Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

BONGO DAS'LAAM - 1

  


IMEANDIKWA NA : KIZARO MWAKOBA

*********************************************************************************

Chombezo : Bongo Das'laam 

Sehemu Ya Kwanza (1)



Pesa ni kitu ambacho kila mmoja anahangaika ili kuweza kuikamata. Wanafunzi wanakwenda shuleni ili waelimike na baadae waweze kuipata pesa kwa urahisi, Wafanyakazi wanakwenda kazini ili mwisho wa siku waweze kupata pesa, Wakulima wanakwenda shambani ili mwisho wa siku wavune na kujipatia pesa, n ahata wale omba omba wa mtaani wanajitahidi ili waweze kujipatia pesa.

Ukiwa na pesa unaweza kupata mahitaji ya kila namna. Ukiwa na pesa unaweza kupata chakula, ukiwa na pesa unaweza kupata sehemu ya kulala, na pia ukiwa na pesa unaweza kupata mavazi.

Mbali na mahitaji muhimu ya kibinadamu, vile vilepesa inatunza heshima ya mtu, pesa inatunza hadhi, pesa inalinda afya, na wakati mwingine pesa inaweza kulinda haki ya mtu. Pesa pesa! Jamani pesa! Wacheni pesa iitwe pesa!

Wimbo huu wa pesa ulikuwa ukizunguuka kwenye kichwa cha AYUBU, kijana mdogo aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika shule ya Sekondari Lusanga Gobo kule mkoani Tanga katika wilaya ya Muheza.

Pamoja na kwamba umri wa kijana Ayuibu ulikuwa mdogo lakini tayari alikwisha kuelewa umuhimu wa kupata pesa na mateso ya kukosa pesa. Ndoto za kijana Ayubu zilikuwa ni kumiliki pesa za kutosha ili kuweza kumiliki mambo mengine yote.

Habariza kuibuka kwa machimbo ya madini ya dhahabu kule wilayani Amani hazikumpitia mbali kijana Ayubu. Alipata taarifa kuwa watu wengi waliokuwa wakijihusisha na uchimbaji wa madini kule wilayani Amani walitajirika ghafla, wakubwa kwa wadogo.

Ayubu alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wakitamani kuacha shule na kwenda kujiunga na shughuli ya uchimbaji wa madini kule Amani. Alipokutana na baadhi ya wanafunzi ambao na wenyewe walikuwa tayari kuacha shule na kwenda Amani ujipatia pesa kwa urahisi kupitia uchimbaji mdogo wa madini ulioibuka ghafla.

Mzee NYIRUKA alikuwa ni mzazi wa kiume aliyewezesha uwepo wa kijana Ayubu hapa duniani kwa kushirikiana na mke wake Mama Ayubu. Mzee Nyiruka alikuwa akijitahidi kufanya kazi za vibarua kwa juhudi zote ili kuweza kupata pesa za kumlipia karo kijana wake. Alitamani sana kijana huyo asome na kusoma hadi elimu ya chuo kikuu ili siku moja aweze kumsaidia kwa namna moja ama nyingine.

Ilikuwa siku ya Jumamosi ambayo mara zote Ayubu alikuwa akiitumia kuwasaidia wazazi wake shughuli mbalimbali hasa za shambani. Mzee Nyiruka alikuwa ameinama akinoa jembe lake tayari kwa safari ya kuelekea shambani.

Ayubu alikuwa ameshikilia jagi la maji mkononi mwake akitoka kuosha uso wake, alisimama na kumtazama kwa makini baba yake jinsi alivyokuwa akinoa lile jembe.

“Baba..!” Ayubu aliita kwa sauti ya chini.

“Naam” Mzee Nyiruka aliitika huku akiendelea kunoa jembe lake.

“Hivi una mpango gani na hilo jembe?” nikahoji kwa umakini.

“Kwanini?” alihoji mzee Nyiruka pasipo kumtazama kijana wake.

“Utaendelea kupambana na jembe hadi lini?” Ayubu alihoji.

Mzee Nyiruka aliposikia swali lile aliwacha kusugua jembe akamgeukia kijana wake na kumtazama usoni kwa sekunde chache kisha akaachia tabasamu la matumaini.

“Unasema unataka kujua mpango wangu juu ya hili jembe?” mzee Nyiruka alihoji huku akitabasamu.

“Maana kila kukicha wewe na jembe, jembe na wewe!” Alizungumza Ayubu kwa umakini mkubwa.

“Plani yangu ni kuwekeza katika elimu yako. Nimejitoa kufanya kazi kwa bidi ili mtoto wangu usome na baadaye uje unifae” Mzee Nyiruka alizungumza kwa umakini wa hali ya juu.

“Sasa baba ngoja nikwambie kitu” Ayubu alizungumza huku akisogelea gogo la mnazi lililokuwa karibu na mama yake kisha akaketi.

“Haya unasemaje” baba alihoji huku akionekana kumsikiliza kwa makini kijana wake.

“Sasa leo hii mimi ndio kwanza nipo kidato cha pili, nisome hadi form Four, nijiunge na kidato cha tano, niingie cha sita, nimalize halafu niende sijui chuo kikuu nisome hukoo mamiaka kibao huoni kama ni mbali sana?” Ayubu alizungumza maneno ambayo baba yake hakuweza kuyaelewa.

“Unataka kusemaje Ayubu mwanangu?” alihoji baba Ayubu kwa umakini.

“Naona unatumia nguvu nyingi sana kuwekeza kwenye jambo ambalo malipo yake ni miaka na miaka ijayo” Ayubu alizungumza kwa umakini.

“Kwahiyo unataka kusemaje?” mzee Nyiruka akahoji kwa mshangao.

“Mimi naona hakuna haja ya kupoteza nguvu zako Zaidi kwaajili ya kitu ambacho faida yake hadi miaka mia huko!” alizungumza Ayubu huku akionekana kumaanisha kwa kile kilichokuwa kikitoka mdomoni mwake.

“Mie hata sikuelewi naona unazungumza utafikri umekunywa maji ya chooni” mzee Nyiruka alizungumza huku akigeuka na kuendelea kunoa jembe lake taratibu.

“Kwamfano nikipata mipesa leo hii haitakufaa?” Ayubu alizungumza kwa kujiamini.

“We umeamka na ndoto za mchana leo” alizungumza mzee Nyiruka huku akilishika jembe lake kwa kidole kuona kama limepata makali.

“Halafu baba unadhani mimi natania, siku sio nyingi nitakuwa tajiri mkubwa sana hapa kijijini” alizungumza Ayubu kwa msisitizo.

“Hebu nenda ukajiandae twende shamba si unaona jua linapanda?” mzee Nyiruka alizungumza baada ya kumuona kijana wake alikuwa akizungumza maneno yasiyoeleweka.

“Hizi shida za shamba karibu zinamalizika” Ayubu alizungumza huku akijiinua kutoka kwenye lile gogo.

“Ndio usome sasa, unafikiri mafanikio yanakuja tu kama ndoto!” Mzee Nyiruka alisisitiza kauli yake.

“Nani asome sasa! Mimi sitaki tena shule nataka pesa” Ayubu alizungumza huku kiweka jagi kwenye pipa la maji lililokuwepo pale nje na kuchukua jembe lake lililokuwa limeegemezwa ukutani.

“Una wazimu wewe hebu twende huko!” alizungumza mzee Nyiruka uku akiweka jembe lake begani tayari kwa safari ya kuelekea shambani.

“Kwanza mi hata siendi huko shamba kwenyewe” Ayubu alizungumza huku akisimamisha jembe pale ukutani.

“Hivi leo una nini we mtoto?” mzee Nyiruka akahoji kwa jazba.

“Baba pesa, mimi nakaribia kupata pesa. Sasa kwanini niteseke” Ayubu alizungumza kwa msisitizo.

“Kwaiyo usipoenda shamba ndio unapata pesa sio?”

“Mi naenda Amani” Ayubu alizungumza kwa sauti ya chini.

“Unasemaje wewe?” alihoji kwa mshituko mzee Nyiruka baada ya kusikia kuwa kijana wake amemtajia safari ya Amani.

“Baba mimi nimeamua kwenda Amani” alizungumza Ayubu kwa msisitizo.

“Unakwenda Amani kufanya nini?”

“Kwenye machimbo” alizungumza Ayubu kwa sauti ya chini huku sura yake ameikunja akiamini baba yake asingeweza kukubaliana na wazo lake lile.

“Mungu wangu we mtoto umempata nani aliyekudanganya huko, kwahiyo shule nayo inakuwaje?” mzee Nyiruka akahoji huku akiwa ameteremsha jembe lake na kuegemea mpini kwa mshangao.

“Shule nitaendelea nikirudi” Ayubu alizungumza huku akivuta hatua kuelekea kwenye lile gogo.

“Hivi husikii shida za huko Amani? Kila siku watu wanakimbizwa na polisi kwaajili ya hayo machimbo. Leo na wewe unataka kujitumbukiza huko huko!” Mzee Nyiruka alizungumza kwa hasira na msisitizo kujaribu kumshawishi kijana wake afute wazo la kwenda kuchimba madini na kuacha shule.

“Baba mimi akili yangu imeshatamani pesa sielewi chochote kile” Alizungumza Ayubu huku akijiweka kwenye gogo na kuinamisha kichwa chake na kukiweka juu ya magoti.

“Sasa kwa taarifa yako, hayo machimbo ya Amani yamefungwa na ndiyomaana kila siku Polisi wanafukuzana na wananchi wanaokaidi agizo la serikali” alieleza mzee Nyiruka kwa sauti ya upole lakini iliyokuwa imejaa msisitizo wa hekima na busara.

“Baba mimi ungeniacha tu nikajaribu maisha” Ayubu alizungumza huku akichora chora chini kwa kijiti michoro isiyoeleweka.

Wakati Ayubu amejiinamia na kuzungumza maneno yale alisikia sauti ya mtu ikiingilia kati mazungumzo yale.

“Kama ni mimi wala nisingepoteza muda wangu kwenda huko Amani” sauti ile ilizungumza huku mzungumzaji akivuta hatua kuwasogelea Ayubu na baba yake.

Ayubu pamoja na baba yake waligeuza shingo zao kumuangalia mtu aliyekuwa ameingilia mazungumzo yao. Walimshuhudia KONDO kijana wa jirani yao akikaribia.

“He Kondo!” Ayubu alizungumza na kuinuka kutoka pale kwenye gogo.

“Achana na mawazo ya kwenda Amani bwana” kijana yule alizungumza huku akimsogelea Ayubu na kumkumbatia.

“We Kondo umekuja lini?” Ayubu alihoji huku akimtazama kwa makini rafiki yake yule jinsi alivyokuwa amependeza.

“Shikamoo mzee Nyiruka” Kondo alisalimia huku ameshika mkono wa Ayubu.

“Marahaba Kondo, habari za Dar?” alihoji mzee Nyiruka huku akimtazama kijana yule kwa tabasamu la upendo.

“Safi tum zee wangu” Kondo alijibu kwa ufupi huku akiachia tabasamu mwanana.

“Umekuja lini?” alihoji mzee Nyiruka.

“Nimeingia muda si mrefu mzee wangu” Kondo alieleza.

“Haya karibu sana”

“We Kondo, huko Daslam ndo kumekupenda hivyo?” Ayubu alihoji huku akimkagua Kondo mavazi aliyokuwa ameyavaa.

“Mjini hakudanganyi kaka” Kondo alijibu kwa ufupi.

“Asee tunaondoka wote” Ayubu alizungumza kwa msisitizo huku akimuangalia baba yeke aliyekuwa akivuta tumbaku lake.

“Shule nayo utamuachia nani?” Alihoji Kondo huku akijiweka kwenye gogo la mnazi.

“Mbona wewe umeacha shule kwani umekufa? tena mambo yako yamenyooka kuliko hata sisi tulionga’nga’nia shule” Ayubu alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama baba yake ambaye alikuwa akiwasikia kila kitu walichokuwa wanakizungumza.

“Kama upo tayari twende tu, mjini raha sio huku kila kukicha shamba” Kondo alizungumza kwa sauti ya chini.

“Yani ukiondoka tu, ujue mzigo wako wa kwanza ni mimi” alizungumza Ayubu kwa msisitizo.

“Kwahiyo Amani huendi tena” mzee Nyiruka aliingilia kati mazungumzo yale na kuhoji.

“Aah we si umenitisha sasa niende kufanya nini?” Ayubu alizungumza kwa kujiamini.

“Kwa taarifa yako sasa, hata huko Daslam wala huendi. Tena wewe nyanga’au usinipotezee mwanangu naomba uondoke haraka” mzee Nyiruka alizungumza kwa msisitizo baada ya kuona kijana Kondo alikuwa anaelekea kumpotosha kijana wake.

“Lakini mzee Nyiruka…” Kondo alitaka kuzungumza lakini alikatishwa na mzee Nyiruka.

“Hakuna cha lakini, naomba uondoke” mzee Nyiruka alizungumza kwa jazba.

“Lakini mzee mbona sijafanya kosa lolote!” Kondo lijaribu kujitetea kwa kulalama.

Mzee Nyirua aliinuka na kuchukua jembe lake kisha akamfuta Kondo na kutaka kumlima kichwani lakini kwa bahati nzuri au mbaya, kijana yule alifanikiwa kukwepa na kuruka pembeni.

“Baba kwanini unafanya hivyo?” Ayubu akahoji kwa mshangao.

“Na wewe nyamaza, mbega wewe!” mzee Nyiruka alizungumza huku akiinua tena jembe kumlima Kondo.


Kondo alipoona balaa lile aliamua kutimua mbio na kumuacha Ayubu na baba yake. Hakutegemea kama ziara yake ile ingemponza na kuonekana adui wa familia ya watu. Hakutamani kurudi tena kwenye nyumba ile.

Mzee Nyiruka alimgeukia kijana wake huku akiwa amekunja sura yake kwa hasira.

“Na wewe, nisikusikie tena unazungumziasuala la kuacha shule, nitakukata masikio hayo” mzee Nyiruka alizungumza na kuweka jembe lake begani kisha akaanza safari ya kuelekea shamba huku akimuacha Ayubu ameduwaa akimkodolea macho.

*****

Mkakati wa Ayubu kuacha shule uliendelea kukua siku hadi siku, pamoja na kwamba baba yake naye hakuwa nyuma kumuwekea vikwazo kijana wake. Msimamo wa mzee Nyiruka ulikuwa ni kuhakikisha kijana wake anasoma na kufanikiwa katika masomo yake. Alikuwa tayari kupambana kwa kila hali kuhakikisha kijana huyo anapata haki yake ya elimu bila ya kipingamizi chochote.

Asubuhi na mapema mzee Nyiruka pamoja na mke wake mama Ayubu waliamka tayari kwa kwenda sambani. Mara nyingi siku za wiki Mama Ayubu alipokuwa akiamka kwaajili ya kujiandaa kwenda shamabani, alitumia nafasi hiyo kumuamsha kijana wake Ayubu ajiandae kwaajili ya kwenda suleni.

“Ayubu Baba” Mama Ayubu aliita kwa sauti ya chini kama ilivyokuwa kawaida yake. Hata hivyo hali ilikuwa kimya tofauti na siku zote.

Mama Ayubu aligonga tena mlango kwa nguvu kidogo lakini bado Ayubu alikaa kimya.

“We Ayubu ebu fungua malango kumekucha” alipaza sauti mama Ayubu uku akigonga mlango kwa nguvu. Hata hivyo bado kimya kilitawala.

“Baba Ayubuu!” Mama Ayubu alipaza sauti kumuita mume wake baada ya kugonga malngo wa Ayubu bila ya mafanikio.

Mzee Nyiruka alipofika alikamata kitasa cha mlango na kujaribu kufungua. Bila ya hiyana mlango ule ukaitika rabeka! Ukafunguka. Waote wawili waliingia chumbani mle kwa haraka sana kuweza kushuhudia kilichokuwa kinaendelea.

Kitanda cha Ayubu kilikuwa kimetawaliwa na upweke uku mwenyewe hakuwepo. Walijaribu kuangaza huku na kule mle chumbani lakini hakukuwa na mtu.

“Atakuwa ametoka” alizungumza mzee Nyiruka.

“Sasa atakuwa amekwenda wapi lakini?” mama Ayubu alihoji kwa wasiwasi.

“Aah Kwani Ayubu ni mtoto mdogo bwana” alizungumza mzee Nyiruka huku akifungua mlango kwa lengo la kutoka chumbani mle.

“Sio kawaida yake kutoka mida kama hii!” alizungumza mama Ayubu kwa mashaka.

“Wanawake bwana sijui mpoje! Sasa mtu asitoke hata kidogo, je kama amekwenda msalani?” Alizungumza mzee Nyiruka huku akitoka na kumuacha mama Ayubu mle chumbani.

Pamoja na kwamba mzee Nyiruka hakuwa na wasiwasi kwa kutomuona kijana wako chumbani mida ile lakini mama Ayubu moyo wake uligoma kabisa kukubaliana na jambo lile.

Wakati mama akitaka kutoka chumbani mle alituma macho dirishani na kuona karatasi imekunjwa vizuri na kuchomekwa kwenye wavu wa dirisha lile. Mama Ayubu alisogelea dirisha na kuchomoa karatasi ile.

“Baba Ayubu! Baba Ayubu!” aliita mama Ayubu huku akitoka chumbani mle mbio na karatasi yake mkononi.

Mzee Nyiruka alikuwa nje akichomeka msumari kwenye jembe lake kwa kugonga na nyundo. Sauti ya mama Ayubu ilimshitua na kumfanya ageuke na kumuangalia Mama Ayubu ambaye alikuwa akitoka ndani huku ameshikilia kipande cha karatasi.

“Haya kuna nini?” alioji mzee Nyiruka kwa mashaka.

“Soma mwenyewe uone! Soma! Soma hii karatasi” alizungumza mama Ayubu huku akimkabidhi mume wake karatasi ile.

Mzee Nyiruka alitupa jembe chini na kupokea karatasi ile kutoka kwa mke wake huku akiwa na wasiwasi.

Laahaula! Ayubu alikuwa ametoroka kuelekea jijini Dar es salaam kwa lengo la kutafuta pesa. Ndani ya barua ile alikuwa ameeleza kuwa maisha magumu ya kijijini yalikuwa yamemchosha hivyo alilazimika kwenda kusaka maisa mjini kwaajili ya familia yake. Vile vile alijaribu kuwatoa wasiwasi wazazi wake kwa kuwaeleza kuwa angefikia kwa rafiki yake Kondo yule mtoto wa jirani yao hivyo wasihangaike kumtafuta.

“Unaona! Unaona kazi yako hii?” mzee Nyiruka alizungumza kwa hasira huku amemtolea macho mama Ayubu.

“Mungu wangu! Jamani mwanangu” Mama Ayubu alizungumza huku akishika tumbo lake kuashiria maumivu ya tumbo la uzazi.

“Mungu wako amefanya nini wakati yote aya umeyataka wewe!” mzee Nyiruka alikuwa akizungumza huku akitetemeka kwa hasira.

“Sasa mimi nimefanya nini Baba Ayubu! Mtoto ametoroka mwenyewe sasa mimi nimesababishaje jamani?” Mama Ayubu aliendelea kuzungumza kwa ucungu mkubwa.

“Tena nyamaza Fukufuku wewe! Hii mipango yote inamaana huijui wewe?” alihoji Mzee Nyiruka.

“Sasa kama ningejua mume wangu, ningenyamaza kweli, au unadhani mimi nimefuraia jambo hili?” mama Ayubu alilalamika kwa uchungu.

“Kwani wanawake mna akili timamu! Wote si akili zenu ni matope tu!” mzee Nyiruka akazungumza kwa hasira huku akiamini mke wake alishirikiana na Ayubu kutoroka nyumbani pale.

“Hivi wanawake tumekukosea nini mume wangu, kosa afanye mtoto wako kutukanwa tutukanwe wanawake wa dunia nzima” mama Ayubu alilalamika.

“Kwani mnajiona mpo sawa?” alizungumza mzee Nyiruka kwa msisitizo.

“Ipo siku moja utakaa na kuwaheshimu wanawake wewe mwanaume” mama Ayubu akazungumza kwa hasira.

“Thubutuuuu! Labda kama sio mimi” alizungumza mzee Nyiruka huku akielekea mlango wa kuingilia ndani.

“Mbona nilivyokwenda kwetu ulinifuata huku unalia lia?” alizungumza mama Ayubu huku akimuangalia mume wake kwa hasira.

“Wewee nililia baada ya kuona umekubali kurudi tena nyumbani kwangu” mzee Nyiruka alizungumza huku akiwa amesimama kumtazama mke wake.

Kauli ile ya Mzee Nyiruka ilimfanya mama Ayubu kusahau tatizo lile na kuangua kicheko.

“Unachekelea enh? Sasa sitaki kumuona tena huyo fukufuku wako hapa nyumbani kwangu” mzee Nyiruka alizungumza huku akigeuka na kuingia ndani.

Mama Ayubu alikwa ameduwaa asielewe kitu cha kufanya juu ya kile kilichokuwa kimetendwa na kijana wake Ayubu. Kitu kibaya zaidi ni kwamba lawama zote zilikuwa zimemuelemea yeye pamoja na kwamba akuwa ameshiriki kutoroka kwa mtoto wao. Alivuta pumzi na kuzitoa nje kwa kuzisukuma kisha akavuta hatua kuelekea ndani.

****

Foleni ya magari kwenye barabara ya Morogoro road ilimshangaza sana Ayubu. Hakuwahi kuona msongamano mkubwa wa magari kiasi kile. Baada ya kusota kwenye foleni kwa muda mrefu, basi la Rahaleo likaingia ubungo na kusimama mahali husika. Watu walipoanza kuteremka Ayubu akagundua kuwa pale ndipo palikuwa kwenye kituo kikubwa cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo.

Kelele za vijana waliotaka kumsaidia zilimchanganya sana, akakumbuka maneno ya watu kuwa pale Ubungo kulikuwa na vibaka wa kumwaga. Akapata wazo la kukumbatia begi lake kwa umakini. alivuta hatua kadhaa na kusimama akiangalia huku na kule, akajikuta akitoa tabasamu na kujiona shujaa kwa kufanikiwa kumtoroka mzee Nyiruka na kufika jijini DareSalaam.

Swali likabaki je aelekee wapi? na huyo rafiki yake Kondo angempataje? Hakujua amuulize nani kwasababu kila mtu alionekana kuwa bize na mambo yake.

Pale aliposimama alipita kijana mmoja aliyeonekana mtanashati kutokana na mavazi yake, Ayubu akaona yule mtu alikuwa anafaa kumuelekeza mahali alipokuwa akiishi rafiki yake Kondo, akamsimamisha kijana yule.

"Samahani kaka, naomba kuuliza"

"Sory nawahi sehemu" alijibu yule kijana na kuondoka pasipo kumsikiliza Ayubu.

Ayubu akatabasamu baada ya kukosa msaada kutoka kwa kijana yule. Hata hivyo hakukata tamaa na kumuendea kijana mwingine aliyekuwa akitembeza maji.

"Habari yako kaka?"

"Safi broo, nikutolee makubwa au madogo?" yule muuza maji alihoji kwa bashasha la mfanya biashara.

"Hapana ndugu, naomba nikuulize kitu"

"Kuuliza ni mia tano, unayo?" yule muuza maji alizungumza baada ya kubaini kuwa Ayubu alikuwa ni mgeni jijini pale hasa kutokana na jinsi alivyokumbatia lile begi lake la nguo.

"Sawa.... hii hapa" Ayubu alijibu na kutoa shilingi mia tano na kumkabidhi yule kijana.

"Okay uliza sasa" alizungumza yule muuza maji huku akitafuta bablish.

"Unafahamu anapoishi Kondo?" Ayubu alihoji kwa umakini.

"Kondo! yeye ni nani hapa Dar?"

"Alikuwa anaishi kijijini kwetu"

"Wewe ni mgeni?"

"Ndio"

"Unatokea wapi?"

"Lusanga mkoani Tanga karibu na Muheza mjini"

"Ndugu yako amekwambia anaishi sehemu gani?"

"Hapa hapa Dar"

"Dar ni kubwa broo, anaishi maeneo gani"

"Mnh kwa kweli sijui"

"Aai... kumbe we chizi! Unamtafuta mtu ambaye hujui anapoishi hapa jijini" yule kijana alimshangaa Ayubu na kumuacha amesimama bila ya kumpatia jibu la swali lake.

Ayubu akabaki ameduwaa akiwa haelewi afanye nini baada ya kupata majibu yale ya kukatisha tamaa kutoka kwa yule mtembeza maji.

Akiwa bado amesimama pale, alifika msichana mmoja mrembo ambaye aliyasikia mazungumzo yale kati ya Ayubu na yule muuza maji na kumsemesha Ayubu.

"Kwani kaka una tatizo gani?" alihoji binti yule kwa sauti ya upendo.

"Namtafuta ndugu yangu" Ayubu akajibu kwa sauti ya kukata tamaa.

"Anaitwa nani?"

"Kondo"

"Yupoje?" msichana yule alioji kwa umakini mkubwa.

"Ni mrefu kidogo, maji yakunde halafu ana mwanya"

"Anhaaa! alikuwa anaishi Lusanga?" binti Yule alizungumza huku akioneka alikuwa anamfahamu vyema Kondo.

"Enhee! Huyo huyo! Si anapenda kuvaa suruali za jeans?" Ayubu alihoji kwa sauti iliyokuwa imejaa matarajio ya kumpata rafiki yake.

"Ah! namjua" Alizungumza dada Yule huku akichezesha kichwa kuashiria kumfahamu vyema Kondo.

"Naomba nielekeze basi anapoishi dadaangu"

"Na mimi naenda hukohuko. Itakuwa vyema tukiongozana” alisema yule dada na kumpokea Ayubu begi.

Ayubu pamoja na yule msichana walisogea hadi karibu na geti la kutokea, yule dada akamfahamisha Ayubu kuwa mizigo ilikuwa ikisajiliwa kwenye kibanda cha pembeni kidogo na pale walipo, hivyo alimwambia Ayubu amsubiri pale pale akasajili ule mzigo.

Ayubu alikubaliana na msichana yule na kubaki akimkodolea macho alivyokuwa akiondoka kwa kupita pale kwenye geti la kutokea.


Ayubu alisubiri kwa muda mrefu lakini yule dada hakurudi tena. Ikabidi amfuate pale getini. Lo! kumbe kijana Ayubu alikuwa amekwisha karibishwa Jijini na matapeli wa Bongo.

Watu wakamfahamisha Ayubu kuwa alikuwa ameibiwa aendelee na shughuli zake nyingine. Ayubu alinyanyua mikono na kuiweka kichwani huku akiwa kama vile amechanganyikiwa. Alitoka nje ya geti na kuanza kuzurula mjini asijue pa kuelekea.

Baada ya kutembea kwa muda mrefu pasipo kumuona mwenyeji wake, Ayubu aliingia kwenye mgahawa kwa lengo la kupata chakula cha mchana kwasababu njaa ilikuwa ikimuuma sana. Aliagiza chakula na kuanza kula taratibu huku akiwaza namna ya kumpata rafiki yake Kondo. Baada ya kumaliza kula alifika dada mhudumu kudai malipo yake. Ayubu aliingiza mkono mfukoni na kujikuta hakuwa na hata senti. Laaahaul! Kumbe alikuwa amekwishaibiwa pesa zote.

Ayubu aliendelea kujisachi katika mifuko yote lakini hakufanikiwa kupata hata senti moja. Hakuelwa pesa zake zilizokuwa mfukoni alikuwa amezipotezea wapi. Alijaribu kuvuta kumbukumbu lakini hakupata jibu akabaki amekodoa macho kumuangalia usoni yule mhudumu wa mgahawa ule.

“Vipi, naomba hela yangu kaka” mhudumu yule alizungumza baada ya kumuona Ayubu akimtumbulia macho pasipo kumpa pesa yake.

“Samahani dada. Nimeibiwa” Ayubu alizungumza kwa sauti ya unyonge.

“Unasemaje?”

“Nimepoteza pesa zangu zote” Ayubu alieleza.

“Kwahiyo?”

“Sina hata senti”

“Baba nipe changu, usilete masihara na biashara yangu” Mwanamke yule alizungumza huku akinyoosha mkono kuomba malipo kutoka kwa Ayubu.

“Kweli Aunt, nimeibiwa hela zote” Ayubu alizungumza kwa huruma.

“Wewe kaka usinitanie. Nipe pesa yangu” alizungumza kwa msisitizo yule dada muuzaji na kumfanya Ayubu kuwa katika wakati mgumu.

Wateja wengine nao waliungana na dada mwenye mgahawa na kumpa Ayubu jina la Tapeli. Walimzogoma na kumlazimisha alipe pesa ya watu vinginevyo wange muitia kelele za mwizi apigwe na kuchomwa moto.

Pamoja na kwamba hakuwa na mtu aliyekuwa upande wake lakini hakukata tamaa ya kujitetea. Hatimaye walifikia hitimisho la kuosha masufuria ili kufidia gharama za chakula alichokula

Baadaya ya kumaliza adhabu aliyopewa ilikuwa imekwishafika jioni. Alitembea tembea huku akifikiria mahali ambapo angeweka ubavu wake usiku wa siku hiyo. Hadi inafika mida ya saa nne alikuwa hajatambua mahali pa kulala.

Mungu hamtupi mja wake. Katika pita pita yake Ayubu alifanikiwa kupata kauchochoro ambacho alikitumia kujihifadhi kwa usiku ule. Kwakuwa hakuwa na nguo ya kujifunika alihisi baridi ikimtesa sana. Alijikunja na kuwa kama kifaranga aliyekuwa amenyeshewa na mvua.

Ilipofika usiku wa manane akiwa pale kwenye kiuchochoro alisikia sauti za watu wakizungumza huku wakitembea kuelekea pale alipokuwa amelala. Aliwasikia wakijibishana.

“Huyu jamaa anapenda kulala maeneo haya”

“Inabidi tuwe makini, huyu mtu ni hatari sana”

“Ni kweli”

“Tulieni, twendeni kimyakimya”

“Kweli jamani, hakikisheni leo hatumpotezi huyu mshenzi” walizungumza watu wale waliokuwa wakitembea kuelekea pale kwenye kauchochoro alichokuwa amejilaza Ayubu.

Watu wale walivyokaribia wakamulika kwa tochi na kufanikiwa kumuona Ayubu amejilaza. Ayubu alivyoona vile alishindwa kuvumilia akainuka haraka na kuanza kutimua mbio ili kuokoa maisha yake. Wale watu nao walimuunganishia kwa nyuma na kumkimbiza huku wakipiga firimbi kama vile walikuwa wakimkimbiza mwizi.

Wakati Ayubu akitimua mbio, ghafla akakumbana na mtu ambaye naye alikuwa akikimbia kuelekea kule alikokuwa akitokea yeye. Wote wawili walidondoka chini kisha waliinuka na kutimua mbio kila mmoja alielekea upande wake. Ayubu hakuamini kama amepona kutoka kwa yule mtu, kichwani mwake alidhani kuwa yule alikuwa ni miongoni mwa wale waliokuwa wanamkimbiza.

Kundi kubwa la watu likatokea mbele yake huku wakipiga makelele ya mwizi. Hapo Ayubu akagundua kuwa kumbe yule mtu aliyekumbana naye alikuwa ni mwizi. Uamuzi aliochukua ni kupinda kushoto kuwakwepa wananci wale. Loo! Kumbe walimuona na kuanza kumkimbiza Ayubu na kumuacha mwizi wao.

Kwakuwa alikuwa mgeni katika zile njia alizokuwa akipita, alitumbukia kwenye mtaro wa maji machafu. Alitaka kuinuka na kuendelea kukimbia lakini aliteleza na kuanguka tena. Wale wananchi wenye hasira kali walikuwa wamekwisha mkaribia. Masikini Ayubu alijivuta hadi kwenye karavati lililokuwa karibu na kujibanza sawia na ukuta wa daraja lile.

Wale watu walifika na kuuruka ule mtaro kwa spidi wakiamini kuwa Ayubu alikuwa amepita. Mmoja kati ya wale watu akasikika akiwashauri wenzie waangalie kwenye mtaro pengine mwizi wao alikuwa ameingia humo.

Mwanga wa tochi ulimmulika Ayubu machoni na kumfanya kufumba macho na kutulia akisubiri matokeo. Alibana pumzi ili asionekane. Akasikia sauti za watu wakibishana.

“Oyaa twendeni bwanaa hawezi kuingia hapa”

“Kwanini asiingie, anaweza kuwa humu humu” mtu mwingine alisisitiza

“Haya mulika na kule kwenye karavati” mwingine akatoa wazo ambalo lilizidi kumchanganya Ayubu.

“Twendeni bwana tusije tukamkosa” walizungumza watu wale walipoona kuwa kumetulia na hapakuwepo na dalili ya kuwepo na mtu maeneo yale.

Baada ya muda kupita na kimya kutawala, Ayubu alitoka taratiibu kutoka kwenye lile karavati kwa umakini wa hali ya juu. Lakini wakati alipokuwa akitoka alisikia sauti za watu wakielekea pale alipokuwa yeye huku wakizungumza

Ayubu alijirudisha nyuma na kujibanza tena kando ya karavati lile. Wale watu walifika na kusimama juu ya lile karavati. Mara alihisi vitu kama maji ya moto yakimdondokea usoni na kutiririka hadi usawa wa mdomoni. Looo! Kumbe mmoja kati ya wale watu alikuwa akikojoa. Harufu ya ule mkojo ilimfanya Ayubu kubaini kuwa yule mtu alikuwa amekunywa pombe kali. Hata hivyo Ayubu aliendelea kujikausha hadi watu wale walipoondoka.

Kulipo pambazuka Ayubu alikuiwa amechoka sana na nguo zake zilikuwa chafu mno. Alikuwa ananuka mwili mzima. Aliangaza huku na kule pengine angepata maji ya kujiosha lakini hakuambulia kitu. Alianza kuzurula vile vile ili kutafuta msaada wa mavazi kutoka kwa wasamaria wema lakini kila alipofika walimfukuza na kumuita mwendawazimu.

Ilipofika mchana Ayubu alianza kuhisi njaa kumfukuzia kwa spidi kali. Alitamani kwenda kwenye magenge ya Mama ntilie lakini mfukoni hakuwa na hata shiringi moja. Alipojaribu kuomba kwa watu wamsaidie akaambulia kufukuzwa na kutukanwa kutokana na kuwa mchafu na kutoa harufu Mbaya.

Waswahili wanasema “Msafiri kafiri” Ayubu alikuta chakula kimemwagwa jalalani. Kwa njaa aliyokuwa nayo alikifakamia chakula kile. Watu waliomuona walishindwa kumtofautisha na vichaa walioko jijini pale. Baada ya kumaliza chakula chake alianza kuzurula tena huku akilini mwake kukiwa na wazo la kumtafuta rafiki yake Kondo.

Ilipofika jioni akajikuta akitamani kupata chakula cha usiku kutokana na tumbo lake kudai. Mfukoni mwake kulisalia harufu ya matope tu. Akaelekea kwenye jalala moja na kupekua pekua angalau kuweza kupata chochote cha kudanganyia tumbo lake.

“Jasho la mtafutaji halimwagiki bure” alifanikiwa kupata mkate na viazi vilivyopikwa. Alitia kwenye mfuko wa rambo na kuondoka nao kutoka pale jalalani. Safari yake ilikuwa haifahamiki mwisho ingawa lengo la safari ile lilikuwa ni kumsaka rafiki yake Kondo.

Alifika kwenye kiuchochoro na kujibanza kwa lengo la kupata chakula ambacho alikiokota kule jalalani. Sehemu aliyokuwa amekaa ilikuwa imetulia vizuri. Haikuwa rahisi kwa mtu yeyote kuweza kumuona kirahisi. Alifungua mfuko wake na kuanza kula taratibu huku akifikiria mahali pa kulala usiku ule.

Sauti za miguu ya watu wakitembea zilisikika zikielekea pale alipokuwa ameketi Ayubu. Mara akaona kivuli cha watu wawili waliokuwa wakizidi kumsogelea. Ayubu alijisogeza nyuma taratiibu na kujifunika na tenga kubwa lililokuwa pembeni yake. Watu wale walifika na kusimama pembeni ya lile tenga.

Ayubu alikuwa akiwaona vizuri kwa kupitia kwenye tundu la tenga. Walikuwa wameshikilia mapanga yaliyokuwa yamelowana kwa damu. Ayubu aligundua wazi kuwa watu wale walikuwa wametoka kufanya mauaji mahali fulani. Mtu mmoja miongoni mwao aliinua mguu na kuupachika juu ya lile tenga. Ayubu alibana pumzi kuzuia mapigo ya moyo ambayo yalikuwa yakimuenda kwa kasi.

“Vipi, hapa panafaa?” mtu mmoja alihoji.

“Inaonekana panafaa”

“Mnh! Watu hawafiki hapa?”

“Hata kama wakifika hawawezi kujua kama kuna mali”

“Enhee! Umeona hilo tenga?”

“Lina nini?”

“Tufiche humo ndani ya tenga”

“Hembu lifunue” sauti ya mtu yule ilizidi kumshitua Ayubu na kumfanya atetemeke.

Ayubu alifahamu wazi kuwa watu wale waliokuwa na silaha zilizokuwa zimelowa damu, wasingeweza kumuacha akiwa hai. Ayubu alifumba macho na kumuomba Mungu atende miujiza.


Yule mtu aliyeambiwa afunue tenga aliliangalia kwa kitambo kisha akaligongagonga kwa ule mguu wake.

“Hakuna sababu ya kulifunua. We weka mzigo tusepe” alizungumza mtu yule kwa sauti ya msisitizo.

“Basi angalia kama kuna mtu anatuona” mtu mwingine alizungumza.

“Hakuna bwana, hebu wacha woga”

“Inabidi kesho tuhakikishe mteja anapatikana” alisema yule mwengine na kutoa kifuko kidogo na kukichomeka kwenye lile tenga. Alishituka baada ya kumgusa Ayubu kwenye mgongo.

“Mnh!”

“Vipi?”

“Hapa kuna mtu nini!” alizungumza mtu yule

“Kwani vipi?”

“Kuna kitu kigumu humu ndani”

“Achana nacho, weka mzigo wetu tuondoke. Mtu hawezi kukaa hapo”

Watu wale baada ya kuficha kale kamfuko kao walielekea upande wa pili wa maeneo yale.

Ayubu alitulia mle ndani ya tenga kwa muda mrefu hadi alipobaini kuwa hapakuwepo na mtu mahali pale. Alijitoa taratiibu kutoka kwenye lile tenga. Alichukua kile kifurushi kilichokuwa kimefichwa na wale watu na kukifungua.

Ayubu alipokifungua kimfuko kile hakuweza kuamini macho yake. Kilikuwa kimefunga madini ya dhahabu, kitu ambacho kilimsababisha kutoroka kijijini na kuja mjini Dar es salaam,

Hakutaka kuchelewa, alikitumbukiza kwenye nguo ya ndani na kuondoka haraka kuelekea kule walikotokea wale watu. Akili yake ilikuwa ikiwaza utajiri. Alijiona ni kiasi gani Mungu amempendelea kwa kumpa utajiri akiwa bado kijana mdogo vile. Taswira ya jumba kubwa la kifahari na magari ya kifahari ilimjia akilini mwake. Kama oja ni pesa, tayari alikuwa amezipata pesa.

Ayubu alipata nguvu za kutembea kwa muda mrefu ili kutafuta mahali pa kulala usiku ule ambapo ni mbali na maeneo yale. Alikwenda kujilaza pembeni ya duka moja kubwa la sonara. Aliamini maeneo yale pasingekuwepo na mtu yoyote ambaye angemfanyia kitu kibaya kwasababu palikuwa peupe na wazi. Hivyo ingekuwa rahisi kuomba msaada hata kutoka kwa walinzi wa maduka.

Ayubu alitandika kirago mbele ya duka moja na kujilaza, aligalagala kwa muda mrefu pasipo kupata usingizi. Muda mwingi aliutumia kuwaza utajiri alioupata na namna ambavyo wazazi wake kule kijijini wangempokea.

Mara ilifika gari ya polisi na askari watatu wakashuka. Ayubu alishituka na kutaka kukimbia kutokana na jinsi askari wale walivyoshuka kwa mbwembwe kutoka kwenye gari. Walimzunguuka Ayubu na kuanza kuongea nae.

“We kijana, unafanya nini hapa” askari wale walioji kwa msisitizo huku wakiwa wameshikilia bunduki mkononi.

“Nime…nime….nimejipumzisha Afande” Ayubu alieleza kwa woga.

“Wewe ni mwizi”

“Ha…ha…ha…hapana”

“Msirichereweshe Afande. Rireteni turipereke Riuaji hiro” alisema askari mwingine aliyekuwa kwenye gari kwa msisitizo.

Ama kweli “kama haipo haipo tu” kwenye lile duka la sonara alilokuwa amelala Ayubu, kulikuwa kumevunjwa na kufanyika kitendo cha wizi. Mbaya zaidi watu walioiba wamefanya mauaji ya mlinzi wa duka lile. Askari walianza kufanya upekuzi kwa Ayubu kuona kama alikuwa amehusika na wizi ule pamoja na mauaji.

Laahaula! Ayubu alikutwa na kifuko cha dhahabu alichokuwa amekificha kwenye sehemu zake za siri.

“Haaa! We kijana kumbe ni rijambazi?” alizungumza askari mmoja baada ya kuona kale kamfuko ka dhahabu.

“Jamani sio mimi” Ayubu alianza kujitetea kwa wasiwasi na woga mkubwa.

“Hii umetoa wapi?”

“Nimeokota, lakini sio hapa” Ayubu akaeleza.

“Pumbavu, umewezaje kuua peke yako au unawenzio?” Askari wale walizungumza kwa mshangao.

“Hapana mimi sijaua jamani” alilalamika Ayubu huku akilia kwa uchungu.

“Utaozea jera kunguni wee” alisema askari huku wakimnyanyua na kumtumbukiza kwenye gari yao.

Ayubu alijaribu kujitetea lakini hakuna askari aliyemuelewa na kuambulia kupigwa virungu vya kutosha kwenye magoti yake. Alijikuta nguvu zikimuishia na kunyong’onyea kutokana na kipigo kile kitakatifu. Ingawa alilia sana na kuomba asamehewe lakini sauti yake haikusikika na hata askari mmoja.

Gari ile ya polisi ilikuwa ikienda kwa mwendo wa kasi sana. Ilikuwa ikielekea kituo kikuu cha polisi cha Ostabey kumpeleka jambazi Ayubu.

Laahaula! Mkosi ndani ya mkosi, kulitokea gari la mchanga ambalo halikuwa na taa na kulivaa lile gari la polisi na kusababisha ajali mbaya. Gari ya polisi ilibingirika mara tatu na mwisho ililala matairi yakiwa juu.

Ayubu alijua amekwisha poteza maisha kutokana na ajali ile mbaya. Lakini haikuwa hivyo kwani alitingisha mkono, mguu, na kuchezesha macho bila matatizo. Maumivu aliyokuwa akiyasikia yalikuwa ni yale ya virungu. Kwa ufupi ni kwamba hakuwa ameumia hata kidogo kutokana na ile ajali.

Siku zote ajali ni kitu kibaya sana, lakini siku ile kwa Ayubu ilikuwa kinyume. Alimshukuru mungu kwa kuwasababishia ajali ile. Askari wote walikuwa wamepoteza maisha pale pale. Alichokifanya ni kujichomoa na kuketi hatua kadhaa kutoka pale kwenye ajali ile. Alishuhudia maiti za askari zikichomolewa na kupakiwa kwenye gari la kubebea wagonjwa.

Pale alipokuwa amekaa Ayubu alihisi mtu anamgusa kwenye bega lake la kushoto. Alipogeuka na kumuona mtu yule, akahisi mapigo ya moyo yakimwenda mbio na matumaini ya kuishi tena yakatoweka ghafla. Mtu yule alikuwa ni mmoja wa wale watu waliokuwa wameficha dahahabu zao kule kwenye tenga.

Mtu yule alitoa tabasamu na kumsalimia Ayubu.

“Habari yako”

“Safi tu, niaje?”

“Shwari”

“Nawewe ulikuwepo kwenye ajali?”

“Amm….ah…hapana sikuwepo”

“Najua ulikuwepo kwasababu nimekuona ukitoka”

“Umenifananisha”

“Sikiliza kijana, ukileta uhuni nawaambia watu wakupeleke polisi. Sema kwanini walikukamata?”

“Aaah! Wamenionea tu. Lakini sio mimi”

“Wamekuonea nini”

“Heti nimeu…..ah! sijui nimevunja duka”

“Umeiba nini?”

“Wanasema nimeiba madini”

“Yako wapi?”

“Amebaki nayo afande mmoja kwenye gari”

“Kweli?”

“Ndio” alijibu Ayubu na kumfanya kijana yule kwenda kwa kasi kwenye lile gari lililopata ajali. Ayubu aliutumia mwanya ule kuondoka maeneo yale. Alihisi kama angeendelea kubaki pale angeweza kutokea mtu mwingine na kumpeleka polisi.

****

Hadi kulipo pambazuka Ayubu alikuwa akitembea. Siku hiyo hakupata kabisa hamu ya kulala tena. Alihisi kuwa ni lazima angeingia mikononi mwa polisi ama vibaka wa jijini kama angelala. Alikuwa ametembea umbali mrefu kutokea pale alipopata ajali usiku. Kwa wakati huo alikuwa amefika maeneo ya Ubungo.

Njaa ilikuwa ikimuuma sana kwasababu tangu chakula alichokula usiku hakutia kitu kingine mdomoni mwake. Aliwaza kitu cha kufanya asubuhi ile ili apate chochote cha kutia mdomoni.

Alisogea hadi karibu na mgahawa mmoja uliokuwa karibu yake. Aliingia na kuwakuta watu wakiagiza na kupata kifungua kinywa. Alimfuata mzee mmoja aliyekuwa amekaa kwenye kona. Mzee yule alionekana kuwa na roho nzuri na sura ya huruma.

“Shikamoo mzee”

“Marahaba hujambo?”

“Samahani mzee wangu”

“Unasemaje?”

“Tangu jana sijala naomba unisaidie nipate chochote mzee wangu”

“Sina hela mimi. Unadhani pesa zinaokotwa?”

“Nisaidie mzee wangu”

“We mhudumu hebu njoo utoe hizi takataka zako hapa. Sisi tunakula nyie mnawaachia machizi waje kutusumbua. Vipi bwana!” yule mzee alizungumza kwa ukali na kebehi dhidi ya Ayubu. Amakweli umdhaniae ndiye kumbe siye. Kwa muonekano yule mzee alionekana ni mtu mtaratibu sana na mwenye huruma kumbe ilikuwa kinyume.



Ayubu aliona kuwa alikuwa amekwisha haribu pale ndani. Aliamua kuondoka kwenda kufikiria cha kufanya. Wakati akiondoka alihisi mtu anamvuta shati.

“We kijana” yule mtu aliyemgusa aliita. Ayubu aligeuka pasipo kuongea kitu na kukutana na mwanamke wa makamo.

“Shikamoo” Ayubu alisalimia kwa heshima.

“Marahaba. Vipi una tatizo gani?” mama Yule alihoji.

“Njaa mama” Ayubu alisema kwa hudhuni.

"Twende ukakae pale upate chochote” alisema yule mama na kuelekea pale alipokuwa amekaa awali.

Ayubu hakuweza kuamini kama amepewa mamlaka ya kuchagua chakula alichokuwa akikitaka. Kutokana na njaa aliyokuwa nayo alijikuta akiagiza ugali na maharage. Yule mwanamke aliamua kumuagizia chai na chapati kwasababu kulikuwa ndio kwanza asubuhi. Chakula kilipofika Ayubu alikifakamia mithili ya ng’ombe anayenyonya akatenganishwa na mama yake kwa muda mrefu halafu wakakutanishwa tena. Yule mwanamke alimuangalia Ayubu na kutingisha kichwa kusikitika.

“Mimi naitwa Mama Suzy, naishi Kijitonyama pamoja na mumewangu na binti yangu” mwnamke yule alizungumza kwa upole kujitambulisha.

“Mimi naitwa Ayubu” Ayubu naye alijieleza.

“Unaishi wapi Ayubu?”

“Mnh! Kwa kweli sina pa kuishi mamaangu” Ayubu alieleza huku akitafuna.

“Unamaanisha wewe ni chokoraa?” mama yule akahoji kwa mashaka.

“Hapana……ndio”

“Sasa mbona sikuelewi. Mara ndio mara hapana. Ok tuwachane na hayo, vp mbona unavidonda usoni imekuwaje?” Mama Suzy aliamua kuachana na swali la kwanza kwani aliamini kuwa jibu lingepatikana tu.

Ayubu aliamua kuzungumza kila kitu kilichomtokea tangu siku aliyofika pale jijini DareSalaam hadi siku ile. Mama Suzy alijikuta machozi yakimtoka kutokana na yale aliyo yasikia.

“Pole sana kijana”

“Ahsante mama”

“Sasa utakwenda na mimi nyumbani kwangu” Mama Suzy alisema kwa huruma.

Ayubu alishituka baada ya kusikia taarifa zile. Aliinua macho na kumtazama yule mama usoni. Akawa kama vile hajasikia vizuri.

“Naam!”

“Utakaa kwangu hadi utakapo mpata mwenyeji wako” alizungumza mama Suzy kw msisitizo.

Ayubu alivuta pumzi na kuzitoa nje kwa nguvu. Hakuamini masikio yake, akataka kupiga magoti ili kutoa shukurani zake kwa mama Suzy lakini mama Suzy alimuwahi na kumzuia asifanye kitendo kile.

“Nashukuru sana mama. Mungu akubariki”

“Usijali mwanangu ni mambo ya kawaida. Maliza kula tuondoke” alisema mama Suzy huku akifungua pochi yake na kutoa pesa za kulipia chakula. Ayubu alipomaliza kula waliondoka pamoja kuelekea Kijitonyama nyumbani kwa mama Suzy.

****

Mama Suzy alikuwa ni mke wa mzee Manyama. Walibahatika kupata mtoto mmoja tu wa kike ambaye ndiye waliyempa jina la Suzy. Walikuwa wakimpenda sana binti yao huyo. Mzee Manyama alikuwa akijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kumtimizia kila alichokuwa akikihitaji bintiye huyo ili asishawishike na majaribu ya kidunia.

Suzy alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha pili sawa na kidato alichoacha Ayubu kule kijijini Lusanga. Kwa maana hiyo rika la Ayubu na rika la Suzy yalikuwa yanawiana.

Mama Suzy alipofika na Ayubu pale nyumbani alimkuta Suzy akifua sare zake za shule. Suzy alipomuona mama yake alimkimbilia na kumkumbatia kwa shangwe. Alimsalimia na kumpokea mfuko mdogo wa rambo aliokuwa ameuning’iniza mkononi.

Suzy alimtazama Ayubu kwa macho yaliyojaa mashaka na chuki. Mavazi aliyokuwa amevaa Ayubu yalikuwa yakimtafsiri kama chokoraa wa mjini ama chizi.

“Mama, huyu nani?” alihoji Suzy kwa kebehi.

“Huyu ni kakaako” alisema mama Suzy kwa ufupi.

Suzy aliposikia jibu alilopewa na mama yake, aliangua kicheko ambacho kilipelekea kukaa chini huku akiwa ameshikilia mbavu zake kutokana na kicheko kile. Alikohoa mara kadhaa huku akiendelea kucheka.

“Mama bwana. Yaani watu woote hukuwaona hadi kuleta haka kachokoraa halafu heti unamwita kaka yangu. Ana hadhi ya kuwa kaka yangu huyu?”

“Suzy shika adabu yako” mama Suzy alimfokea binti yake.

Suzy alipobaini kuwa mama yake alikuwa amekasirika, aliwacha kucheka na kumuomba msamaha. Alipeleka chumbani ule mfuko aliompokea mama yake kisha akatoka nje na kuwaacha Ayubu na mama yake ndani.

Ayubu alioneshwa bafuni na kwenda kujimwagia maji. Alipotoka alioneshwa chumba ambacho angekitumia kulala na kubadirishia nguo. Kilikuwa ni chumba chenye nafasi ya kutosha. Alipotupa macho kitandani aliona amewekewa nguo za kubadilisha. Kumbe walivyotoka kule kwenye mgahawa walipitia Kariakoo kwanza na kununua nguo kwa ajili ya Ayubu. Alivaa T-shirt na jeanse kisha akaenda sebleni.

Alimkuta mama Suzy ameketi sebleni akichambua mboga kwa ajili ya chakula cha mchana. Alipomuona Ayubu hakuweza kuamini. Kumbe Ayubu alikuwa ni kijana mzuri sana ambaye uzuri wake ulikuwa umefichwa na matatizo. Mama Suzy alitoa tabasamu na Ayubu naye alilipokea lile tabasamu na kutoa lakwake.

‘Umependeza sana Ayubu” alisema mama Suzy.

“Ahsante mama” Ayubu alijibu huku akiketi kwenye kochi pale sebleni.

Mama Suzy alipaza sauti na kumuita mwanae ambaye bado alikuwa akiendelea kufua kule nje. Suzy alitegemea kuwa akiingia tu angemkuta yule chokoraa ameketi kwenye kochi alilonunua baba yake. Alipanga kuwa endapo angemkuta ameketi kwenye kochi asingemhofia mama yake, bali angemtimua kama mbwa.

Suzy alisimama mlangoni huku akizunguusha macho pale sebleni. Alikuwa akimtafuta yule chokoraa aliyeingia na mama yake. Kwenye kochi alimuona kijana mtanashati, mzuri, na mwenye mvuto. Hakujua kijana yule aliingia saangapi kwasababu yeye alikuwa akifua nguo karibu na mlango, hivyo kama angeingia mtu ni lazima angemuona. Alivuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu.

“Mama yule Chokoraa wako yuko wapi?” Suzy alihoji kwa kiburi.

“Suzy, hivi kwanini hutaki kusikia?”

“Sio hivyo mama. We unatuletea machizi humu ndani!”

“Hembu kaa hapo. Nimekuita” mama Suzy alitoa amri na Suzy aliitekeleza. Aliingia na kuketi pembeni mwa kijana mtanashati. Alimtupia jicho la pembeni ili kumthaminisha. Alihisi mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio. Hakujua ni kwanini alikuwa vile, lakini hiyo ndiyo ilikuwa hali halisi.

“Suzy mwanagu, huyu anaitwa Ayubu. Ni kaka yako” alisema mama Suzy huku akitarajia kuwa Suzy angeleta upuuzi kama wa awali.

“Anhaa karibu kaka Ayubu”

“Nashukuru sana”

“Ayubu, huyu ni dada yako anaitwa Suzy. Mtakuwa pamoja mkisaidiana hili nalile” alisema mama Suzy na kupelekea Suzy kulipukwa na furaha. Akashindwa kujizuia kuonesha furaha yake.

` “Woow! Kwahiyo tutaishi wote hapa nyumbani?” Suzy alihoji kwa furaha.

“Ndio hivyo. Naomba umpe ushirikiano”

“Sawa mama, hilo halina tatizo”

“umefurahi enh?”

“Sana. Lakini mama…”

“Enhee…”

“Hivi yule chokoraa uliyeingia naye yuko wapi?”

“Suzy, shika adabu yako”

“Lakini mama….”

“Lakini nini koma! mtu niliyeingia naye ni kaka yako Ayubu, na sio chokoraa”

“Haaa!” Suzy alipatwa na mshangao.

“Nyoko nini?”

“Naomba unisamehe kaka Ayubu” Suzy alimuomba msamaha Ayubu kwa yote aliyomfanyia wakati alipokuwa anafika. Hakuamini kama yule mtu mchafu angeweza kuoga na kupendeza kiasi kile.

Ayubu alimwambia Suzy kuwa alikwisha kumsamehe. Suzy alitoka nje na kwenda kuendelea na usafi wa nguo zake na Ayubu alibakia sittingroom akiangalia runinga.

****

Baada ya miezi miwili tangu Ayubu kufika pale nyumbani kwa Mama Suzy alikuwa amebadilika kwa kiasi kikubwa. Alikuwa amenawiri na kupendeza sana. Alikuwa amekwisha sahau matatizo yote ambayo alikumbana nayo wakati anaingia jijini. Alikuwa amekwisha kata tamaa ya kumtafuta rafiki yake Kondo kwasababu hadi muda ule hakuwa amemuona wala kusikia habari zake.

Tabia nzuri ndiyo ilikuwa silaha kubwa katika maisha ya Ayubu pale nyumbani kwa Mama Suzy. Mama Suzy alikuwa ni mama yake na mzee Manyama alikuwa ni baba yake. Hivyo Ayubu aliishi kama mtoto wa familia ile. Mzee Manyama alimtafutia shule kijana wake ili aendelee na masomo ya sekondari. Hivyo Suzy na Ayubu wakawa wanasoma kidato kimoja lakini shule tofauti.

Waswahili wanasema “Ukila muwa huwezi kukosa fundo.” Suzy alikuwa ni tatizo katika maisha ya Ayubu. Mara kadhaa alikuwa akimtia majaribuni lakini Ayubu alikuwa akimuomba sana mungu amuepushie balaa lile. Alikuwa akiwaheshimu sana wazazi wake, hivyo alifahamu kuwa kama ange fanya mzaha angejiharibia mwenyewe.

Siku moja Ayubu na Suzy walikuwa mezani wakijisomea. Wakati huwo wazazi wao walikuwa wamelala chumbani. Suzy alitumia muda mwingi kumuangalia Ayubu kuliko kusoma. Ayubu aliligundua jambo lile na kujikuta akihoji.

“Vipi dada Suzy, mbona husomi?”

“Aah! Nasikia baridi” alijibu Suzy kwa sauti laini.

“Nenda ukavae sweta” alisema Ayubu kwa sauti ya upendo.

Suzy aliinuka na kwenda chumbani. Alipotoka alikuwa tofauti na vile alivyo fikiria Ayubu. Suzy alikwenda kubadilisha nguo na kuvaa kimini kilichoshindwa kuyaficha mapaja yake. Juu alikuwa amevaa blauzi isiyokuwa na mikono ambayo nayo ilikuwa wazi maeneo ya kifuani na kupelekea nusu ya matiti yake kuwa wazi. Alipofika karibu na Ayubu alidondosha kalamu kwa makusudi, aligeuka na kuiokota huku sehemu za makalio zikiwa kwa upande wa Ayubu. Kitendo kile kilipelekea blauzi aliyokuwa amevaa kupanda juu na kuonesha nguo yake ya ndani.

Ayubu alipomuona Suzy alijikuta mwili wake ukimsisimka. Alimtazama binti yule kuanzia chini hadi juu na kumthaminisha ndani ya sekunde kadhaa. Kiukweli Suzy alikuwa ameumbwa vilivyo. Kumbe uzuri wa miguu yake haukuishia nje. Mapaja meupe yaliyo ungana na mlima wa makalio yake yalitosha kumpagawisha mwanaume yeyote aliyekuwa rijali. Kiuno chake kilichokuwa kimepambwa kwa rastiki ya nguo yake nyeupe ya ndani kilikuwa ni cha pekee.

Ayubu alimeza funda la mate kisha kwa haraka sana kabla Suzy hajainuka alirudisha macho kwenye kitabu alichokuwa anasoma. Moyoni mwake alijisemea kuwa endapo Suzy asingekuwa dada yake asingekubali kumuacha.

Suzy alipofika mezani hakwenda kukaa kwenye kiti chake, alisimama pembeni ya Ayubu kwa mapozi. Loo! Ayubu alipoinua macho kumtazama Suzy akaona mambo yanazidi kumuwia magumu. Sehemu kubwa ya chuchu zake zilizo chongoka kama mbilimbi zilikuwa wazi. Ayubu akakwepesha macho yake na kuangalia pembeni.

“Sasa dada Suzy ulisema unasikia baridi, inakuwaje tena umevaa hivyo?” Ayubu alihoji kwa upole. Suzy alimtazama kisha akatingisha kichwa kusikitika.

“Inamaana wewe ni mtoto ndogo?” Suzy alihoji huku akibinua midomo.

“Kwanini unasema hivyo dada Suzy?”

“Ayubu….” Suzy aliita kwa sauti ya kutokea puani.

“Nakusikiliza Suzy”

“Kusoma hujui lakini hata picha pia huoni?” Suzy alizungumza.



“Unamaanisha nini?” Ayubu alihoji swali ambalo lilionekana kumkera Suzy. Suzy alikunja uso na kutoa msonyo mrefu kwa hasira kisha akaenda kuketi kwenye kiti chake.

Suzy alilaza kichwa kwenye meza na kuweka mikono yake miwili kichwani badala ya kusoma. Ingawa Ayubu alikwisha fahamu kitu alichokuwa akikitaka Suzy lakini akawa anajifanya haelewi. Alimtupia jicho la wizi mara kwa mara na kumkuta bado alikuwa amejiinamia.

“Unaumwa Suzy” Ayubu alitupa swali la kizushi.

Suzy aliinua sura na kumtazama Ayubu kwa hasira kisha akaachia tena msonyo na kuinuka kuelekea chumbani kwake. Ayubu alifahamu kuwa Suzi alikuwa amekwenda kulala. Alitingisha kichwa kumsikitikia kisha akaendelea kusongoka. Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya Suzy na Ayubu pale nyumbani kwa mama Suzy.

****

Mzee Manyama alikuwa amesafiri kikazi kwenda mkoani Singida. Mama Suzy naye alipata taarifa za kufiwa na mjomba wake aliyekuwa akiishi Mtwara. Kutokana na hali hiyo ilibidi Suzy abaki na kaka yake Ayubu nyumbani pale.

Mama Suzy aliwasisitizia wanawe wale wawili waishi vizuri kwa upendo pindi watakapo bakia wawili. Moyo wa Suzy ulijawa na furaha kubwa kwa kitendo cha wao kubaki wawili tu nyumbani. Aliamini kuwa ni lazima angekipata kile alichokitafuta kwa muda mrefu kutoka kwa Ayubu.

Siku moja Ayubu alikuwa ameketi sebleni akitazama runinga mara baada ya kutoka shule. Suzy alifika akiwa amevalia kanguo kafupi kama ilivyokuwa kawaida yake. Alikwenda kuketi kwenye kochi la mbele ambalo ni lazima Ayubu angemwangalia.

Ile sketi fupi aliyokuwa amevaa Suzy ilipanda juu na kusababisha sehemu kubwa za mapaja yake kuwa wazi. Ayubu alimtupia jicho lakini alivyokutana na hali ile aliyarudisha macho yake kwenye runinga, kisha akamuomba mungu kimoyomoyo amsaidie kuepuka janga lile.

Suzy alipoona kuwa mtu aliyekuwa akimtega hakuwa na muda wa kumuangalia ilimbidi atumie nguvu ya ziada.

“Ayubu….” Aliita Suzy kwa sauti ya chini.

“Naam” Ayubu aliitika huku macho yake yakiwa bado ameyakazia kwenye runinga.

“Yaani nakuita hutaki kuniangalia?”

“Ah! Samahani dada Suzy” Ayubu alijifanya kuhamaki na kumgeukia Suzy.

Alipomwangalia kifuani matiti yalikuwa wazi kwa kiasi kikubwa, huko chini sasa ndio kila kitu kilikuwa wazi. Akaamua kumtazama machoni pasipo kupanda wala kushuka. Hata hivyo Suzy alionekana kukosa cha kuzungumza. Aliweka kidole mdomoni na kurembua macho. Loo! kumbe Suzy alikuwa amebarikiwa macho jamani. Ayubu alijikuta akishindwa kumtazama na kupepesa macho kuangalia pembeni.

“Vipi mbona huongei sasa?” alihoji Ayubu huku akiwa amegeukia pembeni.

“Unadhani nitaongea nini sasa?”

“Siwezi kujua”

“Aaaah!.....” Suzy alihamaki kama vile alikuwa amechomwa na mwiba.

Alijiinua pale alipokuwa ameketi na kukimbilia alipokuwa amekaa Ayubu. Alijifunua mgongoni huku akilia.

“Hebu niangalie hapa kuna mdudu amening’ata” alilalamika Suzy akiwa ameketi pembeni mwa Ayubu.

“Vipi dada Suzy una nini?” Ayubu alihamaki huku akikagua pale alipokuwa akioneshwa na Suzy.

Mnh! Ayubu alishuhudia mzigo wa shanga kiunoni mwa Suzy. Alivuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu. Alijifanya hakuziona zile shanga na kumuuliza mahali palipokuwa pakimuwasha.

“Mbona sioni kitu” Ayubu alihoji huku macho yakiwa kwenye zile shanga.

“Hapo…..shuka chini…tena….aah! hapo hapo” Suzy alikuwa akimuelekeza Ayubu ili aone zile shanga zake, kumbe Ayubu mwenyewe alikuwa amekwisha kuziona mapeeema sana.

“Hakuna mdudu. Labda awe amekimbia” alisema Ayubu na kutaka kuondoa mkono wake.

“Aaah!...No!...usitoe mkono. Naomba nikune pananiwasha” alisihi Suzy kwa sauti ya kutaka kulia.

Ayubu ilimbidi afanye kile alichoagizwa na Suzy. Wakati Ayubu akimkuna Suzy alianza kutoa sauti na miguno ya mahaba.

“Aaah!.... yeah!.....Oooh!..hapo hapo….Sweety….Mmm….tamu” alilalamika Suzy kwa sauti ya chumbani huku akijilegeza na kujikuta akitaka kumlalalia Ayubu. Sauti ile ilifanya mapigo ya moyo wa Ayubu yaende kasi. Pepo la uzinzi lilikuwa linamkaribia kumkumba lakini alipokumbuka kuwa alichokuwa akitaka kukifanya ni kosa hasa kwa wazazi wa Suzy ilimbidi ajikaze mtoto wa kiume.

“Vipi Suzy?” Ayubu alihoji kwa sauti kavu

“A’m so sweety” Suzy alijibu kwa sauti ya mahaba iliyopenya kwenye masikio ya Ayubu na kupita hadi moyoni. Alitamani kumkumbatia lakini akakumbuka tena kuwa alikuwa anataka kumkosea mama Suzy. Alitoa mkono wake kwenye mgongo wa Suzy na kutaka kusimama kuondoka lakini ilimuwia ngumu kutokana na askari kanzu kusimama wima mlangoni na bunduki yake mkononi. Alichofanya ni kusogea pembeni mbali kidogo na pale alipokuwa amekaa Suzy.

“Mbona unaondoka Mpenzi”

“Mnh!” Ayubu alijifanya hakusikia swali aliloulizwa. Neno mpenzi ndilo lililo mchanganya kabisaa mtoto wawatu wa kitanga. Hakuwahi kulisikia kutoka mdomoni mwa mrembo yule pamoja na vituko vyote alivyokuwa akimfanyia tangu alipoingia mle ndani. Hata hivyo Ayubu bado hakuwa tayari kutembea na Suzy kwasababu alitambulishwa kama dada yake, pia limhofia mzee Manyama kwasababu alimfahamu jinsi mzee yule alivyokuwa mtata hasa kwa mtu aliyejaribu kucheza na binti yake. Ayubu alipokumbuka hayo mzuka wote ulimuisha n ahata askari kanzu alipoteza nguvu na kuzimia. Ayubu aliinuka na kutoka nje akimuacha Suzy akiwa pekeyake sebleni.

*****

Usiku Ayubu akiwa amelala chumbani kwake kutokana na uchovu wa mihangaiko ya mchana alisikia malango wake ukigongwa. Aligundua kuwa aliyekuwa akigonga mlango hakuwa mwingine zaidi ya Dada yake Suzy. Mwanzo alijifanya amelala lakini kwasababu mgongaji hakuchoka ilimbidi kuinuka na kwenda kufungua mlango.

Lahaula! Alimkuta Suzy amesimama mlangoni kwake akiwa ndani ya nguo ya kulalia iliyo onesha maungo yake ya ndani.

“Vipi dada Suzy kuna tatizo?”

“Ndio” alisema Suzy huku akiwa ameng’ata kidole na kuinamia chini

“Tatizo gani?” Ayubu akahoji kwa wasiwsi.

“Naogopa kulala pekeyangu”

“Hee! Una…una….”

“Naogopa kulala peke yangu chumbani” Suzy akazungumza kwa msisitizo.

“Kwahiyo unatakaje”

“Sijui” alijibu Suzy kwa mkato.

“Suzy dadaangu, unaogopa nini wakati mimi nipo?”

“Mi siendi kulala huko, labda tulale wote huku kwako” Suzy alisema huku akiminya minya vidole vyake vya mikono.

“Hapana dada Suzy, huwezi kulala chumbani kwangu wakati vyumba vipo vingi” Ayubu alijaribu kumueleza dada yake yule.

“Hebu nipishe huko!” kabla Ayubu hajamalizia sentensi yake, Suzy alimkatisha kwa kumsukuma na kuingia chumbani, Ayubu akabaki amekodoa macho kushangaa kituko kile.

Suzy alipofika chumbani kwa Ayubu alijitupa kitandani na kulala kama mgonjwa aliyekuwa akisubiria kufanyiwa uparesheni. Ayubu alihema kwa nguvu baada ya kuuona mwili wa binti mrembo aliyeumbwa kila idara akaumbika ukiwa kitandani mwake. Ile nguo ya kulalia ilipanda juu na kuacha mapaja ya msichana yule wazi kabisaaa.

Ayubu alibaki mlangoni akijishauri cha kufanya. Alitamani kwenda kulala sebleni lakini akawaza endapo baba yao angerejea usiku ule na kumkuta Suzy amelala chumbani mwake ingekuwaje. Aliingia ndani kujaribu kumbembeleza labda angekubali kwenda kulala chumbani kwake.

“Suzy dada, unajua sio kitu kizuri unachokifanya!” Ayubu alizungmza kwa upole lakini Suzy alijifanya hasikii.

Ayubu alivuta pumzi na kupumua kwa nguvu, alipeleka mkono wa kushoto kichwani na kujikuna kisha akamsogelea taratibu Suzy na kumgusa mgongoni na kumuita lakini bado binti yule alinyamaza kimya.

“Naomba dada Suzy ukalale chumbani kwako” Alibembeleza Ayubu.

Suzy alijikohoza kisha akazungumza kwa sauti iliyokuwa imejaa jaza na hasira.

“Kwanini hutaki nilale hapa?”

“Sio kitu kizuri” alijibu Ayubu kwa ufupi.

“Mimi ni nani yako?”

“Wewe ni dada yangu”

“Sasa kwanini unaogopa kulala na mimi wakati ni dada yako?”

“Mmm!..aaah!...” Ayubu alijikuta amekosa neno la kuzungumza.

“Nini sasa! kama mimi ni dada yako unahofia nini?”

“Basi wewe lala hapo mimi nitalala chini” alisema Ayubu baada ya kushindwa kumshawishi mrembo yule kwenda kulala chumbani kwake.

“Vyovyote utakavyofanya. Ukipenda hata kwenye kabati we lala tu” alijibu Suzy huku akijipapasa kwenye kifua chake.

Ayubu alichukua godoro lililokuwa juu ya kabati na kulitandika chini kisha akatoka na kuelekea sebleni. Mambo aliyokuwa akifanyiwa na Suzy yalikuwa yamekwisha mchosha. Alitamani wazazi wa Suzy wangerejea hata usiku ule ili vituko vile angalau vipungue. Alikaa kwenye kochi na kuwasha runinga. Haikuwa lengo lake kutazama runinga usiku ule lakini ilimbidi kufanya vile ili kumuepuka ibilisi aliyekuwa amemvaa Suzy.

Siku iliyofuata ilikuwa ni Jumamosi, Ayubu alijikuta amelala palepale sebleni. Alijiinua kutoka kwenye kochi na kwenda chumbani kwake kwa lengo la kumuamsha Suzy akalale chumbani kwake, lakini alikutana naye mlangoni. Suzy alimtazama Ayubu kwa jicho la hasira kiasi cha kumfanya Ayubu kupatwa na hofu.

“Habari za asubuhi dada Suzy” Ayubu alimsalimia binti yule kwa hofu kidogo.

“Mbaya” Suzy alijibu kwa mkato

“Vipi unaumwa?”

“Hivi Ayubu unadhani mimi sina moyo?”

“Kwanini unasema hivyo dada Suzy?”

“Hivi utanitesa hadi lini?”

“Bado sijakuelewa Suzy”

“Sikia Ayubu. Kumbuka kuwa mimi na wewe sio ndugu” alizungumza Suzy kwa msisitizo.

“Hapana dada Suzy usiseme hivyo, wewe ni ndugu yangu”

“Mmm! Wewe unaitwa nani?”

“Ayubu”

“Ayubu nani?”


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG