Chombezo : Housegirl Wa Kitanga
Sehemu Ya Tatu (3)
“Kama njaa inakuuma si uende mezani nimeshaandaa chakula?”
“Sitaki chakula chako”
“Kumbe unataka chakula cha nani?”
“Nataka kunyonya maziwa” Fadhili alizungumza huku akichezesha chezesha miguu kwa kupiganisha mapaja yake na macho yake yakiwa kifuani kwangu huku midomo yake akiig’atang’ata kwa hamasa.
“Maziwa gani?”
“Si hayo hapo! Ona yanavyo vutia”
“Mnh Fadhili wewe!”
“Sijui nani kakuambia kuwa ukivaa hivyo huwa unapendeza. Leo umenifurahisha sana Mwantumu, uwe unavaa hivihivi” Fadhili alizungumza huku nikimuona akimeza mate ya tamaa kwenye koromeo lake.
Maneno ya Fadhili yalinifanya nijihisi kama vile nilikuwa nimemwagiwa maji yabaridi mwilini. Kusema kweli nilikuwa nampenda sana mwanaume yule lakini yeye ndio alikuwa anajifanya haelewi. Sasa nikaona siku ile mwenyewe ameingia mtegoni. Kwa kiasi fulani nikaanza kumshukuru dada Bupe kwa ushauri wake wa kuvaa nguo zile na kunifichia nguo zangu za heshima.
“Nikwambie Fadhili” Nilizungumza huku nikimshika kidevu.
‘Enhe….”
“Twende chumbani kwangu” nikazungumza kwa sauti ya kubembeleza
“Inuka basi twende” kaka Fadhili alionekana kama vile alikuwa amechanganyikiwa. Aliniinua na niliposimama akanipiga busu la kwenye midomo. Nikahisi mwili ukisisimka. Nikamkumbatia na kumbana kwanguvu.
“Oooooh!...... Tumuuu!” nikamsikia akitamka maneno hayo kwa sauti ya kutokea kooni na kuzuiwa kidogo kwenye ulimki kabla ya kuachiwa taratibu kwenye midomo yake. Kama nilivyofanya mimi na yeye akanivuta na kunibana zaidi huku mikono yake ikiwa imekikamata vyema kiuno changu.
Pumbavu kabisa, nikajikuta nikikasirika ghafla na kunga’ta meno yangu kwa hasira.
Ndugu msomaji huwezi kuamini hii sasa ni mara ya tatu, kila jaribio la mauaji lilipokuwa likitaka kutokea honi za magari zilikatisha zoezi. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa nilipokuwa na Fadhili.
Sote wawili tulishituka kutoka kwenye lile pozi tulilokuwa tumekaa na Fadhili. Tulikurupuka mithili ya paka aliyefumwa akiramba kijungu cha mboga jikoni. Nilimuona Fadhili akikurupuka na kuelekea chumbani kwake. Namimi kwa haraka sana nilijiinua na kuuendea mlango wa jikoni ambako nilitoka nje na kuelekea nje kufungua geti.
Nilikuwa kama vile zezeta, sijui teja, au zombie kutokana na akili yangu pamoja na uchovu niliokuwa nao kutokana na shughuli ambazo nilikuwa nimekabiliana nazo tangu asubuhi ya siku hiyo.
Nilipofungua geti mama aliingiza gari na kupaki kisha akaniamuru nisiondoke. Niliogopa sana hasa kutokana na mavazi ambayo nilikuwa nimeyavaa yalikuwa ni tofauti na yale ambayo mama alizoea kuniona nayo. Lakini pia hali yangu niliyokuwa nayo nikahisi pengine angenishitukia kwa kujaribu kuvunja amri ya sita na wanaume wa familia ile.
Mama Alipoteremka kwenye gari alinitanzama kwa jicho la udadisi huku akiwa ameshika kiuno na funguo za gari ameningi’iniza kwa kuzizunguusha kwenye kidole cha kati mkono wa kushoto.
“Mwantumu” akaita kwa sauti ya chini.
“Abee mama” nikaitika kwa heshima huku macho yangu yakiangalia chini kwa aibu. Nilikuwa nahisi kama vile purukushani zote zilizofanyika ndani mle kuanzia asubuhi mama alikuwa ameniona, kumbe ulikuwa wasiwasi wangu tu. Nikasikiliza kwa makini alichokuwa anataka kukizungumza mama.
“Hivi naota au ni macho yangu?” alizungumza mama huku akinikazia macho kwa makini zaidi.
“Abee mama” nikaitika kwa wasiwasi huku nikiwa bado kuelewa mama alikuwa anamaanisha nini.
“Wewe ni Mwantumu ninayemfahamu mimi au ni mtu mwingine?”
“Kwanini mama?”
“Unaniuliza kwanini! Umeanza lini kuvaa nguo za hivyo?” Mama alihoji kwa makini na wasiwasimkubwa. Ndio lazima awe na wasiwasi kwasababu alikuwa anaifahamu vizuri sana familia yetu kule kijijini Tanganyika. Hakuwahi kutegemea kama siku moja angeweza kunikuta nikiwa nimevaa mavazi kama yale. Wakati wote alikuwa akiniona nimevaa magauni marefu na kichwani nimejitanda kwa ushungi ama khanga ndefu.
Basi lile swali lake likanifanya nipoteze muelekeo kabisaaa, Nikapeleka mkono kichwani na kujikuna pasipo kujibu kitu. Sasa ningejibu ninindugu msomajihebunisaidie, hakuna.
“Si nakuuliza wewe, au umekuwa kiziwi?” mama akahoji kwa sauti ya ukali kidogo.
“Aam mama..mimi…nina, nina…” nilishindwa hata kujitetea kwa kuzungumza uongo.
“Hee! Hii ya leo kali” mama alizungumza huku akipiga piga makofi kuashiria mshangao.
Nilibaki kimya huku nikiwa nimetawaliwa na aibu na haya. Unafikiri ndugu msomaji ningezungumza nini? Au ningejitetea vipi mbele ya mwanamke yule ambaye yeye pekeyake ndio hakufurahishwa na mavazi yangu, wengine wote waliyapenda na kunisifia nimependeza.
“Kwanza hebu sogea hapa” alizungumza mama kwa msisitizo huku akiniita kwa mdomo pamoja na ishara ya mkono.
Nilishituka kidogo na kumtazama kwa kuibia huku nikijawa zaidi na wasiwasi, nikaona sasa kiama kilikuwa kimenifikia, kiranga chote kwisha, uchovu wote kwisha, ulegevu legevu wote kwisha.
“Hebu niangalie usoni unakwepesha nini?” mama alizungumza huku akinishika kidevuni na kuniinua kichwa changu nimuangalie usoni.
“Haya niambie, umetoa wapi hizi nguo?” mama aliendelea kuzungumza kwa sauti ya chini lakini iliyokuwa imejaa msisitizo na ukali.
Niliinama chini huku nikihofia kumwambia kuwa nilikuwa nimenunuliwa na kaka Imran. Ningeanzia wapi unafikiri kumtaja kaka Imrani? Thubutuu! Hata akili ya kujiongeza nikose.
“Si nakuuliza wewe?” mama alizungumza kwa sauti ya juu zaidi baada ya kuniona nimekaa kimya.
Mungu hamtupi mja wake ndugu msomaji, baba aliweza kusikia mke wake akinihoji maswali yale yaliyokuwa yakihitaji akili nyingi sana kuweza kuyajibu kwa ufasaha.
“Kuna nini tena?” baba alihoji huku akiwa amesimama mlangoni.
“Sekiza mume wangu umeona hiki kituko?” mama akazungumza huku akinioneshea kidole pale nilipokuwa nimesimama.
“Wewe mwanamke unawezaje kumuita mtoto wa mwenzako kituko?” Baba alizungumza kwa sauti kali huku akionekana wazi hakuwa amependezwa na kauli ile ya mama.
“Inamaana unaona sawa tu hivi alivyofanya” mama alihoji huku akiwa amepunguza jazba kutokana na kukatwa makali na mume wake.
“Amefanya nini?”
“Inamaana mume wangu huoni mambo haya anayoyafanya huyu binti, kweli mume wangu?”
“Mambo gani sasa, si uzungumze?” baba akazidi kuzungumza kwa ile sauti yake ya ukali.
“Haya mavazi na Mwantumu ni wapi na wapi?” mama akazungumza kwa kulalamika na kuhisi mume wake alikuwa akimuona mkosaji.
“Ah! Kama ni mavazi si maamuzi ya mtu bwana, utamlazimishaje mtu kuvaa mavazi ambayo hayapendi” Baba alizungumza kwa sauti ya polepole.
“Lakini mume wangu, wazazi wake wakimkuta hivi binti yao si itakuwa uhasama mkubwa?” mama alijaribu kufafanua na kuitetea hoja yake ionekana kuwa na nguvu.
“Hakuna bwana, huyo naye ni mtu mzima anafahamu bayana zuri” Baba aliendelea kuzungumza kwa kunitetea.
Jamani nyie kumbe baba alikuwa na roho nzuri kiasi kile, sikuweza kuamini kwakweli. Kama wababa wote Tanzania wangekuwa na roho kama ya mzee Sekiza, nafikiri nchi yetu ingekuwa na maendeleo. Mungu ambariki baba kwa roho yake ile.
Wakati baba na mama walipokuwa wakiendelea kunijadili, Fadhili naye akafika kutokea ndani na kusimama hatua chache kutokea pale tulipokuwa.
“Heti Fadhili mwanangu, hebu nisaidie hili jambo” mama alizungumza baada ya kumuona Fadhili amefika pale.
“Kuna nini mama” Fadili alihoji kwa wasiwasi baada ya kuniona nimejiinamia kwa wasiwasi mbele ya watu wale.
“Hivi huyu Mwantumu ndivyo alivyokuja hivi?” alizungumza mama.
“Kwani amekuwaje mama?” Fadhili akahoji kama vile hakuwa ameelewa alichokuwa anakimaanisha mama.
“Hizo nguo kule kijijini kwao anaweza kuvaa kweli?” mama alihoji kwa msisitizo.
“Ah kule ni kijijini mother, huku ni mjini mwache aendane na mazingira” Nikamsikia Fadhili naye akizungumza kwa kunitetea.
“Inamaana na wewe unaunga mkono upuuzi huu?” mama akazungumza kwa mshangao.
“Sio hivyo mama, mbona sister Naya anavaa hivyo hivyo?” Fadhili alizungumza kwa kumtolea mfano binamu yake Mainaya.
“Mainaya ni binti yetu, lakini huyu ni mtoto wa watu Fadhili” mama alizungumza kwa msisitizo.
“Mama nawe unapenda ku-complicate mambo ambayo hayana hata maana” Fadhili alizungumza na kumfanya mama kupoteza makali yote aliyokuwa ameingia nayo.
“Njoo uchukue mizingo hii upeleke ndani” mama alibadilisha mada na kuzungumza huku akitoa mifuko iliyokuwa na vyakula ndani na kuiweka chini. Huku nikiwa na aibu kibinti cha watu niliinama na kuchukua mizigo ile na kuipeleka ndani.
Muda wote huo baba alikuwa amesimama kimya akimsikiliza mke wake Bi. Fatma alivyokuwa akibishana na Fadhili. Kila mara alikuwa akitoa tabasamu hasa Fadhili alipokuwa akimjibu mama yake. Alipoona mama amepoa na kubadilisha mada, baba akajivuta taratiibu kuingia ndani.
Nilishukuru sana uwepo wa Baba na Fadhili katika sakata lile, sijui ingekuwaje kama siku hiyo ningekuwa pekeyangu nyumbani pale. Nilipokuwa naingiza mizigo ile ndani nikamtazama Fadhili kwa jicho la kuibia. Kumbe Fadhili naye alikuwa akinikodolea macho muda wote huo, hivyo nilipomtazama tu, macho yetu yakakutana. Fadhili alibonyeza jicho moja kunikonyeza na kuachia tabasamu kwa mbali ambalo lisingeweza kuonekana na mtu mwingine yoyote zaidi ya mimi. Namimi baada ya kuona mwanaume niliyekuwa nampenda akinikonyeza kimahaba nami nikamjibu kwa kuuma midomo yangu ya chini na kuunganisha na tabasamu huku macho nikiyazunguusha utafikiri nilikuwa nataka kukata roho.
Nilipokuwa nikiingia ndani na mizigo huku nikiwa nimejawa na furaha ya kuuteka moyo wa Fadhili nikakutana tena na Bi. Fatma amesimama kwenye korido akinisubiri. Kwa jinsi alivyokuwa amesimama kwa hasira nikapatwa na hofu tena.
“Hivi wewe unanitafuta nini?” mama lihoji kwa hasira.
“Kuna ninitena mama?”
“Hivi unajua kilichokuleta hapa ndani?” alizungumza mama kwa hasira.
Mnh! Ukiwa na mkosi una mkosi tu, sasa nimemkosea nini tena Bi. Fatma jamani, au kazini kwake walikuwa wamemvuruga? Ah! Kusemakweli hata sikumuelewa. Maana yale ya nje tulikuwa tumeyamaliza.
“Si nakuuliza wewe, usinitumbulie macho kama mwizi” alifoka mama na kunifanya nishituke kidogo.
“Tangu asubuhi umefanya kazi gani?” mama aliendelea kuhoji na kunifanya nibaini kosa langu.
Ni kweli kabisa siku hiyo sikuwa nimefanya kazi yoyote ile zaidi ya kulala na kufanya mambo mengineyo ambayo sikupaswa kulaumiwa mimi. Hapa naomba nieleweke vizuri ndugu msomaji. Mtu wa kwanza kulaumiwa angekuwa ni kaka Imrani, kama asingeingia chumbani kwangu usiku, wala nisingechelewa kuamka na kusababisha watu wasinywe chai asubuhi, Lakini Baba naye pia alikuwa wa kulaumiwa bila ya kumsahau mwanaume kipenzi cha roho yangu Fadhili. Ndio wote hao walikuwa wamechangia kuharibika kwa siku yangu hiyo.
“Hivi ulimpikia Baba yako chai asubuhi?” Mama alihoji swali ambalo lilikuwa gumu sana kulijibu kwasababu sikuwa nimepika chai kama alivyokuwa amenisisitiza asubuhi wakatia anaondoka.
“Nakuuliza wewe kunguru, usiniangalie kama video”! Jamani nyie mwanamke yule aliendelea kuwaka kama kifuu. Sikuwahi kumuona Bi Fatma akiwa amekasirika kiasi kile hata siku moja tangu nilipokuwa nimeingia ndani mle. Nakwambia mwanamke yule alikuwa akitetemeka kwa hasira. Inawezekana kile kitendo cha Baba na Fadhili kule nje kunitetea ndicho kilichompandisha hasira zaidi.
Wakati nimezubaa nikiendelea kutafakari namna ya kujitetea, nikashitukia nimekamatwa na na Bi Fatma na kutikiswa kama vile dawa ya kifua ya maji. Mwanamke yule alikuwa amekusudia kunishikisha adabu siku hiyo. Alinyanyua mkono wake wa kuume juukwa lengo la kunitandika kofi maridhawa kwenye shavu langu la kushoto. Sasa nikahisi kifo kiliwa halali yangu siku hiyo, ikabidi niinamishe kichwa kusubiria maumivu makali.
“Mama unafanya nini?” nikasikia mtu akizungumza kwa sauti ya ukali.
Nilipoinua macho yangu, nikamkuta kaka Imran ameukamata mkono wa mama kuuzuia kutua kwenye shavu langu.
Sikuweza kuamini kwa kile kilichokuwa kimetokea. Hata sijui kaka Imran alikuwa ametokea wapikwasababu muda wote huo alikuwa hajarudi kutoka kazini. Nikamshukuru muumba kwa muujiza aliokuwa amenitendea kwa wakati mwingine.
“Imran niache nimfunze kidogo huyu mshenzi” alizungumza mama kwa hasira huku akiuvuta mkono wake kutoka kwa kaka Imran.
“Kwani ni kitu gani kinaendelea mamaangu?” Imranalihoji huku akiwa bado ameukamata mkono wa mama.
“Tena afadhali umerudi mwanangu, maana humu ndani naonekana wa hovyo kwaajili ya hiki kikunguni” Mama alizungumza huku akiwa ameachiliwa mkono na kaka Imran.
“Kumetokea nini?” Kaka Imran aliendelea kuhoji kwa umakini.
“Hivi leo umekunywa chai asubuhi?” mama alihoji.
“Sikunywa chai, lakini ni kwasababu nilikuwa na haraka sana” kaka Imrani alizungumza kwa kuongopa huku lengo lake lilikuwa ni kunitetea.
“Sawa lakini tangu asubuhi hakuna kazi yoyote ile ambayo ameifanya humu ndani. Vyombo vichafu, choo kichafu, sebule ndio kama unavyoiona vile hata kupangwa pia ameshindikana” mama alieleza.
“Lakini mama umemuuliza kama alikuwa anaumwa?”
“mgonjwa yuko wapi? Huyu mburumundu ndio mgonjwa? Mama alizungumza kwa mshangao kiasi cha kumfanya kaka Imrani kunigeukiamimi kwa hasira.
“Wewe unafanya utumbo gani?” Kaka Imranalihoji kwa hasira huku akiwa amenikazia macho. Tulipokutanisha macho yetu, kaka Imrani akanikonyeza kuashiria nisizungumze kitu hochote.
“Si umeona kalivyo kajeuri, yani unakauliza kamekaa kimyaaa kiburi kimejaa” alizungumza mama baada ya kuona kaka Imran alikuwa upande wake.
“Wewe si nakuuliza, kwanini unafanya hivi?” Kaka Imrani akajifanya kupandisha hasira.
“Nilikuwa naumwa” nikajaribu kujitetea
“Muongo! Wewe asubuhi si nimekuuliza ukaniambia mzima?” mama alidakia baada ya kuniona najaribu kujinasua kwa mara nyingine.
“Sikiliza wewe, naomba usimpigishe kelele Bimkubwa tena, na ukirudia utapata tabu sana” alizungumza kaka Imrani kwa msisitizo.
“Sawa kaka,siwezi kurudia tena” nikazungumza kwa sauti ya chini huku nimejikunyata kwa woga.
“Haya toka hapa!” kaka Imran aliniondoa kwa staili hiyo.
Kama vile nimeachiliwa kwa msamaha wa Rais kutoka kwenye kifungo cha maisha jinsi nilivyoondoka pale.
Baada ya mimi kuondoka kaka Imran akamgeukia mama yake na kumpoza.
“Basi mama naomba umsamehe, unajua foolish age inamsumbua yule” alizungumza kaka Imrani kwa sauti ya upendo.
“Unafikiri mimi nina shida naye, nilikuwa namkanya tu kama mwanangu” mama alizungumza huku akionekana wazi hakuwa na kinyongo tena juu yangu.
******
Asubuhi iliyofuata nakumbuka niliamka mapema sana na kufanya maandalizi ya watu kwenda kazini. Baada ya hapo niliendelea na shughuli za kufanya usafi. Pamoja na kwamba nilifanya kazi zote hizo mapema sana lakini akili yangu haikuwa ya kawaida kabisa. Nilihisikulikuwa na mzigomkubwa sana katika ubongo wangu uliokuwa unahitaji msaidizi wa kuubeba.
Nilipohakikisha nimemaliza kazi zangu zote ndanimle nikatoka kwenda mgahawani kwa dada Bupe. Kwakuwa haikuwa kawaida yangu kwenda mgahawani pale mida kama ile dada Bupe alinishangaa sana aliponiona. Akanitazama kwa sekunde kadhaa kama vile alikuwa akisikiliza shida ambayo ilikuwa imenipeleka.
“Shikamoo da Bupe” nilisalimia mara tu nilipomkaribia.
“Marahaba hujambo?”
“Sijambo, mbona wanitazama hivyo?” nilihoji.
“Nashangaa leo asubuhi sana” alisema dada Bupe.
“Kwani kuna ubaya wowote?”
“Mnh hakuna ubaya wowote lakini saa hizi! Saa moja na nusu upo hapa!”
“Dada Bupe na wewe mbona mie sioni hata kitu cha kushangaza” nilizungumza huku nikivuta kiti kilichokuwepo karibu na mlango wa jikoni na kuketi.
“Sawa, mgeni njoo mwenyeji apone” alizungumza dada Bupe huku akiingia jikoni.
“Ushaanza hivyo, mwenzako nimekuja kupumzika huku sio kufanya kazi” nikazungumza kwasababu nilikuwa naelewa kuwa mara zote ninapokuwa pale dada Bupe huwa ni lazima anipe kazi ya kufanya. Kama ambavyo nilikuwa nawaza ndivyo ilivyokuwa. Dada Bupe alipotoka jikoni alikuwa mkononi ameshika ndoo iliyokuwa na mchele.
“Haya mama kazi kwako” alizungumza dada Bupe huku akiweka chini ndoo ya mchele aliyokuwa amebeba.
“Haaa! Mi nitakuwa siji kwako dada Bupe, ukiniona tu lazima unipe kazi” nilizungumza huku nikiutazama ule mchele ndani ya ndoo.
“Hebu wacha uvivu wako mtoto wa kike, kesho tu unaolewa usije ukatutia aibu kwa mumeo” Dada Bupe alizungumza huku akiinama jikoni kugeuza maandazi yaliyokuwa yanachemka kwenye mafuta.
“Haa mie mwenzio siolewi leo wala kesho” nikasema kwa matani huku nikichukua ungo uliokuwepo umening’inizwa ukutani.
“Usiolewe una kasoro gani?”
“Mie mwenzio bado mtoto” nikasema huku nikichota mchele kidogo kutoka kwenye ndoo na kuuweka kwenye ungo.
“Kefuleee Mtoto nani!......Wewe au unazungumzia nani?” dada Bupe alizungumza pasipo kunitazama usoni huku akitoa maandazi kutoka kwenye karai na kuyamimina kwenye sufuria.
“Mimi ndio mtoto, hata maji naita mma” nikasema huku nikitabasamu na macho yangu yapo kwenye ungo kutafuta mawe na chuya.
“Una utoto gani wewe wakati unatakwa na hata mianaume mizee” dada Bupe alizungumza kauli yake hiyo na kunifanya nishtuke kidogo. Nilihisi mzee aliyekuwa anazungumziwa na dada yule hakuwa mwengine bali ni baba mzee Sekiza. Kumbe nilivyoshituka dada Bupe aliniona.
“Unashituka nini sasa? Au nimekugusa?” alihoji dada Bupe huku akiweka maandazi mabichi kwenye karai.
“Akaa hakuna chochote”
“Kwanza usijifanye mtoto hapo, kuna mkaka amekuja anasema anakupenda” alizungumza dada Bupe.
“Mkaka gani?”
“Anakaa hapo Hosteli”
“Mnh Mwanafunzi?”
“Vipi kwani we unataka walimu?”
“Mie sitaki yeyote yule” nilizungumza huku mkono wangu wa kulia ukichangua changua mchele kwenye ungo uliokuwa mapajani mwangu.
“Wacha ushamba wako wewe, wanafunzi wa chuo wanapesa kama nini”
“Mnh!....” niliguna huku nikihisi kushawishika na maneno ya dada Bupe.
“Unaguna nini?”
“Huyo kaka ni mzuri?”nilihoji.
“Aa we, kaka wawatu ni Handsome la nguvu”
“Lakini naogopa”
“Unogopa nini na wewe wacha mambo ya kijijini!”
“Sio hivyo dada Bupe, je nikipata ujauzito?”
“We yule msomi hawezi kukupa ujauzito, anaelewa afanye nini ili kuzuia mimba zisizo tarajiwa” dada Bupe alizunguza kwa kumsifia kaka huyo.
“Anaitwa nani?”
“Endru”
“Nani?”
“Endrus”
“Jina gumu” nilizungumza huku nikivuta taswira ya mwanaume huyo ndani ya ubongo wangu. Dada Bupe alinitazama akatoa tabasamu, namimi nikampokea kwa kumpatia lakwangu zito huku nimelegeza macho.
“Atakuja saa ngapi nataka nimuone kama tunaendana” Nilizungumza
“Anaweza kuja kunywa chai kama leo hana kipindi cha asubuhi” dada Bupe alieleza.
“Ngoja nimsubiri kwa hamu” nilizungumza huku nikimimina mchele kwenye ndoo nyingine iliyokuwa tupu pembeni kando yangu. Nilichota mchele mwingine kutoka kwenye ndoo kubwa na kuuweka kwenye ungo. Nikaanza kuusambaza kwa vidole vya mikono yangu kutafuta mawe na chuya.
Dada Bupe alijikohoza kidogo kuashiria kuwa alikuwa anataka kuzungumza kitu, niliinua shingo na kumtazama.
“Haya niambie jana ulivyoenda na zile nguo zako ulibabuka sehemu?” Dada Bupe aliuliza swali ambalo lilinishitua sana moyo wangu. Mwenyewe kwa kiasi fulani nilikuwa nimeshasahau mambo yaliyopita. Nikatulia kwa sekunde kadhaa nikawa kama vile nimepigwa na shoti ya umeme.
“Vipi mbona hivyo?” alihoji dada Bupe.
“Mnh! Umeniletea balaa dada wewe!”
“Umefokewa?”
“Si afadhali ningefokewa tu nikaachwa”
“Kumbe balaa gani sasa?”
“Mwenzangu kaka Imrani aliponiona nimevaa vile si akaanza kunitaka” nilizungumza kwa sauti ya chini kama vile kulikuwa na watu wengi nikawa naogopa wasitusikie, kumbe tulikuwa wenyewe wawili tu jikoni.
“Enhe usiniambie!” alihoji kwa shauku.
“Yaani dada wewe nimepata wakati mgumu mimi”
“Wakati mgumu! Kivipi sasa?”
“Unajua namheshimu sana kaka Imrani, sikutegemea kama angekuwa na mawazo kama yale” nikazungumza kwa msisitizo.
“Kwani anayeheshimiwa ndio hana moyo wa kupenda?”
“Mnh lakini sasa yule si ni kaka yangu?”
“Kaka yako umezaliwa naye?”
“Hata kama lakini mi namheshimu bwana”
“Unajua una bahati sana mdogo wangu!” alizungumza dada Bupe huku akiepua karai la maandazi na kuliweka chini. Alikuwa amekwisha maliza kukaanga maandazi.
“Bahati?” nikahoji kwa mshangao.
“Bahati ndio, we unadhani hapo ndani wamepita wadada wa kazi wangapi, lakini sikuwahi kusikia Imrani akimtongoza hata mmoja kati yao” dada Bupe alieleza.
“Kwahiyo dada unanishaurije juu ya hilo?” nilihoji huku nikimtazama kwa makini ili kuweza kupata ushauri kutoka kwa mtu ambaye alikuwa amenizidi sana umri.
“Sikiliza mdogo wangu, hiyo ni bahati ya kuokota embe dodo chini ya mnazi. Kama anakutaka we mkubalie tu, we mwenyewe si umeona mavazi aliyokuletea. Unafikiri ukimkubalia atakuletea vitu vingapi?” dada Bupe alizungumza kwa msisitizo.
“Je mama akigundua?”
“Hawezi kugundua bwana, kwani we mtoto mdogo!” alisema dada Bupe huku akifuta futa kopo la kuwekea sukari kwa kitambaa.
Nilivuta pumzi na kuzijaza kifuani kisha kwa mkupuo nikazimimina nje kupitia mdomoni. Nilitegemea dada Bupe angenipa ushauri wa namna ya kumuepuka kaka Imran, badala yake akazidi kunitumbukiza kwenye dimbwi la mahaba ya kaka yule niliyekuwa namheshimu kupita maelezo.
Nikatamani nimueleze shughuli na matukio yaliyonitokea siku iliyopita lakini moyo ulisita. Unajua ndugu msomaji sio kitu cha kawaida kwa watu wa tatu tena wa familia moja kutaka kukutia majaribuni ndani ya siku moja tena kwa masaa machache tu. Kwakweli katika maisha yangu sitokuja kuisahau siku ile.
“Vipi mbona kimya sana?” dada Bupe alihoji huku akipita na kuelekea mgahawani kuwasikiliza wateja. Nilitabasamu tu kisha nikaendelea kuchambua mchele huku shingo yangu nikiwa nimeipindisha upande kidogo.
“Enhe niambie dogo langu la kitanga” dada Bupe alizungumza huku akirejkea jikoni na kuchukua chenchi kwenye kopo alilokuwa anahifadhia pesa. Mimi pale nilipokuwa nimekaa niliendelea kutabasamu pasipo kutoa neno lolote.
Dada Bupe alitoka tena kwenda mgahawani, baada ya dakika chache alirejea na kikombe cha chai mkononi.
“He! Mteja wako anafriza mdomoni nini?”
“Kwanini?”
“Mara hii keshamaliza kunywa chai!”
“Hamna bwana huyu ni mteja mwengine, yule amekwisha ondoka” dada Bupe alizungumza huku akicheka.
“Anhaa nilifikiri ndo amebugia mara hii”
Dada Bupe aliweka kwenye beseni vyombo vile na kuanza kuviosha. Namimi pale kwenye kigoda nilikuwa anaendelea na shughuli yangu taratibu.
“Mdogo wangu kama Imran anakutaka wala usimkatalie” dada Bupe alizungumza huku akisugua vyombo kwa brashi na sabuni ya unga.
“Unajua nini dada Bupe?” niliamua kutoa dukududku langu kwa dada yule aliyekuwa ananipa ushauri wa kutembea na kaka Imran.
“Enhe niambie”
“Kusema kweli moyo wangu haupo kabisa kwa kaka Imran”
“Najua moyo wako unao wewe mwenyewe, lakini penzi lako mpe Imran”
“Simaanishi hivyo dada Bupe bwana”
“Kumbe?”
“Yaani, kaka Imran siye ninayempenda mimi” nilizungumza kwa umakini huku nikitabasamu.
“Ah! We achana na watu wa vijijini hao, umekuja mjii toka kimjini mjini”
“Wala kijijini kwetu sina mwanaume yoyote”
“Mnh! Kwahiyo mara hii hapa mjini umekwisha pata Bebe? Makubwa basi. Unafungiwa ndani tu hali hiyo, je ungekuwa huru si ndo ingekuwa balaa” Dada Bupe alizungumza kwa mshangao.
“Sio hivyo bwana dada Bupe” nilizungumza huku nikicheka.
“Kumbe vipi?”
“Yani mie moyo wangu ukiuchana hapa pyaaa! Utamkuta Fadhili amejaa” nilizungumza kwa hisia huku nikifumba macho kuonesha hisia zangu.
“Mnh basi makubwa”
“Yaani hilo ndio tatizo”
“kwahiyo wewe na Fadhili ni wapenzi?”
“Mnh….am…eeeh….hapana” nilizungumza kwa kigugumizi. Nilishindwa kuzungumza kama alikuwa ni mpenzi wangu kwasababu hakuwahi kunitongoza, lakini pia nilitaka kusema kuwa ni mpenzi wangu kwasababu ya shughuli ya jana pamoja na vituko vyake. Lakini kama jibu lingekuwa ni ndio basi hata kaka Imran pamoja na baba nao pia ningetakiwa kusema ni wapenzi wangu. Ndio kwasababu nao pia si walitaka kunifanyia kama Fadhili.
“Sasa mbona kigugumizi, kama ni mpenzi wako we nambie kwani mie si ni dada yako?” alihoji dada Bupe.
“Kweli nampenda sana Fadhili” nikasema.
“Wacha kujizunguusha jibu swali langu”
“Hajakuwa mpenzi wangu kabisakabisa lakini ananipenda pia” nilijikakamua na kuzungumza.
“Mapenzi yenu we na Fadhili yameanza lini?” dada Bupe alihoji swali ambalo lilikuwa gumu kidogo kulijibu ingawa jibu lake lilikuwa linafahamika. Nikatulia kidogo na kujifanya nakohoa.
“Haya kohoa useme” mnh dada alizidi kunisisitizia.
“Jana….” nikajikuta nikilitoa jibu hilo pasipo kutarajia mwenyewe.
“He! Kwahiyo jana hiyo Imrani amekutongoza, na jana hiyohiyo Fadhili amekutongoza” Dada Bupe alionekana kuzungumza kwa mshangao. Ndani ya moyo wangu nikajisemea, laiti ungetambua kuwa jana hiyohiyo unayoishangaa wewe na baba naye alikuwemo kwenye mkumbo huwo wa kunitaka kimapenzi, sijui ungeshangaaje. Nikatikisa kichwa kukubali swali lake lile.
“Na yote hayo ni kwasababu ya zile nguo ulizokuwa umezivaa, au uwongo?” alisema dada Bupe.
“Sivai tena!” nikazungumza huku nikiwa nimekauka uso na kuonesha kuchukia kitendo cha jana cha kuvaa vinguo vya nusu uchi. Ndio mimi nilikuwa naviita nusu uchi kwasababu havikuwa vya type yangu. Ebu fikiria ndugu msomaji, wewe mwenyewe unafahamu watoto wengi wa kitanga wanavyovaa mavazi yao. Sasa binti huyo umchukue na kumvisha vimini na viblauzi vya kifua wazi unafikiri atajisikiaje? Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu.
“Sio nusu uchi mdogo wangu” dada Bupe alieleza.
“Kumbe ni kilomoja?”
“Yaani zile ndio katalogi za mjini. We mwenyewe si umeona ulivyotupia tu ndani wote umewamaliza” alizungumza dada bupe maneno ambayo yalinitia wasiwasi kidogo. Nikahisi alikuwa analitambua sheshe lililonikuta jana jioni.
“Haa dada Bupe punguza chumvi bwana, sio nyumba nzima” nikajifanya kutetea ukweli ambao ulikuwa ni kweli.
“Kwani ndani mle vijana si wawili”
“Ahaa, nilifikiri unamuingiza na baba pia”
“Haaa! Naamini kwa jinsi ulivyokuwa umetokelezea jana, hata Mzee Sekiza naye angekuona asingekubakiza” dada Bupe alizidi kuzungumza maneno machachu ndani ya masikio yangu.
“Mnh dada na wewe! Baba anitake mimi, Sasa ndio nini?” nilijibaraguza.
“Ohoo kumbe hujui wanaume wa mjini wewe!”
“Mnh! Sasa kwamfano ndio imetokea mzee Sekiza ananitaka, Nitafanya nini?” nilizungumza baada ya kupata mwanya wa kuuliza swali ambalo nilikuwa sielewi namna ya kuanza kuliuliza.
“Mnh, hapo mdogo wangu ikitokea inabidi uwe makini sana. Tena omba sana isije ikatokea” dada Bupe alizungumza kwa msisitizo.
“Kwanini?”
“Mnh! Hapo sina la kuzungumza lakini unaweza ukajikuta unapoteza kibarua chako” alizungumza dada Bupe kwa umakini mkubwa.
Nilikaa vizuri na kumsikiliza kwa umakini baada ya kuhisi alichokuwa ananipatia kilikuwa ni kitu kizuri na chenye mafanikio kwangu mimi mwenyewe.
“Sasa nitapotezaje kibarua?” nikahoji.
“Kwamfano ukimkataa, anaweza kukuchonganishia hadi ufukuzwe kazi. Na ukimkubali, siku ukibainika na mke wake ujue litakuwa songombingo” alieleza dada Bupe na maneno yake yakaniingi vyema kwenye ubongo wangu.
“Duu! Kweli hilo balaa!” nikazungumza kwa suti ya kukata tamaa.
“Ndio hivyo mdogo wangu, ila ukifanikiwa kutoka na baba mwenye nyumba pasipo mtu mwingine kufahamu unaweza ukajikuta umeula” sasa dada Bupe akaanza kuzungumza maneno ambayo hayakuwa na busara tena. Mimi ndio niliyaona hivyo simaanishi kuwa hata wewe unayaona maneno yale kama niyaonavyo mimi.
“Lakini hata hivyo haipendezi kabisa kufanya kitu kama hicho cha hatari hivyo” nilizungumza kwa umakini.
“Ni hatari lakini kuna maslahi” dada Bupe alizungumza kwa kujiamini.
“Aisee mimi siwezi”
“Wewe huwezi si kwasababu ushachukua watoto wake!” dada Bupe alizungumza huku akicheka.
“Hapana, mimi nampenda Fadhili tu, hao wengine wananilazimisha tu” nilizungumza kwa sauti ya kudeka.
“Kina nani wanakulazimisha”
“Si huyo Fadhili”
“Mnh huna lolote”
“Kwanini unasema hivyo dada Bupe?”nikahoji kwa wasiwasi baada ya kumuona dada Bupe kama vile alikuwa na mashaka na mimi.
“Unajua mimi ni mtu mzima?”
“Sijui unakusudia nini dada Bupe?”
“Kuna kitu kinaendelea hapo ndani kwenu” dada Bupe alizungumza huku akitembea kuelekea mgahawani. Nikabaki na kigugumizi ndani ya nafsi yangu nikiwa sielewi alichokuwa anakimaanisha dada yule.
“Tumuuu” dada Bupe aliniita akiwa mgahawani.
“Abee” nikaitika huku nikimchungulia kwenye tundu ya mlango.
“Njoo maramoja”
Nilijiinua kutoka pale nilipokuwa nimeketi na kuelekea kule kwa dada Bupe. Tulipokutanisha macho yetu dada alinikonyeza kwa ncha ya jicho lake la kushoto. Nikahisi mapigo ya moyo wangu yakibadili muelekeo na kudunda kwa spidi kidogo. Nilihisi kulikuwa na kitu kilichokuwa kinaendelea kati yake, mimi na yule mteja.
“Abee” niliitika mara tu nilipomkaribia.
“Umemuona Endrus?” dada Bupe alihoji huku akinipisha nimuone mteja aliyekuwa ameketi akimhudumia. Maneno yale yanizidi kuushitua moyo wangu. Ghafla nikahisi aibu ikinivaa kwenye sura yangu. Nilipeleka mkono wa kulia mdomoni na kuuma kidole kidogo na kutoa tabasamu kwa aibu.
“Mambo mrembo?” mnh kijana yule alinisalimia.
“Poa” nikajibu huku nikijipindapinda kama jongoo.
“Haya kazi kwako we si ulisema unataka kumuona Endrus? Ndio huyo sasa!” dada Bupe alizungumza huku akiondoka na kutuacha mimi na Endrus mgahawani pale.
“Njoo ukae basi hapa mrembo” kaka yule akaniambia huku akinioneshea kiti kilichokuwa pembeni mwake.
“Ongea tu mi nakusikia” nikazungumza kwa sauti ya kutolea kooni.
Ingawa macho yangu yalikuwa chini lakini nilijitahidi kumtazama kwa umakini. Kusema ukweli Endrus alikuwa ni kijana mzuri. Ninaposema mzuri ni mzuri kweli kweli na mwenye mvuto. Hakuwa mweusi sana na wala hakuwa mweupe, sijui niseme ni maji yakunde. Labda nitakuwa sahihi.
“Aah mrembo bwana haipendezi kuzungumza huku umesimama”
“Abee” nikaitika kama vile siku nimeyasikia yale maneno yake.
“Njoo bwana” Endrus akazungumza kwa kubembeleza.
“Lakini sikai sana” nikazungumza huku nikimtazama kwa macho malegevu. Hata sielewi mwenzenu ilikuwaje maana nilijishitukia macho yangu kuyahisi mazito utafikiri nilikuwa nimebeba mzigo wa matofari kwenye kope zangu.
“Hilo halina shaka mtoto mzuri we njoo” Endrus akanambia.
Nilisogea hadi kwenye kiti kile na kukisogeza pembeni kidogo kisha nikaketi na kumpa mgongo.
“Jamani Tumu mbona unanipa mgongo sasa”
“Haa wewe nani kakwambia jina langu? Mi siitwi Tumu” nikazungumza huku nikijipinduapindua pale kwenye kiti kwa maringo ya kisichana.
“Haa mie nakujua wewe tangu kitambo”
“Kitambo lini?” nikahoji huku nikijigeuza na kutazama mbele.
“Ewaa mambo ndio hayo, utamu wa mazungumzo ni kuonana usoni”
“Jibu kitambo tangu lini?” nikatupa tena swali.
Nikazungumza kwa ile sauti yangu ya kubana na kuitolea puani. Chezea mimi wewe! Habari ndiyo hiyo.
“Tangu nilipokuona siku ya kwanza”
“Lini?”
“Mwezi uliopita”
“Mnh muongo wewe”
“Kweli vile, unajua nilipokuona tu nikahisi moyo wangu ukinienda mbio ghafla” Endrus alizungumza kwa hisia.
“Mnh muongo wewe, moyo ukuende mbio kwa lipi?”
“Unajua wewe ni mrembo sana?”
“Mnh! Inawezekana huwajui warembo wewe”
“Nawajua warembo kibao ila wewe nahisi umewazidi ninaowafahamu mimi?” aliniambia huku akipeleka kikombe cha chai mdomoni.
“Mnh basi haya asante” nikazungumza huku nikijichekesha chekesha kwa nyodo.
“Unajua nini Mwantumu?”
“Enhe….”
“Yani wewe ni mzuri zaidi ya vile nilivyokuwa nakufukiria”
“Mnh we kaka mchokozi” nikazungumza kwa kudeka.
“Unafikiri Mwantumu? Yaani kwa jinsi ulivyo nahisi nina bahati sana kuketi na wewe kama hivi”
“Haya asante, basi mie ngoja niende” nikazungumza baada ya kumuona mtu mwenyewe hakuwa anazungumza kile kilichokuwa inabidi kizungumzwe.
“Aaaa ngoja kwanza jamani mrembo, unataka mwenzio nishindwe kunywa chai?” Endru alizungumza kwa kubembeleza..
“Kwanza we mchoyo, hata kunikaribisha” nikazungumza kwa kumtania kijana yule.
“Ayaaa! Jamani naomba unisamehe dada mrembo”
“Huna lolote we mchoyo”
“Unajua nini? Yaani nilipokuona tu nikahisi mambo yote yamevurugika kwenye ubongo wangu”
“Kwahiyo ukasahau hata kukaribisha wenzio?”
“Kabisa,”
“Mnh basi mkeo anapata tabu sana” nikazungumza na kumuingizia kauli ya kumtega. Ndio maana nilikuwa nahisi alikuwa anachelewa kuelekea kwenye poini mtoto wa kiume.
“Mke atoke wapi bwana Mwantumu?”
“Mnh wacha uwongo, inamaana huna hata msichana wewe?” nikahoji kwa msisitizo.
“Natamani sana kuwa na mpenzi”
“Sasa unasubiri nini?”
“Tatizo bado sijapata”
“Mnh! Basi mi nitakuombea usiku na mchana umpate wifi yangu haraka” nikazungumza huku nikitabasamu
“Amina”
“Kwahiyo hata kumuona bado huyo wifi yangu?” nikahoji swali la uchokozi kwasababu dada Bupe alishanieleza kuwa Endru alikuwa ananitaka.
“Kumuona nimemuona lakini kummiliki bado” alisema Endru.
“Sasa unasubiri nini, je wenzio wakikuwahi?”
“Itabidi unisaidie ili niweze kumpata” alisema Endru huku akipeleka kikombe cha chai kinywani mwake.
“Mnh!”
“Mbona unaguna?”
“Naona unataka kunipa kazi nzito”
“Kama utakuwa na nia kweli ya kuzisaidia sidhani kama itakuwa ni kazi nzito, lakini kama ukiwa hauna nia ya kunisaidia naamini kazi hiyo itakuwa nzito sana kwako” Endrus alieleza huku akimega kipande cha chapati na kukitafuna.
“Nitajaribu kama nitaweza” nikamwambia.
“Nimefurahi sana kusikia mtoto mrembo kama umekubali kusaidiana na mimi”
“Haya niambie huyo msichana mwenyewe ni nani?” nilihoji huku nikianza kuwa na hisia kuwa msichana aliyekuwa anazungumziwa pale hakuwa mwingine bali ni mimi maana mfano wa aina hiyo tayari nilikuwa nimekwisha kukutana nao kijijini kwetu Tanganyika.
“Mbona una haraka, nitakwambia tu” alisema Endru huku akisogeza pembeni sahani iliyokuwa na kipande cha chapati kuashiria alikuwa ameshiba.
“Inamaana ndio umeshiba”
“Yap” Endru alijibu kwa kifupi huku akijinyoosha kwenye kiti na mikono yake akiwa ameilaza kwenye mikono ya kiti huku mguu mmoja ukiwa kulia na mwingine akiwa ameutupa kushoto.
“Mnh! Pozi lako tu”
“Limekumaliza enh?”
“Linaniacha hoi”
“Yani saahizi hapa ningekuwa na mrembo kama wewe hivi, angekuwa nanikunakuna tu tumbo langu lililojaa chapati za dada Bupe” Endru alizungumza.
“Boo! Yaani kushiba ushibe wewe halafu mimi ndio nikukune” nikazungumza kwa kurembua macho na kubinua midomo kwa nyodo.
“Sasa hayo si ndio mahaba”
“Mnh!”
“Usijifanye hujui bwana, nyie watoto wa kitanga si ndio mnao yaweza hayo” Endru alizungumza na kunifanya niangue kicheko cha kujilazimisha.
“Haya bwana mie ngoja nikuache” nikazungumza huku nikijiinua kutoka pale nilipokuwa nimeketi.
“Aaaa! Tulia bwana” Endru alizungumza huku akinishika mkono kunizuia nisiondoke.
“Lakini mi si nilikwambia kuwa sikai sana?” nilizungumza kwa sauti yangu ya kutokea puani na kurembua macho kimahabuba.
“Mnh mtoto unazidi kunikosha na macho yako”
“Mnh macho gani?”
“Si hayo yako macho kumchuzi” Endru alizungumza huku akinivutia kwake.
Huku nikijifanya sitaki nilisogea taratibu hadi alipokuwa ameketi.
“Kaa basi” Endru alizungumza kwa kubembeleza.
“Wapi?”
“Kaa hapa kwenye mapaja yangu”
“Akaa mie naogopa”
“Asa unaogopa nini?”
“Mkeo akinikuta je?”
“Sina mke bwana, ebu kaa kidogo” Endru alizungumza kwa kubembeleza.
“Bwana hapa watu wataingia” nikazungumza huku nikitazama mlango mkubwa wa kuingilia wateja.
“Kwahiyo kama kungekuwa hakuna watu ungekaa”
“Sijui” nilijibu kwa sauti yangu huku nikijibwibwishua kwa mapozi ya mitego.
Endru alibadilika sura na kuonekana mzuri zaidi, macho yake yalikuwa yamelegea na mdomo wake ulikuwa ukicheza cheza huku akionesha meno yake pamoja na ulimi ulikuwa ukichomoka mithili ya kenge aliyeona mjusi. Nilianza kuhisi mwili ukinisisimka na joto likiongezeka kwa kasi ya ajabu.
Pasipo kujitambua namimi nikaanza kuchezesha midomo yangu huku nikimtazama Endru kwa macho yaliyokuwa yamechoka. Taraiibu nilijikuta nikijiweka kwenye mapaja yake huku mapigo ya moyo wangu yakizidi kunienda mbio. Sijui mwenzenu nilikuwaje mie, sijui ndo hayo mapepo ya mahaba? Mie hata sielewi.
Macho yangu na ya Endru yalipokutana kilammoja akaachia tabasamu la mahaba. Kitu ambacho hakikuwa cha kawaida nipale pua yangu na pua ya Endru zilipokuwa zikikaribiana na kubadilishana pumzi.
Yani ndugu msomaji huwezi kuamini, mambo yote hayo yalikuwa yakitendeka palepale mgahawani pasipo kujali kama wateja wangeweza kufika na kutukuta katika hali kama ile. Mbaya zaidi hata mlango ulikuwa wazi na kila mtu ambaye angepita karibu na mgahawa ule angeweza kushuhudia video ile ya laana. Nafiri akili zetu hazikuwa sawa, pengine zilikuwa zimekwishamezwa na mafuriko ya mahaba.
Kuna jinamizi moja ambalo nilitokea kulichukia sana, Kila nilipokuwa nikijaribu kupata mavituzi yangu lenyewe lilijitokeza na kuharibu utaratibu. Ndugu msomaji wangu jinamizi lenyewe lilikuwa ni zile honi za magari yaliyokuwa yakiingia na kutoka pale nyumbani.
“Mungu wangu!” nilizungumza huku nikikurupuka kutoka pale kwenye mapaja ya Endru. Huwezi kuamini balaa hili ndugu yangu, pamoja na kwamba nilikuwa nimelegea na kuishiwa nguvu lakini niliweza kukurupuka na kusimama tayari kwa kuondoka.
“Vipi?” Endru akahoji kwa mshangao.
“Kwaheri” nilizungumza kwa ufupi na kutoka mgahawani mle kwa mwendo wa kukimbia.
“Mwantumu!” dada Bupe aliniita baada ya kuniona natoka nduki.
Kama vile sikuwa nimesikia sauti ya mwanamke yule akiita, nilielekea moja kwamoja hadi getini na kuingia kwenye geti dogo kisha nikafungua kwa ndani. Lilikuwa ni gari la kaka Imran. Mapigo ya moyo wangu yalianza kwenda mbio kwa wasiwasi nikihofia kumkaribia kaka Imran tukiwa wawili. Mwanaume yule aliingiza gari ndani na kupaki sehemu ambayo siku zote ndipo alipokuwa anapaki gari lake.
****
Kule mgahawani Endru alibaki ameduwaa kama vile alikuwa amepigwa na shoti ya umeme. Macho yake yalikuwa yakitazama kwenye mlango ambao niliutumia kutokea. Hakuweza kuelewa nilikuwa nimepatwa na pepo gani hadi kukatisha utamu ghafla na kutimua mbio.
Dada Bupe alikuwa amesimama kwenye mlango wa jikoni amkimtazama Endru kwa jicho la kishambenga huku akiachia tabasamu.
“Umekwisha habari yako msomi” dada Bupe alizungumza huku akimtazama Endru ambaye alikuwa bado ameduwaa akiwa haamini kwa kile kilichokuwa kimetokea sekunde chache mgahawani pale.
“Aisee!” Endru alitamka kwa kuhamaki.
“Vipi?”
“Mbona hata sielewi!” alizungumza Endru kwa mshangao huku akiwa bado amepigwa na bumbuwazi.
“Kwani imekuwaje?” alihoji dada Bupe.
“Sijui, mimi nimeshangaa tu mtu anatimua mbio utafikiri mwana riadha wa Kimasai”
“Wewe utakuwa kuna kitu umemfanyia mtoto wa watu” alizungumza dada Bupe kwa masihara.
“Hapana dada Bupe, unajua sijamgusa kabisa!” Endru alijaribu kuongopa.
“Acha basi uongo Endru”
“Kweli dada Bupe, kale katoto sijakashika hata mkono” Endru aliendelea kusisitiza.
“Ahaa, sasa utakoma! Yule binti huwa ana mashetani, akiguswa na mwanaume tu yanapanda” dada Bupe alizungumza kwa upole.
“Kwahiyo amepandisha mashetani?” Endru alihoji kwa wasiwasi.
"Tena lazima arudi, pale amefuata panga au kisu”
“Cha nini sasa?”
“Unauliza cha nini? Kumchinja mwanaume aliyejaribu kumshikashika” alizungumza dada Bupe huku akionekana kumaanisha kwa kile alichokuwa anakizungumza.
“Mungu wangu! Basi mi nasepa” Endru alizungumza kwa wasiwasi.
“Shauri zako, umezidi kuvamia vamia kila kisichana unachokiona” dada Bupe alizungumza kwa masihara.
“Sasa dada Bupe tusipowagonga hawa huwa wanaumwa” Endru alizungumza kwa masihara.
“Pembavuu! Sasa subiri chamoto utakiona”
“Basi tutaonana baadae” Endru alizungumza huku akivuta hatua kutaka kuondoka lakini dada Bupe alimkamata mkono na kumzuia asiondoke.
“Unakwenda wapi sasa?” alihoji dada Bupe huku akiwa ameukamata mkono wa Endru.
“Unafikiri nani hapendi kuishi?”
“Kwani nani amekwambi anataka kukuua?”
“We si umesema dogo anakuja na mashetani yake?”
“Sasa wewe unaogopa mashetani?”
“Ngoja nikachukue Bible nije tupambane” Endru alizungumza kwa utani.
“Kwani umemgusa?”
“Ah kidogo tu dada Bupe”
“Nyoko! Wewe si ulisema haujamgusa hata mkono?”
“Ah nimekumbuka, kumbe nilikuwa nimemgusa kidogo tu”
“Nakutania basi hakuna shetani wala ibilisi wewe tulia hapo unipe matokeo” alizungumza dada Bupe huku akifuta meza ya chakula kwa kitambaa.
“Duh, umejua kunirusha roho” Endru alizungumza huku akijiweka kwenye kiti.
“Pumbavu, unajifanya kidume kumbe uwoga umekujaa”
“Unafanya utani na uhai wa mtu wewe” Endru alizungumza maneno ambayo yaliwafanya wote wawili kuangua kicheko.
“Haya nipe matokeo sasa mana mimi nilikuwa nimeshamaliza kila kitu” dada Bupe alizungumza kwa kujidai.
“Sasa kwanini amekimbia vile?” Endru aliendelea kuhoji kwa wasiwasi pamoja na kwamba dada Bupe alikuwa amemfariji.
“Kulikuwa na gari inapiga honi huko getini kwao ndomaana ametoka mbio kufungua geti” dada Bupe akafafanua.
“Duh afadhali, mana nilihisi kufa kufa tu”
“Haya nipe basi matokeo?” dada Bupe alirejesha mada baada ya kuona Endru amebadilisha stori.
“Dah mdogo wako mkali utafikiri malaika!” Endru alizungumza huku akijaribu kukumbuka tukio lililokuwa limemtokea kati yake yeye na mimi pale mgahawani dakika chache zilizopita.
“Kwahiyo mkajisahau na kufikiri mpo chumbani?” dada Bupe alihoji kwa ushambenga kumfahamisha Endru kuwa alikuwa ameshuhudia mchezo mzima.
“Hee we dada Bupe!” Endru aliita kwa kuhamaki.
“Nini?”
“Inamaana ulikuwa unatuangalia?” Endru akahoji baada ya kusikia maneno yale kutoka kinywani mwa dada Bupe.
“Kwani mlifikiri mpo guest?”
“Haaa! Lakini dada Bupe na wewe si ungebaki huko huko jikoni?” Endru alihoji kwa aibu.
“Kwani unafikiri niliyeona ni mimi pekeyangu?” dada Bupe alizungumza huku akicheka.
“Mnh!” Endru akashituka kidogo.
“Tazama kule nje” dada Bupe alizungumza huku akimuoneshea kidole Endru nje ambako kulikiuwa na mafundi selemala wakitengeneza vitanda na makabati.
“Mungu wangu!” Endru alihamaki na kuhisi akiingiwa na aibu baada ya kubaini kuwa utumbo aliokuwa akiufanya na mimi ulikuwa ukionekana na wale mafundi selemala.
“Lakini sio tatizo kwani nani asiyejua mahaba?” dada Bupe alijaribu kupoza ukali wa hisia za Endru.
“Hata hivyo kwanza hatukuwa tunafanya kitu chochote kibaya” Endru alizuga na kujipa moyo kwa kile kilichotokea.
“Hebu tuachane na hayo, unaniambiaje sasa?” dada Bupe alibadili mada.
“Mnh! Mdogowako mtamu, Kha!”
“Wacha kusifia nyama usiyoila wewe, unauhakika gani kama ni mtamu?”dada Bupe alizungumza huku akivuta kiti na kuketi pembeni mwa Endru.
“Ah muonekano wake tu unaonesha mtoto mtamu, sijui siku nikimuweka kwenye kumi na nane zangu itakuwaje?” Endru alizungumza kwa hisia kali.
“Unampenda lakini au unataka kumchezea tu mdogo wangu kama unavyochezea visichana vyako vya chuoni?”
“Haa nimchezee yule? Kwanza kuwa naye tu nahisi ni bahati”
“Nyie wanaume si ndivyo mlivyo bwana nani asiye wajua” alizungumza dada Bupe huku akijiinua na kuchukua kopo la sukari kutoka mezani.
“Yaani dada pale mapemaa naoa” Endru alizungumza huku akijipinda kushoto kutoa pesa kwenye mfuko wa nyuma wa suruali yake.
“Angalia tu usije ukamaliza ‘bumu’ lako kwa binti wa kitanga” alizungumza dada Bupe huku akifuta mikono yake kwa eplon aliyokuwa amejifunga kiunoni.
“Ah hata kama likiisha wacha tu liishe, yule mtoto ni mkali dada Bupe” Endru alizungumza huku akimkabidhi dada Bupe noti ya shilingi Elfu kumi.
“Mnh ushaanza na minoti yako, saa hizi chenchi tutapata wapi?” alisema dada Bupe kwa masihara.
“Hiyo chenchi utampa mke wangu” alisema Endru huku akigeuka kuondoka.
“Hee ushajimilikisha tayari?”
“Sasa kumebakia nini kama sio ndoa” Endru alizungumza huku akitoka mgahawani mle.
“Haya bwana” alisema dada naye akielekea jikoni.
****
Nilisimama pembeni nikimtazama Kaka Imran alivyokuwa akipaki gari lake. Baada ya hapo aliteremka na mfuko wa rambo na kunitazama huku akionesha tabasamu zito.
“Shikamoo kaka” nikamsalimia haraka haraka huku nikiwa nimesimama palepale nilipokuwa.
“Marahaba mrembo mambo?”
“Poa” nilijibu kwa aibu.
“Sasa mbona hata hunipokei” kaka Imran alihoji baada ya kuniona nikimkodolea macho pasipo kumpokea tofauti na ilivyo kawaiada ya siku zote. Hata mwenyewe sikuelewa ni kwanini siku ile nilifanya vile. Lakini nafikiri ni kwasababu ya ule wasiwasi wangu niliokuwa nao. Nikamsogelea na kupokea ule mfuko aliokuwa ameubeba.
“Mbona leo mapema sana?” nikahoji kwasababu haikuwa kawaida yake kurudi mida kama ile.
“Nilikuwa nimekumisi na ndio maana nikaona nije maramoja nikuone” alisema kaka Imrani huku akinikabidhi mfuko ule.
“Mnh! Haya asante” nilijibu huku nikiupeleka ndani ule mzigo.
“Vipi upweke haukuchoshi hapa nyumabani?”
“Hamna, nilikuwa kule mgahawani kwa dada Bupe napiga stori” nilijibu.
“Unaweza kupiga stori wewe?” Kaka Imran alihoji huku akiketi kwenye kochi sebleni.
“Ah naweza, kwanini nisiweze?” nilijibu huku nikiwa nimesimama na kamfuko kangu mkononi.
“Hebu uje unipigie na mimi basi” alisema kaka Imran huku akinitazama kwa macho ya mkato.
“Huu mzigo niuweke wapi?” milihoji nikiwa sielewi kama mzigo ule ulikuwa ni wakwake au ulikuwa ni wa jikoni.
“Huwo ni mzigo wako, hebu nenda ukaufungue uangalie kama utakufaa” kaka Imran alizungumza huku akiwa ameketi kwa mgongo kwenye kochi kama vile kwenye makalio yake kulikuwa na majipu.
Niliufungua mfuko ule palepale huku nikiwa na shauku ya kuona kilichokuwemo ndani yake. Nilipobaini kuwa zilikuwa ni nguo nikasita kuzifungua.
“Vipi mbona hufungui?” kaka alihoji baada ya kuniona nimesita.
“Kwani hizi si ni nguo?”
“Kwahiyo kama nguo hazifunguliwi?”
“Basi ngoja nikazifungulie ndani” nilizungumza huku nikiondoka kulekea
chumbani. Nilipofika niliutupa mfuko ule kitandani huku nikiwa na hofu ya kuufungua. Nilikumbuka nguo ambazo alikuwa ameniletea siku chache zilizopita na kunisababishia kasheshe ndani mle. Nikakumbuka jinsi ambavyo kila mwanaume wa ndani mle aliponiona alitamani kuvunja amri ya 6. Pia nikakumbuka vurugu na ugomvi mkubwa kati yangu mimi na Bi Fatma kwasababu ya mavazi yale.
Niliutazama mfuko ule kwa sekunde kadhaa kisha nikausogelea taratibu, niliufungua na kuchomoa nguo moja. Ilikuwa ni taiti moja nyeupe iliyokuwa na maua maua mekundu kwa mbele, niliiweka pembeni taiti ile kisha nikachomoa nguo nyingine. Kilikuwa ni kitopu fulani hivi chekundu. Sikukijaribisha nacho nikakitupa kitandani. Huku nikiwa bado na wasiwasi uliochanganyikana na woga, nikavuta nguo nyingine kutoka kwenye mfuko na kuchomoka sidiria nyeupe iliyokuwa na resiresi kwa pembeni. Niliitazama kwa makini kwa kuipindua pindua kisha na yenyewe nikaiweka kitandani.
Mfuko ulikuwa bado una nguo za kutosha. Nikaona kuchomoa moja moja kungenichelewesha hivyo nikapata wazo la kuzimwaka kitandani.
“Mtume!” nilihamaki baada ya kukutana na nguo ambazo kwangu hazikuwa za kawaida. Kulikuwa na blauzi zisizoziba mwili takribani tano hivi, mini sketi nne, taiti nne, na nguo za ndani zikiwa na rangi mbalimbali kama nane hivi.
“Mungu wangu!” nilihamaki baada ya kushika nguo moja ya ndani na kuipekua vizuri. Haikuwa ya kawaida kama zile nilizokuwa nimezizoea mimi wakati huo. Bali zilikuwa sijui wenyewe wanaita kibini sijui, zile zinazo onekana kwenye video zimevaliwa na wanawake wa kizungu.
Nikiwa nimeshika nguo ile ya ndani nikiishangaa, ghafla nikagutushwa na mlango ukifunguliwa. Nilishituka sana na kuishusha nguo ile huku nikitazama mlangoni kwa wasiwasi.
“Oh pole jamani mtoto mzuri nimekushitua Eh?” ilikuwa ni sauti ya Fadhili akizungumza huku akichungulia chumbani na mwili wake ukiwa kwa nje.
“Umepitia wapi mbona sijasikia honi ya gari?” nilizungumza huku nikiificha nguo ile ya ndani iliyokuwepo mkononi mwangu.
“Leo nimekuja na bodaboda”
“Gari umeacha wapi?” Nikaendelea kuhoji ili kumfanya Fadhili aondoke bila kuona vile viwalo nilivyokuwa nimenunuliwa na kaka Imran.
“Nimeogopa foleni nimeliacha kazini” alisema Fadhili huku akitupa macho yake kitandani kutazama zile nguo zilizokuwa nimeletewa na kaka Imran.
“Umeingia bila hodi umenishitua” nikazungumza kwa kujibaraguza baada ya kuhisi alikuwa ameziona zile nguo.
Kitu cha kushitua zaidi ni kwamba Fadhili aliingia kabisa chumbani kwangu na kuelekea moja kwa moja pale nilipokuwa nimesimama. Pasipo kuzungumza neno lolote alinishika kiuno na kunikumbatia kwa mgongoni huku midomo yake akiizunguusha hadi shingoni kwa mbele na kunipiga busu moja matata sana, ndio naliita ni busu matata kwasababu hadi leo hii sijawahi kukutana na busu kama la siku hiyo, tena hata yeye Fadhili hakuwahi kufanikiwa kunipiga tena busu kama lile.
“Oooh Fadhi…Ahhh!” nikajikuta nikitoa sauti za kimahaba baada ya kukumbatiwa na mwanaume niliyekuwa nikimpenda na kunimwagia busu maridhawa. Ndugu msomaji we acha tu, nilikuwa nampenda sana Fadhili kuliko mwanaume yeyote yule ambaye ungatamani niwe naye. Ghafla nikashituliwa na sauti ya Fadhili ikiniita kwa mashaka.
“We Tumu” aliita Fadhili kwa na kunitoa kwenye lile dimbwi la hisia kali za kimahaba.
“Abee” nikaitika kwa kudeka lakini nikiwa na wasiwasi.
“Hizi nguo mbona sikuonagi ukizivaa, au ni mpya?” alihoji Fadhili huku akizitazama kwa makini na mikono yake ikiwa bado imekamatia kiuno changu.
“Wala sio mpya” nilijibu kwa kujibaraguza huku nikijaribu kumgeuza asiangalie zile nguo.
“Hebu tulia kwanza! Sio mpya hizi wakati bado zina lebo” Fadhili alizungumza huku akiniachia kiuno na kuinama kwa lengo la kushika nguo moja ya ndani. Nikamdaka mkono kabla hajagusa nguo yoyote ile.
“Halafu mbona ni…..” Fadhili alihoji kwa mshangao baada ya kuona aina yenyewe ya nguo za ndani. Kama ambavyo nilikuwa nimeshangaa mimi kumbe hata Fadhili zilimshangaza. Yaani ndugu msomaji si unafahamu zile nguo ambazo zina kakamba fulani hivi kamepita kwa nyuma na vingine kwa pembeni? Enhee sasa hizo ndizo ambazo tulikuwa tunazishangaa mimi na Fadhili wangu.
Nilipoona mwanaume yule alikuwa anaelekea kubaya ikabidi nijiongeze mtoto wa kike, vinginevyo Fadhili angefikia hatua akabaini mtu aliyekuwa ameninunulia viwalo vile.
“Shssss!” Nilimzuia kwa kuweka kidole mdomoni. Nilikunja sura na kujifanya nilikuwa nimekasirishwa na ile tabia yake ya kuchunguza nguo zangu za ndani.
“Inamaana wewe unavaa za hivi?” Fadhili alihoji huku akizioneshea kidole zile nguo kwa mshangao huku macho yakiwa yamemtoka.
“Naomba utoke chumbani kwangu Fadhili” ikabidi nimbadilikie kwasababu sikuwa naelewa alipokuwa anaelekea. Nilijitahidi sana kumficha asibaini kuwa nguo zile zilikuwa zimeletwa na kaka Imran halafu nikakosa penzi la mtu niliyekuwa nampenda.
“Natamani nikuone ukiwa umevaa nguo za hivi” Fadhili alizungumza huku akinitazama kwa jicho la uchu.
“Fadhiliiii” ilisikika sauti ya kaka Imran ikiita kutokea ‘sitting-room’. Kusema kweli nilishituka sana kwasababu nilihisi kama kaka Imran angebaini kuwa Fadhili alikuwa chumbani kwangu ingweza kuwa shida.
“Nenda kaka Fadhili unaitwa” nilimwambia kwa kumhimiza ili atoke mle ndani mwangu na kuniepusha na balaa.
“Kwani wasiwasi wako wewe ni nini?” alihoji Fadhili huku akionekana kama vile hakuwa anataka kutoka chumbani mwangu.
“Sasa unadhani kaka Imran akijua wewe upo huku itakuwaje?” nikazungumza za kumsihi.
“Kwani akijua kuna tatizo gani?” Fadhili alihoji huku akionekana kuhisi kitu fulani kilichokuwa kinaendelea kati yangu mimi na kaka Imrani.
“Mi sijui, lakini si uende halafu uje baadae” nilizungumza vile ili Fadhili atoke chumbani kwangu. Hofu yangu mimi ni kuwagombanisha wanandugu ingawa mtu ambaye nilikuwa nampenda kati ya wale wawili alikuwa ni Fadhili ambaye kwa wakati huwo alikuwa chumbani mwangu.
“Fadhiliii” sauti ya kaka Imrani ilisikika tena kwa nguvu ikitokea usawa wa mlango wa chumbani kwangu.
“Naam” Fadhili aliitika kwa sauti huku akinitazama machoni kwa macho ya kunambia liwalo na liwe.
Kumbe Fadhili alikuwa tayari amekwisha hisi kama mimi na kaka Imran tulikuwa na mahusiano, na kama hatukuwa na mahusiano basi ndio tulikuwa katika mchakato wa kuwa na mahusiano. Masikini ya mungu kijana wa watu inawezekana kabisa kile alichokuwa anakiwaza kilikuwa sahihi, pamoja na kwamba mimi sikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kaka Imra, hata wewe msomaji wangu ni shahidi kwa hili jamani.
“Uko wapi?” sauti ya kaka Imra ilisikika ikihoji.
“Nakuja” Fadhili alijibu kwa sauti kubwa huku akinikazia macho kuona ningechukua uamuzi gani baada ya kufanya kitendo kile.
Mtoto wa kike nilihisi mapigo ya moyo yakipaa hewani kutokana na wasiwasi niliokuwa nao. Sikuweza kuamini kama Fadhili angekuwa mtu mkorofi kiasi kile. Nikaona wazi kuwa alikuwa akinifanyia makusudi ili kuweza kutafuta ukweli.
Fadhili alifungua mlango na kuniacha mimi nikiwa nimesimama kwa wasiwasi huku nikitetemeka kwa hofu. Nilikuwa namuogopa sana kaka Imran, sikuelewa ni kitu gani ambacho kilikuwa kinakwenda kutokea huko nje kati ya Fadhili na kaka Imran.
Fadhili alimkuta kaka Imran amesimama karibu na mlango wa chumbani kwangu akimtazama kwa mshangao.
“Yes Bro” Fadhili aliitika huku akiurudishia mlango wangu.
“Unafanya nini chumbani kwa mtoto?” kaka Imran alihoji kwa sauti ya mkazo na hasira.
“Kwani kuna tatizo gani Brother?” Fadhili alizungumza polepole utafikiri hakukuwa na kitu cha kushangaza.
“Wewe ni mtoto wa kiume, unakaa chumbani kwa mtoto wa kike unabiashara gani?” alihoji kaka Imran kwa msisitizo.
“Bro sijaona tatizo lolote, Mwantumu ni mtoto wa humu ndani na mimi ni mtoto wa humu ndani, sasa kitu cha ajabu ni kipi?” Fadhili akazungumza kwa kujiamini.
“Tena usinijibu utumbo nitakucharaza sasahivi” kaka Imran alizungumza kwa hasira huku akimsogelea Fadhili.
Kule chumbani nilikuwa nimekumbatia mikono yangu kwa wasiwasi wa hali ya juu. Nilikuwa nikiomba dua wana ndugu wale wasiendeleze mzozo ule kiasi cha kugombana. Yaani kweli kabisa wagombane kisa ni mimi? Hapana kwakweli pamoja na tabia zangu zote lakini sikuwa nimefikia hatua ya kuwagombanisha wanandugu heti kwasababu ya mapenzi. Hata wewe ni shahidi msomaji wangu.
“Lakini kaka Imran mimi sijaona kosa langu” Fadhili alijitetea kwa kujifanya kumshangaa kaka Imran alivyokuwa anamlaumu.
“Kimya!” Alitoa amri kaka Imran.
“Enh!” Fadhili akabaki anashangaa.
“We Mwantumu!” kaka Imran alipaza sauti kuniita kule chumbani.
Nikatulia kimya kama vile sikuwa nimemsikia alivyokuwa anaita ingawa nilishituka sana ndani ya moyo wangu. Nikaona wazi balaa lilikuwa linanibusu kwenye mashavu yangu na kunikumbatia kwa hamasa.
“Mwantumuuu” kaka Imran aliita tena kwa sauti zaidi.
“Abee” nikaitika kwa wasiwasi
“Hebu kuja hapa”
Nilitoka kwa wasiwasi huku nikiwa bado nimeikumbatia mikono yangu kifuani kwa wasiwasi.
“Abee” nikaitika mara tu nilipojitokeza huku sura yangu ikiwa chini kwa aibu na wasiwasi.
“Huyu alikuwa anafanya nini huko chumbani kwako?” alihoji kaka Imrani kwa hasira.
“Bwana nimeshakwambia nilikuwa nimekaa sasa unataka kujua nini kingine?” Fadhili alidakia na kuzungumza kabla mimi sijazungumza kitu.
“Sijakuuliza wewe”
“Hata kama akijibu yeye hakuna jipya”
“Unasemaje wewe!”
“Sasa mimi Bro kosa langu liko wapi?”
“Fadhili usinichanganye unajua! Nitakukata mangumi sasahivi!” alizungumza kaka Imran kwa hasira.
“Huko sasa kuoneana, tumeshakuwa watu wazima tusitishiane maisha bwana!” Fadhili naye alizungumza huku akionekana kujawa na hasira kidogo kidogo kadri muda unavyokwenda.
“Unasemaje wewe? Ungekuwa mtu mzima ungeingia chumbani kwa dada wa kazi?” kaka Imrani alizidi kuzungumza kwa hasira huku macho yamemtoka na mate yakimdomdoka mdomoni kila alipokuwa akizungumza.
Jamani nyie mambo yalikuwa ni magumu mno, omba kwa mungu yasikukute na uishie kusoma hivihivi kwenye chombezo. Nakwambia pale nilipokuwa nimesimama nilihisi kijasho chembaamba kikinitiririka mapajani. Nilitamani nimbebe mmoja wapo na kwenda kumtupa nje ili msala ule usiendelee. Kiranga chote kilikuwa kimeniishia nakwambia nikabaki kutetemeka tu utafikiri mgonjwa wadengue.
“Bro unajua tunadhalilishana, angalia tusije tukavunjiana heshima” alizungumza Fadhili kwa hasira.
“Fadili unasemaje? Wewe ni mtoto mdogo mno! Wala usijidanganye hata siku moja nitakuharibu!” Jamani nyie kaka Imran alizidi kupandwa na hasira huku nikimuona wazi alikuwa anatafuta chanzo tu cha kuanzisha mapambano ya masumbwi.
“Okay sawa nimekuelewa, basi na yaishe Bro” Fadhili alizungumza kwa kutaka kumaliza msala ule.
Umeona sasa ndugu msomaji? Nakwambia Fadhili ndio mwanaume wa ukweli, yani aliniburudisha kinoma kwa kile kitendo chake cha kujishusha baada ya kuona moto ulikuwa umewaka balaa. Najua hakuwa anamuogopa kaka Imran bali aliamua tu kujishusha ili kulinda amani ya ndani mle.
“Alaaa!” alitamka kaka Imran huku akijaribu kuteremsha hasira.
“Basi mkubwa na yaishe” Fadhili aliendelea kujishusha kabisa.
“Sasa sikiliza we binti, ole wako nimkute tena Fadhili chumbani mwako” kaka Imran alizungumza kwa jazba huku akininyoioshea kidole cha onyo.
Niliitika kwa kichwa kukubaliana na lile agizo lililokuwa limetoilewa na kaka Imran. Alimtazama Fadhili kwa chuki kisha akageuka na kuondoka. Fadhili alitoa msonyo kwa sauti ya chini ambayo kaka yake hakuisikia. Nafikiri kama angesikia sijui moto ambao ungewaka tena nani angeuzima.
“Unaona sasa” nilizungumza kwa kumtupia lawama Fadhili juu ya kile kilichokuwa kimetokea. Ndio! Kama angenisikiliza na kuondoka mapema chumbani kwangu yote yale yasingetokea. Hata hivyo Fadhili naye hakukubali kulaumiwa na mimi.
“Toka zako na wewe, kama mnabiashara zenu hukoo!” Fadhili akazungumza kwa hasira huku akielekea chumbani kwake. Mtoto wa kike nikabaki shushu limenishuka nakwambia. Nikahisi kukosa bara na pwani.
****
Kitendo cha kuwafarakanisha Fadhiri na kaka yake Imrani kilinifedhehesha sana. Nikajiona kama vile shetani niliyekuwa nimetumwa kuisambaratisha familia ile ambayo ilikuwa ikiishi kwa upendo na amani kabla ya kufika kwangu.
Nilijikuta nikikubalina na wale wanaosema maisha ni shule, Nikweli kabisa maisha ni shule tena ni chuo kikuu. Kwa muda mfupi tu tangu nilipofika pale jijini niliweza kujifunza mambo mengi sana, na moja ya mambo niliyokuwa nimejifunza ni pamoja na kuwa na nidhamu hasa katika masuala ya mahusiano.
Ndio niliamua kuwa na nidhamu kwasababu nilijiona nilikokuwa naelekea kulikuwa siko na matokeo yake ni kuwa mtumwa wa mapenzi. Kwakuwa namimi ni binadamu niliyekuwa nimekamilika ikabidi nichague mwanaume mmoja tu ambaye pekee ndiye ningemkabidhi moyo wangu.
Najua hata kama ningekupa nafasi ya kunichagulia ungenichagulia Fadhili, kama kuna mwengine ambaye unaona angenifaa basi hilo ni chaguo lako wewe, mimi mwenyewe nilikuwa nimemchagua Fadhili kwasababu ndiye niliyekuwa nikimpenda tangu siku ya kwanza naingia pale jijini Dar.
Sasa changamoni ni kwamba, mtu ambaye nilikuwa nimemchagua kumpa mamlaka ya kumiliki penzi langu alitokea kunichukia kupita maelezo. Huwezi amini lakini ule ugomvi kati ya Fadhili na kaka Imran ndio uliopelekea mabadiliko kwa mpenzi wangu Fadhili.
Nikiwa nimeketi sittingroom nikimsubiri kwa hamu Fadhili arudi ili tuweze kupata chakula cha mchana kama ilivyokuwa kawaida yetu. Akili yangu ilikuwa ikiwaza kuolewa tu na mwanaume huyo na kumzalia watoto.
“Fadhili mpenzi wangu ukinioa nitakuzalia watoto hao…wanne” nilizungumza pekeyangu huku nimeketi kwenye kochi na kukumbatia mto mdogo wa kochi kifuani kwangu.
“Mtoto wangu wa kwanza atakuwa wa kiume na atafanana sana na wewe, nitampa jina zuuri la baba yako mzee Sekiza” niliendelea kuzungumza huku nikitabasamu kwa matumaini.
“Nitakuwa namuita, we Sekiza hebu niletee rimoti hiyo niongeze sauti kwenye TV, au nitamuita we Sekizaaa njoo haraka nikutume dukani ukamuite baba aje ale chakula tayari” masikini ya mungu binti wawatu niliendelea kuyajenga maisha yangu ya baadae nitakapokuwa nimeolewa na Fadhili.
Nilikurupuka haraka kutoka kwenye lindi la mawazo baada ya kusikia geti likigongwa. Niliamini kwa asilimia zote kuwa mtu aliyekuwa akigonga geti alikuwa ni Fadhili, baba watoto wangu mtarajiwa, baba yake Sekiza. Nikatoka haraka sana kwenda kufungua geti.
“Ooh kumbe ni wewe!” nilizungumza huku nguvu zikiwa zimeniishia baada ya kufungua geti na kumkuta dada Bupe amesimama nje.
“Vipi shost ulikuwa umelala nini?” alihoji dada Bupe mara tu aliponiona huku akijichekesha chekesha.
“Hapana!” nilijibu kwa mkato.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment