Search This Blog

Monday, January 24, 2022

NINAH - 3

   

Chombezo : Ninah

Sehemu Ya Tatu (3)


“Asante!” niliitikia kwa aibuaibu. Akafurahi kuniangalia tu, lakini mara nyingi alikuwa akinitazama na kuonekana kupotea kwenye dimbwi la mawazo mno na kuwa si mwenye furaha kabisa.

Hali hiyo nilikuwa nikiiona kwake mara nyingi sana lakini alichonishangaza siku hiyo tulipokuwa kitandani alinitaka nilale na bikini alizoninunulia siku hiyo; kwa hofu nilivaa lakini angalau moyo wangu ukapoa, nikajua mwanaume amerudi. Nilipoingia kitandani alinipapasa kwa muda nikakolea, lakini alichonishangaza akageukia tu pembeni na kuwa mwenye mawazo tena.

Sasa nikafikiria na kuona si muda mzuri wa kumuomba ushauri niliokuwa nautaka kuhusu Brighton, cha zaidi pengine nimuulize kitu kinachomsumbua.

“Mr Edgar, nini tatizo? Mbona unakuwaga hivyo kila mara?” niliuliza.

“Ninah, nadhani umekuwa ukijiuliza mara kwa mara, kwanini nimekuwa na wewe pamoja na uzuri wako wote tunalala, lakini sikufanyi chochote.” alisema Mr Edgar. Nikaitikia kwa kutikisa kichwa tu.

“Tafadhali naomba unisikilize na unielewe, kwa sababu sijawahi kumwambia mtu yoyote mambo haya. na nikikwambia lakini sitaki uvujishe kwa sababu nitakasirika na nikikasirika naweza ku..kuku.. Ah tuache tu!” alisema Mr Edgar akibadilika kabisa sura hadi nikaogopa.

Lakini nilimbembeleza anieleze na kumhakikishia siri yake nitaitunza kifuani daima.

Aliponiambia nilisikitika mno .sikuamini na hapo ndiyo nikajua kwanini Mr Edgar yupo tofauti na wanaume wengine. Ama kweli dunia ina mambo!

FANYA KUKISIA MR EDGAR ALIMWAMBIA NINI NINAH?

Itaendelea


NINAH 25

“Nilikuwa zamani, lakini sasa hivi mimi siyo mwanaume tena,” alianza kusimuliza Mr Edgar. Nikashtuka alimaanisha nini kwa kusema vile.

“Ninah siwezi kufanya mapenzi na mwanamke nina matatizo, siwezi kusimamisha ndiyo maana nimekuwa hivi siku zote. Naomba sana unifichie siri hii,” alisema Mr Edgar nikajikuta namsikitikia mno.

Akanieleza kuwa kumbe chanzo cha kugombana hadi na mkewe ni yeye kutokuwa na uwezo wa kusimamisha, lakini uzuri siku hizi kulikuwa na vifaa mbalimbali vyenye shepu ya uume uliosimama ambao unavaliwa na mwanaume na kufanya mapenzi na mwanamke, ingawa hakuna unachojisikia kwakuwa ni kwa ajili tu ya kumridhisha mwanamke.

Mr Edgar alinisimulia kuwa mkewe alijifanya kuridhia hali hiyo lakini kumbe alianza tabia ya kumsaliti kimyakimya, mbaya zaidi akaanza kumtangazia matatizo yake kwa wanaume zake na hiyo ndiyo sababu kuu iliyomfanya Mr Edgar aombe uhamisho na kuja nchini.

“Najua wewe ni mpenzi wa Brighton na kama mwanamke uliyekamilika utashikwa na hamu na utahitaji mtu wa kukufariji. Sitaki ukose hilo naomba endelea tu kuwa na Brighton, usimsaliti, lakini nakuomba uwe na mimi kama wapenzi, naomba pia niwe ninakuchukua na kukupeleka out na kwenye ghafla mbalimbali lakini niwe na kutambulisha kama mpenzi wangu ili angalau watu wasinitasfiri vibaya na sifa yangu iendelee kuwepo,” alisema Mr Edgar.

Nikashusha pumzi na kukubali kuwa nitamsaidia, kwa jambo hilo akafurahi mno na kunibusu shavuni na kunikumbatia, akaniambia kuwa naye kitandani kunampa faraja mno. Tena usiku huo na kuanzia hapo hakuwa na unyonge tena.

Siku zikakatiza sasa kweli nilikuwa na hamu ya mapenzi na Brighton wangu na sikuweza tena kuvumilia tena ile mipapasopapaso ya Mr Edgar ilinivuruga na kunijaza hamu tele. Nilichofanya siku hiyo, nilimtaarifu mapema Mr Edgar kuwa nitaenda kwa Brighton tena mwenyewe alinipa baraka zote na kunipa hela zakutosha nikakodi usafiri hadi Tandale.

Mtaa mzima nilivyopita wale mashoga zangu walinishangaa, hawakuamini kama ni mimi, wengine walidhania ni dada yangu au ndugu yangu, lakini nilivyoongea tu wakajua ni mimi.


NINAH 26

“Enhee shoga kulikoni umepata mshefa nini?” aliuliza mama Sele akiwa anakaanga miguu ya kuku, biashara niliyokuwa nikiifanya mwezi mmoja tu uliopita.

“mshefa wapi, maisha tu.” Nilisema.

“Loh lakini sio kwa kupendeza huko. Naomba basi elfu tano mwenzio nadaiwa Vicoba.,” alisema mama Sele. Nikafungua pochi na kumkabidhi.

“Vipi huyu mwanaume yupo humo ndani?”

“Yupo hajaamka nadhani, maana jana alikuwa bwii anakuimba tu ooh Ninah wangu. Ninah wangu! Mara mkufuu mara mkufuu,” alisema Mama Sele na kutia chumvi humohumo.

Nikainuka haraka na kuusukuma mlango ukafunguka manuu, nikatupia jicho ndani, nikamuona Brighton amelala tu kwenye godoro sakafuni, ndani vitu vyote hamna huenda ameuza kwa ajili ya pombe.

Nilimuamsha, aliponiona tu na wenge lake la pombe likamtoka, alikuwa amekonda hatari na mchafu mno, nikajifunga kitenge mtoto wa kike na kwenda kumuogesha nikamrudisha chumbani nikamvalisha nguo na kumtoa mle ndani.

Tukapanda taksi hadi La Vista Inn pale Magomeni nikaagiza chakula tukala na yeye alikula mno, sasa alionekana kuwa na nguvu, akanitazama machozi yakimtoka.

“Ninah naomba nisamehe mpenzi wangu!” alisema Brighton na kupiga magoti mbele za watu, nikamuinua na kumkalisha kwenye kiti. Nikishindwa kujizuia hata mimi mwenyewe kulia.

Ilikuwa ni stori ya kusikitisha mno. Basi nikachukua chumba palepale hotelini na kuingia naye, kwa hamu zangu nilimpania mno Brighton siku hiyo, lakini naye pamoja na kumdhania alikuwa mchovu alinimudu vizuri tu na alinikuna nikakunika.

Jioni nilioga na kujiandaa kurudi hotelini kwangu, Brighton akanitazama kwa huzuni.

“Ninah mpenzi unaenda wapi?”

“aah ninarudi nyumbani,” nilizuga.

“tulale wote nimekumiss sana,” aliomba Brighton.

“mh hapana, tutakutana tena, lakini sasa hivi nataka ufanye kitu kwa ajili yangu,” nilisema.

“chochote utakachotaka nitafanya Ninah!” alisema kwa unyenyekevu kweli.

“nataka uache pombe, ukiacha tu nakuja kuwa na wewe!” nilisema Brighton akaitikia kwa moyo mmoja. Nikamuachia shilingi laki moja taslimu na kuondoka zangu kurudi kwa Mr Edgar.


NINAH 27

Basi ndiyo nikawa nimezoea hivyo siku nikijisikia naenda kwa Brighton,0 tunakutana hotelini kama kawaida na jioni narudi kwa Mr Edgar nikidanganya kuwa narudi nyumbani.

Nilijua kuwa Brighton hawezi kuulizauliza tena maswali maana alimjua baba yangu alivyokuwa hampendi hivyo akawa ameamini kabisa kuwa narudi nyumbani, laiti kama angejua nawekwa mjini na bosi wake sijui angefanya nini.

Nilijua lazima nifanye siri kubwa mno; ni moja ya siri ambazo wanawake tunaziweka rohoni na kuzifungia huko hata mtufanye nini hatuwezi kuzitoa nje ng’oo.

Basi, ndiyo ilivyokuwa tena nikijipa moyo kuwa mbona sifanyi dhambi yoyote kwa kuwa sifanyi mapenzi na Mr Edgar hivyo sina kihoro cha kusutwa.

Siku zikapita na Mr Edgar alizidi kunipenda mno, nakumbuka alitengeneza picha yangu niliyopiga photoshot na kuweka kwa ukubwa ukutani, mwenyewe akasema akiitazama anajisikia amani.

Nilishangaa upendo wake, lakini na mimi sikulaza damu, kimyakimya nikawa nahifadhi hela alizonipa nikiwa nataka zifike zile milioni 12 ili nilipe deni letu, ili mambo siku yakiharibika maisha yangu na Brighton yarejee.

Wakati huo Brighton naye aliacha pombe kabisa na kurudia utanashati wake. Akaanza kujihangaisha kwenye biashara ndogondogo kila siku akipambana kiume.

Kipindi hicho chote nilisahau kabisa kuhusu shetani nikajua pengine alishaniacha kumbe alikuwa na makusudi yake na hakumalizana na mimi hata kidogo; ona alinivalisha mkufu, ukapotea, nikapitia ufukara wa kutupwa, nikagombana na Brighton; nikajirahisisha kwa Mr Edgar na baada ya hapo kumbe alipanga kisanga kingine.

Picha lilianza hivi: siku hiyo Mr Edgar alinipeleka shopping na kuninunulia nguo nzuri kwa kuwa jioni alitaka tutoke kwenda Selena kwa kuwa kulikuwa na hafla. Kwa mujibu wake alinitaka niwe na yeye muda wote pembeni yake tena akinikumbushia kuwa kama vile nilivyokuwa siku ile na Brighton.

Kweli nilijipula lakini niliogopa mno kuvaa mkufu, nadhani ilikuwa ikinikumbusha ule mkufu uliotugharimu. Hivyo nikaona cheni itatosha tena siyo ya kuazima.

Basi nilijipamba nikapambika, wote mimi na Mr Edgar jioni tukaondoka hadi Selena.

NINAH 28

Ilikuwa ni hafla fupi ya uzinduzi wa Forum ya kijamii ambapo kampuni ya DStv walikuwa wadhamini kama kawaida nilikuwa pembeni ya Mr Edgar nikiweka mkono wake ndani ya mkono wangu kila saa nikiwa ubavuni mwake.

Alinitambulisha kwa watu mbalimbali kama mpenzi wake na mimi sikuharibu kama kawaida yangu, nilikuwa classy na official, sisemi hadi nisemeshwe natabasamu kwa kila mtu.

Sasa kulikuwa na watu wakipiga picha lakini hata sikuwajali na kuwatilia maanani kumbe ni waandishi wa habari na picha zilipigwa kwa ajili ya magazeti, televisheni na mitandao, huwezi amini sikuwa na hili wala lile. Niliweka tu pozi na mtu mzima Mr Edgar.

Tulipomaliza ile hafla tulirudi hotelini na kulala, nikashtuka tu asubuhi simu kutoka kwa Rose yule mtoto wa shangazi ikiingia kwa namba ya nje ya nchi.

Nikapokea na kuongea naye; alichoniambia kilinishtua mno.

“Unajua Ninah nimekuona mitandaoni upo na mshefa mmeng’ang’aniana wenyewe ndiyo bwana ako nini?” alisema Rose nikashtuka na kumuuliza ameona wapi.

“nimeona kwenye blogs, na Instagram, yaani ulipendeza mno hadi umetrend loh, si nilikwambia, achana na vibrazameni havina hela; sasa cousin tulia naye huyo atakupa maisha mimi na mume wangu mpaka leo tunakula raha Dubai, na kesho kutwa tunaenda Paris,” alisema Rose, akizidi kunitibua akili.

Nikakata simu haraka na kuanza kupekua Instagram: Loh kuna picha nyingine wameweka vichekesho kwa caption eti kupatwa kwa Mrembo. Yaani jinsi Mr Edgar alivyonizidi umri na mimi nikionekana pembeni yake.

Nikashangaa kuona nikiwa nimetagiwa na watu kibao kwenye akaunti tofauti za fasheni wakinisifia lakini kwenye kila picha Mr Edgar alikuwa pembeni, loh kumbe imekuwa zimesambaa hivi! nikashangaa mno. Sasa kwa kuwa Mr Edgar alikuwa kazini kwake, nikatulia kimya kwanza nikisubiri arudi tujue tutatatua vipi hili tatizo.

Uoga wangu ukawa pindi Brighton akiziona zile picha itakuwaje, tena hivi juzi tu alikuwa amepata simu ya smart.

Sasa wakati nachakata akili, nikaona kumbe hadi Mr Edgar mwenyewe kwenye profile yake aliweka picha yangu na kuandika, My beautiful wife.

Loh!

Itaendelea..


NINAH 29

“Mr Edgar, nini kinachoendelea?” niliuliza kwa hasira nilipomuona tu Mr Edgar anaingia ndani.

“Nini malaika wangu, mbona upo hivyo?” aliuliza Mr Edgar.

“Leo asubuhi nimeamka na kuona picha zangu mtandaoni nikiwa na wewe sawa ni kosa langu kutowakwepa mapaparazi lakini haitoshi nataka kukupigia naona na wewe kwenye simu yako Whatsapp umeweka picha yetu, umeniandika kabisa wife, mimi wife wako? Brighton akiona je?” niliwaka mno.

“Ninah please calm yourself, kwanza tuongee,” alinituliza Mr Edgar nikatulia kwanza nimsikie anachotaka kusema.

“Ninah sijui nisemeje,lakini kila siku tunayokuwa pamoja inakuwa ngumu mno kwangu, nazidi kuvutwa kwako, nazidi kukupenda mno, na nisamehe niliandika vile kwa ajili tu ya mapenzi, lakini ona naweza kufuta haraka!

“Unajua nini nilikuwa hadi nina mawazo ya kipumbavu nikitamani na kuota tumeenda mbali na hapa na tunaishi peke yetu, tafadhali Ninah usinichulie vibaya wala kuniona mjinga wa kufikiria hivyo ni mapenzi tu natamani ningekuoa na kuwa mke wangu,” alisema Mr Edgar akiwa mpole mno, tena akifuta ile status ya whatsapp huku akitetemeka.

“Mr Edgar, si ulisema una mke na watoto na hauwezi kuwaacha, sasa leo unabadilisha maneno na kutaka kumuacha! Sikudhania kama upo hivyo!” nilisema.

“Hapana sijataka kumuacha, yeye ndiyo ameamua kuniacha, na juzi tu nimetoka kusaini karatasi za talaka nilizotumiwa na mwanasheria wake nipo peke yangu Ninah, I am all alone, na bila wewe naweza kufa,” alisema Mr Edgar kwa uchungu akaanza kulia, kidogo nikapoa lakini hapana siwezi kumuamini kwanza.

“hizo karatasi za talaka ziko wapi!” nilisema. Basi akanitaka nifungue droo ya kushoto, nikafungua na kutoa bahasha nikaanza kuchambua na kweli nikaona ni copy za devorce papers. Nilishtuka mno nikaanza kumuonea huruma kidogo lakini.

“Pole, haya yote kwa sababu ya tatizo lako?” niliuliza nikikaa kitandani pembeni yake.

“Ndiyo tena anaolewa na mtu mwingine mweziuijayo, ili kujipa moyo na mimi ndiyo nikaweka picha yako kwenye whatsapp yangu.


NINAH 30

“Yote ili mradi tu anione kuwa naendelea na maisha yangu vizuri na msichana mzuri kuzidi yeye ambaye amenivumilia pamoja na matatizo yangu; sikujua kama nitakuudhi malaika wangu nisemehe!” alisema Mr Edgar jasho likimtoka.

“Umeniudhi sana kwanini haukuniambia mapema? Ona leo hii Brighton akijua itakuwaje? Unavyosema unatamani ungenioa na kuondoka na mimi mbali, unadhani na mimi nitamuacha Brighton, hapana. Siwezi Mr Edgar!” nilisema kwa uchungu.

“Ninah hapana, sitaki umuache Brighton na sitaki uende mbali na mimi, tunaweza kuishi hivihivi pamoja na ninaweza kuongea na Brighton nikamrudisha kazini na akafahamu kuhusu sisi na tutakuwa na uhuru kwenye penzi letu, hatutamuogopa tena kwa sababu nafasi yake ataijua na nafasi yangu pia itajulikana,” alisema Mr Edgar. Nikastaajabu mno kwa kauli yake hiyo, loh yaani mimi niwe demu wao au? Ana akili kweli Mr Edgar au ana matatizo.

Nilishtuka na kutazama ukutani, nikaona picha yangu ikiwa kwa ukubwa, nikatazama kwenye kifremu cha kwenye dressing tebo kulikuwa na picha yangu pia, nikatazama simu ya Mr Edgar kulikuwa na picha yangu kwenye wallpaper yake, kwenye laptop yake pia picha ilikuwepo.

Na yote anayoyaongea, si bure, huyu mwanaume amekuwa chizi kwa ajili yangu. hapana hayupo sawa na kila anachoongea ni ujinga.

“Ninah, tazama mimi nitakuwa tu kama mpenzi wako na watu nitaawatambulisha hivyo lakini Brighton ataendelea kuwa mpenzi wako kwa sirisiri na nitakupeni chochote mtakachokitaka, tafadhali Ninah! Ukiniacha sitaishi nitakufa!” alisema Mr Edgar hivi macho makavu.

Nilirudi nyuma kwa hofu, Mr Edgar akanikimbilia na kufunga mlango akanikumbatia kwa nguvu nikawa nahangaika kujichomoa huku nikipiga makelele anichie.

Nilipoona ananizidi nguvu nilizuga kukubaliana na upuuzi aliousema, kuwa ananipenda hivi, ananipenda vile. Mimi kichwani nikawa nawaza tu ikiwa Brighton akiniona kwenye mtandao itakuwaje?

Niliogopa mno na kuomba Mungu, nikapanga usiku nimtoroke Mr Edgar niende haraka kwa Brighton mwenyewe, nikamuwahi kabla mambo hayajawa mabaya, tena nikawaza nikitoka hapo ndiyo moja kwa moja sitarudi nyuma.



Basi katikati ya usiku nilisikia mlio wa simu nikatazama na kuona ni meseji kutoka kwa Mama Sele akisema kuwa ameniona mtandaoni na mshefa. Tena alinisema kwanini nilimficha.

Usingizi wote ukakata, nikajua hivi karibu tu taarifa zitafika kwa Brighton, kwa hofu nikaamka saa hiyohiyo na kutaka kusepa. Nikatazama saa na kugundua ni saa tano usiku.

Nilijitoa katika mikono ya Mr Edgar taratibu pale kitandani na kwenda bafuni kunawa uso, nikatafuta nguo zangu ili nivae lakini kuna wazo lilinijia ghafla nikaacha na kumtazama Mr Edgar aliyelala fofofo kwa amani mno nadhani alikuwa akiota hizo ndoto zake za mapenzi kuwa nilikuwa karibu naye huko kwenye ulimwengu mwingine ambao yeye ni rijali tena.

Nilimuonea huruma mno, lakini siku zote nilijua huruma ndiyo hutuponza wanawake na kufanya tujutie kwenye maamuzi yetu baadaye; hivyo hapo niliweka moyo na ubongo na kuamua kutoa wazo moja sahihi. Maana nilikuwa dilema.

Niliwaza kwanza Mr Edgar ni mzee wa makamo pili simpendi kama ninavyompenda Brighton maana nimetoka naye mbali kweli japokuwa ni mwanaume tu wa kawaida ambaye wanawake wengine wazuri hawamuoni ila ananikuna mno kwenye mapenzi na sijaona katika wapenzi wote niliowahi kuwa nao.

Hayo ni maamuzi ya moyo, lakini kwa kutumia ubongo yaani akili niliwaza ikiwa nitaamua kukubali kuwa na Mr Edgar na kweli akanifanyia hayo aliyoyasema kuwa nitakua nauza naye sura mjini na kuogea pesa, nitakachokikosa ni mapenzi na uhuru pia na zaidi nitamkosa Brighton kwa sababu hatataka kushea na mbaya zaidi na bosi wake.

Okey nitamwambia Brighton kuwa mzee wa watu ni nyoka wa kibisa tu ambaye namlia hela yake, kwani yeye atakosa nini? nilijiuliza lakini nikakumbuka onyo la Mr Edgar kuwa hapaswi mtu yoyote kufahamu kama ana matatizo hivyo nikaona bora yeye mwenyewe ndiyo aongee na Brighton ili nione watafikia wapi.

Lakini nikiunganisha mawazo ya ubongo na moyo nikapata wazo moja lililonifanya niamue kuacha kuvaa nguo na kubaki na Mr Edgar.

NINAH 32

Nilifikia uamuzi kuwa; Kama Brighton atakuwa katika mazingira magumu ya kufanya uamuzi kama yangu je, atakubali pesa za Mr Edgar na kuniacha au atanifuata mimi na kunisamehe kuhusu picha zangu na bosi wake?

Niliwaza hivyo na kupanga kumwambia Mr Edgar kesho yake kuwa kabla Brighton hajaniona mtandaoni, ajaribu kumpa fedha Brighton halafu ampime kwa kumwambia achague aidha hela na kuniacha mimi niwe wa Mr Edgar au akatae ili nibaki naye, halafu tuone Brighton atafanya nini?

“Ninah!” alisema Mr Edgar akishtuka usingizini na kukaa kitandani baada ya kuniona nimesimama tu.

“Abee!” niliitikia kwa adabu nikizuga kuwa nimetoka bafuni basi nikarudi kitandani na kulala pembeni yake kama kawaida akanikumbatia na kunibusu.

Tulipoamka asubuhi nikamueleza Mr Edgar kila kitu kilichotokea usiku ule. Mr Edgar akaniambia kuwa atamwambia Brighton matatizo yake na kufanya mpango kama alioniambia jana yake nikaudharau. Lakini nikamshauri kuwa ikiwa Brighton atakataa si itakuwa siri yake imeshavuja tena.

Kweli akaogopa, sasa akakubali kumtega Brighton achague kati ya hela na mimi.

Nikamueleza nia yangu kuwa nataka nimpime kuwa ananipenda kwa dhati au lah! Lakini hiyo pia iwe kuzuga ili lile soo la mimi na Mr Edgar kutembea alipotezee pia. Tena nikamwambia kuwa nataka kushuhudia kwa macho yangu Brighton atakachokiamua na kufanya.

Basi kweli Mr Edgar akampigia simu Brighton, kama nilivyotabiri kumbe Brighton alishajua kuhusu mimi na Mr Edgar nadhani aliandaa kunipiga huko sijui, maana alikaa kimya hakuniambia chochote, lakini kwa Mr Edgar alianza kwa kufoka kwa hasira mno.

Mr Edgar akasikiliza kwa muda kisha kwa sauti yake ya busara akamwambia: “Brighton najua nimekukosea, ila nataka kukurudisha kazini lakini utafanya kazi Sauzi Afrika na nitakupa shilingi milioni hamsini, lakini nataka niachie Ninah tafadhali,” alisema Mr Edgar, Brighton sauti ikakwama.

“Brighton, tukutane Escape One kesho saa kumi na mbili kamili kama utakuwa tayari, ,” alisema Mr Edgar na kukata simu, Ninah akatetemeka akiombea Brighton asiende, lakini mwanaume gani ataacha fedha kisa demu aliyemsaliti kwa bosi wake.

Itaendelea..


NINAH 33

Nikiwa nahofia juu ya uamuzi wa Brighton, Nikajipa moyo kuwa nipo sahihi kwa kuwa kwenye mapenzi kila mtu inabidi ajitoe kwa mwenzake na kuacha baadhi ya vitu au kusamehe mambo hata kama ni makubwa kiasi gani, ili mradi tu kutetea penzi lao.

Mimi niligombana na baba yangu na shangazi kisa yeye, nilimhudumia kwa kila kitu, nilimfumania lakini yote nilisahau na sasa nilikuwa ladhi kumuacha Mr Edgar kwa ajili yake, je yeye alifanya nini kwa ajili yangu? hilo nalo ni swali.

Nikajiapia kimoyomoyo kuwa kama Brighton atachukua pesa za Mr Edgar na kukubali kuniacha basi akya Mungu nitaendelea na Mr Edgar na kuvumilia yote, lakini nikajiapia kama asipokubali kuchukua hizo hela siku hiyohiyo namuaga mr Edgar na kurudisha virago kwa Brighton wangu tuendelee kuganga njaa pamoja.

Tena uzuri nilikuwa wakati huo nilikuwa na vihela kidogo, yaani nikivichanga vinaweza kufika ile milioni mbili, ambayo tungeweza kulipa kule kwa Sonara tuweze kukomboa mali zetu tulizoziweka dhamana.

Basi nikasubiri na kweli ile siku ya pili Mr Edgar aliniambia kuwa tujiandae kwa ajili ya kukutana na Brighton, naye akaandaa mikataba kabisa ya kumpa kazi Brighton katika kampuni ya Dstv huko Afrika Kusini na begi la hiyo milioni 50.

Kwa kung’ang’ania na mimi nikaenda naye hadi Escape One nikajificha VIP kule juu nikiwatazama wote kwa chini.

“Ninah huoni itakuumiza?” alisema Mr Edgar akiwa na uhakika kuwa kumuona Brighton akichagua pesa badala yangu kutaniumiza lakini bado nilisisitiza kukaa hapo ili nishuhudie.

Kweli saa ilipofika Mr Edgar alishuka chini na kuketi kwenye kiti fulani, kidogo akaanza kuzungumza na simu baadaye nikamuona Brighton akiingia, alionekana amejaa hasira mno kiasi kwamba Mr Edgar alipompa mkono wa salamu Brighton hakujibu na alitazama pembeni tu.

Nikamuona mr Edgar akizungumza kwa muda halafu akafungua briefcase yake akatoa karatasi ambazo nilijua ni za ilemikataba akamkabidhi Brighton, Brighton aliichukua kwa nguvu huku akimtazama kwa macho makali Mr Edgar.


NINAH 34

Akaisoma vizuri na kutia saini palepale halafu akamrudishia Mr Edgar aliyetoa begi lililokuwa na hela, Brighton akalifungua na kuchungulia ndani, akalifunga na kuongea maneno fulani kisha akaondoka.

Kuona tu vile moyo wangu ulichoma kama mkuki, huwezi amini machozi yalinitoka kwa uchungu, ile taswira ya Brighton akiondoka na fedha ilijirudia kila wakati.

Ina maana Brighton alinipendea hela, niliwaza na kuyakumbuka maneno ya baba aliyoniambia kipindi kile nipo na Brighton kuwa Brighton ananitumia tu kwa ajili nina hela, lakini sikusikia.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG