Chombezo : Haunikomoi, Tunakomoana
Sehemu Ya Tano (5)
"Yaani Merina amechanganyikiwa aisee hadi alinitajia ulipo na kuwaambia polisi wakuachie. Tumeanza mlemle tangu mlipoonana Facebook, dunia nzima itamjua Merina ni nani?" alisema Producer lakini nilishangaa tu sikuwa nafuraha kabisa kama aliyokuwa nayo yeye, nikajikuta namuonea huruma Merina, lakini nikajisemea moyoni kuwa kama usanii ndiyo uliomtia wazimu basi awe masikini kama zamani ili anipende na kuniheshimu tena.
Nilirudi nyumbani nikadharau simu nilizopigiwa na meseji zilizokuwa zimesheheni kwenye simu yangu, nikalala usingizi mzito. Asubuhi niliweza kutazama vichwa vya habari magazetini kupitia simu yangu, na kusoma meseji mbalimbali za ndugu na marafiki zote zikihusiana na Merina na mimi.
Niliweza kusoma habari zangu kila kona wengine wakinishambulia mitandaoni wakinituhumu kumchafua Merina, wengine wakidhania ni kiki tu na wengine wakinisapoti.
Kama hilo halitoshi nikamtuma hausigelo wangu akaninunulie magazeti ya siku hiyo, kweli niliona magazeti yakiwa yamesheheni sehemu ya pili ya simulizi yangu na Merina, kwa kweli tulikuwa ndiyo habari ya mjini na sura yangu ikawa mbele ya magazeti kwa ukubwa mno.
Merina alikuwa na mengi ya kujibu lakini cha ajabu hakujitokeza kokote kujibu shutuma zile na kwa taarifa nilizozisikia kutoka kwa mchambuzi mmoja wa masuala ya burudani ni kwamba chochote nilichokisema kuhusu mimi na Merina nilikuwa simharibii Merina zaidi ni kwamba mimi ninajishushia heshima yangu mbele ya jamii huku yeye nikimtangaza zaidi ili aendelee kuuza nyimbo zake.
Nilipotafakari niliona huyo mchambuzi hana mantiki kwa upande wangu kwa kuwa Merina alikwisha nichafua mno mwanzo hivyo sikuwa naheshima kwa jamii haya niyafanyayo nikujaribu kuirudisha hadhi yangu..
Hoja ya huyo mchambuzi ilikuwa na mantiki tu kuhusu Merina; ilikuwa ni kweli kabisa kuwa mauzo na show za Merina zilizidi mno na waandishi wa habari walimzonga na maswali naye hakuwajibu chochote zaidi ya kusema; No Comment.
Nadhani hata Merina aliona kuwa nampa kiki pia, kwasababu hata huyo Omary alikuwa hanipigii simu tena na cha kushangaza Merina alikuwa akija nyumbani na marafiki zake, wakajiachia wanavyojua, siku nyingine alifika hata na wanaume zake bila kuniogopa, ingawaje gazeti bado lilikuwa likitoka.
Ilifikia siku Merina alikuja nyumbani na mwanamke mmoja ambaye alivyolivyo ni kama jike dume wakaingia naye chumbani kwake huku Merina akiropoka kwa sauti ilimradi nimsikie; alisema: "Nakupa cha kuandika kesho, nalala na tomboy, kaandike kuwa nasagana siku hizi, mfyuuu."
Aisee yalinifika hapa.. uamuzi wa kuachana na Merina ukawa ndiyo hoja ya msingi kwa wakati huo. Nililala na kuamka na kwenda studio kwa producer wangu kutaka ushauri maana hata kazi zangu dukani zilikuwa haziendi kabisa nilikuwa kama nimechanganyikiwa tu.
"Sikia Cliff usimuache huyo mwanamke sasa hivi ni too late, umechelewa!" alisema Producer nikamshangaa kwanini anishauri nisimuache Merina wakati yeye ndiye mtu ambaye tangu mwanzoni alikuwa akinipa onyo la kuachana na Merina.
"kwanini?" niliomba sababu.
"ukimuacha sasa, wewe utakuwa umepoteza kila kitu hata jina ambalo umeishalitengeneza sasa kwenye vyombo vya habari.. sikia, wakati unaona hauna heshima kabisa duniani, mimi nimekuwa nikijaribu kutengeneza vitu viwili vitatu kuhusu wewe ona!" alisema Producer akinionesha simu yake ambapo juu ya kioo cha simu yake ilionekana akaunti ya instagram ikiwa na jina lililoandikwa; Cliff_mumewaMerina.
Hiyo akaunti ilikuwa na followers laki tisa na post karibia ishirini, kama hiyo haitoshi niliona picha yangu pale kwenye profile. Nilishtuka maana sikuwa mpenzi wa instagram na akaunti yangu niijuayo ilikuwa na followers hamsini tu nikiwa sijapost chochote tena. "Usishangae Cliff, hii akaunti niliitengeneza wiki mbili ziliyopita nijaribu kuangalia wangapi wanakubali unachokifanya na wanampinga Merina.
Ni wengi mno tena kwa muda mchache tu una watu laki tisa wakati Merina ana watu milioni mbili tena kwa mwaka mzima aliokuwa staa; heshima yako ni kubwa mno kuliko unavyodhania, usimuache Merina kupitia yeye wewe tengeneza yako. kama unaumia sana yeye akileta wanaume hadi matomboy ndani, wewe leta wanawake hadi mashoga, akikupa gono, wewe mpe kaswende, akikukomoa na wewe mkomoe, komoaneni!" aliongea Producer wangu maneno makali mno.
"Hapana mimi siwezi kuwa kama yeye," nilisema nikijivutiia taswira na mimi nimekuwa eti mcharuko naanzaje kwanza hata kusimama na mwanamke mwingine nikamtongoza mbaya zaidi namletaje nyumbani..
"Cliff kilichombadilisha Merina ni usupastaa, na waume au wake wa masupastaa wakiona wapenzi wao wanabadilika wanachofanya wanakomoana, hawaachani nakupa siri kwasababu najua muziki vizuri mzee. wewe kwa sasa staa pia badilika, hebu tazama hapa," alisema Producer akinionesha meseji za instagram kwenye ile akaunti aliyonifungulia. Nikaona kuna meseji kibao, nyingi kutoka kwa warembo mbalimbali jijini, wakiomba nimuache Merina na nitembee nao wao. Loh wengine walikuwa wazuri mno, nikastaajabu na kamoyo kakatatarika.
"weee hawa wote wananitafuta mimi!?" niliuliza kwa mshangao nikiivuta simu ya Producer karibu yangu, meseji zilikuwa zaidi ya miamoja. "Sikia, futa ile akaunti yako ya mwanzo, andika hii mpya na hao watu pambana nao mwenyewe, hii ni zawadi yangu kwako..supa staa. na baadaye nataka tutengeneze pesa sasa, ili jina ulilonalo lisiende bure, ila usimuache Merina, mtumie kama anavyokutumia.." alisema Producer na palepale akanibadilishia ile akaunti ikawa kwenye simu yangu, akanielekeza kuwa cha kupost ni vitu vyovyote vinavyomponda Merina na kuwaonesha watu jinsi mimi ninavyoumia, yaani hiyo iwe ndio kiki yangu pia.
itaendelea..
Ile usiku tu nilipofika nyumbani, sikumuona Merina pengine alikuwa ameenda kulala nje na kupitiliza kama kawaida yake. Wakati huo na mimi nikajiunga bando la kutosha na kuanza kufuatilia comments zilizopo kwenye akaunti yangu.
Niliona comments za kunitukana, zingine za kunionea huruma na nyingine za kujibizana watu kwa watu yote kuhusu mimi. Nilichukia na kujaribu kutazama comments kwenye akaunti ya Merina ili kujilinganisha, napo nikaona vilevile; kuna watu walimchamba na wengine walimsifia; hapo nikajifunza kuwa mashabiki wapo wa aina mbili, kuna wale wanaokupenda na kukusifia unachokifanya, wapo wengine wanaokuponda na hawapendi unachofanya lakini bado wanakufuatilia na hata kununua kazi zako.
Kwa hiyo kwa kulijua hilo sikuwa nina hasira hata kidogo, nikatoka huko kwenye comments nikaenda DM ambapo Producer alionesha warembo huko, basi nikaanza kujibu meseji zao, nikachati nao mno, wengine wakaniomba hadi namba yangu ya simu na kuniahidi pumziko kutoka kwenye penzi la Merina.
Wengine walikuwa na hela na wanaheshima zao mjini, wengine chachalamuya tu waliotaka kuambukizwa usupastaa kwa kuomba kupiga picha na kupostiwa ila wote kwa wote walinisifia kuwa mimi ni hendsamu na kuwa sikupaswa kuteswa na mapenzi. Kauli hizo zilinisahaulisha Merina kwa usiku ule maana ni mwaka sasa nilikuwa namuwaza yeye tu na sikujaribu hata kuchepuka; haja zangu nilizimaliza kiutu uzima, lakini sasa nilisema basi! ngoja nijaribu.
Nikaanza na mrembo mmoja, tukakutania gesti, nikachepuka naye na alikuwa mzuri mno, lakini cha ajabu kila nilipotazama inbobo tena nikawa nawaona wazuri zaidi ya yule wa mwanzo, tena na huyo mpya nikamuona mzuri zaidi yake, nikawa na wapenzi wawili; nikawa na watatu, wanne, watano, sita nakadhalika; kuja kushtuka na mimi nikawa malaya; tena malaya mbwa; muongo balaa maana niliweza kumtazama mpenzi wangu huyu nikamwambia hili, na yule nikamwambia lile na bado nilikuwa na Merina nyumba moja.
Nikukumbushe kuwa bado wakati huo gazeti lilikuwa likiendelea tu kuchapishwa na stori yangu ya mwisho na Merina ilikuwa ikitoka wiki ijayo, hivyo nilijiuliza umaarufu wangu utaendelea wakati stori ikiisha gazetini? au ndio itakuwa basi tena.
Na kitu kingine nilichokigundua pesa zilikuwa zikipungua kwa umalaya wangu maana kulala hotelini na lodge na wanawake tofautitofauti na ile kuishi kisupastaa kulinikamua kwelikweli, na hapo ndiyo kulikuwa na ulazima wa kutafuta pesa haraka na ndiyo nikamkumbuka Producer alivyoniambia kipindi kile kuwa siku ataniambia jinsi ya kutafuta pesa kupitia umaarufu wangu na nikiwa tayari niende aniambie.
Basi sikuvunga nikaenda kuzungumza naye ili tujue mustakabari utakuwaje, kwanza akacheka sana akiniambia hivi sasa naonekana ninafuraha mno na mimi nikacheka na kumwambia shukrani zote ziwe kwake yeye kwa sababu alinisaidia mno kimawazo na vitendo, na nikizungumzia vitendo namaanisha hilo tendo la kunipa akaunti ya instagram iliyonitunuku warembo wazuri kuzidi mke wangu pasua kichwa.
"Sasa ndugu yangu, kipindi kile uliniambia jinsi ya kutumia jina langu kutengeneza pesa, naomba tuzungumze sasa hivi, maana hali si hali," nilisema.
"hahaa, kumbe bado unakumbuka.. sikia, nataka uimbe na wewe. najua kwa ulivyomaarufu kawimbo kamoja tu unatoboa," aliniambia Producer akiwa siriaz.
"niiimbe?" niliuliza kama vile nilikuwa sijamsikia vizuri alichokisema.
"ndiyo, inabidi uimbe, sababu kila mtu maarufu bongo akitaka kubakia kileleni inabidi aimbe na kuimba ukishapata jina kunaingiza pesa fasta kinoma," alisema Producer.
"hapana kwa kweli, siwezi," nilikataa.
"sikia, nilitaka kukwambia hili jambo tangu kipindi kile Merina anasumbua, lakini niliona nikae kimya. Unataka kumshusha Merina akupe heshima yako ya ndoa au hautaki?"
"nataka," nilisema.
"Sasa ukweli ni kwamba vita tuliyopigana na Merina tulikuwa hatupigani uwanja sahihi, uwanja sahihi wa vita pamoja na Merina ni kwenye sekta yake ya muziki hukohuko, ile kutoa simulizi gazetini na kujibizana mitandaoni ni uwanja tofauti wa vita, imba." alisema Producer.
"Enhee tunaanzaje?"niliulizia mchakato mzima maana alinitia moto nianze hata muda huohuo kuripuka mistari. Akanipa maelekezo ya awali ikiwemo kunitafutia sauti ya kuimbia kutoka kwenye sauti yangu mbaya. akanielekeza kufuata biti na tempo na mwishoni akaniambia nitafute pumzi kwa kukimbia na kuimba kwa sauti.
Basi na mimi nikaanza harakati za kuimba, mke wangu akienda kudanga na mimi naenda kutembea na mademu zangu, akipiga kelele kwenye sabufa eti anafanya mazoezi ya kuimba na mimi naweka sabufa naimba nyimbo eti nikifanya mazoezi ya kuimba. Akileta ndani mabwana, na mimi nahakikisha namleta mulemule demu mkali hadi anavurugwa, nyumba ilikuwa imechangamka sasa; ngebe zilikatika.
Mwafulani akapatwa na jini kisirani; nyepesinyepesi ni kwamba shoo za Oman hakuitwa tena na Promoter wake, nikasikia Omary aliwabeba wasanii wabichi wakike wadogodogo ndiyo waende, yeye akaambiwa amechuja na Sayeed hamtaki tena, kingine shoo zake zilikuwa zimedorora, akaambiwa ajibadili umbo na atafute kiki kwasababu kiki niliyokuwa nampaga mimi kwenye gazeti ilikuwa imeshaisha, hayo niliambiwa na shoga yake mwenyewe aliyeamua kuuza faili lake kwangu.
Nilicheka nakuona mwisho wa Merina, Nyumbani kukawa hakuna mabwana wala madanga, akauza gari na mwishowe akawa hatoki kabisa, akawa anajifungia tu ndani, huruma nikamuonea. Na mimi sikupunguza nikawaleta wanawake wa kutosha ili kumuumiza na kulipizia.
Mademu zangu wakishtuka kumuona Merina sebuleni, nilikuwa nawaambia; aah muacheni huyo hana shida, kwani mke wangu una shida?" akawa hajibu zaidi ya kupinda mdomo kama anavuta sharubati ya tofaa kwa mrija.
Kumbe akapanga yake na yeye, akawa anakesha kwa waganga na akawa anatumia madawa ya kuongeza makalio, loh yakamjaa kama wa kuchora, na hiyo ilikuwa ni maandalizi ya kurudi upya, maana siku moja jioni nikaona habari zake kwenye televisheni, Merina akihojiwa tena akijibu tuhuma za kipindi kile nilizomchana kwenye vyombo vya habari, loh!
"Niliamua kukaa kimya kama mwanamke niliyefundwa na najua ndoa ni nini, sikutaka kuzungumza wakati mume wangu anafikia hatua ya kuchapisha hadi magazetini mambo ya ndani ya ndoa yetu, ila sasa nimeamua kusema kwasababu watu wamegeuka mahakimu wa ndoa yetu, dharau na matusi ninavyotupiwa na hao wanaonihukumu yamenichosha..Sasa kama mwenzangu alivyoamua kutoa habari kwenye magazeti na mimi nitachapisha simulizi yangu yote kuhusu maisha yangu ya ndoa ya Cliff..
OI TUNAKOMOANA 26
.. na nyinyi mashabiki kama mlivyonihukumu mimi na pia mkamuhukumu yeye kwa ukweli ambao nitausema," alizungumza Merina na kuachia chozi la huruma mbele ya vyombo vya habari.
Nikavurugwa na kuchanganyikiwa. wakati uleule Merina akanitumia picha zake kwa watsapp ambazo amezipiga studio, akiwa na kichupi tu, huku lijishepu lake likiwa wazi akiwa katika mikao tofautitofauti ya kiuchokozi. akaniandikia meseji chini yake ya neno moja tu, HAWACHOMOKI.
Nikamtumia viemoji vya kucheka, huku moyo ukinidunda. Akaniambia; nimerudi upya, hii picha kesho nadhani utaiona sana mitandaoni, sasa wapange mahawara zako, tako ndiyo habari ya mjini, sura hata mbuzi anayo."
Doh nikahisi labda editing ikabidi nimsubiri alivyorudi nikamchungulia dirishani akishuka kwenye bajaji, loh jishepu lake lilikuwa balaa na alijikoroga kama sio mke wangu vile. akanipitia akinitingishia akaingia zake ndani huku akininyali.
Saa ile Producer naye akanipigia simu; "kaka umeona Merina alichokifanya? anataka kiki, sasa vumilia akushambulie usijibu chochote kwenye media, kaa kimya atakachofanya chochote ni kiki kwetu na lazima afeli, na kipindi hichi sasa ndiyo sisi tunarekodi na kuliachia linyimbo letu..
MWISHOOOOOOO
0 comments:
Post a Comment