Chombezo : Corona Akee
Sehemu Ya Pili (2)
Siku ikapita na kesho yake ratiba yao ikawa ni hiyohiyo, kushuka mgahawani na kuzunguka eneo la vivutio vya hotelini na kurudi kulala. hatimaye siku ya nne ikatimia Neema akajikagua na kuona tone la mwisho likishuka kwenye pedi yake, lakini akajikausha kimya.
"Ney, bado tu!" alisema Cliff mara baada ya kurudi chumbani wakiwa wamemaliza kula chakula cha mchana.
"nitaangalia," alisema Neema akimtania Cliff.
"lete tuangalie," alisema Cliff akitaka kumkagua tena Neema.
"wee Cliff bwana, nakutania, nitakupa.. ngoja nikaoge kwanza.. na wewe jiandae maana nataka tumalizane mchana, usiku unirudishe airport nijifanye ndiyo naingia Tanzania na baba nilishamwambia kuwa naingia Arusha leo saa saba usiku."
Loh Cliff alifurahia huyo, akajikoki, akapiga hesabu za masaa atakayomfaidi Neema akaona ni masaa takribani kumi,akajiapia hatoyaachia hivihivi, hatosinzia wala kufikicha kope; ni shoo shoo. sasa wakati Neema anaingia bafuni,yeye akajibust kidogo na mvinyo huku akitoa laptop kwenye begi lake na kuweka muvi ya ngono kwa sauti ya kistaarabu ili ihamasishe tendo litakalofanyika dakika chache zijazo, kisha akatulia kama nyani ngabu.
Kila sekunde kwa Cliff zilikuwa zikithaminishwa na nenge alilokuwa nalo juu ya Neema, akaona anachelewa japo kiukweli hata dakika tano hazikupita tangu Neema aingie bafuni. sauti ya maji yakitiririshwa bafuni ndiyo aliyokuwa akiyasikia; akausihi moyo wake utulie na usiwe na pupa; na kwa wakati huo akawaza staili za kumla bata wake wa anayenukia ukanisakanisa.
Basi ule muda aliokuwa akiusubiria ulitaradadi, Neema akatoka huko bafuni na kitaulo kifuani kwake, akamtazama cliff na kumsogelea akijifuta kiuchokozi na uchokonozi vimajimaji vilivyobakia mgongoni.
Neema akapanda kitandani na kumkabili CLiff aliyekuwa hajauwazia huu mwenendo kabisa kichwani pake, Cliff akampokea sista wa kanisa kama mtoto akamuonesha kuwa yeye ndiye kituji mrina asali akamgeuza na kuanza kumpangua tawi mojamoja akipuyanga kuelekea kwenye mzinga wa asali.
Kila Cliff alivyomkwanyua vikonyo mtoto wa watu ndipo Neema alitamka majina ya watu wa kwenye biblia na watakatifu kadhaa
Haikuwa inaendana na eneo la tukio kabisa na pengine malaika wa dhambi wangemuandikia adhabu kali; lakini utamu ulimfanya aropoke neno lolote lilikuwa karibu na ncha ya ulimi wake, naye ni sista sasa ungetegemea ataje pombe pale au?
Basi robo sentimeta tu kufikia utamu na hatamu zake, ghafla mlango ukapigwa hodi kwa nguvu, Cliff na Neema wakashtuka maana ni nadra mlango wa hoteli kudundwa konzi zito namna hiyo. Cliff akaghafirika kwelikweli akaizima laptop yake; lakini akasita kufungua mlango kwanza; pengine ni tego hili! aliwaza akimtazama kwa jicho kali Neema; Neema naye alimtazama Cliff vivyohivyo akijiuliza kama alivyojiuliza yeye.
mara mlango ukagongwa kwa mara ya pili tena kwa uzito uleule.
"we Cliff mkeo nini amekuja?" aliuliza Neema akijivalisha nguo zake himahima.
"hapana; sina mke mimi?"
"au basi mpenzi wako.."
"hapana hawezi kuja huku hajui.." alijibu Cliff roho ikimuuma jinsi Neema alivyovaa tena wakati mambo yalikuwa tayari siyo mambo.
mara hodi ikakoma kama ilivyokuja awali kukawa kimya tena; Cliff akamtazama Neema aliyejivisha kama vile hakuna kilichokuwa kikiendelea humo ndani.
"watakuwa wamekosea room!" alisema Cliff moyoni akitukana kuanzia aliyegonga mlango wa chumba chake, wahudumu na hadi mmiliki wa hoteli kwa kumharibia gemu yake.
lakini kabla wazo hilo halijamea kichwani pake kumshawishi Neema aliyekuwa tayari na wasiwasi, mara simu ya chumba chake ambayo imeungwa na kule mapokezi ikaita. Cliff akahesabu sekunde kumi kisha akaipokea kwa hofu na ghadhabu.
"hallow, samahani mteja wetu;kuna tatizo limetokea tunawapigia wateja wetu wote waje ukumbi wa hoteli floo ya tatu sasa hivi, ni jambo la kiusalama tafadhali," alisema mhudumu wa kike aliyesikika akiwa na hofu mno.
Haraka Neema alikimbilia kutoka nje ya mlango akimuacha Cliff ameduwaa. Akilini Neema alijua pengine ni tukio la ugaidi linaendelea hotelini hapo kiasi cha mhudumu kutoa taarifa ile, lakini kwa Cliff ilikuwa ni saa nyingine ya kulaani; kwanini vikwazo vinatokea asifanye mapenzi na Neema; au Mungu anamlaani asitende dhambi na mtawa?
Basi naye Cliff haraka akavaa nguo zake na kukimbilia huko floo ya tatu alipopanda Neema, hapo varandani kundi la watu wakiwa ni wateja wa vyumba vingine vya hoteli hiyo, wazungu, waarabu kwa waafrika wote wakikimbilia pamoja naye kwenye floo ya tatu kila mtu akijiuliza; nini kimetokea?
wakaingia kwenye ukumbi huo wa mkutano wao wakionekana ni kundi la mwisho kabisa maana watu walikuwa wengi sana hapo ukumbini, wengine na mashuka kabisa ya kulalia wakiwa wamejizungusha nayo, wengine na mataulo na mabaki ya mapovu masikioni kuonesha kuwa walikurupuliwa na hilo tangazo la dhalura wakiwa wanaoga. Kuona hivyo ndiyo angalau Cliff alituliza pepo lake, akajipenyeza mpaka alipokuwa ameketi Neema naye akaketi pembeni yake macho yakiwa mbele ya ukumbi.
Watu wanne walionekana wakiwa wamevalia suti kuonesha kuwa ni watu wa heshima au viongozi fulani, sura ya mmoja wao ndiyo iliyomshtua Cliff akajiuliza amewahi kumuona wapi mtu huyo, lakini kumbukumbu zake zilimsaliti. Ghafla kidogo kundi la maaskari polisi waliingia ukumbini hapo wachache wakiwa na viziba pua kama madaktari wa oparesheni au wahudumu wa mochwari, na kufanya ukumbi uzidi kuwa na hofu waliingia madaktari sasa wakiwa na makoti ya nailoni, glovuzi za mipira, miwani ya kuziba macho mfano ya watu wanaopiga mbizi chini ya maji na wakipumulia mashine fulani, migongoni mwao wakiwa na mabegi ambayo walienda kuyaweka mbele kabisa kisha nao wakajiunga na wale wengine waliosimama pale mbele ukumbini wakiwatazama wakina Cliff na kundi la wateja wa ile hoteli. "Naitwa Mrisho Gambo, mkuu wa mkoa wa Arusha, samahanini kwa kuvamia hapa hotelini, hawa ni madaktari kitengo cha kuzuia magonjwa ya mripuko. Kama tunavyofahamu dunia ipo vitani dhidi ya ugonjwa hatari wa Corona ambao unaambukiza kwa njia ya kugusana au kukaa karibu na muathirika wa ugonjwa huo
"Ugonjwa huu ni hatari kwa kuwa unaua haraka kama utakosa matibabu; kwa Afrika hadi jana nchi ya Nigeria, Algeria na Kenya zilikuwa zimekumbwa tayari na ugonjwa huu.
Kwa bahati mbaya sana leo naripoti kuwa ugonjwa huu umeingia rasmi Tanzania na mgonjwa wa kwanza amepatikana mchana huu hapahapa hotelini." alisema mkuu huyo wa mkoa kauli yake ikitafsiriwa kiitaliano na kiingereza na meneja wa hoteli na palepale minong'ono ikasikika mle ndani, hofu ikatanda.
Cliff akamtazama Neema aliyejikunyata,akamsogelea na kumkumbatia. "Kwa kauli hiyo basi, hoteli hii itafuata taratibu za shirika la afya la dunia kuwa itawaweka karantini ya siku 15 wagonjwa wote kabla ya kuwaruhusu ili kama kuna mtu atakuwa ameambukizwa bila kujijua asiende kuwaambukiza wengine huko nje. Kuanzia leo hii ninavyotamka hoteli hii naifungwa hakuna atakayetoka wala atakayeingia. Baada ya hayo ninawaachia timu ya madaktari na wanausalama watawapeni maagizo zaidi natumai mmenielewa," alisema mkuu huyo wa mkoa na kuondoka haraka.
Loh kauli ya kutotakiwa kuondoka mle hotelini ilimvuruga kidogo Cliff akawaza demu wake Grace yule polisi atamueleza nini, lakini mwenye mawazo sanasana alikuwa ni Neema akamfikiria baba yake na alivyomdanganya kuwa ataingia Arusha usiku huo je, akisikia alikuwa hotelini atamfikiriaje? kwanza watamuuliza alifuata nini na hata kama aliamua kulala, vitabu vya hoteli si vitamuumbua kuwa alifika Arusha siku nne nyuma? aliwaza Neema macho yake pia yakiwa makini kuona kama kutakuwa na makamera ya waandishi maana sehemu kama hizo waandishi hawakosekanagi. Akafarijika kutomuona hata mmoja akakumbuka kumbe yupo Bongo nchi ya waandishi waoga kama kunguru wa Zanzibar,ona alivyokuwa na hatari mtawa wetu hata hofu juu ya Corona hakuwa nayo, yeye aliwaza kujilinda tu asiumbuke kwa baba yake.
"Naomba wageni waliofika kutoka nchi zilizoathirika wakae upande huu wa kushoto, wale walioingia hapa hotelini kutokea Tanzania hapahapa wakae upande wa kulia," ilikuwa kauli ya meneja wa hoteli aliyeitafsiri vizuri kiasi cha kueleweka na wote waliokuwa hapo.
Haraka kundi likagawanyika, lakini Neema akawa ametatizika hakujua aelekee wapi maana aliona kujitaja kama ametokea Italia ambapo ugonjwa huo wa COrona umeshika kasi ingekuwa ni kuzidi kujichelewesha kukaa hapo hotelini pia akawaza uwezekano wa kuruhusiwa kwa wageni wa hoteli waliotokea hapohapo Tanzania na hakutaka fursa hiyo aikose.
Kwa upande wa Cliff yeye alikuwa tayari anaelekea upande wa kulia na akashangaa kumuona Neema anaelekea huko pia.
"We Neema, si wamesema uende kushoto?" aliuliza Cliff kujiridhisha na sababu ya maamuzi ya Neema.
"Cliff sitaki nibakie hapa Hotelini, lazima nirudi nyumbani leo!" alifoka kichinichini Neema.
"sawa,lakini si unaona hali halisi tunatokaje sasa," alisema Cliff akitazama saa ya simu yake kuwa ni saa 9 kamili za mchana.
"sijui kwanini nilikubali kuja hapa hotelini na wewe agh!" alilalamika Neema akionekana kujilaumu mno.
"usiseme hivyo Neema mimi mwenyewe naona kama vile nina gundu na wewe; majuzi ulianza kubleed,leo corona dah!" aliamua kusema yake pia Cliff.
"hapana labda Mungu ananiadhibu mimi," alisema Neema akikaribia kujibanza kwenye hilo kundi la wageni kutokea Tanzania;lakini akashtuka kuona mmoja wa wahudumu wa mapokezi wa hoteli hiyo akifika na daftari la register kwa yule meneja wa hoteli ambaye alikuwa nyuma yake na maaskari wenye maski zao usoni sambamba na madaktari kama wote.
Haraka Neema akajua ujanja wake wa kujibanza upande wa Cliff utabainika na watamtilia shaka na kama wakimpekua na kugundua anatokea Italia tena ni mtawa ndio kabisa watamgeuza kituko na mbaya zaidi alivyovalia hapo ukumbini ilikuwa kichekesho maana alikuwa na kiskini jinzi na kingwabi kilichomchoresha hadi ncha za matiti yake; akageuza harakaharaka na kurudi upande wa kushoto akijiunga na wahabeshi wenzake akitengana na CLiff aliyekuwa ametumbua macho asielewe mchezo wa Neema.
Basi kama kweli alivyotabiri Neema, majina ya register sasa ndiyo yakatumika kuwatenganisha wageni kutokana na nchi mbalimbali tena kundi la kwanza kupimwa likawa la wale waliotokea nchi zenye maambukizo ya COrona wakianzia Uchina, Marekani na kundi litakalofuata kupima lilikuwa na wageni kutoka Italia ambapo hapo Neema alikuwemo.
Mkojo wa wasiwasi ulimbana Neema wakati akishuhudia foleni ikipungua kuelekea kwenye sehemu ya kupimia, akajua ataumbuka safari hii; akamuomba Mungu amsaidie asiumbuke na akaapa kutorudia kufanya uzinzi huu tena.
"jina na umetokea nchi gani na chumba namba ngapi?" aliuliza meneja akimkazia macho mzee wa kizungu aliyekuwa akipiga chafya mfululizo mbele ya Neema, maana akitoka huyo tu ndiyo Neema angefuatia.
"Diego Poisant, Italy, room 13," alisema huyo Mzee kwa kingereza kilichoathiriwa na kiitaliano cha ndani kabisa. "where is your passport?(passport yako ipo wapi)" aliuliza yule Meneja akipandisha maski yake imzuie vilivyo usoni maana shuku la wote mle ndani lilikuwa juu ya mzee huyo kuwa ana corona maana hata wale maaskari walitetemeka.
"I left it in my room, hey I came in a hurry i didnt know we have to come with it{ nimekiacha chumbani, nilitoka kwa haraka, sikujua kama nilipaswa kukibeba)."
Basi alivyosema hivyo yule meneja akasema kwa sauti, "tafadhali walioacha passport vyumbani wakachukue na warudi haraka hapa."
Loh alivyosema hivyo, Neema akaona ni chansi akarudi haraka kule chumbani; akawaza kutoroka hotelini lakini nje umati wa mapolisi na waandishi wa habari ulimrekebisha wazo lake haraka. Basi akavua viwalo vya kishenzi alivyovivaa na kuvaa vazi lake la usista akabeba na simu yake na kumtumia meseji, Cliff.
"Sikia nitasema wewe ni dereva wa parokia uliyetumwa unipokeena unipeleke nyumbani," aliandika meseji hiyo Neema ikadeliver kwa Cliff maana alikuwa na uhakika alimuona na simu yake pale ukumbini.
"He sasa wakiuliza ilikuwaje jina la pale reception niliandika jina langu, nisemeje?"
"sema ulikuwa umeona usumbufu kubook kwa jina langu,kwakuwa ndege ilighairishwa mara nyingi, sema nilifika jana usiku, nina uhakika muonekano wangu nitakavyotoka huku ndani,hakuna atakayesema aliniona mahali popote.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment