Search This Blog

Monday, January 24, 2022

LOVE INTERVIEW - 4

   

Chombezo : Love Interview

Sehemu Ya Nne (4)


LOVE INTERVIEW 33

“hapana siyo mtu wangu ni mdogo wangu anasafiri kesho,” nilimwambia Zainabu akaumbuka na kuondoka, tena kabla hajafika mbali Shose akaniita huko ndani; “kakaaa!” nadhani Zainabu alisikia vizuri tu na kupata uthibitisho.

Nikaingia ndani na kumkuta amevaa tayari.

“sasa kupika sasa hivi sitaweza, twende tukanunue chipsi, nitakulipia,” alisema Shose tukaondoka wote, lakini nilikuwa mbali kimawazo hadi sikuwa naelewa ni nini kinachoendelea akilini mwangu.

Tukiwa njiani nikamuona Shose anapokea simu ya mtu, akawa amesogea kwa mbali kidogo na kuongea naye, na vile alivyokuwa akizungumza alionekana wazi kuwa anaongea na mwanaume.

Nikajiongeza kuwa huyo huenda ndiyo mwanaume ambaye ameahidi kumuoa. Tena kwa mara ya kwanza nikamuona Shose akiwa anaongea na simu na mwanaume, maana nilijuaga kuwa bwana wake alikuwa ni muvi za kikorea na muvi za Kikorea zilikuwa ndiyo bwana wake.

Kidonge cha uchungu kilinikaa kooni, sikujua kwanini. Ila nilikumbukaga rafiki yangu mmoja mtaani enzi hizo, dada yake kipenzi alikuwa akiolewa, sasa yeye alikuwa amekasirika kweli hadi tukawa tunamtaniaga unamaindi nini sasa!

Sasa mimi ndiyo nilipitia hisia hizo za kipuuzi kwa mdogo wangu Shose, jambo ambalo siyo zuri na ni hatari kwa afya yangu.

Nikanyanyua simu yangu na mimi na kumpigia Grace, yule mdada niliyeongea naye kutokea Msasani ili mradi tu na mimi nilipe kwa alichokuwa amekifanya Shose maana alikuwa akizungumza na kucheka na kutabasamu; inaonekana hilo lijamaa lake lilikuwa limemteka vilivyo.

“Hallow, mzima?” nilianza kwa mbwembwe na mimi ili Shose anisikie, kuwa japo kuwa sina kitu lakini nina demu na mimi.

“Mzima tu, John.. naomba nikupigie baadaye kidogo kuna kitu nafanya mara moja.” Alinikatisha Grace roho ikaniuma, maana Shose bado aliendelea kuongea na simu yake.

Basi kama zali palepale simu mpya ikaingia kwenye simu yangu. nikapokea.

“Hallow nani mwenzangu?”

“Oh naitwa Fifi nakaa mbezi, wewe ni Mr John right?” alisema huyo mdada akionekana ananata kweli, tena vingereza vilianza. Nikaanza kumvutia kasi ya jiko la gesi.


LOVE INTERVIEW 34

“oh nimesikia unataka mchumba, nahisi naweza kukufaa, unaweza nichek instagram at ‘fifi’ under score ‘da’ underscore ‘princessa’, yaani ‘fifi da princessa’.” Alisema hilo jina tu likanitumbukia nyongo nikahisi ni walewalee.

“okey sawa naomba uangalie ukiona nipo poa nijulishe sasa hivi,” alisema huyo fifi maana unaweza kukuta jina lake ni Ifikepunye Puhamba au Ngalambila Ngajzhu Ngajzhule au Bandulile Bandua, lakini akatohoa hadi akawa fifi da princessa yote kwa ajili ya instagram.

Basi nikaitikia na kuingia instagram nikaandika jina lake huku nikitazama mbele maana giza la njiani lilikuwa likinizingazinga.

Wakati huo kumbe Shose naye alikuwa amemaliza kuongea na huyo mpumbavu wake. Nilijikuta namuita ‘mpumbavu’ wake kama vile ananihusu, lakini kwa wivu niliokuwa nao nikampa jina hilo; mpumbavu wake tu, ndiyo; sasa atanifanya nini? kwa ni si naongea na nafsi yangu! kwani yako?

“kaka angalia mashimo,” alitahadharisha Shose akionekana mwenye furaha mno.

Basi nikatazama simu ikajiload na uzuri jina la fifi_da_princessa ndiyo la pekee, mle insta. nikaanza kuangalia picha zake, mh! Ndiyo zilezile za ajabu ajabu ingawa alikuwa mzuri mno.

Lakini nikajisemea moyoni, huyo fifi alijua kisa mzuri ndiyo nitadata naye nini? kidogo tu nikaona simu yake inaingia tena.

“Enhee umeniona?” alisema huyo fifi.

“ndiyo nimekuona, lakini kiukweli hapana naona haufai kuwa mke wangu, siwezi kukuoa.” Nilisema kwa kujisahau kauli hiyo Shose akaisikia akanisogelea karibu na kusikilizia upande wa simu yangu naye ili mradi asikie tu umbea.

Sasa baada ya kusema vile nikajua nitasikia mitusi ya kufa mtu.

Cha ajabu nikasikia sauti za vicheko tena nilikuwa kama nimewekwa laudispika; “Hahaaa! Hongera umefaulu mtihani wa kwanza.”

Nikashangaa ni nani huyo.

“John ni mimi Grace bwana, huyo ni rafiki yangu alitaka tu kukupima, si unakumbuka nilikwambia nimeandaa mitihani kwa ajili yako? Huo ni mtihani wa kwanza. Komaa komaa umalizie maswali yaliyobakia unaweza ukanioa. Nitakupigia baadaye usilale mapema..hahaaa,” alisema Grace na kukata simu nikashangaa mno.

“kaka nini? wewe unataka kuoa!?” aliuliza Shasha kwa mshangao.

Itaendelea..


LOVE INTERVIEW 35

“Ndiyo umri unaenda nataka kuanzisha familia yangu na sioni kama kuna tatizo?” nilijibu Shose akanitazama kwa jicho fulani hivi ambalo sikuwa nikielewa alimaanisha nini.

“Ooh kwa hiyo unataka kusema.. aah mh! Huyo uliyekuwa ukiongea naye kwenye simu ndiyo unataka kumuoa nini?” alisema Shose.

“Aah hapana ninampima kama anafaa, sitaki kukurupukia kumuoa mwanamke atakayenisumbua baadaye.”

“mh ni vizuri kama umechukua uamuzi huo..” alisema Shose akinitazama chini kwa chini. Lakini wakati huo tayari tulifika kwenye kibanda cha chipsi tukanunua, Shose akanilipia tukarudi hadi gheto.

“Baada ya kula na mimi nilienda kuoga na kurudi, Shose akataka kunipisha lakini nikamzuia kwa kuwa nilikuwa na pensi tayari ndani ya taulo na kwa joto la dar nilipanga kulala na hiyo pensi hivyohivyo.”

“kwa hiyo kaka tunalala wote hapa!” aliongea Shose akiwa amelala na night dress yake baada ya kuniona napanda kitandani na kulala pembeni yake.

“kwani kuna tatizo gani? kwani ni mara ya kwanza kulala pamoja au?” niliuliza.

“mh hapana, lakini mimi nitalala kwenye kiti,” alisema Shose na kuanza kuamka, nikamzuia kwa kumshika mkono wake maana alikuwa akitetemeka mno hadi nikajiuliza kwa nini Shose alikuwa hivyo siku hiyo.


“Sikia ukitoka nje ya neti kuna mbu balaa, sasa bora uwe mpole ulale tu hapa kitandani,” nilisema Shose akarudi na kulala kiuogauoga akigeukia ukutani na kuniachia mgongo, nadhani alikuwa akifikiria kama nilivyowahi kufikiria mimi enzi zile kuhusu wazo potofu la kuogopa ushawishi wa kufanya naye mapenzi ikiwa tutalala pamoja.

Basi kwa kufikiria hivyo na mimi fikra potofu zikanibeba na nikajikuta naanza kumvua nguo kimawazo Shose nikamuona akiwa kama vile amevua nguo zake zote na kumuona akiwa mtupu bila ile night dress yake.

Niliendelea kuteseka na hisia hizo ovu kwa nusu saa nzima tena hisia hizo ziligeuka katika vitendo maana mkono wangu ulianza kutambaa na kukaribia kumgusa kiuno chake chembamba, lakini zikiwa zimebakia sentimita zero pointi moja, simu yake ikaita. Nikarudisha mkono wangu haraka na kufumba macho kisungurasungura.


LOVE INTERVIEW 36

Nikamuona Shose akiamka na kuitazama simu yake iliyokuwa nje ya kitanda. Tena uzuri upande wangu ndiyo ule wa kutokea kitandani maana upande wa Shose ulikuwa na ukuta, hivyo akitaka kwenda kupokea simu yake ilibidi lazima anivuke mimi na kuteremka.

Nikamchungulia kwa kijicho nusu nikamuona kama vile anajishauri atanivukaje maana akitaka kunivuka vizuri lazima apitishe mkono na mguu yake juu yangu kama vile anataka kunilalia hivi ndiyo kisha apinduke na kufungua neti.

Basi muito wa ile simu ukamlazimisha avuke tu, akafanya hivyo taratibu, akawa juu yangu bila kunigusa, akafunga neti taratibu na kuchukua ile simu, akarudi kwa mtindo uleule. Haraka akarukia upande wake na kutulia kimya akapokea simu yake na kusema maneno kwa sauti ya chini mno.

“nimelala nitakupigia kesho!”

Lakini huyo mtu wa kwenye simu inawezekana hakusikia hata kidogo. Akawa anazungumza.

Tena kwa ukimya wa usiku mtulivu, niliweza kusikia vizuri sauti ya huyo mwanaume wa kwenye simu, Mh mbona ni kama sauti ya Stanis.

Mh! Ndiyo ni yeye? Ndiyo mtu anayetaka kumuoa Shose, au nimechanganya sauti? Hapana ni yeye. Ni yeye mpumbavu yule. Shit!

Ghadhabu zikanipanda sasa, sikutaka tena kudanganya kama nililala, nikajigeuza na Shose aliposikia tu nimeamka akaikata ile simu yake na kutulia kimya.

“Shose, vipi? Umenishtua!” nilisema nikijaribu kuanza maongezi.

“samahani!”

“hebu geuka kwanza huku!” nilimwambia nikitaka tutazamane uso kwa uso. Akajigeuza na kunitazama.

“Shose kesho unaondoka! Tungeagana kabisa si ndiyo?”

“Mh ndiyo? Haya niage.”alisema kwa kusitasita nadhani alikuwa akiingiwa na fikra potofu.

“Nikamsogelea karibu zaidi, akarudi nyuma kwa uoga, nikazidi kumsogelea, akarudi nyuma zaidi hadi akagusa ukutani na hakuwa na kwa kurudi nyuma tena, nikamsogelea karibu zaidi nikambana hadi nikasikia mapigo ya moyo wake yakidunda kwa nguvu mno.

“Kaka John! Unataka kufanya nini! sitakii bwana!” alianza kulalamika Shose kwa sauti mpya ambayo sikuwahi kuisikia kutoka kwake, ilikuwa ni sauti nyororo ya kitandani ambayo ilisisimua ile mbaya.

Itaendelea..


LOVE INTERVIEW 37

Siyo siri Shose alikuwa kama sumaku iliyonivutia kwake, sikurudi nyuma nikamsogelea zaidi na kumbusu kwenye paji la uso.

Halafu nikasema; “safari njema, Shose.. nitakumiss sana,” kisha nikaganda hapohapo kama sanamu ya askari wa posta. Nikamuona akishusha pumzi na kushindwa kusema chochote. Badala yake akawa ananiangalia tu, bila kupepesa macho.

“Aah anayetaka kukuoa ni yule jamaa aliyekuja kututoa nyumbani si ndiyo?” niliuliza moja kwa moja nikijua kwa ukaribu niliokuwa nimembana Shose hawezi kudanganya.

“Ndiyo,”

“Yule hakufai kataa!” nilimwambia.

“kwanini kaka?”

“Shose usijishushe hadhi yako, wewe ni msichana mzuri sana mwenye heshima zako, yule ni..” nilijikuta nikishindwa kumalizia.

“Kaka, amenitongoza hadi ananipigia magoti, nikamwambia kama yupo siriaz aende kunitolea posa kijijini, huwezi amini alitaka tuongozane wote, ila nikakataa. Hapa ananisubiri tu nisafiri ili aje kijijini. Ila kwanini na yeye ananiulizia kama nipo na wewe leo, tena anaonekana kukasirika hivyohivyo, kwani nini kinaendelea kaka John!?” aliuliza Shose, nikaanza kujadili mwenyewe kichwani aidha nimwambie ukweli au nisimwambie.

“Sikia, kwani yeye amekwambia nini kuhusu mimi?” niliuliza.

“wakati naondoka, aliniambia kuwa anajua mimi na wewe ni wapenzi, lakini alisema hajali yupo tayari kunioa mimi bila kujali nilitembea na nani. Tena akaniambia kuhusu tabia yako na alishangaa kwanini nakuvumilia.”

“tabia gani?”

“si ya kubadilisha wanawake ovyo,”

“mh!”

“mimi nahisi kama vile mnajuana, ndiyo maana nimetatizika, naomba uniambie ukweli kaka,”

“Ok. ndiyo ninamjua vizuri yule mpumbavu ni mfanyabiashara mshindani wangu namba moja, siku zote alikuwa akitamani kuwa na kila kitu nilichokuwa nacho, ndiyo maana wakati benki inatangaza mnada yeye akawa wa kwanza kununua ili mradi tu anikomoe, sasa anakutaka hadi na wewe ili mradi tu afurahi.” Nilidanganya.

“Anhaaa, sasa nimeelewa, ila kaka wa watu anaonekana kunipenda kweli hadi alikuwa akinipigia magoti!” alisema Shose akazidi kuniuzi sasa nikarudi nyuma kwa hasira.

“unajua nini kuhusu mapenzi Shose! kukupigia magoti hakuna maana yoyote, anataka tu akutumie akimaliza haja zake hilo goti utakuwa unampigia wewe.” Nilifoka.


LOVE INTERVIEW 38

Nikajishtukia; nikashusha sauti kidogo: “sikia Shose mimi nakupenda sana, ningetamani sana nikuone unapata mtu mwenye akili zake na mwenye mapenzi ya dhati kuliko huyo mpumbavu.

Kwa haiba yako, hata mimi nakuogopa ndio maana sijawahi kukukosea heshima, lakini siyo eti uende kujiharibu kwa yule mpumbavu kwa taarifa yako yeye ni malaya kuliko mimi!”

“ila kaka..mbona sikuelewielewi?”

“Shose, nimekutazama tangu ukivunja ungo nyumbani kwangu, nimekuzoea sana, sijui kama ukienda kwa mtu mwingine nitaishi vizuri, ulikuwa ukinifanyia kila kitu nimemiss chakula chako na kukutazama ukienda na kurudi. Sema nikupe shilingi ngapi ili mradi tu usiolewe na huyo mtu wako,” nilisema kwa hisia hadi nikapitiliza.

“ha! Kaka, kwa nini unasema hivyo? Angalia mimi ni mdada sasa hivi, sijasoma, masikini tu, hivyo kuolewa kwangu ni bahati mno,kwa sababu mama na baba yangu watafurahi, hayo masuala ya migogoro kwenye ndoa yapo tu, hivyo siwezi kuiacha nafasi hii kwa ajili ya wewe kuendelea tu kuridhisha macho yako kwa kunitazamatazama tu, ushauri wangu hiyo hela fanyia mambo ya msingi kwanza, kwa sababu sitaitaka,” alisema Shose maneno yaliyoniingia mno.

Nikakumbuka ujumbe mmoja hivi niliusoma instagram aliupost @superneyma unasema: Usiolewe kwa sababu rafiki zako wote wameolewa. Usiolewe kwa sababu umemaliza masomo na hauna kazi. Usiolewe kwasababu wazazi wanataka ufanye hivyo. Usiolewe kwa sababu umri unaenda. Ndoa siyo jumuiya. Ndoa siyo kwa ajili ya wazazi wako. Ndoa siyo kuondoa nuksi. Ndoa sio hadhi. Olewa kwa sababu Mungu amekukutanisha na mtu sahihi.

Basi nikamtamkia maneno hayo Shose, nikamuona anashusha pumzi kwanza kisha akasema:

“Kwa hiyo umesema, Stanis siyo mtu sahihi kwangu? Sasa nataka unitafutie huyo mtu unayehisi atanifaa mimi. Nakupa miezi minne na ukishindwa utanioa wewe.” Alisema Shose kwa ghadhabu na kunigeuzia mgongo akionekana amenuna kweli.

Nikasema: “Naapa ndani ya miezi minne nitakutafutia mtu sahihi. Na nikishindwa ndiyo nitakuoa mimi.”

Mara kidogo simu yangu ikaita. Nikacheki ni Grace.

Itaendelea..


LOVE INTERVIEW 39

Nikaichukua simu yangu taratibu kwa sababu Shose alikuwa akinitazama ile mbaya, nikapokea na kuiweka sikioni, lakini Shose akanipokonya na kuiweka laudispika, mimi na yeye tukawa tunasikiliza.

“Hallow, niambie, pole kwa mtihani wa saa ile. Nilikuwa nakupima si unajua tena nyie wanaume mnatamaa sana, sasa nimegundua kuwa kumbe wewe kweli unatafuta mke na si demu tu wa kuzuga naye, ndiyo maana ulienda kutangaza kanisani,” alisema Grace bila kujua yupo laudispika.

“Poa, bwana,” nilisema huku nikiishiwa maneno kadri nilivyokuwa nikimtazama Shose, maana aliamua kukaa kabisa kitandani.

“vipi mbona unazungumza kwa sauti ya chini hivyo, upo peke yako kweli?” aliuliza Grace nadhani alisikia kitanda kikinyekuanyekua wakati Shose alivyokuwa akikaa.

“yah nipo peke yangu!” nilijibu.

“sikia John, kama nilivyokwambia lazima nikupime kabla hatujaonana hiyo kesho, inaonekana mtihani wangu wa kwanza umeufaulu vyema, lakini nina mtihani wa pili; upo tayari?”

“Ndiyo nipo tayari!” nilijibu kinyonge, Shose akatega sikio lake kwa karibu mno kusikiliza, kitanda tena kikalia: “nyeku!”

“Sikia John, moyo wangu unanifanya nihisi leo haujalala peke yako hapo kwako, sasa mtihani wangu wa pili nataka useme kwa sauti sema: I love U baby, wewe ndiye ninayetaka kukuoa, huyu wa hapa pembeni yangu namchezea tu na hana nafasi katika moyo wangu!” alisema Grace nikamtazama Shose naye akanitazama mimi; kichwani nikafikiria huyo Grace ni mtu au shetani, amejuaje kama nipo kweli na mtu?

Lakini atakuwa ameotea tu, kwa sababu nilikuwa na mdogo wangu Shose, na hakuna chochote kilichonizuia kusema maneno hayo; kidume kama boya nikafungua bakuli langu na kusema: “I love U baby, wewe ndiye ninayetaka kukuoa, huyu wa hapa pembeni yangu namchezea tu na hana nafasi katika moyo wangu!”

Wakati namaliza kusema hivi, Shose akaweka mikono mdomoni na kuwa kama vile anazuia kicheko, nikamuwahi na kum-shiiiiii! Ili asije akasikika nikaharibu session.


LOVE INTERVIEW 40

“hahaa! Waoh hongera kumbe kweli upo peke yako, sasa usiku mwema, kesho tuonane pale Mbezi Beach Bondeni saa nne, nataka nikuone kwanza ulivyoulivyo na mimi unione nilivyo ili tupimane kama tunaendana,” alisema Grace na kukata simu.

Mh hata mimi nilishangaa, Grace japokuwa alikuwa akiongea taratibu, lakini alionekana kuniwahi kwa kila stepu. Ilionekana siyo mimi tena namfanyia interview yeye ila yeye ndiye alikuwa kama vile ananiinterview mimi. Na hiyo hali siipendi.

“Mh kaka John kwani vipi? Huyo Grace si ndiyo wa saa zile? Enhe halafu kumbe kwenye kuoa upo siriaz kiasi hicho hadi ulienda kutangaza kanisani?” aliuliza Shose.

“siyo kutangaza bwana, niliomba misa ya kupata mchumba mwema, nadhani padre aliwapa waumini wake namba yangu,” nilijitetea.

“Mh! Kwahiyo kaka, mbona huyo mdada anaonekana kama vile anakuchekecha?”

“aah! Achana naye!” nilisema.

“haya bwana nakuombea awe wifi yangu mzuri, akujali kwenye shida na raha.. japo sitasafiri ila kesho nitaenda kutafuta chumba maeneo ya karibu, sitaki hao watu wako waje halafu wasikie eti unalala na mdogo wako chumba kimoja, itakuwa siyo vizuri. Pia usisahau tulichoahidiana la sivyo utanioa kilazima,” alisema Shose, kidogo nikapata faraja kuwa angalau atakuwa karibu na mimi katika kipindi hiki cha interview halafu nikishampata tu huyo wifi yake haoo tunarudi zetu kwenye raha mustarehe.

“Okey, lakini Shose nataka hata wewe ujifunze kupitia huyu Grace, umeona anavyonipima? Na wewe kuwa unampima mtu wako kwa vipimo hivyohivyo, usimkubali tu kisa eti anataka kukuoa.

“sawa kaka, usiku mwema,” alisema Shose akafumba macho yake, nikamtazama akilala mubashara, bila tena kuniogopa, akaingiza kidole chake mdomoni kama ishara ya usingizi mwanana wenye ndoto njema.

Mara hii nikasema; natamani huyo Grace awe na haiba kama ya Shose.



Kesho yake asubuhi nilichofanya mapema ni kumtafuta dalali ili nimsapraiz Shose aliyekuwa amedamka kudeki na kupika chai, nikatafuta chumba kizuri chenye hadhi zaidi ya hata cha Stanis, nikanunua godoro, dressing tebo na kitanda, na wakati naondoka nikampigia Shose na kumuunganisha na yule dalali ili aende kuangalia hicho chumba chenye choo na bafu ndani, maana nililipia miezi sita full.

Wakati huo huyoo nikapepea kuelekea tulipoahidiana na Grace kule Mbezi beach kituo kinachoitwa Bondeni, nikawa kama mshamba maana sivijui vituo, yote kwa kuwa mara nyingi huwa ninakuwa na usafiri binafsi. Ikabidi nimwambie konda mapema kuwa anishtue nikifika kwa kushukia.

Hapo ndiyo nikatambua kuwa mtu akiwa anajua vituo sana ujue huyo mtu ni wa daladala sana, maana bora mwenye baiskeli, we fikiria kila muda wewe na daladala tu konda anakupigia kelele kituo cha mwanzo hadi cha mwisho, sasa utashindwa vipi kukariri ki lazima.

Hii sikukwambiaga, kuna wakati nilikuwa napokea meseji za wasichana kadhaa, wengine wakiandika tu, Hi! Wengine wakibipu na kujichekesha halafu wanakata simu. Wengine walijitahidi kupiga simu na baada ya kunisikia wakajifanya; ooh nimewrong namba, sasa kwa tekniki hizo sijui walidhania eti nitawapigia na kuanza kuwatongoza?

Hawanijui, ndiyo kwanza wakinianza nilikausha tu kimya, maana kama wanajiamini wanipigie basi kama wenzao, wachache walioamua kabisa hadi kunililia niwaoe. Duh ama kweli ilisikitisha mtu analilia ndoa hadi nikawa najisikia vibaya.

Mmoja aliandika eti nikimuoa yupo tayari kuwa kama mtumwa ili mradi kuniridhisha kwa kila kitu, ninachotaka, nikajiuliza ina maana yeye hatajijali? Huo ni uongo na kutaka kuibiana tu saa hizi.

Mwingine alikuwa mikoani huko sijui namba yangu aliipata wapi, alikuwa akinipigia kila saa na rafudhi yake ya kijijini hadi akawa ananikera.

Basi vimbwanga vyote hivyo nilivikumbuka nikiwa ndani ya daladala nilipokaribia kituoni, Konda alinishtua kuwa nimefika sehemu husika hivyo nikashuka zangu na kusimama pale kituoni maana walikuwa wamepajengea vizuri kweli.

Nikaangalia saa yangu na kugundua kuwa nilichelewa kwa dakika tano, nikapiga simu Grace akapokea.


LOVE INTERVIEW 42

“Hallow, dear John umefeli mtihani wangu. Tuliahidiana saa nne kamili, nimefika hapo kituoni sijakuona nimeamua kuondoka.unaonekana wewe siyo mzuri kwenye kujali muda na maana yake hata kutimiza ahadi unaonekana pia ni mgumu, bye!” huwezi amini Grace alisema hivyo. Nikajiuliza kwa kipi sana alichonacho huyo msichana kiasi cha kunizungusha hivyo, hivi anajua mimi ni nani? yaani dakika tano tu!

“Grace, acha utani bwana, sasa hivi ni saa nne na dakika tano. Ujue nimetokea mbali,” nilianza kulalamika.

“Okey nakuonesha kuwa unatakiwa kuwa mtu wa kujali muda, sijaondoka lakini umeniudhi, haya niambie umevaa nguo gani kwani?”

“nimevaa shati la mistari myeusi, wewe je?” niliuliza.

“gauni la bluu,” tayari nilishakuona.

Aliposema hivyo nikawa natazamatazama kila upande, ili nione wapi huyo Grace alipo, mara nikamuona mdada mmoja bonge ile mbaya mwenye gauni la bluu ananishika bega, nusura nikimbie.

“wewe ndiyo John?”

“hapana siyo mimi!” nilirudi nyuma na kutamani gari lolote lije nitumbukie maana hii ni dhahma, mtu anajifanya ana mitihani mingi kumbe hana muonekano kabisa, hapana yamenishinda.

Wakati nafikiria hivyo, kuna mdada mweusi wa chokleti akatokea nyuma ya yule Grace mbaya; “halloo, John, samahani. Niliogopa kujitokeza kwanza, huyu ni rafiki yangu anaitwa Ndumbagwe, mimi ndiyo Grace uliyekuwa ukiongea naye kwenye simu.”

Moyo ukashuka kasi, nikajisemea kimoyomoyo; “afadhali loh!”

“Asante kwa kukufahamu, tukakae wapi ili tuongee kwa kirefu,” nilisema maana huyo Grace hakuwa mwanamke wa mchezomchezo, alikuwa amepanda, ngozi laini kama ya nanihii wa humu insta atajitag mwenyewe akijijua. Alikuwa na nywele za asili, alizichana tu kwa mtindo fulani, waoh ana dimpoz.. uuuuhuuhuu, jamani ana dimpozi kweli tena kashanivuruga!

Mguu wa bia waooh kanyooka ile mbaya, mazee kifua chake standard, naweza kulala nikaamshwa wiki ijayo.

Hipsi bunduki, shepu ya kila atakapopakalia. tena huyu angalau naweza kumpeleka kwa Shose nikamtambulisha kidogo nikaonekana nimempelekea wifi kweli.

Kwanza nimeghaili na interview yenyewe basi. Narudi kwangu, natangaza ndoa haraka.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG