Search This Blog

Monday, January 24, 2022

JOY, JOYCE - 3

   

Chombezo : Joy, Joyce

Sehemu Ya Tatu (3)



Ama kweli damu nzito kuliko maji, nilijua Joy alivyo na roho nzuri vile atamkatalia dada yake walichokipanga dhidi yangu, badala yake akakubaliana naye mulemule, sasa nikajiuliza tu ikiwa jambo hilo nimeweza kulijua, je, kuna mambo mangapi mabaya ambayo marafiki au ndugu zako wewe msomaji wangu wanakupangia na hauyajui? Cha msingi tumuombe Mungu kabla ya kulala aisee.

Tena mie nilipanga kumwambia kabisa Joy na kumuonesha zile meseji za Joyce alivyomfitinisha na Chriss wake kwa picha na pengine tungepanga kumtumia Chriss pamoja, lakini kwa kuwa alionekana kufuata ushauri wa ndugu yake. Nikaminya, tena nikataka kujua itakuwaje maana niliona hii yaweza kuwa stori nikaiandika hivyo nisiiharibu utamu wake.

“Mh tatizo siyo kama sitaki, lakini huyo Chaxy Chande atakubali vipi wakati unajua fika anaishi na Deborah na wanapendana balaa, si ndiyo nitajidhalilisha, jamani,” alilamika Joy.

“sikia, huyo Chaxy Chande nikimuangalia hata kwa macho tu anaonekana anakupenda mno, kuna kipindi nilipoenda ofisini kwake nikijifanya wewe, alivyoniangalia tu nikajua anakutaka pacha wangu. Na kitu kingine nimefanya uchunguzi wangu na kubaini huyo Deborah ni mchafu balaa.

“Chaxy Chande mwenyewe tu hajui, ninachotakiwa kufanya ni kumuonesha umalaya wa huyo demu wake ili waachane wakati huo wewe ndiyo itakuwa muda wako, si unajua wote wawili mtakuwa mmetendwa. Hivyo kumuaminisha Chaxy Chande kuwa mnapendana ni rahisi tu kama maji. Sasa hivi wewe ukikutana naye mlegezee aone dalili utanikuja kunishukuru,” alisema Joyce, nikaanza kujiuliza huo uchafu wa Deborah wangu ni upi na yeye msichana toka jela aliujuaje? Mh huyu mwanamke balaa; nikajiapiza kusubiri anioneshe huo chafu wa Deborah.

Akaendelea.

“Sasa wakati nyinyi mnaendelea na yenu mimi nitakuwa namrusha roho Chriss kwa picha zako na Chaxy Chande, lakini pia nitamwambia kuwa zile picha nilizomtumia nikiwa na Damian, haikuwa wewe bali ni mimi, nadhani kwa hayo atasahau tu hata kile kidayari,” alisema Joyce na kumaliza kuongea mipango yake ya kifitini. Lakini kwa kuwa alisema atamwambia ukweli Damian nikaona nitulie kusikilizia Joy akinitega nijifanye nategeka.



“Sawa nitafanya hivyo japo gharama hiyo sijui imekujaje kwasababu wewe ndiye uliyeniharibia, sasa inabidi ujenge.”

“Joy nadhani umesahau kuwa nina siri yako kubwa mno ambayo kama nikiiweka hadharani, si Chaxy Chande, wala Chriss atakayekutazama usoni. Kwa hiyo utafuata ninachokwambia tu. Sitaki unijibu.”

“siri gani?”

“inahusu maisha yako ya utotoni, unamkumbuka Anko Kelvin?” alisema Joyce.

“Weee! Joyce tafadhali usije ukaenda huko!!… acha nitafanya chochote unachosema,” alisema Joy akianza kulia upya.

Nikastajabu ni siri gani tena kubwa hivyo iliyopo kati yake na huyo Anko Kelvin kiasi cha Joy kukubali kufanya chochote alichokitaka Joyce.

Baada ya dakika chache za ukimya, nikagundua kuwa nilikuwa si mstaarabu kukaa hapo nikiwachunguza watu, hivyo nikanyata taratibu na kurudi nyuma hadi mlangoni, kisha nikagonga mlango na kujifanya ndio kwanza naingia.

Nilisikia watu hatua zikikimbia ndani, nilipoingia hadi ndani nikamuona Joy peke yake akiwa amesimama na kanga yake aliyojifunga lubega akiniangalia kwa aibu na mimi nikamtazama lakini sijui ndiyo nilikuwa nikimtazama kwa macho ambayo Joyce alisema au lah! kuwa eti yanaonesha wazi nampenda?

Cha kushangaza akaja haraka na kunikumbatia kwa kupitisha mikono yake mabegani mwangu, na mimi nikaipitisha kiunoni mwake. 



“Chaxy Chande, nimeumizwa sana na mapenzi, sijui kama nitapendwa tena na Chriss, nimekata tamaa lakini ninapokuona wewe nakuwa najisikia amani. Natamani.. tuwe.. mh.. kama hautojali.. naomba uwe unanipa kampani, ninapomiss kuwa na mpenzi,” alisema Joy kwa sauti nyororo, maneno hayo yakipita ndani ya sikio aliloniinamia kwenye lile kumbato zito.

KWA MANENO HAYO NIKAJUA TAYARI MUVI LIMEANZA, nani stelingi nani adui kuu nani adui msaidizi, hebu tuone.

Na mimi kwa sababu niliamua kufuatilia mkasa huo kwa ajili tu ya stori ambayo kwa bahati mbaya na mimi nilijikutamo basi kwa shauku nikaamua kucheza na biti lao ili nijue tutafikia wapi.

“Usijali, Joy siku zote nipo kwa ajili yako,” nilisema maneno hayo sasa sijui ndiyo nilikuwa nimemkubalia au lah, lakini huwezi amini nilijisikia nikitamani kuwa na Joy kiukweli kwa sababu ni kweli nilikuwa nikimpenda mno.

Sasa kwa kuwa niliingia mchezoni, nilitakiwa kuwa makini kwa kutokuingiza kabisa hisia binafsi kwenye ligi. Baadaye niliachana na Joy ambaye alikuwa akinitega hapa na pale, na kurudi nyumbani nikijua fika wakati huo wote Joyce alikuwa akituangalia kwa kujificha.

Japokuwa ilikuwa ni usiku wa saa nne, niliporudi nyumbani nilishangaa kutomuona Deborah wala mavi ya Deborah, nikatafuta ufunguo ambao huwa tunawekaga chini ya mlango na kuingia ndani.

Japo nilikuwa na njaa na maswali juu ya alipo Deborah, lakini ilikuwa lazima niandike kisa hiki kwanza maana kilizidi kunoga mno.




Nikainama mwanaume na kuanza kubonyeza vibatani, nikichapisha aya ya kwanza kisha ya pili nikiumba visa na maongezi mnogesheo ili msomaji wangu usome bila kuboreka si kama mnavyosomaga hadithi za akina mwa-fulani ambazo ni mbayaaa!

Asante Mungu nilimaliza kuandika nikatulia kitandani nikiangalia saa iliyoonesha kuwa ni saa sita kasoro lakini Deborah hakuwa hata na dalili.

Nikanyanyua simu nakumpigia lakini hakupokea, na baadaye ikakatwa, ikabidi niangalie kama kuna chochote cha kula nikaona hola. Ikabidi nichukue buku jelo na kwenda kununua chakula ambacho sikipendi mno, chipsi kavu.

Nikarudi na kula zangu, roho yangu ikienda mbio nikiwaza huenda Deborah atakuwa kwenye huo uchafu wake aliosema Joyce. nikaanza kuvutia picha anafanya kila aina ya uchafu ambao mwanamke anaweza kuufanya pindi akikosa uaminifu. Lakini ilipofika saa saba usiku, mawazo yakabadilika nikaanza kuhisi huenda katika huo umalaya wake labda amekutwa na madhila. Huenda amebakwa au ametekwa na hao mabwana zake.

Niliwaza nitafanya nini ikiwa jambo baya litamkuta Deborah kwa sababu nilishakabidhiwa na dada yake, na hata mama zake wadogo wananifahamu mimi ndiye naishi naye.

Mh nikajaribu namba chache za marafiki zake lakini nazo zote hazikuwa zikipatikana. Nikajaribu za dada zake nazo kwa usiku huo nadhani walikuwa wamelala.


JOY, JOYCE 26

Saa zikakatika ikafika saa tisa za usiku, kiukweli tumbo la wasiwasi lilikuwa likinikata, usingizi ulikuwa hauji.

Nilichowaza hapo ni kuwa huenda alikuwa amepata ajali., maana alikuwa akipenda sana kurudi na pikipiki. Lakini nikaomba Mungu anipe amani ya moyo nikalala kimang’amumang’amu lakini asubuhi saa 12 nikaendelea na zoezi la kuwapigia ndugu zake na simu yake mwenyewe ambayo ilikuwa haiiti kabisa.

Wakati nawaza nini cha kufanya meseji ya Whatsapp ikaingia kwenye simu yangu, “najua una wasiwasi alipo huyo ‘pasua kichwa’ wako, muangalie hapo, hana wasiwasi wowote.”

Ujumbe huo uliambatana na picha kadhaa ambazo alionekana Deborah akiwa baa na mwanaume mmoja ambaye ni mwanamuziki maarufu wa bendi fulani hivi. Tena akiwa na kiguo kifupi mno ambacho sikuwahi kumuona nacho hata siku moja. Pembeni alikuwa na dada yake mmoja ambaye ninamfahamu naye akiwa sijui na mpiga gitaa, wakila raha zao.

Lakini kitu kilichonishtua ni kwamba meseji hiyo ilikuwa imetoka kwa Joyce, nikajua kuwa hayo ni matekelezo ya kile alichoongea na Joy jana yake.

Kidogo wasiwasi ukashuka lakini hasira zikanipanda mno, katika maisha yangu huwa sipendi kusaliti wala kusalitiwa na pindi nikigundua nasalitiwa huwa naumia mno. Nikaweka nadhiri kuwa Deborah akirudi tu lazima abebe mizigo yake na aondoke.

Nilijisemea hivyo wakati nilikuwa najua kabisa kuwa huo ni mpango wa Joyce. Sikumlaumu moja kwa moja kwa sababu angalau alinifungua macho kidogo kwa kujua upande wa kiza wa mtu niliyeamini kuwa siku moja nitamuoa.



Asubuhi hiyo nikiwa na mawazo mno, nilifunga mlango na kuelekea zangu ofisini. Kwa hasira nilizokuwa nazo nilishindwa kuendeleza hadithi ya NAKUPENDA Mr X part 3, nilijua nitaharibu hivyo nikaona bora nitazame zangu muvi tena ya kizombi.

Muda wa mchana hivi, ndipo nikapokea simu ya Deborah, nilipopokea akaongea dada yake, yule aliyeonekana kwenye picha wakiwa naye baa na yule wale wanamuziki wa bendi.

“hallo shemeji, samahani sana, jana Deborah alikuwa kwangu hapa nyumbani sasa alikuwa hajisikii vibaya nikampeleka hospitali na baadaye nikampeleka kwa dada yetu mkubwa akalala kule nisamehe nimechelewa kukupa taarifa.”

“usijali, yeye mwenyewe yupo wapi?” niliuliza nikijitahidi kuzuia hasira.

“haloo, nipo hapa kichwa kinaniumaaa! Nimekunywa dawa zinaniendesha kweli, ndo najitahidi kuja hapa,” alisema Deborah bila aibu.

Nikajiuliza ina maana nisingejua ukweli ningekuwa kama boya, yaani ningenunua matunda kwa wingi kwa ajili ya mgonjwa mwongo.

“Sikia najua ulipokuwa jana, sitaki huo uongo wako, cha kufanya njoo nyumbani chukua vyako ondoka nenda kwa huyo (jina kapuni) wako.” Niliongea kwa hasira mno kiasi kwamba Deborah huko alipo alifyata na kukata simu.

“Kaka vipi?” aliuliza Geofrey mfanyakazi mwenzangu baada ya kusikia nimeongea kwa hasira maneno hayo.

“we acha tu,” nilimjibu nikiwa sitaki anichimbe kuhusu maisha yangu ya mapenzi. Kidogo wakati huo akanipigia simu Joy na kuniomba nikutane naye maeneo ya Hongera Baa jioni, nikakubali kwa sababu nilijua huenda Joyce alishamwambia Joy kuwa nimeachana na mtu wangu baada ya kunitumia picha za Deborah, hivyo anaweza akaniingia kirahisi. Nikaona ngoja niipe chansi, shauku yangu ilikuwa je, Joy atafanya nini kati ya vile walivyopanga juu yangu.


JOY, JOYCE 28

Jioni ilifika nikakutana na Joy aliyevaa gauni lake la manjano na kuchana nywele zake upande, alionekana kuvutia mno kiasi kwamba nilisahau kwa muda maumivu ya mwanamke mjinga Deborah.

“Joy, vipi unaendeleaje!”

“salama tu, hahaaa leo ni siku ya furaha kweli kwangu, nimegundua kuacha maumivu yaliyopita ni silaha tosha ya kukaribisha furaha mpya,” alianza kuseti mitego Joy akinilenga mimi.

“yah kweli, “

“hata wewe Chaxy Chande inabidi ujifunze hivyo, si ndiyo eeh..hahaaa angalia hii video,” alisema Joy huku akinionesha video fulani ya kuchekesha kwenye instagram.

Nikajichekesha tu kumsapoti lakini moyo wangu ulikuwa jiwe.

“halafu Chaxy Chande sijapigaga picha na wewe hata siku moja, hebu selfiee!” alisema Joy huku akinyosha simu yake na kupiga picha moja, niliyolazimisha tabasamu, lakini kwa sura yangu ya duara hata nikilazimishaga tabasamu mtu anaweza akaona nimetabasamu kiukweli na nikikasirika kidogo wengine wanaweza wakadhani nimekasirika sana. Kumbe hata.

Basi kwa ile picha nikajuafika itatumwa kwa Joyce, Joyce naye ataituma kwa Chriss ili kumtia wivu, kama walivyosema. Sasa na mimi sikutaka kutumika tu kijinga. Nikamkamata Joy nikamvuta karibu yangu na kumpiga bonge la Kiss la mdomoni.

Akajitoa haraka mikononi mwangu, akiwa hajajiandaa kabisa kwa hilo na kwa kuwa lengo lake ni kunitumia basi hakuwa na lengo kabisa la kuniruhusu nimguseguse.

“Chaxy Chande unafanya nini!” aliongea kwa hasira kidogo, Joy nikaona na mimi mpango wangu umekaa vizuri, nikajifanya siongei nikainuka na kuondoka zangu bila kumuaga akabaki mdomo wazi.

Nikaanza kusubiri kuona jinsi ambavyo mipango yangu itakavyojiseti yenyewe baada ya kitendo kile.

Je, nilitengeneza bomu gani? Usikose kusoma kesho ili kujua



Huwezi amin baada tu ya kutoka pale nilichojua ni kwamba tayari Joy atakuwa amemtumia Joyce ile picha tuliyopiga pamoja, kisha naye atamtumia Chriss, nilijua atamtia wivu ndiyo, lakini nilijua lazima mpango huo utahitaji picha zaidi ya hiyo. Inatakiwa picha inayoonesha bila walakini kuwa sisi ni wapenzi na si kama ile aliyopiga tu tukiwa tumetabasamu.

Hata hivyo nilichojivunia kwa kile kitendo cha kumkiss kwa nguvu Joy ni kwamba, Joy na Joyce wote kwa pamoja hawataniona mjinga tena yaani si wakunitumia kwa ajili ya kumrudisha mpenzi wao burebure.

Akilini nikavuta picha pale Joy atakavyomwambia dada yake kuhusu nilichomfanyia siku hiyo, “Joyce, siwezi kuendelea kwa sababu Chaxy Chande anaonekana ananitaka kweli, nahofia anaweza kuniweka kwenye wakati mgumu ikiwa atataka tufanye mambo mengine.”

Hapo nikavuta picha pia kuwa Joyce atajibu; “mpe tu kila anachotaka cha msingi tupate tunachokitaka umesikia Joy!”

Nilicheka kwa mawazo hayo lakini nilijua lazima iwe hivyo kwasababu kama kweli wanataka kumtia wivu Chriss, nani tena waliyenaye ambaye wanaweza kunitumia zaidi yangu mimi.

Nilipanda zangu gari na kushuka maeneo ya nyumbani, Kijitonyama na kuingia varandani nikielekea chumbani kwangu nikaona mlango umefungwa vizuri, nikapapasa ufunguo na kuufungua.

Chumba kilikuwa kama kimepigwa na upepo wa kisulisuli, maana nguo zangu zilikuwa shagalabagala na ilikuwa wazi kuwa Deborah alikuwa amechukua virago vyake na kusepa lakini alihakikisha ananiachia vitu ovyoovyo ili anikomoe.


JOY, JOYCE 30

Nikajirusha zangu kitandani na kuwaza kama uamuzi niliofanya wa kumfukuza Deborah ni sahihi au nimekosea?

Kuna kitu ambacho nimekuwa nikijifunza kwa muda mrefu, yaani pia kumpa shetani sifa zake kwa mazuri anayoyafanya, yaani hapa nina maana kuwa japo mtu anaweza kuwa na mabaya mengi lakini tazama pia uzuri wake hata kama mdogo kiasi gani.

Kwa Deborah uzuri wake ukiacha sura ni usafi wake wa chumba, na jinsi alivyokuwa akinifulia nguo vizuri, sasa nilikuwa peke yangu na najijua nilivyokuwa rafu.

Yaani neti naweza niikaichomekea miezi hata minne bila kuifunga, ili nikiwa narudi kutoka kwenye mishemishe zangu, nikifika nadumbukia tu, dubwi! Kufua mashuka ndiyo mpaka nihisi mafua.

“Jamani majinzi yangu nani atanifulia tena.” Nilifumba mambo nikayeyusha hisia hizo na kuapa kuwa nitaendelea na maisha yangu kama kawaida, kwani Deborah ni nani hasa! Nitampata mwingine zaidi yake.

Nakumbuka usiku huo nikajisikia tu kutunga wimbo wa kumdisi Deborah, nikainuka na kuanza kutengeneza mdundo kwenye FL Studio, sidhani kama niliwahi kuwaambia kama pia ni mwanamuziki.

Basi nikatunga wimbo nikimpaka Deborah na kesho asubuhi nilipofika ofisini kwa sababu pia nina meneji studio ya muziki inayoitwa Top Town Records, nikamwambia prodyuza wangu anirekodie, nikaingiza voko na wimbo ukatoka. Lakini hadi leo sijautoa redioni wala sehemu nyingine maana si kwa mitusi ya rejareja niliyoiporomosha humo.

Haya basi turudi kwenye songombingo letu




Nilianza kufanya kazi za kawaida pale ofisini lakini baadaye meseji kutoka kwa Joy iliingia kwenye simu yangu, nilipoifungua ujumbe ulikuwa ukisomeka; “mambo umeamkaje mpenzi!”

Nikajibu; “poa tu vipi wewe!”

Sikushangaa sana kwa sababu nilikuwa nikilitegemea hili tangu jana yake, nilijua tu lazima Joyce amwambie Joy kuwa ajirahisishe kwangu ili mradi wapate picha ya pili iliyo-hot zaidi ya ile ya mwanzo.

Nikwambie sasa; baada tu ya kutuma meseji ile si ndo akaniandikia tena kuwa eti anakuja sasa hivi ghetoni kwangu.

Nikapiga mahesabu nikajibu; “Karibu.”

Akaniambia anachukua pikipiki.

Basi ikabidi nimdanganye bosi kuwa tumbo limenishika, na mimi nikachomoka nduki nikiwahi nyumbani kusafisha mazingira japo kuwa nilijua siwezi kula mzigo.

Lakini hata hivyo niliapa kumfanya Joy asinipate kirahisirahisi, yaani hata kama atapiga picha na mimi na kurudiana na huyo Chriss wake, nilitaka ajue kuwa mimi siyo mtu wa mchezomchezo. Nilipanga kumkomesha.

Basi baada ya kuweka mazingira sawa nikapulizia na air freshner ya zabibu na kuweka flashi yenye nyimbo za slow, nikijifanya Mr Romantic.

Nikaanza kuwaza Mr X angekuwa katika hali kama yangu angefanya nini?

Yah lazima angefanya kivyovyote hali iwe mbaya kwa Joy bila kuweka hisia kwenye chochote ambacho angefanya, kwa hiyo kwanza nikakumbuka bigijii zangu za Batook, nikafungua moja na kuiweka mdomoni nikiitafuna taratibu ili nipoteze mihamu isiyokuwa na mpango.

Ndani ya dakika tano, simu yangu ikaita.

“muelekeze huyu mkaka,” alisema Joy akimpa simu dereva bodaboda.

“ni hapa nyuma ya hoteli ya Collabus, pitia barabara ya Akachube, yaah karibu na pale kwa Wema Sepetu alipohamaga,” nilitoa maelekezo na kuweka simu mezani, nikaanza kupata mchecheto kuwa he kumbe anakuja kweli!

Itaendelea…


JOY, JOYCE 32

Basi nikiwa sina hili wala lile, mara Joy huyu nyumbani, nikaenda kumchukua nje na kumpitisha koridoni na kuelekea kwenye chumba changu ambacho baada tu ya kuondoka Deborah, nilikipa jina na kukiita Golgotha, na kifriji changu cha kisela nilikiita Eden kwa sababu ya matundamatunda na majuisi ya msimu yanayokaukaga kipindi chote cha mwezi na kujaa wakati mgeni muhimu kama Joy amekuja.

Basi akaja na kukaa kwenye kochi, akinitazama huku akitabasamu mno kama vile jana hakukuwa na chochote kilichotokea.

Kitu ambacho kilinishangaza ni kwamba nilikuwa nimewaza kuwa Joy akija, lazima atavaa nguo za kubana kama vile skini jinzi, ili zoezi zima la kufanya naye mapenzi liwe gumu, lakini ilikuwa tofauti alivaa kisketi mchanuo na kibrauzi tu juu tena akakaa kimitego mbele yangu mimi wakati huo nilichukua glasi na kumfungulia juisi ya Azam nikimtaka anywe taratibu huku nikipanga stepu zangu taratibu.

Cha kushangaza Joy alikunywa kidogo na kunifuata pale nilipokaa ghafla akanipa nyama ya ulimi. Nikashangaa, nikijua kuwa kwa hapo lazima atanipiga picha tu maana alikuwa na simu yake mkononi.

Lakini kilichonishangaza kingine ni kwamba, mambo hayo ndiyo niliyapanga mimi kumfanyia yeye ili nimkomoe na kamchezo kake na pacha wake, lakini alikuwa kama vile ameniwahi. Tena akaja na kunikalia mapajani nikawa kama nimempakata.

Mwili mzima ukanisisimka, nikasema; “lahaula la kwata!



Hata hivyo na mimi sikulaza damu nikamshikilia na mimi na kumuwekea kidevu changu shingoni mwake nikimpima ataishia wapi na hako kamchezo kake.

Nikaona anahema mno, basi na mimi nikamchokoza tena kwa kuanza utalii wa ndani na mikono yangu. Alichonishangaza alionekana kukubaliana na kila nilipotia mkono wangu na kupapasa.

Kilichonishangaza aliachia ile simu yake mezani na kujiachia kabisa mikononi mwangu ili niendelee na ufundi wangu.

Siwezi kusema kila kilichoendelea kwa sababu ilikuwa aibu yaani full michambuo kama karanga.

Baada ya mchezo wa nusu saa tukalala kitandani tukisikilizia kibaridi cha huko nje maa kulikuwa na kimvua cha baridi kilichotufanya tujisikie kukumbatiana tu.

Nikamuona Joy akawa kama vile anahangaikahangaika, nikajjua anatafuta pozi la kupiga picha, akachukua simu na kujifanya kama anaangaliaangalia mtandaoni. Kwa shauku ya kutaka kuthibitisha nilichokiwaza nikaona ngoja nimpe nafasi ya yeye kufanya anachotaka, basi nikajifanya nimemlalia kifuani makusudi ili kwa kijicho cha pembe nione anafanya nini.

Kabang nikaona anatafuta kamera haraka hapo ndiyo nikafumba mach, akapiga picha ya silent. Nikamuona baadaye akaweka ile simu pembeni . na mimi nikajifanya nimebadili pozi na kumlalia kwenye kifua chake tena tukaanza raundi ya pili.

Mambo yote haya yalinishangaza mno, mara kuna wazo likaja kichwani na sijui kwanini sikulifikiria mapema. “vipi kama huyu siyo Joy bali ni Joyce!”


JOY, JOYCE 34

Nikaanza kupata kiraruraru maana kweli Joy hakuwa na tabia hii ya kujirahisisha kiasi hiki, huenda akawa ni Joyce, mwanamke ambaye hana aibu na ndiye aliyelala na Damian mpenzi wa zamani wa Joy ili mradi tu kuharibu uhusiano wa pacha wake!

Nikajikuta mapigo ya moyo yananienda mbio kama nini, nikajiona mjinga kwa nini sikuwaza kuwa mapacha hao watanichezea mchezo kama huo kabla, lakini bado sikuwa na uhakika.

Nikakumbuka jambo fulani. Kwenye begi langu kulikuwa kikopo cha wino na kumbuka wakati nilipokuwa wakala kipindi cha kupigia kura nilikuwa na ule wino ambao watu waliopiga kura walipakwa kwenye kidole ili wasirudie tena kupiga kura. Sasa kikopo kimoja nilirudi nacho nyumbani.

Hivyo nikaona kupitia wino huo usiotoka kirahisi, naweza kumtia alama msichana huyo ili nijue kuwatofautisha maana walikuwa wakifanana mno kama mayai, hadi nikawa najiuliza ikiwa wote wawili watapiga paspoti saizi wakiwa na nguo moja, je wenyewe wanaweza wakajua picha zipi za nani na zipi za nani?

Basi nikainuka na kufungua begi nikachovya kidole changu kisirisiri nikafika kitandani nikijitahidi nisimwagie kwenye shuka. Nilipofika nikamgusha na kile kidole kwenye bega lake. Alama ya wino ikajichora.

Nikajua kuwa sehemu hiyo siyo rahisi kuiona na kufuta ndani ya siku chache, hivyo hiyo ikawa ndiyo silaha yangu ya kuhakikisha nina watofautisha mapacha hao waliokuwa na mpango wa kunitumia mimi kumpata Chriss.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG