Search This Blog

Monday, January 24, 2022

LOVE INTERVIEW - 1

  

IMEANDIKWA NA : CHANDE ABDALLAH 

********************************************************************************

Chombezo : Love Interview

Sehemu Ya Kwanza (1)


Naitwa John Stephen nina miaka 35, ni mkurugenzi wa kampuni ya masuala ya bima ‘J.S Insurance Company’ ni mkazi wa jijini Dar, sijaoa, sina mtoto; kiujumla maisha yangu ni mazuri tu na ninafuraha na ninamshukuru Mungu kwa kunibariki katika kila kitu katika maisha yangu.

VIjana wananitazama mimi kama mfano wa kuigwa na mimi ninawatia moyo; wafanyakazi wangu wananitazama kama kiongozi wao na mimi ninawaongoza vyema kazini na wanaofanya kazi kwa bidii ninawaongeza mishahara.

Vijana wenzangu wananitazama kwa wivu na mimi nazidi kupambana ili utajiri wangu uongezeke na nisiteremke chini.

Wanawake wananitazama kwa jicho la tamaa kila mmoja ananitaka, mimi nakuwa nao makini mno kwa kuwa najua wanachotaka kutoka kwangu haswa ni hela zangu; na mimi nawataka kwa ajili ya kupoza haja zangu na nikishawapitia tu nawakimbia kama ukoma.

Mama yangu naye ananitazama kama mwanaye kipenzi, kila siku alikuwa akinisisitiza nioe ili afe akiwa ameshuhudia mjukuu maana hata yeye amechoka kusikia nabadilisha wanawake kila siku, pointi yake nyingine kubwa utasikia: “mwanangu, nani atarithi mali hizi zote ukifa leo?”

Maneno yake yana mantiki lakini nina wasiwasi nimuoe nani kwenye dunia hii iliyojaa kila aina ya uchafu, usaliti, kutokuaminiana na maumivu ya mapenzi?

“hapana mama kuoa kuna kuja tu kwenyewe lakini siyo kwa kupanga kama unavyosema,” ndiyo jibu langu kila siku kwa mama.

Nilimvunja moyo nikamuona akizidi kuzee na sura kujikunja kwa unyonge, lakini sikujali kwa sababu suala la ndoa ni langu na mustakabari wa maisha yangu yajayo? Hivyo nilitakiwa kuwa makini mno kwani nikikosea nitakayejuta ni mimi na siyo yeye.


LOVE INTERVIEW 02

Siyo kwamba nakuwa muoga hapana, ni kwavile nimepitia mahusiano, nimejionea kwa marafiki na ndugu na mwishowe kabisa nimesoma vitabu na kuangalia muvi, kote huko nimejifunza natakiwa kuwa makini mno kwenye hili suala, tena ukitilia maanani mimi ni mkatoliki ambaye ndoa ikifungwa haivunjwi tena hadi kifo.

Niliondoka kwenye nyumba niliyomjengea mama na kurudi zangu kwangu, nikiwa kwenye gari yangu aina ya Nissan Murano. Nikapiga honi nilipofika geti la nyumba yangu maeneo ya Bahari Beach. Mlinzi alifungua na kunisalimia kwa heshima zote, nilimuitikia na kuingia moja kwa moja ndani.

Nilikuwa naishi peke yangu na hausigeli wangu ambaye ni kama mdogo wangu, Shose ambaye nililetewa na mama akiwa amemtoa Tanga kwa sababu tu ya kujua kupika. Tangu nikiwa mtoto niliapa nikiwa na hela sitakula chakula kibaya hata siku moja na Shose alikuwa na kazi hiyo tu kunipikia chakula ambacho kikitua kwenye ulimi wangu kinanisisimua.

Aliponiona tu Shose akanipokea begi langu na wakati huohuo harufu ya msosi uliojitosheleza ukapenya kwenye pua zangu na kunifanya niwe na hamu ya kula, hivyo ndiyo nilivyokuwa nikitaka, yaani unarudi nyumbani ukiwa haujui kuna chakula gani ukifika tu unasikia harufu tamuuu! inakuwa kama sapraiz vile.

Niliingia chumbani kwangu na kuoga haraka nikatoka na kukaa dining room ambapo chakula kilikuwa kimesetiwa.

“kaka karibu chakula,” alisema Shose nikakimbilia kufungua poti na kukuta wali uliokola nazi ukinukia, poti jingine makorokoro hadi raha nikala vyakutosha na kwenda zangu sebuleni nikaangalia muvi fulani za kutisha nikishushia na juisi.

“kaka umeniletea, zile Cd za Kikorea?” aliniuliza Shose.

“ooh aisee nimesahau, ngoja kesho nitakupa hela ukanunue mwenyewe, halafu kesho kuna wifi yako mmoja atakuja andaa kila kitu vizuri,” nilimjibu Shose akaonekana amenuna kidogo akaingia chumbani kwake.

Itaendelea..


LOVE INTERVIEW 03

Nikiwa nimekaa pale mara kidogo nikapokea simu kutoka kwa Faraja ikisema; “hi, love umelala?”

Huyo ndiyo huyo demu atakayekuja hiyo kesho, ni msichana mzuri mno kwa kumtazama. Tena kama mademu wengine wanaonishobokea, niliona anakuja kasi kweli, maana nilikutana naye juzi alipokuja ofisini kwangu, alionekana kushangaa kijana mdogo kama mimi halafu ni mkurugenzi wa kampuni kubwa kama ile, palepale alionekana kujibebisha.

Nilipompa business card yangu ndiyo ikawa makosa, akaanza kujichatisha ovyoovyo, na mimi sikulaza damu nikamdumbukizia madini, ha! Eti alikubali siku hiyohiyo na akataka kuja kwangu. Najua atakuwa amenipendea hela na si chochote. Tena Wanawake wa hivyo wanaganda mno watu ila dawa ya kuwagandua ninayo.

Kwa hiyo kesho anataka kuja nyumbani kwangu. Sawa, atapata raha ya kuwa na mimi kwa siku moja na mimi nitapata raha ya kumfaidi na kuongeza idadi ya mademu niliowapitia kwenye dayari yangu na baada ya hapo atanisikia kwenye bomba kama mademu wengine wa dizaini yake.

Nikamjibu, “bado ninaangalia muvi!”

“ooh muvi gani, love story?”

Mh huyu vipi anahisi mimi romantic nini? kwa hiyo hapa angetaka nisemeje; ndiyo natazama love story! Lakini hapana ya nini kudanganya? kwani hata nikimwambia ukweli atanifanya nini? kashanasa huyu, si amenipendea hela? Hapo hata nikisema ninademu mwingine bado tu ananing’ang’ania, si atanitaka cha mfukoni?

Nikamjibu; “Naangalia muvi ya kizombi inaitwa Warm Bodies”.

Basi akanijibu; “waooh na mimi napendaga hizo, kesho nitakuja tuangalie wote au siyo baby?”

Kimoyomoyo nikamjibu; Nyooo! eti unazipenda!. Hata kama hauzipendi utakataa unafikiri?

Ooh sikujua, nitakuandalia kesho. Niliandika meseji hiyo, nikitaraji ataniacha basi angalau niangalie muvi maana ilikuwa imenoga kweli hapo Zombi lilikuwa likimtafuna demu mmoja hivi. Lakini Faraja akaendelea kunichatisha, ikabidi nipozi kwanza muvi yangu nisome meseji yake.


LOVE INTERVIEW 04

“mh haya mpenzi ila ninavyochati na wewe hivi hadi mwili unasisimka!” ilisomeka meseji ya Faraja, nikacheka nakujionea vioja. Huyu hanijui eeh, mimi mwenyewe mtoto wa mjini, niliwaza na kuingia google nikaandika black pen*s nikasachi image, nikaangalia picha mbalimbali za ma-uume nikadownload moja kisha nikaituma kwa Faraja nikaandika: “mh hata mimi umeniwasha ile mbaya angalia, mwenzako.”

Ha! Basi eti akaamini kabisa kuwa nimejipiga picha ya mshedede wangu na kumtumia, eti na yeye ndiyo akanitumia picha zake, akiwa uchi tena nyingine amejimanua kabisa.

Akaandika: “jamani kesho mbali, njoo sasa hivi” niliposoma nikacheka, angejua mwenzake niliigoogle. Basi kwa yeye kunitumia picha zile nikaanza kumfanyia upembuzi yakinifu, nikampembua akapembuka; nikaona ni malaya tu kama malaya wengine.

Yaani kwa wale ambao hawafahamu ni kwamba, malaya ni mwanamke ambaye anakuwa na uhusiano zaidi ya mmoja kwa ajili ya maslahi, lakini anafanya kwa siri; malaya akiwa mstaarabu ndiyo pengine anaitwa goldigger yaani mchunaji, yaani unakuta anatulia kabisa kwa mtu mmoja mara zote mwenye hela zake ‘sponsor’.

Hapo ataigiza kama ana mapenzi ya kweli utapendwa ile mbaya, kumbe ‘ugali-kunguru’ anakuchuna zikiisha anasepa. Hayo ni makundi ya kuyaogopa kuliko hata machangudoa ambao wanajiachia tu barabarani bila siri. Na kwa wanaume nao wapo wa hivihivi.

Kwa hiyo nilianza kumuweka Faraja katika kundi la malaya wa aina ya goldigger ambaye anataka kuwekeza mtaji wa mapenzi kwa ajili ya kupata maslahi kwangu, tena hapo utakuta ana bwana wake lakini yupo tayari kumsaliti kwa ajili yangu, tena unakuta atataka kabisa nimuoe, “Haa! Nani akuoe mwanamke mchafu kama wewe.”nilijisemea.

Nikamtumia viemoji vya vikopakopa kisha nikazima na simu yenyewe kabisa kwasababu kwa wakati huo muvi ilikuwa tamu kuliko yeye, kwa sababu anakitu gani kipya, kama ku** nimeziona nyingi nzuri kuzidi yake, tena hadi zenye tivii ndani.

Itaendelea.

LOVE INTERVIEW 05

Niliangalia ile muvi hadi ikaisha, sasa nikainuka zangu na kwenda kulala chumbani kwangu, tena nilipenda mno Shose alivyonitandikia shuka jeupe, maana naamini lilikuwa likileta ndoto njema na mtu kuamka ukiwa na nguvu.

Basi nikalala zangu doro hadi asubuhi, tena kwa kuwa nilichelewa kulala niliamka nimechelewa pia, lakini sikujali kwa kuwa ilikuwa ni jumamosi sikuwa na nilikuwa mapumzikoni.

Nikaoga zangu vizuri nikaangalia saa kumbe ilikuwa saa tano kasoro na simu yangu sikuwa nimeiwasha, nilipoiwasha tu nikapokea meseji mfululizo kutoka kwa watu kibao, lakini hasa kutoka kwa Faraja meseji kama saba hivi.

“mambo?”

“mh. Mbona kimya jamani?”

“mh au umeniona mbaya!”

“poa tu!”

“usiku mwema..”

“kwa hiyo nijiandae nije?”

“jamani, John mbona haupatikani? Tatizo ni nini..mpenzi wangu, nakupenda mbona unakuwa hivyo?”

Nilisoma meseji zote hizo na kuongezea kwenye upembuzi wangu, kuwa Faraja siyo tu ananitaka kimaslahi lakini pia alikuwa mjinga na mtu asiyejiamini, nawachukia sana wanawake wa aina hii. Ndiyo unakuta unamuoa lakini anakuwa na mawivu hadi utalia. Kwani lazima meseji zote hizo? Moja tu si ingetosha?

Hapo nilizima simu lakini kama ningeiacha hewani ndiyo unakuta missed call mia tatu.

Basi ile naanza kupitia meseji za msingi tu simu yake iliingia.

“hallow, jamani Johnnnnnnyy,” aliongea Faraja akijitahidi kuiweka sauti yake iwe nyororo kama kinanda, ingawa sauti yake ilikuwa ya kawaida. Kwa hiyo alikuwa akifeki sauti. Tena msichana wa hivyo unakuta ana sauti zaidi ya kumi. Ya kuombea hela,ya kuombea ruhusa ya saluni, ya kuombea dela, ya kuombea ruhusa ya kwenda kwenye mdundiko, ya kudanganyia, ya kutoka kulala, ya kudai madeni ya vicoba, ya kumchambia mwenzake, ya kitandani, ya kukusingizia unatembea na fulani na nyingine nyingi mnisaidiage wenyewe.

“mambo! Simu ilikuwa imeishiwa chaji, ndiyo naamka sasa hivi, niambie?” nilimjibu.

“ooh ndiyo najiandaa kuja, nielekeze basi,” alisema Faraja.

“Ni hapa bahari beach kituo kinaitwa Uzunguni,”

“Sawa nakuja na bajaji nikifika hapo nitakupigia simu unielekeze.”

LOVE INTERVIEW 06

“sawa,” niliitikia na kujiongeza kuwa hapo hata hiyo hela ya bajaji natakiwa nilipie mimi, nikacheka kwa dharau na kuingia zangu dinning Shose akiwa ameniandalia chai.

“shikamoo kaka, nataka kwenda sokoni,” alisema Shose nikamuelekeza chumbani kwangu kwenye droo. Akachukua elfu hamsini na kuondoka nazo, shilingi elfu kumi ilikuwa kwa ajili ya hizo tamthilia zake za Kikorea maana mwenyewe alizipenda balaa.

Mimi basi huko nyuma nilipomaliza kunywa chai yangu vizuri, nikaenda kukaa kwenye kochi kiusingizi cha shibe kikinipitia.

Nilishtuka kumbe Shose alikuwa amesharudi tena alikuwa ameweka CD yake palepale sebuleni akiwa anatazama. Nikaona ananikera tu, nikainuka mara simu ikaingia alikuwa ni Faraja: “hallow nipo hapa Uzunguni muelekeze bajaji”. Basi nikamuelekeza na kuingia chumbani kwenda kuangalia kama kuna kondomu zangu maana natumiaga tatu bomba na shoo yangu vile vitatu vyote navimaliza.

basi ile kidogo tu nikasikia honi hapo nje, sikutaka Shose aende, nikatoka zangu nikiwa mkononi na shilingi elfu thelathini, mlinzi akafungua mlango na nikamuona Faraja akiwa amejipigilia kiskini chake kilichomchoresha ile mbaya. Basi nikamuuliza dereva ni shilingi ngapi akaniambia elfu ishirini nikampatia ile hela na kuingia na goma langu ndani.

Njia nzima lilikuwa likishangaa, nikaingia nalo ndani na kupita palepale sebuleni Shose akitutazama na kuzuga kama anaangalia televisheni vile, najua alikuwa ameshazoea maana kwa madude ninayoingiaga nayo ndani kama kutumbuka macho nadhani tayari kashatumbukaga zamani. Ndiyo azoee tena kaka yake siyo mtu wa mchezomchezo.

Basi tukiwa ndani nikampooza Faraja kwa juisi, alipokunywa kidogo tu basi akaanza kunikalia kihasarahasara macho yake yakiniita, nami nikasema rabeeka.

Sikutaka kufanya ufundi sana, kwa kuwa haikuwa na haja yoyote, nikamgusaguza tu kifuani na kunyonya mtindi wake uliolala kama embe za chole, nikavaa mpira na kuingiza upanga wangu ukaingia mzimamzima pyuuu. Mh siyo kwa shimo hili, nilijisemea mwenyewe na kuanza kushindua, eti naye alikuwa akilalamika huyo eti “ooh mpenzi mtamu , unanipasuaa ahaaa Johnyyy ashhhh.” Nikajichekea kimoyomoyo.

Nikatamani nimeambie: “we hebu funga bakuli lako hapa! uongo kapeleke kwa maboya wako huko, siyo mimi.”

itaendelea


LOVE INTERVIEW 07

Basi nikamnyosha vizuri, nilipomaliza nikainuka na kwenda kuoga kutoa nuksi. Niliporudi nikamkuta bado amelala kitandani, ikabidi nimuwahishe kwenda kula maana nilitaka nimkimbize aondoke kwa kuwa mimi mwenyewe nilikuwa nimeahidiana kumtembelea rafiki yangu wa muda mrefu ambaye nilikulia naye mtaa mmoja Mr Stanis.

Faraja akaamka pale kitandani na kuniambia maneno mawili; “baby asante.”

Woah najua vilivyo hii tekniki ya mademu, ukimaliza kufanya mapenzi wamefundishana eti wawashukuru wapenzi wao kwa asante. Hoohooo najua hiyo ujanja. Nikaona nimzungue; “asante ya nini?”

“mh jamani ulivyonifanya unadhani kazi ndogo!” alisema basi nikatabasamu kisungurasungura, akaingia bafuni na kuoga akavaa nguo zake full tukatoka kwenda dining room.

Uzuri wa Shose alikuwa ameshaweka kila kitu mezani na alikuwa hakoseagi.

Basi Faraja akala kisistaduu na mimi nikala kiume.

Nikamchukua kwenye gari na kuondoka naye, nikamuacha Kinondoni Mkwajuni kwao na mimi nikanyoosha Mbagala kwa mshkaji wangu. Nikiwa kwenye gari nilichofanya kwanza ni kuweka blacklist namba ya Faraja na kuondoa flight mode niliyoiweka kwenye simu muda wote niliokuwa na Faraja.

Kwa sasa nadhani umeshanijua mimi ni mwanaume wa aina gani. Siamini katika mapenzi, sipendi, sitopenda, ninachofanya ni kucheza tu na mademu; na siyo kuwachezea hapana maana kuna demu mmoja baada ya kutembea naye na kumuacha akawa analia, eti ooh umenichezea halafu umeniacha!

Wee! nani kasema nimekuchezea, si ulikuwa ukinisapoti kwa viuno, si ulikuwa ukienjoy mchezo, maana yake basi tumechezeana na sijakuchezea.

Mwengine akasema; ooh umenipotezea muda wangu, na hata huyo naye nilimjibu hivyohivyo. Kikubwa natumia muda nilionao kuenjoy ya nini presha ya kuwa na mtu kwenye uhusiano halafu yakukute!

Basi nikafika kwa mshkaji nikamkuta akiwa amekaa kwenye grocery moja hivi, tukawa tunapiga stori mbili tatu yeye akinywa pombe mimi nikikataa kwa sababu situmiagi. Jamaa ni kama mimi tu yaani, umri umeenda lakini hajaoa, wala kuwa na mtoto wa kusingiziwa. Ukiuliza tatizo nini? anasema hayupo tayari.


LOVE INTERVIEW 8

Hata mimi sipo tayari. Tena hasa kuhusu mtoto mimi nawaogopa watoto sana nawaona viumbe wa ajabu wanaoleta fujo na kero ndani ya nyumba na mbaya zaidi, unakuta toto jingine linazaliwa limefanana na wewe hadi unaogopa. Unakaa halafu unajiona; mimi mdogo yulee anatembea. Hapana hata mimi sipo tayari inatisha.

Sasa kwa kuwa tulifanana kimtazamo tuliweza kukaa na kuongelea kuhusu maisha lakini mwishowe lazima tutarudi tu kwenye mada ya wanawake na visa vyao.

Mfano siku hiyo tulikuwa tukizungumzia suala la je, ni vyema kuoa mwanamke anayekupenda au unayempenda wewe?

Mimi upande wangu ukawa; bora uoe mwanamke unayempenda wewe, yaani hapo nikawa namaanisha mwanamke mzuri kama Wema Sepetu au pengine Lulu.

Jamaa upande wake ulikuwa bora aoe mwanamke anayempenda na si yeye kumpenda huyo mwanamke.

Tukajadili na kufafanua, nikakumbuka historia yangu kiukweli nilishawahi kupendaga nikatendwa, ndiyo maana pengine nimekuwa mkakasi kiasi hiki. Uzuri, raha ya kupenda naijua tena unakuwa kama chizi juu ya mtu fulani, hata wakisema nini wewe hewala tu. Hata ukimuona anachepuka unaweza kumsamehe hadi watu wakasema umewekewa limbwata. Pengine kwa sababu tu ya kupenda yaani ukimuona huyo mwanamke moyo wako wasuuzika. Napenda kupenda tena, sijui nitapenda tena lini? Maana tangu yanikute moyo wangu umekuwa ukisukuma damu tu hadi inakera.

Mshkaji katika kutetea hoja yake akasema kuwa yeye bora apendwe, tena akasema msichana akikupenda atakuwa anakufanyia mambo mengi mazuri na kukucare hadi raha na hatakusaliti, kwa shida na raha.

Akakandamizia kuwa madhara ya kupenda mtu asiyekupenda ndiyo hayo mwishowe unajiua kama tukio la juzi Facebook. Mh hiyo nayo ikawa ni pointi.

Na mimi nikamuuliza: “Unakuta sasa umependwa na mtu mbaya ukaamua kutulia naye kisa unapendwa halafu naye akakusaliti. Duh hiyo inaumaga mara mbili aisee bora mtu unayempenda akikusaliti hata ukijinyonga utajinyongea kamba mpya ya dukani, lakini mtu mbaya, nadhani hata kwa tambala la deki. Basi tukacheka hadi tukapaliwa kama mazuri..

Itaendelea

LOVE INTERVIEW 9

“Usiseme hivyo unajua mara nyingine nawazaga ikiwa Mungu atasema, kila mtu amkimbilie anayempenda, utajikuta wewe unamkimbilia @yasintajoseph naye anamkimbilia Ali kiba, Alikiba anamkimbilia Lulu, Lulu anamkimbilia Diamond, basi itakuwa full tafrani,” alisema Stanis.

“Acha zako haitatokea hiyo kitu na kama itatokea maana yake kuna jambo moja tu nitafanya ikiwa ni mimi. Wakati nyie mnakimbizana mimi nitatulia nisubiri kuona nani atanikimbilia mimi na mwisho wa siku nadhani wengine wote nao mkiona mnaowapenda wanawakimbilia wanaowapenda, basi wote mtaniiga na kutulia na mwisho wa siku anayekupenda atakufuata palepale,” nilijibu.

“ooh kwa hiyo tumekubaliana kuwa kumbe bora kuwa na mtu anayekupenda kuliko unayempenda wewe?” alisema Stanis. Bado nikawa nasitasita kukubali maana loh kupenda kuna raha yake, kupendwa nako kuna raha yake, lakini raha kamili ni kupendwa unapopenda.

Basi tukapiga stori nyingine nyingine na baadaye nikarudi zangu home, nakumbuka ilikuwa saa kumi na moja jioni, nikaendesha gari kutokea maeneo ya Charambe na kuigusa Mbagala Rangitatu. Nikakutana na foleni kubwa sana. Nikachungulia nje kituoni kuna dada mmoja mzuri alikuwa amebeba mabegi yake makubwa na alionekana kushindwa kugombania magari, nikamuonea huruma mno. Nadhani na yeye aliniona akanipungia mkono nikasimamisha gari yangu pembeni nikijua tu alikuwa akitaka msaada.

Siri moja ni kwamba wanaume tunasemwa tuna roho nzuri kuliko wanawake, kwa sababu tunatukuza kazi ya Mungu kwa vitendo, mfano msichana akiwa mzuri tunaweza tu kumsaidia pasina kuhitaji fadhila. Mfano huyo mdada alikuwa mzuri mno, kiasi kwamba kumuacha akiteseka vile ilikuwa siyo vyema.

Akasogea karibu kwenye gari nikamfungulia mlango na kumwambia aweke mabegi yake nyuma. Tukaondoka na ndani ya gari akanielekeza anapoelekea.

“huwezi amini kumbe ni mwanafunzi wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, nikaendesha gari nikiwa sina hata nia moja ya kumtongoza, maana kwenye makundi ya wanawake wasumbufu nchini Tanzania, kundi la kwanza ni la wanafunzi wa chuo, mama yangu usiombee ukajitekenya kuwa nao, utaombwa hadi hela ya pini, utagharamia mpaka ukoboke.


LOVE INTERVIEW 10

Kuna mshkaji wangu alifilisiwa kimtaji chake cha chipsi. Bora angekuwa mtu wa kuja tungesema sawa, lakini ni mchaga asili na anaijua hela vilivyo lakini kwa mtoto wa chuo akawa mweupe pee!

Nikawa kimya, sitaki hata kumtongoza japokuwa kuna sauti zilikuwa zikinizonga kimoyomoyo zikinishawishi nimtongoze, tena zingine zikinicheka zikisema; hilooo dume jinga, sauti nyingine zikasema; We John utakuwa mseng* ukimuacha huyo mtoto aondoke hivihivi.

Ahh nilizipuuza sauti hizo, lakini najua wanaume wote wanakuwaga nazo sauti hizi pindi wakiwa wameketi na mwanamke mzuri mfano kwenye siti ya daladala au usafiri wa basi la mkoa. Wanaume wanajua hizi lakini hawasemagi tu, we muulize bwana ako atakwambia tu.

Basi nilimpeleka hadi Mabibo Hosteli, alinishukuru sana, basi nikageuza gari na kurudi nilipotoka, yule denti akanisimamisha na kuniomba namba ya simu. Nikajisemea kimoyomoyo: “oohooo we mtoto weeee soma huko.” Nikatoa simu yangu na kumpa akaingiza namba zake na kujibipu, nikaondoka zangu huyoo hadi home.

Basi nilisahau kabisa kuhusu yule msichana, siku moja akanipigia simu na kujitambulisha kuwa anaitwa Alice. Nikamkumbuka, tukaongea kidogo na mwisho wa siku akataka tuonane, basi nikamkaribisha nyumbani kwangu wikiendi.

Lakini sikutaka kabisa kumfukunyua huyu msichana japo alikuwa mzuri mno halafu alikuwa mweupe kama Mmanga.

Alipofika hata Shose nadhani alishangaa, maana nilikaa naye sebuleni tu na sikuingia naye chumbani kabisa maana siyo chumba tena bali ni gesti, maana looh si kwa umalaya wangu.

“mh kwako pazuri! Kweli haujaoa?” aliniuliza Alice, nikasisimka alipotaja neno kuoa.

“sijaoa..” nilijibu tukapiga stori mingimingi jioni akaniaga kuwa anawahi kufanya assignment chuo, hivyo nikamsindikiza hadi kituoni akapanda bajaji na kuondoka.

Ile nafika tu nyumbani Shose akawa ananicheka.

“ah kaka naona leo haujafanya mambo yako kabisa unaumwa nini?” alisema Shose kimasihara nikamfukuza na kumkamata nikambana kwa kumkumbatia kama watu wa mieleka, lakini nikashangaa kuona amejiachia kabisa mikononi mwangu, nikashtukia mikono yangu ikigusa vikonzi vyake vya kifuani, nikaitoa haraka. Mwenyewe akanitazama tu huku ametulia kimya kama tetea na mimi ndiyo jogoo, kwa hiyo nimpande au?



Hapana haka kasichana ni kastaarabu mno siwezi kukaosha, nitakaharibia, mimi sijatulia. Nilirudi zangu ndani bila kumsemesha nikala zangu chakula na kwenda kulala nikiwaza jumapili ya kesho nimuite nani nyumbani ingawa kuna kitu siku hiyo nilikijua kuhusu Shose ni kuwa hakuwa mtoto tena kama nilivyokuwa nikimchukulia siku za nyuma alikuwa mdada tayari tena kaiva, maana niliishi naye miaka minne sasa, akikua huku namuona nadhani nilikuwa sijagundua kama alikuwa amekua tayari.

Ila mbona aliniangalia kwa macho ya kunitaka! Ah inawezekana muvi zake za Kikorea zinamharibu. Nikajiwekea mwiko mwenyewe; “chezea wote na umalaya wako lakini usimguse Shose,” “Sawa nimesikia,” nilijiitikia kama hayawani.

Nikiwa nimelala zangu mara simu ikanishtuka ile kuangalia alikuwa ni mama nikapokea lakini nilishangaa aliyekuwa akizungumza hakuwa mama bali ni mwanaume aliyejitambulisha kwa jina la Dokta Obeid wa Hospitali ya Sinza Palestina aliniambia mama anaumwa na amelazwa hapo kwa presha.

Ikabidi haraka nikimbie hospitali kwenda kumuona.

Nilipofika nikamuona akiwa amelazwa, Daktari akaniambia kuwa alikuwa amepatwa na stroke baada ya kuanguka chooni.

Nikaanza kupata wasiwasi, nisije kweli nikampoteza mama yangu kabla hata hajaniona nikioa na kumpatia mjukuu kama ambavyo alikuwa akitamani kila siku.

Mh sasa lazima nifanye jambo haraka ili nioe, lakini nitamuoa nani? Ngoja niandae Interview, niliwaza eti nibandike tangazo kuwa eti yule kijana Tajiri John anahitaji kuoa, usaili Jumapili, halafu nikae na timu ya majaji kwenye meza na kuanza kuwachuja wanawake watakaojitokeza.

“hapana hiyo haipo sawa, maana watajitokeza watu hadi nitashindwa pa kukimbilia.”

Nikawaza kufanya jambo, mimi si mkristo ngoja hiyo interview nikaitangaze kanisani, maana nasikiaga kanisani ni moja ya sehemu ambazo mtu anaweza akapata mke au mume mwema, japo siaminigi ila ngoja nijaribu.

Sehemu nyingine ni sokoni, ndani ya mabasi, shuleni, hospitalini, ahh nimekosea, hospitalini hapana, maana unaweza ukatongoza demu aliyeenda kuchukua dozi ya Ukimwi bure halafu akakukubalia ukaenda kujifia vizuriiii.

Oke ngoja niende kanisani, siriaz sasa sitaki mzaha mama yangu anakiharusi sitaki afe kwanza.


LOVE INTERVIEW 12

Basi nilimhamisha na kumpeleka hospitali ya AAR na kumuacha chini ya madaktari wataalamu, hausigeli wake akawa anamsimamia wakati huo nikampigia simu mama mdogo ili naye aje kunisaidia kwa kuwa masharti ya hospitali hiyo ndugu au rafiki wa jinsia moja na mgonjwa ndiyo anayeruhusiwa kumhudumia mgonjwa hospitali muda wote, sisi wengine ni kuja kumtembelea tu katika muda maalumu.

Tena kama nitakosa mtu, kuna manesi wa kulipia hapo wapo wa kiume na wakike ambao wanaweza kufanya huduma hiyo kwa mgonjwa wako.

Basi nikaona nisipoteze muda tena kwa kuwa kesho ni jumapili naweza kuwahi kanisani usiku huohuo kuomba misa lakini nitaomba Mungu anipe mchumba halafu nitafanya ujanja kuacha namba zangu kwa paroko au katekista kwasababu najua ikitangazwa pale mbele eti. “Maombi ya misa ya kupatie mchumba bora, imeombwa na mkristu mmoja,” itakuwa noma tena ikitangazwa kwenye misa zote tatu basi wasichana watatafutana. Tena kuifanya ionekane siriaz sikutaka kutaja jina langu; hivyohivyo mkristu mmoja.

Tena nikaona ili kupata mke mzurimzuri kidogo anayeendana hadhi na mimi bora niende kanisa la St Joseph, St Peters, halafu nitaenda kanisa la Mbezi, siyo usharika wa Tandale au Manzese nitaumia?.

Basi nikatembea kuingia kanisa la St Joseph, wakati naingia ndiyo nikakumbuka nina miaka zaidi ya kumi sijawahi kurudi kanisani kusali. Huenda Mungu alikuwa amenisahau hata dhambi zangu haziandiki tena, lakini kwa kurudi labda nitamkumbusha na anaweza akanilima nyanjo za kutosha katika daftari langu la uzima.

Basi nikaogopa hata kuingia kanisani kwenyewe nikaambaa kwenye ofisi za kanisa na kumuuliza mlinzi aliyenielekeza kwa Katekista.

Nikaandikisha na kulipia misa, nikampa na namba zangu za simu, nikamminyia jicho. Katekista akacheka na kuniuliza; “are you serious? Nikamjibu; “Hell Yeah” nikajishtukia kumbe nipo kanisani? nikabadilisha; “Heaven Yeah!”

Haraka nikazunguka makanisa yote niliyoyapangia na kurudi zangu nyumbani kulala, maana haina haja ya kwenda kanisani kesho zaidi ya kuchaji simu yangu na kusikilizia watoto wakalii. Lakini nilipaswa hao mademu pia niwachuje wachujike nikaandaa mtihani. Je mtihani gani huo?

Itaendelea..

LOVE INTERVIEW 13

Kwanza kabisa, usiku uleule nilimpigia mshkaji wangu Stanis, nikamtaka tuswitch nyumba, yaani yeye aje kuishi kwangu na mimi nikaishi kwake maana yeye hakuwa amejipanga sana kimaisha, alikuwa na chumba tu na vitu vya kawaida tu.

Kwanza alishangaa kuona mimi nataka kuhamia kwake akataka mlolongo wa maelezo, nikamuelezea kwanza hali ya mama kisha nikamwambia lengo langu la kuoa haraka iwezekanavyo.

Nikamwambia kuwa lazima msichana nitakayemuoa apitie interview na interview yangu hatua ya kwanza inanitaka kuishi maisha ya kifukara na kuyaacha kabisa maisha ya kitajiri ili kujua kwanza yupi ananipendea pesa na yupi atanipenda kwa jinsi tu nilivyo.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG