Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

MESSAGE YA FUNDI UMEME - 3

   


Chombezo : Message Ya Fundi Umeme 

Sehemu Ya Tatu (3)


“Lakini nini?”

“Unajua nakuheshimu sana shemeji” Undrea alizungumza kwa sauti iliyokuwa imejaa wasiwasi.

“Kama kweli unaniheshimu mbona umenitamani?” nikamuuliza kwa kumsushua.

“Hapana shem siwezi kukutamani bwanaa” alizungumza Undrea kwa sauti ya kukata kata.

“Haya kama kweli haujanitamani, simama wima”nikazungumza kwa msisitizo.

Maneno yangu yale yalimfanya kijana wawatu ajisikie aibu. Hakupenda mimi nibaini kama alikuwa ameharibikiwa.

“Basi shemu ngoja mi niende nitarudi baadae kufuata vyombo” alizungumza Undrea huku akivuta miguu yake kutaka kuondoka.

Nilivuta hatua ndefu ndefu na kwenda kusimama mbele yake huku nikiwa nimerembua macho yangu na mkono mmoja ukipandisha ile night dress niliyokuwa nimeivaa kwamtindo wa kujipapasa na kupelekea sehemu kubwa ya paja langu la mguu wa kushoto kuonekana.

Nilimshuhudia Undrea akinikodolea macho kwenye paja langu nililokuwa nimelifunua na kumeza funda la mate. Nilimsogelea taratiiibu na kumshika mkono mmoja kiunoni na mwengine nikawa napapasa kifua cha kijana yule taratiibu. Nilifanikiwa kumkamata mlinzi wa shamba lake la zabibu ambaye alikuwa amevimba kwa hasira kwa kutumia mkono wangu ule uliokuwa kiunoni mwake.

“Oooh Shem…shemu wewe! assscccss!” Undrea alitoa miguno ya aina yake kutokana na kitendo nilichomfanyia.

Nilimvutia kwenye kochi. Masikini kumbe alikuwa akiitamani sana nafasi ile kijana wa watu. Alikuja kiulaini na kudondokea juu ya mwili wangu uliokuwa umefunikwa kwa nguo yangu ya kulalia iliyokuwa na kitambaa laini cheupe.

“Ooh shemu uta…uta..utaharibu” masikini kijana wawatu alikuwa akilalamika huku akiishiwa nguvu.

Nilichokibaini ni kwamba kulikuwa na utofauti mkubwa kati ya mume wangu Magesa na kale kakijana kauza chipsi. Yaani mume wangu yeye alikuwa akikomaa na kuwa ngangari wakati wa maandalizi ya mechi, sasa yule Undrea nilikuwa namuona akilegea na kuwa kama vile mgonjwa wa degedege. Sijui pengine ndiyo staili yake nay eye katika kuhakikisha anapambana na adui wake katika mechi hiyo.

Kila nilipokuwa nikijaribu kupita zile kona nilizokuwa nimezoea kupitishwa na Magesa, kijana yule Undrea alizidi kuchanganyikiwa na kulegea zaidi huku akilala mika kimahaba. Nikasema nisipokuwa makini leo lazima kijana wawatu anifie humu ndani.

Ndugu msomaji huwezi amini nilichokuwa nimekutana nacho mwenzenu mie. Kumbe kijana wawatu hakuwahi kucheza mechi kubwa tangu amezaliwa. Alikuwa amezoea vimechi mechi vya mchangani. Alikuwa akipiga kelele kama mwehu huku akicheka cheka utafikiri mtoto wa kike. Nilipojaribu kuchagua nyanyachungu hapo ndipo mchezo ulipoishia.

“We Undrea…” nikaita kwa mshangao.

“Mnnh”

“Vipi...?”

“Dah shem..”

“Nini..”

“Aisee…”

“Hebu zungumza Undrea mbona sikuelewi?”

“Aisee wewe ni gari kubwa..” alizungumza kijana yule huku akionekana kukata tamaa

“Kwahiyo unataka kuniambia nini?” nikahoji kwa mshangao na dharau.

“Mume wako Magesa sio mtu wa kawaida kabisa asee. Kumbe yule jamaa ni noma!” alizunguma Undrea huku akijiinua kutaka kuondoka.

“Wewe hebu ngoja kwanza, unakwenda wapi kuja hapa!” nikazungumza na kumdaka mkono kumzuia asiondoke.




“Shemu mimi mziki umenishinda” alizungumza kijana yule kwa sauti ya chini.

“Kwahiyo unataka kusema umeshamaliza?” nikahoji kwa mshangao.

Undrea aliitika kwa kichwa kuashiria kuwa kwa upande wake mchezo ulikuwa umekwisha.

Nilishangazwa sana na tukio lile mwenzenu mimi. Hivi inawezekanaje mechi iishe kabla hata ya mchezo kuanza. Sijui pengine ni ushamba wangu au kutokana na mazoea niliyokuwa nimeyazoea kwa mume wangu Magesa. Kwakweli nikajikuta nimechoka hoi pasipo kufanya kazi yoyote

Mtoto wa kike payo likanishuka na kujikuta nimetulia kwenye kochi nikimkodolea macho Undrea akijiinua na kukusanya vyombo vyake na kuondoka akiniachia uchovu na ugonjwa wa huba.

Ni afadhali uendelee kuishi na mwanaume mzinzi kuliko kukutana na kituko kama kile nilichokivamia mwenzenu mie.

****

Ndoa ni kitu kizuri na kitamu sana jamani lakini wakati mwingine inaweza kumfanya mtu atamani kupotea hapa ulimwenguni, ama afe halafu azaliwe tena kama kiumbe mwengine mbali na binadamu.

Magesa alikuwa ni miongoni mwa wale watu ambao walikuwa wakisumbuliwa na kuteseka kwasababu ya maisha ya ndoa. Yote hayo ni mimi Priscaria ambaye nilimsababishia changamoto zote hizo. Hakuweza kufahamu ni kitu gani ambacho kilikuwa kimenifanya nibadilike kiasi kile na kuwa kama shetani. Lakini ukweli utabaki pale pale kuwa ile meseji yake aliyokuwa ametumiwa na FUNDI UMEME wake ndiyo chanzo cha yote haya.

Sio mimi tu ambaye nilikuwa nikimchanganya Magesa jamani, tafadhari msinifikirie vibaya na kunichukia bureee! Hata kazini kwake pia kulichangia. Walimpa taarifa kuwa alitakiwa kuendelea kufanya kazi kwa muda wa wiki tatu zaidi. Jamani kuna watu wana roho mbaya! laiti wange fahamu kuwa mtu yule alikuwa na matatizo ya kifamilia wala wasinge endelea kumbakiza pale jijini Arusha.

Akiwa ameketi ofisini mwake huku kichwa amegilaza juu ya meza. Mlio wa simu ya mezani ulimgutusha. Alipo pokea alisikia sauti ya secretary wake akimfahamisha kuwa kulikuwa na mgeni wake anahitaji kuonana naye. Pasipo kipingamizi wala kuuliza jina la mgeni huyo, alimruhusu aingie. Macho yake hayakuweza kuamini pale alipomuona mgeni mwenyewe.

“Yusrah!” Magesa alihamaki.

“Yes Boss Frank”

“Umekujuaje hapa?” Magesa akahoji huku akiwa bado kwenye hali ya mshangao.

“Ah! si unajua tena, siku zote mtaka cha uvunguni…..” Yusrah alizungumza huku akitembea kuelekea pale alipokuwa ameketi Magesa.

“Karibu kiti hicho hapo” Magesa alizungumza huku akimuoneshea mahali pa kuketi. Hata hivyo Yusra alizidi kusonga mbele hadi pale alipoketi mume wangu.

“Chei chei Boss” Yusra alitoa salamu huku akimshika kidevu Magesa na kumpiga busu la shingoni.

Kwa kuwa Magesa alikuwa hakujiandaa kufanyiwa tukio kama lile alishituka hasa pale alipopigwa busu na mrembo yule mwenye asili ya kiafrika na kiarabu.

“Chei chei Yusrah” Magesa naye alijibu salamu ile huku akitoa tabasamu la kuficha kama vile alikuwa akijilazimisha.

“Nimekuja na jambo zuuuri sana, ambalo najua tu utalipenda” Yusrah alizungumza huku akielekea kwenye kiti cha kukalia wageni.

Magesa akatulia kimya akimsikiliza mgeni wake ambaye hakumtarajia.

“Enhe kwanza niambie mkeo anasemaje” Yusra alihoji baada ya kuketi.

“Ah achana naye!” Magesa alijibu kwa mkato huku akionekana hakuwa tayari kuzungumza habari zangu.

“Hapana Frank, lengo langu mimi ni kukusaidia” alizungumza Yusra kwa sauti ya upendo.

“Utanisaidiaje?”

“Siwezi kujua hadi nitakapo lifahamu tatizo lenyeweu”

“Lakini Yusra, hivi ni kwanini umenga’nga’nia kuifahamu familia yangu kiasi hicho?” Magesa alihoji.

“Kwasababu nakupenda Frank” alizungumza Yusra kwa sauti ya upendo.

“Kwanini umenizoea kiasi hicho?”

“Nimekwambia kwasababu nakupenda na nataka kukusaidia” alisema Yusra.

“Kwani nimekwambia nina tatizo?”

“Mficha maradhi, kifo humuumbua Magesa. Tafadhali naomba nikusaidie” Yusra alizungumza kwa kubembeleza.

“Kwa ufupi ni kwamba mke wangu amebadilika” Magesa alizungumza kwa uchungu kutoka ndani ya moyo wake baada ya kuhisi pengine Yusra alikuwa kweli anataka kumsaidia japo kwa mawazo tu.

“Amebadilika kivipi?”

“Kitabia”

“Lakini unakumbuka nilivyo kwambia kuwa ‘mke mkeo ukiwepo…”

“Unasemaje?”

“Huyo atakuwa amekwisha pata wajanja wa mjini wewe”

“Stop Yusra! Unaweza kuzungumza kilicho kuleta?” Magesa alibadilika ghafla baada ya kusikia kauli za Yusra hazikuwa na usalama katika ndoa yake.

“Ndio hicho” Yusra alisisitiza.

“Hujui kama hapa ni ofisini?”

“Najua, lakini….’

“Hakuna cha lakini, naomba uondoke” Magesa alizungumza kwa sauti ya msisitizo huku akigonga meza kwa hasira.

Jamani nyie kumbe nilikuwa napendwa mie mwenzenu. Yaani ukitaka ubaya na Magesa basi zungumza lolote lile baya kuhusiana na mimi, mbona utatolewa macho.

“Lakini ungenisikiliza japo kidogo Frank” Yusra alijaribu kujitetea.

“Inamaana huelewi? au unataka nikutoe na walinzi?” Magesa alizungumza kwa kufoka na kumfanya Yusrah mtoto wa watu wa kimanga kuishiwa na pozi.

“Sawa naondoka, Ila elewa kuwa dawa ya mkeo mimi ninayo” Yusra alizungumza kwa sauti ya upole huku akifungua mlango na kutoka.

Magesa aliegemea kiti chake na kutoa pumzi ndefu mithili ya mtu aliye toka kufanya kazi nzito. Alijikuta akimchukia sana Yusrah kwa kitendo cha kumganda heti kwasababu tu wamekutana kwenya basi. Magesa aliachia msonyo mrefu kisha akafumba macho pale kwenye kiti chake.

****

Waswahili wanakwambia, dawa ya jeuri ni kiburi. Muda wa Magesa kuwa Arusha kikazi ulikuwa umekwisha lakini aliamua kuongeza wiki nyingine tatu. Nilipompigia simu aliniambia heti ofisi ndiyo ilikuwa imempangia hivyo. Haya bwana sasa mimi ninge fanya nini wakati mtu mwenyewe ndio alikuwa amekwisha amua. Nikasema kuwa kama yeye alikuwa anaendelea kuponda raha na Fundi umeme wake huko, namimi nitaendelea kuponda raha na Undrea muuza chipsi wangu huku hata kama alikua ni mbovu kenye mambo yetu.

Niliamka asubuhi nikiwa na nguvu nyingi kwa sababu usiku uliopita sikutoka wala kufanya kazi yoyote ngumu. Hali ya unyonge sikuwa nayo kabisa pamoja na kwamba mume wangu aliamua kunikomesha. Kwa nguvu zote nilifanya usafi wa nyumbani kwangu. Baada ya hapo nilipata kifungua kinywa kisha nikatoka na kwenda mjini Kariakoo kung’aza macho.

Nikiwa mtaa wa Kongo mida ya saa sita hivi mchana nilikutana na Abunaya kijana ambaye nilisoma naye darasa moja huko Korokoroni mkoani Tanga. Kwa kweli ni miaka mingi sana ilikuwa imepita tangu tulipoachana mara ya mwisho. Kipindi hicho nilikuwa nampenda sana kijna yule lakini nilishindwa kumwambia kutokana na mila na desturi zetu za Afrika. Nikabaki nikiumia moyoni hadi tukamaliza masomo na kusambaratika. Hatimaye kijana huyo siku hiyo alikuwa mbele ya macho yangu.

“We Abunaya ndio umekuwa mtu mzima hivyo” nilizungumza kwa kuhamaki.

“Jamani Priscaria” Kijana yule aliyekuwa na urefu wa wastani na weupe wa kunyunyizia alitanua mikono yake tayari kwa kunikumbatia. Ama kweli watu wanabadilika jamani. Enzi zile tulipokuwa shuleni kijana huyu alikuwa na nyodo kiasi cha kuto kuzoewa na msichana yeyote yule. Basi mtoto wa kike nikaingia kati kati ya mikono ile. Joto nililokuwa nikilipata kwenye kifua cha kijana yule nilikuwa sitamani kuchomoka. Alinipiga busu la shingoni na kunisababishia msisimko mwilini na damu kuongezeka kasi kwenye mishipa yake. Niliweza kuyasikia mapigo ya moyo wake yaliyokuwa yakienda kama mshale wa saa, Kwakweli nilijihisi kama vile nilikuwa kwenye baraza la peponi. Hata hivyo kila lenye mwanzo huwa halikosi mwisho. Kijana Abunaya alinichomoa kutoka pale kifuani kwake.

“We Prisca mbona umezidi kuwa mrembo hivyo?” Mnh Jamani kijana yule alianza kuzungumza maneno ambayo yalinifanya kushituka moyoni. Nilifurahi sana kugundua kuwa uzuri wangu umeweza kubainika kwenye mboni ya macho ya kijana yule mtanashati na aliyekuwa akionekana kuwa mstaarabu.

“Jamani Abunaya wewe, haya asante?” nilizungumza huku nikitabasamu kwa ile aibu yangu ya bandia.

“Mnh! kwa hali hiyo jamani….”

“Kitu gani jamani Abunaya?”

“Naona kama vile tunatiana majaribuni”

“Wacha masihara Abunaya, mbona kawaida tu”

“Sio utani Prisca, kwa kweli shemeji yangu anafaidi sana” alizungumza Abunaya huku akiwa amenikazia macho kwenye hipsi zangu zilizokuwa zimetanuka kwa uchokozi.

“Shemeji atoke wapi?” Nilimjibu huku nikirembua macho yangu malegevu na kujinyonga nyonga mwili wangu pasipo kujali kama pale nilikuwa hadharani.

Jibu langu lile lilimfanya Abunaya anitazame kwa makini usoni na kuachia tabasamu la matumaini.

“Samahani kama huto jali, naomba tuingie hapo tupate juice” alizungumza Abunaya huku akinionesha restaurant iliyokuwa jirani na pale.

“Usijali Abunaya, twende tu” nilijibu huku nikianza kuvuta hatua kuelekea kenye ile restaurant aliyoionesha Abunaya.

Tuliketi kwenye meza moja iliyokuwepo nje ya restaurant ile na kuagiza juice. Abunaya aliinua macho yake na kunitazama kwa sekunde kadhaa kisha akameza funda la mate.

“Unataka kunambia hujaolewa?” Alihoji Abunaya baada ya kimya kidogo kupita bila kuzungumza neno lolote.

“Nimeolewa, lakini ni kama sikuolewa” nikaeleza mtoto wa kike.

“Kivipi mbona sikuelewi?”

“Nimetelekezwa” nikazungumza huku macho yakiwa makavu mtoto wa kike.

“He kwanini?” Abunaya alihoji kwa mshangao. Hakuweza kuamini kama ingewezekana mwanaume rijali aweze kumtelekeza mwanamke mrembo kama mimi.

“Wanaume watu wabaya sana. Hakuna sababu yoyote ile” nilieleza huku nikihisi yale maumivu yangu ya kusalitiwa yakirejea upya ndani ya kifua changu.

“Duh pole sana, hajui kama wenzie nafasi tunaililia hii” alizungumza Abunaya kwa utani.

“Ah ndo hivyo tena…nipo nipo tu” nilieleza mtoto wa kike kwa kujibebisha kwa kijana yule.

“Kwahiyo nafasi ipo wazi?” alihoji Abunaya huku akiuma uma midomo yake.

“Wewe tu” Nilijibu huku nikijifanya nimejawa na aibu.

Sasa unadhani ningesema nini wakati mume wangu mwenyewe alikuwa haeleweki. Kila kukicha mitihani, mara Fundi umeme, mara Abiria, mara sijui nani. Hata hivyo ukizingatia zaidi ni kwamba jamaa niliyekutana naye siku hiyo nilikuwa na usongo naye tokea enzi hizo tulipokuwa shuleni. Hivyo safari hii sikutaka kuipoteza tena nafasi ile. Ukizingatia ni kwamba nilikuwa likizo kindoa kwa muda wa siku zisizo fahamika.

Nakwambia nilijishongondoa mtoto wa kike kwa kijana wa watu hadi mwenyewe akaingia laini.

“Prisca…” aliita Abunaya huku akinikodolea macho.

“Abee..” niliitika kwa heshima.

“Hivi huyo jamaa yako ana akili timamu kweli?” alihoji kijana Abunaya.

“Sijui..Nafikiri anazo akali timamu tu”

“Sidhani”

“Sasa tusemeje jamani”

“Mimi nafikiri huyo jamaa yako ni kiazi”

“Mnh Abunaya wewe!”

“Anawezaje kumuacha mwanamke mrembo na mwenye mvuto kama wewe?”alizungumza Abunaya kwa mshangao.

“Aah ningekuwa mrembo nisingeachika bwana Abunaya?” nilizungumza huku

nikijichekesha hekesha.

“Si ndio maana nakwambia jamaa yako ni kiazi” Abunaya alizungumza kwa msisitizo kumpondea mume wangu Magesa.

“Mnha Abunaya una maneno wewe!”

“Nikwambie kitu Prisca…”

“Nakusikiliza we ongea tu chochote”

“Naomba hiyo chance” Abunaya alizungumza kwa umakini wa hali ya juu kuashiria kumaanisha kile alichokuwa anakizungumza.

“Chance gani jamani wewe Abunaya” nilizungumza huku nikicheka cheka na shingo nikiinyonga nyonga kwa aibu.

“Uruhusu moyo wangu ukupende. Nitakupatia mapenzi motomoto ya kule kwetu Songea” alizungumza Abunaya pasipo kutabasamu.

“Mnh! Abunaya wewe, acha utani basi”

“Sio utani Prisca, naomba unipe nafasi mtoto mzuri” masikini kijana wawatu alilalama utafikiri sijui alikuwa anaomba nini.

“Sasa nitakupaje hiyo nafasi wakati mwenzio nimeolewa tayari” nikajaribu kueleza ukweli ili hata ikitokea huko baadae asije akalaumu hakuambiwa ukweli.

“Hivi kama mtu amekutelekeza bado unasema umeolewa tu?”

“Hata kama amenitelekeza bado ni mume wangu kisheria” nikazungumza na

kujifanya naweka kipingamizi kidogo.

“Sasa sikiliza Prisca, naomba unipende japo kwa siku moja tu” alizungumza Abunaya

kwa msisitizo.

“Halafu nikishakupenda kwa siku moja ndio itakuwaje?” nikahoji kwa mshangao kidogo, nafikiri sikuwa nimemuelewa alikuwa na maana gani.

“Sikiliza Priscaria, tumia siku yako moja tu ushinde na mimi kama mume wako” alizungumza Abunaya kwa kujiamini.

Ukweli ni kwamba nilielewa jamaa alikuwa amezimika na mimi na alikuwa anatamani kupata mzigo.

“Halafu..?” nikahoji huku nikijifanya sikuwa nimekielewa alichokuwa anakimaanisha.

“Yani siku moja tu, itakufanya usahau kabisa machungu ya huyo basha wako” Abunaya alizungumza kwa mafumbo.

“Halafu baada ya hiyo siku moja narudi tena kwenye mateso yangu?” nikahoji utafiri kitoto kidogo.



“Hujanielewa Priscaria” alizungumza Abunaya.

“Kumbe?”

“Yani nitakachokufanyia ndani ya siku hiyo, hautokaa umkumbuke tena mume wako katika maisha yako yote” alizungumza Abunaya kwa kujiamini.

“Mnh..kweli au ndio sound?” nikaguna na kuhoji baada ya kusikia maneno yale kutoka kwa Abunaya.

“Sasa kama nikiweza kumiliki mtoto mzuri kama wewe japo kwa siku moja kwanini nivunge” Abunaya alieleza.

“Jamani Abunaya wewe!” nikazungumza huku nikijichekesha hekesha kwa ile aibu yangu ya kinafki.

“Kwahiyo vipi, umekubali?” Abunaya alihoji huku akijaribu kuniangalia kwenye sura ambayo kwa wakati ule nilikuwa nikiinamisha chini kwa aibu.

“Sijui wewe mimi sina shida” nikazungumza kwa sauti ya chini ambayo ilikuwa ya kubania zaidi kuliko mwanzo wa mazungumzo yale.

“Okay..leo una ishu gani?”

“Hamna ishu yoyote nipo tu natanga tanga mshahara kuchoka” nilizungumza kwa kujirahisisha kwa Abunaya.

“Good, kwasababu na mimi leo sina ishu ya kivile hapa town, unaonaje tukamalizia siku hii ya leo pamoja?” alihoji Abunaya huku akiwa haamini kwa kile kilichokuwa kikimtokea siku hiyo.

“Wewe tu, mimi sina usemi” nikazungumza kwa kudeka mtoto wa kike.

Abunaya aliinua macho yake na kunitazama usoni huku akiuma uma midomo yake kuashiria ushindi. Alishusha macho yake na kunitazama kwa matamanio kuanzia miguuni na kunipandisha polepole hadi kwenye nywele.

“Hakika wewe ni mzuri Priscaria” alizungumza Abunaya kwa sauti ya kubembeleza.

“Asante…”

Abunaya hakuzungumza neon lolote zaidi ya kunishika mkono na kuniongoza kuelekea kwenye kituo cha bajaji.

Jamani naombeni tusilaumiane, tena sitaki kulaumiwa naombeni mniache kabisaa. Msifikiri yale mambo aliyokuwa akinifanyia mume wangu Magesa mimi yalikuwa yameninogea. Kama yeye alimwaga ugali na mimi nimeamua kumwaga mboga sasa, liwalo na liwe. Kama noma na iwe noma ngoma droo.

*****

Kauli ya Yusra kuwa alikuwa na dawa ya kunituliza mapepe ilimfanya mume wangu kushawishika na kumtafuta ili aifahamu hiyo dawa na kama ikiwezekana basi amsaidie ili aweze kuokoa ndoa yake. Mume wangu Magesa alikuwa akinipenda sna na nafikiri hakuwa tayari kuona ndoa yake ikisambaratika kwa hali yoyote ile. Alicho fanya ni kupanga appoint menti na msichana yule kwenye hoteli moja iliyokuwa ikifahamika kwa jina la MOUNTAIN LUNCH HOTEL iliyokuwepo pembeni kidogo mwa jiji lile la Arusha.

Kwakuwa Magesa alikuwa na hamasa kubwa ya kuleta mabadiliko kwenye ndoa yake alifika hotelini pale mapema sana. Alichagua sehemu moja ambayo ilionekana ingefaa sana kwa mazungumzo yao. Kwakuwa hakuwa mnywaji wa pombe aliagiza juisi na kunywa taratibu huku akiangalia saa yake ya mkononi kila mara.

Baada ya dakika kadhaa alitokea mtu kwa nyuma yake na kumziba macho. Hakupata taabu kumgundua mtu huyo kwasababu ndiye aliyekuwa akimsubiri maeneo yale.

“Mnh! Yusra” Magesa alitaja jina lile kwa kujiamini

“Nop”

“Its you”

“Wrong”

“Then who are you?”

“Otea”

“Yusra”

“Mother fucker!” Mtu yule aliyekuwa bado amemziba macho Magesa alisikika akitoa matusi kwa sauti ya hasira.

“What?” Magesa alishituka baada ya kusikia matusi yakitoka mdomoni mwa mtu aliyekuwa amemziba macho. Aliishika ile mikono na kuitoa kwa nguvu kisha akamgeukia. Alimuona msichana msichana ambaye alikuwa ni mgeni machoni mwake. Hata yule msichana naye alishituka sana baada ya mume wangu kumgeukia na kumuangalia usoni.

“Wewe ni nani?” Magesa akahoji kwa mashaka.

“Ah….an….samahani kaka” Msichana yule alionekana kujawa na woga kiasi cha kujikuta akishindwa kuzungumza.

“Unanifahamu mimi?” Magesa aliendelea kuhoji kwa wasiwasi.

“Sikufahamu ila….ila nilikuwa nime kufananisha” msichana yule alieleza kwa hofu.

“Umenifananisha na nani”

“Mpenzi wangu amevaa kama ulivyo vaa wewe, kwahiyo nilijua ni yeye. Alisema yule dada kwa sauti ya upole.

Wakati mume wangu alipokuwa anaendelea kuzungumza na msichana yule alifika jamaa liyekuwa amevalia nguo kama alizokuwa amevaa Magesa wangu. Jamaa yule aliyekuwa amejazia kifua sawa kabisa na kifua cha Magesa, alifika na kumkunja mume wangu shingoni. Magesa akazidi kushangazwa na matukio yale ya ajabu ajabu.

“Unafanya nini na mpenzi wangu?” Jamaa yule alihoji kwa hasira.

Kabla Magesa hajajibu kitu jamaa yule alirusha ngumi na kumpiga shavuni mume wangu. Magesa alishika shavu lake na kumtazama jamaa yule kwa jicho la kumpa onyo kwa kitendo alicho kifanya.

“No Benson usifanye hivyo ni mimi ndiye niliyekosea” Kale kasichana kalikokuwa kamemziba macho Magesa kalizungumza huku kakilia.

Jamaa yule aliyetambulika kwa jina moja la Benson alirusha kofi na kutua kwenye shavu la msichana yule aliyesemekana kuwa ni mpenzi wake. Masikini kasichana kale kalipepesuka na kwenda kudondokea meza ya vinywaji vya watu.

Jamaa alimrudia Magesa na kumpiga teke ambalo lilimpeleka chini mume wangu kama gogo la mnazi uliokuwa unakatwa. Haikufahamika Magesa namna alivyo amka kutoka pale chini. Kilichotokea ni kwamba alimvaa jamaa yule na kumtandika ngumi tatu mfurulizo za usoni. Jamaa alipepesuka mara mbili kisha akasimama sawa sawa. Alikunja ngumi na kuanza kumsogelea Magesa taratibu kwa mtindo wa kumzunguuka. Mume wangu mwenyewe hakuwa amekunja ngumi wala nini bali alitulia na kumtazama jinsi jamaa yule alivyo kuwa akijishebedua mbele za watu.

Jamaa alimfuata Magesa kwa kasi na kurusha ngumi kwa nguvu kuulenga uso wa Magesa. Lilikuwa ni jambo la haraka sana ambapo Magesa aliikwepa ile ngumi na kurusha ya kwake iliyokwenda kutua kwenye pua ya jamaa yule. Jamaa alipepesuka na kudondoka chini kama gunia la mkaa. Aliinua shingo na kumtazama Magesa ambaye alikuwa akikung’uta mikono yake kama vile alikuwa ameshika kitu kilichokuwa na vumbi. Baada ya kumuona jamaa ametuliza mapepe pale chini pasipo kuinuka tena Magesa aliamua kuondoka zake taratiibu kama sio yeye aliyeshiriki katika pambano lile.

Magesa alipofika mlangoni alikutana na Yusrah akiingia kwa mwendo wa haraka utafikiri alikuwa anawahi mazishi ya mtu wake wakaribu sana.

“Jamani Frank, samahani kwa kuchelewa” Yusrah alizungumza huku akimshika Magesa kwenye mabega.

“Usijali”

“Vipi mbona unaonekana haupo sawa?”

“Naomba tukutane siku nyingine na mahali pengine hapa hapafai tena” Magesa alizungumza huku akivuta hatua kutoka nje. Yusrah alimdaka mkono kumzuia asiondoke.

“Kwani kumetokea nini Frank?” Yusra alihoji kwa wasiwasi.

“Naomba tuondoke Yusra” Magesa alizungumza kwa kutoa amri baada ya kumuona Yusrah anakuwa mgumu kumuelewa. Kwakuwa halikuwa jambo la hiyari, Yusrah aliamua kufanya vile alivyokuwa anataka Magesa.

*****

Nilikaa na kutafakari aina ya maisha ambayo nilikuwa ninaishi kwa wakati ule. Kiukweli nilibaini kuwa hayakuwa maisha mema hata kidogo. Roho ya imani kwa mume wangu ilianza kunijia na kutamani niishi naye kama zamani. Nikapanga nimfuate huko huko Arusha nikazungumze naye ili tumalize mgogoro wetu na kuishi kama zamani.

Nilichukua simu yangu na kumpigia shoga yangu Fatuma ili nimfahamishe juu ya ule uamuzi wangu nilioufikia. Lakini kwa bahati mbaya simu yake ilikuwa haipatikani hewani. Wazo lililonijia harakaharaka ni kumfuata nyumabani kwake Tabata.

Nilipofika nyumbani kwa Fatuma nilifunguliwa mlango na Shemeji Hashimu.

“Waaaooo! mrembo huyo!” Shemeji Hashimu alinipokea kwa uchangamfu wa hali ya juu ambao ulizidi kawaida yake. Tulikumbatiana huku kila mmoja akionekana kufurahi kukutana na mwenzie. kitu cha ajabu ni pale nilipotaka kutoka mikononi mwa shemeji Hashimu. Alikaza mikono yake na kunikumbatia kwa nguvu. Nilichukizwa sana na kitendo kile, hasa ukizingatia nilikuwa nimeamua kubadilika kitabia.

“Jamani shemeji” nilizungumza kwa chuki na kumsukuma kwanguvu hadi akaniachilia.

“Dah! mtoto una joto tamu wewe” Shemeji Hashimu alizungumza huku akiiramba midomo yake kwa ulimi utafikiri mjusi aliyeona kumbi kumbi. Nilisonya kisha nikamtandika swali.

“Fatuma yupo?”

“Karibu basi kwanza ukae mbona juu juu mrembo?”

“Nijibu, Fatuma yupo?”

“Ndio yupo” alinijibu kwa mkato

“Yuko wapi?”

“Kaa hapo nikuitie” shemu hashimu alinambia huku akielekea chumbani kwake. Nilikwenda kuketi kwenye kochi ili kumsubiri shoga yangu huyo. Baada ya muda kidogo shemeji Hashimu alirejea huku akiwa ameshika gazeti mkononi mwake.

“Ok anakuja shoga yako” Aliniambia huku akiketi kwenye sofa ambalo alizoea kulikalia siku zote. Kama ilivyokuwa kawaida yake alianza kunitumbulia macho huku akitoa tabasamu. Nikajikausha kama vile nilikuwa simuoni.

“Vipi unapendelea kusoma gazeti la udaku” Alihoji huku akifunua gazeti lile.

“Sio sana” Nilimjibu kwa mkato ili asiendelee kunisemesha.

“Lakini la leo lina habari nyeti sana”

“Usijali shemeji, nashukuru kwa ukarimu wako” Niliendelea kutoa majibu ambayo nilihisi yangemkatisha tamaa ya kuendelea kuzungumza na mimi.

“Zaidi ya kuwa ni habari nyeti, pia zinakuhusu” Alizungumza maneno ambayo yalinifanya moyo wangu ushituke na kumgeukia shemeji hashimu.

“Unasemaje?”

“Una hiyari usome ama uache” shemeji Hashimu alizungumza huku akiliweka mezani lile gazeti. Nililitazama kwa sekunde kadhaa kama vile nilikuwa nikijishauri nilichukue ama niliache. Nikalinyakuwa kama vile kipanga anavyo nyakua vifaranga vya kuku. Nilipo tazama juu tu ya gazeti lile nikaona kichwa kilichobeba gazeti lile kikirembwa kwa picha zilizonifanya nianze kutetemeka.

“ALIYE FUMANIA APIGWA HADI KUZIMA, Kimada chupu chupu afe kwa kutetea mchepuko” Uk 2.

Picha ambazo zilibeba kichwa kile zilikuwa zikimuonesha mume wangu Magesa akiwa amekamatwa shingoni na mwanaume mwengine. Picha nyingine zilimuonesha huyo msichana ambaye alikuwa chanzo cha mtafaruku huwo. Haraka haraka nilifunua ndani ili kupata habari kamili kuhusiana na kashfa ile ambayo alikuwa amekumbwa nayo mume wangu.

Ni watu wawili walioonekana kuwa na miili iliyojazia kwenye hoteli maarufu (Mountain Lunch Hotel) jijini Arusha jana. Mabaunsa hao ambao majina yao chanzo chetu kimeshindwa kuyapata, Wamejikuta katika pambano la kutandikana masumbwi baada ya msichana anayesemekana kuwa na uhusiano nao wote wawili kuwagonganisha. Chanzo chetu kimeeleza kuwa…..” Kabla hata sijamalizia habari ile nilijikuta nikiishiwa nguvu na kuanza kumwaga machozi. Shemeji Hashimu alinisogelea na kuanza kunibembeleza.

“Nyamaza shemeji yangu usilie tafadhali”

“Inauma shemu, inauma kwanini ananifanyia hivi Magesa?” Nilizungumza huku nikilia kwa kwikwi.

“Najua inauma shemeji yangu, lakini inabidi ukubaliane na hali”

“Ona sasa, hii si aibu hii?”

“Kubwa sana, ila usijali shemeji mimi nitakuwa na wewe bega kwa bega wala sito kutupa” Shemeji Hashimu alizungumza kwa sauti ya kunibembeleza huku akinivuta na kukikumbatia kichwa changu kwenye kifua chake.

Sikuweza kubisha kwasababu kwa wakati ule yeye ndiye aliyekuwa mfariji wangu. Niliizunguusha mikono yangu kwenye mgongo wake na kumkumbatia huku nikiendelea kulia kwa uchungu.

“Basi Prisca usilie mama”

“Shemu kwanini mapenzi yananitesa mimi?”

“Usijali mtoto mzuri haya yote ni mapito yataisha tu” shemeji Hashimu alizungumza huku akiniinua na kunikokota kuelekea chumbani ambako Fatuma alikuwepo. Sikugoma kutembea kwasababu nilifahamu kuwa alikuwa akinipeleka kwa rafikiyangu nikapate faraja zaidi. Cha ajabu ni kwamba, nilipofika Fatuma hakuwemo chumbani. Kutokana na hali niliyokuwa nayo nilikuwa mpole kwanza.

“Hebu jipumzishe hapo shemeji yangu” Alisema shemeji hashimu na kuniweka kitandani.

“Fatuma yuko wapi?” Nilihoji huku nikifuta machozi.

“Usijali shemeji, Fatuma ametoka maramoja. ila hato chelewa kurudi” Shemeji hashimu alizungumza kwa upole na ukarimu wa hali ya juu Kisha akataka kuondoka na kuniacha pekeyangu chumani. Kwa mbali nilianza kuuona wema wa shemeji Hashimu. Sikuwa nafahamu kama mwanaume yule alikuwa ni mkarimu kiasi kile.




*****

Waswahili wanakwambia siku zote mguu wenye kidonda ndio huo huo utakao jikwalia. Pamoja na kwamba Magesa alikuwa na vitu vingi kichwani mwake ambavyo vilikuwa vikimpotezea amani yake, bado kukatokea na jingine kubwa kuliko.

Alikuwa akipata taabu sana kupingana na nafsi yake ambayo ilikuwa ikimshawishi kunywa pombe ili apunguze msongo wa mawazo. Kwa nguvu za muumba kama yeye mwenyewe alivyo kuwa akiamini, aliweza kufanikiwa kupambana na hali ile.

Akiwa kwenye mgahawa mmoja mdogo uliokuwepo jirani na ofisini kwake kule jijini Arusha aliagiza juisi ya parachichi akawa anakunywa taratibu. Mawazo yalikuwa yakipishana na wakati mwingine kugongana ndani ya ubongo wake. Hakuwa amekaa tu mahali pale bali alikuwa akimsubiria Yusrah, binti wa kimanga aliye jitolea kumsaidia katika matatizo yake.

Akiwa amezama kwenye lindi la mawazo alijishitukia anazibwa machoni na mtu aliyetokea nyuma yake. Mapigo ya moyo wake yakaanza kumuenda mbio na hasira zikamjaa kifuani. Alikumbuka msala uliokuwa umemtokea siku iliyo pita chanzo chake kilikuwa ni kuzibwa macho na msichana wa mtu ambaye alikuwa amemfananisha na bwana wake. Magesa hakujisumbua kumuuliza wewe ni nani ama kutaja jina la mtu yoyote. Aliishika mikono ile na kuiondoa kwa nguvu. Alipogeuka alimkuta Yusrah amesimama nyuma yake.

“Oooph” alipumua kwanguvu huku akiegemea kiti alichokuwa amekalia.

“Vipi, mbona unapumua hivyo?” Yusra akahoji kwa mshangao.

“Dah! unajua uking’atwa na nyoka, hushituka uguswapo na jani” Mume wangu alizungumza huku akichomoa kitambaa cha jasho kutoka kwenye mfuko wa suruali na kujifuta usoni.

“Kwanini unasema hivyo jamani Frank?” Yusra alizungumza huku akivuta kiti na kuketi.

“Yaliyo nikuta jana kwa sababu ya mchezo huwo wa kuzibana macho sitaweza kuyasahau maishani mwangu” Alieleza Magesa kwa unyonge.

“Mnh, mbona unanitisha jamani?”

“Ah we achatu, yaani matatizo juu ya matatizo” alizungumza Magesa na kupeleka kiganja cha mkono na kupangusa uso wake kama vile alikuwa anajifuta vumbi usoni.

“Yepi tena Frank jamani?” Yusrah alihoji kwa kuhamaki.

Magesa hakuzungumza kitu bali alitoa lile gazeti na kumkabidhi Yusra pasipo kumtazama usoni.

“Ni kitu gani” Yusra alihoji kwa wasiwasi huku akipokea gazeti lile.

“We soma hapo juu” Magesa alizungumza huku mikono yake akiwa ameipishanisha kifuani mwake kama vile amefunga swala. Yusrah alifunua gazeti lile kwa pupa ili kufahamu kilichokuwa kimetokea.

“Mtume simama!” Yusra alijikuta akihamaki kwa sauti baada ya kuona kile kichwa cha habari pamoja na zile picha za fumanizi lililomhusu Magesa. Aliinua macho yake na kumtazama Magesa usoni. Hakuweza kuamini kwa kile kilichokuwepo ndani ya gazeti lile.

“Kwanini umefanya hivi Frank?” alihoji kwa mshangao Yusrah.

“Kwasababu ulichelewa kufika” Magesa alijibu kwa ufupi.

“Kwahiyo kuchelewa kwangu ndiko kumekufanya uvamie wanawake wa watu?” Yusrah alihoji kwa hasira.

“Si kama unavyo fikiria”

“Unataka kubisha nini sasa wakati picha hizi hapa zinaonekana” Yusra alizungumza hukua akilipiga gazeti mezani kwa hasira.

“Hebu tulia basi nikueleze hali halisi” Magesa alijaribu kumtuliza Yusrah kwa sauti ya upole.

“Unakatisha tamaa Frank. Kwa hali hiyo wacha mkeo akuchukie tu” Yusrah alizungumza kwa hasira na kusimama kutaka kuondoka. Magesa alisimama kwa mbele na kumzuia.

“Tafadhali Yusrah naomba unisikilize”

“Huna jipya Frank huna jipya Wewe ni mzigo wa misumari hubebeki” Yusra alizungumza na kuchomoka mikononi mwa Magesa kwa kasi ya ajabu.

Magesa akabakia amesimama akimuangalia Yusrah jinsi alivyokuwa akitokomea kwenye kundi la watu. Alikaa kwenye kiti na kupiga meza kwa hasira. Alijiona ni mtu mwenye mkosi hapa duniani. Aliokota lile gazeti na kulichana vipande viwili kwa hasira.

*****

Nilipoona kuwa shemeji Hashimu alikuwa anatoka nje na kuniacha chumbani pekeyangu, nilijisikia vibaya sana ndani ya moyo wangu. Kusema kweli niliutamani sana uwepo wake mahali pale kwa siku ile.

“Shemu” Nilimuita wakati akikaribia mlangoni. Aligeuka na kunitazama kwa makini kusikiliza nilichokuwa nimemuitia.

“Unaniacha peke yangu?” Nilihoji kwa sauti iliyokuwa ikitia huruma. Shemeji hakujibu kitu chochote bali alivuta hatua kurejea kitandani ambako nilikuwa nimeketi. Alinisogelea na kuweka mkono wake kwenye bega langu la kuume.

“Usiwaze shemeji tupo pamoja” alizungumza mwanaume yule kwa sauti ya upole na iliyokuwa imejaa upendo.

“Hivi shemeji na wewe unamfanyia hivi Fatuma?”

“Hapana, siwezi kufanya vitu vya ajabu kama hivi”

“Usifanye hivyo, anakupenda sana shoga yangu” Nilizungumza kwa uchungu huku nikimuonea wivu shoga yangu kwa kuwa na mwanaume mkarimu kiasi kile. Nikawaza endapo na mimi ningempata mwanaume kama yule shemeji Hashimu, ningefurahi sana na nisingethubutu kutoka nje ya ndoa.

“Shemeji” Niliita

“Nakusikiliza shemeji yangu”

“Kwakweli namuonea wivu sana shoga yangu” Nilijikuta nikizungumza maneno yenye utata pasipo kujitambua mtoto wa kike.

“Wivu wa nini jamani?”

“Mimi ningekuwa ndio yeye, ningefaidi sana” Nilizidi kutoa maneno ambayo yalionekana kumuweka utatani shemeji Hashimu. Nilimuona akikosa jibu na kushindwa kuzungumza kitu chochote. Alivuta pumzi ndefu na kuziachia.

“Yaani wewe ni mwanaume unaye eleweka. Kama mapenzi yangekuwa yanagawanyika, ungenipatia nusu” Maneno yote hayo niliyokuwa nikiyazungumza nilikuwa sielewi yalikokuwa yakitokea. Nafikiri ni baada ya kuoneshwa lile gazeti lililokuwa likimuonesha mume wangu Magesa amefumaniwa na mwanamke wa mtu. Niliumia sana ndugu msomaji, nafikiri hata akili yangu haikuwa saw, pengine ndiyomaana hata maneno niliyokuwa nikiyazungumza yalikuwa ni ya ajabu ajabu.

Magesa alinishika kwenye mashavu yangu kwa mikono yake yote miwili akawa akinitazama kwa macho ya huruma. Alinivuta kwake na kinipiga busu la utosini.

“Usijali Prisca, kama nilivyo kwambia kuwa siwezi kukutupa. Nitajitahidi kukufariji kwa kadri niwezavyo” Alisema shemeji hashimu kwa ile sauti yake iliyojaa huruma.

Nilimkumbatia kwanguvu shemeji yangu yule huku moyo wangu ukipata faraja. Kwa mara ya kwanza nilianza kupata ladha ya kifua cha shemeji Hashimu. Siku zote nilikuwa nikichukia sana kukumbatiwa naye, lakini siku hiyo mimi mwenyewe nilimkumbatia kujikuta nikifurahia joto la kifua chake.

“Asante sana shemeji yangu” Nilizungumza kwa sauti ya kudeka utafikiri nilikuwa nazungumza na Magesa.

Shemeji Hashimu aliponiachia alinipiga mabusu kwenye mashavu yangu na kumalizia busu moja la mdomoni. Nilijikuta nimeganda utafikiri nimepigwa na shoti ya umeme kutokana na lile busu la mdomoni alilonipiga shemeji Hashimu.

“Thank you” Nilijikuta nikitamka kwa sauti ya kunong’ona.

Shemeji alitaka kuniachia ili aondoke lakini nilimvuta shati hadi usawa wa uso wangu tukawa tunatazamana kama majogoo. Macho yangu malegevu niliyalegeza zaidi huku nikichezesha lipsi zangu zilizopambwa kwa lipstiki nyekundu.

“Vipi shemu uko sawa?” shemeji Hashimu alijifanya kuhoji.

Siku hiyo Hashimu alikuwa kama vile sio yeye aliyekuwa akiniangalia kwa matamanio siku zote. Siku hiyo shemeji yangu yule alikuwa ni mtakatifu kuliko wanaume wote ulimwenguni kiasi ambacho nikajikuta nikimuamini na kuvutiwa naye.

“Hivi ni kwanini Magesa ananitesa hivi?” nilihoji huku machozi yakinilenga lenga.

“Jamani shemeji mbona nimekwambia usiwe na wasiwasi, mimi nopo” alizungumza mwanaume wa watu kwa sauti ya kubembeleza.

“Hivi wanaume wote ndivyo mlivyo?” nikahoji kwa sauti ya kudeka.

“Hapana shemeji yangu, ni tabia ya mtu tu” Hashimu alieleza.

“Sasa kwanin Magesa amekuwa kati ya watu wenye tabia mbovu?” nikaendelea kulalamika mtoto wa kike.

“Ni watu washenzi tu, ukipata bahati mbaya ukakutana na mwanaume mshenzi basi andika umeumia” alieleza shemeji Hashimu.

“Kwahiyo na mimi nimeumia?”

“Kama mume wako ni miongoni mwao, basi ni lazima utakuwa umeumia” shemeji Hashimu alizungumza kwa sauti ya upole.

“Ni kweli naumia sana! Yani kama ningejua mapema kuwa Magesa ni mzinzi kiasi hiki nisingekubali anioe” nilijikuta nikizungumza huku nikibubujikwa na machozi.

Shemeji hashimu alipoona mtoto wa kike nikilia akanivuta na kunikumbatia mwanaume wa watu. Kwakuwa nilikuwa nimekaa kitandani nay eye ameniinamia kwa pembeni kichwa changu kikaegemea kifua hake.

“Basi shemeji yangu usilie, unajua hata mungu anakupenda na ndiyomaana ameanza kukufunulia uchafu wa huyo mpuuzi” Alizungumza shemeji Hashimu kwa kumpondea mume wangu.

“Hata wewe huwa unamsaliti Fatuma?” nikahoji kwa sauti moja ya chumbani.

“Hapana, sija wahi na wala sitathubutu kumsaliti mke wangu Fatuma” alizungumza Shemeji kwa kujiamini huku akinipapasa mgongoni kama vile ananibembeleza nisilie.

“Basi usifanye hivyo shemeji, usaliti unauma sana” nikazungumza huku nikimvuta zaidi na kujilaza kitandani na shemeji naye akaja juu yangu bila ubishi.

“Usijali mtoto mzuri nakuahidi sitakuja kumsaliti rafiki yako. Nampenda sana Fatuma” alizungumza shemeji hashimu huku tayari alikuwa akipitisha ncha za ulimi wake maeneo ya shingoni mwangu.

Shemeji Hashimu alikuwa yupo shapu kuliko maelezo ya kawaida. ndani ya dakika chache tukajikuta wote wawili tukiwa tumebakiwa na nguo ndogo. Kwa kweli shemeji Hashimu namsifu kwa ushapu wake, yaani mambo yake yote yalikuwa shapu shapu. Kitoto cha watu ujanja wote uliingia kapuni nikaisha habari yangu na kujikuta nikiomba msaada.

“Shem nipe…..nipe shemu….amnhmn” Nilizungumza kwa kifupi kifupi kutokana na mchaka mchaka niliokuwa nikikimbizwa na shemeji Hashimu. Jamani nyie, mume wangu alikuwa ni mtata lakini shemeji Hashimu naye Mnh!.

Mtoto wakike nilijiachia na kusahau kabisa kama nilikuwa kwenye kitanda cha watu ndani ya chumba cha watu na mume wa watu.

“Jamani Shem sikujua kama upo hivi Ooooh Camoon….nipe bwana!” Nilizungumza kwa sauti bila hata woga wowote. Kile nilichokuwa nakifanya sikukiona kama kilikuwa ni kitu kibaya hata kidogo. Kwasababu mume wangu Magesa ndiye aliyekuwa ameanza. Namshukuru sana yule aliyemsevu kwa jina la Fundi umeme kwani yeye ndiye aliyenifumbua macho kuifahamu tabia ya mume wangu.

“Mwache Magesa afanye ushenzi wake. Na mimi nafaidi leooo Hashim…Hashim….oiayayaaya…..” Kutokana na sauti yangu kuwa kubwa ilimbidi shemeji Hashimu afanye kazi ya ziada ya kuniziba mdomo kila nilipojisahau na kuongeza sauti.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG