nimechanganyikiwa nisijue cha kufanya. Hakuamini kama alikuwa amepona kutoka kwenye mikono ya Magesa mtu aliyekuwa akisifika kwa ukorofi.

Niliingia chumbani na kumkuta Magesa akiangaliana na mchungaji kwa macho ya tahadhari na tafadhali. Nilikosa kabisa nguvu za kutembea na kujikuta nikitambaa kuelekea pale alipokuwa amesimama mume wangu. Kisha nikatulia hatua kadhaa nikimsoma hasira zake. Mume wangu akamsemesha Mchungaji.

“Najua una majukumu mengi Baba mchungaji, unaweza kwenda” Magesa alisema kwa kebehi.

Baba Mchungaji alichukua nguo zake na kuanza kuvaa huku akitetemeka kwa woga. Alivyo ondoka hakugeuka nyuma. Nahisi alikuwa haamini kama ametoka salama kwenye nyumba ile iliyo jaa mapepo ambayo yalimshinda kuyafukuza.

Magesa akanisogelea taratiibu huku akitoa tabasamu. Kwa tahadhari kubwa nikawa namsubiria anifikie. Alinishika mikono na kuninyanyua taratiibu kutoka pale nilipokuwa nimepiga magoti. Alinikumbatia na kunipiga busu la kwenye paji la uso. Kisha kwa lugha ya upole sana akazungumza.

“Nakupenda sana Priscaria mke wangu”

“Nakupenda pia Mume wangu” Nilimjibu kwa aibu huku nikibubujikwa na machozi ya aibu na majuto.

“Naomba nikwambie kitu mke wangu kipenzi” Magesa alizungumza kwa ile sauti yake ya upendo.

“Ndio mume wangu”

“Chukua kila unachokitaka humu ndani halafu uondoke” alisema kwa sauti yake iliyojaa upole

“Hapana mume wangu bado nakupenda” nikazungumza huku nikiangua kilio mtoto wa kike.

“Wewe nenda zako tu mama” alinijibu kwa upole kama vile hapakuwepo na kibaya kilichotokea ndani mle.

“Niende wapi mume wangu?”

“Nenda kwenu!” Magesa alianza kuzungumzaa kwa hasira.

Nami sikukata tamaa ya kumtaka radhi nikiamini angenielewa kwa sababu mara nyingi nilipomkosea alikuwa mwepesi wa kunisamehe. Lakini siku hiyo ilikuwa kinyume. Kila nilivyo zidi kumuomba msamaha ndivyo na yeye alivyozidi kupandisha hasira na kutaka kunitandika makofi.

“Sikiliza wewe Malaya. Sikutaki, sikupendi, na ninakuchukia.” Mume wangu Magesa akazungumza kwa hasira huku ametoa macho kama fundi saa aliyepotesa nati.

“lakini mume wangu......”

“Stop! Ishia hapo hapo. Nimesema ondoka” Magesa alisema na kutoka nje akiniacha ndani.

Nikahisi nguvu zikizidi kuniishia, viungo vikaninyong’onyea, na kizunguzungu kikali kikanidondosha chini na kupoteza fahamu.

*****

Asubuhi ilinikuta na kunipita nikiwa sijijui wala sijitambui. Mchana vile vile wa Ijumaa hiyo sikubahatika kuuona. Jua lilizama na giza likakaribia. Hadi kwenye mida ya saa nne usiku ndipo nikaanza kusikia sauti za watu kwa mbaaali. Nilitaka kufumbua macho lakini nilishindwa kwa sababu maco yalikuwa mazito mno. Nikajaribu kunyanyua mkono lakini nao haukusogea, vilevile mguu nao haukuweza hata kutikisika.

Hadi Saa tano na nusu usiku huwo wa Ijumaa ndipo nilipopata nuru ya mwanga na kubaini kuwa nilikuwa Hospitalini. Pembeni nilimuona mama yangu mzazi na mjomba wangu wakitabasamu mara baada ya kuniona nimezinduka. Mtu wa kwanza kumuulizia alikuwa ni mume wangu Magesa.

“Mama mume wangu yuko wapi?”

“Amekwenda kukununulia juisi” Mama aliniambia na kunifanya nitulize mzuka. Nilisubiri sana lakini Magesa hakutokea. Nilipomuuliza mama sababu ya mume wangu kuchelewa kurudi mama akaniambia labda alikuwa amepata dharula.

Mama alipohakikisha kuwa nilikuwa nimepata ahuweni vya kutosha,alinibandika ukweli wa kutosha kuhusu mume wangu. Alisema kuwa Magesa alikuwa ameachana na mimi, kwa hiyo sikuwa tena mke halali wa mwanaume huyo kwa sababu alikuwa amekwenda kanisani na kuandika taraka. Maneno yale yaliniuma sana kwa sababu mume wangu bado nilikuwa nampenda sana.

kwenye kitanda cha mbele yangu alikuwa ameketi kijana mmoja amabaye hakuonekana mgeni sana kwenye macho yangu. mkononi mwake alikuwa ameshika gazeti ambalo lilikuwa na picha ambazo zilinivutia. Ingawa hali yangu haikuwa nzuri sana, nilimuomba gazeti kijana yule. Lo! picha ya mbele ilikuwa ya mume wangu iliyosindikizwa na kichwa kilichokuwa kimeandikwa kwa maandishi ya wino mzito.

“ALIYE FUMANIA APIGWA HADI KUZIMA” Imebainika kuwa taarifa hizi zilikuwa ni tata… Uk 2.

Picha ambazo zilibeba kichwa kile zilikuwa zikimuonesha mume wangu Magesa akiwa amekamatwa shingoni na mwanaume mwengine. Picha nyingine zilimuonesha huyo msichana ambaye alikuwa chanzo cha mtafaruku huwo. Haraka haraka nilifunua ndani ili kupata habari kamili kuhusiana na utata wa kashfa ile ambayo alikuwa amekumbwa nayo mume wangu.

Ni watu wawili walioonekana kuwa na miili iliyojazia kwenye hoteli maarufu (Mountain Lunch Hotel) jijini Arusha mwezi uliopita. Mabaunsa hao ambao jina la mmoja wao ni Magesa (31) mkazi wa jijini Dar es salaam, na mwingine hakuweza kufahamika kirahisi. Wamejikuta katika wakati mgumu baada ya gazeti moja kuandika taarifa za uwongo juu yao kuwa wamefumaniana. Ukweli umebainika kuwa watu ho walikuwa katika migogoro yao binafsi na sio kugombea mwanamke kama ilivyo daiwa. Chanzo cha gazeti hilo kimekiri kutoa taarifa ambazo hazikufanyiwa uchunguzi wa kutosha. Chanzo chetu kimeeleza kuwa…..”

Sikuweza kuendelea kusoma taarifa zile, nilijikuta moyo wangu ukiniuma sana kwa kumhukumu mume wangu kwa kosa ambalo hakuwa amelifanya. Niliwageukia wazazi wangu na kuwaeleza juu ya taarifa zile, mwisho nikawaeleza kuwa niliziamini taarifa zile kutokana na jinsi mume wangu alivyo ondoka pale nyumbani. Niliwaeleza jinsi ambavyo meseji ya fundi umeme ilivyoingia na kupelekea kupoteza imani kwa mume wangu.

“Umeseme ulipokea meseji ya mapenzi kutoka kwa fundi umeme?” yule kijana aliyekuwa ameketi kwenye kitanda cha mbele yangu alihoji. Nilimuitikia kwa kichwa pasipo kuzungumza neno lolote.

“Unaikumbuka hiyo meseji” yule kijana alihoji

“Siwezi kuikumbuka yote, lakini ilikuwa inahusu kupokelewa mume wangu na mpenzi wake” nilieleza.

Kijana yule alitoa simu yake na kuanza kuibonyeza bonyeza kisha akanikabidhi.

“Hebu soma hii meseji”

“VIPI DARLING UTAONDOKA NA GARI GANI? NAKUSUBIRI KWA HAMU NIMELIMISI PENZI LAKO. LOVE U MWAAAAH!” nilipomaliza kuisoma meseji ile nikatuliza macho yangu usoni mwake kwa sekunde kdhaa.

“Vipi, ndio hiyo?” alihoji yule kijana

“We umeipataje?” nilihoji kwa mshangao huku nikiwa nimemkazia macho.

“Pole sana Priscaria, mimi ndio fundi umeme mwenyewe. Siku moja nilikuja kurekebisha shoti iliyotokea pale ndani kwenu” alisema yule kijana kwa upole.

Nikatulia kama vile sikuwa nimeyasikia yale maneno yake.

“Mimi ninamgonjwa wangu kitanda cha tatu hapo. Nimekuja hapa baada ya kuhisi nakufahamu. Pole sana kwa hilo ila nilimpigia simu mume wako na kumueleza ukweli ingawa jibu alilonipa ni kwamba hakuiona hiyo meseji. Ugua pole dada. Mungu atakusaidia utapona tu” alizungumza yule kijana na kujiinua kuelekea kwa mgonjwa wake. Nilijikuta nikizidi kujawa na dukuduku rohoni.

Wakati kijana yule alipokuwa akizungumza, kumbe kitanda cha jiraji kulikuwa na msichana amabaye alikuwa anatusikiliza. Kijana alivyo ondoka tu yule msichana alifika pale kitandani kwangu.

“Poleni jamani” msichana yule alianza na kutoa pole.

“Asante” mama na mjomba waliitikia.

“Mimi naitwa Yusrah, kama sikosei wewe ni mke wa Magesa” alisema msichana yule huku akinitazama pale kitandani.

“Haujakosea”

“Mimi sikufahamu kabisa, ila mazungumzo yenu yamenifanya nikufahamu” alisema yule msichana aliyejitambulisha kwa jina la Yusrah.

“Unamaanisha nini?”

“Kwanza kabisa nikupe hongera”

“Kwa lipi?” nilihoji

“Kwa kupata mwanaume mwenye mapenzi ya dhati na mvumilivu”

“Bado sijakuelewa dada”

“Mimi nafanya kazi pamoja na mume wako” Yusrah alizungumza kwa kuongopa

“Enhe” nilijivuta pale kitandani ili kumsikiliza vizuri.

“Kuna mwanamke alikuwa anamtaka, basi sikumoja alipokea simu ya mke wake yaani wewe, basi Magesa alivyokuja huko alimtimua mwanamke yule kama mwizi na kumwambia ukome kunifuata futa mimi ninandoa yangu na mke wangu nampenda san” Yusra alizungumza kwa vitendo maneno ambayo kiukweli yalinichoma sana. Nikajiona ni mkosaji mkubwa sana mbele ya mume wangu, ni afadhali ningekuwa muwazi kwa mume wangu pengine ingesaidia.

“pole sana dada yangu kwa kuumwa, lakini hongera kwa kuwa na mume mwema” alisema yule mwanamke na kuondoka zake.

Akili yangu haikuwa sawa kabisa baada ya kupata taarifa zile. Nikapata wazo la kumpigia Fatuma ili akaongee na shemeji yake aweze kurudisha nyuma maamuzi yake. Nikavuta namba ya Fatuma kwenye simu na kuanza kuipiga. Haikuchukua muda mrefu simu ilipokelewa.

“Niambie Shoga” Fatuma alipokea simu.

“Best mwenzio nina matatizo”

“Matatizo?”

“Ndiyo. Hivi ninavyoongea nimeachika”

“We Prisca! Sababu ni nini?”

“Mwenzangu, si Magesa jana karudi ghafla”

“He! ikawaje hajakukuta nyumbani?”

“Si bora ingekuwa hivyo”

“Kumbe?”

“Amenifumania na wanaume watatu nyumbani kwake”

“Eee! Na wewe umezidi. Wanaume wote hao ulikuwa unataka sifa?”

”Sio sifa Fatuma. Yani....hee... we achatu”

“Haya pole ndugu yangu. Wenzio ndoa wana zililia wewe unazichezea”

“Naomba unisaidie Fatuma shoga yangu”

“Nikusaidie nini sasa?”

“Naomba ukaniombee kwa Magesa turudiane” nilizungumza huku nikilia.

“We koma! Nikusaidie mimi ndio nilikuitia hao wanaume?”

“Naomba unisaidie Fatuma”

“We mwanamke unikome. Umalaya wako ndio uliokuponza” Fatuma alisema maneno yale na kukata simu.

Niliumia sana moyoni na kumuona Fatuma kama vile ni mchawi wangu. Ni yeye aliyekuwa akinishawishi kujiingiza kwenye mambo machafu halafu mwisho ananikana na kuniita malaya. Nilijikuta nikilia kwa uchungu wa hali ya juu uliochanganyikana na majuto.

Niliongozana na mama pamoja na mjomba kurudi nyumbani kwetu Morogoro. Baada ya wiki kama tatu niliwatuma ndugu zangu wakanichukulie mizigo yangu nyumbani kwa Magesa na kurudi kuishi mwenyewe hapa mjini Morogoro.

Kwakweli baada ya kuachana na Magesa nilijikuta nikiwacha kabisa tabia zote chafu na kumrejea Muumba wangu. Nikapata taarifa kuwa magesa alikuwa ameoa mwanamke mwingine. Ingawa niliumia sana lakini sikuwa na la kufanya.

Baada ya muda fulani nilianza kuumwa homa za mara kwa mara, kifua hakikutaka kupona, na uzito mwilini ulikuwa ukipungua kwa kasi. Sikuweza kuamini pale nilipochukua jukumu la kupima afya yangu. Majibu yalionesha kuwa nilikuwa nimeathilika na virusi vya ukimwi. Niliumia sana ingawa nilikuwa nafahamu kabisa nilipaswa kupata ugonjwa huo kutokana na matendo yangu niliyokuwa nikiyafanya huku nikiamini kuwa nilikuwa namkomesha mume wangu Magesa.

Lakini yote haya yametokana na ile MESEJI YA FUNDI UMEME iliyoingia kimakosa kwenye simu ya mume wangu. Laiti ningelijua mwisho wake kuwa ungelikuwa ni huu,ni afadhali ningelimueleza ukweli mume wangu kabla ya kuifuta ile meseji kwenye simu yake. “Ama kweli mficha maradhi kifo humuumbua”. Nawashauri jamani muwe wawazi kwa wapenzi wenu ama ndoa zenu. Pia sio vyema kutoa hukumu kwa mambo ambayo hayana uthibitisho ama uhakika. Fahamu kuwa ‘Ncha ya mkuki haipigwi kwa konzi’, na ‘Aisifiae mvua imemnyea’

Asante sana kwa kufuatilia mkasa wangu huu wa kusisimua, kuburudisha na kuhuzunisha. Naomba usiache kutoa maoni yako kwa mwandishi wetu ili apate moyo wa kuendelea kutupa ladha katika kazi zake nyingine. Ahsante Sana.


MWISHOOOOO.


0 comments:

Post a Comment

BLOG