Search This Blog

Saturday, February 6, 2021

RISE UP SEHEMU YA 10/10 MWISHO

  

RISE UP

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 10 KATI YA 10 MWISHO





Nikamshuhudia mama Shamsa amcho yakibubujikwa na machozi. Caro, uvumilivu ukamshinda na akaanza kuangua kilio cha uchungu sana na nikawa na kazi ya kumbembeleza. Habari hizi kwa kweli ni habari mbaya kwa kila mtu ambaye alikuwa ana mpenda huyu mzee ila kwa upande wangu kusema ukweli kutoka moyoni ni habari nzuri na yenye kunifurahisha. Furaha iliyo tawala moyoni mwangu kusema kweli imezidi furaha zangu zote.

“Nataka kumuona kaka yangu. Hawezi kufa, nataka kumuona”

Caro alizungumza huku akitembea kuelekea kwenye chumba hicho alichopo raisi. Hiyo ikawa nafasi yangu yapekee na mimi kujidhibitishia kama kweli jamaa amekufa kwani hawa watu wana weza kuchekecha hili jambo na kujikuta mzee yupo hai na ikatangazwa amekufa. Tukaingia ndani ya chumba hichi na Caro, tukaukuta mwili wa raisi ukiwa umezungukwa na madaktari huku ukiwa umefunikwa shuka jeupe. Caro taratibu akafunua shuka la hilo neo la usoni na kweli nikamshuhudia mzee akiwa amecharangwa charangwa uso wake kwa visu vikali sana.

“Huyu aliye kufanyia hivi kaka lazima alipe. Haki ya Mungu ni lazima alipe”

Caro alilia huku akiutazama mwili wa kaka yake.

“Kwa hiyo na nyinyi mulishindwa kuokoa maisha yake?”

“Samahani tulijitahidi kadri ya uwezo watu ila tulishindwa. Kwani hadi ana fikishwa hapa hai yake ilikuwa mbaya zana kwani eneo la moyo wake ulitobolewa tobolewa na visu”

Caro bila ya woga akafunua shuka zima na tukaona jinsi mwili wa raisi ulivyo chanwa chanwa na upanga wenye makali makubwa sana kwani vidonda vyake vimechimbika sana na katika upande wa kushoto wa kifua chake ulipo moyo wake kumetobolewa mara nne.

‘Mmmm aise kauliwa vibaya sana’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikishusha pumzi. Caro akaanza kutoka ndani hapa ikanibidi kumfwata kwa nyuma.

“Nahitaji kumuua aliye husika mume wangu”

“Utampatia wapi Caro acha vyomgo maalumu vihusike kwenye uchunguzi wao”

“Mimi pia ni mpelezi nita lisimamia hili nita hakikisha wana lipa kwa hili jambo”

Caro alizungumza kwa hasira huku kitembea kuelekea nje.

“Rashidi nahitaji kuwa peke yangu sasa hivi. Naomba uniache”

Caro alizungumza huku akininyoshea mkono. Nikasimama na kumuacha akielekea nje. Fatma akanifwata sehemu nilipo simama.

“Ina bidi urudi nyumbani tu una weza kutumia gari yangu kurudi nyumbani”

Fatma alizungumza huku akinikabidhi funguo ya gari lake. Nikamtazama mama Shamsa ambaye bado amekaa kwenye kiti, huku akionekana ni mtu aliye pigwa na bumbuwazi ambalo lina mfanya ashindwe kufanya chochote.

“Poa tuta onana baadae”

“poa”

Nikaondoka eneo hili nikaingia ndani ya gari na kuondoka eneo hili. Nikafika nyumbani na kupokelewa na Shabani.

“Vipi ndugu yangu?”

“Aisee jamaa kanyuti kweli”

“Weee”

“Yaa hapa nina furaha kubwa sana. Ila kauliwa kifo cha mateso makubwa sana kwani amecharangwa charangwa na mapanga aisee.”

“Duu kwani ume uona mwili wake?”

“Ndio niliingia kwa tiketi ya Caro kwenye chumba alipo kuwa anatibiwa.”

“Ila ni jambo la heri, adui mmoja ameanguka sasa bado mwengine mmoja”

“Yaa kwa sasa ngoja nikalale, nimechoka choka sana”

“Poa kaka usiku mwema, nilikusubiria kuhakikisha una nipatia hali halisi iliyo tokea huko.”

“Nashukuru kwa hili ndugu yangu”

“Usijali nipo nyuma yako kwa kila jambo”

“Poa poa kaka”

Nikaingai chumbani na kumkuta Jackline akiwa amelala. Nikavua nguo zangu, nikaingia bafuni nikaoga kisha nikarudi chumbani na taratibu nikapanda kitandani.

“Umerudi mume wangu”

Jackline aliniongelesaha kwa sauti ya upole iliyo jaa usingizi mwingi.

“Nimerudi salama mke wangu”

“Mungu ni mwema, nilikuwa nina omba sana kwa mwenyezi Mungu aweze kukusaidia urudi salama.”

“Asante kwa maombi yako mke wangu. Na nina shukuru kwani kazi haijatendwa na sisi”

“Una maana gani?”

“Raisi ameuwawa na mtu mwengine. Amekatwa katwa na mapanga”

“Weee?”

“Ndio yaani ni kama vile ameuliwa na maninja. Jinsi alivyo katwa aisee ina tisha”

“Duu kwa hiyo nyinyi?”

“Sisi tulimshuhudia huyo muuaji akiingai kwa kupitia dirishani. Sisi tulikuwa gorofa ya pili na hatukuona kilicho fanyika ndani hivyo mambo yalikuwa ndio hivyo yalivyo tokea. Mzee kakon’otwa vya kutosha”

“Aise huyo muuaji tungemjua tungempa zawadi”

“Umeona ehee?”

“Ndio mume wangu”

“Hapa nina furaha sana mke wangu. Sasa nina hisi amani ita nitawala moyoni mwangu.”

“Ita tutawala sote mume wangu kwa maana adui yetu amekufa”

“Yaa ni kweli”

Kutokana na uchovu wa mizunguko ya siku nzima sikufanya chochote zaidi ya kulala fofofo. Asubuhi na mapema nikawasha tv iliyopo chumbani hapa, habari nilizo kutana nazo ni juu ya maaji ya kutisha ya raisi ambaye alipanga kurudishwa madarakani kwa kura za wabunge.

“Umeamkaje mume wangu?”

Jackline alizungumza huku akiingia ndani hapa. Akanikabidhi kikombe cha kahawa.

“Salama mke wangu. Niambie”

“Safi tu mume wangu. Naona habari ni hiyo tu, raisi ameuwawa”

“Ndio mke wangu ni jambo jema na zuri kwa kweli kwa sisi tulio kuwa maadui zake.”

“Kwenye msiba wa huyu mzee wata hudhuria watu wengi”

“Yaa wata kuja viongozi wengi wengi”

“Mmoja wao ni Don. Una onaje tukaajiri wauaji wenye uwezo mkubwa kuhakikisha wana muua DON mara tu baada ya kukanyaga ardhi ya Tanzania?”

“Ni wazo zuri ila DON sio mtu wa kuuwawa kirahisi kama hivyo mke wangu”

“Ua maanisha nini?”

“Don ni mtu wa kubadilika badilika sana na kama unavyo jua ni kwamba mimi nina mfahamu.Na isitoshe nimeonekana pale hospitalini naamini kuna watu watakuwa wamemtonya. Hivyo hawezi kuja kwa sura ya Frenandes Philipe, hivyo ata badilisha sura yake”

“Hawezi”

“Kwa nini una sema hawezi?”

“Ana dili kubwa sana ya pesa kwenye kampuni yangu. Hivyo atataka endelea kuishi na sura yake hiyo hiyo ila asiweze kupoteza pesa hiyo. Isitoshe tuna kikao kingine mimi na yeye mwezi ujao”

Nikapiga fumba la kahawa hii huku nikitafakari maneno ya Jackline.

“Don simuamini sana”

“Najua hilo humuamini mume wnagu. Ila ni wakati wa sisi kumsulubisha kabla hajaleta maafa makubwa kwetu”

“Usijali mke wangu tutapata suluhisho”

Mlango ukagongwa nikavaa pensi na tukamruhusu anaye gonga mlango aingie ndani hapa. Shamsa akaingia huku akiwa amejawa na huzuni kidogo.

“Vipi baby una nini?”

Nilizungumza huku nikimpa mkono Shamsa na nikamvutia kitandani.

“Shikamoo dady”

“Marahaba vipi mbona una huzuni?”

“Nasikia baba yule mwengine amefariki?”

Mimi na Jackline tukatazamana.

“Ndio mwanangu”

“Nataka nikaudhurie msiba wake”

Jackline akanitazama kwa sekunde kadhaa, nikashusha pumzi huku nikimtazama Shamsa usoni mwake.

“Kwa nini una taka kwenda?”

“Nahitaji kukutana na mama. Nahitaji kumueleza ni jinsi gani ninavyo mchukia”

“Hivyo tu?”

“Ndio baba”

“Basi tuta kwenda. Usiwe na wasiwasi mwanangu”

“Nataka twende na mama Jackline pia”

“Usijali Shamsa mwanangu tuta kwenda na baba yako pia. Sote tuta kwenda”

“Sawa mama, nakupenda mwaaaa, Dady mwaaaa”

Shamsa akatubusu wote kishaa katoka ndani hapa akikimbia.

“Una jua sina mpago wa kuelekea huko msibani”

Nilizungumza huku nikishuka kitandani.

“Sasa uta fanyaje mume wangu na mtoto amehitaji. Ina bidi twende tukahudhurie msibani”

“Ngoja tupate kwanza update za huko msibani kisha tutajua nini cha kufanya.”

“Sawa mume wangu. Alafu mama ameniambia ukiamka umtafute kwenye simu”

“Sawa mke wangu”

Nikaoga kisha kwa pamoja tukaelekea sebleni, nikasalimiana na watu wote.

“Rashidi”

“Ndio mama”

“Mpigie mama yako ana kutafuta kwenye simu”

“Sawa mama”

Nikatoka nje na nikampigia simu mama.

“Bi mkubwa”

“Vipi wewe mbona napiga simu yako hupokei, ulikuwa wapi?”

“Nilikuwa nimelala mama vipi?”

“Unanipa wasiwasi mwenzi. Vipi naona habari?”

“Ndio mama tuta zungumza. Vipi umefikia wapi?”

“Tulifika leo alfajiri na saa sita hivi nita elekea kwa wenyeji wetu kukamilisha kazi”

“Sawa mama”

“Ila upo salama?”

“Mimi nipo salama kabisa”

“Sawa nina rudi leo hii hii”

“Poa, sasa nani ana kuendesha?”

“Kuna dereva Tina amemtafuta”

“Sawa”

“Badae”

“Poa mama”

Nikakata simu na Chausiku akanifwata nilipo simama.

“Naona hatukumbukani, una nipotezea kama vile sipo”

“Una maanisha nini?”

“Rashidi una jua nini namaanisha. Umenifanya nina ishia kwa mateso humu ndani kana kwamba sijui nipo kuzimu. Yaani ingekuwa sio mama yangu basi ningekuwa nimesha ondoka”

“Usisema hivyo mpenzi”

“Haki ya Mungu vile Rashidi. Nina wivu, huyu mzungu wako naona ana nichefua tu mimi”

“Amekukosea nini na usisahau huyu ni mke wangu wa ndoa”

“Okay tuachane na hayo. Nina nyeg** sana leo utanisaidiaje?”

“Daa mshakaji wangu huoni amekaba hadi penati”

“Ndio naona ila wewe mwanume bwana. Kwani ukimuaga sasa hivi una toka una hisi ata kufwatilia.”

“Basi ngoja nifanye utaratibu alafu tuta ona nini cha kufanya”

“Sawa usiniangushe kwa maana natamani sana kukubaka wewe”

“Duu haya mama”

Chausiku akaondoka huku akinitingishia makalio yake kimakusudi. Shabani akashuka ndani ya gari na tukasalimiana.

“Ulikuwa umetoka?”

“Yaa nilieleka kwenye zile ofisi za mabasi, kuna mambo nilikuwa nina kwenda kuyakagua”

“Asiee ina bidi leo twende na shemeji yako tukapaone”

“Hakuna shaka kaka. Nimepata fununu fununu kwa baadhi ya wana usalmaa. Wanadia kwamba muuaji ni mwanamke”

“Yaa ni mwanamke si tulimuona”

“Ndio ila Sheila una ambiwa amemuona mwanmke huyo”

“Amemjua?”

“Sijajua ila wanavyo dai mke wa raisi ana mjua. Sasa kama ni yule demu wa Kibrazil ita bidi umtafute na kumuatarisha.”

“Ngoja tuone tusikurupuke. Msiba ni lini?”

“Sijajua ratiba ya msiba ni lini”

Baada ya kifungua kinywa mimi, mke wangu na Shabani tukaelekea zilipo ofisi zetu za mabasi. Kusema kweli, Shabani amefanya kazi kubwa sana na kwa umakini wa hali ya juu kwani ofisi hizi zimetengenezwa vizuri na eneo hili lina uwezo hata wa kuingiza basi thelathini kwa wakati mmoja.

“Pazuri sana shemeji hongera”

“Nashukuru shemeji, ndio maandalizi bwana ya mabasi yetu”

“Hongereni sana. Una jua jambo zuri ni kuhakikisha kwamba muna fanya kitu kizuri na chenye ushindani kwenye soko hilo lenu”

“Ni kweli shemeji ndio kitu ambacho tuna jitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kutuletea jambo zuri”

Ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yangu kwa njia ya SMS ya kawaida.

‘HONGERA’

Nikautazama ujumbe huu ambao ume toka kwenye namba mpya ambayo sio yangu.

“Ngoja niongee na simu”

Nilizungumza huku nikitoka nje. Nikaipiga namba hii, ikaita na baada ya muda mfupi ikapokelewa.

“Halooo”

Nilizungumza ila mtu wa upande wa pili wa simu akaka kimya.

“Haloo”

“Hongera”

Niliisikisa sauti ya DON, nikastuka kidogo.

“Hongera ya nini?”

“Najua wewe ndio umehusika na mauaji haya. Hongera sana”

“Mzee naona umezeeka vibaya. Sijahusika na tukio lolote na sijajua ni nini kinacho endelea. Vita yangu ni mimi na wewe. Kama ulishindwa kuniua Madagascar na ukaishi kunining’iniza kama nyama buchani. Basi tukikutana safari hii sinto kupa nafasi kama niliyo kupatia ile siku pale chooni”

“Hahah una hisi ni rahisi kama unavyo dhani?”

“Ni rahisi sana kama nilivyo mpa ujauzito mke wako wa ndoa na akanizalia mtoto wangu”

Kauli yangu ikamfanya DON kukaa kimya kwa sekunde kadhaa.

“Ume sema?”

“Ohoo kumbe ulikuwa hutambui. Nilimpa ujauzito bwana mke wako au kwa lugha nyingine mdhamini wangu”

“Nilipanga hii vita niifanye kiustarabu sasa umenichokoza. Nitahakikisha nina kuwinda, nina kuua. Safari hii simto ach ahata damu yako moja ikikaa hapa ulimwenguni”

“Hahahahaa, mzee una jipa matumaini ambayo kwa kweli hayapo kwenye hii dunia.”

“Eti ehee?”

“Ndio hayapo”

“Sasa subiri uta pata matokeo yake. Utajua kama mimi ndio Diaz Frenandez Maquilan”

Don alizungumza kwa hasira sana kishaa akakata simu na kunifanya nishushe pumzi kwani hili jina la Diaz sijawahi kulisikia wala kulifahamu kwenye maisha yangu yote. Nimezoea kumuita DON au Frenandez Philipe.




ENDELEA

Nikaitazama simu yangu kwa sekunde kadhaa, nikataka kuipiga namba ya DON ila nikajiona nitakuwa nina fanya makossa kwani siwezi kumnyenyekea wala kumuogopa tena. Nikarudi ndani na kumkuta Shabani akimuelekeza Jackline maeneo yaliyomo ndani ya ofisi zetu hizi mpya.

“Kumbe DON jina lake halisi ni Diaz Frenandez Maquilan”

“Mmmmm umejuaje mume wangu?”

“Ametoka kunipigia simu, adai sisi tumehusika na kifo cha rafiki yake na atatukomesha na tuta mjua jina lake halisi kwamba yeye ni nani”

“Mmmm mume wangu huyo anamaanisha asije akatufanyia kweli”

“Usijali nita dili naye”

“Sawa mume wangu”

Baada ya kumaliza kukagua ofisi hii tukaondoka eneo hili.

“Hivi msibani uta kwenda kweli mume wangu?”

“Kwa ajili ya kumridhisha mtoto acha twende”

“Mmmmm mimi sipendi kuonana na yule mwanamke. Una nijua nina wivu mume wangu”

“Basi uta baki nyumbani na mama, mimi nita kwenda na Shamsa”

“Sawa mume wangu”

Tukamtembeza Jackline kwenye maeneo mengi ya jiji hili la Dar es Salama. Majira ya jioni tukarudi nyumbani na kumkuta mama akiwa amesha rudi.

“Imekuwaje?”

Nilimuuliza mama huku tukiwa tumekaa katika kibanda cha kumpumzikia.

“Kila kitu kime kwenda vizuri. Hivyo kilicho salia ni ndoa tu”

“Ahaa kuoa kwa sasa hapana. Nina ishu hapa ina niumiza kichwa”

“Ishu gani?”

“Mjukuu wako ana hitaji kuonana na mama yake”

“Nani?”

“Shamsa”

“Ana wazimu huyu mtoto ehee?”

“Sio wazimu mama. Ila yule ni mama yake na anahaki ya kumuona”

“Hata kama au amesahau kile alicho fanyiwa na mama yake”

“Ana kumbuka ila ana hitaji kuzungumza na mama yake na ana hitaji nimpeleke msibani”

“Na wewe umeamuaje?”

“Nimeamua kumpeleka, sasa tuta fanyaje”

“Haya ila kuwa makini”

“Usijali”

“Ehee imekuwaje juu ya kazi iliyo kurudisha haraka haraka?”

“Sio mimi niliye muua kabla ya sisi kutimiza lengo kuna mtu aliwahi kuingia na akamuua”

“Una mjua?”

“Hapana”

“Upelelezi una semaje?”

“Naamini bado wata kuwa wana endelea kupeleleza hilo tukio.”

“Kuwa makini bwana. Maswala ya kukimbizana kimbiza kwenye nchi yetu wenyewe mimi sitaki”

“Sawa bi mkubwa nimekuelewa”

Simu yangu ikaanza kuita, niakitoa mfukoni na kuona namba ya Caro. Nikastuka kidogo kwa maana namba yangu hii sikumpatia.

“Hei”

“Jamani mume wangu, yaani na msiba wote huu hata huonekani jamani”

Caro alilalama.

“Nitakuja upo wapi?”

“Nimerudi nyumbani kwangu, nyumba ilisha fanyiwa ukarabati”

“Msiba upo wapi kwa sasa?”

“Upo ikulu”

“Sawa basi bye saa mbili hivi nita kuja hapo”

“Poa mpenzi, usishangae namba yako alinipatia Fatma”

“Ohoo sawa sawa”

“Haya”

Nikakaya simu huku mama akinitazama kwa macho ya kunidadisi.

“Nani huyo?”

“Ehee?”

“Huyo nani?”

“Mdogo wake raisi?”

“Ndio huyo uliye mpa ujauzito?”

“Ndio”

“Yaani wewe. Eheee ana taka nini jioni yote hii”

“Anataka nikamuone”

“Ukamuone ikiwa mke wako yupo hapa. Hembu muheshimu basi mwenzio. Maswala ya kutoka toka usiku na kurudi umechelewa na umetoka kwa mwamke mwengine hivi huoni una mpandikiza mwenzako majanaba. Na hivi una kumbuka kutimiaga kinga wewe?”

“Watoto wangapatikanaje?”

“Wee sema watoto wanapatikanaje utakufa na ukimwi wewe na nimesikia pia umetembea na lile jimama linani sijui Fatma”

“Nani kakuambia?”

“Nani ameniambia, wewe jifanye una fanya mambo kimya kimya ila data zako zote ninazo hapa mkononi na hadi za huyo Chausiku pia ninazo”

“Mama jioni njema”

“Una enda wapi. Kaa hapa nikupe vidonge vyako”

“Mama mbona siku hizi umekuwa hivyo lakini. Una hisi mimi napenda hayo maneno yako ya rejareja?”

“Upende usiyapende ila mimi ni mama yako na nitakueleza ukweli. Wewe sasa hivi ni baba, una watoto wadogo ambao hata maisha bado hawajayajua. Ukifa leo una hisi wataishije hao?”

“Kama nilishindwa kufa kwa risasi siwezi kufa kwa ukimwi mama”

“Ona ulivyo mpuuzi?”

“Nakuambia mama. Ukimwi una dawa una kunywa maisha yanasongo mbele. Risasi ikipiga mwilini maeneo mabaya una kufa”

“Yaani chizi kweli wewe hujionei huruma”

“Tuachane na hizo mada mama”

“Asiye sikia la mguu huvunjia guu Rashidi. Wee haya”

Nikasimama na kuondoka eneo hili. Nikaingia chumbani na kumkukuta Jackline akizungumza na simu.

“Sawa baba”

Jackline akakata simu.

“Vipi?”

“Nimezungumza na baba hapa, nimemuelezea swala la Frenandes Philipe na ameniambia ata lishuhulikia, ata tafuta wauaji maalumu na wata muua”

“Una uhakika wana weza kulishulikia hilo?”

“Asilimia mia moja”

“Ila kumbuka Don sio mtu wa kumchezea kirahisi hivyo. Ana badikika badilika kama kinyonga”

“Najua hili mume wangu ila hatuwezi kusubiria atudhuru nasi ndio tuzinduke. Pia nimesha itaarifu serikali ya Marekani wana lifwatilia hilo kwa umakini”

“Una haribu sana mke wangu”

“Sasa naharibu nini mume wangu”

Don ana watu ndani ya FBI, CIA yaani ashirika yote makubwa ya kujasusi duniani. Ndio manaa alikuwa ana kaa Marekani na hakamatwi mke wangu ikiwa ilikuwa ana julikana ana uza dawa za kulevya. Hembu kuwa makini mke wangu kabla ya kufanya kitu na kama akisha jua kwamba ana julikana kwa jina la Frenando Philipe lazima ata jibadilisha sura na ita kuwa ni ngumu sasa kumfahamu”

Nilizungumza kwa msisitozo na kumfanya Jackline kukaa kimya.

“Sikulijua hili mume wangu naomba unisamehe?”

“Huja nikosea ila ina bidi usifanye mamauzi kama hayo bila kunishirikisha. Tuna watoto mke wangu, tuna family, nina walinda vipi. Wewe mwenyewe una jua shida zote tulizo pitia Somalia. Kwa nini hao CIA wasinge kuja Somalia kukusaidia”

“Sasa ita kuwaje mume wangu”

“Nahitaji wewe na watoto muwe salama. Nyinyi ndio macho yangu kwa sasa, sinto hitaji muende sehemu yoyote bila ya uangalizi wangu”

“Sawa mume wangu. Naomba unisamehe sana”

Taratibu Jackline akanikumbatia kwa nguvu.

“Huwa sipendi kukuudhi mume wangu”

“Usijali nimekusamehe”

“Asante mume wangu nina kupenda sana”

“Nina kupenda pia. Saa mbili hivi baada ya chakula cha usiku kuna sehemu nita elekea mara moja”

“Wapi mume wangu”

“Nahitaji kufwatilia hili swala la hili tukio. Nataka kujua upelelezi wao wana ufanyaje ili nijiepushe vipi kwenye hili sekeseke kama unayvo jua. DON ana nishuku mimi hivyo asije akapandikiza chuki kwa vyombo vya usalama na wakanifwatili mimi”

“Sawa mume wangu, una nipa wasiwasi”

“Usijali mke wangu. Kama mambo mengi ya nyuma yalisha pita kwa nini hili lisipite. Nina imani kwamba mwenyezi Mungu ata jalia maisha yetu yatakuwa ya amani na furaha”

“Sawa mume wangu”

Baada ya chakula cha usiku, nikaondoka nyumbani kwangu na moja kwa moja nikaelekea nyumbani kwa Caro, nikakuta ulinzi ukiwa umeimarishwa. Kutokana walinzi hawa wana habari juu ya ujio wangu hivyo ikawa ni rahisi kwa wao kuniruhusu kuingia ndani. Nikaingia sebleni, Caro akanikimbilia na kunikumbatia kwa furaha.

“Heri umekuja mume wangu nilikuwa ni mnyonge sana, sikuwa na mtu wa kuzungumza naye”

“Niambie wewe na mwanangu muna endeleaje?”

“Tuna mshukuru Mungu tuna endelea vizuri. Ila nakuomba unisamehe mume wangu kwa yale niliyo yafanya jana usiku”

“Usijali najua uligadhibika na hali ilivyo kuwa”

“Nashukuru kwa kunielewa”

“Ehee wana semaje juu ya upelelezi?”

“Aliye fanya tukio ni mwanamke, hadi sasa hivi ana tafutwa”

“Aise sasa ilikuwaje kwani hapakuwa na ulinzi?”

“Ulinzi ulikuwa mkali sana ila inavyo sadikika wana dai kwamba aliingia kupitia dirishani eneo ambalo kwa akili za kawaida haikuwa rahisi kwa mtu kufikiria kwamba ana weza kuingia mtu kwa maana chumba chao kilikuwa gorofani. Juu”

“Mmmm kwani juu ya gorofa hapakuwa na walinzi?”

“Walikutwa wameuwawa wote”

“Duuu”

“Yaani ina onyesha mwanamke huyo alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kininja”

“Pole sana mke wangu”

“Nimesha poa nawe pia pole sana natambua kaka na Don ndio walihusika kwenye ile ajali ya kule Madagascar na niliopo kuja kuzinduka sikuweza kukuona na kaka akadia kwamba ina bidi tuondoke nchini Madagacar japo nilitamani kubaki nikutafute ila akadai kwamba zawadi ya ujazito niliyo kuwa nayo tumboni nisiipoteze hivyo na nikakumbuka ulivyo kuwa una nisisitizia kuhusiana na hii mimba hivyo nikaona ni bora nimlinde mtoto wetu”

“Usijali kwa maana najua aliye sababisha yale yote ni nani?”

“Ni nani?”

“DON”

“Don”

“Ndio”

“Mbona tulikuwa naye na akadai kwamba amekuja kutisaidia na tiketi za ndege tukakatiwa na yeye na akapanga na kaka namna ya kumrudisha madarakani na waka husika na kumuua jenerali Ngatuma na aliye mpatia pesa ili kuchukua madaraka”

“Ndio hivyo mke wangu hapa kuna kamchezo kanacho endelea. Don ni mtu ambaye ana zungusha kete zake kwa akili sana. Yaani Don akiwa amekusudia lake basi ana weza kufanya kitu chochote kuhakikisha ana mdhuru adui yake”

“Unataka kuniambai DON amehusika kwenye kifo cha kaka?”

“Sijui kama amehusika ila kama walitalifiana basi ana weza kuhusika kwani DON ata kutumia leo kwa manufaa yake ukishindwana naye ana kuua”

“Mmmm”

“Ndio hivyo mke wangu”

“Hivi una tambua kwamba DON yupo hapa Tanzania?”

“Yupo wapi?”

“Hapa hapa Dar ila sijajua ni wapi kwa maana aliniambia amefika kwa ajili ya msiba wa kaka”

“Kwa hiyo unanishaurije mke wangu?”

“Ngoja nifanye kitu”

Caro akachukua simu yake na akampigia Don.

“Kaka habari?”

“Salama Caro mbona muda huu”

“Najaribu kutafakari juu ya nani amemuua kaka yangu ila ninakosa usingizi. Nina omba msaada wako, nakuomba tuonane usiku wa leo ili niweze kuendeleza pale alipo ishia kaka”

“Tena umeniwahi, nilikuwa nina fikiria hilo hilo jambo. Ina bidi tuonane leo kwani kaka yako alikuwa ni mtu wako na wangu wa karibu sana ivyo nahitaji kujua huyu mwanamke aliye muua ni nani kwa maana yule boya naona hajausika na kifo cha kaka yako”

“Nani huyo?”

“Ahaa tuachane naye. Tuonane wapi?”

Caro akamueleza Don ni eneo gani ambalo waonane ambalo ni pembezoni mwa fukwe ya bahari, eneo ambalo sio rahisi kwa mtu kuweza kutembelea eneo hilo. Baada ya makubaliano hayoa kakata simu.

“Nahitaji leo hii hii umuondoe duniani Don”

“Usijali mke wangu”

“Una weza kuifanya hiyo kazi?”

“Kwa nini nishindwe”

“Njoo”

Tukaingia kwenye moja ya chumba kiloichopo humu ndani. Caro akafungua mlango wa siri kwa kutumia picha kubwa iliyopo ukutani hapa. Mlango huu una ngazi za kuelekea chini ya ardhi.

“Hichi ni chumba changu cha tatu cha siri ambacho sio rahsii kwa mtu kukijua”

“Hii nyumba yako umeitengeneza kitalamu ehee?”

“Sana”

Caro akawasha taa na nikaona makabati ya chumba yenye bunduki za kila aina.

“Kuna hizo suti hapo huwa haziingizi risasi”

“Hizi?”

“Ndio ni bulet proof, nilizipata nchini Ujerumani. Kuna tisheti zke pia ambazo nazo haziingizi risasi. Hivyo ina bidi uvae suti moja kwenye hili tikio.”

Nikatazama suti moja kisha nivua nguo na nikaijaribisha. Ni suti moja ambayo ime imenipendeza vizuri sana mwilini mwangu.

“Kaa nijarubu kukufanyia majaribio”

Caro alizungumza huku akichukua moja ya bastola na akaikoki.

“Ngoja kwanza haziingizi kweli?”

“Huniamini mume wangu?”

“Nakuamini ila?”

Caro akafyatua risasi mbili zilizo piga kifuani na sikadunda na kuanguka chini.

“Fuc** ila zina uma”

Nililalama huku nikijipapasa eneo nililo pigwa risasi hizi kwani lina uma uma kidogo.

“Pole mume wangu, hivyo ukivaa hizo ita kuwa salama zaidi”

“Nawe ina bidi uvae”

“Kwa nini?”

“Usimuamini kabisa DON”

“Nitavaa tisheti hiyo”

Nikachagua bunduki moja yenye uwezo wa hali ya juu. Nikabeba bastoka nne pampoja na magazine karibia kumi na sita kwani muda wa DON na Caro kuonaan ni saa sita usiku katika bichi hiyo. Baada ya maandalizi haya tukatoka ndani hapa huku Caro naye akiwa na bastola mbili.

“Ina bidi niwahi kufika eneo la tukio mamepa kabla yenu”

“Sawa mume wangu kuwa makini”

“Usijali”

Nikampiga denda la nguvu Caro kisha nikaondoka nyumbani kwake. Nikiwa njiani nikajipiga picha kadhaa kisha nikamtumia Jackline kwani katika kazi hii sijui kama nita rudi nikiwa hai au nime kufa.



Simu yangu ikaanza kuita na ikanifanya nisimamishe gari langu kwa maana ni Jackline ana nipigia kwa mfumo wa video call.

“Yes baby”

“Mbona ume vaa hivyo mume wangu na una silaha. Una kwenda wapi?”

“Don yupo Tanzania”

“Hapa Tanzania?”

“Ndio tena hapa Dar es Salaam. Nimejua ni eneo gani ambalo yupo. Hivyo nina kwenda kupambana naye, muambie Shabani kwamba nyinyi nyote muondoke hapo nyumbani na kuelekea nyumbani kwa Rashidi kwa zamani hadi nitakapo imaliza hii kazi”

“Ngoja ngoja nikazungumze naye sasa hivi usikate simu”

“Sawa”

Nikamuona Jackline akitoka chumbani na kushuka hadi sebelni.

“Shem kuna simu yako”

Wakatoka nje na kusimama eneo moja.

“Vipi ndugu mbona ume vaa suti tena”

“Don yupo Dar es Salama nina kwenda kumuwinda sasa hivi. Nahitaji kuimaliza hii vita usiku wa leo. Nahitaji uilinde familia nzima hadi nitakapo malia kazi hii. Nilikuwa nina shauri kwamba muende kule nyumba ya Kimara?”

“Usijali kaka hapa hapa ila hii nyumba ina handaki kibwa la kujificha ambalo lime lindwa vizuri hivyo chcohote kitakacho tokea basi nita kuwa makini kuwalinda”

“Nashukuru sana ndugu yangu.”

“Mume wangu nakuonba sana uwe makini. Tambua nina kutegemea mimi, watoto na mama”

“Usijali mke wangu. Mungu ata kuwa pamoja nami”

“Ame mume wangu”

“Sawa nina iwahi hiyo sehemu hivyo nita wapigia simu”

“Sawa kaka kuwa makini na mwenyezi Mungu akutangulie”

“Amen”

Nikakata simu na kuendelea na safari hii. Nikafika eneo la karibu na bichi walio kubaliana nika, nikalisimamisha gari langu eneo ambalo sio rahisi kwa mtu kuliona. Nikashuka ndani ya gari na nikakimbilia eneo ambalo nina weza kuyaona makutano ya DON na Caro. Hazikupita hata dakika tano nikaona gari mbili zikifika eneo hili la bichi wakashuka watu nane na wakatawanyika na kujificha kitu kilicho nifanya nistuke kidogo. Nikatoa mlio katika simu yangu na nikamtumia meseji Caro na kumuuliza kama amewaagiza watu kutangulia eneo hili.

‘Hapana’

‘Basi kuwa makini kuna watu wamegizwa’

‘Sawa baby’

Nikaiweka simu yangu mfukoni na baada saa sita juu ya alama, nikalion gari la Caro likisimama kwenye fukwe hii. Wakashuka walinzi wake wanne kisha nay eye akashuka. Baada ya muda kidogo nikaona gari mbili zikisimama mbele kidogo ya gari la Caro. Wakashuka walinzi wengine nane kisha DON naye akashuka ndani ya gari, huku akiwa katika sura yake hii bandia. Wakapeana mikono na Caro kisha wakaanza kuzungumza huku walinzi wakiwa wamegawanyika kuhakikisha ulinzi una kuwepo wa kutosha. Galfa Don akachomoa bastola yake na kumnyooshea karo usoni na ikawafanya walinzi hawa Caro na Don kunyoosheana mitutu ya bunduki. Nikaishika bunduki yangu vizuri huku nikivuta pumzi nyingi. Caro akamkabidhi Don simu yake. Akaiminya minya kisha akaipiga. Nikaitoa kidogo mfukoni na kuona amenipigia mimi kupitia simu ya Caro. Nikatamani kuipokea ila nikakausha. Simu ikaita hadi ikakatika, Don akapiga tena ila sikuhitaji kupokea kabisa. Gafla nikashuuhdia Don akimtandika Caro risasi ya kifua na Caro akaanguka chini, walinzi wake wakafanya mashambulizi ya galfa ila wakaishia kushambuliwa kwa risasi na wakaanguka chini mmoja baada ya mwengine. Walinzi walio kuwa wamejificha kwenye maeneo niliyo waona nao wakajitokeza na kuungana na Don kuingia ndani ya magari walio jia na kuanza kuyageuza kwa kasi sana na kuondoka eneo hili. Nikakimbilia hadi eneo alilo lala Caro.

“Baby”

Nilimuita Caro na akafumbua macho yake.

“Wameondoka”

Caro aliniuliza huku akinitazama machoni mwangu.

“Ndio nyanyuka na tuingie ndani ya gari.”

Nikamsaidia Caro kunyanyuka. Tukaingia ndani ya gari lake na tukaanza kuzifukuzia gari hizi kwa nyuma.

“Aisee ingekuwa sio hii tisheti ningekufa mimi”

“Ndio maana nilikuambia usimuamini Don”

“Mshenzi sana, eti ana dai nimekuambia juu ya kukutana kwetu na nimekuwa msaliti. Nahisi pale ndani kuna kifaa cha kunasa sauti kimefungwa”

“Tuta kifwatilia kesho. Endesha gari hii”

Tukapishana juu kwa juu huku gari hii ikiwa katika mwendo wa kasi. Nikashusha kioo cha pembeni taratibu kisha nikajitokea huku nikiwa nimeshika bastola mbili mkononi mwangu. Nikaanza kufyatua risasi kwa gari ya nyuma kati ya hizi nne tunazo zifukuzia. Risasi zangu zikawafanya walinzi wa Don walipo kwenye gari hii ya nyuma kuanza kujibu mashambulizi ambayo hayakuwa na amdhara kwetu. Nikapiga risasi kadhaa kwenye tairi za nyuma za gari hili na kulifanya liyumbe, likaacha barabara na kuanguka pembeni likiwa na watu wake. Zikabaki gari tatu ambazo nazo zina kwenda kwa mwendo wa kasi sana.

“Wasogelee kwa ukaribu wasikuache mke wangu”

“Sawa, gari hii bullet proof”

“Safi”

Caro akazidi kukanyaga mafuya na tukazigelea kwa ukaribu gari hizi mbili za nyuma ambazo zina ilinda gari ya mbele ya DON. Nikazirudisha bastola hizi kiunoni kisha nikachukua bunduki hii aina ya HK416. Nguvu ya bunduki hii ikanisaidia kuangusha gari la mbele yetu na likapata ajali mbaya sana kwa kugonga nguzo ya umeme hadi umeme ulipo katika eneo hili ukakatika. Nikabadilisha magazine na kulishambulia gari hili la nyuma pamoja na walinzi wake. Mashambulizi yangu mengi nina lenga kioo cha nyuma ambapo walio kaa siti za nyuma ni lazima wafe kisha nina hamia kwenye matairi na gari kuzipasua pasua vibaya tairi za magari hayo na kusababisha ajali kubwa sana. Ikabaki gari ya Don na walinzi wake wachane.

“Hiyo gari nayo haiingii risasi si kwenye tairi wala vioo”

Caro aliniambia huku tukiendelea kufukuzia gari hii.

“Nipishe kwenye siti”

Taratibu tukapishana kwenye siti.

“Hamia siti ya nyuma”

“Una taka kufanya nini?”

“Wewe hamia siti ya nyuma”

Caro akahamia siti ya nyuma.

“Funga mkanda”

Nilizungumza huku nikifunga mkanda wa siti yangu.

“Tayari baby”

Caro alizungumza huku akiwa amekaa siti ya nyuma. Nikaongeza mwendo wa gari hili na nikaanza kuligonga kwa nguvu gari la Don kwa nyuma. Dereva wa gari Don akajitahidi kuongeza mwendo ila kutokana na kuto kuwa na uzoefu wa barabara za Tanzania zenye matuta mengi ya kustukiza, ikawa ni nafasi kwangu kuendelea kuligonga gonga kwa nyuma hadi likaanza kuyumba vibaya mno. Nikazidi kukaza mguu, nikalisogelea kwa ukaribu na nikawa kama nina anza kulipita kidogo, kisha nika libamiza kwa ubavu mlango wa nyuma na kusababisha dereva kushindwa kulihimili gari lake na kujikuta akianza kuparamia kuta ndogoz ilizo jengwa pembezoni mwa barabara na mwishowe likadumbukia mtaroni. Nikafunga breki na nikashuka huku nikiwa na bundiki yangu mkononi. Kitendo cha dereva kufungua kioo ili anishambulie nikamtandika risasi ya kichwa. Nikatoa bomu la machozi mfukoni mwangu na nikalirishia ndani ya gari hii ya Don kupitia mwanya mdogo wa kioo alicho fungua dereva. Moshi ukaanza kusambaa ndani gari hili jambo ambalo najua fika hawawezi kuvumilia bomu la machozi ni lazima watoke tu. Mlango wa upande wa nyuma ukafunguliwa, akatoka mlinzi huku akikohoa.

Sikutaka kuwa na swalie mtume, nikampuga risasi kadhaa za kifua na akafa. Nikamuona DON akitoka huku mikono yake ameitanguliza mbele.

“Umeshinda Malcom umeshinda”

Don alilalama. Ili kumdhihirishia kwamba leo ni siku yake ya kufa. Nikampiga risazi za miguuni na kuvunja miguu yote miwili. Walinzi wake walipo ndani ya gari nikaawalizia kwa kuwamininia risasi zisizo na idadi.

“Baby askari wana kuja”

Caro alizungumza huku akiwa amefungua mlamgo wa siti ya nyuma.

“Bado nina mazungumzo na wewe. Caro hamia siti ya mbele endesha gari”

Nilizungumza huku nikiburuta Don hadi siti ya nyuma na nikamuingiza ndani ya gari. Nikamvua nguo zake zote na nikauchukua bastola yake huku tukiondoka eneo hili. Njia nzima Don an alia kama mtoto mdogo kwani si kwa maumivu haya makali niliyo mpatia.

“Mzee nilikuwa nina kutamani sana aisee. Yaani ushawahi kuhonga demu vitu vingi alafu akawa ana kubania uchi wake. Sasa siku ukimkamta hicho kitomb** utakacho mtembezea yeye mwenyewe ata furahi na roho yake sasa ndio leo utakavyo furahi na roho yako.”

Tukapishana na gari kadhaa za polisi zikielekea eneo la tukio kwa maan milio ya risasi ilisikika vizuri sana.

“Tuna kwenda wapi mke wangu”

“Nyumbani kwangu. Pale hakuna anaye weza kuingia”

“Sawa”

Nikatoa simu yangu mfukoni na kumpiga picha kadhaa Don. Tufika nyumbani kwa Caro, nikawa wa kwanza ksuhula ndani ya gari, kisha nikamvuta kwa nguvu DON na kumuangusha chini kama gunia la mkaa likishushwa kwenye pikipiki.

“Ngoja baby”

Caro aliungumza huku akichukua kifaa cha ugunduzi wa GPRS. Akakipitisha kuanzia kwenye unyayo wa Don hadi kichwani mwake.

“Hana GPRS”

“Ilikuwa kwenye nguo zake zile”

“Mlete huku mume wangu”

Tukamuingiza Don kwenye chumba kilichopo nje ila chini ya ardhi. Nikamkalisha Don kwenye kiti cha chuma kisha nikaifunga mikono yake pamoja na kiti hichi.

“Asiee siamini kama nimekukamata tena”

“Kaka una niua uniue ila sio kunipiga piga picha kwani hazito kusaidia chochote hata pale nitakapo kuwa nimekufa”

“Una mkumbuka rafiki yangu uliye mkta miguu na mikono. Aliniomba kitu kimoja kwamba siku nikikukamata nikukata mikono na miguu. Sasa leo nime kukamata, nahitaji kukamilisha ahadi ya rafiki yangu BRIAN”

Don macho yakamtoka huku akionyesha dhahiri kwamba ana woga.

“Mume wangu ina maana una mkata kweli?”

Caro aliniuliza huku akitazama jinsi ninavyo chukua mashine maalumu ya kukatia vitu vigumu kama kuta vyuma.”

“Ndio mke wangu”

“Mmmmm ngojan nitoke sitaki kushuhudia huo ukatili”

“Ni wewe tu mke wangu”

Caro akatoka ndani hapa na kutuacha mimi na DON.

“Umea watu wengi sana Don, mwenyewe ukajibadilisha sura ukahisi sinto kujua”

Nilizungumza huku nikisikilizia mlio wa mashine hii jinsi inayvo kwenda kwa kasi sana.

“Kwa sasa nipo tayari kukupa utajiri wangu wote. Pesa yangu yote ili uniache hai”

“Mamae zako. Pesa uliyo nipa ina nitosha. Yaani nitakula mimi, wanangu na kila mtu anaye nizunguka na haito kwisha hadi tuna kufa. Siwezi kukuacha hai tena. Tena nimeshau jambo”

Nikatoa simu yangu mfukoni na kumpigia kwa mfumo wa video call.

“Ohoo asante Mungu. Nilikuwa nina sali mume wangu ili uwe salama”

“Yeah nipo salama”

“Vipi ume fanikiwa?”

“Ndio baby”

“Kweli?”

“Yeaa”

“Uongo”

Nikageuza kamera na kumuonuyesha Jackline jinsi Don nilivyo mdhibiti kwenye kiti. Jackline akashangilia kwa furaha kubwa sana.

“Ndio yeye huyo mshenzi aliye jifanya kuingia kwenye kampuni yangu. Pumbavu kweli huyo”

“Hivi namba ya Brian ninayo?”

“Ndio ninayo mume wangu”

“Muunganishe kwenye haya mazungumzo yetu”

“Dakika moja, na nina muunganisha na Shabani pia”

“Sawa”

Ndani ya muda mfupi tukauganisha simu hizi na sote tuna onana sasa.

“Kaka za masiku?”

“Salama ndugu yangu una endeleaje?”

“Mii nipo salama kabisa. Umenitenga?”

“Ni kweli nimekutenga kwa sababu moja tu”

“Ipi?”

“Niliohofia kuto itimiza ahadi yako, ya kumpata yule bwege. Leo hii nimekamata sasa niambie nimfanye nini?”

Nikaigeuzia kamera kwa Don.

“Mshenzi huyo, mpumbavu alinitesa, natamani kuwa hako kaka. Natamani kumfanya kitu ambacho angejutia hadi kufa kwake.”

Brian alizungumza kwa hasira kali sana.

“Nilijua tu ipo siku yako wewe mbwa uta kamatwa”

Brian alizungumza kwa uchungu sana hadi machozi yakaanza kumwagika.

“Najua haya mazungumzo sio salama yana weza kurekodiwa. Nimewapigia ili kuwaoyesha kwamba ile kazi yangu ya kipindi kirefu sasa ina fikia mwisho. Nime mpata huyu mshenzi”

“Kaka natamani umfanye alicho nifanya mimi”

“Usijali nita muondoa mikono na miguu”

“Nashukuru kaka”

“Asanteni tuta wasiliana baadae”

Nikakata simu hii na kuingiza mfukoni.

“Huyu malaya wako ana jua kwamba una mke?”

“Ndio ana jua nina mke wa ndoa na familia. Na sio malaya”

“Nisikilize Rashidi, hata ukiniua mimi ila huto kwenda kua kile kitu ambacho nimekipandikiza kwa mke wako”

Nikakaa kimya kidogo kisha nikaizima mashine hii.

“Kitu gani umekipandikiza kwa mke wangu?”

“Niue huna haja ya kukijua”

“Nimekuambia nini umeopandikiza kwa mke wangu”

“Niueeeee”

Don alizungumza kwa sauti ya juu na kunifanya nimpiga risasi nne za paja la mguu wa kulia. Nikakinyanyua kichwa chake kuu na kumuingizia bustola hii mdomoni mwake.

“Niambie umepandikiza nini kwa mke wangu?”

Machozi ya maumivu yakaendelea kumwagika DON machoni mwake. Ujanja wote ume muisha.

“Narudia kwa mara ya mwisho ni nini umepandikiza kwa mke wangu”

“Na….s….e.ma”

Nikaichomoa bastola hii huku nikihema kwa hasira sana.

“Zungumza usinitumbulie macho”

“Hahaahahahahahaa……”

Don alicheka kwa kejeli na kunifanya niichukue mashine hii, nikaiwasha na bila ya huruma, nikaipitisha juu ya paja lakela mguu wa kushoto na taratibu ukaanza kukata paja hili huku damu nyungi zikinirukia usoni ila sikutaka kulijali hili. Haikuwa kazi ngumu kutenganisha paja la Don na kiwiliwili cha mwili wake. Kwa maumivu makali Don akazimia.

Roho ya kishetani na ukatili imenivaa mwilini mwangu na hata hili ninalo lifanya sijuitii kabisa. Caro akaingia ndani hapa akashangaa kuniona nimeushika mguu wa Don huku damu zikiwa zimetapakaa.

“Mungu wangu. Mume wangu ume mkata kweli”

“Kaa nje”

Nilizungumza kwa sauti iliyo jaa mikwaruzo mingi itokanayo na hasira inayo endelea kunitafuna. Caro akanitazama kwa muda kisha akatoka ndani hapa bila ya kuniongelesha chochote. Nikafungua moja ya kabati la dawa na nikasoma soma dawa hizi, nikaona dawa ambayo ina mzindua mtu aliye zimia. Nikachukua kichupa hichi, nikakitingisha kicha nikakifungua, moshi ulio toka ndani ya kichupa hichi ukamfanya DON kuzinduka, akautazama mguu wake na akapiga yowe la woga.

“Huu ni mguu wako. Nina weza kuukata mguu wako wa pili niambie ni kitu gani ulicho kipandikiza ndani ya mke wangu”

Nilizidi kukoroma na kumfanya DON kutetemeka mwili mzima kwani akifanya masihara nina mkata mguu wa pili bila ya kutumia ganzi na mateso haya yata muua taratibu kitu ambacho nina imani hato penda kukiona kina tokea kwene maisha yake kwani ni hari kumpiga risasi ya kichwa na akafa haraka kuliko hivi kumkata kata vipande vipande tena akiwa bado hai.



“Ni…ni….ni;….”

“Nini ongea?”

Don machozi yakaendelea kumwagika hadi makamasi yakaanza kumwagika.

“Ka…ti…ka vi..nywaji vyake vinavyo ingia nchini Mexco tumepandikiza virusi vya H.I.V hivyo maelfu ya watu wanao kuywa wana pata maambukizi hayo”

Nikastuka sana kwa unyama ambao DON ana ufanya kwa raia ambao hawana hatia. Nikatoa simu yangu mfukoni na kumrekodi.

“Rudia umesema”

“Tumepandikiza virusi vya ukimwi kwenye vinywaji vya mke wako hivyo wanao kunywa wana pata maambukiz na virusi hivyo vina nguvu kubwa sana ambayo vita kwenda kuua maelfu ya watu ndani ya mwaka mmoja ujao”

“Kwa nini una waua watu wako mwenyewe”

“Una hisi hiyo kesi nita ipata mimi, ata ipata mke wako na una jua nini kitakacho kwenda kumpata ni kuhukumia hukumu ya kifo tena cha kunyongwa na mazi zake zita binafsishwa”

Don alizungumza kwa dharua na kejeli. Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama usoni mwake. Nikaihifadhi simu hii, kisha nikachomoa bastola yangu na kumuangalia usoni mwake.

“Una dakika moja ya kutubu”

“Sina haja ya kutubu kama una niua niuue, ila kumbuka kwamba mimi ndio niliye kufanya kuonekana mtu. Mimi ndio niliye kitoa gerezani na kukufanya mpambanaji. Mimi ndio niliye nikufanya ukawa mtu kati ya watu”

“Na wewe ndio uliye nifanya kuwa gaidi kati ya magaidi.”

Nikampiga risasi ya bega la kulia Don na akazidi kulia kwa maumivu. Nikampiga risasi ya mkono wake wa kushoto na kumfanya azidi kupata maumivu.

“Kanisalimie rafiki yako huko kuzimu”

“Ngoja kwanza”

Don alizungumza na kunifanya niachane na swala la kumuua.

“Kwenye maisha yangu yote nimekuwa ni mtu wa kutafuta pesa nyingi, ndio mana nina miliki pesa nyingi. Nilikuwa nina uwezo wa kukuaa wewe na familia yako. Nilikuwa nina weza kukumaliza muda wowote kama vile kidole kinayvo weza kumgandamiza sisimizi kwenye ukuta. Una jua kwa nini nilikuacha hai?”

Don alizungumza kwa maumivu makali sana anayo pitia.

“Ehee?”

“Kwa sababu wewe ni mwanangu.”

Nikatabasamu kwa maana anacho kizungumza Don ni upuuzi.

“Kama huamini chukua damu yangu na yako kisha nenda kapime DNA, ukikuta ni kweli uta elewa”

“Una nipotezea muda”

Nilizungumza huku nikimnyooshea bastola ya kichwa.

"Kaka huniamini kama mimi ni baba yako mzazi, kamuulize Aisha”

“Aisha ndio nani?”

Don akanitazama usoni mwangu kwa sekunde kadhaa.

“Ina mama hujui jina la mama yako”

“Mama yangu?”

“Ndio hujui jina la mama yako.”

“Aise mam yangu haitwi Aisha”

“Anaitwa Aisha Ngombali, baba na mama yake walikuwa ni waalimu wa shule inayo itwa Mbwade. Kwao alizaliwa yeye peke yake. Baba yake na mama yake walifariki kwa ajali ya pikipiki kwa kundumbukia kwenye maporomoko yaliyopo kwenye mlima Chamanyani, kipindi hicho mama yako alikuwa na umri wa miaka kumi na nane. Nilikitana naye Mererani nilipo kuwa nina simamia migodi yangu. Kipindi hicho nilikuwa mwembaba, sikuwa menen kama hivi na mimi ndio nilimtoa bikra mama yako na katika mechi yetu ya kwanza mama yako alishika ujauzito na kutokana na migogoro iliyo tokea pale migodini dhini yake na mke wangu wa kwanza alitoroka na mimba yangu. Nilikaa Mererani kwa mwaka mzima nikiamini kwamba ata rudi ila hakurudi na ndipo amua kuondoka na kurudi nchini Marekani na nilijibadilisha sura na kuwa na ile sura yangu ya awali uliyo nikuta nayo. Nilifanya biashara ya madawa ya kulevya ili niwe na pesa nyingi sana. Ila niliendelea kumtafuta mama yako bila ya mafanikio na nikaamua kusamehe. Sijui ni kwa nini hakunikumbuka siku nilipo kutana naye Marekani. Shida zilimfanya aonekana mzee kabla ya umri wake wa kuwa mzee. Ila sasa hivi amekuwa kigori. Nenda kamuulize Brian Pinda ni nani alafu rudi hapa uje kuniau”

Nikahisi nguvu zikiniisha, kusema ukweli hadi leo hii simfahamu baba yangu kabisa. Na kila nilivyo kuwa nikimuuliza mama yangu alinitajia jina la Pinda n ahata nilipo muuliza historia ya maisha ya kwao hakuweza kunieleza kwa kina.

“Nenda kamuulize, ume fanana sana na mama yako ndio maana ni ngumu sana kumpata baba yako”

Maneno ya Don yakazidi kuninyong’onyeza. Nikaichomeka bastola yangu kiunoni, nikatamani kumpigia simu mama ila nikajikuta nikishindwa. Damu zinazo endelea kumwagika Don zina weza kumpelekea kifo chake muda wowote kuanzia sasa kwani eneo hili zima limepatakaa damu. Nikampigia simu Caro na akaja eneo hili.

“Mpigie simu daktari unaye mjua”

Nilizungumza huku nikibabaika sana.

“Wa nini?””

“Mpigie daktari simu yoyote aje kumuhudumia Don”

“Nini, una hisi ana weza kupona?”

“Wewe mtafute”

“Usijiangaishe mwanangu”

“Mwanangu!!?”

Caro aliuliza kwa mshangao.

“Siwezi pona nita kufa na siwezi kuishi kilema usigangaike kunishuhulikia. Kabla ya kumuuliza mama yako chukua damu yangu unayo mwagika, kaipime DNA, ukipata uhakika uta muuliza mama yako vizuri”

“Baby mbona sielewi”

“Nitafutie kichupa”

Caro akafungua kabati moja na akatoa kichupa kisicho na kitu, nikakinga matone ya damu yanayo toka kwa kwenye mguu wa Don nilio ukata kwa mashine ya kukatia vitu vigumu.

“Ja…..j….mbo la mwiho…..”

Don alizunguzma kwa sauti ya kukata kata huku dalili zikionyesha dhairi kwamba ana karibia kukata roho.

“Na…..na….ne…nda Morogo…ro kw…enye ile….e nyumba yangu. Katik…a chumba change nilicho kuwa nina lala….kuna picha ukutani. Ito…e hiyo….picha uta ona mlango wa shelf….nama yake ya siri ni….674326758. Fungua u…ta kuta urith…thi….wako na….we.eee.. ndio mridhi…..i wa….ma…li….zangu…..uuu”

Don akainamisha kichwa chini nikamsogelea kwa haraka nikaweka vidole kifuani mwa Don na mapigo yake ya moyo yamesimama, jambo lililo nifanya nizidi kuchanganyikiwa.

“Hei hei Rasidi usichanganyikiwe. Tulia tupime kwanza hii damu kisha mengine yata fwata. Huwezi muamini mtu kwa maneno tu.”

“Eti ehee?”

“Ndio na isitoshe watu kama Don wana trick nyingi za kudananya mtu. Hivyo usichananyikiwe mume wangu”

“Ila kweli?”

“Ndio mume wangu ana weza kukushawishi hapa na akapotea na akikukamata wewe wakati mwengine ata kuua”

Nikapata ujasiri wa hali ya juu. Nikachomoa bastola kiunoni na kupiga Don risasi karibia sita za kifuani mwake na mbili nikazimalizia kichwani na akakata roho. Nikavua nguo zangu zote na nikatoka ndani hapa nikiwa na boksa tu. Moja kwa moja nikapitiliza bafuni huku nikiwa na kichupa chenye damu ya DON.

“Baby”

Caro alizungumza huku akifungua mlango wa bafuni hapa. Nikamtazama Caro huku nikiwa nimekaa sakafuni na maji ya bomba la mvua yakiendelea kunimwagikia mwilini mwangu.

“Honey”

“Mmmm”

“Usiwaze sana mume wangu, mimi nina imani kwamba Don ana kuongopea”

“Ikiwa haniongopei je mikobo yangu itakuwa ime muua baba yangu mwenyewe?”

“Nisikilize mume wangu. Ulicho kifanya ni haki kwani Don amesababisha mauji ya wengi sana. Je kama leo ningeku kuwa nimevaa bullet proof sasa hivi si ningekuwa nimesha kufa na angekuwa ameniua.”

Nikamtazama Caro machoni mwake kwa sekunde kadhaa kisha nikatazama kichupa hichi chenye damu ya Don.

“Nihitaji unitafutie dokta akataye pima DNA yangu na ya Don kisha nahitaji kupata majibu usiku huu huu?”

“Vipimo vya DNA huchukua muda sio kama vipimo vya HIV au Malaria vya hapo kwa hapo. Hivyo ita tubidi tusubirie”

“Nahitaji twende sasa hivi”

Nikaoga haraka haraka kisha nikavaa nguo zangu nilizo jia hapa nyumbani kwa Caro na tukaelekea hospitali ya Muhimbili huku sasa hivi ikiwa ni saa kumi na moja asubuhi. Tukaelekea kwa daktari ambayo Caro ana mfahamu na tukampa jukumu la kupima damu yangu na damu ya Don. Akatuomba turudi hospitalini hapa baada ya siku mbili.

“Nipatie hicho kichupa cha damu”

Nilimuomba dokta.

“Kwa nini ndugu?”

“Nusu ya damu pia nyingine ninaiomba”

Nilizungumza kwa msisitizo na dokta hakuwa na kipingamizi. Tukaondoka hospitali hii ya Muhimbili na tuka elekea Agakhan. Nikamkabidhi dokta kichupa hichi cha damu naye nikampa maelekezo ya kunipima DNA, kisha tukaanza safari ya kurudi nyumbani kwa Caro.

“Maiti ya Don tutaifanya nini?”

“Tuichome sindao ya kuikausha tu asioze hadi hadi majibu halisi yatoke”

“Sawa mume wangu”

Tukafika nyumbani kwa Caro akanipa kichupa cha dawa ya kukausha maiti. Nikamchoma sindano nne Don za dawa hii. Kisha tukashirikiana kwa pamoja kusafisha chumba hichi huku mikononi tukiwa tume vaa gloves.

“Saa sita ina bidi nielekee ikulu kwenye msiba”

“Sawa nita elekea kwangu, kwani mke wangu na familia yangu wapo chini Tanzania”

“Mbona hukuniambia?”

“Saa ngapi ningekuambia”

“Natamani kuwaona”

“Uta muona Shamsa msibani kwani ata kuja kwenye msiba huo”

“Sawa mume wangu”

Tukahakikisha kwamba kili kitu kipo sawa. Tukafungulia AC ya chumba hichi hadi mwisho ili ubaridi uwe mkali katika chumba hichi. Baada ya kuoga kwa mara nyingine tukaondoka nyumbani hapa na tukapitia katika eneo nilipo lisimamisha gari langu. Nikaingi ndani ya gari na kurudi nyumbani kwangu huku Caro akielekea ikulu. Jackline akanipokea kwa furaha huku akinikumbatia kwa furaha sana.

“Hongera sana mume wangu”

“Nashukuru mke wangu”

“Amekufa kweli?”

Nikamuonyesha picha nizlizo mpiga DON mara baada ya kumchoma sindano ya kuukausha mwili wake.

“Aise huyu mpuuzi wametusumbua sana”

“Kazi imekwisha ila kama vile haijakwisha”

“Una maanisha nini”

“Vinywaji vinayo kwenda Mexico, vina zalishwa moja kwa moja Ufaransa au Mexico?”

“Kuna kiwanda changu Mexico ambacho ndio kina zalisha vinywaji vinavyo sambazwa huko Mexico”

“Una weza kusimamisha uzalishaji?”

“Mmmmm kwa nini mume wangu”

“Nahitaji uzalishaji usimamishwe”

“Kuna tatizo gani mume wangu?”

Nikamuwekea Jackline video hii. Akaitazama macho yakamatoka.

“Mungu wangu”

“Ndio maana nakuambia kiwanda kifungwe kwa muda”

“Ngoja mume wangu”

Jackline alizungumza huku jasho likimwagika usoni mwake.

“Kwa nini Don amekuwa katili kiasi hichi”

“No usi panic”

“Sasa mume wangu si watu wengi watakuwa wamekufa”

“Ina bidi tuzifanyie vipimo kabla ya kupanic hivyo mke wangu. Tuliza akili, mpigie mkemia wa Mexico unaye mfahamu”

“Ngoja”

Jacklien akachukua simu yake na akampigia simu mkemia wa kiwanda chake. Akampa maagizio ya kupima vinywaji vilivyo toka mwezi mmojua ulio pita na mwezi huu na akatuomba tusubiri majibu baada ya masaa mwili.

“Mama sijamuona ameenda wapi?”

“Ametoka na wajukuu wake. Amekwenda kuwatembeza”

“Ulimuambia nime mkamata Don?”

“Hapana”

“Sawa”

“Shabani je?”

“Shabani pia yupo pamoja nao”

“Sawa sawa”

Baada ya lisaa moja mkemia akatupigia simu.

“Ndi”

“Mkuu vinywaji vipo salama kabisa na havina tatizo lolote”

“Kweli?”

“Ndio na uzalishaji ni bora na wananchi wengi wana visifia. Tumepima kila na tumedhibitisha ni salama kwa matumizi ya binadamu”

“Nashukuru sana Pablo”

“Karibu sana mkuu”

Jacklinie akanikumbatia kwa furaha, huku machozi yakimwagika.

‘Kwa nini Don alinidanganya?’

Nilijiuliza huku nikiendelea kumkumbatia mke wangu.

“Mungu ni mwema kwa kweli”

“Yaa ni kweli mke wangu. Kuna jambo moja nahitaji kukuambia”

“Jambo gani mume wangu?”

Jackline alizungumza huku akiniachia.

“Ila naomba likikamilika nikuambie”

“Kwa nini usiniambie sasa hivi mume wangu”

“Naomba univumilie kwenye hilo”

“Sawa mume wangu hakuna tatizo”

Baada ya siku mbili dokta wa hospitali ya Akaghan akanipigia simu. Kutokan nilikwenda na Caro ikabidi nimuombe anisindikize kwenda kupokea majibu haya japo imesali siku moja kabla ya mazishi ya kaka yake. Tukafika Agakhan na moja kwa moja tukaelekea katika chumba cha daktari.

“Karibuni sana”

“Tuna shukuru”

“Nyinyi ni mke na mume?”

“Ndio”

Niliwahi kujibu.

“Hii damu ni ya nani”

“Mzee wangu”

“Okay vipimo vinaonyesha kwamba damu zenu zina endana.”

Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi sana.

“Ina maana…..”

“Huyu mwenye hii damu ni ndugu yako”

“Umepima vizuri dokta?”

“Ndio vizuri na vipimo vyetu huwa hazidanganyi kabisa”

Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama daktari huyu. Simu ya Caro ikaita, akaipokea.

“Sawa”

“Haya tutapita hapo”

Akakata simu. Daktari akatupatia karatasi yenye majibu na tukajiridhisha, tukaondoka hospitalini hapa juku mwili mzima ukiwa umekufa ganzi. Kusema kweli katika kitu ambacho sikukitarajia kwenye maisha yangu ni hichi.

“Dokta wa Muhimbili ana sema majibu tayari”

“Twende”

Caro akaendesha gari hadi Muhimbili na tukaelekea kwa daktari.

“Majibu yapo vipi?”

Niliuliza hata ya salamu.

“Habari zenu”

“Nzuri tu dokta, msamehe mume wangu kwani amegadhibika huko tulipo toka”

“Hakuna shaka na ana onekana. Ahaa majibu yametoka na vipimo vinaonyesha kwamba damu zina endana”

Nikasimama na kuanza kutembea kuelekea mlangoni huku kichwa changu kikitawaliwa na mawazo mengi sana. Nikaingai ndani ya gari na baada ya dakika tano Caro akaingia huku akiwa na bahasha yenye matujibu.

“Nahitaji unipeleke kwenye fukwe yoyote, nataka kuwa mwenyewe”

“Sawa mume wangu”

Caro akanifikisha kwenye moja ya fukwe iliyo jitenga zaidi.

“Utakapo nihitaji utaniambia”

“Naomba hizo bahasha”

Caro akanipatia bahasha hizi na akaondoka. Machozi yakanimwagika huku nikisoma majibu haya.

“Kwa nini hakuniambia kwamba yeye ni baba yangu?”

Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na uchungu mwingi sana. Nikapiga yowe moja jali huku nikihisi maumivu makali ya moyo wangu. Nikajaribu kumfikiria mama yangu kwa namna moja ama nyingine ana makosa. Nikatoa simu yangu mfukoni na kumpigia Jackline.

“Honey”

“Njoo nilipo”

“Mbona una zungumza kwa sauti nzito. Una tatizo gani?”

“Njoo nilipo, nina washa location ya simu yangu. Itrack uje peke yako na usimuambie mtu”

“Sawa nina kuja mume wangu”

Nikakata simu na kuwasha location ambayo ita kuwa rahisi kwa Jackline kufahamu ni wapi nilipo. Baada ya dakika kumi na tano akafika eneo hili. Akanikimbilia hadi sehemu nilipo.

“Vipi baby una tatizo gani?”

“Una hisi mimi ni mwanaume sahihi kwako?”

“Ndio mume wangu, ndio maana leo hii nipo hapa na nipo na wewe”

“Una hisi mimi ni mtu wa aina gani?”

“Mwanaume jasiri aliye toka mavumbili hadi kwenye kiti cha ufalme. Niambie baba Shamsa una tatizo gani?”

Nikamkabidhi bahasha hizi Jackline akafungua bahasha ya ndani akasoma karatasi hii kisha akanitazama usoni kwa macho yaliyo jaa maswali mengi. Akafungua bahasha ya pili na akaisoma.

“DNA test za nani hizi mume wangu?”

“Hili ndio lile jambo nililo kuambia nita kuambia”

“Sawa ni DNA za nani na nani?”

“Yangu na DON”

“Nashindwa kukuelewa ni ya nani?”

“Yangu mimi na DON”

Nilizungumza kwa ukali huku machozi yakinimwagika machoni mwangu.

“Kivipi na imekuwaje hadi DNA zenu ziendane?”

“Kabla ya kumuu alinieleza hilo jambo kwamba yeye ni baba yangu mzazi. Na kama nina mbishia basi nikapime DNA na hayo ndio majibua yake”

“Ohoo Mungu mama ana lijua hili?”

“Sijui”

“Sasa ita kuwaje mume wangu”

“Nahitaji kumsikia mama, nataka kujua mama ni kwa nini alifanya hili jambo. Miaka yote nina kazi ya kupambana na mtu ambaye ni baba yangu kwa nini. Isitoshe nimekuja kumuua, mimi kwa mikono yangu kwa nini”

Nilizungumza kwa uchungu sana huku machozi yakinimwagika. Taratibu Jackline akanikumbatia na nikaendelea ulia kwa uchungu sana kwani hakuna kitu kinacho umiza kama kumua mzazi wako tena una fahamu ni mzazi wako dakika za mwisho za uhai wake.


Jackline akandelea kunikumbatia kwa nguvu huku machozi yakiendelea kunimwagika.

“Ina bidi tukazungumze na mama tufahamu ukweli zaidi mume wangu usilie”

Tukaka ufukweni hapa kwa lisaa moja zaidi kisha tukarudi nyumbani. Unyonge wangu dhauri ikawaashiria watu kwamba nina tatizo. Sikuhitaji kuzungumza na yoyote na nikaingia chumbani kwangu huku nikiongoza na mke wangu. Mlango ukagogwa na Jackline akamruhusu anaye gonga kuingia ndani. Mama akaingia ndani hapa.

“Vipi una umwa?”

Mama aliniuliza huku akinitazama machoni mwangu.”

“Nina kutengenezea kahawa mume wangu”

Jackline akatoka ndani hapa na akaniacha na mama.

“Vipi mbona macho mekendu hivyo, una umwa?”

Mama alizungumza huku akiniweka mkono shingoni..

“Mama nahitaji unieleze ukweli”

“Ukweli wa nini?”

“Wa maisha yangu na baba yangu”

“Ahaa hizi sasa mada za nini, ni maisha ya zamania ambayo kwa sasa sitaki kuyakumbuka wala kuyasimulia kwa maana baba yako hakuwahi kuihudumia mimba yako, kuzaliwa kwako na hadi umekuwa mtu mzima, hajawahi kuitoa hata shilingi mia mia nyekundu”

Maneno haya ya mama sio mara ya kwanza kuniambia na amekuwa ni mtu wa kupotezea mada hii.

“Isitoshe baba yako alisha fariki kipindi kirefu na wala sijui kaburi lake lipo wapi. Laiti kama ningefahamu ninegkuambia twende tukalione kaburi lake”

Nikamtazama mama kwa macho makali hadi akajistukizia.

“Tuachane na hizo mada, una nikumbusha machungu mengi”

“Yapi?”

Mama akanitazama kwa mshangao kwa maana nimemuuliza kwa hasira.

“Una nini wewe?”

“Nina taka kumjua baba yangu ni nani sitaki kusikia stori nyingi. Kwa nini umekuwa ukinificha historia yako ya ukweli hadi jina unalo litumia sio lako kwa nini mama?”

Nilifoka haku machozi yakianza kunimwagika.

“Weee mtoto umerogwa au, kumbuka una zungumza na mama yako, niliye kuweka tumboni miezi tisa”

“Haijalishi ila kwenye kuhitaji kukujua wewe ni haki yangu ya msingi kama mwanao. Niambie Aisha Ngombali ndio nani?”

Mama akastuka sana kwani jina lake sio hilo.

“Usinitumbulie macho niambie jina la Aisha Ngombali ndio nani?”

“Nani amekuambi?”

“Hakuna haja ya kuniambia nani amekuambia, nijibu Aisha Ngombali ndio nani?”

Mama akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akapiga hatua hadi kwenye friji ndogo iliyopo chumbani hapa. Akafungua na akatoa chupa ya wyne, akamimina katika glasi kisha akapiga hatua hadi kitandani. Akaka huku akinitazama. Akanywa wyne hiyo kidogo kisha akajikoholesha kidogo.

“Una hitaji kujua ukweli?”

“Ndio”

“Aisha Ngombali ni jina langu nililo pewa na wazari wangu”

“Mwanaisha Juma limetokea wapi?”

“Nilijipa mwenyewe?”

“Kwa nini miaka yote umekaa una nificha jina lako halisi…..?”

“Hapakuwa na haja yoyote ya mimi kukueleza jina langu halisi. Kwani halito kusaidia chochote. Maisha yangu ya nyuma yaliharibika baada ya baba yangu na mama yangu kufariki kwa ajali mkoni Morogoro ambapo ndipo nilipo zaliwa. Sikuona haja ya kuishi na mshangazo walio kuwa na roho mbaya. Roho za kikatili, ndipo nilipo amua kutoroka myumbani na kuwaachia mali zote ambazo wazazi wangu walikuwa wana miliki.

“Ulikwenda wapi?”

“Nilitimkia Merelani ambapo nilipo fika kule nilipata ajira kwenye kibanda kimoja nikiwa kama mama Ntilie”

“Ndipo ulipo kutana na Brian Pinda?”

Mama akastuka kidogo huku akinitazama kwa mshanga.

“Umekutana naye wapi huyo mtu?”

“Nijibu?”

“Ndio, nilikuta na Brian Pinda alikuwa ni Mmarekani, alinishawishi na akanipatia ujauzito ambao mke wake aliweza kufahmu na nikaamua kukimbia na kuja kuishi jijini Dar es Salama”

“Huyo Brian Pinda ukimuona una weza kumkumbuka?”

“Siwezi kuisahau ile sura ya yule mwanaume kwani kuna vitu vingi sana umerithi kwake”

“Kama”

Mama akamalizia wyne yake huku akinitazama.

“Macho na sura zenu zina endana kwa mbali”

“Kwa nini ulikimbia?”

“Mke wake alitishia kuitoa mimba yangu, isitoshe walikuwa ni watu wenye pesa na wanao miliki mgodi. Kwa kipindi kile Merelani maswala ya ujambazi na uuaji yalitapakaa sana. Niliogopa kuuwawa, bosi aliye kuwa ameniajiri kwenye kibanda chake alinisaidia kunitorosha na nikaondoka kabisa mkoani hapo”

Moyo wangu ukazidi kujawa na maumivu kwani alicho niadithia Don ndio hichi anacho niadithia mama.

“Niliamua kuilea mimba yangu mimi mwenyewe, na kipindi hichi ndipo nilipo kutana na mama Chausiku kwenye kiwanda kimoja cha kutengeneza Sababu. Mwenzangu alikuwa na kwake hivyo niliishi naye kwenye chumba kimoja hadi nikapata chumba changu. Nililea mimba yangu kwa shida na tabu, kitu ambacho kilinifanya niwachukie wanaume kwa kipindi chote cha maisha yangu. Hadi miaka ya hivi karibuni nilipo amua kuufungua moyo wangu kwa baba Jackline”

Mama alizungumza kwa sauti ya upole huku akinitazama machoni mwangu.

“Niambie ni wapi alipo Brian?”

Swali la mama likanifanya niendelee kumwagikwa na machozi.

Nikamuonyesha mama bahasha zenye majibu ya DNA. Mama akaanza kusoma karatasi moja baada ya nyingine.

“Hii DNA ni yako na nani?”

“Na Brian”

“Aisee wewe mtoto msiri sana yaani umekuna na baba yako na ukapima naye DNA bila hata kunijuza. Ehee niambie yupo wapi?”

“Kuzimu”

“Nini?”

“Kwa sasa yupo kuzimu kwa maana sikumpa hata nafasi ya yeye kutubu”

“Mmmm sijakuelewa. Ina mana kwamba ume muua baba yako?”

“Ndio kwa sasabu sikujua kama ni baba yangu na alikuwa ni miomgoni mwa adui zangu.”

Mama macho yakamtoka kwa mshangao.

“Niambie ni nani?”

“DON ndio Brian Pinda?”

Mama akapigwa na bumbuwazi moja takatifu. Glasi ya wyne aliyo ishika mkononi mwake ikamponyoka na ikaanguka chini na kupasuka vipande vipande. Akajarubu kusimama ila akashindwa na kujikuta akihema kwa shinda.

“Mama”

Mapigo ya moyo ya mama yakazidi kuenda kasi hadi macho yakaanza kumtoka kwa kubanwa.

“Jack…..Jack”

Niliita kwa nguvu huku nikianza kumpatia mama huduma ya kwanza ya kumlaza kitandani.

“Mama mama”

Niliita. Jackline akaingia ndani hapa kwa kasi.

“Ohoo Mungu wangu ni pumu. Sheila kimbia ndani mletee bibi kidude cha kupumulia”

Sheila ambaye alikuwa anaingia mlangoni hapa akageuza na kukimbilia chumbani kwa bibi yake. Baada ya dakika kama mbili akarudi akiwa na kifaa cha kumsaidia mtu mwenye pumu kupumua. Jackline akakiweka mdomoni mwa mama na akakiminya na kumfanya mama kupumua kwa nguvu na kifua chake kuanza kushuka taratibu kwani kilikuwa kama kimetanuka. Baada ya muda kidogo hali ya mama ikakaa sawa.

“Tukupeleke hospitali?”

Nilimuuliza mama.

“Hapana”

“Kwa nini sana?”

“Niacheni peke yangu”

Tukatoka ndani hapa.

“Mama ameanza lini kushikwa na pumu?”

“Mwaka wa pili sasa huu, na dokta alimkataza asiwe ana tumi wyne nyekundu. Sasa sijui imekuwaje leo amekunywa”

“Hajapatiwa matibabu ya kupona kabisa?”

“Ina kwisha ila akifwata baadhi ya masharti. Vipi umeongea naye?”

“Ndio na alicho nieleza DON ndio alicho nieleza mama”

“Mungu wangu kwa hiyo?”

“Nahisi kuchanganyikiwa sasa”

“Usichanganyikiwe mume wangu. Kwa sababu umefanya kwa kuto kujua”

“Una jua Don alikuwa na uwezo wa kukuua wewe na wanangu na hata mimi alikuwa na uwezo wa kunia sema lilicho kuwa kinanifanya niendelee kuwa hai ni hii siri aliyo kuwa ameiweka moyoni mwake”

“Sasa ni kwa nini hakuambia mapema?”

“Sijui”

“Sasa ita kuwaje juu ya maiti yake?”

“Sijui ila nahitaji usiku tuelekee Morogoro ilipo nyumba yake”

“Leo?”

“Ndio”

“Sawa mume wangu si si mbali sana?”

“Ndio sio mbali sana”

“Vipi kaka salama?”

Shabani aliniuliza baada ya kufika eneo hili nipo kaa na Jackline.

“Yaa nipo vizuri”

“Niwalete juisi?”

“Mimi niletee kahawa mke wangu”

“Shem na wewe?”

“Niletee juisi ile uliyo tengeneza jana ni tamu sana”

“Hahaaha sawa shem”

Jackline akaondoka eneo hili.

“Aiase ekaka hongera sana. Yaani hai umemkamata Don sio jambo la kawaida”

“Yaani kumkamata ilikuwa habari nzuri ila kumuua imekuwa habari mbaya”

“Una maanisha nini ndugu yangu?”

“Don ndio baba yangu mzazi”

“Ehee!!?”

Shabani alishangaa sna ahuku akinitazama.

“Ndio”

“Acha utani itakuwaje awe baba yako mzazi mtu katili kama yeye?”

“Kipindi nilipo kuwa nina mpatia mateso akanieleza hilo, sikumuamini, nikamuua na kuchukua damu yake nikaenda kupima DNA. Zimefanana kabisa”

“Mmmmm”

“Yaani amenielezea historia ya nyuma ya mama, nimekuja kumuhoji mama hapo naye akanieleza kile alicho nieleza Don”

“Kwa hiyo bi mkubwa ana jua Don kwamba ndio baba yako sasa kwa nini asiseme kipindi chote hicho?”

“Ishu ni kwamba ile sura tunayo muona nayo Don sasa hivi sio sura yake halisi, yaani alipo kuwa na mama alikuwa na sura halisi ambayo ina endana na mimi. Alipo rudi Marekani akabadilisha na kuwa na ile sura yakle ya awali. Baada ya mikiki mikiki akabadili tena na akawa na sura hiyo ya Frenandes Philipe”

“Aisee”

“Kwa hiyo ni ngumu kwa mama kumjua. Na kitu ambacho kilikuwa kina nipa maswahili ni kwamba kwa nini Don ana isogelea karibu familia yangu na ana shindwa kuiua moja kwa moja. Kuna kipindi alimteka Jackline nchini Somalia, ila hakumuua hadi nikamuokoa. Kuna kipindi alikwenda nyumbani kwa Jackline ila hakuidhuru familia yangu. Pia hapa juzi alinitekea nikiwa Madagascar ila hakuniua ikiwa mimi ni mtu na adui yake. Laiti ingekuwa ni mimi ningefanya kama nilivyo mfanya”

“Aisee sasa ina kuwaje kwa maana si kwa habari hii kwa maana ni nzito”

“Tena sana ndugu yangu. Nimekuwa ni mtu wa mawazo, una mjua baba dakika za mwisho ikiwa umesha mfanyia ukatili”

“Sasa hapa ndio nimenza kuelewa maana ya bi mkubwa anavyo tusisitizia kama tuna watoto wa nje ya ndoa huko tuwalete wajulikane”

“Umeona ehee. Nahihitaji utusindikize Morogoro mida kama ya saa mbili hivi usiku”

“Kuna nini Morogoro?”

“Naelekea nyumbani kwa Don ameniambia kuna urithi wangu nahitaji kwenda kuuona”

“Sawa hivi umetambua kwamba kesho jamaa ana zikwa?”

“Yaa nimetambua”

“Uta kwenda?”

“Nitampeleka Shamsa kwa maana ni haki yake kuonana na mama yake”

“Sawa, tuna ondoka na gari ipi?”

“Yoyote poa basi ngoja niandae mazingira.”

“Kwani zina itilafu”

“No mzingira kwa mke wangu, kidogo tumepishana bwana”

“Imekuwaje?”

“Bi mkubwa wako alinisisitizia sana niweze kumuambia mke wangu kama nina mtoto wa nje. Sasa nikauchukua ule ushauri mama na kwenda kumueleza ukweli mke wangu juu ya mtoto huyo hivyo toka jana nimenuniwa mwenzako. Akiwa na watu ana ongea kwa furaha sana ila tukiwa wawili ni shida na jana huwezi amini nimelala kwenye kochi”

“Weee”

“Yaa nimelala kwenye kochi hataki hata nipande kitandani”

“Hembu kamuite asituletee za kuleta bwana”

“Utazungunmza naye?”

“Ndio, watu tuna mambo ya msingi ya kufanya una hisi akikuchanganya akili yako sasa hivi mambo yata kwenda ikiwa wewe ndio master plan ninaye kutegemea”

“Umeona ehee?”

“Ndio hivyo”

Shabani akaondoka baada ya dakika tano nikamuona Jackline na mke wa Shabani wakiwa wameongozana. Wakafika kwenye kibanda hichi. Jackline akanitengea kahawa.

“Mama ana endeleaje?”

“Yupo na wajukuu wake chumbani”

“Sawa”

“Shem una mauzngumzo na mimi?”

“Ndio”

Jackline akaondoka eneo hili na kutuacha mimi na shem.

“Kuna nini kina endelea?”

“Sijakuelewa shem”

“Shabani ameniambia kwamba umemnunia kwa nini?”

“Ila shem alicho kifanya ndugu yako sio kitu kizuri kwa kweli. Hawezi kukaa miaka yote hiyo kumbe ana mtoto nje ya ndoa alafu haniambii chochote jana ndio ana niambia. Shem kama kweli ni wewe una weza kulikibali hio jambo”

“Ndio”

“Shem usimtetee kwa sababu ni rafiki yako ila she mina umiza sana. Kuletewa mtoto wan je kwenye familia”

“Nikuulize kitu?”

“Niulize”

“Dini yetu ya kislamu ina turuhusu wanaume kufanya nini?”

“Kuoa wake wanne ila sio kuzaa nje ya ndoa shemeji. Alicho kifanya Sheby ni kuzaa nje ya ndoa hicho ndio kinacho niimiza mimi zaidi.”

“Ila mtoto ndio amesha zaliwa ni damu yetu tuna fanyaje?”

“Shem kusema kweli nimeumia. Nimapitia kipindi kigumu sana na Shabani kabla ya hii neema kutujia. Sasa shemeji kama nikiwa mrahisi kwenye hili kesho na kesho kutwa ata niletea watoto wengine jambo ambalo kusema kweli mimi sinto lipenda wala kuridhika nalo”

“Una mpenda Shabani?”

“Ndio nina mpenda”

“Basi usichukie juu ya hili, mpende yeye pamoja na mwanaye huyo na mchukulie kama mwanao wa tumbo moja. Uchungu ulio pitia wewe ndio uchungu anao pitia huyo mama aliye zalishwa na ndugu yangu. Sinto penda kuona ndoa yenu ina vurugika wala kuachana kutokana na mtoto wa nje na unavyo mkataa, ina onyesha dhahiri kwamba una roho mbaya. Hivyo tuta mleta huyo mtoto nyumbani hapa na tua ishi naye hapa nyumbani. Sinto penda kuona una mchukia au kumnyanyasa. Tuna elewana?”

Shemeji taratibu akashusha pumzi huku akinitazama usoni mwangu kwa macho ya masikitiko kiasi kwamba hata akikubali haya maamuzi yangu basi ni kutokana na heshima aliyo niwekea ila uweli ni kwamba hajamkubali kabisa mtoto wa Shabani aliye zaa nje ya ndoa.


“Sawa shem”

Shem alijibu kwa sauti ya upole na iliyo jaa unyonge.

“Ila shem nikuulize swali?”

“Niulize”

“Kama wewe mke wako akakuzalia mtoto ambaye sio wako na umefunga naye ndoa ya dini kabisa. Utamfanyaje?”

Swali la shemeji likanifanya nishushe pumzi taratibu huku nikimtazama usoni mwake.

“Yaani nijibu kama mwanaume unaye mpenda mke wako, uta mfanya nini mkeo?”

“Nitamsamehe?”

Shem muongo. Lazima umzabe makofi na hata kumfukuza una weza kumfukuza.”

“Ina tegemea lakini na hasira ya muda huo”

“Sasa kwa nini sisi wanawake muna tuonea”

“Ila shem sisi na nyinyi ni tofaui. Sisi tumeumbwa kuwa wanaume, tumenyimwa uvumilivu, ila nyinyi mumepewa uvumilivu. Kama hii ndio mara yake ya kwanza msahame tu”

“Haya bwana shem, mimi moyo wangu upo mweupe hauna shida. Ila kikubwa nahitaji huyo mwanamke ambaye amezaa naye nimjue na aniheshimu kwa maana maswala ya kuletewa mtoto amejazwa chuki na dharau ina weza kupelekea ukamchapa ukaonekana mama wa kambo una roho mbaya kumbe ni roho aliyo pandikizwa na mama yake huko”

“Sawa hilo tuta lishuhulikia. Pia usiku saa mbili tuta elekea mkoani Morogoro kuna swala tuna lifwatilia”

“Na nani?”

“Na Rashidi pamoja na mke mwenzako”

“Sawa shemeji ila ongea bwana na rafiki yako. Maradhi mengi siku hizi, ukiona hadi mtu ana weka mimba kwa mwanamke ujue hajatumia kinga wala nini. Tafadhali bwana sitaki kufa mapema mwanangu bado mdogo”

“Poa sheme nimekuelewa”

Shemeji akanyanyuka na akaondoka eneo hili. Baada ya muda kidogo Shabani akanifwata na nikamueleza alicho kizungumza mke wake.

“Shukrani naona hata nimesemeshwa”

“Hahaaa wazoee wanawake ni watu wa kukasirika kwa muda na hasira zao zikiisha wana rudi na kuwa wa kawaida”

“Una jua sijawahi gombana na mke wangu hadi akanichunia kiasi hichi”

“Una jua alikuwa ana kuamini sasa ulivyo mletea mawenge hayo basi moyo wake mekuwa umepata kama ganzi.”

“Na kuujenga uaminifu wa mwanamke ina taka moyo”

“Kama anakupenda hawezi kuacha kukuamini kwa maana dini ina ruhusu tuoe wake wanne, sasa wana babaika nini?”

“Umeona ehee”

Meseji ikaingia kwenye simu.

‘Mama ana kuhitaji’

Nikairudisha simu mfukoni kwani ni meseji kutoka kwa mke wangu.

“Ngoja nikamcheki mama”

Nikaingia chumbani na kumkuta mama akiwa amekaa na Jackline.

“Nasikia muna kwenda Morogoro”

“Ndio”

“Usiku huu?”

“Ndio”

“Muna kwenda kufanya nini?”

“Kuna ishu tunakwend akuiangalia”

“Mwili wa Don upo wapi?”

“Kwa nini una uliza?”

“Nina haki ya kujau”

“Ngoja tukirudi nitakuambia mwili wake upo wapi?”

“Sawa kuwani makini”

Baada ya chakula cha usiku tukaawaga wana familia na safari ikaanza huku Shabani akiwa ndio dereva.

“Honey”

“Naam”

“Sijapenda ulivyo kuwa una mjibu mama vile, najua unajua fika sio kosa lake kama alivyo kuadithia. Usimchukie”

“Sijamchukia ila naona maisha yangu sijui yamekuwaje. Najiona nimekuwa ni mtu wa tofauti sana, nahisi hii damu ya Don haito futika mikononi mwangu”

“Usijali mume wangu. Muombe Mungu akongoze kwenye hili”

Kila sehemu tunayo pita nina mtajia jina Jacklieni kwa maana ni mgeni. Tukafika mkoani Morogoro majira ya saa nne usiku. Tukaelekea moja kwa moja kwenye eneo ambalo Don amejenga.

“Mmm mbona kuna ukimya”

Shabani alizungumza huku akizima taa za gari hili.”

“Ina onyesha hakuna anaye ishi”

“Chukua bastola, kwa maana lolote lina weza kutokea”

Nikaichukua bastola aliyo nipa Shabani na kuichomeka kiunoni mwangu. Nikashuka ndani ya gari, nikatembea hadi getini, nikajaribu kusukuma geti dogo na kukuta likiwa limefungwa. Nikatazama fensi hii iliyo zungushiwa nyaya za umeme. Huku taa za nje ya ukuta huu zikiwaka.

‘Ina bidi niruke’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikitazama urefu wa ukuta huu ambao ni mrefu ila nina uwezo wa kuuruka bila kugusa nyaya hizi. Nikarudi nyuma hatua kumi kisha kwa kasi nikakimbia na kuruka ukuta huu. Nikajizungusha hewani mara kadhaa kisha nikatua chini vizuri. Nikatazama eneo hili jinsi lilivyo tawaliwa na ukimya. Nikapiga hatua hadi kwenye geti dogo nikafungua.

“Ingieni”

Jackline na Shabani wakaingia ndani.

“Wewe ni mtu au nyani khaaa kaka si kwa kuruka huko”

Hahaa vitu vya kawaida”

“Aisee una jua mimi na shemeji tulikuwa tuna shangaa jinsi ulivyo kuwa unajivuta tukahisi uta gusa ukuta ila umedumbukia mzima mzima”

“Sasa pata picha kipindi kile tuna iba, ningekuwa na uwezo huu sijui raisi ningewaachaje”

“Hahaa”

“Shiii”

Nilizungumza na sote tukaka kimya, nikachomoa bastola yangu mfukoni mara baada ya kuona mtu ana kuja akitokea nyuma ya nyumba hii. Mtu huyu anaye piga mluzi ina dhihirisha kabisa hajahisi uwepo wetu hapa. Tukajibanza kwenye moja ya kona na mtu huyu akatupita.

“Mikono juu”

Nilimuamrisha mzee huyu na akastuka sana, fimbo aliyo ishika akaitupa pembeni.

“Geuka mikono ikiwa juu, ukileta ujinga nina kutandika risasi ya kichwa na una kufa”

Mzee huyu akageuka taratubu.

“Rashidi”

Mzee huyu akaniita kwa jina langu na nikastuka kidogo ila sikutaka kumuonyeshea kwamba nimestuka.

“Umelijuaje jina lako”

“Wewe si mtoto wa Sir Don?”

“Nini?”

“Ndio wewe ni mtoto wa Sir DON, alinipa maelekezo ya kwamba nilinde hii mali hada siku utakapo kuja”

Nikaishusha bastola yangu hii chini na kuiruidisha kiunoni mwangu.

“Ninaitwa mzee Digidigi. Ni miongoni mwa wafanyakazi wa zamani sana wa Sir Don. Karibuni”

Mzee huyu alizungumza huku akielekea katika moja ya nyumba ya pembeni. Akatukaribisha katika nyumba hii ambayo ana onekana ndipo anapo ishi.

“Umejuaje kwmaba mimi ni mtoto wa Don?”

“Aliniambia kwamba ana kijana wake hapa nchini Tanzania na akanionyesha picha zako kadhaa. Huyu ndio mke wako Jacklien?”

“Ndio”

“Karibu sana mkwe”

“Nashukuru”

“Niwaandalie nini?”

“Sisi tupo vizuri mzee. Eehee tuambie mahusiano yako na Don yapo vipi?”

“Kipindi nikiwa kijana, nilikuwa ni mlinzi wake katika migodi yake iliyopo Merelalani. Alinisaidia sana kwenye maisha yangu mengi sana na pia nilimsaidia sana kwenye ishu ya kumtafuta mama yako toka alipo toroka kule Merelani, ila kwa bahati mbaya hatukufanikiwa kumpata mama yako, hivyo DON aliondoka.”

“Niliendelea kuwa muaminifu wa kuilinda migodi yake hadi aliopo amua kuiuza. Hivyo hata alivyo jenga haya mabangaroo mimi ndio niliyasimamia hadi ujenzi ukaisha”

“Ehee alikuambia lini kwamba mimi na yeye ni mtu na mwanaye”

“Siku nyingi sana, alinieleza kwamba Mungu alimfanyia muujiza kwa mke wake kumletea kijana wake kotokea nchini Tanzania na ulikuwa mpiganaji wake wa ulingoni au sio kweli?”

“Ni kweli”

“Alniambia haitaji kujitambulisha kwa mama yako wala kwako kwa maana maisha yalisha badilika na alihitaji kukufanya wewe uwe jasiri, mpambanaji ndio maana alikutengenezea mazingira ya kumuona adui ila hakuwa adui kwako. Njooni niwaonyeshe jambo”

Tukatoka katika nyumba hii na tukaingia katika jumba kubwa. Mzee akawasha taa za ndani. Tukaingia kwenye moja ya chumba kikubwa kilicho hifadhiwa picha nyingi zilizo bandikwa ukutani.

“Hizi ni picha alizo kuwa ana nitumia kipindi ukiwa ulingoni. Mimi nilikuwa nina zisafisha na kuzibandika ukutani”

Nikajikuta nikiishiwa pozi kwani picha hizi ni nyingi sana na ni picha za karibia historia ya maisha yangu niliyo kuwa nchini Marekani, Ufaransa na katika gereza nchini Congo.

“Kuna watu aliwaweka maalumu kwa ajili ya kukufwatilia. Hizi ni picha za harusi zenu na mke”

“Kwa nini alikuwa ana fanya haya yote?”

“Kwa sababu alikuwa ana kupenda sana. Ila yupo nchini Tanzania kwa sasa, siku mbili tatu hizi sija wasiliana naye na simpati hewani hivyo nina imani una weza kuonana naye siku yoyote. Uzuri mukionana safari hii itakuwa ni mtu na baba na sio mtu na adui yake.”

Maneno yam zee digidigi yakauumiza moyo wangu kiasi kwamba nikajikuta nikishusha pumzi nzito kwani huyo anaye mzungumzia tayari nimesha muu.

“Kuha chumba kipo gorofa ya pili. Aliniambia ni chumba ambacho wewe pekee ndio una paswa kuingia. Sasa ijajaua kama una weza kujua code za chumbani hapo kwani ili kuingia ndani ya chumba hicho ni lazima kuingiza code namba”

“Twende tukaone”

Tukapandisha gadi gorofa ya pili. Nikasimama katika mlango wa chumba hichi, nikaingiza namba ambazo Don alinitajia na taratibu mlango huu wa chuma ukafunguka. Tukaingia ndani haoa, chumba hichi kina tv kubwa na makabati yenye mafaili kadhaa, huku kukiwa na meza kubwa ambayo kwa nyuma ina kiti cha ofisi. Nikakaa kwenye kiti hichi na kufungua moja ya droo.

“Hichi chumba alikuwa ana kitumia kama nini?”

“Alikwua ana kitumia kama ofisi”

“Ofisi?”

“Ndio na alinieleza wewe pekee ndio una paswa kuingia.”

“Sawa”

“Ngoja nitoke”

Mzee huyu akatoka ndani hapa nikampa ishara shabani ya kumuangalia mzee huyo kwa makini kwani bado simuamini.

“Ila kwa nini alikwua msiri sana?”

Jackline aliuliza.

“Hata sijui, ngoja tuangalie kilichoopo ndani yah ii laptop”

Nikaiwasha laptop hii na ikanihitaji namba za siri. Nikaziingiza nanba hizi za siri na ikafunguka. Nikaona mafaili mawili, nikaanza kufungua faili la kwanza na nikaona video, nikaifungua video hii sote tukaanza kuitazama. Tukamuona Don akiwia amekaa eneo hili kwenye hichi kiti nilicho kalia.

“Nilikuwa na ndoto ya kuwa tajiri. Hivyo nilifanya kila linalo wezekana kuhakikisha kwamba nina kuwa tajiri. Nina kijana mmoja anaye itwa Rashidi. Ni damu yangu japo yeye mwenyewe ana jua mimi ni adui yake. Ila nina mpenda sana na ninahitaji awe kama mimi. Nina hitaji ahakikishe kwamba ana rithi mali zangu zote na kuziweka kwenye uangalizi mzuri. Faili namba nili lita kupa maelekezo ya nani ukutane naye na lina listi ya mali zangu. Nina imani ukiona faili video hii nitakuwa tayari nimesha kufa”

Video hii ikaishia hapa na sote tukajikuta nikitazamana mimi na Jackline.

“Fungua hilo faili”

Jackline alizungumza na nikafungua faili la pili. Tukaanza kuona nyaraka zinazo nionyesha mimi ndio mrithi wa mali zote za DON. Viwanda, makampuni makubwa na watu ambao nina paswa kuonana nao. Katika mali hizi pia zipo kampuni zake za siri zinazo sambaza madawa ya kulevya”

“Hizi mali zake zina damu za watu wengi sana hivyo siwezi kuzirithi mke wangu”

“Kwa nini?”

“Hizi zote ni damu mke wangu?”

“Mume wangu kila mtu anahitaji utajiri, kila mtu ana fanya kila linalo wezekana kuhakiksiha kwamba ana kuwa tajiri. Huwezi kuachana na hizi mali, una watoto wana paswa kurithi hizi pesa”

“Pesa aliyo nipatia ina tosha”

“Mume wangu hii pesa ni yako. Kikubwa ni kuitakatisha na isiwe pesa haramu na kuwe pesa halali”

“Nina itakatisha vipi?”

Nitakuambia nini cha kufanya”

Tukaanza kukusanya mafaili yote yaliyomo ndani hapa na tukayaingia kwenye begi tulilo muomba mzee Digidigi. Tukazunguka nyumba mzima na kuikagua. Baada ya kujiridhisha kwa kuikagua nyumba hii mzee Digidigi akanipatia funguo ya nyumba hii na nikamuomba endelee kuishi kwenye nyumba hii. Majira ya saa tisa usiku tukaondoka hili.

“Mume wangu”

“Naam”

“Mwili wa baba tuta uzika lini?”

Nikashusha pumzi huku nikipunguza mwendo wa gari hili kwani mimi ndio dereva huku Shabani akiwa amekaa siti ya nyuma na kulala kutokana na uchovu.

“Kesho nikitoka msibani nita kuambia lini tumzike”

“Tuna mziki kwa dini gani?”

“Dini ya kikristo kwani sio ndio dini yake”

“Nikuulize swali?”

“Niulize tu mke wangu”

“Una weza kubadili dini?”

“Hapana”

“Ila baba ni mkristo”

“Hata kama ila dini ya kiislamu ndio imenikuza hadi nimekuwa mtu mzima na mtu mwenye akili zake. Hivyo siwezi kubadili kisa baba alikuwa ni dini fulani na isitoshe sikuwahi kumuona huyu mzee akiingia kanisani wala kuzungumzia mambo ya kanisani”

“Sawa mume wangu nilhitaji kuuliza tu”

“Usijali, nahitaji hizi faili uzipitie moja baada ya nyingine kwa maana mimi kuzisoma ni shida na kama unavyo jua kwamba sina ufahamu mkubwa sana kwenye maswala ya biashara.”

“Wala usijali”

Majira ya saa kumi na moja alfajiri tukafika nyumbani. Majira ya saa nne asubuhi mara baada ya kuamka, nikajiandaa mimi na Shamsa na tukaelekea katika kanisa ambalo misa ya msiba ndio ina endelea.

“Baba”

“Naam”

“Watu ni wengi ehe?”

“Ndio mwanangu watu wengi na walinzi pia ni wengi”

“Sasa mama tuta muonaje?”

“Usijali tuta muona tu yupo kule mbele”

“Rashidi”

Caro aliniita, akanifwata na kunikumbatia kwa nguvu.

“Vipi misa imesha anza?”

“Bado, mambo Shamsa”

“Safi wewe ni nani?”

“Ohii mimi ninaitwa anti Caro ni mdogo wa raisi aliye kufa”

“Ahaa wewe ndio kaka yako alimuiba mama yangu?”

Nikashusha pumzi ndefy kwani kauli ya Shamsa ikamfanya hata Caro kushangaa kidogo ila akafanya kupoteza kwani Shamsa amekuwa ni binti mwenye akili kubwa kuliko.

“Hapana Shamsa”

“Una weza kunikutanisha na mama?”

“Ndio yupo kule mbele twendeni kuna viti vyenu pia”

Tukapita katikati ya kanisa hili hadi tukafika kwenye viti vya wana familia. Mama Shamsa akastuka sana mara baada ya kumuona Shamsa huku akiwa ameongozana nami. Shamsa akamtazama mama yake kwa sekunde kadhaa kisha akaka pembeni yake huku akiwa hajamsalimia wala kuonyesha furaha yoyote ya kukutana na mama yake.


Ukimya ukatawala kati yetu. Ibada ya kumuombea marehemu ikaanza huku mara kwa mara nina muangalia Shamsa, ila yupo bize na kusikiliza mahubiri ya mchungaji huyu ambaye ana tusisitizia tuishi kwa amani. Wakati wa maombi nikamshuhudia mama Shamsa akijaribu kumshika Shamsa mkono ila akautoa mkono wake kwa nguvu kwa mama yake. Muda wa kuuangalia mwili wa Marehemu ukawadia, wakaanza wana familia huku mimi na Caro tukiambanata kama mtu na mume wake. Nikaushuhudia mwili wa raisi ukiwa umelala kwenye jeneza hili, baada ya kuutazama tukarudi kwenye viti huku viongozi wengine walio jitokeza kuuaga mwili huu sasa ikiwa ni zamu yao. Vilio vingi kwa kweli vime tawala ndani ya kanisa hili. Baada ya zoezi hili kuisha, tukaondoka kanisani hapa na kuelekea makaburini ambapo kuna ibada ndoto kabla ya jeneza kuingizwa katika kaburi. Taratibu ya mizinga ya heshima ikapigwa ikiwa ni taratibu za maziko ya viongozi wakubwa wa nchi kama huyu mzee.

“Pole”

Nilimuambia mama Sheila mara baada ya mazishi kumalizika. Akanikata jicho moja kali kisha akamtazama Shaila aliye simama pembeni yangu huku nikiwa nimemshika mkono.

“Sheila mwanangu”

“Mimi sio mwanao. Ulisha nikataa na kunitoa kwenye maisha yako toka siku ulivyo nikataa pale. Hivyo hakuna haja ya wewe kuniita mimi mwanao”

Kauli ya Shamsa ikamshangaza sana mama Sheila.

“Kwa hiyo baba yako ndio amekufundisha usema huu upuuzi”

“Wala sio baba yangu. Wewe ndio umenifanya niwe jasiri na mkakamavu na toka nipo hivi mdogo nina kuwa ni mtafutaji wa pesa ili badae nije kuwa na maisha mazuri ili nisihadaike na pesa za mwanaume na nikamuacha mwanaume ambaye nina mpenda. Baba yangu hakuwa na pesa kipindi kile ila hapakuwa na haja ya kumfanyia ulicho mfanyia. Ushetani ulipo ndani yako tambua malipo yake yapo hapa hapa duninai”

Sheila alizungumza kwa ujasisi sana hadi nikamshangaa. Uzuri eneo tulilo simama, watu wapo mbali kidogo kwani yeye ndio aliye tufwata.

“Wewe usinijibu hivyo, una jua nimekuewa tumboni miazi tisa”

“Haijalishi. Uisnge nizaa wewe, baba yangu angenipata kwa mwanamke mwengine mzuri, mwenye akili na uwezo wa kufanya maamuzi mazuri kuliko wewe. Nina kuchukia, nitaendelea kukuchukia hadi nina ingia kaburini. Sikupendi na sinto kaa nikupende tena kwenya maisha yangu. Huwa nina jiuliza ni kwa nini hukufa siku nyingi na una endelea kung’ang’ania kuishi duniani. Dunia hii sio kwa watu kama nyinyi, dunia ni kwa watu salama na wenye amani ila sio kama wewe”

Shamsa akatema mate pembeni, kisha akauchia mkono wangu na akaanza kukimbilia iliopo gari yangu.

“Hongera ume fanikiwa kumkuza na kumtia sumu mbaya sana moyoni mwake?”

“Sijamfundisha wala kumtia sumu. Ila haya ni malipo ya zile mbinu zako chafu ulizo kuwa una nifanyia kipindi chote. Hivyo pambana na hali yako”

“Hahahahahahaa. Ngoja nikuambie jambo moja, usione nikemaa kimya ikahisi sijui nini umefanya. Yule malaya wako uliye mtuma kuja kumuua mke wangu amezungumza kila kitu kwamba wewe ndio muhusika. Sasa nikuambie jambo moja. Nita dili na wewe, nita hakikisha una lipa kwenye hili, haki ya Mungu nita kuua Rashidi”

“Kabla ya kuniua nina muhitaji mwanangu. Weka akili yako kichwani muda wowote na siku yoyote nita mchukua mwanangu kutoka kwako, sasa jichanganye kunidhuru mimi, mwanangu au mtu yoyote ndani ya familia yangu. Nita kuua kwa kukukata kata vipande bila ya huruma. Malaya mkubwa wewe”

Mara baada ya kuzungumza maneno hayo nikaondoka eneo hili na kumuacha mama Shamsa akinisindikiza kwa macho, Nikafika lilipo gari langu na nikaingia na kumkuta Shamsa akiwa amekaa siti ya pembeni mwa dereva huku akilia kwa uchungu sana.

“Namchukia mama, namchukia mimi”

Shamsa alilia kwa uchungu huku akiwa amejiinamia katika siti. Nikamtazama kwa sekunde kadha, kisha taratibu nikamsogeza pembeni yangu.

“Usilie mwanangu mimi nipo kwa ajili yako”

“Baba nikuombe kitu?”

“Niombe mwanangu”

“Una weza kunifundisha jinsi ya kumuua mtu?”

Nikastuka sana na kumtazama Shamsa usoni mwake.

“Ndio baba nifundishe namna ya kumuua mtu, Tafadhali nina kuomba usije ukanikatalia kama mama Jackline alivyo fanya”

“Una taka kumuua nani?”

Nilimuuliza Shamsa kwa sauti ya upole huku nikimtazama usoni mwake, taratibu Shamsa akanitazama huku midomo ikimtetemeka kwa hasira ambayo kwa namna moja ama nyingine amirithi kutoka kwangu.

“Shamsa”

“Beee”

“Hivi una jua kuua ni dhambi ehee?”

“Najua baba ila kuna watu ni lazima wafe ili tuwe na amani. Hata kwenye biblia kuna wafalme walikuwa wana ua watu ili watawale. Ina kuwaje sasa hivi watu wengine wasife baba”

Shamsa alizungumza kwa ujasiri hadi nikashangaa.

“Umesoma wapi biblia?”

“Nyumbani zipo na mama hatukatazi kusoma na nimekuwa nikipenda kuisoma kila siku usiku”

“Sasa mwanangu huko huko kwenye biblia si kuna maneno yana tuusia tusiue”

“Ndio baba ila ina tupasa tusiwaue wasio na hatia ila hawa wenye hatia ni lazima wafe”

Nikawasha gari kabla ya kuondoka nikamuona Caro akija huku nilipo. Nikashusha kioo kioo cha gari taratibu.

“Rashidi naomba tuongee”

Nikashuka ndani ya gari na tukasogea pembeni kidogo.

“Sasa ina kuwaje ule mwili mume wanngu?”

“Nina kuja kuutoa leo usiku”

“Kwa leo usiku hapana”

“Kwa nini?”

“Kuna wana ndugu wata lala nyumbani kwangu. Alafu nina wazo moja”

“Wazo gani?”

“Kwa nini tusi uyayushe kwenye acid ili kufuta ushahidi kwa maana kuuzika uchunguzi una weza kufanyika na ikajulikana ni wapi mwili wake upo””

“Basi jaribu kuandaa hiyo acid nitakuja kuuyayusha mimi mwenyewe”

“Sawa, nakupenda sana Rashidi”

“Nakupenda pia”

Caro akanibusu shavuni mwangu kisha nikaurudi ndani ya gari.

“Yule mwanamke ana kupenda ehee?”

Shamsa alizungumza kwa utani.

“Nani?”

“Anto Caro”

“Hahaaa umejuaje?”

“Mimi najua tu mtu akimpenda mtu huwa ana kuwaje”

“Hahahaaa hivyo mwanangu.”

“Baba una weza kunipeleka sehemu kula icream”

“Una penda?”

“Ndio”

“Basi tuwapitie na wengine nyumbani ili kama kwenda kula tukale wote”

“Nataka tykale sisi wawili. Ni muda mwingi sana baba hatujakaa pamoja nahitaji kukaa na wewe tuzungumze”

Nikajifikiria kwa sekunde kadhaa kisha nikamkubalia Shamsa. Tukaondoka makaburini hapa na moja kwa moja nikampeleka katika mgahawa mmoja mkubwa ambapo una uza kila aina ya chakula. Tukatafuta viti vilivyopo pembezoni mwa bustani nzuri iliyo tengenezwa kwenye mgahawa huu, kisha tukakaa. Baada ya muhudumu kutuletea icream tunazo zihitaji, tukaanza kula.

“Baba”

“Naam”

“Beirut ulikwenda kupokea mafunzo ya kijeshi ehee?”

“Nani kasema”

“Ati Fatma”

“Anti Fatuma gani?”

Shamsa akatoa simu yake mfukoni, akaiminya minya na akanigeuzia picha. Nikastuka kidogo kumuona Fatma.

“Usijali baba sinto muambia mama kwamba una mdogo wetu mpya”

“Mmmmm!!”

“Yaa najua amejifungua mtoto last week ila sikukuambia kutoka na ubize. Ngoja nikuonyeshe”

Shamsa akaipekua tena simu yake na akanionyesha picha.

“Tumepata mtoto wa kike baba”

Shamsa akanionyesha picha za mtoto wa Fatma ambaye nilimuacha nchini Uingereza.

“Napanga siku moja twende tukamuone”

“Nani?”

“Mtoto wetu baba. Hivi baba una jua nina jua siri zako nyingi kuliko mtu yoyote?”

“Weee mtoto”

“Ndio baba, najua kuhusian na anti Fiifi wa Ghana na nina zungumza naye.”

Nikajikuta nikishusha pumzi nyingi sana kwani mtoto naona ana anza kunizidi ujanja.

“Hao wote umewajuaje?”

“Mimi ni Star, huwa nikiweka picha za nyinyi wazazi wangu huku nakutana na maoni mengi sana kwenye picha kwenye upande wa meseji na watu wengi huwa wana kuja, sasa kama huyu Fatma alikuja kwa lengo la kama shabiki wangu na tukaanza kuzungumza kwa video call akanitumia picha zenu mulipo kuwa Beirut hivyo nikajua nini kinacho endelea”

“Kazi kweli kweli”

“Ata wa Ghana naye alinifwata kwa njia hiyo hiyo kama shabiki wangu na akanionyesha mtoto wetu. Na ubaya sura zetu hazikimbii”

Nikabaki nikitabasamu.

“Alafu baba naomba jambo moja baba”

“Jambo gani?”

“Una jua mziki wangu una julikana kwa nchi kama Marekani. Ufaransa, Uingereza na baadhi ya nchi za Afrika zinazo tumia lugha ta Kingereza. Ila kwa hapa Tanzania bado haujafahamika sana ikiwa mimi ni mzawa wa hapa, hivyo ina nipasa kujulikana pia nyumbani. Hivyo nakuomba uwe meneja wangu na nitakuwa nina kulipa kama ninavyo mlipa mama Jackline”

“Hahahahahaa Shamsa mwanangu kwa hiyo una taka kutuajiri wazazi wako?”

“Ndio baba, dunia imebadilika, dunia kwa sasa ni kubwa na dunia sasa hivi ni biashara hivyo tukiwa kwenye biashara nita wachukulia kama wazazi wangu na tukiwa kwenye maisha ya familia muta kuwa ni wazazi wangu”

Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama Shamsa.

“Mama Jackline ana kulea vizuri?”

“Zaidi ya alivyo kuwa ana nilea mama yangu mzazi. Mama Jackline ni mwanamke wa kipekee na nina kuahidi sinto mvujia heshimu siku hata moja kwenye maisha yangu. Ananipenda, ana nijali na kunisikiliza kile ninacho kihitaji na kukitimiza kwa wakati sahihi. Ila nikuambie kitu baba”

“Niambie”

“Mimi ndio mwanao wa kwanza si ndio?”

“Ndio”

“Nakuomba umpende mama Jackline kwa moyo wako wote. Usimdanganye, ana kupenda na ana kuhitaji kwenye maisha yake. Ni wanawake wachache sana ambao wana weza kumlea mtoto ambaye sio wake kwa moyo mmoja kama anavyo walea wake. Kama mama yangu mzazi tu alinikana na kunionyeshea roho mbaya, pata picha angekuwa ndio mama yangu wa kambo ingekuwaje?”

“Mmmm ingekuwa mziki”

“Basi nakuomba usije ukamuacha mama Jackline ambaye amefanya kila kitu kwa ajili ya familia yetu”

“Sawa mwanangu sinto muacha”

“Ehee nimekumbuka”

“Umekumbuka nini?”

“Nilimsikia bibi akizungumza kwa siri na mtu ana itwa Tina na ana muulizia mjuluu wake ana endeleaje. Huyo naye ni nani?”

Nikajikuna kidogo kwenye paji la uso wangu huku nikimtazama Shamsa.

“Ni nani eti?”

“Ni mama yako mdogo”

“Ina maana huyo pia ana mdogo wangu?”

“Yaa ila bado hajazaliwa”

Sheila akatabasamu huku akijifuta mdomo wake kwa tishu.

“Nina furahi kusikia idadi ya wadogo zangu wana ongezeka. Ila ina bidi mama Jackline naye awajue?”

“Ishu sio kuwajua, ishu nina anzaje kumueleza na ata chukuliaje hiyo idadi ya watoto”

“Mmmm hapo ni mtihadi kweli”

“Ndio nina juuliza, je akikasirika na kuamua kuniacha ita kuwaje?”

“Ila kwa mama Jackline sidhani kama ana weza kukuacha kwa maana ana kupenda kwa maisha yake yote na hicho kitu huwa ana niambia kwa mara kadhaa”

“Ila maisha yana badilika?”

“Ndio yana badilika ila kama uta mueleza ni kwamba tayari imesha tokea. Hivyo huwezi badilisha ukweli. Ila muheshimu kuanzia sasa hivi. Alafu baba yule anti Caro ni mjamzito?”

“Ndio”

“Ile nayo ni mimba yako?”

“Ndio”

“Jamani baba”

“Shamsa tuachane na mambo hayo kwa maana ni mambo ya wakubwa”

“Sawa baba, kama nimekukasirisha nina kuomba unisaheme”

“Hujanikasirisha.”

“Basi nina kuomba baba mambo mawili niliyo kuomba uweze kuyazingati”

“Lipi na lipi?”

“Swala la kuwa meneja wangu na swala la kunipa mafunzo ya kumuua mtu”

“Sinto kufundisha kuua mtu nita kufundisha kujilinda mwenyewe. Kama ikitokea umevamiwa na hauna msaada wa karibu”

“Utanifundisha kutumia bastola?”

Nikakaa kimya kwa sekunde kadhaa.

“Ndio”

“Shukrani sana baba yangu. Nakupenda nakupenda”

Shamsa akanikumbatia kwa furaha. Tukamaliza kula icream hizi, tukanunua icream za kopo kwa ajili ya kupelekea walipo nyumbani.

“Una weza kuendesha gari?”

“Ndio”

Nikamkabidhi funguo ya gari Shamsa na bila ya woga wa aina yoyote, akazunguka upande wa dereva na akaingia ndani.

“Funga mkanda baba”

Nikafunga mkanda taratibu na safari ya kuondoka eneo hili ikaanza taratibu huku nikimuelekeza njia za kupita.

“Baba twende kule tulipo kuwa tuna kaa”

“Kimara?”

“Ndio”

“Sawa”

Safari ikazidi kusonga mbele, jambo ninalo shukuru Mungu Shamsa japo ni mdogo ila amerithi urefu wangu na ameukimbia ufupi kiasi wa mama yake. Tukafika kwenye mtaa tunao ishi.

“Nyumba yetu mbona siioni baba?”

“Mama yako aliuza hicho kiwanja hapo, ikajengwa hiyo gorofa”

“Kwa nini, ikiwa bibi mwenyewe ana seme eneo lake hilo ana lipenda na alipanga safari hii aje kutengeneza kitu cha ukumbusho kwenye mtaa wake alio anzia maisha”

“Akili za mama yako ziliishia hapo hivyo hatuna namna ya kufanya mwanangu”

“Hapana baba ina bidi ufanye jambo”

“Jambo gani sasa mwanangu”

“Ikiwezekana tuwaondoe hapa”

“Haiwezekani mwanangu tuta gombana tu na watu”

“Ngoja nikuonyeshe”

Shamsa akashuka kwenye gari, akaziweka vizuri nywele zake ndefu kisha akaanza kupiga hatua hadi lilipo geti la nyumba hii ya gorofa iliyo jengwa kisha akaanza kugonga geti hilo kwa fujo na kunifanya niduwae kwani sijui ana mpango gani unao endelea kichwani mwake.



Geti likafunguliwa na akatoka mlinzi. Kutokana nipo kwenye gari sijui wana zungumza kitu gani, nikamuona mlinzi akijaribu kumzuia Shamsa kuingia ndani hapo ndipo nami nikashuka ndani ya gari ila kabla sijawafikia nikashuhudia Shamsa akimpiga teka la sehemu za siri mlizi na akaanguka chini na ikawa rahisi kwa Shamsa kuingia ndani.

‘Ehee dogo bangi huyu’

Nilizungumza huku nikimfwata kwa nyuma.

“Weee mtoto weee”

Mlinzi alilalama huku akijaribu kunyanyuka.

“Tulia ndugu”

Nilizungumza huku nikimrudisha chini mlinzi anaye endelea kusikilizia maumivu ya sehemu zake za siri.

“Nyinyi nani hadi piga kekelele gonga gonga tu geti yangu kosa heshima na starabu ya kubisha hodi”

Mama huyu wa kiarabu alizungumza kwa ukali huku akitutazama.

“Nahitaji kuonana na mume wako”

“Wewe nani hadi uliza mimi wapi mume wangu?”

“Mama nahitaji kuonana na mume wako”

“Wewe Juma pumbavu sana kuwa boya hadi geti fungua watu ingia ndani”

Mama huyu aliendelea kufoka kwa hasira hadi walipo ndani wakatoka.

“Kuna nini mama?”

Binti mmoja mrefu na mrembo alizungumza huku akimtazama mama yake.

“Hii toto na sijui nani yeka ingia humu ndani, hi toto taka ona baba yenu.”

“Samahani kaka, muna hitaji nini?”

“Nahitaji kumuiona mmiliki hii nyumba kwa maana, hili eneo mulipo jenga hii nyumba ni eneo langu. Sasa nina shangaa kuja leo kukuta gorofa refu namna hii”

“Mmmm basi karibuni ndani”

“Wewe karibisha watu hujui weza leta jambazi ndani?”

“Mamaa hembu nyamaza basi, jambazi ana muonekano huu na ana weza kuja nab inti mdogo kama huyu. Kaka yangu naombeni mumsamehe mama yangu ana onge sana. Karibuni sana ndani.”

“Tunashukuru”

Tukaingia ndani na kukaribishwa sebleni.

“Ngoja nikawaitie baba”

Binti huyu akapandisha gorofani na nikaishia kumtazama kwa macho ya matamanio, kama unavyo jua wanaume haturidhiki kwa nyama moja. Baada ya dakika tatu hivi binti huyu akashuka akiwa ameongozana na mzee mwenye kitambi kwa haraka haraka una tambua kwamba ni baba yake kwani si kwa kufanana huko.

“Shikamoo mzee”

“Marahaba”

Tukasalimiana na mzee akaka kwenye sofa kwa ajili ya kutusikiliza huku mkewe akitutazama kwa mcho ya kadhiba na chuki.

“Ndio tuwasaidie nini?”

“Ahaa kwa jina nina itwa Rashidi ni mfanya biashara mkubwa. Huyu binti ana itwa Sheila ni mwanangu wa kwanza. Lengo lililo tuleta hapa ni kuhusian ana hichi kiwanja mulicho uziwa. Nina imani kwamba kuna nyumba ya kawaida muliuziwa pamoja na hichi kiwanja?”

“Ndio”

“Na muliiuziwa na huyu mwana mama?”

Nilizungumza huku nikimonyesha picha ya mama Sheila.

“Ndio alikuwa na huyu mume wake ambaye leo hii amezikwa, raisi”

“Sawa huyo mwanamke aliweza kunikimbia na akakimbilia kwa huyo baba. Akaniachia mtoto wangu huyu akiwa bado binti mdogo pamoja na mama yangu. Kabla ya kumpata huyo mwana mama nilikuwa nina ishi na mama yangu. Ambaye yeye ndio alijenga kwenye hichi kiwanja na alinirithisha mimi kutoknaa na kuwa mimi ndio mwanaye wa pekee”

“Ngoja kwanza bwana Rashidi”

“Ndio”

“Una jua hii sehemu tuliinunua kisheria. Na uziri kila aina ya nyaraka za manunuzi tunazo. Hivyo ingekuwa ni jambo jema na zuri kama hili swala tungelizungumza ukiwa na yeraka za umiliki kihalali”

“Mzee”

Shamsa aliita kwa sauti ya kujiamini.

“Ndio binti”

“Unahisi mimi na baba yangu ni waongo, jinsi baba alivyo mfanyia baba pamoja na sisi una hisi ni jambo la uongoo. Tumepitia magumu mengi hususani baba yangu. Ilibidi akili yangu itanuke na kuwa na uelewa mkubwa kabla ya muda wake. Mama alikuwa na nguvu na baba alikuwa masikini hakuwa na nguvu yoyote kwa wakati huyo ndio maana mambo yamekuwa kama yalivyo kuwa. Ila hili sehemu ni mali ya baba yangu na bibi yangu na ndio sehemu yangu. Kwani hapa ndipo ilipo ardhi yangu, nilipo zaliwa mimi na sinto penda eneo nililo zaliwa liondoke kizembe”

Kujiamini kwa shamsa kuka mshangaza kila mtu ndani hapa.

“Sema una hitaji bei gani tukurudishie utuachie eneo letu”

“Ahaa ahapana binti sidhani kama mutakuwa na pesa ya kununua hili eneo”

“Mzea acha kutudharua kwa sababu sisi ni ngozi nyeusi ukahisi hatuna pesa ya kununua. Tena hili eneo nina linunua kwa pesa yangu na sio pesa ya baba yangu. Nahitaji kurekebisha makossa aliyo yafanya mama yangu kwa baba yangu”

“Mmmm”

Mzee huyu akatazamana na mke wake, kisha wakanong’onezana.

“Kwanza mzee inakuwaje una jenga jumba kubwa hivi kwenye mtaa wa uswahilini kama huu huoni ni kama kumwaga mchele katikati ya kuku wengi”

“Una maanisha nini binti?”

“Una watoto wazuri wa kike, na hapa ni uswahili kuna vijana choka mbaya wana wasulubu hata mukiwazuia vipi, uswahilini ni uswahilini”

Nikajikuta nikitabasamu kwa maana Shamsa ana maneno mengi.

“Kijana huyu binti ni kweli ni binti yako au?”

“Ndio mimi ni biti yake na mama yangu ni yule mshenzi pale”

Shamsa akamuonyesha baadhi ya vipindi vya marudio ya msiba wa raisi kipindi tukiwa kanisani na kwabahati mbaya tumekaa pamoja na kwa jinsi Shamsa alivyo fanana na mama yake hapakuwa aliye bisha kwamba yule sio mama yake.

“Tumezungumza na mke wangu, tumefikia muafaka kwamba hatuwezi kuuza hii nyumba. Hata tukiondoka eneo hili tuta hakikisha kwamba tuna kodisha”

“Bilioni moja nitawapa”

Shamsa alizungumza na kunifanya nimuangalie kwa mshangao.

“Hapana kwa kweli?”

“Shilingi bilioni tatu?”

Mzee na mke wake wakatazamana huku wakitamani kujibu kitu.

“Hatuuzi binti”

“Dollar milioni mbili”

Shamsa akawa kama mtu ambaye yupo kwenye mnada wa bidhaa fulani.

“Binti kusem kweli hatuuzi”

“Dola millioni tatu nina wapa leo hii hii nina waandikia cheki. Najua hii nyumba na kiwanja chake havifiki thamani ya hiyo pesa.”

Shamsa ili kudhihirisha ana juamini. Akakunja nje nne huku akiziweka vizuri nywele zake ndefu.

“Wee hiyo pesa unayo au?”

Nilimnong’oneza Shamsa sikioni mwake. Akanionyeshea ishara ya dole gumba akimaanisha kwamba hiyo pesa anayo.

“Hembu nina omba nafasi ya kuzungumza na familia yangu, kama hamto jali tusubirini hapo nje”

“Hakuna shaka”

Tukatoka na tukaa kwenye eneo lililo tengenezwa kwa ajili ya kupumzikia.

“Hiyo pesa unayo kweli Shamsa?”

“Ndio baba ngoja nikiuonyeshe”

Akatoa simu yake mfukoni na kuanza kuminya minya kisha akanionyesha kiasi kilichopo kwenye akaunti yake ni dola milioni ishirini na nne?”

“Hizi pesa umezitolea wapi mwanangu?”

“Ni kutokana na mziki wangu na baadhi ya biashara za mama ambazo aliniwekezea hisa toka nilipo kuwa mdogo”

“Aisee kumbe wezangu matajiri ehee?”

“Sasa baba una mama tajiri kama Jackline una shindwaje kuwa tajiri”

“Na hii stahili ya kumpandishia mtu pesa umejifunzia wapi?”

“Hiyo amenifundisha mama, yaani ana kuambia kama una hitaji kitu chochote na muuzaji ana jishaua shaua basi wewe muongezee pesa yenye kupita bei ya kile kitu chake. Hawezi kuchomoa, ndio hawa, wana jishaua, dola milioni tatu ni sawa na shilingi ngapi ya Kitanzania?”

“Mmmm kwa reat ya sasa hivi ni kama dila bilioni sita na ushenzi hivi”

“Sasa hiyo pesa kweli wana shindwa kwenda kufanya ujenzi mwengine”

“Sasa mwanangu una nunua hii nyumba na hili eneo una pango wa kufanya kiti gani?”

“Baba hii sehemu ina fursa”

“Fursa gani?”

“Kwenye hii nchi kuna vipaji vingi sana vya vijana. Kama mukiniruhusu basi tunavunja hili eneo na tuta tengeneza gorofa ambalo litakuwa na studio kubwa na za kisasa zainazo husiana na mziki. Tuta rengeneza rekodi lebo ambayo itakuwa ina toa kazi za wasanii na kuzipeleka internation. Uzuri mimi nimetokea juu kwa juu, ila hawa wa huku chini wana paswa kushikwa mkono na kunyanyuliwa.”

Nikamtazama Shamsa kwa sekunde kadhaa. Kusema kweli nimezaa mtoto mwenye akili iliyo kamilika, enzi zangu umri kama wa Shamsa nilikuwa sisishiki mtaani hapa nilikuwa ni mtoto mkorofi, ukinichokoza kidogo tu tuna pigana, iwe ni nijwe, chupa, gongo ilikuwa ni lazima nihakikishe nina shinda mtanange wangu.

“Au sio wazo zuri?”

“Ahaa ni wazo zuri mwangu kwa sababu mimi sio mtaalamu sana wa hayo mambo”

“Kila kitu ni kujifunza tu baba. Hivi baba wewe una kipaji gani?”

“Mimi?”

“Ndio”

“Mmmm labda ninacho kijua ni kupigana”

“Kweli?”

“Ndio mwanangu, kipaji changu mimi kikubwa ni kupigana hilo ndio nijualo. Nilikuwa nina penda sana kupigana kipindi changu hicho”

“Ila kipaji hicho ndio kimemvutia mama naye pia si alikuwa mpiganaji wa uliongoni?”

“Ndio”

Akatoka binti wa mzee huyu.

“Baba anawaita”

Tukaingia ndani na kukaa sehemu tulipo kuwa tume kaa.

“Ndio mzee”

“Tumejadiliana kama familia, na tumefikia maamuzi ya pamoja”

“Ndio ndio”

“Tumekubali kuiuza hiyo nyumba kwa dola milioni tatu ila kwa ombi moja”

“Ombi gani?”

“Kutona ni jambo la kustukiza, tungeomba tuweze kukaa mwezi mmoja baada ya nyumba kununuliwa, ili iwe rahisi kujipanga kwa ajili ya kuhamia makazi mapya.”

“Sawa hilo halina tatizo ila kabla ya kufanya manunuzi ina bidi tuzungumze na mwanasheria wetu, ili aweze kuja hapa na mambo yote yafanyike kisheria”

“Halina shida karibuni sana”

Nikaangalia saa yangu ya mkononi.

“Sasa mbili usiku tungeomba kurudi kwa ajili ya kufanya biashara nanyi”

“Sawa bwana Rashidi, tuna weza kupeana namba ili tuwasiliane”

“Hakuna shaka”

Tukapeana namba na mzee huyu kisha tukatoka ndani hapa.

“Baba una elfu kumi hapo”

“Ndio”

“Naomba”

Nikamkabidhi elfu kumi, tukafika getini na akamkabidhi mlinzi.

“Usipende kutumia nguvu kwa mabinti”

Shamsa alizungumza kisha akaanza kutangulia kuelekea lilipo gari. Tukaingia ndani ya gari huku wakati huu mimi ndio dereva wa gari.

“Baba mwezi mzima ni mwingi kwa wao kuishi mule ndani?”

“Usijali mwanangu kikubwa waondoke”

“Sawa baba”

“Hiyo pesa nitaitoa mimi”

“Pesa ya nyumba?”

“Ndio”

“Kwa nini baba?”

“Mimi ni baba yenu. Muna paswa kuishi maisha mazuri nawajali, hata kama muta kuwa na pesa kunipita mimi ila nita hakikisha nina wajali kwenye kipindi chote cha maisha yenu”

“Asante sana baba, hakika wewe ni baba bora kwenye maisha yangu. Sikuzote huwa nina sikia kwamba baba ndio wanao kimbia majukumu ila kwa upende wangu imekuwa ni tofauti sana kwani mama yangu ndio alikimbia majukumu kisa mwanaume”

“Ndio hivyo mwanangu, ila usijali tupo pamoja kwenye kila hatu”

Tukafika nyumba tukagawa zawadi za icream tulizo zinua, nikawakalisha kikao mama, Jackline pamoja Shabani. Tukawaeleza adhima ya kununua nyumba hiyo ambayo ipo kwenye kiwanja cha mama.

“Mmm ila dola milioni tatu ni nyingi sana kaka”

Shabani alizungu huku akitutazama.

“Ni kweli hilo nalifahamu ila pale ndio chimbuko langu lilipo tokea nikishindwa kuitetea ardhi iliyo nunuliwa kwa jasho la mama yangu nitakuwa nimekosea sana”

“Kwa nini tusifwate sheria kwa maana hizo hati za nyumba na kiwanja ninazo.”

“Sasa mama wewe hati ya kiwanja si ile iliyo pimwa na kijiji kipindi hicho, ila sasa hivi mambo yamebadika. Isitoshe mahakamani mambo yanaweza kuwa ya kuzungushana sana”

“Sawa kaka, kama mahakamani tuta kuwa tuna poteza muda ila dola milioni tatu ni nyingi sana kwa maisha ya hapa Tanzania”

“Naweza kuchangia?”

Jacline aliuliza.

“Ndio mke wangu, kwa nini usichangie”

“Ahaa ardhi ni kitu kikubwa na muhimu kwa maisha yoyote ya binadamu. Hata uwe tajiri namna gani hauto weza kujenga nyumba angani. Kwa umri wangu huu nilio fika hadi sasa sijapata ona kitu kama hicho. Kikubwa ambacho nina penda kuwaomba tuikomboe hiyo ardhi na baada ya hapo pesa hiyo tuta irudisha taratibu taratibu”

“Daa seme shemeji nyinyi muna pesa kwa kweli. Yaani ingekuwa ni mimi tungeinunua kwa milioni mia moja tu. Washenzi wale waarabu Wahindi wa Kariakoo kaka, kwanza niwaibie siri”

“Siri gani?”

“Yule mzee ana fanya biashara za magendo nyingi sana, pili hana kibali cha kuishi hapa nchini Tanzania. Tukidili naye kwa mlango wa nyuma huyu mzee ana kimbia nchi”

“Kwa hiyo una taka tutumie udhaifu wake huo kumpokonya mali yake?”

“Ndio kaka”

“Ila jamani, kumbukeni jasho la mtu haliliwi. Japo siifahamu hiyo mtu ila jasho la mtu haliliwi kiurahisi kama hivyo. Hata kama aliuziwa na adui yeny, ila hampaswi kumdhulumu. Kama hamto toa hiyo pesa, nita toa mimi mume wangu”

“Hapana nimeshakubaliana na Shamsa juu ya kuitoa hiyo pesa. Hiyo pesa”

“Sawa mume wangu”

“Hivyo jambia tumekubaliana kuitoa hiyo pesa”

“Sawa kaka”

“Honey nakuomba tuzungumze”

Tukaondoka sebleni hapa na mke wangu na kuingia chumbani kwetu. Nikakuta mafaili mengi tuliyo yatoa nyumbani kwa DON yakiwa yamesambaa kitandani.

“Vipi tena?”

“Otea ni nini?”

Mke wangu alizungumza huku akiwa amejawa na furaha sana.

“Ni nini mke wangu?”

“Nimepitia faili moja baa ya jengine otea nimeona nini?”

“Ehee niambie mke wangu?”

“Baba yako amekuachia urithi wa kampuni kubwa mia moja na ishirini ambazo zipo dunia nzima na katika kila kampuni amaendika jina lake. Ukichanganya kampuni zote utajiri wake una fika dola bilioni mia nne na hamsini.”

“Waoooo”

“Sasa kwenye upande wa pili wa pesa zake haramu ambazo hakuna serikali yoyote inayo ijua zaidi ya hizi nyaraka zake za siri. Huku ana utajiri dola trilioni mia mbili na ishiri, kwa dakika moja baba yako ana ingia dola milioni mbili kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Na huko pia ameandikisha jina lako yaani mume wangu sisi ni matajiri. Sisi tuna pesa sasa mume wangu”

Jackline alizungumza huku akinirukia na akanikumbatia kwa furaha kubwa sana kwani kiwango hichi cha pesa nina uhakika baada ya kukubali kurithi kila kitu basi mimi ndio nitakuwa tajiri namba moja duniani.



“Ila hizi pesa zote nitazifanyia nini mke wangu?”

“Kuna mambo mengi ya kuweza kufanya na pesa hizo. Tuna weza kufungua organazition ambazo zina weza kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali kwenye haya maisha”

Simu yangu ikaanza kuita, nikaitoa mfukoni na kuona namba ya mzee ambaye tuna hitaji kunua nyumba.

“Yule mzee ana piga”

“Mpokelee”

Nikaipokea simu na kuiweka sikioni mwangu.

“Ndio mzee wangu”

“Bwana Rashidi naona muda ulio sema umekaribia”

“Usijali mzee wangu nina kuja hapo na wana familia yangu pamoja na mwana sheria”

“Sawa mzee wangu”

“Wahini kwa maana kuna mtu amejitokeza naye kuinunua?”

“Una maana gani kusema hivyo?”

“Ahaa wahi tu bwana Rashidi”

Simu ikakata na kujikuta nikiitazama kwa sekunde kadhaa.

“Kuna nini mume wangu?”

“Ana dai kuna mteja mwengine amejitokeza”

“Mmmm”

Mlango wa chumbani kwetu ukagongwa. Nikatembea hadi mlangoni na kuufungua.

“Kaka mwanasheria amesha fika”

“Sawa ndugu yangu tuna toka sasa hivi jiandae”

“Poa”

Shabani akaondoka, ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yangu. Nikaufungua na kuukuta ukiwa umetoka kwa Tina.

‘Nakuhitaji leo mume wangu uje nyumbani’

Nikaiweka simu yangu mfukoni, tukaingia bafuni na Jackline tukaoga kwa pamoja kisha tukajiandaa kwa safari hii. Tukawakuta Shabani, Shamsa na bibi yake wakiwa tayari wapo ndani ya gari.

“Habari naitwa bwana Mgonja ni mwanasheria wa kampuni ya Mgonja Law. Pia nina shirikiana sana na bwana Shabani kwenye maswala mengi ya kisheria”

Bwana Mgonja alijitambulisha huku tukipeana mikono.

“Nashukuru sana kukufahamu bwana mgonja. Huyu ni mke wangu ana itwa Jackline”

“Nashukuru kukufahamu Mrs Rashidi”

“Nashukuru sana”

“Kumbe una zungumza Kiswahili?”

“Ndio nina zungymza Kiswahili vizuri sana”

“Aisee hongera sana. Kama hamto jali tuna weza kutumia gari langu ili tuweze kuzungumza juu ya hili swala na unielezee jinsi ilivyo kuwa kwa maana bwana Shabani alinieleza ila nahitaji kusikia kutoka kwako”

“Hakuna tabu”

Tukaingia ndani ya gari la mwanasheria na tukaianza safari. Ujumbe mwengine ukaingia katia simu yangu, nikaufungua.

‘Haki ya Mungu usipo kuja nina kuja leo hii na mke wako aone namna nilivyo na ujauzito wako na nitamuonyesha picha nikiwa na mama mkwe ili ajue kwamba nami pia ni mke mwenzake na nimesha kubaliwa na mama mkwe.’

Meseji hii ikanifanya nishushe pumzi kidogo na kwa bahati nzuri nimekaa siti ya mbele pamoja na mwanasheria huyu huku Jackline akiwa amekaa siti ya nyuma.

“Ndio bwana Rashidi niambie ilikuwaje kuwaje hadi kiwanja kikauzwa na aliye kuwa mzazi mwenzako?”

Nikaanza kumuelezea bwana Mgonja hali ilivyo tokea.

‘Hujibu meseji zangu ehee?’

Nikaitazama meseji kisha nikairudisha simu yangu mfukoni. Tukashuka katika gari na kuingia katika nyumba hii. Tukafunguliwa geti na magari haya yakaingia, tukakuta gari nyingine tatu aina ya Range Rover huku nje kukiwa na walinzi kama wanne wakiwa wamesimama huku wamevalia suti nyeusi.

“Karibuni”

Binti wa mzee huyu alitukaribisha. Tukaingia ndani, tukastuka sana kumkuta mama Shamsa akiwa amekaa kwenye moja ya sofa huku akinywa juisi taratibu huku akiwa amekunja nne na walinzi kama sita wakiwa ndani ya seble hii pamoja na wenye nyumba.

“Karibu sana bwana Rashidi?”

Mzee huyu alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake. Tukakaa kwenye sofa huku bado nikiendelea kumtazama mama Shamsa ambaye amejawa na tabasamu.

“Ahaa bwana Rashidi huyu ndio yule aliye niuzia hili eneo naamini muna fahamiana?”

“Endelea?”

Nilizungumza huku nikimkata jicho kali mzee huyu.

“Na huyu pia anahitaji kununua hii nyumba hivyo makubaliano yetu ya kwanza naomba munisamehe sinto pokea dola milioni tatyu kwa maana dau hapa limesha pandishwa na kufika dola milioni nne”

“Kwa hiyo umetusaliti?”

Shamsa alizungumza huku akimtazama mzee huyu.”

“Hapana binti, biashara ni biashara. Hivyo nimetazama wapi kuna weza kuwa na mashlahi kwangu”

“Mzee mimi nina itwa bwana Mgonja. Sijui wewe una itwa nani?”

“Bwana Faruku”

“Sawa bwana Faruku, hawa unao waona hususani huyu mama ana hati halisi za hichi kiwanja ambapo kulikuwa na nyumba yake. Tukisema tusimame mahakamani hauto onja hata shilingi mia na utaondoka hapa mikono mitupo kwa amri ya mahakama kwa mana aumevamia eneo la mtu”

Bwana Mgonja alizungumza kwa kujiamini.

“Hati za umiliki munazo?”

“Ndio zipo?”

Bwana Mgoja akafungua brufcase yake na akatoa karatasi kadhaa na kiziweka juu ya meze.

“Hizi hati ulikuwa nazo?”

Nilimnong’oneza mama siokoni mwake.

“Wala sina”

“Hizi nazo zimetokea wapi?”

“Wala sijui mwanguu”

Mama naye alinijibu kwa kunong’oneza.

“Una weza kusoma na kuona hichi kiwanja kilimilikiwa zamani kuliko hati uliyo pewa na kununua hivi karibuni. Isitoshe huyo mwana mama alikuwa ni mmoja wa hawa wana familia hapa. Baada ya kuwa muasi wa famila basi akaamua kufanya anayo yafanya. Hivyo mzee Faruku andika kwamba ume umia”

“Hembu nione”

Mama Shamsa alizungumza kwa sauti ya nyodo, mzee Faruku akamkabidhi karatasi hizo na akazisoma kisha akatabasamu kwa kejeli.

“Mama umesahau?”

“Nimesahau nini?”

“Nahisi akili yako siku hizi haifanyi kazi vizuri”

“Aisee chunga kinywa chako wewe. Usije ukathubutu kumkejeli na kumdharau mama yangu. Nitakuwasha mabao sasa hivi”

Nilizungumza kwa kufoka sana kwani katika vitu ambavyo kama una taka univuruge, basi mdharua au mtukane maam yangu huwa nina badilika dakika sifuri hata kama ninakuwa nipo kwenye hali ya kicheko.

“Una panic, muulize mama yako, kama hakuniandikisha kwenye hati ya umiliki wa kiwanja chake mara baada ya kukuona wewe huna akili ya maisha. Mama ni uongo?”

Mama akaka kimya huku akinitazama kwa macho ya huruma.

“Mama kiri mbele za watu. Mara baada ya kujifungua Shamsa si uliniandikisha kwenye umiliki wa kiwanja chako ukaniambia kwamba wanaume watatafuta mali zao”

“Mama anacho zungumza yule mshenzi ni kweli?”

“Ndio ila nilimuandikisha kutokana nilikuwa nina mpenda na alinizalia mjukuu wangu wa kwanza”

“Sasa kwa nini mama hukuzungumza hadi tumekuja kudhalilishana hapa?”

Nilkizungumza kwa kufoka kidogo.

“Hivyo hichi kilicho andikwa hapa ni feki. Mama mwenyewe amekiri bwana nani wewe mwana sheria?”

“Mgonja”

“Yaa nivyo hata mukienda kwenye mahakama ganoi, mimi ndio mmiliki halali wa hili eneo na mzee wa watu huyu alinunua kwa mtu halali hivyo hayo makaratasi yenu muliyo foji ni feki”

“Turudi kwenye biashara sasa. Nyumba yangu nina pokea dola milioni nne kutoka kwa mama hapa”

“Dola milioni sita”

Jackline alizungumza na kutiufanya watu wote tumtazame kwa mshangao.

“Honey”

Jackline akaniyooshea kiganja ikiwa ni ishara ya kusubiria. Mama Shamsa akamuita mmoja wa walinzi wake na wakanong’onezana.

“Dola milioni sita na nyusu”

“Nane”

Jackline alizungumza kwa kujiamini, roho ikaniuma sana kuona nyumba hii ina panda thamani kila dakika. Mama Shamsa akapiga fumba la juisi.

“Wewe ndio mke mwenzangu?”

Mama Shasa alizungumza kwa nyodo huku akumtazama mama Jackline usoni mwake.

“Mzee dola milioni nane chukua tukulipe tumalizane”

“Dola milioni nane pointi moja”

Mama Shamsa alizungumza. Jacklien akanitazama kwa macho ya kuhitaji kuzungumza jambo.

“Alafu wala hamjaendana aisee. Hivi una jua sisi waswahili ni watamu sana kuliko nyingi wazungu, ndio maana huyo mume wako hachoki kuni miss”

‘Nita mpiga huyu malaya’

Jackline alininong’oneza.

“Ni wewe tu mke wangu”

Nilimpa ruhusa hiyo Jackline kwa maana tayari amesha anza kujawa na hasira.

“Sisi waswahili, tumejazia, nyama nyama, tako tako, sasa wewe ulivyo pigwa pasi sijui kama Rashidi ana ridhika. Eti Rashidi ana kukatikia kama nilivyo kuwa nina kikatikia mimi hadi ukaamua kunioa na kiniweka ndani?”

“Wewe biti umepatwa na jini gani mbona umekuwa na kinywa kichafu namna hiyo eheee?”

Mama alizungumza kwa kufoka.

“Mama na wewe tuliza kiboribo chako”

Jackline uvumilivu ukamshinda. Akanyanyuka kwa kasi, akakanyaga meza hii ya kioo kwa bahati nzuri haijavunjika. Akamrukia mama Shamsa kwneye sofa alilko kaa na wakabingirika hadi chini. Walinzi wa mama Shamsa wakajaribu kumshika mke wangu, mimi na Shabani tukanyanyuka na kuwazuia. Mlinzi mmoja akatoa bastola na kutunyooshe.

“Yoyote atakaye mgusa mkuu nita muua”

Jambo ambalo mlinzi huyu ana paswa kumshukuru Mungu ni kutokana amesimama mbali na mimi laity kama angesimama karibu yangu ningesha mpiga pigo ambalo angesimulia kwa ndugu zake. Taratibu Jacklie akamuachia mama Shamsa huku akisimama na kumtazama mlinzi huyu.

“Jamani naomba mutulie”

Mzee Faruku alizungumza huku akimtazama mama Shamsa anaye simama huku pembeni yam domo wake akivujwa na damu.

“Naombeni mukae”

“Usipok uwa na damu tuta kufundisha adabu mpuuzi sana wewe”

“Mama safi sana”

Shamsa alizunguzma huku akimpigia makofi Jackline.

“Uta lipa hii”

Mama Shamsa alizungumza huku akijifuta damu kwa kitambaa chake. Akaka katika sofa alilo kalia.

“Kumbe shemeji yupi vizuri?”

Shabani alininong’oneza sikioni mwangu.

“Sana”

“Si kwa kuruka huko”

“Hahahaa”

Nasi tukaa katika sofa tulizo kuwa tumekaa hapo awali.

“Umeumia?”

“Hapana mume wangu”

Jackline alizungumza kisha akanishika shingoni mwangu na akaanza kuninyonya denda la taratibu huku watu wote wakitutazama kwa mashangao.

“Mzee dola milioni kumi tufanye biashara, na muondoke usiku huu au asubuhi muondoke mutuachie hili eneo”

Nilizungumza huku nikimtazama mzee huyu. Akashusha pumzi huku akimtazama mama Shamsa ambaye anaonekana mashindano yamemshika. Mama Shamsa akasimama hukua kiwa ameshika pochi yake.

“Nina waahidi nyinyi ngedere ni lazima mulipe kwa hili miulilo fanya, nita waua kenge nyinyi”

Mama Shamsa alizungumza kisha akaanza kutembea kuelekea mlangoni.

“Jiandae nina kuja kumchukua”

Nilizungumza na kumfanya mama Shamsa kusimama kwa sekunde kadhaa kisha akageuka na kunitazmaa. Akaninyooshea kidole cha katikati.

“Stress za msiba zita muua yule hana pa kwenda”

Mama alizungumza huku sote tukimtazama mama Shamsa jinsi anavyo toka ndani hapa na walinzi wake.

“Mzee tuna rudi kwenye biashaera. Makubaliano yetu ya kwanza ndio yana fanyika”

“Ila si tumekubaliana milioni kumi bwana Rashidi?”

“Una hisi mimi ni punguani au?”

“Una maanisha nini?”

“Ipo hivi, nina mjua yule mpuuzi kuliko unavyo hisi. Amekuambia kabisa tuje hapa tushindane kununua hii nyumba alafu hicho cha juu una mpatia yeye si ndio?”

Mzee huyu akatazamaa na mke wake.

“Nina akili hapa mulicho kuwa munakifanya ni udalali. Nikupe dola milioni tatu biashara iishie hapa”

“Ongeza hata moja?”

“Siongezi hata shilingi mia makubaliano ya awali ni awali.”

“Sawa ila ule mwenzi mmoja ina bidi munipatie”

“Hakuna shaka”

Tukaanza kuandikishana mikataba ya manunuzi. Nikamuingiza mzee huyu kiasi hicho cha pesa kupitia benki na akatukabidhi hati ya nyuma hii.

“Nashukuru sana kwa kufanya nanyi biashara”

“Kuwa makini siku nyingine acha udalali”

Tukapenaa mikono na wanandugu hawa ikwa ni ishara ya kuagana. Binti yake mkubwa ambaye alitupokea tulipo kuja na Shamsa. Akanikabidhi kikaratasi pasipo mtu yoyote kuweza kuona. Tukatoka ndani hapa na tukaingia ndani ya magari tulio jia na safari ya kurudi nyumbani ikaanza.

“Mume wangu ina bidi tujipange kwa chochote”

“Una maanisha nini?”

“Yule mwananmke ni lazima ata tuwinda”

“Chizi yule”

“Usipuuzie mume wangu”

“Sawa mke wangu”

Simu yangu ikaanza kuita nikaitoa mfukoni na kuona namba ya Tina. Nikatazama saa ya simu hii ina onyesha sasa hivi ni saa nne usiku. Nikapokea simu hii na kuiweka sikioni.

“Ndio”

“Yaani mseji zangu hujibu, una niona mimi fala si ndio. Sasa hapa nina kodisha ndege na nina kuja na tumbo langu, siwezi mimi kuwa nina pigwa na baridi alafu wewe una kumbatia mke wako. Sasa leo nataka ukweli ujulikane tusifanyane machine.”

Tina alizungumza kwa sauti ya kofa na simu ikakatika jambo ambalo likanifanya nijawe na wasiwasi mwingi sana kwani endapo Jackline ata jua tulicho kifanya kwa Tina mimi na mama yangu basi ata tuona sote mimi na mama yangu ni wasaliti kwake.



Nikajaribu kuipiga simu ya Tina, ikaanza kuita na akaikata. Nikamfwata mama na kumnong’oneza sikioni mwake.

“Yule mpuuzi anal eta shida”

“Nani?”

“Si mkweo wa Tanga, hapa amecharuka ana dai kwanba ana kuja hapa ili kuonana na Jackline”

“Ana wendawazimu?”

“Sio ana wendawazimu hiyo kijidai kumdekaza dekeza kwako ukahisi basi una dekeza mtu wa maana kumbe boksi tu”

“Usiongee hivyo”

“Ohoo mimi bwana sitaki familia yangu iingie migogoro ya kipuuzi. Sasa utajua namna ya kumzuia na ana dia na achukua ndege, nimempigia simu amenikatia. Sasa kama wamekaa yeye na mama yake wameamua kushauriana upumbavu asiee mama nina roho mbaya, nitamtoa ile mimba”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama mama usoni mwake.

“Acha uchizi. Ngoja nimpigie sasa hivi”

“Piga hapa nikusikie”

Tukasogea kwenye kibanda cha kupumzikia huku watu wengine wakiwa wametangulia ndani.

“Weka loud speaker”

Simu ikaita na ikapokelewa.

“Shikamoo mama”

Tina alizungumza kwa sauti ya upole.

“Marahaba mwanangu pole bwana nimekupigia usiku huu”

“Wala usijali mama yangu una endeleaje?”

“Nina endelea vizuri mwangu. Vipi wewe na mjukuu wangu pamoja na bibi yake?”

“Kwa kweli mama tuna mshukuru Mungu tuna endelea vizuri. Mwenyezi Mungu ametusaidia kwa sasa tupo salama kabisa”

“Sawa sawa mwanangu. Upo wapi?”

“Mama nime lala sasa hivi”

Nikashusha pumzi nzito.

“Naweza kukupigia video call?”

“Ndio mama nipigie tu”

Mama akakata simu hii ya kawaida na akampigia video call ili kudhihirisha kwamba yupo Tanga na hajaanza safari kama alivyo kuwa anatishia.

“Niambie mama yangu”

“Salama mwanangu, vipi una jisikiaje?”

“Najisikia vizuri mama yangu ila mbona Rashidi siku hizi hanijali, hanipigii simu?”

“Ohoo pole sana mwanangu. Hapa katikati alikuwa na pambana na wale maamdui zake kidogo siku hizi mbili ndio amepata unafuu”

“Sawa mama yangu nafurahi kusikia hivyo. Mama nakuomba umuambie awe ana wasiliana na mimi. Kuna wakati huwa nina hitaji uwepo wake ila nina shindwa kuupata mama. Nakuomba unisaidie kwa hili mama yangu”

“Usijali mwanangu ata wasiliana na wewe na nita msisitizia aje huku kesho tu”

Nikamtazama mama kwa macho ya mshangao.

“Kweli mama?”

“Ndio kesho tu saa nne uta kunywa naye chai hapo kwake”

“Nashukuru sana mama yangu, najisikia furaha kuwa na mama kamaa wewe”

“Ni jikumu langu kuwaangalie wote. Kwa sababu nyote nyinyi ni wangu na munao wazaa wote ni wangu.”

“Nashukuru mama kwa upendo wako kwa kweli ninajisikia vizuri sasa”

“Usijali kesho tu. Rashidi ata kuwa hapo”

“Asante sana mama yangu.”

“Basi nikutakie usiku mwema”

“Nawe pia mama, nakupenda sana mama yangu”

“Nakupenda pia mwanangu”

“Haya”

Mama akakata simu hii huku akinitazama usoni.

“Kesho saa kumi na mbili nahitaji uelekee Tanga”

“Mama bwana. Nina mambo mengi sana ya kufanya nahitaji kufany……”

“Sio ombi ni amri”

“Ila mama nimesha kuwa mtu mzima sio mtu wa kuapngiwa amri……”

Mama akaweka kidole kimoja mdomoni mwake akimaanisha kwamba nifunge kinywa changu.

“Sio kwangu na kaa ukijua kwamba kwenye maisha yako yote hata uwe na miaka hamsini. Mimi kwako ni mama yako na utabaki kuwa mwanangu tu na huto kuja kunipanda kichwani mwangu siku hata moja. Una nielewa?”

Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama mam usoni mwake.

“Umenielewa?”

“Nimekuelewa”

“SItaki yule binti apate tabu kama nilivyo pata tabu kwa mimba yako. Una jua niliteseka vipi, una jua ni mateso ya aina gani nilipitia hadi nina kuzaa. Una jua ni hali gani ambayo mama ana kuwa nayo pale anapo kuwa mjamzito. Wanaume japo muchukue dakika moja kutushehimu sisi, sisi ndio tuna wafanya muonekane ni watu, sisi ndio tuna wafanya mukipitisha mabichwa yenu huko muitwa baba fulani. Ikiwezekana ukake hata wiki”

“Aha…wiki mama”

“Nimekuambia, kama ni shuhuli zako toa maelekezo Shabani azishuhulikie”

“Kwa hiyo amshuhulikie hadi mke wangu au?”

“Hayo mimi sijui. Kikubwa yule binti ana kuhitaji, mpe mapenzi kama mume na sio kijifanya sijui nipo bize sijui vimepanda vimeshuka. Sitaki huo upumbavu”

Mama akanyanyuka na akaondoka kibandani hapa na akaniacha peke yangu. Simu yangu ikaanz akuita nikaitoa mfukoni na kuiona namba ya Caro.

“Caro”

“Samahani Rahidi kwa kukupigia simu muda kama huu”

“Bila samahani”

“Nimepata pipa la acid na limepelekwa kwenye moja ya shamba langu. Hivyo kama huto jali usiku huu tuje kushuhulika na lile swala”

“Sawa mpenzi wangu ila ulisema una wageni?”

“Wapo ila sidhani kama wata fahamu ni kitu gani kitakacho fanyika”

“Una waamini?”

“Siaminigo mtu. Ila nina imani kwamba hawato tufwatilia”

“Kweli?”

“Ndio”

“Basi nita kuja hapa saa nane usiku”

“Sawa nina kusubiria honey”

“Poa”

Nikakata simu, nikanyanyuka na moja kwa moja nikaeleka chumbani kwangu. Nikamkuta Jackline akiwa amejilaza kitandani huku akiwa amevalia bikini pekee.

“Mume wangu”

“Niambie”

“Njoo nikunong’oneze”

Nikapanda kitandani, taratibu Jacklien akanisogelea sikioni mwangu. Akaanza kuninyonya sikio la uapnde wa kulia.

“Mmmmm”

Nilitoa miguno ya msisimko huku taratibu Jakcline akifanya uchokozi ambao nina jua nini anacho kihitaji. Nikaanza kumnyonya maziwa yake kisha nikashuka katika kitumbua chake na kuendelea kukinyonya taratibu. Baada ya kumuandaa tukaanza mtanange wa kukata kwa shoka. Kila aina ya mkao nikamkalisha mke wangu ili mradi kuhakikisha kwamba nina mpa starehe na haki anayo stahili. Hadi nina maliza mzunguko wa kwanza Jackline yupo hoi.

“Leo mume wangu umenikimbia daaa”

“Vipi umeridhika mke wangu?”

“Naachaje kuridhika mume wangu. Yaani umenipeleka pute pute yaani ningekuwa ni mgeni kwako ningesema umeninywea dawa leo ila daa. Nafurahi kumpata mwanamume kama wewe”

“Nashukuru mke wangu kwa kunivumilia kwa kipindi chote hicho kwenye maisha yetu. Umenifanya kuwa mtu mwerevua ambaye nina jua nini maana ya familia”

“Asante mume wangu”

“Alafu mwanao bwana ana taka niwe meneja wake wa mziki”

“Hahahaha hata mimi niu meneja wake”

“Sasa napewa kazi ambayo hata kusomea sijasome”

“Ahaa mume wangu kazi hii sio ngumu. Ngoja nitakufundisha na tukimsimamia mtoto wetu nina imani utajiri uta zidi kutawala katikati yetu”

“Nitashukuru mke wangu. Kuna jamnbo moja nahitaji kulifanya usiku huu”

“Jambo gani tena mume wangu”

“Nahitaji kwenda kuuondoa mwili wa DON sehemu nilipo muua nahitaji kuuyayusha kwenye pipa la tindikali”

“Mmmm mume wangu, hutaki kumzika kawaida?”

“Siwezi kumzika kawaida. Hivyo nataka kufanya kama hivyo”

“Hutaki mama ashuhudi mazishi hayo?”

“Hapana, nimemuua kwa mikono yangu hivyo sihitaji mtu yoyote kushiriki kwenye hili. Hii dhambi ni yangu mke wangu”

“Sawa mume wangu hakikisha kwamba una kuwa makini sitaki kukaa mbali na wewe kwa manaa adui yetu amesha ondoka”

“Usijali mke wangu nipo pamoja na wewe . Na nimefanya haya yote kwa ajili yetu na watoto wetu”

“Sawa mume wangu”

“Kwa sababu namtoa nje ya mji hivyo naenda mashambani hiyo ili kusiwe na ushahidi wa mtu wa aina yoyote”

“Nimekuelewa mume wangu japo nilitamani kuandama nawe”

Taratibu nikamsogelea mke wnagu na kuishika mikono yake.

“Mikono yako ipo salama mke wangu, haina damu na sinto penda iwe na damu ya mtu yoyote wala kushirikia uovu wowote kwa maana mikono hii ndio inayo nilelea wanangu kipenzi. Hivyo nikimalizana na hili nitakuwa mwanaume wa familia. Mwanaume wa kuwa nawe kila wakati. Nakupenda sana Jackline wangu”

“Nakupenda pia mume wangu kipenzi, ndio maana nimejitoa kuwa na wewe kwenye kila hali”

“Nashukuru mke wangu”

Nikakumbatiana na Jackline, akaniandalia nguo, nikavaa, nikaagana naye kwa mabusu motomoto kisha nikaondoka nyumbani hapa. Saa nane usiku juu ya alama nikafika nyumbani kwa Caro akanipokea na moja kw amoja tukaelekea katika chumba nilicho fanya mauaji ya DON. Nikaukuta mwili wa DON ukiwa umewekwa kwenye begi ya plastiki zitumikazo kubeba maiti.

“Nani ameifanya shuhuli hii”

“Mimi mwenyewe mume wangu”

“Ukiwa na ujauzito?”

“Ndio mume wangu kwani kuna tatizo gani?”

“Hujaogopa?”

“Jamani mume wangu, niwatu wangapi nimewau kwa risasi, visu na kuwanyonga. Ni maiti ngapi za ajabu ajabu nimezishuhudia. Ina kuwaje maiti hii jamani”

Nikamtazama Caro kwa sekunde kadhaa nikafungua begi hii na kumuona DON. Nikaifunga zimu kulitazama eneo hili lote.

“Umesafisha na sakafu?”

“Ndio mume wangu, ume sahau mimi ni mpelelezi, hivyo nina jua njia zote za kufuta ushahidi wa mauji kama haya”

“Sawa mke wangu. Tuna kwenda na gari yangu au yako?”

“Gari yangu ita pendeza zaidi”

“Kaisogeze hapa basi”

Caro akatoka ndani hapa na akasogeza gari lake hadi eneo hili. Akafunga mlaggo wa nyuma wa gari hii aina ya Land Cruiser VX V8. Nikaubeba mwili huu wa DON na nikauuingiza ndani ya gari na tukafunga. Tukaingia ndani ya gari huku mimi nikiwa ndio dereva wa hili gari. Tukaondoka eneo hili huku Caro akinielekeza njia za kupita.

“Mbona una onekana una mawazo mume wangu?”

“Una jua kipindi chote cha maisha yangu nimeishi bila ya kumjua baba yangu. Sasa leo hii nime mbeba baba yangu kama maiti tena yupo nyuma ya gari. Kidogo ina nipa mawazo. Nilitamani hata ningepata dakika kumi za kuzungumza naye kama baba na mzazi kabla ya kufikia hatua ya kufyatua risasi yangu ya kwanza.”

“Mume wangu?”

“Naam”

“Usijilamu kwa chochote juu ya hili. Kwani alikuwa ni adui yako na alikusuma uwe adui yake. Japo alikuwa ana jua kwamba wewe ni mwanaye ila alindela kuishi na wewe kama adui. Hukwua na shida, ulifanya kwa ajili ya watu uwapendao. Hata ingekuwa ni mimi ningefyatua risasi yangu ya kwanza kuhakikisha nina linda niwapendao. Hivyo mume wangu usiwe katika mawazo kama hayo”

Caro alizungumza huku akinishika mkono wangu wa kushoto.

“Sawa mke wangu. Hivi zile maiti za walinzi wako vipi na watu wa Don tulio waua nao vipi?”

“Walinzi wangu walizikwa na serikali kwa maana wale ni wana usalama hivyo walichukuliwa kwamba wamefia kazini. Wale wa DON walizikwa na serali ya jiji”

“Ahaa sawa sawa”

Tukafika katika shamba kubwa la Caro ambalo limezungushiwa fensi kubwa.

“Ni heka ngapi hili shamba?”

“Heka mia”

“Duu ni kubwa sana”

“Ya ni kubwa sana kwa maana hapa nina lima kilimo cha minazi hiyo pamoja na maembe. Kwa kule mbele kule nimepanda nanasi hivyo kikubwa ni kupambana mume wangu”

“Ni kweli mke wangu”

Nikasimamisha gari kwenye moja ya nyumba iliyopo hapa shambani.

“Anaishia nani hapa”

“Kuna vijana wawili wanao niangalizia shamba langu hivyo jana niliwapigia simu kwamba wapumzike kutokana na kujianda na mazishi ya kaka. Hivyo hawapo”

“Sawa”

“Tuuingize huo mwili ndani”

Nikautoa mwili wa DON ndani ya gari na tukaingia ndnai ya nyumba hii. Caro akafungua moja ya chumba na nikakuta pipa moja. Nikalifunua na kuona tingikali ambayo endapo un igusa kwa kidole basi kidole chako kina yayuka mithili ya plastiki katika moto. Tikavaa nguo maalumu ambazo hata kama tindikali hii ita turikia katika miili yetu hatuto athiriwa. Nikafungua begi hili nikautoa mwili wa dona na kidogo.

“Nimepata wazo”

Nilizungumza.

“Wazo gani?”

“Tumuwekewe na na hili begi lake”

“Hapana honey tuuuweke mwili wake”

“Sawa”

Nikautoa mwili wa DON na tukaudumbukiza katika pipi hili na tindikali hii ikaanza kutokota huku mwili wa Don ukiyayuka mithili ya barafu linavyo yayuka.

“Dunia nzima hakuna atakaye fahamu kwamba wewe ndio ume mumuua Don”

Nikamtazma Caro na sikuhitaji kumjibu chochote. Nikaushuhudia mwili wa DON ukiteketea hadi dakika ya mwisho Nikashusha pimzi nzito huku nikimtazama Caro machoni mwake.

“Una mpango gani?”

Caro aliniuliza.

“Mpango wa nini?”

“Kuhisiana na haya maisha ya sasa jua kuishi bila aidui”

“Unahisi kumuua DON kuna weza kunipunguzia maadui?”

“Ndio kwa maana kaka yangu naye alikuwa ni adui yako ila naye ndio hivyo amesha tangualia mbele za haki”

“Bado nina adui anaye nijua?”

“Nani?”

“Wifi yako”

“Amefanyaje tena?”

“Naona ana nifwatilia na ana tafuta chochoko choko na familia yangu. Ana jihisi ana akili nyingi kuliko mimi sasa muambie, kama ana hitaji kuishi kwa amani akae mbali na familia yangu ila kama anahitaji afe kikatili kana nilivyo muua DON. Athubutu kufanya kile alicho mfanyia mama yangu mzazi. Nitamuua mbele ya dunia nzima ikishuhudia”

Nilizungumza kwa msisitizo na kumfanya Caro atingine kichwa akimaanisha ataufikisha ujumbe huu ipaswavyo kwani ameshuhudia nikimua DON hivyo kumuua mama Shamsa ni jambo jepesi sana kwa upande wangu.



“Anna ni mtu hatari kuliko unavyo fikiria”

Caro alizungumza huku akinitazama machoni mwangu.

“Uhatari wake ni nini?”

“Kaka amemrithisha Anna mali zake zote na hivyo ana nguvu kubwa ya pesa na kuna mabidili mengi sana ambayo kaka alikuwa ana yapiga. Hivyo amempa kiburi kikubwa sana hiyo kama una hitaji kupambana naye ina bidi utumie akili nyingi, hicho ndio ninacho weza kukuambia tu kuhusiana na Anna”

Tukamaliza shuhulia iliyo tuleta eneo hili na tukaondoka na kurudi nyumbani kwa Caro.

“Hulali”

“Hapana kuna sehemu nahitaji kuelekea”

“Wapi?”

“Mkoani Tanga”

“Usiku huu?”

“Ndio tuta onana kesho mchana”

“Sawa mume wangu

Nikaingia ndani ya gari langu na nikaianza safari ya kuelekea mkoni Tanga huku nikipita barabara ya Bagamoyo. Majira ya saa kumi na moja kasoro alfajiri nikifika katika mkoni Tanga. Nikasimamisha gari getini, walinzi wawaili wakashuka wakiwa na bunduki. Nikashusha kioo.

“Mkuu habari yako”

“Salama nifungulieni geti”

“Sawa mkuu karibu sana”

“Nashukuru”

Mmoja akafungua geti na nikaingiza gari ndani. Nikashuka ndani ya gari na nikajaribu kufungua mlango wa mbele n akukuta ukiwa umefungwa. Nikampigia simu Tina zaidi ya mara tano na hajapoke.

“Vipi boss?”

“Hawa watu wapo?”

“Ndio mkuu wapo ndani”

“Hawajatoka?”

“Hapana labda watakuwa wamelala”

“Napiga simu zao naona hazipokelewi”

“Jaribu kuminya kengele boss”

“Sawa”

Nikarudi mlangoni, nikaminya kengele mara kadhaa na baada ya dakika kama kumi hivi mlamgo ukafunguliwa na mama mkwe.

“Shikamoo”

“Marahaba baba, ehee mbona usiku huu tena, vipi kwema?”

“Kwema mama yangu muna endeleaje hapa?”

“Salama tu baba yangu.”

Nikaingia ndani hapa, nikatazama seble jinsi ilivyo badilishwa baadhi ya vitu.

“Vipi za safari?”

“Salama mama yangu. Mungu ni mwema ana bariki kwa kweli”

“Karibu sana mwanangu”

“Nashukuru, si yupo juu?”

“Ndio”

“Asante mama na sahani kwa kukusumbua usiku usiku wote huu”

“Usijali mwanangu”

Nikaingia chumbani kwa Tina, nikamkuta akiwa amelaza uchi kabia kitandani. Nikawasha taa na taratibu nikaka kitandani huku nikisikilizia harufu ya udi iliyo tawala ndani hapa.

‘Ila haka katoto kazuri?’

Nilizungumza huku nikimpapasa makalio yake, nikazichezea chezea shanga zake kiunoni na kumfanya afumbue macho yake na kunitazama.

“Umekuja mume wangu?”

“Ndio niambie una endeleaje?”

“Naendelea vizuri baby vipi wewe?”

“Namshukuru Mungu nina endelea vizuri”

“Vipi mtoto tumboni?”

“Ndio ana kua si una ona tumbo lina zidi kwenda mbele”

“Yaa”

Tina akalijaza chali na akaipanua miguu yake, akauchukua mkono wangu wa kulia na akaugusisha katika kitumbua chake.

“Joto limekuwa kali mume wangu. Please naomba kidogo”

Tina alizungumza kimahaba huku akinipapasa katika zipu yangu.

“Ngoja nikaoge”

“Jamani mume wangu”

“Yaa nina oga”

Nikanyanyuka na kuingia bafuni, nikaoga haraka haraka kisha nikatoka bafuni huku nikiwa uchi kabisa. Nikapanda kitandani hapa na taratibu tukaanza kunyonyana denda. Msisimko wa mahaba ukatufanya tuzame katika dimbwi kubwa la mapenzi. Vilio vya Tina kwa mara kadhaa vikanifnaya nimzibe mdomo wake kwani nina hisi vina toka hadi nje ya chumba chetu.

“Niache bwana baby nifurahie penzi langu”

Tina alizungumza huku kwa mara kadhaa akitoa kiganja changu mdomoni mwake na akaendelea na vilio vyake. Hadi tuna maliza Tina akajilaza chali huku akihema sana.

“Una nguvu sana wewe binadamu. Mmmm yaani una sugua hadi nikahisi mimba ina toka”

“Umeyataka mwenyewe”

“Sio nimeyataka mwenyewe mume wangu. Nilikuwa nina hamu kubwa sana na wewe “

“Kweli?”

“Ndio mume wangu, yaani nilikuwa nahisi hadi nina changanyikiwa vile”

“Hivi mwanamke akiwa na mimba huwa ana kuwa na nyege?”

“Ndio kwani mimba kitu gani?”

“Mmmm”

“Ohoo ndio hivyo, yaani nilikuwa natamani hata kuja Dar yaani usinge kuja leo hadi kesho, yaani ungeshangaa nipo nyumbani”

“Kazi kweli kweli”

“Tuachane na hayo vipi lakini mama yangu hajambo?”

“Hajambo yupo salama kabisa”

“Wanao na mkeo je?”

“Wapo salama”

Tina akanitazama kwa jicho kali.

“Nini sasa?”

“Hamna, tumalizie usingizi tu, nikumbatie mgongoni”

“Mmmmm”

“Nini?”

“Sijazungumze chochote mke wangu”

Nilizungumza huku taratibu nikikumbatiana Tina kwa nyuma. Kutokana na uchovu nilio kuwa nao kutokana na mizunguko ya siku nzima. Nikapitia na usingizi mzito.

Mwanga mkaliwa jua unao piga machoni mwangu ukanifnaya nifumbue macho yangu.

“Akhaha funga pazia bwana”

“Kumekucha mume wangu”

“Ndio funga dirisha naumia macho”

Fatma akafunga patiza.

“Nimekueletea kifungua kinywa mume wangu, amka unywe”

“Ngoja kwanza usije ukaniungaza mimi”

“Nikakuunguzaje sasa?”

“Huja ona ile clip demu ana mpelekea mume wake chai kitandani mwishowe kamwagia chai ya moto”

“Hahaa sijaona”

“Ngoja niiangalie kwenye simu kama ninayo nikutumie. Nipe simu yangu”

“Niliiweka chaji kwa maana niliishika asubuhi na kuikuta ikiwa na asilimia tano. Ila kwa nini mume wangu una weka ma passoword hadi ya macho kwani kunwa mtu humuamini?”

Tina alialalama huku akinikabidhi simu yangu.

“Una taka kuiona clip au una lalamika juu ya passoword zangu?”

“Yaishe sitaki kukukera bwana. Kunywa chai tende clinic asubuhi hii”

“Kufanya nini?”

“Una hisi Rashidi hii mimba nina ielea kimungu Mungu si ndio. Ina bidi nipate uangalizi wa kidaktari sihitaji sihitaji siku mimba yangu iweze kutokana bwana wala kukumbwa na matatizo yoyote”

Nikamatazama Tina kwa mara kadhaa. Akaanza kukata kipande cha chapati katika sahani hii na kunilisha.

“Kula bwana mume wangu. Kama nimekuudhi nisamehee”

“Nitakula mwenyewe”

Nilizungumza huku nikianza kula taratibu. Baada ya kumaliza kula tukaingia bafuni, tukaoga kwa pamoja kisha tikajiandaa kwa ajili ya safari ya kuelekea hospitalini. Tukaagana na mama mkwe na tukaondoka nyumbani hapa.

“Hujafurahia kuongana na mimi?”

Tina alivunja ukimya mara baada ya ukimya kutawala ndani ya gari hili kwa dakika kama tano.

“Ndio unacho kiwazia?”

“Ndio Rashidi. Umekuwa ni mkimya, umekuwa ni mtu ambaye hutaki kuniongelesha. Una tatizo gani lakini”

“Nisikilize kichwa changu kina waza mambo mengi”

“Kama?”

Tina alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama.

“Nimemuua DON”

“Waoooo hilo ni jambo zuri na la kumshukuru Mungu kwa maana yule mshenzi alitusumbua sana mume wangu. Alikufanya uwe ni mtu wa mawazo”

Tina alizungumza kwa furha huku akinitazama machoni mwangu.

“Mbona ufurahii kuna nini?”

“Una jua Don ni nani?”

“Una maanisha nini kusema ni nani?”

“Nimekuuliza una jua ni nani?”

“Ndio si adui yako?”

“Ni baba yangu, babu wa hao wajukuu munao kwenda kuwazaa”

Tina macho yakamtoka kwa mshangao huku akinitazama machoni. Nikasimamisha gari nje ya geti la hospiytali hii, likaufunguliwa na taratibu tukaingia.

“Sijakuelewa Rashidi una sema?”

“DON ni baba yangu mzazi, damu yangu ndio damu ya hao wajukuu zake wote hivyo hapo hakuna cha kufurahia?”

“Kivipi…imekuwaje na nani kasema?”

Tina aliuliza kwa sauti ya upole na iliyo jaa unyonge huku akinitazama usoni mwangu. Nikasimamaisha gari katika magegesho, nikafungua mkanda wa siti yangu.

“Tuingie ndani”

“Ngoja kwanza mume wangu. Sijaelewa yaani ilikuwaje kuwaje?”

“Muulize mama yako mkwe kwa maana yeye ndio mama kwani nyinyi wanawake muna siri kubwa sana nyuma ya mimba zenu hizo”

Nikafungua mlango wa gari na nikashuka. Tukaanze kutembea kuelekea eneo wanalo hudumiwa wamama wajawazito.

“Nesi huyu ndio mume wangu”

“Ohoo karibuni sana shemeji”

“Nashukuru”

Tukaka katika viti hivi.

“Vipi una endelea sasa hivi?”

“Namshukuru Mungu, ila hali ya kichomi siisikii”

“Shemeji amekuja”

“Haaaa yaani weee acha tu sio kwa kichomi kile”

“Shem pole kwa safari”

“Nashukuru sana”

“Shemeji kuna utaratibu ambao wazazi wana paswa kuchekiwa afya zao. Mara ya kwanza tulimcheki bibie haoa na tumemkuta yupo salama kabisa. Kutokana na uhitaji wa miili yenu najua hamuto jizuia hadi miezi tisa kukamilika. Hivyo kwa usalama wa mama na mtoto aliyepo tumboni ina bidi na wewe tukupime afya yako”

Nesi huyu alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake.

“Shem”

“Nakusikiliza”

“Kama upo tayari tuna weza kurudia kuwapima tena wote wawili”

Nikashusha pumzi nzinto kwani katika vitu ambavyo sipendagi kujaribisha ni kupima H.I.V kwa maana njia nilizo zipita ni nyingi sana na zote nimepita huku nikipiga show za kibabe. Show ambazo unakisugua kitumbua hadi kina waka moto,

“Sawa”

Nilizungumza kwa kujikaza.

“Katika kupima kuna majibu ya aina mbili tu. Negative na Postive…..”

“Dada hayo maelezo yote najua. Shida si kupima nipime muda wangu mchache aisee”

Nilizungumza kwa hasira kidogo hadi nesi wa watu akaanza kutetemeka.

“Baby jamani kwani si usubiri akuelekeze”

“Alafu, kuna kipi kisicho julikana kwenye H.I.V sasa hivi. Au anataka kuniambia kama nita kutwa nao nianze kula vizuri, nilale mapema nifanye mazoezi na niishi kwa matumaini. Nesi fanya shuhuli yako”

“Sawa shemeji”

Nesi huyu akavaa gloves mikononio mwake. Akachukua vipo vinavyo pimia H.I.V(H.I.V test)

“Nianze na mama au baba?”

“Mimi”

Nikanyoosha mkono wangu wa kulia. Akanichoma sindano akachukua damu kiasi na zoezi hilo nalo likafanyika kwa Tina.

“Ina chukua muda gani?”

“Dakika kadhaa wala usijali shemeji”

“Poa”

Baada ya muda kidogo nesi akanyanyuka na kuviangalia vipimo vyetu sehemu alipo viweka. Akachukua karatasi mbili na akaanza kuziandika andika kisha akarudi katika kiti chake huku akitutazama kwa nyuso za simamzi hadi nikatamani ninyanyuke na kuondoka eneo hili kwani kwa umalaya nilio ufanya nikikosa hirusi basi itakuwa ni ngekewa kwa upande wangu.



“Majibu yenu yapo tayari, je mungependa nimpe mmoja mmoja au wote kwa pamoja?”

“Kwani ulitumipa kila mtu kwa muda wake. Tuambie nini kinatusumbua”

“Majibu yenu yapo vizuri. Wote muna onekana hamuna virusi vya ukimwi. Hongereni sana”

Nesi huyu alizungumza huku akiwa na tabasamu. Tina akashusha pumzi nyingi huku akimtazama nesi huyu.

“Yaani ulivyo weka sura ya huzuni nikajua kwamba ndio hivyo mambo yamekuwa sio mambo”

“Hamna nilitaka kuona sura zenu zina bebaje jambo hili.”

Simu yangu ikaanza kuita, nikaitoa mfukoni na kuona namba ya mama.

“Mkweo”

Nilizunguzma huku nikipokea simu hii.

“Mama nita kupigia”

“Nisikilize Rashidi kwa umakini, mwanao ametekwa, nilikuwa naye hapa dukani, gari moja nyeusi imekuja na kumnyakua. Tafadhali nisaidie”

Mama alilalama na kunifanya nisimame kwa kasi kama msumari.

“Umesemaje?”

“Shamsa ametekwa na watu wasio julikana.”

“Upo wapi wewe?”

Nilizungumza huku nikianza kutoka ndani hapa kwa mwnedo wa kasi.

“Nipo huku Kinondoni madukani huku nilikuwa nimekuja naye kumcheki”

Mama alizungumza huku akilia na katika maisha yangu sijawahi msikia akilia kama hivi.

“Nina kuja mud huu. Kaa hapo hapo Shabani ana kuja kukuchukua sawa”

“Sawa”

“Baby baby”

Tina alizungumza huku akinifwata ninapo elekea.

“Nisikilize Shamsa ametekwa, hivyo nahitaji kurudi Dar sasa hivi”

“Mungu wangu!! Ni kina nani hao wamefan ya hivyo?”

“Sijui nahitaji kurudi muda huu. Hapa mama amechanganyikiwa Analia lia tu”

“Sawa mume wangu wahi na kuwa makini sana usije ukapata ajali. Au nikuendeshe?”

“Hapana nitakuwa makini. Hakikisha kwamba una rudi nyumbani na nikumbushe nikuagizie gari la kukupeleka clinic sawa mke wangu”

“Sawa mume wangu. Nenda”

Nikakimbilia eneo la magesho ya magari, nikaingia ndnai ya gari langu na nikaondoka hospitalini kwa mwendo wa kasi. Nikapita katika moja ya sheli, nikajaza mafuta na nikaendelea na safari hii, huku nikiendesha mwendo wa kasi sana. Simu yangu ikaita na nikaipokea.

“Mume wangu”

Jackline alizungumza huku nikiendelea kuliendesha gari hili.

“Mupo wapi, mama amenipigia simu kwamba Shamsa ametekwa?”

“Ndio mume wangu na tupo naye hapa na shemeji hapa”

“Mpatie simu”

“Kaka”

“Mupo wapi sasa hivi?”

“Tumekuja kutoa ripoti hapa central police”

“Imejulikana hiyo gari?”

“Ndio wamechukua maelezo kwa mama hapa na wana dai wana lifwatulia gari hilo”

Nikashusha pumzi huku nikipunguza mwendo kutokana na tuta kubwa lililopo mbele yangu.

“Unaweza kuhisi ata kuwa ni nani?”

“Sijahisi chochote kaka”

“Poa mchukue mama na mke wangu na urudi nao nyumbani hakuna mtu yoyote kutoka”

“Sawa kaka”

“Mume wangu nina wasiwasi”

Jacklien alilamana.

“Usijali mke wangu atapatikana tu”

“Sawa honey upo wapi?”

“Nina kuja nipi njiani”

“Kuwa makini”

“Sawa”

Nikakata simu na kumpigia Caro.

“Honey”

“Upo wapi?”

“Nipo nyumbani bado nime lala”

“Amka nahitaji namba ya mama Shamsa”

“Kuna nini mbona una zungumza kwa hasira.”

“Shamsa ametekwa”

“Mungu wangu, ametekwa na nani?”

“Sijui ila nahitaji namba ya huyo mpuuzi”

“Sawa mume wangu na kutimia je nikusaidie kwenye nini katika hili?”

“Nahitaji kufahamu gari la walio mteka.”

“Sawa mume wangu, kwani alitekwa akiwa na nani?”

“Mama, hembu mpigie simu Shabani ata kueleza kilicho tokea”

“Sawa mume wangu”

Meseji ikaingia katika simu yangu na ikaifungua na kuona namba ya mama Shamsa. Nikamapigia simu ikapokelewa.

“Haloo”

“Nisikilize wewe mpumbavu nahisi unijui”

“Mmmmm Rashidi?”

“Ndio Rashidi, nakuambia hivi hunijui vizuri”

“Kwa nini tena?”

Mama Shamsa alizungumza kana kwamba hajui kinacho endelea.

“Nakupa lisaa moja nahitaji hao washenzi wako wamuachie mwanangu”

“Mwanao! Mwanao gani?”

“Usijifanye ujui mshenzi wewe. Shamsa ametekwa na wajinga wako sasa wewe lete upumbavu”

Nilizungumza kwa kufoka sana huku nikipiga piga mskani wa gari hili.

“Mungu wangu, usiniambie mwanangu umeshindwa kumlinda hadi akatekwa”

“Kuma**ko mseng** wewe. Unalisaa kama una taka kufa endelea kumshikili”

Nikakata simu na kuendelea kuendesha gari hii kama mwenda wa zimu. Kila mara nilijikuta niki yapita mabasi kwa spidi kubwa sana. Kuna kituo polisi walijaribu kunisimamisha ila nikapita.

“Musinisumbue na nyinyi”

Nilizungumza huku nikiendelea kuchanja mbuga. Baada ya mwendo wa kama dakika kumi na mbili hivi nikajikuta nilipunguza mwendo mara baada ya kuona gari mbili za polisi zikiwa zimefunga barabara. Huku wakiwa wamejipanga na kuninyooshea bunduki zao. Taratibu nikasimamisha gari, wakaniamrisha kwa sauti ya juu nishuke kwenye gari huku nikiwa nimenyoosha mikono juu. Nikatii amri hiyo na nikashuka katika gari huku mikono yangu ikiwa juu.

“Nina kosa gani afande?”

Nilimuulia afande mmoja anaye nisogelea huku akiwa amenielekezea bunduki yake.

“Geuka nyuma”

Askari huyu alizungumza na nikatii huku nikitazama lori linalo kuja kwa mwendo wa kasi. Lori hili linalo shuka kwenye mporomoko nikagundua kwamba limefeli breki kwa maana spidi yake ina ongezeka kila linavyo zidi kushuka.

“Huyu vipi?”

Askari alijikuta akishikwa na mshangao huku lori hili likizidi kutusogelea na dereva huyu wa lori amelenga gari langu.

“Ohhoooooo”

Nikamsikia askari akizungumza na akakimbilia pembezoni mwa barabara. Mwenye lori hili akazidi kujitahidi kukwepa gari langu, nami mikajirusha pembeozoni mwa barabara. Kwa bahati nzuri lori hili la vinywaji likakwepa gari langu na kuzivaa gari za polisi na kuzitawanyisha na kusababisha lori hili kuanguka chini na vinywaji vyote vikatapakaa barabarani. Nikaingia ndani ya gari langu kwa haraka na nikaondoka eneo hili kwa mwendo wa kasi sana huku nikiwaacha askari wakipaga kwa ajali hii. Mama Shamsa akanipigia simu tena.

“Nini?”

“Rashidi najua mimi na wewe tuna mifarakano ila kusema ukweli kwenye hili jambo la shamsa sijalifanya. Haki ya Mungu nife sasa hivi, sijamteka Shamsa. Japo sikuwa mama mmbaya kwake ila sikuwahi kuwazia kumfanyia kitu kama hicho”

Mama Shamsa alizungumza hukua kilia, akanifanya niachie msunyo mkali wa hasira.

“Haki ya Mungu Rashidi niamini siwezi mteka mwanangu. Siwezi haki ya Mungu”

Mama Shamsa alilalama huku akilia.

“Una dakika chache namataka mwanangu. Haki ya Mungu nita mchukua hata huyo uliye naye. Tusileteane upuuzi wewe”

“Haki ya Mungu Rashidi sijawahi kuwaza kumteka Shamsa, haki ya Mungu niamini. Kama una taka kumchukua Ruben mchukue tu kwa sababu ni damu yako na siwezi kukukataza ila sijawahi firikia hilo unalo nihisi nalo. Niamini Rashidi”

Nikakata simu kwa maana mwendo ninao kwenda nao ni mkali sana na endapo nita fanya uzembe nita kufa. Nikafika jijini Dar es Salaam na moja kwa moja nikaelekea nyumbani kwangu na nikakutana na baadhi ya askari. Nikamkuta Caro naye akiwa hapa kitu kilicho nifanya nistuke kidogo. Jackline akanifwata na kunikumbatia huku akilia.

“Tuta fanya nini mume wangu. Mtoto wangu”

Jackline alilia kwa uchungu sana na dhauri ni kwamba ana mpenda sana Shamsa.

“Usijali nita fanya kila liwezekanalo apatikane”

“Sawa mume wangu”

“Mama yupo wapi?”

“Chumbani kwake, yupo na daktari presha imempanda”

Nikamuachia taratibu Jackline na nikapandisha garofani. Nikamkuta mama akiwa amelala kitandani huku ametundikiwa dripu.

“Mama”

“Vipi mume mpata mjukuu wangu?”

“Wana endelea kushuhulikia. Walio mteka uliwaona?”

“Niliona jinsi walimuiongiza kwenye gari na walikuwa wamevaa vinyago vyeusi kwenye nyuso zao.”

“Walikuwa na gari gani?”

“Toyota Alphad nyeusi. Mimi nilikuwa ndani ya dula la nguo. Shamsa alikuwa nje ya gari akichati chati na marafiki zake”

“Simu yake?”

“Ilianguka pale pale. Naomba umlete mjukuu wangu tafadhali Rashidi mwanangu”

Mama alizungumza huku machozi yakimwagika. Mlango wa chumba hichi ukagongwa kidogo.

“Ingia”

Caro akaingia ndani hapa.

“Dokta naomba utupishe”

Nilimuambia daktari na akatupisha.

“Shikamoo mama”

“Marahaba”

“Mama anaitwa Caro na Caro na huyu ni mama yangu”

“Nashukuru kukufahamu mama. Mimi nina itwa Caro ni mpelelezi, nina imani mtoto wetu wangu ata rudi mikooni mwakako”

“Nashukuru ila sija elewa unapo sema mwanangu”

“Najua huu sio wakati mzuri wa kukutambulisha mama. Huyu ni mdogo wake raisi aliye fariki, na hii mimba ni yangu. Una kumbuka nililiekeza juu ya hili”

“Ehee. Ahaaahaa ndio wewe?”

“Ndio mama”

“Naomba unisaidie mjukuu wangu apatikane, jamani yule ndio mjukuu wangu wa kwanza”

“Ata patikana mama hakuna tatizo juu ya hilo”

“Asante”

“Mimi natoka nipo nje”

“Sawa”

Caro akatoka ndani hapa na nikabaki na mama.

“Walio mteka walikuwa wangapi?”

“Mimi niliona watatu, na kuna dereva wa gari hiyo jumla ni wanne.”

Nikashusha pumzi huku nikijiuliza mara mbilimbili ni nani amehusika kwenye kumteka mwanangu. Simu yangu ikaanza kuita, nikitoa mfukoni na kuona namba ya Tina.

“Vipi?”

“Umefika mume wangu”

“Ndio nita kupigia’

“Sawa mume wangu, nina wasiwasi naomba unijulishe kila kinacho endelea”

“Pao”

Nikakata simu.

“Maadui zako kweli hawawezi kumteka mjukuu wangu?”

Mama alilalama.

“Sina adui kwa sasa?”

“Huna kweli wewe?”

“Ndio mama, adui yangu mkubwa alikuwa ni Don. Sasa Don hayupo kwa sasa nani amehusika. Mimi nahisi ni mama yake mshenzi yule”

“Sidhani, hakuna mama ananaweza kufanya upuuzi kama huo”

Mlango ukafungulia na akaisngia shemeji, mke wa shabani.

“Shem njoo njoo watu wako wana uwana huku”

Nikasimama kwa haraka na tukatoka chumbani hapa huku tukipishana na dokta akiingia ndani hapa ili kumuhudumia mama. Nikashuka katika ngazi kwa haraka na kumkuta Shabani akiwa ameshikilia Jackline aliye fura kwa hasira huku baadhi ya askari wakiwa wamemshikilia mama Shamsa ambaye naye amefuraha kwa hasira huku nywele zake zikwia zimechangukana na wanarushiana matusi kana kwamba ni wamama wa uswahilini.



“Waachieni”

Kauli yangu ikawashagaza watu wote waliopo sebleni.

“Nimesema waachieni na kama muna taka kupigana njooni huku”

Nilizungumza huku nikitangulia kutoka nje.

“Kaka una fanya nini?”

“Hawa ni maadui na kila mtu ana hasira na mwenzake. Njooni nje hapa kuna uwanja mkubwa. Mupigane atakaye shindwa ata muheshimu mwezake”

“Rashidi acha uchizi”

Mama Chausiku alizungumza huku akinitazama.

“Sio uchini mama. Nina jua nini ninacho kifanya. Haiwezekani watu wazima wenye watoto wapigane kwenye kipindi kigumu kama hichi cha mwanangu kupotea. Si wanataka kupigana njooni”

“Twende nikakuonyeshe mimi ni nani malaya mkubwa wewe”

Mama Shamsa alizungumza huku akijotoa mikoni mwa walinzi wake. Jackline akanitazama na nikampa ishara ya macho kwamba nime mruhusu kupigana na huyu mwenda wazimu. Shabani taratibu akamuachia na watu wote tukatoka nje na tukasimama kwenye bustani kubwa ya maua huku tukiwatazama. Mama Shamsa akampiga Jackline kibao kizito kilicho mfanya Jackline kukisikilizia kwa sekunde kakdhaa. Mama Shamsa akajaribu kumfwata Jackline ila safari hii akakutana na ngumi mbili nzito za uso na kumfnaya apoteze muelekeo. Akapigwa mtama na kuangushwa chini na Jackline akamkalia tumboni mwake na aakaanza kumtandika vibao. Mama Shamsa akajaribu kujinasua mikononi mwa Jackline ambaye ni mwaka kick bokxer, ila akashindwa.

“Nisamehe, nisamehe”

Mama Shamsa ilibidi akiri kushindwa kwani mdomo mweingi nguvu hana.

“Utamuheshimu mume wangu?”

Jackline alizungumza huku akiwa amemuelekezea ngumi ya kichwa.

“Ndio nita muheshimu”

“Una uhakika?”

“Ndio”

“Mwanangu yupo wapi?”

“Sijui”

“Nani amemteka mwanangu?”

“Haki ya Mungu sijamteka na sijui alipo, kweli vile”

“Hii ni kwa ajli ya kumdharau mama mkwe wangu”

Jakcline akaishusha ngumi yake usoni mwa mama Shamsa na kumfanya atulie tuli. Taratibu Jackline akanyanyuka na waloinzi wa mama Shamsa wakaanza kumnyanyua mpiganaji wao ambaye bado ana sikilizia maumivu ya kupigwa huko.

Jackline akaondoka eneo hili na kuwaacha waacha watu wakimsindikiza kwa macho.

“Shem yupo vizuri”

Shabani alizungumza hukua akinitazama machoni mwangu

“Mpiganaji huyo, huyu mpuuzi amejichanganya”

“Kiherehere kime muisha kwa maana yeye ndio alikuwa ni mchokozi.

“Hawa askari wamesemaje”

Nilimuuliza Shabani huku nikimtazama usoni mwake.

“Ndio wana fwatilia hawa wapo hapa kwa ajili ya ulinzi kwani wana hisi watekaji wana weza kuja kuvamia hapa”

Nikashusha pumzi huku nikimtazama Shabani usoni mwake.

“Kaka kwani huisi adui yoyote?”

“Niliye kuwa nina muhisi ni huyu mama Shamsa, ila umeshuhudia alicho ulizwa na kujibu”

“Ila ana weza kutuigizia?”

“Sidhani ila kama ata igiza”

“Ila kumbuka kaka alicho tufanyia kwenye ile nyumba pale. Wewe mwenyewe uta weza kuona namna alivyo tengeneza dili na yule mzee hadi wakafikia hatua ya kutaka kutiingiza mjini”

“Ngoja tuone. Unajua watekaji kama wata kuwa ni watu wanao hitaji pesa wata tupigia. Na sidhani kama kuna jambo jengine tofauti na pesa”

“Sawa kaka tumuombe Mungu”

“Poa ngoja nikamuen Jackline”

“Hakuna shaka kaka”

Nikaingia ndani na moja kwa moja nikapitiliza chumbani kwangu nikamkuta Jackline akiwa amekaa katika moja ya sofa huku akinywa wyne.

“Hei”

NIlizungumza kwa sauti ya upole huku nikikaa pembeni yake. Akashusha pumzi nyingi huku akinigeukia.

“Ameondoka?”

“Bado yupo?”

“Naomba umuondoke nyumbani kwangu”

“Ila yule ni mpuuzi wala usiumize kichwa mke wangu?”

“Rashidi mimi ni mke wako wa ndoa. Siwezi kukaa katika nyumba moja na mwanamke wako wa zamani. Mwanamke amabaye hana heshima. Ana hisi kila mtu ni malaya, ana nitukania mama yangu, ana mjua mama yangu yule ehee.

Jackline alizungumza kwa kufoka.

“Najua amekukera mke wangu ila punguza jazba”

“Rashidi nina kupenda ten asana. Ila maisha haya ya kipumbavu siyawezi. Yaani nina tukanwa mbele ya wanangu. Unahisi wanangu wata jifunza nini. Nimekaa na Shamsa miaka yangu yote, nina uchungu naye kama ilivyo kuwa kwa hawa wangu wawili. Sijawahi kumnyanyasa wala kumuonyesha kwamba mimi si mama yake wa kumzaa. Nilimpa upendo halisi, upendo ambao watoto wengi wa kambo wana uko kwa mama wa kambo. Leo hii nina lipwa matusi, nina tukaniwa hadi makaburi ya ndugu ukoo wangu. Ana nijua mimi, ana hisi mimi ni mpumbavu au mjinga siwezi kuumia eheee?”

Jackline aliendelea kufoka hadi machozi yakaanza kumwagika usoni.

“Sipendi kudharauliwa Rashidi, sipendi mwanamke mwenzangu, ambaye an akum** kama mimi. Mazima kama mimi anidharau. Tafadhali Rashidi, kamuondoe yule malaya, asinichukuli mimi poa. Mimi ni mwanamke mbaya kuliko anavyo jifikiria. Nina uwezo wa kupigana na wanauem hata wanne wenye miraba sita na sio mwanamke mwenye maziwa kama mimi.”

Jackline aliendelea kulalama.

“Nisikilize mke wangu?”

“Rashidi sina cha kukusikiliza. Mimi ni nani kwako?”

“Mke wnagu?”

“Nini kina kunfanya una pata kigugumizi cha kwenda kumfukuza. Au una mpenda?”

“Hapana mke wangu nina mpendaje mshenzi kama yule”

“Basi kama hutaki kumfukuza niache niaondoke. Uta nifwata Ufaransa”

“Usifike huko, yeye ni nani hadi aukuondoke hapa nyumbani kwako”

“Basi kamuondoe tafadhali”

Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama Jackline usoni mwake. Kusema kweli toka nimfahamu Jackline sijawahi muona akiwa na hasira kwa kiwango hichi. Nikapiga hatua mbili simu yangu ikaanza kuita, nikaitoa mfukoni na kuona namba ngeni. Jackline akanitazama huku nikiipokea simu hii na kuiweka sikioni.

“Haloo”

“Naomba unisikilize”

Nilisikia sauti nzito na mbaya mbaya.

“Ndio nakusikia”

“Nina mwanao Shamsa, ninacho kihitaji ni kunipatia utajiri wote wa DON”

Nikaiweka simu hii loud speaker ili Jackline nay eye aweze kusikia nilicho elezwa.

“Umesema?”

“Nahitaji unipoatie urithi wa mali zote za DON la sivyo mwanao uta kikuta kichwa chake”

“Mupo wapi niwaletee”

Jackline kwa haraka akasimama na akanisogelea nilipo simama huku akiwa na wasiwasi.

“Don gani?”

“Usijifanye ufahamu chochote. Nina tambua kwamba Don ni baba yako na amekurithisha kila kitu chako”

“Sijui una zungumza nini?”

“Baba….baba….baba”

Nilisikia sauti ya Shamsa ikatufanya tustukee sana.

“Mtoto wenu ana masaa kumi na mbili ya kuwa hai. Zaidi ya hapo muta kuja kuchukua kichwa chake”

“Mupo wapi niwaletee?”

Jackline alianza kuzungumza kwa wasiwasi.

“Weee ni nani?”

“Mimi ni mama mzazi wa Shamsa tuambie ni wapi tukuletee hizo faili”

“Ohoo wewe ndio Jackline?”

“Ndio mimi”

“Tupo mpakani mwa Kenya na Tanzania. Eneo moja linaitwa Horohoro. Hakikisha mukija muna kuja mukiwa nyunyi peke yenu. Endapo muta kuja na askari wa aina yoyote mtoto wenu ata kuwa maheremu. Tuna elewana?”

“Ndio, tukutane saa ngapi?”

Niliuliza huku mapigo yangu ya moyo yakinienda kasi sana kwa hasira.

“Mutakapo fika Hororo yiyi tuambieni tu”

“Sawa”

Simu ikakatwa na tukatazamana na Jackline.”

“Jiandae tuondoke”

NIlimuambia Jackline kwa maana mejifunga taulo tu. Akafungua kabati na kwa haraka akavaa nguo zake.

“Utanikuta nje, angalizo hakuna kumuambia mtu wapi tuna kwenda.”

“Sawa mume wangu”

Nikatoka ndani hapa nikamuita kwa ishara Shabani akanifwata nje.

“Vipi kaka”

“Nina toka na shemeji yako. Hakikisha amani ina kuwa salama hapa ndani”

“Una kwenda wapi?”

Nikashusha pumzi nyingi huk nikimtazama Shabani ambaye ni mtu wangu wa karibu sana na ana nitunzia siri za mambo mengi.

“Naelekea Horohoro”

“Kuna nini?”

“Watu walio mteka Shamsa kwa sasa wapo Horohoro, hivyo ina bidi niende mimi na shemeji yako”

“Kwenda nyinyi wawili ni hatari kaka. Tuwashirikishe askari?”

“Tena nina kuomba kwenye hili usidhubutu kumueleza mtu. Sawa, yule ni mwanangu, acha nikafanye ninacho kifanya sawa”

Nilizungumza kwa msisitizo hadi Shabani akatingisha kichwa akimaanisha amenielewa.

“Ukimuambia yoyote, haki ya Mungu tuta gombana”

“Nimekuelewa kaka”

“Nahitaji silaha umeziweka wapi?”

“Zipo kwenye chumba cha siri”

“Kaniletee bastola pamoja na bunduki kubwa”

“Sawa”

Jackline akatoka ndani hapa huku akiwa ameshika fili mkononi mwake.

“Kila kitu kupo tayari?”

Jackline alizungumza huku akifungua mlango wa gari na kuingia ndani. Shabani akato akiwa na bagi la mgoni na akanikabidhi.

“Bunduki kubwa imetengenishwa tengenishwa hivyo una weza kuiunga. Bastlola pia ipo ndani”

“Nashukuru”

“Mama nimuambie mume kwenda wapi pamoja na hawa watu?”

“Waambie kwamba kuna swala tuna shuhulikia”

“Ila wana weza kuhoji mengi?”

“Wajibu unacho weza ila mengine sihitaji uwaambie”

“Sawa kaka”

“Kuwa makini na huyu fala pamoja na watu wake”

“Sawa kaka”

Nikaingia ndani ya gari na tukaondoka nyumbani hapa.

“Umeba nyaraka zote?”

“Ndio baby”

“Ni nani anaye fahamu kwmaba nime muua Don?”

“Sijui baby kutakuwa na mtu ambaye ana kufwatilia”

“Nani?”

“Sijui ni nani mume wangu ila tukienda huko tuta jua”

“Hizo hati halisi?”

“Ndio mume wangu”

“Fungua katika hilo begi humo kuna bunduki nahitaji uiunganishe”

Jackline akafungua mkanda wa siti lake na akahamia siti ya nyuma na akaanza kuiunganisha bunduki hii kubwa yenye uwezo wa kumuua mtu aliyopo eneo la mbali sana(sniper gun). Baada ya kumaliza akaiweka siti ya nyuma na akarudi kukaa siti ya mbele. Ukimya ukatawala ndani ya gari hili.

“Baby”

“Naam”

“Naomba unisamehe”

“Kwa?”

“Kukuongelesha kwa hasira”

Nikamtazama Jackline huku nikimtazama usoni mwake.

“Una haki ya kuwa na hasira ila nisamehe mimi ambaye nilishindwa kumzuia yule mshenzi kuja nyumbani”

“Huna kosa kwa manaa nina imani sio wewe uliye mleta pale nyumbani”

“Ndio mke wangu”

“Watu wa DON una wafahamu?”

“Wachache sana na sina kumbukumbu nao vizuri”

“Ila mtoto wangu ni muhimu kuliko mali”

“Nalifahamu hilo mke wangu ila hatuwezi kuwapa kirahisi namna hiyo”

“Mume wangu usije ukahatarisha maisha ya mtoto.”

“Wewe niamini. Una weza kutumia hiyo bunduki?”

“Ndio”

“Kiufasahau?”

“Ndio mume wangu. Kule kutekwa na Don na kupelekwa Somali niliweza kujifunza mambo mengi sana mara baada ya kurudi Ufaransa na ilibidi nipate mafunzo ya kijeshi kwa miezi sita hivyo najua kutunia hiyo bunduki”

“Basi tukifika eneo hilo tuta jua nini cha kufanya”

“Sawa mume wangu”

“Ayaaa”

“Nini tena honey”

“Ina bidi tubadilishe gari”

“Kwa nini?”

“Hii gari wana ifahamu hivyo ina weza kuwa hatari kwa sisi”

“Sasa gari tutapata wapi mume wangu?”

“Ina bidi tununue nyingine?”

“Nyingine ya nini tena mume wangu. Ikiwa ina tupasa kumpata mtoto”

“Nisikilize mke wangu. Nilipo kuwa nina rudi Dar es Salaam. Niliwatoroka maaskari hivyo hii gari wana weza kuwa wana iwinda barabarani. Je kipi bora, kukamatwa na kupotezewa muda na mbaya tuna silaha hizo hapo nyuma na hazina vibali. Au tubadilishe gari?”

“Mmmmmm sawa tubadilishe gari tu, kwani hayo matatizo mengine yana weza kuwa makuhwa kuliko lililopo mbele yetu”

Nikageuza gari na tukarudi kwenye moja ya show room ya magari ambayo tuliipita. Moja kwa moja tukaelekea kwa muuzaji.

“Nahitaji hii Lexux LX 570”

Nilimuambia muuzaji huyu huku nikionyesha gari hii mpya na kwa kawaida ni magari ya garama sana.

“Sawa bossi”

“Tupatie namba ya kulipia na nahitaji usajalili wote ukamilike ndani ya muda mfupi. Na hii gari yetu tuta iacha hapa na atakuja kuichukua mmoja wa watu wangu”

“Sawa boss”

Nikakabidhiwa akaunti namba na nikalipia gari kiasi wanacho kihitaji. Usajili wote wa kiserikali ukakamilika ndani ya muda mfupi, nikampigia simu Shabani na kumueleza ni wapi tulipo iacha hii BMW X5 na sisi tukaingia ndani ya gari hili jipya tukiwa na bunduki hizi na nikaondoka eneo hili kwa mwendo wa kasi huku nikiwa na uchu mkubwa sana watu walio mteka mwanangu kwani katika maisha yangu ni bora ukacheza na mimi kuliko ukacheza na maisha ya watoto wangu au mke wangu.




“Baby unaendesha rafu. Kuwa makini”

Jackline alizungumza mara baada ya kuona nina yapita magari kadhaa bila ya mpangilio wa kuangalia kama kuna kona hatari au gari mbele yetu.

“Nahitaji kwuahi”

“Sawa tuna wahi ila kumbuka tukipata ajali hata huko tunapo kwenda hatuto fika huko tunapo kwenda mume wangu”

“Nimekuelewa”

“Hiyo sehemu tunapo kwenda una ifahamu?”

“Ndio”

Tukafanikiwa kufika jijini Tanga na moja kwa moja tukaeleka katika mji wa Horohoro ambao ni mpakani mwa Tanzania na Kenya. Nikasimamisha gari pembezoni mwa barabara, nikaichomeka bastola yangu kiuono mwangu.

“Nahiataji kwuapigia ili kufahamu kwamba wapo wapi”

“Sawa mume wangu”

Simu ya watekaji ikaanza kuita na baada ya muda ikapokelewa.

“Wapo tufike”

“Vukeni boda”

“Hatuna vibali?”

“Basi hatuwezi kukutana”

“Nhgoja kwanza umetuambie tukutae Horohoro na sasa hivi nipo Horohoro una niambia nivuke boda ikiwa hati ya kusafiria nimeiacha nyumbani”

“wewe ni mwanaume una weza kujiuongeza na ukifika hapo Boda uta ona gari nyeusi aina ya Mark X ingia ndani ya gari na utakuta dereva ata kuleta hadi tulipo”

“Sawa”

Simu ikakatwa na kunifanya nishushe pumzi.

“Wana semaje?”

“Tuvuke boda”

“Passport zitakuwaje?”

“Ngoja”

Nikaendesha gari hadi eneo la ofisi askari wa uhamiaji. Nikafungua wallye yangu na kuona ina dola elfu moja na mia mbili.

“Nisubirie”

“Sawa mume wangu”

Nikashusha ndani ya gari, nikaingia katika moja ya ofisi.

“Habari yako afande”

Nilimsalimia askari wa kike ambaye nimekuta eneo hili.

“Salama nikusaidie nini?”

“Naweza kuonana na mkuu wako”

“Kwa nini ukutane naye?”

“Ahaa nahitaji kuzungumza naye”

Askari huyu wa uhamiaji akanitazama.

“Tafadhali”

“Hayupo”

Nikaingiza mkono wa suruali na kutoa elfu kumi n akumkabidhi kisiri. Akanitazama kisha akanyanyua mkonga wa simu na kumpigia bosi wake.

“Mkuu kuna mgeni”

“Sawa”

Akakata simu.

“Msubirie hapo kwenye kiti”

Kutokana nina shida na mkuu wake ikabibidi nikae tu kwani sihitaji kwenda moja kwa moja kwa askari wapiga mihuri wana weza kunisumbua sana. Baada ya dakika tano mlango wa kamishina huyu wa uhamiaji ukafunguliwa na akatoka mwana mama mmoja.

“Mgeni yupo wapi?”

“Ni huyu kaka”

“Karibu”

Nikanyanyuka na kumfwata mwana mama huyu.

“Karibu ukae tukusaidie nini?”

“Nashukuru, naitwa Rashidi nahitaji kuvuka mpaka mara moja ila kwa bahati mbaya mimi na mke wangu tumesahau hati za kusafiria Dar es Saalam”

“Sasa ndugu yangu kama umesahau hati ya kusafiria ume kuja kufanya nini huku. Ikiwa ulitambua kabisa kwamba kuna safari ya kuja kuvuka nje ya mji”

“Tafadhali nina omba unisaidie kwenye hilo”

“Umekuja na usafiri gani?”

“Hiyo Lexus hapo nje”

Mwanamama huyu akanyanyuka na akachungulia dirishani kisha akarudi kwenye kiti,

“Ni yako?”

“Ndio”

Akanitazama kuanzia kwa umakini sana.

“Nisaidie nami nikusaidie”

Nikafungua wallet na kuweka dola mia nne mezani kwake.

“Ahaa boss, gari hiyo na hichi ulicho kiweka haviendani”

Nikaongeza dola mia nne nyingine”

“Hapo sawa”

“Nipo mimi na mke wangu”

“Ehee nikajua mwenyewe”

“Naomba unisaidie kuna swala muhimu sana nina kwenda kulishuhulikia”

“Ongeza kiasi kingine bwana”

Mwana mama huyu alizungumza huku akitabasamu. Nikaongeza dola mia mbili nyingine na kumfanya atabasamu.

“Majina yenu”

Nikamtajia majina yetu kamili, akatuandikikia passport za muda zinazo tuwezesha kuvuka na kuingia nchini Kenya n ahata katika mpaka wa Kenya na hatu tosumbuliwa na maofisa wa uhamiaji wa nchi ya Kenya. Nikamtoa dola mia mbili nyingine.

“Sihitaji gari yangu kukaguliwa hivyo hiyo naomba unisafishie njia”

“Mmmm ume beba nini katika gari lako?”

“Hakuna cha maana”

“Nahitaji kuliona kwa maana hii ni dhamana na endapo chochote kikitokea ina weza kula kwangu”

Nikashusha pumzi.

“Nakuomba”

“Mimi na wewe ni marafiki twende kwenye gari lako nione la sivyo biashara itaishia hapa”

Mwana mama huyu alizungumza kwa msisitizo na kujikuta nikishusha pumzi nyingi sana.

“Sawa”

Tukatoka ofisini hapa na tukaongozana hadi kwenye gari.

“Fungfua nyuma”

Mwana mama huyu alizungumz anan ikafungua mlango wa nyuma kabisa wa gari hili na hakuona chochote.

“Fungua mlango huu”

Kidogo wasiwasi ukanipata kwa mane eneo hili la nyuma ndipo tulipo iweka bunduki. Nikafungua na nikashangaa baada ya kuto iona bunduki. Jackline akatutazama.

“Habari yako”

Mwana mama huyu alimsalimia Jackline.

“Salama”

“Safari njema”

Mwana mama huyu akaturuhusu kuondoka. Tukapita getini na kugongewe mihuri ya kuvuka na tukaingia nchini Kenya. Tukatembea kama kilomita moja na tukaioan gari nyeusi aina ya Mark X, yenye rangi nyekundu ikiwa imesimama pembezoni mwa barabara.

“Gari ni ile pale”


Nilizungumza huku nikipunguza mwendo wa gari na kusimama.

“Bunduki umeiweka wapi?”

“Niliichangua na kuiweka ndani ya begi.”

“Sasa nita hitaji uifwatilie gari hii kwa umakini wasijue”

“Sawa mume wangu”

“Naomba hizo hati”

Jackline akanikabidhi hati kisha tukayonyana denda na nikashuka katika gari hili. Nikaanza kutembea kama dakika tano hivi na nikaifikia gari hii. Nikamkuta dereva wa gari hili akiwa amejilaza kwenye siti. Nikamgongea.

“Hei”

Dereva akashusha kioo kidogo.

“Naamini ni wewe uliye ambiwa unichukue”

Dereva akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akachukua picha iliyopo pembeni mwa siti yake akanitazama na nikajiona na picha hii imepigwa siku ambayo nilikuwa na Shamsa.

Dereva akashuka ndani ya gari

“Nyoosha mikono juu”

Nikatii amri ya jamaa huyu, akanipapasa na akaitoa bastola yangu kiunoni na kuichomeka kiunoni mwake.

“Ingia upande huo wa agri. Endapo uta fanya ujinga wowote uta kufa wewe na mwanao””

“Sawa”

Nikaingia upande wa pili wa gari na taratibu tukaondoka eneo hili kwa mara kadhaa nina angalia katika kioo cha pembeni mwa gari ili kuliangalia gari analo endesha Jackline ila silioni. Gari ikaacha barabara ya lami na ikaingia katika barabara ya vumbi na safari ikaendelea, tukaanza kuingia kwenye misitu mikubwa na kadri tunavyo kwenda ndiyo jinsi ninavyo shindwa kuiona gari anayo endesha Jacklie.

“Ina chukua muda gani kufika”

“Tulia kwani tatizo lako ni nini?”

“Hapana nime uliza tu”

“Tulizana”

Safari ikazidi kusonga mbele. Tukafika katika eneo moja ambalo kuna kiwanda cha kutengeneza mbao.

“Tumefika”

Jamaa huyu alizungumza huku tukishuka katika gari. Tukashuka katika gari hili.

“Nifwate”

Nikaanza kumfwata kwanyuma.

“Simama hapa”

Nikasimama katika mzigo mmoja wa wa magogo mengi yaliyo pangwa kimo cha basi la abiria. Nikaona kundi kubwa la walinzi wenye asili ya Kimexco wakitoka kwenye moja ya nyumba iliyo tengenezwa kwa mbao. Akatoka mzee mmoja mnene kiasi huku mkononi mwake akiwa ameshika mkongojo, na mkono wake wa kulia akiwa ameshika sigara kubwa.

“Rashidi pole sana kwa safari”

Mzee huyu alizungumza huku akiwa amesimama mita ishirini kutoka sehemu nilipo huku walinzi wake wakiwa wametuzunguka na mikononi mwao wana bunduki.

“Mwanangu”

“Nahitji nyaraka za mali zote za Don kwa maana najua umesha muua baba yako”

“Sihitaji mali zake kwa maana nina zangu”

“Hili mimi sijali, ninacho jali ni kuziweka sahihi karatasi hizo kisha unikabidhi”

“Nahitaji kumuona mwanangu”

Mzee huyu akanyoosha kidole chake juu na nikamuona Shamsa akitolewa katika nyumba hiyo huku akiwa amefungwa mikono yake pamoja na mdomo wake. Jamaa huyu aliye mtoa ni mrefu na amejazi mwili wake mithili ya mwana myereka Big Shoo.

“Mwanao alikuwa muongeaji sana ndio maana tume mfunga hivi”

“Sawa pen”

Mzee huyu akachomoa Pen katika mfuko wake wa Kaunda suti aliyo vaa na akanirushia.

“Wewe ni nani?”

“Swali zuri. Don alikuwa ni mtu wangu wa karibu. Nilisimamia mali zake kwa kipindi cha miaka thelathni sasa. Nimefanya naye mambo mengi sana ila alinikera alipo amua kukuandikisha wewe ikiwa hukuwahi hata kutusaidia kwenye jambo moja zaidi ya kutupa hasara ya kuwaua watu wetu”

Nikaiokota kalamu hii, nikatoa hati hii ambayo nikitia sahihi basi nina mpa mali zote za DON jamaa huyu.

“Unaitwa nani?”

“Kulifahamu jina langu sio jambo muhimu”

“Nahitaji kufahamu?”

“Rabit”

“Panya?”

“Vvyoyote utakavyo niita yote ni majina yangu”

Jina hili sio geni masikoni mwangu kwani, kipindi nipo chini ya Don nilisikia mara kadhaa akizungumza na mtu anaye itwa Rabit, kumbe ndio huyu.

“Sawa”

Nikatia sahihi kwenye hati hizi zote nne.

“Namuhitaji mwanangu”

Akampa ishara mtu huyu na kijana wake mmoja akanisogea na nikamkabidhi karatasi hizi. Akazisimsoma.

“Ni zenyewe mkuu”

Shamsa akaachiliwa na akanikimbilia hadi sehemu nilipo simama. Akanikumbatia kwa furaha. Galfa kijana aliye shika nyaraka za mali kichwa chake kikatengenishwa na kiwili wili jambo lililo wafanya watu kupagawa. Nikambebea Shamsa na nikakimbia kwa kasi hadi zilipo anguka nyaraka hizi. Nikaziokota huku nikiendelea kushudia namna wanavyo pigwa risasi na wana piga risasi kwa kuchanganyikiwa kwani eneo hili limezungukwa na miti mirefu na hawajui ni wapi risasi hizo zinapo tokea.

“Mfwateni yuleeee”

Rabit alizungumza huku akiwa amejibaza kwenye baadhi ya magogo.

“Jibanze hapo”

Nilizungumza huku nikimshusha Shsma chini na akajibanza kwenye magogo haya. Nikaruka sarakasi kdahaa na nikampiga teke la kifuaa mmoja wa jamaa na akaanguka chini, kitendo cha kutua chini, nikaokota bunduki yake nikabingiria hadi kwenye magogo nilipo muacha Shamsa. Wingi wa magogo ya eneo hili ukatufanya majibizano ya risasi yawe ni ya kuviziana kwani sote tumejificha. Nikamtazama Shamsa usoni mwake namna anavyo nitazama kwa ujasiri pasipo kuwa na woga.

“Upo salama mwanangu”

“Sawa baba”

Nikajaribu kutazama kwenye misitu hii ili kuona ni wapi Jackline alipo jivicha na kufanya mashambulizi haya ila nikashindwa. Nikamuona Rabit na vijana wake wawili wakikimbilia ndani ya nyumba hiyo ya mbao. Kijana wake mmoja akapigwa risasi ya mhuuni na mguu wake ukakatika na akaanguka chini. Rabi akajirusha ndani ya nyumba hiyo pamoja na kijana wake. Nikamalizia kwa risasi jamaa huyu huku watu wegine wa Rabit wakiwa wamesha kufa.

“Panda mgongoni”

Nilizungumza huku nikichuchumaa kidogo na Shamsa akanidandia mgogoni. Nikaanza kukimbilia katika nyumba ambayo Rabit ameingia.

“Lazima na huyu afe ata tusumbua.”

Nilizungumza huku nikijibaza katika eneo la kuingilia mlangoni.

“Nisubirie hapa”

Nikamshusha Shamsa chini na nikaingia kwa kasi ndani hapa nikaona mfuniko wa kuingilia chini ya ardhi ukiwa wazi. Nikaona ngazi za kushuka chini ya ardhi, nikataka kushuka ila nikakumbuka mwanangu yupo mwenyewe na pia hati za umiliki ninazo. Nikatoka nje, nikamshika mkono Shamsa na tukaingia katika gari ambayo nilijia eneo hili na kijana wa Rabit. Nikaigeuza kwa kasi tukaondoka eneo hili. Nikaanza kuifwatisha barabara gtulio jia na nikaliona gari nikapunguza mwendo.

“Baba mbona una simama”

“Gari yetu hiyo”

Nikamuona Jackline akijitokeza katika msitu huu huku mikono yake ikiwa juu. Nyuma yake yupo jama mmoja mwenye mwili mkubwa na amemuwekea bunduki ya kichwani jambo lililo sababisha mimi na Shamsa kustuka sana.



“Mama”

Shamsa aliita huku akipagawa.”

“Usishuke ndani ya gari”

Nilizungumza huku nikimzuia Shamsa. Nikashuka ndani ya gari hili huku mikono yangu ikiwa ipo juu huku mkono wa kushoto nikiwa nimeshika hati za umiliki wa mali za Don.

“Najua nini unacho kihitaji, muache aende chukua hati”

Nilizungumza huku nikimtazama Jackline pamoja na mtu huyu.

“Amewau ndugu zangu hivyo sihitaji hizi nyarak…..”

Kabla hajamalizia sentensi yake Jackline akampiga kisukusuku cha sehemu za siri na kumfanya agugumie kwa maumivu, nikakimbai kwa kasi ya ajabu kitendo cha kumfikia karibu nikarusha teke lililo ipiga bunduki yake na ikaangukia pembeni.

“Nenda kwenye gari?”

Nilimuambia Jacklien huku nikinimtazama usoni mwake.

“Tuna pamaban pamoja”

Jackline alizungumza huku akikunja ngumi. Jamaa hili refu na lenye miraba minne, likakunja sura huku likitutazama kwa macho ya hasira. Nikaitama bunduki yake ilipo angukia na kwa bahati mbaya imea gukia eneo mbali kutoka sehemu tulipo. Nikampa ishara ya macho Jackline ya kuiwahi kuiokota bunduki hiyo huku nami nikijiatahidi kulizua jitu jili kuisogela familia yangu sehemeu ilipo. Jackline akafanikiwa kuikota bunduki ya jitu hili. Jitu hili likarusha ngumi iliyo nipiga kifuani na kuanguka chini. Kitendo cha mimi kuanguka chini Jackline akafyatua risasi kadhaa katika mwili wa mtu huyu na akaanguka chini mzima mzima. Nikanyanyuka na Jackline kwa haraka akanikumbatia kwa furaha huku akilia kwa furaha. Shamsa akatoka ndani ya gari na tukamkumbatia kwa pamoja.

“Ingieni ndani ya gari”

Nilizungu za huku nikiwaachia, Jackline akanikabidhi bunduki, nikamsogelea mtu huyu na nikampiga risasi mbili za kichwa na nikahakikisha kwamba amefariki ndipo nami nikaingia ndani ya gari upande wa dereva, nikaliwasha na kuondoka msituni hapa.

“Nawashukuru wazazi wangu kwa kuniokoa”

Shamsa alizungumza huku akiwa amekaa siti ya nyuma.

“Usijali ni jukumu letu kuhakikisha kwamba una kuwa salama wakati wote”

Jackline alizungumza huku akimgeukia Shamsa aliye kaa siti ya nyuma.

“Nawapenda sana wazazi wangu”

“Nasi pia tuna kupenda.”

Tukafika mpakani mwa Kenya na Tanzania, kwa bahati nzuri askari aliye simama getini hapa alituruhusu bila ya kipingamizi chochote. Tukafanikiwa kupita mpaka huu na kuianza safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam”

“Baba”

“Naa”

“Nina njaa”

Shamsa alizungumza kwa sauti ya upole.

“Hata mimi nina njaa”

Jackline naye alizungumza.

“Ngoja tuulize hapa kwa hawa bodaboda kama kuna sehemu nzuri ya kupata chakula”

“Sawa honey”

Nikasimamisha gari pembeni ya barabara.

“Mambo vipi viongozi”

Niliwasalimia waendesha bodaboda hawa.

“Salama kiongozi mambo vipi”

“Salama aisee. Hivi hapa pana itwaje?”

“Hapa panaitwa Chumvini”

“Ohoo je naweza pata sehemu wanayo uza chakula?”

“Ndio kiongozi. Unaona ile kona pale mbele?”

“Ndio”

“Kunja kulia, pandisha hicho kilima, tembea hadi pale kwenye mataa uta ona eneo lina vitiviti vingi, pale pale wana uza chakula.”

“Nashukuru sana ndugu zangu”

“Pamoja sana kiongozi”

Nikapandisha kioo cha gari taratibu na kufwata maelekezo niliyo pewa na muendesha pikipiki. Tukafika katika eneo ambalo kweli lina onyesha ni sehemu ya watu kupata chakula kwa maana nimekuta watu wakiendelea kula.

“Hapa sin ahata mia”

Nilimuambia mke wangu huku nikisimamisha gari kwenye eneo la maegesho.

“Hata mimi sin ahata pesa”

“Baba si umpigie simu anko Shabani”

“Eti ehee?”

“Ndio”

Nikaitoa simu yangu mfukoni na kwa bahati mbaya nikakuta ikiwa imezima chaji.

“Ohoo chaji imeisha”

“Mmmm”

“Halafu sijabeba chaji”

“Na mimi nimesahau kutoa usb waya kwenye ila gari nyingine”

“Nisubirini”

Nikashuka ndani ya gari na nikajiweka vizuri nguo zangu. Nikatembea hadi kwenye duka lenye huduma ya tigopesa.

“Habari yako dada”

“Salama”

“Una chaji yah ii simu?”

“Samsung?”

“Ndio”

“Hapana sina, hizo chaji zake sio kama za hisi smartphone nyingine”

“Una weza niazima simu nikampigia mtu akanisaidia pesa kwa maana pesa ipo kwenye hii simu na haina chaji”

Dada huyu akanitazama huku akinisadisi.

“Sawa”

Akanikabidhi simu ndogo. Nikanza kuingiza namba na kwa bahati mbaya nimeisahau namba ya Shabani.

“Ohoo tatizo hili”

Nilizungumza huku nikijitahidi kukumbuka namba ya Shabania mbayo kwa kweli sijaishika kichwani mwangu. Nikajifikiria kwa haraka haraka na kukumbuka namba pekee inayo nijia kichwani ni namba ya Tina. Nikampigia simu na kwa bahati nzuri ikaanza kuita.

“Haloo”

“Ni mimi”

“Rashidi….”

“Ndio naomba unisaidie kitu kimoja”

“Vipi lakini mume wangu, mumempata mtoto?”

“Ohooo asante Mungu, yupo mzima?”

“Mzima kabisa na ana afya nzuri. Simu yangu imezima chaji na nina hitaji pesa”

“Nikutumie sh ngapi?”

“Nitumie laki tano, nipo kwa wakala hapa nikutajie namba yake utoe hicho kiasi”

“Sawa mume wangu”

Nikamtajia namba Tina na akanitoa kiasi hicho cha pesa kwa wakala.

“Mmm”

Muhudumu wa duka hili kidogo akaguna.

“Kuna tatizo”

“Hii namba ndio uliyo piga?”

“Ndio”

Akanikabidhi simu.

“Umeiona mume wangu”

“Ndio shukrani sana”

“Upo wapi kwani kwa maana hiyo namba ya wakala ni namba ya duka langu”

“Duka lako?”

“Ndio mume wangu, nimefungua duka pamoja na hiyo sehemu ya chakula. Samahani kwa kuto kukuambia ila niliona nifanya kwanza hiyo biashara ikikua kiasi basi nikuambie kama suprize’

“Una taka kuniambia hili eneo zima hapa ni eneo lako?”

“Ndio mume wangu”

“Umejitahidi mama watoto”

“Asante baby. Kama upo hapo basi nisubirie ni kuone tu japo kwa dakika moja”

“Kusema ukweli nahitaji kuiongia Dar es Salaam usiku huu. Pia nipo na Jackline hivyo naaminia haito kuwa picha nzuri’

“Nimekuelewa mume wangu, sitaki mafarakano na huyo mzungu. Hembu mpe simu huyo binti niongee naye”

Nikamkabidhi simu muhudumu huyu.

“Ndio boss”

“Ahaa ndio huyu”

“Nashukuru kumfahamu”

“Ndio yupo”

“Sawa ngoja nimuite”

Dada huyu akatoka dukani hapa”

“Sefu, Wee Sefu”

Akaja kijana mmoja aliye valia mavazi ya upishi.

“Ongea na boss”

“Haloo boss”

“Ahaa sawa sawa, boss”

“Nimekuelewa”

“Ehee”

Nikaichukua simu hii na kuiweka sikioni.

“Honey nimemuambia Seif awahudumie, kuleni chochote munacho kihitaji”

“Nashukuru”

“Nakupenda sana Rashidi wangu?”

“Nakupenda pia mke wangu”

Nikakata simu hii na kumrudishia dada huyu. Muhudumu huyu akanikabidhi kiasi cha pesa kilicho tolewa na Tina.

“Shemeji hongera bwana kwa kumfanya dada yangu kuwa na furaha”

“Usijali pia nashukuru kwa huduma yako”

“Hakuna shaka shemeji”

“Chief nisubirie hapa niwaulize hawa wana kula chakula gani kisha nita kurudi, si upo jikoni pale?”

“Ndio”

“Poa”

Nikaondoka na kuingia ndani ya gari.

“Muta kula nini jamani?”

“Mmmm wana nini na nini mume wangu?”

“Ahaa sija jua ila mtu wa jikoni nimemuambia asubirie tumpatie oder”

“Kwa nini tusishuke na kwenda kula baba”

“Hili eneo lina watu wengi na hatuji nani mzuri nani mbaya. Isitoshe bado tuna safari ndefu. Nina imani toka tulipo ondoka walikuwa wana tutafuta katika simu. Wata kuwa na wasiwasi na bibi yako tumemuacha katika hali ambayo sio nzuri kidogo”

“Basi mume wangu muite huyo kijana atuambie wana pika nini na nani na tununue”

“Sawa mke wangu”

Nikarudi jikoni, nikamuita Sefu na kurudi naye kwenye gari. Akatueleza chakula kilichopo na tukamuagiza tulicho kihitaji na akaondoka. Kijana wa juisi akatuletea juisi tulizo agizia.

“Hii ndio shektende?”

Nilimuuliza kijana huyu huku nikiionja juisi hii.

“Ndio boss”

“Mmm”

“Hembo nionje mume wangu”

Jackline akaonja juisi hii.

“Waoo ni nzuri”

“Chukua hii mimi nipe hiyo”

Tukabadilishana juisi na Jackline na mimi nikanywa kuisi hii ya ukuwaju.

“Juisi zao ni zuri sana”

“Umezipenda mke wangu?”

“Yaa nimezipenda, mume wangu”

Tukaendelea kunywa juisi hizi. Tukaletewa chakula tunacho kihitaji tukaagana na kijana huyu na tukaendelea na safari yetu. Kazi ya Jackline ni kunilisha chakula hichi huku nami nikiendelea kuendesha gari hili.

“Baba hii gari mpya ehee?”

“Ndio mwanangu”

“Ni zuri naiomba”

“Hujafikia umri wa kuendesha gari”

“Mbona Ufaransa naendesha baba”

“Wee”

“Ndio ana endesha na nidereva mzuri”

“Alafu baba una jifanya kama hujui ikiwa ile siku nilikuendesha”

“Sawa mwanangu, kuanzi sasa hii ni gari yako”

“Waooo asante baba”

“Ehee nilitaka kusahau mke wangu. Ulikuwa una tuwatilia vipi kwa maana nilikuwa nina jaribu kukutazama kwenye side mirrow ila sikuwa nakuona”

“Una jua nilifanya kitu kimoja, niliipiga picha ile gari na nikaanza kuitrack kupitia simu yangu. Hivyo nilivyo ona ile gari ime simama, nikatafuta eneo moja nikapanda juu ya mti kwa bahati mti ule ulikuwa mrefu na ulikuwa na eneo ambalo nina weza kuiweka ile bunduki. Hivyo nikaanza kuwadungua mmoja baada ya mwengine”

“Aisee mke wangu upo vizuri”

“Nashukuru mume wangu”

“Alafu mama, nilimuambia baba anifundishe kutumia silaha ila amekataa?”

“Jamani Shamsa si uliniambia nikufundishe kuua na sio kutumia sihahaa”

“Ohoo Shamsa una taka kumuua nani?”

“Yoyote yule anaye taka kunidhuru. Umeona nimetekewa ila ningekuwa nina weza kupigana, ningewapiga”

“Ila hilo ni jambo la kweli mume wangu ina bidi tumfundishe mtoto namna ya kujilinda yeye mwenyewe”

“Sawa mwanangu nita kufundisha”

Tukaendelea na safari hii. Tukaingia katika moja ya sheli, nikajaza gari mafuta na tukaondoka. Majira ya saa saba usiku tukafika nyumbani na kukuta ulinzi wa askari ukiendelea kuimarishwa. Baadhi ya wana familia wakaanza kutoka nje mara baada ya kuona ujio wetu.

“Usishuke kwanza”

Nilimuambia Shamsa huku nikimkonyeza. Tukashuka ndani ya gari.

“Vipi kaka, mbona mulikuwa hampatikani, namba ya sehemeji tunapiga ila hampokei”

Shababani aliuliza huku akiwa na wasiwasi.

“Wee acha tu simu yangu kwanza ilizima chaji”

“Vipi lakini, mtoto mumempata?”

Tukatamana na Jackline huku tukiwa katika nyuso za huzuni.

“Mjukuu wangu yupo wapi?”

Mama aliuliza hukua kiwa na shahuku kubwa. Nikageuka nyuma na kumfanya ishara Shamsa na akashuka ndani ya gari kwa haraka wakakimbiliana na mama na kukumbatiana kwa furaha na watu wakapiga makofi kwa furaha kwani walikaa katika wakati wa mawazo mengi sana.

“Daa kaka hongera sana”

“Nashukuru sana ndugu yangu”

Tukaingia ndani na sote tukakaa sebleni hapa.

“Ehe imekuwaje kuwaje?”

Shemeji aliuliza huku uso mzima ukiwa umetawaliwa na furaha.

“Yaani wee acha tu”

Tukaanza kuwaadhithia kila kilicho tokea baada ya kujisalimisha mikononi mwa watekaji. Tukaeleza namna jinsi tulivyo pamanana na watekaji hadi tukafanikiwa kumuokoa Shamsa.

“Kwani DON una mahusiano naye gani hadi akakurithisha mali zake?”

Mkuu wa kitengo cha upelelezi aliye kuwa ana shuhukikia swala hili la kutekwa kwa Shamsa aliniuliza swali lililo wafanya watu wote kukaa kimya na kunitazama huku wakishubiria jibu la swali hili na mbaya zaidi ni kwamba ni watu wachache tu ndio wana jua kwamba DON ni baba yangu mzazi.




MWISHO WA MSIMU WA KWANZA


ENDELEA KUFUTAILIA MSIMU WA PILI


TAMATI


0 comments:

Post a Comment

BLOG