Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

HOUSEGIRL WA KITANGA (2) - 4

   


Chombezo : Housegirl Wa Kitanga (2)

Sehemu Ya Nne (4)


“Mama..” Fadhili akajibu kwa ufupi.

“Mama…Mama atawezaje kukueleza jambo kama hilo?” nikahoji kwa kutaharuki.

“Tumu, mama anafahamu ninavyokupenda. Na pia anafahamu kama na wewe unanipenda pia” Fadhili alizungumza kwa kujiamini na kunifanya nikumbuke maneno ya Binamu Mainaya.

“Usijidanganye Fadhili, hakuna mwanaume anayependwa na mimi hata mmoja katika huu ulimwengu” nilizungumza kwa msisitizo na kujiamini.

Maneno yangu yale yalimfanya Fadhili kuachia tabasamu ambalo sikuweza kubaini kuwa lilikuwa ni tabasamu la matumaini, la hudhuni au tabasamu la kebehi.

Endelea…

“Suluhisho hapa baba ni moja tu” Fadhili alizungumza kwa kubadilisha mada huku akijiweka kwenye kochi.

“Usizuge dogo, fafanua hilo zee la kazi ndio lipi?” alihoji kaka Imran kishambenga akiwa ameelewa Fadhili amemaanisha zee la kazi ni baba mzee Sekiza.

Endelea…26

“Jambo la kufanya we baba mtafute Bi mkubwa umshawishi arudi home” Fadhili alizungumza na kupuuza maneno ya kaka Imran ya kutaka aseme huyo zee la kazi alikuwa ni nani.

“Nimeshaongea sana na mama yenu lakini haelewi, sasa mimi nifanye nini!” Baba alieleza.

“Kama uliweza kumshawishi akakubali kufunga ndoa na wewe, utashindwaje kumshawishi arejee kwako?” Fadhili alizungumza kwa msisitizo huku akiendelea kutafuna chakula kilichokuwepo mdomoni.

“Swadakta, tangu uzaliwe leo peke yake ndio umezungumza maneno ya msingi dogo” kaka Imran aliunga mkono wazo la Fadhili.

“Kama ukishindwa mzee sisi tutaingilia kati, Bi mkubwa hawezi kukataa” alizungumza Fadhili kwa msisitizo.

“Unajua mzee usichukulie poa. Hakuna kitu ambacho sikipendi kama kujipikilisha” kaka Imran alizungumza kwa msisitizo.

“We unasema kupika, mziki upo kwenye kuosha vyombo na kusafisha choo” Fadhili aliongezea.

“Mkakati uliopo hapa kuanzia sasahivi ni kuhakikisha Bi Mkubwa anarejea ndani ya mjengo” kaka Imran alizungumza kwa msisitizo huku akichukua birauli iliyokuwa na maji ya kunywa na kuituma mdomoni.

Maneno ya kaka Imran na Fadhili yalimuingia sana baba kiasi cha kumfanya akili yake ifanye kazi mara tatutau zaidi. Alibaini ukweli na umuhimu wa maneno ya vijana wake pamoja na kwamba mziki wa kumrudisha Bi. Fatma pale ndani ulikuwa ni mzito.

“Sasa nani anajua anapoishi?” mama alihoji.

“Hiyo ni kazi rahisi sana, tukitaka kufahamu tutafahamu tu” alizungumza kaka Imran huku akipeleka kijiko cha chakula mdomoni.

“Sio lazima kufahamu anapoishi, hata dukani kwake tunaweza kumzukia tu” Fahili alizungumza huku akitafuna.

“Hapana mambo haya ni yakuzungumzia nyumbani na sio dukani” Kaka Imran akatoa wazo.

“Sasa nyubani kwake unapafahamu?” alihoji Fadhili.

“Tutamtuma Mainaya afuatilie” alizungumza kaka Imran kwa kujiamini.

“Mainaya hawezi kuwa msaada kwa hili, umesahau mziki wake wa vibao vya mbuzi?” baba alizungumza kwa tahadhari na kumfanya kaka Imran kuangua kicheko.

“Usijali mzee, Naya nimeshamtuliza kwa kumueleza ukweli kama nilivyomueleza mama na mamkubwa kule Tanga. Sasa hivi nimeshamuweka kiganjani hafurukuti” kaka Imran alizungumza kwa kujiamini.

“Kale kabinti kanavuta bangi sijui” baba alizungumza.

“Sasa kwa taarifa yenu mimi Mwantumu ameshanieleza kuwa Bi. Mkubwa anaishi Kijitonyama” kaka Imran alizungumza kwa kujiamini.

“Kijitonyama ni kubwa, anaifahamu nyumba yenyewe?” Fadhili alihoji kwa umakini wa hali ya juu.

“Amesema hafahamu nyumba wala mtaa lakini ni Kijitonyama” alizungumza kaka Imran kwa msisitizo.

“Huo ni mwanzo mzuri, nitafuatilia na nitawapa jibu ndani ya muda mfupi” Fadhili alizungumza kwa kujiamini.

Kikao kile cha dharura kilimalizika kwa makubaliano ya kuhakikima Bi. Fatma anarejea na kuishi kama zamani ndani ya nyumba ile. Kukosekana kwa uwepo wa mama ndani mle kulionesha pengo kubwa sana.

*****

Mkwara na maneno ya dada Mainaya yalinitikisa kwa kiasi fulani na kunifanya nitamani kurudi kijijini kwetu kuendelea na shughuli za kilimo, lakini maneno ya Bi. Fatma yalinitia moyo na nilipokumbuka maneno ya mama angu mzazi kuwa walikuwa wakinitegemea mimi kwa kiasi kikubwa katika shughuli za kilimo nilijikuta nikipata nguvu na ujasiri wa kuendelea kubaki jijini Dar.

Kama ilivyokuwa kawaida yangu nilifanya shughuli zangu na kumaliza kazi zangu mapema kabisa. Nilikuwa nikitumia muda mwingi kupumzika na kusoma vitabu va simulizi kwasababu nilikuwa najituma ipasavo katika majukumu yangu. Ukizingatia zaidi familia yenyewe haikuwa kubwa kama ile ya kule mabibo. Kule Kijitonyama tulikuwa tukiishi watu wawili tu yani mimi na Bi. Fatma.

Nikiwa sebleni nimekamatia kitabu cha simulizi kilichokuwa kikijulikana kama BONGO DASLAM kile cha yule kijana Ayubu wa Tanga. Nilisikia mlango ukigongwa na kunifanya niweke kitabu kwenye kochi na kuelekea mlangoni.

Ndugu msomaji huwezi kuamini mtu aliyekuwa akigonga mlango alikuwa ni Fadhili. Nilishituka sana kwa sababu sikuwa nimetegemea kukutana na kijana yule katika mazingira yale. Nilichokuwa ninakifahamu mimi ni kwamba hapakuwa na mtu ambae alikuwa anapafahamu nyumbani pale zaidi ya Mainaya. Hivyo niliishi kwa uhuru na kujiachia pasipo kuwa na hofu wala shaka.

Fadhili hakuwa ameshangazwa baada ya kuniona kama ambavyo mimi nilikuwa nimeshangazwa na kitendo cha kumuona yeye pale nyumbani. Zilipita kama sekunde thelathini hivi tukitazamana pasipo kuzungumza neno lolote lile kati yetu.

“Kwanini unanipenda hivyo?” Fadhili alivunja ukimya na kuhoji swali ambalo sikuelewa maana yake.

“Nani amekuelekeza huku?” nikahoji kwa umakini.

“Hata kuzimu hapafahamiki lakini watu wanafika” Fadhili alijibu na kuingia ndani akiniacha nimesimama nikimkodolea macho kwa mshangao.

“Mama hayupo lakini!” nikaeleza huku nikiwa bado nimesimama pale mlangoni.

“Najua…” alijibu Fadhili na kuchukua rimoti ya runinga na kuwasha.

“Sasa kama unajua hayupo umekuja kufanya nini huku?” nilihoji huku nikivuta hatua kuelekea kule sebleni.

“Mama hayupo lakini wewe si upo, au hata wewe haupo?” alizungumza Fadhili huku akibadilisha vipindi kwenye runinga.

“We umejuaje kama mimi nipo hapa?” nilihoji huku nikiegemea juu ya mguu wa sofa nikawa kama vile nimesimama.

“Wacha maswali yako bwana, unafikiri mama anaweza kunificha kitu mimi?” alizungumza Fadhili kwa sauti ya kujiamini.

“Kwahiyo mama ndio amekwambia kama mimi nipo hapa?” nikahoji kwa mshangao kwasababu makubaliano yetu mimi na Bi. Fatma ni kwamba wale watoto wake pamoja na baba wasifahamu uwepo wangu pale nyumbani kwake.

“Mimi nimekufuata wewe, hebu kaa hapo tuzungumze” alisema Fadhili huku akinielekeza niketi kwenye kochi.

Nilipumua kwa nguvu na kwenda kuketi kwenye kochi na kumsikiliza Fadhili kama ambavyo ametaka.

“Nani amekwambia kama mimi nipo hapa?” nikaendelea kuhoji kwa msisitizo mara tu nilipoketi.

“Mama..” Fadhili akajibu kwa ufupi.

“Mama…Mama atawezaje kukueleza jambo kama hilo?” nikahoji kwa kutaharuki.

“Tumu, mama anafahamu ninavyokupenda. Na pia anafahamu kama na wewe unanipenda pia” Fadhili alizungumza kwa kujiamini na kunifanya nikumbuke maneno ya Binamu Mainaya.

“Usijidanganye Fadhili, hakuna mwanaume anayependwa na mimi hata mmoja katika huu ulimwengu” nilizungumza kwa msisitizo na kujiamini.

Maneno yangu yale yalimfanya Fadhili kuachia tabasamu ambalo sikuweza kubaini kuwa lilikuwa ni tabasamu la matumaini, la hudhuni au tabasamu la kebehi.




“Sikiliza Tumu, mimi ni baba wa nyumba hii na wewe ndio mama wa nyumba hii. Bi. Fatma tunamtunza kama mzazi wetu” Fadhili alizungumza kwa kujiamini huku akiachia tabasamu lake lile.

“Fadhili wacha kujidanganya! Mimi sio Mwantumu yule wa Mabibo mliyekuwa mmezoea kumchezea. Mimi ni Mwantumu mpya kabisa ninayejiheshimu na kuitambua thamani yangu!” nilizungumza kwa msisitizo wa hali ya juu kiasi cha kumfanya Fadhili mwenyewe akubaliane na maneno yangu. Aliinua mikono na kuanza kupiga makofi ya kunipongeza.

“Ndio nini sasa?” nikahoji kwa mshangao baada ya kumuona akinipigia makofi ya pongezi.

“Hilo ndilo lililonifanya nikulete hapa. Mwantumu ninayempenda mimi ni huyu Mwantumu wa leo na sio yule Tumu wa Mabibo aliyekuwa hana muelekeo” alizungumza Fadhili na kupandisha mguu wake wa kushoto juu ya mguu wa kulia, akawa ameweka nne huku akiuchezesha mguu wake.

“Wacha kubwabwaja Fadhili! Mimi nimeletwa hapa na Bi.Fatma na sio wewe” nilizungumza kwa msisitizo na sauti ya kujiamini.

“Usilolijua ni sawa na usiku wa giza” alisema Fadhili kwa kebehi.

“Sasa kama huna unalolijua kwanini unaropoka tu?” nilizungumza kwa jazba.

“Tuwachane na hayo Tumu. Kilichonileta hapa ni kutaka kukueleza rasmi kuwa NINAKUPENDA” Fadhii alizungumza kwa msisitizo.

Maneno ya Fadhili hayakuwa na uzito wowote ndani ya moyo wangu. Yalikuwa ni maneno ya kawaida sana ambayo nilikuwa nimezoea kuambiwa na wanaume mbalimali kila kulipokucha. Hivyo kwangu neno Nakupenda halikuniletea msisimko wala mguso hata chembe.

“Una lingine au ni hilo tu?” nilihoji.

“Tafadhali Mwantumu safari hii usiumize tena moyo wangu amini Nakupenda sana” Fadhili alizungumza kwa msisitizo.

Nafikiri kama maneno yale angeyatamka kipindi kile nilipokuwa nikitamani kuyasikia kutoka kinywani mwake pengine mabalaa yote yale nisingekutana nayo. Lakini alikuwa amechelewa na maneno yale hayakuwa na thamani tena masikioni mwangu.

“Unanipenda?” nikahoji kwa msisitio huku nikiachia tabasamu la bandia.

“Hakika Nakupenda Mwantumu” Fadhili alizungumza kwa msisitizo.

“Asante, Nashukuru kwasababu hata Mungu anasisitiza tupendane” nilizungumza huku nikijifanya sikuwa nimeelewa muelekeo wake.

“Sina maana hiyo Mwantumu, Nakupenda nataka tuwe wapenzi” Fadhili alizungumza huku akishusha guu lake kutoka kwenye nne aliyokuwa ameweka.

“Unamaana unataka tuwe wapenzi sio?” nikahoji kwa umakini mkubwa.

“Hapana, namaanisha tuwe mke na mume” Fadhili alizungumza kwa upolena unyenyekevu mkubwa.

“Ahaa, sasa mbona umechelewa jamani Fadhili” nikazungumza kwa masikitiko makubwa.

“Unamaanisha nini Mwantumu, tayari umeshapata mwanaume mwingine?” Fadhili alihoji kwa mshituko wa hali ya juu bada ya kusikia maneno yangu.

“Simaanishi hivyo Fadhili..” nikazungumza huku nikiachia tabasamu la matumaini.

“Kumbe unataka kusemaje?”

“Neno Nakupenda kwangu halina thamani tena. Nilikupa nafasi lakini hukuwa tayari kulitamka wakati nilipodhani lina thamani” nilizungumza kwa msisitizo huku nikitengeneza tabasamu la kebehi kwenye midomo yangu.

“Unataka kuniambia nini Mwantumu?”

“Ukweli ni kwamba, ukinambia Nakupenda kwangu ni kazi bure kwasababu si sisimki wala siguswi. Sana sana nitakuona tapeli tu kama walivyo matapeli wenzako” nikazungumza kwa msisitizo kisha nikachuku kitabu changu na kufunua kurasa mbili tatu kama vili nilikuwa nataka kuendelea kusoma.

Fadhili alijiinua kutoka pale alipokuwa ameketi na kuvuta hatua kujaribu kusogea pale nilipokuwa nimeketi mimi.

“No! Fadhili naomba uishie hapo hapo! Usiongeze hata hatua moja mbele!” nikazungumza kwa msisitizo mkubwa huku nikimuelekezea kidole cha onyo.

“Naomba nikushike hata mkono tu Tumu” alizunguma Fadhili kwa sauti ya kubembeleza.

“Jaribu kuwa muelewa Fadhili, nimekwambia mimi sio yule Mwantumu wa Mabibo wa gusa unate” Nilizungumza kwa msisitizo huku nimetoa macho.

“Najua Tumu” Fadhili alijibu kwa unyonge.

“Sasa kama unajua mbona unakuwa mkaidi?”

“Nakupenda Tumu! Nakupenda sana” Fadhili alirudia meneno yale yale ambayo kwangu yaliniletea kichefuchefu.

“Fadhili…” nikaita kwa sauti ya umakini na utulivu.

“Naam mama” Fadhili naye akaitika kwa unyenyekevu.

“Umesema unanipenda?”

“Hakika mama!”

“Kweli?”

“Nakupenda Mwantumu, Nakupenda kuliko unavyofikiria wewe” Fadhili alizungumza kwa unyenyekevu na sauti ya kubembeleza.

“Eeeh we baba! nimekwambia sitaki kusikia hayo mashairi yako ya Nakupenda!” nikapaza sauti na kuzungumza kwa sauti ya ukali kidogo.

“Sasa nifanye nini Mwantumu?”

“Unatakiwa kuonesha matendo na sio maneno kama unaimba kwaya” nikazungumza kwa kujiamini.

“Wewe unataka nifanye matendo gani sasa?”

“Ahaa vizuri sana. Unatakiwa kufanya kile nitakachokuambia” nilizungumza na kuuma midomo yangu ya chini kwa meno ya juu.

“Usijali mrembo. Chochote utakacho nitafanya ili uamini kuwa Nakupenda” alizungumza Fadhili kwa unyenyekevu

“Nimekwambia sitaki kusikia hilo neno Nakupenda kutoka kinywani mwako. Unafeli wapi wewe?” nilizungumza kwa msisitizo baada ya kusikia amerudia tena yaleyale niliyokuwa siyapendi.




Endelea…

“Sawa mama” Fadhili alijibu.

“Haya geuka nyuma kama askari jeshi” nikazungumza kwa amri.

“Mnh!” Fadhili akaguna huku akiwa amesimama vilevile.

“Hutaki au?” nikahoji kwa msisitizo.

“Sawa mama” alisema Fadhili na kugeuka nyuma kama askari mgambo yupo kwenye gwaride la asubuhi.

“Bila kugeuka nyuma na kuchapa mkono, mbele tembea” nilizungumza kwa amri utafikiri mkuu wa majeshi ya msituni.

“Lakini mimi sio mwanajeshi Tumu. mimi ni muuza duka tu!” alizungumza Fadhili huku akiwa amesimama.

“Kwahiyo unabishana na mimi?” nikazungumza kwa onyo.

“Sawa bwana, lakini jeshi na Tanga sijui wapi na wapi!” Masikini ya Mungu Fadhili wawatu alifanya kama vile ambavyo nilikuwa nimemuamuru huku akilalamika.

Fadhili alianza kutembea kama askari jeshi na kufungua mlango wa kutokea nje akatowekea huko. Nafikri na yeye aliamua kuondoka kwa staili hiyo kwasababu hakurudi tena muda huo na kuniacha pekeyangu nikiangua kicheko kwa sauti utafikri nilikuwa natazama katuni za vihekesho.

*****

Kitendo cha Fadhili kunikuta nyumbani pale kwa Bi. Fatma kilimpa wakati mgumu sana hasa kwa kazi ambayo alikuwa amepewa na familia yake ya kuhakikisha anafanya upelelezi na kubaini mtaa na nyumba aliyokuwa akiishi Bi.Fatma.

Hakutegemea kabisa kama angekutana na mimi ndani mle. Jambo ambalo lilimchanganya zaidi ni baada ya kuniona jinsi ambavyo nilikuwa nimenona na kupendeza zaidi ya vile alivyokuwa ananifahamu.

Akaamua kujitoa muhanga siku hiyo kwa kuipoteza pasipo kufanya biashara. Aliongoza moja kwa moja hadi Kariakoo kwenye duka la mama yake na kufanikiwa kumkuta akiendelea na shughuli zake za dukani. Wateja walikuwa ni wa kutosha ukiachilia mbali wale waliokuwa wakipita na kuulizia bei bila kununua.

Fadhili alifika dukani pale na kujichanganya na wateja wengine. Alichagua nguo kadhaa za kike na kuja nazo hadi pale alipokuwa muuzaji. Bi. Fatma hakushituka sana kumuona Fadhili ingawa alishangazwa na kile kitendo cha kukusanya baadhi ya nguo na kutaka apewe mahesabu.

“Shikamoo mama” alisalimia Fadhili huku akigeuza geuza blauzi moja ya buluu iliyokuwa na kitambaa laini.

“Haya nawewe umekuaje?” alihoji mama huku akimtazama Fadhili kwa macho ya udadisi.

“Ukiona hivyo ujue umekuza mama. Naomba hesabu yangu” Fadhili alizungumza huku akiketi kwenye stuli moja ndefu iliyokuwepo dukani pale.

Kwakuwa mama alikuwa ni mfanya biashara hakuendelea kubishana wala kuhoji zaidi. Alichokifanya ni kuchukua kikokotoo na kuanza kupiga hesabu zake na baada ya sesekunde kadha aliinua macho kumtazama Fadhili usoni.

“Miambili Hamsini” mama alijibu kwa sauti kavu.

“Laki mbili na nusu!” Faadhili alihamaki baada ya kusikia kisi kile cha pesa.

“Wacha ubahili wako, unataka vitu vizuri halafu unakuwa bahili” mama alizungumza.

“Lakini Bi Mkubwa anakwenda kuvaa mkwe wako hizi nguo. Punguza kidogo basi” Fadhili alizungumza kwa msisitizo.

“Tena inabidi utoe zaidi kwasababu unanunua nyumbani” mama alizungumza kwa msisitizo huku akiendelea kuwasikiliza wateja wengine.

Fadhili alifungua pochi na kuhesabu pesa kisha akamkabidhi Bi. Fatma kiasi cha Laki mbili na nusu tasmlim.

“Naomba unisaidie kuupeleka huo mzigo” Fadhli alizungumza huku akimkabdhi mama yake zile pesa.

“Mzigo gani?”

“Hizo nguo..”

“Wapi..?”

“Kwa Mwantumu!” Fadhili alijibu huku uso wake ukiwa mkavu na kumfanya mama ashituke kidogo.

“Ndivyo mnavyodanyanyana na huyo Mainaya wako!” mama alizungumza kwasababu alifahamu mtu pekee aliyekuwa anafahamu uwepo wangu pale nyumbani kwa Bi. Fatma alikuwa ni Mainaya.

“Tunadanganyana nini tena Bi Mkubwa?” alihoji kwa mshangao Fadhili.

“Huyo Mwantumu mmemuona wapi?” mama akahoji.

“Mama hivi ninavyokwambia natokea nyumbani kwako” Fadhili alizungumza kwa msisitizo.

“Nyumbani wapi?” mama akahoji kwa mshangao.

“Kijitonyama” alijibu Fadhili.

“Ni nani amekwambia kuwa mimi ninaishi kijitonyama?” mama alihoji

“Jamani mama hata mimi unanificha! Kwani kosa langu mimi ni lipi?” Fadhili alizungumza kwa kulalamika.

Maneno ya Fadhili yalimfanya mama kumeza mate mengi kisha akajiegemeza kwenye stuli na kupiga bweho kisha akaramba midomo yake ya juu kwa ncha ya ulimi.

Mama aliamua kumuweka wazi Fadhili kuwa hakuwa anataka hata mtu mmoja aifahamu sehemu ambayo alikuwa akiishi kwa kuhofia usumbufu hasa kutoka kwa baba mzee Sekiza na kaka Imran. Pamoja na kwamba baba alikuwa akijitetea mara kadhaa pamoja na kuomba radhi kwa yale ambayo yalikuwa yametokea lakini mama alishindwa kukubaliana na hoja zake. Hivyo aliamua kujiweka mbali kabisa na familia ile.

“Mama mimi nimefika nyumbani na nimepokelewa vizuri na Mwantumu” alieleza Fadhili.

“Naomba sana jambo hili liwe siri, sitaki watu wafahamu ninapoishi na wala wasijue kama nipo na Mwantumu” alizungumza mama Kwa msisitizo.

“Umechelewa mama, kila mtu anafahamu kuwa unaishi Kijitonyama. Kitu cha msingi ni kumuweka mbali Mwantumu na hii familia” Fadhili alizungumza kwa msisitizo mkubwa.




“Kama nyote mnafahamu endeleeni tu kufahamu na hakuna sababu ya kumficha Mwantumu wangu. Ufirauni wenu hukohuko Mabibo kwenu!” mama alizungumza kwa jazba kwasababu alichokibaini ni kwamba mawazo ya Mwantumu hayakuwa yakitofautiana na mawazo ya Fadhili ya kutunza siri ile.

“Mama kusema ukweli mimi nampenda sana Mwantumu. Natamani awe mke wangu” Fadhili alizungumza kwa msisitizo na hisia za hali ya juu.

Maneno ya Fadhili yalimfanya mama kukumbuka siku ambayo kaka Imran alifunga safari hadi Tanga kwaajili ya kueleza hisia zake juu ya huyo huyo Mwantumu ambaye siku hiyo Fadhili ndio alikuwa anadai kuwa anampenda.

“Mwenyewe Mwantumu anafahamu kama unampenda?” mama akahoji kwa umakini mkubwa.

“Ndio mama, tangu zamani kabla ya matatizo kutokea mimi nilikuwa na mahusiano na Mwantumu” Fadhili alizungumza kwa nia ya kumshawishi mama yake.

“Kwahiyo na wewe ni miongoni mwa wale washenzi?” alihoji mama kwa mshangao na mshituko.

“Hapana mama! Sikuwahi kukutana kimwili na Mwantumu hata siku moja” alieleza Fadhili kwa tahadhari.

“Yeye Mwantumu ana mtazamo gani juu ya hilo penzi lako kwake?” ilibidi mama ahoji kiutu uzima kwa maana mambo alikuwa akiyaona yanazidi kuwa magumu kila kulipokucha pamoja na kwamba tatizo lile alihisi limekwisha kwa kulikimbia. Alivuta pumzi na kuziachia kwa nguvu, alihisi kuchanganyikiwa kwa kitendo cha watoto wake wawili kuangukia katika penzi la msichana mmoja tena dada wa kazi. Alitamani kufanya maamuzi ya kunirejesha kijini lakini alipokumbuka maneno ya mama yangu kwamba alikuwa ananitegemea akakaza moyo.

“Nitazungumza naye na nitafahamu mbivu na mbichi” alizungumza mama kwa msisitizo huku akimsogelea mteja aliyekuwa anachomoa nguo kutoka kwenye henga.

Fadhili aliuma meno huku akijaribu kutafakari umuhimu wa kuishi karibu na mimi ilia pate nafasi ya kunitega na kuchota penzi langu.

“Ni lazima nihakikishe mama anamrudisha Tumu nyumbani ili nifanikishe malengo yangu!” alizungumza kimoyomoyo huku akimeza funda la mate. Alipeleka macho yake na kuzitazama zile nguo alizokuwa ameninunulia na kuachia tabasamu la matumaini.

Fadhili alipobaini kuwa mama alikuwa bize na wateja wake, akaamua kujiongeza na kuondoka dukani pale pasipo kumuaga mama yake.

*****

Kwa kiasi fulani hali ya amani ndani ya moyo wangu ilianza kutoweka. Kikubwa ambacho kilikuwa kimenichanganya zaidi ni yale maneno ya Fadhili yaliyohusu mapenzi. Kwa upande wangu tayari nilikuwa nimekwisha chukia kitu mapenzi. Sikuhitaji wala sikutamani tena kusikia habari za mapenzi. Sijui nilikuwa ninawaza juu ya nini lakini huo ndio uliokuwa msimamo wangu. Sasa siku hiyo Fadhili alikuja kuiharibu siku yangu kwa kuzungumzia habari zile zile za mahusiano na mapenzi.

“We Mwantumu!” sauti ya Bi. Fatma ilinigutusha kutoka katika lindi la mawazo nililokuwa nimezama.

“Abee mama!”

“Mbona hauli una tatizo gani?” mama alihoji baada ya kuniona nimezama kwenye mawazo na kusahau kula.

“Hapana mama mbona mimi nakula” nilijaribu kujitetea.

“Una mawazo gani, au unamuwaza Fadhili?” mama alihoji swali la mtego ambalo kwa upande wangu lilikuwa lamoto utafikri kaa la mawe.

“Hapana mama hakuna mtu ninayemuwaza” nikazungumza kwa sauti ya msisitio lakini iliyokuwa imejaa aibu kwasababu nilikuwa ninamuheshimu sana Bi. Fatma. Hivyo sikutegemea kama angeweza kunieleza maneno kama yale.

“Kwanza hebu niambie ukweli, wewe na Fadhili mpoje?” Bi. Fatma alihoji huku akitafuna chakula polepole.

“Nani..?” nilijifanya kuitikia kama vile sikuwa nimesikia swali lile.

“Fadhili” alijibu mama Kwa msisitizo.

Nilitikisa kichwa kuashiria kuwa hapakuwepo na jambo lolote ambalo lilikuwa likiendelea kati yangu mimi na Fadhili.

“Fadhili amesema anataka akuoe” alieleza mama na kupeleka kipande cha nyama mdomoni.

“Mnh!” nikaguna kwa mshituko kiasi cha kupelekea kupaliwa na chakula na kusababisha nikohoe mfurulizo.

Bi. Fatma alinitazama kwa macho ya udadisi huku akihisi kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kinaendelea kati yangu mimi na Fadhili, akaachia tabasamu la kunyapia ambalo nililiona kwa mbali sana kisha likapotea ghafla.

“Inamaana Fadhili hajawahi kukueleza kitu chochote kuhusu jambo hilo?” mama alihoji huku akinitazama kwa macho yaliyokuwa yamejaa udadisi wa hali ya juu.

“Aaam..amee…amee hapana..haja..haja..alini..hapana mama” nilijikuta nikipata kigugumizi na kushindwa kutoa jibu la swali lile. Sasa ningejibu nini kwasababu ni kweli nilishawahi kuwa na uhusiano wa kimapeni na Fadhili pamoja na kwamba sikuwahi kukutana naye kimwili, lakini pia kwa wakati huo sikuwa na uhusiano wowote na kijana huyo amabaye mchana wa siku hiyo alifika nyumbani hapo na kunieleza masuala hayo hayo ya mahusiano.

Kigugumizi changu kile kilimfanya mama abaini na kupata jibu la moja kwa moja kuwa mimi na Fadhili tulikuwa na mahusiano kama ambavyo Fadhili mwenyewe alimueleza mama kule dukani.

“Vipi mbona umeacha kula?” mama alihoji baada ya kuniona nikiacha kuendelea kula na kuosha mikono yangu.

“Nimeshiba mama” nikajibu kwa ufupi.

“Au maneno yangu ndio yamekukera?”

“Hapana mama, leo nimechelewa kula chakula cha mcahana” nikaeleza.

“Nenda chumbani kwangu ukalete ule mfuko wa kijani niliotoka nao kazini” mama alizungumza.

Niliinuka haraka na kuelekea huko chumbani. Akili yangu ilikuwa kama vile imechanganyikiwa juu ya masuala yale ya mahusiano ambayo niliona yakiwa yananifuata kwa spidi ya ajabu. Ukweli ni kwamba nilikuwa ninampenda sana Fadhili kuliko mwanaume yeyote yule. Tatizo ni kwamba moyo wangu ulikuwa tayari umeshatumbukia nyongo juu ya masuala ya mahusiano.

Nilichukua mfuko ule wa kijani na kutoka nao hadi pale sebleni alipokuwa mama anaendelea kupata chakula cha jioni.

“Fungua huo ni mzigo wako” alizunguma mama kwa sauti ya upendo.

Ndugu msomaji nilipofungua mfuko ule nilijikuta nikijawa na furaha kiasi cha kusahau mambo yote ambayo yalikuwa yakiuchanganya ubongo wangu. Mfuko ule ulikuwa na nguo nzuri kupita maeleo. zilikuwa ni nguo za heshima lakini zenye kuleta mvuto kwa mvaaji. Nikaona hakika Bi. Fatma alikuwa ananijulia na kunipatia hasaaa!

“Vipi umefurahi?” Bi. Fatma alihoji huku akinitazama kwa tabasamu.

“Mama unanijulia mnoo, hakika nimefurahi sana” nikazungumza kwa furaha huku nikizikumbatia nguo zile.

“Haya jaribisha basi nikuone” mama alizunguma huku akisogeza maji na kunawa mikono.

Kitendo bila kuchelewa nilibadilisha nguo palepale mbele ya mama na kujaribisha blauzi ya mikono mirefu na sketi moja nzito na ndefu iliyokuwa na maua ya rangi ya kibuluu na nyekundu.

“Hakika umepoendeza mwanangu” mama alizunguma kwa sauti huku akitabasamu na kuzidi kuongeza furaha ndani ya moyo wangu.

“Asante sana Mama, Mungu atakulipa kwa hili na mengine yote!” nikazungumza kwa shukurani za dhati kutoka moyoni mwangu.

Bi.Fatma alivuta pumzi na kuziachia kisha akachukua birauli ya maji ya kunywa na kuipeleka kinywa. Alipoiteremsha birauli ya maji alipiga mbweo na kuachia tabasamu.

“Fadhili ndiye aliyenunua hizo nguo, na amesisitiza nizifikishe kwako” alizungumza mama na kufuta mdomo wake kwa kiganja cha mkono wake wa kushoto.




Nakwambia pale nilipokuwa nimesimama nilipigwa na ubaridi na kuganda utafikiri nilikuwa nimepigwa shoti ya umeme. Lile tabasamu langu zito lilitoweka taratiibu na kubaki mdomo wazi.

“Vipi haukutegemea kama angetenda jambo kama hilo?” mama alihoji huku akiamini nilikuwa nimeshituka kutokana na ile surprise niliyokuwa nimefanyiwa na kijana wake.

“Lakini mama…” nilitaka kuzungumza lakini nikakosa neno la kuzungumza.

“Nafikiri Fadhili atakuwa anakupenda sana mwanangu” Bi.Fatma akazungumza kwa msisitizo.

Nilikumbuka ile kauli ya Fadhili ya kwamba hata mama alikuwa anafahamu kwamba mimi na yeye tulikuwa tunapendana sana. Nikameza funda la mate machachu na kujikuta nikikosa neno la kuzungumza na kutoa toa macho kama mchawi aliyeshikwa kwenye nyumba ya Shekh akiwanga.

“Sasa mwanangu nataka leo unieleze ukweli” mama alizungumza kwa msisitizo mkubwa huku amenikodolea macho.

“Ukweli gani mama?” nikahoji kwa hofu na mashaka.

“Kati ya Fadhili na Imran unampenda nani?” mama alihoji kwa msisitizo.

Mnh! maneno ya Bi. Fatma hayakuwa yakiniingia akilini hata kidogo. Maana siku hiyo utafikri alikuwa amekunywa pombe kwa maana kila dakika zilivyosonga ndivyo mama yule alivyokuwa akiniletea vituko na utata. Sasa sijui kwa swali lake lile mimi ningempa jibu gani kwa maana kati ya watu wake hao wote wawili hapakuwepo na hata mmoja ambaye nilikuwa namuhitaji.

“Najua unampenda sana Fadhili, sasa ninachotaka kukueleza ni kwamba uwe na msimamo” alizungumza Bi. Fatma kwa msisitizo wa hali ya juu.

Bado nilikuwa katika hali ya mshangao na kuchanganyikiwa huku nikiwa sijielewi wala sijitambui tena. Nilijiona kama vile zigo la uchafu lililotolewa lilikotoka na kupelekwa dampo pasipo kufahamu hatma yake. Nilichokuwa nimekibaini hadi wakati ule ni kwamba mama alikuwa amedhamiria kunirudisha Dar es salaam ili nikawe mke wa kijana wake Fadhili.

Nikiwa bado katika hali ile ya bumbuwazi nilishituliwa na sauti ya mama ikiniamuru niende kufungua mlango.

“Si unasikia mlango unagongwa? Nenda kafungue” alizungumza mama kwa msisitizo baada ya kuniona bado nimezubaa.

Nilikimbilia mlangoni na kufungua haraka haraka huku nikiwa sifahamu mtu aliyekuwa anagonga mlango majira yale ya usiku. Macho yangu yakakutana na macho ya Fadhili akiwa amesimama mlangoni.

“Kah! Ni wewe tena!” nilizungumza kwa sauti ndogo baada ya kumuona Fadhili mlangoni. Nilisogea pembeni kumpisha aingie ndani lakini bado alikuwa amesimama kama nguzo ya umeme.

“Ingia basi mbona umesimama kama mlinzi, au bado una hamu ya kupiga kwata za kijeshi?” nilizungumza na kujaribu kumtania kidogo kwa kumkumbusha yaliyokuwa yametokea mchana wa siku hiyo alipokuja nyumbani.

“Naona umependza kuliko kawaida, aliyekuchagulia hizo nguo hakika ni hodari” Fadhili alizungumza baada ya kuniona nimevaa zile nguo alizokuwa ameninunulia yeye.

“Unajua unaingiza mbu ndani, kama hauingii nedazako nifunge mlango” nilizungumza kwa jazba hasa baada ya kusikia yale maneno yake ya kuniambia heti nimependeza.

“Siko pekeyangu Mwantumu” Fadhili alizungumza na kusogea pembeni.

“Mungu wangu! Na wewe?” nikajikuta nikihamaki baada ya kumuona Binamu Mainaya amesimama nyuma ya Fadhili huku akinitazama kwa tabasamu.

“Vipi hutaki wageni? Na kama kweli hupendi wageni basi leo utatufuka” Mainaya alizungumzakwa kebehi.

Nikiwa nimepumbazika na wageni wale wawili walio onekana kuwa machachari, nilijikuta nikivurugwa zaidi baada ya kusikia sauti ya mgeni wa tatu akijitokeza kutokea pembeni.

“Kilichonifurahisha zaidi ni kufunguliwa mlango na wewe” Ilikuwa ni sauti ya kaka Imra aliyekuwa akizungumza huku akijitokeza kutokea pembeni.

Nilijikuta nikitoa macho huku nikiangaza angaza nyuma yao ili kuona kama kungekuwa na mtu mwingine maana nilikuwa naona kama vile Fadhili ameamua kunifanyia mazingaombwe.

“Unanitafuta mimi?” ni kweli kabisa kama nilivyodhania ndivyo ilivyokuwa. Baba alikuwa amesimama nyuma yao na alipoona naangaza maho akanisemesha.

Ndugu msomaji nakwambia nilijikuta magoti yakiniishia nguvu pale nilipokuwa nimesimama. Nilichofanya ni kurudi sebleni mbio na kuwaacha wageni wale wale mlangoni.

“We vipi mbona kama umekutana na jini?” Bi. Fatma alihoji baada ya kuniona nimerejea huku nikiwa kama vile nimepagawa.

“Hao hapo mama, hao hapo nje wote…wote” nilizungumza kwa kuchachawa huku nikipagawa hasa.

Bi. Fatma naye alianza kupatwa na hofu kutokana na hali yangu. Akahisi pengine mtoto wa watu nilikuwa nimepandwa na malaria. Lakini kabla hajatafakari alishangaa kuona wageni wakiingia ndani mle huku wakiwa wamebeba mabegi. Mama akabaki amekodoa macho utafikiri alikuwa anatazama sinema za mazombi.

“Hodi…hodi…hodi” waliingia wageni wale huku wakibisha hodi.

Mimi na mama bado tulikuwa tumewatumbulia macho tukiwashangaa. Hatukuwa tumetegemea kabisa ugeni ule. Jambo la kushangazazaidi ni kwamba wageni wale walikuwa wamebeba mabegi makubwa makubwa utafikiri wanasafiri au wanahama.

Wageni wale waliweka mabegi yao sehemu moja na kisha kila mmoja alichagua kochi lake na kuketi huku wakionekana kujawa na furaha kuliko wenyeji wao.

“Shikamoo mama” Mainaya alisalimia.

“Kama ni mali weka mfukoni, mimi sina shida nayo!” alizungumza mama kwa hasira.




“Jamani mbona kama hamkufurahishwa na uwepo wetu hapa?” Baba alihoji kwa msisitizo huku akijiegemeza kwenye kochi na mkono mmoja ameupachika juu ya kiegemeo cha kochi.

“Tuwasaidie nini labda?” Mama alivunja ukimya na kuhoji.

“Kwa sasa hatuhitaji msaada wowote pengine siku nyingine” alizungumza Baba kwa sauti ya kujiamini iliyokuwa imejaa nyodo.

“Sasa Kwanini mko hapa?” Mama aliendelea kuhoji.

“Kwasababu tumechoka kuishi pekeetu” Kaka Imran alizungumza huku akijiinua na kwenda kuchukua rimoti ya runinga na kubadilisha kipindi kilichokuwa kikiendele.

“Mnataka kuishi na nani?” Mama alihoji kwa msisitizo.

“Tunataka familia yetu iungane na kuishi pamoja kama zamani, mambo ya huyu anaishi kule na yule anaishi huko yamepitwa na wakati” kaka Imran alizunguza kwa msisitzizo.

“Kwahiyo mndhani kujibeba kwenu huko hadi hapa ndio itasaidia?” mama naye akahoji kwa nyodo na kebehi.

“Shangazi jaribu kuangalia nafsi zetu, hakika unahitajika sana katika familia yetu” Mainaya naye alizungumza kwa sauti ya heshima na iliyojaa chembe chembe za majuto na huruma.

“Nyumba yetu inatutosha sisi wawili tu, hatuhitaji mtu wa ziada” mama alizungumza kwa msisitizo.

“Kusema kweli tumeshika adabu, tunautambua umuhimu wako mama” alizungumza Fadhili kwa sauti ya kubembeleza na kusihi.

“Sikilizeni ninyi watu, ninawaomba mtoke ndani mwangu na mtuache kama tulivyo!” mama alizungumza kwa ukali kidogo.

Kaka Imran alishuka kwenye kochi na kupiga magoti, dada Mainaya naye akafuata, kaka Imran hakubaki nyuma na mwisho kabisa huwezi kuamini mzee Sekiza naye akapiga magoti mbele yetu mimi na mama.

“Mke wangu Fatma, tambua kuwa hakuna mkamilifu katika huu ulimwengu. Tunakiri makosa yetu na tunahitaji huruma yako ituweke huru” mzee Sekiza alizungumza huku akiwa amepiga magoti.

Vituko vyote vile nilivipa kisogo lakini kitendo kile cha baba kupiga magoti mbele ya mama pamoja na watoto wake na kumuomba mama msamaha kiliniuma sana. Nilihisi hali ya huruma ikiniingia ndani ya moyo wangu na kutamani kuwaruhusu wainuke pale chini. Nafikiri walikuwa wamejirekebisha kama ambavyo walikuwa wanasema wenyewe.

“Mnajua msiniletee vituko nyie watu! Hebu inukeni muondoke mbele ya macho yetu tusije tukapiga kelele za wezi” mama aliendelea kushikilia msimamo wake uleule ambao nilianza kuuona kama mzigo kwangu na umejaa ukakasi.

“Mama tupo tayari kupigwa na wananchi wenye hasira kali hadi watuue kuliko kuishi bila ya wewe mama” kaka Imran alizungumza huku machizi yakimbubujika kwenye macho yake. Dah hadi huruma jamani nyie, nilimhurumia sana kaka Imran.

“Haya kama ni maonesho tunashukuru kwa burudani sasa inatosha. Tunaomba muondoke na mje tena kesho” mama alizungumza kwa msisitizo huku akitetemeka kutokana na hasira alizokuwa nazo. Hakika alikuwa akimaanisha kwa kile alishokuwa anakizungumza mbele ya wana ndugu wale.

“Hivi mama unahisi raha gani kupigiwa magoti na Baba mbele ya watoto wake? Hata kama ni kosa, ni kosa gani hilo ambalo haliwezi kusamehewa mtu ambaye amekiri kosa na kuomba msamaha?” alizungumza Fadhili maneno ambayo nilijikuta nikitoa machozi bila kupenda.

Pasipo kushauriwa wala kulazimishwa na mtu, na mimi nilijikuta nikiungana na wageni wale na kupiga magoti mbele ya mama. Moyo wangu ulikuwa umesafishika kabisa na kuridhika na msamaha ule waliokuwa wameuomba wale viumbe wa Mwenyezi Mungu.

“Haya na wewe umeambukizwa ugonjwa gani?” Bi. Fatma akahoji kwa mshangao baada ya kuniona na mimi nimepiga magoti pamoja na wageni wale waliokuja na upepo wa kisulisuli.

“Mama ninaungana na familia yako kuomba msamaha kwa kila ambacho kimetokea. Tafadhali wapokee na uishi nao kama zamani” nilizungumza kwa sauti ya kubembeleza.

Maneno yangu yalimshangaza zaidi mama. Pamoja na kwamba alianza kuhisi roho ya huruma lakini alichokuwa anakiamini ni kwamba na mimi nimeungana nao kwasababu ya penzi la Fadhili.

“Nafikiri mnanifahamu vizuri watoto wangu, nikiseme hii ni nyekundu haiwezi kubadilika na kuwa nyeupe. Kwa hivyo ondokeni haraka sana na kinyume na hapo napiga simu Polisi kuomba msaada” Mama alizungumza kwa msisitizo.

Maneno ya mama yaliwafanya wageni wale wote kwa pamoja kuangua kilio kwa sauti. Na mimi pasipo kujielewa nikajikuta nikilia kama wao, tukawa kama vile tupo msibani.

Mama aliziba masikio na kukunja sura zaidi, hakuwahi kufikiria katika maisha yake kama kungekuwa na watu vichaa kama sisi. Alitamani kutubeba na kwenda kututupa mbali sana na macho yake.

“Heeei! Hey!, asee nyie!” Bi. Fatma akapaza sauti kututuliza.

Saiti ya mama ilikuwa kama vile anazima moto kwa kutumia mafuta ya taa. Vilio viliongezeka na kuzidi. Ikabidi mama akae kimya na kutukodolea macho huku akiwa haelewi jambo la kufanya kwa mshangao.

Zilipita kama dakika tano hivi ndipo kila mmoja alionekana kushusha kilio na kubaki vilio vya chinihini.

“Hivi mna akili timamu nyie watu?” alihoji mama baada ya vilio vile kupungua.

“Mama haya ndiyo maisha yetu, haipiti siku hata moja hatujamwaga machozi kwa kukosekana kwako” kaka Imran alizungumza kwa msisitizo na kumalizia na kilio tena cha kwikwi.



ENDELEA...

“Mama, rejesha moyo wako na uungane na watoto wako, hakika wanateseka sana kwa kukosekana kwako. Tazama lawama zote hizi nitazibeba mimi kwa maana mimi ndio sababu yayote haya. Hakika hata ufalme wa Mungu sitauona kwa kosa hili” nilizungumza kwa kuomboleza kiasi cha kumgusa kila mtu ndani mle.

Maneno yangu yalimshangaza zaidi Bi. Fatma. Hakuweza kuamni kama ingetokea hata siku moja nikaungana na watu wale kutaka wasamehewe.

“Hakika hakuna mkate mgumu mbele ya chai” alizungumza mama na kuachia tabasamu la kujilazimisha. Alikumbuka kule Tanga siku ambayo kaka Imran alikuwa akijitetea kwa kueleza ukweli juu ya lile tukio lililokuwa limetokea na kujinasua katika kesi ile. Pamoja na kwamba ukweli wenyewe ulikuwa umepinda pinda lakini ikabidi ajilazimishe kuamini. Hivyo maneno yangu yalimtia nguvu na kuanza kuhisi nafsi yake ikifunguka na kuingiwa na chembe chembe za huruma. Alijiinua kutoka pale alipokuwa ameketi na kuvuta hatua hadi alipokuwa amepiga magoti mume wake mzee Sekiza.

“Haya amkeni nimewaelewa” mama alizungumza huku akimuinua baba kutoka pale alipokuwa amepiga magoti na kumkumbatia huku akitokwa na machozi.

Kila mmoja alishindwa kuzuia furaha aliyokuwa nayo kujidhihirisha hadharani. Walikuwa wakikumbatiana na kupongezana huku kila mmoja akitokwa na machozi ya furaha. Hakika upendo ndani ya familia ni raha jamani nyie Dah!

*****

Maisha mapya ya familia ya Bi.Fatma na mzee Sekiza yalikuwa ni maisha ya kuvutia kuliko kawaida. Amani na upendo ndani ya nyumba ile ilikuwa imeongezeka mara mia zaidi ya maisha yale ya zamani. Kila mmoja alionekana kuwa na furaha wakati wote. Hata dada Mainaya naye alihamia nyumbani kwa mjomba wake na kuishi pamoja nasi kama familia moja yenye upendo na amani.

Familia ile ililazimika kurudi tena kule Mabibo kulipokuwa na nyumba kubwa yenye nafasi. Pamoja na kwamba mazingira ya nyumbani pale Mabibo yalikuwa yakinikumbusha mengi ya nyuma lakini niliyapenda kama yalivyo.

“Tumuu..” sauti ya Binamu Mainaya ilinigutusha nilipokuwa jikoni nikisafisha jiko kwa kitambaa.

“Abee dada Naya..” niliitika kwa heshima.

“Unafanya nini saa hizi?” Binamu alihoji kwa sauti ya upendo.

“Namalizia kufuta jiko nianze maandalizi ya chakula cha jioni” nami nikajibu kwa upole na heshima.

“Kuna kitu nataka tuzungumze mdogo wangu” alisema Mainaya kwa sauti yake ile ya upendo.

“Sawa dada hakuna shida” nikajibu na kumsikiliza kwa makini.

“Humu ndani tunaishi na wewe kama vile ndugu yetu wa damu” alisema Mainaya kwa sauti ya chini.

“Ni kweli dada Naya”

“Kwanini usikubali tukaungana moja kwa moja sasa?” Mainaya alizungumza kwa umakini mkubwa.

“Unamaanisha nini dada Naya?”

“Natamani uwe wifi yangu” mainaya alizungumza maneno ambayo niliyaunganisha na ule wimbo wa Fadhili aliokuwa akiniimbia mara kwa mara kuwa ananipenda. Nikahisi kijana yule alikuwa amedhamiria hasa kutimiza malengo yake.

Nilimeza funda la mate na kujikuta nikihisi kurejewa na hisia za mapenzi kwa Fadhili. Hakika nilimpenda sana Fadhili tangu nilipokuwa nimekuja kwa awamu ya kwanza. Matatizo tu ndiyo mbayo yalitutenganisha.

“Unataka kuniambia nini dada Naya?” nikajifanya sielewi na kuhoji huku ndani ya moyo wangu nikihisi furaha ya kumuona mwanaume niliyekuwa nikimpenda tangu zamani akipata taabu kulisaka penzi langu.

“Imran ameniambia anataka akuoe” alizungumza dada Mainaya na kunifanya nishituke kidogo na kuhisi kuishiwa nguvu.

Mimi nilifikiri alikuwa anamzungumzia Fadhili pale kumbe alikuwa anataka kumzungumzia yule mshenzi firauni. Nilijisikia vibaya sana kusema kweli baada ya kupata taarifa ile.

“Wala usiogope mdogo wangu, Imran anakupenda sana. Hakika atakutunza ipasavyo” Binamu Mainaya alisisitiza baada ya kuniona nimevaa sura ya kupoteza matumaini.

“Lakini dada Naya, mimi sipo tayari kuolewa sasa hivi” nikazungumza kwa sauti ya unyonge.

“Usiogope Tumu, Imran hawezi kufanya tena utumbo kama alioufanya kipindi kile” alizungumza Mainaya kwa sauti ya ushawishi.

“Hapana dada Naya, mimi sitaki kabisa mambo hayo sasa hivi” nilizungumza kwa unyonge.

“Wala usinijibu sasa hivi, naomba ulipe muda jambo hili utanijibu hata wiki ijayo” Mainaya alizungumza kwa sauti ya chini lakini iliyosikika kuwa na umakini na uzito wa hali ya juu.

Wakati uleule nilipokuwa nikizungumza na dada Mainaya kule jikoni, mlango wa jikoni ulifunguliwa na mtu akachungulia.

“Acha we! Nawaona mtu na wifi yake” alikuwa ni Fadhili alizungumza akitabasamu huku kiwiliwili kikiwa nje na kichwa ndio amechungulia jikoni.

“Nakwambia wenyewe tunayasuka yetu tu hapa” alizungumza Mainaya huku akitabasamu.

“Safari hii lazima tuoe, hatutaki mchezo tena” Fadhili alizungumza huku akinitazama kwa macho ya uchu.

“Lazima tuchukue kitu hiki, haiwezekani toto zuri kama hili lihukuliwe na jitu lingine la hovyo hovyo” Mainaya alizungumza huku akicheka.

“Haya nawatakia mazungumzo mema wapendwa wangu” alizema Fadhili na kuondoka akituacha mimi na Mainaya kule jikoni.

Mazungumzo yale kati ya dada Mainaya na Fadhili yalizidi kunichangaya na kuniweka njia panda. Nakumbuka kabisa Fadhili alikuja nyumbani na kunitamkia kuwa nlikuwa ananipenda kwa dhati na alitaka kufunga ndoa na mimi. Tena haikutosha jioni alimuagiza mama yake aniletee nguo na kumueleza kuwa ananipenda. Sasa imekuwaje ameungana na Mainaya kutaka niolewe na kaka Imran? Kwa kweli sikuwaelewa kabisa.

“Mwenyewe unaona Tumu, kila mtu anatamani uolewe na Imran ili uwe mwanafamilia” alizungumza Mainaya na kutoka jikoni akaniacha nikiwa katika utata. Nilishindwa kabisa kukubali kuolewa na kaka Imran kwasababu hakuwa chaguo langu hata kidogo.

Niligeuka na kuendelea kufuta jiko huku bado mawazo yalikuwa yakinitawala. Nikaona ni afadhali niache kazi na kurudi kijijini kwetu kuliko kukubali kuolewa na kaka Imran mwanaume ambaye sikuwa ninampenda.

Nilijikuta nikifuta jiko kwa muda mrefu pasipo kujitambua kutokana na mawazo yaliyokuwa yakizunguuka kichwani mwangu. Sauti ya mlango wa jikoni ukifunguliwa ulinigutusha kutoka kwenye yale mawazo niliyokuwa nao. Nilipotupa macho mlangoni nikakutana na Fadhili akinitazama huku akitabasamu.

“Mrembooo!” aliniita huku akitabasamu.

“Karibu” nikaitika kwa ufupi.

“Mbona hauna furaha, inamaana maneno ya binamu Mainaya yamekukera?” Fadhili alihoji huku akivuta hatua na kunisogelea pale nilipokuwa nimesiamama. Nikabaki kimya nikimtazama huku nikihisi hasira zikinijaa sekunde kwa sekunde.

“Si unaona mrembo, Binamu naye pia anatamani nikuoe. Kwanini usikubali tutengeneze familia Mwantumu?” Fadhili alizungumza maneno tena ambayo ndiyo yalizidi kunichanganya kuliko hata vile nilivyokuwa nahisi nimechanganyikiwa.



“Kwanini usiniache niendelee na kazi zangu Fadhili?” nikazungumza kwa ufupi baada ya kuhisi mazingaombwe yalikuwa yakiendelea mbele yangu.

“Mwantumu mimi sipo kama hao wanaume wengine, tafadhali niambie kuwa unanipenda” Fadhili alizungumza kwa kubembeleza.

“Kwani nikikwambia kuwa nakupenda halafu nikawa sikupendi utakuwa umepata nini?” nikazungumza kwa msisitizo baada ya kuhisi watu wale walikuwa wamepanga kunijaribu.

“We nambie tu mi nitaridhika” Fadhili alisihi.

“Halafu nikikwambia sasa ndio itakuwaje?” nikahoji kwa ile sauti yangu ya kujiamini ambayo haikuwa na hata chembe ta tabasamu.

Fadhili aliramba midomo yake huku akitaka kuzungumza neno lakini kabla ya kusema chochote mama aliingia jikoni na kumkuta Fadhili amesimama karibu kabisa na nilipokuwa nimesimama mimi.

“Nilijua tu utakuwa huku” mama alizungumza akimwambia Fadhili.

“Hapana mama, nimekuja kumjulia hali kidogo” Fadhili akazungumza.

“Najua mnapendana sana wanangu, lakini nawaomba sana muwe na mipaka na mambo yenu. Mjipange kisha mtuambie tufuate utaratibu ili mambo yaende katika misingi sahihi” mama alizungumza yakwake nayeye

“Kwakweli tunapendana sana mama, niliteseka sana Tumu wangu alipokuwa mbali” Fadhili alizungumza kwa msisitizo huku macho yake yakionesha msisitizo kwa kile alichokuwa anakizungumza mbele yangu na mama yake.

“Nililijua hilo, na ndiyo sababu pekee iliyonifanya nikubali kurudi hapa nyumbani kuishi na wanangu” mama akazungumza lake la rohoni.

“Mwantumu umesikia maneno ya mama?” Fadhili alihoji huku akiachia tabasamu la mahaba.

“Kwaherini, we Fadhili mwache mwenzio afanye kazi” mama alizungumza na kuondoka jikoni akituacha mimi na Fadhili tukitazamana kama majogoo.

“Hivi Fadhili wewe ndio umemtuma Binamu?” nikahoji kwa umakini baada ya mama kutoka jikoni mle.

“Yeah..Yeah…hata Mainaya anafahamu ukweli jinsi ninavyokupenda” Fadhili alizunguma kwa kujiamini huku akiwa hafahamu Maneno aliyokuwa amenieleza Mainaya.

“Unauhakika?” nikahoji kwa msisitizo huku nimemkazia macho.

“Asilimia zote!” Fadhili alizungumza kwa kujiamini.

“Haya, kila lakheri” nilijibu na kuendelea na shughuli yangu huku nikimuacha akinikodolea macho.

Kule nyuma Fadhili alikuwa akinikodolea macho na kunichambua kuanzia kwenye kisigino hadi kwenye kisogo. Aliporidhika akavuta pumzi ndefu na kumeza mate.

“Mwaka huu nisipokufa nitazikwa nikiwa hai” Fadhili alijizungumzisha huku akinikodolea macho.

“Utajiju..” nilimjibu pasipo kumuangalia.

“Nichumu basi..” Fadhili alizungumza.

“Utazoea…” nikajibu kwa sauti ya kudeka.

“Kidogo tu…”

“Nitakuchumu kesho..” nikazungumza kwa kudeka.

Fadhili aliachia tabasamu la matuamaini na kuondoka pasipo kuongeza neno lolote. Kwa upande wake aliweza kujiona mshindi kwa kuwepo na dalili zote za kupata kile alichokuwa anakitafuta kwa udi na uvumba. Wakati huo huo upande wangu nilijikuta katika mtihani mzito ambao sikuweza kufahamu ni namna gani ningeweza kuung’amua na kubaki salama.

******

Miongoni mwa watu ambao walikuwa wamefurahi sana baada ya mimi na mama kurudi nyumbani pale alikuwa ni kaka Imran.Furaha yake iliongezeka mara dufu baada ya mimi kuambatana na mama kurejea nyumbani pale.

Kama alivyokuwa akirejea mapema nyumbani kipindi kile ndivyo alivyoanza tabia hiyo mara tu mimi niliporejea ndani ya nyumba ile. Madai yake alikuwa akirudi nyumbani kwaajili yakupata chakula cha mchana.

Kwa upande wangu tabia ile haikuwa mzigo kwasababu niliona ni jambo la kawaida sana. Hivyo nilikuwa nikijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuhakikisha chakula kinakuwa tayari kila aliporudi nyumabni awe yeye ama mtu mwingine yeyote yule. Kwa ufupi nilitekeleza majukumu yangu kiufasaha zaidi.

Honi ya gari la kaka Imran ilinigutusha kutoka chumbani kwangu na kutoka moja kwa moja hadi getini ambako kama ilivyokuwa kawaida nilifungua geti na kaka Imran aliingiza gari ndani.

Siku hiyo kaka Imran alikuwa ametangulizana na mtu mwingine ambaye kwa haraka usingeweza kubisha kuwa alikuwa ni mfanya kazi mwenzie. Sikujali sana juu ya ugeni ule bali niliingia ndani na kwenda kumalizia kuandaa meza ya chakula.

Kaka Imran alifika moja kwa moja na mgeni hadi kwenye ukumbi wa kulia chakula. Macho yangu yalipomtazama vizuri mgeni yule yalipata kigugumizi huku moyo wangu ukikataa kuamini.

Mgeni yule alikuwa ni Sheby yule kijana niliyekutana naye ndani ya basi siku nilipokuwa nikisafiri kutokea Dar kuelekea kijijini kwetu Tanganyika. Sheby ndio yule kijana aliyejitambulisha jina lake kwa kirefu kuwa ni Shebughe, kijana huyo ndio yule ambaye nilimpigia simu na kujifanya ni mchumba wangu ambaye tulikuwa na mpango wa kufunga ndoa.

Sheby aliponiona naye alionekana kunikumbuka vizuri sana. Lakini nilimuwahi na kumkonyeza kwa ishara ya kumtaka akae kimya na asibainishe kufahamiana kwetu.

“Karibuni chakula..” niliwakaribisha kwa heshima kubwa kaka Imran na mgeni wake kisha nikavuta hatua kutaka kuondoka.

“We tumu..” kaka Imran aliniita.

“Abee..” nikaitika na kusimama kwa heshima kusikiliza wito ule.

“Tunashukuru kwa kutukaribisha chakula, lakini unaondokaje bila ya kutunawisha?” kaka Imran alihijo kwa sauti ya upole.

“Samahani kaka Imran” niliomba radhi na kusogelea meza ya chakula ambapo Kaka Imran na mgeni wake walifikia.

“Umemsalimia mgeni lakini?” alihoji kaka Imran kwa sauti ya upendo.

“Shikamoo..” nikasalimia huku nikijifanya simfahamu kabisa mtu yule.

“Marahaba mtoto mzuri hujambo enh?” Shebughe aliitikia salamu yangu bila hata ya aibu. Pamoja na kwamba nilikutana naye siku moja tu lakini nilifahamu wazi kuwa umri wake sikupaswa kumuamkia. Lakini nilifanya vile makusudi ili kuzuga tu mbele ya kaka Imran.

“Huyu anaitwa Sheby, nafanya naye kazi ofisini kwangu” kaka Imran alimtambulisha kijana yule.

“Karibu sana kaka Sheby” nikamkaribisha huku nikijifanya kumuonea aibu Shebughe.

“Asante sana Mrembo” Kijana Shebughe akanijibu huku akinitazama kwa jicho la uchu na kuhisi malengo yake yalikuwa yanakwenda kutimia.




“Sheby, huyu ndio yule msichana niliyekueleza kuwa nataka kumuoa” alizunguma kaka Imran kwa kujiamini.

“Oooh kumbe shemeji yetu ndio huyu! Hakika yupo vizuri” alizunuma Shebughe na kujifanya akinimwagia masifa.

“Basi mi naenda jikoni kuna kazi nataka kumalizia” niliungumza kwa kuinamisha shingo chini kuashiria kumezwa na aibu.

“Inaonekana ana aibu sana?” alihoji Shebughe kwa sauti ya chini.

“Hivyo ndivyo alivyo” alijibu kaka Imran kwa sauti ya chini.

Nilipokuwa nikiondoka Shebughe alijaribu kunitupia jicho la wizi na kuzidi kunipa thamani ya urembo.

Kitu ambacho kilikuwa kimemchanganya Shebughe ni kile kitendo changu cha kumpigia simu na kumwambia kuwa nilikuwa na mpango wa kufunga ndoa na yeye. Hadi kufikia siku hiyo hakuwa ameelewa sababu ya mimi kumpigia simu na kumuelea maneno yale. Hata hivyo alishindwa kufanya mawasiliano na mimi kwasababu sikuwa na simu na alipojaribu kupiga kwenye simu ya Bi. Fatma hakupata ushirikiano wa kutosha.

“Kaka huyu mtoto ni kisu aisee” alizunguma Shebughe kwa sauti ya chini.

“Nakwambia nikishafunga naye ndoa maisha yangu yatakuwa yamekamilika kila idara. Nampenda sana asee” alizungumza kaka Imran kwa majigambo.

“Umesema anaitwa nani vile?” Shebughe alihoji kuwea kuthibitisha hisia zake juu yangu kama ni kweli nilikuwa ni yule binti aliyesafiri naye kutokea Dar hadi Tanga.

“Anaitwa Bibie Tumu, au Mwantumu” alielea kaka Imran.

Jibu la kaka Imran lilimletea utata Shebughe kwasababu jina ambalo nilikuwa nimemtajia siku tulipokuwa tunasafiri ni Ndwadwa. Sasa jina la Mwantumu lilikuwa ni tofauti kabisa na jina hilo alilokuwa analifahamu yeye.

“Mwanangu umeokota dodo chini ya mnazi, sijawahi kuona House girl mzuri hivi” Shebughe alizungumza kwa msisitio.

“Huyu hapaswi kuwa House girl bali anatakiwa kuwa na House girl” aliungumza Kaka Imran kwa majivuno na majigambo.

Kule jikoni nilipokuwa nilijikuta nguvu zikiniishia. Siku nilipomdanganya kaka Imran kuwa nina mchumba nilimpigia Shebughe na kuweka loud speeker mbele za watu na Shebughe alidhihirisha uma kuwa mimi nilikuwa ni mchumba wake. Mwenyewe nilidhani mimi na yeye tusingewea kukutana tena daima milele. Sasa njia ya uongo imegonga mwamba kwa kijana yule kafika hadi nilipokuwa nikiishi. Sijui kungetokea kitu gani kwasababu hata yeye alikuwa akihitaji kuwa na uhusiano wa kimapeni na mimi.

Baada ya dakika kadhaa kaka Imran aliniita nikaenda kuwanawisha mikono huku kila mmoja akionekana kufurahishwa na mapishi yangu.

“Hakika haya mapishi ni ya kitanga. Chakula chako kitamu sana” Shebughe alinisifia nilipokuwa nikimnawisha kaka Imran mikono.

“Hiki ni chakula tu, unadhani chakula chake kitakuwaje?” alizungumza kaka Imran kwa mafumbo laini.

“Kwa kawaida sisi watu wa Tanga hatuna masihara katika kila idara” alizunguma Shebughe kwa majigambo.

“Watanga ni wazuri ila Tumu ametia fora" alizungumza kaka Imran huku akichukua kitambaa na kufuta mikono.

“Hakika toto limeumbika na linaleta mshawasha ndani ya moyo” Shebughe alizungumza huku akichukua kipande cha sabuni na kupaka kwenye mikono.

“Ukimiliki zigo kama hili hauwezi kuugua ugonjwa wa nguvu za kiume hasilani abadani!” kaka Imran alizunguma maneno ambayo nilihisi yakinidhalilisha kijinsia na kujikuta nikipatwa na aibu ya ukweli kabisa.

“Utauguaje sasa wakati dawa unayo ndani, kila ukimtazama unapona na mziki unaendelea” Shebughe alizungumza kwa msisitizo huku akinitupia lile jicho lake la kiwizi wizi.

Kaka Imran alipomalia kujifuta mikono akainuka na kuelekea chumbani kwake. Pale sebleni tukabaki mimi na Shebughe tukinawishana mikono.

“Imekuwaje sasa mbona kila ulichonieleza kilikuwa ni uwongo” Shebughe alihoji kwa sauti ya kunong’ona.

“Nimekudanganya nini?” nikahoji kwa sauti ya kunong’ona na mimi.

“We si unaitwa Ndwadwa, mbona leo wanakuita Tumu?” Shebughe alihoji kwa umakini.

“Kwani kuwa na majina mawili ni dhambi?” nikahoji.

“Mbona ulisema hauna mchumba, halafu leo jamaa nasema wewe ni mchumbaake?” Shebughe aliendelea kuhoji kwa kulalamika kama vile ametendewa dhambi.

“Yeye ndio amesema, umesikia mimi nimesema kitu?”

“Sikuile uliponipigia simu uliniita mchumba ulikuwa unamaanisha nini?” Shebughe alitumia mwanya ule kutoa lake la moyoni.

“Sahau hayo, sikuwa mimi. Umenifananisha” nilijibu kwa ufupi kwasababu niliona alipokuwa anaelekea kijana yule kulikuwa ni kwengine.

“Kama ni hivyo hata mimi bado nakupenda. Siwezi kukubali jamaa anyakue bahati yangu kirahisi rahisi” Shebughe akaunguma kwa msisitizo huku akionekana kumaanisha kwa kile alichokuwa anakizungumza.

“Acha upuuzi wewe!”

“Kama ni hoja ya kuoa hata mimi nitakuoa” Shebughe aliunguma kwa msisitizo.

“Shiiii!” nikamnyamaisha baada ya kusikia sauti ya mlango wa kaka Imran ukifunguliwa.

Nilikusanya vyombo na kuelekea jikoni na kuwaacha wageni wale wakijiandaa kuondoka kurudi kazini kwao.

*****

Miongoni mwa mambo ambayo yalikuwa yakinipa amani na faraja ndani ya nyumba ile ilikuwa ni tabia na mwenendo wa baba mzee Sekiza. Kusema kweli yule mzee alikuwa ni mtu mzuri sana, mwema, mpole na mwenye roho ya huruma. Nafikiri shetani tu ndio alikuwa amemuingilia kipindi kile na kujikuta akiingia katika majaribu na kutaka kutumbukia kwenye dhambi ya uzinzi.

Mzee Sekiza alikuwa akijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kukaa mbali na mimi. Hakuruhusu kabisa nafsi yake irudie kosa lililokuwa limejitokeza awali. Hakuwa tayari kuona familia yake inasambaratika tena kwasababu ya mambo ya kipuuzi ambayo yasingekuwa na maana yoyote katika jamii zaidi ya kashfa na kujishushia hadhi yake katika jamii.

Siku moja nakumbuka nilikuwa katika shughuli zangu za kila siku za nyumbani pale. Kwakuwa watu wote walikuwa wametoka kwenda kazini nilibaki peke yangu. Kutokana na hali ya joto la jiji lile la Dar es salaam nililazimika kupunguza mavazi na kujikuta nimebakia na sidiria huku kiunoni nikiwa nimejifunga kaka moja tu. Nilifanya kazi kwa uhuru zaidi na sikuteseka sana na lile joto la jiji. Wale wenyeji wa jiji lile watakuwa wanaelewa ninachokizungumza hapa.

Waswahili wanasema siku ya kutembea uchi ndiyo siku ya kukutana na baba mkwe. Huwezi kuamini ndugu msomaji, wakati nimejikunja nikisugua kapeti la kufutia miguu kumbe siku hiyo Baba alikuwa amepata dharura na kurudi nyumbani mapema.

Macho ya mzee Sekiza hayakuweza kuamini kilichokuwepo mbele yake. Masikini ya Mungu mzee wa watu alihisi mapigo ya miyo wake yakienda mbio. Aliweka mkono mdomoni akishangazwa na yale mauzauza aliyokuwa anayaona mbe la macho yake.

Mwenyewe nikiwa sina hili wala lile mtoto wa watu wa kitanga, nilikazana kusugua lile kapeti na kupelekea lile zigo langu zito kulewalewa utafikiri lilikuwa linataka kudondoka. Mbaya zaidi kwakuwa nilikuwa nikitumia nguvu zaidi kusugua kapeti lile kiuno changu kilibinuka juu zaidi na kuwa kama chura wa kihansi.

Mzee Sekiza alikumbuka kipindi kile nilipokuwa nimempatia nafasi ya kuushika mwili wangu na kuutomasa tomasa. Alitamani sana fursa ile ijirudie tena na kuhakikisha hafanyi tena kosa la kiufundi.

Masikini ya Mungu Zee la watu lilibaki limeuma kidole huku akikuna kichwa utafikiri kulikuwa na jambo zito sana lililokuwa likiutibua ubongo wake. Yale mandevu yake yakazidi kuchachamaa na kusimama utafikiri miba za nungunungu. Alitamani anirukie pale chini na kutuliza maruhani yaliyokuwa yamempanda.



“Mambo mazuri hayataki haraka, hapa lazima hekima itumike ili niweze kula tunda hili kiulaini” alizungumza Baba na kukunja kona kuelekea chumbani mwake huku akiniacha mtoto wa kike nikiendelea kujimwaya mwaya pale sebleni bila habari kama kulikuwa na mtu ananifaidi.

Nilisikia mlango wa chumbani kwa baba ukifunguliwa na kufungwa. Nilishituka sana na kuondoka haraka sana sebleni pale. Niliingia chumbani kwangu na kuvaa nguo zangu za kujistiri kisha nikarejea hadi kwenye mlango wa Baba na kusikiliza kwa makini kama kulikuwa na mtu ameingia.

Huku nikiwa na wasiwasi uliochanganyikana na hofu niligonga malango ule wa chumbani kwa Bi. Fatma taratibu huku nikisikiliza jibu. Hata hivyo sikuwa nimesikia sauti wala dalili yoyote ya kuwepo na mtu ndani mle.

Akili yangu ilinituma kusukuma mlango ule kuona kama kulikuwa na mtu ndani mle kwasababu nilikuwa nimesikia vizuri sana wakati mlango unafunguliwa na kufungwa.

Laahaula Walakuwata Illa Billahi Laaliyul Adhim! nilikutana macho kwa macho na Baba akiwa amevua nguo na kubakiwa na boksa tu Mungu wangu! Nikarudishia mlango haraka na kuondoka maeneo yale huku akilini mwangu nikiwa kama vile nimefanya kosa moja kubwa sana kuliko makosa yote ulimwenguni.

Moja kwa moja nilikimbilia chumbani kwangu na kujitupa kitandani. Nilijaribu kuwaza na kuwazua namna ambayo ningejitetea kwa kitendo kile. Ni kweli nilikuwa nimemkuta akiwa uchi lakini nitasema nilikuwa nachungulia nini? Jamani nyie ni kitu kigumu sana kikikukuta hasa kwa mtu ambaye unaheshimiana naye.

Nikiwa nimejilaza kitandani huku nikijaribu kutafuta namna ya kujitetea kwa kosa nilililokuwa nimelifanya la kuchungulia chumbani kwa mama na kumkuta baba akiwa na uchi, ghafla nikagutushwa na sauti ya baba ikiniita usawa wa chumbani kwangu.

“Mungu wangu, kibarua leo kimeota nyasi” nilijisemea huku nikijizoa zoa kutoka kitandani.

“We tumu..” baba aliita kwa sauti zaidi baada ya kuona siitoki chumbani mwangu.

Nilifungua mlango na kumkuta Baba amesiamam hatua kadhaa kutokea mlangoni kwangu.

“Shikamoo Baba” nikasalimia kwa hofu na mashaka.

“Pole mwanangu, nimeingia ndani bila kubisha hodi” mzee Sekiza alizungumza huku akinitazama kwenye macho kiasi cha kunifanya nipepese macho yangu na kutazama chini.

“Sikujua kama umerudi baba” nikazungumza kwa sauti ya hofu.

“Pole sana, ulifikiri umeingiliwa na mwizi nini?” Baba alijizungumzisha na kunifanya nipate ahuweni.

“Sawa baba” nikajibu kwa sauti ya heshima huku nikitazama chini.

“Lakini naona umekua siku hizi, uwe makini mwanangu na wanaume wakora sawa?” Mwanaume yule alizungumza kwa msisitizo.

“Ndio baba” nikajibu.

“Na hata hawa ndugu zako humu ndani uwe nao makini yasije yakajirudia makossa tena, sawa mwanangu?” mzee yule aliniusia.

“Ndio baba”

“Haya mimi narudi kazini, endelea na shughuli zako” Baba alizungumza na kuondoka kwa spidi akiniacha nimekodoa macho huku payo limenishuka mtoto wa kike.

Sikuweza kuelewa kama baba alikuwa ameniona jinsi nilivyokuwa nimejiweka kihasara hasara au laa, kwasababu ilikuwa ni vigumu kuingia chumbani mwake pasipo kuangalia pale nilipokuwa nikisugulia kapeti lile.

“Potelea mabali kama ameniona au haja niona atajua mwenyewe.” Nikajisemea na kwenda kuendelea na shughuli zangu.

Dada Mainaya ndiye aliyekuwa wa kwanza kurudi kutoka kazini na kama ilivyokuwa kawaida alinikuta jikoni nikiendelea na maandalizi ya chakula cha jioni.

“Wifiii” aliita dada Mainaya mara tu alipoingia jikoni.

“Shikamoo dada Mainaya” nikasalimia kwa heshima kubwa.

“Mimi napenda unite wifi bwana, mambo ya dada dada wala hayaninogei mimi” alizungumza Mainaya huku akitabasamu.

“Halafu wewe unapenda utani!” nikazungumza kwa kujichekesha chekesha.

“Kila siku mimi nakwambia kubali kuwa wifi yangu uachane na masuala ya uhouse girl hutaki shauri yako” alizungumza Mainaya huku akivuta kiti kilichokuwemo jikoni mle na kuketi.

“Acha basi bwana..” nikazungumza huku nikichukua kibao cha mbuzi na kukiweka chini tayari kwa kukuna nazi.

“Nipe basi kazi nikusaidie wifi yangu” Mainaya alizungumza kwa sauti ya upendo.

“Umetoka kazini bwana we pumzika tu” nilizungumza huku nikiketi kwenye kibao cha mbuzi na kuanza kukuna nazi.

“Leo nina habari njema kwako” alizungumza dada Mainaya huku akitabasamu.

“Nawewe kila siku hukosi habari.Haya nipe hiyo ya leo” nilizungumza huku nikiendelea kukuna nazi.

“Kila siku mimi nakwambia Imran anakupenda hutaki kuamini. Sasa leo nataka kuthibitisha maneno yangu” Mainaya alizungumza huku akifungua pochi yake.

Niliwacha kukuna nazi na kutumbua macho kwenye ile pochi alimokuwa ametumbukiza mkono. Dada mainaya alichomoa simu na kunikabidhi.

“Chukua mdogo wangu” alisema Mainaya baada ya kuchomoa simu ile na kuinyoosha kwangu kunikabidhi.

“Chukua ni ya kwako..” alizungumza Binamu kwa msisitizo.

Nilipokea simu ile na kuiangalia huku nikiwa sielewi nianzie wapi kuitumia. Kusema kweli ilikuwa ni simu nzuri sana. Ilikuwa imeandikwa Samsung sijui ngapi vile, lakini ilikuwa nzuri hadi nikajikuta nikitetemeka.

“Hiyo simu ipo full kila kitu, kuna laini humo, umejaziwa salio la mwezi mzima humo, na chaji umeshawekewa kazi kwako” Mainaya alizungumza kwa mbwembwe huku akijitikis tikisa kwa matumaini.

“Unasema nani ameninunulia?” nikahoji kwa umakini.

“Ni mchumbaako Imran” Mainaya alizungumza kwa msisitizo.

Jamani nyie duniani hapa kuna majaribu! Ni kweli kabisa nilikuwa nimeipenda ile simu, lakini sasa si ndo wanaseme sijui vishawishi sasa sikuelewa hata kitu cha kufanya.



“Imran hapendi uteseke kabisa” alizungumza Mainaya kwa msisitizo.

“Lakini dada kwanini kaka Imran anafanya haya yote?” nikahoji kwa umakini.

“Kwasababu anakupenda”

“Lakini mimi simpendi mbona!” nikazungumza kwa msisitizo.

“Mapenzi ndivyo yalivyo, ipo siku utampenda tu kama anavyokupenda yeye” Mainaya alieleza.

“Hapana dada mimi hiyo simu sitaichukua, irudishe tu kwa mwenyewe” nilizungumza kwa msisitizo huku nikiendelea kukuna nazi.

“Kwahiyo unataka kusema kakaangu amepoteza pesa zake bure?” Mainaya alihoji kwa ile sauti yake kavu aliyowahi kuitoa siku alipokuja kule Kijitonyama na kunikuta nyumbani kwa Bi. Fatma.

“Labda huelewi tu dada Mainaya, Imran hayupo kabisaaa moyoni mwangu” nikazidi kusisitiza.

“Unampenda nani Fadhili?” akahoji kwa msisitizo.

“Sina hakika sana” nikajibu kwa ufupi.

“Unajua wacha upuuzi! Nilikwisha kueleza wazi kuwa sahau kuhusu Fadhili” Mainaya akazungumza kwa jazba.

“Lakini wewe ndiye unayesema, mimi sikusema kuwa nampenda Fadhili” nikazungumza kwa kujiamini huku nikinyoosha mkono kumkabidhi ile simu yake.

“Sasa unampa nani hilo lisimu lako! Kama haulitaki si uje ulirudishe kwa mwenyewe!” alizungumza kwa jazba mwanamke yule.

“Wewe ndiye umelileta, tena kama nikiona mnanisumbua sana, nitamwambia Bi. Fatma” nikazungumza kwa sauti ya msisitizo ambayo hata mwenyewe hakuwahi kutegemea kama ni yule yule Mwanatumu aliyekuwa anamfahamu au ni Mwantumu mpya kutoka Tanga.

“Sasa chagua moja, kuolewa na Imran au kuondoka hapa nyumbani kwetu” Mainaya alizungumza kwa hasira na jazba zaidi.

“Siondoki na Imran simtaki!” nikazungumza kwa kujiamini baada ya kubaini mwanamke yule alikuwa na mkakati wa kunirudisha kule kwenye maisha yale ya kunyanyasika kwasababu ya mapenzi.

“Ahaa kama kuna mtu anakutia kiburi, ujue anakudanganya. Nitakupeperusha kwa upepo wa kisurisuri” alizungumza Mainaya kwa msisitizo na jazba.

“Usinitishe dada Mainaya, nipo hapa kikazi na sio kutafuta wanaume wa kunioa. Kama ni hoja ya wanaume hata kwetu wapo tena wanaume wanaojielewa” na mimi nikaporomosha yakwangu mtoto wa kike. Shenzi! Walikuwa wamezoea kuninyanyasa heti kwasababu ni House girl, Eboo!

“Mtoto unakumbuka niliahidi kukutenganisha na familia hii kwa gharama yoyote ile?” dada Mainaya alizungumza kwa kujiamini.

Maneno yake yalinifanya niangue kicheko cha dharau na kebehi huku nikiinuka kutoka pale kwenye kibao cha mbuzi kwaajili ya kuanza kuchuja nazi ile niliyokuwa nimekuna.

“We chekelea tu, siku moja utalilia” alisema Mainaya huku na yeye akiinuka kutoka pale alipokuwa ameketi.

“Usijidanganye Mainaya, futa kabisa hayo matumaini yako” nikazungumza kwa kujiamini.

“Siku nitakayokutoa humu ndani huto amini” Mainaya alizungumza.

“Umechelewa Mainaya, tena usipokuwa makini utatoka wewe na mimi utaniacha humuhumu” nilizungumza kwa kujiamini huku nikiwa sielewi kiburi kile nilikuwa nimekitoa wapi.

“Hivyo ndivyo unavyojidanganya?” Mainaya alisema.

“Haya tutaona mimi na wewe ni nani anayejidanganya” na mimi nikajibu kwa jazba vilevile. Kule kwetu Tanga wanasema Kama mbwai mbwai.

Nakwambia mwanamke yule alichukua simu lake na kutoka nalo mle jikoni kwa hasira utafikiri ameporwa hawara. Na mimi kule nyuma niliachia msonyo mrefu ambao ulinisaidia kushusha hasira zilizokuwa zimenipanda.

Wakati nikiendelea kufanya shughuli zangu huku nikiwa na hasira zangu, alifika Fadhili na kama ilivyokuwa kawaida yake alipitiliza moja kwa moja hadi jikoni kunisabahi.

“Mchumbaa!” Fahili aliita kwa sauti ya deko.

Nilisikia sauti yake ikiniita lakini sikutaka kugeuka wala kuzungumza naye kutokana na hali niliyokuwa nayo.

“Jamani mrembo nakuita unanichunia?” Fadhili alihoji.

“Naomba uniache Fadhili” nikazungumza kwa ufupi pasipo kumgeukia.

Fadhili alipoona vile akahisi pengine kulikuwa na kitu kinachonisumbua. Alinisogelea na kunichungulia usoni huku amenishika mgongoni.

“Mungu wangu! Mwantumu una tatizo gani?” Fadhili alihoji kwa kuhamaki baada ya kuona machozi yakitiririka mashavuni mwangu.

“Hapana sina kitu” nikajibu kwa sauti ya kulia huku nikifuta machozi.

“Huna kitu huku unalia! Hebu nambie ni kitu gani kinaendelea?” Fadhili alizidi kuhoji kwa msisitizo.

“Fadhili mimi naondoka hapa kwenu, siwezi kuendelea kunyanyasika kila siku” nikajikuta nikilia kwa kudeka.

Fadhili alinikumbatia na kichwa changu akakilazia kwenye bega lake. Huku akinipapasa mgongoni kuniliwaza.

“Ni nani amekunyanyasa?”

“Dada Mainaya hapendi kuniona kabisa humu ndani” nikazungumza kwa kudeka.

Fadhili aliniachia na kutoka jikoni mle kwa spidi na kuelekea moja kwa moja hadi kwenye mlango wa chumbani kwa dada Mainaya. Kule jikoni nikajikuta nikifarijika na kuachia tabasamu la faraja.

Nafikiri nilikuwa na chembehembe za kumpenda Fadhili pamoja na kwamba sikuwa nimepatia jibu la moja kwa moja kama nampenda au laa.

Kabla Fadhili haja bisha hodi kwenye chumba cha dada Mainaya mwenyewe alifika akitokea nje.

“Haya niko hapa unasemaje mdogo wangu?” alizungumza Mainaya kwa sauti ya upendo.

“Enhee njoo hapa nakutafuta sana” Fadhili alimsogelea Binamu na kumkamata mkono kwa nguvu na kuanza kumvutia kuelekea kule jikoni nilipokuwepo mimi.



“Umepatwa na nini Fadhili mdogo wangu?” Mainaya alihoji kwa mshangao.

“Kelele! Kuja huku” Fadhili alizungumza huku akimvuta mkono Mainaya hadi mle jikoni. Walipofika akamuachia mkono na kumtazama usoni.

“Haya niambie ni kitu gani unakitafuta kwa huyu binti?” Fadhili alizungumza huku akihema juu juu kutokana na hasira.

“Unataka kusemaje Fadhili?” Mainaya alijifanya kushangazwa na maneno ya Fadhili.

“Sikiliza Mainaya! Wewe huijui thamani ya huyu binti. Akiondoka hapa na wewe unajikata kwenu, mateso yanabakia kwetu” Fadhili alizungumza kwa ukali huku akitetemeka.

“Lakini Fadhili mdogo wangu..” dada Mainaya alitaka kuzungumza kitu.

“Nyamaza! Kuanzia leo sitaki kusikia huyu binti analalamika heti kwasababu yako. Nakwambia nitaichonga miguu yako hiyo!” Fadhili alizungumza kwa hasira.

“Unajua unanionea Fadhili” dada Mainaya alizungumza kwa kulalamika.

“Ondoka hapa!...nisije nikakubamiza na milango mie” Fadhili alizungumza kwa jazba zaidi.

“Fadhili mimi ni dada yako na nimetangulia kuliona jua ujue” alisema Mainaya kwa msisitizo.

“Kwahiyo?”

“Wewe ni dogo tu na utabaki kuwa mdogo wangu, tazama mchezo nitakaokuchezea. Mwenyee hutaamini maishani mwako” Mainaya akazungumza kwa jazba.

“Unajua usinitishe we mwanamke. Angalia sana tusije kuvunjiana heshima” Fadhili akazungumza kwa msisitizo huku akimuoneshea kidole dada Mainaya.

“Kama wewe ndiye unayemtia kiburi huyu kwa kujidanganya kuna kitu utakipata kutoka kwake, ni afadhali usahau” alisema Mainaya.

“Halafu nakwambia uondoke we unaendelea kubwabwaja, ngoja nikuoneshe” Fadhili alizungumza huku akivuta hatua kumsogelea zaidi dada Mainaya kwa lengo la kumtandika makofi.

Mainaya hakuweza kuendelea kusubiria Fadhili amporomoshee kipigo bali aligeuka na kuondoka mbio na kutuacha mimi na Fadhili mle jikoni. Fadhili akanisogelea na kunishika mikoni huku akinitazama kwa macho ya huruma.

“Pole sana mtoto mzuri, nitahakikisha unakuwa salama wakati wote na hakuna kiumbe wa kukusumbua” Fadhili alizungumza kwa msisitizo huku akinifuta machozi na kunipiga busu la shavuni ambalo kusema kweli nililipokea kwa moyo mmoja na kuhisi mwili wangu ukisisimka utafikiri ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kupigwa busu na mwanaume.

*****

Kitendo kile cha baba kunikuta nikifanya usafi huku nikiwa nimevalia kanga moja tu kifuani kilimtoa katika mstari. Alianza kuhisi msimamo wake ukivunjika na kuzalisha kitu kipya ndani ya ubongo wake.

Ni kweli kabisa Baba alikuwa ameapa kuto rudia tena ile tabia yake ya kuwataka kimapenzi wasichana wa kazi lakini kutokana na hali aliyokuwa amenikuta nayo siku ile alijikuta akipoteza muelekeo. Alikuwa akitumia muda mwingi sana kukumbuka tukio lile na kujaribu kujipa mamlaka ya kunimiliki. Kilichokuwa kikimkwamisha ni namna gani angeweza kunirudisha kwenye kishawishi hadi nikaridhia kuwa naye na kufanya alichokuwa anakidhamiria kwa siri.

Baada ya kuumiza kichwa kwa muda mrefu mzee yule alipata suluhisho la tatizo lake. Alipata mbinu ya kutumia ili aweze kuwa na mimi pasipo kuleta madhara yoyote yale katika jamii iliyokuwa inamzunguuka.

Baba akiwa kitandani pamoja na mke wake Bi. Fatma alitamani kufanya jambo lakini nafsi yake ilisita. Alijifikiria sana na mwisho wake akaamua kujichetua.

“Mke wangu” mzee Sekia aliita kwa sauti ya chini.

“Abee mume wangu” Bi. Fatma akaitika kwa sauti ya unyenyekevu.

“Unajua nakupenda sana mke wangu” mzee Sekiza alizungumza.

“Nakupenda pia mume wangu”

“Kuna jambo la msingi nataka unishauri”

“Nakusikiliza mume wangu”

“Nilikuwa nataka kufanya sunna”

“Sunna ya nini?”

“Ninaomba uniruhusu nifanye Nusrah” alizungumza mzee Sekiza kwa sauti yakukata kata.

Mama alijiinua kutoka pale kitandani na kuketi kitako kama vile hakuwa amesikia vizuri maneno ya mume wake.

“Hebu rudia unasemaje vile?” mama akahoji kwa msisitizo.

“Naomba uniruhusu nioe mke wa pili” alizungumza baba kwa sauti ya upole.

“Kuna kitu chochote umekikosa kutoka kwangu?” alihoji mama kwa sauti ya upole.

“Hapana mke wangu, lakini si unajua dini yetu inaruhusu kuoa hata wake wanne” baba alizungumza.

“Unajifanya unajua dini wakati hata msikiti hujui upo mtaa gani!” alisema mama kwa hasira.

“Kama nimeanza kusimamisha dini kwanini usinitie moyo?”

“Wacha masihara na Mungu we mwanaume, dini haisimamishwi kwa kuoa” mama alizungumza.

“Kwahiyo unaniambiaje sasa?”

“Nimekataa…” alijibu mama na kujilaza huku akigeukia ukutani na kumpa mgongo Baba.

“Hilo ndilo tatizo lenu wanawake, usiposhirikishwa unalalamika. Ukishirikishwa unaleta kiburi” baba akazungumza kwa jazba.

“Dini inasema mke wa pili anaongezwa kwa ridhaa ya mke aliyetangulia” mama alizungumza.

“Kwahiyo unataka kusemaje?”

“Naomba uniruhusu niongeze mke wa pili” Mama alizungumza kwa sauti kavu

“Mimi nikiwa mke wako, sijaridhika uongeze mke wa pili” mamaalizungumza kwa sauti ya upole lakini yenye msisitizo.

“We mwanamke utakuwa chizi. Sasa utake usitake lazima nioe mke wa pili” Baba alizungumza kwa msisitizo.

“Labda kama sio mimi” Mama akasisitiza kauli yake.

“Nitaoa sasa, tena naoa katoto kadogooo” alizungumza Baba kwa lengo la kumuumiza mama.

“Tumekuzoea kwani nani asiyekujua” mama alizungumza huku akiwa amejifunika shuka kuanzia miguuni hadi usoni.

“Laitani ungemjua mwanamke mwenyewe nafikiri ungefurahi sana kwa maana atakuheshimu na kukuthamini pia” Baba alizungumza kwa msisitizo.

“Sitaki hata kumjua”

“Wala siendi mbali mke wangu nataka kuoa humuhumu” Baba alizungumza kwa upole.

“Humu humu wapi?” alihoji mama kwa mshituko kidogo huku akihisi hali ya hatari katika ndoa yake.

“Humu ndani!” baba alijibu kwa msisitizo.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG