Search This Blog

Sunday, April 18, 2021

HOUSEGIRL WA KITANGA - 5

   


Chombezo : Housegirl Wa Kitanga 

Sehemu Ya Tano (5)


“Kama ndio hivyo basi nimekusamehe” alizungumza baba huku akivuta hatua kutoka jikoni.

“Ndio ukome!” nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikicheka wakati baba alipokuwa anatoka jikoni.

Niliuinua mwiko wangu juu na kuuangalia kwa kujidai huku nikiachia tabasamu la matumaini.

“Kumbe hii ndio dawa yao! Nitatembea na mwiko wangu kila nitakapokuwa” nilizungumza huku nikiangua kicheko kwa kuziba mdomo nisije kusikiwa na baba akagundua kama nilikuwa namcheka yeye.

Nikiwa naendelea na shughuli zangu za upishi kule jikoni, nikasikia sauti ya baba ikiniita. Nikanyamaza na kujifanya kama vile sikuwa nimesikia wito ule.

“We Mwantumu!” baba aliita tena, safari hiyo aliita kwa sauti kubwa zaidi.

“Abee..” sikuwa na namna ikabidi niitike.

“Njoo mara moja?” baba aliamuru.

Nilisita kidogo lakini nikajipa moyo na kuutazama mwiko wangu kwa sekunde kadhaa kisha nikauweka chini.

“Nisubiri hapa mtoto wangu nakuja” nilizungumza wakati naweka mwiko ule chini.

Nikavuta hatua kuelekea kule sittingroom alipokuwa ameketi baba.

“Abee baba” nikaitika kwa heshima mara tu nilipofika sebleni.

“Umemaliza kupika?” baba alihoji

“Bado sijamaliza lakini ndio namalizia baba”

“Mbona sikuhizi hauvai zile nguo zako nzuri?” baba alihoji huku akitabasamu na kusababisha ile pua yake niliyoipiga mwiko kuzidi kuonekana kubwa. ilikuwa nyekundu utafikiri kipande cha mnofu wa nyama ya kiboko.

“Nguo gani baba?” nikahoji na kujifanya sielewi alichokuwa anakizungumza.

“Zile zilizokupendeza juzi” baba alieleza.

“zile fupi?”

“Ewaaa!, mbona hujavaa tena nikakuona?”

“Sina nyingine baba” nikajaribu kuongopa huku nikimtazama baba kwa jicho la kuibia kwenye ile pua yake iliyokuwa imefutuka kwa kupigwa mwiko na binti wa kitanga. Sijui hata mke wake alikuwa anakuja kumueleza nini akaeleweka.

“Huna nyingine! Sasa mbona husemi?” baba alizungumza.

Nilikaa kimya huku ndani ya moyo wangu nikiomba amalize haraka kuongea ili niondoke na kumuacha mwenyewe. Siku hiyo nilikuwa makini sana na kujitahidi kutomkaribia mtu mzima yule hata kidogo.

“Hebu nenda chumbani kwangu ukaniletee briefcase yangu” baba aliagaza.

Maagizo yale niliyokuwa nimepewa na baba yalinifanya nikumbuke siku ambayo kaka Imran alinituma niende chumbani mwake kumtafutia begi halafu matokeo yake akanifuata na kutaka kunanihii.

“Tumu si nimekutuma au haujasikia” baba akahoji kwa sauti kidogo baada ya kuniona bado nimesiamama utafikiri sikuwa nimesikia agizo lake.

Nilitamani kukataa agizo lile lakini sikuwa na sababu ya msingi ambayo ningeitoa na kunitetea. Ikabidi nigeuke na kuelekea chumbani kwa baba kwa mwendo wa haraka huku nikiwa nimejawa na wasiwasi. Nilipoukaribia mlango wa chumbani nikasita kuingia. Nikakumbuka kitu ambacho kilinipa nguvu. Niliacha kufungua mlango wa chumbani kwa baba na kuelekea jikoni kitendo ambacho kilimshangaza baba.

“Wewe imekuwaje tena?” baba alihoji baada ya kuniona narudi na kuelekea jikoni.

“Naleta baba” nikajibu huku nikiingia jikoni.

Moja kwa moja nilinyoosha hadi pale nilipokuwa nimeweka mwiko wa mboga na kuuchukua.

“Naomba nisindikize mdogo wangu” nilizungumza huku nikiuficha ule mwiko kwenye kanga niliyokuwa nimejitanda kichwani.

Nilitoka haraka jikoni na kuelekea chumbani kwa baba kuchukua hiyo briefcase niliyokuwa nimeagizwa. Safari hii nilikuwa najiamini kwasababu nilikuwa nimekamatia mwiko wangu kisawasawa.

“Akijipendekeza tu atajuta kuzaliwa” nikazungumza kwa kujiamini huku nikikamata kitasa cha mlango na kuzama chumbani.

Wakati wote huo baba alikuwa akinikodolea macho nilivyokuwa nikiingia na kutoka. Hakuwa anaelewa mipango yangu siku hiyo. Maumivu ya pua yaliyotokana na kupigwa na mwiko yaliendelea kumfanya awe kama zezeta.

Tofauti kabisa na ambavyo nilikuwa nimetarajia. Niliingia chumbani kwa baba na kuchukua briefcase kisha nikafanikiwa kutoka salama pasipo kubugudhiwa na mtu yeyote.

Nilirejea sittingroom nikiwa nimekamatia vyema briefcase ya baba na kwenye kwapa langu la kushoto nimeubana vizuri mwiko wangu. Nilipotokelezea tu, pua ya baba ikanikaribisha, ilikuwa imezidi kuvimba na kuonekana kama pulizo. Masikini ya mungu nikamuonea huruma kwa kiasi fulani baba wawatu. Nilifika na kumkabidhi ile briefcase yake.

“Haya asante mtoto mzuri” baba alizungumza huku akipokea.

Baada ya kumkabidhi nikataka kuondoka kuelekea jikoni kwaajili ya kuendelea na maandalizi ya chakula cha jioni.

“Unakwenda wapi sasa?” baba alinizuia.

“Nakwenda kumalizia kupika”

“Aah kupika nini bwana njoo kwanza. Utapika hata baadae” alizungumza baba huku akifungua briefcase yake.

Nikasimama kama vile nilikuwa namsikiliza amalize kuzungumza niondoke zangu. Lakini macho yangu yalikuwa yamekodoka kwenye ile briefcase aliyokuwa anaifungua. Mnh! Sikuweza kuamini kile ambacho nilikuwa nimekiona.

“Haya kazi kwako sasa” baba alizungumza huku akitoa nguo kutoka kwenye briefcase ile.

Sikuweza kuamini maho yangu, lakini hicho ndicho kilichotokea. Kwakuwa alikuwa ni baba yangu hivyo sikuona sababu ya kukataa zawaidi ile, nilipokea kwa shukurani kibao. Yani nyie pamoja na kupigwa na mwiko baba wa watu lakini bado alinipa zawadi, Mnh!

“Asante sana baba” nikatoa shukurani za dhati huku nikiachia tabasamu laini.

“Haya mtoto mzuri ndenda ukavae sasa nikuone” baba alizungumza kwa sauti ya upendo. Nilipokea viwalo vile na kuelekea chumbani kwangu huku nikiwa nimejawa na furaha ndani ya moyo wangu.

Nilijikuta macho yakinitoka baada yakuzikunjua nguo zile, zilikuwa ni kama zile ambazo alikuwa ananinunulia kaka Imran.

“Mbona kila mtu ananiletea nguo za hivi! Au ndio swaga za mjini hizi?” nikajiuliza huku nimeketi kitandani. Alikuwa ameniletea miniskate na blauzi pamoja nguo za ndani kama zile alizokuwa ameniletea kaka Imran zenye Kamba kwa nyuma.

“Ngoja leo nitoe ushamba, hizi nguo inawezekana ndio mpango mzima” mtoto wa kike nikasogea karibu na kioo na kuanza kusaula mavazi yangu na kujivisha zile nguo ambazo mwenyewe nilikuwa nikihisi ni nguo za kijanja kwa watoto wa mjini.

Naam! Nilikuwa nimetokelezea hasaa na nikajikubali mwenyewe. Nakumbuka zilikuwa ni kimini cha jeans kilichokuwa kifupi kilichoishia juu ya magoti, na kiblauzi cha rangi ya chungwa ambacho kilikuwa na kitambaa lainii kilichoweza kuonesha alama za sidiria yangu nyeusi niliyokuwa nimeivaa kwa ndani huku mikono yake ilikuwa ni ile ya kukata na kifuani kameacha nafasi kiasi na kupelekea mashina ya madafu yangu kuonekana. Nikajigeuza geuza pale kwenye kioo mara mbilimbili huku nikijichezesha chezesha pekeyangu.

“Hapa nakwambia Endrus akiniona lazima achanganyikiwe” nikajizungumzisha mwenyewe.

Nilipojiona kuwa nilikuwa sawa na nguo zimenikaa vyema nilivuta hatua kuelekea sebleni ambako baba alikuwa akinisubiri kwa hamu.

“Woow! Wonderfull! “Baba alishindwa kuzuia hisiazake mara tua aliponiona nikitokelezea.




Nilitembea kwa mwendo wa taratibu huku nikijaribu kutengeneza muondoko wa kuendana na mavazi yale ambayo nimekuwa nikiyaona kwenye video.

“Hapo sasa ndipo penyewe, sitaki nikuone tena umevaa yale makorokocho yako” Mh! Jamani nyie mzee yule, heti zile nguo zangu za kujistiri ndio alikuwa anaziita makorokocho. Siju labda ni kweli kwa kule mjini mavaziyale yalikuwa yakionekana kama makorokocho.

Baba alivyonisifia kuwa nimependeza nikajikuta bichwa likinivimba kwa masifa kiasi cha kuhisi kinapasuka.

“Asante baba” nikashukuru kwa tabasamu murua.

“Kuanzia leo sitaki nikuone tena umevaa maronywa ronywa yakohayo” baba alizungumza kwa amri.

“Sasa baba nguoza hivi nitazipata wapi?” nikahoji.

“Usijali, nitakutoa out hivyo zitajaa kiba ndani humu” baba alizungumza.

“Asante baba” niliitika kwa furaha.

“Hebu geuka nikuone huko nyuma” baba alisema.

Kwasababu nilikuwa na furaha ya kununuliwa nguo mpya na za kisasa ambazo nilikuwa nafikiria kumpagawisha nazo Endrus nikajigeuza kwa pozi na kumuachia baba madafu yangu ya uani ambayo yalisababisha kimini kile kubinuka kwa juu na kubelekea sehemu kubwa na mapaja yangu kuonekana.

“Mnh! Tumu” baba aliita kwa sauti ya kutafuta kooni.

“Abee baba” Niliitika nakugeuka kumuangalia baba.

Rudisha hii briefcase chumbani” baba alizungumza huku akionekana hayupo sawa usoni.

Pasipo kuzungumza neno lolote niliinama na kuchukua briefcase ile kwaajili ya kuipeleka chumbani kwa baba. Nilipokuwa nikivuta hatua, nikakumbuka sikuwa nimebeba mwiko wangu wa kugeuzia mboga na pua za watu kama baba.

Bila ya kujiuliza maswali mara mbili mbili, nilikunja kona na kuelekea jikoni ambakonilichukua mwiko na kuushika mkononi. Kwakuwa nguo nilizokuwa nimezivaa hazikuweza kuficha mwiko ule nikaubebakwa kuuningi’niza mkononi.

“We Mwantumu” baba aliita baada ya kuniona natokea jikoni.

“Abee baba” nikaitika

“Huo mwiko ni wanini sasa?” baba alihoji pasipokuelewa kazi ya mwiko ule.

“Ah, nilikuwa nageuzia mboga nikasahau na kutoka nao” nilijaribu kuongopa, hapakuwa na mboga iliyogeuzwa wala nini.

“Haya rudisha mzigo wangu chumbani” alisema baba huku akipeleka macho yake kuangalia feni lilivyokuwa likizunguuka juu ya dari.

Huku nikiwa na mwiko wangu mkononi nilivuta hatua kuelekea chumbani kwa baba. Nilitembea kwa kujiamini kwasababu mkononi nilikuwa na silaha yangu matata ambayo ilikuwa ni dawa kwa waroho.

Niliingia chumbani na kwenda haraka kwenye kabati na kuweka mzigo ule. Pamoja na kwamba nilikuwa najiamini lakini ndani ya moyo wangu kulikuwa na vipande vidogo sana vya hofu vilivyochanganyikana na chembechembe za wasiwasi.

Ghafla nikasikia mtu akikohoa nyuma yangu na kunishitua. Sikuweza kuamini nilipogeuza macho yangu na kumkuta baba ameingia chumbani mwake. Nilimtazama baba kwa macho ya wasiwasi huku nikisubiri athubutu kufanya jambo lolote la kipuuzi.

“Mwantumu mwanangu!”

“Baba!” nikaita kwa wasiwasi.

“Umependeza sana” baba alizungumza huku akitabasamu na kuuma midomo yake mara kwa mara.

“Baba, naomba niende nje” nilizungumza kwa sauti kavu.

“Hapana Mwantumu, mimi nimekufuata wewe, kwanini unataka kutoka?” baba alizungumza huku akivuta hatua taratiibu kunifuata.

“Baba naomba usisogee!” nilijikuta nikizungumza kwa ujasiri huku nikimuoneshea ule mwiko wangu.

“Unataka kunipiga tena na mwiko?” baba alizungumza na kunifanya nimtazame kwenye ile pua yake iliyovimba. Ilikuwa inachekesha kidogo na wala haikumpendeza kwasababu alikuwa anatisha.

“Naomba nitoke nje!” nikazungumza kwa msisitizo huku nikivuta hatua kurudi nyuma.

“Kaa basi mtoto mzuri tuzungumze” baba alizungumza huku akisogelea kitanda.

“Baba kwani unataka nini?” nikazungumza kwa msisitizo.

“Sikiliza Mwantumu, mimi nakupenda kama nilivyokueleza tafadhali usiunyongo’nyeshe mtima wangu” alizungumza baba kwa sauti ya kubembeleza huku akinikodolea macho kwenye mapaja yangu ambayo yalikuwa wazi kutokana na ile minisketi fupi niliyokuwa nimeivaa.

“Mbona sikuelewi baba?”

“Mwantumu, mbona haya yote tulishayamaliza na tukakubaliana nikuongezee mshahara?” alizungumza baba kwa sauti ya kulalamika huku akiamini mimi ni yulee Mwantumu wa kipindi kile ambaye sikuwa naweza kujisimamia. Hakufahamu kama mtoto wa kike nilikuwa nimeamua kumkabidhi moyo wangu mwanaume mwingine kabisa nje na mule ndani. Ndio, Endrus ndiye aliyekuwa chaguo langu kwa wakati huo. Masuala ya kugombanisha ndugu nilikwisha yakataa tangu siku ya kwanza walipogombana Fadhili na kaka yake kwasababu yangu. Nikamtaama baba usoni kwa kumkazia macho.

“Lakini baba, huoni kama tunamkosea mama?” nikahoji kwa kusihi.

“Atajuaje sasa, kwani nani atamuambia?” baba alizungumza.

“Hapana baba mimi sihitaji tena!” nikazungumza kwa msisitio na kutikisa kichwa kuashiria mkazo wa maneno yangu.

“Sasa kama ulikuwa hutaki kwanini mara ya kwanza ulinikubalia” baba alihoji kwa sauti kavu kidogo baada ya kuona mtoto wa kike nikileta misimamo ya ajabu ajabu.

“Mimi naogopa baba, sipendi kuwagombanisha na mama” niliendelea kufafanua kwa misimamo yangu ileile.

“Sawa nimekuelewa, basi naomba hata kidogo tu!” Jamani nyie baba yule aliendelea kunga’anga’ania utafikiri ruba.

“Lakini baba nakuheshimu unajua?” nikazungumza kwa msisitizo.

“Hata kama tukifanya heshima yetu haitafutika Mwantumu” alizungumza baba huku akilegeza macho utafikiri alikuwa amelewa.

Nilipoona baba alikuwa na misimamo juu ya kile alihokuwa amekusudia kukifanya kwangu ikabidi nibadilike zaidi na kuvaa sura ya mbwa mwitu. Nilikamata vyema mwiko wangu wa mboga na kumkazia maho baba.

“Utanipisha au hunipishi?” nikazungumza kwa msisitizo.

“Unataka kazi hutaki?” baba naye akahoji kwa msisitizo.

“Sitaki!”

“Unasemaje wewe mtoto?” baba alizungumza huku akinisogelea pale nilipokuwa nimesimama.

“Kama kufanya kazi za ndani inahusisha biahara hii, kuanzia leo nimeacha kazi” nilizungumza kwa msisitizo huku nikivuta hatua kuelekea mlangoni ambako baba alikuwa ameziba njia.

Baba alipobaini lengo langu lilikuwa ni kutoka chumbani mle akapata wazo la kutumia nguvu. Alitaka kunidaka mkono lakini nilifanikiwa kuchomoka na kurukia pembeni. Akanisogelea tena na kunirukia kwanguvu akiwa na lengo la kunidondosha chini lakini mtoto wa kike nilimkwepa na kusababisha mtu mzima yule kudondoka chini kama zigo la dhambi, Puu!

Kitendo bila ya kuchelewa, baada ya mzee yule kudondoka chini nilimfuata kwa kasi na kuvuta ule mwiko wangu juu kisha nikauteremsha usawa wa usoni mwake. Nilikuwa nimekusudia kufanya fundisho kwa mwanaume yule. Mungu si Athumani, baba wa watu alifanikiwa kukwepa mwiko wangu kwa kujibingirisha pembeni. Kwakuwa nilikuwa nimekusudia kufanya tukio lile nikamfuata tena na kumrushia tena mwiko usawa wa kichwani kwa kutumia nguvu zangu zote lakini alifanikiwa kunikwepa tena na safari hiyo alisimama.

“No Tumu wacha…wacha tafadhali” baba alizungumza huku akirudi nyuma taratibu.

Mtoto wa kike nilikuwa kama vile mbogo aliyejeruhiwa, hata baba mwenyewe hakuweza kuamini. Nilipoona ameanza kuniogopa nikaona nitumie mwanya uleule kuweza kuchomoka kwenye mikono ya mwanaume yule. Nikavuta hatua ndefu na za haraka sana kumfuata huku mkononi nikiwa nimekamatia vyema mwiko wangu.

Baba alipoona kitoto cha kitanga kimepagawa naye akajiongeza na kuanza kutimua mbio kutoka chumbani mle. Waswahili wanasema ukipungiwa punga, baada ya kuona baba anatimua mbio, namimi nakamuunganishia kwa nyuma huku nimeshikilia mwiko wangu tayari kwa kumteremshia kipigo kitakatifu mume wa mtu. Yani nikawa kama vile nafukuza mwizi. Nakwambia babambele na mimi nyuma utafikiri tulikuwa tunacheza mchezo wa kidali po!

“Acha…wacha mtoto wangu!” baba alizungumza alipokuwa ananikimbia.

“Subiri we si umesema nikupe kidogo!” namimi nikamjibu huku nikimkimbiza kwa nyuma.

Ndugu msomaji huwezi amini kitu ambacho kilitokea wakati mimi na baba tulipokuwa tunakimbizana kutoka chumbani kwa baba kuelekea sitting room, Kumbe mama alikuwa akitukodolea macho ya mshangao utafikiri alikuwa akiangalia mashindano ya riadha.

“Hivi mna wazimu au mmerogwa?” alihoji mama kwa mshangao.

Sote wawili tulishituliwa na sauti ya mama. Hakuna ambaye alitegemea kama mama angeweza kuwepo nyumbani mida kama ile. Sote tulifikiri mama alikuwa angali yu kazini.

Tukajikuta katika wakati mgumu sana huku sote wawili tukiwa hatueewi mama angelichukuliaje tukio lile.

Kitu kibaya zaidi mimi na baba tulikuwa tunakimbizana kutokea chumbani mwake na ukiunganisha na yale mavazi niliyokuwa nimeyavaa ndio usiseme. Mama hakuwa anapenda kuniona nimevaa nguo za aina ile, pamoja na kwamba watu wengine walikuwa wakinitetea na kunishawishi nivae mavazi yale.

Baba alipobaini mama alikuwa anatuangalia tukifanya vituko vile, alianza kuhisi tumbo la kuhara likimchomachoma. Alitamani ile siku ambayo Yesu aliahidi kurudi iwe imefika ili asipate nafasi ya kuhojiwa na mke wake ambaye kwa siku za nyuma alikuwa ameshaanza kuhisi penzi lake lilikuwa na dalili ya kudokolewa na house girl.



Sio baba tu ambaye alikuwa amechanganyikiwa kutokana na tukio lile bali hata mimi nilihisi miguu ikigongana kadri nilivyokuwa nikikimbia.

Kwa akili ya kuzaliwa ambayo baba alikuwa amejaaliwa ilifanya kazi kwa haraka na kukimbia hadi alipokuwa amesimama mke wake na kumshika kwa nyuma kama vile alikuwa akiomba msaada.

Na mimi ikabidi nijiongeze na kuendelea kumkimbiza baba, tena ikabidi nianze na kupiga kelele zisizo eleweka. Nilielekea moja kwa moja hadi alipokuwa amesimama mama na kuvuta mwiko uliokuwepo mkononi na kutaka kumtandika mama kichwani.

Kama vile picha la kichina mama alifanikiwa kukwepa mwiko ule na kusogea nyuma kidogo kuusoma mchezo ambao hakuwa anauelewa. Niliendelea kupiga kelele huku nikirusha mwiko hovyo hovyo nikijifanya nataka kuwatandika wote wawili.

“Ni kitu gani kinaendelea jamani?” mama alihoji huku na yeye akitimua mbio kunikimbia.

“Kimbia mke wangu atakuua huyo mtoto!” baba alizungumza huku akimshika makono mama na kutimua nae mbio kuelekea sebleni.

Nakwambi mtoto wa kike kama vile nilikuwa nimechochewa, baada ya kubaini tulikuwa tumefanikiwa kumchanganya mama. Niliwaunganisha wote wawili na kuwatimua utafikiri nimechanganyikiwa.

Nikaingia jikoni ambako nilichukua ndoo ya maji na kujimwagia mwilini huku nikijifanya nilikuwa nimepandwa na mapepo. Nilipiga kelele na kujitupa chini huku nikigalagala. Wote wawili baba na mama walikuwa wamejawa na woga na wasiwasi. Hata baba mwenyewe hakuelewa kama ile ilikuwa ni kweli ama picha la kihindi.

“Amepatwa na nini mtoto wa watu Mungu wangu” mama alihoji huku akihofia kunikaribia.

“Hata sielewi, nimeshangaa tu anapiga kelele na kunifuata chumbani huku ameshika mwiko na kuanza kunitandika nao” alizungumza baba huku akishikilia pua yake.

“Mungu wangu, ndio amekuumiza hivyo?” alihoji mama kwa wasiwasi baada ya kuona pua la mume wake limevimba kama andazi.

“Au malaria yamepanda kichwani?” baba akahoji.

“Nenda sasa kamsaidie” mama alisema.

“Nenda wewe!” baba alizungumza huku akionekana kuogopa kunisogelea.

“Mwanaume mzima unaogopa! Nenda kamsaidie mtoto bwana” mama alizungumza huku akisogea nyuma.

“Niende ili anipige tena! Nenda wewe si mwanamke mwenzio?” baba alijitetea.

Nikiwa pale chini nimelowana na maji nakwambia mtoto wa kike nikazidi kujigalagaza huku nikiwasikiliza walivyokuwa wakibishana kunisogelea.

“Au amepandwa na mashetani?” mama alihoji.

“Kwani ana mashetani?” baba akahoji.

“Sasa mimi nitajuaje”

“Kwani wewe si ndio umemleta humu ndani!” baba alizungumza na kujifanya kulaumu mimi kuletwa ndani mle.

Nilipoona mambo yamekuwa sawa nikatulia taratibu huku nikiwa nimelala chali, mguu mmoja mashariki na mwingine mgagharibi, moko wa kushoto huku na wa kulia kule.

“Ametulia sasa, haya nenda ukamsaidie” mama alizungumza.

Kwa tahadhari kubwa baba alinyata na kunisogelea pale nilipokuwa nimelala. Masikini ya mungu kumbe kile kitendo cha kujimwagia maji na lile pozi langu nililokuwa nimelala nilikuwa namuweka baba katika wakati mgumu.

Mwili wangu ulikuwa ukionekana waziwazi kutokana na kulowana na maji. Madafu yangu ya kifuani yaliyokuwa yametuna kisawaawa na ncha kali kwa mbele yaliweza kuonekana waziwazi kutokana na ile blauzi laini niliyokuwa nimevaa kulowana kwa maji.

Kale kasketi kafupi nako kalizidi kuniwacha wazi kutokana na kuchoshwa na maji niliyokuwa nimejimwagia mwilini kwa makusudi ya kuua soo.

Baba aliinama huku akijifanya kuogopa lakini macho yake akiwa ameyakodoa kifuani kwangu. Akapeleka mkono wake kwenye mashavu yangu na kujaribu kunitikisa huku akiniita.

“Mwantumu mama” baba aliita huku akihamishia mkono wake wa kushoto na kuuweka kiunoni kwangu. Nafikiri lengo lake lilikuwa ni kunisaidi ingawa sina uhakika sana.

Mama naye akasogea na kuchutama pembeni ya mume wake huku akinitazama kwa macho yaliyokuwa yamejaa hofu na mashaka.

“Vipi mume wangu, tumpeleke hospitali” alizungumza mama alipokuwa akichutama.

“Hebu ngoja kwanza” baba alizungumza huku akijaribu kunitikisa kwa mikono yake ambayo mmoja ulikuwa kwenye shavu langu na mwingine kwenye kiuno changu kilichokuwa kimechongoka na kuugawanyisha mwili wangu kwa mpangilio mzuri.

Niliposikia masuala ya kupelekana hospitali ikabidi nijikohoze na kujigeuza kulala kwa upande wa kulia.

“We Mwantumu” mama aliita.

Nilitoa sauti ya kuitika kama vile nilikuwa kwenye usingizi mzito sana kisha nikajikohoza.

“Asante Mungu!” alizungumza mama.

“Hebu lete nguo tumfunike” baba alizungumza huku akijishaua heti hakuwa anapenda kuniona nikiwa nimelala kihasara hasara kiasi kile.

Maneno ya baba yalizidi kuongeza Imani kwa mume wake juu yangu, hivyo alielekea chumbani kwaajili ya kuchukua nguo ya kunifunika.

“We mama wa mwiko hebu amka” baba alizungumza kwa sauti ya chini huku akinipapasa mama alipoondoka. Nikafumbua macho na kumtazama baba kwa hasira.

“Ahaa bado unanishika eeh? Au nikachukue mwiko wangu” nikazungumza kwa msisitizo baada ya kumuona akinipapasa kwenye mapaja yangu pamoja na kifuani.

“Pumbavu, hebu lala huko!” baba aliniamuru baada ya kuniona naendelea na misimamo yangu ileile.

“Ukinipapasa tena nalianzisha upyaaa” nikazungumza kwa msisitizo huku nikiendelea kufumba macho.

Mama alirudi mbio huku ameshikilia upande wa kitenge kwenye mikono yake. Alipokaribia tu nikafumbua macho kama vili nilikuwa nimeamka kutoka usingizini.

“Vipi anaendeleaje?” mama alihoji masikini ya mungu.

“Ndio amefumbua macho” baba akajibu huku akipokea lile tenge na kunifunika kuanzia kifuani hadi kwenye miguu.

“Vipi Mwantumu unaendeleaje mama” Bi Fatma alihoji kwa sauti ya upendo.

“Sijambo” nikajibu kwa sauti ndogo utafikiri nilikuwa mogwa mahututi.

“Haya inuka twende hospitali” mama alizungumza.

“Ngoja kwanza mke wangu, mbona hata sio mgonjwa wa hivyo huyu” alizungumza baba kwasababu alikuwa akifahamu kilichokuwa kinaendelea.

“Unasema sio mgonjwa huyu wakati amekuhondomola pua lako hilo” mama alizungumza kwa msisitizo.

“Hapana mama mimi nipo sawa” nikazungumza baada ya kuona mama alikokuwa anaelekea kulikuwa siko.

“Si nimekwambia mimi” baba akaniunga mkono.

“Umeniambia nini! Mtoto wawatu akitufia hapa utasemaje?” mama alizungumza kwa msosotizo kidogo baada ya kubaini baba hakuwa analiunga mkoso suala la mimi kupelekwa hospitali.

“Hapana mama siumwi, hali hii iliwahi kunitokea nikiwa kijijini” nikazungumza ilikupinga suala la kupelekwa hospitali wakati sikuwa naumwa kitu chochote.

“Imewahi kukutokea?” mama akahoji kwa mshangao baada ya kusikie maneno yangu yale.

“Ndio lakini ni zamani sana” nikaongopa.

“Sababu ni nini?”

“Walinambia sijui mashetani” nikaendelea kudanganya nakwambia wakati tangu nimezaliwa sikuwahi kupandwa na huyo shetani sijui pepo sijui ibilisi.

“Eeh haya tena makubwa!” mama alizungumza kwa kuhamaki.

“Usijali, hebu amka ukapumzike ndani” baba alizungumza huku akitaka kuniinua kutoka pale chini.

Mtoto wa kike nikajiinua na kusimama huku nikijifanya kuyumbayumba na kupepesuka.

“Hebu mshike, mpeleke chumbani kwake” baba alizungumza baa nay a kuniona nikikosa nguvu za kutembea mwenyewe.

Mama alinikamata vyema na kunikokota kuelekea chumbani kwangu huku nikijifanya sikuwa na nguvu za kutosha.

Tulipofika chumbani mama aliniweka kitandanikisha akasimama pembeni na kunitazama kwa umakini.

“Mwantumu” mama aliita.

“Abee mama”

“Vipi unaendeleaje?”

“Kwa sasa sijambo”

“Au nikurudishe kijijini?” mama akahoji kwa umakini.

“Hapana mama, naomba usinirudishe kijijini” nikazungumza kwa kuhamaki baada ya kusikia wazo la kurudishwa kijijini. Heti ndugu msomaji, raha zote hizi ninazozipata huku mjini halafu mtu anakwambia akurejeshe kijijini kweli inahusu? Kwakweli kijijini harudi mtu labda wanibebe nikiwa nimelala.

“Hakikisha unabadilisha nguo, ndipo upumzike” alizungumza mama alipokuwa anaondoka, nani nilijiinua nipokuwa nimlala na kuketi kitako. Ndani ya kichwa changu nikavuta taswira ya matukio yote yaliyotokea tangu baba aliporejea kutoka kazini hadi wakati ule. Nikaachia tabasamu la ushindi na kujitupa tena kitandani.

Nikiwa pale kitandani mawazo juu ya kipenzi changu yakaanza kunijia. Sikuona sababu ya kuyakatisha bali niliyapa nafasi yautawale ubongo na muda wangu. Ndio, nilijikuta nikimpenda sana mpenzi wangu Endrus nafikiri ni kwasababu ya vituko nilivyokuwa nikiletewa na wanaume wa mle ndani.

Nilikumbuka yale maneno ya Fadhili ya kunikataza kwenda kule mgahawani kwa dada Bupe. Sikuweza kufahamu ni kwa namna gani ningeweza kukutana na mpenzi wangu Endrus pasipo kufika mgahawani kwa dada Bupe.

Vilevile maneono ya kaka Imran kuniruhusu niwehuru kwenda kwa dada Bupe yalinipa matumaini ya kuweza kuonana na kipenzi cha roho yangu. Nilitamani nitoke na kwnda kwa dada Bupe hata wakati ule lakini vigezo havikukidhi. Nikakumbatia mikono yangu kifuani huku nikivuta taswira ya kukumbatiwa na mpenzi wangu Endrus.

*****


Baada ya siku chache kupita maisha ya kufungiwa kwenye geti kubwa yalielekea kunishinda. Jambo kubwa ambalo lilikuwa ni kama mzigo mzito kwanu ni kushindwa kuonana na mpenzi wangu Endrus. Nilitamani sana japo kuonana na dada Bupe ili anipe habari za kijana yule aliyekuwa amenichanganya akili yangu. Lakini niliheshimu sana maneno ya Fadhili aliyosema hataki kuniona nikipeleka pua yangu kule kwa dada Bupe.

Nikiwa mezani nikiandaa kifungua kinywa kwaajili ya siku mpya Fadhili alifika na kuketi mezani.

“Dogo naona sikuhizi upo ‘on time’ kabisa” Fadhili alizungumza huku akiosha mikono yake tayari kwa msosi.

“Naipenda kazi yangu baba” nikazungumza kwa sauti laini.

“Inapendeza sana, si unaona hata mother hapigi kelele tena” Fadhili alizungumza huku akipakua chakula kutoka kwenye hotpot.

“We si hunipendi bwana, nimeona labda niimarishe kazi yangu pengine unaweza ukarudisha moyo wako nyuma” nilizungumza kwa kumtania huku nikiachia tabasamu la upendo.

“Unafikiri sikupendi Tumu, Mimi nakupenda sana tena sana” Fadhili alizungumza huku akimimina chai kwenye kikombe.

“Mnh yani wewe!” nikazungumza huku nikitabasamu nikiwa siamini masikio yangu.

“Unafikiri Tumu! Mimi nakupenda sana, tena nilikuwa natamani hata uwe mama watoto wangu” Fadhili alizungumza huku akipeleka mdomoni kipande cha mkate.

Maneno yale ya Fadhili yaliufanya mwili wangu usisimke utafikiri sijui nilikuwa nimemwagiwa kitu gani. Nikamtazama machoni kwa umakini zaidi kuona kama kile alichokuwa anakizungumza hakikuwa na masihara.

“Kwani tatizo liko wapi?” nikahoji kwa umakini.

“Tatizo lipo Tumu!” alizungumza huku akitafuta kipande cha mkate.

“Niambie sasa, tatizo ni nini?” nikaendelea kuhoji.

“Tatizo mimi sikuelewi Mwantumu”

“Kivipi?”

“Kwanini Imran akinikuta na wewe ananimaindi?” Fadhili akahoji.

“Kwa kweli hata mimi sielewi”

“Basi mimi nafikiri jamaa ameshakula zigo” alizungumza Fadhili huku akiachia tabasamu na macho yake akinitazama kwa kuniiba.

“Hakuna bwana Fadhili, mimi humu ndani sitakuja kutembea na mwanaume yeyote yule na nimeapa hivyo” nikazungumza kwa msisitizo.

“Mnh hata mimi?” Fadhili akahoji kwa mtego.

“Sijui labda wewe…lakini sijui kama itawezekana pia” nilijikuta nikizungumza kwa kigugumizi. Nilishindwa kumpa jibu la kuwezekana kwasababu tayari nilikwisha amua kuwa na Endrus peke yake.

“Kwanini isiwezekane, au ndio hunipendi siku hizi” Fadhili akazungumza kwa sauti ndogo lakini iliyokuwa ikikoroma kama redio mbovu.



“Mbona mimi nimeshawahi kukuambia kama nakupenda, wewe tu ndo umenikataa” nikazungumza kwa sauti ya kudeka.

“Kwahiyo vipi bado unanipenda au?” Fadhili alihoji huku akifuta mikono yake kwa kipande cha tishu.

“Mi sijui, we mwenyewe mkali huko” nikazungumza huku nikichukua vyombo vichafu alivyokuwa ametumia Fadhili.

“Sio hivyo Mwantumu, unajua mambo mengine yanakera sana!” Fadhili alizungumza huku akijiinua kutoka kwenye kiti.

“Mambo gani?” nikahoji kwa sauti ya kubana.

“Ngoja niende, leo nitarudi mapema nije tuyajenge” Fadhili alizungumza huku akivuta hatua kuondoka.

“Fadhili..” nikaita kwa sauti ya wasiwasi.

“Enhe..” akaitika na kugeuka kunitazama kwa makini.

“Kuna kitu nataka nikuombe” nikazungumza kwa ile sauti yangu ya mashaka.

“Nakusikiliza endelea, au unataka twende wote kazini?” Fadhili akazungumza kwa masihara.

“Sijui utanikubalia lakini” nikazungumza huku nikijiuma uma vidole na kuzunguusha miguu safafuni.

“Ndio uongee sasa”

“Unajua kukaa ndani pekeyangu kunachosha sana” nikazungumza kwa mtego.

“Umeshaanza hivyo, haya kajiandae basi twende wote dukani kwangu” alizungumza Fadhili.

“Sio hivyo Fadhili bwana”

“Kumbe unatakaje, au nisiende kazidi tubaki wote wawili hapa ndani” Fadhili aliendelea kuhoji kwa masihara yake.

“Sina maana hiyo bwana Fadhili”

“Haya ongea basi”

“Naomba nikimaliza kazi za hapa ndani niende nikajichangamshe kule kwa dada Bupe” nikaeleza.

“Dah! Tumu mdogo wangu, hivi unamjua Bupe vizuri?” Fadhili akazungumza kwa mashaka.

“Nitakuwa makini Fadhili, hakika hatothubutu kunifanyia kitu kibaya” nikaeleza kwa upole na sauti ya kubembeleza.

“Unaniachaje?”

“Abee..”

“Unaniachaje ili nikuruhusu?” Fadhili akazungumza kwa masihara.

“Nitakuapa chochote kile utakachokitaka” nikaeleza.

“Mnh! Je nikitaka nini…?

“Nini ndio nini?” nikahoji huku nikiachia tabasamu la mahaba.

“Sawa nenda lakini uwe makini kwelikweli” Fadhili alizungumza kwa msisitizo.

“Kweli Kaka Fadhili?” nikazungumza kwa furaha huku nikiwa siamini kwa kile ambacho kilikuwa kimezungumzwa na Fadhili.

“Nawewe hadi uwe na shida ndio unaniita kaka, mbona siku zote unaniita jinalangu” Fadhili alizungumza kwa yale masihara yake.

“Basi kuanzia leo nitakuwa nakuita kaka” nikazungumza kwa sauti ya kujidekeza.

“Lakini sikia nikwambie kitu” Fadhili alizungumza kwa sauti ndogo lakini iliyokuwa na msisitizo.

“Enhe….?”

“Nenda lakini naomba utambue kuwa mimi ninawivu kuliko unavyonifahamu” Mnh jamani nyie Fadhili alizungumza maneno ambayo yaliniweka njia panda. Siku zote nilikuwa nafahamu Fadhi hanipendi na alikuwa amenichukia, sasa cha kuniambi heti anawivu ni kipi? Au alikuwa anamaana gani? Sasa kama alikuwa anamaanisha ya kunionea wivu mimi ingekuwaje maana tayari nilikuwa nimekwisha ukabidhi moyo wangu kwa Endrus.

“Mnh Fadhili wewe!” ikabidi nijichekeshe chekeshe.

“Haya msalimie Bupe” Fadhili alizungumza huku akianza kuondoka na kuniacha nimesimama.

“Nimwambiaje?” nikazungumza kwa bashasha baada ya kuruhusiwa kwenda kwa dada Bupe.

“Mwambie simpendi” Fadhili akazungumza na kuondoka akiniacha pale mezani nikipaweka sawa kwaajili ya watu wengine kupata kifungua kinywa.

Mazungumzo baina yangu na Fadhili yalikuwa yamenifurahisha sana siku hiyo. Sikuweza kuamini kama siku hiyo ningeweza kukutana kwa mara nyingine na mpenzi wangu Endrus. Nampenda jamani mwanaume yule mnh! Niacheni tu nideke.

Nikiwa naendelea na maandalizi yale pale mezani alifika kaka Imran na kuketi kwenye kile kiti ambacho alikuwa amekikalia Fadhili.

“Jamani mtoto mzuri upo?” Kaka Imran alizungumza huku akinitazama usoni.

“Shikamoo kaka Imran”

“Mahaba!” kaka Imrani akaitika kwa utani.

“Mahaba ndio nini sasa?” nikahoji huku nikiwa nimevaa lile tabasamu langu la siku zote.

“We si umeniamkia, nami nimeitika mahaba” Alizungumza kaka Imran.

“Kwahiyo sio marahaba bali ni Mahaba?”

“Kwani wasambaa kule kwenu wanaitikiaje? Si mahaba”

“Mnh haya bwana”

“Njoo basi uninawishe” kaka Imran alizungumza huku akinikodolea macho.

Nilisogea na kuinua jagi la maji na kuanza kumnawisha mikono kaka Imran.

“Nisugue basi mbona unaniachia mwenyewe” kaka Imrani alizungumza.

“Mnh jamani…” nilizungumza na kuingiza mikono yangu kwenye bakuli na kuanza kusugua mikono ya kaka Imran taratibu huku nikimtupia jicho la wizi usoni. Nakwambia mtoto wa kiume alikuwa kama vile ananawishwa kwa maji ya tindikali kwa jinsi alivyokuwa akisisimka mwili.

“Jamani Tumu una mikono mitamu kiasi hiki?” Alizungumza kaka Imran nilipokuwa nikimsugua mikono.

“Kaka Imran muongo, mitamu kwani umeila?” nilizungumza huku nikimsugua kidole cha kati.

“Unafikiri utamu hadi uonje kwa mdomo?”

“Sasa utajuaje bila kuonja?”

“Hata macho yanatosha kuonja na kukufanya uhisi utamu au uchahu”

“Mnh kaka Imran wewe” nikajizungumzisha huku nikimalizia kumnawisha mikono mwanaume yule aliyekuwa amejaa vituko na matendo magumu.

Nilipokuwa namalizia kumnawisha mikono, tulishituliwa na sauti ya mtu mwingine akitusemesha.

“Jamani hayo nayo yameanza lini?” ilikuwa ni auti ya mama ambaye alikuwa akitokea chumbani kwake akielekea pale dining room kwaajili ya kujipatia chochote kabla ya kwenda kazini.

“Karibu mama” Fadhili alizungumza kwa kujishebedua mara baada ya kubaini mama alikuwa ameshuhudia kitendo kile.

“Huo ubwenyenye wa kuoshwa mikono umeanza lini?” mama alihoji huku akivuta kiti na kuketi.

“Aah mama bwana, mbona kawaida tu” kaka Imran alizungumza kwa kujiamini.

“Kawaida kumtesa mtoto wa watu awaoshe hadi mikono, mbona ni mambo ya kikoloni hayo” mama alizungumza huku akiweka sukari kwenye kikombe chake cha chai.

“Sio utumwa mama, haya yanaitwa MAHABATI” alizungumza kaka Imran maneno ambayo hayakuwa yameninogea hata kidogo.

“Mahabati ya kitanga ndio haya?” mama alihoji huku akiamini kaka Imran alikuwa akizungumza kwa masihara kumbe mwenzake alikuwa anamaanisha.

“Nakwambia hata maji ya kuoga yatiwa hiliki ati” alizungumza kaka Imran huku akiiga lafunzi yangu ya kitanga na kumfanya mama kuangua kicheko huku akinitazama kwa macho ya uchokozi.

“Heti Tumu ni ya kweli hayo?” mama alihoji huku akinitazama na kuniachia tabasamu.

“Sijui…” nikazungumza huku nimeziba uso wangu kwa viganja vya mkono kwa aibu.

“Mama mimi naoa huyu mtoto” alizungumza kaka Imran na kuuma kipande cha mkate.

“Mwantumu hawezi kukubali kuolewa na mwanaume ana gubu utafikiri kitu gani” alizungumza mama.

“Hamna mama, mimi sina gubu. Hata Tumu mwenyewe anaelewa, muuleze” alizungumza Kaka Imran kwa kujiamini.

“Heti Tumu utakubali kuolewa na Imran?” alihoji mama kwa utani.

Mama alihoji huku akiamini mazungumzo yale yalikuwa ni ya masihara masikini ya Mungu. Hata hivyo kabla ya kutoa jibu la swali lile kulisikika mtu mwingine akinijibia swali alilokuwa ameuliza mama.

“Wala hakuna atakaye olewa hapo” ilikuwa ni sauti ya baba mzee Sekiza akizungumza akiwa anatokea chumbani kuelekea pale mezani kwaajili ya kifungua kinywa.

“Mnh disco limeingia Mmasai” kaka Imran akazungumza kwa sauti ya chini.

“Enhe hebu niambieni ni nani anayetaka kumuoa Tumu?” alihoji baba huku akijiweka kwenye kiti.

“Mwanao naona amekufa ameoza kwa binti wa kitanga” mama aliendelea kuchombeza akiamini yote yale yalikuwa ni masihara ya wanafamilia.

“Nani huyo?”

“Si huyo Imran”

“Pumbavu, hebu wacheni upuuzi wenu!” baba akazungumza kwa sauti ya kukoroma.

“He mwenzetu kwani vipi?” mama akahoji kwa mshangao baada ya kuona mume wake akikasirika kwa vitu visivyo na msingi.

“Mama acha!” kaka Imran akazungumza kwa sauti ya chini baada ya kubaini mazungumzo yale hayakuwa yamemnogea baba.

“Makubwa basi” mama alizungumza kwa mshangao huku akiwa haelewi kilichokuwa kinaendelea kichwani mwa baba.

“Mmejiachia wenyewe mnazungumza masuala ya kuolewa kwa mtoto mdogo hamuoni hata aibu” baba aliwachana live kaka Imran na mama yeke.

Mama alitaka kuzungumza kitu lakini kaka Imran akamkanyaga mguuni kumzuia asizungume neno lolote.

“Haya bwana, na yaishe” alizungumza mama huku akiosha mikono yake na mdomoni akimalizia kutafuna.

“Sitaki kusikia tena ujinga ujinga wenu” alizungumza baba kwa sura ya ukauzu.

Mama alitazamana na Kaka Imran na kupeana ishara ya kuondoka. Wote kwa pamoja walianza kuondoka wakituacha mimi na baba.

“Haya kwaherini” mama alizungumza wakati wanatoka na kaka Imran.

“Na muende moja kwa moja wala msirudi tena” alizungumza baba kwa msisitizo kuashiria alikuwa amekasirishwa na yale mazungumzo ya Mama na kaka Imran.

Baba alinitazana na kuangua kicheko kwa sauti ambacho sikuelewa kilikuwa kimetokea wapi.

“Nimewakomesha!” baba akazungumza huku akipeleka kikombe kinywani na kupiga funda la chai.

Mara zote nilikuwa nakwepa sana kukaa na baba tukiwa wawili tu kutokana na vitendo vyake alivyokuwa akiniletea mara tu anapopata fursa kama hiyo. Wakati mama na kaka Imran walipokuwa wakiondoka na mimi nikawa navuta miguu taratiibu kumuacha baba pekeyake mezani.

“Wewe unakwenda wapi?” baba alihoji baada ya kubaini nilikuwa nataka kumtoroka.

Niliposikia vile nikajikuta nguvu zikiniishia na kugeuka kumtazama baba kwa macho makavu yaliyokuwa yamekosa nuru ya amani.

“Vipi ndio unakwenda kuleta mwiko nini?” baba akahojikwa masihara.

“Nilikuwa naenda kuwafungulia geti wakina mama” nikajieleza.

“Wachana na mageti watafungua wenyewe” Baba alizungumza huku akisogeza kiti nikae pembeni yake.

“Lakini baba…” nilitaka kujitetea.

“Lakini nini au unataka kuleta habari zako za kufukuzana na miko” baba alizungumza huku akiendelea kukata kipande cha mkate na kukituma mdomoni.

Nilivuta pumzi na kuziachia kwa nguvu, sikuelewa mzee yule nimfanye nini ili asiendelee na mpango wake wa kunitaka kimapenzi. Mbonamimi nilikuwa kama mtoto wake tu ndani mle? Wazee wengine wa mjini sijui wapoje?

“Unaogopa nini njoo ukae, leo hakuna cha mwiko wala mashetani lazima kieleweke” baba akazungumza kwa msisitizo baada ya kuniona sikuwa na mpango wa kumpa ushirikiano.

“Lakini baba unachelewa kazini” nikajibaraguza mtoto wa kike baada ya kuona maji yalikuwa yanaelekea kunifika shingoni.

“Nimekwambia hakuna cha kazini leo, lazima utamu tupeane” alizungumza baba kwa msisitizo pasipo kunitazama usoni.

Mtoto wa kike nikahisi siku hiyo nilikuwa nimepatikana. Nilipomtazama usoni mzee yule nikabaini alichokuwa anakizungumza hakikuwa na masihara. Sikuwa na namna nyingine maana mbinu zote zilikuwa nimemaliza. Ikabidi mtoto wa kike nijilainishe mwenyewe kwa baba.

“Baba…” nikaita huku nikiketi kwenye kile kiti kilichokuwa jirani yake.

“Enhe nakusikiliza”

“Mbona ule mshahara wangu haujanipa?” nikahoji huku sauti nimeilegeza mtoto wa kike na macho nimerembua kimahaba utafikiri nilikuwa na mpenzi wangu Endru kumbe nilikuwa na Mzee Sekiza.

“Sasa ningekupaje wakati kila nikitaka kukupatia unanisumbua, tena hadi tunapigana miko ya kugeuzia mbona” alizungumza baba baada ya kuniona nimelainika mrembo wa kitanga.

“Basi nipe leo…” nikazungumza kwa kudeka huku nikiegemeza kichwa changu kwenye bega la baba.

Huhuuu! nakwambia baba alijisikia kama vile alikuwa peponi. Hakutegemea kama kitoto kisirani kama mimi ningeweza kujibebisha kwake kiasi kile. Nikapeleka mkono wangu wa kusho kifuani kwake na kuanza kumpapasa taratiibu.

“Tu..tu..tumu” baba aliniita kwa sauti ya kukatakata kama vile ana kigugumizi.

“Abee..” nikitika kwa ile sauti yangu ya kudeka.

“Nimekwambia nitakulipa kiasi gani vile kwa mwezi?” baba akahoji kwa sauti nzito huku akizunguusha mkono wake wa kushoto kwenye mabega yangu.

“Si ulisema unaniongezea Laki moja kila mwezi jamani baba umesahau?” Nikazungumza kwa kudeka huku nikijiweka vizuri pale kifuani kwa baba. Masiki ya Mungu mzee wa watu alizidi kuchanganyikiwa na toto la kitanga.

“Hapana Tumu umekosea” baba akazungumza kwa sauti ya kukoroma.

“Kumbe uliniambia kiasi gani?” nikahoji huku nikimtazama usoni na kupeleka mikono yangu kwenye kidevu hake na kuchezea ndevu za baba yule.

“Mimi nilikwambia nitakuongezea laki tatu kila mwezi” baba alizungumza kwa kunibembeleza huku akiutoa mkono wake kwenye mabega na kuuweka juu ya paja langu la mguu wa kulia.




Jamani huo si mshahara wa msomi kabisa jamani! Heti mwenzenu ndio nilikuwa nimeahidiwa kupewa kwa kufanya kazi za ndani tu. Mnh kuna wanaume wakiamua mambo yao hata nyumba wanaweza kuuza kwajili ya mchepuko.

Kusema ukweli mpenzi wa Mungu taarifa ile ilinishitua sana. Sikuweza kuamini baba alikuwa anazungumza vile kunilainisha tu au ni kweli alikuwa amekusudia? Majibu mwenzenu sikuwa nayo. Lakini ka laki tatu kalinivutia sana.

“Kwahiyo laki tatu yote ni yakwangu kwa kila mwezi?” nikahoji nikijifanya sikuwa nimeelewa maelezo ya mzee yule.

“Na ukijumlisha na ile utakayopewa na mama yako itakuwa ngapi?” aliendelea kuzungumza kwa kujidai mwanaume mtumzima yule baada ya kubaini alikuwa amenimaliza makali yote.

“Nitakuwa na mihela mingi kumbe!” nikazungumza kwa kujidai baada ya kupata taarifa ile.

“Aah hizo tu mbona cha mtoto, kama ukinifurahisha zaidi nitakujengea hata nyumba” baba alijitapa huku akimeza funda la mate ya uchu.

“Mnh baba wewe, kumbe na mimi nitakuwa mama mwenye nyumba? Nikahoji kwa madeko mtoto wa kitanga, chezea mshiko weye!

“Na mimi nitakuwa baba mwenye nyumba” baba akazungumza huku akinikumbatia na kunivutia zaidi upande wake.

“Aaah Baba taratibu basi” nikalalamika mtoto wa kike nakwambia. Najua unanishangaa lakini utanisoma tu.

Sasa ndugu msomaji shughuli ilikuwa inaelekea kuanza, nakwambia hakuna marefu yasiyo na ncha. Waswahili wanakwambia mbio za sakafuni huishia ukingoni. Na maneno ya wahenga yanasema ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu.

“Baba baby..” nikaita kwa sauti ndoogo kama vile nilikuwa shimoni.

“Unasemaje mtoto baby” baba akaitika kwa sauti ya kutokea kooni.

“Naomba nichumu hapa” nikazungumza kwa deko nakwambia si unajua tena mambo ya kujibebisha.

“Wapi mtoto mzuri?” baba akahoji kwa sauti yake iliyozidi kuwa nzito.

“Hapa shingoni bwanaaa” nikaeleza kwa sauti ya kulalamika iliyokuwa imejaa deko.

Mzee wawatu akajipinda na kuniachia busu moja matata sana. Nilikuwa namsikia akipumua kama nguruwe mwenye njaa aliyemwagiwa maganda ya mihogo.

Sasa nikashuhudia baba akijipinda na kulekea midomo yake kwenye madafu yangu ya kifuani. Mapigo ya moyo wangu yakaanza kwenda mbio kama farasi wa mazoezi.

“Baba subiri kwanza!” nikazungumza kwa sauti kabla midomo ya baba haijatua kwenye madafu yangu.

“Vipi mpenzi unasemaje?” baba alisita kuituma midomo yake na kunisikiliza kwa makini.

“Nikwambie kitu?” nikahoji huku nikionekana kuwa hoi bin taaban.

“Haya niambie mtoto mzuri” baba naye akahoji huku akionekana akipumua juu juu kama fisi mwenye njaa kali aliyeona mfupa mbele yake.

“Nenda kazini” nikazungumza kwa sauti kavu.

Jamani nyie kumbe kauli yangu ile iliniponza. Nakwambia mzee Sekiza hakutoa jibu lolote bali alinichota utafikiri mchanga kwenye koleo, lile ambalo wengine wanaita sijui sepetu sijui chepe, aah nafikiri umenielewa. Kitoto cha kike nikabebwa juu juu utafikiri kipande cha mkate.

Moja kwa moja baba alikwenda na mimi hadi chumbani kwake na kunitupa kitandani kama zigo la kuni ‘Puuu’. “Hatimaye yametimia” nikajisemea nikiwa pale kitandani kwa baba.

Nilimshuhudia baba akisaula viwalo vyake kwa kuanza na shati. Nikainuka kutoka pale kitandani na kwenda kumdaka kisha nikamvutia kitandani na kuanza kufungua vifungo vya shati.

“Tumu leo umenifurahisha sana, yani kama vile sio wewe uliyenifurumusha na mwiko” baba alizungumza huku akichezea nywele zangu.

“Ngoja leo nikupe mambo ya kitanga original” nilizungumza kwa kujiamini.

“Mnh lazima nikujengee nyumba na nitakununulia gari Tumu” masikini mwanaume wawatu alikwisha oza akabakia garasa tu.

Niliendelea kufungua vifungo vya shati la baba huku mikono yangu ikitetemka kwa wasiwasi na woga. Hata kama ningeamua kutumia nguvu ili kusitisha zoezi lile nisingeweza. Pepo la uzinzi lilikuwa limeshamtawala baba hivyo shughuli ilikuwepo.

“Mungu wangu!” nilihamaki kwa sauti na kuacha kufungua shati la baba nikabaki nimeweka mkono wangu wa kulia mdomoni na macho nimeyatoa kwa hofu.

“Kitu gani tena mrembo” baba akahoji kwa wasiwasi baada ya kuniona nimeshituka kiasi kile.

“Baba nipo mkoani” nikazungumza kwa sauti ya wasiwasi.

“Aaah Tumu utaniua sasa!” masikini ya mungu mzee wawatu alizungumza kwa sauti ya kukata tamaa na kujitua chali pemnbeni.

“Nisamehe baba nilikuwa nimesahau” nikajieleza baada ya kumuona baba amekata tamaa ghafla.

“Upo huko mkoani tangu lini?” aihoji baba huku akiangalia pembeni.

“Ndio nimeanza leo?” nikaeleza huku nikimpapasa kifuani.

“Na unamaliza lini?”

“Mimi huwa nachukua siku nne au tano, tuseme sita kabisa ndio nakuwa poa” nikaeleza kwa sauti yangu ya kudeka.

“Kwahiyo unaniahidi lini?” baba alihoji kwa umakini huku akinitazama usoni.

“Usijali, nikimaliza tu nitakukumbusha mwenyewe” nikazungumza kwa kudeka huku nikimchezea ndevu zake zilizokaa kama miba ya michongoma.

“Sasa kwanini usingeniambia mapema?” baba alijaribu kulalamika.

“Nilisahau mwenzio, nawewe umezidi utundu huko” nikazungumza huku nikimpiga baba kakofi ka mahaba kwenye shavu lake.

“We mtoto utanifanya nisiwe naenda kazini” baba alieleza.

“Aaaah baba, ukitaka tuelewane naomba uende kazini” nikazungumza kwa sauti ya msisitizo.

“Basi nitaenda kesho mpenzi wangu”

“Hapana naomba uende leo, tena amka sasahivi” nikazungumza kwa amri.

“Haya bwana kwaajili yako nitaenda” aliniambia huku akijiinua kwaajili ya kujiandaa kwenda kazini.

Nilimtazama mzee yule na kutikisha kichwa kusikitika huku nikiachiata basamu la ushindi. Alipomaliza kujiandaa alinigeukia na kuniachia tabasamu la bashasha lililochanganyikana na huba ya penzi.

“Nibusu hapa” nilimwambia huku nikimgeuzia shavu langu la kusoto.

“Mmmwaaah!” baba wa watu aliachia busu moto moto kwenye shavu langu kama nilivyomuomba.

“Asanteee!” nikashukuru na kujiinua kutoka kitandani.

Baba alipohakikisha yupo sawa alinikonyeza na kunipiga busu la mbali kisha akageuka kuondoka kuelekea kazini huku akiniacha nimesimama mlechumbani nikimtazama alivyokuwa anapotea.

“Pumbavuuuu!” nikazungumza kwa sauti ya chini mara baada ya kubaini mwanaume yule alikuwa ameondoka na kuniacha salama.

Zee zima halina hata haya, linaona raaaha kupumulia watoto wa wenzake. Heti laki tatu, kama ni mali kwanini asibaki nazo mwenyewe. Yaani niuze utu wangu kwaajili ya laki tatu! Kweli jamani? Akwende zake huko, nikasema kama amenikosa leo ndio hanipati tenaaa. Na ningefanya mchezo siku hiyo ningetumbuliwa kiulaiiiini.

*****


Shughuli na mikakati kabambe niliyokuwa nimeifanya kuukwepa mtihani wa baba ilikuwa ni pevu na hatari sana. Sishauri msichana yoyote yule kujaribu kutumia mbinu kama hii kukwepa mitihani ya wanaume kama baba. Maana ni hatari, kuna wanaume wengine hawadanganyiki jamani. Yale mapepo yakishawapanda sijui wanakuwaje, yaani hakuna cha muazini wala cha mnadi swala, utashitukia umeshadonolewa. Nashukuru mungu mzee Sekiza hakuwa wa namna hiyo vinginevyo mbuzi angekuwa kafia kwa muuza supu.

Pamoja na uchovu niliokuwa nao lakini bado nilikuwa na mpango wa kwenda kwa dada Bupe kupata taarifa za mpenzi wangu Endrus. Najua kuna watu wakisikia namtaja Endrus huwa wanachukia sana, lakini hakuna namna maana ndio lilikuwa chaguo langu mtoto wa kitanga.

Nilipohakikisha nimemaliza kufanya kazi za ndani nilichoropoka na kwenda kumtembelea dada Bupe kule mgahawani. Usikasirike msomaji wangu mimi kwenda mgahawani kwa dada Bupe, huko ndiko kulikokuwa kunapatikana kipenzi cha rohoyangu Endrus.

Nilifika na kumkuta dada Bupe akiendelea na shughuli zake za kila siku katika kuhakikisha uchumi wake unakuwa sawa.

“Hodi…Hodi….hodiii” nilibisha hodi kwa sauti huku nikiingia na kupitiliza moja kwa moja hadi jikoni.

“Haya na wewe umetokea wapi?” dada Bupe akahoji kwa kuhamaki kwasababu hakuwa na mategemeo ya kuniona siku hiyo.

“Nimetokea kuzimu” nikajibu huku nikiketi kwenye kiti pale jikoni.

“Huyo bwana wako Fadhili akikukuta hapa si hapata tosha shoga?” alihoji kwa mashaka dada Bupe.

“Mbona ameniruhusu mwenyewe nije” nikazungumza kumuondoa wasiwasi dada Bupe.

“Mnh mwanaume wako ana wivu yule” alizungumza dada Bupe.

“Mbona hata sio mwanaume wangu” nikaeleza.

“Kama sio mwanaume wako, mbona anakuonea wivu sasa?”

“Hamna Fadhili ananipenda tu kama mdogowake” nilieleza.

“Basi haya karibu mjengoni” dada Bupe akanikaribisha huku akikaanga rost ya nyanya.

“Vipi Endrus anasemaje?” pasipo kupoteza muda nikazungumza kile kilichokuwa kimenipeleka pale kwa dada Bupe.

“Na wewe unataka kunivuruga tena, Endrus wa nini wakati ulimkataa?” dada Bupe alizungumza maneno magumu ambayo hayakunifurahisha.

“Lakini hayo si yaliisha dada Bupe!” nikazungumza.

“Kwanza bora umekuja, nina salamu zako hapa” Dada Bupe alizungumza taratibu kama vile hataki.

“Salamu gani tena jamani?” nilizungumza huku nikijiweka vizuri kwenye kogodanilichokuwa nimekalia.

“We unadhani zitatoka wapi?” dada Bupe alizungumza huku akitabasamu.

“Asa mi nitajuaje jamani dada Bupe na wewe” nikazungumza huku nikiamini kwa asilimia zote salamu hizo zilikuwa zinatoka kwa Endrus, kwasababu hakuwepo mtu mwingine yeyote ambaye nilikuwa nimemzoea kiasi cha kuniletea zawadi.

“Nenda pale juu ya kabati ukachukue” aliniambia dada Bupe huku akionesha kidole juu ya kabati lililokuwepo jikoni.

“Niambie kwanza umetoka kwa nani?” nikahoji huku nikijishebedua ilhali nilikuwa nafahamu mzigo ule ulikuwa umeletwa na Endrus.

“We nenda ukachukue, mtoaji utamfahamu huko huko” alisema dada Bupe.

Niliinuka kwa shauku kubwa na kuelekea kwenye kabati. Nilipeleka mkono na kuchukua kiboksi kidogo kilichokuwa na ukubwa wa mkate mkubwa wa bofulo.

“Ndio hili boksi?” nilihoji huku nikiwa nimelishikilia boksi lile.

“Ndilo hilohilo babu chukua” alisema dada Bupe huku akiendelea na shughuli yake.

Nilivuta hatua kutoka na boksi lile huku nikilitazama kwa makini. Katika kichwa changu kulikuwa na taswira ya Endru. Nilitokea kumpenda sana mwanaume huyo, sifahamu ni kwanini lakini ndani ya siku zile chache tu mtoto wa kitanga nilikuwa kwisha habari yangu. Hata sielewi alikuwa amenifanya nini kijana yule. Jamani Endru nyie we acha tu. Nikafungua boksi lile kwa tabasamu kubwa.

Tabasamu langu liliongezeka zaidi baada ya kukuta simu ya mkononi ikiwa imewekwa juu ya nguo za ndani zenye rangi mbalimbali zilizokuwa zimekunjwa vizuri. Niliinua macho yangu na kutazamana na dada Bupe ambaye naye alikuwa anatabasamu kama mimi.

Ghafla tabasamu langu lilianza kutoweka taratibu baada ya kukuta picha ya mtumaji pamoja na jina lake. Picha haikuwa ya mpenzi wangu Endrus na jina lake lilikuwa ni HANCE. Niliinua macho tena na kumtazama dada Bupe, nilivuta pumzi ndefu na kuzibana kisha nikaziachia huru kwa pamoja.

Dada Bupe aligundua utofauti uliokuwepo kwenye uso wangu, akatoa kicheko kidogo cha kishambenga.

“Vipi kuna tatizo?” alihoji dada Bupe alipomaliza kile kicheko chake cha kishankupe.

“Huyu ndio nani tena?” nikahoji huku nikimuonesha ile picha ya kijana yule.

“Huyo ni ‘handsome boy’ anaitwa Hance” alijibu dada Bupe huku akijiinua kutoka pale alipokuwa ameketi.

“Sasa mbona ameniandikia ‘I Love you?” nikahoji kwa mshangao.

“Ndio hivyo tena, kijana amekwisha kufa na kuoza” dada Bupe alizungumza huku akiepua karai la kuchomea chapati kutoka jikoni.

“Sasa inakuaje hapa mbona sielewi?” nikahoji kwa mshangao huku nikikumbuka maneno ya Fadhili kuwa dada Bupe hakuwa mtu mzuri hasa kwa mabinti wa wenzie.

“Acha kujishebedua wewe mtoto wa kitanga, kijana wa watu anaomba nafasi ndani ya moyo wako” alizungumza dada Bupe kwa msisitizo kuonesha alikuwa anamaanisha kwa kile alichokuwa anakizungumza.

“Sasa na Endru naye itakuwaje?” nikahoji kwa mshangao zaidi huku nikiwa sina hata chembe ya bashasha usoni mwangu.

“Kwani tatizo liko wapi?”

“Tatizo hulioni dada Bupe?

“Mi sioni tatizo lolote, kwani kupenda ni dhambi?” alizungumza dada Bupe huku amenikazia macho usoni.

“Endru akigundua je itakuwaje?”

“Kwani amekuoa babu? Hata hivyo hawezi kugundua”

“Mnh! Dada Bupe mie naogopa mwenzangu Akaa!” nikazungumza huku nikikumbuka lile songombingo lililokuwa limetokea nyumbani kwa Fadhili na kaka Imran kwa sababu hiyo hiyo ya kuwachanganya wanaume. Lakini pia nikakumbuka tena maneno ya Fadhili ya kusema kuwa dada Bupe alikuwa na tabia ya kutongozea vitoto vya kike wanaume.

“Wacha woga wewe, unafikiri wanawake wote hawa unao waona wana mtu mmoja tu, kikubwa ni kucheza nao kwa umakini” dada Bupe alizungumza pasipo na hata chembe ya wasiwasi wala aibu mwanamke yule.

“Kwahiyo we dada Bupe unanishaurije?” nikahoji huku nikiwa sielewi cha kufanya.

“Ushauri wangu mimi ni huu, Usipoteze bahati, mtu amejileta mwenyewe we kanyaga twende kwani shida nini?” dada Bupe akazungumza kwa msisitizo.



“Laskini si unajua mwenzio tayari nishampenda Endru?” nilizungumza kwa hisia na wasiwasi wa kumpoteza Endru wangu.

“Kama unampenda Endru, huyu Hance mlie visenti vyake halafu basi” alizungumza dada Bupe kwa kujiamini.

“We dada Bupe wewe, hivi unanionaje?” nikahoji kwa msisitizo.

“Usiwe na wasiwasi Tumu wala hauto gonganisha”

“Haiwezekani mwanamke mmoja kuwa na wanaume zaidi ya mmoja” nikazungumza kwa msisitizo huku nikitamani kunyanyuka na kuondoka.

“Hivi utastaarabika lini Mwantumu, kila siku unakuwa yule yule wa kule kijijini kwenu Tanganyika” Alizungumza dada Bupe huku akibenjua midomo yake kwa nyodo.

“Mi mwenzio hata sikuelewi, yani hapa kwa Endru ndio nimefika” namimi nikazungumza kwa nyodo nikibenjua midomo yangu kwa maringo ya kitanga.

“Yani mimi unanikera na huyo Endru wako, maana hatunywi hata maji. Ukiingia Endru, ukitoka Endru. Kama mwehu vile!” dada Bupe akanichana makavu live.

“Dada Bupe mimi kwa Endru sio mwehu tu bali ni chizi” nikazungumza maneno ambayo niliona wazi hayakuwa yamemfurahisha dada Bupe.

“Karaga baho na ubwezi wako” alizungumza dada Bupe maneno ambayo maana yake ni mtu asiyejielewa.

Kumbe wakati nazungumza na dada Bupe kaka yule aliyenitumia zawadi alikuwa amekwisha kuingia mgahawani na kusimama kwa nyuma yangu akinitazama kwa macho ya uchu. Nikamuona dada Bupe akikonyezana naye ndipo na mimi nilipogeuka na kumkuta Hance amesimama akinitazama kwa tabasamu la huba.

“Haaaa wewe!” nilishituka na kukimbilia jikoni. Sikutaka hata kukutana na mwanaume yule maana ningeweza kujikuta nashawishika na kumsaliti kipenzi changu, ua la moyo wangu, asali wangu Endrus.

“Karibu Hance” dada Bupe alimkaribisha Hance.

“Asante, sasa mbona mrembo amekimbia jamani?”

“Anakuona aibu heti” alizungumza dada Bupe huku akitabasamu.

“Naweza kuja huko?”

“Karibu” alizungumza dada Bupe huku akimuoneshea ishara ya kuingia kule jikoni nilipokuwa nimejificha mimi. Hance alivuta hatua moja moja hadi kule jikoni na kunikuta nimejibanza nyuma ya mlango. Nilishituka sana baada ya kumuona.

“Aaah wewe!” nilizungumza kwa kuhamaki baada ya kumuona kijana yule amenifuata kule jikoni.

“Jamnai mtoto mzuri usiniogope bwana” alizungumza Hance kwa sauti ya kubembeleza huku akinisogelea zaidi.

“Wewe! Naomba usinisogelee” nikazungumza kwa ukali kidogo huku nimemnyooshea kidole kwa ishara ya onyo.

“Mambo vipi mrembo?” alinisemesha Hance kwa sauti ya chini huku akisita kunikaribia.

“Poa” nikaitika kwa sauti ya kujiuma uma.

“Umepata zawadi zako?”

“Zawadi gani?”

“Dada Bupe hajakupa kabahasha?” Hance alizungumza huku akitamani kunigusa, lakini kutokana na ndita niliyokuwa nimeiweka usoni, akaahirisha.

“Mungu wangu, huyu mwanamke yupoje?” Hance alionekana kukasirika kutokana na kitendo cha dada Bupe kutonipa bahasha ya zawadi zangu.

“Sijui”

“Naomba basi nikubusu kidogo?” Hance alihoji huku akiwa amevaa sura ya huruma na kubembeleza.

“Wewe! Unibusu kama nani?” nilizungumza huku nimetoa macho bila mzaha.

“Unajua nakupenda sana Mwantumu” Hance alizungumza kwa ile sauti yake ya kutia huruma.

“Ahsante kwa hilo, nashukuru” nikajibu kwa mkato huku nikiwa mkavu usoni.

“Naomba basi uwe mpenzi wangu” akafunguka kijana wa watu.

“Mbona umechelewa sasa!” nikazungumza kwa ufupi.

“Inamaana tayari una mpenzi?” alihoji Hance huku akionekana kuishiwa nguvu na matumaini.

“Tena nampenda sana mpenzi wangu” nikaeleza kwa msisitzo.

“Duh! basi fanya niwe hata kidumu chako” Hance alizungumza.

“Kwani unanionaje kaka, naonekana kamalaya enh?” nikazungumza kwa hasira.

“Sio hivyo Mwantumu mwenzio nakupenda sana”

“Ndio nimeshakwambi hivyo umechelewa” nikaongea kwa sauti ya msisitizo.

****

Wakati mimi na Hance tulipokuwa jikoni tukiendelea kubishana, Endru alifika mgahawani na kupitiliza moja kwa moja hadi alipokuwa ameketi dada Bupe kama ilivyokuwa kawaida yake.

“Hodiiiii” Endru aliingia kwa mbwembwe.

Dada Bupe alishituka baada ya kumuona Endru, akawa kama vile amewekewa bomu kwapani kutokana na vile alivyokuwa anahangaika.

“He wewe, mbona leo hukunipigia simu kama unakuja?” alihoji dada Bupe huku akisogea zaidi mlangoni ili Endru asipate wazo la kuchungulia kule jikoni.

“Leo nimekuja kumfumania mke wangu” alisema Endru kwa masihara huku akicheka.

“Acha wivu wa kijinga wewe, mtoto wa watu hana tabia za kishenzi kama hizo” dada Bupe alizungumza kwa sauti ndogo ili Hance kule jikoni asimsikie na kugundua kama nilikuwa na uhusiano na mwanaume mwengine.

“Haya niambie yuko wapi mtoto mzuri?” alihoji Endru kwa mbwembwe.

“Asubuhi yote hii unamuulizia mtoto, yupo kwao huko” dada Bupe alijibu kwa mkato.

“Mbona siku nyingine anakuwepo mida hii?”

“Hiyo ilikuwa ni zamani, sasahivi haruhusiwi kutoka tena ndani kwao”

“Kwanini?”

“Kuna watu waliwaona wakati unamchezea, wamekwenda kushitaki kwao” dada Bupe alizungumza maneno hayo ya kumkatisha tamaa Endru ili aondoke.

“Daaah sasa itakuwaje, maana mwenyewe nimekuja kwa lengo la kuonana naye, unajua nampenda sana mdogo wako?” Endrus akazungumza kwa unyonge masikini kaka wawatu pasipo kuelewa kama mpenzi wake nilikuwa nimebananishwa jikoni na kimtu fulani hivi kijinga jinga.

“Usijali, baadaye atakuwepo” dada Bupe alimjibu Endru kwa mkato.

“Basi naomba chai” Endru alizungumza huku akijiweka kwenye kile kiti nilichokuwa nimekalia mimi karibu na mlango wa kueleke jikoni ambako mimi na Hance tulikuwemo.

“Usikae hapo!” dada Bupe alipaza sauti kumtahadharisha Endru asiketi kwenye kiti kile.

Endru alijiinua harakaharaka na kugeuka kukitazama kile kiti kama kulikuwa na kitu ambacho hakutakiwa kukikalia.

“Kuna nini?”

“Sikuhizi wateja hawaruhusiwi kukaa huku”

“Lakini mimi nipo tofauti na wengine”

“Huna utofauti wowote, kwangu nyote ni wateja tu” dada Bupe aliendelea kumjibu kwa mkato Endru kiasi cha kumfanya aingiwe na mashaka.

“Lakini dada Bupe leo unaonekana haupo sawa?” alihoji Endru kwa mshangao.

“Niwe sawa nisiwe sawa, nenda ukakae huko”

“Kwani nimekosea wapi dada Bupe?”

“Bwana nenda huko!”

“Mnh!” Endru akabakia na mshangao.

“Fwee nini? Mteja kwangu ni fala tu” alizungumza dada Bupe huku akikoroga uji wa ulezi uliokuwa ukichemka kwenye jiko la mkaa pembeni na pale alipokuwa ameketi.

“Haya bwana, lakini mpenzi wangu hajambo?” Endru akahoji kwa unyonge.

“Nenda huko kwao ukamuulize” dada Bupe alizungumza huku akionesha kwa mwiko upande wa nyumbani kwetu.

Endru alipoa na kuwa mpole zaidi ya alivyo, hakutegemea kama siku ile angepokelewa kwa dizaini ile. Alitamani dunia ipasuke atumbukie ili asiendelee kuonana na dada Bupe wa siku.

Kule jikoni, mimi na Hance tulikuwa tukiendelea na mazungumzo pasipo kufahamu kilichokuwa kikiendelea huku nje kati ya dada Bupe na Endru. Hance alikuwa akinikera kiasi cha kunifanya nizungumze kwa sauti kubwa na yenye ukali.

Kule nje Endru alisikia sauti ile niliyokuwa nimeitoa nilipokuwa nazungumza na Hance. Alishituka kidogo na kumtazama dada Bupe usoni. Dada Bupe naye akamtazama kwa jicho la kebehi na kumpotezea.

“Si sauti ya Tumu hiyo?” alihoji Endru kwa mashaka.

“Kwani vipi?” dada Bupe alizungumza kwa mkato.

“Sasa mbona umeniambia hayupo?”

“Kwani umemuona wapi?”

“Nimesikia sauti yake huko jikoni” Endru alizungumza huku akijaribu kuchungulia jikoni.

“Weee! Shika adabu yako, huku jikoni hakukuhusu. Tena ondoka!” alizungumza dada Bupe kwa ukali huku akijifanya amekasirika.

Kutokana na msimamo wangu niliokuwa nikiuonesha kule jikoni, Hance alikata tamaa na kuamua kutoka nje na kuniacha mle jikoni. Alikuwa mpole na mdogo utafikiri amenyeshewa na mvua.

Endru alizidi kupatwa na kigugumizi baada ya kumuona Hance akitokea jikoni ambako alikuwa amesikia sauti.

“Ni nini kinaendelea hapa?” alihoji Endru kwa mashaka huku mapigo ya moyo wake yakiongezeka spidi.

“Kama unacho kiona” alijibu dada Bupe kwa kebehi.

Wakati Endru akiwa katika ile hali ya mshangao, namimi kule jikoni pasipo kuelewa kama Endru alikuwepo pale, nikatoka nje. Macho yangu yakakutana na macho ya Endru.

“Mungu wangu! Mwantumu, Kumbe upo hivyo?” alihoji Endru kwa mshangao huku akitetemeka kwa wivu.

“Sio hivyo unavyofikiria Endrus!” nikazungumza kwa kuhamaki.

“Pumbavu wewe! Nakuheshimu kumbe Malaya tu” Endrus alizungumza kwa hasira.

“Mungu wangu Endru unanikosea!” nikazungumza kwa kuhamaki.

“Dada Bupe nakuheshimu kumbe unamuuza mke wangu!” Endrus alilalamika huku akiwa amemtumbulia macho Bupe.

“Bwana Ebu tuondokee hapa, mkeo umemuoa lini!” dada Bupe alizungumza kwa ufupi huku akionesha ishara ya kumfukuza Endru.

“Kwani nini kinaendelea hapa?” Hance ambaye tulikuwa pamoja jikoni alihoji.

“Achana naye chizi huyo” dada Bupe akajibu.

“What! Unaniita mimi nani?” Endru alizungumza huku akivuta hatua kumsogelea dada Bupe kwaajili ya kumtandika makofi angalau mawili matatu.

Hance alisogea mbele ya dada Bupe haraka sana na kumkinga asiingie katika hatari ya kutandikwa. Endru alijaribu kumsukuma Hance ili amfuate dada Bupe lakini Hance akamzuia.

“Weee! Chezea kwingine, usichezee dada Bupe na mke wangu Mwantumu” Hance alizungumza kwa kukoroma huku akimuelekezea kidole Endru.

“Mke wako! Ivi unajielewa wewe, huyu ni mpenzi wangu mimi” alizungumza Endru kwa kujimwambafai.

“Ondoka Endru, nitakufunga kwa kunifanyia vurugu hotelini kwangu” dada Bupe alizungumza kwa vitisho ili kupunguza jazba za Endru.

Hance ambaye alikuwa na hasira za kunikosa mimi, alimsukuma kwa nguvu Endru wangu ambaye alipepesuka na kutaka kudondoka, lakini akajizuia kwa kuweka mikono chini.

Endru alijiinua na kumfuata Hance kwa kasi ya ajabu na kumtandika ngumi maeneo ya chini ya jicho. Hance alipepesuaka hadi tulipokuwa tumesimama mimi na dada Bupe. Pasipo kujishauri mara mbili Hansi alimfuata kwa kasi Endrus lakini Endru alimpokea kwa kumtandika ngumi moja takatifu chini ya kidevu. Akapepesuka tena hadi pale tulipokuwa tumesimama mimi na dada Bupe.

Nilipoona msala ule nilikimbia na kujificha nyuma ya mgongo wa dada Bupe. Hance akawa amesimama mbele yetu.

Endru alichukua sufuria iliyokuwa ikichemka uji wa ulezi jikoni na kuumwaga kwa nguvu usawa wa uso wa Hance. Lakini sijui ni kwa bahati mbaya au ni nzuri, Hance aliinama haraka na ule uji ukatua usoni mwa dada Bupe.

“Ma ma na ku fa a a a !” dada Bupe ambaye alikuwa amesimama mbele yangu alipiga yowe la maumivu makali yaliyotokana na kuunguzwa na ule uji wa ulezi.




Endru umeua!” nilipaza sauti huku nikimuinamia dada Bupe ambaye alikuwa akiendelea kupiga kelele za maumivu akiwa chini.


Endru na Hance walipobaini kuwa dada Bupe alikuwa ameungua vibaya usoni, wote wawili walichomoka na kutokomea kusiko julikana.


Ndani ya dakika moja tu watu walikuwa wamejaa mgahawani pale. Kila mmoja alikuwa akijitahidi kuhoji kilichokuwa kimetokea. Hata hivyo kati yangu mimi na dada Bupe hakuna ambaye alithubutu kueleza chochote zaidi ya kuomba msaada wa kumpeleka mgonjwa hospitali.


****


Amani ya moyo wangu ilikuwa imetoweka jioni ya siku ile. Niliogopa sana kwasababu kama baba na mama ndani mle wangebaini chanzo cha kuungua kwa dada Bupe ingekuwa ni tatizo kwangu. Na niliamini kwa asilimia zote kuwa safari ya kwenda kwetu kijijini ilikuwa ikinukia.


Nilijitahidi kufanya kazi zangu na kuzimaliza mapema sana siku hiyo. Niliandaa meza ya chakula kama kawaida yangu kisha nikaingia chumbani na kujifungia. Kikubwa ambacho nilikuwa nakisubiria ni kesi jioni hiyo kisha kupigwa ‘out’ kurudi kijijini.


Mnamo majira ya saa nne usiku nilitoka chumbani na kukuta taa za sebleni zimezimwa, nikabaini kila mtu alikuwa amelala. Nilinyata taratibu na kwenda mezani kuangalia chakula ambacho nilikitenga. Nilifurahi sana nilipokuta kimeliwa. Nikarudi chumbani kwangu na kujilaza kitandani nikawa naendelea na mawazo ya tukio lililokuwa limetokea mchana kule mgahawani kwa dada Bupe.


Jambo lingine kubwa sana ambalo lilinichanganya zaidi ni usalama wa mahusiano yangu na Endrus. Nilikata tamaa na kuamini kuwa mimi na Endrus ndio ilikuwa basi tena na isingewezekana kuwa pamoja milele abadan. Pamoja na kwamba nilimpenda sana na kumheshimu kwa kulinda penzi lake lakini mwisho wake ndio ulikuwa ule. Niliumia sana na kujikuta nikishindwa kuzuia machozi kutiririka kwenye mashavu yangu.


Hadi ilipofika kwenye majira ya saa saba hivi ndipo usingizi ukawa ukiniiba iba kutoka kwenye lindi la mawazo. Nilijitegesha vizuri ili niweze kulala na kuachana na habari za kuwaza jambo lile.


Sauti ya mlango wangu wa chumbani ukigongwa ilinishitua. Niliinua shingo na kusikiliza kwa makini. Mlango ulikuwa ukigongwa taratibu na kwa umakini wa hali ya juu.


“Nani?” nilihoji kwa wasiwasi.


Mlango uliendelea kugongwa kwa mtindo uleule wa pole pole. Nikaanza kuhisi mapigo ya moyo yakinienda mbio. Nikahisi ni lazima angekuwa baba au kaka Imran. Sikuweza kumhisi Fadhili kwasababu Fadhili hakuwahi kunifanyia vituko kama wengine.


Huku nikiwa na wasiwasi niliusogelea mlango na kuufungua taratibu huku nikichungulia nje. Nikamuona baba amesimama mlangoni huku akiwa na kawoshi na bukta tu.


Wakati nimesimama nikimtazama kwa mshangao, alinisukuma kidogo na kuingia chumbani kwangu kwa spidi. Alizunguka na kusimama nyuma yangu huku akinioneshea ishara ya kufunga mlango. Baada ya kuhakikisha kuwa nimetia komeo kwenye mlango, alininyanyua juu juu.


“Aai baba!” nikazungumza kwa sauti ya aibu huku nikiwa hewani nimebebwa na baba.


“Njoo hapa mtoto mzuri leo unipe mambo matamu” baba alizungumza huku akiniweka kwenye kitanda.


“Lakini baba si unajua nipo mwezini?” nikahoji kwa kujihami.


“Wala usijali hata mimi nilikuwa na safari ya kuja huko huko mwezini” baba alizungumza bila kujitambua huku akianza kunipapasa kwenye mapaja yangu ambayo yalikuwa yamefunikwa kwa kanga ambayo nilikuwa nimejisitiri nayo kwa kuifunga kifuani.


Nilianza kuhisi lile pepo langu la huba likianza kunipanda taratibu kutokana na hisia nilizokuwa nazipata kutoka kwenye mikono ya baba.


Potelea mbali nikaona afadhali baba amekuja pengine angenisaidia kuniliwaza kutoka kwenye ule wakati mgumu niliokuwa nao. Ndugu msomaji asikuambie mtu, hakuna kitu kinachouma kama kuachwa na mtu unayempenda. Nakwambia usipokuwa makini unaweza ukajikuta unagawa kama njugu na ukija kushituka umeshaliwa sanaaa.


“Asssccc aaaah subiri badadaba….” Nilishindwa kuvumilia na kujikuta nikizungumza maneno yasiyoeleweka.


Baba alinibana pale chini kwa goti lake la mguu wa kushoto kisha midomo yake aliituma kwenye madafu yangu ya kifuani na kuanza kuramba koni kwa ufundi. Jamani nyie daaaa! Nashindwa kuelezea kwa vile nilivyokuwa najihisi pale kitandani.


Baba alikuwa akinifanyia vitu vigeni ambavyo vilinifanya nisahau shida zote ambazo zilizokuwa zikinikabili. Sidhani hata huyo Endru niliyekuwa nimemnga’nga’ni kama angekuwa na uwezo pamoja na utundu kama aliokuwa akinionesha baba.


Mnh nikabaini kumbe mama alikuwa anafaidi sana na ndiyo maana alikuwa akimuonea wivu sana mume wake. Kumbe wakubwa wanafaidi jamani nyie kaaa! Sijui kipi kilikuwa kinanichelewesha hadi kufikia kumfurumusha na miko fundi yule.


Baba aliendelea na shughuli yake ya kunipagawisha mtoto wa kitanga. Kusema ukweli nilijikuta nikiwa hoi bin taabani na kuomba matibabu kutoka kwa daktari wangu yule ambaye alikuwa amenisababishia mwenyewe maradhia.


Wakati mimi nipo katika hali ile ghafla nikamuona baba akihangaika mle chumbani kama vile kulikuwa na kitu anakitafuta. Nilishituka kidogo na kuinua kichwa kumtazama. Nikamuona akielekea nyuma ya kabati ambako kulikuwa na upenyo kidogo, akatumbukia na akajibanza.


Wakati naendelea kushangaa vioja vile, nikasikia mlango ukigongwa tena. Nilishituka sana na kuogopa kwa kuhisi pengine mama aliamua kumsaka mume wake kutokana na kuto kumuona chumbani kwao. Nisikufiche ndugu msomaji, nilikuwa natetemeka. Ukizingatia zaidi ugongaji wa safari hii haukuwa wa polepole kama vile alivyokuwa akigonga baba.


Nilipofungua mlango tu kabla hata sikumtazama kwa makini mgongaji, nikajikuta nikivamiwa na kudondokea ndani. Kumbe alikuwa ni kaka Imran, jamani nyie. Alichofanya yeye ni kuurudisha mlango kisha akanishika mkono na kuninyanyua kutoka pale chini nilipokuwa nimedondokea, safari hiyo mlango haukuwa umefungwa.


“Mwantumu mpenzi nimeshikika mpenzi wangu!” alizungumza kaka Imran huku akinikokota kuelekea kitandani.


Kwakuwa nilikwisha amua kujitoa kumpa utamu baba nikagoma kusogea kitandani kama alivyokuwa akitaka kunikokota Imran.


“Hapana kaka Imu bwana mie sitaki” nilizungumza huku nikijaribu kujitoa mikononi mwake.


“Nisaidie Mwantumu mpenzi wangu, kesho nitakupa zawadi” kaka Imran alijaribu kunibembeleza, huku akijaribu kunifunua khanga na kunipapasa kwenye mapaja.


Na mimi nikajitahidi kukwepesha mwili wangu asiuguse hasa kwenye maeneo ya mapaja lakini kaka Imran akawa king’anga’nizi. Kusema kweli akili yangu haikuwa sawa kabisa kwasababu niliamini baba alikuwa anashuhudia kila kitu alichokuwa ananifanyiakaka Imran. Pengine kaka Imran angekuwa ametangulia chumbani mle nafikiri ningempa mzigo pila hata kipingamizi kutokana na hali ya kuchanganyikiwa niliyokuwa nayo baada ya kuachwa na mpenzi wangu Endrus.


Wakati kaka Imran akiendelea kuminyana na mimi, mlango ulifunguliwa na Fadhili akachungulia. Kumbe na yeye alikuwa ameamua siku hiyo kunitembelea chumbani kwangu kumaliza migogoro yetu na kurejesha mapenzi yetu kama zamani. Mazungumzo yetu ya mchana wa siku hiyo yalimtia moyo na kumrejesha katika mstari wa penzi langu.


Macho yangu na macho ya Fadhili yakakutana. Nguvu za kuminyana na kaka Imran zikaongezeka zaidi. Nilimsukuma kwa nguvu kaka Imran kiasi cha kudondokea kule kwenye kabati usawa na sehemu aliyokuwa amejificha baba.


Fadhili hakuweza kuamini macho yake kwa kile kitendo alichokishuhudia. Wivu na hasira vikampanda na kujikuta akipayuka pasipo kujishauri.


“Mama…. Mama….njoo uone hukuu” Fadhili alipaza sauti kumuita mama yake.


Imran aliweza kumuona Fadhili alivykuwa akimshangaa kama video ya mazombi. Aibu zikamvaa na kujihisi kuishiwa nguvu. Alipogeuza shingo yake upande wa kushoto akajikuta macho yakimtoka zaidi na kuchanganyikiwa baada ya kumkuta baba naye amejibanza nyuma ya kabati tena akiwa hana hata nguo moja mwilini.


Mama alitoka chumbani kwake mbio na kufika eneo la tukio. Mimi nilibakia nimesimama huku nikijifanya kulia kutokana na kitendo alichokuwa anataka kunifanyia kaka Imran.


“Umemuona mwanao, siku zoite anajifanya kunifokea fokea kumbe ana lake jambo” Fadhili alizungumza kwa sauti huku naye wivu ukizidi ukimsokota moyoni. Ukweli ni kwamba alikuwa ananipenda sana lakini visa vya kaka Imran vilimkatisha tamaa na kujifanya ananichukia.


Kaka Imran alijiinua taratibu kutoka pale alipokuwa amedondokea na kwenda kusimama kwa kuegemea ukuta.


“Imran mwanangu, unataka baba yako akuue? Jana mwenyewe umemsikia alivyokuwa akitufokea kwa kumtania Tumu, saa hizi unafaya hivi. Unatafuta nini lakini wewe?” mama alizungumza kwa hasira huku akitamani kumkunjakunja kaka Imran na kumtafuta.


“Tena nimemkuta anaminyana kabisa kumbaka mtoto wa watu” alizungmza Fadhili kwa ushabiki.


“Aibu hii tutaiweka wapi mwanagu Imran? Umerithi wapi huwo upuuzi, mbona sisi hatuna tabia hiyo?” alizungumza mama kwa hasira huku akinisogelea pale nilipokuwa nimesimama huku nikijifanya kulia.


“Pole sana mwanangu, amekuumiza?” mama aliniuliza huku akinitazama kwa macho yaliyokuwa na huruma.


Nilitikisa kichwa kuashiria kuwa sikuwa nimeumia mahali popote kutokana na purukushani zile. Mama alinivuta na kunikumbatia kwenye kifua chake huku akichezea nywele zangu kwa mkono wake wa kulia. Nilihisi machozi yakinidondokea kwenye shingo yangu kuashiria kuwa mama alikuwa analia.


Kule nyuma ya kabati baba alikuwa amejibanza kimya akiomba Mungu asibainike. Lakini kutokana na mazingira yenyewe kuwa na vumbi, chafya ikamuumbua.


Mama na Fadhili walishituka na kutazamana kwa mshangao. Imran hakushituka kwasababu alikwisha kuelewa kuwa kule nyuma ya kabati kulikuwa na mtu. Mama akampa Fadhili ishara ya kwenda kuchungulia.


Fadhili alikwenda kwa shauku kubwa ya kutaka kufahamu kilichokuwa kinaendelea ndani mle.


“Heeee!....” Fadhili alishituka na kushika kichwa kwa mshangao.


Baba aliweka mkono mdomoni kumzuia fadhili asizungumze kama alikuwa amejibanza kule nyuma ya kabati.


“Kuna nini?” mama alihoji kwa wasiwasi.


“Mtu mzima anamwaga radhi huku!” alizungumza Fadhili huku akiziba macho yake kwa viganja vya mikono.


“Mtu mzima ndio nini?” mama akahoji huku akionekana kuto kuelewa maneno ya Fadhili.


“Zee la kazi!” Fadhili akazungumza kwa ufupi.


“Mbona sikuelewi Fadhili, una nini na wewe?”


“Unafikiri nitaanzia wapi mama kuzungumza?” Fadhili alizungumza huku akiondoka eneo lile ambalo alikuwa amesimama na kumshuhudia baba akiwa amejificha huku hana hata nguo moja mwilini mwake.




Mama aliniachia na kwenda kule nyuma ya kabati kushuhudia mwenyewe kwa macho yake kile kilichokuwa kinamshangaza Fadhili na kumfanya ashindwe kuzungumza akaeleweka.



Mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio ghafla baada ya kumkuta mume wake amejibanza akitumbua macho kama mwizi.

Mama alidondoka chini na kupoteza fahamu. Mshike mshike tena ikahamia kwa mama. Ilibidi baba atoke kule nyuma ya kabati na kuvaa bukta yake kisha akamuendea mke wake na kumsaidia kwa kumpa huduma ya kwanza.

Ulipita muda pasipo mama kurejewa na fahamu. Ikabidi safari ya kuelekea hospitali kwaajili ya matibabu ianze.

Walitoka watu wote kuelekea hospitali na kubakia pekeyangu nyumbani. Akili yangu ilikuwa imezidi kuvurugika. Sikuweza kufahamu kama huko hospitali mama angepata nafuu ama ndio ingekuwa bahati mbaya. Na kama angepona na kurudi nyumbani mimi ningekuwa katika hali gani? Kwa ambavyo mama alikuwa na wivu, angenibakisha salama kweli? Na kule kwa dada Bupe ambako nilisababisha majeruhi ningeachwa salama kweli kwa kosa la kusababisha vurugu? Masikini mimi mwenzenu nikajihisi kuwa na mkosi kuliko kiumbe yeyote duniani.

Akili ya kutoroka ilinijia, nilianza kujiandaa haraka haraka. Kikwazo kikanijia katika namna ya kuondoka jijini pale. Pesa za mshahara nilizokuwa napewa nilizikataa na kumwambia mama aniwekee. Sasa ningeondoka vipi? Nikajiuliza mara mbilimbili huku nikiwa nimeketi kitandani na mikono yangu ikiwa kwenye mashavu.

Waswahili wanakwambia ‘Raha ni wa mpumbazi na shida mwana mgunduzi’ nilikwenda chumbani kwa mama na kuanza kupekua sehemu mbali mbali. Kwa bahati nzuri nilipofungua droo ya kabati, nikakuta pesa za kutosha kama milioni mbili hivi.

Nilichofanya ni kuhesabia na kuchukua shilingi laki tatu tu. Niliamini kiasi hicho cha pesa kingeweza kunifikisha kwetu Tanga na pesa nyingine ningefanyia mambo yangu huko baadae.

Nilivaa juba na kujiziba usoni huku nikiacha macho tu. Nikachukua begi langu na kuanza safari ya kuelekea Ubungo kwaajili ya safari siku ambayo ingefuata. Ilikuwa tayari ni saa tisa za usiku, hivyo nilifanikiwa kupata daladala na kwenda hadi Ubungo.

Nilipofika nilikwenda kwenye jengo la abiria na kukuta abiria wengine wamelala na wengine wamekaa. Namimi nikaweka begi langu pembeni na kujikunyata kwenye benchi kusubiri kupambazuke nitoroke jiji.

Ilipofika majira ya saa kumi na moja nilielekea kwenye ofisi ya basi la Raha_Leo ambalo lilikuwa likiondoka saa kumi na mbili asubuhi. Nilikata tiketi na kwenda kuketi kwenye siti yangu tayari kwa safari.

Nikiwa kwenye siti yangu huku sina wasiwasi kutokana na mavazi niliyokuwa nimeyavaa kuwa vigumu kutambulika, Nilishitukia watu watatu wakiingia kwenye basi lile na kuja kusimama pale kwenye siti yangu. Mmoja kati ya watu wale alikuwa mwanamke na wengine wanaume.

“Naomba tiketi yako” alizungumza mtu mmoja huku akinyoosha mkono kwangu.

“Tiketi yangu?” nikauliza kwa wasiwasi.

“Ndio, lete tiketi” alizungumza kaka yule kwa amri.

“Ya nini?” nikazidi kuhoji kwa wasiwasi.

“Acha maswali lete tiketi” kaka yule alizungumza kwa ukali kidogo.

Kutokana na mchecheto niliingiza mkono kwenye pochi yangu na kutoa tiketi yangu kisha nikawakabidhi.

Kaka yule aliipokea tiketi ile na kuisoma, kisha akawapa wenzake nao wakaisoma. Nikaona wakinitazama kwa mkazo huku wakitikisa vichwa vyao. Yule kaka alirudi nyuma kisha yule mwanamke akanisogelea.

“Hebu vua hicho kitambaa?” alisema yule mwanamke.

“Kwanini?” nikahoji kwa mshangao.

“Sisi ni maafisa wa polisi, tuna mashaka na wewe, tunataka kukukagua” alizungumza yule mwanamke huku akionesha kitambulisho chake.

“Lakini mimi sikufanya kitu” nikazungumza kwa wasiwasi.

“Vua bwana usitucheleweshe” mwanaume aliyekuwa ananihoji awali alizungumza kwa ukali.

Nilijikuta nikiondoa kitambaa kile kilichokuwa kimeziba sura yangu huku nikitetemeka.

“Unatoroka sio?” yule mwanamke alihoji baada ya kuniona sura yangu.

“Hapana!” nilizungumza kwa mshituko.

“Kuanzia sasa hivi upo chini ya ulinzi” alizungumza mwanamke yule huku akinikamata mikono na kunifunga pingu.

“Nimefanya nini jamani?” nikahoji kwa wasiwasi hukunikitetemeka kwa hofu.

“We twende utakwenda kujua huko mbele ya safari” askari wale walinichukua msobemsobe huku wakinisukuma na pingu zangu mikononi.

“Lakini ni haki yangu pia kufahamu kosa langu!” nikajikaza na kuzungumza.

“Sikiliza binti, kwanza kabisa unatuhumiwa kusababisha vurugu na kupelekea uharibifu mkubwa wa mali na majeraha kwa mwenye mali” alizungumza askari mmoja kwa sauti ya msisitizo baada ya kuona nimekazana kutaka kufahamu kosa langu.

“Mimi! Nimeleta vurugu? Mnanionea kwakweli” nikazungumza kwa kulalamika.

“Hapa sio mahakamani binti utaeleza mbele ya safari” yule askari wa kike alidakia na kunisukuma.

“Na kama hilo halitoshi, ukatembea na bosi wako na kupelekea mke wake kupoteza….”

“Achana naye” Askari yule wa kike alidakia na kumkatiza kauli mwenzake.

“Mungu wangu jamani nyie mwanionea miye” nikazungumza kwa kulalamika huku nikitiririsha machozi kwenye mashavu yangu.

“Acha kufuru Malaya wewe! Mungu ndio amekutuma ufanye ufirauni wote huo? Utaozea jela ngedere wewe” Jamani nyie nikasukumwa na kupakiwa kwenye kipira cha polisi.

Sijui niseme nini mie, sijui nimlaumu nani mwenzenu mie. Tazama leo nimeishia wapi huku? Kwani kosa langu mimi ni lipi? Mbona kama ulimwengu unanionea na kunikanyaga bila huruma! Kama ni mapenzi nimekosea wapi? Ona mnaniita Malaya, mnaniita kicheche, limbukeni wa mapenzi, maji maramoja na majina kibao ambayo sio ya kiungwana. Lakini sikuwahi kutoka na hata mwanaume mmoja kati ya hao wote mnaowafahamu.

Nilizungumza moyoni huku nikiwa nimekaa kwenye karandinga la polisi huku machozi yakibubujika kiasi cha kuzamisha mboni za macho yangu.

Hakika majuto ni mjukuu, Laiti ningelijua kama yote haya yangenikuta kamwe nisingeacha majukumu yaliyonipeleka jijini na kujiingiza kwenye mapenzi ya kiholela yaliyokosa msimamo ambayo matokeo yake ni haya ya kwenda kuozea jela.

MWISHO!


Ndugu msomaji natoa shukrani za dhati kwa kufuatilia kazi zangu mwanzo hadi mwisho. Tafadhali usiache kutoa maoni yako ili kuboresha msimu wa pili wa simulizi hii. Tafadhali usikubali kupitwa na Simulizi ya kusisimua ya Bongo Daslam itakayoanza kesho saa 12 kamili Asubuhi.


MSIMU WA PILI WA HOUSE GIRL WA KITANGA UTAENDELEA BAADA YA KUMALIZIKA KWA SIMULIZI YA BONGO DASLAM.


MWISHO


1 comment:

BLOG