Search This Blog

Monday, January 24, 2022

MCHEPUKO WA ZANZIBAR - 1

  

IMEANDIKWA NA : CHANDE ABDALLAH 

********************************************************************************

Chombezo : Mchepuko Wa Zanzibar

Sehemu Ya Kwanza (1)


Mtu akitaja neno Zanzibar, kinachotakiwa kuja kichwani kwako haraka ni harufu ya karafuu, mandhari ya mji mkongwe na fukwe nzuri, ndiyo; hiyo ni kwa wanaoijua Zanzibar vilivyo kuanzia Unguja; Pemba na visiwa vyake.

Lakini kwa wengi wetu ukitajiwa Zanzibar, kichwa kitavuta taswira za fukwe safi, mitumbwi, minazi, wapemba na mavazi yao na ile lafudhi yao maridhawa ya Kiswahili.


Hiyo ni kwao hao watu wengine, lakini si kwa mzee Damian Shirima, yeye kwake neno Zanzibar lilimtia ashki na midadi kumpanda maana taswira iliyomjia ni ya Naifathy binti wa Kipemba anayekutana naye akiwa Mangi huko Zanzibar miaka mingi mno iliyopita.

Nini alichofanyiwa akiwa Zanzibar na binti huyu kiasi cha kumfanya apagawe na akili zimruke kama Zamwamwa ilihali angali mzee wa miaka sitini na mke na watoto kajaliwa.

Hii ndiyo simulizi yenyewe, tulia uisikie.

Damian katika hangaika zake za kimaisha jijini Arusha aliamua kufunga safari kujaribu maisha mahala pengine nchini. Naye kama ndugu zake wa Kichaga mishipa yake ilipitisha damu yenye vinasaba vya biashara na uthubutu.

Alihitaji sehemu nzuri kwa mtaji wake mdogo,

Kati ya mikoa yote iliyopo Tanzania akaamua kwenda Zanzibar akiwa hana ndugu huko wala hajuani na mtu yoyote.

Naye alivutwa Zanzibar na taswira zilezile zilizomjia kichwani mtu mgeni, yaani fukwe, minazi, majengo yaliyochakaa na wapemba. Hakuwahi kuwaona kabla isipokuwa kwenye vipande vya gazeti tu, ukizingatia maneno ya Arusha vijijini aliyokulia yeye palikuwa hapana wageni sana kutoka mikoa mingine.

Kwa hiyo basi mchaga aliyetumwa pesa akaanza safari yake ya basi akaingia Dar na kujionea jiji hilo enzi hizo likimetameta kuanzia magomeni, akaogopa watu hapo, aliona watamzidi ujanja, akalala kwa tahadhari siku ile kwenye nyumba ya wageni.

Kichwani hakuwa na ujuzi wowote zaidi ya kujua kuzitunza pesa, kuzihesabu pesa, kuzitumia kwa nidhamu pesa na pia kuzitafuta pesa hususani kupitia kazi ya dukani, kwani kuuza duka alijifunzia kwenye duka la mjomba wake Urio; duka la kwanza kijijini baada tu ya mkoloni kuondoshwa.



Damian kijana wa miaka ishirini na tatu, peke yake sasa alfajiri alipanda boti pale bandarini, safari ya kwenda Zanzibar ikamtimilia, hapo ndipo alianza kuona wanawake wachache wa Kizanzibari waliokuwa wakirudi makwao. Aliwashangaa mno na kuwasikiliza lugha yao. Akaona wanaongea vizuri mno na walaini kwa mitazamo ya rangi zao. Lakini walivaa mabaibui akagundua hawakuwa na mizigo kuwafikia wanawake wa Kiarusha hivyo hawataweza kumfilisi kiduka chake kwa kishawishi.

Boti ilianza kuondoka na kuingia baharini, mawimbi ya Msasani yakiichezesha boti kama kawaida na kuwafanya abiria kadhaa waombe mifuko. Hata Damian alijisikia kichefuchefu naye akakaa na Malboro lake akikaza meno kwa kadri anavyoweza ili asitapike.

“pole kaka, kwani hii ni safari yako ya kwanza kwenda Unguja!?” aliongea kwa lafudhi ya Kipemba mwanamama Fulani aliyeketi pembeni ya Damian huyu alikuwa amevaa ushungi wake vizuri lakini hakuvaa baibui.

“ ndiyo,” alijibu Damian akijitahidi asiongee maneno mengi maana alihisi tumbo lake limemchachamaa zaidi akajizibia ufuko na kuinama akitabika tapiko lake.

Punde saa ile abiria wengi wakafanya hivyo na mchafuko wa tumbo ukaisha kadri walivyozidi kusonga mbele ndani zaidi ya bahari indi.

Safari ikaenda kwa masaa takribani matatu na vidakika vyake, wakatia nanga hapo bandari wakashuka aridhini na Damian kuingia rasmi humo kisiwani hiyo ikiwa ni mapema mchana.

Kichwani alifahamu kuwa alipofika ni mjini, hivyo hakupaswa kuwa hapo, alitaka mahali mbali mno na mjini.

Akapanda usafiri asiouzoea wa vigari vya chai maharagwe, akaenda mbali na mbali akitajiwa majina asiyoyajua, yakiwemo Unguja Ukuu, Jozani, akakutana na njia panda ya Kizimkazi Dimbani akanyoosha Paje, na kuambaa na ufukwe hadi Jambiani hapo ndiyo akashuka akasema: hapa nitakaa na kufanya biashara. hapo ndiyo akaomba sasa kupata nyumba ya kupanga akitafuta madalali kwenye ofisi zao.

Akazungushwa jioni ile na kupata chumba cha elfu tatu kizuri lakini masharti lukuki ambayo hakuwahi kuyasikia tangu azaliwe.

Subiri usitoke.




“Ami nitakupeleka kwenye nyumba nyingine, lakini sasa hivi, danganya kidogooo, utakosa pa kulala!” aliongea huyo dalali aliyezungumza kipemba baada ya kutoka na Damian nyumba ya kwanza aliyoambiwa masharti lazima awe ameoa, marufuku kulewa na kurudi mwisho saa moja usiku.

Damian alimwambia ukweli yule baba mwenye nyumba kuwa sharti la kutolewa angelitekeleza mara moja, lakini suala la kuchelewa kurudi eti mwisho saa moja usiku kwa mwanaume mtafutaji lingemshinda na kama haitoshi alisema kuwa hajaoa hivyo hiyo nyumba waliishindwa. “vyumba vipo. Ila masharti hapa, lazima uwe umeoa, uswali swala tano, usilewe na kuleta nguruwe maana watu wa bara sie twawajua, wakorofi,” alisema mzee Abdullah. Huyo ni mwenye nyumba mwingine waliyeenda kumuona na dalali.

“Mzee mimi ni mkristo, ila silewi, wala sitaleta nguruwe nyumbani kwako, sio mkorofi, nimeoa ila mke wangu yupo Arusha, nimekuja huku kote kutafuta mzee wangu, sina hata ndugu, nategemea kama nitaishi hapa nyinyi ndiyo mtakuwa ndugu zangu,” alisema Damian.

“nimekupenda, umekuwa mkweli, wengine wanajifanya kubadilisha majina kujifanya waislamu wakifika huku, sasa sawa, chumba ndiyo hiko kione, bei yangu ni elfu mbili kwa mwezi,” alisema Mzee huyo aliyeonekana mstaarabu walau. Dalali wa watu akashusha pumzi maana walizungumka mno.

Wakaona chumba kizuri haswa kikiwa kimesilibwa vyema kuta zake kwa dongo na chokaa, ikawa kama kuta za mji mkongwe, kulikuwa na miti mikubwa darini na sakafu lake lilikuwa limekomaa na halina vumbi huku ukutani kukirembwa na simbi mbalimbali za baharini.

wakalipana pale na kuandikishana, Damian akaweka vitu vyake ndani na kwenda kununua mkeka nje, akaingia kulala haraka maana alikuwa amechoka mno kwa safari ndefu.

Asubuhi iliingia na sasa nyumba iliamka. Ilikuwa kubwa, chumba chake kilijaa mwangaza na kuwa kizuri. Akafungua mlango na kuutia komeo, akakutana na vyumba vikuukuu vingi na watoto lukuki wakichezacheza hapo koridoni.

“saa aleku,”

“aleko musalam,” aliitikia Damian akigundua huko hakukuwa na shikamoo



Akatoka barazani na kumuona Mzee Abdullah mwenyewe akivuta kiko.

“Karibu, Damian, umeamkaje, hali waionaje visiwani, njoo unihadithie ya huko kwenu bara haaahaa,” aliongea kwa harakaharaka Mzee Abdul.

Damian akagundua mzee huyo alikuwa mcheshi sana, akakaribishwa chai akaionja, ilikua tamu sana, Damian hakuwahi kuinywa tangu azaliwe.

“Enhee kijana umekuja kufanya biashara gani huku?” aliuliza Mzee Abdullah, Damian akamwambia malengo yake ya kufungua duka. Mzee Abdullah alifurahi mno na kumtaka azunguke kujionea mandhari na kumwambia kuwa mahali popote aendapo ikiwa atakutana na kikwazo chochote aseme ametokea kwa mzee Abdullah wa Jambiani ataachwa salama kabisa, kwa sababu alidai yeye ni mtu mashuhuri mno.

Kweli Damian siku hiyo alioga na kuvaa nguo zake akachukua shilingi mia tano na kuzunguka nayo akipanga kununua vyombo, ndoo, kandili, na vitu vingine vidogovidogo,. Huku nikisavei eneo zuri la kuweka duka lake.

Alizunguka akigundua watu wa fukwe walivyo; wanawake hawakuonekana mitaani, na wakionekana wachache hujitanda kwa kuvaa kininja kabisa, wanaume wengi walikuwa wamekaa vivulini wakichambua nyavu zao, Mtu mmoja akamwambia Damian kuwa nyakati za usiku wanaume wote kijijini hapo huondoka kabisa kwenda kuvua na majumbani huwaacha wake na watoto tu, wao huwa baharini wakivua samaki hadi alfajiri mno ndiyo hurudi.

Kijiji kingine kilikuwa cha changanyikeni, walilima na kufanya shughuli nyingine pia ikiwemo utalii na ufugaji, hivyo basi Damian biashara yake akaona ingeweza kufanyika vizuri ikiwa duka atafungua mahali katikati ya kijiji cha wavuvi na cha changanyikeni.

Loh akabahatika kuona mahali safi kabisa kwa duka lake, akapakariri na kutafuta eneo jingine tena, ili awe nayo kama matatu hivi, kweli aliyapata na kuyanakiri yote tena yalikuwa karibu na barabara ya magari maana yake itakuwa rahisi hata bidhaa kuzileta kutoka duka la jumla.

Damian akarudi sasa, akiwa nyumbani pale nje kibarazani, akagundua sasa uzuri wa Zanzibar kwa kujionea wanawake walau sura zao, maana majumbani walivua uninja na kuacha nyuso zao. Loh walikuwa wazuri, nusu waarabu nusu wa afrika.



Wiki ilipita sasa Damian akiwa amelisimamisha duka lake vizuri. Akajua bidhaa zipi wanazozipenda wateja wake, kuanzia mikate ya boflo, unga wa ngano, dengu, tambi na ndoano, mpaka mafuta ya taa, iriki, mdalasini na asali.

Akaanza kuzoeleka kijijini wengi wakimuita kwa jina la Mangi na ndiyo hivyo walipendelea na pengine Damian akawa ndiyo Mangi wa kwanza huko visiwani.

Wiki ya pili iliingia akaanza kuona faida maana aliweza kuzungusha bidhaa zake haraka mno, yote hayo yakifanya matarajio yake ya kujichanua kibiashara sehemu ile kuwa ni makubwa mno.

Kwa wiki zile chache hizo alijikuta akijulikana na watu wengi sana, akajua pia sehemu ya kupata chakula, na mahitaji mengine madogomadogo, lakini yote kwa yote hakuwa ametazamia timizo la hitaji moja tu kubwa.

Awali hakuliona la lazima kulitimiza isipokuwa sasa, maana lilimfanya asilale na lilimtafuna ndani kwa ndani, nalo si jingine bali ni hitaji la kufanya mapenzi.

Ona Damian alikuwa mtu mzima, alikula chakula cha moto, nacho kikameng’enywa na kufanya mwili urutubishwe kwa protini na nishati joto, zote hizo ni malighafi muhimu katika kutengeneza mbegu za kiume na homoni zake chochezi.

Wiki za kwanza hakuona tabu sana, lakini kadri siku zilivyozidi kwenda na tena kwa kula samaki wa pwani huyo wamuitaye Pweza, tabu ilimuandama, dudule likamsimama kutaka suluhisho.

Vinyweleo vilidinda kila sauti ya kike iliposikika kwenye kingo za kuta za chumba chake, pengine ni mke mdogo wa Mzee Abdullah au bintiye kindakindani, Sabrina.

Hakujua lakini hakika alihitaji kutumbukiza toto lake tunduni. Usiku huu akachukua mafuta ya mgando na kulisugua rungule akilifanya dhihaka ya njia mbadala, likafukuta na kutema hasira zake kisha likapoa walau, lakini Damian alijua kesho yake hamu ingerudi kwa kasi mno Zaidi ya siku hiyo.

Kama mwanaume alijua njia pekee ni kunjunja tu, laiti kama angekuwa Arusha angeweza kutembea na mwanawake kirahisi tu, lakini Zanzibar, Unguja huko Jambiani, wanawake adimu mno, hata dukani wanafika wanaume tu, atampata wapi mwanamke amtibie! Aliwaza Damian.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG