Chombezo : Nyoo Nipe Mumeo
Sehemu Ya Tatu (3)
“Kiukweli, mimi niliingia kuchezwa nikiwa mdogo kuliko wote pale ndani nilikuwa na miaka 7 na sikuwa na akili kabisa hivyo sikuyatilia maanani yote niliyofundishwa, kuliko Fatuma yeye alikuwaga ndo mkubwa wetu na alikuwa Mwali kigego.”
“Mwali kigego? maana yake nini!”niliuliza maana alikuwa amenichanganya tayari kwa Kiswahili.
NYOO NIPE MUMEO 32
“Mwali Kigego ni msichana aliyeanza michezo ya wanaume na kutolewa bikra kabla hajachezwa,”
“Mh! kwahiyo Fatuma alikuwa mtambo tangu zamani?” niliuliza.
“ndiyo lakini elimu ya mapenzi hasa na jinsi ya kumridhisha mwanaume hakuna sehemu aliyojifunzia zaidi ya pale unyagoni,” alisema Hadija.
“kwa hiyo shoga wewe mambo yote uliyofundishwa unyagoni, umeyasahau na haujawahi kuyafanya kwa mumeo?”
“Kiukweli, sikuwa naona umuhimu wowote, nilijuaga mwanaume akikupenda na kukuoa ndiyo anakupenda tu ili mradi umtimizie haja zake, sasa kumbe tuliyofundishwa yana umuhimu wake. Yaani huyu Steve ndiyo kanifumbua macho kumbe wanaume wanapenda kweli haya mambo?” alisema Hadija akionekana kweli kufunguka kiakili.
“Sasa Hadija naomba unisaidie kumpata huyo Kungwi,”
“ngoja nimpigie dada Hawa Mtwara nimuagize anitafutie huyo bibi,” alisema Hadija na kunyanyua simu yake akipiga na kuanza kuongea Kilugha kisha baadaye akamuelezea kuhusu huyo Kungwi ndiyo nikasikia jina lake anaitwa Bibi Gululi. Akamuagiza huyo ndugu yake amtafute siku hiyohiyo ili aongee naye, kisha akakata simu na kunitazama, akaniambia:
“Sikia Mary, hapa unaponiona tangu nimeachana na mume wangu sijaweza kuolewa tena nimekuwa mtu wa kutongozwa na nikitembea na mwanaume tu mara moja mbili ndio basi hanitaki tena. Hata mimi mwenyewe nataka kujifunza hayo masakarasi nimrudishe mume wangu aka mwenzangu tupo wote!” aliongea Hadija angalau nikafurahi nimepata shoga mwenye shida kama yangu.
Basi baada ya mazungumzo ya hapa na pale, tukaagana mimi nikarudi zangu nyumbani nikaanza kuwaza kuwa kama itatokea huyo Kungwi Bi. Gululi akatutaka twende huko Mtwara itakuwaje? Mume wangu atanielewa kweli? Mh na hapa Bongo tuna mwezi mmoja tu wa kukaa kabla ya kurudi, nikajiuliza hayo masomo yatachukua siku ngapi? Nikajihisi nimekurupuka. Nikafikiria na kuona mbona najihangaisha wakati tukimaliza shughuli za sherehe yetu ya utambulisho tunaondoka zetu Marekani, huyo Fatuma atampatia wapi mume wangu?
NYOO NIPE MUMEO 33
Nikawa njia panda, nikimsikilizia Hadija kuwa kama akimpata huyo Kungwi nitafanyaje au nimwambie aache kwanza, ili mradi siku ziende nikimvumilia Fatuma hadi siku nitakayoondoka na Mr X wangu.
Nikiwa nafikiria hayo nikagundua mume wangu hakuwepo nikamuuliza mama.
“Aliniaga hapa muda si mrefu, nilijua mmepishana hapo nje maana hata barabarani hajafika.” Sijui hisia gani zilipita akilini nikainuka harakaharaka na kuanza kukimbilia nje uelekeo wa barabarani harakaharaka. Nikala kichochoro cha kwanza cha pili nikashtuka kumuona Fatuma kwenye duka moja la vitenge pale barabarani, na mume wangu alienda hapohapo kwenye duka.
Nikabana kuangalia nini kinachoendelea. Huwezi amini niliona Fatuma akichagua doti ya Khanga, halafu mume wangu akatoa hela kutoka kwenye waleti na kulipia. Alimaliza bila kuongea chochote na Fatuma akaanza kurudi huku Fatuma akiondoka na njia yake.
Sikutaka kuamini nilichokiona nikajikausha na kukimbia haraka nyumbani kwa kuwa mume wangu nilimuona akiwa anarudia njia ileile.
“Hi honey how ‘ve you been?” alinisalimia mume wangu na kunibusu akaja kukaa pembeni yangu kwenye kochi akinipetipeti, japo nilikuwa na hasira mno lakini nilitulia kimya nikimtazama tu.
“Unajua nini mpenzi? Ningependa tuongeze siku za kukaa hapa nyumbani hata miezi mitatu hivi mbele,” alisema Jermaine. Mama yangu! nikajua Fatuma tayari kaishanimalizia mume wangu.
“Unasemaje?” niliuliza kwa ukali.
“yah itabidi tukae kidogo niendelee kuwajua ndugu zako, halafu huku kumenivutia sana,” alisema mume wangu nikaanza kukumbuka maneno ya Steve nikajua hamna lolote hapo huenda na mume wangu anamuwaza Fatuma tu na misuguo aliyoipata.
Akyanani, nikakata shauri hata kama Kungwi yupo mwezini au sayari nyingine nitamfuata tu hadi huko, Fatuma siyo mtu wa kumuacha hivihivi.
Itaendelea..
NYOO NIPE MUMEO 34
Nakumbuka siku hiyo nililala nikiwa nina donge zito moyoni sikuwahi kuwa hivyo tangu nizaliwe. Hata nilipopitiwa na usingizi sikuwa najijua. Hatimaye niliamka asubuhi nikiwa nimechelewa mno tofauti na siku nyingine ambapo huwa naamkaga mapema na kwenda kutayarisha kifungua kinywa na kumuogesha Kendrick.
Siku hiyo nadhani mama na dada ndiyo walikuwa wanachakarika jikoni maana nilisikia kukurukakakara za vyombo. Wakati naenda nikasikia mama anaongea: “ndiyo hivyo nakwambia ole wako umwambie Mary, kama hauna kifua sema kabisa mapema, sitaki familia ivunjike kwa sababu yako! Umesikia!”
“Nimesikia ndiyo, lakini mimi nahisi Mary anajua, wewe unafikiri rafiki zake hawajamwambia hadi leo!” alisema dada nikajiuliza wanachoongelea ni nini?
“Hajui chochote, rafiki zake wote niliwaonya kama ninavyokuonya wewe. Siku ile yeye alikuwa amelewa na mapema kabla ya tukio alirudishwa kulala, usitafute sababu ya kumwambia!” alisema mama akionekana hana utani hata kidogo kwa aliyokuwa akiyaongea.
Hapo moja kwa moja akili yangu ikanituma kuwa ilikuwa ikizungumziwa siku ambayo nililewa na kurudishwa nyumbani, nikajiuliza huenda tukio la mume wangu kufanya mapenzi na Fatuma kule kwenye migomba lilijulikana na hapo familia nzima ilikuwa inanificha.
Kumbe ndiyo maana hata wakina Cathe walikuwa wakisitasita kunijibu, nikajisikia aibu yaani kama vile nimevuliwa nguo, yaani ilikuwa bora hata mume wangu angetembea na huyo Fatuma na watu wasijue lakini wameshajua jamani kumbe nikitembea wenzangu wananichora tu.
Nilipanda hasira ile mbaya, ubaya zaidi hasira zangu zikinipanda sitakagi kula wala kuongea na mtu.
Je, ingekuwa wewe ni Mary ungefanya nini?
NYOO NIPE MUMEO 35
Siku hiyo lile donge nililolala nalo jana likarudi na kuzidi, machozi yakanitoka kama mtoto mdogo, sikuamini kama Fatuma angeweza kuniliza hata siku moja tena kwa kunizidi mapenzi.
Mama aliyekuja ndani, aligundua ninalia, akawa anajishtukiashtukia akaja kunibembeleza, nikatamani kumwambia ukweli lakini nilimuacha tu kimya aendelee kunibembeleza.
“mwanangu vipi? Mumeo kakuudhi au? Nieleze mimi mama yako?” alisema mama kwa sauti ya upole lakini mimi nikamtafsiri kama mnafiki tu, yaani kumbe mume wangu anachepuka na yeye ananificha tu! au mume wangu kuwa Mmarekani wao wanaona wamuogope? Nikajiuliza au aliwaomba radhi? Lakini kama aliwaomba radhi kuwa hatarudia tena mbona jana nilimuona tena na Fatuma kule dukani!
Mama akanibembeleza akashindwa na kwenda kumuamsha Jermaine, naye si akaja hadi ndani, akaanza kunibembeleza, kunibusu na kunikumbatia lakini wapi sikuwa vizuri kabisa nilimuona kama siyo mwili mmoja na mimi, hata harufu ya jasho lake ilinikera nilihisi imechanganyika na ya jasho la Fatuma, mate yake wakati ananibusu nilijifuta kwa kuwa yalikuwa na shombo la Fatuma.
“Jermaine niache sitaki! Jus leave me alone!” nilimfukuza mume wangu kwa hasira pale chumbani, akashangaa lakini aliniheshimu akatoka, mama akiwa ametoa macho kwa mshangao.
Wakati huo nikawaza huenda Fatuma akamshawishi Jermaine aniache mimi nyumbani na kutoroka naye kuelekea Marekani maana hashindwi yule malaya! Wazo hilo lilinijia na kunishawishi kuwa huenda ni kweli kabisa.
Nikajizoazoa pale kitandani na kwenda kuichukua paspoti ya kusafiria ya mume wangu na kuificha, nikaenda kuoga na kidogo nilipoa. “shoga upooo!” ilikuwa sauti ya Hadija kwenye simu.
“nipo, vipi!” nilimjibu kwa sauti ya kinyonge akaonekana kunionea huruma akaanza kunibembeleza na kudai hata yeye alikuwa kama mimi baada ya Fatuma kumchukulia mume wake.
NYOO NIPE MUMEO 36
“Sikia nimekupigia kukwambia kuwa yule bibi nimempata na kwa bahati nzuri yupo hapahapa Dar kwa mwanaye,” alisema Hadija moyo wangu ukaripuka kwa furaha kidogo.
“Hee yupo wapi?”
“yupo Chanika. Nimeongea naye nimemwambia tatizo amesema twende, sasa muda wako tu wewe shosti,” alisema Hadija, sasa kwa nilivyokuwa nimevurugwa nikamwambia zege halilali siku hiyohiyo nilitaka kwenda.
“Hee! Leoleo mbona kazi, mimi ndiyo kwanza nimefungua duka na sina mtu wa kumuacha hapa!” alisema Hadija.
“sikia nitakupa hela unayoingiza kwa siku ili mradi tu unipeleke leoleo,” nilimwambia basi hakuweza kubishabisha tena, akanipigia simu nikamuelekeza nyumbani kwetu akaja nikamkutanisha na mama, baba, mume wangu na dada nikadanganya kuwa naelekea kwenye party ya birthday ya rafiki yetu wa zamani.
Mume wangu alikubali mara moja, tena akatupa na hela ya kukodi taksi.
Basi tukiwa njiani, Hadija alianza maneno yake.
“Mh shoga mumeo kama ndiyo yule roho lazima ikuume!”
“unamaanisha nini?”
“wewe si unamuona mwenyewe anavyovutia, kama wale wanaume kwenye mabango ya matangazo! Mh hata kama mimi ningekuwa Fatuma ningekupindua.”
“nini? Hadija usitake kuniudhi tutagombana!” niliwaka kwa hasira na kutojiamini.
“sikia nakutania bwana, enhe niambie kwani yule mwingine ndiyo baba yako?”
“ndiyo, kwani vipi?”
“mh shoga nikwambie ukweli japo kuwa utakasirika, yule mzee alishawahi kunitongozaga, sema tu nilimkataa kwa sababu hakuwa na hela, ila nasikia akiwa na hela anatawanya ile mbaya,” alisema Hadija. “nini! acha uongo wako Hadija. Sitaki nikusikie ukimuongelea vibaya Dady umesikia?”
“ukubali ukatae ukweli ndo huo, mkimtumiaga hela huko Marekani mwenzenu anazimalizia kwa visichana vidogo tena mwendo wake ni wa dolari tu,” alisema Hadija huku akisimamisha taksi tukapanda na safari ya kuelekea Chanika ikianza huku maneno ya Hadija yakinivuruga kweli. “Mh Baba yangu hapana!”
Baada ya kushuka mwenzangu akaanza kuongea na simu kwa ajili ya kuelekezwa kwa kwenda, basi palepale kituoni Chanika Mwisho tukasubiri, akatumwa mtoto mmoja hivi akaja kutuchukua, tukaanza kuingia ndanindani.
Kwa umbali wa dakika chache tukawa tumefika kwenye nyumba moja iliyomaliziwa vyumba viwili tu huku upande mwingine ukiwa na nyumba ya udongo.
Tukamsalimia mwenyeji wetu ambaye ni mdada mmoja hivi saizi yetu mimi na Hadija. Yule mdada akiwa ametuchangamkia akatueleza kuwa Bibi Gululi alikuwa anaoga hivyo tumsubiri hapo sebuleni. Sasa mimi akili yangu ikadhania kuwa huyo Bibi Gululi alikuwa bibi haswaa, lakini nilishangaa alipokuja maana japo alikuwa mtu mzima lakini hakuwa mzee kiasi hicho.
Alipofika alitusalimia lakini kwa Hadija alimchangamkia kweli hadi wakakumbatiana nikathibitisha kuwa kweli walikuwa wakifahamiana kwa muda mrefu, basi akatutaka tusubiri mara moja wakati yeye anaingia ndani na kuvaa.
Kilichonishangaza mimi ni kwamba yule bibi akiwa hukohuko chumbani, nikasikia akimuita yule mdada na kumtaka ampelekee moto kwenye chetezo, alipopelekewa nikasikia harufu ya udi ukifukizwa.
Hadija aliyejiachia pale ndani kama kwake, akasema kwa sauti; “Mh Bibi Gululi kumbe na wewe haujambo?”
Yule bibi hakujibu kitu hadi alipotoka, akiwa amependeza ndani ya dela lake huku kichwani akiwa amejifunga kilemba vizuri.
“Hadija! Mwanamke usafi mwanangu.” Alisema Bibi Gululi na kuja kukaa kitako kwenye kigoda, sisi tuliokaa kwenye viti kwa heshima tukashuka chini na kukaa kwenye mkeka, yule mdada aliyetukaribisha mwanzo naye akaja na kukaa pale chini na sisi.
“Enhee wanangu niambieni, kipi kilichokunyanueni miguu yenu kuja hapa?” aliongea Bibi Gululi, ikabidi nimuachie mwenzangu aongee na kuanza kwa kunitambulisha.
NYOO NIPE MUMEO 38
“Bibi, nadhani unanikumbuka nilikuwa mkoleni Masasi, mwaka 1999 kipindi kile cha Mwenyekiti Abdarahmani,” aliongea Hadija, Bibi Gululi akacheka na kumkatiza akisema; “Ha! We Hadija nikusahau mie! Umenichukulia mzee sana au?”
“Mh haya! bib, huyu ni mwenzangu niliyekwambia anaitwa Mary, tumekuja kwa ajili ya yale matatizo na wewe tu ndiyo wa kutusaidia,” alisema Hadija.
“Karibu Mary,” alisema Bibi Gululi akatutambulisha yule mdada tuliyekaa naye kuwa ndiye Gululi mwenyewe ambaye ni mwanaye. Basi yule bibi akawa kila akiongea ananiangalia sana mimi hadi nikaona aibu.
Ikabidi Hadija aanze kumuhadithia mwanzo mwisho kuhusu masahibu yake, na mimi ikabidi nimuelezee yangu, lakini alishtuka baada ya kujua kuwa Fatuma ndiye aliyetuliza wote wawili.
“Fatuma yuleyule mwali kigego?” aliuliza Bi.Gululi kwa mshangao.
“Ndiyo huyohuyo bibi, amekuwa moto wa kuotea mbali, fisadi wa kuvunja ndoa za watu huko mtaani,” alijibu Hadija.
“Mh! Kazi ipo?”
“kwa hiyo wewe Mary, haujawahi kuchezwa?” aliniuliza Bibi Gululi.
“kwetu hatuchezwi bibi.”
“anhaa! Hee poleni wanangu poleni sana,” alitupoza moyo Bibi Gululi, akaanza kutuambia mengi kuhusu umuhimu wa mwanamke kuchezwa na kuzingatia mafunzo yote baada ya kuolewa. Akatuambia kuwa hata mwanaye Gululi naye alikuwa na tatizo kwenye ndoa yake maana mumewe kamtelekeza na mtoto ndilo hasa jambo lililomfanya yeye aje hapa Dar kwa ajili ya kumfariji.
Nikajiuliza inakuwaje mtoto wa Kungwi naye akaachika au ndo ukaribu wa Kanisa sio ndiyo kusali sana. Bibi Gululi kama alijua mashaka yangu akasema kuwa Gululi naye ni kama mimi hakuchezwa kwa sababu alikuwa akiumwa sana kipindi cha usichana wake. Akakumbuka kuwa hata Hadija alikuwa mdogo sana kiumri hivyo kuibiwa mumewe na wanawake wajanja kama Fatuma ilikuwa ni jambo la kawaida tu. Kwa hiyo wote hapo tulikuwa sawa tu.
NYOO NIPE MUMEO 39
“Kwa kifupi mimi nimekubali nitawafundisha kila kitu nyinyi ni watu wazima, hivyo natarajia mtajifunza haraka sana ndani ya wiki tu tutakuwa tumeshamaliza kutegemea na ratiba yenu. Ila mna kazi kubwa kama mtu mwenyewe mnayeshindana naye ni Fatuma huyuhuyu niliyemfunda mimi.”
“Bibi kwa nini unasema hivyo?” niliuliza maana niliona ananikatisha tamaa.
“Fatuma kwanza alipokuja kwenye Chiputu changu hakuwa mtoto kama wengine alikuwa ameshavunja ungo miezi sita kabla, pia niligundua kuwa mama yake aliwahi kumpeleka unyago wa Kizaramo kabla ya kuja kwangu, kwa hiyo alikuwa mtundu sana wa kuuliza maswali ya vitu ambavyo alikuwa havijui nadhani kilichomsaidia sana kingine ni kutokana na yeye kuanza mambo ya kikubwa mapema, ndiyo maana akapewa hilo jina la mwali kigego,”
“Mh sasa kwani bibi wewe ulimfundaje huyo Fatuma sisi ukashindwa?” aliuliza Hadija.
“Itabidi nisiwafunde kwa utaratibu wa Kimakonde peke yake, nitatumia utaalamu wote wa pwani ninaoujua na nyinyi inabidi mjifunze sana,” alisema Bibi Gululi nikamtazama Hadija naye akanitazama mimi, wote tukakubali kuwa hatuna budi kufanya anachotuambia.
“Sawa wanawali wangu, kwa kuwa nilikuwa pia na mafunzo ya mwanangu basi itabidi niwaunganishe wote watatu, lakini leo kwa kuwa mmetoka mbali nataka msiondoke bure. Nitamuita mmojammoja ndani ili niwakague kwanza.” Alisema Bibi Gululi huku akiamka na kuingia kule ndani.
Akaanza kumuita Hadija, wakakaa kama dakika tano hivi kisha Hadija akatoka. Akafuatia kumuita mwanaye naye hivyohivyo akakaa dakika tano, kisha nikafuata mimi.
Nilipoingia akaniambia nilale kitandani halafu nimuoneshe uchi wangu, nikashangaa lakini nilifanya kama alivyoniambia nikapandisha gauni kwa juu na kuvua chupi kisha nikatanua miguu, huku akikunja sura, akaniambia nivae.
“unatumia nini kunyolea bustani yako?” aliniuliza Bi. Gululi.
“natumia kiwembe.” “mh ndiyo maana,” alisema Bibi Gululi nikawa ninastaajabu kwa nini aliniambia maneno hayo na kwanini alikunja sura wakati aliponiangalia uchi wangu.
Je, ni kwanini? usikose kesho..
NYOO NIPE MUMEO 40
“Mwali wangu unakosea sana, wewe hauoni ulivyokuwa na rasharasha kama kuku ametoka kunyonyolewa, halafu kipapito kimechunjuka kama siyo mrembo bwana aah,” alinisema Kungwi Bibi Gululi nikashangaa mbona mimi nilijiona msafi tu kuanzia sura hadi uchi wangu.
“Ngoja nikuoneshe,” alisema Bibi Gululi akapandisha gauni lake na kulala pale kitandani utupu akaniambia; “haya niangalie mimi.
Mh jamani japo kuwa alikuwa mtu mzima lakini nilipochungulia niliona kile kipapito chake kikiwa kumeumuka vizuri na kilikuwa na ngozi kama ya mtoto mdogo, yaani hakuwa na unywele wala kijipele kilichochomoza, tofauti kabisa anavyoonekana kwa nje. Mh kweli wanawake wa kimakonde noma.
“Usiogope, papasa kwa mkono hapo juu kwenye ngozi ya bustani uone kama kuna urashirashi wowote wa nywele,” alisema Bi. Gululi basi nikapeleka mkono wangu kwa woga na kupapasa, yaani alikuwa mlaini hadi nikashangaa. “mwali wangu, wenzako wote wapo kama mimi, lakini wewe tu ndiyo nimegundua upo tofauti, tatizo unanyolewa wembe na hayo madawa yenu sijui shevu! si vizuri kwa mwanamke kwa sababu unapoteza umbo la kipapo chako kinatakiwa kitune vizuri kivutie mwanaume hata kwa kukiona tu.” Alisema kungwi wangu akawa amenichanganya.
“Ina maana bibi, mimi changu hakijatuna kwa sababu ninanyolea wembe?”
“ndiyo mwali wangu, wenzako wakiwa ndo kwanza wamelumuka mwogo yaani wakiwa wamevunja ungo na kuota vile vimalaika vya kwanza tu, hupakwa jivu au asali mbichi halafu hunyolewa kwa kuvivuta vyote na Likolo wake, na hivyo ndiyo wanatakiwa kunyoa siku zote, ili kushepu kitumbua chako kiumuke vizuri, kiwe na ngozi laini na hata nywele zinachelewa sana kuota,” alisema Kungwi wangu.
“Mh makubwa! sasa mimi mtu mzima, kweli kinaweza kuumuka kama wewe kama nitanyoa unavyosema?” niliuliza kwa shauku kweli.
“mh hilo sina uhakika nalo nisikudanganye.”
NYOO NIPE MUMEO 41
Basi baada ya kuniambia hivyo tukatoka pale sebuleni kwa wenzangu, kichwani nikawa nakumbuka maongezi ya Steve aliposema kuwa alikiona kitumbua cha Fatuma kimeumuka tena kina meremeta. Hakika kinaweza kuwa sawa na cha Kungwi pamoja na akina Hadija kama nilivyoambiwa.
Sasa nikajisikia mpweke kuwa ni mimi pekee ambaye ndo sina kitumbua; sijui nina chapati maana nilikuwa flati tu hapa juu.
“wanawali wangu, mwanamke yoyote anautamu tofautitofauti kutegemea na Mungu alivyomuumba, lakini kikubwa inategemea na alivyofundwa kwa sababu hakuna mtu anayezaliwa na kujua tu mapenzi bila kufundishwa.
“Utamu wa mwanamke unatengenezwa kwanza na kauli yako mwanamke kwa mumeo, pili sauti yako muwapo faragha, tatu muonekano wako kuanzia mavazi, urembo na vikolombwezo kibao, lakini cha nne wanamwali zangu ni utundu wa juu ya kitanda.
“Mungu kamuumba mwanaume vizuri sana, yaani hana shida yeye kama vile mtoto tu, anachokiona anakitamani anakitaka kukishika na kukitia mdomoni, akikiona kitamu hata akikinai, kesho atarudi tena mwenyewe.
“sasa nyie wanawali wangu mnatakiwa mjue akili hiyo ya wanaume, na ubaya zaidi kwenu, najua wote hapa mna watoto, na mkishazaa mnajua lazima kule ndani kuwe kumetanuka tofauti na mlivyokuwa zamanii.
“tena vifua vimekushukeni na shombo maziwa ikiwa ndio harufu yenu, wakati huo kumbuka zamani ulivyokuwa unavutia mwali mbichii. Hapa ndiyo wanaume wanakosaga uvumilivu na kulazimika kuchepuka tena kwa wasichana wadogo nje huko.
“Sasa tatizo lisiwe ameenda kwa mtu fundi kama Fatuma huyo ndio harudi tena,” alisema Kungwi yote nikaona kama madongo kwangu nikawa na wasiwasi hivi ndo tangu nizae nimekuwa siyo mtamu tena kwa Mr X kama mwanzo, kwa sababu kipapito changu kimelegea au? Nikiwa najiuliza hayo Kungwi aliyekuwa akiendelea kuongea yake akaongea pointi moja kubwa ambayo ndiyo nilikuwa nikiisubiria kwa hamu.
NYOO NIPE MUMEO 42
“lakini pamoja na hayo yote wanamwali wangu, Mungu kaumba vitu ambavyo vitakusaidia kurudisha heshima yako kitandani na kuonekana mbichi kama vile haujazaa, uke wako utakaza kama kawaida, nitakufundisha jinsi ya kujiswafi, jinsi ya kummudu mwanaume, kiasi kwamba hata huyo Fatuma ataonekana upuuzi mtupu mbele ya waume zenu. na kwako mwanangu Gululi huyo mumeo atarudi mwenyewe tena kwa kukupigia magoti,” alimaliza kusema Kungwi wetu kidogo nikapata moyo sasa.
Tukaagana kwa makubaliano ya kurudi kesho yake tena tukapanga muda mzuri wa kuanzia saa tano asubuhi hadi saa nane, wakati tunaagana nikafungua mkoba wangu na kumkabidhi kungwi shilingi elfu ishirini ya soda, akafurahi mno na kutusindikiza hadi barabarani.
Tukapanda teksi hadi nyumbani, njiani kote nikiwa ninafikiria jinsi ya mimi pia kuwa na kijitumbua na ngozi laini kama vile Kungwi, Hadija, Gululi na Fatuma tena kwakuwa nilikuwa ndiyo kwanza zilianza kuota basi nikaona ngoja nikanyoe nikirudi tu nyumbani.
Nilimwacha Hadija dukani kwake nikampa shilingi elfu thelathini kama gharama ya kukatisha mauzo yake ya siku na nilifika nyumbani na kumkuta mume wangu na baba wakiwa wanaongea pamoja, mume wangu akionekana kama vile anapinga jambo fulani kwa nguvu huku baba akimlazimisha, lakini nilipofika tu walibadilika na kujifanya wananichekea.
Nilijua hapo lazima walikuwa wakiongelea uchafu wa mume wangu tu na Fatuma, na waliponiona walikaa kimya ili eti nisijue chochote. Nilikasirika mno, nikapita zangu na kwenda kumtazama mwanangu Kendrick.
Baadaye nikachukua jivu jikoni na kuingia nalo chumbani nikajipaka vizuri na kusubiri nusu saa kama nilivyosikia kwa kungwi, tena mimi nikakaa lisaa lizima. Kisha nikaenda bafuni na maji yangu ya kuoga lakini lengo langu kubwa likiwa ni kujinyofoa vivuze vyangu niwe na kitumbua kinono.
Je, Mary atafanikiwa? Itaendelea..
NYOO NIPE MUMEO 43
Nilianza kwa kukivuta kinywele kimoja lakini aisee maumivu yake siyo mchezo, nilitamani kulia kwa jinsi kilivyouma, nikahisi nimetoka hadi na damu.
Nikajaribu kingine tena lakini hapana kiliuma kuliko kile cha mwanzo, sasa hicho ni kivuze kimoja tu ndiyo kiliuma hivyo sembuse kuvimaliza vyote ambavyo vipo zaidi ya milioni, hapana zoezi lilinishinda.
Tena pale nilipokinyofoa kile kivuze cha kwanza pakawa panavimba nakufanya kipele. Aisee ikabidi tu nioge zangu na kutoka chooni nikiwa nachechemea maana si kwa maumivu yale.
Nilirudi chumbani nikiwa nimekata tamaa kabisa ya kuwa na kipapito chenye mvuto kama wenzangu.
Nikaona kama Fatuma kapendewa hicho basi atanishinda tu. Nikarudi zangu chumbani na kuanza kujifuta na taulo huku nikijitazama mbele ya kioo nilivyoumbika.
Kwani lazima kila mwanamke awe na kipapito kilichoumuka kama Wamakonde waliochezwa! Nikajiangalia vizuri kipapito changu na kugundua kuwa mbona kilikuwa kizuri tu, ingawa hakijatuna. Tena kilikuwa kimebana kama vile herufi ‘w’, kiyoni changu kilikuwa kimejificha vizuri katikati na kikisimama kinachomoza vizuri kiasi kwamba enzi hizo Mr X alipokuwa akininyonya alikuwa haishi kunisifia jinsi nilivyokuwa na kipapito kizuri.
Tena mapaja yangu hayakubana yalikuwa yameacha kiuwazi fulani pale karibu na mlango wa bibi, nilikuwa na matege fulani hivi amaizing, ukichanganya na shepu yangu hakika mimi mzuri.
Au labda nilikuwa nimepungua tu huo utamu! au labda huyo Mr X alikuwa amenichoka tu hana lolote. Niliwaza yote hayo huku nikigeukageuka kujitazama kwenye kioo.
Hata hivyo maneno ya kungwi, kuwa baada ya kuzaa utamu unapungua kwa sababu njia inakuwa imelegea, yalikuwa yakinichanganya kweli, ikabidi nijitest kwa kujiingiza kidole kidogo na kupima ukubwa wangu ndani nikaona kukubwa kweli. Lakini kwa mdudyu wa mume wangu mbona niliona ananifiti tu vizuri ndani au inakuwaje? Nikapanga swali hilo nikamuulize Kungwi kesho.
NYOO NIPE MUMEO 44
Basi nikavaa zangu kanga na kulala kitandani na mwanangu, jioni hiyo nikapitiliza hadi usiku tena ndugu zangu ndiyo walikuja kuniamsha kwa chakula cha usiku. Wakati nilipotoka mume wangu alionekana kuwa na wasiwasi sana na mimi, akajua huenda nimepatwa na jambo.
Akanipakulia chakula na kunitaka twende kukaa uwani, basi akanishangaza kwa kuanza kunilisha chakula huku akinibembeleza kwa mahaba mazito hadi akanikumbusha enzi zetu zile.
Nilijua lazima tu alikuwa akijikomba tu maana wanaume wengi pindi wanapowasaliti wake zao hujifanya wanamapenzi sana utakuta hata kama hakwambiagi; I Love U, siku hiyo utasikia I Love U au atakuletea vizawadizawadi ili akuzuge usimshtukie.
Sasa nikaanza kujiuliza mume wangu alikuwa ametokea wapi siku hiyo maana niliporudi jioni sikumkuta au ndo alikuwa ametokea kufanya uzinzi na Fatuma?
Basi wakati yeye akiniongelesha maneno yake pale nje akinisifia na kujiapiza kunipenda siku zote za maisha yake, mimi kichwani nilikuwa navuta picha yeye akifanya mapenzi na Fatuma hasira zikanipanda.
“Hapana haiwezekani!” nilijikuta nikisema na kuinuka kwa hasira pale nilipokaa hadi mume wangu akashtuka na kuniuliza kulikoni.
Akanifuata pale niliposimama na kunitaka nimwambie kinachonisibu. Kwa wivu na uchungu niliokuwa nao nikatamani nimfungukie kuwa najua kila kitu wanachofanya na Fatuma, lakini nikakumbuka maneno ya mama aliyoniambia kuwa napaswa kuwa mvumilivu yakanijia nikatuliza hasira zangu.
“Hamna sina kitu!” niliongea maneno hayo huku machozi yakinitiririka.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment