Search This Blog

Monday, January 24, 2022

JOY, JOYCE - 5

   

Chombezo : Joy, Joyce

Sehemu Ya Tano (5)


“huruma? Kwanini?”

“si nilikuachanisha na Deborah kwa sababu ya ushahidi niliokutumia, so nikaona utakuwa mpweke ndiyo nikaja nikiwa na mawili kichwani.”

“duh!”nilisema nikiona Joyce amenizidi akili.

“kwa hiyo kwa huruma utampa mtu penzi, ni simpo hivyo kwako?” niliuliza japo nilijua swali hilo litamkasirisha.

“unataka kumaanisha pengine nitarudia kulala na wewe kwasababu bado unatia huruma? Hahaa,hapana mimi siyo Malaya wewe..” aliwaka.

“hapana sitii huruma, umekosea kunisoma akili,” nilijibu.

“mmm ..hahaa.. ni Deborah nini umerudiana naye!?”

“labda, maana ulidhani nitaachana naye kweli kwa ajili yako!?” nilimtupia dongo akakasirika zaidi maana nilimchokonoa. Nikasimama na kuondoka zangu bila kuaga. Nikijisemea moyoni kuwa hajui kuwa mimi ndiyo Jonta, John, Kapten Tinonko, Ashrafu, Ubala, na wahusika wote wa kiume kwenye stori zangu? Sasa acha aparangane maana nilijua nimemtia moto wa shauku na atarudi tu. Mfyuu



Niliondoka hapo nikiwa nimetumia tekniki ya Jonta kuwa, ikiwa msichana yoyote ukamuacha kwa kumdhalilisha, au kwa kosa lake, nakuapia hatokaa kwa amani lazima arudi ili arekebishe na kama kukuacha akuache kwa kosa lako wewe.

Na ndiyo kama vile Deborah alivyorudi, yaani wanawake wapo hivyo bora hata aondoke huko akawatangazie wanawake wenzake kuwa amekufumania, aridhike na roho yake. Lakini si eti kabisa akae kwa amani hali akijua umemfumania yeye!

Atakuomba msamaha hadi ulainike na ikiwezekana atarudiana na wewe kabisa kukuthibitishia hana tabia hiyo na ndiyo ilivyo kwa wasichana wote wa kawaida, na sio kwa gubegube lililomshinda mtume ukategemea litakuomba msamaha kama likikukosea lah hasha hiyo itakula kwako maana hii ni saikolojia ya wazi kwa msichana wa kawaida tu.

Na kwa Joyce nilifanya kwa mtindo huu; nilipomwambia nimerudiana na Deborah na kumnanga kuwa penzi lake la siku moja kuwa halina thamani. Hapo nitakuwa nimemuumiza roho vibaya mno na amekasirika. Tena alikasirika zaidi akihisi namchukulia kama Malaya au mama huruma kwa kunipa penzi kirahisi eti kisa nilitia huruma.

Nilijua tu hapo atakachofanya hapo aidha ni kuhakikisha mimi na Deborah tunaachana, tena kwa kunitumia maushahidi mengine ya kuniumiza roho, au arudi yeye kwa spidi akitaka sasa kunithibitishia yeye si mrupo. Na njia zote nilikuwa nimejiandaa.

Lakini sasa hapo nilichopanga ni kuongea na Joy ili nimuombe kabla ya Christmass nikamtambulishe kwa mama Mbagala, halafu mama atupe hicho kihela nikichikichie zangu na mimi na Joy kila mtu ale zake, duh sasa sijui atakubali? Na hivi alisharudiana na mtuye?

Tena kwangu ilikuwa rahisi maana mama yangu na mimi kuongea kwa mwezi mara moja au tusiongee kabisa. Siyo kama hanipendi lakini ndiyo kama ipo hivyo kwetu, si mimi hata kaka na mdogo wangu, yaani hata ninapokaa hawapajui. Basi nilijua kwa mwanya huo nani atajua kama Joy na mimi ni gelesha tu!

Sasa nilienda job na kupiga zangu kazi, kisha nikarudi nyumbani.

JOY, JOYCE 44

Nilirudi nyumbani na kukuta msosi, nikala vizuri na kama kawaida Deborah alikuwa pale, nikiona akijitahidi kama nini kufuata sheria tulizoziweka kwenye mkataba. Alikuwa akiropoka na kuomba msamaha. Akatulia hivi, lakini tabia yake ya zamani ilimuwasha ndani kwa ndani na kwa siku moja tu niliona anateseka na ndiyo nikathibitisha usemi wa wahenga kuwa tabia ya mtu ni ngozi haifichiki.

Siku ya pili yake, ikamshinda akaanza kuniaga na kupitiliza saa kumi na mbili, baadaye akaanza mtindo wa kuangalia series kwa jirani, lakini kwa kuwa nilikuwa napenda kuona msosi ukiwa tayari nile niandike mastori yangu. Basi na yeye akawa ananipatia, akaweka chakula mapema na kwenda kuangalia hizo muvi hapo kwa jirani. Sio kwamba hawezi kuangalia hapa ndani, lakini alitaka ile ushabiki wa kutoangalia peke yake.

Pia na mimi sikuwa napenda makelele, nilitaka utulivu nikiwa naandika madudu haya. Na wakati huo nikiwa nimekosa cha kuandika kuhusu Joy na Joyce, nilikuwa ndiyo naandika ile Love Interview.

Loh! Hizo series sasa zikazidi maana aliangalia hadi saa 2 usiku, siku nyingine akaongeza ikawa hadi saa 3, na siku alipofikisha saa 4; nikaona imefikia too much. Maana eti nalala halafu yeye hayupo. Wewee! Mie siyo boya. Ndani yangu ni Jonta, Ubala, John, Farudume na Tinonko na nilimuumba Shose, Georgina, Salma, Winnie, Ninah nakadhalika hawezi nibabaisha huyu mshenzi mmoja!

Nikamuamshia dude.

“bwana eeh na wewe umezidi unagubu!” aliropoka.

“we mshenzi nitakufumua!” nilikoroma taratibu maana sikutaka niwe mswahili kama yeye wa ugomvi wa ndani majirani wasikie.

“weee thubutu jaribu uone! Una gubu nisise..”

Nakuapia hakumaliza sentensi yake. nilirusha kibao bila kuki-edit. Akya nani sikuwahi kuwaza nitampiga mpenzi hata siku moja, lakini siku hiyo kilishuka kwa kasi ya 4G.

Akakaa chini, akajiachia kwenye kochi na kulala moja kwa moja, akaanza kutetemeka akagalagala na kunguruma kwa sauti za ajabuajabu. Mate yakimtoka mdomoni kisha akakakamaa. Hivi ukiua unafungwa jela eeh?



Basi nilichofanya haraka nikawasha sabufa nikaipandisha sauti juu , ili mradi tu watu wasisikie ndani mtu anavyokata roho wakajazana kutoa ushahidi kuwa nimeua maana hapo tu nilikuwa nimechanganyikiwa balaa.

Sasa uzuri huwa nakuwaga na mipango mapema, mfano kabla hata demu hajaingia ghetto ninawazaga je akifia ghetoni nitafanyeje! ‘nitasubiri hadi usiku, nitachukua nailoni ya godoro jipya nitaitandika chini na kumuweka huyo maiti juu yake, nitachukua kisu na kuanza kukata viungo kimoja baada ya kingine, nitaweka kiungo kimoja kimoja kwenye mfuko na kwenda kukitupa usiku mtaani hadi mwili umalizike, na sehemu ya kutupa ni moja tu pale kwenye mfereji wa Kajenge sio mbali na pale nilipokuwa nimepanga.’

Tena nilishapangaga kama nikimfumania demu wangu na mtu. cha kwanza nitazuia hasira zangu, kisha huyo mshkaji nitamruhusu aondoke na huyo demu wangu, tena nitawaaga vizuri tu.

Halafu pia nilipanga kama Deborah akinipandishia sauti, nitamfukuza usiku arudi kwao, lakini loh! sasa mbona niliteleza na kujikuta nampiga kibao! Ona sasa anakufa, nifanyeje?

Nikatulia nisubiri afe ili huo mpango wa kumkatakata viungo na kumtupa mferejini kipande baada ya kipande uanze.

Mh lakini uzuri kwao wananijua hata dada zake. Nitawaelezea tu halafu tutazika wote, tena kwenye msiba nitajifanya nalia saaana! Maana ishu yangu itakuwa imefanana kama ya Kanumba na Lulu, angalau Watanzania watanielewa kidogo kuwa niliua bila kukusudia.

Lakini kuna jela loh! nikawa nimechanganyikiwa maana japo kuwa nilijifanya mtu wa mipango lakini nilikuwa nimepatikana siku hiyo.

Mara nikaona Deborah anahema kwa nguvu. Halafu akajinyonga shingo na kukaa huku akiwa amefumba macho. Akaanza kuongea Kiarabu kisha akatulia na kuongea Kiswahili cha pwani. Mimi akiniita kwa jina la “mwanadamu”

Nilipata ahueni nikajua kumbe hajafa! Lakini la pili nilijua tu kuwa hapo amepandisha majini. Sasa uzuri mimi mwenyewe hayo majini yaliniendesha vilivyo tulivyokuwa Boarding wale waliosoma habari zangu na Moses Mbarafu kwenye ile stori, watagundua kuwa mimi sio mgeni wa visa vya majini.


JOY, JOYCE 46

Hivyo nikatulia na kusikiliza jini huyo anataka kusema lipi? Maana niliona inaweza ikawa stori nzuri sana ya kuandika. Haraka nikapunguza sauti ya sabufa na kuchukua simu yangu, nikawasha upande wa rekoda na kurekodi sauti ili nami siku nijisifie kuwa niliongea na jini ana kwa ana (sauti hiyo ninayo hadi hivi leo).

basi huyo jini akaanza kuongea kwa ukali.

“mwanadamu kwanini unapiga kiti!”

“kiti!?” nilijifanya kuuliza kijeuri nikitaka kumpoteza maboya kwa maana ya kiti cha kukalia au?

“Mwanadamu unajifanya jeuri sana, hautalala kwa raha, unajua sisi tuna nguvu kubwa sana, mwanadamu. Huyu hapigwi hata siku moja na wewe umempiga, unajua adhabu ya kupiga kiti wewe!” alikoroma tena huyo jini. Niliogopa lakini nikajikaza na kulazimisha kucheka kimoyomoyo ili kuuweka moyo thabiti maana nilijua ukiogopa tu basi nguvu za giza zitanitawala na kuniendesha zinavyotaka, sasa kwa jeuri nikajibu:

“sikilizeni nyie sijui ni majini au mashetani, sijawahi kumuona Deborah anapandisha! Lakini kwa mara ya kwanza nimejua; sasa niwaambieni ukweli, kuanzia leo hii usiku huu, mkimaliza kuniambia hiyo mikwara yenu, huyo Deborah sijui kiti wenu namtimua anarudi kwao sipendi mtu mwenye mapepo hata siku moja!” niliwaka na mimi kijeuri sijui niliutoa wapi huo ujasiri.

“sikia mwanadamu, sisi hatupo hapa kukutenganisha wewe na mwenzio, lakini huyu ana adhabu zake akikosea na sisi ndiyo tunamuadabisha, sio wewe haupaswi hata kidogo!” walisema hao majini nikagundua kuwa safari hiyo walipoa kidogo, pengine waliogopa mkwara wangu basi nikataka sifa nikakaza tena.

“sikieni huyu ni mtu wangu, anaponikosea na kunijia juu, mimi kama mwanaume wa kiafrika lazima nimshushe chini, kwa hiyo nyie ni kama nani muingilie uhusiano wetu! Halafu huko mnakosema mnamuadibisha yeye akikosea ni kwa mtindo gani yaani sijawaelewa?”

“tuna adhabu zetu wenyewe, mwenyewe kiti anajua..”

“sasa kwani hivi nyie ndiyo watoa adhabu wake au!”

“haahaa! We mwanadamu mbishi sana, sisi tuna faida nyingi sana tunamuepushia mabalaa kiti, tunampa bahati na tunamuongoza kufanya yaliyo mema.”


JOY JOYCE, 47

“Kusema kweli hizo faida zenu mie sizioni, naona tu vilevile, huyo kiti wenu anaumwa kila mara, hata hela nampa mimi, mara ya mwisho niliachana naye kwa usaliti, hayo mema mnayomuongoza yapi? Niwaambieni ukweli tu ningewakubali kama siku naamka asubuhi naona mahela hapa ndani, lakini shidashida tu halafu na nyie tena juu.”

“hahaaa! Mwanadamu sikiliza, dunia huijui hii na huyu asili yake huijui, tupo tunazunguka kila siku humu ndani, tunakuona ukilala ukiamka, kote unapoenda, unaitwa Chande Abdallah, jina la ubatizo Charles Chande, mbishi, mpole wa nje, mama yako anaitwa Marietha John Hyera, wewe mtoto wa kati, baba yako amefariki mwaka, hufanyi chochote bila kumsikiliza mama yako una…”

“So what?” nilimkatisha huyo jini maana hiyo tekniki ya majini kujifanya wanakutajia vitu vyako vingi niliijua vizuri tu, Mie wala hawakunipata, tena nikagusa simu kuhakikisha rekodi ilikuwa inaenda vizuri kisha nikamgeukia tena.

“hahaa Chande wewe Jeuri, sana,”

“sikilizeni, mnamuumiza kiti wenu ona mnavyomsumbua usiku kama huu, halafu mnaniita jeuri! cha msingi mwacheni alale kesho akisharudi kwa dada yake pandeni tani yenu, lakini kwangu sitaki!”

“hapana sitaki muachane, ila jaribu kutusikiliza umesikia mwanadamu, aya sisi tunaondoka eeeh!” alisema huyo jini kwa upole zaidi wakati huo Deborah akajinyonganyoga kisha akabeua na kuegemea ukuta.

Mimi nikazima rekodi yangu, nikamuita. “we Deborah!”

“abee!”

“kumbe una majini?”

“kwani ilikuwaje?”

“umepandisha,” nilisema mwenyewe akawa anatumbua tu macho.

“sasa nimeamua kesho urudi kwenu tusijuane maana siwezi kukuvumilia yote hayo wewe tu, hapana kwa kweli!”

“yote kivipi kwani mimi nimependa kuwa hivi?” alianza kulalamika.

“hapana hata kama haujapenda lakini ni too much, jeuri wewe! Msaliti wewe! domo la kuropokaropoka wewe! mashetani pia wewe! hapana kwa kweli, na hao mashetani wako nimewaambia wakapandishie kwenu hapa sitaki, ndio maana nimesema bora urudi tu kwenu, na ningependa hata usiku huu maana naogopa usije ukanikosea nikakupiga ukafa!” nilichora mstari wa mwisho.

“hivi we Chande unaringia nini hasa!” Deborah alijizoazoa na kuanza kuongea taratibu.

“kivipi?”


JOY, JOYCE 48

“mmmh aya tu, yaani mie baba yangu angekuwa hai, nisingefika hapa, nisingepata shida hizi, na mie ningekuwa nimesoma huko nimepata kazi nzuri, nisingenyanyaswa na mwanaume, sawa bwana, naondoka lakini utanikumbuka!”

“sikukumbuki naapa!”

“jamani Chande usifanye hivyo, sitaki kuondoka naomba nisamehe sirudii tena kukujeuria! Na sasa hivi bora nikikosea unipige tu, hayo ya kufukuzana sitaki bwana, mie kila siku kurudi kwa dada nitaonekana nina tabia mbaya,” alilia Deborah kumbe alitikisa kiberiti; nikamuonea huruma.

Usiku ule nikamsamehe na kuweka makubaliano mapya. Akaandika kuwa ataacha kuangalia series usiku kwa majirani, ataacha kuropoka na etc. na mie nikakubali lakini sikuona upya wake maana habadiliki.

Asubuhi niliamka nikamsikilizisha ile rekodi Deborah, mwenyewe aliisikiliza akacheka kama mazuri. Mie ndiyo siku ile nikapata idea ya kuandika kisa cha Interview na Lusifa, maana nilijiuliza vipi kama sasa sitaongea na mashetani ya Deborah bali na baba yao Lusifa, nikawaza je, nitaamuuliza maswali gani kama tukikutana naye ana kwa ana?

“loh! ila na mie ujeuri nimezidi ” alijisema mwenyewe Deborah. Nikashangaa ina maana kumbe anajijua eeh!

“ila na wewe mume wangu umezidi mineno duh una maneno makali ya kuumiza sana!” aliposema hivyo nikashtuka, nikatafakari maongezi yote, nikajikuta loh kweli huwa nina maneno mabaya sana na makali mno, hapana sikuwa hivi! Au ndiyo huyu Deborah kanibadilisha? Maana wanasema ukimpata demu wa uswazi, ukajipa moyo eti ukiwa naye ndani utambadilisha tabia; ndugu yangu imekula kwako maana atakubadilisha wewe, niliwaza na kujiona huku ninapoenda ninayumba. Huyu Deborah yale niliyoongea kwake ni ukweli mtupu maana pengine Mungu ananionesha kuwa huyo sio demu wa kuoa kwa hizi dalili za mwanzo tu.

Nikamvumilia lakini siku moja aliponiudhi kwa kurudia yaleyale nikamropokea: “ unajua nini Deborah, mimi na wewe hatuwezi kufika mbali, siwezi kukuoa, ndoto hizo futa!” nilisema bila kupepesa.

“weeh hatoki mtu hapa ndani!” alisema nikafungua begi nikatoa laki tatu na kuweka mezani. Nikaona anapepesa macho. Nikamfafanulia.

“Chukua sepa, au baki uambulie kufukuzwa tu bila kitu!”



Basi Deborah akachukua hela vizuri tu na kupaki vibegi vyake akaondoka asiongee chochote. nikacheka kama mazuri ila niwaambie ukweli leo hii kama ukimpa hela mpenzi wako akuache, akya nani asilimia 80 watakubali; wakugande we nani mbele ya hela!

Sasa wakati huo na mimi nikahama pale Kijitonyama na kuhamia sinza Mapambano ili mradi nianze upya kabisa na sikutaka kunukia udeborah-deborah.

Wakati huo ndiyo nikakumbuka Christmass inakaribia; Nikampigia Joy na kumuomba kwanza awe sehemu peke yake. Hapo nikaanza kumwambia kuhusu mtihani wangu baada ya kumpost picha yake mtandaoni.

“duh sasa itakuwaje!”

“mimi nakuomba twende tu mara moja tu akuone halafu basi,” niliomba.

“mm kiukweli Chaxy sitaweza, labda nikuombee kwa Joyce,”

“hapana Joyce mcharuko sitaki!”

“wee Joyce katulia balaa hizi siku mbili, we ngoja nikuitie uone!” alisema Joy.

Dakika chache baadaye, namba mpya ikaingia nilipopokea alikuwa Joyce.

“mtu mwenye kiburi, niambie?” alinisalimia kwa upole.

“poa tu, lakini mimi sina kiburi,” nilisema.

“aya bwana ila kwa sababu nilikuwa sikujui vizuri, ila sasa nimekujua ndiyo maana hata ukiniropokea sitakasirika,” alisema.

“unanijua kivipi!?”

“nimesoma stori zako insta na fb, unajua kuandika kwa kweli, lakini mara nyingi mtunzi huandika vitu vinavyomtokea mwenyewe au alivyoviona kwenye mazingira yake au anavyovitaka. Na tabia yake inaonekana kwa jinsi tu anavyoandika, na nikwambie tu, wewe ndani yako ni soft tu japo unajifanya mbishi na mgumu,”

“mmmh,” niliguna tu.

“enhee niambie maana Joy ameniambia sikumuelewa!” alisema Joyce ikabidi nimuhadithie ninachotaka nikiahidi kumpa laki moja.

“sikia nitafanya bure kabisa hata usijali, lakini si ungempeleka Deborah?”

“hapana Yule matatizo mengi, na sasa hivi nimeachana naye,”

“mmh na wewe ulishikwa kweli! Basi utanishtua.”

Siku ya mkesha wa Kristmass akanipigia mwenyewe akasema atakuja ninapoishi, eti pia alitaka kuona jinsi ninavyoandika. Nikamwambia aje.

Akaja, Nikiwa naandika nikagundua Joyce amekuwa mpole kweli akitazama stori na kunitazama mimi, nikamshangaa.

“mmh wewe ni Joyce kweli?” nilisema na kumlazimisha kumnyanyua ile brauzi ili nione ile alama kama ipo.

JOY, JOYCE 50


He! Kwa mbali niliiona ipo, lakini akawa ananitazama kwa jicho Fulani hivi asinijibu chochote. Nikashtuka na kuwaza nimeshawahi kuona wapi hilo jicho. Sikuelewa.

Basi nikiwa naandika akaenda kuoga na kanga yake akarudi, na kuja kulala kitandani, nilipomtazama nikaona amelala na kidole amekitia mdomoni. Nikashtuka na kuwaza hivi nimewahi kuona wapi kidole chatiwa mdomoni?

Tena usiku ule nilisikia akihema taratibu, na alipolala alikuwa mtulivu na mzuri, tena alionekana mtamu akiwa hivyo.

Loh haraka nikashtuka kuwa niliwahi kuyaandika hayo, ndiyo nikarejea sifa za Shose kwenye chapisho lililopita, hata vile alivyotia kidole mdomoni, alivyonitazama kwa jichole lenye kope ndefu, rangi yake ya maji ya kunde siyo ya maharage.

Alivyohema. Ona, niliandika hivi vitu, nikitamani mimi mwenyewe niwe na Shose, lakini siku hiyo nilimuona eti Joyce ndiyo anavyo. Loh nikajikuta natikisika moyo usiku mzima na sikumgusa naapia.

Asubuhi tukajiandaa kwa kuwa ndiyo ilikuwa Christmass basi safari ya kwenda Mbagala ikaanza.

Tulivyofika Rangi tatu, Joyce kwa hela yake akachepuka sokoni na kununua khanga doti moja. Sikumuelewa. Tukiwa mitaa ya nyumbani. Mtoto alivyo mkali washkaji na majirani walionijua walitoa vichwa nje. Na mie nikawa na punga tu mkono kama mwanasiasa.

Tulipogonga geti, dada yangu akaja kutupokea, akamkumbatia Joyce aliyetabasamu tu na kumkaribisha ndani kwa furaha mno. Mama akaja, Joyce akapiga goti hivi na kusalimia na mama alinishangaza maana alimnyanyua kwa furaha na kumbusu shavuni Joyce. Sikuwahi kuona hayo. Roho ikanisisimka. Tulikaribishwa ndani. nikaona mama na dada wakihangaika kuweka chai. Joyce akasimama na kuambatana nao eti akisaidia kabisa kazi za pale japo aliombwa atulie.

“duh mwanangu wifi sio wa nchi hii!” alikuja kusema dada nikacheka tu nafsi ikinisuta kwa mchezo wa hatari niliokuwa naucheza. Ila hapa naweza kupata stori tena ikawa kali balaa maana; mama ndani, dada ndani, mimi ndani, na Joyce ndani. Uwiiii!



MWISHOOOOOO


0 comments:

Post a Comment

BLOG