Search This Blog

Saturday, February 6, 2021

RISE UP SEHEMU YA 5/10

  

RISE UP

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 5 KATI YA 10


RX akampa Leticia mkono wa kulia na taratibu Leticia akamshika na akamshusha katika kiti hicho kirefu. Taratibu wakapenyeza katikati ya watu huku akiwa ameongozana na mabaunsa wake. Wakaingia ndani ya lifti na moja kwa moja wakaelekea hadi gorofa ya sita ambapo kuna vyumba vya hoteli. Wakaingia katika moja ya chumba.

“Mali mpya hii, subirini hapa”

RX alizungumza na kuwaacha walinzi wake hao sita mlangoni. Leticia akatazama chumba hichi kizima ikiwa ni ishara ya kunifanya niweze kuona kila kitu kilichopo eneo hili.

‘Nimekiona huyo, tumtolee dirishani’

Nilimuambia Leticia na akanijibu kwa ishara ya dole gumba.

“Mmmm mtoto ume tokea wapi wewe kwa maana leo ndio mara yangu ya kwanza kukuona”

“Ni kweli leo ndio mara yangu ya kwanza kufika kwenye hii club nina sikia ni club nzuri”

Leticia alizungumza huku akimtazama RX. Taratibu akamsogeza na kumla kitandani.

“Waooo nipe vitu vitamu mpenzi”

RX alizungumza huku akimtazama Leticia ambaye taratibu akapanda kitandani hapo na kumkalia kiuononi mwake. Taratibu Leticia akavua cheni yake na kumchoma sindano ndogo RX shingoni mwake.

“Aiii”

RX alizungumza huku akijishika shingoni mwake, akajarubu kunyanyuka ila nguvu zote zime muishia na hata sekunde ishirini hazijaisha akapitiwa na usingizi na kulala fofofo.

“Kazi ime kamilika. Nina mtoa vipi huyu jamaa ikiwa walinzi wake wapo wengi sana”

“Nimekuambia tumtolee kupitia dirishani”

“Una utani wewe. Kutoka gorofa ya tano hadi chini nina msushuje”

“Hicho chumba kipo eneo gani?”

“Kaskazini mwa gorofa hili”

Nikatazama eneo hililo, nikashuka katika gari na moja kwa moja nikaelekea hadi upande wa kaskazini mwa gorofa hili na kwa bahati nzuri upande ambao chumba hicho kipo kuna gorofa jengine ila ni gofofa tatu na katika eneo hilo kuna njia ndogo kiasi ambayo haina watu wanao katiza na kuna mwanga hafifu.

“Nipo chini hapa”

Nilizungumza huku nikitazama juu. Leticia akachungulia dirishani na nikamuona, nikasimama usawa wa chamba hicho.

“Hapa nina mshusha vipi Rashidi”

“Sikia mrushe nita mdaka”

“Una wazimu wewe. Una wezaje kumdaka mtu ana kido zake”

“Ndani ya hicho chumba hakuna kama?”

“Nimetazama hakuna kamba kabisa”

Nikaitazama bomba bamba mbili kubwa zinazo pelekea maji gorofa za juu.

“Funga mlango nina kuja”

“Nimesha funga. Una kuja kwa njia gani?”

“Subiria”

Nikavaa hloves ngumu kisha nikaanza kupanda kwa kutumia bomba hizi ambazo zime tengenezwa kwa uimara mkubwa sana.

“Rashidi una jua una hatari”

Leticia alizungumza hukua kiendelea kunitazama jinsi ninavyo panda hizi bomba mithili ya mtu anaye kwea mnazi mrefu. Ndani ya dakika moja na sekunde kadhaa nikafanikiwa kufika juu kabisa. Nikaingia katika dirisha la chumba hichi.

“Vipo walinzi wake hawajastuka?”

“Hawajastuka ehee tuna mshushaje?”

Nikaangaza juu ya angaza ndani ya chumba hichi. Nikachukua moja ya shuka kubwa nikalikunja mara mbili.

“Mnyanyue na umuweke mgononi mwangu”

“Alafu”

“Nina shuka naye kwenye hiyo bomba”

Leticia akanitazama kwa sekunde kadha kisha akafanya kama nilivyo muagiza, nikambeba RX mgononi mwangu na nikamfunga mthili ya mama wa kiafrika akimbebe mtoto wake mgongoni.

“Amekaa vizuri?”

“Yaa hapa hadondoki”

Nilizingumza huku nikilikaza shuka hilo vizuri kifuani mwangu. Taratibu nikatoka dirishani hapa kwa ustadi wa hali ya juu kwa maana nikifanya kosa nina dondoka na mzee huyu na sijui tukianguka ita kuwaje tukifika chini. Nikashika bomba hii kwa mikono yangu miwili, kisha taratibu nikaanza kushuka chini kwa mfumo wa kurereka tena kwa umakini mkubwa sana. Jambo la kumshukuru Mungu mikononi mwangu nina gloves ngumu hivyo sio rahisi kwa mikono yangu kuchubuka. Nikafika chini, nikamtazama Leticia ambaye naye ana shuka kwa mfumo kama nilio shuka chini. Akatua chini huku aamini kama amefanikiwa katika zoezi hili hatari.

“Kalete gari na liweka eneo la karibu na hapa”

Nilimuambia Leticia na akaondoka. Akatembea hadi eneo lilipo gari, akaligeuza na kulitea eneo la usawa huu. Nikamuingia RX katika gari pasipo mtu yoyote kumuona kisha nami nikaingia ndani ya gari na tukaondoka kwa mwendo wa taratibu ili kuto kustukiwa.

Baada ya kukunja kona ya kushoto mwa mtaa huu. Leticia akaanza kuongeza mwendo kasi wa gari hili huku nami nikigeuka na kumtazama mzee huyu ambaye naamini akiniona ata shangaa sana. Tukafika katika nyumba tunayo ishi salama salmini, na moja kwa moja Leticia akasimamisha gari katika maegesho na tukashuka. Nikamshusha mzee huyu na kumuingiza katika moja ya chumba. Nikamkalish katika kiti cha mbao, nikamfunga mikono, miguu na mwili wake eneo la kifuani nikalifunga kamba kwa kuizungushia katika kiti hichi.

“Simu yake unayo?”

“Hakuwa na simu”

“Hana track divie yoyote kwenye nguo zake?”

“Sijamcheki”

“Kalete kile kifaa”

Leticia akaka ndani hapa na baada ya dakika mbili akarejea akiwa na kifaa maalumu kinahco tumika katika kutafuta chip ambazo humuonyesha mtu popote anapo kwenda, mara nyingi huwa zina wekwa mwilini, au katika nguo alizo vaa. Nikamkagua na kwa bahati nzuri hana kifaa hicho. Nikavuta kiti kimoja na nikaa mbele ya mzee huyu.

“Usingizi una mchukua muda gani hadi kuzinduka?”

“Masaa manne”

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tz EPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

********************************************************************

“Tumuamshe sasa hivi, tunacho kihitaji ni kudili naye sasa hivi na kumalizana naye sasa hivi”

Leticia akatoka ndani hapa na baada ya muda akarudi akiwa na ndoo ndogo iliyo jaa maji na vipande vya barafu.

“Ana zinduka huyu”

Leticia alizungumza huku akimwagia RX maji ya kichwani mwake na kumfanya aanze kutingisha kichwa chake. Akafumbua macho yake mara baada ya Leticia kumwagika maji yote kwa mkupuo.

“Nipo wapi hapa na nyinyi ni kina nani?”

RX alizungumza kwa kujiamini sana. Akanitazama kwa sekunde kadhaa.

“Wewe”

“Ndio ni mimi mzee habari yako”

“Ume….u….wewe mwanamke?”

RX aliweweseka huku akiendelea kututazama mimi na Letica.

“Mzee wangu najua una jua kinacho endelea kwa DON. Mimi jambo langu ni dogo sana endapo uta nijibu kuifahsaha basi nitakuacha uendelee kula bata lako, ila ukinidanyanganya basi leo uta kuwa ni mwisho wako wa maisha.

“Kum** wewe”

RX alinitukana huku akinitazama usoni mwangu kwa macho yaliyo jaa hasira kali. Nikamtazama kwa sekunde kadhaa nikisha nikasimama, nikasogelea meza iliyo jaa vifaa vidogo vidogo vya kumpatia mateso mtu vya kila aina. Nikachukua plaize pamoja na mkasi, nikaanza kuichana tisheti yake kwa mkasi, kisha nikafwatia suruali, nikamalizia na boksa.

“Najua una penda sana kutomb**a sasa leo nina kwenda kuvunja korodani zako na tuone kama uta kuwa na ujasiri wa kushika makalio mwanamke”

“Ngoja ngoja una taka nini ehee?”

RX alizungumz kwa woga mara baada ya kuona nimashika makend** yake kweli.”

“DON yupo wapi?”

“Hki ya Mungu nina apa sifahamu ni wapi alipo”

RX alizumgumza huku akitetemeka kwa woga. Kwa ishara nikamuomba Leticia kunipatia saltape kubwa. Nikakata paande na kumziba nacho RX mdomoni mwake ili ninapo mpa mateso haya basi ajihisi vizuri sana. Nikamkita mkasi huu katika paja la mguu wake wa kulia na kumfanya RX kulia kwa nguvu sana ila sauti yake haitoki kwa maana nime mziba mdomo. Nikauzungusha mkasi huu ukiwa ndani ya paja la RX kama mara mbili kisha nikauchomoa huku damu zikimwagika.

“Niambie Don yupo wapi?”

Nilizungumza huku nikimtazama RX mdomoni mwake, nikafungua saltape hii niliyo mfunga mdomoni mwake.

“Hahahahaa…..sijui mimi”

RX alizungumza huku akicheka kwa maumivu makali. Watu aina ya RX ni watu ambao ni wagumu sana kutoa siri za mabosi wao, ni watu ambao wapo tayari kuhakikisha kwamba wana mlinda bosi wao kwa namba yoyote. Nikamfunga saltape hii kisha nikamkita katika paja la mguu wa kushoto na kilio kwa RX kikazidi kuongezeka.

“Mpenzi muache uta muua”

“Acha ata ongea tu”

Niliamuambia Leticia huku nikimtazama usoni mwake. Nikaifungua saltape tena

“Nipati Don”

“Siwezi kukuambia mtoto wa kahaba wewe”

Tusi hili likianifanya nisimame kwa haraka nikachukua nyundo iliyopo juu ya meza pamoja na misumari minne mirefu yenye inchi kama tisa hivi.

“Nataka kukuonyesha kwamba mimi ni mtoto wa malaya”

Nikamfunga saltape hii ambayo ina msaidia kutotokwa na saunti, Nikauweka msumari mmoja katika goti la mguu wa kushoto na bula ya huruma nikagonga nyundo kwa nguvu na msumari ukapita. RX akatikisika vya kutosha kwa maumivu makali sana huku akilia. Leticia akanitazama kwa macho ya mchangango kwa maana kwa muonakano wangu tu, sionyeshi kama ndani yangu mimi ni katili kiasi hichi. Nikamkita msumari mwengine katoka bega la mkono wa kushoto na ukazama wote ndani. Kwa maumivu makali ambayo RX ana yapata akalia kwa uchungu hadi akazimia.

“Baby uta muua huyo mzee kama hana jambo la msingi tuachane naye”

“Ata pata jambo la msingi na nina hitaji kuwaonyesha hawa jamaa kwamba mimi ni katili kiasi gani kama nilikuwa nina pambana uliongoni na nina ua watu na wao wana shangilia basi wata shangilia juu ya kifo cha huyu mzee”

“Kwa mfano amekufa ina kuwaje?”

“Tuna utupa mwili wake”

“Wapi ambapo hato patikana”

“Wana eneo lao ambalo, wakisha watesa watu bas iwana kwenda kuitupa miili hiyo kwenye hilo eneo ni kama pango humo ndani kuna chui anye kula nyama za watu. Hivyo basi na yeye ata kuwa chakula cha huyo chui”

“Una pafahamu?”

“Ndio”

“Sawa mume wangu wewe endelea kufanya unacho weza kuhakikisha kwamba tuna pata kilicho tufanya tufunge safari hadi hapa”

“Usijali”

Leticia akatoka ndani hapa, nikamuamsha mzee RX kwa kumpulizia dawa ya kumzindua mtu aliye zimia.

“Karibu tena duniani, ulikuwa kuzimu sasa ume rudi duniani. Nina endelea kukukita msumbari mmoja baada ya mwengine. Sasa hivi nita kukita hapa. Msumbari mmoja tu. Habari yako kwisha”

Nilizungumza huku nikiuweka msumari huu msuri huu katika shina la uume wake na ambapo nikiukita na ukazama ndani basi uta vuruga mfumo mzima wa nguvu za asili za RX na kuanzia hapa hato weza kudindisha tena



“Naongea naongea”

RX alizungumza kwa uchugu huku akilia kama mtoto mdo na nikasitisha zoezi langu hili la kikatili.

“Yupo wapi?”

“Kwa sasa ana elekea Somalia, ana kwenda kujificha kule”

“Una nitania wewe?”

“Haki ya Mungu vile ana kwenda kuishi kule kwa muda”

“Somalia ni kubwa nina weza kumpata eneo gani?”

“Kuna kisiwa kimoja kinaitwa Socotra ndio ana jumba lake kule na ana ishi kule. Niamini na sina sababu ya kukudanganya”

Nikatoa simu yangu mfukkoni na kumpigia Leticia kwa maana ametoka chumbani hapa.

“Njoo”

Nilizungumza mara baada ya Leticia kupokea simu. Haikuisha hata dakika moja, Letici akaingia ndani hapa.

“Vipi?”

“Amezungumza ni wapi alipo DON”

“Ni wapi?”

“Socotra”

“Hicho ni kisiwa kilichopo Somalia”

“Una kifahamu?”

“Sijawahi kukitembelea ila ni sehemu ambayo niliisoma katika historia ya Somalia. Kisiwa hicho huwa wana kitumia sana kwa mambo ya utalii, ila ni kikubwa, yupo eneo gani?”

“Yupo mlima Hajhiri”

Kwa haraka Leticia akaingia kwenye mtando na kutafuta kisiwa hicho na kweli tukafanikiwa kuona milima hiyo.

“Baby unahisi alicho kizungumza huyu mzee ni kweli?”

“Sina uhakika tuna weza kuhamishwa upande tukiwa wajinga”

“Sasa tuna fanya nini kwa maana kufunga safari ya kwenda Somalia, ni parefu na kama unavyo fahamu ile nchi ni nchi hatari nchi ambayo ina kila aina ya uchafu”

Nikashusha pumzi huku nikimtazama RX jinsi anavyo mwagikwa na damu.

“Kuna mtu ana weza kunieleza ni wapi alipo Don”

“Nani”

“Usijali yeye ata ongea tu”

“Huyu mzee je?”

Nikamtazama RX kwa sekunde kadhaa, kisha nikachukua moja ya bastola, nikaifunga kiwambo cha kuzuia sauti kutoka. Nikampiga risasi.

“Baby una taka kufanya nini?”

“Nina muua”

“Hapana usimuue sasa hivi”

“Hana faida kwetu”

“Najua ila kwa sasa usimue. Zungumza kwanza na huyo unaye hitaji kuzungumza naye kisha ndio ufanya maamuzi ya kumuua huyu mzee”

Nikamtazama Leticia kwa sekunde kadha akisha nikasitisha zoezi langu. Nikavua gloves zilizo jaa damu ya RX kisha nikatoka ndani hapa bila ya kuzungumza jambo lolote. Nikapandisha juu kabisa ya gorofa ya nyumba hii na nikatoa simu yangu. Nikaiandika namba ya Claudia ila kwa bahati mbaya sikuweza kuipata hewani. Nikaitafuta namba ya Brian na kwa bahati nzuri nikafanikiwa kuipata.

“Ni mimi”

“Malcom!!?”

Brian aliuliza huku akiwa na mshangao.

“Ndio”

“Naona namba yako ina code ya Mexico?”

“Ndio upo wapo?”

“Nipo nyumbani kwangu”

“Claudia yupo wapi?”

“Claudia alitoroka na amekwenda sehemu ambayo hata mimi sifahamu”

“Kwa nini ametoroka”

“Alicho niambia ni kwamba ana mimba yako.”

“Mimba?”

“Ndio na ameondoka na kuniacha peke yangu na hakuhitaji kuambatana na mimi”

“Don?”

“Don nimesikia habari za kutafutwa kwake na sijajua yupo wapi kwa kweli ndugu yangu”

“Alitoroka kipindi gani?”

“Kipindi ambacho wewe ulisadikika ume tekwa na watu wasio julikaa. Nin aimani ata kuwa amesha jifungua ni muda mrefu sana”

“Kwa mtazamo wako una hisi ata kuwa amekwenda wapi?”

“Kusema kweli sifahamu ndugu yangu na mimi na DON mkataba wetu ulikwisha mara baada ya mke wako kutoroka. Alinipiga na kunitesa akiamini kwamba nina fahamu ni wapi alipo mke wake ila alipo gundua kwamba sifahamu chochote basi akaniachia huru”

“Aisee pole sana, nina kuomba basi uende nchini Ufaransa”

“Rashidi ndugu yangu siwezi”

“Huwezi kwa nini?”

“Don alinikata miguu yote miwili kipindi ana nitesa. Jamaa ni mkatili sana n anime kuwa kilema ndugu yangu.”

Maneno ya Brian yakaniumiza sana moyo wangu.

“Nina kutumia picha zangu nikiwa katika muonekano mpya”

Picha kumi zikaingia katika simu yangu na nikazifungua huku simu ikiwa hewani. Kusema kweli, moyo wangu ukajawa na gadhabu kubwa sana kwani ni kweli Brian amepoteza miguu yake yote miwili huku uso wake ukiwa umejawa na makovu mengi sana.

“Nime kuwa ni mtu wa kulala kitandani ndugu yangu, sina uwezo kama zamani wa kwenda popote nninapo hitaji kwenda. DON ni shateani na kesi yangu FBI wana ifwatilia na wana msaka na hadi sasa hivi hayupo nchini Marekani”

Brin alizungumza huku akilia kwa uchungu sana kiasi cha kunifanya machozi yanibubujike.

“Nina kuahidi rafiki yangu nita muua DON. Nita hakikisha mateso aliyo kupatia wewe na yeye ana yapata. Umenielewa kaka”

“Nime kuelewa ndugu yangu ila familia yako kuwa nayo makini kwa maana katika kipindi chote alisema ni lazima aishuhulikie familia yako kutokana na usaliti wako”

“Usijali ila usimuambie mtu kama tume wasiliana”

“Usijali ndugu yangu”

Nikakata simu na nikaanza kutazama picha Brian jinsi alipo kuwa hospitali akiwa amekatwa miguu yote miliwi. Hasira ikanipanda, nikarudi katika chumba alipo RX na Leticia akanifwata kwa nyuma.

“Una ona alicho kifanya DON kwa mtu wangu”

Nilimuambia RX huku nikimuonyesha picha hiyo.

“Sasa nita kufanya kama alivyo mfanya huyu”

Nilizungumza kwa hasiraa sana huku nikichukua moja ya panga lenye makali makubwa sana.

“Baby tulia acha hasira. Kuna mambo nina muhoji”

“Mambo gani?”

“Tulia mume wangu. Tafadhali”

“Ona DON alicho mfanya rafiki yangu”

Nilizungumza huku nikimuonyesha picha hizi Leticia.

“Amemkata mguu yote miwili kwa ajili yangu. Sasa kama yeye ni katili basi na mimi ni katili na nina roho mbaya kama shetani”

“Baby tulia kila kitu kita kwenda sawa. Katika hii kazi ni lazima tuweze kupata msaada wa kijeshi. Tuna hitaji kuteketeza baadhi ya maghala ya DON ya kuhifadhia madawa ya kulevya pamoja na kiwanda chake kinacho zalisha madawa ya kulevya kwa wingi na kwa bahati nzuri kipo hapa hapa Mexico. Tulia basi mume wangu”

Leticia alizungumza kwa sauti ya upole huku akinishika kifuani mwangu ili kuituliza hasira yangu ambayo kusema kweli nime kusudia kuikata miguu ya RX.

“Endapo una pigana na mtu mwenye nguvu ni lazima uhakikishe kwanza una mdhohofisha. Njia ya kumdhohofisha DON ni kuteketea maghala yake hayo ya madawa ya kulevya pamoja na kiwanda hicho ambacho RX amenieleza”

“Uan hisi sisi wawili tuna weza kuifanya hii kazi?”

“Hapana, tume wasiliana na mkuu wangu wapolisi na kumueleza kila kinacho endelea na ameniambia kwamba ana zungumza na raisi na raisi ata zungumza na raisi wa Marekani na tuta patiwa kikosi maalumu cha DEA(Drug Enforcement Administrition) kuja kutusaidia mimi na wewe”

“Hili swala ume wahusisha Wamarekani?”

“Ndio mume wangu. Hatuna njia nyingine, hii ni Mexico, tukihitaji kufanya sisi kama sisi tuta kufa mapema mume wagu nielewe”

Leticia alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu. Nikamshika mkono na nikatoka naye ndani hapa.

“Mke wangu kumbuka kwamba mimi sio askari na nikama ngekewa tu nime weza kupewa na serikali yako hao DEA wakija kusaidiana nasi wata weza kunikamata na mimi”

“Hahahaa, mume wangu utendaji wa kazi zetu hauendi kama hivyo unayo hisi. Ipo hivi, wewe ni askari mpelezi kutoka Brazili. Hata aje nani, nchi yangu ina kukingia kifua. Hayo mengine sijui yaliyo pita juu ya maisha yako, serikali yangu yame iweka kapuni. Hivyo tujiandae kuwapokea hao jamaa wa DEA na huyu mzee ina bidi akae hai hadi pale jamaa watakapo kuja?”

“Lini?”

“Naamini kesho wata kuwa wamefika hapa”

“Ila kumbuka kwamba huyu mzee ana mwaga damu nyingi sana”

“Usijali Luiz atakuja na damu ya kumuongezea mzee huyu”

“Watu wake una taka kuniambia kwamba hadi sasa hivi wata kuwa hawajastuka kwamba bosi wao ametoweka na sura yako wana itambua?”

“Hilo lisikipe wasiwasi mume wangu kila kitu kina kwenda vizuri”

“Sawa, ila huyu mshenzi ni lazima nile naye sahani moja tu”

“Usijali mume wangu, punguza jazba”

Leticia alizungumza kwa sauti nyororo, akanisogelea na akaninyonya lipsi zangu.

“Ngoja niendelee kufanya mazungumzo ya utaratibu na huyu mzee”

“Poa, mimi nipo juu gorofani kabisa nina punga upepo”

“Kuwa makini usichungulie chungulie na pia muda ume kwenda”

“Usijali”

Nikapanda eneo la juu kabisa la nyumba hii, nikajilaza chali kwenye moja ya meza iliyopo eneo hili. Nikaanza kutazama nyota nyingi zilizo tawala angani

‘Aise maisha yana kwenda kasi sana’

Nilijisemea kimoyo moyo huku nikianza kutathimini maisha yangu niliyo kuwa nina ishi mtaani nchini Tanzania, maisha ya kuwa mlinzi wa maduka na nyumba za matajiri hadi leo hii nina fanya kazi katika vikosi vya usalama tena katika nchi ya Brazil.

‘Ila hawa jamaa wameniaminije kirahisi hivi?’

Swali hili likanifanya nikae kitako kwa maana ni kweli wame nikubalia ila wamenikubaliaje kirahisi ikiwa nina rekodi mbaya na pia nime ingia nchini kwao na kutumia kitambulisho feki na jina feki pia.

‘Hapa kuna kitu kitakacho nitokea puani hapa’

Niliwaza huku nikifikiria jinsi Leticia alivyo kuwa ana ingia ofisini na kuzungumza na wakuu wake na hakuniambia ni kitu gani wlaicho kuwa wana kizungumza.

‘Rashidi kuwa makini, Rashidi una maadui wengi sana ambao wame baki’

Niliendelea kujisemesha nafsini mwangu mimi mwenyewe.

‘Hawa wana nitumia alafu wakimaliza wata nitelekeza au kunikamata. Ina bidi kucheza kama Pelle hapa’

Nikatoa simu yangu mfukoni, nikaingia katika mtandao wa instegram na moja kwa moja niakelekea katika akaunti ya Jackline na kukuta picha ya mwisho kuiweka katika mtandao huo, ni siku mbili nyuma jambo ambalo sio la kawaida kwake kwa maana kila siku alikuwa na waomba watu wanao fahamu ni wapi nili basi wamfwate inbox.

‘Ata kuwa wapi huyu?’

Nilijiuliza kwa maana hili sio jambo la kawaida kabisa. Nikashusha pumzi huku nikitafakari, kwa sekunde kadhaa kisha niampigia simu Brian.

“Ndio kaka”

“Brian najua upo kwenye wakati mgumu sana ndugu yangu. Ila nina tambua akili yako na mikono yako vina fanya kazi vizuri sana”

“Ndio kaka”

“Nina kuomba unisaidie jambo moja. Mke wangu nime ingia kwenye akaunti yake ya Instergram na kukuta akiwa amepost picha siku mbili zilizo pita. Nahitaji kufahamu kama bado yupo Ufaransa au ameondoka?”

“Sawa nina namba ya mama ngoja nimuunganishe na wewe muzungumze”

“No mpigie na umuulize tu yeye yupo wapi”

“Sawa nita kupigia mara baada ya kumaliza kuzungumza naye”

“Pao”

Nikakata simu baada ya dakika saba Brian akanipigia simu.

“Ndio kaka”

“Nimempiagia mama na kumuuliza kuhusiana na ni wapi alipo Jackline, ameniambia kwamba amepokea habari za kuaminika kutoka nchini Somali kwamba upo huko, hivyo ameondoka jana asubuhi kuelekea Afrika Somalia akiwa na walinzi wake wawili tu”

“SOMALIAAAA…….!!”

Niliuliza kwa mshangao mkubwa sana.

“Ndio kaka, hata mimi mwenyewe nime shangaa sana ila sikuhitaji kumueleza kuwa mimi na wewe tume ongea”

“Watoto?”

“Wameachwa nyumbani wote wapo salama”

“Nashukuru sana Brian naomba unipatie kila kitakacho endelea katika familia yangu. Umenielewa?”

“Nime kuelewa kaka. Ila kwa nini ume shangaa sana juu ya Jackline kuelekea Somalia?”

“Ameongopewa, na DON yupo huko huko Somalia, sasa hiyo ni moja ya njia ya kumteka Jackline kiakili sana. Ina bidi nielekee Somalia muda huu”

“Sawa kaka”

Nikakata simu na kurudi katika chumba alipo RX na Leticia.

“Baby vipi?”

“Njoo tuzungumze”

Nilizungumza na Leticia akanyanyuka katika kiti alicho kikalia na tukatoka nje.

“Mama wa watoto wangu, amepigiwa simu na watu anao wajua yeye na wakamdhibitishia kwamba mimi nipo nchini Somalia, kwa kupagawa au kwa kuto kuelewa ameelekea nchini Somalia na walinzi wake wawili tu. Nina amini kwamba huu ni mpango wa DON kuhakikisha kwamba ana mteka mama wa wanangu”

Leticia akashusha pumzi nyingi huku akinitazama usoni mwangu.

“Ina bidi niondoke muda huu huu kuelekea Somalia?”

“Huwezi kwenda Somali”

“Kwa nini ikiwa mama wa wanangu yupo kule na atatekwa. Eheee?”

Nilizungumza kwa ukali kidogo.

“Kwa hiyo mimi niliyepo hapa sina umuhimu kwako si ndio?”

Leticia naye akaja juu huku akinitazama kwa macho ya msisitizo.

“Una hisi nina ambatana na wewe kwa ajili ya nini eheee? Nina kupenda ndio maana nime iweka kazi yangu kwenye mstari kwamba endapo mission hii ikifeli basi, mimi nina poteza kazi na wewe uta uwawa. Ndio maana nina kaa hapa na kutumia akili. Tumia akili Rashidi, hata DON leo akimshikilia sijui nani yako huyo hato weza kumua, ata hitataji kupitia wewe akukamate. Nenda na mbinu sio una kwenda kwa ajili ya hasira. Acha upuuzi Rashidi”

Leticia alizungumza kwa kufoka huku akiwa ana jiamini mbele yangu.

“Ohoo kwa hiyo wewe una tazama kazi yako na utazami maisha ya mwanamke anaye ilea familia yangu si ndio?”

“Kwa sasa yeye hana umuhimu”

“Una sema”

“Nina kuambia hivi kwa sasa huyo mwanamke wako hana umuhimu. Mimi ndio wa muhimu kwako kwa muda huu, nimeyashika maisha yako mkono na sinto kuruhusu uondoke na uniache hapa kwa ajili ya huyo malaya mmoja”

Maneno ya Leticia yakanipandisha hasira zaidi kwa haraka nikamkaba koo na kumgandamiza ukutani huku nikimtazama kwa macho ya hasira. Galfa Leticia akanipiga teke la sehemu zangu za siri na nikajikuta nikimuachia bila kupenda, akanipiga mtama mmoja na nikaanguka chini, kwa haraka akachomoa bastola yake na kunielekezea usoni mwangu.

“Usinilazimishe nikuue na ukitaka nita fanya hivyo Rashidi, sinto jali nina kupeda kiasi gani ila nina ipenda kazi yangu kuliko kitu chochote, hivyo siwezi kuweka mkund** wangu hatiani kwa ajili ya mwanamke asiye nihusu kwenye maisha yake. Mimi ni mwanamke na yeye ni mwanamke, ajilinde mwenyewe.”

Leticia alizungumza kwa msisitizo kiasi cha kunifanya nimshangae sana na hapa ndipo nikapata majibu ya maswali yangu niliyo kuwa nina jiuliza muda mchache ulio pita, huyu mwanamke na serikali wana nitumia ili kufanikisha oparesheni yao na baada ya hapo watanitelekeza.



Gafla tukaanza kusikia milio ya bunduki jambo lililo tufanya tusitishe mazungumzo haya kwa uharaka, nikakimbilia katika chumba tulicho muhifadhi RX, nikachukua moja ya bunduki, nikachomoa magazine na kukuta ina risasi za kutosha.

“Kama ni vijana wako wamekuja kukuokoa basi hesabu wamekufa”

Nilimuambia RX huku nikimtazama usoni mwake. Nikatoka ndani hapa na kumkuta Leticia akiwa anatazama laptop hi-i ambayo ina tuwezesha kuona kila kitu cha nje kutokana na kamera zilizo fungwa eneo la nje ya nyumbani.

“Naona ni majambazi wana pambana na askari”

Leticia alizungumza huku sote tukitazama pambano hayo jinsi yanavyo endelea.

“So tuwasaidie?”

“Hapanam, si polisi wala majambazi ambao wana paswa kutambu kwamba sisi ni kina nani”

Tukazidi kutazama jinsi askari hao wanavyo pambana na majambazi hawa wanao onekana kuvamia katika moja ya nyumba. Ndani ya nusu saa majambazi hawa wakauwawa kwa kuzidiwa nguvu na polisi ambao wanaonekana kujizatiti kisawa sawa.

“Nahitaji kulala”

Nilizungumza huku nikiingia chumbani, nikajitupa kitandani kwa maana kichwa changu kina mawazo mengi sana kuhusiana na Jackline na sijui nita msaidiaje.

‘Au nitoroke?’

Nilijiuliza akilini mwangu ila sikupata jibu. Leticia akaingia ndani hapa na kukaa pembeni yangu hapa kitandani. Akanitazama kwa sekunde kadhaa.

“Baby samahani kwa kilicho tokea muda ule. Samahani kwa maneno yote niliyo yazungumza, natambua uta nifikiria vibaya mume wangu ila samahani sana sikuwa nina maana ile niliyo zungumza. Kitu kikubwa nina hitaji kuhakikisha kwamba tuna fanya vitu kwa kutimia akili na sio hasira kwani hasira ni hasara baby”

Leticia alizungumza kwa sauti ya upole huku akionyesha kujutia sana kufanya kile alicho nifanyia.

“Siku nyingine ukininyooshea silaha nita kuua.”

Nilizungumza kisha nikalala chali na kugeukia ukutani. Leticia akaka kimywa kwa dakika kama moja hivi kisha akanishika mgoni mwangu.

“Rashidi natambua nime kuudhi ila samahani sana mume wangu”

“Nime kuelewa, ila endapo mama wa watoto wangu akifa. Sahau kama uliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mimi. Nipo hapa kwa ajili tu ya kunisisitizia niwepo hapa, ila nikihitaji kuondoka ni muda wowote nita ondoka na si wewe wala serikali yako ina weza kunizuia na yoyote ambate ata jaribu kuingia katika njia yangu nita muua. Leticia mimi ni mtu mbaya sana, nione tu kwa muonekano wangu. Ila roho mbaya ipo hapa moyoni mwangu na nina mission nyingi sana za kuzikamilisha katika maisha yangu, hivyo nina hitaji kuzikamilisha kabla sijakufa”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwa nime mgeukia Leticia.

“Nimekuelewa mume wangu, hakuna jambo baya litakalo jitokeza tena kati yetu”

“Poa”

Leticia akamshika jogoo wangu na kuanza kumpapasa.

“Nimechoka nina omba nipumzike”

“Tafadhali mume wangu, nina hamu na wewe, nina omba kidogo”

“Nimechoka na nina mawazo mengi hivyo hatuwezi kufanya chochote sasa hivi. Tusubiiri hao DEA waje hapa tumalize kazi na niendelee na kazi zangu binafsi”

Nilizungumza kwa msisitizo hadi Leticia akapoteza furaha usoni mwake.

“Sawa nipo sebleni”

Leticia akatoka ndani hapa na nikabaki peke yangu. Nikaito simu yangu mfukoni nia kuikagua kwa muda kidogo, nikajaribu kutuma ujumbe katika akaunti ya instegram ya Jackline ila sikujibiw kabisa na ina onyesha mara ya mwisho aliingia siku mbili zilizo pita.

‘Sijui nimuweke wazi?’

Nilizungumza huku nikitazama meseji upande huo wa meseji ambao una meseji kadhaa ambazo tulichati kwa akaunti yangu hii ambayo ni feki. Leticia akaingia ndani hapa.

“Luiz amefika na tayari nimesha andaa kifungua kinywa”

“Poa”

Leticia akanitazama kwa sekunde kadhaa, kisha akatoka ndani hapa. Nikanyanyuka kitandani na kuelekea sebleni, nikasalimiana na Luiz kisha nikaka kwenye moja ya sofa.

“Aisee mume mteka RX ni mtu hatari sana na uwepo wake hapa uta waletea matatizo makubwa”

Luiz alizungumza huku akitutazama mimi na Leticia.

“Nina jua nini tuna fanya”

Nilizungumza kwa ufupi huki nikimtazama Luiz usoni mwake.

“Sasa mume pata nini kutoka kwake?”

“Amesha tueleza sehemu alipo DON”

Leticia alijibu Luiz.

“Kweli?”

“Ndio”

“Ni wapi?”

Luiz aliuliza kwa shahuku kubwa kiasi cha kumtila mashaka na uliza uliza yake hii.

“Tuna fanya uchunguzi, tukipajua kama ni kweli basi tuta kujuza”

Nilimjibu Luiz na kumfanya Leticia kunitazama.

“Aha kwa hiyo ni ndani ya hapa hapa Mexico?”

“Luizi tuta kueleza”

Nilizungumza kwa msisitizo na kumfanya Luizi kukaa kimya huku akionekana kutafakari jambo. Simu ya Leticia ikaanza kuita, akaitoa mfukoni na kuiweka sikioni mwake.

“Ndio nimimi Leticia”

“Sawa karibuni sana. Nina imanai mume pata detail zote”

“Poa”

Leticia akakata simu huku akitutazama kwenye nyuso zetu.

“Askari wanne wa DEA wana kuja hapa nyumbani muda huu. Hivyo kama ni kunywa chai basi tunywe haraka haraka kwa maana leo ni kazi kazi”

Wote watatu tukajumuika pamoja na Leticia na kuanza kupata kifungua kinywa alicho kianda kisha akampelekea RX kifungua kinywa hichi tulicho kula.

“Ume kuwa askari kwa kipindi gani?”

Luiz aliniuliza huku akinitazama kwa macho ya udadisi.

“Sijawahi kuwa askari”

“Kwa hiyo wewe ni mwanajeshi?”

“Sijawahi kuwa mwanajeshi”

“Sasa wewe ni kachero au?”

“Luiz una weza ukaacha kunijoji maswali kwa maana kichwa changu kina mambo mengi ya kujiuliza kipekee na kujijibu mimi peke yangu. Tafadhali dogo.”

“Samahani sana”

Gari nyeusi aina ya Range Rover ikasimama nje ya geti.

“Wamefika”

Luiz alizungumza huku akitazama video ya kamera inayo onekana katika laptop. Leticia akatoka ndani ya chumba tulicho muweka RX. Huku simu yake ikiwa ina ita.

“Ndio”

“Sawa kijana wangu ana kuja kuwafungulia geti”

Letici akakata simu na kumpa ishara Luiz kwenda kufungua geti hilo.

“Hivi una muamini Luizi?””

“Kwa nini una uliza?”

“Nina kuuliza una muamini?”

“Ndio ni mfanyakazi mzuri na mpelelezi hodari sana katika nchi yetu”

“Poa”

“Vipi una mtilia mashaka?”

“Ndio simuamini hata kwa asilimia tano”

“Mmmm kwa nini?”

Kabla sijamjibu wakaingia wanaume wanne warefu, ambao miili yao imejazia kwa mazoezi. Wanaume hawa wamevalia nguo za kawaida, ila wamevalia majaketi ya kuzuia risasi yaliyo andikwa DEA huku mikononi mwao wakiwa wamebeba bunduki na wamevalia kofia nyeusi. Tukasalimiana nao na Leticia akatutambulisha kwao.

“Tuna weza kumuona RX?”

Kiongozi wa askari hawa alizungumza.

“Ndio”

Leticia akatangulia mbele na jamaa huyo akamfwata kwa nyuma na wakaingia katika chumba alichopo RX. Baada ya dakika kama mbili hivi wakatoka wakiwa na RX.

“Rashidi, jindaaeni tuna ondoka na RX tuna hitaji kumpeleka katika makao makuu ya polisi”

Leticia alizungumza huku akitutazama mimi na Luizi.

“Tuna weza kuzungumza?”

“Ndio”

Tukaingia chumbani na Leticia.

“Hii ni Mexico. Hakuna mualifu mkubwa kama RX akawekwa mahabusu. Munacho kwenda kukitafuta huko ni kusababisha damu kama zilivyo tokea katika kituo chenu cha polisi mara baada ya kumkamata DON.”

“Ila sio amri yangu hiyo baby. Ni amri ya wakuu wanahitaji tumkabidhishe RX mikononi mwa jeshi la polisi la Mexco kisha ata hojiwa na askari hawa wa DEA hapo makao makuu ya polisi”

“Alafu na sisi kazi yetu ita kuwa ni nini?”

“Tuta subiria hatua inayo fwata tuna fanya nini”

“Ina maana hadi sasa hivi hujui hatua inayo fwata ni nini?”

“Sijajua mpenzi. Tufwate oder na tusipoteze muda. Tujiandae”

Leticia akanibusu ndani hapa kisha akawa wa kwanza kutoka ndani hapa. Nami nikatoka na kuingia chumba cha kuhifadhia silaha, nikajindaa haraka haraka na nikabeba bastola nne, mbili nikazichomeka mguu wa kulia na kushoto na mbili nikazichomeka kiunoni. Nikavaa jaketi la kuzia risasi(butlet proof). Nilipo hakikisha nimajiandaa vya kutosha tukatoka ndani hapa na kumkuta Leticia na watu watu wengine nao wakiwa wananisubiria. Nikavaa earphone ndogo na kumvisha Leticia na earphone hii ni kwa ajili ya kuwasiliana sisi wawili. Tukatoka nje huku tukiwa makini, Luiz akaingia katika gari la jamaa hawa wa DEA huku sisi katika gari letu tukipanda na jamaa mmoja na safari ya kuondoka eneo hili ikaanza huku gari letu likendeshwa na jamaa huyu wa DEA huku tukiwa tumetangulia mbele. Ukimya ukatawala ndani ya gari hili huku mikononi mwangu nikiwa nimeishia bunduki yangu aina ya SIG Sauer MPX vizuri sana tayari kwa chochote kitakacho tokea. Tukaendelea kukatika katika barabara hii iliyopo katikati ya mitaa katika jiji hili. Mapigo yangu ya moyo yakaanza kunienda kasi huku wasiwasi mwingi ukinitawala.

“Simamisha gari”

Nilimuambia jamaa huyu wa DEA ambaye nime kaa naye siti ya mbele.

“Kwa nini?”

“Wewe simamisha gari”

“Tupo katikati ya msafara hatuwezi kusimamisha gar……”

Jamaa hakumalizia sentensi yake risasi moja ikapenya kwenye kioo cha mbele upande wake na kumpiga kichwani na akafariki hapa hapa.

“Fu…..**”

Nilizungumza huku nikijaribu kuushika vizuri mskani wa gari kwani tayari limeyumba na kwa kasi ya ajabu likagonga katika moja ya nguzo ya umeme iliyopo pembezoni mwa barabara na kusababisha airbag za gari hili kufumuka. Risasi zikaanza kurindima kulifwata gari letu, nikafungua mkanda wa siti yangu na kuruka siti ya nyuma alipo keti Leticia

“Upo vizuri?”

Nilimuuliza Leticia huku nikimtazama usoni mwake, jinsi anavyo vuja damu katika paji la uso wake..

“Yaani nipo poa”

Leticia alizungumza huku akiikoko vizuri bunduki yake.

“Nilisema mimi”

Nilizungumza huku nikifungua mlango wa upande wnagu nikajirusha nje huku nikibingirika na nikajibaza kwenye moja ya duka lililopo wazi. Nikaanza kujibu mashambulizi ya jamaa hawa walio jificha kwenye magorofa haya. Katika msafara hakuna kiti kibaya kama kupita sehemu ambayo barabara ipi katikati ya magorofa au barabara kuwa katikati ya milima kwa maana ambushi yake inakuwa sio ndogo. Watu hawa wana onekana wamejipanga sana kwani hata upigaji wao wa risasi ni wa kujiandaa vizuri. Nikaona gari alilo panda RX na askari wengine pamoja na Liuz linarudishwa nyuma kwa kasi ya ajabu, wakakunja kona moja kwa kasi na kupotea katika upeo wa macho yangu.

“Toka ndani ya gari wewee”

Nilimuambia Leticia huku nikimtazama usoni mwake.

“Mguu ume banwa na siti”

Leticia alilalama kwa maumivu huku akijitahdi kuutoa mguu wake wa kulia ulio banwa na siti.

‘Lazima nimuokoe siwezi kumuacha afe’

Nilizungumza kimoyo moyo. Nikatoa mabomu mawili ya moshi katika mfuko wa jaketi hili la kuzuia risasi, nikayachomoa vipini vya mabomu haya na kuyarusha upande ambao wapo majambazi na kusababisha moshi mwingi sana ambao ukaniwezesha kukimbia hadi ndani ya gari, nikamuangalia Leticia kwa kwa kweli mguu wake ume banwa na endapo nita hangaika kuuchomoa moshi uta isha na mvua ya risasi ya majambazi hawa ita tunyenyeshea, kwa haraka nikafungua mkanda wa askari huyu wa DEA, nikailaza kwa nyuma siti yake na kumsukumia katika upande wa siti za nyuma alipo kaa Leticia, nikakalia siti hii, nikaliwasha gari jambo la kumshukuru Mungu likawaka. Nikalirudisha nyuma kwa kasi ya ajabu huku nikiligeuza kuelekea walipo kwenda wezetu. Tukaondoka eneo hili kwa mwendo wa kasi huku nikiwa sioni ni wapi walipo kwenda askari wengine wa DEA.

“Vipi ume vunjika mguu?”

Nilimuuliza Leticia.

“Hapana ila ume banwa”

Kwa kasi hii ninayo endesha nikashindwa kabisa kumsaidia Leticia. Kwa kupitia kioo cha pembeni nikaona pikikipi kama nne hivi zilizo jaa watu wenye silaha zikitufukuzia.

“Ohoo Mungu wangu, Baby jitahidi kuuchomoa mguu”

“Okay”

Leticia alizungumza huku jasho likimwagika, taratibu na kw aumakini mkubwa akafanikiwa kuuchoa mguu wake eneo ambalo ulibanwa.

“Una uma balaa”

“Tuna mikia nyuma una weza kudili nao?”

“Dakika moja”

Leticia akachaja kipande cha shati alilo vaa huyu askari wa DEA na akajifunga mguu ni mwake kisha akaupiga piga ikiwa ni ishara ya kuuweka sawa.

‘Watoto wa malaya hawa, acha nidili nao shenzi’

Letici alizungumza kwa hasira kisha akarukia katika siti ya nyuma kabisa kwa maana katika hili gari kuna siti za mbele, za katikati na nyuma kabisa. Akaanza kumimina risasi kuelekea kwa watu ambao wana tufukuzia kwa risasi.

“Polisi ni wapi?”

Nilimuuliza Leticia.

“Minya hapo kwenye screen ita kupatia maelekezo ya wapi kitua cha polisi kilipo”

Nikaminya screen ya pembeni yangu, na kweli tukaanza kuelekewa na ramani hii ya GRPRS.

“Ohoo Mungu wangu”

Nilizungumza huku nikiishiwa pozi.

“Nini?”

Leticia aligeuka huku sote tukitazama foleni kubwa iliyopo mbele yetu na ubaya ni kwamba njia hii ni ya kuingia tu na sio njia ya kutokea na tayari nyuma yangu kuna gari kama nne hivi raia wa kawaida zimeziba kwa nyuma.

“Bado wana kuja?”

“Ndio Rashidi”

“Mguu wako vipi?”

“Una uma uma”

Nikafunga breki nyuma ya moja ya lori kubwa. Nikashuka kwenye gari na nikaanza kufyatua risasi kuelekea kwa madereva pikipiki ambao wana jipenyeza katikati ya magari ili kutufikia.

“Toka na kimbia”

Nilimuambia Leticia na akatoka ndani ya gari.

“Na wewe?”

“Achana na mimi, wanao muhitaji hapa ni mimi. Okoa maisha yako kimbia”

Nilimuambia Leticia kwa ukali huku macho yakinitoka huku jasho likinimwagika. Leticia machozi yakamlenga lenga ila nikampa ishara ya kukimbia na akaanza kukimbia huku akichechemea kukatika katikati ya barabara hii iliyo jaa magari. Risasi katika bundiki yangu hii zikaniisha na kujikuta nikivua mkanda wake na kuitupa pembeni. Nikachomoa bastola na sasa nime jitolea kufa na kupona kwa maana kadri muda unavyozi kwenda ndivyo jinsi genge la majambazi wa RX wana zidi kuongezeka kuhakikisha kwamba wana nikamata.



Nami nikaanza kukatika katikati ya foleni hii ya magari huku nikikimbia kwa uwezo wangu wote. Jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba kuna baadhi ya maeneo magari yamebabana kiasi cha kuwafanya wenye pikipiki kuishindwa kupita.

“Baby”

Nilita kwa maana nime vaa earphone ninayo weza kuwasiliana na Letica.

“Niambie mpenzi wangu”

“Upo wapi?”

“Nimefanikiwa kufika ubalozi wa Marekani, wewe upo wapi kwa maana nina hitaji kuja kukuokoa”

“Wale jamaa walio mbeba RX?”

“Nao wamesha fika ubalozini. Tuambie upo wapi?”

“Itafute signa ya simu yangu utajua nipo wapi. Mimi sifahamu mitaa hii”

Foleni ya magari ikaanzza kutembea.

“Ingia ingia”

Bibi mmoja aliniambia niingia katika gari yake huku akinifungulia mlango wa gari lake hadi nikajikuta nikishanga. Nikazama ndani ya gari la bibi huyu na akanipisha kwa kukaa siti ya nyuma nami nikashika uskani wa gari hili na kuanza kuyapita magari yaliyopo mbele yetu.

“Pole sana”

Bibi huyu alizungumza huku akinitazama machoni mwangu.

“Nashukuru”

Nilizidi kuongeza kasi ya gari hii aina ya BMW X3.

“Ubalozi wa Marekani kwa hapa upo wapi?”

Bibi akaanza kunieleleza wapi kwa kupita, kutokana gari hii ina uwezo wa kuhimili mikiki mikiki ya spidi, tukapita hata katika njia ambazo sio rasmi na tukafanikiwa kufika ubalozi wa Marekani, nikafunga breki getini kwa maana wanajeshi wanao linda walinisisitizia kufunga breki huku wakininyooshea bundiki zao.

“Nakushukuru sana bibi yangu”

“Karibu sana. Una jua mume wangu alikuwa ni mpelelezi, na nilipo kuona uka nikumbusha baadhi ya matuko ya mume wangu kipindi cha uhai wake. Hawa washenzi wa RX ndio walio muua na hapakuwa na kitu chochote kilicho fanyika kwa ajili ya kuwashuhulikia. Nambaya yangu hii uta nipigia, mimi ni professa chuo kikuu. Muda wowote ukihitaji kufahamu mambo ya huyu RX na gende lale hili, nitafute. Haya shuka sasa wasije wakatupiga risasi.”

Bini huyu alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake. Nikaiweka mfukoni kadi yenye namba zake aliyo nipatia kisha nikashuka katika gari huku mikono yangu ikiwa juu. Leticia na askari wawili wa DEA wakatoka getini hapa na kuwazuia wanajeshi hawa wa ubalozini kuto nishambulia. Kabla sijaingia ubalozini hapa, nikaona pikipiki kama sita za watu wa RX wakiwa kwa mbali, wakitazama jinsi ninavyo ingia ubalozini hapo. Nikamtazama bibi huyu aliye nipa msaada akanipa ishara ya kwamba niende tu ndani kwa maana nami nina yahofia maisha yake kwani jamaa hawa wanashuhudia kila kitu.

“Kuna huyo bibi ndani ya gari amenisaidia sana na gari lake. Hembu mpatieni msaada”

Niliwaambia askari hawa wa DEA na wakamfwata bibi huyu huku wanajeshi kama sita wakiwa makini sana wakiwatazama watu wa RX ambao hawadhubutu kusogelea eneo hili kwani wakisogea tu, watakacho kutana nacho si mchezo. Bibi naye akakubali kuingia eneo la ubalozi huu wa Marekani.

“Pole mume wangu, hawajakuumiza?”

Leticia alizungumza hukua kinikagua mwili mzima.

“Hawajaniumiza”

Nilizungumza huku nikitazama bandeji aliyo fungwa katika paji la uso pamoja na mguuni.

“Mguu vipi?”

“Ulitenguka tu”

“Mwili wa mwezetu upo wapi?”

Askari mmoja wa DEA aliniuliza huku akinitazama kwa macho makali kidogo.

“Katika lile gari”

“Shiti ina bidi mwili wake tuufwate. Hatuwezi kumuacha mwezetu eneo kama hilo”

“Sawa, Leticia si una fahamu lile eneo?”

“Ndio nilisha waelekeza”

Moja kwa moja tukaelekea katika chumba cha kupumzika, nikawakuta askari wengine wa DEA pamoja na Luiz.

“Aisee ume pona?”

Swali la Luiz likanifanya nimtazame kwa sekunde kadhaa kisha nikaka kwenye moja ya kiti.

“Nime kufa”

Jibu langu likawafanya watu wacheke japo tupo katikati ya shida kubwa sana.

“Samahani”

“RX yupo wapi?”

“Ana hojiwa”

Leticia alizungumza.

“Wapi naweza kumuona?”

“Hapana ana hojiwa na kitengo kingine”

Leticia alizungumza kwa sauti ya upole.

“Naomba tuzungumze”

Tukatoka eneo hili na tukasimama kwenye kordo iliyopo nje ya chumba hichi.

“Nisikilize mke wangu. Nina hisi kwamba katikati yetu kuna msaliti”

“Mmmmm msaliti ni nani?”

“Jiulize, walijuaje kama tuna msafirisha RX ikiwa hatukuwa na escort ya polisi wala hatukuwa na ishara yoyote kwamba magari yetu ni ya wana usalama”

Leticia akashusha pumzi taratibu huku akinitazama.

“Wewe jiulize tu hilo jambo. Hapa ninavyo ona kuna kamchezo kana endelea mke wangu. Hembu tuhakikishe kwamba tuna kuwa makini bwana”

“Wewe una muhisi nani?”

“Namuhisi aliye niuliza kama nime pona. Ina maana alikuwa ana tambua kabisa kwamba nita kufa ndio maana alishtuka kwa uwepo wangu na isitoshe. Watu wa RX waliwekeza nguvu kubwa sana kwangu ya kunifwata huku wewe na hawa askari wengine wakiwaacha ingali walisha jua kwamba RX yupo kwenye gari walilo panda Luiz.”

Nilizungumza kwa kumnong’oneza Leticia.

“Kweli mume wangu nimesha anza kupatwa na mashaka katika hili. Tufanye hivi, tuwe makini sana na hatua za Luiz kwa maana japo amekuwa ni mpelelezi ila ana maisha fulani ambayo alipo kuwa Brazil hakuwa nayo”

“Nikigundua kama ni yeye uta nisamehe. Msaliti hapaswi kuishi kwenye haya maisha”

“Usije ukafanya maamuzi ya kuhisi ikiwa hata hawa jamaa wa DEA wana weza kutusaliti na isitoshe wao na sisi ni nchi mbili tofauti na sijawahi kufanya nao kazi zaidi ya leo. Macho yetu tukayageuza kwenye tv iliyopo katika kordo hii ikionyesha habari za hivi punde. Tukaona gari letu tuliko kuwa tumepanda likiteketezwa kwa moto na watu wa RX huku mwili wa askari wa kikosi cha DEA ukiwa ndani.

“Wamarekani. Mume ingia katika nchi yetu na mume mshikilia Mungu wetu, tuta muua kila Mmarekani aliyopo hapa Mexico, la sivyo muachieni Mungu wetu RX tuna toa masaa matano la sivyo kitakacho wakuta Wamarekani itakuwa ni halali yenu. Hatuto jali wewe ni nani, wapi ume tokea na nini una taka kufanya tuta kuua”

Clip hii ndogo ya video kutoka kwa watu wa RX ikaishia hapo na muandishi wa habari akaendelea kuzungumza maneno ambayo hatukuhitaji kuyasikiliza zaidi ya kurudi ndani ya chumba cha mapumziko na kuwakuta askari hao wa DEA wakitazama habari hiyo.

“Huyu mtu ina bidi asafirishwe haraka kuelekea Marekani”

Kiongozi wa askari hawa wa DEA alizungumza huku akiwatazama wezake. Wakatoka ndani hapa huku nyuso zao zikionekana kujawa na hasira sana.

“Hii ni shida sasa madame”

Luiz alizungumza.

“Naomba simu yako”

Leticia alizungumza huku akimtazama Leticia.

“Ehee!!?”

“Nimesema nina omba simu yako”

Letica alizungumza kwa ukali sana na kumfanya Luiz kuitoa simu yake mfukoni taratibu. Taratibu mkono wangu wa kulia nikaishika bastola iliyopo kiunoni mwangu na endapo Luiz ata fanya jambo kolote la kipuuzi nita muua.

“Neno la siri”

Leticia alizungumza huku akimkazia macho Luiz.

“Ila mkuu…..”

“Neno la siri nahitaji”

Luiz akaanza kujishauri kichwani mwake, nikaichomoa bastola na kumnyooshea usoni mwake kwa maana hii jishauri yake ina tudhihirishia kabisa ana jambo ambalo ana lificha.

“4366maria”

Luiz alizungumza huku akitetemeka mwili mzima. Leticia akaifungua simu hiyo na kuanza kuikagua, kadri jinsi muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi uso wa Letica una jawa na ndita za hasira.

“Mkuu naomba kuelezea”

Luiz alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mkubwa sana. Letici akamzaba teka la kifua ambalo ni la kustukiza na kumfanya Luiz kuanguka chini mzima mzima kwani hakutegemea teke hilo. Nikamuwahi Luiz na kumgeuza kwa haraka na kumlaza chali, nikachomoa pingu aliyo ining’iniza kuinoni mwake na kuifunga mikono yake kwa nyuma.

“Luiz nilikuamini sana mdogo wangu, ila kwa hili, sio mimi pekee hadi nchi ya Brazil haito kupenda milelele daima”

Leticia alizungumza kwa uchungu sana. Akatoka ndani hapa na baada ya dakika moja akarudi akiwa ameongozana na wanajeshi.

“Mpelekeni kizuizini”

Wanajeshi hawa wakampokonya Luiz silaha zake zote alizo zificha, kisha wakamtoa ndani hapa na kutuacha.

“Ningekusikiliza mapema wala nisinge msogelea huyu Luiz. Askari mmoja wa DEA akaingia ndani hapa.

“NImeona kijana wenu amekamatwa?”

“Jaama ni msaliti, meseji zake alizo kuwa ana chati na msaidizi wa RX hizi hapa. Hapa ana waelez mpamgo mzima wa sisi kutoka”

Leticia alizungumza huku akimuonyesha askari huyo meseji zilizopo kwenye simu ya Luiz. Askari huyu akazisoma maseji hizi kisha akatoka ndani hapa na simu hiyo.

“Hii ni aibu mume wangu. Luiz ana liletea taifa aibu”

Leticia alizungumza kwa uchungu huku machozi yakimwagika usoni mwake.

“Hisia zangu hazikumkubali kabisa jamaa, ila ndio hivyo, laiti kama ninge zungumza, nina imani kwa asilimia mia moja unge nipinga.”

“Daaa hii ni aibu kubwa sana sijui nita ificha wapi uso wangu”

Akaingia msichana aliye valia suti nyeusi huku mkononi mwake akiwa na simu.

“Ni simu yako kutoka kwa raisi wa nchini kwako”

Binti huyu alizungumza huku akimtazama Leticia machoni mwake. Taratibu Leticia akaipokea simu hiyo na kuiweka sikioni mwake, huku uso wake ukionekana kujawa na wasiwasi mwingi sana.

“Ndio muheshimiwa”

Leticia alizungumza kwa sauti ya upole. Akaanza kuelezea jinsi tulivyo mgundua Luiz kwamba ni msaliti dakika za mwisho.

“Sawa mkuu”

Leticia akakata simu na kumkabidhi mwana dada huyu na akatoka ndani hapa.

“Muheshimiwa amekasirika sana”

“Duuu”

“Yaa hapa amefuka balaa, kwa jambo hili inapaswa sisi kuachana na oparesheni hii mara moja na vikosi vya Marekani vina chukua nafasi hii, ila ana fanya mpango wa kuzungumza na raisi wa Marekani ili ikiwezekana sisi tuendelee na oparesheni hii”

Leticia alizungumza kwa sauti ya upole na unyonge wa hali ya juu.

“Ila sio kosa lako kwa maana hukulijua”

“Ndio ila si una jua samaki mmoja akioza ndio wote. Yaani hapa tumepoteza uaminifu kwa serikali ya Marekeni na mbaya zaidi ni kwamba askari wao mmoja ameuwawa na ametolewa kwenye vyombo vya habari”

“Duu”

“Yaa ndio hivyo mpenzi wangu. Sasa hivi hatuwezi kuhusishwa kwenye jambo lolote”

Mlango ukafunguliwa na wakaingia wanajeshi wawili wakiwa na bundiki mikononi mwao.

“Tunaomba silaha zenu na uongozaneni nasi”

Mwanajeshi mmoja alizungumza na hatukua na kipingamizi cha aina yoyote, tukampatia silaha zetu na tukaongozana nao.

“Samahani”

Mwanajeshi mmoja alizungumza huku akifungua mahabusu iliyopo katika jengo hili la ubalozi wa Marekani.”

“Samahani kwa nini tuna fungiwa?”

Nilimuuliza mwanajeshi aliye tuomba msamaha.

“Tuna fwata amri”

Tukaingia ndani ya mahabusu hii na wakafunga na funguo geti hili lene nondo nene ambazo sio rahisi kwa mtu kuzipindisha wala kupita.

“Hapa ni lazima tuwekwe chini ya uangalizi wa kijeshi, hadi pale upelelezi wao utakapo malizika”

Leticia alizungumza huku akikaa chini.

“Ila sisi tumejitahidi kadri ya uwezo wetu kuokoa maisha yetu na lili lilikuwa ni ambush”

“Ndio ila ndio hivyo mume wangu, tuwe wavumilivu tu”

Tukakaa ndani hapa kwa masaa mawili, mlango ukafunguliwa na wakaingia wanaume wanne, huku mmoja akiwa ni mzee kidogo na amevalia suti nyeusi.

“Balozi wetu amefika”

Leticia alizungumza huku akitunong’oneza.

“Habari zetu”

“Salama mkuu”

“Tumekuja kuwachukua, tuna elekea ubalozini kwetu”

Mwanaume mmoja ambaye ni mmarekani, akafungua geti la bahabusu yetu na tukatoka. Tukaongozana na balozi huyu na watu wake hadi katika ofisi ya balozi wa hapa Marekani.

“Vijana wenu wapo salama kabisa. Majeraha yake aliyepata kwenye oparesheni hii”

“Hakuna shaka, tuna shukuru kwa ushirikiano wenu”

“Karibuni tena”

Tukapewa fomu mbili kila mtu yake, tukaonyeshwa eneo la kusaini. Nikaipitishia macho ya haraka fumo hii ina onyesha ni kiapo cha sisi cha kujivua katika oparesheji ya kumtafuta Don na wamarekani wameamua kuifanya wao kama wao.

“Tia saini”

Jamaa mmoja aliye tupa fomo hizi aliniambia huku akinitazama machoni mwangu. Nikatia saini eneo alio nionyesha kisha tukaondoka eneo hili. Tukaingia kwenye moja ya range rover kati ya Range rover hizi tatu ambazo zina bendera ya nchi ya Marekani. Mimi na Leticia tumeingia katika Range rover ya nyuma pamoja na dereva huku gari ya katikati akiwa amapanda balozi na walinzi wake na gari ya mbele ina walinzi wake.

“Kwa hiyo habari ya kumtafuta DON ndio imekwisha?”

“Ndio hivyo”

“Duu ila nilikuambia kwamba tusiwasiliane na hao DEA ila hukunisikia mke wangu na ukaniona mimi sijui nina kufelisha, sijui sina uwezo wa kufikiria. Haya turudi Brazil na mimi ndio mission yangu imeisha hapa baada ya hapo nina endelea namishe mishe zangu”

“Rashidi jamani”

“Hakuan acha jamani baby muda mwengine nikizungumza uwe una nisikiliza na kunielewa”

“Nisamehe, nita kuwa nina kusikiliza kwa kila jambo kuanzia sasa”

Gafla dereva akafunga breki na kutufanya tustuke sana.

“Kuna nini?”

Leticia alizungumza kwa mshangao.

“Gari ya mbele ime simama gafla, sijui kuna nini? Jamani kuna nini?”

“Sawa”

Dereva huyu akaugeukia nyuma.

“Kuna wanafunzi wana katiza barabara”

“Sawa”

Leticia alizungumza huku akijigemeza vizuri kwenye siti. Nikageuka nyuma na sioni gari hata moja ikiwa ina kuja katika barabara hii. Taatibu taa ya hatari ikaanza kunicheza kichwani mwangu.

“Hao wanafunzi ni wengi?”

Nilimuuliza dereva huku nikiendelea kuangaza kila kona. Gafla mlipuko mkubwa ukatokea katika gari ya mbele kabisa, tukashuhudia jinsi gari ya walinzi wa balozi ikipaishwa juu kwa mlipuko na kitendo cha kutua chini, wakajitokeza watu wa RX kusipo julikana na wakaanza kutushambulia kwa risasi kitu kulicho tufanya tuchanganyikiwe kwa maana mimi na Leticia hatuna silaha ya aina yoyote.



“Rudisha gari nyuma”

Leticia alizungumza huku sote tukiwa tumeinama katika siti hii ya nyuma. Dereva akafanya kama alivyo agizwa huku gari iliyo mbeba balozi nayo ikianza kurudishwa nyuma kwa kasi.

“Una bastola?”

Nilimuuliza dereva akachomoa bastola yake nakunikabidhi.

“Usifungue kioo gari hizi haziingizi risasi”

Dereva alizungumza huku akizidi kurudisha gari hii kwa kasi. Nikanyanyua kichwa changu na kutazama nyuma na kweli, risasi zinazo pigwa na maadui zetu zina piga kwenye vioo na kuweka nyuma ila haziingii ndani. Kwa utaalamu wa hali ya juu dereva akaligeuza gari kuelekea katika barabara ya mashariki mwetu. Akaisubiria gari iliyo mbebea warizi kutangulia mbele kisha nasi tukafwatia nyuma huku watu hawa wakiendelea kutufukuzia na magari yao.

“Daaa hawa jamaa wametupania”

Nilizungumza huku nikitazama jinsi gari zao zinavyo kuja kwa mwendo wa kasi.

“Hii ndio Mexico na hapa hatupati msaada wowote kutoka kwa maaskari kwa maana wana ogopa sana haya makundi ya kihalifu.”

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tz EPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

********************************************************************

“Hii nchi sijui wana ishije jamani”

Leticia alilalama huku akitazama nyuma. Laiti ingekuwa sio umahiri wa hii gari aina ya Range Rover Sentinel hakika sote tungekufa. Tukafika katika ubalozi wa Brazil na gari hizi zikaingia ndani na wanajeshi walio getini wakaanza kujibu mashambulizi ya kundi la RX, nikashuka katika gari kwa haraka.

“Sihaha kubwa nahitaji”

Nilizungumza na dereva akanieleza kwamba silaha hizi zipo nyuma ya gari hili ambalo nimeshuka, nikafungua buti ya nyuma na kuchukua bunduki.

“Nenda kapumzike haupo sawa”

Nilimuambia Leticia huku nikimtazama usoni mwake.

“Hapana”

“Nenda kamlinde balozi, sio ombi ni amri?”

“Ila hauna cheo juu yangu”

“Ni amri kama mume wako, chukua hii kamlinde balozi”

Nikamkabidhi Leticia bastola, akanitazama usoni mwangu.

“Kawe makini mume wangu”

“Usijali”

Nikavaa jaketi la kuzuia risasi, na Leticia akakimbilia ndani walipo kimbiliwa walinziwa balozi. Nikajiandaa vya kutosha kisha nikakimbilia eneo walipo wanajeshi wa getini. Tukaaza kujibua mashambulizi kuelekea walipo watu wa RX ambao umbali wao ni kama mita stini hivi kutoa sehemu tulipo. Gari nne wa wanajeshi wa Marekani zkafika eneo hili na kuongeza nguvu iloyo wafanya watu wa RX walio salimika kukimbia.

“Mupo salama?”

Mwanajeshi mmoja wa Marekania lituulizaa huku akitutazama.

“Ndio ytupo salama”

“Balozi yupo wapi?”

“Ndani”

“Twendeni tukamuone”

Nikaongozana na wanajeshi wawili wa Marekani na tukaingia ndani na walinzi wakatupeleka hadi alipo balozi wa Brazil.

“Nina itwa kanali John. Ni USA NAVY”

“Nashukuru kukufahamu”

“Tumepokea ombi kutoka kwa raisi wenu wa kuwasidia kulinda ubalozi wenu kwa maana muna ona hali halisi inayo endelea hapa”

“Ndio tuna iona na shukrani sana”

“Jeshi langu pia lina endesha oparesheni ya kuwasala kundi zima la hawa wauza madawa ya kulevya hii ni vita, hivyo tungependa kuanzia sasa hivi, asitoke nje mtu yoyote wa ubalozi wako”

“Una maana kwamba?”

“Maana yangu kama kuna wafanyakazi, wewe si munaishi nje ya ofisi hizi za ubalozi?”

“Ndio”

“Basi asitoke mtu yoyote kueleka kwake”

“Kanali samahani”

Nilizungumza huku nikimtazama usoni mwake.

“Ndio”

“Je nina weza kuungana nanyi kwenye hiyo oparesheni?”

“Wewe ni nani?”

“Ahaa huyu ana itwa Rashidi ni mmoja wa askari nilio nao kwenye timu yangu”

Leticia aliwahi kuyatoa maelezo hayo. Kanali John akanitazama usoni mwangu kwa dakika kadhaa kisha akatingisha kichwa.

“Karibu kwenye timu”

“Nina shukuru”

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tzy EPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

********************************************************************

Tukapeana mikono kwa kukaribishwa kufanya kazi na wajaeshi wa Marekani.

“Wanajeshi wangu ishirini nita waacha hapa, wata walinda na wengine nita endelea kuwa nao kwenye oparesheni. Ni lazima tuwapige na kuimaliza hii kazi leo leo”

“Sawa sawa kanali”

“Kijana ongazana nami”

“Kuwa makini”

Leticia alizungumza huku akinitazama machoni mwangu.

“Usijali”

Tukatoka ndani hapa na kanali John pamoja na kijana wake. Akagawa majukumu kwa wanajeshi wake ishirini kisha akanitambulisha kwa kikosi chake kwamba nita jumuika nao kwenye oparesheni hii na tukaingia katika magari na kuianza safari ya kuwasaka watu wa RX.

“Hawa washenzi ni lazima wafe”

Kanali John alizungumza huku akivuta sigara kubwa.

“Ume sema kwamba una itwa nani?

“Rashidi”

“Sura yako sio ngeni kwangu wewe?”

“Ina weza ikawa?”

“Ni kweli, nimekumbuka wewe si mpiganaji wa DON?”

“Ndio nilikuwa ni mpiganaji wake ila kwa sasa ni adui yake”

“Ilikuwaje ume kuwa adui yake?”

“Nimekataa kufwata matakwa yake”

“Matakwa gani?”

“Alinipa kazi ya kumdhuru mke wangu ili apate mali zake, nilikataa na uadui ukaanzia hapo na mimi ndio niliye mkamata DON na kumkabidhi katika jeshi la polisi la Brazil ila wakashindwa kummudu akawavamia na kuwatoroka”

“Usijali ata patikana”

“Ila nina sikia kwamba DON yupo nchini Somalia”

“Nani amekueleza?”

“Ipo hivi mke wangu nina miaka kama miwili na miezi kadhaa sija oana naye. Hivyo alikuwa akinitafuta kweny kwa kutangaza katika mitandao. Nimepokea taarifa kwamba amepigiwa na simu na mtu aliyopo Somalia na kumueleza kwamba yupo kule jambo ambalo sio kweli na tayari amesha kwenda kule na sifahamu nini ambacho kimempata”

“Miaka yote miwili ulikuwa wapi?”

“DR Congo. Nilipelekwa katika gereza moja na….”

“Kwa nini ulipelekwa gerezani na ni nani aliye kupeleka grerezani”

“Raisi wa sasa nchini kwangu Tanzania, alinichukulia mke wangu, akanisingizia mambo mengi sana kiasi kwamba maisha yangu yaliharibika na yakawa ya kuruka ruka, akanifunga gereza moja la Tanzania, nikatoroka, akanifunga kwenye gereza jengine la huko Congo nika toroka na nikaingia mikononi mwa Obote ambaye kwa sasa ndio raisi wa Congo. Nikapata mafunzo ya msituni na kwa kusaidiana naye tukaipindua serikali na akaingia madarakani”

Sikutaka kumficha kitu chochote kanali John kwa maana nimejifunza madhara ya kuficha mambo yaliyo pita kwani ningeweza kumueleza ukweli Caro asinge nitimua. Gari zikasimama kwenye moja ya mtaa ulio tulia na wenye vumbi jingi sana.

“Dogo kuwa makini”

Kanali alizungumza huku wanajeshi kadhaa wakishuka kwenye lori la mbele, wakatawanyika na kujibanza kwenye magorofa haya yanayo onyesha hayaishi watu. Nasi tukashuka kwenye gari hili dogo aina ya Hammer na tukakimbia hadi kwenye moja ya nyumba na kujibaza. Kanali akatoa ishara ya wanajeshi wawili kuvunja mlango ulipo pembeni yetu. Wanajeshi hawa kwa kutumia mateke wakauvunja mlango na ukaanguka chini. Tukaanza kuingia ndani ya jengi hili kwa umakini wa hali ya juu sana huku tukipandisha ngazi kuelekea gorofani. Jambo linalo niwia ugumu ni kwamba sijui tuna msaka nani kwenye haya majengo ambayo hayaishi watu.

“Grenadeeeee”

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tzz EPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

********************************************************************

Mwanajeshi aliye tangulia mbele alizungumza huku akirudi nyuma kwa kasi, tikajirusha chini na bomu hili la mkono likalipuka na kusababisha vumbi jingi kutawala eneo hili. Mvua ya risasi ikaanzza kutujia, nikabingirika na kuingia kwenye moja ya chumba huku nikiwaacha wajashi kadhaa wa Marekani wakiuwawa.

“Tuna hitaji msaada, narudia tuna hitaji msaada”

Nikamshuhudia kanal John akiwa ameanguka chini huku mguu wake mmoja ukiwa uemjeruhiwa vibaya kwa risasi, kwa haraka nikatoka ndani ya chumba hichi nikamshika jaketi lake la kuzuia risasi na kuanza kumvuta kuingia ndani ya chumba hichi. Wanajeshi kama wanne hivi wameuwawa huku mmoja akiwa amekatwa miguu yake kwa bomu.

Wanajeshi wengine wa Marakani walio kuwa nje wakaingia ndani hapa na kuanza kujibu mashambulizi ya watu hawa walipo juu ya gorofa. Hakuna kitu kibaya kama anaye kushambulia akiwa juu na wewe unaye shambuliwa ukiwa chini.

“Tunahitaji helicopter, narudia tuna hitaji helicopter washambuliaji wapo gorofa ya tatu, sisi tupo chini kabisa”

Mwanajeshi mmoja alizungumza kwa kutimia simu ya satelaite.

“Ombi lako lime sikika, tokeni kwa haraka katika jengo hilo kwani jeti za jeshi zipio njiani. Narudia tokeni kwenye majesho hayo jeti zina kuja eneo hilo”

Tulisikia sauti kutoka kwenye kipaza sauti. Wanajeshi wakaanza kubeba miili ya wezao na kutokana nayo humu ndani huku nami nikimsaidia kanali kutembea. Tukaingia katika magari na tukaanza kuondoka katika mtaa huo ambao kama jangwani na una onyesha wanao ishi hapa wote ni waalifu. Mwanajeshi mmoja akaanza kumuhudumia kanali jeraha lake.

“Tupo mita mia mbili kutoka kwenye eneo la vita hivyo muna weza kushambuli”

Mwanajeshi huyu aliye kaa pembeni yangu alizungumza.

“Tumekupata”

Tukaanza kusikia mitikisiko mikubwa nyuma yetu nikageuka nyuma na kuona moto mkubwa sana ukiwa umetawala katika eneo hili jambo lililo wafanya baadhi ya wanajeshi kushangilia kwa furaha. Moja kwa moja tukaelekea katika kambi ya jeshi la Wamarekani iliyopo mpakani mwa Mexico na Marekani. Wanajeshi walio jeruhiwa wakaanza kuhudumiwa vizuri huku walio poteza maisha miili yao ikielekea kuhifadhiwa kwenye chumba cha maiti.

“Samahani nina weza kupata simu?”

“Ndio”

Mwanajeshi mmoja alinikabidhi moja ya simu. Nikaingiza namba ya Leticia na kumpigia kwani simu yangu imezima chaji.

“Hei ni mimi”

“Rashidi, vipi mume wangu”

“Ahaa safi kiasi”

“Kwa nini?”

“Tumeingia Marekani”

“Weee”

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tzEPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

********************************************************************

“Ndio, kwa maana wanajeshi wamejeruhiwa na ule mji umeshambuliwa kwa mabomu ya anga”

“Basi ngoja nifunge safari nije Marekani”

“Vipi hali imetulia?”

“Ndio na raisi ameagiza ubalozi ufungwe kwa muda na balizo na wafanyakazi wote warudi Brazili hivyo na mimi bado sijajua kama nita amriwa kurudi Brazil au nije Marekani”

“Fanya hivi mke wangu. Nenda kwanza Brazil, kuna rafiki yangu nina hitaji kumuona hapa Marekani kisha nita kuja Brazil”

“Kweli mume wangu?”

“Ndio nina kuahidi tumuombe Mungu mambo yasiharibike”

“Nakusubiria kwa hamu mume wangu”

“Nashukuru mke wangu, nikifika Las Vegacy nitakupigia”

“Sawa”

Nikakata simu na kumrudishia mwanajeshi huyo. Nikaelekea katika hema alilo ingiwa kanali John. Nikamkuta akizungumza na simu hivyo ikanibidi kumsubiria amalize kuzungumza na simu, ndio nizungumze naye.

“Una jisikiaje?”

Nilimuuliza kanali John mara baada ya kumaliza kuongea na simu.

“Maumivu yamekwisha sasa, nina shukuru kwa kunisaidia”

“Usijali maisha ni kusaidiana. Ahaa nina ombi moja kama hauto jali”

“Zungumza tu”

“Nina hitaji kuelekea Las Vegacy”

“Kutoka hapa Texas hadi Las Vegacy ni mbali sana kwa usafiri wa gari ita kuchukua kama masaa kumi na tano hivi. Ila kwa ndege ni masaa manne na dakika kama arobaini hadi arobaini na tano”

“Ita pendeza kama nikaenda na ndege”

“Una kitambulisho?”

“Ndio”

Nikatoa kitambulisho nilicho tengenezewa na jeshi la polisi Brazil pamoja na hati ya kusafiria ambavyo muda wote ninatembea navyo. Kanali John akamuita mmoja wa wanajeshi wa kike.

“Kamshuhukike kamanda hapa ana hitaji kusafiri”

“Sawa mkuu”

“Hakikisha ana fika Las Vegacy ni mwezetu na ametusaidia sana”

“Sawa mkuu”

“Rashidi, nikutakie safari njema”

“Asante sana”

“Silaha uta uta mkabidhi pia huyo binti na atakupelekea hadi uwanja wa ndege na kukukatia tiketi”

“Sawa nashukuru sana”

“Una simu hapo uandike namba yangu, ukiwa na taarifa yoyote alipo DON basi usisite kunifahamisha”

“Simu yangu kwa sasa ime zima”

“Nipatie karatasi nimuandikie namba”

Mwanajeshi huyu akampatia karatasi kanali John, akaniandikia namba kisha tukaondoka eneo hili, nikakabidhisha silaha zangu zote kwa binti huyu, pamoja na jaketi hili la kuzuia risasi, tukaingia katika gari ndigo ya jeshi na tukaondoka hapa na safari ya kuelekea uwanja wa ndege ikaanza. Tukafika uwanja wa ndege na binti huyu akanisaidia kukata tiketi kwa pesa ya jeshi kisha akanikabidhi kiasi cha dola elfu moja.

“Ita kusaidia ukiwa Las Vegacy”

“Nashukuru”

“Karibu tena”

“Asante”

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tz EPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

********************************************************************

Mwanajeshi huyu akaondoa, kutoka ndege niliyo kata tiketi ina ondoka baada ya dakika arobaini, nikaingia kwenye moja ya dula la nguo, nikanunua nguo mpya kabisa kisha nikaeleka katika moja ya bafu lililopo hapa uwanjani, nikaoga haraka haraka kisha nikabadilisha nguo, na nguo nilizo kuwa nime zivaa, nikaziweka katika ndoo ya taka. Nikanunua chaji, niwani nyeusi pamoja na kofia. Muda wa safari ukawadia, nikaingia ndani ya ndege pamoja na abiria wengine na safari ikaanza.

‘Asante Mungu’

Nilizungumza kwa maana nimeweza kusalimika katika vita ambayo bado nusu tu initie roho.

“Haiwezekani, Marekani ishambulie nchi yangu, mji wangu iue familia zilizo kuwa katika ule umji kikatili sana alafu nikae kimya au nisizungumze. Nipende kuwaahidi wananchi wangu wa Mexico, hii ni vita, tuta pambana na Marekani hadi dakika ya mwisho na nita hakikisha Marekani nayo ina baki kuwa majivu kama walivyo fanya kwenye mji wangu”

Abiria wengi wakahamaki ikiwemo mimi kwa maana raisi wa Mexico amedhamiria kurudisha mashambulizi yatokanayo na mashambulizi yaliyo fanywa na ndege za jeshi la Marekani kwa lengo la kuangamiza magaidi walio kuwa wamejificha katika mji ambao watu nao wana ishi.



Sikuhitaji kuzungumza chochote zaidi ya kuvaa earphone zangu masikioni na kusikiliza mziki kwani haya ni mambo ya kisiasa na hayanihusu kabisa. Tukafika jijini Legacy, nikashuka katika ndege na moja kwa moja nikaelekea nyumbani kwa Brian na kwa bahati nzuri nikamkuta akiwa na daktari maalumu anaye muhudumia. Kitendo cha Brian kuniona tu machozi yakaanza kumwagika usoni mwake, nikamsogelea katika sofa alilo kaa na taratibu nikamkumbatia huku nami machozi yakinigela lenga usoni mwangu.

“Kaka nimeamini ile misemo yenu ya kiwashili ya kwamba kabla hujafa hujaumbika”

Brian alizungumza hukuakilia kwa uchungu sana, kusema kweli, Brian alitokea kunipenda na kunisaidia kama ndugu wa karibu toka siku ya kwanza kuonana naye.Japo alikuwa ni msaidizi wa Claudia ila hakuchukulia ukaribu wetu kama kazi, aliufanya ukaribu wetu kuwa kama ndugu”

“Don….Don mwisho wa siku amenifanya hivi ndugu yangu”

“Natamani sana kukuuliza kwa mara nyingine ilikuwaje kuwaje ila nina ona nita kuumiza. Vipi una endeleaje?”

“Namshukuru Mungu maumivu yamepungua sasa hivi na endapo Mungu akibariki kidonda kikipona basi nita vaa miguu ya bandia”

“Pole sana ndugu yangu?”

“Nimesha zoea. Hapo awali hii hali ilinichanganya sana ila kwa sasa nina mshukuru Mungu kisaikolojia nipo vizuri”

“Sawa usijali. Nimekuja hapa ila nina hitaji kueleka nchni Somalia, nina imani kwamba Don ata kuwa amelengasha mke wangu eneo hilo ili mradi kuhakikisha ana mteka kirahisi”

“Hata mimi nilikuwa nina lifikiria hilo, ehee niambie ime kuwaje ukawa Mexico?”

“Kuna taarifa ya shambulizi wa jeshi la Marekani kwenye mji ambao walikuwa wapo magaidi?”

“Yaa niliiona?”

“Nami nilikuwa ni miongoni mwa wanajeshi wa Marekani katika oparesheni hiyo ila nilijiunga nao kwa tiketi ya jeshi la polisi la Brazil kwani kama ulifwatili DON alikamatwa nchini Brazil”

“Yaa nilisikia nikajiuliza ime kuwaje DON akakamatwa ila pole sana kwa jeshi la polisi la Brazil kwa maana kilicho wapata ni jambo kubwa sana”

“Ni kweli na mimi ndio niliwafanikishia katika mpango wa kumkamata DON ila huko mbeleni mambo yamekuwa kama yalivyo kuwa”

“Ndio hivyo ndugu yangu.”

“Brian hivi una mfahamu mtu yoyote Somalia akanipokea?”

“Nawafahamu wengi sana ila kama una kwenda kumtafuta Jackline usiwasiliane na mtu yoyote kwani hao watu ninao wafahamu kwa namna moja ama nyingine wana muunganiko mkubwa sana na DON, nitakuwa kama nime kutoa sadaka kwa don.

“Nimekuelewa wala usiwe na wasiwasi wa aina yoyote”

Siku nzima nikaka nyumbani kwa Brian huku akinielezea mambo mengi ya DON na mke wake CLaudi.

“Kwa nini hutaki kuwasiliana na familia yako?”

Swali la Brian likanifanya nishushe pumzi taratibu huku nikimtazama usoni mwake.

“Naipendafamilia yangu. Npo katikati ya matatizo makubwa sana hivyo nisinge familia yangu kuigia katika matatizo haya.”

“Ila wapo kwenye matatizo hususani mke wako. Mke wako amepoteza furaya ya kuishi, mke wako amezaa watato ila katika udogo wao naamini angetamani sana siku watoto hao uje kuwashika na kuwalea kama baba”

Brian alizungumza kwa sauti ya upole huku akinitazama.

“Rashidi maisha ni mafupi sana. Tena sana, kipindi nina miguu yangu miwili, niliamini kwamba kuumwa au kufa ni kwa ajili ya wazee, ndio maana tulikuwa tuna fanya dhambi za kila aina. Ila nilpo kuja kugundua kwamba hii miili yetu, muda wowote na wakati wowowte ina weza kubadilika na hivi ndio unavyo niona. Endapo ningekuwa na familia labda mke na watoto sasa hivi wangekuwa karibu yangu wakinifarii, ila kwa bahati mbaya sina hao watu, kama wewe unao usijaribu kukaa nao mbali eti kisa ni matatizo kaa nao karibu wata kusaidia hata kwenye kipindi cha wewe kuwa katika matatizo”

“Nimekuelewa Brian nita lifanyia kazi”

Simu ya Brian ikaanza kuita, akaitaza kwa muda kisha akanigeuzia.

“Mmaa ana piga video call”

“Mma yangu?”

“Ndio”

“Mpokelee ila usimuambie kwamba nipo hapa”

“Sawa”

“Mama habari yako”

“Sio nzuri kabisa Brian kuna matatizo makubwa.”

Sote tukastuka huku tukitazamana.

“Matatizo gani mwanangu?”

“Jackline ametekwa na watekaji wameomba wapatiwe pesa dola za kimarekani bilioni tano, na wametupa masaa sabini na mbili. Yaani hapa tulipo tumechanganyikiwa mwamangu hatujui hata ni nini cha kufanya”

“Mungu wangu”

Brian alizungumza huku akinitazama. Kwa kuchanganyikiwa huku nikajikuta nikizunguka zungukuka ndani ya chumba hichi.

“Nina kutumia video ya watekaji hao ambao ni Al-Shabab”

“Sawa mama na je mume ripoti kwenye chombo chochote cha usalama?”

“Wamesema tukidhubutu kufanya hivyo wata mkata kichwa”

“Sawa mama nitumie”

“Haya”

Mama akakata simu, huku mapigo yangu ya moyo yakinienda kasi.

“Don Don nilijua tu ata mteka mke wangu ili apate pesa”

Brian akanitazama tu jinsi ninavyo zunguka zunguka ndani ya chumba hichi.

“Video imefika”

Brian alizungumza na kwa haraka nikaichukua simu yake na kuanza kuitazama video hii huku mikono ikinitetemeka kwa hasira.

“Ila maisha yake yaendelee kuwa salama. Tuna hitaji kiasi cha dila bilioni tano. Baada ya masaa ishirini na nne tuta kupigia simu kukueleza ni jinsi gani na namna gani utatutumia hizo pesa na kumpata mwanao”

Mwanaume huyo aliye funika uso wake alizungumza huku akiwa ameweka kisu kikali sana shingoni mwa Claudia aliye fumbwa mdomo kwa kitambaa cheusi. Nikamkabidhi simu Brian naye akaitazama video.

“Masaa sabini na mbili yana nitosha sana kufika nchini Somali”

“So una hitaji kwenda peke yako?”

“Ndio”

Brian akanitazama kwa sekunde kadhaa.

“Ngoja”

Bria akaminya minya simu yake kisha akiweka sikioni mwake.

“Ni mimi”

“Upo Somalia?”

“Basi kuna ndugu yangu ana kua nchini kwako. Ningependa uweze kumpokea”

“Nashukuru”

“Nampatia namba zako sasa hivi”

Brian akakata simu kisha akanitajia namba za mtu aliye mpigia.

“Huyo alikuwa ni mpelelezi wa kikosi cha FBI ila aliweza kuach na kuanzisha kikosi chake ambacho kazi yake ni kulipwa kisha hufanya kazi kutokana na kile wanacho agizwa kufanya. Kwa sasa serikali ya nchi ya Somalia wamemlipa yeye na kikiso chake kusaidiana na jeshi la nchini humo kupinguza uhalifu au makali ya AL-Shabab”

“Nashukuru sana ngoja nimpigie video call”

Nikampigia video call jamaa huyu.

“Nina itwa Rashidi nimepewa namba yako na Brian”

“Sawa sawa, mimi pia nina itwa Brian. Karibu sana”

“Nashukuru ninaye hapa Brian mwenzako, hivyo nina hitaji kuja nchini Somalia, ila nita hitaji kupitia nchini Kenya kisha niingie Somalia kwa usafiri wa gari?”

“Kinacho kuleta nchini Somalia ni nini haswa?”

“Mke wangua metekwa na kundi la Al-Shabab. Hivyo nikikuwa nina hitaji kumkomboa?”

“Al-Shabab ni kundi kubwa sana ambalo lina maeneo mbalimbali wanayo tawala na isistoshe wao ni watu hatari sana.”

“Nalitambua hilo ndugu yangu ila ninacho omba ni kufika nchini Somalia, kabla ya masaa sabini na mbili kuisha”

“Sawa, kutokana namba yangu unayo basi tuta wasiliana”

“Nina shukuru”

“Hembu nimuoene Brian”

Nikamkabidhi simu Brian.

“Kaka”

“Aisee pole sana ndugu yangu”

“Daa nina shukuru. Na mtu aliye nifanyia hivi ndio huyo aliye mteka mke wa jamaa yangu”

“Una taka kuniambia DON yupo hapa Somalia?”

“Tuna amini hilo. Mara baada ya kufanya uhalifu nchini Brazil tuna imani kwa asilimia mia moja amekimbilia Somalia na ndio sehemu alipo jificha kwa sasa”

“Basi ngoja niwataarifu vijana wangu, tuanze kumsaka kimya kimya. Kwa hilo alilo kufanyia basi nita hakikisha naye lazima ana pata haki anayo istahili”

“Nashukuru sana ndugu yangu”

“Basi nita mpokea kijana wako mimi mwenyewe mpakani mwa Kenya na Somalia kisha tuta ni namna gani ambayo tuna weza kumsaka huyu fala.”

“Asante sana ndugu yangu. Mungu akubariki”

“Usijali”

Brian akakata simu huku machozi yakimwagika.

“Rashidi”

“Ndio kaka”

“Naomba unihakikishie uta muua DON”

“Nakuahidi nita muua DON”

“Naomba usimuue haraka, muue kwa mateso ya taratibu taratibu na nita hitaji nishuhudie kifo chake”

“Usijali ndugu, nitafanya kama upendavyo”

“Nashukuru”

Brian akanisaidia wa kupata visa ya haraka ya kuingia nchini Kenya na akanipatia namba za mtu atakaye nisaidia kusafiri naye ndani ya nchi ya Kenya pasipo usumbufu wowote na kunipeleka hadi mpakani mwa Kenya na Somalia. Majira ya saa tisa usiku nikaeleka uwanja wa ndege na safari ikaanza huku nikiwa na hamu kubwa sana ya kuhitaji kumpata DON.

“Naitwa Cecilia wewe je una itwa nani?”

Dada aliye kaa siti ya pembenii yangu ambayo ipo dirishani alizungumza baada ya ukimya wa kama dakika thelathini hivi toka niingie ndani ya ndege hii.

“Ooho mimi ni Rashidi”

“Nashukuru kukufahamu”

“Nashukuru sana”

“Nimeona sio vyema tukae kimya safari nzima ikiwa sisi ni binadamu”

“Yaa ni kweli, samahani kwa kuto kukusalimia”

“Usijali, una jua sasa hivi binadamu tuna kuwa na mambo mengi ambayo yanapekekea vichwa kuwa bize kweli kweli”

“Ni kweli, vipi una elekea wapi?”

“Narudi nyumbani Nairobi, nikikuwa Marekani kwa ajili ya masomo. Vipi wewe una kwenda wapi?”

“Huko huko Kenya”

“Wewe ni mkenya?”

“Hapana mimi ni Mtanzania”

“Ahahaa sawa, Tanzania nina rafiki zangua wanaishi Tanga mjini”

Kitu nilicho kigundua kwa Cecilia ni mzungumzaji sana na ni mtu wa kumzoea mtu asiye mjua kwa muda mfupi sana. Safari ikazidi kusonga mbele huku Cecilia akinisumulia mambo mengi sana ambayo yapo ninayo yajua na yapo ambayo siyajui, ilimradi kuchangamsha safari. Baada ya masaa karibia ya ishirini na mbili katika ndege, tukafika nchini Kenya majira ya saa saba usiku. Nikawasiliana na jamaa ambaye nikimpa taarifa ya kwamba nina kuja nchini Kenya.

“Rashidi nina shukuru sana kwa kampani yako yote uliyo nipatia. Vipi una msubiria nani?”

Cecilia alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Kuna jama nina msubiria”

“Sawa, mimi naona dereva wa baba amekuja kunichukua. Tuta wasiliana”

“Poa”

Cecilia akapokelewa mizigo yake na dereva wao, akanikumbatia kwa nguvu kisha akaniachia huku uso wake ukionyesha kukosa furaha kabisa. Akaondoka nami nikasubiri kwa dakika kama kumi hivi jama huyu anaye itwa Luto akafika, haikuwa ngumu kumfahamu kwa maana nina picha yake. Tukaingia ndani ya gari na kuianza safari ya kuelekea mpakani mwa Kenya na Somalia.

“Karibu sana Kenya”

“Nina shukuru sana”

“Mkuu kila mara ananipigia simu na kuniuliza kama nimekupokea”

“Mkuu wako kivpi?”

“Ahaa….Brian ana kampuni yake kubwa hapa Kenya na Afrika mashariki kwa ujumla. Kampuni yake ina shuhulika na maswala ya hizi takisi pamoja na magari ya usafirihaji hivyo liniambia wewe ni mgeni wake muhimu sana na nina paswa kukupokea vizuri”

“Ahaa sawa sawa. Hadi mpakani ina weza kutugarimu muda gani?”

“Kusipo kuwa na magari mengi sana, ina weza kutugarimu hadi masaa ishirini na sita. Tuna kilomita kama 1679 za kutembea barabarani ila kutokana tuna gari ndogo tuna weza kutembea masaa machache kama wanao tumia basi”

“Duuu nina haraka sana ya kufika Somalia, siwezi kupata usafiri wa ndege hata ya kukodi hadi mpakani?”

“Zipo kampuni nyingi una weza kupata”

“Basi turudi uwanja wa ndege”

“Sawa”

Luto akageuza gari na tukarudi uwanja wa ndege, kwa msaada wa Luto, nikafaniakiwa kupata ndege ndogo inayo ingia watu watano. Nikalipia safari ya kuelekea katika mji Liboi wa mkoa wa Kaskazini-Mashariki. Ndani ya masaa mawili tukafika katika mji wa Liboi majiara ya saa nane usiku. Nikakodisha taksi na moja kw amoja nikaeleka hadi katika mpaka wa Kenya na Somalia, nikaonyesha vibali vyangu vyote na nikaingia upande wa pili wa nchi ya Somalia. Nikapokelewa na Brian na nikaingia katika gari lake aina ya Hammer H3.

“Karibu sana Somalia”

“Nina shukuru sana tena sana”

“Nimeshindwa kuja na timu yangu kwa maana sasa hivi wapo kwenye oparesheni ya kuweza kufahamu kwamba ni wapi alipo DON”

“Kuna kisiwa kimoja kina itwa Sokotra?”

“Nakifahamu”

“Basi nina sikia yupo hapo”

“Ngoja tufike home”

Brian alizungumza huku akiendesha gari hili kwa kasi.

“Ehee niambie una utaalamu wowote wa kutumia silaha?”

“Ndio”

“Una weza kutumia ipi na ipi?”

“Karibia zote nina uwezo wa kuzitumia. Nilipa katika mafunzo ya msituni na kikosi cha Obote na nilisaidiana naye kuipindua serikali iliyo kuwa madarakani na hadi akafanikiwa kuwa raisi”

“Waoo safi sana, ina bidi tukifika uninyeshe ujuzi wako kwa maana huwa mimi ni mgumu sana wa kuamini maneno kuliko vitendo”

“Usijali”

Majira ya saa kumi na moja tukafika katika nyumba iliyo jitenga kidogo na mji na ipo jwangani kiasi. Tukaingia ndani ya geti kubwa la nyumba hii ambayo ime fungwa kamera nyingi. Akanikaribisha sebleni hapa na nikawakuja jamaa wanne walio jazia miili yao kwa mazoezi wakiwa wamekataa sehemu mbalimbali za masofa.

“Karibu sana”

Walinikarimu vizuri huku nikikumbatiaa nao ikiwa ni ishara ya kusalimiana nao.

“Pole sana kwa mke wako kutekwa?”

“Nina shukuru”

“Ehee ripoti mume gundua nini?”

“Tumegundua kwamba DON yupo katika kisiwa cha Sokotra”

Jama ammoja aliye jitambulisha kwa jina la Alex alizungumza, mimi na Brian tukatazamana ikiwa ni ishara ya kwamab nilicho mueleza nikiwa ndani ya gari ni jambo sahihi.

“Kisiwa hicho kwa sasa kime imarishwa ulinzi, na hizi ndio picha za drone tuliyo ituma hapo”

Kijana mwengine anaye itwa Poul alizungumza huku akihamishia anacho kioo kwenye laptop yake hadi kwenye tv hii kubwa iliyo hapa sebleni. Tukaona eneo zima la kisiwa kwa juu, jinsi lilivyo jaa walinzi wenye silaha.

“Na habari mbaya kwamba hatuwezi kwa kwenda kwa njia ya maji kwa maana hapa DON alikuwa amewekeza ufugaji wa Papa wakali sana na endapo ukiingia ndani ya maji na wakikutafuna basi wana kupoteza ndani ya muda mfupi.

“Kwa hiyo Poul una taka kusema njia ya pekee ni kupitia juu?”

“Ndio mkuu na ni hatari sana kwa maana wamefunga kamera zenye uwezo wa kubainisha watu wake na watu wageni na kama una kuw ani mgeni basi Alarm ya eneo zinaanza piga kelele hivyo ina kuwa ni rahisi kwa wao. Pia jengo alilo fungiwa Jackline ni hili hapa na lipo karbu kabisa na nyumba anayo ishi DON kwa sasa”

Poul alizungumza huku akituonyesha nyumba hiyo kwa juu jambo lililo nifanya nitamani hata nianze kufanya taratibu za kumuokoa mke wangu muda huu.



“Tuna weza kupita kupitia njia ya baharini”

Nilizungumza kwa kujiamini na kuwafanya watu wote kunitazama.

“Kivipi kwa maana hatuwezi kwenda na boti hadi kwenye fukwe za hicho kisiwa ni lazima watajua na kutushambulia kabla ya kushuka”

Brian aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Kuna dawa fulani ya majani hivi sidhani kama hapa Somalia ipo. Endapo una jipaka mwilini mwako hakuna mnyama wala kiumbe chochote cha hatari kina weza kukusogelea na hata papa na ukali wake wote hawezi kukusoegela”

“Duuu jamaa hiyo ni bahati na sibu sasa. Mimi kama mimi ninavyo wafahamu papa ni samaki wakali sana, hawana mchezo na endapo tone moja tu la damu likaingia katika maji basi ni msiba”

“Nalitambua hilo Alex ila niamini?”

“Kusema kweli, nisiwe muongo kwa njia ya maji siwezi kwenda, nina omba munisamehe kwenye hilo.”

“Hata mimi mkuu, kwenye swala la maji siwezi kwenda”

“Nimefunga safari kutoka Marekani hadi hapa. Siwezi kuondoka mikono mitupu ni lazima nimuokoe mke wangu”

“Jamaa una zungumza je una mfunzo au una zungumza kutokana na hisia?”

“Nina zungumza kwa maana nina ua nini cha kufanya. Nitakwenda mimi mwenyewe. Ninacho waomba nina omba muniwezeshe nyezo za utendaji wa kazi”

Nilizungumza kwa kujiamini sana huku nikimtazama Brian na wezake machoni.

“Jamani tusikilizaje”

Brian alizungumza mara baada ya ukiya mrefu wa kusikiliz atulicho kuwa tuna kizungumza.

“Huyu ni sawa na ndugu yetu ana shida na yule alishi shikiliwa pale ni mke wake. Endapo mmoja wetu kati yetu ndio mke wake ameshikiliwa je tungekuwa tuna mkatisha tamaa kama hivi angejisikiaje?”

Brian aliwauliza wezake na wote wakaka kimya huku wakionekana kukosa jibu la swali la kuiongozi wao.

“Sasa kama kila mmoja najua angejisikia vibaya. Basi tukae kwa pamoja na kutafuta mbinu ya kuingia kisawnai pale na kumuokoa mke wa ndugu yetu pamoja na kumuua DON. Don amemkata miguu ndugu yetuambaye kwenye kuanzishwa hichi kikosi alikuwa nasi kwa ushauri na mambo mengine ya kututafutia baadhi ya biashara ndio maana kwa sasa familia zetu zina ishi maeneo mbalimbali ya dunia kwa ajili ya pesa nyingi tulizo kuwa tuna pata madili kwa mgongo wa Brian. Hembu tujifunze hata kumrudishia fadhila hata kwa kidogo tu. Haitaji pesa ila ana hitaji kuona DON ana uwawa.”

Brian alizungumza kwa sauti iliyo jaa ushawishi mwingi sana.

“Mkuu tume kuelewa na hakuna aliye kataa kuifanya hii kazi. Ila njia ambayo ya sisi kumfikia adui ndio ngumu, njia ambayo ina hatarisha maisha yetu, je tukifika kwa adui tuna pambana naye vipi. Labda niwaambie papa hawezi kufa kwa risasi moja ama mbili. Hembu jamani tujaribu kutafuta njia, labda tunge ruka kwa maparachuti hapo kidogo ninge waelewa”

“Mkuu anacho sema Alex ni muhimu. Kumbuka kazi yetu tuna ifanya kwa weledi wa hali ya juu. Sasa kwenye hilo la kutumia maji kusema kweli nina ona tuna feli mapema kabla ya oparesheni yenyewe kuanza.”

“Brian”

“Naam”

“Mimi nina omba muniwezeshe baadhi ya mambo baada ya hapo nina kwenda kuifanya kazi mimi mwenyewe wala usijali”

“Vitu gani?”

“Naomba nikuandikie katika karatasi”

Brian akanikabidhi notebook pamoja na kalamu, nikaandika mahitaji yangu yote ninayo hitaji kwenye kazi ya kwenda kumuokoa mke wangu.

“Una uwezo wa kungeneza mabomu?”

Brian aliniuliza mara baada ya kumaliza kuyasoma mahihitaji yangu.

“Ndio”

“Upo vizuri basi. Alex hembu google kama haya majani yana weza kupatikana hapa Somalia”

Brian akamkabidhi Alex notebook hiyo kisha akaanza kuyatafuta kwenye mtando kama mimea hiyo ina patikana na hapa Somalia.

“Yaa ina patikana la wana dai ina kaushwa na kupondwa pondwa na kuwa kama unga. Je ina kufahaa mkuu?”

Alex aliniuliza huku tukitazama dawa ya majani hayo zikiwa zime fungwa vizuri kwenye vikipo.

“Ndio zina faa”

“Poul uta chukua gari na kwenda kununua haya mahitaji ya jamaa huko sokoni”

“Sawa mkuu”

Baada ya mazungumzo haya kukamilika tukapata kifungua kinywa kwa pamoja kisha Poul akaondoka, kuelekea sokoni. Nikaanza kundaa silaha ninazo kwenda kuzitumua, huku nikianza kutengeneza mabomu madogo kwa maumo ila yenye uwezo mkubwa wa kulipua eneo hilo. Mabomu haya niliyo yatengeneza nimeuawake kaika kalamu sita zinazo fanana.

“Nimefanyakazi na watu wa aina mbalimbali, ila sijawahi kukutana na mtu mwenye akili ya haraka ya kuengeneza mabomu kama wewe”

Brian alizungumza huku akizitazama kalamu hizi nilizo zipanga vizuri kwenye meza.

“Ni ujuzi. Ukilitazama hili bomu ni dogo kw amacho ila mzinga wake ni kuanzia mita mia nne kwa mzunguko”

“Duu ni sawa na viwanja vinne vya mpira wa miguu?”

“Ndio”

“Aiisee ni kubwa sana”

Poul akarudi na vitu nilivyo vihitaji na nikaanza kuandaa hawa maalumu ambayo hata nikipita katikati ya kundi la papa hakuna ambaye ata nidhuru.

“Ninge waomba munisaidie katika jambo moja la mwisho”

“Jambo gani?”

“Muweze ku hack kamera za kisiwa kile”

“Hilo nimejaribu ila nime shindwa”

Poul alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Kweli?”

“Yaa mimi ni master wa maswala ya I.T il nimeshindwa na jamaa wana tumia mfumo ambao hakuna satelaite yoyote inayo weza kunasa picha zakisiwa hicho ndio maana nilitumia drone kupiga picha maeneo juu.”

Poul alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Basi nita jua nini cha kufanya”

“Umepanga kuianza oparesheni yako muda gani?”

“Mchana huu”

“Mmmm ndugu mcha kweli?”

Brian aliniuliza huku akiwa na mshangao mkubwa.

“Ndio saa saba nina kwenda kuianza kazi”

“Sawa”

Kitu nilicho kigundua ni kwamba jamaa hawa hawawezi kuifanya kazi ya bure bure, ni Brian pakee ndio aikubali kuifanya kazi hiyo bure ila wezake walinikatalia kisiasa, Nikajianda kwa kila kitu, majira ya saa sita mchana tukaondoka nyumbani hapa. Wakanipeleka kwenye moja ya fukwe, tukapanda boti kwa moja kisha wakaniepeka hadi usawa ambao rada za DON haziwezi kutunasa na Brian akasimamisha bonti. NIkavua nguo zangu za kazi na kuziweka ndani ya begi la mgongoni ambalo ndio nime weka baadhi ya silaha zangu. Nikaanza kujipaka dawa hii mwili mzima ambayo kusema kweli ina nuka vibaya sana. Nikavaa mtungi mdogo wa gesi ya oksijeni, nikaagana na Brian na vijana wake kisha nikazama baharini na nikaanza kuogelea kilipo kisiwa anacho ishi DON.

Kusema kweli jambo hili ninalo lifanya ni hatari sana kwani katika hii bahari kuna sakamaki wa kila aina hadi papa wakali sana. Ila kutokana na dawa hii niliyo jipaka mwilini mwangu hapakuwa na samaki wa aina yoyote aliye weza kunisogelea na kunidhuru. Nikafanikiwa kufika kwenye ufukwe ulio jaa mawe mengi makubwa, nikatafuta moja ya jiwe lililo kaa kama pango nikaingia na kujipata mafuta ya kukata harufu mbaya inayo toka mwilini mwangu. Baada ya harufu kuisha, nikavaa nguo zangu ambazo ni suruali nyeusi, tisheti nyeusi, jaketi la kuzui risasi ambalo lina rangi nyeusi, kofia nyeusi pamoja na buti za jeshi zenye rangi nyeusi. Nikavaa gloves ngumu nyeusi. Nikaziunganisha bunduki nilizo kuwa zimezigawanyisha ili ziwe rahisi kuingia ndani ya beki. Maandalizi haya yote nikayafanya ndani ya dakika kumia nikamaliza. Nikatoa simu yangu na kuitazama ramani ya kisiwa hichi ambayo Poul aliniigizia katika simu yangu.

‘Mungu niongoze katika kazi hii’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiikoki bunduki yangu. Nikaifunga kiwambao cha kuzuia risasi. Ubaya wa kiwa hichi hakina miti mingi na mbaya zaidi ni kwamba miti mingi ni mifupi fupi hivyo mtu huwezi kujificha. Nguo hizi nilizo vaa zina fanania na walinzi wa DON ambao wana randa randa karibia kisiwa kizima. Nikaanza kutembea kwa kujiamini huku begi langu lenye dawa ya kujipaka nikiliacha katika pango la jiwe nililo kuw animejificha.

Kutokana na wingi wa walinzi ambao wote wamevalia kofia nyeusi pamoja na nguo kama zangu ni ngumu sana wao kunigundua kwani lengo kubwa ni kuimarisha ulinzi wa DON. Nikafika katika jumba la Don, nikaingia getini pasipo kustukiwa. Nikazidi kusonga mbele huku nikiwa makini kutafuta jengo ambalo Jackline amefungiwa. Nikafanikiwa kuliona jengo hili, kwabahati mbaya jengo hili lina lindwa na walinzi zaidi ya kumi.

‘Fuc**’

Nilizungumza huku nikitazama walinzi wengi walio lizunguka jengo hili.

“Hei”

Niliisikia sauti ya mwanaume ikiniita nyuma yangu. Nikageuka huku kofia nikiishusha nusu uso.

“Kuna gari la vinywaji limefika, nenda kasaidiane na wengine ushushe”

“Sawa mkuu”

Nilimjibu mlinzi huyu ambaye nina mfahamu ni mmoja wa walinzi wa DON ambaye kila sehemu anapo kwenda huwa yupo naye. Nikapiga hatua kama nne hivi jama akaniita tena.

“Subiri kwanza”

Nikageuka na kumtazama jamaa huyu ambaye ana nifahamu na mimi. Akapiga hatua za makini kunisogelea kabla hajanifikia simu yake ikaanza kuita akaitoa mfukoni na kuipokea.

“Ndio mkuu”

“Sawa nina kuja sasa hivi”

Akaondoka kwa haraka pasipo hata kuniaga. Nikashusha pumzi kwa maana eneo hili nililipo ni eneo la wazi na limejaa walinzi wengi ambao hata kama ninge pigana nao vipi nisinge fanikiwa kuwamaliza, Nikaelekea eneo la la lori lilolo jaa maboksi ya vinywaji, nikaungana na walinzi wengine kushusha mizigo hii na kwa bahati nzuri mizogo hii ina elekea katika jengo alilo wekwa Jackline.

“Nifungulieni nyinyi washenzi, nitawaau, haki ya Mungu vilee”

Nikastuka kidogo mara baada ya kuisikia sauti ya Jackline ikiokea kwenye moja ya chumba huku akigonga gonga mlango kwa nguvu.

“Nawaapia nitawauaaaa”

Jackline alizidi kupiga kelele na kunifanya nitamani kufanya shambulizi la haraka ila mazingira ni magumu sana kufanya shambulizi. Nikaliweka vizuri boksi la chupa za wyne katika eneo yalipo maboksi mengine kisha nikatoka na kueleka kwenye gari huku kazi yangu ikiwa ni kusoma mazingira ya eneo hili kwa umakini wa hali ya juu. Tukamaliza kuingiza mzogo huu ndani ya lori. Nikatafuta sehemu na mimi nikasimama huku nikisubiri kuona ni namna gani ambayo nina weza kupata nafasi ya kumkomboa Jackline.

“Sherehe ya leo usiku itakuwa sio mchezo”

Niliwasikia walinzi wezangu wawili wakizungumza huku wakitiza mbele yangu.

“Yaani nina uchu balaa natamani hata muda uweze kwenda haraka”

Wakakunja kona na sikuhiyaji kuwafwatilia wasije wakanistukia. Jambo linalo nisaidia ni kwamba nime fanya kazi na DON na alinionyesha mambo mengi sana na nina jua ni namna gani ambavyo walinzi wake wanasalimiana kwa ishara hivyo ime kuwa ni kazi rahisi sana kwa mimi kutoa ishara pale ninapo salimiwa kwa ishara.

Majira ya saa kumi na moja jioni yakaingia mabasi sita yaliyo jaa wasichana walio valia bikini pamoja na sidiria tu. Wanawake hawa ina onyesha kwamba wame kuja kwa ajili ya sherehe inayo tarajiwa kufanyika usiku. Mabasi haya nina imani yameletwa na pantone kubwa ya mizigo.

‘Afadhali kazi yangu ita kuwa nyepesi’

Muda ukazidi kwenda mbele na sherehe ikaanza majira ya saa mbili usiku. Kazi ni moja tu kwa watu wote walio katika eneo hilo la DON. Kula na kunywa, DON mwenyewe ndio anaye engoza starehe hii huku wanawake wengine wakifanya mapenzi na walinzi hadharani.

“Vipi hamuli gambe leo?”

Niliwauliza walinzi wawili walio baki nje ya jengo alilo fungwa Jackline.

“Hatuna mtu wa kumuachia hapa”

“Nendeni mukawatomase wanawake wawili watatu mimi nina washikia zamu yenu”

“Sawa sawa. Asante sana”

“Poa masaa mawili basi”

“Usijali kaka”

Walinzi hawa wakaondoka pasipo kunitambua kwamba mimi nipo kinyume na wao. Mziki mzito una rindika eneo hili na shangwe za watu ukanifanya kwa haraka niingia ndani ya jengo hili. Nje ya mlango alio fungwa Jackline kuna kufuli kubwa. Kwa kutumia kitako cha bundiki yangu nikalivunja kufulia hili kisha nikaingia ndani na kumkuta Jackline akiwa amekaa kitako huku akiwa amelegea kwa kuchoka.

“Hei baby ni mimi”

Nilizungumza huku nikivua kofia yangu. Jackline macho yakamtoka japo amechoka, ila hakishindwa kusimama na kunikumbatia kwa furaha. Tukanyona denda la kutosha kisha tukaachiana.

“Ohoo mume wangu, asante Mungu ume kuja”

“Sikia sasa nina hitaji tutoke hapa umenielewa?”

“Ndio”

“Hawajakudhuru?”

“Hapana hawajanidhuru?”

“Vua nguo zako si una chupi na siridiria?”

“Sina diria”

“Basi baki maziwa wazi.”

Jackline hakuhitaji kuuliza maswali mawili. Akafanya kama nilivyo muagiza, tukatoka ndani ya chumba hichi, nikaingia ndani ya chumba cha vinjwani nikachukua chupa mbili za wyne.

“Shika hii na mimi nina shika hii. Tutajifanya kama tume lewa sawa”

“Sawa mume wangu”

Nikazilaza nywele za Jackline usoni mwake kisha tukatoka ndani hapa huku nikiwa nimemshika kiuno. NIkapishana na walinzi wengine ambao nao wamelewa chakari wakiwa na wanawake hawa walio letwa. Hapakuw ana mtu wa kutuuliza tuna kwenda wapi kwani kila mlinzi alimchukua mwanmke anaye mhitaji kwa ajili ya kwenda kustarehe naye.

“Nahitaji kumuua DON ila mazingira na muda haotoshi mke wangu. Jambo la msingi ni wewe kwanza”

“Tuondoke tu hapa mume wangu”

Tukaelekea hadi kwenye eneo nililipo acha begi langu. Nikavua nguo zanangu na kuanza kuipaka dawa hii mwilini mwangu huku Jackline naye akiipaka.

“Tuta tumia kuhema kwa zamu. Hili neo kwa mita kama mita tano hivi kuna papa wakali hii dawa itatusaidia papa kuto kutudhru”

“Mume wangu papa?”

“Ndio, niamini sawa baby”

“Sawa”

Nikavaa begi mgonini mwangu kisha Jackline naye akavaa mtungi wa geni. Nikaishika bunduki yangu vizuri na tukaanza kuelekea baharini. Mwanga wa Mbalamwezi ukatusaidia sana kuona tunapo elekea. Tukaendelea kugelea tukiwa chini ya maji. Kuna muda Jackline akaanz akuogopa mara baafa ya kuona kundi la papa wakija mbele yetu ila nikamshika mkono na tukazidi kwenda chini ya bahari na papa hawa wakapita juu yetu. Kutokana na uchovu wa Jackline tukatumia kama lisa moja na nusu kutokea eneo ambalo Brian na wezake waliniacha. Nikatoa simu yangu ndani ya begi na kumpigia Brian.

“Nimefanikiwa kutoka na mke wangu. Mupo karibu na ufukwe?”

“Ndio tuna kuja hapo muda huu”

“Poa”

Nikakata simu na kuirudisha ndani ya begi, uzuri ni kwamba simu hii haiingi maji kabisa. Ndani ya dakika kumi Brian na wezake wakafika eneo hili na tukaingia katika boti.

“Aisee plan yako ime fanya kazi?”

Alex aliuliza huku akinitazama machoni.

“Ndio maana nipo hapa”

Nilizungumza huku nikitoa shati ndani ya begi na kumvalia Jackline anaye tetemeka kwa baridi.

“Pole sana shemeji”

“Nina shukuru”

“Hawa ni wezangu walioni saidia hapa Somalia”

“Nashukuru kuwafahamu”

“Karibu Somalia. Vipi DON ume mmaliza?”

“Sijamuua kutokana kuna watu wengi sana ambao hawana hatia ya kufa pamoja naye. Ila kwa kupotea kwa mke wangu nina imani wata changanyikiwa na wata msaka na wakimsaka wata msaka mtaani huku Somalia na wakijaribu kuzileta pua zao basi tuta muua mmoja baada ya mwengine na huo ndio utakuwa mwisho wa DON.”

Nilizungumza huku nikitazama kisiwa hichi ambao tuna kiona kwa mbali sana na safari ya kurudi Mogadishu Somalia ikaanza Jackline akiwa amekilaza kichwa chake kifuani mwangu na mara kwa mara ana nitazama na nina hisi ana ona hili linalo endelea sasa hivi ni kama ndoto kwake.



ENDELEA

Tukafika Mogadishu na moja kwa moja tukaeleka katika nyumba ya Brian. Kutokana na baridi kali sana iliyo mpiga Jackline baharini, akaandaliwa kikombe cha chai kahawa na akaanza kunywa.

“Kahawa na wewe”

Brian aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Sihitaji”

“Aiisee Rashidi kumbe plan yako ilifanya kazi?”

“Ndio”

“Hongera sana”

“Nashukuru”

Jackline akamaliza kikomba hichi cha kahawa, kisha tukatengewa chakula na tukala kwa pamoja. Tukaonyeshwa chumba cha kulala natukaingia ndani. Hapakuwa na maongezi yoyote zaidi ya kupeanama mapenzi motomoto kwani kila mmoja ana hamu na mwezake. Mtanange wetu ni wa kukata na shoka, hadi tukaridhishana.

“Asante mume wangu kwa kuja kuniokoa”

“Usiali, vipi wamekudhuru kwa chochote?”

“Hapana, ila wamewaua walinzi wangu wawili nilio kuwa nime ambatana nao”

“Pole sana”

“Nashukuru Mume wangu. Ulikuwa wapi siku zote hizo?”

Cauther alizungumza huku akiwa amekilaza kichwa chake kifuani mwangu.

“Nikashusha pumzi nyingi huku nikijaribu kupangilia matikio ya kumdanganya Cauther juu wa wasichana nilo kuwa nao kwenye mahusiano kipindi nilipo toka nchini Congo. Nikaanza kumuadithia Cauther kuanzia siku nilipo tekwa hadi nilio jikuta nikiwa gerezani nchini Congo. Nikamueleza jinsi nilivyo pitia mateso ya msituni kabala ya kujiunga na wanajeshi wa Obote na kumpindua serikali yake. Nikakiruka kipande cha maisha niliyo fanya nchini Tanzania, nikamueleza mara baada ya ungozi wa Obote kusimama vizuri, nikaelekea nchini Brazili kumsaka DON.

“Sasa kwa nini mume wangu usirudi nyumbani kwanza kuwaona wanao, kuniona mimi, mama na baba.”

“Najua ingekuwa ni jambo gumu sana kwa mimi kurudi kwa kipindi kile kabla sijaikamilisha kazi yangu kwani adui angeniondokea furaha yangu na angeidhuru familia yangu kwa kuwa karibu nayo. Ila nisemehe sana mke wangu kwa maana nime kuumiza moyo wako na ume jawa na maswali mengi sana. Ila raisi wa sasa Tanzaia na Don hawa ndio maadui zangu kwa sasa”

“Pole mume wangu, nina imani kwamba hii vita tuta ishinda tu”

“Mungu ni mwema, lazima tuishinde. Nina kupenda sana mke wangu”

“Nina kupenda pia mume wangu. Ulijuaje nimekuja huku?”

“Brian aliniambia”

“Wee kumbe Brian ana mawasiliana nawewe alafu hakuniambia?”

“Hapana, nimewasiliana naye juzi juzi tu na nilipo toka Mexco nika enda Marekani kumuona kwa kweli Don amefanyia ukatilia mkubwa sana”

“Aliniambia kwa kweli nilijisikia uchungu mwingi sana. Sasa mume wangu si turudi Ufaransa tukaendelee na maisha ya kuelea familia yetu. Hadi sasa hivi watoto wako hawajakuona na hawajui baba ni nani. Tafadhali mume wangu. Sihiaji kuwa ndani ya hii nchi na nina juta ni kwa nini nime kuja hapa kwani nime wapoteza walinzi wangu mahodari wawili.”

“Tukirudi Ufaransa ndivyo jinsi tutakavyo wapoteza watu wetu wa karibu. Mke wangu hii ni vita, ni vita tunayo pigana na mtu mwenye mtandao mkubwa sana duniani. Ni vita ambayo endapo tusipo kuwa makini. Mimi wewe, watoto wazazi wote wata kufa mke wangu. Ndio maana niliachagua kujitoa sadaka kwajaili yenu, nielewe mke wangu nini namaanisha ninacho kizungumza”

“Nime kuelewa mume wangu. Nini kina fwata?”

Jackline aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu. Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama Jackline usoni mwake.

“Ni kurudisha mashambulizi kwa Don. Nitakacho kuhitaji ni kuwapigia wazazi na kuwaambia kwamba upo salama ila usiwaambie kwamba mimi ndio nime kuokoa”

“Mume wangu kwa nini?”

“Moja, ni lazima mama ata hitaji nirudi Ufaransa na kama unavyo fahamu nguvu ya mama kwa manaye wa kiume. Mama anaweza akaongoza na hisia za kuhitaji kuniona pasipo kujua ni uzito gani wa mambo tunayo pitia kwa sasa. Hivyo kama una hitaji tummalize Don huku huku, ni lazima nipambane naye kabla ya kurudi nyumbani na nikirudi nyumbani nipokelewe kama shujaa mke wangu”

“Nakupenda sana Rashidi”

“Nina kupenda pia mke wangu”

Tukalala hadi saa mbili asubuhi nikawa wa kwanza kuamka, nikoga kisha nikatoka chumbani hapa na kumkuta Brian na wezake wakitazama video inayo rekodiwa na drone, ina oneysha jinsi wasichana walio pelekwa nyumbani kwa Don wakiwa wamepanga katika mistari miwili huku wakikaguliwa na anaye kaguliwa ana ingia ndani ya basi. Nikasalimuana nao kisha nikajumuika katika kutazama video hiyo.

“Wana wafanyaje hao?”

Niliuliza huku nikindela kuitazama video hiyo.

“Wamegundua kwamba shemeji ametoroka naona wana msaka kwa nguvu zote”

“Sidhani kama wanaweza kuhisi kwamba nime toroka kupitia njia ya baharini”

“Yaa hapo wala sidhani kama wanaweza kufikiria hilo”

“Lazima wata fwatila cctv kamera zao kuchhunguza alitotokaje”

“Akijua kama ni mimi ana weza kufa kwa mawazo DON”

“Nahisi Saomalia nzima ana weza kuifunga. Alafu ubaya wa nchi hii. Kuanzia vionogozi wa ngazi za juu hadi za chini wana penda sana kulako rushwa. Hivyo kama ukijitokeza huko uraiana bas ina kuwa ni rahi sana kwa wao kukutaha ili maradi wapate pesa”

“Kama bado nipo hai ni lazima Don nimuue tu”

Zoezi la kuwakagua wasichana hao likaisha na msimamizi wa zoezi hilo ni mlinzi namba moja wa DON. Tukamuona kijana mmoja akimnong’oneza mlinzi huyo sikioni mwake na akamuonyesha kitu kwenye ipad aliyo ishika.

“Poul hembu Zoom”

Brian alimuambia Poul ambaye ndio anaiendesha drone hiyo iliyopo juu ya anga la jumba hilo la DON. Akavuta picha ya karibu katika ipad hiyo na sote tukatazamana mara baada ya picha yangu na Jackline kuonekana tukitoka ndani hapo.

“Wametambua”

(UKIHITAJI MUENDELEZO WA HADITHI HII EPISODE MOJA SH 250. UTA PATA KUPITIA WHATSAPP 0657072588 AU FACEBOOK INBOX KATIKA UKURASA WANGU WA Story Za Eddy-tz KARIBU SANA)

Tukaanza kuona walinzi wakitawanyika na wangine wakikimbilia baharini na kupanda maboti na kuanza kutawanyika wakihakikisha wana tusaka. Tukamuona DON akitoka ndani ya jengi hilo, naye akaelekea ufukweni na kupamba moja ya boti na oparesheni ya kutusaka mimi na mke wangu ndani ya bahari ikazidi kupamba moto.

“Hivi yale mabomu yako ya kalamu uliyaacha kule?”

Brian aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Hapana”

“Daa huu ungekuwa wakati sahihi wa kulipua jumba lake hilo ili tumtie wendawazimu”

“Hivi hiyo drone hawezi kubebe silaha?”

Niliwauliza huku nikiwatazama usoni mwao.

“Zile hatuna kwa maana zina milikiwa na jeshi la Marekani, drone zile ni kubwa na zina kwenda kwa mwendo wa kasi sana. Ma opareta wake huwa wana kaa Marekani, wana lipua Somalia”

“Habari za asubuhi jamani”

Salamu ya Jackline ikakatisha mazungumzo yetu”

“Salama shemeji umeamkaje”

Kila mmoja akamsaimia Jackline kwa furaha.

“Salama jamani”

Jackline akaanza kupika kifungua kinywa na kwa pamoja tukapata kifungua kinywa hicho.

“Mke wangu ina bidi uwasliane na nyumbani na uwaeleze kwamba upo salama ila usiwambie kwamba tume oanana”

“Usijai baby. Nitawaambia kwamba Brian na vijana wake wama niokoa, baba yangu ata furahi sana na nina Imani ata mpatia shemeji zawadi kubwa sana na rafiki zake”

“Hilo ni jambo zuri mke wangu au una semeje?”

“Ila sisi hatujafanya kazi yoyote kaka. Tuta kuwa tuna pata ujiko wa bure kabisa”

“Hata kunipokea na kuniwezesha kwenda nilipo kwenda nao pia ni msaada mkubwa sana. Anacho kifanya mke wangu ni sahihi”

Tukakubaliana kwa pamoja kwamba Jackline ata waeleza wazazi kwamba Brian na kikosi chake ndio wailio muokoa. Jackline akapiga video call kwa baba yake.

“Halloo baba”

“Jack una endeleaje mwanangu”

“Nina mshukuru Mungu, hi mama mkwe”

“Oho Jackline una endeleaje?”

“Nina mshukuru Mungu nipo salama wazazi wangu. Nimefanikiwa kuokolewa kutoka mikononi mwa DON”

“Ni kina nani walio kuokoa”

“Brian ana ndugu zake ambao mmoja wao ni Brian alimueleza hai halisi ilivyo tokea hivyo akaniokoa”

“Ooohh Mungu ni mkubwa sana mwanangu. Ina bidi urudi Somalia haraka iwezekanavyo”

“Hapana baba”

“Una maana gani kusema hapana?”

Jackline akanitazama huku nikiwa nimesmama pembeni yake.

“Eti”

“Baba, nikirudi sasa hivi Ufaransa DON ata itwafwata familia nzima. Ata wadhuru na nyinyi pia. Ndio maana nime ona ni heri kukaa huko kuliko kuja huku”

“Hapana Jackline, ukiendelea kukaa huko hali ina weza kuwa mbaya zaidi, ana weza akakukamata tena na safari hii ana weza akakuu kabisa. Kama uta shindwa basi mimi nita kufwata. Wanao kila siku wana niuliza babu, mama na baba wapo wapi. Sheila kama unavyo jua kila siku una mdanganya kwamba baba yupo kazini na anakubaiana na wewe, sasa hivi nani wa kumdanganya. Sheila amekuwa ni mnyonge sana, hali na hata shule haendi kabisa ana kata. Hata bibi yake amemshindwa, na jana tu ametuuliza je baba na mama Jackline wame kufa. Tulishindwa kujibu swai hilo kutokana na kigumizi. Sisi ni watu wazima tuna weza kuelewa, je Sheila na wadogo zake ina kuwaje kwa upande wao”

Baba mkwe alizungumza kwa uchungu sana na huku machozi yakimtiririka sana na kumfanya Jackline naye kumwagikwa na machozi.

“Niambie mwanangu, sisi tuna fanya nini hawa wanao. Baba yao hatujui kama yupo hai au amekufa”

“Mume wangu hajakufa na ata rudi tu”

Jackiline alizungumza kwa msistizo huku machozi yakimwagika usoni mwake.

“Baba wa wanangu yupo hai nina amini hilo”

“Una aminije ikiwa ni mwaka wa pili sasa hatupo pamoja naye. Tafadhali mwangu kama una endelea na oparesheni yako ya kumsaka baba Shamsa ni vyema ukaisitisha. Au muna taka watoto wenu wabaki yatima?”

Swali la baba mkwe likaniumiza sana moyoni mwangu na kujikuta machozi yakianza kunilenga lenga. Kwenye maisha yangu nimesha kutana na rafiki zangu walio ishi yatima kipindi tupo watoto. Kuishi kwao kulikuwa ni kwa shida nameteso. H apakuwa na hata mmoja niliye mshuhudia akiishi maisha mazuri na mbaya zaidi walikuwa kwenye genge langu la wauni.

“Jackline mkwe wangu”

“Ndio mama”

“Mimi ndio mama mzazi wa Rashidi. Nina fahamu uchungu wa kupoteza mototo. Nina Imani maumivu uliyo yapata siku una jifungua ni maumivu ambayo niliyapata mimi. Tafadhali kwa moja mmoja nina kuruhusu mwanangu rudi Ufaransa. Kama baba Shamsa yupo hai basi mwenyezi Mungu ata msaidia na ata rudi salama ila kama hayupo hai, tuta fanya ibaya ya kumuombea na mwenyezi Mungu ata ilaza roho ya marehemu mahai pema peponi ameni”

Mama alizungumza kwa hisia kali iliyo ambatana na machozi mengi sana. Jackline akanitazama kisha akakata simu, akanyanyuka na kuondoka sebleni hapa na nikajikuta nikimfwata kwa nyuma na tuka ingia chumbani.

“Rashidi niambie ni nini una taka mume wangu. Nimejikaza kuwadanganya wazazi ila nime shindwa. Ona mama na baba wanavyo lia. Vipi machozi yao hayakuumizi wewe. Hupati maumivu yoyote moyoni mwako wewe eheee?”

Jackline alizungumza huku akilia,

“Don, Don, Don, amekuwa ni nani kwako hadi una itekelekeza familia yako kwa madai ya kuilinda. Hembu achana na mawazo yako. Nina taka turudi nyumbani pamoja”

Jakcline aliongea kwa msisitizo huku macho yakimtoka.

“Kam mimi ni mke wako, mama wa wanao na kama una nipenda tuna rudi Ufaransa ila kama hutupendi. Usikae ukafikiria kurudi Ufaransa hata kama ukiwa umesha maliza kumuua huyo DON wako unaye muona ni wa muhimu sana kwako”

Jackline mara baada ya kuzungumza akavua suruali yake na akapanda kitandani na kulala kifudi fudi huku akilia.

“Mke wangu”

“Sitaki uniongeleshe chochote hadi pale utakapo niambia kwamba upo tayari kwenda Ufaransa au laa”

Nikashusha pumzi taratibu kwa maana hili linao endelea sasa hivi ni mtihani na Jackline hatambui ugumu na uzito wa jambo hili.

“Sawa tuta rudi Ufaransa”

Jackline akageuka na kunitazama usoni mwangu.

“Una maanisha unacho kizungumza”

“Ndio”

“Kesho nina hitaji tuondoke”

“Kesho haiwezekani”

“Kwa nini?”

“Hatuwezi kupanda ndege, meli wala chochote kwa maana watu wa Don wapo kila sehemu. Mke wangu hili jambo lina uhatari mkubwa kuliko unavyo fikiria. Don ni lazima ata fanya chochote kuhakikisha ana kupata. Hivyo tafadhai mke wangu kuwa makini kwa kila jambo, hisia zisikuongoze”

“Kwawa hiyo nilicho kizungumza ni upumbavu?”

“Huko unapo elekea mke wangu una taka kuni udhi umenielewa”

Ili nibidibi kumjia juu kidogo Jackline kwani bila ya kufanya hivyo mambo ana weza kufanya ujinga ambao una weza kutugarimu. Jackline akakanitazama machoni mwangu na kweli akaanza kuona hasira yangu ikitawala usoni mwangu.

“Nimyatoa maisha yangu kwa ajili yengu kwa ajili yenu na nina fanya kila linalo wezekana ili wewe na wangu muweze kuwa salama salmini. Unahisi kuna mwanaume gani ambaye ana weza kupita kwenye bahari iliyo jaa papa wakali na akahatarisha maisha yake. Kuna mwanaume gani anaye weza kuingia kwenye ngome ya mtu hatari kama DON akiwa ana jiamini kwa ajili ya mke wake. Fikiria mara mbilimbili mke wangu. Usitake sasa hivi nianze kurudi tena mikononi mwa DON na kuwa mtumwa wake. Umenielewa”

Nilizungumza kwa ukali ambao Jackline toka anifahamu hakuwahi kuniona nikiwa katika hai hii.

“Tutaondoka Somailia pale tu nitakapo sema tuna ondoka kwa maana DON ametambua kwamba mimi ndio nimekutorosha hivyo hapo aipo ana hasira na chuku dhidi yangu. Tulizana mama”

Mara baada ya kuzungumza hivyo nikatoka ndani hapa na kumuacha Jackline kwenye hali ya unyonge. Nikawakuta Brian na vijana wake wakiwa sebleni.

“Nina hititaji kumuwinda DON, ametoka kwenye himaya yake sasa ni wakati wa kupambana naye”

Nilizungumza kwa msisitizo, Brian na vijana wake hawakunijibu chochote. Brian akaminya remote ya tv na kuiweka habari inayo endelea. Nikatazama habari kutoka CNN ikonyesha video ambayo DON alinitishia kuisambaza kwenye vyombo vya habari akidai kwamba mimi ni mkuu wa kundi la Al Shabab na nimehusika katika kuilipua meli ya kivita ya jeshi la Tanzania.

“Una lipi la kujitete katika hili?”

Brian alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Nikawatazama wote kisha nikakaa kwenye moja ya sofa huku nikiwatazama.

“Imetengenezwa hiyo video”

“Ime tengenezwaje ikiwa hapo ina onyesha wana kikosi cha NSS wakiwa wana kukabidhisha mikononi mwa kundi la AL Shabab ambao waliiteka hiyo meli ili wewe uachiwe huru?”

Alex ainiuliza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu”

“Ndio nina fahamu hilo. Ila huyo ni DON na watu wake na aisha nionyesha hiyo video kipindi tupo Brizil na ainikabidi kazi ya kwuaua matajiri alio hitaji walio kuwa nchini Brazil. AIiniambia kwamba endapo sinto ifanya kazi hiyo basi ata isambaza video hiyo na kila mtu ata iona na nita tangazwa kama gaidi wa dunia. Kwa jinsi nilivyo siwezi kuisaiti nchi yangu, nina ipande nchi yangu japo kuna watu wana hitai niiishi kama mkimbizi kama muna hitaji udhibitisho dhaidi waslianeni na Brian”

Jackline akatoka ndani na kuifwatilia video hiyo, akanitazama huku akiwa na macho ya mshangao.

“Kuna nini kinacho endelea?”

Jackline alituuliza na sote tukaa kimya pasipo kumjibu. Vijana wa Brian kila mmoja mkono wake amauweka karibu kabisa na bastola yake ili kama nikifanya madhara yoyote basi wanimalize. Brian akampigia simu Brian wa nchini Marekani.

“Ndugu yangu una endeaje?”

“Nina mshukuru Mungu, kuna kitu gani kinacho endelea. Mbona Rashidi ametangazwa kama gaidi anaye sakwa na nchi ya Tanzania na raisi wa Tanzania ametangaza kitita cha dola milioni mia moja kwa mtu atakaye fanikishwa kukamatwa kwake. Ina kuwaje hapo?”

kishwa kukamatwa kwake. Ina kuwaje hapo?”

Watu wote tulilisikia swali la Brian na kuwafanya watu wote kunitazama mimi kwani jamaa hawa wapo kwa ajili ya pesa na kama serikai ya nchi ya Tanzania wametangaza kiasi hicho cha pesa bas kuna asilimia kubwa sana kwa wao kunikamata na kunikabidhisha katika serikali ya Tanzania na kama wakinikabidhisha kwa serikali ya Tanzania basi kinacho fwata ni mimi kunyongwa hadi kufa kitu ambacho kwa sasa sikihitaji wala kufirikia kwenye maisha yangu.




“Hata sisi tulikuwa tuna hitaji kufahamu kutoka kwako kwamba mtu uliye tuletea je ni gaidi kweli kwa maana kama unavyo fahamu sisi tuna dili na magaidi sasa kama gaidi yupo kwenye kikosi chetu ina maana emakuja kutumaiza”

Brian alizungumza huku akinitazama kwa macho makali sana ya kunidadisi.

“Kwa Rashidi ninaye mfahamu mimi, nina uhakika wa asilimia mia moja hawezi kujiunga na Al Shabab na nyinyi muna ujuzi wa kumjua gaidi na mtu wa kawaida”

“Sawa ila pia ni ngumu sana kumfahamu mpelelezi”

“Najua ila hili linalo endelea sasa hivi nina imani ni mipango ya DON kwani DON nimefanya naye kazi kwa kipindi kirefu na nilikuwa sambaba na mke wake ambaye ana jua siri zake nyingi sana hivyo hata hili linao endelea ni mpango wa DON.”

“Sawa kaka nime kuelewa”

“Rashidi yupo wapi?”

“Nipo naye hapa”

“Naomba nizungumze naye”

Brian akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akanikabidhi simu na nikatazamana na Brian.

“Kaka pole kwa hili linalo endelea”

“Nina shukuru sana ndugu yangu”

“Najua ni DON ndio aliye fanya hivyo. Ila kuidhibitishia dunia kama wewe sio gaidi hakikisha kwamba una mkamata na kumfanya akiri mbele ya video kwamba yeye ndio yupo nyuma wa mipango yote miovu duniani. Nina kuandaia mawakili wenye uwezo wa kukusimamia kwenye hii kes ila kikubwa tu tumpate DON”

“Nashukuru ndugu yangu na nime fanikiwa kumuokoa shemeji yako”

“Kweli?”

“Ndio”

Nikamuita Jackline na akakaa pembeni yangu kwa maana mawasiliano haya ni kwa njia ya video.

“Shemeji pole sana”

Brian alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.

“Asante sana shemeji nipo salama sasa”

“Aisee tulipata wasiwasi mkubwa sana nilipo sikia ume tekwa”

“Poleni niliwapa wasiwasi, ila nime okolewa sasa hivi nipo salama kabisa”

“Sasa ina bidi muwe makini kwa maana Don amesha mpatia kashfa kubwa sana ndugu yangu hivyo nina imani kwamba atakuwa ana sakwa dunia nzima sasa hivi”

“Sawa shemeji naomba umsaidie sana mume wangu”

“Usjali mimi nina andaa wanasheria hodari sana duniani wana weza kusmamia kesi kama hizi”

“Asante sana shemeji, najua DON amekufanyia ukatili mkubwa ila nina kuahidi kwamba ni lazima apatikane na akipatikana ata lipa kwa mabaya yote aliyo yafanya”

“Nashukuru kwa kunitia moyo shemeji yangu”

“Usijali shemeji”

“Rashidi”

“Ndio kaka”

“Usijaii kaka mimi nina dili na hili swala kisheria.”

“Nashukuru sana ndugu yangu”

“Usijali tupo pamoja”

“Poa”

Nikamrudishia Brian simu yake.

“Ndio kaka”

“Musiwe na wasiwasi na kijana ni mtu mzuri na mumpe ushirikiano wa kutosha kabisa”

“Sawa kaka”

Briana akakata simu huku akinitazama. Nikawatazama vijana wake na wana onekana hawana uchangamfu kama walio kuwa wana nionyesha hapo awali.

“Kikos chetu au changu hakidili na watu ambao sura zao zipo public kama sasa. Tukiendelea kukaa na wewe na dunia ikafahamu kwamba tupo na wewe wana weza kutuchukulia sisi nasi ni magaidia ikiwa sisi tuna dili na magaidi. Hatuhitaji kukuchafulia mipango yako wala dhana yako ya kumsaka DON. Tuta kuruhusu uondoke salama salmini mikononi mwetu. Tuambie nini una hitaji tukupatie kwani kuendelea kukaa nasi hapa ina weza kutufanya akatokea mmoja wetu akatusaiti kwa ajili ya hizo milioni mia mija moja namambo yakawa ndivyo sivyo”

Nikashusha pumzi nyingi sana huku nikitazamana na mke wangu. Kusema kweli Brian amefanya maamuzi makubwa tena ya kiume.

“Usiogope zungumza”

Alex alizungumza huku akinitazama usoni mwangu”

“Nahiahitaji sihala, gari pamoja na pesa itakayo niwezesha kutoka nchini hapa”

“Kama kias gani?”

“Kama ina wezekana tuna omba dola elfu ishirini. Mutaniambia ni namba gani niwaingizie hicho kiasi cha pesa, bei ya gari pamoja na silaha”

Jackline alizungumza huku akiwa na uchungu mkubwa sana machoni mwake kwa maana hili swala la DON kuitoa video hiyo kwa waandishi wa habari ita msaidia sana katika kunitafuta kwani nikikamatwa na jeshi lolote, nina imani ana watu wake ambao wata nikabidhi kwanza kwake kabla ya kufikishwa katika serikali ya nchini Tanzania.

“Sawa”

Maandalizi ya vitu ninavyo hitaji yakaanza kufwanya. Tukapewa nguo za kijeshi la Somalia, pamoja na kofia zake. Wakatukabidhi gari aina ya Range Rover Sport yenye rangi nyeusi. Safari ya kuondoka nyumbani kwa Brina na vijana wake ikaanza.

“Hakuna binadamu mwema duniani”

Jackline alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Kwa nini mke wangu”

“Kulikuwa na haja gani ya wao kuturuhusu kuondoka, kisa video ya kusingiziwa. Yaani sijui hata tuna elekea wapi mume wangu”

“Ina bidi tubadilsihe kila kitu”

“Una maanisha nini mume wangu”

“Nguo, gari, ina bidi tubadilishe. Wana weza kufunga device tracker ambayo ina weza kutuonyesha kila tunapo kwenda alafu waka tuzunguka na kuwapatia code hizo wahusika wa Tanzania na mwisho tukajikuta tuna kamatwa kisha wao wakajipatia milioni mia moja hizo kirahisi kabisa”

“Hapo ume nena mume wangu. Sasa hapa Somalia kuna mtu unaye mfahamu?”

“Sina ninaye mfahamu ila usijali tuta mpata. Hizo nywele zako ndefu ina bidi uzikate na kuziweka brichi sijui nini”

“Sawa mume wangu”

Nikasimamisha gari nje ya duka moja la nguo. Nikaiweka vizuri kofia yangu na nikashuka ndani ya gari huku nikimsisitizia Jackline kuto kushka ndani ya gari. Nikanunua nguo za mke wangu. Nikanunua miwani pamoja kofia kisha nikarudi ndani ya gari.

“Utabadilisha hizi nguo”

“Sawa mume wangu. Nibadilishe sasa hivi?”

“Hapana nita kuambia”

Tukafika kwenye moja ya gereji kubwa. Nikashuka ndani ya gari na kuingia ndani ya gereji hii na watu wote walipo ndani hapa wakaacha kazi na kunitazama, kutokana kofia yangu nime ishusha nusu uso skuwa na wasiwasi wowote.

“Ndio mkuu”

Kijana mmoja alizungumza huku akinisogelea. Akanipa mkono wake wa kulia, nikautazama kwa sekunde kadhaa kisha nikampa mkono wangu.

“Nahitaji kufanya mabadilishono ya gari. Nahitaji sport car, je naweza kupata?”

“Hilo ni swala la kuzungumza na mmiliki wa gereji”

“Muite”

Kwa saikolojia niliyo wasoma watu wote humu ndani wana onekana kuogopa sana mavazi niliyo vaa na hapa nikagundua kitu kwamba hawa jamaa wana dili na gari za wizi kwani asilimia kubwa ya gari nilizo zikuta ndani hapa zina badilisha badilisha ili mradi zisifananie na za mwanzo. Akaja mzee mmoja mnne na mwenye tumbo kubwa kiasi. Nikasalimiana naye huku nikimtazama kwa kujiamini.

“Ndio”

“Nina gari yangu hapo, nahitaji kubadilisha na kupata gari ambayo ni sport car”

“Wewe ndio uliye simamisha hiyo Range sport hapo nje?”

“Ndio”

“Una weza kuingiza humu ndani?”

“Ndio”

“Ilete basi tuiangalie”

Nikatoka ndani ya gereji hii kubwa. Nikaingia ndani ya gari na kumtazama Jackline usoni mwake.

“Baby si una weza kutumia bastola”

“Ndio mume wangu, yaani kukaa na wainzi kipindi chote hicho nisweze kwa kweli?”

“Tuna ingia ndani na hawa jamaa wana onekana ni majambazi wanao teka magari. Chochote watakacho jaribu kukifanya kibaya dhidi yetu basi sisi tuwe tayari mke wangu”

“Poa na nina muda mrefu sana sija pambana”

Nikatabasamu huku nikitazama jinsi geti kubwa la gereji hili likifunguliwa. Taratibu nikaingiza gari ndani ya gereji hii, kisha nika shuka huku nikimtazama mzee huyu. Jackline naye akashuka huku macho yake akiangza angaza kwa watu wa humu ndani.

“Muna hati miliki ya hii gari”

“Ndugu tunacho hitaji ni gairi. Tena nyenye nguvu, nina imani katika gari hizi hapa ndani hakuna hata gari yenye bei kubwa kulilo gari hii, si ndio?”

“Ndio mkuu”

“Nipatie gari nzima, inayo tembea kwa mwendo mrefu. Yenye uwezo wa kuhimili mikiki mikiki ya barabarani”

“Ila mkuu hii gari ni nzuri pia?”

“Ndio ni nzuri ila nina hitaji nyingine. Mbona hujamini kama sio mfanya biashara. Hizo gari zote hapo s za wizi?”

Nilimchimba mkwara kana kwamba ninacho kizungumza nina kijua vizuri ila ukweli ni kwamba nina bahahitasha tu.

“Nime kuelewa mkuu tusifike mbali”

Mzee huyu alizungumza huku akitembea hadi kwenye gari moja lililo funikwa kwa turubai akalifunua gari hilo.

“Waooo”

Jackline alizungumza kwa furaha huku tukitazama gari hii aina ya bmw 5 series.

“Mkuu hii gari tumeiongezea uwezo wa kukimbia na kuifunga turbo zenye nguvu kubwa hivyo una weza kuitazama kwa ndani”

Nikaingia ndani ya gari hili, nikaitazama vizuri na uzuri gari hii ina nguvu na uwezo wa kuhimili hata kwenye barabara zisizo na lami. Baada ya makabiziano haya, tukahamisha mizigo kwenye gari hii na kuondoka gereji hili.

“Hii gari ni nzuri sana mume wangu”

“Yaaa”

“Tuna elekea wapi?”

“Nahitaji tutoke hapa Somalia, tuelekee Kenya”

“Mmmm Kenya ita kuwa salama kweli kwako?”

“Ndio sehemu ambayo nina imani tuta pata tulizo”

“Mume wangu hapana, bora twende Congo kwa yule rafiki yako ambaye ni raisi ata tusaidi”

“Yeye na Don akili zao ni sawa”

“Una maana gani kusema hivyo?”

“Niligombana naye kutokana na uongozi wake wa unyanyasaji kwa watu wake ikiwa sio kile alicho kuwa amekidhamiria siku ambayo alichukua madaraka.”

“Duuu, nime pata wazo mume wangu”

“Wazo gani?”

“Tusiondoke Somalia”

Nikajikuta nikisimamisha gari pembezoni mwa barabara na kumtazama Jackline usoni mwake.

“Ndio mume wangu.Kuondoka kwetu Somalia kuna dhihirisha kwamba tuna muogopa DON. Tunapaswa kurudisha mashambulizi kwake, tuna pasa kumpiga yeye. Japo tupo wachache, ila nina anza kuielewa maana yako ya wewe kukataa kuondoka huku Somalia. Tupambane pamoja mume wangu kwa ajili ya familia yetu”

Jackline alizungumza kwa msistizo huku akinitazama usoni mwangu.

“Katika siku uliyo zungumza point ni leo mke wangu”

“Nashukuru mume wangu. Kama ni kufa basi tufie hapa ila kama ni kulisafisha jina lako basi tulisafishie hapa hapa”

Taratibu nikamsogelea Jackline na tukaanza kunyonyana denda taratibu.

“Nakupenda mke wangu”

“Nina kupenda pia mume wangu. Kama uliyahatarisha maisha yako kwa ajili yangu bas ni wakati wa mimi kushikamana nawe kwenye hii shida, snto jali dunia ina kuitaje ila kikubwa nina jua mume wangu haupo kama vile wanavyo kuita kwa sasa”

“Nashukuru mke wangu”

“Nashukuru nawe pia mume wangu kwa kunikaribisha kwenye maisha yako”

“Amen”

Tukaachiana na Jackline kisha tukatafuta hoteli ya bei ya chini sana, ambayo ipo katika maeneo ambayo kundi kubwa la watu wanao ishi huku ni masikini ambao hawawezi kumiliki vitu vya garama kama tv. Tukapata chumba kimoja ambacho kina kitanda cha chumba ambacho godoro lake lime isha sana.

“Uta weza kuishi hapa mke wang

“Popote nina ishi mume wangu. Mimi sio yule Jackline wa kuishi katika majumba ya kifahari. Jackline wa sasa ni yule aiye pata funzo la kuhusiana na maisha maisha magumu na maisha yaliyo jaa tabu na mateso”

“Asante sana”

“Karibu mume wangu”

Katika nguo nilizo zinunua kuna kanzu na ijabu ambazo nina jua ndio mavazi makubwa ya watu wa hapa Somaia. Hatukuitaji kupoteza muda, nikatoa mkasa na kuzikata nywele ndefu za Jackline na akabakiwa na nywele fupi fupi. Nikamaka brichi iliyo badilisha nywele zake kutoka kwenye rangi nyeusi hadi rangi ya dhahabu. Nilipo hakikisha sasa mke wangu amebadilika kwa asilimia kubwa, nikabandika ndevu za bandia nilizo zinunua wakati tuna tafuta vyumba. Ndevu hizi zika nifanya nifananie kabisa na wanaume wa hapa Somalia ambao wengini ni waislamu. Tuliopo hakikisha mionekano yetu ipo tofauti kabisa na hapo awai, tukaondoka eneo hili na kuelekea katika hoteli yenye hadhi kidogo.

“Kwa nini tuna badilisha badilisha hoteli mume wangu?”

“Kwa sababu nahitaji kutengeneza maeneo ya kupanga matukio na maeneo ya kupumzikia. Hata tuta kuwa tuna pumzika. Nahitaji tukodishe gari ya kawaida. Inayo fanania na gari nyingi hapa Somalia”

“Na hii?”

“Hii tunaiacha hapa hotelini na hiyo gari ya kawaida ndio tuta kuwa tuna itumia kwenye maembezi yetu. Una ona hizi kalamu?”

“Ndio mume wangu”

“Haya nimabomu makubwa sana ambayo nili yatengeneza”

“Mmmm”

“Ndio, ila kwa sasa sihitaji kuyatumia kwa maana yana uwezo wa ulipua eneo kubwa sana. Cha kufanya sasa hivi ni kutafuta laptop ili tuweze kufwatilia kila kitu kinacho endelea duniani pamoja na simu itakayo tuwezesha kufanya mawasiliano muda na wakati wowte tukao hitaji”

“Sawa mume wangu”

Tukatoka chumbani hapa na kufungua mlango wetu huku kila mmoja kwa ndani akiwa amevalia surulia na kiunoni mwake amachomeka bastola mbili zilizo jaa risasi za kutosha. Tukafika mapokezi na nikamfwata muhudumu wa kike ambaye yeye ndio tume kodisha chumba kwake.

“Dada”

“Abee”

“Ni wapi wana kodisha magari kwa watu binafsi?”

“Zipo sehemu nyingi tu wana kodisha”

“Nielekeze”

“Ukitoka hapo nje getini, tembea hadi kwenye ile kona inayo kunja kushoto. Ukifika pale hesabu fremu ya kwanza, hadi ya nane, uta ona show room ya magari pale.Sasa hapo hapo ndipo wanapo kodisha na kuuza magari”

“Sawa nashukuru”

“Poa kaka”

Nikamfwata Jackline sehemu alipo simama.

“Tuondoke amenieekeza”

“Sawa mume wangu”

Kabla hata hatujapiga hatua ya kutoka ndani hapa, vijana sita wa DON wakaingia huku wakiwa wemeongozana na mlinzi namba moja wa DON ambaye kwa sekunde kadhaa akatutazama kisha akatusogelea huku akionekana kuhisi jambo kati yangu mimi na Jackline.



“Samahani shehe”

Mlinzi wa DON aliniongelesha huku akinitazama usoni mwangu. Jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba tume weka mboni za bandia. Mboni ambazo ni za kupachika na zime badilisha kabisa muonekano wa macho yetu na sura zetu.

“Salama shehe”

Nilizungumza kwa kujiamini huku nikiibadilisha kabisa sauti yangu ya kuzungumza kwa maana minzi huyu ana ifahamu sauti yangu.

“Kuna hawa watu tuna watafuta je mume waona sehemu yoyote?”

Mlinzi huyu wa DON alizungumza huku akinikabidhi picha mbili. Moja ikiwa ni yangu na nyingine ikiwa ni ya Jackline.

“Eti mke wangu ume waona hawa watu?”

Nilimuuliza Jackline huku nikimtazama elekea akusoni mwake.

“Hapana mume wangu. Ni kina nani kaka?”

Jackline naye alizungumza huku akiwa amebadilisha sauti yake jambo lililo mfanya mlinzi huyu kuishiwa na pozi kabisa hata ya kuendelea kutuuliza.

“Usijali shemeji. Tuna omba mutakapo waona muwasiliane nas kwa namba hii. Kuna zawadi nono ina tolewa”

Mlinzi huyu akanikabidhi kadi yenye namba mbii za simu.

“Sawa tuta wasiliana”

Nilizunguza kwa kujiaini sana huku nikimtaza mlinzi huyu wa DON machoni mwake. Jamaa akanitazama kwa sekunde kadha kisha akaelekea mapokezi nasi tukatoka ndani hapa.

“Usiwe na wasiwasi hawajatujua”

Nilimuambia Jackline ambaye kidogo ana oneana kuwa na wasiwasi. Tukaelekea eneo ambalo dada wa mapokezi alituelekeza. Tukanunua gari moja ambayo ni ya zamani kidogo na tukaondoka eneo hili. Tukaingia kwenye moja ya dula la simu na tukanunua simu mbili aina ya Samsung S10+. Tukanunua laptop kisha tukatafuta hoteli nyingine ya kawaida na tukapanga chumba kimoja kwa siku saba.

“Una fanya nini mume wangu?”

Jackline aliniuliza huku nikiwa nina minya minya laptop hii.

“Nina weka software zitakazo tuwezesha kui hack hii namba ya simu ya huyu jamaa kwa kupitia yeye tuta weza kumpata DON kiurahisi”

“Ahaa kumbe una ujuzi wa haya mambo?”

“Wee acha kwenye hilo jeshi la waasi wa CONGO nilijifunza mambo mengi sana mke wangu, yaani hadi kutengeneza mabomu”

“Hongera sana mume wangu, nina imani hukukutana na hao waasi kwa bahati mbaya ila ni mpango wa Mungu”

“Ni kweli mke wangu, kuna mbinu nyingi sana nilijifunza kwenye mafunzo hivyo hawa watu wa DON tuta wamaliza taratibu”

“Sawa mume wangu”

Nikamaliza kufanya nincho kifanya na sasa nina weza kuona kila eneo ambalo mlinzi namba moja wa DON ana eleekea.

“Sasa utajuaje kama yupo na DON ikiwa hapa kina onekana kiji alama?”

Jackline aliniuliza huku akinitazama machoni mwangu.

“Una jua tatizo ya hii nchi ipo gizani sana”

“Una maana gani?”

“Yaani tenknolijia ya hapa ndogo, mitaa haina kamera kama Marekani. Ingekuwa ni marekani tunge weza ku hack kamera za eneo ambalo yupo kisha tukaona yupo na nani”

“Sasa uta fanyaje?”

“Ina bidi tumfwatilie kwa kutumia gari kila anapo elekea”

“Basi twende tumwafwatilie”

“No ngoja ifike saa mbili usiku sasa hivi tupumzike kwani hii kazi ita kuwa ni usiku kucha”

“Sawa mume wangu”

Jackline akanikalia mapajani na akaanza uchokozi wa kimapenzi. Taratibu tukaanza kunyonyana denda na ndani ya muda mchache tukazakama katika penzi zito lililo tawaliwa na hisia kali sana za kimapenzi kati yetu. Kutokana ni tisa alasiri, tukalala hadi saa moja usiku. Kisha tukajianda kwa kazi iliyo mbele yetu. Kazi ambayo ni lazima tuhakikishe tuna ipunguza kwa asilimia kadhaa. Tukaondoka nyumbani hapa huku tukifwata signal ya mlinzi namba moja wa DON ambayo tume ihamishia kwenye simu yangu na Laptop tumeicha nyumbani. Haikuwa kazi ngumu kufika kwenye eneo ambalo mlinzi wa DON yupo. Katika eneo hili kuna baa moja kubwa na iliyo jaa watu wengi wakiendelea kupata burudani ya vinywaji.

“Yupo kwenye ile baa pale”

Nilimuonyesha Jackline.

“Vipi nishuke nika muone?”

“Hapana. Nina hitaji tumuue nje ya baa hii kwa maana ina watu wengi sana”

“Sawa mume wangu”

Tukaendelea kusubiri hadi saa tano usiku na tukamuona mlinzi wa DON akitoka ndani ya baa hiyo akiwa na wasichana wawili ambao kwa uvaaji wao wana onekana ni machangudoa. Akafunguliwa mlango wa gari na kijana wake aliye kuwa ndani ya gari kisha akaingia ndani ya gari hilo na machangudoa kisha taratibu wakaanza kuondoka eneo hili. Nikawasha gari hili na taratibu tukaanza kuwafwatilia taratibu.

“Baby”

“Yes”

“Nahitaji uendeshe gari hili, njoo ushike mskani”

Taratibu tukapishaba katika siti ya dereva nami nikahamia kwenye siti aliyo kuwa amekaa Jackline. Nikaikoki vizuri bastola yangu kisha nikamuomba Jackline alipite garo hilo kwa kasi na kulizuia kwa mbele na mke wangu akafanya kama nilivyo muagiza. Akalipita gari hili la kijana wa DON na akalizuia njia kwa mbele. Bila ya kupoteza muda nikapiga risasi mbili katika kioo cha mbele upande wa dereva na dereva akafa. Wasichana walio ingia siti za nyuma wakafungua milango ya nyuma na kila mmoja akakimbia na kuokoa maisha yake. Nikamuwahi mlinzi wa DON kwa kupiga risasi ya bega kabla hata hajafanya chochote na ubaya ni kwamba amelewa chakari. Nikamchomoa ndani ya gari huku akigugumia kwa maumivu. Nikaichukua bastola yeka na kuichomeka kiuoni mwangu, kisha nikampapasa na kiitoa simu yake mfukoni. Nikaona jina lililo andikwa Big Boss. Nikapiga namba hiyo na ikaanza kuita.

“Jay ume fikia wapi?”

Niliisikia sauti ya DON akizungumza.

“Ohoo samahani mkuu, msikilize Jay anacho kizungumza?”

Nikamuwekea Jay simu sikioni mwake huku bastola nikiigandamiza katika jerala la bega lake na akaanza kufurukuta hapa chini alipo lala huku nikiwa nime mzuia vizuri kwa kigoti cha mguu wangu kilocho kita kifuani mwake. Jay akalia kwa maumivu sana.

“Nina anza na huyu kisha nita fwata na wewe mpuuzi kama umenichafulia kwenye ulimwengu na nina itwa gaidi basi nita kuua kinyama”

“Malcom ni wewe?”

“Ndio ni mimi na sikiliza hii”

Nikanyanyuka huku nikiwa baso sijakata simu. Nikampiga Jay risasi tatu za kifua na moja ya nne nikaimalizia kifuani mwake.

“Naamini ume sikia kijana wako anavyo kufa. Kudhibitisha kwamba nime muua nina kutumia picha zake.”

Nikampiga Jay picha kadhaa akiwa tayari amesha kata raho kisha nikamtumia picha hizo DON na simu nikaiweka sikioni mwangu.

“Nina imani ume ziona. Kama niliweza kuingia kwenye himaya yako na kumchukua mke wangu na kukuacha hai basi ni wakati wa kukuua.”

Nikakata simu, nikaikremisha namba ya DON kisha nikaivunja simu hii. Nikamuingiza Jay ndani ya gari kisha nikampa ishara Jacklien kuendesha gari mbali kidogo kisha nikapiga risasi katika tank la mafuta ya gari la Jay na likalipuka kwa moto. Nikakimbilia ndani ya gari na tukaondoka eneo hili kwa mwendo wa kasi sana.

“Ume muambieje DON?”

Jackline aliniuliza kwa maana yeye hakushuka ndani ya gari.

“Nimemchimba biti ambayo naamini hato kuja kukaa na kusahau, una jua kama una taka kupambana na adui yako ni lazima kwanza umpatie hofu. Kama niliweza kuingia kwenye himaya yake na nikakakutorosha, leo nime muua mlinzi wake, basi ujue hilo ni pigo jengine kwake. Lazima ata changanyikiwa, ana weza kutusaka kwa nguvu zote na akifanya hivo basi amejimaliza”

“Amejimaliza kivipi?”

“Ata mwaga vijana wengi ndani ya Mogadishu na Somalia kwa ujumla. Vijana wengi wakiwa wamezagaa basi ita kuwa ni njia rahisi sana sisi kumfikia yeye kwa maana ata kuwa amebaki na ulinzi mdogo sana hivyo kumuua ita kuwa ni jambo rahisi sana na isitoshe nina namba yake”

“Kazi nzuri mume wangu”

“Nashukuru. Huyu DON ina bidi tumpate usiku huu huu”

Nilizungumza huku nikijaribu kui hack namba ya DON ili niweze kujua kila anapo kwenda.

“Shit”

“Nini baby”

“Ana tumia simu ambayo huwezi ku hack”

“Duu”

“Yaa turudi hoteli tuliyo toka”

Tukarudi katika hoteli tuliyo toka. Nikawasha laptop na kujaribu kuipata ramani ya juu ya nyumba ya DON na nikafanikiwa kuipata.

“Hii ndio nyumba ya DON. Sasa hapa sijui tuta pata wapi Drone yenye mabomu ili ishambulie angani”

Nilizungumza huku nikiitazama nyumba hiyo kwa juu.

“Mke wangu mbona ume kaa kimya”

“Kuna jenerali mmoja wa vikosi vya anga vya jeshi la ufaransa ni rafiki wa baba na pia ni kama baba yangu. Sasa ndio nina wazia namna ya kuzungumza naye ili kama wanaweza kulipua hiyo nyumba basi wafanye hivyo”

“Hiyo haiwezekani mke wangu sio rahisi kama unavyo fikiria”

“Kwa nini?”

“Kwa sababu, endapo ita gundulika kwamba Ufaransa ime vamia Somalia, basi uta ibuka mvutano kama ulipo sasa hivi kati ya Marekani na Mexco. Hapo ni lazima wana diplomasia waingilie mgogoro huo la sivyo nchi hizo zita ingia kwenye vita”

“Sasa tuna fanyaje mume wangu”

“Tupumzike kwa sasa mambo mengine yata fwata mke wangu”

Nilizungumza huku nikijilaza kitandani kwani uwezo wangu wa kufikiria mambo sasa ume fika mwisho.

“Nime pata wazo mume wangu”

“Wazo gani?”

“Una jua hii vita sisi tuna pigana na DON na sio watu wake”

“Ndio”

“Una onaje tuka fanya mpango wa kumkamata yeye. Najua ume fanya naye kazi kwa kipindi kirefu kidogo”

“Ndio”

“Una jua udhaifu wake ni nini?”

“Ndio nina ufahamu, ana penda sana starehe na wana wake. Ila kwa sasa sidhani kama ata kuwa ana wapenda hao wanawake isitoshe kijana wake namba moja amekufa. Nina imani kubwa sana ata kuwa ni muoga wa kila mtu kuhofia kuuwawa”

“Duu sasa sijui ita kuwaje”

“Tulale kwanza mke wangu”

Taratibu Jackline akajilaza pembeni yangu na akawa wa kwanza kupitia na usingizi ila mimi sikuweza kulala fofofo kwa maana nina lala kwa machale sana kwani hali ya usalama wetu na hii nchi kwa ujumla ni mdogo sana.

Asubuhi na mapema nikaamka, nikafungua dirisha la chumba chetu na kutazama mandhari wa nyumba nyingi chakazu zilizopo eneo hili. Japo hoteli hii sio nzuri kivile ina ina gorofa mbili kwenda juu.

“Ume amkaje mume wangu”

Sauti ya Jackline ikanifanya kugeuka nyuma na kumtazama.

“Nime amka salama mke wangu niambie”

“Poa mwili ume choka choka”

Jackline alizungumza huku akijinyoosha viongo vya mwili wake.

“Ni kutokana na uchovu na harakati za jana usiku”

“Ni kweli, yaani jana sikuamini kama nina weza kuendesha gari kwa uwezo ule”

“Somalia, Mogadishu…….Nipe wazo basi”

Nilizungumza huku nikiendelea kuangaza nje ya hoteli hii. Nikaona watu wengi wakiwa wamevalia kanzu na mabaibui meusi wakikatiza barabarani huku wakiwa wameshika mabango yaliyo andikwa kwa lugha ya kisomalia.

“Kuna nini mume wangu?”

Jackline alizungumza huku akikimbilia dirishani hapa na sote tukawatazama watu hao.

“Nahisi wana maandamano yao kwa maana mabango yana onyesha wana hitaji huduma za afya. Wana hitaji amani, ina onyesha wana mshinikiza raisi na serikali yake kutoka madarakani kwani wananchi wana ishi maisha ya shida sana”

Nilizungumza kwani nina kijua kisomali vizuri.

“Ahaa sasa hayo haya ni maandamano salama?”

“Hata sijui mke wangu”

“In……”

Gafla mlipuko mkubwa ukatokea kwenye moja ya gari lililo kuwa lime simamisha pembezoni mwa barabara hiyo inayo pita waandamaniji. Mtetetemeko wa bomu hili uka nifanya nimvamie Jackline na umlaza chini huku mimi nikiwa juu kuhakikisha mke wangu hapati madhara yoyote. Mtetemeko ukapungua, kwa haraka nikasimama huku nikiwahi bastola yangu niliyo iweka juu ya meza iliyopo chumbani hapa. Nikachungulia dirishani na kuona moshi mwingi ukiwa ume zagaa angani huku vilio vya watu vikizagaa kila sehemu.

“Shiti mke wangu jiandae haraka haraka tuondoke hapa”

Kwa haraka tukavaa nguo zetu na sisi tukavaa kanzu na mke wangu akavaa baibui. Tukabeba kila kilicho chetu na tuka toka dani hapa. Tukaanza kushuka kwenye ngazi huku tukiambaatana na wageni wengine wa hoteli huu kushuka kwenye ngazi huku kila mmoja kijitahidi kuokoa maisha yake. Tukatoka nje huku nikiwa nimemshika mkono Jackline.

Tukiwa tuna angaza angaza jinsi watu wanavyo kimbia pasipo utaratibu. Tukasikia mlipuko mwengine wa bomu katika mtaa mwengine na kuwafanya watu wazidi kuchanganyikiwa na kuendelea kuranda randa.

“Turudi ndani”

“Ndani tena mume wangu”

“Ndio haya mabomu ina onyesha yame tengwa sasa hii kimbia kimbia, tuna weza kujikuta tukilipuliwa na sisi’

Sikutaka kushauriana na Jackline kwa mara mbilimbili. Tukarudi gorofani kwa mwendo wa spidi. Hatukuingia katika chumba chetu, tukapitiliza moja kwa moja hadi juu kabisa ya gorofa hili. Nikakimba hadi kweye moja ya ukuta na nikajibanza huku nikitazama chini namba watu wanavyo kimbia kimbia.

“Ume ona chochote mume wangu?”

“Naona askari wana wapiga watu”

Jackline akakimbia kwa kuinama hadi sehemu nilipo chuchumaa, kisha sote tukachungulia. Kwa haraka akatoa simu yake mfukoni na kuanza kurekodi matukio hayo ya kinyama. Badala ya askari hao kuokoa watu, wao wana watembeze kipigo kisawa sawa.

“Hawa sio askari”

Nilizungumza huku nikiwatazama vizuri.

“Kivipi?”

“Hawa ni Al-Shabab ila wamevalia mavazi ya askari. Wanafanya mashambulizi ya namna hiyo iki kulichafua jeshi lao la polisi”

“Duuu”

Tukaendelea kutazama mateso wanayo pata raia hawa walio amua kuandamana. Tukaaa eneo hili la juu ya hii hoteli kwa masaa sita hadi kukatulia tuli kwani Al-Shabab hawa waliamua kutumia risasi za moto kujibizana mashambulizi na wanajeshi walio fika kuzuia vurumai hizo.

Majira ya saa nane tukatoka juu ya gorofa hili na kutoka nje, tukaingia ndani ya gari letu ambalo kwa bahati nzuri halikupata majanga ya mashambulizi ya risasi. Tukaelekea katika hoteli ya kifahari tuliyo panga ambayo kidogo ipo pembezoni mwa bahari. Habari zinazo tawala katika vyombo vya habari vya hapa Somalia na nje ya nchi ni kuhusiana na mashambulizi hayo ya waananchi. Raisi wa Somalia akahutubia taifa na kusisitiza kwamba ata hakikisha kwamba Al-Shabab wana husika katika uuaji wa watu karibia mia nne na stini.

“Wajinga wana ua watu kama kuku”

Nilizungumza huku tukitazama habari hiyo mimi na mke wangu.

“Yaani hawana hata huruma”

“Washenzi sema mifumo yao ya ulinzi ni ya kijinga sana”

“Umeona ehee. Ila mume wangu una onaje tukaondoka hapa Somalia kwa maana leo ni Al-Shabab kesho ni DON huoni kama tuna weza kufa kijinga kwa maana bomu halichagui una visasi vyako au huna”

“Tuna ondoka tuna kwenda wapi mke wangu?”

“Nchi yoyote ili mradi tukajipange. Pesa tuliyo kuwa nayo Cash ina karibia kwisha. Hapa hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kutoa au kuingiza pesa. Hembu jaribu kulifikiria hilo mume wangu”

“Sawa mke wangu tuna ondoka hapa Somalia na tuna elekea nchini Tanzania. Ila kabla ya kwenda nchini Tanzania nahitaji kufanya jambo moja muhimu sana”

Nilizungumza huku nikimtazama Jackline machoni mwake na kumfanya aduwae kwani hajui ni jambo gani ambalo nime kusudia kulifanya.



“Jambo gani hilo mume wangu?”

Jackline aliniuliza huku akinitazama kwa macho ya udadisi.

“Mimi sio gaidi kama ninavyo chukuliwa na watu. Nahitaji unirekodi video nitakayo iweka kwenye mtandao wa kijamii na nita waeleza watu kwamba mimi sio gaidi, nina watoto sasa, nina familia sasa ambayo endapo nisipo kanusha hizi tuhuma basi wanangu na familia yangu ita jisikia vibaya, Wewe mke wangu una elewa hali halisi, je watoto wetu wata elewa?”

Nilizungumza kwa sauti ya upole sana huku nikiendelea kumtazama Jackline machoni mwake.

“Je hilo unalo taka kulifanya mume wangu halito wasaidia vyombo vya usalama kukukamata?”

“Hawawezi kunikamta, njoo nikuonyeshe kitu”

Nilizungumza huku nikichukua shuka lililopo hapa kitandani, nikachomoa misumari miwili iliyopo mlangoni mwa kitanda kisha kwa kutumia kitako cha bunduki kuikita misumari hiyo ukutani kisha nikalining’iniza shuka hili ukutani.

“Kwa nini una fanya hivyo?”

“Una jua kwa sasa tekonolojia imekua kwa kiwango cha hali ya juu. Kama nikirekodi video hiyo na ukuta nyuma yangu uka onekana, wana weza ku scan ukuta na wakafahamu ni jengo gani na endapo wakaja hapa ina kuwa shida”

“Kumbe hilo lina wezekana?”

“Ndio mke wangu lina wezekana kuna wadadisi wengi wa mambo mke wangu. Hili shuka lita ficha taswira nzima ya eneo tulipo. Kama umesha wahi kushuhudia video nyingi za magaidi, kwa nyuma ni lazima wawe wameweka kitambaa, kiwe ni cheusi au cha rangi yoyote ili mradi nyuma ya video zao wana weka kitambaa. Hicho kina saidia wao kuto kujulikana”

“Ahaa ni kweli hata kwenye filamu huwa nina ona hivyo?”

“Yaaa. Nina toa hizi mboni za bandia pamoja na ndevu. Nahitaji kubaki kwenye sura yangu ya kawaida hivyo nahitaji uni rekodi”

“Sawa mume wangu”

Nikatoa kila kitu kilichopo usoni mwangu na nikabaki katika sura yangu ya kawaida. Nikaivua kanzu hii na nikabaki na tisheti nyeupe kisha nikasimama mbele ya kitambaa hichi na Jackline akaanza kunirekodi kwa kutimia simu yake.

“Habari Watanzania wezangu. Nina imani sura yangu haito kuwa ngeni kwa sasa machoni mwenu. Wapo munao nifahamu kwa jina langu halisi la Rashidi Pinda na wapo ambao wana nifahamu kwa hili jina jipya nililo pandikizwa kwamba nina itwa gaidi.”

“Kwenye maisha yangu nime pitia mambo mengi ikiwa moja wapo ni la kuzulumiwa mke n jengine likiwa ni kusingiziwa kesi nyingi ili mradi yule mwenye nguvu na aliye mchukua mke wangu kinguvu kunididimiza chini. Nikiachana na hilo swala, ukweli wa mambo ni kwamba, mimi sio gaidi. Huyu aliye ivujisha video hii ana itwa DON, alikuwa ni miongoni mwa watu walio kuwa wakinisimamia kwenye michezo ya ulingoni, michezo ambayo ili uweze kushinda ni lazima mmoja aweze kufariki duniani. Nime yahatarisha maisha yangu na kuyaweka rehani. Don alinishinikiza kuwaua baadhi ya matajiri nchini Brazil akitishia kuiangamiza familia yangu. Ila sikuweza kukubaliana na hilo zaidi ya hivyo nilimfanikisha kumkamatisha mbele ya jeshi la polisi la nchi ya Brazili na akafanikiwa kutoroka kwa kufanya majanga makubwa sana.”

“Video inayo endelea kuruka kwenye vyombo vya habari ikinionuyesha nikikabidhiwa mikononi mwa jeshi la Al-Shabab nikitolewa mikononi mwa askari wa kitengo cha NSS, hiyo video ni kweli nilikabidhiwa kwa wanajeshi hao wa Al-Shabab ambao walikuwa wameteka meli ya kivita ya nchini Tanzania. Ila sihusiki nao na wala mimi sio mkuu wao. Kilicho fanyika ni kwamba DON alihakikisha kwamba ana tengeneza mfumo wa kuonekana mimi ni miongoni mwa hao Al-Shabab ili kunichafulia kwenye jamii na iwe rahisi kwa yeye kunikamata pale tu ninapo kwenda kinyume naye. Isitoshe DON alimkamata mke wangu na nilifanikiwa kumuokoa kutoka mikononi mwake.”

“Watanzania wezangu, maisha yangu yana historia kubwa sana. Yana shuka na yana panda, kwa sasa nita hakikisha kwamba nina ilinda familia yangu, nina mkamata DON kisha nikimalizana na yeye, aliye yafanya maisha yangu yawe hovyo naye nina muhakikishia kwamba maisha yake yata kuwa hovyo ya yangu yata panda tena.”

“Mama najua una iona video hii, nipo hai mwanao na nipo na mkwe wako wa sasa, tuta rudi nyumbani kuwalea watoto wetu. Ila nina nina waomba wewe na baba mutupatie muda mchache tu kabla ya kurudi. Kuna biashara nina hitaji kuimaliza. Nina kupenda sana mama, baba, na wanangu. Mungu awalinde”

Nikamaliza kuzungumza ujumbe huo na Jackline akanikabidhi simu, nikaitazama video hiyo na nikaridhika nayo. Nikafungua akauti feki ya mtandoa wa Youtube akaunti ambayo sio rahisi kufahamika mmiliki ni nani kisha nikaiweka video hii ambayo nina imani ita wafikia watu wengi sana ndani ya muda mchache kwani sura yangu imesha kuw amaarufu.

“Sasa tuna ondoka mke wangu”

“Ngoja kwanza baby, tuangalie hii video ina weza kutuletea muitikio gani kwenye jamii”

“Sawa mke wangu”

Nikapiga simu mapokezi na kuagizia chakula. Siku ya leo nzima hatukutoka ndani hapa na kazi yetu ni kufwatilia kila kinacho endelea kwenye mitandao ya kijamii.

“Baby baby njoo uone”

Jackline aliniita na kujikuta nikikatisha haja ndogo iliyo niiingiza bafuni na kurudi chumbani.

“Video yao CNN wameionyesha”

Jacklien alizungumza huku akionionyesha video yangu inayo rushwa kwa sasa kwenye chaneli hiyo kubwa duniani. Video yangu ina tafsiriwa kwa lugja ya kingereza ili watu wote duniani wana jua lugha hiyo kuielewa kwani nime tumia kiswahili fahasa kabisa kuzungumza.

“Youtube hadi sasa hivi ina watazamaji wangapi?”

“Ngoja niangalie mume wangu”

Jacklien akaingia katika mtando wa Youtube na kuitazama video hiyo.

“Aisee muda ule ilikuwa na watazamaji elfu ishirini na sasa hivi ina watazamaji laki nane na hamsini na mbili elfu. Aisee imepanda”

“Yaa ni lazima watu duniani kwa ujumla wata taka kusikia. Nikuambie jambo moja mke wangu”

“Ndio baby”

“Akauti yako ya Instergram siina fanya kazi?”

“Ndio ina fanya kazi”

“Anzisha kampeni ya kunitetea kwamba mimi sio gaidi”

“Wazo zuri sana hilo mume wangu. Sasa kampeni tuna iitaje?”

“RASHIDI SIO GAIDI, au una onaje hilo jina mke wangu?”

“Rashidi sio gaidi ni jina zuri. Ngoja niingie Instergram na niianze hiyo kampeni”

Usiku kucha ikawa ni kazi ya mke wangu kuhakikisha kwamba kampeni hii ina kuwa ya kidunia. Muitikio watu ambao wana iendeleza kampeni hiyo ukazidi kututia moyo. Hadi kuna pambazuka, karibia watu milioni tatu duniani nzima wama isambaza kampeni hiyo ya kunitetea.

“Nguvu ya watu ni kubwa sana mume wangu, nina imani kwamba hili jambo litakwisha”

“Naamini hivyo”

“Kwa hiyo tuna kwenda Tanzania”

“Hapana nahitaji wewe urudi Ufaransa”

“Nini?”

“Ndio nahitaji urudi Ufaransa. Nahitaji hii kazi kuimaliza peke yangu”

“Mume wangu hapana, kumbuka kwamba niliapa kuwa nawe kwenye kila jambo, kwa nini una taka kunikatili kiasi hicho. Una hitaji nirudi kukaa mpekwe na mawazo na kuendelea kujawa na mawazo kama miaka miwili iliyo pita”

“Sio hivyo mke wangu”

“Ila?”

“Tazama watoto wetu. Wewe ndio mtu wa pekee wa kwenda kumuelewesha Shamsa na mama kwamba mimi nipo”

“Rashidi, kama ni kufa acha tufe wote, ila siondoki na kukuacha peke yako. Haki ya Mungu vile nina apia siondoki”

Jackline alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.

“Baby”

“Noo zungumza jengine ila sio la mimi kuondoka hapa Somalia.”

Jackline akaendelea kushikilia msimamo ambao kwa maono yangu nina hisi kabisa uta kuwa na madhara makubwa sana kwangu. Madhara ambayo kwa namna moja ama nyingine ni lazima kuhakikisha nina muepusha mke wangu na madhara haya.

“Yaani kama una hitaji mimi kuondoka, tuna ondoka wote na kumuacha DON aendelee na maisha yake. Kwanza tuna mambo mengi ya kufanya. Kusafisha jina lako na mambo mengine ya kifamilia”

“Una hitaji tufe pamoja si ndio?”

“Ndio, kwa sababu nina kupenda na nina kuhitaji”

“Vaa nguo zako”

“Ehee?”

“Vaa nguo zako”

Nilizungumza huku nami nikivaa nguo zangu na kuzirudisha mboni zangu za bandia machoni, kisha nikabandika ndevu zangu za bandi, nikavaa barakashia pamoja na miwani yangu kisha tukatoka ndani hapa. Tukaingia ndani ya gari nakuondoka hotelini hapa.

“Mume wangu tuna kwenda wapi?”

Sikumjibu kitu chochote Jackline zaidi ya kumtazama kwa macho makali. Nikasimamisha gari mbele ya duka moja la sonara.

“Usishuke ndani ya gari”

Nilizungumza kwa sauti nzito kidogo ambayo kidogo ikamtisha Jackline. Nikaingia ndani ya duka hili la sonara. Nikatazama pete mbili zinazo fanana na zenye maduara yanayo weza kutosheleza katika vidole vyetu. Nikalipa dola elfu moja kwa pete zote mbili kisha nikarudi ndani ya gari, huku usoni mwangu nikiwa nime nuna.

“Mume wangu”

“Nini?”

Nilijibu kwa hasira kidogo huku nikiwasha gari na kuondoka eneo hili,jambo hili likamfanya Jackline kukaa kimya na kuogopa kutuongolesha. Tukafika kwenye moja ya msikiti, nikashuka na kuingia ndani, nikazungumza na mmoja wa mashehe niliye mkuta ndani hapa. Kisha nikarudi ndani ya gari na kumuita Jackline.

“Tuna funga ndoa na una kuwa mke wanga halali leo hii”

Jackline macho yakamtoka huku akinitazama kwa mshangao.

“Mbona una shangaa?”

“Siamini mume wangu. Sasa tuna fungaje ndo ikiwa sijui taratibu za kiislamu?”

“Una hitaji ndoa au huitaji ndoa?”

“Nahitaji”

“Basi kila kitu uta jua mbele ya safari”

Shehe akaandaa taratibu zote za ndoa kisha akatufungisha ndoa ya haraka haraka, nikamvisha pete Jackline naye akanivisha na tukaondoka msikitini hapa.

“Yaani mume wangu una vituko sana”

Jackline alizungumza huku akiwa amejawa na fiuraha sana.

“Kwa nini?”

“Yaani kuninunia kote kule nika hisi ume kasirika na kung’ang’ania kwangu kubaki na wewe hapa kumbe ume amua kunifanyia suprize ya ndoa”

“Ndio hivyo mke wangu, nimeamua kukuoa na uwe wangu wa maisha kabisa kwa ni kwa kipindi kile tulijaribu kufunga ndoa ila nilitekwa kabla hatujakamilisha mpango wetu. Sasa nina imani wewe ni mke wangu halali sasa”

“Nashukuru sana mume wangu kwa kulitambua hilo.”

“Jack”

“Bee”

“Nakuomba ukawaangalie watoto. Watoto ni muhimu sana kwenye maisha yetu. Tafafhali mke wangu nina kuomba kiustarabu na hekima yote na nina zungumza kama mume wako halali, tafadhali nina kuomba hii vita niipigane mimi mwenyewe”

Jackline akakaa kimya kwa sekunde kadha kisha akanivamia mdomoni mwangu na kuanza kuninyonya denda kwa hisia kali sana huku machozi yakimwagika usoni mwake.

“Rashidi nina kupenda na nina kuhitaji. Nakuomba uimalize kazi yako haraka.”

“Nakupenda pia mke wangu. Nashukuru kwa kunielewa”

“Uta ifanya ndani ya muda gani?”

“Haito maliza miezi mitatu”

“Sawa mume wangu nakuomba uwe hai”

“Usijali mke wangu, nita kuwa hai kwa uwezo wake mwenyezi Mungu”

Tukarudi hotelini, hapakuwa na jambo jengine la kufanya zaidi ya kuitumia siku hii yote kupeana raha na kucheza michezo mbalimbali ya kimapenzi kitandani. Kila mmoja wetu akafurahia sana juu ya ndoa yetu tuliyo ifunga leo. Tukanywa na kula kwa kufurahi sana. Tukapiga picha nyingi za ukumbusho na kurekodi video nyingi sana kwa ajili ya kuwatumia salamu watoto wangu na mama yangu mzazi. Nikawasalina na Brian na kumueleza hali nzima ilivyo kuwa kwa Brian mwezake. Nikamuomba aweze kunisaidia kupata hati ya kusafiria ya Jackline na akatuelekeza kwa mzee mmoja ambaye ni bingwa wa kutengenezza hati za kusafiria feki.

Siku iliyo fwata asubuhi na mapema tukaelekea kwa mzee huyo aitwaye Al-Seidy. Tukafika kwake kwa maana Brian alitupatia jina la mtaa na jina namba ya nyumba hiyo.

“Tuna muulizia mzee Al-Seidy”

Tulimuambia mlinzi mmoja tuliye mkuta katika nyumba hii.

“Nyinyi ni kina nani?”

“Nina itwa Rashidi, muambie Brian ametuelekeza kwake na tuna imani kwamba amesha zungumza naye.”

Jama huyu akatoa simu ya upepo na kuzungumza na bosi wake na akamueleza juu ya uwepo wetu sehemu hii hapa.”

“Waruhusu kuingia”

Mlinzi huyu akaturuhusu kuingia ndani, tukamkuta mzee mwenye uwaraza mkubwa kichwani mwake pamoja na ndevu nyingi nyeupe. Tukasalimiana naye kisha tukaanza kumueleza haja iliyo tuleta hapa.

“Hilo halina shida, muta pata hati za kusafiria. Je muna hitaji na visa?”

“Ndio”

“Sawa hakuna shaka muta pata”

Mzee Al-Seidy akaanza kufanya kazi ya kumtengenezea Jackline hati ya kusafiria.

“Mzee”

“Ndio Rashidi”

“Una mfahamu DON?”

Mzee Al-Seidy akanitazama kwa macho ya udadisi kisha akakoa kidogo.

“Ndio, kwa nini una muulizia?”

“Nasikia ni mtu hatari sana”

“Wewe nani ame kuambia?”

“Ni fununu fununu za mtaani”

“Huyo mtu unaye muulizia ndio mtu aliye mkata miguu Brian. Sio mtu mzuri na ni mtu hatari sana hivyo kijana nina kushauri ni bora uka kaa mbali naye.”

Mzee Al-Seidy alizungumza kwa msisitizo huku akionekana kutuonya vikali juu ya DON.

“Una weza kunisaidia kukutana naye”

“Rashidi, nime kueleza mtu huyo ni hatari sana hivyo, sihitaji kuingia kwenye matatizo ya namna yoyote. Huyu Brian alikuwa ni mfanyakazi wake, na malipo yake ndio hayo kukatwa miguu”

“Mzee nahitaji kulipiza kisasi kwa ajili ya Brian”

“Hahaa kijana, humuwezi DON. Don ana miliki uchumi wa hii nchi kwa asilimia sabini, sijui una nielewa. Yaani huyu raisi aliyopo hapa ana msujudia DON na ni mtumwa wake, DON ana pesa, DON ana nguvu. Jeshi la nchi hii lipo mikononi mwake. Hivi una elewa maana ya mtu akiitwa DON. Maana yake ni mtu mwenye mamlaka na hilo DON sio jina lake alilo pewa na wazazi wake. Jina lake kimetokana na pesa na nguvu aliyo nayo ndio maana nina kuambia kwamba DON sio mtu wa kawaida. Na kama ulifikiria kupambana naye basi kijana ume potea njia”

Mzee Al-Saidy alizungumza kwa msisitizo.

“Una taka kuniambia DON ana imiliki hii nchi?”

“Ume anza kunielewa sasa. Wananchi wa kawaida hawajui kinacho endelea, ila DON ameingiza mkono wake kwenye uchumi wa hii nchi na akisema kwamba autoe basi hii nchi ita kuwa ni ya mwisho kabisa katika nchi Masikini duniani. Hivyo kijana wangu, nielewe vizuri”

“Mzee”

Jackline alizunguzm akwa sauti ya upole.

“Ndio binti yangu”

“Ume sema kwamba DON ni mtu anaye miliki uchumi wa hii nchi, hivi ina wezekana kweli mtu akamiliki uchumi wa nchi?”

“Mwanangu, hii ni AFRIKA na hii ndio Somalia. Kila kitu kina wezekana. Yaani hata wewe ukitaka kwenda kununua mji wowote hapa Somalia, na ukawa na watu wake ndani, una weza kuununua. Ndio maana una ona Al-Shabab wana gombana sana na serikali hii. Yote ni kutokana na mamlaka mabovu ya viongozi walipo serikalini”

“Duu, je hao Al-Shabab wapo pamoja na DON?”

“Hapana na wasipo angalia wata malizwa, kwani DON ana nguvu kubwa sana kuliko hao Al-Shabab. Anacho kifanya sasa hivi DON ni kuwakamata na kuwaua wale wote ambao wana ifadhili Al-Shabab kwa pesa, silaha na chakula. Hivyo hawana maisha marefu, wata kufa. Hata wale walio shambulia maandamano wote waliuwawa lile jeshi lililo fika pale lina milikiwa na DON, japo walivaa sare za jeshi la Somalia, ila ni watu wake na wamepata mafunzo makubwa sana kutoka nchi mbalimbali na sasa hivi hilo jeshi lina endelea kuwasaka watu wawili ambao wame muua kijana wa DON. Watu hao ni nyinyi na picha zenu hizi, nilitumiwa mimi mwenyewe na DON kwamba endapo nita waona au muta kuja hapa kwangu basi nimtaarifu haraka iwezekanavyo”

Mzee Al-Seidy akatuonyesha picha yangu mimi na Jackline kwenye computer yake kubwa iliyo ofisini hapa na sote tukajikuta tuki stuka sana.



Tukatazamana mimi na Jackline huku tukiwa na wasiwasi mwingi sana.

“Ndio maana maana nime waonya sana. Ondokeni Somalia, sio sehemu sahihi ya nyinyi kuishi. Rashidi nita kuelekeza sehemu mmoja kwa mtu mmoja ambaye nina imani ata kusaidia na kukupatia uwezo angalao kidogo wa kupamabana na huyu DON. Ila kwa sasa uwezo wako ni mdogo sana tena sana”

Tukakaa kimya huku tukikosa hata la kuzungumza.

“Mimi nilikuwa ni miongoni mwa wanajeshi wapelelezi wa nchi hii miaka ya tisini na tatu huko. Nime shuhudia mambo mengi sana kuhusiana na hii nchi. Nime shuhudia njaa, vita na kutamani madaraka kwa baadhi ya viongozi. Hadi nimefikisha umri huu, ina maana nime pitia mambo mengi sana ambayo yana nifanya niweze kuwatambua watu kiurahisi sana. Mume vaa mboni za bandia na ndevu bandia, ime kuwa ni rahisi kwa mimi kuwajua. Mimi nina ujuzi wa hayo mambo je endapo muta kutana namtu kama mimi ita kuwaje na ni adui yenu?”

Swali la mzee Al-Seidy likatufanya tuwe kimya.

“Ondokeni Somalia kwa sasa sio salama kwenu. Mama ongea na mume wako, hilo munalo lifikiria sivyo jinsi munavyo liona.”

Mzee Al-Seidy akanyanyuka na kuondoka eneo hili na kuniacha mimi na mke wangu.

“Mmm mume wangu ume sikia hilo?”

“Ndio”

“Sasa ina kuwaje?”

“Wewe rudi Ufaransa na mimi acha niende huko anaopo hitaji mzee niweze kwenda”

“Niahidi jambo moja mume wangu”

“Jambo gani mke wangu”

“Niahidi uta rudi salama mikononi mwangu”

“Nakuahidi mke wangu nita rudi salama. Kama Mungu aliweza kunipitisha kwenye matatizo hayo yote hadi leo hii nipo hapa. Basi nina imani huko napo ata nipitisha na nita kuwa salama. Nakuahidi nikirudi nita hakikisha nina fanya harusi kubwa sana ya ndoa yetu na dunia nzima ita shuhudia ni jinsi gani ninavyo kupenda”

“Nashukuru sana mume wangu. Nina kupenda sana mume wangu”

“Nina kupenda pia mke wangu”

Baada ya dakika kumia mzee Al-Sheidy akarudi akiwa ameshika hati mbili za kusafiria. Visa mbili na akaziweka mezani na taratini nikazichukua na kuanza kuzipitishia macho taratibu.

“Beirut Lebanon!?”

Niliuliza huku nikiwa na mshangao mkubwa sana machoni mwangu kwani hii nchi sijawahi kufika toka kuzaliwa kwangu na ni nchi ambayo ina sifikia wa matukio mengi sana ya kigaidi, hususani kwenye mji wake huu wa Beirut.

“Ndio, Beirut. Hii ndio nchi pekee ambayo DON hajaingiza watu wake, hapa utaishi kwa amani na kujifunza baadhi ya mambo ambayo una paswa kujifunza. Yale uliyo jifunza Congo, achana nayo hayato kusaidia na wala kukufanya kuwa ujuzi ambao ukifikia nita kuambia sasa ni wakati sahihi wa kupambana na DON.”

“Ngoja kwanza mzee wangu. Mume wangu ana weza kupigana na kutumia silaha za kila aina na nina imani kwamba uwezo huo una faa sana kummaliza DON”

“Walinzi ulio ambatana nao hawakuwa na uwezo wa kupambana na kutumia silaha? Ilikuwaje wakafa kirahisi namna ile?”

Swali la mzee AL-Seidy likamfanya Jackline kustuka kidogo.

“Binti hii Somalia hususani hapa Mogadishu ni sehemu ambayo hata kukivunjika glasi sehemu fulani, nina pata taarifa ya eneo hilo. Na kila anaye ingia ndani ya nchi hii basi nina fahamu kwa maana mifumo yangu ya siri ina nguvu na ina uwezo wa kunipatia taarifa muda wowote ule. Ndio maana hata ulivyo tekwa na DON nilishindwa kufanya chochote kwani ume tekwa na mtu ambaye hashikiki”

“Ila mzee mimi niliingia hadi kwenye ngome yake na kumuokoa mke wake?”

“Kwa nini hukumuua?”

“Ahaa…nilihitaji kuhakikisha kwanza mke wangu ana kuwa salama kisha nina mrudia tena”

“Ndio maana nime kuambia ume fanikiwa kwenye moja ila la kumrudia lita kuangamiza. Hakikisha una kwenda kwenye hiyo nchi na una kutana na huyo mtu na ata kupatia kile ambacho nina imani kina uwezo wa kukusaidia kupambana na DON. Kwa sasa huwezi kuelewa ila kwa baadae uta elewa.”

Mzee Al-Seidy akafungua droo yake na akatoa kibunda cha dola za kimarekani.

“Hii ni dola elfu tano. Muta jua ni jinsi gani ya kuigawanya na kuhakikisha muna ondoka hapa Somalia. Hii ni flasha ya mtu ambaye uta kwenda kukutana naye Beirut. Hakikisha kwamba huipotezi hii flash kwani ndio code yako pale utakapo kutana naye. Endapo uta ipoteza huto muona wala kukupokea. Umenielewa Rashidi?”

“Ndio mzee wangu. Shukrani sana”

“Mshukuruni Brian, kwani yeye ndio aliye weza kulainisha moyo wangu na kuhakikisha kwamba nina wasaidia kwa kiwango hichi ninacho waambia. Kuna ndege kuelekea nchini Ufaransa majira ya saa sita mchana leo na ndege nyingine ya kuelekea Lebanoni. Muna weza kuziwahi kwa kukata tiketi na bado zina nafasi. Ondokeni Somalia kabla ya jua leo halija potea ngani kwa maana DON ameagiza watu wenye ujuzi wa utambuzi wa watu kama mimi na wata ingia saa kumi usiku. Na wana kuja kwa kazi moja tu ya kufahamu ni muonekano gani ambao nyinyi kwa sasa muta kuwa muna onekana, hata ikitokea mume fanya upasuaji na kuweka sura bandia. Sasa kwa mboni hizo za bandia amazo mume ziweka ni rahisi sana kujulikana ni sawa na kumsukuma mlevi kwenye kiporomoko”

Tukamshukuru sana mzee Al-Seidy. Tukaondoka nyumbani kwake hapa, majira ya saa nne asubuhi. Tukafika hotelini. Tukaanza kuvuana nguo zetu huku tukinyonyana denda. Tartaibu nika mlaza Jackline kitatandani na tukaanza kupeana burudani ya kukata na shoka. Burudani ya kuhakikisha kwamba kila mmoja ana muaga mwezake kwa kumpa penzi motomoto. Majira ya saa tano na dakika kumi, tukaondoka hotelini hapa huku tukiwa tume beba kila kilicho chetu. Tukawahi uwanja wa ndege na tukakata tiketi ya Jackline kuelekea nchini Ufaransa.

“Kuwa makini mume wangu”

“Nashukuru mke wangu. Nawe waangalie watoto na waambie kwamba nina wapenda sana”

“Nita waambia mume wangu”

“Asante mke wangu”

Tukakumbatiana kwa muda na mke wangu kisha akaelekea katika eneo la abari wanao kaguliwa mizigo yao, akapita katika kizuizi hicho na kuingia eneo la ndani zilipo ndege. Majira ya saa sita na dakika sita ndege aliyo panda Jackline ikaondoka nchini hapa na nikabaki peke yangu uwanjani hapa. Nikakata tiketi yangu, kutokana yamesalia masaa mawilili kabla ya ndege kuondoka, nikavumilia kwa kukaa kwenye moja ya mgahawa huku nikiwa nimevalia miwani nyeusi. Jackline akanitumia meseji kwenye mtandao wa Whatsapp.

‘Namuomba mwenyezi Mungu azidi kukulinda mke wangu na kukupatia maisha yaliyo mema na bora. Nina kupenda sana mume wangu’

Ujumbe huu ukanifanya nitabasamu kidogo kisha nikamjibu.

‘Nina kupenda pia mke wangu, kipenzi. Ukifika usisite kunitumia picha zako na watoto na pia hakikisha kwamba ulinzi una kuwa ni wa kutosha’

‘Usijali mume wangu, kwa sasa ulinzi ni mzuri sana na nita waambia kila ulicho niambia niwaambie’

‘Nashukuru mke wangu’

Muda wa mimi kuelekea katika ndege ninayo ondoka nayo ukawadia. Nikapanga mstari kwa abiria wanao andoka. Nikamkabidhi muhudumu wa kukagua hati za kusafiria uwanjani, akaitazama hati yangu hii ya kusafiria kwa sekunde kadha huku akinitazama machoni mwangu kisha akanigongea muhuri wa kuondoka nchini hapa.

“Safari njema”

“Asante”

Nikaelekea moja kwa moja hadi katika ndege. Nikaitafuta siti yangu na nikaikuta ikiwa ipo nyuma kabisa na kwenye kona. Nikakaa, nikafunga mkenda na nikaifungua laptop yangu, nikaichomeka flash hii kisha nikachomeka earphone kwa ajili ya kuweza kusikiliza kama kuna audio yoyote katika fail hili la flash. Nikafungua faili moja na lina document moja tu. Nikaifungua na nikaanza kusoma maelezo ya mzee ambaye nina kwenda kuonana naye. Katika document hii kuna namba za simu picha za mzee huyo pamoja mji na eneo analo ishi. Nikainakili namba hiyo kwenye simu yake na maeneo ambayo ata ishia kisha nikaizima laptop yangu. Baada ya abiria wote kukamilika, safari ya kuondoka eneo hili ikaanza, nikapiga dua ya kimoyo moyo ya kumuomba mwenyezi Mungu kunisaidia niweze kufika salama huko ninapo kwenda. Kwa kutumia simu yangu nikatazama muda ambao tuta tumia kutoka hapa Mogadishu hadi Beirut.

‘Masaa saba na nusu tukipitia Adiss Ababa’

Nilizungumza kimoyo moyo kwani nime panda katika ndege ya shirika la Air Ethiopian, Nikailaza siti yangu vizuri kisha taratibu nikaanza uutandika usingizi kwani usiku sikulala vizuri kwani tulikuwa na kazi ya kufanya mapenzi tu na mke wangu. Sauti ya muhudumu wa kike ika nistua kutoka usingizini, nikafumbua macho yangu na kuona abiria wakijifunga mikanda yao.

“Kuna nini?”

Nilimuuliza bibi niliye kaa naye siti ya pembeni yangu.

“Ndege ina tua”

“Ina maana tume fika?”

“Kwani wewe una kwenda wapi?”

“Beirut”

“Ina tua Addis Ababa”

“Ahaa sawa sawa nina shukuru na heshima yako”

“Nashukuru”

Baada ya ndege hii kutua, bibi huyu akawa ni miongoni mwa abiria walio shuka ndani ya ndege. Wakapanda abiria wengine na nikakaa na mwana mama wa kawaida kidogo huku akiwa amevalia baibui lake na amazifunika nywele zake vizuri tu. Tukasalimiana huku tukionyesha nyuso za furaha.

“Naitwa Rashid”

Nilianza kuzungumza huku nikimtazama mwana mama huyu usoni mwake, kwani ana uzuri wa kumvutia kila mwanaume anaye muona.

“Nashukuru kukufahamu Rashidi.”

“Je wewe una itwa nani?”

“Hahaaa kwa nini una hitaji kufahamu jina langu?”

“Ahaa nina imani kufahamiana sio dhambi”

“Ni kweli sana, ila jina langu huwa sipendi sana watu kulifahamu. Niiite mama Leila”

“Leila”

“Yaa”

“Una jina zuri sana”

“Nashukuru sana.”

Simu ya mama Leila ikaanza kuita na akaipokea.

“Ndio mume wangu?”

“Yaa nimepata siti namshukuru mwenyezi Mungu kwa kweli kwa maana ndege lezo zime jaa sana”

“Nimepata siti ya mwisho kabisa”

“Sawa mume wangu nita kukuta hapo uwanjani”

“Nakupenda pia”

Mama Leila akakata simu, maongezi yake yote yakakata furaha yangu, kwani nilihisi kwamba ni mwanamke asiye na mume, na nilijipiza kwmaba hadi tuna fika Beirut basi ata kuwa ni mwenyeji wangu.

“Mume wangu huwa ana nipenda sana na ana wivu kweli kweli”

Mama Leila alizungumza huku akiwa na tabasamu usoni mwake. Nikauweka mkono wangu wa kushoto vizuri ili nayeye aweze kuona peta yangu ya ndoa, nikiashiri kwamba nime oa na nina mke. Mama Leila akaitazama pete yangu na akatabasamu.

“Ume sema unaitwa nani vile?”

“Rashidi”

“Ohoo nashukuru kukufahamu kwa mara nyingine”

“Hata mimi”

“Beirut una kwenda kufanya nini?”

Swali la mama Leila linanifanya nikae kimya kwa sekunde kadhaa.

“Biashara”

“Biashara gani?”

“Kwa nini unahitaji kujua mengi sana kuhusiana na biashara”

“Ohoo samahani kama nime kukera”

“Poa”

Nikavaa earphone zangu masikioni na kugeuza shingo yangu dirishani na kutazama jinsi tunavyo katika katika mawingu. Mama Leila akanishika paja na kunifanya nigeuka na kumtazama, nikachomoa earphone yangu sikioni na kumtazama.

“Samahani sana kama nime kukera, mimi ni mtu ninaye penda sana amani na sipendi kumkwaza mtu yoyote kwenye maisha yangu”

“Huja nikwaza”

“Najua nime kukwaza kwani furaha uliyo itumia kwa mara ya kwanza kukutana na mimi sio hii uliyo nayo sasa hivi. Samahani kwa kujujibu kwamba siwezi kukueleza jina langu.”

“Usijali sio muhimu sana. Pia ina bidi sana umpende mume wako kama anavyo kupenda”

Mama Leila akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akinitazama machoni mwangu.

“Mume wako ndio kila kitu kwenye maisha yako. Mpende sana kwa maana hata mimi mke wangu ni kila kitu kwenye maisha yangu”

“Rashidi”

“Naam”

“Kuzungumza na mume wangu hilo ndio lime kukera?”

“Kwa nini linikere ikiwa una mume wako, siwezi kukereka kwa jambo hilo”

“Rashidi tafadhali niambie ukweli?”

“Ukweli kuhusiana na nini?”

“Kwamba ume kereka kwa ajili ya mazungumzo na mume wangu?”

“Hapana kwa nini nikereke dada”

“Okay, ngoja nikuambie jambo moja. Nina ishi na mwanaume ambaye kipindi ana niona, alinioa kutokana na shinokizo la wazazi wangu. Mume wangu ni mtu wa Lebanoni na mimi ni Muethiopia. Kipindi ana nioa mimi nilikuwa ni mdogo sana, nina miaka kumi na saba. Kutoka kipindi hicho sikuwahi kumpenda mume wangu hadi leo hii. Nina ishi naye hiyo basi kwa sababu, moja nina mtoto naye mmoja wa kike, mbili ana wasaidia wazazi wangu kwa hali na mali na amenisomeshea ndugu zangu hadi wengine sasa hivi wana kazi.”

“Mume wako ana fanya kazi gani?”

“Ni afisa upelelezi katika jeshi la polisi Lebanoni”

“Sawa na pole”

“Pole ya nini?”

“Kwa kuolewa na mwanaume usiye mpenda.”

“Nashukuru na huwa nina muogopa sana mume wangu kwani mume wangu ni mtu mwenye wivu. Mtu ambaye ana weza kumua mtu kutokana na wivu wa mapenzi. Ndio maana sipendi sana kuwa karibu na wanaume”

“Nime kuelewa na je upo tayari kutoka kwenye ndoa yako?”

“Mmm mbona ni swali gumu ulilo uliza?”

“Nijibu”

“Sasa hivi siwezi kutoka, ukitegemea umri umesha kwenda. Nina fanya mambo mengi sana kwa jina lake. Yaani nikitoka, nita poteza mtoto na mali zote kwani hata biashara yangu amendikisha jina lake”

“Okay, kutokana nita kuwa nipo Beirut kwa muda muda nita hitaji kukusaidia”

“Kunisaidia kwenye nini?”

“Kutoka kwenye ndoa yako”

“Hahaa Rashid, nimesha kubaliana na kila kitu kwenye maisha yangu. Hivyo siwezi kutoka na kuenenda kinyume na maisha niliyo yazoea”

“Ana kupiga?”

Mama Leila akaka kimya huku akinitazama machoni mwangu kwa masikitiko.

“Mbona kimya?”

“Kupigwa nimesha zoea Rashid. Nime kuwa ni kama salamu kwenye maisha yangu. Ni mwanaume katili sana, anacho kijali yeye ni furaha yake na sio furaha za wengine. Hivyo nimesha zoea”

“Umesha wahi kustaki sehemu yoyote?”

“Una staki kwa nani ikiwa yeye ndio mkuu wa kitengo cha upelelezi Lebanoni. Sikuwa na mtu wa kumueleza na wewe ndio mtu wa kwanza kukuambia kwmaba mume wangu ana nipiga. Nikiwa naye hivi mbali, tuna zungumza vizuri sana, ila hataki apige simu zaidi ya mara moja na usipokee, ana weza kukutukana hadi ukachanganyikiwa”

“Duuu”

“Ila nimesha zoea. Nina mwaka wa ishirini na sita sasa kwenye ndoa hivyo nimesha zoea”

“Ina maana una umri wa miaka arobaini na tatu sasa hivi?”

“Ndio”

“Nipatie namba yako nikifika Beirut tuta kuwa tuna wasiliana”

“Mmmm ni ngumu sana Rashidi”

“Kwa nini ni ngumu?”

“Mume wangu ameiunganisha simu yangu hii, kila meseji, simu zinazo ingia na kutoka kwenye simu yangu ana zipokea kiasi kwamba watu ninao weza kuwasiliana nao ni baba, mama na mtoto wetu ambaye ana soma chuo kikuu Addis Ababa”

“Wewe nipatie na nina kuahidi jambo moja nita hakikisha kwamba mume wako ana pata funzo la jinsi gani ya kuishi na mwanamke mzuri kama wewe, hawezi kukupiga kiasi hicho na watu kama sisi tukawa tuna tazama manyanyaso yako”

Nilizungumza kwa kujiamini kana kwamba huko ninapo kwenda ni mwenyeji na nina jua chochoro zote kumbe ni mgeni na huyu ninaye zungumza naye ni mke wa mtu ambaye akiamua kunizima kabla hata ya kutoka Air port basi ana weza kufanya hivyo.



“Mmm Rashidi wewe una zungumza tu. Humjui mume wangu, na huwa sipendi kukuingiza mtu matatizoni”

“Una niamini”

Nilizungumza huku nikimshika mama Leila mkono wake wake wa kushoto, akanitazama usoni mwangu na taratibu nikaupapasa. Ulaini wa mkono wake uka nifanya nisisimke.

“Niamini mimi nita jua nini cha kufanya”

Taratibu mama Leila akatoa kiganja chake kwenye mkono wangu na akashusha pumzi nyingi sana inayo ashiria ana pambana na wasiwasi ulio mtawala.

“Naomba simu yako”

Nikamkabidhi simu yangu kisha taratibu akaanza kuandika namba yake ya simu kisha akanikabidhi.

“Ila tafadhali usipige simu wala kutuma meseji”

“Sasa ya kazi gani hii namba”

“Rashidi ni bora ukanipatia namba yako. Nimekupe hiyo yangu kwa maana nina ona kama nikikunyima uta kasirika tena”

“Mimi ni mgeni Lebanoni hivyo sijapata namba ya nchini kwenu”

“Hee, basi siku ukiwa na uhakika wa kunitoa kwenye hili tatizo nililo nalo basi ndio unipigie kwa maana hatuto kaa Lebanoni tena”

“Usijali, ila nikuulize swali”

“Niulize”

“Kama ukitoroka kwa mumeo ita kuwaje kwa wazazi wako?”

“Najua hato weza kuwafanya jambo lolote kwa maana wapo nchini Ethiopia”

“Sawa”

Tukaendelea kuzungumza mambo mengi sana na ndani ya mambo hayo, nikamtongoza mwana mama huyu na kumuhakikishia usalama wa maisha yake. Mama Leila hakuwa na kipingamizi kikubwa kwangu kwa maana ucheshi na uhodari wa kuyatengeneza maneno yangu kukamfanya kulainika na kunielewa.

“Hivi uwanja tunao ufikia una itwaje?”

“Una itwa Beirut-rafic Hariri”

“Ahaa sawa sawa”

“Una jua kwenye maisha yangu sijawahi kumkubalia mwanaume yoyote aliye wahi kunitongaza na wewe ndio wa kwanza”

“Kweli?”

“Haki ya Mungu vile. Mume wangu hakunitongoza ila niliolewa kilazima japo sikuwa nina mpenda. Ila wewe ndio ambaye nime jikuta nikikufungulia moyo wangu kwa asilimia themanini. Japo nita hitaji kukufahamu wewe zaidi”

“Usiali, uta nifahamu, ikiwa umesha nielekeza unapo ishi basi nita kuwa nina kuja kukuona”

“Nashukuru mpenzi.”

Tukafika Beirut majira ya saa nne usiku.

“Ila hujainiambia jina lako unaitwa nani?”

Mama Leila akatabasamu na kunikabidhi hati yake ya kusafiria, nikafungua na kukuta ana itwa Leila Al Bashir”

“Mwanangu haitwi Leila, ila mimi ndio ninaye itwa Leila”

“Ohoo nashukuru sana kukufahamu”

“Nashukuru nawe pia. Tuna shuka kwenye ndege sasa, ila fanya kama nilivyo kuambia. Ukijihakikishia kwamba una uwezo wa kunitoa mikononi mwa mwanaume huyo tafadhali fanya hivyo. Na nina kuomba usiwe una nitazama tazama sana tunapo kuwa tuna shuka kwa maana mume wangu ana watu wake hapo uwanjani na tujifanye kama hatujuani”

“Usijali nina kuelewa”

“Sawa nikutakie maisha mema na karibu sana Beirut”

“Nashukuru”

Tukapena mikono na Leila kisha akaanza kushuka yeye kwenye ndege kisha nami nikafwatia huku nikiwa na begi langu mgongoni. Nikapita sehemu za ukaguzi na jambo la kumshukuru Mungu sija pata tatizo la ina yoyote. Nikamuona Leila akipokelewa na mwanaume aliye valia kanzu nyeupe. Wakakumbatiana na wakaingia kwenye gari ya kifahari aina ya Range Rover, mbele ya gari hiyo ikatangulia gari ya polisi na nyuma nayo ikafwata gari ya polisi.

‘Mmm kumbe mume wake ni mtu mkubwa kiasi cha kupatiwa escort ya polisi?’

Nilijiuliza huku nikitazama gari hizi jinsi zinavyo tokomea. Nikaita taksi kisha nikaingia ndani ya taksi hiyo.

“Asalam Aleykum”

Nilimsalimia dereva taksi huyu.

“Wa ‘alaykum al-salaam”

Dareva alonijibu huku akinigeuka.

“Nahihitaji unipekele Deir El Ahmar”

“Sawa, umbali wa kutoka hapa uta soma katika crean yako hapo na uta weza kuona ni bei gani hadi pale tunapo fika”

“Hakuna shaka”

Safari ikaanza huku nikitazama tazama mji huu jinsi ulivyo jengwa.

“Hadi kufika ina weza kuwa ni kilomita ngapi?”

“Ni kilomita mia moja”

“Sawa sawa”

Safari ikazidi kusonga mbele na mjira ya saa saba usiku tukafika katika mji huu ambao ume jengeka vizuri sana. Japo ni kijijini ila una weza kupafananisha na masaki yetu ya Dar es Salaam. Nikamuelekeza dereva kwenye mtaa ambao nina kwenda na akanifikisha. Nikamlipa doka mia na ishirini, kisha nikashuka ndani ya taksi. Nikatazama nyumba zilizopo katika mtaa huu na sikuweza kuina namba ya nyumba niliyo elekezwa. Ukimya ulipo eneo hili kidogo ukanifanya niwe na wasiwasi. Nikaendelea kuikumbua ramani niliyo iona ndani ya faili lililopo katika flash hii. Nikakumbuka maelezo niliyo pewa na nikaanza kuzunguka mtaa huu na nikafanikiwa kuiona nyumba ya mzee Omari, ikiwa imejitenga kidogo na mtaa huu na ipo katika shamba kubwa. Nikatembea kwa hatadhari katika barabara hii ya kuingia katika shamba hili hadi nikafika mlangoni kabla hata sija gonga mlango, nikasikia bundukiki ikikokiwa nyumba yangu.

“Nyoosha mikono yako juu na usijaribu kufanya chochote. Nita kuua”

Sauti kali ya mwanaue ikasikika nyuma yangu na nikatii agizi hili.

“Wewe ni nani na ume fwata nini hapa”

“Nina itwa Rashidi Ngoda. Nina tokea Somalia, nime elekezwa na mzee Al-Seidy.”

“Geuka tararibu”

Nikageuka taratibu na nikamuona mzee Omari akiwa ameshikilia bunduki aina ya Ak-47.

“Code yako”

Mzee huyu alingumza na nikaingiza mkono mfukoni mwangu na nika toa flash ambayo nilipewa na mzee Al-Seidy. Kwa ishara akaniamrisha nifungue mlango ulipo nyuma yang na nikatii. Akaniamrisha nianze kuingia ndani na nikaingia ndani huku yeye akifwata kwa nyuma na bunduki yake akiendelea kuninyooshea. Akaisogelea computer iliyopo kwenye meza ya kusomea na kuichomeka flash hiyo. Akaikagua huku akiwa makini sana na mimi. Alipo ridhika akaishusha bundiki yake chini, kisha akanipatia mkono wake wa kulia ikiwa ni ishara ya kusalimiana. Tukepeana mikono na akanikaribisha nikae kwenye moja ya sofa lililopo hapa sebleni na akawasha taa zenye mwanga mkali kiasi.

“Habari ya Somalia?”

Mzee Omari alizungumza huku akifungua chupa ya wisky, akamimina kwenye glasi mbili, kisha akanikabidhi glasi moja na akaka kwenye sofa ambalo lina tazamana na sofa hili.

“Salama tu”

“Ume kuja kufanya nini Lebanoni?”

“Nimekuja kupata mafunzo”

“Ya nini?”

“Kutoka kwako. Nina hitaji kujiimarisha kwenye mafunzo ya kupambana na watu. Kwani kuna adui nina muwinda ila ana niwinda”

Mzee Omari akanitazama, kwa muonekano ni mzee wa miaka karibia stini ila kwa jinsi alivyo imarika kimazoezi ana oenkana mtu menye umri wa miaka arobaini na tano.

“Kunywa hicho kinywaji”

Nikatazama wisky hii iliyo wekwa kwenye glasi kidogo, kisha nikapiga mfumba moja la nguvu na nikaimeza hadi nikajikuta nikifumba macho kwa ukali wake nilio uhisi kooni mwake.

“Pumzika kwa sasa tuta zungumza asubuhi”

Mzee Omari alizungumza huku akinitazama. Nikajaribu kumjibu chochote ila nikashindwa kwani hichi kinywaji kime nilevya kwa uharaka tofutti na nilivyo fikiria. Tatatibu macho yakajawa na ukungu na kujikuta nikijlaza kwenye sofa hili mzima mzima.

“Hei”

Nilisikia sauti ya ukali ikiniamsha, nikafumbua macho yangu na kuona mtu aliye valia nguo nyeusi huku kichwnai mwake akiwa amejifunika uso na kubakikisha macho yake. Mkononi mwake amashika bastola aliyo ninyooshea kifuani. Kwa kasi ya ajabu nikanyanyuka kwenye sofa hili huku nikimvamia mtu huyu na bastola yake ikaangukia pembeni. Mtu huyu akanipiga ngumi mbili za mbavu na akanigeuza na kunilaza chini na akanikalia kifuani mwangu. Akaanza kunishambulia kwa kunipiga ngumi za usoni mwangu na nikajikinga uso wangu kwa mikono yangu miwili. Nikiendelea kulala chali hivi ana weza kuniharibu uso wangu, nikambamiza teke la mgongo na kumfanya angukie mbele yangu. Nikanyanyuka kwa kasi na yeye akanyanyuka. Nikaangaza ndani hapa na kuona damu nyingi sakafuni na sija muona mzee Omari jambo lililo nifanya nijue sasa nipo kwenye hatari na kilicho salia sasa hivi ni kuhakikisha kwamba nina yaokoa maisha yangu. Mtu huyu akaanza kurusha mateka ya kasi sana kiasi cha kunifanya nishindwe kukwepa mateke mengine. Sikuta kuwa mnyonge zaidi ya mimi nami kujibu mashambulizi haya kw akumpiga ngumi zilizo shiba, ngumi ambazo ukipigwa hata uwe jasiri kiasi gani ni lazima uta zisikilizia tu. Kutokana na mimi sio mzembe nikaanza kumshushia mapigo ya uhakika mtu huyu hadi akaanza kuzidiwa. Nikapiga teke moja zito la kifua lililo mrusha hadi katika meza ya kioo na akaingukia na ikapasuka yote. Nikaiokota bastola yake na kumpiga risasi mbili za kifuani, ila nikajikuta nikishangaa kwani risasi hizi ni risasi bandia.

Mzee Omari akaingia ndani hapa huku akipiga makofi taratibu.

“Mzee!!”

Niliita kwa mshangao huku nikimtazama mzee Omari usoni mwake kwani nilihisi kwamba tume vamiwa.

“Upo vizuri kijana una hitajika kufanyiwa marekebisho machache”

Mzee Omari alizungumza huku akitabasamu. Mtu huyu niliye pigana naye taratibu akanyanyuka na akavua bushori alilo vaa kichwani mwake. Macho ya mshangao yakanitoka mara baada ya kukutana na sura nzuri ya mtoto wa kike.

“Kutana na binti yangu wa pekee anaitwa Fatma. Fatma huyu ndio yule mgeni ambaye nilikueleza jana kwamba tuna weza kumpokea ana itwa Rashidi”

“Nashukuru kukufahamu Rashidi”

“Hata mimi nina shukuru kukufahamu”

“Binti yangu alikuwa ana kufanyia mtihani. Na tulihitaji kufahamu kwamba tuna mtu wa aina gani”

“U..na taka kuniambia kwamba huu ulikuwa ni mtihani?”

“Ndio”

Mzee Omari alijibu huku akitabasamu.

“Fatma”

“Ndio baba”

“Nenda kamuonyeshe Rashidi chumba chake cha kulala”

“Sawa baba”

Nikabebe begi langu huku jasho jingi likinimwagika mwilini mwangu. Tukaondoka sebleni hapa na kutoka nje ya nyumba hii, tukazunguka nyuma na nikaona nyumba ndogo iliyopo pembeni mwa shamba hili.

“Pole”

Niliuambia Fatma huku tukitembea kuelekea kwenye nyumba hiyo.

“Pole ya nini?”

“Kw kila kitu”

“Usijali, sija umia kwa lolote.”

Fatma alizungumza. Urefu wake na wembamba wa mwili wake vina endana kabisa na uzuri wa sura yake. Akafungua mlango wa nyumba hii.

“Kuna chumba, seble, bafu na choo ndani. Jisikie upo nyumbani”

“Nashukuru”

“Jiandae uje kupata kifungua kinywa”

“Sawa”

Fatma akatoka ndani hapa na kuondoka. Nikaurudishia mlango huku nikitazama chumba hichi ambacho kina sofa mbili, tv ndogo na meza moja. Nikaingia chumbani na kukuta kitanda cha futi nne kwa sita. Nikaliweka begi langu kitandani hapa na nikaingia bafuni, nikajaribu kufungua maji ya bomba la mvua na yakaanza kumwagika taratibu. Nikazitoa ndevu zangu za bandia, kisha nikavua nguo zangu zote na nikaoga. Nikamaliza kuoga, nikabandika ndevu zangu za bandia kisha nikabadilisha nguo na nikatoka ndani hapa na kurudi katika nyumba kibwa ya mzee Omari.

“Rashidi”

“Ndio”

“Ukiwa hapa hauna haja ya kuvaa ndevu za bandia na mboni za bandia. Tuna jua wewe ni nani na nini kimetokea kwako. Ndugu yangu Al-Seidy aliweza kunieleza kila kitu”

Mzee Omari alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Sawa sawa”

“Karibuni tupate kifungua kinywa”

Tukanyanyuka kwenye sofa hizi na kuelekea kwenye meza ya chakula ambayo, Fatma ametuandalia kifungua kinywa. Wote watatu tukajumuika kwa pamoja na kuanza kula chapatti hizi na chai.

“Sheria namba moja ya kuwa hapa”

Mzee Omari alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Mwanangu ni bikra. Hupaswi kumtamani, wala kunpenda kimapenzi. Endapo ukikiuka hilo jambo hakuna msamaha wowote zaidi ya kifo”

Mzee Omari alizungumza kwa msisitizo huku akinikazia macho, nikamtazama Fatma na yupo bize na kuendelea kunywa chai hii.

“Ukiwa hapa uta fanya kila shuhuli inao endelea hapa nyumbani. Ikiwemo kupiga, kufagia, kulima na hakuna kutegea wala kusema mimi ni mgeni au mtu fulani. Una nielewa?”

“Ndio mzee”

“Ukiwa hapa huruhusiwi kutoka kwenda huko kijijini pasipo ruhusa yangu na isitoshe kwa sasa kuna hoteli kubwa ime funguliwa hapo mbele, nisije kukuona siku hata moja una peleka miguu yako pale pasipo ruhusa yangu”

“Mazoezi ni muda wowote, haijalishi ni usiku, mchana, asubuhi. Kuwe na mvua, baridi, jua au nini, na kwenye mezoezi ni lazima uhakikishe una tii na kuheshimu kile unacho fundishwa na mkuu wako. Una nielewa?”

“Ndio mzee”

“Mawasiliano yote uta kuwa una yafanya kupitia simu yangu. Kama una simu, laptop hakikisha una nikabidhi mara baada ya kumaliza kifungua kinywa hichi”

“Sawa”

“Fatma sheria nyingine?”

“Huruhusiwi kutongoza mwanamke yoyote hapa kijijini, wala kuwa na mazoea nao.”

“Sawa sawa”

“Endapo uta fanya hivyo, nita dili na wewe”

Fatma alizungumza kwa msisitizo.

“Hakuna shaka”

Fatma akanyanyuka na kuingia ndani ya moja ya chumba, baada ya dakika tatu akatoka akiwa ameshika nguo za mazoezi zilizo kunywa vizuri. Akaniwekea pembeni yangu.

“Maliza kunywa chai, uta kimbia pamoja nami”

Fatma alizungumza huku akinitazama machoni mwangu.

“Sawa”

Nikamaliza kupata kifungua kinywa nikarudi kwenye nyumba ninayo ishi, nikava track suit hii pamoja na raba kisha nikatoka nje na kumkuta Fatma akiwa amepandaa pikipiki yenye matairi manne.

“Nikiendesha taratibu, kipimbia taratibu, nikongeza mwendo, ongeza mwendo wako wa kukimbia. Tume elewana?”

“Ndio”

Nikamtazama Fatma aliye valia nguo za mazoezi huku mkononi mwake akiwa amevalia gloves ngumu. Tukatoka eneo la uzio wa shamba la mzee Omari huku akiendesha pikipiki hii taratibu. Tukapita pembezoni mwa hoteli moja kubwa na nikaona magari mengi ya kifahari. Katika kuangaza angaza kwangu, nikastuka sana mara baada ya kumuona Claudia akishuka kwenye moja ya gari huku akiwa amemshika mkono mtoto wa kiume mdogo ambaye katika kuichunguza sura yaka ana fanania sana na mimi jambo lililo nifanya nipunguze mwendo na kujikuta nikisimama hadi Claudia naye akanigeka na kunitazama ila usoni mwake ana onyesha bado hajanijua kwa jinsi nilivyo na ndevu hizi nyingi za bandia pamoja mboni za bandia.



Fatma akapiga honi kali iliyo nistua. Nikamtazama na akanipa ishara ya kwamba nikimbie, sikuwa na jinsi zaidi ya kumfwata yeye. Akaanza kuiendesha pikipiki hiyo kwa kasi na kunifanya nizidishe kasi ya kukimbia, Fatma akazidi kusonga mbele huku akinipitisha katika mabonde na vilima. Tukafika juu ya moja ya kilima na Fatma akasimamisha pikipiki hii kisha akashuka huku akinitazama usoni mwangu kwa macho ya hasira.

“Ume vunja sheria. Nilikuambia usimtamani mwamke yoyote wala kumtongozamwanamke yoyote yule”

“Nina omba unisamehe mkuu”

Nilizungumza huku nikihema sana kwa maana nimekimbia kwa umbali mkubwa sana. Fatma akanitazama jinsi ninavyo vunywa na jasho.

“Tuna endelea”

Fatma alizungumza huku akipanda katika pikipiki hiyo.

“Nina kiu”

“Shauri yako”

Fatma akawasha pikipiki na akaanza kushuka kilima hichi taratibu. Kutokana nina hitaji mfunzo kwao, sileti ubishi wa aina yoyote zaidi ya kuwa mnyenyekevu. Fatma akanipeleka aeneo la mashamba ambalo lipo kimya kabisa. Jua la saa sita likazidi kuninyong’onyeza hadi ikafika kipindi mwili ukachoka kabisa kukimbia.

“Siwezi zaidi ya hapa”

Nilizungumza huku nikikaa chini mimi mwenyewe kwa maana toka kuzaliwa kwangu sijawahi kukimbia zaidi ya masaa manne mfululizo. Fatma akageka pikipiki na kunifwata sehemu nilipo kaa.

“Simama na upande nyuma”

Nikajikaza na taratibu nikapanda nyuma ya pikipiki hii, Fatma akaendelea kusonga mbele hadi tukafika kwenye moja ya bwawa kubwa ambalo limezungukwa na miti mingi. Fatma akashuka katika pikipiki hii na akaniacha nikimtazama.

“Una kiu, maji ya kunywa hayo hapo?”

“Hapana kwa sasa ime katika”

“Poa”

Fatma akavua nguo zake na akabakiwa na chupi na siridia kisha akaingia ndani ya maji haya na kuanza kuoga taratibu.

‘Rashidi usiwe mjinga huu ni mtihadi ana kutega’

Nilizungumza na nafsi yangu huku nikiendelea kumtazama jinsi anavyo oga.

“Ingia uoge”

“Hapana mkuu”

“Nimesema ingai uoge”

Fatma alizungumza kwa msisitizo, nikashuka katika pikipiki hii kisha nikavua nguo zangu na nikabaki na boksa kisha nikaingia ndani ya bwana hili lenye maji masafi naya baridi sana.

“Una dakika kumi za kuzama ndani ya maji bila kuibuka juu”

“Ehee?”

“Una shangaa nini una dakika kumi”

Fatma alizungumza hukua kinikazia macho. Taratibu nikazama ndani ya maji na kutokana nina mazoezi na pumzi ya kutosha hivyo dakika kumi hazikuwa tabu sana kwangu. Baada ya dakika kumi nikanyanyuka na kw abahati mbaya sikuweza kumuona Fatma wala pikipiki yake. Jambo hili likanipa wasiwasi mkubwa sana na kujikuta nikitoka ndani ya maji kwa haraka. Kitu kingine cha kushangaza sioni nguo zangu na alama za matairi zinaonyesha Fatma ameondoka eneo hili, nikaanza kuzifwata alama hizi huku nikikimbia nikiwa na boksa tu. Nikafika katika njia tatu zilizo gawanyika na kukuta alama hizi za matairi zime zimepita katia njia zote tatu.

‘Mazoezi mengine ni kuzalilishana’

Nilizungmza huku nikiwazatama watu walio mashambani wakinishangaa jinsi nilivyo baki na boksa tu.

‘Ina bidi nirudi nyumbani. Ila hatukupita huku’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikijaribu kutafakari njia tuliyo pita ambayo ina urefu mkubwa sana kwani ni vilima na mabonde. Nikaiweka aibu yangu pembeni na nikaanza kuitafuta njia ya kurudi kwa mzee Omar. Kila nilipo pita watu hawakusita kunitazama kwa maana watu wa nchi hii hawana utamaduni wakuona mtu ana tembea nusu uchi. Majira ya saa kumi na mbili jioni nikafika nyumbani kwa mzee Omari na kumkuta akiwa nje anavuta kiko. Nikaitazama pikipiki ya Fatma na kujikuta nikiachia msunyowa ndani kwa ndani.

“Pole, ume weza kupakumbuka”

Mzee Omari alizungumza huku akitoa moshi mwingi sana puani mwake.

“Ndio mzee”

“Kaoge na nguo zako hizo hapo juu ya pikipiki”

Nikazichukua nguo na viatu vyangu na kuingia katika nyumbani ninayo ishi. Kwa uchovu nilio nao nikajikuta nikikaa kwenye moja ya sofa, kausingizi kakanipitia huku kichwani mwangu nikijiuliza kile nilicho kiona ni kweli au nilikuwa ndotoni.’

‘Alitoroka mara alipo gundua kwamba ana mimba yako’

Kumbukumbu ya sauti ya Brian ikajirudia kichwani mwangu.

“Hei hamka”

Nilistushwa na sauti kali ya Fatma. Nikakurupuka na kujikuta nikisimama.

“Hujakuja kulala. Nenda kaoge uje kupata chakula cha usiku”

“Sawa”

Nilijbu kinyonge huku nikiingia chumbani na moja kw amoja nikapitiliza hadi bafuni. Nikaoga haraka haraka, nikavaa nguo safi na nikatoka ndani hapa na kuelekea nyumba kubwa. Kwa pamoja tukaanza kupata chakula cha usiku.

“Usirudie makosa kama uliyo yafanya leo. Ndio maana ulipewa adhabu ya kurudi nyumbani peke yako”

“Sawa mkuu”

Tukamaliza kupata chakula cha usiku na nikaomba nafasi ya kuzungumza na mzee Omari na tukatoka nje.

“Ndio, niambie”

“Mzee kwanza samahani kwa kuweza kukiuka moja ya sheria. Kuna mwana mama mmoja hivi nilimuona na ni mtu ninaye mfahamu. Nilimuona kwenye hoteli ile kubwa maeneo yale. Yule mwana mama ana kitu changu muhimu sana, ninge uomba kupata nafasi ya kuweza kuonana naye hata kwa dakika ishirini.”

Kama bado hujajiunga katika group. Hadithi ya AIISISI U KILL ME CHAPTER FOUR(killer)imesha anza na leo ina endelea sehemu ya 3. Ada ya group kwa mwezii ni sh 4000. Karibu whatsapp 0657072588 au 0742334453

LIKE PAGE YANGU Story Za Eddy-tz

“Sitaki kujua ana kitu gani nacho. Ila sinto kuruhusu kwenda sehemu yoyote ndani ya miezi mitatu. Kuwa mvumilivu kwa miezi hiyo mitatu au kaonane naye na ondoke moja kwa moja na usirudi tena hapa kwangu”

Baada ya mzee Omari kuzungumza hivyo akaondoka na kuniacha nikimsindikiza tu kwa macho kwa maana nilicho muomba kime shindika.

“Nenda kalale kwa maana asubuhi uta kuwa na mimi”

Mzee Omari alizungumza kisha akafunga mlango wa nyumba yake na nikabaki peke yangu. Nikaingia katika chumba changu hichi, nikawasha tv na kuanza kutazama chaneli hizi za kiarabu ambazo vipindi vyake vingi sivielewi. Nikazima tv hii na kuingia chumbani mwangu na kujilaza kitandani huku taswira ya Claudia ikiendelea kujirudia rudia kichwani mwangu.

Saa kumi na moja alfajiri mzee Omari akanigongea dirishani. Kutokaa nime lala kimachale nikarupuka, nikatoka ndani hapa huku baridi ikiwa ni kali kuliko hata jana. Mzee Omari akavuta sigara yake, huku akinitazama kuanzia chini hadi juu.

“Nahitaji umakini wako. Jiandae tuondoke”

Nikavaa nguo za mazoezi pamoja na suruali raba za mazoezi na nikatoka ndani hapa. Mzee Omari akanionyesha begi kubwa la kubeba. Nikalinyanyua hadi nikajikuta nikiguna. Kwa makadirio ya haraka group hili lina kilo zisizo pungua hamsini. Mzee Maulid akapanda kwenye pikipiki aliyo kuwa anaiendesha Fatma jana, kama ilivyo kuwa jana ndivyo ilivyo leo. Jinsi mzee Omari anavyo endesha kwa kwa mwendo wa taratibu pikipiki hii ndivyo jinsi nami ninavyo paswa kukimbia akiongeza mwendo basi nami nina paswa kuongeza mwendo, ila leo ubaya nina begi lenye uzito mkubwa hata kasi yangu sio kama ile ya jana.

Mazoezi haya ya kukimbia milimani nikiwa na begi lililo wekwa vitu vizito mgononi, likafanika ndani ya wiki mbili mfululizo, hadi nikajikuta nime zoea n anime pata pumzi ya kutosha. Kusema kweli kile alicho kisema mzee Al-Seidy kwamba mafunzo niliyo yapata jeshini hayana maana ni kweli kwani mzee huyu amenifunza kitu cha tofauti. Kitu ambacho kina nisaidia kwenye uwepesi wa mwili wangu na kupata pumzi nyingi hata nikikutana na watu zaidi ya watano nina weza kupigana nao kwa muda mrefu pasipo kuchoka. Mazoezi ya kupambana yakaanza kuchukua nafasi yake. Mzee Omari akanipatia mafunzo ya kareti, taikondo, kung fu, judo, kick boxing na boxing. Mafunzo haya yakazidi kuniboresha kwenye upiganaji wangu. Yule Rashidi wa zamani kama nilikuwa kwenye asilimia kumi basi sasa nipo kwenye asilimia tisini. Umakini wangu na utiifu wangu ukamfanya mzee Omari kujivunia sana kuwa na mwana funzi kama mimi kwa maana nime kuwa ni mtu ambaye nina fanya kile anacho nielekeza nifanya na huwa nina kifanya kwa kiwago cha hali ya juu. Ndani ya miezi miwili tukamaliza mazoezi ya viungo.

“Sasa tuna ingia kwenye mafunzo ya kujifunza matumizi ya silaha. Najua una jua kutumia bastola na silaha nyingine. Ila kutumia kwako ni kwa hali ya chini. Ngoja”

Mzee Omari alizungumza huku akifungua moja ya chumba ambacho toka nifike hapa kwake sijawahi kuingia. Nikaona bunduki za kila aina.

“Hizi bundiku zipo aina ishirini na moja na zote ndani ya mwezi huu ina bidi uweze kuzitumia kiufahasa, tumeelewana?”

“Ndio mzee”

“Tuta anza na silaha ndogo, kisha tuta fwata na hizi silaha kubwa. Nilazima ujifunze namna ya kumdungua mtu akiwa zaidi ya mita elfu moja kutoka sehemu ulipo. Ilimradi tu uwe na bunduki yenye uwezo huo na awe ana onekana”

“Mzee una taka kuniambie Fatma ana weza kuzitumia hizi bundiki zote?”

“Tena toka alipo kuwa binti wa miaka kumi na nane alikuwa ana weza. Fatma ni mtu pekee ambaye nime ishia naye kwenye maisha yangu. Toka mama yake alipo fariki dunia akiwa na miaka sita. Niliamua kuachanana kazi zangu zote za kijasusu na kuamua kumlea mwanangu. Niliamua kuja kuishi huku mashambani, kipindi ambacho hata mji huu haujakuwa kwa namna hii. Kutokana sikubahatika kupata mtoto wa kiume. Ilinilazimu kumlea Fatma kama mtoto wa kiume. Nilimfanyisha mazoezi magumu, nilimfundisha mbinu zote za kujilinda binafsi, kumshambulia mtu. Kiufupi ujuzi wnagu wote niliuhamishia kwake ndio maana hadi amefikisha umri ule, amekuwa ni binti hatari sana.”

“Hongera sana mzee”

“Hongera ya nini?”

“Kwa kumkuza Fatma kwenye mazingira hayo”

“Ni jambo la kawaida. Hata wewe nina imani ukitoka hapa uta kuwa ni mtu wa tofauti sana.”

“Ni kweli na nina shukuru kwa hilo”

“Usiali”

Mazoezi ya utumiaji wa silaha yakaanza rasmi, huku mzee Omari akinifundisha mbinzo zote za kijasusi. Mbinu ambazo zita nisaidia kuwa mpelelezi hatari wa kujitegemea. Kutoana na wingi wamazoezi ambayo mzee Omari ana nipatia, nikaongeza miezi mingine mitatu ya kukaa hapa nyumbani kwake na upendo wa mzee Omari ukazidi kuongezeka na nikawa kama kijana wake wa kiume, huku mimi na Fatma tukichukuliana kama kaka na dada.

“Tusikilizane”

Mzee Omari alizingumza huku akiingia sebleni hapa huku mkononi mwake akiwa ameshika laptop yake.

“Tuna kazi ambayo tume pewa na serikali”

“Serikali gani?”

Fatma aliuliza huku akimtazama baba yake usoni.

“Ya hapa Lebanoni. Kuna daktari ana itwa Razack Mohamed. Ni mtalamu wa kutengeneza mabomu ya nyuklia. Ameshikiliwa na mgaidi nchini Siria. Ina bidi aweze kuokolewa, hivyo serikali ime hitaji msaada wetu. Nina imani Fatma na Rashidi muna weza kuifanya hii kazi na pia ita kuwa ni mtihani wako wa kwanza Rashidi kwa kufanya kazi nje ya eneo hili ulilo lizoea”

“Sawa mkuu”

Nilijibu huku nikiwa na furaha sana kwani kwa miazi hii mitano niliyo ishi nao sijawahi kupambana kiukweli ukweli na adui.

“Wamelipa kiasi gani baba?”

“Wametangulia dola kiki mbili na nusu baada ya kazi kukamilika wata lipa dila laki tatu na nusu tuliyo kubaliana mimi na wao”

“Dola laki sita sio mbaya”

“Ya sio mbaya. Mukikamilisha kila mmoja nita mpatia dola laki moja si ina watosha”

“Sanaa”

Nijibu kwa furaha sana kwani sio kwamba nina hitaji pesa ila nina hitaji kuhakikisha kwamba nina uona uwezo wangu kwa kupambana na hao magaidi.

“Kumbukeni Syria ni majirani zetu. Pia ni nchi ambayo usalama wake ni mdogo ina wapasa kuwa makini kuliko kitu chochote na muhakikishe hamkamatwi kwa manaa mukikamatwa kuna mawaili, kuuwawa ua kuziingiza hizi nchi kwenye mapigano ya kivina na kama munavyo jua Syria na Lebanoni ni maadui”

“Usijali baba kila kitu kita kwenda salama. Hao magaidi wapo wapi?”

“Wapo katika mji wa Talkalakh”

“Ni mpakani kabisa na Lebanoni”

Fatma alizungumza.

“Ndio, huyu daktari ana fumular ya kutengenezea nyuklia na magaidi wa Islamic State wana hitaji hiyo fumular kuweza kutengeneza hizo silaha hivyo wana mtumia yeye kutanegeneza hizi silaha. Tuna siku tatu za kuikamilisha siku hii kwa maana ame tekwa jana usiku akiwa ana shuka Airport ya Damascus International.

“Ila siku tatu ni chache saba baba, kwa maana hatujui uwezo wa hao magaidi upo vipi”

“Ndio maana niliwafundisha kuwa watu wenye uwezo wa kufikiria na kupambana kuliko, polisi, wanajeshi na watu wengine wote kwenye vitengo vya usalama. Ndio maana hili dili nikapewa mimi kwani uwezo wangu una julikana na una tambulika kiserikali. Hivyo nahitaji nyinyi hii kazi muweze kuifanya ndani ya siku mbili. Tuna elewana?”

Mzee Omari alizungumza kwa msisitizo huku akitutazama kwenye nyuso zetu, nika tingisha kichwani nikimaanisha kwamba nime muelewa na hii kazi nina uhakika tuta imaliza ndani ya muda mchache kuliko mzee Omari anavyo fikiria.



“Usijali mzee wangu hili jambo lita kwisha kama tukiondoka leo”

“Safi, mutaondoka leo usiku”

“Sawa baba”

Tukaanza kufanya maandalizi ya safari yetu huku tukiendelea kujifunza jinsi mji wa Talkalakh jinsi ulivyo kwani ndio mara yetu ya kwanza kwenda.

“Baba tumezungumza mengi ila tuta ondoka na usafiri gani?”

“Nita wapeleka kwa helicopter na nitakuja kuwachukua kwa helicopter pale tu kazi itakapo kamilika. Nitawashusha mpakani hivyo man weza kuembea na kuingia ndani ya mji huo”

“Sawa”

“Mzee kmbe una helicopter?”

Nilimuuliza mzee Omari kwa maana katika kipidi chote nilicho kaa hapa sikuwahi kumsikia wala kuona helicopter.

“Ndio nina miliki, ila haipo hapa”

“Sawa mzee”

Majira ya saa moja usiku tukaingia ndani ya gari na kuondoka eneo hili. Tukafika kwenye moja ya mlima ambao leo ndio mara yangu ya kwanza kufika eneo hili. Tukaingia ndani ya pango.

“Hili eneo nililitengeneza maalumu kwa kuweza kuhifadhi nyaraka zangu muhimu za kiserikali pamoja na silaha kubwa za kijeshi. Kabla ya kuwa mpelelezi nilikuwa ni kapteni wa jeshi la anga.”

Mzee Omari alizungumza huku akiwasha taa zilizopo ndani ya pango hili. Akaingiza namba za siri katika simu yake na mlango mkubwa wa chuma ulipo ndani ya hili pango ukafunguka na tukaingia ndani kabisa ya ukumbi mkubwa uliopo eneo hili.

“Waoooooo!!”

Nilizungumza huku nikishangaa vifaa vilivyomo ndani hapa. Nikaona helicopter mbili kubwa za kijeshi.

“Mzee hizi zote ni zako?”

“Ndio ni zangu, mwenzako Fatma ana weza kuziendesha helicopter hizi”

“Wee!!”

“Mtoto wa nyoka ni nyoka, hawezi kuwa kifaranga”

Mzee Omari alizungumza huku akitabasamu. Tukaingia ndani ya helicopter moja ambayo sio kubwa sana.

“Tuna tokaje hapa mzee”

“Usijali wewe kaa uone mambo”

Taratibu akawaisha helicopter hii na ikaanza kupanda juu. Eneo la juu la pango hili likafunguka kitendo kilicho nifanya nizidi kushangaa sana kwani vitu hivi vimetengenezwa kisayansi zaidi.Taratibu tukaondoka eneo hili huku nikishangaa jinsi pango hilo linavyo jifunga na mtu akipita kwa una ona ni mlima kama kawaida.

“Fatma mbona upo kimya?”

“Huwa nikiwa nina kwenda kwenye mission kama hivi huwa sipendi kuzungumza. Nina tumia muda gani wa kufikiria nini nitakacho kifanya kwenye mission yangu”

“Nimekuelewa”

Kwa mwendo wa lisaa moja tukafika katika msitu ambao mzee Omari akaniambia tayari tumesha ingia nchini Syria na hato weza kusonga mbele kwani tume ingia nchini Syria pasipo kibali maalumu kwani hii ni oparesheni ya siri sana. Tukashuka ndani ya helicopter huku kila mmoja akiwa na bunduki mkononi mwake na mgongoni tukiwa tume vaa mabegi yenye silaha, ramami, pamoja na vyakula maalumu vinavyo kaa katika makopo na maji ya kunywa. Mzee Omari akaondoka na helicopter nasi tukaanza kutembea huku tukifwata ramani inayo tuongoza katika simu zetu.

“Hadi saa tisa usiku tuku tumeingia kwenye zone ya maaadui wetu”

Fatma alizungumza huku akiwa ametangulia mbele.

“Sawa”

“Washa earphone yako kwa mana ni lazima tuwasiliane na mzee”

“Sawa”

Nikwasha earphone ndogo ambayo ina tuwezesha kuwasiliana na mzee Omary akiwa nchini Lebanon.

“Aise kuna baridi”

Nilizungumza huku nikiweka vizuri skafu kubwa shingoni mwangu huku kifuani nikiwa nime vaa jaketi la kuzuia risasi.

“Kwani ina tofauti gani baridi ya hapa na Lebanoni”

“Hii naiona kama ime zidi”

“Zipo sawa tu”

Tukazidi kusonga mbele huku tukupita kwenye mabonde na vilima. Majira ya saa tisa na dakika ishirini na tano tukafika katika eneo ambalo magaidi wameificha na katika eneo hili ndio tulipo ambiwa kwamba dokta Razack Mohamed ameshikiliwa.

“Hili eneo ni eneo hatari kuliko maeneo yote uliyo wahi kuyasikia kwenye maisha yako”

“Mmmm”

“Ndio na hatuwezi kuingia pasipo kulifanyia uchunguzi. Eneo hili lina kadiriwa kuwa na magaidi mia nane hadi elfu moja. Ndio maana nilikuwa nina kushangaa unavyo zungmza na baba kwamba hii kazi muna weza kuifanya ndani ya muda mchache tu ikiwa ni jambo gumu sana kuingia kwenye ngome ya magaidi na ukatoka na mtu ambaye kwoa ana faidia”

Tulizungumza huku tukiwa kwenye moja ya kilima kikubwa huku kwa chini kukiwa na mji ambao ndipo walipo mgaidi hao.

“Sasa tuna fanyaje?”

“Ndio tuna fikiria nini cha kufanya”

Fatma alizungumza huku akitoa darubini na kuanza kutazama eneo hilo. Nami nikatoa darubini yangu na kutazama eneo hilo, nikaona wanajeshi wengi wa kundi la Ilsamic State wakiwa na salaha huku wengine wakiwa na mabomu aina ya RPG.

“Kwa akili ya haraka haraka mulikuwa muna fikiria hapa muna ingiaje ikiwa muda kama huu saa tisa usiku hakuna aliye lalala ina kuwaje pale”

“Ngoja kwanza nifikirie Fatma”

“Nikakaa kimya kwa dakika huku nikiendelea kuchunguza eneo hilo kwa kutumia darubini. Kusema kweli ni kambi kubwa sana. Kambo iliyo tengenezwa nyumba za udongo pamoja na mahema.

Ukishuka katika mlima, mita sabini kabla ya kufika katika hiyo kambo kuna mabomu ya kutega yamechimbiwa ardhini”

Fatma aliniambia, nikatazama saa yangu niliyo ivaa mkono wangu wa kushoto na kukuta ni saa kumi usiku.

“Nisubirie hapa”

“Una kwenda wapi”

“Nina ingia ndani ya kambi hii. Hakikisha kwamba huondoki eneo hili”

NIlimuambia Fatma huku nikivua begi langu mgongoni.

“Una akili wewe?”

Fatma alizungumza kwa ukali kidogo.

“Ninazo ndio maana nime kuambia nisubirie hapa”

Nilizungmza huku nikiwa nimesimama. Nikazikagua bastola zangu mbili nilizi zichomeka kiunoni na zote zipo sawa. Nikakagua kisu changu nikicho kichomeka katika buti ya mguu wa kulia na nikakikuta kikiwa kipo.

“Rashidi na taka kufanya nini?”

Niliisikisa sauti ya mzee Omari akizungumza kwenye earphone.

“Nina kwenda kumchukua dokta Razack. Fatma nisubiri”

Mara baada ya kuzungumza maneno hayo nikaanza kushuka kwenye umakini sana huku nikikatiza katika eneo lenye mabomu yaliyo tegwa ardhini. Uzuri na jinsi walivyo yapagnga mabomu yao ni kwamba wameacha nafasi ndogo ambazo mtu una weza kupita bila shida na kama utakuwa mzembe ukakanyaga moja basi lina kulipukia na kukupasua vpande vipande.

“Rashidi kweli wewe ni kichaa”

Fatma alizungumza na nilimsikia vizuri kwani naye amevaa earphone hii. Nikafanikiwa kupita katika eneo hili na nikafika katika fensi iliyo andikwa kwa maandishi ya kiarabu ambayo nina ielewa vizuri. Maandishi hayo yana maanisha hatari, yanya ina shioti. Nikachomoa kisu changu hichi ambacho kina pande mbili, upande wa kwanza ni upande wenye makali na upande wa pili umekaa kama msumeno. Nikaanza kukata fensi hii ya nyaya za chuma taratibu na kwa umakini wa hali ya juu na nikapata tundu kubwa ambalo lina niwezesha kupita. Nikaingia katika kambi hii, nikakimbia hadi kwenye moja lori kubwa lililopo eneo hili. Nikaingia chini ya lori hili mara baada ya kuona wanajeshi wawili wakija upande wangu. Nikajikausha kimya na wakapita pasipo kuhisi chochote. Nikatoa ramani ndogo iliopo mfukoni mwangu naa kuanza kutazama ni jengo gani ambalo dokta Razack yupo. Kwa bahati nzuri eneo nililopo ni mbele kabisa ya jengo ambalo dokta Razack yupo. Nikachomoa bastola yangu kiunoni. Nikaifunga kiwambo cha kuzuia risasi. Kisha nikasubiria taa kubwa inayo zunguka na kumulika ndani ya hii kambi ipite eneo langu, kisha taratibu nikatoka chini ya gari hili na nikakimbilia hadi katika mlango wa jengo hili. Nikachungulia ndani na kuona ngazi zinazo elekea chini. Kwa mwendo wa kunyata nikaingia ndani ya jengo hili na nikaanza kushuka kuelekea chini. Nikwaona walinzi wawili wakiwa wamesimama katika eneo hili ambalo lina vymba vingi vingi. NIkawapiga risasi na kuwaua. Nikamsogelea mmoja na kuichukua funguo nyingi alizo zining’iniza kiunoni mwake. Vyumba hivi vyenye mageti ya nondo, vina wafungwa wengi sana. Wanaume kwa wanawake jambo lililo nifanya nishangae sana. Kutokana nina picha ya dokta Razack, sikuona haja ya kuita jila lake. Nikaendelea kutazama vyumba hivi ishirini na nne ambavyo kila upande vipo kumi na mbili. Nikamuona dokta Razack akiwa katika chumba cha mwisho kabisa.

“Hei dokta”

Nilzingumza huku nikipiha magoti chini.

“Nai wewe”

“Nime kujua kukuoa nyanyuka tuondoke”

Nilizungumza huku nikijaribisha kila funguo hadi nikapata funguo ya mlango huu, nikaufungua na dokta Razack akatoka.

“Kaa nyuma yangu”

Dokta Razack akaka nyuma yangu na tukaanza kutembea kueleke mlangoni kwa umakini sana.

“Kaka na sisi”

Msichana mmoja aliye koendeana kwa kukosa chakula, alizungumza kwa sauti ya unyonge huku akinitazama usoni mwangu. Nikashusha pumzi huku nikiwatazama kwenye chumba walicho fungiwa. Wapo wasichana wasipo pungua kumi na nane.”

“Nina rudi”

Nilimuambia msichana huyu huku nikizidi kusonga mbele. Tukafika mlangoni, nikachungulia nje na kuona askari wakiendelea na harakati zao za ulinzi.

“Una ona lile gari pale?”

Nilizungumza kwa sauti ya kunong’oneza.

“Ndio”

“Kimbia hadi pale ukabingirike na kuingia chini ya lile gari”

“Sawa”

Dokta Razack akakimbia kwa kasi na akatii kama nilivyo muagiza. Nami nikakimbia na kubingirika na kuingia chini ya lori hili.

“Wale wasichana mule ndani wana teseka sana”

“Kazi yangu ni kuja kukuokoa wewe. Hao wengine mimi siwezi kuwaokoa, naona una ona hali halisi ilivyo hapa”

“Ndio”

“Kuna ile fensi pale una liona lile tundu pale?”

“Ndio”

“Ule waya una shoti ya umeme kimbia hadi pale upenye kwa umakini sana”

“Sawa”

Dokta Razack akatoka ndani ya gari hili na akaanza kukimbia hadi katika fensi hiyo akapenya kwenye waya huo kisha nami nikamfwata kwa nyuma na tukaanza kupandisha kilima hichi.

“Hakikisha kwamba ninapo pita mimi nawe una pita kuna mabomu chini yamefukiwa”

“Sawa”

Dokta Razack akanishika shati kwa nyuma na tukaanza kupandisha mlima huu kwa umakini.

“Mungu wangu”

Dokta Razack alihamaki.

“Nini?”

Nilizungumza huku nikigeuka nyuma.

“Nimekanyaga bomu”

Nikastuka sana huku nikimtazama dokta Razack usoni mwake. Nikautazama mguu wake wa kulia ambao ndio ume kanyaga bomu hilo.

“Fetty”

“Nakusikia”

“Una tuona?”

“Ndio”

“Tulinde”

“Usijali”

Nilizungumza huku taratibu nikichuchumaa. Nikatoa siku changu mfukoni na taratibu nikaanza kuchimbua kuzunguka bomu hili ambalo endapo ata nyanyua mguu tu basi sote tuna lipuka. Kutokana na giza ikanilazimu kuwasha tochi ndogo niliyo nayo mfukoni.

“Fety mimi sielewi hili bomu ina kuwaje”

“Kivipi?”

“Lina nyaya sita, mbili ni bluu, mbili ni nyano na mbili nu nyekundu”

“Mmmm baba hilo ni bomu la aina gani?”

“Hata mimi sijui hapa nyaya gani ya kukata”

“Baba una tusikia?”

“Ndio, Rashidi hembu piga picha hilo bomu”

Nikatoa simu yangu mfukoni na kupiga picha na nikamtumia mzee Omari pamoja na Fatuma. King’ora cha hatari kilicho anza kusikika katika kambi ya magaidi kikatustua sana na kumfanya dokta Razack kuanza kutetemeka.

“Mungu wangu wamejua tume toroka”

Dokta Razack alizungumza huku akitetemeka mwili mzima.

“Usitetemeke sasa tuta lipuka”

Nilizungumza kwa ukali huku nikianza kusikia mlio ya risasi nyuma yetu.

“Fuc**”

“Kata waya wa bluu”

Nilisikia sauti ya mzee Omari

“Zipo mbili, ipi nikate?”

“Kata zote”

Nikakata kwa haraka huku milio ya risasi ikiendelea kurindima na Fatma ndio ana jibu mashambulizi hayo.

“Moja, mbili tatu”

Nilimuhesabia dokta Razack kunyanyua mguu na akafaya hivyo. Nikafumba macho kwa sekunde kadhaa huku nikisikilizia kama bomu hilo lita lipuka na kwa bahati nzuri halijalipuka. Nikaanzakujibu mashambulizi kwa magaidi hao wano anza kutoka kwenye fensi sehemu niliyo toboa. Safari hii si kutembea tena bali ni kukimbia kuyaokoa maisha yetu. Tukafanikiwa kunaliza eneo lililo tegwa mabomu na kufika juu kabisa ya kilima alipo Fatma.

“Tuondoke tuondoke”

Nilizungumza huku nikivaa begi langu mgongoni. Fatma akatoa mabomu mawili ya kutega na kuyabandika katika miti miwili kisha tukaanza kukimbika kwa mwendo wa kasi sana.

“Dokta ongeza mwendo”

Nilizungumza huku nikimtazama dokta Razack.

“Nimechoka siwezi kuendelea tena”

Dokta Razack alizungumza huku akiinama chini. Nikamshika mkono wake wa kulia na tukazidi kukimbia.

“Bado mita mia moja nahitaji kulipua ule mlima, mabomu yana nguvu kubwa tusipo kuwa makini tuta lipuka na sisi”

Fatma alizungumza huku akizidi kukimbia kwa kasi anayo imudu yeye. Nikamtazama dokta Razack jinsi anavyo hema.

“Shitii”

Nikamnyanyua dokta Razack na kumuweka begani mwangu kwani ni mwembamba kiasi sema anavyo onekana hana mazoezi ya kutosha. Nikaanza kukimbia hapa ndipo nilipo ona faida ya mazoezi ya kukimbia na begi lenye mawe yenye kilo kuanzia hamsini hadi mia mia moja mgongoni mwangu.

“Mita ishirini”

Fatma alizungumza huku nikiwa ninamkaribia. Nyuma yetu tukaanza kusikia milio ya risasi ikimaamisha magaidi hao tayari wamesha vukuka mlima na wana tufukuzia.

“Lipua”

Nilimuambia Fatma kwa maana risasi zina tupunyu punyua na nyingine zina piga miti. Fatma akaminya kifaa chenye batani ya kulipua mlima huo. Ikia mimi na dokta Razack tumebakisha mita kumi kabla ya kufika eneo salama ambalo mlipuko huo wa bomu hauto tuathiri.



Nikatumia nguvu zangu zote kuhakikisha nina zimaliza mita hizo kumi bila ya mlipuko huo kunipata. Jambo la kumshukuru Mungu nikafanikiwa kumaliza mita hizo kumi huku upepo mkali utokano na mlipoko huu wa bomu ukituangusha chini wote watatu.

Taratibu nikawa wa kwanza kunyanyuka huku nikiwa nimejaa vumbi jingi mwili mzima kwani bomu hili lime kivunja vunja kilima hichi na magaidi wote walio kuwa wana tufwata wamefia kwenye mlipuko huo.

“Mupo salama?”

Niliwauliza wezangu huku nao wakiwa wana nyanyuka.

“Ndio”

Fatma alijibu.

“Hata mimi nipo salama”

Dokta Razack alizungumza huku akijipangusa mavumbi mwili mzima. Hapakuwa na muda wa kupoteza zaidi ya kukimbia eneo hili ili tuzidi kujiweka salama zaidi.

“Ina bidi kuvuka boda na muingie Lebanoni. Fatma si unafahamu njia za siri za kuvuka boda?”

Mzee Omari alizungumza.

“Ndio baba”

“Siwezi kuja kuwachukua Syria kwa maana sasa hivi kuna oparesheni kali ina pitishwa kwenye huo msitu”

“Ina pitishwa na kina nani?”

“Jeshi la Syria”

“Sawa nime kuelewa. RS mpango ume badilika, hapa hadi tupate boder ya Lebanoni na Syria kwa miguu ni kama masaa matano hivyo ina bidi tuwe makini sana kwenye kutembea kwetu kama munavyo jua wananchi wa nchi hii ya Syria. Pia ina bidi hizi jaketi za kuzuia risasi tuziva ndani ya mashati yetu ili tusijulikane kama ni wapelelezi”

Fatma alizungumza na mara nyingi huwa ana penda kuniita RS kufipisha jina langu la Rashidi.

“Sawa sawa”

Tukavua mabegi, kisha tukavua majaketi haya ya kuzuia risasi na mashati, kisha tukaanza kuvaa majakati haya(bullet proof) kisha tukavaa na mashati kwa juu kusha tukaanza safari ya kukatiza kwenye milima kuhakikisha tuna pata mpaka wa Lebabon na Syria. Kutokana na dokta Razack hana mazoezi ilitulazimu kwa mara kadha kusimama njiani na kupumzika hapo kwa dakika tano au kumi kisha safari ina endelea. Safari hii ikatuchukua masaa sita kufika mpakani mwa Syria na Lebanoni kisha tukavuka na kuendelea na safari. Tukafika eneo ambalo mzee Omari tutamkuta. Tukamkuta akiwa ndani ya gari lake aina ya BMW X5. Tukaingia ndani ya gari na safari ya kuondoka eneo hili ikaanza.

“Wanalalamika balaa”

“Kina nani baba?”

“Serikali ya Syria ina lalamika kwa mlipuko mkubwa ulio tokea kwenye mlima wake. Ume sababisha maafa makubwa sana ikiwemo kulipuka kwa Volcano?”

“Weee una taka kutuambia Volcano ililipula kwenye ule mlima?”

“No milima ya jirani kwa maana kama munavyo tambua ule mtetemesho wa bomu haukuwa mdogo kabisa. Ulipekekea baadhi ya miamba katika milima ya jirani kupasuka na Volcano ikapasuka. Ila sio kubwa sana”

“Kazi kweli kweli”

“Dokta Razack nina itwa Omari hawa ni wanangu. Huyu ana itwa Fatma na huyu ana itwa Rashidi. Tulipewa kazi ya kukuokoa na jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba kazi ime kamilika ndani ya muda ambao tuliagizwa na serikali”

“Nina washukuru sana. Allah yeye mwenyewe ndio atakao walipia”

“Amen, je ume wapatia chochote magaidi?”

“Walinilazimisha kutoa fomular ya kutengeneza nyuklia, ila sikuweza kuwaeleza ukweli na nilicho waleza ni kitu tofauti. Hivyo walinihifadhi ili asubuhi waweze kuniingiza kwenye chumba cha kutengeneza hiyo nyuklia. Ila kwa bahati nzuri mume niokoa nina washukuru sana”

“Watu wakuwashukuru ni serikali yetu. Kwani wana jua umuhimu wako”

“Hata nyinyi kwani mulihatarisha maisha yenu kwa ajili yangu”

“Usijali”

Tukafika nyumbani kwa mzee Omari majira ya saa nne asubuhi. Tukapata kifungua kinywa kwa pamoja na daktari huyu.

“Mujiandae kwa maana tuna mpeleka dokta mjini Beirut”

“Waoo leo nina rudi mjini”

“Ndio, pia una weza kuitumia simu yako sasa. Nenda pale chumbani kwangu kuna droo ya kabati ya chini upande wa kushoto kwako. Fungua uta kuta laptop yako pamoja na simu yako”

“Nashukuru sana tena sana mzee wangu”

Nilizungumza kwa furaha sana kwani toka nije hapa sikupata muda wa kuwasiliana na mke wangu Cauther wala familia yangu. Nikaingia chumbani kwa mzee Omari na kuchukua simu yangu pamoja na laptop yangu niliyo jia nayo huku. Nikaiwasha na kitu cha kwanza kufanya ni kumtafuta Jackline kwenye namba yake anayo itumia nchini Ufaransa. Kwa bahati nzuri simu yake ikaanza kuita. Jackline akapokea simu yangu hii ninayo piga kupitia whatsapp video call.

“Rashidi!!”

Jackline alizungumza huku akiwa haamini macho yake. Nikatoka nje kabisa ili kuzungumza nao.

“Niambie mke wangu?”

“Nime kumiss mume wangu. Haki ya Mungu nilitamani kuja Beirut kukutafuta ila wazazi wakanizuia, kwani toka tulipo achana Somalia kwa nini hukunitafuta?”

“Nisamehe mke wangu sikuweza kukutafuta kutokana na sababu za huku nilipo niliweza kupokonywa simu na laptop hivyo sikuweza kuwasiliana na mtu yoyote.”

“Upo salama lakini?”

“Ndio, zaidi ya kuwa salama. Sasa hivi nina mafunzo makali sana mke wangua mbayo nina weza kupambana na mtu yoyote anaye kuja mbele yangu”

“Hongera sana mume wangu. Yaani nilichanganyikiwa nikahisi labda ndio sinto kuona tena”

“Umenieona hivi mke wangu. Kuna mafunzo nita nalizia kisha tuta jumuka Ufaransa pamoja. Watoto na wazazi wapo wapi?”

“Wapo sebleni, ngoja niwapelekekee simu”

Jackline alizungumza kwa furaha kubwa sana, akatoka katika chumba ambacho tulikuwa tuna lala.

“Mama mama ni Rashidi”

Jackline alizungumza na akasimama pamoja na mama. Mama akaanza kumwagikwa na machozi na kunifanya nami nianze kulengwa lengwa na mchozi. Ndani ya dakika tano mama hakuweza kuzungumza chochote zaidi ya kunitazama tu kwani ni mwaka wa tatu huu hatujaonana jambo ambalo sio la kawaida.

“Upo salama mwanangu”

Mama alizungumza huku ajipangusa machozi usoni mwake.

“Ndio mama nipo salama mama”

“Waone wanao, muangalie Shamsa amekuwa mdada sasa”

Mama akawawekea simu Shamsa na wadogo zake wa kiume ambao ni mapacha.

“Baba, ulikuwa wapi, nime kutafuta sija kuona siku zote hizo?”

Shamsa alizungumza kwa furaha. Hakika Shamsa ana fanana na mama yake na amekuwa binti mkubwa mkubwa na jinsi alivyo na ombo kubwa kama mama yake basi amekuwa haraka sana. Nikajipangusa machozi huku nikimtazama.

“Baba mbona una lia?”

“Nina furahi kukuona mwanangu. Nita rudi nyumbani siku si nyingi, umesha anza shule?”

“Ndio baba na nime anza kuimba nyimbo. Mama wiki iliyo pita alinipeleka studio kurekodi wimbo wangu wa kwanza”

“Waoo hongera sana mwangu.”

“Ngoja nikuimbie”

Shamsa akaanza kuimba, sauti yake nzuri na mashairi yaliyo pangiliwa vizuri hakika yakanifanya nisisimke mwili mzima. Nikamuona Fatma akisimama mbele yangu huku akisikilizia wimbo huo wa Shamsa.

“Waooo hongera sana mwanangu. Wimbo wako ni mzuri sana”

“Katika chati ya hapa Ufaransa wimbo wake katika Youtube upo nafasi ya tano kwenye kumi bora ya nyimbo zinazo trend kwa sasa”

Jackline alizungumza kwa kuchungulia kwenye simu hii.

“Hongera sana mwanangu na mke wangu”

“Tuna shukuru sana baba. Ona wadogo zangu, huyu anaitwa Rahim na huyu ana itwa Karim ni majina niliyo wachagulia mimi au ni mabaya?”

Shamsa alizungumza huku akionionyesha wadogo zake hawa ambao kwa sasa wana mwake wa tatu. Kwa kweli Jackline amenizaa mimi mwenyewe, kwani nina fanana na watoto hawa kwa asilimia tisini na tisa.

“Msalimieni baba”

Jackine alizungumza huku akiwa amechuchumaa nyuma yao na simu ameishika kwa mbele.

“Shikamoo baba”

“Marahaba. Muna endeleaje?”

“Salama baba, uta kuja lina”

Karim aliniuliza.

“Hivi karibuni nita rudi”

“Utuletee zawadi. Mimi nataka Chocolate”

Rahim alizungumza huku akitabasamu.

“Usijali nita waletea”

“Mimi nataka bastola”

“Sawa nita waletea nyote”

“Sawa baba nakupenda”

Karim alizungumza.

“Mimi pia nina kupenda”

“Nawapenda pia”

Jackline akasimama huku akiwa ameshika simu hiyo.

“Rashidi kusema kweli ume yabadilisha maisha yangu. Umenifanya kuwa mwanamke wa furaha sana kwenye maisha yangu. Wanao wana fanan sana na wewe, huwa kila ninapo watazama basi nina jisikia amani na kuona kama upo karibu yangu mume wangu. Tafadhali jilinde na uwe salama. Rusi nyumbani”

“Mungu akibariki, nikitoka huku Lebaboni moja kwa moja nita rudi Ufaransa. Vipi baba yupo wapi?”

“Amesafiri yupo kwenye mkutano wa wafanya biashara Barcelona Spaine”

“Ana ulinzi wa kutosha?”

“Ndio. Pia ile video yako niliweza kuikabidhisha kwa serikali ya Marekani. Ikachunguzwa na kugundulika kwamba zile shutuma ni za uongo hivyo mashtaka yote kuhusiana na ugaidi yame futwa. Hivyo DON bado anaendelea kusakwa na serikali ya Marekani.”

“Nashukuru mke wangu”

“Ni jukumu langu mume wagu kukutetea kwenye kila jambo. Wewe ni wangu na mimi ni wako. Kama ni kuanguka tuta anguka pamoja na kama ni kunyanyuka tuta nyanyuka pamoja mume wangu”

“Nina shukuru sana mke wangu. Nina kupenda sana”

“Nina kupenda pia”

Fatma akanionyeshea ishara ya muda akimaanisha muda wa kujiandaa ume wadia. Nikampa ishara ya dakika moja kwamba nina malizia kuzungumza na akaninyooshea dole gumba.

“Mke wangu naomba nizungumze na mama dakika moja ina bidi nikate simu sasa”

“Sawa”


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG