Search This Blog

Wednesday, January 25, 2023

HANITHI MPEVU - 4

   

Chombezo : Hanithi Mpevu

Sehemu Ya Nne (4)



“nani anayetaka kwenda kwa Kuruthumu?!” aliuliza kwa hamaki Bi Ummy. Basi wakina Renee na wenzake akina Mercey na Samrath wakajitia kuinama chini wasiseme chochote maana Mwajabu aliwaumbua kwa mpango wao.

“na we dada Renee si useme, kwani unaogopa nini sasa!” alisema Fetty.

“Renee ndiyo unataka kwenda huko?” aliuliza Bi,Ummy sura yake ikioneshwa kuvunjwa moyo na mwanafunzi aliyempenda mno darasani humo.

“hapana Bi.Ummy sio kwa maana hiyo, kweli umetufundisha vyema kabisa lakini kusema kweli wengine bado tuna shauku ya mambo haya, tunataka tujue vitu vingine zaidi, sielewi kwanini tusiwe huru kwenda kujifunza tunapotaka!” alisema Renee akizungumza kwa niaba ya wenzake.

“siwezi kuwazuia, lakini..ila kuweni makini,” alisema Bi.Ummy, akawa tayari kwa kutoka nje aondoke zake haraka.

“samahani eti Bi, Ummy, hivi ni kweli, Kuruthumu alikuibiaga mumeo pamoja na elimu yote ya ukungwi uliyonayo!?” aliropoka Fetty. Bi, Ummy aliyekuwa anaukaribia mlango akashindwa kupiga hatua zaidi. Akageuka nyuma kwa ghadhabu, macho yakawa mekundu mno. Lakini akavuta pumzi na kuzishusha kutafuta amani ya moyo kwanza kisha bila kusema jambo akaondoka zake moja kwa moja.

“weee, Fetty, unayoyasema ni kweli!?” aliuliza Mercey na wenzake.



“ndiyo, Kuruthumu mwenyewe alituambia, ndio maana Bi.Ummy anamchukia, sasa ndiyo uone kati ya Bi.Ummy na Kuruthumu nani anajua zaidi,” alisema Mwajabu.

“mh, kama ndiyo hivyo basi huyo Kuruthumu ni noma,” kila mmoja alisema hivyo. “sawa, tutamuita, namba si tunayo! Cha msingi sasa tufanyeni kama mapumziko tukutane mwezi ujao maana wengine mambo yetu yamesimama,” alisema Samira.

Basi darasa likavunjwa asubuhi ile, Renee akaagana na akina Fetty na Mwajabu akiwataka wasimwambie mama yao kama yeye na wenzake wana mpango wa kumuita Kuruthumu.

“sawa, dada Renee,” waliitikia kwa adabu Fetty na Mwajabu, Renee akawaacha zake huyoo akaenda zake mjini kuchenji hela zake na kuzitia kwenye simu, Loh ilikuwa ni milioni tano na laki nane.

Akawaza sasa afanye nini?

Akafanya kuwapigia ndugu zake, akapokea lawama zao, akatukanwa na Martin akashutumiwa na kila mtu aliyejaribu kumtafuta kwenye simu. Akaona hata hivyo anastahili mitusi na maneno ya ukali, lakini angalau alikuwa akijua kuwa nduguze wapo salama.

Alimaliza kuzunguka jiji zima, akanunua nguo na vipodozi mbalimbali, lakini bado alikuwa na muda mwingi hakujua afanye nini? Akatafakari ana mwezi mzima hadi kumsubiri huyo Kungwi wa Tanga, ulikuwa ni muda mrefu, basi kwa kipindi hiki atafanya nini? Biashara ?atafute kazi? au arudi kijijini kwao kuomba radhi!? aliwaza Renee, lakini hayo ni mambo ya muda mrefu kidogo, kwa sasa je, kwanini asimtafute Hermez!

Alishtuka Renee kwa wazo hilo.

Akaona ngoja ajaribu kwenda mitaa ileile ya ghetto lake, akamuulizie na kumuona kama yupo kweli hai, ili mradi amdadisi tu.

Basi akavaa nguo zake akapanda pikipiki hadi Kimara Temboni, mitaa ileile ambayo alikuwa hausigelo enzi hizo. Akajitia mtandio kichwani asigundulike kwa haraka.

Akapita uchochoro na kichochoro, akaiona nyumba ile alimopanga Hermez lakini hapo nje umati ulijaa watu wakishangilia na visimu mkononi, wakiwarekodi wanawake wawili wakipigana mmoja uchi, mwingine na kijora. Wanapigana hatari.

“Hermez ni wangu, wewe ni Malaya tu, utanitambua!” alisema mwanamke mmoja akimtimba mwenzake ilikuwa shari kamili, yaani kama kafa shoga..



“Jamani wanampigania mwanaume, wanajidhalilisha jamani, dah!” alisema mdada Fulani akiwa amesimama karibu kabisa na Renee.

“mh hata kama mimi, Hermez angekuwa bwana angu ningempiga mtu, kuibiwa mwanaume kama Hermez inauma!” alisema mdada mwingine.

“mi nashangaa mnavyomsifia huyo Hermez, mnampa sifa tu za bure, kha! Hamjielewi nyie,” alijibu yule mdada wa mwanzoni.

“heee, pole yako usiyejua utamu wa muwa wa bungala, kamuonje uje hapa kama na wewe hujajiunga kupigana, nyoo!”

“kwahiyo wewe nawe ulishapitiwa?!” “ndiyo, na niliamua tu kumuacha mwenyewe maana umalaya kazidi,”

“loh hata kama uliachwa utasema weewe!” alisema mdada mwingine, Renee kwa kifupi akajua hapo anayezungumziwa ni Hermez yuleyule aliyemfahamu lakini alishindwa kuzuia kustaajabu kwake maana misifa aliyosikia hapo kuhusu Hermez ilimshangaza na hakutegemea eti yule Hermez wakubusti na midawa ya nguvu za kiume nusura imuue leo hii kugeuka muwa wa bungala hadi agombewe na wengine wamuongelee! Kweli!?

“mh labda siyo yeye,” alijilazimisha kukataa ukweli Renee. Akaona cha kufanya ni kuwauliza maswali machache hao wadada ili aelewe kinachoendelea vizuri maana alihisi alihitaji ufafanuzi wa kutosha mno kuhusu Hermez anayemjua yeye na huyo aliyetajwa hapo.

“samahanini kwani Hermez mnayemuongelea mwenyewe yupo wapi?” aliuliza Renee.

“nimemuona anakimbilia kwa rafiki yake, chumba kile pale pembeni,” alisema mdada yule roporopo.

“mh, ni mrefu hivi mwembamba si ndiyo?” alisema Renee akijitia kuuliza kama mbea tu wa kawaida.

“ndiyo,” alijibiwa, basi yeye akatoka huko na kwenda kwenye kiglosari cha karibu akiwa ametulia kusubiri vanga lipungue na kigiza kianze ndipo arudi hapo kungongea Hermez maana bado alikuwa na kiushungi na hakutaka kugundulika na watu wanaomjua.

Akaagiza soda na kunywa taratibu, uzuri jua lilikuwa limeshaanza kuzama na ghasia ziliondoka kabisa. Akaona ni muda mzuri kwenda kwenye ghetto la Hermez sasa, Akasimama taratibu na kutembea, kichwani mwake akiwa na fikra mpya kabisa kuhusu mwanaume huyo maana kwa aliyoyasikia yalimsisimua kwa kweli, akahisi anaweza kufanya kitu na Hermez.




Pengine kuendelea kumfanya shamba darasa kama alivyomfanya kipindi kile, huenda sasa hivi alikuwa si hanithi mpevu tena bali ni kazikazi.

“hodii!” alibisha hodi Renee, lakini cha kushangaza mlango wa chumba cha jirani ndiyo ulifunguliwa na mtu akafanya kama vile anachungulia na kurudisha mlango tena.

“jamani huyu mwenye chumba hiki yupo?” aliuliza Renee kwenye kile chumba kilichokaa kishilawadu.

“unasemaje?” alijibu huyo mtu wa humo ndani kiuoga, lakini hakuonesha sura yake hata kidogo. Renee akashtushwa na sauti ile aliitambua mara moja kuwa ni ya Hermez.

“Hermez!” alisema Renee kwa mshangao.

“ndiyo, AKA sukari ya warembo, we nani?” alijibu Hermez akiwa bado kajificha.

“we Hermez mimi hunijui?”

“sikujui sista, sikia nimeshasababisha msala hapa, mademu wamegongana, sasa kama na wewe unataka huduma, leo sipo, njoo kesho,”

“hahaa we Hermez siku hizi unajiuza au!?” alisema kwa mshangao Renee. Hermez huko chumba cha jirani akakaa kimya akafungua mlango na kutoka akiwa na kitaulo ili amtazame msichana huyo aliyezungumza kama vile anamjua sana.

“wee ni nani?” aliuliza Hermez, Renee akahisi huenda shungi lake lilimchanganya Hermez akavua ushungi na kumtazama vizuri uso kwa uso.

“mh, mbona sikujui!” alisema Hermez akimtazama kwa karibu Renee.

“we Hermez, hebu acha mambo yako, twende ndani kwanza,” alisema Renee akidhania anafanyiwa mzaha.

“kweli sikujui, we nani?”

“we mimi ni Renee bwana,” “weeee, weeee, Renee!?” alishangaa Hermez akapiga kelele kulitaja jina lake, Renee akaogopa akahisi anataka kukamatwa au?

“wee umekuwa mzuri hivyo, hebu nikutazame vizuri,” alisema Hermez akizunguka kumtazama Renee upande upande.

“weee njoo ndani, duh! Karibu, kwanza nisamehe kwa maneno yangu,” alisema Hermez akifungu mlango wa chumba chake na kutazama nje kama anaangalia msala.

Loh kitandani mapakiti ya kondomu, khanga, vichupi, mafuta ya karafuu, vitambaa, tishu, CD za ngono, na kama haitoshi kijitabu kile cha kwanza cha Mary alichokinukuu kilikuwa pale kitandani kimefunguliwa chanuu, doh!




Renee akaachana kutazama hivyo vitendea kazi vya kunjunjana na macho yake yakikitazama kile kijidaftari chake. Hermez kwa wakati huo alikuwa akipaparika kufichaficha vitu kadhaa na kurudisha chumba chake salama ili Renee aliyempendaga asiruke na kuondoka zake. “samahani, Renee, umekuja ghafla ndio maana, nisamehe kwa ulivyopakuta humu ndani..” alisema Hermez, akionekana amebadilika hata kuongea, aliongea kikubwa na sauti yake ilijaa bezi la kiume tofauti na enzi zile alipoongea kama kavulana kasichojiamini, hadi akawa anakakoromea.

“wala usijali, nasikia umekuwa kidindadinda cha mtaa?” alisema kwa kebehi Renee, akizuga kujisahaulisha kuhusu kile kijidaftari chake kwanza.

“unanipa sifa au unanipa kichambo?” aliuliza Hermez. Akiendelea na kupangapanga vitu vyake sawa. Akalikung’uta shuka lake lilelile chafu akilichomekea tena.

“hivi, Renee, ulikuwa wapi?” alisema Hermez sasa akiketi kitandani kwake akimtazama Renee asimmalize.

“sikia Hermez, twende sehemu, hapa sikai kwa kweli nasikia harufu ya papa tu yanikera,” alisema Renee. Hermez akavaa shati jingine na kulipulizia tu pafyumu.

“sikia nimejizuia kuongea lakini naomba uje na kitabu changu hicho,” alisema Renee akipointi kile kijidaftari chake alichokiona kitandani, na aliona vyema tu Hermez akikizonga na nguo zake kukitumbukiza kwenye jalo la nguo chafu.

“kipi?” aliuliza Hermez.

“si hicho chenye kava la bluu,” alisema Renee akionesha na kidole kabisa. Hermez akashtuka.

“wee kwani ni chako?”

“ndiyo, nilikiacha nilivyoondokaga hapa,” alisema Renee akishindwa kuendelea mbele maana alifahamu siku ile alivyoondoka na alivyomuacha Hermez katika hali ya kifo.

“samahani Hermez, naomba tukaongelee vyote hotelini, sitaki tuongee hapa pananikumbusha mengi,” alisema Renee, uchungu ukimshika kifuani.

“ooh poa, twende,” alisema Hermez na kuvaa viatu vyake wote wakaambatana kuondoka pamoja.

Wakatoka nje na kupanda bajaji watu mtaani wakishangilia:

“wooyooo Hermez noma, kaopoa mwingine, mamaee, leo anakula mademu watatu kwa siku moja!” Loh Hermez akaona aibu, Renee akastaajabu lakini akayaweka kifuani pake. “enhee niambie umetaka kuniambia kitu gani kwanza?” alisema Hermez akiwa kaingizwa chumbani kabisa




“aaaar nimesikia sifa zako, na ninataka nione huo utamu wako,” alisema Renee jicho kaliangusha maana naye muda mrefu hakuwahi kujiachia na mwanaume kwa ukaribu huo na aligundua kabisa kuwa Hermez alipagawishwa na muonekano wake mpya, ukiachana na enzi zile za uhausigelo.

“hahaa, Renee mimi sio hanithi mpevu tena, ni mashine, gusa unase, usije ning’ang’ania wewe tu hapa,” alisema Hermez kwa kujiamini.

“hahaa, haunywi tena busta?”

“ule utoto, sasa hivi ni fayaa..” alijisifia Hermez.

“njoo utoe shombo kwanza, usiongee mengi,” alisema Renee,wakakokotana mtuye wakaenda kuogeshana huko, wakaletana kitandani.

Renee akijiamini kaiva huko alipokuwa na Hermez akijiamini kaiva huko alipokuwaga, sijui wapi?

Loh ikawa pokeza ni kupokeze, panda nikupande, beba nikubebe. Renee akakunika, Hermez akashangaa mambo mapya ya Renee akazidi kudata maana alisikia harufu ya udi, akanyonyewa mkubinduli wake kwa vikuba, akavurugwa na harufu za asumini na mpacholi.

Akastaajabu kula tunda huku akilishwa komamanga na tende.

Renee naye alipewa vitu hadi akashangaa. Katikati ya susu akauliza kwa sauti ya mahaba: “Hermez, umejifunzia wapi?”

Hermez akajibu: “ kile kidaftari chako, dia, kile kidaftari chako, na wewe wapi mambo haya?”

“Zanzibar hermezi, Zanzibar..” alijibu Renee kwa sauti ya nane, Hermez akikuna nazi kwa mbuzi lake tena beberu hadi tui likawamwagika wakalala chali hoihoi.

“Hermez duh masaa manne?!” alisema Renee.

“kawaida! so vipi umeona hanithi mpevu au?”

“mh hapana kwa kweli, wacha wanawake wakugombanie..”

“sitaki wanigombanie, nakutaka wewe tu, ukiwa na mimi unanitosha,” alisema Hermez akimchezea nywele Renee.

“mh, mimi bado kwanza nina mambo mengi, halafu naomba kwanza unisamehe, nililazimika kukukimbia Hermez, nilijua umekufa..” alifukua makaburi Renee na kuanza kujiliza. “najua utakua uliogopa sana, pole yote ni ujinga wangu, nilitumia madawa ya kuongeza nguvu za kiume ambayo hayatakiwi kwa uzito wangu, nashukuru siku ile jirani yangu alikuja na kuniwahisha hospitali, nashukuru nimepona.. nilikuwa nakutafuta sana Renee, nikutoe wasiwasi lakini haukuwa unapatikana,” alisema Hermez.




“yaani niliposikia upo hai nilimshukuru sana Mungu, hujui tu,” alisema Renee.

“usiwaze hayo tena bwana, kuwa na amani,” alisema Hermez akianza kumbusubusu tena Renee ishara kuwa anataka tena.

Doh Renee akastaajabu uwezo wa Hermez akakumbuka kuwa kile kijidaftari kina sehemu kimeandikwa na Mr X, ile topic ya Mr X and how to become one. Hakujua maana ya maneno yale lakini huenda kulikuwa na mambo humo kuhusu wanaume ambayo yamemtengeneza Hermez. Aliwaza Renee akapindwapindwa na kugeuzwageuzwa na kuchambuliwa na kupepetwa na mtu asiyechoka.

Basi asubuhi ilipofika Renee na Hermez wakaachana kwa miadi ya kukutana siku hiyo usiku kama dawa. Renee akaenda mjini kuzunguka huko na huku ili apate wazo la biashara ya kufanya. Akaona jambo pekee pengine ni kufungua biashara ya mitandao ya simu, yaani Tigopesa, Mpesa, Airtel money na HaloPesa. Akarudi na wazo hilo hotelini na kujiandaa kwenda kupanga pia.

Usiku kama kawaida, wakanjunjana na Hermez, na Hermez akatokea kumpenda haswa Renee. Lakini katu Renee hakuwa kabisa kwa Hermez alikuwa akimfanya uwanja wa mazoezi kama kawaida yake.


Sasa kumbe wale wote waliofundwa na BI Ummy walijiunga kwenye grupu lao la Whatsapp. Huko ndiyo wengine wale walioolewa wakaelezeana jinsi walivyosifiwa na waume zao walivyorudi na kuyatekeleza mafunzo ya Bi Ummy.

Wale ambao pia wanawachumba na wapenzi sugu, nao hali kadhalika walikuwa wakitoa majibu mazuri mno. “shoga mimi si kwa mafunzo yale, nikisifiwa tu na mume wangu basi namtumia Bi Ummy hela ya soda tu, yaani vitu unaweza kudhania vidogo lakini vikubwa mno.” Aliandika Rose mdada Fulani hivi akimtag Samrath.

“sasa ule mpango wa Kuruthumu vipi au mnazingua?” aliandika Mercey baada ya kuona kila mtu kawa wa kumsifu Bi Ummy tu.

“tumletee..” alicomment Renee, lakini akajikuta peke yake.

Wengine wote wakadai wapo bize na visingizio kibao. Wakabakia Mercey na Renee peke yao.

“loh, mimi na Renee, tutamuita Kuruthumu, na msituulizeulize hapa tulichojifunza,” aliandika Mercey.

“nyie nendeni, hiyo kuwauliza inahu..!” alicommenti Rose. Samira akacheka.



“na wewe usijifanye unaandika kwa kebehi, we si uliibiwa mume ndiyo ukaja unyagoni, sasa hiyo kumpelekea vimahaba vya siku mbili vya Bi Ummy ndiyo unaona umemtuliza mwenyewe.. ngoja ulizwe tena mshenzi weee!” alisema Mercey akituma voicenote maana maneno aliona yatachelewa.

“He! Jamani mbona matusi tena.” Aliandika Samrath.

“Mercey haujiheshimu, ndiyo maana umekaa kichanguchangu na kusema za ukweli ndiyo maana mnataka kwenda huko kwa Bi kuruthumu mkafunzwe uchangudoa hamna lolote, oleweni mtulie na ndoa zenu, umalaya tu..” aliandika Rose kujibu mapigo.

Wote watuma viemoji vya vimtu vimeziba macho na mdomo.

“we Rose, siku nikija kukuibia bwana ako nadhani ndiyo utanipa heshima mshenzi weee, ngoja.. na grupu lenyewe nalivunja,”alisema Mercey maana ndiyo Admin basi grupu likavunjwa na kuchati ikawa basi tena.

Renee sasa akajiuliza mwenyewe kama alikuwa na haja ya Kuruthumu. Akawa na kusita kwa moyo lakini kidogo simu ya Mercey iliingia.

“sikia mdogo wangu, kesho nampigia Kuruthumu, tutahudhuria hata kama sisi wawili tu, au siyo?”

“sawa,” alijibu Renee akifanya kusapoti tu.

Basi wiki ikapita, Renee akahamia uswazi, akafungua biashara yake ya uwakala wa simu, majuma yakapita, siku ya siku Mercey akampigia simu Renee kumwambia Kuruthumu kashafika tena camp la unyago alilidhamini mwenyewe, yaani kwa maana kwamba Mercey alimkaribisha Kuruthumu awafunde unyago kwake kabisa nyumbani.

Loh, ikambidi Renee kipindi kile afunge duka lake jipya na kwenda huko kwa Mercey na kibegi chake akiwa na shauku ya kungwi aliyeiba mume wa kungwi mwenzake.

Akakaribishwa kwenye nyumba nzuri ya kupanga ambapo upande mmoja mzima, aliuchukua Mercey. Alikuwa na fenicha nzuri na televisheni kubwa. Alikuwa kajipanga kwa kweli. Renee akashangaa kuona humo Mercey alikuwa haishi na mwanaume, na ana gari yake ndogo pia.

“karibu..” alisema Mercey.

“mh huyo kuruthumu yupo wapi?” aliuliza Renee kwa hamu.

Doh kakaja kamama kana sura mbaya kwa kweli, ila kamedamshi macho juujuu kama nini, halafu kamevaa gauni la bei mbaya, nywele ya bei mbaya Loh.. ndio Kuruthumu huyo!!?



“mambo we mdada! eti Mercey hapa kuna hata kasichana nijibusti maana najisikia kichwa chanigonga kweli!?” aliongea huyo Kuruthumu harakaharaka kama kafungwa mashine ya kushona mdomoni maana hata Renee hakuweza kujibu salamu yake akajikuta kashaachwa kwa maelezo.

“kasichana?” aliuliza Mercey.

“ndiyo kasichana.. agh konyagi ndogo bwana we wa wapi?!” alifafanua Kuruthumu. Renee akastaajabu maana aliona maajabu mwanamke kuulizia konyagi.

“mh, nina Henessy na St Anna, kama vipi ngoja nikakununulie,” alisema Mercey akitoka nje.

“enhee, we ndo mwali mwingine eeeh?” aliuliza Kuruthumu akimuongelesha Renee huku akimtazama vizurivizuri kuanzia juu hadi chini kama anamthaminisha hivi.

“ndiyo,” alijibu Renee, naye akimuibia kumtazama vizuri huyo kuruthumu maana ukiachilia makorombwezo ya bei aliyoyavaa, bado sikioni alijitoboa matundu hadi juu, tena kayatia maheleni ya kutosha tu. Halafu puani alikuwa na heleni nyingine. Kama haitoshi vidoleni mapetepete tu kama mke wa sonara.

Loh mguuni alikuwa na vikuku huku na huku, na kwenye kidole gumba cha mguu mmoja pia kulikuwa na pete. “unaitwa nani? maana mie ulishaambiwa naitwa kuruthumu?” aliuliza Kuruthumu. “naitwa Renee.” Alijibu Renee baada ya kugundua kumtazama sana Kuruthumu kunamfanya asomeke mapema kuwa anamshangaa, basi akawa anajibu huku anatazama pembeni angali amejivuta kukalia sofa.

“ayaa, hiyo hela yangu nipe kwanza hapahapa, nimtumie mwanangu, maana nilivyotokatoka allah anajua,” alisema kuruthumu , ikawa hata Renee asipumue akalifungua begi lake na kutoa laki moja kumpatia. “sikiliza si uniongezee na yakutolea mdogo wangu!”

Basi Renee akaongeza na elfu tano juu, akijionea vioja tupu.

Akalinganisha sasa aliyoambiwa kuhusu Kuruthumu na kuruthumu mwenyewe alivyo. Akapata shaka kama ni kweli alimuiba mume wa Bi Ummy aliyemzuri kama malaika na ujuzi wake, je huyu mwanamke na ubaya wake alikuwa na nini haswa cha ziada, Maana kuongea kama mzaramo, ustaarabu ziro, ulevi ndiyo usiseme maana hapo kashaagiza konyagi bapa eti ajibusti, sasa kujichaji kabisa si atamaliza kreti?

“aya Kuruthumu hii hapa, konyagi yako,” alisema Mercey akiingia pale sebuleni.



Doh kuruthumu mzoefu alionekana maana alianza kwa kuipigapiga kitako ile chupa, kisha akaifungua na kuitia kooni kama anakunywa maji. Akainamisha kichwa chini na kukiinua akashusha pumzi na kuwatazama wali wake kwanza.

“vipi tuanze?” aliuliza baada ya pafu la tano na kuweka chupa mezani ikiwa kavuu.

“mh, nilijua tutaanza baada ya kujipanga kwanza, au?” alisema Renee.

“kujipanga nini?” aliuliza kuruthumu akionekana kama amekasirika kidogo.

“weee, huyo akinywa tu hapohapo anadondosha mambo, wewe chukua daftari tu hapo, akimaliza tunalala hadi kesho hiyo.” Mercey alimnong’oneza Renee.

“hamna, Bi kuruthumu tuendelee,” alisema kwa adabu Renee, akitoa midaftari yake humo ndani na kuweka peni yake kwenye vidole sahihi vya kuandikia, namaanisha dole gumba na la shahada.

“sikiliza ninapoimba nyie mfanye kwa vitendo,” alisema Kuruthumu.

“mwali saula asogee shabani,saulaa, ooh ujitikise asimame bakari, saulaa.. inama mchungulie ndani saulaa,’ aliimba Bi Kuruthumu akishangaa si Mercey na Renee waliyefanya alivyoimba kwa vitendo,bali walimtazama macho wamekodoa kodo.

“nyie wasenge mnanitazama nini, si nimewaambia mfanye ninachoimba.. we Mercey nenda kaniletee hayo mapombe yako, kwanza mshanichefua, mnaandikaandika nini?!” alifoka Kuruthumu Mercey akatazama na Renee,. Loh ama kweli waliingia dambwe siyo.

Basi haraka Mercey akaenda kuchukua hizo pombe na kumletea Kuruthumu akatia tena St anna kwenye glasi na kuibugia, akainama na kuinua uso wake tena akisema tena maneno yaleyale aliyoyasema mwanzoni.

“sikiliza ninapoimba nyie mfanye kwa vitendo,” alisema Kuruthumu..

“mwali saula asogee shabani,saulaa,” basi haraka kila mmoja hakuwa na la kufanya wakahangaika kuvua manguo yao.

Mwali saula asogee shabani saulaa!” alirudia kuimba Kuruthumu hadi pale walipovua wote na kubakia watupu mingaka njeee!

“ooh ujitikise asimame bakari, saulaa..” alendelea Kuruthumu, Loh hapo ikabidi kila mtu ajitikise anavyojua yeye. Na Kuruthumu kama kapandwa mashetani akawa anapiga na makofi kabisa akifanya mziki wake unoge, loh Mercey na Renee wakajitikisa kila mtu anavyojua yeye.

“ooh inama mchungulie kwa chini saulaaa.” Aliendelea kuimba Bi Kuruthumu, wali wake wakainama kabisa



Mwali saula asogee shabani madobe, saulaa!” alirudia kuimba Kuruthumu hadi pale walipovua wote na kubakia watupu mingaka njeee!

“ooh ujitikise asimame bakari, saulaa..” aliendelea kuimba Kuruthumu, Loh hapo ikabidi kila mtu ajitikise anavyojua yeye. Na Kuruthumu kama kapandwa mashetani vile akawa anapiga na makofi kabisa akifanya mziki wake unoge, loh akina Renee walinyooka kwa kungwi asiye na masihala na mitusi yote yake.

“ooh inama mchungulie kwa chini saulaaa.” Aliimba Kuruthumu, waali wake wakainama kabisa.

“ooh lala chali asichoke kudumbukia kisimani saulaaa..” doh waali wakalala chali.

Wakafanywa kufuata wimbo huo kwa saa nzima. Mara wajibunue hivi mara walale vile, mara wagande tu kama mahayawani. ikawa maneno mengine yalikuwa magumu kuelewa wafanye nini maana kuna mahali Kuruthumu aliimba: mpe ale mbundu saulaa.. sasa mbundu ndiyo nini?

Loh.

Jasho tiritiri, wanawali, viungo viliuma, Kuruthumu aliyekuwa akigida mipombe akiimba akanyamaza kufanya miisho ya wimbo wake. Sasa akawatazama waali wake akawasonya.

“sikieni nyie misungo, sijui kawafunza nini huyo Ummy wenu. Ila nawaambia kabisa kuwa kwangu ukija hata kama kakufunza nani. Kwangu we msungo tu, kwasababu hakuna nyakanga anayeniweza si bara si pwani mamaee zao. Hapa mitusi, hapa kuchanana waziwazi.

“Huko sijui mmefundishwa kupika, kuosha vyombo sijui, hizo ni kazi za dada wa kazi na mwanamke asiyejielewa, mwanamke haswa hafanyi huo upumbavu, mwanamke ni pambo, mwanamke ni malkia, na kwangu, mwanaume ndiyo anafua na anaosha vyombo na kupika. Kama hawezi namfukuza. Mwanaume ni mtumwa wa mwanamke..”

“sasa sheria yangu ya kwanza, sifundi mwali aliyevaa nguo, utakaa uchi mpaka ujue kuutumia uchi wako kumfanya mwaname awe mtumwa wako, ndiyo uwe mwali uliyefuzu mkole wa Kuruthumu.

“kumfanya mwanaume awe mtumwa wako kuna siri zake,yule kijuso hawezi kuwaambia maana hazijui. Nazijua mimi na marehemu bibi yangu wa makorora. kwanza nyakanga sugu haolewi? Kama akiolewa huyo msungo tu kama misungo mingine. “Kwa hiyo mtakaa uchi hivyohivyo hadi siku nawaruhusu mvae nguo kweli mtakuwa mmefuzu haswa.




Na nguo namaanisha nguo, bazee, juba, dela na kijora, sio mivazi niliyowaona nayo hapa.

mnatembea tu na vimini na hivyo viskini, hamjui mnauza utamu wenu bure mchana eboo!

“wanaume wanawazoea anaona shepu yako ilivyojichora, kabla hajakulala anakuwa ameshajua ndani upojeupoje, lakini ukijivika madela, magauni, baibui, mwanaume akiingia anga zako, aseme aone mguu anasisimka maana hajawahi kuuona; aseme shingo ndio kuweweseka, kiuno ndiyo anahema tu juujuu, sasa pale penyewe ndio kabisa anajikojolea kabla msalani hajaingizwa.” alisema Kuruthumu mfululizo. Akanyamaza na kumtazama Renee aliyekuwa akimtazama Kuruthumu kwa adabu, lakini alipogundua Kuruthumu anamtazama akakwepesha macho yake kwa kutazama chini.

“wewee..ndiyo unaitwa Renee si ndiyo?!”

“ndiyo..dada..’

“mimi ndiyo kuruthumu kama ndiyo hunijui nijue, sifananiii eeh? lakini ndiyo mie sindano inayoshona makoti, najua mambo na hakuna mwanamke anayenizidi, hakuna mwanaume ninayemtaka nikamshindwa. Nimetembea na magumegume na mabuberi. Nimekutana na wenye bamia teke, mkungu wa ndizi na mihogo ya Nyankagire. Sasa mwali wangu nisichokijua kipi?”

“wanasema eti Ummy anakuzidi..” alisema Mercey.

“hahaaa… Ummy ni mjingamjinga mmoja tu, akajisifu simuwezi, nikamuibia mumewe. shehe uwesu, akanijengea nyumba akanifungulia saluni, na kila nikija Dar analilia penzi langu ananipa laki kwa usiku mmoja. Sasa mimi na Ummy nani mjuvi?”

“mh, wewe..” waliitikia kwa pamoja Mercey na Renee kama waliambiana.

“sikilizeni, nikikufundisha kuvunja ndoa ya mtu utaweza, ukiamua kupindua mchumba wa nani sijui utaweza, ukitaka utapindua hadi meli na nanga lake mamaee, ukitaka kujengewa nyumba, uhongwe mpaka ukatae pesa, hapa ndiyo mahala pake. Msione uzuri mlio nao ndiyo mkauringia, kama ingekuwa uzuri, mume wa Ummy na madanga zaidi ya thelathini yasingenililia mimi yakawaacheni nyie.

“mh mimi kutembea na mume wa mtu hapana!” alisema Renee akiona mambo yamekuwa si mambo.

“kelelee! Sikia wewe,itafikia wakati, kijanamke kitakudharau na njia pekee ya kukikomesha ni kukiibia mumewe..” alifoka Kuruthumu. Renee akafunga bakuri lake akamkumbuka Mary alivyojitia jeuri enzi zile, akaona ni kweli kabisa maneno ayasemayo Kuruthumu

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG