Chombezo : Nyoo Nipe Mumeo
Sehemu Ya Nne (4)
“No, something is absolutely wrong with you, please tell me what is it! (hapana, lazima kuna kitu hakipo sawa kwako, tafadhali niambie ni nini).” “unanipenda kweli?” nilimuuliza huku bado mashavu yangu yakitiririsha machozi.
Akatabasamu kwanza kama anayonifanyia mazuri, halafu akatumia mikono yake kunifuta michirizi ya machozi mashavuni mwangu kisha akaniambia:
“Umenipa furaha kwenye maisha yangu, umenipa mtoto, umenipa mapenzi ambayo hakuna mwanamke ameweza kunipa. Yes I Love You so much and you Know it,” alisema na kunibusu midomoni.
NYOO NIPE MUMEO 45
Nikatamani kumuuliza; kama kweli ananipenda kwanini alikuwa anatembea na Fatuma? lakini nikaminya nikaona ngoja nimpime.
Unajua mwanaume akitoka kutembea na mwanamke mwingine siku hiyohiyo ukamwambia una hamu naye ya kususu, utamuona anazugazuga.
Sasa nikamvuta karibu mume wangu na kumpa denda kwanza palepale nje, halafu nikachukua mkono wake wa kulia na kumnyonya kidole chake katikati, tena nikawa nakinyonya kwa manjonjo kama vile nanyonya koni.
Nikajua tu lazima ishara yangu ameishaisoma, hiyo ni lugha yetu ya zamani ya mapenzi kuwa nikimnyonya kidole cha kati maana yake nina hamu yakufanya naye mapenzi lakini kwa staili za ajabuajabu ‘Wild sex’ yaani staili zisizohusu kitanda wala kuchezeana.
Nikamvuta taratibu naye akanifuata kwa nyuma, unajua nini nilimpeleka kule bondeni kwenye ile midizi ambayo alifanyaga mapenzi na Fatuma nikamuona kama anasitasita lakini nikamvuta kwa nguvu akajileta.
Kwa kuwa ilikuwa usiku kisehemu kile kilikuwa kizuri mno kilijificha mno, basi nikambana kwenye midizi akiwa anashangaashangaa.
Na mimi nilimfanyia kusudi kumleta hapo kumpima, kama atanifanya basi atakuwa hajalidhishwa na Fatuma siku hiyo, lakini kama hatasimamisha maana yake lazima tu atakuwa amekolezwa na Fatuma .
Nikamtazama usoni na kumfungua zipu na kumtoa jongoo wake aliyeinama kwa masikitiko kama amefiwa, nikapandisha gauni langu juu, tena ndani sikuvaa chochote nikamuinamia staili ya chuma mboga huku nimeshikilia shina la mgomba tena nikajipiga kikofi kwenye wowowo langu nikimtaka anishindue kisawasawa.
Nikatulia kimya na kuanza kuhesabu sekunde, nikiombea asishindwe kunifanya maana kama atashindwa nitaumia sana na sikuwa tayari kwa hilo. “Come on baby, bang me harder!” nilisema kumhamasisha.
Je, Mr X ataweza kusimama au atashindwa?
Post jibu lako kwa kukoment hapo chini.
Itaendelea..
NYOO NIPE MUMEO 46
“Mary una tatizo gani leo?” alisema mume wangu huku akifunga zipu yake na kunitoa pale kwenye lile eneo. Kweli nilithibitisha hana hisia kabisa na mimi na kweli alikuwa ametoka kunisaliti,si kitu kingine.
Hasira zilinipanda nikampiga kofi, nikamuona akishangaa kinafki, nikaingia ndani kwangu kwa hasira nikiwapita mama na baba waliokaa sebuleni wakitazama uchaguzi wa Marekani, nikachukua begi langu na kuondoka bila kujali kama ni usiku au lah.
Mume wangu aliyekuwa nje bado akijiuliza kwa kile kibao, alinishangaa nikimpita nikiwa na begi langu dogo mkononi.
“Mary! Nini kinaendelea? Unaenda wapi?” alisema Jermaine huku akijitahidi kunizuia lakini hapana sikutaka hata kidogo kuongea naye, lakini alinilazimisha nikaropoka. “Najua kila kitu kinachoendelea y’all jus bunch of hipocrates! Wote wanafki wakubwa!”
Baada ya kutupa dongo hilo nikamuona ameganda pale aliposimama kama amelowa maji ya baridi. Nikamuona mama ametoka nje na baba wakihangaika kuniita lakini sikugeuka wala kutazama nyuma nikaenda moja kwa moja barabarani na kupiga simu kwa Hadija.
Alipokea nikamuelezea kuwa nimegombana na mume wangu na nimeondoka nyumbani, nikamuomba japo nilale kwake kwa siku hiyo tu, akakubali na kunielekeza.
Basi nikapanda pikipiki hadi Mwananyamala nyuma ya Hospitali. Nikampigia akatoka nje na kunipeleka kwenye chumba alichopanga.
“He shoga ni yaleyale ya Fatuma au?” aliniuliza kwa shauku nikamuelezea ilivyokuwa akashangaa sana.
“Ndiyo hivyo bora ajue kuwa anachofanya siyo kizuri! Jamani polee!” alinibembeleza Hadija akanitayarishia maji ya kuoga nikaenda kuoga na kurudi ndani nikajilaza kitandani kwake, wakati huo yeye mwenyewe pia alienda kuoga na kurudi chumbani.
NYOO NIPE MUMEO 47
Kwa kuwa tulikuwa wote wanawake hakuona aibu. Akavua taulo na kuanza kujifuta maji taratibu. Nikiwa nimelala kitandani nikaanza kumchungulia kuona kipapatilo chake kimevimba kweli, kama alivyosema Bi Gululi?
Mh ilikuwa kweli kabisa, tena alikuwa mule mule kama alivyokuwa Bi. Gululi, hiyo ikazidi kunitia hasira mno, nikajiapiza kujifunza kwa bidii zaidi kwa Kungwi wangu hata kama sitakuwa na hicho kipapito kinene lakini angalau nifanye vizuri kwenye mafunzo yote na hiyo ndiyo iwe silaha yangu ya kupambana na Fatuma.
Tena nilijifikiria jinsi silaha hiyo ya mapenzi ilivyonikutanisha na Mr X kwa mara ya kwanza na kupata bahati ya kuolewa naye na kuishi Marekani. Sikufichi shoga yangu unayesoma hapa, mwanamke yoyote anaweza kuwa mtu yoyote duniani akiwa anajua mapenzi na akiwa na akili.
Kwani wangapi wameolewa na matajiri kwa mapenzi tu! Sembuse mimi ambaye kwanza ni mzuri tena nikiongezea na ujuzi wa mapenzi si ndiyo kabisa nikimuonjesha hata Obama anaweza kumkimbia mkewe?
Nililala usiku huo huku nimezima na simu yangu kabisa kwa sababu sikutaka usumbufu kutoka nyumbani. Kwa sababu nilijua mume wangu angenipigia usiku kucha, lakini hali kadhalika mama na ndugu zangu wengine.
Siyo siri nilimkumbuka sana mwanangu Kendrick lakini kwa sababu alikuwa na mama nilijisikia ahueni.
Nikapanga kuwa nikiwa chimbo najifunza siku namaliza tu mafunzo, nitaomba mechi mmoja tu na Mr X nimuoneshe utamu wangu na kama baada ya kumpa atachepuka tena Akyamungu naapa kuwa wanaume hawapendeki na hakuna mapenzi ya kweli ya kumtuliza mwanaume asichepuke.
NYOO NIPE MUMEO 48
Nililala hadi asubuhi wakati huo Hadija yeye ndiyo akanishangaza kusema hawezi kwenda kule kwa kungwi tena akataja sababu zake kama za jana eti hakuna mtu wa kumuacha dukani. Nikajua anataka nimpe hela na hana moyo wa kujifunza kama wangu.
Nikaamua kumuacha na mimi kuchukua begi langu na kuondoka zangu nikielekea kwa Kungwi Gululi uzuri nilikuwa na namba yake tayari na niliijua njia kwa hiyo sitaweza kupotea.
Nikapanda bajaji hadi Chanika Mwisho, nikashuka na kupita njia tulizopita jana yake na Hadija, uzuri nilikuwa nikizikumbuka vizuri, nikafika hadi nyumbani kwa Bibi Gululi, mwenyewe akishangaa nimefikaje peke yangu tena nikiwa na begi.
Basi nikamuelezea kwanza yaliyonitokea na nikamtoa hofu kuwa nitafikia kwenye gesti ya jirani na kukaa kwa siku saba mfululizo nikimuomba kunifundisha kila kipengele bila kuacha kitu. Huwezi amini Bibi Gululi alionekana kuwa mkarimu kweli, akaniambia ananikaribisha kuishi nao kwa siku hizo saba za mafunzo hapohapo nyumbani. Nikamshukuru sana, of coz nilimwambia kuhusu Hadija kutofika siku hiyo akashangaa.
“Usijali mwanangu, walio karibu yangu wanadharau, lakini utaona tu matokeo yake. Kama kweli una moyo, siku saba nyingi sana.” Alisema Kungwi akaingia ndani na kumuita yule mwanaye Gululi, aliponiona alifurahi na kunipokea begi langu.
Ilipofika saa tano kamili mafunzo yakaanza tukiwa mule ndani. Somo la kwanza lilikuwa ni jinsi ya kukatika kiuno na faida zake nje na ndani ya sita kwa sita.
Bi. Gululi akamwambia mwanaye aweke ngoma ya Sindimba kwenye simu yake, alipoiweka akaanza Bi.Gululi kukatika yeye kwanza, akaanzia juu huku amesimama, halafu taratibu akishuka chini hadi akachuchumaa huko kote kiuno chake kilionekana kilaini kikizunguka kwenye mhimili wake kama feni.
Tena akainama na kutupa mauno ya nyumanyuma, halafu akalala akapiga msamba huku kiuno kikiwa kilaini vile vile, halafu akainuka bila viuno kukoma akasimama na kuanza kukatika kiupandeupande viuno kama vya Shakira, alipofika hapo akatulia akiniangalia mimi niliyeganda nikimshangaa, nikijiuliza huyu mtu mzima gani!
“Hapo, mwanangu sikuibii!?” alinitania na kumtazama mwanaye akimwambia na yeye aoneshe ufundi wake Akyanani Gululi naye alianza kukatika kiuno mtetemeko yaani kama anagandishagandisha fulani hivi, naye akaenda hadi chini na kulala kama anakatikia mashine akainuka na kutulia lakini hakika kama ningewashindanisha asingemfikia mama yake, duh huyu bibi amenishinda tabia.
“Haya, Mary zamu yako sasa!” aliniambia Kugwi na Gululi akaenda kuurudisha ule wimbo kuanzia mwanzo.
Nikavuta pumzi ndani kwa hofu, lakini nikamjaza akilini Fatuma, nikamuweka Mr X, nikapandisha mzuka na kuanza kukizungusha kiuno cha Kimarekani, kile cha harakaharaka, cha taratibu, cha mviringo, cha mpepeto nikaenda hadi chini nikainama kisha nikajibinjua kichalichali nikainuka juu na vya Shakira nikimaliza na vya Ray C.
Huwezi amini Kungwi na mwanaye walikuwa wametoa macho kama wamebanwa na mlango, nikajiuliza nimeharibu au?
Itaendelea.. Mpe marks mary ameharibu; ameua?
NYOO NIPE MUMEO 50
“Mary! Nani kakufundisha hayo yote?” aliuliza kungwi kwa mshangao.
“kwani nimeharibu!”
“hapana, una kiuno laini kiasi hicho halafu unaibiwa mume! Sikia mwali wangu nimeangalia kwa makini nimeona unavyokatika hautikisiki miguu wala mwili mzima, nimeona unavyokizungusha kiuno chako inaonekana kabisa unaweza kubana na kukatikia mashine vizuri bila kuchomokachomoka. Hili zoezi kwako halina haja kabisa,” alisema kungwi akionekana haamini.
“kweli!” niliuliza kwa furaha, nikikumbuka yale mafunzo yangu na Mr X na enzi zile za darasa la Dr Ben yalikuwa yamenisaidia mno. Nilijisikia faraja kuwa angalau ninajua kitu, (wale wasomaji ambao hawajui, Mary alijifunza haya yote kwenye hadithi ya Mr X Part One kuisoma follow @hadithi.unono anzia chini kabisa.)
Basi Kungwi Gululi akaanza kumuelekeza mwanaye kuwa kwenye kukatika kawaida alikuwa ameweza lakini kwenye kukatikia dudumizi, alikuwa anatoka nje ya mstari kwa sababu hakuzingatia mhimili wa dyudyu, lazima kwanza aibane kwangwaa! Halafu ndiyo azungushie kiuno hapo kwa chini, tena kiuno tu ndiyo kicheze. Siyo kutikisa matako halafu ndiyo ujifanye unajua kukatika, kitandani utashindwa, hapa nyonga tu.
Kungwi akaniambia mimi nilale chini, yaani niwe kama vile mwanaume, Bibi Gululi akamuelekeza Gululi anikalie kwa juu na kuanza kunikatikia kama vile anakatikia ngunga. Bibi Gululi alikuwa akiangalia kwa makini akihakikisha mwanaye hatoki nje ya mstari, na kama akitoka alikuwa akimsema mno.
Hadi Gululi saa nyingine alikuwa akikasirika lakini nilimpa moyo kuwa lazima ataweza ajitahidi tu. Alivyomaliza Bibi Gululi akaja kunikalia na yeye na kumtaka Gululi amwangalie vizuri, basi alichonishangaza yule bibi alikuwa akizungusha kiuno akipanda juu taratibu na kushuka chini huku akivutia kabisa hisia kama kweli vile alikuwa akiumeza mhogo.
“Ukiwa unakata siyo ndiyo unakuwa bubu jamani, Mary umesikia? Ongeza; ladha ya sauti yako ya kitandani ili unogeleshe mchezo,” alisema Bibi Gululi akaanza manjonjo.
NYOO NIPE MUMEO 51
“Aaaah.. ohhhhh! Ashhhhhhh! Happoooooo!” akajigeuzageuza huku akijipapasapapasa kifua chake, akyanani walahi huyu bibi alionesha kujua hadi kupitiliza. Gululi aliyekuwa akimtazama mama yake alionekana kuwa makini kuchunguza vizuri.
“Mama ngoja na mimi nijaribu tena,” alisema Gululi basi Bibi. Gululi akainuka na Gululi naye akaja pale juu yangu akaanza na yeye za kwake akaneng’emula na sauti za mahaba yenye mchanganyiko wa kwikwi. Safari hii alikamua bila kukosea hadi Bibi Gululi nikamuona anafurahi na kumpongeza.
Gululi akafurahi mno. Na mimi nikapewa nafasi nikiwa nimekalia Gululi kwa juu, nikaanza kufanya kama wenzangu, nikawa najisahau hadi nikawa nalalamika kizungu “ooh shit, fuck me baby!” haraka bibi Gululi akanisahihisha akaniambia nisithubutu kulalama kwa kingereza na kunitaka nitumie kiswahili au kilugha changu.
Basi nikafanya hivyo hata mimi wakanisifia mno, tukawa sasa tumekaa chini Bibi Gululi akaanza kutupa mizungu na umuhimu wa viuno.
“Wanamwali wangu, kiuno ni sehemu muhimu ya ladha na utamu wa mwanamke, msuguano unaotokea wakati unapokatikia mashine ya mwanaume unapokuwa unaisugua pipi yake kila upande ndiyo unatengeneza moto wa utamu. Kwa kiuno pekee unaweza kumfanya mwanaume hata kama umefanya naye mapenzi siku moja tu, akakuwaza siku zote za maisha yake.
“We unadhani, kwa nini wanawake wa pwani waliwateka wanaume wa bara miaka ya sabini, kiuno tu wanamwali wangu!
“Nilichowafundisha leo, inabidi mkifanyie mazoezi kila siku za maisha yenu na kwa kila mkao, hata ukija kuwa mtu mzima, mnene, hakikisha kiuno chako kinabakia kuwa laini vilevile kama msichana. Usije kamwe ukakaa tu kama gogo kitandani hata kama umechoka, bora umnyime mumeo kuliko ukampa halafu usimzungushie nyonga.
“Wanaume ni wajinga sana kwa hivyo vitu vidogovidogo tu, tena nimesikia wanaume wajanja kwa kuangalia tu mwanamke anavyotembea, wanajua yupi anaweza kuzungusha nyonga na yupi hawezi,” alisema Bi. Gululi.
NILIPOISHIA
NYOO NIPE MUMEO 52
Hapo nikaanza kuvuta picha ya Fatuma anavyotembea tena vile alivyo mwembamba unaona tu hata hatikisiki mwili mzima, shingo anairefusha halafu, unaona tu kiuno kinashuka na kupanda kadri unavyopiga hatua. Siyo kama mamisi wanavyotembea hapana wale wamezidi mikogo na wanakanyaga ardhi kwa nguvu.
Nikajaribu kumuangalia hata bibi Gululi alikuwa hivyohivyo, Gululi naye, nikajiangalia na mimi nikahisi na mimi nipo hivyo. Nikamkumbuka Hadija ambaye akitembea nyumba ya saba wanasikia anavyokwatua hatua zake. Yaani ukitembea naye anakokota vumbi kiasi kwamba akifika kwa wenyeji lazima anawe miguu au kufuta viatu, yaani mtu anatembea na mwili mzima unayumba.
Bi. Gululi alikuwa sahihi hadi akina shoga yangu Getrude na Cathe walikuwa wakitembea kama Hadija tu; wanaburuza miguu. Mh ina maana walikuwa hawajui kukatika kweli! Nikaona ngoja niliwekee kiporo jambo hilo.
Tulimaliza na bibi Gululi akatuambia kesho atatufundisha jinsi ya kurudisha utamu ndani ya kipapatio kilicholegea baada ya kuzaa, hapo ndiyo nilipokuwa napataka. Nikafurahi mno. nikaombea kesho ifike mapema sana.
Basi baada ya kungwi kuondoka, tuliongea mengi na Gululi, tena tukaanza kurudia yale mazoezi ya kukatika kiuno kama alivyotufundisha bibi Gululi, saa nyingine mimi ndiyo nikijifanya mwanaume nikimkunja Gululi kwenye kila staili na yeye alihakikisha nyonga yake inanyongeka mulemule.
Na mimi akanifanyia hivyohivyo, huwezi amini tukajikuta tunafika jioni tukiwa hata kula tumesahau.Yaani hapo ni kama vile makomando wakike wawili tulikuwa vitani kuwakomboa waume zetu, na hatukuwa tunafanya mchezo.
Basi ikawa ndiyo utaratibu wetu, yaani hadi nilipokuwa nikioga nilikuwa nikizungusha kiuno kukipa wepesi, nikiwa nimelala nilikuwa hivyohivyo yaani hadi kiliniuma lakini taratibu kiliachia na kujikuta nimekuwa mwepesi zaidi hadi nikitembea wowowo lilikuwa linatikisika lenyewe wakati nilikuwa sijifanyishi lakini nilishangaa nikipokea lawama kila nilipokuwa nikienda sokoni na Gululi.
Haya sasa ngoja nikurudishe kidogo ile siku ya pili ya mafunzo ya kukaza kipapatio.
Usikose kesho.
NYOO NIPE MUMEO 53
Siku hiyo kama kawaida ilipofika saa 5, Bi Gululi alituita chumbani, tukiwa tumekaa chini kwenye mkeka na yeye kwenye kigoda.
Akatutaka tuanze kujikumbusha mazoezi ya jana ambayo tuliyafanya vyema hadi mwenyewe akashangaa maendeleo yetu, yaani kama tungekuwa ndio wanafunzi wa chekechea nadhani tungerushwa darasa maana tuliiva mno.
Basi baada ya kuona tupo vizuri akatufunda kuhusu yale mafunzo ya kukaza kipapatio, maana kama unakumbuka alisema kuwa utamu wa mwanamke unatokana kwanza na usafi, muonekano mzuri wa kipapatio, sauti, na utundu wake kitandani. Hapo kwenye utundu wa kitandani ndipo kwenye hayo mambo ya viuno na ladha ya msuguano inayozidi kama mwanamke atakuwa mnato.
Tena alikuwa akizungumza taratibu akitaka tufahamu anachokiongelea vizuri, akatumbia kuwa mwanamke anaweza kuambiwa siyo mnato kutegemea pia na saizi ya mdyudyu wa mwanaume anayefanya naye mapenzi.
“unakuta mwanaume ana kibamia au kidudu chembamba hata akikuchomeka haujui kama kimeingia, halafu anaondoka na kuanza kukusema mtaani ooh Mary amelepweta! Kumbe kosa lake yeye.
“Sasa kama umeolewa na mtu mwenye kibamia kama huyo, hata usijiangaishe kukaza kipapatio mwali wangu umesikia! Yeye ndiyo akaongeze kishedede chake kwa sababu hakitoshi ati!
“Hapa nazungumza pale unapopwaya wakati mwanaume wako ana mshedede wa inchi 4.8 hadi 5, unene wa inchi 1 hadi 1.5, hapo ndiyo ujue kuwa bibi yangu uke wako umelegea, na haya mafunzo yana kuhusu, lakini hata nyinyi mliozaa hii inawahusu sana.
“hapa wengi wanaambiwa mara ooh wajikamulie ndimu,sijui waweke nini ndani ya kipapito, hapana usije ukajaribu hata kidogo kuingiza kitu ndani ya uke wako si sabuni wala makemikali ya siku hizi. Kuna madhara makubwa mno ukifanya hivyo na huko ndani siyo kwa kukuchezea.
NYOO NIPE MUMEO 54
“Dawa zote za kweli ambazo hukaza uke huwekwa nje kwenye mlango wa kipapatio tena kwa kufungwa na kitambaa cha cotton/pamba vizuri kama pedi na si kuingiza ndani, hapo nadhani tumeelewana,” alisema Bi. Gululi lakini wakati tukisubiri kwa hamu hayo maelekezo ghafla simu ya bi Gululi ikaita. Akapokea na kuonekana akiulizia mahali fulani, halafu akatuangalia na kukata simu.
“Hadija huyo anakuulizia Mary! Anasema anakutafuta na haupatikani, nimemwambia upo hapa siku ya pili leo.” Alisema Bibi Gululi.
“anasemaje! “ niliuliza.
“anasema na yeye anakuja, nadhani amejiona mjinga, sasa mimi sitarudia chochote zaidi nitaendelea kuwafundisha kama atataka maelekezo mengine mtamfundisha nyinyi. “Mimi yule nilimshindwa tangu akiwa mtoto, kiuno chake ni kigumu balaa, hadi tulikuwa tukimfungia kibwebwe na kukijaza mchanga ilimradi kiuno kilainike lakini bado alikuwa kama vile hajitumi.
“nilishangaa sana ulipokuja naye juzi, kwa kuwaona tu niliona wewe ndiyo mwenye shida na siyo yeye,” alisema Bi Gululi kisha akaendelea na mafunzo yake lakini kwa harakaharaka.
“Enhe haya kuna dawa na mafunzo ya kukaza huko kwenye utamu wa dunia, wanamwali wangu. Dawa ya kwanza ni asali mbichi. Hii unaipaka kwenye kitambaa vizuri halafu unakikunja na kukibana kwenye chupi kama vile pedi, usikitoe hadi ifikie nusu saa. Fanya hivyo kwa wiki mbili mfululizo utaona matokeo yake.
“Lakini pia kuna ile mboga ya mgagani, nayo inakuwa hivihivi, unaitwanga na kuiweka kwenye kitambaa unakivaa hivyohivyo. Hizi dawa zote zinasaidia mno na wengine kwa matokeo ya haraka zaidi wanachanganya kwa pamoja,” alisema Bi. Gululi nikatamani kuanza kuweka hizo dawa muda huohuo maana alikuwa nazo akaanza kutuonesha huo mgagani, na asali mbichi. Halafu akasema kuna funzo moja la kukaza uke atatuambia baadaye.
NYOO NIPE MUMEO 55
Uzuri naye alionekana kuwa na harakaharaka, akatuachia tuziandae hizo dawa, akatuambia kuwa akija Hadija tutamuonesha mazoezi ya jana na yote tuliyojifunza, yeye amepata safari mara moja.
Kama kawaida yake wakati mimi na Gululi tukiwa bize kuandaa madawa yetu ya kukaza kipapatio, Kungwi tulimuona akiingia zake bafuni kuoga muda mrefu kweli, akatoka na kuingia chumbani tukaanza kusikia harufu ya udi, akatoka akiwa amejipara kweli, halafu alionekana bize kweli akiongea na simu.
Basi wakati ameinama anavaa viatu blauzi yake ikapanda juu kidogo, nikaona kiunoni shanga za rangirangi lakini juu kulikuwa na shanga nyeupe.
Alipoondoka tu nikawa na maswali kweli kuhusu shanga maana nilikumbuka Steve alisema alimuona Fatuma amevaa. Ikabidi nimuulize Gululi akaniambia: “Shoga shanga ni kama kibwebwe ngomani, unajua ukiwa unakata kiuno ukiwa na kibwebwe unaonekana una katika sana, sasa kitandani ndiyo sisi tunavaa shanga, ukikatika kidogo tu mwanaume anaona kiuno feni.
“Tena wanaume wanavurugwa kweli wakiona shanga tu kiunoni. Kuna wanaume wajuzi wa kuchezea shanga, wanachezea kwa ulimi tu kuzunguka kiuno kizima, hadi raha,” alisema Gululi.
“sasa si bora kuvaa cheni, hayo mashanga nayaona kama yamekaa vibaya,” nilisema hisia zangu.
“mh wewe tu, lakini pamoja na hayo hizo shanga zina maana yake shoga, kila rangi ina maana yake, tofauti na cheni.
“mh we Gululi rangi za shanga zina maana gani?” niliuliza kwa mshangao. *Usikose kujua somo la shanga kutoka kwa mtoto wa kungwi kesho.
NYOO NIPE MUMEO 56
“Shoga kwa taarifa yako rangi za shanga zina maana na ujumbe kwa mtu unayemvalia, anaweza kuwa mume, mpenzi au kimada, hapa wanaume walioenda jando la pwani tu ndiyo wanaweza kujua.
“Ukimvalia mwanaume shanga za rangi fulani akiangalia tu kabla ya kukuvua chupi anapata maana kabla wakati hata hamjaanza kuhondomora,” alisema Gululi akiweka pozi kama vile bibi Gululi alivyokuwa akifundisha.
Akaanza na shanga za rangi nyekundu, akasema mwanamke anatakiwa kuvaa shanga za rangi nyekundu akiwa katika siku zake za hedhi, kwa hiyo hapa hata kama mwanaume ana hamu kiasi gani ajue kabisa atumie kinga au akubali kujichafua, au ndiyo asubiri hadi umalize siku zako.
Akasema kuwa kuna shanga nyeupe, mwanamke unatakiwa kuzivaa pale ambapo unakuwa huna tatizo lolote litakalokuzuia kumpa mwanaume wako raha na utamu, tena kwa shanga hizo inamaanisha yupo free kukuchezea atakavyo mwili wako wote na kwa kifupi shanga nyeupe inamaanisha wewe ni msafi. Akaniambia mwanaume unayemvalia shanga nyeupe inabidi uwe umemtunuku kweli kiasi kwamba hata yeye mwenyewe akiona anachanganyikiwa.
Akaniambia kuwa wengine wanaweza kuvaa cheni ya rangi ya gold kama mbadala wa shanga nyeupe.
Mh! basi wakati tunaendelea kuongea na kutengeneza dawa zetu, Hadija akiingia ndani, akajichekeshachekesha, ikabidi maongezi yetu tuyakatize bado maana kiukweli Gululi alikuwa amenifungua macho mno he! kumbe shanga ndiyo zilivyo? Na hapo bado hajazimaliza zote. “Mh mashoga zangu mie, vipi Kungwi yupo wapi?” alianza kujichekeshachekesha Hadija.
“ameondoka sasa hivi, amesema tukufundishe alichotufundisha jana,”
“mh! Haya na hizo ni nini?”
“asali na mgagani,” nilijibu.
“Mh niambie mke wa Mmarekani nakuona hapo!” alisema Hadija nikamkata kijicho na kuona aliongea kwa dhihaka fulani hivi.
Labda alinidhihaki kwa kuwa nimeibiwa mume na Fatuma, au kwa vile najituma kwa mafunzo ya kungwi! Bado sikumpatia picha maana dhihaka kubwa ilikuwa kwenye neno “mke wa Mmarekani.’
NYOO NIPE MUMEO 57
Nikageuka na kumtazama Gululi tukamaliza kufunga dawa zetu vizuri kwenye vitambaa na kuzihifadhi vizuri maana tulipanga kuzivaa mara baada ya kuoga.
“Enhe nasikia bi wewe ndiyo umehamia kabisa hapa!” aliendelea kuninanga Hadija.
“ndiyo nimeweka kambi, kwani kuna ubaya?” nilijibu na kuuliza nikaona amejishtukia fulani hivi kwa kuwa nimejibu mapigo; “vipi na wewe umepata mtu wa kumwacha dukani leo?”
“ndiyo shoga aisee nimeona napitwa, Aku na mie nimeibiwa mume wangu baba Abduli nataka arudi,” alisema lakini muda huo wote alikuwa bize na simu. Nikaona anahangaika kusoma kitu.
“Eti Mary samahani mtu akiandika hivi (akachora hewani) ina maanisha nini?” alisema Hadija.
Nilichokiona alikuwa ameandika neno ‘cute’ linalomaanisha ‘mzuri’ lakini kabla sijamtajia maana yake nikajifanya namchimba.
Kabla ya neno hilo kuna neno gani?
Akachora chini huku akitazama kwenye simu yake neno zima likawa ‘you are not that cute’ maana yake ‘hauna uzuri huo’.
Nikawaza kama meseji hiyo atakuwa ametumiwa na mtu na mimi nikamtafsiria hivyohivyo, lazima atajisikia vibaya. Uzuri wake alikuwa hajui kingereza kiasi hicho kwa hiyo nikaona ngoja nimpoze kidogo.
“imeandikwa wewe ni mzuri lakini uzuri wako umejificha,” nilipomwambia hivyo nikaona anafurahi na kuendelea kuchati.
Nikawa najiuliza anachati na nani kwa furaha kiasi hicho, huwezi amini nikajisikia wivu nikamkumbuka mume wangu mr X na mwanangu, nikakumbuka mapenzi yetu enzi hizo kabla ya kidudu mtu kuyaingilia.
Unajua vile unampenda mtu hadi unachanganyikiwa, ndiyo mapenzi yetu yalivyokuwa na Mr X nilikuwa tayari kufanya chochote kwa ajili yake na yeye alikuwa kama mimi, moyo wangu kila mara ulikuwa unashtuka nikimuona japo kuwa tulikuwa pamoja. Akiongea sauti yake tu nilikuwa nikisisimka, akinigusa mwenzenu chupi yangu ilikuwa inaloa, akinibusu ndiyo naota hadi vile vijipele vya baridi. nikawaza mapenzi hayo sasa hivi yako wapi maana nimemisi kumpenda tena Mr X wangu kiasi hicho.
NYOO NIPE MUMEO 58
Basi kila nilipokuwa nikifikiria kuhusu mr X, picha ya Fatuma ilikuwa ikinijia nikakasirika mno lakini sikuwa na cha kufanya zaidi ya kuwa mpole nikipanga mashambulizi.
Baadaye tulimfundisha Hadija jinsi ya kukata viuno lakini alikuwa mzito kweli yaani kama Bibi Gululi alivyosema, maana alikuwa akitikisa matako tu na kukata tumbo, lakini siyo nyonga. Ikabidi tumuwekee kibwebwe tukakijaza na mchanga na kumshauri kuwa anafanya mazoezi hayo kila mara.
Lakini mwenzetu kuona vile, akahisi tunamdharau, akakasirika na kuacha, akaenda kuoga zake na kuingia chumbani kuvaa nguo. Mimi nilikuwa sina hayo mambo ya kubembelezana kwa sababu nilijua nini nilichokifuata hapo, kwa hiyo nikamuacha Gululi eti akienda chumbani kumbembeleza.
Mimi nilipokaa pale nje nikakichukua kile kibwebwe alichokitupa Hadija kikiwa na uzito uleule wa mchanga nikakivaa, nikaanza kujaribu kuzungusha kiuno changu taratibu basi nikajaribu staili za mtetemesho za Hadija halafu nikapiga magoti na kukaa kitako chini kabisa nikawa najaribu kufanya mazoezi ya kuinua tako moja juu na jingine chini nikajaribu kukaza moja nikaona linainuka yaani kama vile unakonyeza jicho, Ha! nilikuwa sijui kama najua nikaanza kujibinua sarakasi hivi huku nikikatika kama vile Steve alivyosemaga kuhusu Fatuma. Nikaona ni ngumu kwa sababu sijazoea. Nikajaribu kuinama na kuendelea kukatika kwa staili ya chumba mboga. Nikapandisha mguu mmoja juu ya meza dirishani na kuanza kukatika kama vile nakatikia dyudyu.
Nikawa najiangalia huku nikifurahi maana kiuno kilikuwa kilaini mno. Huwezi amini kumbe Hadija na Gululi walikuwa wamesimama mlangoni wameduwaa wakiniangalia tu jinsi ninavyoneng’emula. Lakini cha kushangaza Hadija alionekana kuchukia eti.
Nilipowaona nikaacha mara moja na kuvua kile kibwebwe nikaenda zangu kuoga. Niliporudi sikumuona Hadija,nikaingia chumbani na kuchukua kitambaa changu nilichofunga ule mgagani niliochanganya na asali na kukibana kwenye chupi.
NYOO NIPE MUMEO 59
Nikakumbuka simu yangu, nikawasha kwa mara ya kwanza tangu juzi nilipoondoka nyumbani. Nikashangaa meseji zaidi ya ishirini zinaingia kwa mpigo. Zote zilikuwa za mume wangu. Dakika hiyohiyo ni kama vile mume wangu alikuwa na simu mkononi akishuhudia meseji zilivyokuwa zimedeliver, simu yake ilikuwa ikiingia.
Nikakata. Na kuweka flight mode ili nisipatikane. Nikaanza sasa kusoma meseji moja baada ya nyingine. zote zilikuwa ni za kunibembeleza nirudi ili tuyamalize.
Kuna moja akaandika kuwa angalau tu nimwambie kuwa nipo salama. Meseji ya mwisho, ndiyo iliniyoshtua kuliko zote. Ilisema hivi:
“I now know where you are, yesterday I was with your friend Hadija, she keeps telling me about u, Im glad to know that you’re ok, she is wierdo though. Love u wife, Kendrick loves u too, come back home,” (sasa najua ulipo, jana nilikuwa na rafiki yako Hadija, yeye ndiyo hunieleza kuhusu wewe, nafurahi kujua ni mzima. Simwelewielewi lakini. Nakupenda mke wangu, Kendrick pia anakupenda. Rudi nyumbani)
Mwisho wa meseji, nikawa najiuliza Hadija alionanaje na mume wangu, ina maana alienda nyumbani kwetu jana. Kwa nini afanye hivyo? Na kwanini hajaniambia leo alipofika tu.
Lakini pia kauli ya mume wangu kuwa hamwelewielewi Hadija ilinishangaza, hamwelewielewi kivipi? Maana ninavyomjuaga Mr X wangu japo unaweza kuona ni mjanja lakini tangu nilipokuwa naye akitongozwaga tu na watu ninao wajua huwa ananiambiaga; rafiki yako fulani simuelewi.
Ina maana Hadija amejitongozesha kwa mume wangu au?Ili kujua nikatoa ile flight mode na kumpigia simu mume wangu maana ili kuwa too much. Mara Fatuma mara Hadija hapana, kwa ni wanaume wengine hawawaoni au kisa Mmarekani.
Itaendelea..
NYOO NIPE MUMEO 60
“Hallow!” niliongea baada ya kuona simu imepokelewa haraka kuliko nilivyotarajia.
“oh wife I miss u so much, are u ok?” aliongea mume wangu
“skip that, Hadija amefanya nini?” nilihoji kwa hasira.
“ameniambia kuhusu ulipo na unachokifanya huko, ndiyo maana moyo wangu kidogo umepoa, lakini bado sijajua hasa sababu ya wewe kutotaka kabisa kuongea na mimi,” aliongea mume wangu kwa upole kama kawaida yake.
“nataka kujua Hadija amekufanyia nini? mbona unazunguka!”
“Ok, amekuwa akianza kuwasiliana na mimi kwenye simu, akiniambia ananipenda and stuffs like that, but I’m not into her, so nikamwambia plainly kwamba hafanani na wewe mke wangu, lakini nahisi ni stucker maana ananiganda, chaa!” aliongea mr X wangu na kwa hiyo Chaa! Nilijua tu anataka kunichekesha lakini nikajizuia nisioneshe hisia yoyote.
“ok nilitaka kujua hayo tu, naweza kuongea na Kendrick!” nilisema moyo wangu ukilainika kiukweli japo kuwa nilijifanya kiburi, bado niliwamiss wapendwa wangu, na hasa mwanangu kendrick.
Nilikuwa na wasiwasi kila siku lakini nilijipa moyo kwamba wiki ikiisha tu nitarudi na sasa ndiyo kwanza siku mbili lakini kuwamiss kwake kulikuwa zaidi ya mwezi.
“Da da daaaa….” Nilisikia sauti ya mwanangu, chozi likanitoka, kimoyomoyo nikanung’unika nikimuomba msamaha mwanangu kwa kuwa mbali naye tena niliapia kuwa lazima nirudi kwa sababu ninapigania penzi langu ili baba yake asiniache kwa ajili ya mwanamke mwingine.
“umemsikia! Anasema amekumiss sana,” alisema mume wangu kwa furaha. Sikutaka anisikie nikilia hivyo nikakata simu haraka. Dakika hiyohiyo ikaingia meseji kutoka kwake ikisema: “plz wife, I beg you don’t switch off your cell (tafadhali mke wangu nakuomba usizime simu yako).” Alisema Mr X wangu nikaamua ngoja tu nisiizime.
Baadaye nikaanza kutafakari vizuri maneno ya mume wangu, ni wazi alikuwa akinielezaga watu wanaomtaka na hata mimi pia nilikuwa nikimueleza, ni uamuzi tuliojipangia kwenye maisha yetu, yaani hatukuwa na usiri wowote.
Na hapo alikuwa ameniambia kuhusu Hadija, lakini bado nilikuwa na mashaka, mbona hakuniambia kuhusu Fatuma?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment