Search This Blog

Monday, January 24, 2022

LOVE INTERVIEW - 3

   

Chombezo : Love Interview

Sehemu Ya Tatu (3)



“anhaa, basi nilikuwa nakufananisha tu, kwa hiyo utakuwa na sisi hapa si ndiyo eeh.”

“ndiyo niponipo.”

“Stanis mwenyewe yupo wapi?”

“amesafiri kidogo,” nilijibu.

“basi sawa, lakini kama utakuwa una tatizo lolote naomba uwe unaniita mimi, baba namjua hapo kashaniliza,” alisema Zai huku akiendelea kudeki nikamtoa wasiwasi kuwa nitampa hela na yeye.

Akafurahi na baada ya kumaliza nikaingia ndani na kuona muujiza wa mwanamke. Ama kweli Mungu alimuumba mwanamke kwa sababu ya msingi sana nyie ndiyo mamalkia wa nyumba zote duniani.

Kila kitu kilifutwa vizuri na kuwekwa kwenye sehemu yake.


LOVE INTERVIEW 24

Nikashtushwa na simu yangu ikiita, nikaipokea na kutazama ni namba ngeni fulani ya jana. Nikapokea.

“Hallow mambo?” ilisema sauti ya kike iliyonyooka.

“poa,”

“Naitwa Grace, jana dada yangu alikuwa kanisani akasikia tangazo kwa katekista kuwa unataka mchumba, amenichukulia namba yako na kuniletea, hivi kweli unatafuta mchumba au nimharibifu tu?” alisema huyo Grace, sauti yake nikaiona haina wenge, sikuona kosa.

“Yah ni kweli natafuta mchumba,” niliongea huku nikishusha sauti ili Zainabu aliyekuwa akisugua masufuria yangu nje asinisikie.

“Mh! Hata mimi natafuta mchumba lakini nyie wanaume nawaogopa sana, ila kwa sababu wewe hadi umeomba misa kanisani inaelekea ni mkweli, lakini nataka kukuona ili nikupime vitu kadhaa. Kama nitaona vigezo vyangu umetimiza nitakubali unichumbie, na wewe unaweza kunipima kama nafaa,” alisema Grace kwa sauti ya utulivu. nikaona mh huyu mbona kama aina ya mwanamke ninayemtaka!

Anajiamini naye anataka kumpima mwanaume amtakae, siyo eti umepata mtu anasema anakusoma tabia na wewe unakaa kweli ukisubiri usomwe kama hadithi za Chande na akina Chande Rapa.

“Sawa, ila nataka uniambie una miaka mingapi? una mtoto?” niliongea maana ndiyo kipimo changu cha awali.

“Nina miaka 25, sina mtoto, na wewe naomba nikurudishie swali hilohilo,” alinifurahisha kwa majibu yake. Huyu msichana ni smart, nikamjibu maswali yake.

“Ahaa unafanya kazi gani?” aliniuliza swali ambalo wanaume wengi tunadanganyia kazi kubwakubwa, lakini mimi ni rahisi tu. Nasemaga kazi yangu ni Shamba-boy.

“Mh yote kheri kwa kuwa Mungu ndiye anayepanga, mimi mwenyewe nimeajiriwa nauza duka la nafaka, hapa Msasani,” alisema Grace. Nikajisemea, Yap huyu ni mtafutaji, siyo demu wa nyumbani pili hajali umaskini wangu.

Nikampongeza na nikamuitia nyumbani, akaniambia atakuwa bize hivyo akaniambia ataniambia kwa kukutana naye mapema kesho, akakata simu. Nikaangalia simu yangu nyingine nikaona Shose anapiga nikaikata. Mara kidogo Stanis akapiga, aliongea mengi lakini kilichonasa kwenye sikio langu ni: “Ha! Kaka kumbe ulikuwa na hausigeli mzuri hivi! na haukuniambia?”

Itaendelea..


LOVE INTERVIEW 25

“unasemaje!?” niliuliza kwa ukali.

“Si anaitwa Shose.” Alijibu Stanis.

“sikuelewi upo naye hapo au?”

“sikia, nilimuona ukiwa naye hapa sebuleni mwanzoni hadi nikasisimka, sasa mimi sikuwa na hili wala lile nilichukua gari yako moja na nilikuwa natoka nje nikamkuta kituoni anataka kupanda bajaji, nikampa lifti alikuwa akienda Ubungo kukata tiketi ya kwenda Mwanza.”

“enhe?”

“amekata tiketi lakini inabidi asafiri kesho sasa nimempa hifadhi hapa kwako hadi kesho asubuhi ndio asafiri.” Alisema Stanis.

Mama yangu! ninavyomjua Stanis, sidhani kama Shose atapona hiyo kesho.

“Sikia Stanis ole wako, kwanza sitaki.. ngoja nimpigie!” nilichanganyikiwa nikiwa sielewi kama nimevurugwa au nipo mzima.

“Sikia, John. Huyu hausigeli wako, Akya mungu vile namtaka, tena nataka kumuoa kabisa, kanivuruga ile mbaya. Akya mungu sitamchezea,” alisema Stanis na kuzidi kunivuruga, sijui nini kiliniingia maana nilikuwa na wivu, hasira, ghadhabu vyote kwa pamoja.

“sitaki, uwe naye! ole wako umkaribie!” nilikoroma na kukata simu. Nikaanza kutafuta namba ya Shose huku mikono yangu ikitetemeka.

Sikia, Shose ni msichana spesho, tena nataka awe na mtu mwenye heshima zake siyo chapailale kama Stanis.

Mshkaji wangu namjua ni malaya kinoma. Bora mimi, tena kwa upole wa Shose, naona si mimi wala Stanis tunaweza kustahili kuwa naye. Sisi ni wachafu, labda mtu mwingine lakini Stanis No!

“Hallow!” nilisema baada ya simu ya Shose kupokelewa.

“Hallow kaka!” aliitikia Shose huku akisikika amenyong’onyea lakini pia alikuwa kama vile ananiogopa, nadhani baada ya kumchenjia asubuhi.

“Kwanini umerudi tena pale nyumbani?” niliwaka.

“samahani kaka sijawahi kulala gesti na nitasafiri kesho kuelekea Mwanza, huyu kaka mbona anaonekana mstaarabu amenisaidia kulala hapa hadi kesho,” alisema Shose.

“Shose kwani kwenu si Tanga? Huko Mwanza kwa nani tena?!”


LOVE INTERVIEW 26

“Leo uliponiacha wakati nampigia mama ili wajiandae kunipokea, akaniambia kuwa wametengana na baba ana mke mwingine, hivyo akanitaka niende kwake Mwanza. Yote sikuwa najua kabla, nilikupigia mapema lakini haukupokea simu yako,” alisema Shose.

Nikashusha pumzi kwanza, maana katika vitu ambavyo sikuwahi kuvitegemea, sikutegemea kama hayo yangetokea, na kumuacha Shose akae na Stanis hata kwa usiku mmoja ilikuwa kama vile nimeuacha mfupa kwa fisi.

“Sikia Shose, panda bajaji chukua kila kitu, njoo nilipo sitaki ukae hapo hata dakika moja hapo?” nilisema.

“lakini kaka kesho natakiwa kusafiri asubuhi sana, huko Mbagala ni mbali hadi Ubungo!”

“nimekwambia panda bajaji njoo!” nilikoroma tena. Shose alitaka kusema neno lakini akashindwa, akakubali nikakata simu. Nikaanza kujiuliza ninachofanya ni sahihi au?

Mara kidogo Stanis akanipigia.

“kaka kwanini unanifanyia hivi? mbona unataka kuharibiana? Kosa langu nini? si ni hausigeli wako tu au na wewe unamtaka?” alilalama Stanis.

“Sikia ole wako unyanyue kimkono chako kichafu umshike, huyo msichana ni zaidi ya unavyodhania.” Nilisema Stanis akacheka akijilazimisha kukubali kuwa rafiki yake sitaki mchezo kwa jambo hilo.

“kwani kaka wewe nia ya kwenda huko Mbagala si kutafuta demu wa kuoa au? sasa kwa nini unanibania huyu? Mimi namtaka, wewe inakuuma nini? ooh au ulikuwa unagonga siku moja moja? Maana nyumba nzima hii ulale na mtoto mzuri kama yule.. si haba.” alisema Stanis nikakata simu maana niliona anaongea upuuzi.

Sikukaa kwa raha, nikapiga simu kwa Shose tena, nikasikia yupo kwenye upepoupepo; “upo wapi?” niliuliza.

“nipo kwenye bajaji ndiyo nakuja..”

“sawa mwambie dereva Mbagala Charambe ukifika utaniambia,” nilisema roho ikipoa kidogo.

Nikaanza kutafakari, lakini mie Shose si nilimfukuza mwenyewe? Sasa kwanini nimevurugwa niliposikia yupo kwa Stanis? Huu wivu vepee?

LOVE INTERVIEW 27

Hapana siyo kama nampenda kihivyo, ni vile tu ninampenda kama mdogo wangu na namtaka asidhurike wala kupata gumegume bali mwanaume aliyenyooka kiheshima na maadili. Narudia tena mwanaume huyo si Stanis wala mimi.

Hapa ndiyo unafikia kipindi unafahamu kuna aina nyingine za mapenzi ambazo tulikuwa hatuzijui, mfano kuna upenzi unaoanzia na ushabiki mfano wasichana wanavyompenda Alikiba, wengine wanapitiliza na kuota waolewe na Alikiba kabisa tena wengine wanafikia hatua wanasema; “mimi Alikiba akinitongoza nipo tayari kumsaliti hata mpenzi wangu;” mnajijua.

Pia kuna mapenzi ya kumpenda mtu kindakindaki, kama mimi nilivyogundua siku hiyo, ninavyompenda Shose, yaani nampenda nimlinde nimtunze, sitaki achezewe, sitaki apate shida hasa kwenye mapenzi. Natamani hata kama ningekuwa na rafiki mzuri mwenye mapenzi ya dhati nimpe Shose tena kwa gharama haswaa kwa sababu thamani yake ni kubwa mno.

Ndiyo ameishia darasa la saba, lakini ni mkarimu, mcheshi, ana huruma, hana makuu, anaamini kuna mapenzi ya kweli, siyo muongo hata kidogo, hana tabia mbaya, hafichi hisia zake na mwisho wa yote ana sifa zote za kuwa mama wa familia tena hapo anapapatia kweli maana anavyonitunza mimi mwenyewe najisikia kama vile nipo na mama yangu.

Na kikubwa kuliko vyote ni rahisi kumsoma, ananuna akikosa furaha, analia akiumizwa anacheka akifurahishwa na kutabasamu akioneshwa shukrani ya thamani ya kile alichokifanya kwa mtu.

Siyo kama wanawake wengine unakuta pa kulia yeye anacheka, pa kucheka yeye analia, pa kutabasamu ananuna. Mwisho wa siku mtu wa hivyo hata ukimkosea anaficha tu kwenye tabasamu na kuua ukilala. Naogopa mno kuwa na mtu wa hivyo katika maisha yangu.

Nikiijua thamani ya Shose hadi kuwaza hivyo kwa kuwa hakuwepo kwenye upeo wa macho yangu kwa saa chache tu na nilianza kumiss kumuona.

Nikatazama saa na kuona ilienda kuwa saa kumi jioni pengine Shose atakuwa anakaribia. Wakati huohuo simu ikaingia ilikuwa kutoka kwa yule denti wa chuo niliyempaga lift kutokea Mbagala siku moja na alikujaga nyumbani anaitwa Alice nadhani unamkumbuka.


LOVE INTERVIEW 28

“Alice mambo?” nilipokea.

“poa tu, upo nyumbani? Nilitaka kuja,” alisema Alice.

“Hapana sipo nimesafiri,” nilimjibu Alice hivyo kwa kuwa kiukweli, kama nilivyosemaga siwapendi wanafunzi wa chuo na hata sikumuweka kwenye listi ya mademu wa Interview hivyo haikuwa na haja ya kumwambia kuwa eti nimefilisika nipo Mbagala, ya nini?

“ooh owkey, basi poa,” alisema kiunyonge na kuwa kama vile anasikilizia niongee. Nikahisi anajibaraguza tu ilimradi nimtongoze na hakuna kingine. Ubaya ni kwamba msichana mzuri akikutega umtongoze au ufanye naye mapenzi, dhamira asili ya kiume inakabiliana na dhamira yako yenye msimamo. Inakulainisha na kukukumbusha kutumia akili ya kichwa cha chini na siyo kichwa cha juu.

Ni kama vile hiyo asilidume inasema; “Wewe bozo ukimuacha huyu demu mwenzako atakuona shoga shauri yako.” Basi ile dhamira yako itajibu: “ila kweli wewe kama vipi mpitie tu mara moja, wewe ni mwanaume.”

Basi huo ndiyo mchezo wa akili unaotusumbua kichwani wanaume kama mimi na Stanis na asilimia tisini ya wanaume marijali duniani. Ndiyo maana nasema hivi, ili nioe nahitaji mwanamke siyo wa mchezomchezo, awe amejitosheleza hasa kiasi kwamba hizi sauti za dhamira zisiniweze kunishawishi hata kidogo.

Lakini kwa wakati huo sasa natakiwa kumtongoza huyo Alice aliyekuwa akijibaraguza kwenye simu, mademu wa hivyo ni rahisi kuwatongoza kwa sababu si anataka kitu, atakipata tu.

“Alice, unajua tangu nilipokuona siku ya kwanza nilitokea kukupenda mno, tunaweza tukawa wapenzi?” nilimwambia kisimpooo. Eti baada ya kumwambia hivyo akajifanya kama vile anashangaa na kuanza zile ngebe wanazofanyaga mademu wakitongozwa, ile kama wanajifanya wanaweka ugumu kama dalali anataka kukuuzia kiwanja Kariakoo!

Wenyewe wanaambiana kuwa eti wakikubali haraka eti ndiyo sisi wanaume tutawaona malaya. Nani kasema? Eti wanaume wenzangu kweli? Mimi naonaga inanikeraga saa nyingine hadi kutongoza naona uvivu, maana ile kuzungushana na vimaswali eti, nitajuaje kama unanipenda? Mara ooh subiri nikufikirie.. ukikubaliwa sasa unaambia ooh tusifanye mapenzi hadi tuoane. Ptuuuh! Mfyuuu!

Itaendelea..


LOVE INTERVIEW 29

Huyo Alice akajibu; “Mh hapana mimi mbona nakuchukulia kama kaka yangu na rafiki yangu tu.”

Nikajibu: “Ooh okey nilikuwa sijajua kumbe unaniona kama kaka yako, basi samahani mdogo wangu, kwa kuwa nimekukosea heshima kukwambia hisia zangu.”

“hapana, siyo vibaya, haujakosea kitu.. aah basi ngoja nitakufikiria,” alisema Alice, nikabetua mdomo pembeni nakucheka kimyakimya. Kisha nikaweka simu yangu sikioni.

“Mh lakini nataka nilale nikiwa nasikia sauti yako nzuri, nitumie basi voice note whatsapp,” nilimwambia Alice na ndiyo hapo nilipokosea maana ile tabia ya wanafunzi wa chuo sasa ikaanza. Angalia alichoniambia:

“ooh sorry ningekutumia ila simu yangu ina tatizo la whatsapp yaani siwezi kabisa kutuma voice note dia, ninunulie basi simu,” aliongea Alice kwa sauti nyororo, ile ya kuombea kitu kama wanawake wengine wa Kitanzania.

“Okey nitakuchekia wikiendi hii, usijali,” nilijibu.

“Mh halafu dia.. ah sina hata vocha naomba nitumie basi,” alisema tena Alice, sasa kengele ya kichwa changu ikalia ngriiiii nikasema kimoyomoyo ; umekosea njia ngoja nikunyooshe ukasimulie wenzako, nikamuuliza swali hili ambalo nataka wanawake wote mjifunze leo maana nilimwambia mwenzenu awaambie lakini sijui kama aliwafikishia.

“owkey nitakutumia, lakini nilikuwa nataka kukuuliza jambo moja?” nilianza.

“Uliza tu dia.”

“hivi, unapomtongoza mwanamke wakati unasubiria jibu lako, kwanini wanawake wanapenda kuleta matatizo yao kwa aliyewatongoza? je mnatutestigi wanaume tupoje? Au ni hulka tu mliyofunzwa na mwalimu wenu ambaye bila shaka ni mmoja?”

“mh..hapana..hata mimi sikumaanisha hivyo, nimekuomba vocha kama rafiki, aa.. mbona siyo wewe tu hata rafiki yangu yoyote naweza kumuomba vocha akanitumia,” alianza kubabaika Alice.

“bado haujanijibu kwa sababu hao ulionitajia kama mfano hawajakutongoza, na siyo vocha tu, hata simu pia umeniomba au umesahau?”

“..aah.. Sikia basi nilivyokuomba vyote usinipe, nimekosea!”


LOVE INTERVIEW 30

“Sikia mbona unakuwa mkali, mimi nimekuomba tu uniambie, mnatutestigi? Au ni hulka tu, nifundishe basi,”

“sitaki basi niache!” alipaniki Alice

“Sikia nilishakutumia elfu tano, usijali,”

“haya asante lakini si kwa michambo hiyo, sitakuomba tena,”

“sikia inategemea utaniomba wakati gani, lakini kikubwa mfahamu tu kwamba, hiyo tabia yenu mkitongozwa tu mnaanza kujifanya mnawabwagia matatizo yenu wanaume, yanawafanya wanaume wajiulize swali ambalo mimi pia nimejiuliza ila nimejiuliza kwa sauti.

“Lakini kwa niaba ya wanaume nimekwambia, na usinichukie kwa sababu kosa langu pengine ni kuwa wa kwanza kukuchana ukweli, sasa hii kawaambie wasichana wenzako wote wenye tabia kama yako.”

“mh, aisee basi nimekoma baba, umemaliza?”

“bado, ni hivi, kutengeneza mazingira ya kuombanaombana vitu kabla hata jibu haujanipatia, inafanya na mimi nitengeneze mazingira ya nipe nikupe. Nitakwambia ukitaka kitu njoo uchukue gheto, na ukija nitakufanya ninachotaka ndiyo nitakupa hela, sasa utakuwa na tofauti gani na changudoa tu.

“Halafu leo au kesho ulalamike ooh boyfriend wangu nikimuomba kitu hanipi paka nimpe mzigo, kumbe ulitengeneza mazingira wewe mwenyewe.”

“hee basi nimeshasema nimekoma. Haya umemaliza?”

“bado.. kingine nataka kukuuliza vipi? Kwa hiyo utanikubalia tongozo langu au ndiyo baada ya kukuosha haunitaki.”

“aisee,mh! Inategemea wewe utatakaje?” alijibu Alice kwa aibu maana mh. Mimi naye nimezidi.

“mimi naamua sitaendelea kukutongoza. kama tulivyokuwa hatujuani mwanzo, wewe endelea na yako maana nilishajua ulitegemea niwe sponsor wako, lakini mimi sitaki hiyo michezo, sasa hivi nimekua,” nilisema sura kavu na kukata simu, na imani atakuwa ameipata freshi ya shamba.

Wakati huo nakata tu simu ya Shose iliingia kuwa yupo barabarani nikawaelekeza nilipo, mtu wa bajaji akamleta mpaka nilipokuwa, Shose aliponiona tu akanikimbilia na kuniwaoh huku akilia tena kilio cha kwikwi.

Huwezi amini kule uswazi tukio kama hilo ni la ajabu, na kila mtu alipata tafsiri kuwa ni mtu wangu. Nikajitoa kwanza na kumlipa dereva bajaji lakini Shose alinishika mkono hakunipa hata nafasi sijui alijua nitamuacha tena?



Tuliingia ndani, Sasha akakaa kwenye kochi pembeni yangu na kunitazama, kama vile ananikagua kuona ninachofikiria. Nikajishtukia mno maana katika sehemu kama hizi ndiyo mtu anapaswa kuomba msamaha si ndiyo au?

“Shose, kwanza nisamehe kwa kukuacha kule barabarani, sikudhani kama utapata tabu kusafiri leo,” nilianza kusema. Shose akaanza kulia tena kama kawaida yake. Nikamfuta machozi kwa kiganja changu hadi akapoa.

“Sawa, kwa hiyo umeniita huku ili iweje?” aliuliza Shose akionekana kuchukia kweli.

“hapana, sikutaka ulale kule, simuamini yule mtu,” nilisema.

“kwanza ulijuaje kama nilirudi kule?” aliuliza Shose nikaanza kubabaika maana sikuwa nimejiandaa kwa swali hilo hata kidogo na Shose hatakiwi kufahamu kama mimi na Stanis tunafahamiana na eti kwamba tumecheza dili.

“Aah, nilipigiwa na majirani, ndiyo nikakupigia. Sikia Shose, sikukuacha kwa kupenda angalia haya mazingira niliyokuja kuishi, siwezi kukutunza tena mdogo wangu, nisamehe kama nilikosea,” nilijitetea.

“Nimekusamehe, lakini sijapenda hata kidogo kwa sababu katika furaha tuliishi vizuri na ulinisaidia kama mdogo wako, kwanini na mimi nisilipe wema wako ukiwa kwenye matatizo?”

“Mh, Shose unadhani utanisaidiaje wakati na wewe mwenyewe unahitaji msaada?”

“kiukweli, kwanza nikwambie tu, nilipokuwa mfanyakazi wako ulikuwa ukinilipa pesa nyingi kiasi kwamba nikimwambia mtu ulikuwa ukinilipa laki tatu kwa mwezi hakuwa akiamini. Hata hivyo ulikuwa ukinipa na hela ya nguo,nilikuwa na kula na kulala bure. Hivyo nimehifadhi hela, najua ninaweza kukusaidia tu,” alisema Shose.

“ooh, sawa, lakini hizo hela wewe kaa nazo kwa sababu ni zako.”

“hapana, nitafanya kila kitu kukusaidia kabla sijaondoka kesho, ukubali au ukatae.”

“kwani unataka kuondoka kweli?” niliuliza.

“ndiyo lazima nisafiri kesho..” alisisitiza Shose.

“usiondoke bwana unawezakukaa na mimi..” nilisema kwa hisia bila kufikiria kwanza maana nilionekana kama vile nambembeleza yeye wakati mwanzo yeye ndiye aliyetaka kukaa na mimi halafu nikamkimbia.

“mh hapana, chumba chenyewe ni kimoja hatuwezi kukaa pamoja, watu watatufikiria vibaya, hata hivyo lazima nisafiri kwasababu kuna kitu cha muhimu naenda kukifanya,” alisema Shose.

“Kitu gani hicho cha muhimu?”


LOVE INTERVIEW 32

“ngoja nikwambie ukweli? kuna mtu anataka kunitolea posa ndiyo nimemuelekeza aende kijijini kwetu kama kweli yupo siriaz, sasa natakiwa kuwahi mimi kwanza ili nipajue alipoishi mama kwanza ili huyo mtu akija nimuelekeze vizuri, maana hata mimi sipajui,” alisema Shose nikashangaa.

“Mh kwa hiyo Shose, huyo mtu unafahamiana naye au?” niliuliza moyo ukinipigapiga lakini sikujua kwanini.

“Simfahamu sana ila ni mkaka mstaarabu tu.”

“Kwani yupoje yupoje?”niliendelea kudadisi.

“ni mkubwamkubwa kama wewe tu hivyo..”

“anaitwa nani?”

“He! kaka kwani kuna tatizo?”

“Sikia Shose kama haumfahamu vizuri utakubali vipi kuolewa naye akija kukubadilikia huko ndani itakuwaje?” niliuliza.

“hayo mengine nitavumilia lakini kama anataka kunioa ni bora, nikaolewa maana hali ya sasa hivi wanaume wa kuoa wapo wapi?” alisema Shose, nikawaza laiti angejua kama mwenzake nataka kuoa ila wanawake wa kuoa siwaoni sijui angesemaje?

“Mh wanaume watulivu wapo lakini hauwaoni tu.” Nilijibu nikiwa mbali kweli kimawazo.

“Mh nani mtulivu! Mfano mzuri wewe ulivyo malaya hadi naogopa wanaume wote,” alisema Shose. Nikaona aibu na kujishtukia kwa mara ya kwanza, mh kumbe mimi ni malaya kiasi hicho?.

“Haya bwana, basi kesho asubuhi nitakukodia taksi hadi Ubungo,” nilisema nikiwa nimeshushuka, nikajiuliza ina maana ndiyo hivyo tena Shose anaenda kuolewa na mapishi yake na usafi wake na vyote alivyonifanyiaga ndiyo anaenda navyo kwa mtu mwingine?

Ni fundo gumu la mua ambalo nilibidi kulitafuna tu.Basi wakati huo Shose akachukua maji na nikamuelekeza bafuni, akaenda kuoga nyumba nzima ikimuangalia huko koridoni hadi uwani, aliporudi chumbani ilibidi mimi nimpishe ili abadilishe nguo, nikaenda zangu kukaa kibarazani kigiza cha saa moja kikianza kutanda mawinguni.

Wakati huo yule mtoto wa baba mwenye nyumba, Zainabu ambaye alinidekia chumbani na kunisafishia, akajipitisha na kuniambia; “mh kaka hongera naona umetuletea chuma cha nguvu hapa mtaani kiukweli wifi mzuri sana. Aaaar… Kwa hiyo dili la kukusafishia chumba ndiyo baibai tena!”

Itaendelea..


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG