IMEANDIKWA NA : CHANDE ABDALLAH
********************************************************************************
Chombezo : Corona Akee
Sehemu Ya Kwanza (1)
"Neema naona umeamua kunifanyia makusudi, haiwezekani ukaingia siku zako leo wakati ndiyo unajua kabisa unakuja kukutana na mimi baada ya maika zaidi ya saba," alilalamika Cliff sauti yake ikifanya mngurumo mdogo ndani ya chumba cha hoteli ya kifahari ya Red Spice iliyopo huko Arusha mjini.
"Hapana, sikujua kabisa, kama itakuwa hivi, imeanza sasa hivi nakuapia Cliff sikuwezi kukufanyia makusudi, hata mimi mwenyewe nimekumiss," alijibu Neema akijitetea ikiwa ni baada ya mipango yao ya kufanya unzinzi kuonekana kuvunjika siku hiyo na hata kesho na hata siku nne zijazo hadi pale bidada atakaporudi kutoka mwezini.
"hapana siamini nataka nione," alisema Cliff akinusa harufu ya uongo wa Neema kuwa pengine anambania makusudi baada ya kumlia vitu vyake; we fikiria makuku, mabia, mastarehe waliyoyafanya usiku huo na kama haitoshi vile gharama za kulipia chumba cha hoteli halafu eti anakuja kubaniwa kirahisi hivi, hapana kwa kweli, lazima amkague.
"He, Cliff aya, nitazame," alisema Neema akifumba macho yake kwa aibu na hasira, akapandisha kisketi chake na kutanua miguu akionesha chupi yake ikiwa imeanza kuloa tone la damu pale katikati.
Cliff akawehuka macho yake yakitazama kitu anachonyimwa wala siyo maumivu ya mwenzie, zipu zikazidi kungangamara badala ya kuvyondea, akamtazama Neema kwa uchu rohoni akajisemea:"kwani damu nini bwana anipe tu kidogo naingiza kichwa tu."
"tayari umeamini?" alisema Neema akijiandaa kuishusha gauni yake.
"hapana,sijaamini, nataka nione kabisa,je kama umejipaka lipstiki!?" "loh mimi nikufanyie hivyo, aya ona, ona!" aliongea Neema akimsusia na chupi yenyewe, Loh Cliff akatazama uroho ukimuisha, ni kweli Neema alikuwa kwenye siku zake, haitakuwa ustaarabu kumlazimisha.
"Ndiyo uende tena, ukaninunulie pedi," alisema Neema, Cliff akajizoazoa na mapombe yake aliyomnywea mtoto wa watu na mkongo aliompakia mtoto wa watu, akatoka chumbani kuelekea supermarket hali akitukana na kuilaani siku hii na siku nne zijazo.
akanunua na kurudi nazo ndani. akampa Neema na kujifanya anampa pole.
kichwani akawa anapiga mahesabu yake, ikiwa atamuachia Neema aondoke kesho yake, basi kumpata hapo ni majaliwa, lazima ahakikishe anatembea naye kabla hajamuachia. Hela kwake siyo tatizo kabisa akamtazama kwa uroho ulioanza kuamka tena, akamuuliza.
"Neema basi tukae na mimi hapahapa hotelini hadi ukimaliza kubleed, pesa ipo,usirudi kwenu kwanza, kwani baba yako anajua kama umesharudi?"
"mh we Cliff, kubakia hapa ni noma, bora niende kwa baba kwanza halafu nikishamaliza nitarudi," alisema Neema.
"wee hapana, sitaki, yule mzee wako anakuchunga sana, na kukupata tu leo kama bahati, naomba ubakie hapahapa kwani wewe unableed kwa siku ngapi?"
"siku nne tu nakuwa poa, lakini ubaya baba anajua tumeshafunga kwa sababu ya huu ugonjwa wa corona na nilishamtumia picha nipo airport," alijibu Neema.
"sawa cha msingi tusitoke, na mzee wako akikuuliza we mwambie bado haujasafiri umesikia eee!"
"tatizo nilishamtumia picha nipo airport na najua atakua ananingojea nirudi kesho, sasa sijui nitamdanganyaje?"
"we unajua bwana, mwambie tu kuwa ndege ilighairisha safari,"
"aya sawa,"
" enhee kwani corona ni nini na unakuwaje?
"taarifa tu kuwa unapata mafua na homa na unaambukiza wengine, watu wengi wanaumwa Italia wamefunga makanisa na vyuo ndiyo maana tumeruhusiwa kurudi, nasikia hapa hakuna hata mgonjwa," alisema Neema.
"Afrika hatuumwi, sisi tuna ngozi ngumu," alisema Cliff. Basi wakajikuta wanapiga stori za Corona na kumpeperusha pepo wa ngono aliyewazingira siku hiyo.
kama ulikuwa ukijiuliza ilikuwaje Cliff na Neema wakutane siku hiyo ni kwamba, hawa walikuwa wapenzi tangu sekondari kumbukumbu halisi zilionesha tangu kidato cha tatu, Cliff akamuomba penzi Neema lakini Neema akamwambia Cliff msimamo wake wa kutaka kuwa sista na umuhimu wa kutunza bikra yake. Cliff alijua ni uongo tu wa Neema kumkimbia lakini ni kweli hakuambulia kitu kwani Neema alivyomaliza kidato cha nne, akapotelea seminari na kuenda huko Italia kusomea utawa na akawa mtawa kweli.
walipotezana kwa miaka saba, kwa njia ya ajabu akakutana Neema akiwa ni mtawa wa shirika la wa Benedictini
Cliff yeye ni mfanyakazi wa bodi ya utalii, kijana wa mjini mwenye uchu wa kulionja penzi la Neema maana hakuwa tu na Neema bali alikuwa na msururu wa wanawake huko nyuma; kilichomfanya amsubiri Neema kwa kiasi hicho ni jinsi alivyolivyo, maana kwanza hafananii na kuwa sista jamani ni mzuri mno kufa na bikra yake. Lakini cha pili ni hulka tu za Cliff, hakuwahi kumuonja Neema na ndiyo alitaka kumuonja kwa gharama yoyote; na mpaka sasa alikuwa ameshagharamia vya kutosha na kumfanya usiku huo sista wa watu avue kiremba na gauni la kitawa na kuvaa viatu vya mchuchumio na vijinzi kisha kuingia club na hotelini kama hakuna kitu vile.
Huenda Cliff alishagundua walakini katika tabia za Neema maana hakuonekana mgeni wa mambo ya kucheza muziki wala vilevi. Alikunywa tu vilevi vikali na hakulewa kama Cliff alivyotarajia. Muziki wa kidunia ulipopigwa na yeye nyimbo nyingine aliziimba vizuri kabisa na kuzungusha kiuno chake. Mara kadhaa alijiuliza; Loh mtawa anazijulia wapi nyimbo za aina hii? lakini akakausha akidhania pengine huko utawani kama pombe huzinywa kwenye divai na kama nyimbo pengine huwa na masherehe yao na huzisikiliza.
Usiku ule wakati wakiwa wanalala baada ya stori akajua Neema atamsalisha sala za salamu Maria na Baba yetu, lakini wapi! sista Neema alilala fofofo kama mpagani.
Siku ikapita na asubuhi yake, Neema akatuma meseji ya whatsapp kwa baba yake akimtaarifu kuwa ndege ilighairisha safari yake hivyo alitarajia kurudi nyumbani siku nne mbele. Baba mtu, mzee Benson Swai akaitikia na kutuma voice note ya kumuombea mwanaye safari njema na kuamuru malaika wamlinde.
Cliff alimkumbuka mzee Benson enzi zile walipokuwa kidato cha nne na Neema, yeye alipenda kumuita mkoloni, maana kila alipojaribu kupanga wakutane uchochoroni na Neema, Mzee Benson angetokea na kuzua tafrani. Neema akawa anafungiwa tu hata kutembea akiwa nyumbani alikuwa hawezi. Sehemu pekee Cliff angeweza kuonana na Neema ni kanisani kwa kuwa hakukosa misa; daima na siti yake ilikuwa ya upande wa kulia baada ya benchi za mbele za wanakwaya.
Cliff akawa anajibanza na Neema huko walau, lakini kitu kibaya ni kwamba, baba yake Neema huyo mzee Benson alikuwa pia ni mzee wa kanisa pale kigangoni, na alimzuia Cliff hata huko kanisani ashindwe kupakanyaga. hivyo basi aliposikia voice note ya mzee Benson, Cliff alikumbuka mbali akacheka kidogo huku akimtazama Neema.
"haha mzee wako bwana hivi bado mkali vilevile?" aliuliza Cliff, Neema akakatisha ile sauti ya maombi na kumtazama Cliff aliyejilaza bado.
"Ndiyo, tena kazidi," alijibu Neema akionesha kuwa na huzuni. Cliff akagundua jambo akaropoka.
"Neema, hivi baba yako ndiyo aliyekutaka uwe sista au wewe mwenyewe tu?"
"mh kwanini umeniuliza hivyo?
"hapana naona haupendezi kuwa sista Neema, kiukweli roho inaniuma kukupoteza nilitaka nikuoe ujue.."
"mh, muone! ila ni kweli mimi sikupanga ni baba alinitaka niwe sista; no way ndiyo ilishakuwa tena," alisema Neema akiinuka na kwenda kuoga.
Cliff wakati huo akawasha televisheni kutazama habari za dunia. Huko duniani habari zilikuwa ni kuhusu Corona tu.
Kipindi hicho ndiyo kwanza ilikuwa inasamba ughaibuni, kwa Afrika ugonjwa huo ulikuwa ni ndoto kuja, hivyo hakuna aliyeutilia manani na hata yeye pia aliupuuzia, akamsubiri Neema alipotoka kuoga na yeye akaingia bafuni maana ni uungwana tu kumuacha mpenzi wako aingie bafuni peke yake hasa akiwa katika siku zake ili ajiswafi kwa nafasi sio kumganda kama kupe sugu.
Basi bwana baada ya kuoga wakatoka zao hapo kwenye mgahawa wa hoteli na kunywa chai, Cliff akigharamia kila kitu japo mara kadhaa akatoka kwenda kupokelea simu kwenye gari yake aliyoiegesha kwenye parking akimzugisha mpenzi wake ambaye ni afisa wa polisi Mwanza, Grace,;kuwa bado yupo kwenye vikao hivyo asimpigie sana kisha angerudi kwa Neema kusubiria windo lake akihesabu siku kwa makini kuwa ni siku ya pili hiyo ya Neema kubleed hivyo bado siku mbili tu mbele.
Neema wakati huo naye alikuwa akichati na simu na kukwepa macho ya wanaume wa kizungu waliofika hotelini hapo wakishangaa kumuona mtoto wa kike mzuri wa kipekee akiwa ameketi peke yake, lakini kabla hawajafanya jitihada kumsogelea, Cliff angetokea haraka na kuketi karibu na Neema; goma lake.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment