Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

BONGO DAS'LAAM - 4

   


Chombezo : Bongo Das'laam 

Sehemu Ya Nne (4)


“Mgambo wametufukuza, pesa na samaki vyote nimeviacha”

“Alaa! Mi nilidhani ni tatizo kuubwa kumbe ni hako tu. Mimi nina wiki sijauza samaki umeona nimekufa?” Alizungumza Naima huku akionekana hakuguswa na taarifa zile za tatizo la Suzy.

“Naima nitaishije mimi?”

“Hapa Bongo Utaishi tu, kwani mimi naishije. Nenda ukajiandae tukadange mama” Alizungumza Naima maneno ambayo yalizidi kumvunja nguvu Suzy.

“Lakini Naima si unajua hali yangu?”

“Kwahiyo unadhani ni nani atakayebeba mzigo wa kukulisha? Tena wawili wewe na kijusi chako huko tumboni. Mama kila mtu atakula kwa jasho lake” Naima alisema na kurudi chumbani kuendelea na maandalizi ya kwenda viwanja.

Suzy akawa amechanganyikiwa asijue la kufanya. Alitamani kurudi nyumbani kwao lakini alipomkumbuka baba yake mzee Manyama akajikuta akikata tamaa kabisa ya kurejea kwa wazazi wake wale. Akiwa pale kwenye kiti akatamani kuwa kama angekuwa na uwezo basi mgambo wote wa jiji angewatilia sumu na kuwaua.

Ghafla mawazo juu ya Ayubu yakamjia kichwani mwake. Alikumbuka visa vyote alivyokuwa akivifanya ili kupata penzi la kijana yule. Kutokana na uzuri wa kijana aliyekuwa akimfikiria muda ule akajikuta akitoa tabasamu la matumaini. Akapeleka mkono wake wa kuume kwenye tumbo na kuanza kulipapasa taratiibu. Taswira ya Ayubu iliendelea kutawala kichwani mwake. Alimuona Ayubu akicheza na mtoto wao wa kiume huku yeye akiwa amesimama akiwatazama kwa furaha.

Naima alitoka chumbani na kumkuta Suzy amezama katika dimbwi la mawazo huku sura yake ikiwa imepambwa kwa tabasamu zito lililoashiria furaha. Naima akamtazama kwa kitambo na umekini mkubwa Suzy kabla ya kumshitua.

“Suzy….” Naima aliita.

Suzy hakuitika na kuonekana kutosikia sauti ya Naima. Aliendelea kutabasamu huku akiuma uma midomo yake.

“We Suzy!” Naima akaita tena kwa sauti zaidi

“Abee…” Suzy alishituka mithili ya mtu aliyegutusha kutoka usingizini.

“Vipi mbona unaonekana mwenye furaha wakati umerudi unalia?” Naima alihoji kwa mshangao.

“Ah! Nilikuwa mbali sana” Suzy alijibu.

“He! Haya habari za huko?” Naima akahoji kwa masihara.

Suzy alibaki kukodoa macho kama paka mwizi pasipo kujibu kitu.

“Sasa mwenzio ndio nakwenda kibaruani. Hii ndiyo BONGO DASLAM, ukiwa tayari niambie nitakufundisha kazi” Alisema Naima na kuondoka huku akiwa tayari amevalia nguo zake za biashara.

Suzy alimtazama rafiki yake yule hadi alipotoka na kufunga mlango. Alivuta pumzi na kuzipuliza nje kwa sauti kupitia mdomoni. Macho yake yakapoteza nuru kutokana na machozi yaliyokuwa yakishindana kutoka kwenye mboni ya macho yake.



Ingawa Suzy alikuwa amezaliwa na kukulia ndani ya Jiji lile la Dar Es Salaam, lakini makucha ya jiji lile lililokuwa likifahamika maarufu kwa jina la Bongo hayakumuonea huruma hata kidogo. Akakubali kuwa ni kweli jijini pale palikuwa panahitaji kutumia ubongo vizuri vinginevyo unaweza kuumia kama alivyokuwa akiumia yeye.

“Ama kweli hii ni Bongo Daslam, haina mwenyeji wala mgeni” Suzy alijikuta akitamka mwenyewe pale kwenye kochi.

*****

Mama Suzy alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kumtafuta Ayubu lakini hakuwa amefanikiwa. Siku aliyokwenda kwenye gesti ambayo Ayubu alikuwa amepanga aliambiwa kuwa mtu yule aliondoka kama mwezi mmoja na nusu uliopita. Majibu hayo yakamkatisha tamaa mama Suzy na kurejea nyumbani akiwa hana nguvu.

Pamoja na kwamba mzee Manyama alihusika kwa kupotea binti yake na hakuwa tayari kumtia machoni, lakini roho yake ikawa inamuuma kwasababu Suzy alikuwa ni mtoto wake wa pekee. Lawama zote akamtupia mke wake kwasababu ndiye aliye mpokea Ayubu na kumkaribisha pale nyumbani kwake.

Siku moja mzee Manyama akiwa sebleni akajiwa na kumbukumbu juu ya binti yake wa pekee. Alipaza sauti kumuita mke wake ambaye kwa wakati ule alikuwa chumbani. Mama Suzy alitoka na kumkuta mume wake akiwa katika hali isiyo ya kawaida.

“Abee mume wangu” mama Suzy aliitika baada ya kufika sebleni.

“Nyokooo!” alizungumza kwa hasira mzee Manyama.

“Kwani vipi baba Suzy?” mama Suzy akahoji kwa mshangao.

“Unajifanya hujui sio?”

“Mnh!” mama Suzy akaguna kwa mashaka.

“Unaguna nini? Sasa sikiliza, ondoka ukaniletee mwanangu Suzy hapa leo hii. Na usipompata usirudi” alisema Mzee Manyama kwa sauti yenye mkazo.

Damu ni nzito jamani nyie. Yaani mzee yule pamoja na hasira zote zile alizokuwa nazo dhidi ya Suzy hatimaye anajirudi na kumhitaji tena binti yake nyumbani.

“Lakini mume wangu…..” mama Suzy alitaka kuongea kitu.

“Hakuna cha lakini. Naomba uondoke sasahivi” alisema mzee Manyama kwa ukali kidogo huku amekodoa macho yake.

Mama Suzy akawa anasuasua kuondoka kwasababu hakuelewa angeanzia wapi katika jiji lile la Dar es salaam kumtafuta Suzy.

“Sasa nitakwenda kumtafutia wapi jamani mume wangu” mama Suzy alijaribu kueleza ukweli.

“Utajua mwenyewe, nenda ukamtafute yule mshenzi wako chokoraa anirudishie mtoto wangu” mze Manyama akazungumza kwa msisitizo.

“Lokini mume wangu, wewe si ndio umemfukuza mtoto hapa nyumbani” Mama Suzy akajieleza.

“Mimi nimemfukuza mtoto wangu? Au unataka kujisafisha kwa kutupa lawama kwangu?” Mzee Manyama akazidi kupandwa na hasira.

“Basi tukatoe taarifa polisi ili watusaidie kumtafuta mtoto wetu” mama Suzy alijaribu kutoa wazo kwa mume wake yule aliyekuwa amepandwa na hasira.

“O n d o k a a a!” Mzee Manyama akapaza sauti kuashiria kuwa alichokuwa akizungumza mama Suzy hakikuwa na maana.

Mama Suzy alitoka mbio kwa hofu ya kupokea kipigo kutoka kwa mume wake. Hakujua aelekee upande gani wa jiji lile ambako angeweza kumpata binti yake. Kutokana na hasira alizokuwa nazo mzee Manyama nyumbani pale mama Suzy akapaona pachungu. Akaanza safari ya kuelekea mahali asipopafahamu.

****

Kutokana na hali ngumu ya maisha pamoja na mateso aliyokuwa akiyapata Suzy, kwa kiasi fulani Suzy alianza kufikiria kuunga mkono ushauri wa Naima. Ingawa hakuwa tayari kuua kiumbe kilichokuwa tumboni kwake, lakini hali ya maisha iliyokuwa ikimkabili ilikuwa ikimsukuma kufanya vile. Ukizingatia hakuwa anafahamu mahali alipokuwa baba wa mtoto yule.

Suzy akiwa ameketi kwenye kochi sebleni, Naima alipita akitokea nje kuelekea chumbani. Alimtazama kwa jicho la mashaka kiasi ambacho mwenyewe akajishitukia.

“He! mwenzangu mbona unanitazama hivyo?” Naima alihoji kwa kiburi.

“Kwani kuna ugomvi shoga yangu?” alisema Suzy huku akitabasamu

“Achana na mimi!” Naima alisema na kuelekea jikoni. Suzy akamfuata na kusimama mlangoni. Naima alipomuona akavuta midomo yake na kutoa msonyo.

“Ondoa tumbo lako hapa nisije kulitufua” alisema Naima kwa hasira.

“Mnh! Mama Kimaya unashida wewe” Suzy alimtajia Naima jina ambalo alikuwa akilihusudu sana. Kitendo kile kilimfanya Naima kupunguza hasira na kutoa tabasamu bila kutarajia.

“Shemeji yangu Kimaya anashida kwakweli”

“Dah moyo wangu burudaani ukinitajia hilo jina” alisema Naima huku akitabasamu.

“Hata mi najua, sijui amekupa nini Kim” Alizungumza Zuzy kisha wote wawili wakaangua kicheko.

“Haya nambie ulikuwa unasemaje?” alihoji Naima.

“Mmmm….”

“Vipi mbona huongei?”

Suzy hakujibu kitu bali aliinua mkono na kunyooshea kidole tumbo lake.

“Tumbo?” Naima akahoji.

Suzy akajibu kwa kichwa kuwa alikuwa akizungumzia tumbo lake.

“Lina nini au unataka kuzaa?” Naima akahoji kwa masihara yaliyochanganyikana na kejeli. Suzy akapumua kwa nguvu kabla ya kuzungumza kitu.

“Nimeamua kuitoa” alisema Suzy kwa sauti kavu.

“Unasemaje ?…nahisi sijasikia vizuri. Hebu rudia tena”

“Nataka kutoa mimba” Suzy akajibu kwa msisitizo

“Unanipima au…..?” alihoji Naima kwa umakini mkubwa.

“Naima, nimechoka kuteseka na tumbo lisilo na baba” alisema Suzy huku akilengwalengwa na machozi.

Naima alimkumbatia na kuanza kumbembeleza Suzy huku akionesha wazi kufurahishwa na habari ile. Pasipo kuchelewa alichukua simu yake ya mkononi na kumpigia daktari ambaye alikuwa akimtumia mara nyingi kuporomosha mimba zake. Daktari yule aliyekuwa akifahamika kwa jina la Dr. Mtaturu alikuwa akijihusisha na shughuli ya kuchomoa mimba kinyume na sharia kwa siri kubwa. Dr. Mtaturu alikuwa ni mzoefu sana katika shughuli yake hiyo ambayo alidumu nayo kwa muda mrefu pasipo kutiwa nguvuni mwa sharia.

*****

Ayubu alipokuwa akitoka chumbani kwa Bi Sada akajikuta katika mshangao baada ya kukuta nguo zake zimekwisha fuliwa. Akapeleka macho kwenye kamba ya kuanikia nguo na kumuona Asha mtoto wa mama Asha akimalizia kuanika nguo yake ya ndani. Yasini hakuamini macho yake, akasogea hadi kwenye ndoo yake aliyokuwa akifulia akakuta mapovu matupu.

Wakati akiendelea kushangaa Asha aligeuka na kumuona Ayubu akiwa amepigwa na butwaa. Akatoa tabasamu huku akielekea pale alipokuwa amesimama. Macho yake makubwa aliyarembua na kuyazunguusha kama goroli. Akajitingisha kimaringo na mapozi mbele ya Ayubu huku akipishanisha midomo ya juu na ya chini.

“Vipi kaka Ayubu?” alihoji Asha kwa sauti laini

“Aaah!.... Shwari” Ayubu akajikuta akijibu pasipo kujitambua.

“Vipi unaonekana haupo sawa. Au hukupenda nikusaidie?” Asha alihoji kwa sauti ya kubana huku akipeleka mikono yake kwenye mabega ya Ayubu.

Mikono ya Asha ilipotua kwenye mabega ya Ayubu ilisababisha damu za kijana wawatu kusisimka. Kwa haraka sana Ayubu aliitoa mikono ya Asha huku akilamba midomo yake kama mjusi aliyekuwa ameona kumbikumbi.

Asha akaondoka kwa mwendo wa kiulimbwende huku akimuacha Ayubu ametumbua macho akimkodolea mtoto yule aliyekuwa anatishia usalama wa Amani yake pale nyumbani kwa Bi Sada.

Asha alikuwa tofauti na mama yake kimaumbile. Yeye alikuwa ni mwembamba mwenye umbo la kimisi. Weupe wa rangi ya ngozi yake haikutofautiana na ule weupe wa ngozi ya mama Asha.

Kanga ya Asha aliyokuwa ameshusha kidogo kukata makalio ilimfanya avutie zaidi mbele ya macho ya Ayubu. Binti yule alipoingia ndani Ayubu akatingisha kichwa kusikitika kwa kile alichofanyiwa na Asha. Alishindwa kuelewa binti yule alifanya yale kwa malengo gani, lakini akajipa moyo pengine aliamua kumsaidia tu. “Sasa ndio afue hadi nguo za ndani?” Ayubu alijiuliza mwenye pasipo kuwepo wa kumpatia jawabu la swali lake.

Ayubu alimwaga mapovu yaliyokuwa kwenye ndoo na kuisuuza kisha akaingia chumbani kwake. Alijitupa kitandani kisha akaanza kufikiria mambo yaliyomtokea siku hiyo. Kubwa zaidi ni kile kitendo cha kupeana mahanjumati na Bi Sada mama mwenye nyumba wake. Hakuweza kufahamu ni kivipi alikuwa mwepesi kufanya mapenzi na mama yule aliyekuwa amemzidi umri mara tatu zaidi. Hata hivyo pamoja na kwamba mama yule alikuwa ni mtu mzima lakini aliweza kumpagawisha vilivyo utadhani alikuwa na kijana mwenzie.

Ayubu alipokumbuka kuwa hakuwa amekoga baada ya shughuli ile nzito ya kukanda mguu wa Bi Sada. Alijiinua kutoka pale kitandani na kuelekea bafuni. Bomba la mvua lilimwagia maji na kuyasikilizia hadi kwenye ubongo jinsi yalivyokuwa yakitiririka juu ya mwili wake. Alipohakikisha kuwa alikuwa ametakata alijifuta maji kwa taulo na kurejea chumbani kwake.

Alipofika chumbani aligutushwa na sauti za watu wakizungumza karibu na dirisha la chumbani kwake kwa sauti ndogo huku wakilitaja jina lake. Alisogea hadi karibu na dirisha na kutega sikio.

“Hapana mama Ashubae, Ayubu hawezi kufanya hivyo” ilisikika sauti ya mwanamke mmoja ikizungumza na kumfanya Ayubu kuvutiwa na mazungumzo yale.

“Haa! Unabisha” mwanamke mwengine alisema.

“Kijana wa watu mpole vile” ile sauti ya kwanza ilisema.

“Mpole! Nimesikia kwa masikio yangu mwenyewe” sauti ya yule aliyeitwa mama Ashubae ilikazia na kutetea hoja yake.

“We Asha usibishe. Watu wapole ni wabaya wewe uwaone hivyo hivyo” mwanamke mwengine alidakia.

Ayubu aliposikia jina la Asha akashituka kidogo. Ingawa hakufahamu alichokuwa anasemwa lakini kitendo cha kugundua kuwa Asha naye alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wakimsengenya kilimnyima nguvu, hakuelewa ni kwanini alishituka vile.

“Mnh! Basi makubwa” sauti ya Asha ilisikika ikiguna.

“Lakini mambo anayaweza jamani” mama Ashubae alizungumza kwa sauti ya chini lakini iliyojaa chumvi na magadi.

“Kale?” alihoji mama mwengine kwa mshangao.

“Wee! Ukaone vilevile kadogodogo. Mambo yake mazito” mama Ashubae alizidi kunogesha taarifa zake.

“Wacha we!” Asha alisema kwa shauku ya kutaka kujua zaidi.

“Nakwambia wacha Bi Sada alalamike, utafikiri alikuwa ndio mara yake ya kwanza kulamba asali” alizungumza mama Ashubae na kuwafanya wote kuangua kicheko kwa sauti.

Ayubu aliposikia maneno yale akabaini kuwa soo lilikuwa limebumburuka. Akajihisi kama vile alikuwa amevuliwa nguo kati kati ya kundi la watu. Akawasikia wanawake wale wakitawanyika kama vile walikwenda kuzungumzia pale ili kumfikishia ujumbe kuwa walifahamu vitu walivyofanya na mama mwenye nyumba asubuhi ya siku ile. Ayubu alisogelea kitanda na kuketi huku mikono yake ameipachika kichwani kwa masikitiko.

****

Suzy na Naima waliamka asubuhi na mapema sana kuliko siku zote. Walijiandaa na kwenda muhimbili kwa Dr. Mtaturu. Wao ndio waliokuwa wa kwanza katika wale waliokuwa na shida kama yakwao. Hali ya woga ilikuwa imemtawala Suzy kiasi ambacho hata Naima akagundua.

“Ondoa wasiwasi shoga huyu Dr. ni mtaalamu” Naima alimfariji Suzy.

“Mbona mi siogopi Naima” Suzy alijifanya hakuwa na woga.

Muda ulipofika wakaingia kumuona Daktari ili waweze kupata matibabu ya ugonjwa uliokuwa ukiwasumbua kiasi cha kuwafanya wafike pale.



Dr. Mtaturu alishangazwa na hali aliyokuwa nayo Suzy. Tumbo lilikuwa limetangulia kabla ya yeye mwenyewe kuingia chumbani mle. Ilionekana wazi ujauzito ule ulikuwa umekomaa. Hata hivyo Dr. Mataturu akahisi pengine aliyekuwa amekwenda kuchomolewa alikuwa ni Naima.

“Karibuni” alisema Dokta.

“Ahsante Dr.” Naima na Suzy walijibu na kuketi kwenye viti vilivyokuwa mle chumbani.

“Mnh nani mhusika?” alihoji Dr. Mtaturu.

Naima na Suzy wakatazamana kisha wakatoa tabasamu lililoambatana na kauli kutoka kwa Naima.

“Ni huyu mrembo”

“Mnh!” Dokta akaguna aliposikia kuwa kile kitambi kikubwa ndicho kilichokuwa kinasubiria kuharibiwa.

Naima na Suzy wakashituliwa na mguno ule uliotolewa na Dokta. Kwa utaalamu na ubingwa aliokuwa nao Daktari yule asingeweza kuonesha hali ya hofu kama alivyokuwa ameonesha siku hiyo.

“Vipi mbona unaguna Dr?” Naima alihoji.

“Hiyo mimba ina miezi mingapi?” Dr. naye akawatupia swali.

Naima na Suzy wakatizamana tena kisha Suzy akajibu kama vile hakuwa na uhakika na jibu lake.

“Kam a sio saba ni nane" Suzy alijibu.

“Hiyo mimba ni kubwa sana jamani” alizungumza Doctor mtaturu kwa sauti ya mashaka.

“Kwahiyo utatusaidiaje Dokta?” alihoji Naima kwa wasiwasi.

Dr. aliinamisha shingo kwa sekunde kadhaa kisha akavuta pumzi na kupumua kwa nguvu kama vile alikuwa akipulizia moto jikoni.

“Okay. Nitawasaidia” alisema Dr. mtaturu huku akiinuka na kwenda kwenye kabati lake la kuhifadhia vitendea kazi. Alichukua vifaa na kuvipanga kwenye trei kisha akarejea na kumtaka Naima atoke nje ampishe afanye kazi yake. Naima alipotoka Dr. akamwambia Suzy alale kwenye kitanda kilichokuwepo mle chumbani.

Kitu cha kwanza alichokifanya Dr. ni kupima ujauzito ule ulikuwa na miezi mingapi. Jibu alilolipata kwenye vipimo vilizidi kumpa changamoto Daktari. Ujauzito wa Suzy ulikuwa na ukubwa wa miezi tisa. Kengere ya hatari ikagonga kichwani mwa Daktari. Ni wazi kitendo cha kutoa mimba kubwa vile kilikuwa ni hatari kwa maisha ya mama na mtoto.

Pamoja na vikwazo vyote vili alivyokuwa akivifahamu Daktari lakini hakupenda kushindwa katika kazi yake na kupelekea kupoteza uhodari wake katika kazi yake ile iliyokuwa haramu kwa haki za binadamu n ahata mbele za Mungu. Aliendelea kumshughulikia mteja wake yule na baada ya muda kidogo akamaliza na kumruhusu Naima aingie tena kwa daktari.

“Vipi Dr. Mbona haraka hivyo?” Naima alihoji kwa mshangao akionekana kuwa mzoefu katika mambo yale.

“Hebu keti basi tuongee” alisema Dr kwa sauti ya chini.

Naima aliketi kwenye kiti lakini wasiwasi wa kushindikana kwa zoezi lile ulikuwa umemtawala. Hakutaka kabisa kuona Suzy akijifungua katoto kale kalichokosa baba wa kukalea.

“Vipi Daktari imeshindikana?” alihoji Naima huku amekunja sura yake kwa mashaka na macho ameyatupia kwa Suzy ambaye alikuwa bado amebebelea tumbo lake.

“Naomba utulie Naima” alizungumza Daktari huku akivua glovs kutoka kwenye mikono yake.

“Naona leo mambo ni tofauti nasiku zote” Naima alizungumza.

“Ni kweli leo mambo ni tofauti” Daktari alizungumza huku akijiegemeza kwenye kabati na kufunga mikono kifuani kwake.

“Kwahiyo umeshindwa Daktari?” alihoji Naima kwa sauti ya kukata tamaa.

“Nishindwe! Nani amekwambia mimi huwa nashindwa?” Daktari yule alizungumza kwa kujiamini.

“Sikiliza Naima, hii mimba ni kubwa mno” Daktari alieleza.

“Kwahiyo haiwezekani tena?”

“Kwanini isiwezekane? Kwangu hakuna jambo linaloshindikana Naima au umenisahau” Dakatari yule alizungumza kwa kujisifia.

“Sasa kama haushindwi kinachosubiriwa hapa ni kipi?” Naima alizungumza kwa jazba.

“Mimba ikiwa kubwa hivi huwa haichomolewi kwa kuchokolewa” Daktari alieleza kwa sauti ya upole.

“Fanya basi hivyo inavyowezekana tumalize”

“Tayari mimi nimemaliza” Daktari yule alieleza huku akitabasamu.

“Acha basi utani Mtaturu, tumbo naliona hilo limetuna unasema umemaliza?” alizungumza Naima kwa mshangao.

“Tumbo lipo lakini mimba haipo” Dr Mtaturu alieleza kwa kujiamini.

“Sasa ndio inakuwaje hiyo?” alihoji Naima kwa umakini mkubwa huku matumaini ya kuteketeza ujauzito ule wa Naima.

“Mimba kubwa huwa tunaichoma sindano, ndani ya masaa 24 kwisha” alieleza daktari kwa kujiamini.

“Hii ya leo kali Dokta”

“Ndio hivyo, na tayari nimemchoma sindano yenyewe” Daktari alieleza.

“Halafu?”

“Nendeni tu nyumbani msikilizie, hali yoyote ikijitikeza tutaarifiane” Dokta Mtaturu alieleza.

“Lakini haina madhara Daktari?” Suzy ambaye alikuwa amekaa kimya muda mrefu akatupia swali.

“Hiyo haina madhara kabisa. kama kutatokea shida mtanipigia simu” alisema Dr. Mtaturu kwa kujiamini na kuwafanya Naima na Suzy kuwa na Imani juu ya huduma waliyokuwa wamepatiwa.

***

Vitendo na vituko alivyokuwa akifanyiwa Ayubu na wapangaji wenzake vilimfanya atengeneze wazo la kuishi na mwanamke kama mke ili heshima yake isije ikapotea. Alihisi kuwa pengine wanawake wa pale ndani wangemuogopa na kumheshimu.

Mwanamke aliyekuja haraka kwenye akili ya Ayubu hakuwa mwengine bali ni Naima yule aliyekutana naye kule mgahawani. Uzuri wa binti yule ulikuwa unatosha kumfanya kuwa mke wake wa muda hadi pale atakapofanikiwa kumpata mpenzi wake Suzy.

Sauti ya mlango ukigongwa ilimgutusha Ayubu kutoka kwenye lindi la mawazo. Alikurupuka na kuvaa bukta kisha akaenda kufungua mlango ule. Macho yake yakakutana na macho ya Asha. Moyo wake ukampasuka mithili ya pulizo lililojazwa upepo uliopitiliza.

“Vipi ulikuwa umelala nini?” Asha alihoji kwa sauti yake ile ya kubania.

Ayubu aliitikia kwa kichwa pasipo kutoa sauti yake na kujifanya kufikicha macho kama vile alikuwa kwenye usingizi mzito.

“Samahani kaka Ayubu” alisema Asha na kuinamisha kichwa chini kama vile alikuwa akimuonea aibu Ayubu.

“Bila samahani” Ayubu akajibu

“Mama hayupo” Asha alisema kwa woga huku akibonyeza bonyeza vidole vyake vya mikono.

Ayubu alimtazama kwa makini Asha kutokana na yale maelezo yake ambayo hayakuwa yanaeleweka.

“Kwahiyo?” alihoji Ayubu.

“Nilikuwa naomba tule chakula pamoja” alisema Asha kwa upole na kuinua macho kumtazama Ayubu usoni. Kiukweli kanjaa kalikuwa kanamsokota Ayubu, hivyo akaona ilikuwa dhambi kubwa sana kuiachia bahati kama ile. Pia hakuona kitu kibaya kula chakula pamoja na Asha kwani hata yeye pia alikuwa hapendelei kula pekeyake. Alitoa tabasamu huku akimuangalia Asha machoni.

“Usijali dada Asha nimekuelewa”

“Asante sana kaka Ayubu, ngoja nikamalizie kuandaa basi” alisema Asha kwa furaha na kuondoka kuelekea chumbani kwao. Ayubu naye akarudi chumbani na kufunga mlango wake.

Baada ya dakika kadhaa Asha alirejea akiwa na sinia mkononi lililokuwa na chakula. Baada ya kubisha hodi aliingia na kumkuta Ayubu amejilaza kitandani. Safari ile Asha alirejea akiwa amejifunga kanga moja tu kifuani. Kanga ambayo iliruhusu chuchu za dada yule zilizokuwa na ncha kali kukaribia kuitoboa ile kanga. Urefu wake ulisababisha kanga kuishia juu ya mapaja yake ambayo hayakuwa manene lakini yaliyokuwa yamenona na kuvutia. Michirizi ya kufuli lake ilishindwa kujificha isionekane juu ya kanga ile. Ayubu alipomtazama akajikuta akiguna ndani kwa ndani.

Asha Alivuta kistuli kilichokuwa pembeni na kuweka chakula juu yake. Harufu ya ndizi zilizokuwa zimepikwa kwa kuchanganywa na nyama ilimuingia Ayubu na kujikuta akimeza mate. Asha akachukua maji kutoka kwenye ndoo moja iliyokuwemo ndani mle na kutia kwenye jagi la maji ya kunywa. Baada ya maandalizi akasimama na kumtazama Ayubu ambaye alikuwa amejilaza kitandani akimtazama mwanamke yule alivyokuwa akijishughulisha kwa juhudi.

“Kaka Ayubu” Asha aliita huku akikutanisha viganja vya mikono yake na kuvisugua.

Ayubu alijiinua pale kitandani na kuketi kitako huku macho yake yakiwa kwenye lile sinia lililokuwa na msosi.

“Karibu chakula” alisema Asha.

“Asante, lakini mbona wewe uko wima?” Ayubu alihoji.

“Nakaa nilikuwa nakukaribisha kwanza wewe” alizungumza Asha huku akivuta stuli nyingine na kuketi. Alikuanya kanga yake na kuibana katikati ya mapaja na kupelekea mapaja hayo kuzidi kuwa wazi. Akachukua maji na kumnawisha Ayubu halafu akainua bakuli na kuliweka juu ya mapaja yake na kuanza kuosha mikono yake taratibu.

“Tuendelee kaka Ayubu” alisema Asha huku akiendelea kunawa.

“Usijali Asha, mimi tena unanibembeleza kula? Subiri nikuoneshe” alisema Ayubu huku akichota ndizi kwa kijiko na kupeleka mdomoni.

Asha alikuwa bado akimtazama Ayubu huku akiendelea kujimiminia maji kutoka kwenye jagi.

Kitendo kile cha Asha kumshangaa Ayubu huku akinawa kilipelekea mwanamke yule kukoea kulenga na kujikuta akijimiminia maji kwenye mapaja yake badala ya kumimina kwenye bakuli.

“Mamaaa!” Asha alishituka na kupiga kelele.

“Oh! Pole sana dada Asha” Ayubu akazungumza kwa huruma.

“Asante” Asha alijibu huku akijiinua. Kanga ilikuwa imegandamana kwenye ngozi yake na kuzidi kuonesha lile umbo lake la kimisi.

Asha alikusanya pembe za kanga yake na kuanza kuikamua. Kitendo kile kilipelekea kujifunua ili kupata uwezo wa kufanya zoezi lile la kukausha nguo yake. Ayubu akajikuta akizidi kuwa katika wakati mgumu baada ya kukiona kiuno cha mrembo yule kikiwa kimepambwa kwa shanga. Akakumbuka kiuno cha mpenzi wake Suzy ambacho kilikuwa na furushi la chachandu.



“Nenda kabadilishe nguo dada Asha” Ayubu alizungumza baada ya kuona Asha alikuwa akizidi kumuweka katika wakati mgumu.

“Ah! Usijali kaka Ayubu nimesha kauka.” Alisema Asha huku akijiweka kwenye stuli na kuvuta bakuli la maji. Safari hii akanawa kwa uangalifu mkubwa, na baada ya hapo waliendelea kupata msosi.

****

Ilipofika mida ya saa kumi na moja za asubuhi kule kwa Naima, hali ya Suzy ilibadilika na kuhisi maumivu makali ya tumbo. Akamfahamisaha Naima na kuambiwa ajitahidi kuvumilia pengine mimba ndio ilikuwa ikianza kuharibika. Dakika zilivyozidi kuongezeka ndivyo maumivu nayo yalivyo zidi kumtesa. Suzy alishindwa kuvumilia na kujikuta akilia kama mtoto mdogo. Mwanzo alikuwa akilia kimya kimya lakini baadae akajikuta akilia kwa sauti. Maumivu yale yaliambatana na damu nyingi.

Naima alipoona mambo yamekuwa magumu, akachukua simu yake na kubonyeza namba za Doctor Mtaturu.

“Halloo Doctor” aliita Naima.

“Karibu nakusikiliza” Sauti ya Dokta Mtaturu ilijibu.

“Dokta hali ya mgonjwa wangu ni mbaya sana”

“Ni yupi huyo?”

“Yule wa Naima”

“Ahaa, nyumbani si ni pale pale Msewe?”

“Ndio Doctor”

“Sawa nakuja sasahivi”

“Naomba usichelewe Doctor, hali ni mbaya sana asije akanifia mtoto wa watu” Naima alizungumza kwa hofu kubwa.

“Usijali mimi ndio natoka”

“Sawa” alijibu Naima na kukata simu.

Hali ile aliyokuwa nayo Suzy ilimuogopesha sana Naima. Alijikuta akijuia uamuzi wake wa kumshawishi Suzy kuharibu mimba ile. Pamoja na kwamba alikuwa amezoea kuchomoa mimba lakini wasiwasi bado ulikuwa umemuandama.

Baada ya muda mfupi Daktari alikuwa amekwisha fika pale nyumbani kwa Naima. Alimkuta Suzy katika hali mbaya sana. Alichofanya ni kuvaa gropsi na kumuweka Suzy kitandani.

“Naima naomba unisubiri nje” Dokta alizungumza huku akimuweka sawa Suzy pale kitandani.

Naima hakutoa neno lolote zaidi na kutoka nje kumpisha daktari atoe msaada wake kwa mgonjwa yule.

“Binti, nipo hapa kuokoa maisha yako, tafadhali unipe ushirikiano” Daktari alizungumza kumueleza mgonjwa wake.

Kule nje alipokuwa Naima amani ilitoweka na wasiwasi kutawala moyoni mwa Naima. Aliogopa sana kushuhudia Suzy anakufa mikononi mwake tena kwa kumlazimisha kutoa mimba. Wakati akiwa katika lindi la mawazo akasikia sauti ya mtoto mchanga ikilia kutokea chumbani mle.

Kitendo kile kilimshitua sana Naima. Ingawa yeye alikwisha fanya tukio lile la kutoa mimba mara kadhaa lakini hakuwahi kusikia mtoto aliyeharibiwa akilia.

“Hongera binti, una mtoto wa Kiume.” Alisema Daktari kumueleza Suzy na kuendelea kutoa huduma zake kwa mama mzazi.

Suzy hakuamini macho yake, moyo wake ukawa umetumbukia nyongo. Alichokuwa amekitegemea sicho kilicho tokea. Alikwisha dhamiria kuharibu mimba ile, na ndivyo walivyokuwa wamekubaliana na Daktari yule. Akabakia kimya akimtazama yule mtoto ambaye alikuwa amefanana kabisa na Ayubu.

Naima aliposikia sauti ya mtoto mchanga akafungua mlango na kuingia chumbani pasipo kubisha hodi.

“Vipi Daktari?” alihoji Naima kwa wasiwasi.

“Mgonjwa wetu amejifungua mtoto wa kiume” alizungumza Daktari huku akitoa tabasamu.

Naima hakufurahishwa hata kidogo na habari ile, alikunja uso na kutoa msonyo kwa hasira.

“Kwani tulikubaliana nini Doctor?” Naima akahoji

“Tulikubaliana kuharibu mimba, lakini kwa bahati nzuri amejifungua salama” Daktari yule alizidi kumtia hasira Naima kutokana na maneno yake.

“Huu ni ujinga Doctor! sisi sio wapumbavu tuliokwambia uharibu hii mimba” alizungumza Naima huku akinyooshea kidole pale alipokuwa amelala yule mtoto akinyonya maziwa ya mama yake.

“Lakini sidhani kama kuna kitu kimeharibika” Dactari alizungumza huku akikusanya vifaa vyake na kuviweka kwenye box lake maalum.

“Kwakweli umeniudhi! Dokta umeniudhi sana leo. Nani amekwambia anashida na kitoto hapa?” Naima aliendelea kuzungumza kwa jazba na hasira.

“Unatakiwa kumshukuru Mungu, vinginevyo mama na mtoto wote tungewapoteza” Daktari yule alizungumza kwa sauti ya chini lakini kwa kujiamini sana.

“Kama ulikuwa huwezi si ungetuambia tutafute mtu mwingine wa kutusaidia” Naima aliendelea kulaumu.

“Nimeshaua sana mama ngoja hata mara moja moja nimfurahishe Mungu” Daktari alizungumza huku akiweka sawa vifaa vyake.

“Acha unafki Dokta, kama kweli unataka kumfurahisha Mungu mbona ulimchoma sindano ya kutoa mimba?” alizungumza Naima.

“Ile ilikuwa ni sindano ya kuleta uchungu na sio ya kuharibu mimba mama” Dakari alieleza kwa ile sauti yake ya upole.

“Unazungumza nini? Naomba uondoke nyumbani kwangu Dokta!” Naima alizungumza kwa hasira zaidi huku amekunja sura yake.

“Hata hivyo naondoka unafikiri nitabaki hapa?” alizungumza Dokta Mtaturu.

“Nenda sasa unasubiri nini?” alifoka Naima.

“Kama kukitokea tatizo lolote kuhusu mgonjwa naomba mnifahamishe. Usiache kumchemshia juisi ya rozela ili kurejesha damu iliyopotea” Daktari alizungumza na Naima

“Kwenda zako ufahamishwe utumbo gani?”

“Sawa ila mi nipo hewani muda wote” alizungumza Doctor Mtaturu huku akiondoka.

“Hivi we mwanaume umetumwa? Si uondoke?” alizungumza Naima kwa jazba.

“We mama mtunze mwanao atakusaidia kesho yako” alizungumza Daktari kumwambia Suzy kiasha akachukua begi lake na kuondoka akimuacha Naima amefura kwa hasira na Suzy akiendelea kumnyonyesha mtoto wake mchanga.

****

Kule chumbani Ayubu alikuwa akijitahidi kukwepesha macho yake kuangalia kwenye mapaja ya Asha ambayo yalikuwa yamefunikwa kwa ile khanga aliyokuwa amevaa ambayo ililowana kwa maji. Kimya kilitawala kwa muda mrefu hadi pale walipokutanisha macho yao na kujikuta kila mmoja akitoa tabasamu.

“Vipi” Asha alihoji kwa sauti laini huku akitabasamu kwa aibu.

“Hamna kitu. Ila chakula kitamu” Ayubu akaunguruma

“Kimepikwa hicho na mwanamke anayefaa kuolewa” Asha akazungumza huku akinyonga nyonga shingo yake.

“Kwakweli shemeji yangu atafaidi sana” Ayubu akanogesha mazungumzo yao.

“Hata wewe unaweza kufaidi”

“Si ndio hivi nafaidi”

“Bado huja faidi. Lakini ukitaka utafaidi” Asha alizungumza kwa mafumbo

“Mnh!” Ayubu akaguna baada ya kusikia maneno yale kutoka kwa Asha.

“Vipi mbona unaguna?”

“Walaa hamna kitu” alizungumza Ayubu huku akipeleka kijiko mdomoni kilichokuwa kimejaa ndizi. Kwa bahati mbaya mchuzi wa ndizi ukamdondokea kifuani. akataka kujifuta lakini Asha akamzuia.

“Ngoja kwanza usijifute” alisema Asha huku akijiinua kutoka pale kwenye stuli alipokuwa ameketi. Akamsogelea Ayubu taratibu na kuinua upande wa kanda aliyokuwa amejifunga na kuipeleka hadi kifuani kwa Ayubu na kuanza kumfuta taratibu.

Wakati Asha alipokuwa anamfuta Ayubu ilimlazimu kuinua mguu na kuweka goti moja kitandani ili kanga ile iweze kufika vizuri pale ilipokuwa imekusudiwa. Kitendo kile kiliruhusu kanga ile kukaa upande na nguo ya ndani ya Asha ambayo ilikuwa imelowana kwa maji kuonekana waziwazi.

“Basi Asha inatosha” alizungumza Ayubu kwa sauti ya chini iliyo kwaruza.

“He! Mbona nimefuta lakini bado havitoki!” alisema Asha baada ya kuangalia pale alipokuwa akipafuta. Aliachia kanga yake na kupeleka mdomo wake kwenye kifua cha Ayubu. Alitoa ulimi na kuanza kumramba kifuani kijana wawatu. Jamani nyie mnh!

Ayubu alianza kusisimkwa kwenye mwili wake kutokana na kitendo kile alichokuwa akifanyiwa na Asha. Akawa anajitahidi kumuondoa Asha kutoka kwenye kifua chake lakini msichana yule alikuwa ameganda kama ruba.

“No Asha usifanye hivyo” Ayubu akajitahidi kumsihi msichana yule.

Wakati Ayubu akijitahidi kumshawishi binti yule kusitisha zoezi lake lile alijikuta akisukumwa na kudondokea kitandani.

Ayubu alidhani tabia ile ya ushawishi na kulazimishana kumega tunda ilikuwa ni ya Suzy peke yake, kumbe kalikuwa ni katabia ka wanawake wengi hasa wa mjini. Ndio ni wa mjini kwasababu hata siku moja kule kijijini Yasini hakuwahi kukutana na vitukokama vile.

Asha akiwa alidondokea juu ya Ayubu na kupeleka mkono wake haraka sana kushika bunduki ambayo ilionekana kujaa risasi tayari kwa mapambano. Kitendo kile kilimpandisha Ayubu maruhani yake ya kitanga na kuanza mishe mishe ambazo hazikujulikana zilitokea wapi.

Kufumba na kufumbua ile kanga ya Asha ilikuwa pembeni ikishuhudia mpambano ule. Kama kawaida ya Ayubu, wakati wote alipokuwa katika uwanja kama ule hakuwa mvivu kufanya majambozi ambayo wadada wengi walikuwa wakiyahusudu. Asha alikuwa akilalamika kama vile alikuwa akitolewa roho. Yale aliyokuwa akihadithiwa aliweza kuyashuhudia mwenyewe. Ndani ya dakika chache tu akajikuta akiomba aonje kidogo asali ile iliyokuwa imerambwa na mama mwenye nyumba wao.

“Ay…Ayub…Ayububu..bu….nipe na mimi usisisi.. ooh!...Yes!” Asha alisikika akilalamika.

Asha alikuwa tofauti kabisa na Bi.Sada. Ingawa alikuwa na umbo dogo lakini alishindwa kujituma ipasavyo. Alikuwa ni mchovu mno, kiasi cha kulala kama mgonjwa wa degedege huku akilalamika. Kama angekutana na mwanaume mchovu hakika angeambulia patupu na mchezo usingenoga.

“Asssccss…..aaah!...mmnh!....Ayubu nipe…nipe Oyubu…ooooh!..” Asha alizidi kulalama kwa sauti yake iliyoshindwa kutofautiana na ile ya mgonjwa aliyekuwa mahututi.

Wakati Ayubu na Asha wakiendelea kupeana mavituzi, Mama Asha alikuwa akirejea kutoka safari zake. Alipokuwa akipita kwenye mlango wa Ayubu akajikuta mapigo ya moyo wake yakimuenda mbio. Akaelekea chumbani kwake kwa haraka. Lengo lake lilikuwa ni kuhakikisha kama Asha alikuwemo. Alipobaini hakuwemo akatoka kwa mbio sana na kwenda kusimama mlangoni kwa Ayubu.

Baada ya sekunde kadhaa alitoka nje na kumuulizia kwa wapangaji wenzie lakini walimfahamisha kuwa Asha alikuwa ndani. Walihakikisha kuwa Asha alikuwa ndani kwasababu wao walikuwa wameketi pale barazani kwa muda mrefu na hawakumuona akitoka nje.

Mama Asha akapumua kwa nguvu na kurejea ndani. Aliingia tena chumbani kwake kuhakikisha kama kweli mtoto wake hakuwemo. Jibu alilolipata lilikuwa ni lile lile, Asha hakuwemo ndani mle.

Alisogelea mlango wa Ayubu kwa maranyingine, alitazama kwamakini pale mlangoni kulipokuwa na viatu vilivyo fanana ya viatu vya binti yake Asha. Aliinama na kuokota kimoja kisha akawa anakiangalia kwa makini. Akahakikisha kwa asilimia zote kuwa kiatu kile kilikuwa ni kiatu cha mtoto wake Asha.



Mapigo yake ya moyo yakazidi kumuenda mbio na kuhisi mwili ukimtetemeka. Akatoka tena nje kwa wale wapangaji wenzake. Walipomuona tu wakamuuliza kabla yeye hajazungumza kitu.

“Vipi Asha umemuona?” alihoji mama Kobelo.

“Ndio nimemuona, kumbe alikuwa chumbani amelala” mama Asha akaongopa huku akili yake ikiwa imevurugika.

“Nasisi tulitaka kushangaa maana hatukumuona akitoka”

“Hivi jamani huyu Kijana amesharudi?” mama Asha akahoji.

“Kijana gani, Ayubu?”

“Ndiye huyo huyo”

“Alaa kumbe kidume vha mbegu, leo hakutoka kabisa. Amejifungia ndani kama utumbo” alisema mama Kobelo na kusababisha wale wapangaji wengine kuangua kicheko baada ya kusikia jina la kidume ambalo alipewa Ayubu.

“Vipi Shoga unataka akutibu nini?” mama Mariamu alihoji kwa masihara.

“Unataka baba Asha aniue nini?” alizungumza mama Asha kwa kujilazimisha.

“Jamani raha za Kidume tuachieni sisi ambao hatujaolewa. Yaani hapa nilipo ninavyo mtamani sijui siku akiingia mikononi mwangu itakuwaje” alizungumza Zuhura msichana aliyekuwa akisukwa nywele.

Mama Asha akasonya na kuingia ndani kwa hasira. Maneno ya Zuhura yalikuwa yamemchoma sana na kujikuta akimuonea wivu binti yake ambaye alikuwa na uhakika wa asilimia zote kuwa alikuwa chumbani kwa Ayubu akipewa hizo raha alizozizungumzia Zuhura.

Alikwenda hadi kwenye mlango wa Ayubu na kujishauri agonge ama asigonge. Wakati akiendelea kukata shauri, alishtushwa na sauti ya mahaba ikitokea chumbani mle. Sauti ile aliifahamu kabisa. Haikuwa ya mtu mwingine bali ilikuwa ni sauti ya binti yake Asha. Akasogeza zaidi sikio lake mlangoni ili kusikia vizuri na kupata uhakika kamili.

“Aaaaamnh!....Ayubu….usinibanie…ooohmn!.....taratibu. Ayubu….Oshaaa!” mama Asha alisikia vizuri sauti ya binti yake ikitokea kwenye chumba kile.

Mama Asha hakutaka kukubaliana kirahisi na masikio yake na kuamua kutega tena kupata uhakika zaidi.

“Oooo….Yeah!....Tamu….asccsscs….Baby…tarat…ta..ta…oh!” Asha aliendelea kulia kwa raha zilizochanganyikana na uchungu mtamu mle chumbani mwa Ayubu huku wakimtesa mama Asha aliyekuwa mlangoni.

***

Mama Suzy alihangaika kwa muda mrefu pasipo kuona hata dalili ya kumpata mwanawe. Alikuwa amechoka kuliko kawaida. Akakumbuka jinsi mume wake alivyomtoa mkuku kwenda kumtafuta Suzy. Kwakweli ilikuwa ni kazi ngumu sana ambayo haikuwa na matumaini hata chembe. Kwasababu mtu mwenyewe waliyekuwa wakimtafuta haikufahamika kama alikuwa yumo ndani ya jiji la Bongo au ametoka.

Mama Suzy akaamua kurejea nyumbani akamfahamishe mume wake kuwa hakufanikiwa kumpata mtoto wao waliyekuwa wakimpenda sana. Alitembea taratibu huku akihisi nguvu zikimuishia kila alipokuwa akikaribia nyumbani kwake. Hakufahamu angemuelezaje mzee Manyama ili amuelewe.

Alipobakiza hatua kadhaa kufika kwenye mlango wa nyumba yake alisimama na kutafakari cha kufanya. “Kama usipompata mwanangu usirudi hapa ndani” ilikuwa ni sauti ya mzee Manyama ikijirudia ndani ya upongo wake. Akapumua kwanguvu kisha akausogelea zaidi mlango.

Mama Asha alikamata kitasa cha mlango na kuusukuma taratibu ili kama mume wake alikuwemo ndani asiweze kumsikia mapema. Akafanikiwa kuingia ndani pasipo kuona dalili yoyote ya kuwepo kwa mtu mle ndani. Akajikuta akishukuru mungu na kuzidi kuomba mzee yule awe bado kurejea kutoka kazini.

“Naamini upo pamoja na Binti yangu” ilikuwa ni sauti ya mzee Manyama. Kumbe mzee yule alikuwa ameketi kwenye kochi lililokuwepo kwenye kona pale sittingroom.

Mama Suzy akashituka kiasi cha kutaka kudondoka chini. Hakuamini macho yake pale alipomuona mume wake ameketi kwenye kochi akimkodolea macho.

“Mtoto wangu yuko wapi?” alihoji mzee Manyama kwa sauti ya chini huku akiwa ameegemea kwenye kochi na mguu wake wa kulia akiuchezesha chezesha.

“Sikufanikiwa mume wangu sijui….” Mama Suzy alizungumza lakini kabla ya kumalizia akakatishwa na mume wake.

“Kefuleee!....sasa umerudi kufanya nini?” alihoji mzee Manyama kwa ukali.

“Mume wangu jiji kubwa hili na sijui ameelekea wapi” Mama Suzy akajaribu kujitetea.

“Kumbe ni mgumu kuelewa we mwanamke, Suzy ndiye moyo wangu. Ninashindwa kufanya kazi zangu kwasababu ya kumpoteza mwanangu. Wewe ndiye uliyesababisha” alizungumza mzee Manyama kwa sauti nzito.

“Lakini mume wangu wewe si ndiye uliye mfukuza” Mama Suzy akajitetea.

“Kefuleee!...kama sio kale kajitu kako ulikokaleta Suzy wangu angeharibikiwa?” alihoji Mzee manya kwa hasira.

“Lakini baba Suzy….” Mama Suzy alitaka kuzungumza kitu.

“Shutup!...naona nakubembeleza. Hebu ondoka mbele ya macho yangu” Mzee manya akaunguruma kwa hasira. Mama Suzy alipoambiwa vile akataka kuondoka kuelekea chumbani lakini akazuiliwa.

“Wee Kunguni unakwenda wapi?” alihoji mzee Manyama kwa sauti kali.

“Naenda chumbani mume wangu”

“Naomba tuelewane mwanamke, kwanini unataka tugombane?”

“Kwani vipi mume wangu?”

“Ni hivi, naomba…utoke…nje…ukamtafute…mtoto….wangu….umenielewa?” Mzee manyama akazungumza kwa kukazia maneno yake. Macho yake yalibadilika rangi na kuwa mekundu kama nyanya mbivu, dalili ambayo haikuwa nzuri machoni mwa mama Suzy. Midomo ya mzee yule ilikuwa ikitikisika kwa hasira na mara kazaa alisikika akikung’uta pua zake kama vile zilikuwa zimeziba.

*****

Wakati Ayubu na Asha walipokuwa wakiendelea kuburudishana kule chumbani mwa Ayubu, Mama Asha alikamata kitasa cha mlango na kukinyonga. Kwa bahati mbaya au nzuri mlango ule haukufunguka kwasababu ulikuwa umefungwa kwa ndani. Alivyoona vile akagonga mlango kwa nguvu akimtaka Ayubu afungue.

Zoezi lile la mama Asha liliwakata stimu Asha na Ayubu kule ndani ya chumba cha Ayubu. Utamu wote ukaisha na kugeuka kuwa uchungu. Sauti ya mama Asha ndiyo iliyo watisha zaidi. Chumba chenyewe hakikuwa na sehemu ambayo Asha angeweza kujificha asionekane zaidi ya uvunguni.

“We Ayubu ebu fungua mlango, ukisubiri baba Asha arudi utapata shida” alisema mama Asha kwa sauti ya msisitizo.

Ayubu akamuelekeza Asha aingie chini ya uvungu ili ajifiche asije akaonekana na mama yake. Asha akaingia uvunguni pasipo kuzungumza kitu chochote. Ayubu akajivisha vizuri kisha akauendea mlango.

Ayubu alipofungua tu mlango mama Asha akajitoma ndani. Alipofika akaanza kuangaza kila mahali mle chumbani.

“Asha yuko wapi?” alihoji mama Asha huku akihema kwa hasira na mikono ameiweka kiunoni.

“Asha! Mbona mi sijui alipo” Ayubu akajifanya kushangaa.

“Sikiliza kijana, tusisumbuane. Nimesikia kila kitu namuomba mwanangu. Nikimtafuta mwenyewe utapata tabu” alizungumza mama Asha kwa hasira.

Kitu cha kushangaza kule chini ya uvungu Asha alikuwa akitaka kucheka. Alifahamu kabisa kuwa Ayubu alikuwa akitamaniwa na wanawake wengi mle ndani, akiwemo na mama yake huyo. Hivyo akaona ile ilikuwa ndiyo nafasi pekee ya kudhihirisha uma kuwa Ayubu alikuwa ni wake.

“Mama mimi nilikuwa nimelala sijui chochote” Ayubu alijitahidi kujitetea.

“Hivi vyombo si vya kwangu huku vimefikaje?” alihoji mama Asha baada ya kuona vyombo vyake ambavyo Ayubu alikuwa akivitumia kula chakula na Asha.

“Nimekuja navyo mimi mama” Sauti ya Asha ilisikika ikitokea chini ya uvungu.

Ayubu akajikuta akiishiwa na pozi baada ya kumsikia Asha akijibu swali ambalo hakuulizwa yeye kule chini ya uvungu.

Asha akajichomoa kama vile mzimu uliokuwa ukitokea kaburini. Macho yake yaliyokuwa makavu yasiyo na hata chembe ya aibu yalikuwa yakipepesa bila kutulia. Ayubu akawa ameinamisha kichwa chini kwa aibu huku akimtafakari mwanadada yule aliyefanya vitu vya ajabu. Asha akamtazama mama yake kisha akamtazama Ayubu na kujikuta akiangua kile kicheko chake alichokuwa anakizuia kwa muda mrefu kule chini ya uvungu.

“Pumbavu, unacheka unadhani yamenifurahisha haya?” alihoji mama Asha kwa ukali.

“Kwani tatizo liko wapi mama?” Asha akajibu huku akimuegemea Ayubu. Alifanya vile makusudi kwasababu aliwahi kumsikia mama yake akizungumza na mama Kobelo kuwa ni lazima ampate Kidume Ayubu. Kwahiyo lengo lake lilikuwa ni kuvuruga nia ya mama yake kwa kijana aliyempa vitu adimu.

“Sikiliza kijana, huyu binti atakuponza. Lazima nije kumueleza baba yake. Haiwezekani anidharau hivi” alisema mama Asha huku akitetemeka kwa hasira.

“Hapana mama, nisamehe mimi sina dharau” Ayubu aliomba radhi.

“Mimi sielewi subirini wenyewe mtaona” alisema mama Asha na kutoka mle chumbani.

Tabia ile ya Asha ilikuwa imeumuacha hoi Ayubu. Hakuweza kuelewa kama hapa ulimwenguni kulikuwa na wanawake vichaa kama Asha. Lile balaa alilokuwa amelikimbia kule kwa mzee Manyama hatimae lilimfuata kule kule alipokuwa akiishi kwa mara nyingine.

“Umefanya nini sasa Asha?” Ayubu alihoji kwa hasira baada ya mama Asha kutoka na kuwaacha wao wawili chumbani mle.

“We niachie mimi yule namuweza” alizungumza Asha kwa upole.

“Umeshaniharibia Asha” Ayubu alizungumza kwa unyonge.

“Nimekwambia usijali. Mama yangu mi namjua” alisema Asha na kumpiga busu Ayubu kisha akatoka chumbani mle na kumuacha Ayubu katika wakati mgumu.

Ayubu akajikuta akijilaumu kwa uamuzi aliouchukua wa kukubali kula chakula pamoja na Asha. Alitambua kuwa mwisho wa yeye kuishi pale ulikuwa umefika. Akajiinua kwa taabu na kwenda kujimwagia maji ya baridi na baada ya hapo alitoka kwenda kunyoosha miguu huku maneno ya Asha yakimfariji. Alifahamu jinsi Asha alivyokuwa akipatana na mama yake, hivyo akaamini kuwa Asha angezungumza na mama yake na kusinge haribika kitu.

****

Baada ya daktari kuondoka kule Msewe, Naima alimkazia macho Suzy ambaye alikuwa akimnyonyesha mtoto wake pale kitandani.

“Nawewe unafanya nini sasa? Huyo mtoto hana haki ya kuishi” Alizungumza Naima kwa jazba huku akimsogelea Suzy.pale kitandani na kumgusa yule mtoto kwa kidole chake cha shahada kama vile alikuwa akimbonyeza.

Suzy ambaye muda wote alikuwa kimya alimkodolea macho mtoto wake kwa makini na kubaini kuwa alikuwa amefanana kopiraiti na Ayubu. Akavuta pumzi na kuzitoa kwanguvu. Naima alijishika kiuno na kuwatazama kwa makini Suzy na mtoto wake walivyokuwa wakinyonyeshana.

“Mamaa wa mtoto unasemaje?” alihoji Naima huku akijitingisha tingisha kwa kebehi.

“Naima nimefurahi kumuona Ayubu wangu. Yaani unavyomuona huyu mtoto na Ayubu hakuna tofauti.” Alisema Suzy huku akitabasamu.

“Ebu wacha upumbavu Suzy! Utaishije na haka katoto?” alihoji Naima kwa hasira.




“Kwahiyo unataka kunifukuza Naima?” Suzy akahoji kwa hofu.

“Ebu fikiria maisha uliyokuwa ukiishi kipindi ulipokuwa unaweza kujishughulisha, sasa hivi umekuwa mzazi utaishi vipi?” Naima akahoji huku akijiweka kitandani na kuwapa mgongo Suzy na mtoto wake.

“Sasa tufanye nini shoga yangu kama ni mgeni ndio huyu tunaye?” alihoji Suzy.

“Unataka ushauri?”

“Ndio” Suzy akajibu kwa mkato.

“Rudi kwa mzee Manyama” Naima alizungumza huku akiwa amegeukia ukutani.

“ He! Yamekuwa hayo Naima. Yaani ni afadhali kwenda kufia porini kuliko kurudi pale kwa yule mzee katili. Unataka nikafe kibudu huko?” Suzy akazungumza kwa uchungu.

“Sasa unadhani utaishije na hako kapanya kako?” Naima alihoji.

“Nionee huruma Naima rafiki yangu”

“Huruma gani nitakayokuonea, Unataka ukae hapa mimi nikulishe?”

“Sina maana hiyo Naima”

“Kumbe?...utawezaje kusaka pesa huku unakatoto kasikokuwa na baba?”

“Hata mimi nimechanganyikiwa Naima, sijui nifanye nini?” Suzy akazungumza huku akibubujikwa na machozi. Naima aliinamisha kichwa chake kwa dakika kadhaa na baada ya pale akainuka na kumgeukia Suzy.

“Dada hii ni Bongo, lazima ubongo utumike ili kupapambana. Mimi nimepata wazo.” Alisema Naima huku akimpigapiga Suzy miguuni. Suzy akatulia na kumsikiliza pasipo kuongea neno.

“Unajua hako kajusi katatuvurugia mipango yetu. Cha msingi tuendelee na wazo letu lilelile” alizungumza Naima.

“Wazo gani?” Suzi akahoji.

“Unakumbuka tulienda kwa Doctor Mtaturu kufanya nini?”

“Si tulikwenda kutoa mimba, au?”

“Unadhani kama mimba ingetoka hako katoto kangekuwepo?”

“Hapana” Suzy akajibu kwa sauti ya upole huku akisikiliza kwa makini wazo la ndugu yake yule.

“Basi, hatupaswi kuendelea kuwa nako” alizungumza Naima kwa kujiamini.

“Unamaanisha nini Naima?” Suzy akahoji kwa wasiwasi.

“Ili uishi kwa uhuru, ni lazima hako katoto tukakatupe” alizungumza Naima kwa sauti isiyo na hata chembe ya wasiwasi. Suzy akajikuta mwili ukimzizima kama vile alikuwa amemwagikiwa na maji ya barafu na maumivu makali sana yalipita chini ya kitovu.

“Yaani tumtupe mwanangu?” alihoji Suzy kwa mshangao mkubwa.

“Sikiliza Suzy, sina maana ya kumuua. Nimekwambia tumtupe kwani kuna ubaya gani?” alisema Naima.

“Sasa tukimtupa huoni kama atakufa?” alizungumza Suzy kwa hofu.

“Naomba unielewe Suzy, huyu mtoto hatwendi kumtupa porini au dampo”

“Kumbe?”

“Tunakwenda naye mbali na hapa, halafu tunamuweka karibu na njia. Lazima watu wakipita watamuona na kumuokota. Hivyo watamlea vizuri katika mikono iliyo salama kuliko hata wewe mwenyewe” alizunguma Naima kwa msisitizo.

Maneno ya Naima yakaonekana kumuingia vyema Suzy. Akamtazama mtoto wake na kujikuta akifuta machozi yaliyokuwa yakimtoka kwenye jicho lake la kushoto pekee. Akainama na kumpiga busu la utosini

***

Ayubu aliamua kwenda mbali kidogo na pale nyumbani ili kukwepa kukutana na macho ya mama Asha. Kichwani mwake kulikuwa na mawazo lukuki juu ya lile tukio lililomtokea. Alikwenda hadi maeneo ya Ubungo maji na kuporomosha kwenye njia iliyoshuka bondeni upande wa kushoto. Simu yake ya mkononi ikaita na kuitoa. Ilikuwa ni namba ya baba yeke mzee Nyiruka. Akapokea na kuiweka sikioni.

“Halloo baba…”

“Niambie mwanajeshi wangu, hujambo?”

“Sijambo baba shikamoo”

“Marahaba. Haya niambie umefikia wapi?”

“Baba nahitaji kurudi Tanga, maisha ya huku yamenishinda” Ayubu alieleza.

“Kwani nani amekwambia utafute maisha? nimekwambia mtafute mwenzio”

“Sawa baba lakini mtu mwenyewe hajulikani hata alipo. Hakuna hata dalili ya kumpata” Ayubu alimwambia baba yake.

“Tatizo ni nini pesa?” mzee Nyiruka akahoji.

“Hilo likiwemo, pia kuna mambo mengi sana ya ajabu ajabu huku mjini”

“Pesa nitakutumia. Hayo mambo mengine ni kawaida hapo jijini, na ndio maana watu wanapaita Bongo” alieleza mzee Nyiruka kwa msisitizo.

“Sawa baba nitajitahidi”

“Cha msingi ni kutumia ubongo vizuri, vinginevyo unaweza usifikie lengo lako” alisema mzee Nyiruka kwa sauti ya upole.

“Sawa baba nitakuwa makini”

“Haya nakutakia mafanikio katika shughuli yako” alisema Mzee Nyiruka na kukata simu.

Ayubu akatupa macho mbele na kuona sehemu iliyokuwa wazi isiyo na nyumba wala mti. Akapata wazo la kwenda kupumzika maeneo yale ili kutuliza ubongo wake.

Wakati akivuka daraja dogo lililo tenganisha ubungo na msewe akashituliwa na sauti ya mtoto mchanga ikilia ikitokea pembeni kidogo mwa daraja lile, akajikuta mapigo ya moyo wake yakimuenda mbio.

Kwa tahadhari kubwa Ayubu akasogea hadi sehemu ambayo sauti ile ilikuwa ikitokea. Lahaula! Kulikuwa na katoto kamelazwa kwenye boksi huku kimefunikwa vizuri kwa kanga na taulo. Ayubu akabaki kushangaa asijue nini cha kufanya. Baada ya kushindwa kuchukua maamuzi alitoa simu yake na kumpigia mzee Nyiruka.

“Vipi mwanajeshi wangu?” Sauti ya mzee Nyiruka ilisikika kwenye spika ya simu.

“Baba, nimekuta mtoto ametupwa sijui nifanye nini?”

“Mtoto ametupwa?” Mzee Nyiruka akahoji kwa taharuki.

“Ndio baba amewekwa kwenye boksi” Ayubu akaeleza.

“Sasa sikiliza Ayubu..”

“Ndio baba…”

“Mchukue huyo mtoto, halafu uendenae hadi kituo cha polisi.” Alisema mzee nyiruka.

“Sawa baba” Ayubu alijibu kisha akakata simu.

Ayubu alimuokota yule mtoto na kumbeba kwa tahadhari kubwa hadi kwenye kituo kidogo cha polisi kilichokuwepo karibu na pale. Baada ya kufika kituoni na kutoa maelezo ya kutosha walimruhusu Ayubu amchukue mtoto na kwenda kumlea huku uchunguzi ukiendelea.

Kitu kilichompa moyo Ayubu kumchukua mtoto yule ni mpenzi wake Naima. Aliamini kwa asilimia zote msichana yule mrembo asingekataa kumlea mtoto yule aliyedhulumiwa na wazazi wake haki yake ya kuishi.

Alipokaribia kufika nyumbani akakumbuka msala aliouacha wakati anaondoka. Mapigo yake ya moyo yakaanza kumuenda mbio. Akapiga moyo konde na kusogea taratibu huku akisikilizia.

Alifika salama pasipo kuona dalili yoyote mbaya. Wapangaji wenziwe wakawa wakimshangaa walipomuona akirejea huku mkononi mwake akiwa na katoto kachanga. Walitamani kufahamu kijana yule aliyekuwa akiwakosha wanawake wengi mle ndani alipata wapi kale katoto.

Bi.Sada alipokuwa akitoka chumbani kwake akakutana na Ayubu akiingia huku amebeba katoto kachanga.

“Vipi Ayubu?” Mama mwenye nyumba alihoji kwa mshangao.

“Mtoto Bi.Sada” Ayubu akajibu.

“Umemtoa wapi?”

“Nimemuokota” Ayubu akajibu kwa sauti ya chini.

“Hee! Wewe! Hembu njoo huku ndani” Bi.Sada alihamaki na kuingia chumbani kwake, Ayubu naye akamfuata mama mwenye nyumba wake na kuingia mle chumbani.

“Haya sema umemtoa wapi?” alihoji Bi.Sada huku ameshika kiuno.

“Nimemuokota kule kwenye bonde la Msewe na Ubungo” Ayubu alijibu.

“Ukikamatwa sasa?”

“Nimempeleka kituo cha polisi. Nilipomuomba wakanipa nimlee”

“Sasa utamleaje?”

“Itabidi unisaidie kumuangalia, hadi pale nitakapo pata mtu wa kumlea” alizungumza Ayubu.

Bi.Sada hakuwa na kipingamizi kwasababu hakuwahi kuzaa hivyo mtoto yule akamuona kama vile alikuwa ni bahati sana kwake.

“Usiwe na shida ya kumtafuta mtu wa kumlea, wewe atakuita baba na mimi ataniita mama” alisema Bi.Sada huku akimpokea mtoto yule kutoka mikononi mwa Ayubu. Ayubu alimtoa mtoto yule pasipo kuzungumza neno Kisha akatoka kuelekea chumbani kwake.

Alipofika akachukua simu na kutafuta namba za Naima yule msichana ambaye ndiye aliyemkusudia amsaidie kumlea mtoto yule. Nyumbani pale hakuwa na imani napo kutokana na tabia za wapangaji wa pale kuto mfurahisha. Simu ilipoanza kuita akaiweka sikioni.

***

Baada ya mama Suzy kuhangaika kwa muda mrefu, alikwenda maeneo ya Stop-Over ambapo rafiki yake mpendwa aliishi huko. Shoga yake huyo hakuwa mwengine bali ni Bi.Sada yaani yule mama mwenye nyumba wake Ayubu.

Alipofika pale Bi.Sada akashituka sana kwasababu muda ulikuwa umekwenda sana. Hakutegemea kumuona mama yule pale nyumbani kwake usiku kwasababu haikuwahi kutokea hata siku moja.

“Vipi Shoga kwema huko utokako?” alihoji Bi.Sada

“Huko kwema sio kwema” alisema Mama Suzy

“Haya karibu ndani basi”

“Nimekwisha karibia” alijibu mama Suzy na kuingia ndani kwa Bi Sada.

Mama Suzy alikuwa amechoka sana kutokana na kutembea kwa muda mrefu akimtafuta binti yake mpendwa bila ya mafanikio. Sauti ya mtoto aliyekuwa Analia chumbani mle ilimshitua mama Suzy na kumshangaza, hakuamini macho yake kumuona mtoto mchanga amelala kwenye kitanda cha shoga yake yule ambaye hakuwahi kupata mtoto kutokana na vitendo vya kuharibu mimba alivyokuwa akivifanya wakati wa usichana wake.

“Shoga unalea?” alihoji mama Suzy kwa mshangao

“Nalea Shoga yangu”

“Eh hongera!”

“Ahsante shoga”

“Ni mtoto wa nani?”

“Wakwangu” alisema Bi.Sada.

“Hiyo mimba umebeba lini? Na umejifungua lini?”

“Hamna shoga. Kuna mpangaji wangu ameniletea amesema amepewa na serikali baada ya kumuokota” Bi.Sada alieleza.

“Amemuokota?”

“Ndio, na hivi ninavyokwambia mimi ndio mama yake na huyo mpangaji wangu ndio baba yake” alisema Bi.Sada huku akitabasamu.

“He! Kwahiyo umeshajipatia na buzi kabisa”

“Tena usiongee shoga, kijana anavyojua kulisakata kabumbu” Bi Sada alieleza

“Wacha wee!... kwahiyo kumbe amemleta kwa mkewake kabisa?”

“Ohoo! Sasa unadhani kwanini amemleta mtoto kwangu!”

“Hongera Shoga yangu”

“Nakwambia kijana mdogoo! Lakini anavyoyajua”


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG